Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

KAMISHANA WA UHIFADHI TFS PROF.SILAYO AELEZA WALIVYOJIPANGA KUWAKABILI WAHALIFU BAHARINI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii 

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa wakala huo umejipanga vema kukabiliana na kila aina ya uhalifu na ujangili ukiwemo wa kutorosha rasimali zitokanazo misitu kwa njia ya bahari na nchi kavu.

Prof.Silayo ameyasema hayo wakati wa akifunga mafunzo ya mbinu za kujiokoa baharini yaliyofanyika katika Chuo cha Baharia cha Dar es Salaam ambapo watumishi wa 15 wa TFS Kanda ya Kusini wanaofanya kazi kwenye misitu ya mikoko, misitu iliyopakana nayo na vikosi vya ukaguzi na udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu.

"Niwapongeze watumishi ambao wamehitimu mafunzo haya muhimu , hii inamaanisha kwamba kwa sasa TFS tunao askari na wakati huo huo ni mabaharia ambao wanakwenda kusimama kidete kwa kushirikiana na watumishi wengine kukabiliana na kila aina ya uhalifu hasa baharini.

"Mafunzo haya kunatoa ujumbe kwa wahalifu kuwa sasa hawana nafasi.TFS tumejipanga na tutaendelea kujipanga siku hadi siku kwa kuendelea kuwajenge uwezo watumishi wetu ikiwa pamoja na kuwafundisha mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu,"amesema Prof.Silayo.

Hata hivyo amesema wakati watumishi wa TFS wakati wa kutekeleza majukumu lao lazima usalama wao pia uangaliwe kwa hali ya juu, hivyo mafunzo hayo ya mbinu za kujiokoa yatasaidia wanapokuwa katika mapambano kuwa na uhakika wa usalama wao.

Ametumia nafasi hiyo kueleza wakati watumishi hao wakipata mafunzo kuna changamoto zimeibuliwa ikiwemo ya uhaba wa vifaa, hivyo TFS itahakikisha inapata vifaa ili kuimarisha utendaji kazi wao ili kufikia malengo na kuongeza kuna boti zimenunuliwa kuimarisha doria.

Awali akisoma rasala ya wahitimu wa mafunzo hayo, Msaidizi Misitu daraja la II Herieth Balua amesema kuwa mafunzo hayo yalianza Oktoba mwaka 2019 hadi Novemba 8 mwaka huu na kutumia nafasi hiyo kuushukuru uongozi wa chuo cha Baharia Dar es Salaam kwa kukubali kutenga muda wao kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.

"Mafunzo haya ya mbinu binafsi za kujiokoa unapokuwa unafanyaka kazi katika maeneo ya bahari ikiwemo misitu ya mikoko ni kitendo au uwezo  ama jitihada za mtu au kundi la watu zinazotumika kuokoa maisha iwapo janga lolote litatokea.Mafunzo haya ni muhimu kwa watendaji tunaofanya kazi katika maeneo ya misitu inayoota sehemu zenye maji.

"Mafunzo haya yalikuwa ni ya nadharia na vitendo .Kwa upande wa nadharia washiriki tumefundishwa aina ya visababishi vya madhara kwenye vyombo vya baharini.Mafunzo kwa vitendo yalishirikisha kwenda kujionea vifaa vya uokozi na namna vinavyotumika iwapo hatari itatokea,"amesema Balua.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Baharia Dar es Salaam Dk.Erick Massami amesema chuo hicho kilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.22 ya mwaka 1991 kwa lengo la kutoa mafunzo ya ubaharia ,utafiti na ushauri katika sekta ya bahari.

Amesema katika ubaharia , chuo kinatoa mafunzo kuanzia ngazi ya awali ya usalama wa vyombo vya majini na maofisa wa meli kuanzia daraja la nne mpaka daraja la kwanza na wanazo aina tano za kozi , hivyo watumishi wa TFS wamepata mafunzo katika moja ya kozi hizo.
 Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(aliyevaa suti nyeusi) akiwa na watumishi wa Wakala huo kutoka Kanda ya Kusini ambao wamehitimi mafunzo ya mbinu zakl kujiokoa baharini ikiwa ni mkakati wa kuwajengea uwezo wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku
 Mkuu wa Chuo cha Baharia Dk.Erick Massami akizungumza wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya mbinu za kujiokoa Bahari ambapo watumishi 15 wa TFS kutoka Kanda ya Kusini wamehitimu na kutunukiwa vyeti 
 Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ambao wamehitimu mafunzo ya mbinu za kujiokoa baharini ambayo yametolewa na Chuo cha Baharia jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya mbinu za kujiokoa kwa Herieth Balua ambaye ni Msaidizi Misitu daraja la pili

Barabara ya kutua na kuruka ndege Kiwanja cha Arusha kurefushwa zaidi

$
0
0
BARABARA ya kutua na kuruka ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Arusha itaongezwa urefu, ili iweze kuruhusu ndege kubwa za abiria kuanzia 70 ziweze kutua na kuruka bila tatizo, imeelezwa.

Mhe. Husna Malima, Mbunge wa Kigoma Kusini mwishoni mwa juma hili (Ijumaa) alihoji Je serikali inampango gani wa kuboresha Kiwanja cha Ndege cha Arusha ili wananchi wa mikoa ya Singida, Manyara, Simiyu, Manyara, Mara na Dodoma wahamasike kutumia usafiri wa ndege, ambazo zinatosheleza kwa sasa?

Amesema mafaniko ya uwepo wa ndege nyingi za abiria nchini ni pamoja na ndege hizo kutumika kwa wananchi kuzipanda.Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Issac Kamwelwe amesema kurefushwa huko kutafanikisha ndege aina ya Bombardier ambayo inabeba abiria kuanzia 70 kutua na kuruka bila tatizo.

Mhe. Kamwelwe amesema tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo kiwanja hicho ni cha tatu nchini kwa kutua na kuruka ndege nyingi zaidi ya 125 kwa siku.

“Tumeweka bajeti kuendeleza kiwanja cha ndege cha Arusha na tayari tenda
imetangazwa, kiwanja hiki kinaongoza kwa kutua ndege nyingi zaidi kwa siku nibiashara kubwa na ndio maana tunataka ndege ya Bombardier itue hapo,” alisisitiza Mhe. Kamwelwe.

Amesema mikoa jirani na Arusha ya Manyara, Singida, Dodoma, Simiyu na Maraitafaidika na maboresho ya kiwanja hicho kwa kuwa wataweza kukitumia ipasavyo.

Naye Meneja wa Kiwanja hicho, Mhandisi Elipid Tesha amesema barabara ya kutua na kuruka ndege itaongezwa urefu kwa meta 200, ambapo sasa inaurefu wa meta 1600 na itakuwa 1800, na pia patajengwa eneo la kugeuza ndege.

Mhandisi Tesha amesema kwa sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege (Apron), ambayo yakikamilika yatapunguza msongamano kwa asilimia 30; pia barabara ya kupita ndege kwenda katika maegesho (taxiway); ujenzi wa maegesho ya magari yapatayo 350 kwa kiwango cha lami ambapo unakwenda sambamba na ujenzi wa mfumo wa malipo ya maegesho hayo.

Pia amesema ujenzi huo wa maboresho ya kiwanja cha ndege cha Arusha utahusisha ujenzi wa eneo la kupumzika abiria, ofisi za waegesha ndege (mashellers), kibanda cha ulinzi na vyoo .

WADAU WA ZAO LA ALIZETI MKOA WA SINGIDA WAKUTANA KWA PAMOJA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO HILO

$
0
0
 Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida, Thomas Nyambo (katikati) akifungua kikao cha wadau walioliwezesha zao la alizeti katika mkoa huo kilichoandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima Mkoa wa Singida (SIFACU LTD). Kulia ni  Mwenyekiti wa SIFACU LTD, Hamis Rajab na  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company) , Tom Sillayo.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company),  Tom Sillayo, akizungumza katika kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Thomas Lijaji akizungumza kwenye kikao hicho namna benki hiyo ilivyoboresha huduma zake, hususani huduma zote za vikundi zinatolewa bure.
 Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
 Viongozi wakiwa meza kuu.
 Wadau kutoka Taasisi za kifedha PASS wakiwa kwenye kikao hicho. Kulia ni Meneja wa Pass-East Central Zone na Busines Development Officer, Meema Meela.
 Meneja Mkuu wa SIFACU LTD, Ramadhan Sephu akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea
 Mwenyekiti wa SIFACU LTD, Hamis Rajab, akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Pyxus, Dickson Kilonzo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Meneja  wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company),  Mkoa wa Singida, Chistopher Mkondya, akizungumza kwenye kikao hicho. Na Waandishi Wetu, Singida MENEJA Mkuu wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company), Tom Sillayo ameiomba Serikali kuendelea kushirikiana na kampuni hiyo ili kuwawezesha Wakulima kuondokana na umaskini.
Sillayo aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau na wakulima wa zao la alizeti kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Luluma mkoani Singida kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa zao hilo.
"Kampuni yetu inashirikiana vizuri na serikali hasa ya mkoa wa Singida na kutengeneza mnyororo mzuri, hivyo naiomba serikali iendelee kutoa ushirikiano hata baada ya sisi kumaliza mkataba wetu,mfumo huu uendelee kwa nia ya kuwasaidia wakulima wetu " alisema Sillayo. 
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Thomas Lijaji alisema kwa sasa benki hiyo imeboresha huduma zake ambapo vikundi hususani vya wakulima vitakapoenda kufungua akaunti watafungua bure na bila makato yoyote hivyo amewashauri wakulima kuunda vikundi ili iwe rahisi kukopesheka. 
"Katika kuelekea msimu wa kilimo NBC tumejipanga kwa kuwawezesha wakulima kupata Mikopo itakayowasaidia kufanya shughuli za kilimo, hivyo nitumie fursa hii kuwakaribisha kwenye benki yetu kwa ajili ya kufungua akaunti na kupata mikopo" alisema Lijaji. 
Awali akifungua kikao hicho Mgeni rasmi ambaye ni Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Singida,  Thomas Nyamba aliwataka wadau kutafuta namna ya kuweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, huku akivitaka vyama vya ushirika kuwashirikisha wakulima kwa kukaa pamoja .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU LTD) Hamis Rajabu  alisema lengo la kikao hicho kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa alizeti ni kuhakikisha uzalishaji wa zao hilo unaongezeka kwa msimu ujao kwani msimu uliopita wakulima walishindwa kuzalisha kwa wingi kutokana na taasisi za kifedha kuchelewesha taratibu za mikopo hadi mwishoni mwa msimu jambo ambalo lilipelekea wakulima kushindwa kuutumia vizuri msimu.
Baadhi ya wakulima wa zao hilo wameshukuru kwa mafunzo yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali kwa wakulima, na kuiomba serikali kuwawezesha wakulima kupata mitaji itakayowasaidia kuongeza kipato kupitia zao hilo la alizeti. 

SPIKA NDUGAI AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI 2019 JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge, Viongozi mbali mbali wa kiserikali na Viongozi kutoka asasi mbali mbali zisizo za kiserikali baada ya kufunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wafanyakazi wa asasi zisizo za kiserikali wakati akifunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu, Ndg. Ludovick Utouh kwa ajili ya kufunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Rais wa asasi zisizo za kiserikali, Ndg. Stigma Tenga na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu, Ndg. Ludovick Utouh alipowasili kwa ajili ya kufunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akigawa tuzo ya Mshindi wa Jumla kutoka Femina, iliyopokelewa na Mkurugenzi wa Habari wa Shirika hilo, Ndg. Amabili Batamula, kwa asasi zisizo za kiserikali wakati akifunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell na kulia ni Rais wa asasi zisizo za kiserikali , Ndg. Stigma Tenga.

Bei ya korosho yaongezeka

$
0
0
Bei ya korosho kwa mnada wa pili  umeongezeka na kufikia 2717 kwa kilo moja ambapo mzigo wote uliopo tan 13,115  umeuzwa

Akitangaza Bei hiyo Meneja Mkuu wa TANECU Mohamed Mwinguku amesema kuwa korosho zilizopo kwenye maghala ya Chama Cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU) zimenunuliwa zote

Amesema kuwa korosho kwa Wilaya ya Tandahimba imenunuliwa kwa sh 2717 kwa mnunuzi wa kwanza,wapili kanunua kwa sh 2697 na mnunuzi wa tatu amenunua kwa sh 2658  

"Korosho iliyopo maghalani tayari tumeiuza yote kwa makampuni matatu Kati ya makampuni 37 yaliyojitokeza," amesema Mwanguku

Naye mkulima Hamis Hassan amesema pamoja na ongezeko Hilo malipo yafanyike kwa muda muafaka ili fedha zimfikie mkulima kwa wakati.

Katika mnada huo makampuni 37  na yalijitokeza,mnada mwingine wa tatu unatarajiwa kufanyika Wilaya ya Newala.

 Meneja wa Chama Cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU) Mohamed mwinguku akizungumza na w
Wadau wa zao la korosho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.

TOAM YAHAMASISHA WATANZANIA KUJIKITA KATIKA KILIMO HAI

$
0
0
*Lengo ni kujipatia chakula kisicho na maradhi yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye kemikali 

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

SHIRIKA la kuendeleza Kilimo hai Tanzania(TOAM) limeeleza kwa kina kuhusu faida zinapatikana kwa kujihusisha na kilimo hicho huku likitoa rai kwa Watanzania kuhakikisha wanajihusisha nacho ili kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla na kuepukana na kula vyakula vyenye kemikali.

Akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kilimohai, Mshauri wa Kilimohai kutoka TOAM Costantine Akitanda amesena ipo haja ya watanzania kuwekeza nguvu zao kwenye kilimo hicho.

"Tunapozungumzia kilimohai tunamaanisha ni kilimo ambacho kinaendeshwa kwa kutumia uasilia na sayansi.Uzuri wa kilimo hiki kinalipa na mazao ya organic yanasoko la uhakika.TOAM kwa kutambua faida za kilimo hicho katika maeneo mbalimbali nchini tumeendelea kuwahamasisha wakulima kulima kilimo hiki na tumekuwa tukiwatambua kwa kuwasajili kwa wale wanaokidhi vigezo na tutaendelea na jukumu letu,"amesema Akitanda.

Kuhusu faida za kilimohai, Akitanda amesema zipo nyingi mojawapo ni kwamba kilimo hicho ni rafiki wa mazingira na kubwa zaidi hata mazao yatokanayo a kilimo cha aina hiyo hayana madhara kiafya kwani uzalishaji wa mazao hautokani na mbolea za viwanda na kimekali.

"Wanaojihusisha na kilimo hiki ndani ya mashamba yao kila kitu kinapatikana humo, kama anahitaji mbolea basi itatokana na mbolea ya mifugo ambayo mara nyingi iko shambani.Kama atahitaji dawa ya kufukuza wadudu shambani nayo itatokana na mimea iliyomo humo humo.Hivyo ni kilimo ambacho hakitumii dawa na kemikali.

"Wanaokula vyakula ambavyo asili yake ni organic kwa sehemu kubwa hawana matatizo ya kiafya kama wanaokula vyakula vyenye kemikali. Pia kilimo cha organic mazao yake yana thamani kubwa ukilinganisha na mazao yasiyo ya kilimo hai,"amesema.

Akitanda ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa kilimo hicho shirika lao limeweka nguvu ya kuhamasisha, kuelimisha, kushauri na kueleza namna bora ya kukifanikisha.

Kuhusu sera,Akitanda amesema sekta ya kilimo hao inatambuliwa na Serikali kwa kuwepo na sera na miongozo na ndio maana hata wao wamekuwa na uwezo wa kuendelea kukisimamia na kukiendeleza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo hai ndani ya nje ya Tanzania.

"Serikali ilishaweka sera kwa ajili ya sekta hii ya kilimo hai , ndio maana TOAM tumekuwa huru kuhamasisha na kusimamia kilimo hiki kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.Kwa kuwa zipo sera inayotuongoza hata Serikali imetoa kipaumbele, kuna vituo vya utafiti kuhusu kilimo hai ambavyo pia vinazalisha mbegu asili na tunashirikiana vizuri tu,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimekuwa na changamoto ya kuwepo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo mengi yanatokana na ulaji wa vyakula vyenye kemikali na kutoa mfano wa ugonjwa kansa, hivyo ameshauri ili kuepukana hali hiyo umefika wakati wa kujikita katika kilimo hai.

Kuhusu waandishi wa habari walioko katika semina hiyo Akitanda amesema ili kuhakikisha taarifa za kilimo hao zinafika kwa uhakika kwa wananchi wameamua kutoa elimu kuhusu kilimo hicho kwa waandishi wa vyombo vya habari hasa kwa kutambua nafasi waliyonayo katika jamii kuhusu masuala yanayohusu jamii ikiwemo ya sekta ya kilimo.

"Tunaamini baada ya kukutana na waandishi wa habari na kupeana mafunzo kuhusu kilimo hai, kwanza mtakuwa bega kwa bega kushirikiana nasi na pili mtatua mabalozi wazuri wa kilimo hiki,"amesema Akitanda.

Wakati huo huo amesema Jauari mwakani kunatakuwa na maonesho yanayohusu kilimo hai ambapo wakulima zaidi 12,000 watakutana mkoani Kilimanjaro.Pia kabla ya maonesho hayo kuna mikutano mingine kadhaa itafanyika mwaka huu ikiwa ni mchakato wa kuelekea katika maonesho hayo ambapo watanzania wataoneshwa namna kilimo hai kinavyoendeshwa na faida zake.

Kwa upande wake Ofisa Mawasiliano kutoka Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO) Emmanuel Kihaule ametumia nafasi hiyo keueleza kuwa kilimo hicho ni muhimu na matumani yao baada ya waandishi kupata mafunzo hayo watatumia kalamu zao kuleta mapinduzi makubwa katika sekta inayohusu kilimo hicho kwa ujumla.

Pia amesema katika kuhakikisha kilimo hai kinasonga mbele, FAO pamoja na mambo mengine wamekuwa wakiangalia sera, mipango na mikakati iliyopo kuhusu kilimo hicho.Mengine ni kufuatilia uzalishaji ambapo katika hilo wamejikita kuangalia namna gani jami imejikita kushghulika na kilimo.

Kihaule amesema FAO inaangalia pia uongezaji wa thamani ya mazao ya organic pamoja na usimamizi wa rasilimali za asili ikiweko ikolojia ambayo maana yake rahisi ni sawa na kusema mahusiano ya binadamu na mazingira.

"Tunayo maswali ya kujiliuza kama leo hii ndani ya miaka 40 hata mito ambayo ilikuwa inatoa maji kutokana na uwepo wa ikolojia sasa imekauka, je baada ya miaka 500 tujiulize hali itakuaje? Tumekuwa na viwavijeshi na aina nyingi ya wadudu waharibifu wa mazao yawapo shambani lakini ukweli ni kwamba kuna tatizo la uharibifu wa ikolojia, hivyo tunahimiza kila mmoja wetu sasa aone umuhimu wake.Kila kiumbe ambacho unakiona shambani au katika mazingira yanayokuzunguka wanafaida zake.Lima shamba lako bila kuharibu ikolojia hii,"amesema Kihaule.
 Moja ya shamba ambalo linalimwa kwa mfumo wa kilimohai linavyoonekana baada ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenda kujifunza kwa vitendo kuhusu kilimo hicho mkoani Kilimanjaro.Mafunzo hayo yameandaliwa na TOAM kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa( FAO)
Mwanafunzi wa kidato cha pili James Lemy Temba anayeishi Kijiji cha Uru Shimbwe akiwa shambani kwao.Kwa mujibu wa baba mzazi wa James , Lemy Temba amesema kijana huyo anamuandaa katika kulima kilimohai ambalo yeye ameririthi kwa baba yake mwaka 1979 na hivyo naye anajiandaa mtoto wake ambaye ndio wa mwisho kuzaliwa kati ya watoto wake tisa.
Baadhi ya waandishi waliopata fursa ya kujifunza kuhusu kilimohai wakiwa  nyumbani kwa moja ya wakulima wa kilimo hicho mkoani Kilimanjaro .Waandishi hao walikwenda kujifunza kwa vitendo kilimo hicho

UKATILI WA KIJINSIA NI UJAMBAZI MPYA –DKT NDUGULILE

$
0
0
Waziri wa Afya Maeandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Semima iliyofanyika jijini Dodoma.
Mshauri Mbobezi wa Sera na Mipango kutoka Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Usu Mallya akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na katika Semima iliyofanyika jijini Dodoma.
Baaadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo kuhusu Mpango wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na katika Semima iliyofanyika jijini Dodoma.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


Na Mwandishi Wetu Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Maeandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Mwaka 2017 Tanzania ilikuwa na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia takribani 41elfu na kati ya vitendo hivyo ukatili dhidi ya watoto pekee ni 13 elfu.

Naibu Waziri Ndugulile amesema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Semina ya wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Jijini Dodoma.

Aidha Naibu Waziri Ndugulile ameifananisha changamoto ya vitendo vya ukatili Nchini kuwa ni ujambazi mpya unaozidi kuwakumba wanawake na watoto kutokana na vitendo hivyo kuendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Dkt. Ndugulile amesema unapoongelea ukatili wa kijinsia unazungumzia maeneo makubwa matatu ambayo ni ukatili wa kimwili, kisaikolojia na ukatili wa kiakili na kuongeza kuwa changamoto ya ukatili wa kijinsia imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Ameyataja matendo hayo yanayozidi kuongezeka kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, ubakaji na ulawiti dhidi ya wanawake na watoto ndio maana ili kukabiliana na vitendo hivyo serikali tangu mwaka 2016 ilianzisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa juhudi za Serikali katika utoaji elimu bure hapa nchini umepunguza suala la mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa mtoto wa kike anapozidi kukaa shuleni ndivyo uwezekano wa mimba za mapema unapozidi kuwa mdogo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amewambia wajumbe wa Kamati hiyo na Wizara kuwa jamii bado ina mila potofu zinazoendeleza vitendo vya ukatili kama vile ukeketeji na kuwataka Wabunge kuelimisha Jamii dhidi ya Vitendo hivyo.

Aidha Mhe. Serukamba amelitaja suala la elimu kwa umma kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukatili kupewa kipaumbelae huku akisifu mpango wa Serikali wa kutokomeza umasikini kwa kiwango cha kaya kupitia TASAF na kuongeza kuwa umasikini pia ni chanzo cha ukatili dhidi ya wawanawake na watoto. 

Naye Mshauri Mbobezi wa Sera na Mipango kutoka Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Usu Malya amesema shirika lake litaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto hapa nchini.

Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ulianza tangu mwaka 2016 na umewezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika utekelezaji wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuondoa mwingiliano, upotevu wa rasilimali watu, fedha na muda unaotumika katika kushgulikia suala moja.

“Dkt. Gwajima, Urudi kutukatia hii Shule Mwanza”- Kiomoni.

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali nchini Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba akiwasilisha maombi ya Darasa kwa Naibu Katibu Mkuu (Picha Atley Kuni).
Diwani viti Maalum Chausiku Hassan Salumu Diwani Viti maalum Halmashauri ya Shinyanga vijijini akipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Nne kwakutekeleza ahadi za Ilani ya Chama cha mapinduzi ya mwaka 2015-2020 kwa vitendo.
Naibu Katibu Mkuu akiongea na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Festo Dugange akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wakati wa Ziara hiyo.

Na Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Mwanza

Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, Wakili Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, amewakilisha maombi maalum kwa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akimsihi kumpatia darasa maalum kwa ajili yakutoa somo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo namna bora yakuweza kupangilia rasilimali watu katika sekta ya Afya kwenye Jiji hilo.

Wakili Kibamba ametoa ombi hilo muda mfupi mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, kutembelea Kituo cha Afya Igoma na kukagua miundominu kisha kuzungumza na watumishi wa kituo hicho sambamba na timu ya Afya ya Halmashauri, ambapo katika maongezi yake Naibu Katibu Mkuu alihimiza suala la uwajibikaji lakini pia matumizi sahihi ya rasimali pamoja na huduma bora kwa mteja.

Akizungumza na watumishi hao, Dkt. Gwajima alisema inashangaza unakuta kituo kimoja cha afya kinaelemewa na wagonjwa ili hali kituo kingine kilichopo karibu hakina mgonjwa na chanzo kikuu ikiwa ni huduma mbovu na kutokumjali mgonjwa. Lakini pia suala la mtu mmoja kung’ang’ania eneo alilopangiwa ilihali uapande wa pili unaelemewa.

“Ndani ya kituo kimoja unakuta Muuguzi anasema mimi nimepangiwa wodi ya Mama na Mtoto kwaajili yakuzalisha, lakini ndani ya kituo hicho hicho upande mwingine mathalani wa wagonjwa wa nje wagonjwa wamejaa na ukitazama unakuta mtoa huduma huyo amezidiwa na hana msaada wakati yule wa wodi ya wazazi yeye yupo tu anasubiri mama aje ajifungue hili halina afya hata kidogo na ni matumizi mabaya ya rasimali watu” alisema Dkt. Gwajima.

Mara baada ya darasa hilo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza hakuficha furaha yake na badala yake akaomba somo kama hilo angependa lifundishwe kwa watumishi wote wa afya wa Halmashauri hiyo kwa muda maalumu na ndipo alipo wasilisha maombi yake.

“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, tumekuelewa sana, sasa mimi naomba niwasilishe maombi maalumu, nikuandalie darasa japo uje wewe na jopo lako unifundishie watu wa Halmashauri hii kwakweli naomba sana sana” alisihi Wakili Kibamba.

Kufuatia maombi hayo Naibu Katibu Mkuu alimkubalia ombi hilo na kuahidi kurudi katika Jiji hilo kwaajili yakwenda kutoa somo kwa watumishi hao.

Kituo cha Afya Igoma kituo kilicha anzishwa mwaka 1982 na nimiongozi mwa vituo vilivyopo katika Jiji la Mwanza ambacho kinauwezo wa kuhudumia watu 41,293 na watumishi wapatao 62 na katika mwaka wa fedha 2017/18 kilipatiwa fedha na serikali milioni 400 kwaajili ya upanuzi kwa majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi, jingo la maabara, jingo la mionzi, jingo lakufulia sambamba na jingo lakuhifadhia maiti, ambayo yote yamekamilika kwa kujali thamani ya fedha na hivyo kumfurahisha Naibu Katibu Mkuu.

Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza Shinyanga na Tabora ambapo katika ziara hiyo, amekuwa akitoa somo la matumizi bora ya rasimali watu na vitu lakini pia suala huduma bora kwa mteja.


SIMBACHAWENE ATAKA LIFANYIKE KONGAMANO LA MAZINGIRA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha kupokea tathmini ya uharibifu wa uoto wa asili iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine.

Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu tathmini ya uharibifu wa uoto wa asili iliyofanywa katika Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni agizo la Makamu wa Rais. Mhe. Samia Suluhu Hassan


Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Kijiografia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Benedict Mugambi akiwasilisha maelezo ya kazi iliyofanyika katika Mkoa wa Shinyanga ya upimaji uoto wa asili na ukusanyaji takwimu mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene pamoja na wajumbe.


Sehemu ya wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia kikao cha kupokea taarifa ya kazi ya ukusanyaji takwimu na upimaji wa uoto wa asili iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Shinyanga.


Wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia kikao cha kupokea taarifa ya kazi ya ukusanyaji takwimu na upimaji wa uoto wa asili iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Shinyanga.

……………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema ipo haja ya kufanya kongamano la taifa la mazingira na mabadiliko ya tabianchi ambalo litawahusisha wadau ili kuboresha sekta hiyo.

Simbachawene amesema hayo wakati akipokea taarifa ya tathmini ya uharibifu wa uoto wa asili iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika maeneo ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni maagizo ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanyika ziara mkoani humo mwanzoni mwa mwaka huu.

Waziri huyo alisema kuwa suala la mazingira linamhusu kila mtu hivyo kuna umuhimu wa kuwahusisha wadau kama wafanyabishara, sekta binafsi na taasisi za dini ambao watatoa mchango wa hali na mali katika kuchangia mfuko wa mazingira.

“Upo umuhimu kwa Ofisi ya Makamu wa Rais na NBS kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kupata takwimu sahihi za hali halisi ya mazingira ili kuweza kukabiliana nazo na ningependa kuona pia utafiti na takwimu zichukuliwe katika mikoa mingine ikiwemo Geita, Singida, Dodoma na Tabora ambayo inaathiriwa na ukataji miti,” alisema.

Aidha alisisitiza kuwa masuala ya mazingira yaelekezwe katika ngazi ya Serikali za Mitaa ambako kule ni rahisi kuwafikia wananchikwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

LONGIDO YAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA SOMALIA,WAKUTWA NA NGAMIA 200

$
0
0
Na Woinde Shizza,Globu ya Jamii Arusha

MKUU wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe ameongoza operesheni ya kuwakamata waahamiaji haramu kotoka nchini Somalia wakiwa na ngamia 200 pamoja nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya Kenya.

Akizungumza leo wilayani hapa mara baada ya kuwakamata baadhi ya wahamiaji hao haramu

kutoka nchini Somalia,Mkuu huyo wa Wilaya wamefanikiwa kuwakamata baada ya kupata taarifa kuwa katika mpaka wetu wa Namanga upande wa Magharibi ndani ya kata ya Kimkoa ambayo ina karibu kilometa 30 kutoka Mjini Namanga kuna watu wasiojulikana wameweka makazi(kempu).

Amesema baada ya kupata taarifa hizo walikwenda kufanya operesheni na kufanikiwa kuwakamata watu wawili wenye asili ya nchi ya Somalia na hakuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili huku wengine wao wakiwa wamekimbia

"Tulienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na baadhi ya askari kutoka mkoani, katika eneo hilo tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji hao haramu wawili.Wengine wamekimbia,"amesema Mkuu wa Wilaya Mwaisumbe

Amefafanua baada ya kuwakamata walifanikiwa kuwakuta na mifugo aina ya na ngamia zaidi ya 200 pamoja na nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya jirani ya Kenya.

Amesema kuwa operesheni hiyo haitaishia hapo bali itaendelea kwa lengo la kuhakikisha watu wote ambao wameingia nchini bila utararibu na kuweka makazi ya kudumu wanachukuliwa hatua na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa wanapoona kuna watu wameingia nchini kwetu.

Wakati huo huo Mwaisumbe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano ambao umefanikisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na mifugo yao ya ngamia.Kwa upande wake Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha

Udhibiti na Usimamizi wa mipaka Mkosa wa Arusha Elisamia Mmari amesema kwa utaratibu wa uhamiaji watuhumiwa hawa watapelekwa katika ofisi za uhamiaji na watachukuliwa maelezo baada ya hapo watafikishwa katika vyombo vya sheria ili iwefundisho kwa watu wote wanaiongia nchini na kufanya shuhuli za bila kufata taratibu.

Mwisho

ASILIMIA 97 WAREJESHA FOMU ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amesema jumla ya wananchi waliochukua fomu za kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini walikuwa  555,036 na waliorejesha 539,993 sawa na asilimia 97.29 na asilimia 2.7 hawakurejesha kwasababu mbalimbali

Mhe Jafo amesema zaidi ya rufaa 13,500 zimewasilishwa na vyama vya siasa kwenye kamati za rufaa za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi huo jina la mgombea likiteuliwa linabaki kwenye katarasi za kupigia kura hata kama amejiengua kushiriki.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vilipeleka rufaa zao kwenye Kamati za maeneo yao

Amesema vyama vyote vimewasilisha rufaa zao ikiwemo Chama cha Mapinduzi, CUF, ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi ambapo rufaa zilizowasilishwa ni 13,500 na kusema Kamati zinaendelea kufanya maamuzi na tayari zingine zishatoa majibu ya rufaa na kesho watatoa hali halisi ya mchakato mzima wa uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

" Baada ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu kukamilika, kulikuwa na nafasi ya kushughulikia mapingamizi mbalimbali ambayo yamewasilishwa kwenye kamati za rufaa za maeneo husika ambapo mwisho wa kupitia rufaa hizo ni leo.

Kuna ngazi za mapingamizi na jambo hili ni la kidemokrasia huwa linafanyika, ibara ya 23 ya kanuni zetu inasema kamati za rufaa zina majukumu ya kupitia rufaa zote zinazojitokeza,”amesema.

Aidha amesema katika ziara yake aliyoifanya mikoa mbalimbali kukagua shughuli zinazofanywa na kamati za rufaa kwenye mikoa mbalimbali Singida, Dodoma, Manyara, Iringa na Njombe alipitia baadhi ya fomu zilizokuwa zimepitiwa na kamati hizo na kubaini kuna makosa kwenye ujazaji fomu.

“Kama vile mtu ameandika umri amezaliwa mwaka 2019, sehemu zingine mtu ameandika hata halmashauri yenyewe haiitwi hiyo msaidizi wa uchaguzi afanye nini?, mwingine sehemu ya saini ameweka tarehe halafu sehemu ya tarehe ameweka saini, fomu zingine mtu amejidhamini mwenyewe, wasimamizi walifanya kazi yao kwa mujibu wa kanuni,”amesema.

Ametaja mapungufu mengine ni kutofautiana majina kwenye fomu na daftari la wapiga kura wa uchaguzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana na mchakato mzima wa uchukuaji na urejeshaji fomu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

HAKI RASILIMALI YAKAZA KAMBA KUBORESHA SEKTA YA UZIDUAJI

$
0
0
Na Leandra Gabriel,  Michuzi TV

JUKWAA la uziduaji lililoandaliwa na Taasisi ya Haki Rasilimali kwa mwaka 2019 limefanyika Jijini Dodoma na kutoka na mapendekezo mbalimbali ikiwemo ufaidi wa rasilimali kwa wananchi pamoja na matumizi sahihi ya mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji inayojumuisha rasilimali za mafuta  madini na gesi asilia pamoja na kuwashiriki sha wanawake katika sekta hiyo.

Kupitia jukwaa hilo lililowakutanisha wadau kutoka kote nchini mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo duru ya kisiasa na uzalendo wa rasilimali, ushirikishwaji wazawa na ufaidi wa wananchi kwenye sekta ya uziduaji, pamoja na mapato na matumizi yatokanayo na sekta ya uziduaji, ambapo masuala makubwa yaliyotawala ni pamoja na kutowaminya wanawake kuwashiriki katika sekta ya uziduaji aidha kwa imani potofu au vinginevyo.

Pia washiriki wameishauri Serikali kutunga sheria bila kuweka vikwazo ambavyo vitawaumiza wananchi wa chini na hiyo ni pamoja na wabunge kutopitisha  sheria kwa hati ya dharura kwa manufaa ya wote hasa wananchi wa kupata cha chini.

Vilevile washiriki wametoka na kauli moja ya kushirikiana, kuaminiana na kuhabarishana baina ya Serikali na azaki za kiraia kwa kujenga ubia katika kuhakikisha sekta ya uziduaji inaleta tija zaidi.

Kupitia jukwaa hilo washiriki waliotoka katika Mikoa yenye Rasilimali za madini ikiwemo Geita na Shinyanga wamezishauri kampuni zinazofanya shughuli za uziduaji katika maeneo hayo kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa wamiliki wa rasilimali hizo (wananchi) ikiwemo kujenga miundomiu ya shule, hospitali na miundombinu ya maji.

Pia kupitia jukwaa hilo washiriki wameishauri Serikali kwa kushirikiana na Azaki mbalimbali kuelekeza makampuni yaliyowekeza kwenye sekta ya uziduaji nchini kuto nafasi za ajira kwa wazawa na hiyo ni pamoja na kutoa nafasi za kusambaza huduma na  bidhaa katika maeneo ya kisekta.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na taasisi ya Haki Rasilimali lilitanguliwa na wiki ya Azaki ambapo viongozi  na wadau mbalimbali wa sekta ya uziduaji walitoa maoni ya kujenga na kuboresha sekta hiyo.

 Mkurugenzi mtendaji wa Haki Rasilimali  Racheal Chagonja akichangia mada wakati wa jukwaa la uziduaji lililofanyika jijini Dodoma,  Chagonja  amesema kuwa wataendelea kuhabarisha wadau kuhusiana na fursa zitokanazo na sekta ya uziduaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki Rasilimali Racheal Chagonja (kulia) wakionesha kitabu maalumu cha sekta ya uziduaji kilichozinduliwa na taasisi hiyo wakati wa jukwaa la uziduaji lililofanyika jijini Dodoma.
 Balozi  wa Canada nchini Pamel O'Donnell's (katikati) akichangia mada kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika sekta ya uziduaji ambapo ameeleza kuwa nafasi ya wanawake katika sekta hiyo ni muhimu, leo jijini Dodoma.

SPIKA NDUGAI ASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KATI YA BUNGE LA TANZANIA NA UNICEF, AFUNGUA MAFUNZO YA UWAJIBIKAJI NA UWAZI

$
0
0



Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF), Ndg. Rene van Dongen wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNICEF tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Katika Makubaliano hayo UNICEF itawezesha Bunge katika kufanya kazi zake kwa urahisi ikiwemo kuwapatia semina na mafunzo ili wawe na uelewa wa kuwatetea haki za watoto Bungeni, ikiwa ni pamoja na kuwasemea kuhusu haki zao za kimsingi;- Haki ya Kuishi, Mavazi, Kusoma na Kusikilizwa, Pia kutetea kupitishwa kwa Bajeti nzuri ya watoto itakayowezesha kufikia malengo


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF), Ndg. Rene van Dongen wakionyesha Mikataba wa Makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNICEF tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Katika Makubaliano hayo UNICEF itawezesha Bunge katika kufanya kazi zake kwa urahisi ikiwemo kuwapatia semina na mafunzo ili wawe na uelewa wa kuwatetea haki za watoto Bungeni, ikiwa ni pamoja na kuwasemea kuhusu haki zao za kimsingi;- Haki ya Kuishi, Mavazi, Kusoma na Kusikilizwa, Pia kutetea kupitishwa kwa Bajeti nzuri ya watoto itakayowezesha kufikia malengo


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF), Ndg. Rene van Dongen wakibadilishana Mikataba wa Makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNICEF tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Katika Makubaliano hayo UNICEF itawezesha Bunge katika kufanya kazi zake kwa urahisi ikiwemo kuwapatia semina na mafunzo ili wawe na uelewa wa kuwatetea haki za watoto Bungeni, ikiwa ni pamoja na kuwasemea kuhusu haki zao za kimsingi;- Haki ya Kuishi, Mavazi, Kusoma na Kusikilizwa, Pia kutetea kupitishwa kwa Bajeti nzuri ya watoto itakayowezesha kufikia malengo


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua mafunzo ya Uwajibikaji na uwazi katika Mikataba ya Manunuzi ya Umma kwa Kamati za Usimamizi za Bunge za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo katika Ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Usimamizi za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) akifungua mafunzo ya Uwajibikaji na uwazi katika Mikataba ya Manunuzi ya Umma kwa Kamati za Bunge leo katika Ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SERIKALI YAKAMATA POMBE KALI IMETELEKEZWA PORINI KUKWEPA KODI SHINYANGA

$
0
0

Serikali mkoani Shinyanga imekamata pombe kali aina ya Shujaa, ambayo ilikuwa imetelekezwa porini eneo la Lubaga manispaa ya Shinyanga, ikiwa ndani ya gari aina ya Roli lenye namba za usajili T 391 AES, kwa madai ya kukwepa kulipa kodi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba 9, 2019 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa kwenye kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga, eneo ambalo gari hilo limewekwa chini ya ulinzi, amesema kuwa serikali itawashughulikia wawekezaji wote ambao wanatabia ya kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Telack ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga, amesema Serikali inahitaji sana wawekezaji hapa nchini ili kukuza uchumi wa taifa, lakini siyo wawekezaji wa kukwepa kodi na kufanya biashara kiujanja ujanja.

“Pombe hii kali ya Shujaa Katoni 1,490 tumeikamata ikiwa imefichwa porini eneo la Lubaga manispaa ya Shinyanga, ikiwa ndani ya gari hili ambalo mnaliona hapa, na wamiliki wa kiwanda hiki wamekuwa na tabia ya kukwepa kulipa kodi na siyo mara ya kwanza kukamatwa,”amesema Telack.

“Hivyo naagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Kesho wafike hapa, ili kufanya tathmini ya kujua kiasi gani cha kodi ambacho watu hawa wanapaswa kulipa, ili Serikali iweze kukusanya mapato na kupata fedha za kutekeleza maendeleo kwa wananchi,”ameongeza.

Pia ameonya baadhi ya Askari Polisi kushirikiana na waharifu hao wa kiwanda cha Shujaa, na kuwapa mbinu za kukimbia ili kukwepa mkono wa Serikali, na kumuagiza Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Shinyanga, kuwa ndani ya siku nne, wamiliki wa kiwanda hicho wawe wameshakamatwa.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao, alithibitisha kukamata Pombe hiyo ya Shujaa, na kuahidi kutekeleza maagizo hayo ya mkuu wa mkoa, huku akitoa wito kwa wamiliki hao wa kiwanda cha Shujaa wajisalimishe wenyewe kwa usalama wao kwani watakamatwa tu popote pale walipo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akionya wawekezaji kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi za Serikali hasa kiwanda hicho cha Pombe Kali ya Shujaa, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, na nyuma yake ni gari likiwa na Pombe za Shujaa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisisitiza zoezi hilo la kusaka bidhaa ambazo hazilipi kodi ni endelevu ambapo wamiliki wa kiwanda hicho cha Pombe ya Shujaa siyo mara ya kwanza kukamatwa na umekuwa mtindo wao wa kukwepa kulipa Kodi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Richard Abwao, akithibitisha kuikamata Pombe hiyo ya Shujaa ikiwa porini na kuahidi kuwatia nguvuni wahusika ambao wamekimbia.
Pombe kali za Shujaa Katoni 1,490 zikiwa kwenye Gari eneo la kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack mkono wa kulia, akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko Kushoto wakiangalia Pombe hiyo Kali ya Shujaa.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

HASUNGA AAGIZA VIONGOZI WA SACCOS YA KURUGENZI JIJINI ARUSHA WAKAMATWE Inbox x

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

 Sehemu ya wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019. 
Aliyekuwa Meneja wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi  Christina Sumaye (Kulia) akiwa na aliyekuwa karani wa SACCOS hiyo Edith Malley wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kabla ya kuagiza kukamatwa kwa viongozi hao wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019. 
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mkuu wa Upelelezi, na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuwakamata viongozi mbalimbali wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za wanachama.

Waziri Hasunga ametoa maagizo hayo leo tarehe 9 Novemba 2019 mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wanachama wa chama hicho wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wanapaswa kukamatwa haraka iwezekanavyo kuanzia waliokuwa viongozi mwaka 2004 mpaka 2015 ili kurudisha fedha zote walizozizihujumu za wanachama na walizokopa.

Wengine alioagiza wakamatwe ni pamoja na wajumbe wote wa kamati za mikopo, Kamati ya usimamizi wa SACCOS iliyokuwepo kipindi chote hicho, Wajumbe wote wa Bodi ya SACCOS iliyokuwepo awali kabla ya Bodi iliyopo sasa. “Tunachotaka sisi fedha zote za wanachama zirudi na hata leo wakirudisha fedha hizo hatutaendelea na kesi” Alisema

Pia ameagiza mwanachama wa SACCOS hiyo Bi Zainab Nassor aliyeanzisha vikundi hewa 14 akamtwe, huku wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa SACCOS Dkt Freedom Makiago,  Makamu Mwenyekiti Gasto Gasper, Meneja Christina Sumaye, na wajumbe Andrea Sekidio, Joseph Kuhamwa na Mwanahamisi Gembe.

Katika hatua nyingine Mhe Hasunga ameagiza kukamatwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Usimamizi Bi Mwanahawa Kombo, na wajumbe Samwel Mushy, Estomin Chang’ah. Huku akiagiza pia karani wa SACCOS hiyo Edith Malley kukamatwa.

Katika hatua nyingine ameagiza viongozi wote walioandikwa kwenye vikundi vya mikopo kukamatwa haraka iwezekanavyo na kuchukuliwa hatua za haraka ikiwemo kurudisha fedha za wanachama.

Mhe Hasunga amesema kuwa lengo la kunzishwa vyama vya ushirika ilikuwa ni kuwanufaisha wananchi kupitia umoja huo muhimu kwani mafanikio yanahusisha nguvu ya pamoja.

Hata hivyo ameagiza Bodi iliyopo madarakani kubainisha taarifa za kumbukumbu zote za chama hicho kwa kuonyesha idadi ya wanachama na akiba walizonazo katika chama, idadi ya hisa na kiasi cha fedha zinazodaiwa na kila mwanachama.

Kwa sasa chama kinadaiwa fedha kiasi cha shilingi 2,486,365.68 zilizotokana na mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha, Amana, Akiba na Hisa za wanachama hususani wastaafu ambazo zilichukuliwa kwa kutumiwa na wahusika hao bila utaratibu na kwa malengo yao binafsi.

Wanachama wastaafu wanadai zaidi ya shilingi 831,764,924.87 zitokanazo na fedha za Amana walizoweka katika chama kutumia viinua mgongo vyao baada ya kustaafu utumishi, Akiba na Hisa walizowekeza tangu wajiunge na chama hicho.

Wanachama wanaoendelea na chama na waliojitoa wanadai zaidi ya shilingi 770,181,745.56 zitokanazo na Amana, Akiba na Hisa walizowekeza tangu wajiunge na chama hicho.

Kadhalika, Taasisi za kifedha zinazodai ni pamoja na (CRDB, NSSF na TUMAINI SACCOS) wanaodai zaidi ya shilingi 874,575,517.25 bakaa ya mikopo iliyotolewa bila kuzingatia utaratibu wa kifedha na kwa kutumia taarifa za udanganyifu.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 2 kwa mualikowa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo ambapo pamoja na mambo mengine atashuhudia shughuli za sekta ya kilimo.

MWISHO


WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA SHEREHE ZA MAULID MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, kumwakilisha Rais Magufuli, katika sherehe za Maulid, zitazofanyika mkoani humo. Novemba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili, kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, kumwakilisha Rais Magufuli, katika sherehe za Maulid, zitazofanyika mkoani hapo. Novemba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI NORDIC NA AFRIKA WATEMBELEA MRADI WA SGR

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Bw. Masanja Kungu Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari wakati mawaziri wa mambo ya Nje wa nchi za NORDIC na Afrika wakipotembelea kujionea ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR eneo la Vingunguti Kiembembuzi leo.
Mmoja wa mawaziri hao akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo.
Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Nordic na Afrika watembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam hadi Vingunguti jijini Dar es Salaam Novemba 09, 2019.

Lengo la ziara hiyo ni kuona hatua kubwa ambayo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji ukizingatia miundombinu ni moja kati ya vitu muhimu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi za Nordic na Afrika.

Mawaziri hao walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa eneo la stesheni jijini Dar es Salaam, daraja la treni lenye urefu wa KM 2.5 pamoja na maendeleo ya Mradi kwa ujumla kipande cha Dar es Salaam – Morogoro ambao umefikia zaidi ya 70%.

Miongoni mwa Mawaziri waliopata fursa ya kutembelea mradi ni kutoka nchini Egypt, Nigeria, Angola pamoja na Niger. Ziara hii ni matunda ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Nordic na Afrika uliojadili mambo kadhaa kuhusu kuboresha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi za Afrika na nchi za Nordic uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es salaam.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amewashukuru Mawaziri hao kwa kuchagu kutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kuwa ipo Miradi mingi ya kimkakati.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje nchini Nigeria Mhe. Zubairu Dada amesema kuwa amefurahishwa na emeipongeza Tanzania kwa kutumia fedha zake za ndani kujenga reli ya kiwango cha kimataifa kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora Singida. Ameongeza kuwa Afrika haiwezi kuendelea kusubiri maendeleo hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kufanywa ili kuhakikisha miradi ya miundominu inakamilika haraka ili watu wapate huduma.

WAAJIRI WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WATUMISHI WANASHIRIKI KATIKA MICHEZO

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifungua tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akito vifaa vya michezo mbalimbali wakatimwa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma.
Venance Mwamoto Mbunge wa Kilolo ni akiendelea na mazoezi kabla ya ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma wakati timu ya Bunge akijiandaa na mchezo dhidi ya watumishi wa umma leo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Katibu Mkuu Wazara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Naibu Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainabu Chaula.
Watumishi wa Umma waliendelea na mazoezi mbalimbali leo uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza. 
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)


Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Waajiri wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa kuhakikisha watumishi wanashiriki katika michezo na kufanya mazoezi maeneo yao ya kazi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza leo wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza linalofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa. 

“Mnaweza kuanzisha timu mbalimbali za michezo na kutenga siku maalum katika mwezi kwa ajili ya mabonanza ya michezo kwa kuweka mazingira rafiki ya kufanyia mazoezi kazini kwa kununua vifaa na kutenga vyumba vya mazoezi. Hii itaimarisha afya za watumishi na kupunguza gharama za matibabu katika taasisi husika.” Naibu Waziri Juliana Shonza.

Naibu Waziri Shonza amesema kuwa tamasha hilo linalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo mbalimbali na mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini. 

Magonjwa yasioyoambukiza hutokana na mitindo isiyofaa ya maisha kama matumizi ya tumbaku, lishe duni, matumizi ya pombe kupita kiasi, pamoja na kutoshughulisha mwili au kutofanya mazoezi ya viungo mara kwa mara. 

Magonjwa hayo ni kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na mishipa, saratani, pumu na magonjwa ya akili ambayo yamekuwa sugu na yana gharama kubwa za matibabu ambapo amesema kuwa watu wengi hufikiria mazoezi ni lazima ukimbie au ucheze mpira, la hasha. Mazoezi ni jambo lolote linalohusisha misuli na kusababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kasi ya kupumua. 

Wataalam wa afya wanasema kuwa kiwango cha mazoezi kinacholeta faida ni mazoezi yasiyopungua dakika 30 kwa siku angalau siku tatu kwa wiki na yanayomfanya mtu kutokwa na jasho. 

Aidha, Naibu Waziri amesisitiza kuwa kupitia tamasha hilo, ufanyike uhamasishaji wa watu kupima afya hususani wa magonjwa yasiyoambukiza. Tiba ya mapema inapunguza uwezekano wa kupatwa na madhara zaidi. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewakaribisha washiriki wa tamasha hilo mkoani Dodoma ambalo limeshirikisha washiriki kutoka ndani na nje ya mkoa huo na hata nje ya nchi.

Odunga amewataka wakazi na wananchi wa mkoa wa Dodoma kutumia fursa ya tamasha hilo kwa kushiriki michezo mbalimbali hatua ambayo itwasaidia watu na jamii nzima kuweka afya zao katika hali bora ambayo inawatenga na magonjwa yasiyoambukiza. 

Tamasha hilo ni la wiki moja ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma, pamoja na Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo limeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, kikapu pamoja mchezo wa kuvuta kamba. Tamasha hilo linaongozwa na kauli mbiu yetu ya mwaka huu; “Tutembee Pamoja Katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza”

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MHE.MPINA ATENGUA UTEUZI WA KAIMU MENEJA MKUU NARCO

WAZIRI LUKUVI AWATAKA WAFUGAJI KUWEKA UZIO ILI KUEPUSHA MIGOGORO NA WAKULIMA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza wafugaji wote wanaomiliki maeneo yenye hati kuweka uzio katika maeneo yao ili kuepuka mifugo yao kwenda maeneo ya wakulima na kusisitiza kufanyika ufugaji wa kisasa.

Lukuvi alitoa agizo hilo wilayani Kilosa mkoani Morogoro wakati akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kilosa na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara ya kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kilosa pamoja na Watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani Morogoro.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ameomba kufanyika ukaguzi wa ardhi za vijiji kwa kuwa baadhi yake watu wamejimilikisha, wameuza na mengine kufanyika mgawanyo usio sahihi.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema vijijji viwili vilivyosajiliwa katika maeneo ya hifadhi wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro vitaendelea kubaki katika maeneo hayo kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia vijiji 920 vilivyokuwa katika maeneo ya hifadhi kuendelea kubaki maeneo hayo.

Lukuvi amevitaja vijiji vya Mjambaa kilichoko katika shamba la Mbugani Estates lenye ukubwa wa ekari 1600 na kile cha Mambegwa kuwa vitaendelea kutambuliwa na kuagiza halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwenda kuvipima na kuanisha shughuli za kilimo na makazi katika vijiji hivyo
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images