Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA UNHCR KANDA YA MASHARIKI, MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (UNHCR), Kanda ya Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu,  Clementine Nkweta-Salami (kulia). Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Naibu Waziri, jijini Dodoma, leo. Wapili kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo Nchini, Chansa Kapaya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (UNHCR), Kanda ya Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu,  Clementine Nkweta-Salami, alipokuwa anamfafanulia jambo katika mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dodoma, leo. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo Nchini, Chansa Kapaya. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (UNHCR), Kanda ya Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu,  Clementine Nkweta-Salami, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisi za Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma. 

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (UNHCR), Kanda ya Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu, Clementine Nkweta-Salami, na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Shirika hilo. 

Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Mhandisi Masauni, jijini Dodoma, leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano hasa katika kuhakikisha wakimbizi wanalindwa na kuhudumiwa ipasavyo. 

Naibu Waziri Masauni alimuhakikishia Mkurugenzi huyo Tanzania itaendelea kulinda haki za wakimbizi kama ilivyokuwa kwa miaka mingi, na pia inasimamia zoezi la kuwarejesha kwa hiari nchini kwao Wakimbizi kutoka Burundi. 

“Nikuhakikishie tu, Serikali ya Tanzania inawajali wakimbizi, ndio maana kwa miaka mingi inaendelea kuwahifadhi, hivyo katika kipindi hiki cha kuwarejesha nchini kwao tunahakikisha wanarudishwa wakimbizi wote kwa hiari,” alisema Masauni. 

Aidha, Masauni alisema mazungumzo zaidi kuhusu wakimbizi waliopo nchini yatajadiliwa zaidi na kukubaliana katika mkutano wa pande tatu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. 

Naibu Waziri alimshukuru Mkurugenzi huyo ambaye aliambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Chansa Kapaya.

GESI TULIYONAYO LAZIMA ITUMIKE KUJENGA UCHUMI WA VIWANDA – DKT KALEMANI

$
0
0
Veronica Simba – Dodoma

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema mpango wa serikali wa miaka 30 wa matumizi sahihi ya rasilimali za gesi na mafuta, pamoja na mambo mengine, umelenga kuhakikisha gesi inatumika kujenga uchumi wa viwanda.

Akizungumza katika ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji, Novemba 6, mwaka huu jijini Dodoma, Dkt Kalemani alisema kiasi cha gesi futi za ujazo trilioni 57.54 ambazo zimeshagunduliwa hadi sasa nchini, zimepangiwa matumizi mbalimbali yanayolenga kufanikisha azma hiyo.

Akitoa takwimu, alibainisha kuwa, gesi futi za ujazo trilioni 5.64 zimetengwa kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya mbolea na ‘petrochemicals’ pamoja na kuunganishia wananchi majumbani kwa matumizi ya kupikia.

“Kazi hizo zimeanza ambapo tayari mabomba manne ya gesi yamejengwa Dar es Salaam na hadi sasa zaidi ya wananchi 500 wameshaunganishwa,” alieleza.

Aidha, alisema kuwa gesi futi za ujazo trilioni 1.1 ni kwa ajili ya kuunganisha katika magari ambapo alibainisha kuwa zaidi ya magari 320 nchini, yameshaunganishwa na zoezi linaendelea.

Kuhusu matumizi ya gesi katika kuzalisha umeme, Waziri alieleza kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya gesi inayotumika nchini hivi sasa ni katika kuzalisha umeme. “Zaidi ya asilimia 56 ya umeme tunaopata unatokana na rasilimali ya gesi.”

Akifafanua zaidi, alisema sekta ya gesi inaendelea kukua hapa nchini ambapo mahitaji kwa sasa yamefikia kiasi cha futi za ujazo milioni 190 kutoka milioni 175 ya mwaka 2015.

Alisema, watanzania wana haki ya kujivunia kukua kwa sekta husika kwani gesi ilipovumbuliwa kwa mara ya kwanza nchini, mwaka 1972 hadi 1082 huko SongoSongo na Mnazi Bay, ilikuwa futi za ujazo mbili tu na sasa imefikia futi za ujazo trilioni 57.54.

Katika hatua nyingine, Waziri alizungumzia suala la ushirikishwaji wazawa katika sekta husika ambapo alieleza kuwa Sheria ya Mwaka 2015 imeweka ukomo wa watanzania kushirikishwa kwa asilimia zisizopungua 25 katika uwekezaji, usimamizi na biashara ya mafuta na gesi nchini.

“Hata hivyo, sharia pekee haitoshi, ndiyo maana serikali ikaweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha utekelezaji wake ikiwemo kuunda timu ya uratibu, serikali yenyewe kufuatilia ili kujiridhisha na pia kuna kanzidata maalumu kwa ajili ya kuwatambua wawekezaji wazawa katika sekta husika.”

Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa washiriki wa Jukwaa hilo, kuhusu fidia kwa waliopisha mradi wa kuchakata gesi eneo la Likong’o, Kilwa Masoko; Waziri alisema kiasi cha shilingi bilioni 56 za Tanzania zimetengwa na kwamba zoezi la uhakiki likikamilika, wote wanaostahili watalipwa.

Jukwaa hilo lilifanyika chini ya uratibu wa Taasisi ya kiraia ya Haki Rasilimali na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya uziduaji wakiwemo viongozi wa serikali, wabunge na wajasiriamali.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akielezea mafanikio ya sekta ya nishati, wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji, lililofanyika Novemba 6, 2019 jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa pili-kushoto), akishiriki katika Jukwaa la Tisa la Uziduaji lililofanyika Novemba 6, 2019 jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na kulia ni waratibu wa Jukwaa hilo kutoka Taasisi ya Haki Rasilimali.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati-waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za kiraia walioshiriki Jukwaa la Tisa la Uziduaji, Novemba 6, 2019 jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati-waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge walioshiriki Jukwaa la Tisa la Uziduaji, Novemba 6, 2019 jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Sehemu ya umati wa washiriki wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa Jukwaa hilo, Novemba 6, 2019 jijini Dodoma.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINAADAMU IKULU ZANZIBAR LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadam na Watu.Mhe.Jaji Sylvain Ore, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Ujjumbe wake leo 7-11-2019.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza mgeni wake (kulia) Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu.Mhe. Jaji Sylvain Ore, akiwa na Ujumbe wake wa Majaji, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 7-11-2019.(Picha na Ikulu)

DC NDEJEMBI AGAWA MICHE LAKI NNE YA KOROSHO KWA WAKULIMA

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhe Deo Ndejembi amegawa mbegu za Korosho kiasi cha tani tatu kwa wakulima ikiwa ni jitihada ya kukuza zao hilo wilayani humo.

DC Ndejembi amesema wamegawa mbegu hizo baada ya kukaa kikao kikubwa ambapo waliazimia kuanza kilimo cha korosho ndani ya Wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wa kukuza uchumi wa wananchi na Serikali ndani ya Halmashauri yao.

Amesema mbegu hizo ziliagizwa na Mkurugenzi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mhe Job Ndugai ambapo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuondokana na kilimo cha mazoea na kujikita sasa katika kufanya kilimo chenye tija na maendeleo.

" Tunatambua Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, na sisi Kongww tumedhamiria kwa dhati kabisa kupiga hatua kubwa kupitia zao hili la korosho. Tumefanya utafiti na kugundua ardhi yetu ni rafiki kwa zao hili hivyo hatuna budi kuchangamkia fursa hii.

Lengo kubwa ni kuwainua wananchi wetu kiuchumi na kupitia kampeni yetu ya Ondoa Njaa Kongwa (ONJAKO) tumeamua sasa kuongeza zao la korosho na kila kaya itabidi ilime ekari mbili," Amesema DC Ndejembi.

Jumla ya miche za korosho zinazohitajika ni miche Milioni mbili na laki mbili lakini kiasi walichoamua kuanza nacho kwa kugawa ni miche Laki nne ambapo kila kaya itaanza kupanda ambapo baada ya wiki nne watagawa tena miche Laki nne.

DC Ndejembi amesema wao kama Wilaya wamedhamiria kuhama kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kwenda kwenye kilimo cha biashara ili kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kunyanyua uchumi nchini na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

" Rais wetu anahimiza sana katika kukuza uchumi kupitia viwanda hivyo ni lazima sisi wasaidizi wake kuwahamasisha wananchi wetu kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kwenda kwenye biashara maana viwanda hivi ambavyo Serikali ya Dk Magufuli inajenga vitahitaji malighafi ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na kilimo.

Hivyo sisi kama Kongwa tumeona njia pekee ya kufanikisha hilo ni kuwafanya wananchi wetu walime kwa wingi korosho kwa sababu licha ya wao kufaidika kiuchumi lakini pia watakuza mapato kwa serikali," Amesema DC Ndejembi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akigawa miche ya korosho kwa wananchi wa Wilaya hiyo. DC Ndejembi amesema lengo lao ni kufanya kilimo cha kibiashara.

CHINA GIFTS EAC 12 CARS WORTH US$400,000 FOR CAPACITY BUILDING PROGRAMMES

$
0
0
 The People’s Republic of China has made a commitment to give the East African Community 12 cars worth US$400,000 to be used in various capacity building programmes at the Community.
Making the announcement, Mr. Liang Lin, the Political Counselor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, Tanzania, said that China was keen on working with the EAC in, among other fields, education, infrastructure development, trade, prevention of Ebola, peace and security, and capacity building initiatives.
Mr. Lin, who paid a courtesy call on the EAC Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko, at the EAC Headquaters in Arusha, Tanzania, disclosed that China was working on infrastructure projects that would promote connectivity across the entire African continent including road and railway networks, adding that other areas were developing hydropower, power transmission and expansion of seaports.
The Chinese envoy further said that China would also assist in building industrial parks in the EAC Partner States, and is looking forward to more discussions on the EAC initiative on Bamboo farming in the region.
He revealed that plans were underway to implement infrastructure development projects worth US$16 billion to be implemented over a three period on the entire African continent courtesy of the 2018 Beijing Summit of the Forum on China-Africa Cooperation.
On capacity building, Mr. Lin said China would be providing 50,000 scholarships to African countries and urged EAC to tap into these study opportunities.
Mr. Lin, who represented the Chinese Ambassador to Tanzania and the EAC, further presented a donation of US$200,000 from China’s Ministry of Foreign Affairs to the Secretary General, which monies will go towards capacity building programmes in the EAC.

On his part, EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko expressed his appreciation to the People’s Republic of China for its generous donation towards the Community’s capacity building programmes.
Amb. Mfumukeko informed Mr. Lin that the EAC integration process was well on course with consistent implementation of the EAC Customs Union, Common Market and Monetary Union Protocols.

Amb. Mfumukeko said that EAC Partner States had agreed to harmonise cross-border rules and procedures and to open their borders thereby increasing intra-regional trade.

On the free movement of persons, the SG said that there were no visa fee requirements for East Africans traveling across the region with some Partner States allowing the use of national identity cards as traveling documents, adding that the countries were issuing the International East African e-Passport which enables travel within the region and beyond.

On infrastructure development, the SG informed the Chinese envoy that the EAC Partner States were jointly implementing regional infrastructure projects that had been agreed upon by the biennial infrastructure development retreats by the Summit of EAC Heads of State.

He urged China to upscale multilateral financing for development projects in East Africa to complement the current bilateral financing for the same.

On the EAC Political Federation, the SG informed Mr. Lin that the Community’s ultimate goal was to become a Federation and that it would launch the national stakeholders’ consultations on the Draft Constitution for the EAC Political Confederation before the end of the month, adding that Partner States had provided a budget for the process.

Amb. Mfumukeko said that each EAC Partner State had nominated two Constitution Making Experts and one Legal Draftsman to assist in drafting a basic law for the proposed Political Confederation which is a transitional model to the Political Federation.

EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (back to camera) in bilateral with Mr. Liang Lin (right) of the Chinese Embassy in Dar es Salaam at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko in discussions with Mr. Liang Lin (centre), the Political Counselor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam who had paid a courtesy call on the Secretary General at the EAC Headquarters in Arusha. On the left is an official at the Embassy’s Political Division.

The Political Counselor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, Mr. Liang Lin, exchanging particulars with the EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko after the two signed the framework agreement under which China has granted EAC US$200,000 to support various capacity building programmes.

EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko bids farewell to Mr. Liang Lin (back to camera) of the Chinese Embassy after they held talks at the EAC Headquarters. Looking on right is Dr. Kamugisha Kazaura, the Director of Infrastructure at the EAC Secretariat.



PROF. KABUDI AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY, FINLAND NA DENMARK

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana ofisini jijini Dar es Salaam. Mawaziri hao wapo Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania katika nchi za Nordic, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Sa



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Denmark, Finaland na Norway ambao wamekuja nchini kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamezungumzia na kukubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kirafiki na kihistoria yaliyopo baina ya nchi hizo.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amezieleza nchi hizo kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania katika kujiimarisha kiuchumi kupitia ukusanyaji wa mapato ya ndani ili iendelee kutoa elimu bure na bora kwa watoto wa kitanzania, huduma bora za afya kwa watanzania, kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote na kufikisha huduma za Nishati kwa watanzania wote hasa wa vijijini.

Amesema kwamba Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwa Siasa za maendeleo ili kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa viwanda inafikiwa.

“Tanzania haiangalii Siasa za nguvu, tunaangalia Siasa za kuletea wananchi maendeleo, na kwa mpango huo tutaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na kumfanya kila mtanzania kulipa kodi ili tuendelee kutoa elimu bure ya msingi na sekondari kwa watoto wa Kitanzania, kuboresha huduma za afya hadi vijijini, upatikanaji wa maji safi na salama na kuhakikisha huduma za nishati ya umeme zinawafikia watanzania wote hadi wa vijijini,” alisema Prof. Kabudi.

Amewahahakishia mawaziri hapo kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano ya Kimataifa hasa katika suala la wakimbizi na kuwafanya watu wanaokuja kutafuta hifadhi za kisiasa nchini kwetu wana pata hifadhi hizo.

Akizungumza alipokutana na Prof. Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Koffod amemuhakikishia Prof. Kabudi Serikali ya Denmark itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha huduma za jamii kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya na maji salama. 

Pia amesisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono mpango wa utoaji wa elimu ya ufundi nchini na kuwafanya vijana wa kike na wa kiume Nchimbi kushiriki katika harakati za ujenzi wa taifa lao.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto ameahidi nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo ya misitu, utawala bora, ukusanyaji mapato, haki za binadamu na Tehama.Amesema Finland pia itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye Elimu kwakuwa Elimu imekuwa na mchango mkubwa na hivyo kutoa viongozi wa baadae. 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya ya kupambana na rushwa na ufisadi na hivyo kuongeza imani ya Norway kuwezesha zaidi nchini. Aidha, ameahidi kuwa nchi yake itaendeleza Ushirikiano wake na Tanzania.

Prof. Kabudi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Jose Pacheco na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuimaraisha mahusiano baina ya Msumbiji na Tanzania.

Mawaziri hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Mafia katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

$
0
0
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mafia katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya kuhamasisha usajili wa Laini za Simu kwa alama za Vidole katika uwanja wa Kilindoni Wilayani Mafia mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA Thadeo Ringo akizungumza na mwananchi wa Mafia katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Mafia.
Wananchi wakisajili laini za simu kwa alama za vidole.
Mwananchi akisoma kitabu cha muongozo cha TCRA

**********************************

Wakazi wa wilaya ya Mafia na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 17 lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia kufika katika uwanja wa Kilindoni kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.

Mhandisi Odiero amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano..

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Mhandisi Odiero amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwakuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa.Amesema TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.“TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema.Mhandisi Odiero.

Odiero amesema kuwa Kampeni hiyo imeanza kwa Mkoa wa Pwani hivyo wilaya zote zitakuwa.Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Wachinja Nyama Ya Ng'ombe Nzega Watia Mgomo

$
0
0

Na Editha Edward-Tabora 

Umoja wa wachinja nyama ya ng'ombe wa halmashauri ya mji wa Nzega mkoani Tabora wametangaza mgomo usio kuwa na mwisho wa kutokuchinja ng'ombe kutoka na kukithiri kwa uchafu kwenye machinjio wanayoyatumia kuchinja mifugo kwa kile kinachodaiwa kuhofia milipuko ya magonjwa kwa afya za wakazi wa mji wa Nzega na maeneo jirani

Akizungumza Mwenyekiti wa umoja wa wachinja ng'ombe kassimu jumanne amesema kuwa machinjio Hayo yamekithiri kwa uchafu uliomo kwa ndani ambao unaweza sababisha magonjwa ya mlipuko ambapo amesema kuwa wameamua kusitisha huduma hiyo kwa muda usiojilikana hadi pale watakapopata ufumbuzi wa machinjio hiyo itakapopata maji na kufanyiwa usafi

"Nafikiri hatuwezi kuendelea kufanya kazi hii kwani mazingira siye wenyewe tunayaona Siyo salama hatutaki kusubiri hadi machinjio haya yafungwe na maafisa afya sisi kweli ni wafanyabiashara na kweli tunatafuta pesa lakini kwa mazingira haya Siyo rafiki ni hatari kwa afya za kibinaadamu"Amesema Jumanne

Nae mmoja wa wafanyabiashara wa ng'ombe Hamis Bakary amesema kuwa ng'ombe zinazochinjwa katika machinjio Hayo ni zaidi ya ng'ombe  thelathini kwa siku ambazo zinasambazwa kwaji Mzima wa Nzega lakini kinachoshangaza ni ukosefu wa maji katika machinjio Hayo pamoja na ushuru wanaoutoa kila siku kutojulikana unapokwenda

Kwa upande wa Afisa  afya halmashauri ya mji wa Nzega Hiyobo Simba na Mkaguzi wa nyama Kilinga Mbaga wote wamebaini adha hiyo ya kukithiri kwa taka ngumu zinazotishia afya za watumiaji ambapo wameekeza mkakati uliopo ni kuhakikisha usafi unafanyika ma maji yanapatikana kwa wakati. 
Pichani ni Mwenyekiti wa umoja wa wachinja ng'ombe wa halmashauri ya Nzega kassimu Jumanne akizungumzia suala hilo la mgomo wa wachinja ng'ombe.

TWASWIRA KUTOKA MTAANI

$
0
0


 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji wakiwa wamejumuika kujitafutia mahitaji mahitaji yao mbalimbali katika eneo  Stendi ya Daladala Mbezi Luis wilaya ya Ubungo  jijini Dar es Salaam leo, kama waoenkanavyo pichani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

 Wajasiriamali maarufu kama machinga katika eneo la Stendi ya Daladala Mbezi Luis  wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wao kama wanavyo onekana pichani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michizi Tv) T

BENKI YA NMB ILIVYOJIKITA KUSAIDIA NYANJA YA ELIMU MAENEO MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo(kushoto) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha wakati wa hafla ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya shilingi 10 milioni vilivyotolewa na benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo - Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NMB.Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB juzi shuleni kwao.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya  - Simon Chacha akiwa ameketi na wanafunzi  wa shule ya Msingi Minigo juzi (Jumanne) katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya NMB  ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo. Wengine ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi) – Amos Mubusi.

VIONGOZI MKOA WA SINGIDA,WADAU WA MAENDELEO WACHANGIA UJENZI SHULE YA MSINGI MITUNDU B

$
0
0
Shule ya Msingi Mitundu B iliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida ambayo viongozi mbalimbali na wadau wengine wamechangia ujenzi wake. 

Na Dotto Mwaibale, Singida. 

VIONGOZI wa Mkoa wa Singida wamechangia ujenzi wa Shule ya Msingi Mitundu B iliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani humo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ally Minja alisema viongozi hao wamejitokeza na kutoa michango hiyo baada ya shule mama ya Mitundu kuzidiwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaoandikishwa shuleni hapo. 

Mwenyekiti huyo alisema Shule ya Msingi Mitundu B ilitokana na kugawanywa na shule mama ya Mitundu ambayo awali ilikuwa na jumla ya wanafunzi 2566 wavulana wakiwa 1293 na wasichana 1273.

Minja alisema kutokana na msongamano huo wa wanafunzi uongozi wa shule kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Serikali ya Kata ya Mitundu pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu kwa pamoja waliasisi ujenzi wa shule mpya ya Mitundu B kwa lengo la kupunguza msongamano huo. 

Alisema kutokana na juhudi hizo, uongozi wa mkoa uliamua kuunga mkono juhudi hizo, ambapo mkuu wa mkoa huo Dk .Rehema Nchimbi amechangia Sh. 750,000, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa, Mbunge wa Viti Maalumu Martha Mlata wamechangia sh. 2,250,000, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni amechangia Sh. 500,000, pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ambaye ametoa sh.500,000.

Wengine ni Taasisi ya kifedha ya Benki ya NMB ambayo imechangia Sh. 5,000,000, Shirika la TEA (The Employers Association) limechangia Sh. 50,000,000, pamoja na wananchi waliojitokeza kushiriki katika zoezi hilo kwa namna mbalimbali. 

Kwa upande wake Mdau wa Maendeleo wa kata hiyo ya Mitundu Mhandisi wa Ujenzi, Felix Dagaki naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha watoto wanajifunza kwenye mazingira tulivu yeye amechangia mifuko 20 ya saruji na sh.milioni moja huku akiihimiza jamii kujitokeza kuchangia ujenzi wa shule hiyo.

TUNAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE ZAO LA KOROSHO - MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 13 wa shirikisho la wadau wa korosho Afrika (ACA) unaofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam tarehe 7 Novemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 13 wa shirikisho la wadau wa korosho Afrika (ACA) unaofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam tarehe 7 Novemba 2019.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 13 wa shirikisho la wadau wa korosho Afrika (ACA) unaofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam tarehe 7 Novemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika Tasnia ya Korosho nchini Tanzania ili kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo kuwekeana katika viwanda vya korosho.


Katika kipindi kirefu serikali imekuwa ikiuza korosho ghafi jambo ambalo nitapunguza kipato cha wananchi na pato la serikali hivyo kuagiza wafanyabiashara kuwekeza kwenye viwanda vya korosho.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 7 Novemba 2019 wakati akifungua mkutano wa 13 wa shirikisho la wadau wa korosho Afrika (ACA) unaofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.


Waziri Hasunga amesema kuwa kwa sasa uwezo wa ubanguaji wa korosho ghafi nchini ni tani 50,000 ambayo ni sawa na takribani asilimia 20 ya uzalishaji wa korosho ghafi msimu wa 2018/2019. 


Amesema uwezo huo ni mdogo ikilinganishwa na uzalishaji uliopo sasa na hivyo nchi inapoteza fursa ya ajira viwandani hususani kwa wanawake na vijana, kukosa mapato yanayotokana na bidhaa zilizoongezwa thamani kama vile mafuta ya ganda la korosho (Cashewnut Shell Liquid), vyakula vya mifugo na kupanua wigo wa soko la korosho. 


Amesema kwa sasa kuna jumla ya viwanda 25 vya ubanguaji korosho nchini vyenye uwezo wa kubangua tani 78,000 kwa mwaka. Kati ya hivyo, ni viwanda 12 vyenye uwezo wa kubangua tani 24,660 ndivyo vinavyofanya kazi hivyo kuna fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya ubanguaji korosho.


Aidha, Waziri Hasunga amesema kuwa kwa upande wa wabanguaji wadogo wa korosho nchini kupitia umoja wao (UWWKT) wameendelea kuimarisha Umoja wao kwa lengo la kuongeza kiasi cha korosho kinachobanguliwa nchini. 


Mpaka sasa kuna jumla ya vikundi 209 vidogo vya kubangua korosho nchini kutoka Wilaya 14. Katika msimu wa 2018/2019 vikundi hivi vimefanikiwa kubangua korosho tani 78 tu. Ukosefu wa mitaji, mashine za kubangua korosho, na masoko ya uhakika ni baadhi ya changamoto zinazokabiliwa na wabanguaji katika kundi hili.


Kwa ujumla Serikali kupitia Taasisi zake inaendelea kusimamia mikakati iliyopo ya kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi kufikia wastani wa tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2023/2024. 


Mikakati hiyo ni pamoja na kupanda mikorosho mipya 15,000,000 kila mwaka kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2023/2024, kuanzisha mashamba mapya ya kuzalisha mbegu bora za korosho hususani katika maeneo mapya ya kilimo cha korosho, Kutoa elimu ya ugani kwa wakulima juu ya kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu vya zao la korosho na kuhakikisha upatikanaji wa uhakiki na wa bei nafuu wa viuatilifu vya zao la korosho kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyataja maeneo ambayo yapo wazi kwa ajili ya uwekezaji katika Tasnia ya Korosho hapa nchini ni pamoja na; Ubanguaji wa korosho ikiwa ni pamoja na usindikaji wa bidhaa zitokanazo na korosho; Ufunguaji wa mashamba makubwa ya korosho (Cashewnut plantations/Block farming); Usambazaji na uuzaji wa mashine za kubangua korosho; Uwepo wa ardhi ya kutosha iliyotengwa katika mikoa inayozalisha korosho kwa wingi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho; Uwepo wa sera ya viwanda katika ngazi ya Taifa.


Mhe Hasunga amesema kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozalisha korosho ghafi yenye ubora wa hali ya juu. Korosho ya Tanzania inapendwa katika masoko mbalimbali ya Kimataifa kutokana na kuwa na ladha nzuri na ya kuvutia, rangi nyeupe ya asilia ya korosho karanga na ukubwa unaofanana (Uniform size); sifa inayopunguza gharama ya kudarajisha kabla ya kubanguliwa. Pia, faida ya kijiografia (Geographical Advantage) ya kuwahi kwa msimu wa korosho nchini miezi 6 kabla ya nchi nyingine duniani zinazozalisha korosho kwa wingi hazijaingia sokoni.


Sifa hizo pamoja na usimamizi mzuri wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ndio kimsingi imepelekea kuimarika kwa bei ya korosho ghafi za wakulima kutoka mwaka 2007/2008 hadi mwaka 2017/2018, ambapo bei ya korosho ghafi imekuwa ikiongezeka  na kufikia ya juu kuwahi kupatikana ya Shilingi 4,128/= kwa kilo katika msimu wa 2017/2018.


Zao hili huzalishwa kwa wingi hapa nchini kutoka mikoa mitano ambayo ni mikoa ya Kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na mikoa ya Mashariki ambayo ni Pwani na Tanga. Kutokana na faida za kiuchumi zitokanazo na zao la hili, uwepo wa eneo la kutosha kwa kilimo na hali ya hewa maridhawa kwa kilimo cha korosho hapa nchini zao hili kwa sasa linalimwa na zaidi ya mikoa 17 ikiwemo Singida, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Songwe, Njombe, Iringa, Katavi, Tabora, Kigoma, Shinyanga na Kilimanjaro.

WADAU UNGANENI KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MISTU NCHINI - RAS TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imewataka wadau kuunganisha nguvu zao pamoja katika  kukabiliana na uharibifu wa misitu ya miombo ili kulinda uoto wa asili na kuwa na mistu endelevu kwa ajili ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania.

Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali na wadau bado kuna kiwango kikubwa cha uharibifu wa mistu ikiwemo ile ya miombo na kusababisha kuwepo na tisho linaloweza kupelekea upotevu wa uoto wa asili.

Makungu alisema uharibifu wa mistu usipothibitwa utasababisha kuwa na gharama kubwa ya kurejesha uoto wa asili uliopotea na wakati mwingine kusababisha kizazi kijacho kushindwa kupata matunda ya mistu iliyoharibiwa.

Alisema Mradi huu wa Uhifadhi wa Misitu ya miombo katika nyanda kame umekuja wakati muafaka ambapo kila wadau wanatakiwa wajiwekee malengo ya pamoja ili kutekeleza Mkakati wa Kuondoa uharibifu wa ardhi na kukabiliana  mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) nchini Jonathan Sawaya  alisema takwimu zinaonyesha kuwa uharibifu wa mistu hapa nchini ulifikia hekta 469,420 kwa mwaka 2018.

Alisema hali inasababishwa na kuwepo na jitihada kubwa katika kupunguza uharibifu wa mistu na ardhi unaotokana na shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia nchi.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kushoto) akibadilishama mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama(kulia)  leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akifungua leo warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania
Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) Jonathan Sawaya  akitoa maelezo mafupi kuhusu hali ya uharibifu wa mistu leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania. Picha na Tiganya Vincent
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau wa ukanda wa miombo wa Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.

KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA JAJI MSTAAFU DE MELLO, VIONGOZI WENGINE BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Joaquine De Mello alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akisalimiana na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) kabla ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilihusu ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya katibu wa Bunge na MISA TAN, ugeni huo ulioongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania, Ndg. Gasirigwa Sengiyumva (wa pili kulia)

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

NANDY APISHANA NA RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Faustina Mfinanga Maarufu kama Nandy anayetamba na wimbo wake mpya wa Magufuli amepishana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Nandy aliyetakiwa kutumbuiza leo katika ufunguzi wa Mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ameshindwa kufanya hivyo baada ya kuchelewa kufika na kutokuruhusiwa kuingia ndani.

Taarifa zinasema, Nandy alitakuwa kuwasili mapema saa 2 asubuhi kabla Rais hajafika ila alijikuta anafika saa 3 na tayari ufunguzi wa Mkutano huo ukiwa umeanza.

Kutokana na tukio hilo, nenda ambaye alikua ni msanii.pekee aliyetakiwa kutumbuiza kwenye ufunguzi huo ameshindwa baada ya kushindwa kufika kwa muda aliopangiwa.

Nandy amekuwa ni miongoni mwa wasanii waliopata fursa ya kutumbuiza katika mikutano mikumbwa mbalimbali na kibao chake kipya kiitwacho Magufuli

Rais Dkt Magufuli amefungua mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao umeanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania.

BREAKING NYUZZZZ....: Bibi aliyemuua mjuu wake kwa kipigo ahakumiwa kunyongwa hadi kufa

$
0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mwanamke Esther Lyimo (47) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mjukuu wake kwa kipigo.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 8,2019 na Naibu  Msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

taarifa kamili itakufikia hapa hapa hivi punde.

WAHITIMU WA VETA CHANG’OMBE WAASWA KWENDA KUONESHA UJUZI WAO KATIKA SEKTA YA VIWANDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
Wahitimu wa vyuo vya Ufundi Stadi wameaswa kutumis taaluma zao katika kutengeneza ajira kutokana na ujunzi wao kwani serikali iko katika mkakati wa kwenda uchumi wa kati wa viwanda.

Akizungumza na katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Meneja Uajiri wa Kioo Limited Jacob Msuya amesema kuwa wahitimu wana kila sababu ya kwenda kuongeza fursa za ajira kwa kutumia mafunzo walioyapata.

Msuya amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kuwa na ueledi wa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu wa baadhi ya vitu kutokana na taaluma walioipata katika Chuo cha VETA Chang’ombe.

Aidha amesema kuwa wahitimu wa VETA wamekuwa wakifanya vizuri kwani Kioo Limited kimepata kufanya kazi na wahitimu na wengine kuwaajiri katika kiwanda.

“Ninategemea baada ya kutoka hapa watakwenda kuleta matokeo ya taaluma walioipata kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kuwa na cheti kisichokuwa na kazi ilhali kuna watu waliwekeza katika kuhakikisha kijana wao ana ujuzi wa kwenda katika ajira au kujiajiri na kujiletea maendeleo”

Amesema viwanda viko vichache ikilinganishwa na wahitimu katika vyuo mbalimbali  vinaendelea kujengwa kutokana serikali kuwa na mkazo katika sekta ya viwanda hivyo vijana lazima wapambane katika suala la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa.

Nae Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Chang’ombe Vaileth Fumbo amesema wahitumu katika mahafali ya 49 wako 556 ambapo kazi yao kubwa ni kuwenda kutumikia taifa kwa ujunzi waliopata katika kipindi cha miaka miwili.

Amesema kuwa wahitimu waende na mfumo wa kuanzisha kikundi ambapo wanaweza kuanzisha kiwanda na taasisi fedha kuwakopesha katika kiwanda ambacho wamekianzisha.

Fumbo amesema wasibweteke na vyeti  kwani ndio mwanzo kwenda mbali zaidi kwa kuongeza ujuzi katika kutanua uwigo wa ajira au kujiajiri.

Rais wa Serikali ya Wanafuzi wa VETA Chang’ombe Nurdin Chambalini amesema kuwa watanzania wajue kauli ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ya Viwanda hivyo wahitimu wakaendeleze kauli hiyo katika ujenzi wa viwanda.
 Meneja wa Uajiri wa Kioo Limited Jacob Msuya akizungumza na waandishi habari katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe  yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Chang’ombe Vaileth Fumbo akizungumza katika mahafali ya 49 ya chuo kuhusiana na historia ya uzalishaji wa ujuzi wenye mafanikio yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Serikali ya Wanafuzi wa VETA Chang’ombe Nurdin Chambalini akitoa ushauri kwa wahitimu katika kwenda kutekeleza dhana ya Rais Dkt.John Magufuli ya ujenzi wa viwanda.
Wahitimu wakionesha vipaji vyao uimbaji katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa fani ya ubunifu wa mitindo ya nguo wakiimba wimbo wa Taifa mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KATIKA SALA YA IJUMAA KATIKA MSIKITI WA NUNGE, JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza mawaidha, kabla ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Alhaji, Ismail Dawood, baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi, wakati akitoka kwenye Msikiti wa Nunge, Jijini Dodoma, Novemba 8, 2019, baada ya kushiriki sala ya ijumaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC KATIKA UKUMBI WA JNICC JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania katika mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic mara baada ya mkutano huo wa Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Ine Marie Eriksen Soreide kabla ya kuanza mazungumzo katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Ann Linde katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Ine Marie Eriksen Soreide mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa Mawaziri wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa Mawaziri wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Ann Linde mara baada ya kumkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili na Kingereza pamoja na kitabu cha Kiswahili mara baada ya kufungua mkutano wa Nordic uliofanyika  katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya kinyago cha mpingo Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Ine Marie Eriksen Soreide kabla ya kuanza mazungumzo yao katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland  Pekka Haavisto  kabla ya kuanza mazungumzo yao katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC). PICHA NA IKULU

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA USAFIRISHAJI:WAZIRI MHAGAMA

$
0
0
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi.

Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

“Moja ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama

Kutolewa kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.

Alifafanua kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali, wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona namna sheria za kazi  zinavyozingatiwa.

Azimio jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.

“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew  Masawe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1, 2019 Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama na Naibu wake Mhe Antony Mavunde wakishuhudia zoezi la utiaji saini wa maazimio ya kikao cha pamoja kati ya wadau wa sekta ya uchukuzi na Serikali kilichofanyika Novemnba 1, 2019 Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa TABOA Bw. Enea Mrutu akichangia jambo wakati wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.
 Kaimu Kamishana wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Andrew Mwalwisi akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
 Baadhi ya washiriki wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.
 Viongozi wa vyama vya  wa wamiliki wa  vyombo vya usafirishaji  wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).
Viongozi wa vyama vya  wa wamiliki wa  vyombo vya usafirishaji  wakiwa kwenye picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images