Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 320 | 321 | (Page 322) | 323 | 324 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 01/10/14--01:00: SHUKURANI
 • Marehemu Jane Lillian Samatta
  Familia ya Mh. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas A. Samatta inatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine, katika kuwafariji katika msiba wa mpendwa wao, Jane Lilian Samatta, aliyefariki tarehe 09 Disemba, 2013, katika Hospitali ya TMJ hapa Dar Es Salaam.


  Shukrani za kipekee ziwafike wafuatao: Mh. Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman; Mh. Jaji  Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu; Waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu ya rufaa na wa Mahakama kuu; Waheshimiwa Majaji Wastaafu; Mtawala Mkuu wa Mahakama Bw. Hussen Kattanga; Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe; Prof. Mkude, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe; Prof. Joseph Kuzilwa, Makamu Mkuu wa Chuo na Makamu wake, Prof. F. Kamuzora na Prof. J.S. Itika, na jumuia ya chuo Kikuu hicho cha Mzumbe.

  Mh. Makamu Mwenyekiti wa Judges and Magistrates Vetting Board ya Kenya

  Bi. Roseline Odede, Mh. Mjumbe na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Waheshimiwa Justus Munyithya na Reuben Chirchir, pamoja na Viongozi wengine na Watumishi wa Bodi hiyo;

   Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw. Abdo Majd, Viongozi na Watumishi wote; Menejimenti na Watumishi wa Management And Development For Hearth (MDH);

  Walimu na Watumishi wa Shule ya Msingi ya Libermann; Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya TMJ; Dr. Mwandolela, Dr. Paschal na Wauguzi wa Heameda Medical Clinic; Majirani wa Mtaa wa Bongoyo na Mitaa ya jirani; Majirani wa Oyster Bay Neighborhood Association (CONA); Vikundi vya  Green Women na Great Sisters; Wanajumuia wa Jumuia ya Mtakatifu Agostino wa Hippo; Bi. Eliaebeth Mwella; Bw. Aaron Tesha; Bi. Diana Mkapa; Bi. Magdalena Ingi; Bi. Gloria Sindano; Viongozi, Kwaya ya Kanisa na Waumini Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano; Ndugu, Jamaa na Marafiki.

  IBADA YA SHUKRANI

   Itafanyika katika kanisa kuu la mtakatifu Albano jijini Dar es salaam kesho Jumamosi saa 2 asubuhi  tarehe 11 January 2014. 
  MPENDWA WETU JANE, MIKONONI

  MWA MWENYEZI MUNGU PUMZIKA,


  MIOYONI MWETU ISHI DAIMA.


  0 0

  On 18th January Tanzania will have the honour of receiving the Queen’s Baton for the Commonwealth Games- The Baton symbolizes the coming together of all Commonwealth nations and territories in preparation for the four-yearly festival of sport and culture. The Baton is travelling over 190,000 km through 70 Commonwealth countries. Its journey will end on 23 July 2014 in Glasgow, Scotland, for the Opening Ceremony of the XX Commonwealth Games, which Glasgow is hosting.

  You are invited to celebrate the Baton’s arrival in Tanzania and the forthcoming Glasgow Commonwealth Games at a reception hosted by the British High Commissioner at her Residence on Saturday 18th January from 1900-2100 Hrs.

  The themes for the reception include a celebration of the Commonwealth and its values; sport; and young people, in particular, ending violence against children. The evening will feature a strong Scottish flavour to reflect the country that is hosting the 2014 Commonwealth Games. The Baton is being accompanied by a BBC film crew that will record its complete journey and.

  This will be the fifth time Tanzania has received the baton. The baton will be in Tanzania for 3 days, helping to sensitize, unite and raise the morale of the citizens, athletes and especially the young people on what the Commonwealth Games are about.

  The Baton will be presented by Mr Filbert Bayi, the Tanzanian holder of the Commonwealth 1500 metre record for the past 40 years, accompanied by Olympic champion Kipchoge Keino, and the team accompanying the Baton on this leg of its global journey.

  The Queen’s Baton Relay Sunday 19th January

  The relay of the Queen’s Baton through the streets of Dar es Salaam will be on Sunday 19th January starting at 1400 Hrs from the National Stadium and ending at State House where the Baton will be presented to HE President Kikwete.

  All are welcome to come and watch the Baton’s journey along the route. Beforehand, the British Council through its International Inspiration programme and Unicef have organized a morning of sports - athletics, football and netball- at the National Stadium commencing at 0900. Spectators are welcome- just turn up! On Monday 20th beyond.

  the Baton will visit Zanzibar before its onward journey to Seychelles and Further background on the Commonwealth Games can be found at www.glasgow2014.com and www.thecgf.com. The international journey of the Commonwealth Baton can be followed at: http://www.thecgf.com/qbr .

  0 0

   Kikosi kazi cha Golden Bush 
  Kikosi kazi cha Wahenga FC

  Napenda kutoa taarifa kwamba ule mpambano wa marudiano kati ya Golden Bush na Wahenga utapigwa katika uwanja wa TP pale Tandale siku ya kesho kuanzia saa kumi na nusu juu ya alarma. mechi hii ni ya maduriano baada ya ile ya kwanza kushuhudia Golden Bush wakilambishwa mchanga na kukubali kipigo cha goli 1-0. 

  Kwa katambua umuhimu wa game hii ya watani wa jadi, tumelazimika kumtafuta refa aliyeobobea katika shughuli za uamuzi wa mpira Tanzania bwana Othmani Kazi ambaye atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na waamuzi wasaidizi watatu. tumelazimika kuwa na waamuzi wa kutosha kama sharia za FIFA zinavyotaka.


  Kwa maandalizi tuliyofanya Golden Bush, na kwa kutambua uwezo wa wapinzani wetu, nathubutu kusema kwamba game yako ya kesho huenda tutavunja record tuliyoweka mwaka jana ya kuwafunga goli 4. target yetu ni kufunga goli 3 kila kipindi. tunaweka Malengo hayo kwasababu kesho timu yetu itakuwa sawasawa, wachezaji wetu wote wapo na wako tayari kupiga soka la kufa mtu.

  Ni mechi itakayosheheni ufundi, utaalam na mambo ya jadi kwa mbali kidogo ili kuhanikiza ile football ya kiafrika.

  Karibuni sana mashabiki ili mje mpate burudani iliyotoka darasani.

  Asanteni kwa Kunisikiliza.

  Onesmo Waziri "Msemaji wa Golden Bush Veterans"

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara yake katika shamba la Mkulazi lililopo katika kata ya Mkulazi mkoani Morogoro Alhamis wiki hii. Wengine ni Meneja Kitengo cha Ardhi kutoka Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bw. Desiderius Narwango (kushoto) Mkurugenzi wa Huduma wa TIC, Bi. Nakuala Senzia (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro vijijini, Bw. Said Amanzi (wa pili kushoto).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja Kitengo cha Ardhi kutoka Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Bw. Desiderius Narwango (kushoto) wakati wa ziara katika shamba la Mkulazi lililopo katika kata ya Mkulazi mkoani Morogoro Alhamis wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma wa TIC, Bi. Nakuala Senzia na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro vijijini, Bw. Said Amanzi (wa pili kushoto).


  0 0


  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kujaa maji eneo kati  ya stesheni za Godegode na Gulwe mkoani Dodoma na kuharibu tuta la reli,  unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya usafiri wa abiria kuanzia leo Ijumaa Januari 10, 2014 hadi itakapotangazwa tena.
  Wasafiri wote wenye tiketi halali wafike katika stesheni walizokatia tiketi hizo kwa ajili ya kurejeshewa fedha  kuanzia leo!

  Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.

  TRL Makao Makuu,

  Dar es Salaam.

  Januari 10, 2014


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wasanii wa asili na vikundi vya ngoma wakati Fensi katika barabara ya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wengine waliokaa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
  Wasanii wa fensi ambao hujipaka mafuta machafu (mobile) wakiwa na mishale wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbnali na wananchi waliohudhuria kuangalia fensi hiyo iliyoshirikisha kazi za taasisi za Serikali na Binafsi,katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wasanii wakionesha namna ya tiba za asili kwa njia ya kupandisha mizuka ikiwemo ngoma za pungwa, wakati wa Fensi iliyopita katika barabara ya Kibandamaiti,Wilaya ya Mjini jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Ngoma ya ndege ni miongoni mwa burudani za asili katika fensi zilizopita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiangalia Fensi iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Ngoma ya Beni (Mbwa kachoka) ikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Aina mabali mbali za miti ya asili ikiwemo katika fensi, iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Kazi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zikioneshwa kwa wananchi mbali mbali waliofika kuangalia fensi katika barabara ya Kibandamaiti jana ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na wadau mbali mbali wa maendeleo wakati ziara yake ya kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Wa tatu kushoto ni Diwani wa kata hiyo,Edward Lenanuu.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu mhandisi wa maji wa wilaya ya Monduli,Bw. Wasiwasi Mgala (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Katikati mwenye shati jekundu ni mwenyekiti wa CCM Monduli,Ruben Kunayi.

  0 0

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Mb akiwa na mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania anayemaliza muda wake Bwana Abeeric Kacou (kushoto) mara baada ya Mwakilishi Mkazi huyo kufika Ofisini kwa Spika leo kwa nia ya kumuaga.
  “Kwaheri na asante kwa kazi nzuri na karibu tena Tanzania ”…. Ndivyo Spika anavyomwambia Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bwana Kacou baada ya kumaliza miaka minne ya utumishi hapa nchini Tanzania.
  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda, Mb, akimkaribisha Balozi mpya wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) ofisi kwake leo ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kuendeleza ushirikiano wanchi mbili hizi. Picha na Owen Mwandumbya - Bunge.

  0 0

  Na Athumani Shariff

  Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe leo amekutana na balozi wa Ubelgiji Koen Adam makao makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya maji.

  Profesa Maghembe alimuomba Balozi Adam asaidie wilaya ambazo zinakabiliwa na matatizo makubwa ya uhaba wa maji, ambazo aliziainisha kuwa ni Makambako, Songea, Wanging’ombe na Makonde ambapo jumla ya Dola 20,000,000 za Marekani zinahitajika kutatua shida hizo.

  Wakati wa mazungumzo hayo, Profesa Maghembe alisema wananchi haswa waishio vijijini wanapata tabu sana kutokana na shida ya maji. “Wananchi wanapata tabu sana kupata maji, inawagharimu kati ya saa moja hadi mbili kuchota ndoo moja ya lita ishirini, hivyo ili kukamilisha mahitaji ya matumizi ni wazi kuwa muda mwingi utatumika na hatimaye kuzorotesha shughuli nyingine za uzalishaji”. Alisema Waziri Maghembe.

  Akijibu swali la Balozi Adam juu ya maswala ya umeme, Profesa Maghemebe alisema hiyo ni changamoto kubwa sana kote mijini na vijijini. Gharama za Tanesco na zile za Diseli zipo juu. Alisema tayari amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamaba na baadhi ya wataalamu kutoka wizarani kwenda nchi za Uchina na Jamhuri ya Watu wa Czech kutafuta kampuni zinazojishughulisha na umeme wa nguvu ya jua (Solar Power) ili miradi yote ya maji vijijini itumie umeme wa jua ili kuwapunguzia gharama za maji wananchi na hiyo kuifanya kuwa ndiyo sheria.

  Waziri pia alieleza umuhimu wa upatikanaji wa maji safi katika kukabiliana na afya bora kwa wananchi. Alisema, baada ya kuanza kutumika mradi mkubwa wa maji wa Kahama Shinyanga sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu hawendi hospitali juu ya magonjwa mbalimbali yaliyokuwa yanawasumbua awali. Hivyo maji yanamchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi alisisita Profesa Maghembe.

  Pia alisema kwa kuwapatia wananchi huduma ya maji safi karibu na makazi yao ni njia kubwa kutika kuwainua kiuchumi, kwani muda mwingi ambao wangeutumia katika kutafuta maji watafanya shughuli nyingine za kiuchumi, hivyo kupandisha kipato chao.

  Akielezea maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji, Profesa Maghemebe alisema ni moja ya changamoto tunazokabiliananazo, maji hupungua ingawa mahitaji yawatu huongezeka hivyo jitihada zetu kubwa sasa kwakupitia Idara ya Rasilimali za maji ni kutunza vyanzo vya maji ili haya yaliopo sasa yaendeleee kuwepo kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

  0 0
 • 01/10/14--04:34: RAHA YA DEMOKRASIA YA KWELI
 • Rais Barack Obama akiwa na Marais wastaafu wa Marekani waliomtangulia. Toka Kulia ni George W. Bush, Bill Clinton na Jimmy Carter. Nchi chache duniani zinaweza kupata taswira ya namna hii kama ilivyo kwa Marekani na Tanzania. Picha kwa hisani ya White House.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo shuleni hapo.


  0 0

  washiriki wa mafunzo ya namna ya kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, wakati wa kufuata mafunzo ya kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia na watoto, yaliyofanyika mkoani Morogoro, mafunzo hayo yaliwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji mkoa wa Morogoro.( Picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi).

  Na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi

  Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amewataka wananchi kote nchini, kutofumbia macho vitendo vya ukatili na unyanyasaji ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii yetu huku vikiathiri idadi kubwa ya wanawake na watoto.

  Kauli hiyo ameitoa jana wakati akifunga semina ya mafunzo kwa askari Polisi ya namana ya kutambua viashiria vya makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto, mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa siku tano katika mkoa wa Morogoro, huku yakiwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji wa mafunzo hayo mkoa wa Morogoro.

  Hata hivyo, Kamishna Chialo, alisema kuwa, lengo la mafunzo haya kwa askari na maofisa wa Jeshi la Polisi, ni kuwajengea uwezo katika kutoa huduma bora katika kazi za dawati la jinsia na watoto, ikiwa pamoja na kufahamu mbinu mbalimbali za kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia huku wakitambua kuwa suala la utoaji wa huduma bora kwa mteja si hiari bali ni lazima.

  Naye kwa upande wake mwakilishi wa Kituo cha Sheria ( legal Sector) waliofadhili mafunzo hayo, Bi. Wanyenda, alisema  kuwa, Jeshi la Polisi linamchango mkubwa katika kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia na hivyo kutokana na mafunzo haya yatawasaidia askari katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitendeka katika jamii.

  Bi. Wanyenda, aliongeza kuwa, ni vyema askari waliopatiwa mafunzo haya wakaitumia  fursa hii waliyoipata kuweza kutoa elimu kwa askari ambao hawakuweza kushiriki katika mafunzo haya kwa lengo la kuwajengea uwezo na namna ya kutambua viashiria vya makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.

  Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya washiriki wenzake, Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Letea Mofuga, alisema kuwa, mafunzo waliyopatiwa yamewasaidia kutambua na kubaini viashiria pamoja na dalili za mtu aliyefanyiwa ukatili na hivyo kuahidi kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo waliojifunza.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Kichina ya China Merchant Holdings International (CMHI) Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 10, 2013. Kushoto kwake ni Kiongozi wa Ujumbe huo , Hu Jianhua na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Mary Nagu. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Kampuni ya kichina ya China Merchant Holdings International (CMHI), Bw. Hu Jianhua kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam Januari 10, 2014. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga kampuni mpya ya Bagamoyo. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Baadhi ya wanafunzi wa halaiki wa skuli mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara wakijiandaa kwa ajili ya sherehe za mapinduzi ifikapo Januari 12 mwaka huu wa 2014.
  Gari za Polisi zinazotumika wakati wa fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali nchini zikiwa katika matayarisho ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakazofanyika huko uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
  vijeba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } wakionyesha umwamba wao wakati wa matayarisho ya mwisho ya maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Kifaru cha kivita cha JWTZ kikifanya matayarisho ya mwisho kwa ajili ya maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika uwanjani hapo Jumapili ya Januari 12 mwaka 2014.
  Askari wastaafu wa Jeshi la Ukombozi la Unguja { JLU } ambalo linatarajiwa kuonyesha vitu vyao wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { jwtz } wakionyesha ustadi wao wakati wa mazoezi ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia nusu karne ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma .

  Kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma, nyumba 127 zimebomolewa na mafuriko ambapo watu 493 wamekosa makazi ya kuishi, pia nyumba 240 zimezingirwa na maji katika Kijiji cha Chipogolo Kata ya Chipogolo Tarafa ya Rudi Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na kusababisha jumla ya wakazi 1390 kukosa makazi ya kuishi.

  Akiongea na wakazi wa Kijiji hicho Naibu Waziri wa Nishati na madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa Mh. George Boniface SimbaChawene amesema katika kikao cha tathmini kilichofanyika mara baada ya kukagua eneo lililoathilika na mafuriko wamekubaliana kuwa hatua mbalimbali zichukuliwe ikiwemo kujenga upya madaraja yaliyopo pamoja na kuongeza kimo na urefu wa madaraja hayo kwa kuwa madaraja yaliyopo ni mafupi na yanazidiwa na maji jambo ambalo linapelekea maji hayo kushindwa kupita kwenye madaraja hayo na kuelekea kwenye makazi ya watu.

  Pia Mbunge huyo ameiomba kamati ya maafa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba wakazi wa kijiji hicho wanapata huduma mbalimbali zikiwemo za Afya kwa kuwapa madawa, elimu pamoja na kuwaongezea wataalamu wa afya, kuwapatia Mahema, mablaketi na magodoro na chakula.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Christopher Ryoba Kangoye amewaomba wakazi wa kijiji hicho kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu wakati serikali kupitia kamati ya maafa Mkoa wa Dodoma ikiendelea kushughulikias matatizo yao.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime amewataadharisha wakazi wa kijiji hicho kuwa watulivu kwani matatizo kama haya hayatatuliwi kwa vurugu badala yake watumie vikao vinavyostahili kutatua matatizo yao “matatizo kama haya hayatatuliwi kwa kufanya fujo na kufunga barabara”

  Wakati huohuo Kituo cha Polisi Kata ya Chipogolo na nyumba tano za Askari wa kituo hicho zimeanguka kutokana na mafuriko hayo, Kamanda Misime ametoa pole kwa Askari wa kituo hicho na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa maadili ya Jeshi bila kujali wakati tatizo lao linashughulikiwa na mamlaka husika kwani vituo vya Polisi kama hivyo vipo chini ya Mkurugenzi na wananchi kwakuwa vilijengwa kwa nguvu zao.
  Hii ni moja kati ya nyumba za polisi ambazo zimeharibiwa na mafuriko.
  Hili ni eneo lililokumbwa na mafuriko hayo.


  0 0

  Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
  Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani.


  0 0

   PHOTOGRAPHER AND PUBLISHER JAVED JAFFERJI SHOWING COFFEE TABLE BOOK, ZANZIBAR PHOTOGRAPHIC JOURNEY - 50 YEARS OF REVOLUTION  TO FORMER PRESIDENT OF ZANZIBAR DR ABEID AMANI KARUME IN HIS OFFICE WHICH HE DID FOREWORD FOR THE BOOK. 
  THE BOOK WILL BE LAUNCHED OFFICIALLY WITH A PHOTOGRAPHIC EXHIBITION  AT THE PEACE MEMORIAL MUSEUM IN ZANZIBAR.


  0 0

  Ilikuwa inaongozwa na Super woman Joyce Kiria, safari hii inarudi ikiwa na watangazaji wapya kabisa. Je, unawafahamu? Usikose kuiona studio mpya full red carpert. Kauli mbiu ya msimu mpya ni WASANII TUWE MIFANO BORA KATIKA JAMII.
   Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kutazama luninga yako kupitia kituo bora cha vijana Ting'a namba moja EATV hivi karibuni Bongo Movies inatua tena. 
  Yes, ni very SOON! Tuwe pamoja katika kuhakikisha tunanyanyua na kuendeleza tasnia ya sanaa na wasanii hapa nchini. Bongo Movies, inachonga barabara, wengine wanafuata!
   Msanii Pastor Myamba akiwa na crew ya Bongo Movies wakionesha alama ya 5 kama ishara ya kutua EATV hivi karibuni.
   Msanii anayefanana na marehemu Kanumba Lutazwa akiwa na crew ya Bongo Movies
  Lutazwa, Selina na Hagai


  0 0

  Wateja wa Vodacom sasa kufurahia Dabo Dabo kwa kupata dk. 40 za muda wa maongezi wikiendi hii na hiyo yote ni kutokana na kuzinduliwa kwa promosheni ya vifurushi vya wiki.

  Akizungumzia juu ya promosheni hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa amesema, “wateja wetu watapata muda wa maongezi wad k 40 kupiga ndani ya mtandao na pia wataweza kupata sms 250 na vilevlie vifurushi vya intaneti yenye kasi ya MB 100 wikiendi nzima”.

  “Promosheni hii iliyopewa jina la Dabodabo itafikia kikomo wikiendi hii ya Januari 12, hivyo nawataka wateja wetu waitumie ipasavyo kwa kuwasiliana na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wapendwa wao.” Alisema Twisa na kuongeza

  “Mbali na hayo ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa miaka mingi sasa, na hicho ndicho kilichotupelekea kuwaletea promosheni hii kama ishara ya shukrani zetu kwao. Zaidi ya hapo kuna ofa, huduma na bidhaa kemkem zipo njiani zinakuja kwa ajili yao.” Alisema

  Ili kujiunga na promosheni hiyo mteja anatakiwa kupiga *149*01# au *147*500#

older | 1 | .... | 320 | 321 | (Page 322) | 323 | 324 | .... | 3278 | newer