Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

DC NDEJEMBI AGAWA MICHE LAKI NNE YA KOROSHO KWA WAKULIMA

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhe Deo Ndejembi amegawa mbegu za Korosho kiasi cha tani tatu kwa wakulima ikiwa ni jitihada ya kukuza zao hilo wilayani humo.

DC Ndejembi amesema wamegawa mbegu hizo baada ya kukaa kikao kikubwa ambapo waliazimia kuanza kilimo cha korosho ndani ya Wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wa kukuza uchumi wa wananchi na Serikali ndani ya Halmashauri yao.

Amesema mbegu hizo ziliagizwa na Mkurugenzi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mhe Job Ndugai ambapo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuondokana na kilimo cha mazoea na kujikita sasa katika kufanya kilimo chenye tija na maendeleo.

" Tunatambua Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, na sisi Kongww tumedhamiria kwa dhati kabisa kupiga hatua kubwa kupitia zao hili la korosho. Tumefanya utafiti na kugundua ardhi yetu ni rafiki kwa zao hili hivyo hatuna budi kuchangamkia fursa hii.

Lengo kubwa ni kuwainua wananchi wetu kiuchumi na kupitia kampeni yetu ya Ondoa Njaa Kongwa (ONJAKO) tumeamua sasa kuongeza zao la korosho na kila kaya itabidi ilime ekari mbili," Amesema DC Ndejembi.

Jumla ya miche za korosho zinazohitajika ni miche Milioni mbili na laki mbili lakini kiasi walichoamua kuanza nacho kwa kugawa ni miche Laki nne ambapo kila kaya itaanza kupanda ambapo baada ya wiki nne watagawa tena miche Laki nne.

DC Ndejembi amesema wao kama Wilaya wamedhamiria kuhama kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kwenda kwenye kilimo cha biashara ili kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kunyanyua uchumi nchini na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

" Rais wetu anahimiza sana katika kukuza uchumi kupitia viwanda hivyo ni lazima sisi wasaidizi wake kuwahamasisha wananchi wetu kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kwenda kwenye biashara maana viwanda hivi ambavyo Serikali ya Dk Magufuli inajenga vitahitaji malighafi ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na kilimo.

Hivyo sisi kama Kongwa tumeona njia pekee ya kufanikisha hilo ni kuwafanya wananchi wetu walime kwa wingi korosho kwa sababu licha ya wao kufaidika kiuchumi lakini pia watakuza mapato kwa serikali," Amesema DC Ndejembi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akigawa miche ya korosho kwa wananchi wa Wilaya hiyo. DC Ndejembi amesema lengo lao ni kufanya kilimo cha kibiashara.

TOAM YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA SOKO LA UKAHAKIKA MAZAO YA KILIMOHAI, YASEMA NI KILIMO KINACHOLIPA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu-Kilimanjaro

SHIRIKA la Kuendelea Kilimohai Tanzania(TOAM) limewahakikishia wakulima ambao wamejikita katika kilimo hicho na hasa katika zao la kahawa kuwa soko la uhakika, hivyo waendelee na jitihada za kuzalisha kwa wingi mazao ya kilimohai nchini.

Limesema linatambua namna ambavyo mazao kama kahawa iliyozalishwa kwa mfumo wa kilimohai ilivyo na soko kubwa na la uhakika duniani na kwamba wanaojihusisha na kahawa hiyo hupata fedha nyingi ukilinganisha na wanaozaisha kwa kutumia sumu na kemikali katika mashamba yao.

Haya yameelezwa leo na Constantine Akitanda, Mshauri wa Mawasiliano wa TOAM mbele ya baadhi ya wakulima wanaofuata mfumo wa kilimohai hai katika kulima zao la kahawa walioko Kata ya Uru Shimbwe mkoani Kilimanjaro baada ya kutembelewa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliokuja mkoani Kilimanjaro kwenye mafunzo maalumu kuhusu kilimohai.

Katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofadhiriwa na Shirika Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) yanayofanyika mjini Moshi, wanahabari hao watatao 21 kutoka vyombo mbalimbali walipata fursa ya kufanya ziara ya kimafunzo mashambani wakiambatana na maofisa wa TOAM pamoja na FAO huko Shimbwe Juu, kata ya Uru Shimbwe.

Mafunzo kwa Waandishi hao yameandaliwa na TOAM kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kuandika kwa umahiri habari za kilimohai.

Akizungumza mbele ya wakulima hao wa kahawa Akitanda amesema kuwa shirika hilo linawahakikishia wakulima kuwa bei ya kahawa iliyozalishwa kwa mfumo wa kilimohai ni bei bora na inayotia matumaini makubwa kwa Wakulima na kwamba mahitaji yake kahawa hai huongezeka kila siku duniani.

"Tunawahakikishia kahawa inayopatikana kupitia mfumo huu wa kilimohai, ina bei inayopendezesha moyo, ndio maana hata hapa kwetu bei ya chini kabisa ni dola za Kimarekani kati ya tano hadi saba ambayo ni wastani wa kuanzia shilingi 10,000/- hadi 15,000 kwa kilo au hata zaidi ya hapo,"amesisitiza Akitanda.

Kwa kukumbusha tu Akitanda aliamua kueleza suala la bei kutokana na kuwepo kwa taarifa ya kwamba bei ya kahawa ya kilimohai kwa wanachama wa AMCOS ya Uru Shimbwe kulalamikiwa vikali na Wakulima hao walipokuwa wakielezea changamoto wanazokumbana nazo katika kuendesha shughuli zao za kilimohai.

Mzee Remmy Temba, mkulima maarufu Shimbwe Juu, aaliwaambia waandishi kuwa kahawa hai kwa sasa wao hulipwa shilingi 4,500 tu kwa kilo moj, napo fedha hizo hulupwa kwa awamu, 2,000awamu ya kwanza na zinazobaki hulipwa awamu ya pili jambo linalowaumiza sana Wakulima wa kilimohai kwa kuwa tofauti ya bei ni ndogo sana baina yao na Wakulima wa kawaida wanaotumia sumu kuulia wadudu na kemikali kukuzia mimea.

Akijibu hoja iliyotolewa na mzee Temba, Akitanda aliwataka Wakulima kuwa na subra wakati jambo hilo likifanyiwa tathimini na uchunguzi.

“Niwaombe sana ndugu zangu wakulima, siku chache zijazo kunafanyika mkutano wa kitaifa kuhusu kilimohai huko Dodoma, kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kufikia uhakika na usalama wa chakula, uboreshaji maisha, viwanda na utayari wa kuyakabili mabadiliko ya tabianchi kupitia ubunifu wa kilimohai” aliongeza Akitanda na kusema changamoto hizi zitajadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi.

Awali akiwatambushisha Waandishi wa Habari kijijini Shimbwe Juu, Akitanda alisema walifikia uamuzi wa kuwaleta wanahabari Shimbwe kujifunza kwa vitendo kilimohai baada ya kuona jitihada kubwa zinazofanywa na Wakulima wa eneo hilo katika kusimamia misingi ya kilimohai ambayo pia inaheshimu sana kanuni za uhifadhi wa mazingira.

Awali wakulima wa kahawa hai katika mazungumzo yao na waandishi wa habari, waliweka bayana faida za kilimohai na kwamba walisisitiza kuwa hiki ndicho kilimo salama kwa mkulima na mlaji hivyo hawanabudi kukiendeleza na kukirithisha toka kizazi kimoja kwenda kingine.

Wakulima pia walieleza faida anuai za kilimohai pamoja na mambo mengine walisema mazao yake yana thamani kubwa ukilinganisha na mazao yatokanayo na kilimo kisichohai ambacho kwa sehemu kubwa kinategemea mbolea zenye kemikali pamoja na sumu inayotumika kuulia wadudu.

Mzee Remmy Temba amesema kuwa amekuwa akijihusisha na kilimo cha kahawa kwa mfumo wa kilimohai tangu mwaka 1979 kwenye shamba alilorithishwa na marehemu baba yake.

Hata hivyo amesema kuna faida nyingi ambazo anazipata kutokana na kilimo hicho kwa kutoa mifano kadhaa huku akieleza wazi ni kilimo ambacho kimekuwa na tija kubwa kwao ya kijiendesha kiuchumi lakini pia anayekula vyakula vinavyotokana na kilimohai anakuwa ni mtu mwenye nguvu na hatetereki ovyo kiafya kwasababu za magonjwa.

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Uru Shimbwe Bertin Mkami amesema kuwa ni kweli changamoto ya wakulima ni bei lakini akatumia nafasi hiyo kueleza sababu zinazosababisha bei kuwa chini. Hivyo Maofisa wa TOAM na FAO walimhakikishia kuwa kilichosemwa kimesikika.
Mkulima wa Kilimohai Lemy Temba wa Kijiji cha Huru Shimbwe akiwa shambani kwake akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kutembelea shamba hilo kama sehemu ya kujifunza kuhusu kilimo hicho.Mafunzo yameandaliwa na TOAM
 Mimea ya zao la kahawa ambayo inalimwa kwa mfumo wa kilimohai yakiwa shambani katika Kijiji cha Huru Shimbwe mkoani Kilimanjaro. Shamba  hill ni mali ya mzee Lemy Temba (hayupo pichani)ambaye ameamua kujikita katika kilimo hicho
 Baadhi ya waandishi waliokuwa katika mafunzo ya Kilimohai yaliyoandaliwa na Shirika la Kuendeleza Kilimohai Tanzania( TOAM) wakiwa katika  shamba la Lemy Temba(57) baada ya kwenda kujifunza kuhusu kilimo hicho kwa vitendo. Temba amekuwa akilimiki shamba  hilo tangu mwaka 1979 baada ya kurithi kutoka kwa baba yake.
 Ofisa Mawasiliano wa Shirika la  Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa( FAO) Emmanuel Kihaule (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya kilimohai mkoani Kilimanjaro ambapo waandishi hao walipata nafasi ya kutembelea baadhi ya mashamba yanayolimwa kwa mfumo wa kilimohai yaliyopo Huru Shimbwe mkoani hapa
 Mtalaam  Mshauri wa Kilimohai kutoka Shirika la Kuendeleza Kilimohai Tanzania(TOAM) Costantine Akitanda  akizungumza kuhusu umuhimu wa kilimo hicho na mikakati ya Shirika hilo katika kuhakikisha Watanzania wengi wanaojihusisha nacho kwani kinalipa na kinafaida nyingi za kiafya kupitia mazao yanayotokana na kilimohai kuwa ya asili na yasiyo na kemikali
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa katika semina ya kilimohai iliyoandaliwa na TOAM kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazohusu kilimo hicho na faida zake.Semina hiyo imefanyika jijini Moshi mkoani Kilimanjaro

PETROBENA YATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA MADARASA KATIKA MANISPAA YA TABORA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (kushoto) akipokea msaada mifuko ya mbolea kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Peter Kumalilwa (kulia) kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira katika Manispaa ya Tabora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Peter Kumalilwa akitoa maelezo mafupi leo kabla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(wa pili kutoka kushoto) .
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akitoa maelezo mafupi leo kuhusu kampeni ya kuboresha miundombinu ya elimu kabla ya kupokea mifuko 100 ya saruji kutoka Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena.
Bwana shamba na Mauzo wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Khaji Halidi akitoa maelezo leo kuhusu matumizi ya mbolea za aina mbalimbali wakati walipokabidhi mbolea za kukuzia miti kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala( mwenye shati nyeupe) 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (kushoto) akipokea msaada mifuko ya saruji 100 kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena Peter Kumalilwa (kulia) kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Tabora.PICHA NA TIGANYA VINCENT

……………………………………………………

KAMPUNI ya Petrobena East Ltd imetoa mifuko 100 ya saruji na mifuko 10 ya mbolea katika Manispaa ya Tabora ikiwa ni kuunga mkono juhudi Serikali za ujenzi wa madarasa na utunzaji wa mazingira.

Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Peter Kumalilwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala.

Alisema kuwa Kampuni hiyo imefurahishwa na juhudi za Serikali za kuboresha elimu nchini zinazoendelea na hivyo wameamua kushiriki katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia.

Kumalilwa alisema kuwa sanjari na utoaji wa saruji hiyo wameamua kutoa mbolea mifuko 10 kwa ajili ya kukuzia miti ambayo imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora ili kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala alisema kuwa msaada huo utasaidia kuunga mkono jitihada zao za kuboresha miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Tabora kwa ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu ikiwemo kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.

Alisema mifuko 50 itakwenda kata ya Uyui na iliyobaki 50 itapelekwa Kata ya Ifucha ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Kitwala alisema wako katika kampeni ya kuhakikisha kuwa inaondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kutembea umbali mrefu kutoka kwao hadi shule , jambo linalodhofisha ufaulu wa wanafunzi.Aidha alisema kuwa pia wanampango wa kujenga Sekondari katika Kata ya Ifucha ambayo haina Sekondari.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ifucha Juma Abdallah aliishukuru Serikali kwa hatua ya kuamua sehemu ya msaada uliotolewa na Petrobena kusaidia wananchi wa eneo hilo ili kuongeza vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi.

Aliongeza kuwa tayari wananchi wa endeo hilo wamekusanya vifaa mbalimbali kama vile mchanga na mawe wakisubiri kuungwa mkono ili nao waweze kujenga Sekondari yao ya Kata kwa ajili ya kuondolea adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wanasoma Sekondari katika Kata jirani.

Naye Said Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Petrobena kwa kutoa msaada huo ambao sehemu ya mifuko hiyo itasaidia kujenga vyumba vya madarasa katika Shule shikizi.

Alisema shule shikizi zinasaidia kupunguza tatizo la watoto kutembea umbali mrefu kutafuta haki yao ya kupata elimu.Aidha Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena kwa kuamua kushughulikia tatizo la zao la tumbaku ikiwemo usambazaji wa mbolea mapema.

KAMPUNI ya Petrobena East Ltd imetoa mifuko 100 ya saruji na mifuko 10 ya mbolea katika Manispaa ya Tabora ikiwa ni kuunga mkono juhudi Serikali za ujenzi wa madarasa na utunzaji wa mazingira.

Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Peter Kumalilwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala.

Alisema kuwa Kampuni hiyo imefurahishwa na juhudi za Serikali za kuboresha elimu nchini zinazoendelea na hivyo wameamua kushiriki katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia.

Kumalilwa alisema kuwa sanjari na utoaji wa saruji hiyo wameamua kutoa mbolea mifuko 10 kwa ajili ya kukuzia miti ambayo imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora ili kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala alisema kuwa msaada huo utasaidia kuunga mkono jitihada zao za kuboresha miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Tabora kwa ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kupata elimu ikiwemo kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.

Alisema mifuko 50 itakwenda kata ya Uyui na iliyobaki 50 itapelekwa Kata ya Ifucha ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Kitwala alisema wako katika kampeni ya kuhakikisha kuwa inaondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kutembea umbali mrefu kutoka kwao hadi shule , jambo linalodhofisha ufaulu wa wanafunzi.

Aidha alisema kuwa pia wanampango wa kujenga Sekondari katika Kata ya Ifucha ambayo haina Sekondari.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ifucha Juma Abdallah aliishukuru Serikali kwa hatua ya kuamua sehemu ya msaada uliotolewa na Petrobena kusaidia wananchi wa eneo hilo ili kuongeza vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi.

Aliongeza kuwa tayari wananchi wa endeo hilo wamekusanya vifaa mbalimbali kama vile mchanga na mawe wakisubiri kuungwa mkono ili nao waweze kujenga Sekondari yao ya Kata kwa ajili ya kuondolea adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wanasoma Sekondari katika Kata jirani.

Naye Said Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Petrobena kwa kutoa msaada huo ambao sehemu ya mifuko hiyo itasaidia kujenga vyumba vya madarasa katika Shule shikizi.

Alisema shule shikizi zinasaidia kupunguza tatizo la watoto kutembea umbali mrefu kutafuta haki yao ya kupata elimu.

Aidha Ntahondi aliishukuru Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Petrobena kwa kuamua kushughulikia tatizo la zao la tumbaku ikiwemo usambazaji wa mbolea mapema.

AUWSA YAHARAKISHWA KUPELEKA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA NAMANGA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji mhandisi Anton Sanga  amewataka mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha ( AUWSA) haraka iwezekanavyo kuhakikisha maji yanawafikia wakazi wa mji wa  Namanga wilayani Longido ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya maji kwa muda mrefu

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi katika chanzo cha maji cha mto simba kilichopo ndaniya hifadhi ya taifa ya Kinapa Naibu katibu amesema kuwa Ameridhishwa na ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji ambao ujenzi wake umeendana na thamani halisi ya fedha na umeshakamilika

Sanga Alisema kuwa maji yanayotoka katika chanzo hicho ni mengi ila bado hayawatoshelezi kwa muda mrefu kwani mradi huo ni wa miaka mitano hivyo waangalie uwezekano wa kuongeza uwezo wa maji hayo kuingia katika chanzo hicho ili yaweze kuwafikia wakazi wa mji wa namanga.

“nimewaagiza mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha waongee haraka iwezekanavyo watu wa bonde la pangani ambao wao ndio wanatoa huduma ya maji katika mikoa minne ambayo ni Tanga ,Kilimanjaro ,Arusha na manyara kuungana nao na kuangalia kama kunauwezekano maji haya yanayochukuliwa kutoka chanzo cha mto Simba kwenda Namanga yaongezewe kidogo ili yaweze kufika na kuwatosha wakazi wa mji wa Namanga”alisema Sanga

Aidha pia aliwataka AUWSA kuongeza kasi ya kuwaunganishia wateja wao maji kwa kasi na kwa haraka ili wananchi wote wa mji wa Namanga waweze kupata huduma hii ya maji kwa haraka na kwawakati.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justini Lijomba Amesema wamepokea maelekezo ili kufikisha maji hayo katika mji wa namanga hivyo watahakikisha maji hayo yanawafikia kwa wakati wakazi hao

Aidha alibainisha kuwa mradi huo umegarimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 15 na unatarajiwa kuhudumia kaya zoto za mji wa Namanga,alitumia muda huo kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kuwapa kipaumbele wakazi wa Namangan a Longido.

Kamati ya Rufaa Isifungwe Na Maamuzi Ya Wasimamizi

$
0
0

Nteghenjwa Hosseah, Iringa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo ameelekeza Kamati za Rufaa za Uchaguzi kutofungwa na
maamuzi yaliyofanywa na Wasimamizi/wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi
katika maeneo yao.

Jafo ameyasema hayo Mkoani Iringa wakati wa muendelelezo wa ziara
yake Mikoani kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unaotarajiwa kufanyika Tar 21/11/2019.

Katika kikao hicho na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamati ya
Rufaa pamoja wasimamizi wa Uchaguzi ngazi za Wilaya Mhe. Jafo
ameelekeza Kamati za Rufaa kutofungwa na maamuzi yaliyofanywa na
Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakati wa zoezi zima la
Uteuzi.

“Wasimamia wa Uchaguzi wamefanya kwa nafasi yao kwa kadiri
walivyoona inafaa sasa ni wakati wenu kuyachambua na kujiridhisha na
kazi waliyoifanya maamuzi yao sio ya mwisho ninyi ndio mnatakiwa mtoe
maamuzi ya mwisho katika malalamiko yatakayowasilishwa” Alisema Jafo
Nimelisema hili na naendelea kusisitiza nendeni mkafanye kazi kwa weledi
na mkazingatie haki mkamalize malalamiko yote yatakayowasilishwa
kwenu ili wagombea wawe na amani na Uchaguzi ufanyike salama
alisisitiza Jafo.

“Rufaa iwe rufaa kweli kweli yaan mlalamikaji akifikisha malalamiko yake
kwenu apate suluhisho la malalamiko yake, fanyeni maamuzi yenu kwa
kuzingatia haki” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa msiwe na mashaka katika kazi yenu, mjiamini na
mkatende kwa weledi, mkapitie malalamiko yote kwa makini mkiona mtu
anastahili mrudisheni kwenye kinyang’anyiro msifumgwe na maamuzi ya wasimamizi angalieni uhalisia wa malalamiko anayestahili mpeni na asiyestahili msimpe.

Wakato huo huo Waziri Jafo aliitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama
kuhakikisha wanalinda amani wakati wote wa Uchaguzi.

Waziri Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa na Njombe, Morogoro
na Tanga.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA AFYA WA NCHI ZA SADC

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergmena Tax  baada ya kufungua Mkutano wa siku tano kwa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi  kwa Nchi Kumi na Sita Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Unaojadili Mustakbali wa Masuala yote ya afya,  Mikakati dhidi ya Ukimwi, kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya Mwaka 1999,  Mpango Mkakati wa Kanda wa Masuala ya Afya na kuridhia kwa pamoja Maazimio mbalimbali yanayohusiana na  Afya kwa Nchi za SADC.  Mkutano huo Umefunguliwa leo Novemba 07,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipowasili katika Ukumbi wa  Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT  CC) Jijini Dar es salaam leo Novemba 07, 2019 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa siku tano kwa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi  kwa Nchi Kumi na Sita Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Unaojadili Mustakbali wa Masuala yote ya afya,  Mikakati dhidi ya Ukimwi, kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya Mwaka 1999,  Mpango Mkakati wa Kanda wa Masuala ya Afya na kuridhia kwa pamoja Maazimio mbalimbali yanayohusiana na  Afya kwa Nchi za SADC.  Pichani kati ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergmena Tax  .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (kushoto) akiwa ameambatana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergmena Tax  (kulia)  pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiondoka baada ya kufungua Mkutano wa siku tano kwa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi  kwa Nchi Kumi na Sita Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Unaojadili Mustakbali wa Masuala yote ya afya, Mikakati dhidi ya Ukimwi, kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya Mwaka 1999,  Mpango Mkakati wa Kanda wa Masuala ya Afya na kuridhia kwa pamoja Maazimio mbalimbali yanayohusiana na  Afya kwa Nchi za SADC.  Mkutano huo Umefunguliwa leo Novemba 07,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa siku tano kwa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi  kwa Nchi Kumi na Sita Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Unaojadili Mustakbali wa Masuala yote ya afya,  Mikakati dhidi ya Ukimwi, kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya Mwaka 1999,  Mpango Mkakati wa Kanda wa Masuala ya Afya na kuridhia kwa pamoja Maazimio mbalimbali yanayohusiana na  Afya kwa Nchi za SADC.  Mkutano huo Umefunguliwa leo Novemba 07,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT CC) Jijini Dar es salaam. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Baadhi ya Wajumbe baada yakufungua Mkutano wa siku tano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi  kwa Nchi Kumi na Sita Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Unaojadili Mustakbali wa Masuala yote ya afya,  Mikakati dhidi ya Ukimwi, kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya Mwaka 1999,  Mpango Mkakati wa Kanda wa Masuala ya Afya na kuridhia kwa pamoja Maazimio mbalimbali yanayohusiana na  Afya kwa Nchi za SADC.  Mkutano huo Umefunguliwa leo Novemba 07,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam. 

TIMU NANE ZATINGA HATUA YA NANE BORA ASAS SUPER LEAGUE 2019

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) Cyprian Kuyava akisalimiana na moja ya timu ambayo imetinga hatua ya nane bora ligi ya ASAS SUPER LEAGUE mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalah akiwa na viongozi wa chama cha soka mkoa wa Iringa wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Young Stars ambayo nayo imetinga hatua ya nane bora


NA FREDY MGUNDA, IRINGA

TIMU za 8 zilizokuwa zikishiriki ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa inayojulikana kwa jina la Asas Super league 2019 zimefanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika kuelekea kumpata bingwa wa mkoa atakayeondoka na kitita cha milioni mbili.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya nane bora ni,Mafinga Academy Fc, Mkimbizi Fc, Young Stars, Ismani Fc, Irole Fc,Kalinga Fc, Kidamali Fc timu moja kati ya Nzihi na Mbegamwekundu atajihakikishia kuingia katika nane bora za ligi hiyo mkoani hapa.

Wakati timu hizo zikiingia katika nane bora timu za Acosato fc, African Wanderas hizo zimeshuka daraja hadi la nne wakati timu za Mapanda Fc, Mshindo fc na Magulilwa zikicheza mchezo wa mtoano kuendelea kubaki ligi hiyo ama kuungana na walioshuka daraja. 

Katika ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Maziwa ya Asas mchezaji, Emmanuel Geka wa Kidamali Fc anaendelea kuongoza kwa ufungaji wa magoli baada ya kufikisha magoli 8 huku akifatiwa kwa karibu na wachezaji, Riziki Kelvin (Ismani Fc) na Luka Duma (Irole Fc) wenye mabao 7 kila mmoja.

Wachezaji wanaofatia katika mashindano hayo ni Baraka Athuman (Mafinga Academy) mwenye magoli 5 huku wachezaji Kelvin Msafiri (Kalinga Fc), Conrodgers Mhavile (Irole fc) na Mohamed Rashid (Ismani fc) wakiwa na magoli manne.

Na katika mechi zilizopigwa juzi Upendo Fc ilitoshana nguvu na timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Iringa kwa goli 1 – 1 yaliyofungwa na Elisha Chuma (Chuo cha Iringa) na Jemin Fred kwa upande wa Upendo Fc.

Wakati michezo mingine ilikuwa kati ya Ismani fc dhidi ya Acosato ambapo Isman waliibuka na ushindi wa magoli 4 -1 kwa magoli yaliyofungwa na Mohamed Rashid, Riziki Kelvin na Razack Kibuga huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Acosato likifungwa na Mohamed Salufu.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Kidamali Fc dhidi ya Irole fc ambapo Kidamali walishindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kukubali kipigo cha mabao 3 -1 kwa magoli ya Luka Duma aliyefunga mawili, Conrodgers Mhavile .

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa, Cyprian Kuyava akizungumza na Tanzania Daima alivipongeza vilabu vyote vilivyofuzu hatua ya nane bora licha ya changamoto zilizojitokeza kutokana na ugumu wa mashindano hayo mwaka huu.

Kuyava alisema kwamba kuna baadhi ya timu zimecheza kwa nidhamu kubwa hali iliyosababisha kuweza kufuzu katika hatua hiyo kubwa kabisa na kuwapongeza waamuzi, makamishna na wasimamizi wa ligi kwa umakini na umahiri wanaoendelea kuonyesha katika ligi ya Asas.

Aidha alizipongeza timu zote zilizoshiriki ligi hiyo kwa nidhamu, ushindani weredi mkubwa wakati wote wa mashindano hayo yalipokuwa yakifanyika katika hatua za makundi na kuzitaka timu zilifuzu hatua ya nane bora kufanya maandalizi mazuri kuweza kuibuka na ubingwa.

Alisema kuwa changamoto zilizojitokeza katika hatua ya makundi zinatakiwa kufanyiwa kazi katika hatua ya nane bora ili kuweza kumpata bingwa mshindani katika ligi za mabingwa ya mikoa Tanzania Bara.

Bingwa wa mashindano hayo atapata kombe na sh. 2,000,000,jezi seti moja,mipira mitatu, na nafasi ya kushiriki ligi ya mikoa. Mshindi wa Pili shilingi 1,000,000, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki huku Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1

Halmashauri ya Tandahimba yaongoza kimkoa Kampeni ya Chanjo ya Taifa

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba  ameipongeza Idara ya Afya kwa kushika nafasi ya Kwanza katika Halmashauri tisa za Mkoa wa Mtwara katika Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa

Ameyasema hayo  wakati akipokea taarifa ya tathimini ya Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa Wilayani humo.

"Kazi mliyoifanya idara ya  Afya ni ya kubwa kuwa washindi wa kwanza katika Halmashauri tisa si kazi ndogo,hongereni Sana,"alisema Waryuba

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya, Antipas Swai alisema kuwa halmashauri imepata asilimia 117 kwa Surua Rubella na asulimia 115 kwa polio ya sindano

Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa katika Wilaya ya Tandahimba ilianza Oktoba 17 Hadi Oktoba 21 mwaka huu ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kuleta watoto kupatiwa huduma hiyo
 Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akitoa pongezi kwa idara ya Afya
 Mganga Mfawidhi wa hospital ya Wilaya Antipas Swai 
 



Amcoss zitakazopatikana na vyeti hewa kukiona-dc Tandahimba

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka viongozi wa vyama vya msingi (Amcos) kuacha vitendo vya ubadhilifu na utoaji wa vyeti hewa katika msimu huu wa Korosho

Akizungumza na Viongozi wa vyama vya msingi amesema wao  wamekuwa ni chanzo Cha vyeti hewa.

"Sitaki kusikia  vyeti hewa  anayeleta  mzigo wake  ndiye  anayepaswa kulipwa  na si vinginevyo,hatutawavumilia hatua kali tutawachukulia,wakulima wapewe haki zao,"amesema Waryuba

Amesema viongozi ili waweze kuitenda kazi hii kwa weledi  ni lazima wapate makarani waaminifu ambao wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi

Hakikisheni  makarani wenu wawe na mkataba  na wadhaminiwe  na watu wenye dhamana hatutaki makarani wababaishaji,"amesema Waryuba

Aidha aliwataka wakulima kukausha korosho zao ili waweze kupata kilo sahihi wanapopeleka ghalani 

"Wakulima kausheni vizuri korosho ili zinapokwenda ghalani ziwe na kilo sahihi,mnapopeleka korosho hazijakauka vizuri zinapokaa zinakauka hivyo zinapokuja kupimwa Tena zinaonekana zimepungua utata unaanzia Hapo,"anasema Waryuba.
 Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba  akifafanua Jambo kwa viongozi wa Amcos 
Afisa Ushirika wa Wilaya Sudi Rajabu.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kikao hicho.

PONGEZI ZA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA WAZEE WALIOTUMIKA KATIKA UKOMBOZI WA NCHI NA UJENZI WA TAIFA

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Sima amesema kuwa Serikali inatambua michango ya watu mbalimbali walioshiriki katika ukombozi na Nchi yetu na ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja wazee wetu walioshiriki katika tukio la kuchanganya udongo tarehe 26 Aprili, 1964.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis (Mb.) lililouliza Je, Serikali inawaangalia vipi wazee wetu wane walioshiriki katika kuchanganya udongo siku ya Muungano mwaka 1964, kwa kuwapa asante baada ya utu uzima kuwafikia.

Naibu Waziri aliongeza kuwa Kundi hili ni moja kati ya makundi mengi yaliyotoa mchango wa hali na mali katika kulijenga Taifa hili ikiwemo wastaafu na walioshiriki katika Vita vya Kagera. Hata hivyo, kwa sasa hakuna sheria mahsusi ya asante au malipo kwa watu waliofanya mambo makubwa yanayojenga historia ya Nchi.

“Kuwashirikisha Wazee hawa katika maadhimisho ya sherehe za Muungano ni sehemu ya kutambua mchango wao na kukumbuka tukio muhimu la uchanganyaji wa udongo wa Tanganyika na Zanzibar. Ushiriki wao huwezeshwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aidha, pamoja na wazee hawa, yapo makundi mengine ya wazee ambao kwa namna moja au nyingine walitoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa ambao pia hualikwa kushiriki katika maadhimisho hayo mfano Viongozi Wastaafu na Wanasiasa Wakongwe” alisema Waziri Sima.

Aidha Naibu Waziri Sima akijibu swali la Mh Jaku Hashim Ayoub (B.L.W) lililouliza Kwa mujibu taarifa rasmi ya Serikali Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) iliyotolewa mwaka 2014, Kisiwa cha Latham (Fungu Mbaraka) ni mali ya Zanzibar tangu kilipotangazwa rasmi mwaka 1898. Hata hivyo zipo taarifa zilizothibitishwa kuwa Serikali ya Muungano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliiandikia SMZ kuwataarifu kwamba Kisiwa hicho ni cha Tanzania Bara:-
Je, Serikali hizi mbili ambazo ni ndugu wa damu watakaa kutatua kero hii ya muda mrefu; na Je, Serikali haioni kuwa umefika muda muafaka kulifanyia kazi suala hilo.

Waziri Sima alisema kuwa Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 Ibara ya 2 (1) inatamka wazi kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na sehemu ya bahari ambayo imepakana na nchi za Kenya, Shelisheli, Comoro na Msumbiji. Hivyo basi, kwa mujibu wa tafsiri ya mipaka hiyo, Kisiwa cha Latham (Fungu Baraka) kiko ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na pia hakuna mgogoro wa umiliki wa eneo la kisiwa hicho kwa vile kimo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.

WADAU WA AMANI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wadau wa amani na viongozi wa dini kuhubiri suala la amani sambamba na kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo udhalilishaji, ubakaji na
matumizi ya dawa za kulevya.

IGP Sirro ameyasema hayo leo akiwa kisiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi
ambapo amewataka wananchi na wadau wa amani kushirikiana kwa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuifanya nchi kuwa salama.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohamed Hassan ameeleza kuwa, suala la
kutunza amani ni jukumu la kila mmoja na kwamba ni vyema wananchi kwa
pamoja wakashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha suala la usalama linazidi kuimarishwa.

Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa, viongozi wa dini ni daraja kati ya waumini na Mwenyezi Mungu daraja ambalo viongozi wengine hawana.

Hivyo amewataka viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuendelea
kuhuisha Kamati za Ulinzi na Usalama katika nyumba za ibada.

Naye askofu wa kanisa la Kianglikana Dk. Michael Hafidh amesema kuwa,
wamejipanga katika kuendelea kuhubiri amani kwa waumini wao hili kuisaidia jamii kuacha kujihusisha na uvunjivu wa amani na kwamba kwa upande wa viongozi wa dini anayetaka kujihusisha na masuala ya kisiasa ni vyema akaachana na kujificha kwenye kivuli cha dini.

WAZEE WA BARAZA WAISHAURI MAHAKAMA KUU KUMTIA HATIANI MTUHUMIWA ANAYEDAIWA KUMUUA MTOTO WA DADA YAKE

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

WAZEE wa Baraza  katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mwanamama Esther Lymo (47) anayedaiwa kumuua mtoto wa dada yake, Naomi John (7) wameishauri Mahakama Kuu kumtia hatiani mshtakiwa kwa mauaji ya kukusudia.

Mahakama Kuu liyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 7,2019 imeelezwa hayo na wazee watatu wa baraza wakati wa majumuisho ya kesi hiyo baada ya mashahidi tisa wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi mbele ya Msajili, Pamela Mazengo huku mshtakiwa alileta mashahidi watatu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wazee hao wa walitoa maoni yao kwamba kutokana na ushahidi wa Andrew John (9) ambaye alishuhudia tukio la kupigwa kwa marehemu Naomi John inaonesha wazi mshtakiwa alikusudia kufanya mauaji.

Walidai watoto walikuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma lakini malengo hayo hayakutekelezeka kwa sababu watoto Naomi na Andrew hawakupelekwa shule matokeo yake walikutana na huo ukatili wa kuteswa na kunyanyaswa na mshtakiwa ambae alikuwa mama wa ubatizo wa mtoto Naomi (marehemu)

Wamedai, kulingana na ripoti ya daktari iliyoonesha marehemu alikutwa na majeraha mwilini huku mshtakiwa mwenyewe alikiri kuwa alimchapa kwa fimbo ya mpera, hivyo inaonesha wazi kuwa aliua kwa kukusudia.

Moja ya ushahidi wa upande wa mashtaka ulidai kuwa, mshtakiwa alimpiga marehemu, kumng'ata mwilini na kisha kumwagia maji ya moto ya chai ambapo inadaiwa ilikuwa tabia yake kuwafanyia ukatili watoto hao Andrew na marehemu Naomi.

Katika utetezi wake mshtakiwa huyo ameiomba Mahakama imuonee huruma na kumuachia huru  huku akidai alikuwa akimchapa marehemu kwa kumkanya na kwamba vidonda na makovu aliyokutwa nayo mwilini alitoka nayo kijijini kwao mkoani Kilimanjaro sababu alikuwa anachunga mbuzi.

Akielezea jinsi namna marehemu Naomi na Andrew John wanavyomuhusu alidai ni watoto wa dada yake na aliwachukua kuishi nao baada ya kuombwa awasomeshe  kwa kuwa dada hakuwa na uwezo ambapo aliishi nao nyumbani kwake Tuangoma Kigamboni kwa takribani miezi 10.

Ambapo alikaa na watoto hao kwa miezi hiyo 10 nyumbani kwake Twangoma mbako pia kuna mapori kama kijijini kwao  Moshi.

"Watoto hao ni watundu sana, huwa wanakimbizana na kucheza vichakani ambako huku nako kuna mapori kama kilimanjaro hivyo ndio maana mwili wake ulikuwa na vidonda na makovu, sijamuua Naomi, nilikuwa nawapenda , naomba Mahakama iniachie huru.

"Machi 25, mwaka 2016 wakati natoka kufanya usafi Saloon kwangu,  nilielezwa na Andrew kuwa Naomi ameamka, amejikojolea yupo barazani. Nilipoingia ndani nilimwambia Naomi akapige mswaki, lakini aliendelea kukaa barazani , Andrew akaniambia tena hapigi mswaki anachezea maji, nikaongea kwa sauti kwamba nikitoka ndani nitàmchapa, nilipotoka Naomi akakimbia nikamwambia Andrew amkamate.

" Alipoletwa nilichuma fimbo katika mti wa mparachichi na kumchapa kwa nia ya kumkanya kama mzazi, wakati namchapa Naomi akasema amechoka, mi nilizani ni utani kwasababu ya kukimbia na ujeuri wake, nilimnyànyua na kumweka barazani, nikaenda kutafuta dawa, nilivyorudi nilikuta amelegea sana, nikachukua gari ya jirani na kumpeleka hospitali Temeke amapo daktari alitufahamisha kuwa Naomi alifariki dunia.

Hata hivyo kesho mchana Mahakama hiyo inatarajia kusoma hukumu dhidi ya mshtakiwa huyo.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MRADI WA KOKOTO GEREZA MSALATO, MKOANI DODOMA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya eneo la kulipulia mawe ya kokoto katika eneo la Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) wanaofanya kazi za uzalishaji kokoto katika mradi huo wa Gereza hilo. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia mtambo wa uzalishaji katika mradi wa uzalishaji kokoto wa Gereza Msalato, Dodoma leo alipofanya ziara ya kikazi. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(SHIMA) limewekeza mradi huo wa kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje(katikati) akimwelezea jambo Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) kabla ya kutembelea eneo la mradi wa uzalishaji kokoto. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidiziwa Magereza, Keneth Mwambije(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia kokoto zinazozalishwa katika mradi huo wa Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije na Kulia ni Mkuu wa
Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje.

External Service ya RTD ilisaidia nchi za kusini mwa Afrika kupata uhuru

$
0
0

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Serikali imesema kuwa Idhaa ya External Service iliyokuwa inarushwa na Radio Tanzania Dar es Salaam ilianzishwa mahususi wakati wa harakati za kupigania uhuru.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na michezo Juliana Shonza alipokuwa akijibu swali Na. 38 na Mbunge Taska Restituta Mbogo (Viti Maalum) alilotaka kujua ni kwa nini TBC ilifuta kipindi cha External Service kilichokuwa kikitangaza taarifa ya habari kwa Lugha ya Kiingereza na kwa kutangaza taarifa ya habari kwa Kiswahili tu tunawanyima wageni fursa ya kujua kinachoendelea nchini.

Miongoni mwa mataifa yaliyonufaika na Idhaa ya External Service ya Radio Tanzania Dar es Salaam ni nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika ya Kusini.

Naibu Waziri Shonza amesema kuwa viongozi wa wapigania uhuru katika nchi hizo waliishi na kuratibu harakati za ukombozi katika nchi zao kutokea Tanzania ambapo walirusha matangazo ya Radio ya kuhamasisha wananchi wao kushiriki katika mapambano hayo kupitia idhaa hiyo ya External Service na haikuendelea kurusha matangazo yake baada ya nchi hizo kupata uhuru.

“Ni kweli kwamba kwa kutangaza taarifa ya habari kwa lugha moja ya Kiswahili kunawanyima wageni fursa ya kujua masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.

Lakini yapo magazeti mbalimbali yanayochapisha habari hizo hizo zinazotokea nchini kwa lugha ya Kiingereza ambapo inawarahisishia kupata habari hizo kupitia magazeti ya Daily News, The Guardian pamoja na The Citizen.”

Aidha, Naibu Waziri Shonza aliongeza kuwa kwa sasa TBC kupitia stesheni ya TBC International inayopatikana katika masafa ya 95.3, hutangaza kwa lugha ya Kiingereza hatua inayowafanya wageni kuendelea kupata habari na taarifa za mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

Zaidi ya hayo, Naibu Waziri Shonza alisisitiza kuwa TBC1 na TBC Taifa zinarusha baadhi ya vipindi kwa Kiingereza ikiwemo vipindi vya “This Week in Perspective” na “International Sphere” na TBC Taifa ina vipindi “Breakfast Express”, “Daily Edition”, “Day Time” na Overdrive kwa Kiingereza ambapo vipindi hivi huzungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi pamoja na kijamii.

Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Wabunge Kakoso Selemani (Mpanda Vijijini), Deogratias Ngalawa (Ludewa) na Sikudhani Chikambo (Viti Maalum) kuhusu usikivu wa TBC, Naibu Waziri Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kupanua usikivu maeneo yote nchini ambapo usikivu umeongezeka kutoka wilaya 87 mwaka 2017 sawa na asilimia 54 ambapo hadi Machi 2019 wilaya 102 zimefikiwa na matangazo ya radio ambayo ni sawa na asilimia 63.

Maeneo ambayo Serikali imefanyia marekebisho ni pamoja na ujenzi wa vituo vitano katika wilaya za mpakani za Rombo, Tarime, Kibondo, Kakonko, Namanga, Nyasa hadi Mbambabay umekamilika ambapo wilaya za Ruangwa, Lushoto na Mtwara ambazo usikivu wake ulikua hafifu umeimarika na mkakati wa Serikali ni kujenga mitambo ya Redio katika mikoa ya Katavi, Simiyu, Unguja, Pemba, Njombe, Songwe na Lindi.

Kuhusu makakati wa kukuza Kiswahili kama moja ya lugha nne rasmi za nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Naibu Waziri Shonza amesema kuwa Baraza la Kiswahili la Taifa kupitia mkakati wake wa miaka mitano 2015/2016 hadi 2019/2020 limejizatiti kutumia fursa hiyo likilenga kuimarisha fani ya tafsiri na ukalimani kutoka na kwenda Kiswahili pamoja na kuendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo na matumizi ya Kiswahili Afrika ya Mashariki, Afrika na duniani kote.

CRDB YAWAKUMBUKA WAKANDARASI

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi Tv,Arusha

Mkuu wa Arusha ,Mrisho Gambo amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililowashirikisha wakandarasi ,wazabuni  na wadau wa benki ya CRDB lengo likiwa ni kuwapatia elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Amesema kuwa,wakandarasi ni sekta muhimu Sana katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo wanapaswa kuboresha utendaji  kazi wao kwa kuchukua mikopo toka taasisi za fedha na mabenki.

Hata hivyo Gambo alipongeza benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya 'niwezeshe "mikopo ambayo imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiashara wadogo hasa wamachinga.

Ameongeza kuwa,changamoto kubwa inayowakabili wakandarasi wengi ni ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto hiyo huchangia kutomalizika kwa miradi kwa wakati.

Ameongeza kuwa,benki hiyo imekuwa benki ya kimkakati inayofuata misingi ya serikali katika kupambana katika kukuza uchumi na kuchangia kuunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati inayoanzishwa na serikali.

Awali Mkurugenzi wa wateja wa Kati na wadogo ,Boma Rabala amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya kuwakutanisha wazabuni na wakandarasi ili kuwajengea uwezo namna ya kutumia fursa za kibenki zinazoanzishwa na benki hiyo.

Amesema kuwa,hivi karibuni benki hiyo imeanzisha huduma ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogo 'machinga'inayofahamika kama jiwezeshe kwa ajili ya kuwapatia mikopo isiyo na masharti yoyote inayoanzia shs 10,000  hadi 500,000 lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara hao wanakuwa na mikopo ya kutosha.

Ameongeza kuwa,benki hiyo ambayo ni ya kizalendo kwa kuelewa changamoto imeamua kuja  na huduma ambayo inaendana na mazingira ya kitanzania ili kuwawezesha wazabuni na wakandarasi kuweza kupata mkopo wa haraka ambao hauna masharti ambayo inachukua muda mrefu.

Naye mmoja wa Wakandarasi Felix Nnko ambaye ni Mkurugenzi wa  kampuni ya Felix constructors T Ltd , amesema kuwa,swala zima la uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto kubwa ilikuwa ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Amesema kuwa,kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika kujua fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa  kazi na kurudishwa kwa wakati.

Naye mkandarasi mwingine kutoka  kampuni ya Raz Builders T Ltd,Zuberi Abdallah amesema kuwa,wanashukuru sana benki hiyo kuja na ubunifu wa kuwapatia mikopo kwani changamoto kubwa ilikuwa katika upatikanaji wa mikopo,ila kwa sasa hivi wana imani wataboresha shughuli zao.

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifungua  kongamano lililowashirikisha wakandarasi ,wazabuni  na wadau wa benki ya CRDB lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mounti Meru.

WAZIRI HASUNGA AVITAKA VYAMA VYA USHIRIKA KUAGIZA MBOLEA KWA PAMOJA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akiongoza kikao kazi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb)  akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa yaliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Pamoja na Serikali kusisitiza wakulima kuvitumia Vyama vya Ushirika katika utatuzi wa changamoto za kiuchumi na Kijamii, bado wanaushirika wameshindwa kubuni mfumo madhubuti wa kuwaunganisha katika ununuzi wa Pembejeo ambazo zingewapa unafuu wa gharama za uzalishaji pamoja na kwamba Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002, kusisitiza kwamba Ushirika ni chombo pekee cha kumletea mwananchi mnyonge maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Waziri wa Kilimo Mhe Japht Hasunga (Mb) ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko iliyofanyika Jijini dodoma novemba 05, 2019


Alisema kuwa pamoja na mafanikio ya Ushirika katika kutatua changamoto za kiuchumi za wanachama wake na wakulima, bado kumekuwa na changamoto za kuwepo kwa gharama kubwa za upatikanaji wa Pembejeo kutokana na Vyama vya Ushirika wa aina moja kuwa na njia zake za kupata Pembejeo.


Hivyo, ili kuondokana na gharama kubwa za upatikanaji wa mbolea na kuleta tija katika uzalishaji, Serikali imeanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS – Bulk Procurement System)kupitia Kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer (Bulk Procurement) Regulations, 2017).


Lengo la mfumo huo ni ili wakulima wawezekunufaika na punguzo la bei litokanalo na ununuzi na usafirishaji wa mbolea nyingi kwa wakati mmoja (Economies of Scale).


Katika Mafunzo hayo Mhe Hasunga amewataka washiriki hao kuagiza mbolea kupitia BPS, ambapo watatakiwa kupata mahitaji ya jumla ikiwa ni pamoja na dhamana za Benki (Bank Guarantees) zinazowezesha kupata mbolea na kulipia ndani ya siku 180 kwa tozo ndogo tu za benki za asilimia 1 hadi 2 baada ya kufungua muamana (LC – Letter of Credit).

Pamoja na kwamba BPS inawalenga zaidi wakulima, bado kuna changamoto ya wakulima wadogo kupitia Vyama vyao vya Ushirika kutoshiriki katika BPS kwani tangu kuanza kwa BPS mwaka 2017, uagizaji wa mbolea kupitia BPS umekuwa ukitumiwa na wafanyabiashara wakubwa peke yake na, wanapoifikisha mbolea kwa wakulima na kuwakuta hawana fedha za kununua mbolea, wakulima hao hulazimika kuwekewa dhamana za mikopo (Credit Guarantees) na wanunuzi wa mazao na/au wenye viwanda vya mazao ya kilimoili wapate mikopo ya Benki yenye riba kubwa (asilimia 15 – 20 ya fedha iliyokopwa).


“Gharama za usambazaji nchini ni kubwa sana ikilinganishwa na gharama za kuingiza mbolea nchini. Jambo hili limekuwa likiwafanya wakulima wadogo wapate mbolea kwa bei kubwa sana kutokana na faida kubwa za wafanyabiashara, riba za mabenki na mifumo ya uingizaji wa mbolea nje ya BPS isiyo na uwazi na hivyo kufanya hata bei ya mbolea kwa wakulima kuwa kubwa kuliko uhalisia wa gharama ” Alisisitiza Mhe Hasunga



MBOLEA YA UREA


Katika zabuni ya uingizaji wa mbolea aina ya Urea kupitia BPS iliyofanyika Julai 04, 2019;bei ya mbolea katika chanzo ilikuwa US$ 275 na bei ya kusafirisha baharini  na bima ilikuwa US$ 29 kwa tani 1. Hii ilifanya gharama ya kufikisha mfuko mmoja wa mbolea bandari ya DSM iwe Tshs 34,500/=. Kama nilivyozungumza siku ya kutangaza bei elekezi kwa mbolea ya Urea, gharama ya kutoa mfuko mmoja bandarini, kuufungasha, kuusafirisha hadi kwa mkulima na faida za wafanyabiashara hadi Sumbawanga ni Tshs 22,500/=. Hii inafanya bei ya mkulima wa Sumbawanga iwe Tshs 57,000/=.


Kwa lugha nyingine, gharama ya kufikisha mbolea kwa mkulima ni asilimia 60 ya gharama za kuufikisha mzigo bandari ya Dar es salaam (CIF). Ukubwa wa gharama hizi umechangiwa sana na faida za wafanyabiashara (Tshs 6,700/= ambayo ni zaidi ya mara mbili ya gharama za kusafirisha mzigo hadi bandari ya DSM). Gharama hii ingeweza kuepukika kama vyama vya ushirika vingeagiza mbolea moja kwa moja kwa kutumia dhamana za benki.


Gharama zingine zinazochangia kwenye kuongezeka kwa bei ya mkulima ni kukosekana kwa mfumo wa uratibu wa usaifirishaji wa mbolea kutoka DSM hadi kwa mkulima. Kwa sasa mbolea husafirishwakwa kutumia mikangafu/malori yanayobeba mzigo mdogo wa tani 30 kwa Tshs 5,500/= kwa km 1,000.Hii ni karibu mara mbili ya gharama za kuusafirisha mfuko huo kutoka kwenye chanzo (Tshs 3,336/= kutoka Qatar ambayo iko zaidi ya km 5,000 kutoka bandari ya DSM). Gharama hizi zingepungua endapo usafiri wa Reli ungetumika.


Aidha, kutokana na riba za Benki (asilimia 20 au Tshs 11,400/=), mkulima hulazimika kulipa Tshs 68,400/=. Endapo vyama vya ushirika vitaingia katika BPS, gharama hii itaepukika.


Pamoja na kuepuka gharama za usafirishaji kwa kutumia mikangafu badala ya reli, faida kubwa za wafanyabiashara na riba za mabenki, bei ya mbolea aina ya urea kwa wakulima itashuka kwa takriban Tshs 8,000/= ikilinganishwa na bei elekezi zilizopo.

MBOLEA YA DAP

Waziri Hasunga alisema kuwa Pamoja na kwamba, wakati wa ufunguaji wa zabuni kupitia BPS uliofanyika Juni 21, 2019, bei ya mbolea ya kupandia (DAP) iilkuwa kubwa sana katika soko la Dunia (US$ 350 - 380) na bei za mbolea aina za NPK ilikuwa ndogo sana (US$ 265 – 300), bado mbolea za NPK hapa nchini zimekuwa na bei kubwa sana ikilinganishwa na bei za mbolea aina DAP ambayo ni Tshs 58,000 hadi 60,000/= katika mikoa ambako tumbaku huzalishwa (Tabora, Katavi, Ruvuma na Mbeya). Bei ya NPK ya tumbaku katika mikoa hiyo hiyo ni US$ 34.5 (Sawa na Tshs 79,400). Kwa vile wakulima hupewa kwa mikopo ya mabenki, hulipa fedha hizo pamoja na riba (asilimia 7 – 10) na hivyo kufanya mkulima ainunue mbolea hiyo kwa Tshs 85,700/=.

Ili mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja uweze kunufaisha wakulima wadogo kwa kupunguza bei za mbolea kwa kadri inavyowezekana Waziri Hasunga ameagiza Vyama vikuu vya ushirika kuratibu ukusanyaji wa mahitaji ya mbolea kutoka kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwa wakati na kutathmini gharama zitakazohitajika, Vyama vikuu vya ushirika vihakikishe kwamba vinatunza kumbukumbu sahahi za mahesabu ili hati za ukomo zitolewe kwa wakati ili kurahisisha upatikanaji wa dhamana za Benki.

Maagizo mengine ni pamoja na Mrajis wa ushirika kusimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa ukomo wa madeni ili kurahisisha upatikanaji wa dhamana za Benki kwa wakati, wauzaji wa mbolea kuwa mawakala wa vyama vya ushirika na/au viwanda (mahali inapohitajika) ili kurahisha zoezi la utoaji wa mbolea bandarini na kuisambaza kwa wakulima, na Mbolea zote zitasafirishwa nchini kwa pamoja (Bulk Domestic Distribution)


Kadhalika Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameagiza Usafiri wa Reli utatumika badala ya barabara. Kikotoo cha bei elekezi kimechukulia usafiri wa mikangafu (Trucks) kwa Tshs 5,500 kwa km 1,000. Gharama hii inaweza kupungua endapo mbolea itasafirishwa kwa reli kwa Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA). Gharama hii inaweza kupungua zaidi kama mbolea nyingi itasafirishwa kwa wakati mmoja.

DKT. KIJAJI: WATANZANIA WAFUNGUE KAMPUNI ZA BIMAKUONGEZA USHINDANI

$
0
0
Na Peter Haule na Ramadhani Kissimba, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewataka watanzania ambao wamepata elimu ya Bima kufungua Kampuni za Bima za ndani ili ziweze kuingia katika ushindani na kampuni za nje.

Rai hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau cha kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030.

Dkt. Kijaji amesema kuwa, kampuni za bima nchini ni takribani 31 na kati ya hizo za kitanzania hazidi tatu, kwa hiyo kuna  kazi kubwa ya kufanya ili vijana waliopata elimu kwenye eneo la Bima waweze kuanzisha kampuni za kitanzania  na kuwa na ushindani iwapo kama Taifa limeamua kwenda  kwa pamoja.

Aidha alisema kuwa,  kuna taasisi za huduma ndogo za fedha takribani 450 lakini jambo la kushangaza ni asilimia 12 tu ya wakina mama ndio wamefikiwa na taasisi hizo hivyo kikao kazi cha kujadili Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030 utangalia njia mwafaka ya kutatua tatizo hilo.

Alisema kuwa Serikali imeendelea kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa miaka mitano ambao ulianza mwaka 2016/17 na unaelekea kukamilisha mwaka 2020/21, dhima kuu ilikuwa ni kujenga uchumi wa Viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.

“Dhima ya Mpango huu ni uchumi wa Viwanda lakini tusiwaache watanzania nje ya uchumi huu na miongoni  mwa vipaumbele ni kuondoa umasikini wa kipato kwa watu, uimara wa sekta ya fedha ndio nyenzo muhimu ya uimara wa Sekta ya viwanda”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya fedha katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, Serikali inandaa Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha ambao utatumika kuongeza upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha, upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu, kulinda watumiaji wa huduma za fedha na  kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha

Naibu Waziri Dkt. Kijaji, amewataka wadau wa kikao cha uboreshaji wa  rasimu ya Mpango Sekta Ndogo ya Fedha kujadili na kutoa maoni kwa weledi wa hali ya juu yatakayo saidia kuwa na sekta ya fedha iliyo endelevu na himilivu kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kuchangia kupunguza umaskini wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

Kwa upande wake Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionesia Mjema, alisema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji yatafanyiwa kazi na makundi ya wadau waliopo wakiwemo wa Benki, huduma za Bima na kundi litakalo angalia Sekta ndogo ya fedha, lengo ni kuangalia namna ya kutatua changamoto za Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka kumi ijayo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza kuongezeka kwa  wigo na fursa za upatikaji wa huduma za fedha kwa wananchi utakao tokana na  Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, katika Kikao  kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adlof Ndunguru, na kulia ni Mchumi Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dionisia Mjema.
 Baadhi ya wadau wa Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, wakifuatilia kwa makini maagizo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu Sekta ya Fedha kuchangia katika uchumi wa nchi.
 Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema, akitoa mada katika Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, uliofanyika Jijini Dodoma.

 Wadau kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia majadiliano ya uboreshaji wa rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, uliofanyika Jijini Dodoma.

Wadau wa Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2029/2030, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema.(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)

Wagombea wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa walioenguliwa ni ujinga wao wenyewe-Polepole

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Chama  cha Mapinduzi (CCM) kimesema  kuwa wagombea walioenguliwa katika uchaguzi wa serikali za Mtaa ni kutokana na ujinga wao wa kutofuata sheria za uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama hicho,  Katibu wa Itakadi na  Uenezi  Hamphrey Polepole amesema kuwa CCM haihusiki kwa kuenguliwa kwa wagombea katika uchaguzi wa serikali za Mtaa kwani wao ndio wamekosea kutofuata sheria.

Amesema kuwa CCM iliwekeza katika elimu kuhusiana na uchaguzi wakati vyama vingine vilishindwa kufanya hivyo badala yake wanaitupia lawama kuwa CCM imefanya hujuma.

Polepole amesema kuwa walijipanga katika uchaguzi huo na watashinda kwa kushindo kutokana na kazi walizozifanya za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015.

Amesema kuwa CCM ni Chama kikubwa hakiwezi kushindana  vyama ambavyo hata taratibu za uchaguzi .Aidha ameema kuwa na watu wengine walikuwa wanagombea katika vyama visivyokuwa katika orodha ya msajili.

Polepole amesema serikali kteuacha kuwaonea huruma kwani wanashindwa kufuata taratibu na mwisho wa siku wanategemea.

Amesema kuwa vyama visitafute huruma wakati vinashindwa kuwekeza elimu kwa wanachama wao. Polepole anasema kuwa watu wengine wameenguliwa kwa kutokuwa na kazi wakihojiwa kazi wanazozifanya wanasema tupo tunapambana hapo.
Katibu wa Itakadi na Uenezi wa CCM Hamphray Polepole akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa jijini Dar es Salaam.

WFP YAENDELEA KUBEBA DHIMA YA KUHAKIKISHA JAMII ZA WALIMWENGU ZINAISHI MAZINGIRA YENYE AFYA BORA

$
0
0
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} Bado litaendelea kubeba dhima ya kuhakikisha Jamii za Walimwengu zinaishi katika mazingira yatayowawezesha kuwa na Afya bora katika maisha yao ya kila siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo akitoa baraka zake wakati akiufungua Mkutano Maalum wa Kimataifa wa Siku Nne uliowakutanisha Wawakilishi wa Shirika hilo la {WFP} wa Kanda ya Mataifa ya Kusini na Kaskazini mwa Bara la Afrika pamoja na Mashariki ya Kati.

Mkutano huo unaopokea Ripoti za Majukumu ya Wawakilishi wa Kanda hizo kwa Mwaka na kupanga Mikakati ya uwajibikaji kwa Mwaka ujao ulifanyika katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kama Wilaya ya Magharibi “A”.

Balozi Seif Ali Iddi alisema bado yapo Mataifa Mengi Duniani Wananchi wake wanaendelea kukumbwa na lishe Duni inayosababishwa na uwepo wa Wakimbizi kutokana na vita, Ukame, Mafuriko pamoja na Mabadiliko ya Tabia Nchi yanayoiathiri pia Dunia Kimazingira.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitolea mfano hai wa matukio ya mabadiliko ya Tabia Nchi yaliyoukumba Ukanda wa Bara la Afrika kwa mujibu wa Repoti za Shirika hilo ya Mwaka 2018/2019 ambao umebainisha uwepo wa uzalishaji mdogo wa chakula katika sekta ya kilimo.

Alisema hitilafu hiyo iliyotokana na upungufu wa uzalishaji wa mazao umepelekea Watoto wadogo kukumbwa na lishe duni inayoathiri Maendeleo ya Bara zima la Afrika kutokana na upungufu wa Chakula unaowakumba zaidi ya Watu Milioni Mia Mbili na Ishirini.

Akizungumzia uwajibikaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika mikakati yake ya kuimarisha ustawi wa lishe bora, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema upo ushirikiano mwema kati ya Tanzania na WFP katika kuona lishe bora inatengamaa.

Alisema Shirika la Mpango wa Chakula Duniani bado linaendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuwapatia Wananchi wake mafunzo ya Elimu ya lishe bora, kusaidia moja kwa moja Wakulima Wadogo sambamba na huduma za usafiri zinazosaidia kurahisisha mfumo mzima wa muelekeo wa kukua zaidi kwa Uchumi wa Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi mzima wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} kwa uamuzi wake wa busara ulioamua Wawakilishi wake wa Kanda ya Kusini mwa Bara la Afrika kukutana Zanzibar kitendo ambacho kitatoa nafasi kwa Zanzibar kufaidika na matunda ya Shirika hilo.

Mapema Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} Kanda ya Bara la Afrika Bwana Michael Danford alisema Shirika hilo limependekeza kuanzisha Miradi Mitatu Visiwani Zanzibar itakayosaidia kusukuma mbele masuala ya Ustawi wa Wananchi.

Bwana Danford alisema uamuzi huo wa Shirika hilo umekuja kufuatia mchango mkubwa uliotolewa na Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa Kiongozi wa ngazi ya juu ya Shirika hilo miaka ya nyuma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akibadilishana mawazo na Wakuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} mara baada ya kuufungua Mkutano wa Wawakilishi wa Shirika Hilo Kanda ya Kusini mwa Bara la Afrika.Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} Kanda ya Kusini mwa Bara la Afrika Bwana Michael Danford na wa kwanza Kulia ni Mkurugenzi Kanda wa WFP Bibi Margaret Malu.
Balozi Seif akisisitiza umuhimu wa Viongozi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani {WFP} Kanda ya Kusini mwa Bara la Afrika kusimamia utekelezaji wa ahadiu waliyotoa ya kuanzisha Miradi Mitatu Visiwani Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images