Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 6,2019


Mradi Hospitali ya Wilaya Bunda Hoi, Serikali yawapa siku 30 Tu

$
0
0
Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Bunda

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa siku thelathini kuanzia Oktoba 05, 2019 kwa Halmashauri ya Wilaya Bunda mkoani Mara, iwe imekamilisha miradi yake yote yenye utata na ianze kutoa huduma kwa wananchi, ifikapo tarehe 25 Desemba, 2019. Dkt. Gwajima ameagiza pia jopo la wataalam kutoka OR-TAMISEMI kwenda wilayani humo kufanya ukaguzi maalum kwa miradi yote yenye utata.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo  jana wakati wa ziara yake kwenye mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo alionekana kutoridhishwa na mwenendo wa miradi ya Halmashauri husuani ni ule wa Hospitali ya Wilaya ambao ulipokea fedha kiasi cha bilioni 1.5 toka mwezi Januari, 2019 lakini ujenzi wake ukaanza mwezi Mei, 2019 kutokana na malumbano baina ya viongozi wa eneo hilo. 

“Kwakweli mimi ambaye nimepewa dhamana yakusimamia sekta hii katika, mwendo huu hauniridhishi kabisa, jana nilikuwa Rorya, Umoja, Mshikamano na kutenda kazi kwa mshikamano nilio uona pale siuoni kabisa ndani ya Halmashauri hii ya Bunda” alisema Gwajima na kuongeza kwamba, “ninataka ndani ya siku 30 yaani mwezi mmoja kuanzia sasa Mkurugenzi, Miradi yote inayo lalamikiwa iwe imekamilika na taarifa tuipate TAMISEMI” aliagiza Gwajima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kusaja Amos, ilionesha, katika mwaka wa fedha wa 2018/19, Halmashauri ilipokea kiasi cha bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hata hivyo kutokana na malumbano baina ya viongozi hao, shughuli rasmi za ujenzi zikaanza Mwezi Mei, 2019 na ilipofika tarehe 31 Juni,2019 fedha zote ambazo zilikuwa hazijaingia katika mpango wa manunuzi zilirejeshwa hazina kama sheria za fedha zinavyo elekeza.

Pamoja na Mkurugenzi kujitetea mbele ya Naibu Katibu Mkuu kuwa, ujemzi huo umefikia asilimia 70 ya ujenzi wote hali ni tofauti na uhalisia kwani hadi siku ya ziara baadi ya Majengo yaliwa ndio kwanza yanamwagiwa zege ili yaanze kunyanyuliwa.

“Mkurugenzi ukisema jingo limefikia asilimia 50, tutegemee kuona majengo yote yaliyoelekezwa yawe yamefunikwa na mmeanza umaliziaji, sasa wewe hapa ndio kwanza majengo takrinan manne ndio yameanza kupigwa paa na kuezekwa na jingo linguine ndio kwanza wanamwaga zege wewe unasema asilimia 70 huku sikuudanganya umma wa watanzania?” Alihoji Dkt. Gwajima.

Kufuatia kulalamikiwa kwa miradi mingi ya Halmashauri hiyo, ikiwapo ule wa ujenzi wa Ofisi ya Mbunge, Zahanati ya Namalabe pamoja na pamoja na kituo cha Afya Mugeta kilichopelekewa fedha kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu lakini hadi siku ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu kulikuwa na kasoro nyingi za kitaalam.

Katika Hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu akiwa katika ziara hiyo, amewaelekeza wakurugenzi kote nchini kufanya sensa ya watumishi waliojiendeleza kielemu na sasa wapo tayari kufanyiwa recategorization lakini bado wanasomeka kwenye miundo ya kizamani ilihali kimajukumu wameongezewa mzigo.

“Nitumie fursa hii nikiwa hapa katika kituo cha Nyasho, kupeleka salaamu zangu kwa Wakurugenzi na Maafisa Utumishi, wapitie na kufanya sensa kubaini watumishi wanaohitaji kubadilishiwa muundo, lakini kwa hila tu za Afisa mtumishi huyo amekaa zaidi ya miaka saba hajabadilishiwa kazi lakini anapewa majukumu ya kazi mpya bila maslahi yake kuboreshwa” alikemea Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima yupo katika ziara ya ufatiliaji utendaji kazi na hali ya miundombinu ya Afya ambapo katika siku yake ya pili ametembelea na kukagua vituo cha Afya Nyasho na Makoko vyote vya Musoma mjini, Hospitali ya Wilaya ya Musoma vijijini, Hospitali ya Wilaya Halmashauri ya Bunda sambamba na Zahanati ya Mugeta.
 Naibu Katibu Mkuu Dkt. Dorothy Gwajima akihojiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama juu ya sakata la kuchelewesha ujenzi huo.
 Mkuu wa Wilaya Bibi Lydia Bupili akitoa ufafanuzi juu ya mawasiliano
 Baadhi majengo yanayo elezwa kutokamilika kwa wakati (Picha zote na Atley Kuni)

ALAT YAPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA AZAKI NCHINI, YAZITAKA KUSIMAMIA MALENGO YAO

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mikoa na Tawala za Mitaa (ALAT) Elirehema Kaaya amezitaka Asasi za Kiraia nchini (Azaki) kusimamia malengo ambayo wamejiwekea ili kunufaisha wananchi.

Kaaya amesema ni ukweli usiopingika kuwa Azaki hizo zimekua zikifanya kazi kubwa kwa kutoa elimu katika sekta mbalimbali katika kuwajengea wananchi uwezo wa kujitambua pamoja na kuwasaidia katika mambo ambayo yamekua yakihitaji msaada.

Amesema wao kama ALAT ambao wanafanya kazi katika maeneo ambayo wanakutana moja kwa moja na wananchi wamekua wakijionea mchango mkubwa unaofanywa na Azaki hizo kwa kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

" Sisi kama ALAT ni wadau wakubwa wa Azaki hizi kwa sababu zinagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wetu, na sisi kumbuka tunaziunganisha Halmashauri zote 185 na malengo yetu ni kutoa huduma mbalimbali kwa jamii hivyo nizitake Azaki hizi kuungana na Serikali kwa pamoja katika kuleta maendeleo.

Tumekua tukifanya kazi kwa karibu na Azaki hizi na kwa kweli zimekua zikionesha mchango mkubwa sana, na ndio maana tumeona ndani ya miaka mitatu wamechangia Bilioni 236 kwenye uchumi wa Nchi yetu, hii ni kuonesha wanashirikiana na Serikali yetu kuleta maendeleo chanya kwa manufaa ya Taifa letu," Amesema Kaaya.

Kaaya ametoa rai kwa Azaki hizo kujikita zaidi katika kuwajengea wananchi uwezo wa kujitegemea kiuchumi, kujenga miundombinu ya elimu, afya na kuwawezesha kujikomboa kimaisha kupitia miradi mbalimbali wezeshi ya kibiashara.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imeweka sera ambayo Halmashauri zote nchini zinatenga asilimia 10 za bajeti zao kwa ajili ya makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu hivyo amezitaka Azaki kujikita zaidi katika kuwajengea uwezo makundi hayo ili waweze kufaidika na mikopo hiyo.

" Mimi napenda kuona matokeo, Watu wetu wa kijijini anapenda kuona maji salama, huduma ya afya iliyo bora, nitoe rai kwa Azaki zetu nchini zijikite katika mambo yanayoonekana, tujikite katika mambo yanayogusa maisha ya watu wetu, tusiangalie sana matakwa ya wafadhili wetu bali mahitaji haswa ya wananchi ambao tumeamua kuwafanyia kazi," Amesema Kaaya.
 Katibu Mkuu Jumuiya ya Serikali za Mikoa na Tawala za Mitaa nchini (ALAT), Elirehema Kaaya akizungumza kwenye siku ya kwanza ya majadiliano ya maadhimisho ya Wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) yanayofanyika kwa siku tano jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Asasi za Kiraia yanayofanyika jijini Dodoma wakiwa kwenye mijadala mbalimbali inayohusu haki za watu wenye ulemavu.

Mbwana Samatta: Mshambuliaji kinara wa Tanzania afunga bao la kufutia machozi Genk ikilazwa 2-1 na Liverpool

$
0
0
Mshambuliaji kinara wa klabu bingwa ya Ubelgiji KRC Genk na nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta, hatimaye amepachika goli dhidi ya vigogo wa England klabu ya Liverpool jana usiku.

Goli hilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania.

Hata hivyo, matokeo ya mwisho ya mchezo huo wa Klabu Bingwa Ulaya yalikuwa mabaya kwa Genk kwa kulazwa kwa goli 2-1.

Samatta, aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona mpaka wavuni katika dakika ya 40 ya mchezo.

Mshambuliaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Ulaya tayari ameshapachika magoli mawili katika mechi nne.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Liverpool, Samatta pia alipachika bao la kichwa ambalo hata hivyo lilikataliwa baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Liverpool kabla ya kupachika bao.

Goli la kwanza la Liverpool katika mchezo huo lilifungwa na Georginio Wijnaldum katika dakika ya 14 baada ya safu ya ulinzi ya Genk kufanya uzembe wa kuondosha krosi iliyochingwa na winga wa Liverpool James Milner.

Samatta aliirejesha Genk mchezoni kwa kombora la kichwa dakika tano kabla ya mapumziko, hata hivyo Alex Oxlade-Chamberlain aliiandikia Liverpool bao la ushindi katika dakika ya 53.

Kwa matokeo hayo, Liverpool imepanda mpaka kileleni mwa kundi E kwa kufikisha alama tisa baada ya michezo minne. Napoli imeshuka mpaka nafasi ya pili baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na RB Salzburg. Genk inashika mkia kwa kusalia na alama moja.

Genk haina historia nzuri kwenye michuano hii, ikiwa hii ni mara ya tatu kwa klabu hiyo kucheza hatua ya makundi ya Champions League. Haijawahi kupata ushindi hata mmoja kwenye mechi 16 sasa.

Katika misimu hiyo ya 2002-03 na 2011-12 Genk ilimaliza mkiani kwenye makundi iliyopangiwa, kama ilivyo mpaka sasa kwenye msimu huu ikisalia na mechi mbili tu kujikomboa na 'nuksi' hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBCSwahili.com

SERIKALI YAOMBWA KUKOMESHA MAUAJI NA UBAKAJI KWA KINAMAMA NA WATOTO WA KIKE .

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mwenye shati jekundu)akiteta jambo na diwani wa kata ya Olasiti,kushoto kwake ni Katibu Tawala wa mkoa huo Richard Kwitega,kulia kwake ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Serikali ya mkoa wa Arusha imeombwa kukomesha vitendo vya mauaji na ubakaji katika kata hiyo vilivyoshamiri na kuwa tishio hasa kwa kinamama na watoto wa kike ambao wamekua wahanga wa matukio hayo ambayo yamekua yakijitokeza mara kwa mara

Akizungumza Diwani wa kata ya Olasiti Alex Martin katika ziara ya Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo aliyetembelea katika shule ya sekondari Mrisho Gambo ambapo alikagua ujenzi unaondelea na kuzungumza na wananchi ,Diwani huyo ameiomba serikali iweze kutumia vyombo vyake vya ulinzi kukomesha mauaji hayo.

Diwani huyo ameiomba serikali kujenga kituo kidogo cha polisi kitakachosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia kwani eneo hilo halina kituo cha polisi hivyo suala la ulinzi wa watu linakua gumu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Mrisho Mashaka Gambo akijibu Diwani huyo,ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Mkoa kufika katika kata olasiti na kushughulikia tatizo la mauwaji kwa kina mama na watoto pamoja na viteno vya ubakaji ili kutokomeza vitendo hivyo na kurejesha hali ya usalama.

Mhe.Gambo anetoa agizo hilo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ya ukaguzi wa maendeleo ya jiji la Arusha katika ukaguzi wa mradi wa elimu shule ya sekondari Burka iliyopo kata ya olasiti Na kupokea jumla ya madawati na viti zaidi ya 170 kutoka katika taasisi ya kifedha ya NMB Kanda ya kasikazini pamoja na mifuko Hamsini ya simenti kwajili ya ujenzi wa shule hiyo kutoka kanisa la EAGT mkoani Arusha.

Aidha amesema kuwa tukio la kinamama na watoto kuuliwa na kubakwa linasikitisha kwani serikali haiwezi kuvumilia kuona matukio hayo yakiendelea huku kukiwa na watu wanaokisiwa kufanya matukio hayo ambapo ameitaka kamati ya ulinzi na usalama mkoa huo kufanyia uchanguzi na kushuhurikia swala hilo.

Kwa upande wao Wananchi Zainab Kasanga na Joseph Simon wa kata hiyo wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kushukuru ujio wa Mkuu wa Mkoa ambao unaweza kuwa suluhu kwa changamoto hiyo ya matukio ya ubakaji na mauaji ambao yamekua yakitikisa kata hiyo

BILIONI 3.200 KUJENGA BWAWA LA ICHEMBA WILAYANI KALIUA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI inatarajia kutoa shilingi bilioni 3.200 kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Maji katika eneo la Ichemba wilayani Kaliua.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kukamilisha usanifu kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa hilo kwa gharama ya shilingi milioni 40.8 kwa kutumia mapato yake ya ndani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua ya kukagua miradi ya maji na kutatua kero za maji.

Alisema kukamilika kwa mradi huo utasaidia jumla ya wakazi 229,290 wa Kata za Ichemba, Kanoge, Mwongozo, Nhwande, Makingi, Sasu, Kanido, Milambo na Igombenkulu na wakimbizi kutoka Burundi.

Waziri huyo alisema ujenzi wa bwawa hilo unatarajiwa kuanza mara baada ya mvua za masika yam waka huu kumalizika.

Aidha Profesa Makame Mbarawa alisema kwa kutabua tatizo la maji katika eneo hilo , Serikali imetoa shilingi milioni 571 kwa ajili ya mradi wa dharura wa kutatua tatizo la maji Kaliua Mjini wakati wakisubiri utekeleza wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria.

Alisema mradi wa uletaji maji kutoka Ziwa Victoria katika mji wa Kaliua ni sehemu ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 ya Tanzania ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi triolioni 1.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema eneo hilo linakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji ardhini na kutokuwa na vyanzo vya kutosha vya maji.

Alisema msaada wa kuwasaidia wakazi wa Wilaya hiyo ni kupitia kujengewa mabwawa katika maeneo yenye uwezo wa kujengwa na kupata maji kutoka katika vyanzo kama vile Ziwa Victoria na mito iliyokaribu.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE, LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai(hayupo pichani), leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma.

 .  Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma kwa mazungumzo maalum.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa  Magereza nchini, Phaustine Kasike  mara baada ya mazungumzo alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije(Picha zote na Jeshi la Magereza).



Benki Ya Exim Yakamilisha Rasmi Umiliki Wa Benki Ya UBL

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania imeendelea kujitanua zaidi baada ya kufungua rasmi tawi lake jipya katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam kufuatia benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.

Hatua hiyo inafanya Benki ya Exim Tanzania kuwa benki ya kwanza miongoni mwa benki za sekta binafsi hapa nchini zilizofanikiwa kuunganisha benki nyingine na hivyo kuifanya kuwa miongoni mwa benki tano kubwa hapa nchini ikiwa na ukwasi wa kiasi cha Tsh 1.7 Trilioni.

"Tunafurahishwa na ongezeko kubwa la wa wateja wa aina tofauti ambao watajiunga na familia ya benki ya Exim na tunawahakikishia kuwa tunafurahi kuwa nao kwenye safari yetu na tunajitoa kuhakikisha kwamba wanaendelea kufurahia huduma zenye ubunifu kutoka kwetu.''

''Wateja wakiwa ni sehemu muhimu zaidi ya biashara yetu, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanafurahia huduma zetu,'' Alisema Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim.

Kwa mujibu wa Bw. Matundu hatua hiyo inakwenda sambamba na msimamo wa Rais Dk John Magufuli ambae amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na benki kubwa zaidi na ndogo nchini kwa kuwa ni hatua muhimu kwa afya ya kifedha katika ukuaji wa uchumi hususani katika kutoa huduma kamili na zenye ubunifu kwa wateja.

"Tanzania ina benki nyingi ukilinganisha na mataifa mengine ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria. Sekta ya benki imekuwa ikishuhudia uunganishwaji wa mabenki ambao mwisho wa siku utaziacha benki zikiwa na uwezo wa kusukuma ukuaji wa uchumi kikamilifu. ''

"Dar es salaam ni soko muhimu kwa Benki ya Exim na hivyo uwepo wa tawi jipya la Mkwepu ambalo lenye teknolojia, ubunifu na muundo ambao utawawezesha wateja kukutana na maafisa wa benki kwa njia ambayo inawafaa na katika mazingira ambayo ni yanafikika kwa wote,'' alisema.

Aidha Bw Matundu alisema mchanganyiko wa benki binafsi na zile za umma zilizosambaa kote nchini utahakikisha kuwa kuna mtiririko mzuri wa huduma za kifedha.

"Wajasiriamali watakuwa wamehakikishiwa upatikanaji wa kutosha wa mitaji inayohitajika kupanua biashara zao, ambayo itasababisha kasi kubwa ya ongezeko la ajira na hivyo kupunguza kabisa tatizo la ukosefu wa ajira nchini,'' alisema

Ujio wa tawi hilo jipya unaifanya benki ya Exim Tanzania kuwa kuwa na jumla ya matawi 33 kote nchini.

Kwa zaidi ya miaka 22, benki ya Exim imefanikiwa kupata hadhi ya kuwa benki kimbilio si tu Tanzania bali pia nje ya nchi ambapo imeweza kujitanua kwa kuanzisha matawi yake ikiwemo nchi za Djibouti, Comoros na Uganda.

Meneja wa Huduma kwa wateja na Uendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la jipya la Mkwepu, jijini Dar es Salaam Bw Brian Bennet (Kushoto) akimkaribisha mmoja wa wateja wa benki hiyo aliefika kwenye tawi hilo ili kupata huduma za benki hiyo. Tawi hilo jipya ni mkakati wa benki hiyo kujitanua zaidi baada ya kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.
 Ofisa Huduma kwa wateja na Uendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la jipya la Mkwepu, jijini Dar es Salaam Bi Helen Muhenga (Kushoto) akimkaribisha mmoja wa wateja aliefika kwenye tawi hilo ili kupata huduma za benki hiyo. Tawi hilo jipya ni mkakati wa benki hiyo kujitanua zaidi baada ya kukamilisha taratibu za umiliki rasmi wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WALENGWA WA TASAF KULAZIMISHWA KUCHANGIA BIMA ZA AFYA NA MICHANGO YA KIJAMII

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Mhe. Omary Ahmed Badwel Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vyote nchini. 

Na. Aaron Mrikaria-Dodoma

Serikali imewaagiza Viongozi wa Vijiji kutowalazimisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kukatwa ruzuku kwa ajili ya kuchangia bima za afya na michango mbalimbali ya kijamii kwani ruzuku hiyo hutolewa na Serikali kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

Agizo hilo limetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Mhe. Omary Ahmed Badwel aliyetaka kujua Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vyote nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, ruzuku inayotolewa na Serikali kwa walengwa ni kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula, gharama za elimu na Afya na kuwekeza katika kuanzisha miradi itakayowaongezea kipato na hatimaye kujikwamua na umaskini, hivyo ni maamuzi ya kaya husika kupanga matumizi ya ruzuku wanayoipata.

“Katika baadhi ya maeneo, Viongozi wa Vijiji wamekuwa wakiwalazimisha walengwa kukatwa ruzuku ili kulipia bima za afya na michango mbalimbali jambo ambalo si sahihi na halikubaliki”, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameelekeza walengwa kutokatwa ruzuku moja kwa moja bila ridhaa yao bali wapewe stahiki zao na kama kuna michango ya shughuli za maendeleo ya kijiji inapaswa kutozwa kwa wananchi wote wa kijiji husika. 

Dkt. Mwanjelwa amewataka viongozi wote waliokuwa wanatoa amri ya kukatwa kwa ruzuku za walengwa wa TASAF moja kwa moja bila ridhaa yao, waache mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu na iwapo wataendelea, Serikali itawachukulia hatua za kali za kinidhamu na kisheria. 

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini tangu uanze kutekelezwa na Serikali mwaka 2013 umezinufaisha kaya maskini kwa asilimia 70, na hivi sasa Serikali inajiandaa kuanza utekelezaji wa Awamu ya Tatu sehemu ya pili mwishoni mwa mwaka huu baada ya Serikali kupata fedha lengo likiwa ni kuzifikia kaya zote maskini nchini. 

SEKTA YA NGOZI, NYAMA NA MAZIWA ZAUNDIWA KOZI FUPI VYUONI

$
0
0
Na. Edward Kondela

Serikali imewataka wadau kwenye sekta ya ngozi, nyama na maziwa wanaoandaa mitaala kwa ajili ya vyuo kufundisha kozi fupi katika sekta hizo ngazi ya cheti na diploma kupitisha mitaala bora itakayohakikisha wanafunzi watakaohitimu mafunzo wanaleta matokeo chanya katika sekta hizo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kilichowahusisha wadau katika sekta za ngozi, nyama na maziwa kutoka serikalini na taasisi binafsi Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema ili kupata malighafi bora zinazotokana na sekta ya ngozi, nyama na maziwa ni lazima wataalam ambao wamesomea sekta hizo ngazi ya cheti na diploma wawekewe mazingira ya kuhakikisha wanatumia utaalam watakaoupata kupitia vyuo mbalimbali baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo ili iwe na tija kwa taifa.

“Mitaala mnayokwenda kupitia na kuzungumzia lazima ijibu mahitaji ya wadau katika sekta tatu yaani ngozi, nyama na maziwa isiwe kuwa na cheti baada ya kuhitimu mafunzo ngazi ya cheti au diploma hawa wataalamu wa ngazi ya kati ndiyo wanaotegemewa kwenda kufanya kazi za vitendo, hakikisheni mnapata mitaala ambayo itakuwa na manufaa.” Amesema Prof. Gabriel

Aidha Prof. Gabriel amewataka wadau hao kubainisha njia bora za kufundishia mara baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo ili kuhakikisha wanafunzi watakaodahiliwa wanaelewa vizuri pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa kuwapata watu ambao wanafundishika na wawe tayari kupokea mafunzo hayo.

Akibainisha juu ya jamii kuwa na ufugaji wenye tija, katibu mkuu huyo amewaasa wadau wa mifugo wajenge utamaduni wa kuwatumia wataalam hususan wa ngazi ya kati ili waweze kufuga kisasa na kunufaika kupitia mifugo yao badala ya kufuga kwa mazoea na hatimaye kupata hasara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti, Ugani na Mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa amesema mjadala wa kuandaa mitaala kwa ajili ya kufundisha vyuoni kozi fupi katika ngazi ya cheti na diploma kwenye kwenye sekta ya ngozi, nyama na maziwa umetoka kwa wadau, hivyo wizara ikashirikisha taasisi mbalimbali likiwemo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kukamilisha mitaala hiyo.

Dkt. Mwilawa amefafanua kuwa mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kuandaa mitaala hiyo vyuo vya serikali kwa kushirikiana na binafsi vitaanza kutekeleza kwa kutoa mafunzo ya tasnia ya ngozi, nyama na maziwa katika ngazi ya cheti na diploma.

Akielezea umuhimu wa serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuandaa mitaala hiyo, Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuhakikisha sekta ya mifugo inasimamiwa vyema kupitia mambo ya kisera na kisheria ambayo ndiyo yamekuwa yakisimamia pamoja na kutunga kanuni mpya zenye lengo la kuhakikisha sekta ya mifugo inathaminiwa zaidi.

Bw. Makoye amesema sekta ya mifugo ambayo inaajiri watu wengi kote nchini kupitia mafunzo yatakayoanza kutolewa vyuoni mara baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza thamani ya sekta ya ngozi, nyama na maziwa kwa kuwa wafugaji sasa wataongezewa taarifa na maarifa kupitia kwa wataalamu watakaohitimu mafunzo hayo.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya ngozi, nyama na maziwa pamoja na taasisi mbalimbali likiwemo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) inapitia mitaala kwa ajili ya kuanzishwa kwa kozi fupi ngazi ya cheti na diploma katika sekta hizo kwenye vyuo vya serikali na binafsi ili kuyaongezea thamani zaidi mazao ya ngozi, nyama na maziwa kwa kuwa na waatalamu wengi zaidi ngazi ya kati walipobobea katika sekta za ngozi, nyama na maziwa.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kikao cha wadau sekta ya ngozi, nyama na maziwa kujadili umahiri wa mitaala ya sekta hiyo ngazi ya cheti na diploma jijini Dodo
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafugaji ambao ni sehemu ya wadau wa sekta ya ngozi, nyama na maziwa ambao wameshiriki kwenye k
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa sekta ya ngozi, nyama na maziwa mara baada ya kufungua kikao kujadili umahiri wa mitaala ya sekt

DKT.ABBASI: SERIKALI IMEWEKA MIFUMO IMARA YA KITAASISI NA KISHERIA INAYOCHOCHEA MAENDELEO ENDELEVU KWA WATANZANIA

$
0
0

SERIKALI imesema imeweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria inayohakikiwa kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na itakayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea kuleta manufaa endelevu kwa faida ya Watanzania wote.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Vyombo vya Habari aliozungumzia kuhusiana na tathimini ya miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Abbasi alisema yapo mambo mengi na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na itakayotekelezwa na Serikali ya Awamu hivyo ili kuwezesha mafanikio yake yanaleta matokeo chanya kwa Watanzania na jamii kwa ujumla, Serikali imeweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria kwa ajili ya kulinda mafanikio hayo hata baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kumaliza muda wake.

‘‘Tanzania kwa sasa ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano tumeweza kufanya mambo mengi ikiwemo suala la rushwa ambalo limekuwa kero kubwa kwa Watanzania na hilo kwa sasa tumeunda Mahakama maalum ya Mafisadi ambayo tayari imesikiliza kesi zaidi ya 50’’ alisema Dkt. Abbasi.

Aidha aliongeza zipo ahadi za utelezaji wa miradi na mipango mbalimbali ya Serikali iliyoahidiwa kufanywa na Rais Dkt. John Magufuli ambayo awali ilikuwa ikileta kero na kuchelewesha maendeleo ya Watanzania, ambapo ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano yameweza kutekelezwa.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi alisema ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali ya Awamu ya Tano imeweza kutimiza ahadi mbalimbali ambazo tayari zimeanza kuleta matokeo chanya kwa Watanzania ikiwemo ununuzi wa ndege za Serikali ambapo awali jambo hilo lilikuwa na ugumu katika utekezaji wake.

‘Jambo jingine ni suala la kuhamia Dodoma, jambo hili kwa sasa si ndoto tena kwani kwa sasa asilimia 90 ya watumishi wa Serikali katika Wizara na baadhi ya Idara, Taasisi na Wakala za Serikali wamehamia Dodoma na Serikali imeweza msingi wa kisheria wa kuitangaza Dodoma kuwa ni makao makuu ya Serikali’’ alisema Dkt. Abbasi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema ili maendeleo hayo yazidi kuleta manufaa endelevu kwa vizazi vijavyo, Watanzania hawana budi kuwa wazalendo na kuwa walinzi wa mali za umma na kutoa taarifa katika mamlaka za serikali kuhusu uharibifu na ubadhirifu unaofanywa na mtu au kikundi chochote katika jamii.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema Serikali ya Awamu ya Tano kupitia ushirikiano wake na wananchi imeweza kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, maji, elimu na barabara, ambayo imeendelea kuwagusa wananchi wengi zaidi hususani wa kipato cha chini.

Akitolea mfano, Dkt. Abbasi alisema Serikali inatekeleza miradi ya maji 1600 nchi nzima ikiwemo miradi 300 inayotekelezwa katika maeneo ya vijijini na kutumia kiasi cha Tsh Bilioni 700 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo katika maeneo ya mijini ili kuhakikisha kuwa inafikia kiwango cha asilimia 85 vijijini na asilimia 95 maeneo ya mijini ifikapo mwaka 2020.

Kuhusu sekta ya afya, Dkt. Abbasi alisema Serikali kwa sasa imeendelea kuimarisha sekta hiyo kwani kwa sasa Tanzania imekuwa nchi mfadhili kwa kuweza kufanya huduma mbalimbali za kibingwa ambazo zilikuwa zikifanyika nje ya nchi na kuifanya Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha fedha za Watanzania.

‘Ndani ya kipindi cha miaka minne Serikali imeweza kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Tsh Bilioni 31 mwaka 2014/15 hadi kufikia Bilioni 270, na pia kuajiri waganga wataalamu zaidi ya 6000 wanaohudumia wagonjwa katika hospitali zetu za Mikoa, Wilaya, Vituo vya Afya katika Kata na Zahanati katika maeneo ya vijijini’’ alisema Dkt. Abbasi. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani), kuhusu tathimini ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019) Jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza Jambo kwa  Waandishi wa Habari (Hawapo pichani), kuhusu tathimini ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019) Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu tathimini ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019), Jijini Dar es Salaam.



 Waandishi wa Habari wakitekeleza majukumu yao katika Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, kuhusu miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019), Jijini Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.

 

(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).



27 WAITWA TAIFA STARS, KUKIPIGA NA EQUATORIAL GUINEA NOVEMBA 15

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA Mkuu wa Timu ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije ameteua kikosi cha wachezaji 27 kitakachochea mcheo wa kwanza wa kufuzu mataifa Afrika (AFCON) 2021.

Ndayiragije ametangaa kikosi hico leo kitachoingia kambini mwishoni mwa wiki kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Equatorial Guinea Novemba 15 utakaochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Kikosi hicho kitawajumisha na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania akiwemo Mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta, Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya nchini Morocco Simon Msuva, Kiungo wa Tenerrife ya Hispania Farid Mussa. Beki wa Kulia wa Nkana ya nchini Zambia Hassan Kessy , David Kisu (Gor Mahia )na Eliuter Mpepo kutoka Buildcon Zambia.

Wachezaji wengine ni Magolikpa Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga) na mabeki ni Salum Kimenya (TZ Prisons), Mohamed Hussein (Simba), Gadriel Michael (Simba), Erasto Nyoni (Simba)Bakari Nondo (Coastal Union), Kelvin Yondani (Yanga), Dickson Job (Mtibwa).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Abdul Aziz Makame (Yanga), Iddi Suleimani (Azam), Salum Abubakar (Azam),  Mzamiru Yassin (Simba), Frank Domayo (Azam), Miraji Athuman (Simba), Hassan Dilunga (Simba).

Kwa upande wa safu ya usambuliaji wenine ni Ditram Nchimbi (Polisi TZ), Shaban Iddi (Azam),Kelvin John ( Football House) na Ayoub Lyanga (Coastal Union).

Taifa Stars ina kibarua cha kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza ili kuanza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenda AFCON 2021.

MIAKA 4 YA RAIS MAGUFULI IKULU

$
0
0

Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza miaka 4 tangu achaguliwe kuwa Rais.

Naam! Ni miaka 4 ya Rais Magufuli Ikulu ambapo sote mashuhuda wa haya:-

1. Ameisimamia na kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha amani na usalama wa nchi unazidi kuimarika. Amekomesha kabisa matukio aliyokutana nayo awali anaingia madarakani ya ujambazi, migomo na mauaji ndani ya jamii. Hata Umoja wa Mataifa (UN) ulishampongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kudumisha amani na usalama ndani na nje ya Tanzania.

2. Amekuwa Mlezi na msaada kwa Watoto wa Watanzania wanyonge ambapo Serikali yake imewawezesha kusoma elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne. Zaidi ya Tsh. Bilioni 937 zimetumika tangu mwaka 2016.

3. Ameonyesha kivitendo kuchukia na kukemea rushwa na ufisadi nchini. Ambapo leo nchi ya Tanzania inashika nafasi ya pili (2) kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

4. Ametekeleza kivitendo ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kuhamia Dodoma. Leo hii Serikali nzima mpaka yeye Rais Magufuli amehamia Dodoma, makao makuu ya nchi.

5. Ameongeza na kusimamia mapato ya nchi kutoka wastanj wa makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia wastani wa makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.7

6. Rais Magufuli amejipambanua kivitendo juu ya sera ya Tanzania ya viwanda ambapo ndani ya miaka 4 zaidi ya viwanda vikubwa na vidogo 4000 vimejengwa.

7. Uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma umeongezeka na kuimarika sana. Hakuna majivuno, uchelewaji makazini, ugoigoi badalq yake huduma kwenye ofisi za umma zimeimarika sana.

8. Rais Magufuli amesimama kidete kufufua mashirika yetu ya umma ambayo yalikuwa hoi bin taabani. Leo hii shirika la simu Tanzania limefufuka; Shirika la ndege nchini ATCL nalo pia limefufuka kwa kununuliwa ndege mpya 7 za kisasa na nyingine 4 zimeagizwa. Nani kama Rais Magufuli?

9. Serikali imeanzisha na kufanya miradi mikubwa ya kimkakati nchini. Mathalani ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme kwa kiwango cha standard gauge unaogharimu zaidi ya Trilioni 7.1; Mradi wa ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha Megawatts 2115; Ujenzi wa flyovers Tazara,  Ubungo na sealander.

10. Kwa mara ya kwanza tangu Dunia iumbwe tumeshuhudia uwazi kwenye mikataba ya madini na maboresho ya Sheria za madini kulinufaisha Taifa. Hii imeleta matokeo chanya ya ongezeko la makusanyo yatokanayo na madini kupitia mfumo mpya wa uuzaji na ununuzi kwenye masoko ya madini. Leo hii wawekezaji wa madini wanabanwa na tija ya mapato imeongezeka. 

11. Ukuaji wa uchumi umezidi kuongezeka kwa kasi kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2015 hadi kufikia ukuaji wa asilimia 7.2 mpaka sasa. Ukuaji huu unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Barani Afrika kwa kasi ya ukuaji kiuchumi.

12. Ujenzi wa hospitali 73 za wilaya na vituo vya afya zaidi ya 352 nchini vinavyotoa huduma ya upasuaji. Ujenzi huo umeenda sanjali na uimarushwaji wa vifaa tiba vya kisasa na Madaktari wa kutosha. Leo hii upasuaji mkubwa na tiba kubwa ambazo awali ilikuwa zinapatikana nje ya nchi sasa zinafanyika nchini.

Hakika ni miaka 4 ya uchapakazi, uzalendo, ufuatiliaji na uadilifu katika ujenzi na uletaji matokeo chanya kwa Taifa. Watanzania tumekuelewa, tunakushukuru na tupo pamoja kwani Tanzania moya tunaiona na tunaiishi ndani ya miaka 4 ya uongozi wako. 

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais Magufuli kwa kumpatia ulinzi, afya njema na maarifa zaidi.

*Shilatu E.J*
0767488622

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA ZBC REDIO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akizungumza Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Utangazji la ZBC Redio katika Ukumbi wa jengo la zamani la utangazji Rahaleo Mjini Zanzibar leo ambapo mkutano ulizungumzia masuala mbali mbali ya kiutendaji (kulia) Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo na (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Utangazaji la ZBC Nd,Chande Omar Omar ,[Picha na Ikulu] 06/11/2019.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee alipokuwa akitoa ufafanuzi na majibu ya masuala mbali mbali yaliyoulizwa katika mkutano wa Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Utangazaji la ZBC Redio na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,uliofanyika leo katila ukumbi wa jengo la zamani la utangazji Rahaleo Mjini Zanzibar, [Picha na Ikulu] 06/11/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Utangazaji la ZBC Nd,Chande Omar Omar alipowasili katika Ukumbi wa jengo la zamani la utangazji Rahaleo Mjini Zanzibar katika mkutano na Wafanyakazi wa ZBC Redio uliofanyika leo,[Picha na Ikulu] 06/11/2019.
Mtangazji wa Habari wa Shirika la Habari la Utangazji la ZBC Redio Khadija Ali Hassan alipokuwa akiuliza suala wakati wa Wafanyakazi wa Shirika hilo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) uliofanyika leo katika ukumbi wa jengo la zamani la utangazji Rahaleo Mjini Zanzibar, [Picha na Ikulu] 06/11/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akizungumza Wafanyakazi wa Shirika la Habari la Utangazji la ZBC Redio katika Ukumbi wa jengo la zamani la utangazji Rahaleo Mjini Zanzibar leo ambapo mkutano ulizungumzia masuala mbali mbali ya kiutendaji (kulia) Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo,[Picha na Ikulu] 06/11/2019.

WIZARA YAIPELEKA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA KWA WADAU

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati timu hiyo ilipofika mkoani hapo kwa lengo la kukisanya maoni kutoka kwa wadau wa Maendeleo ya Waanwake na Jinsia katika kuboresha Sera yao.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango sehemu ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sophina Mjangu akitoa maneno ya awali kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia mkoani Singida.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu akifafanua jambo katika kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia mkoani Singida.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Singida ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Bw. Stanslaus Choaji akifungua kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia mkoani Singida.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

*************************************

Na Mwandishi Wetu Singida

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeamua kufanya tathimini ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 200 na Mkakati wa utekelezaji wa mwaka 2005 ili tathimini hiyo isaidie kufanya mapitio ya Sera itakayozingatia makubaliano ya mikataba mbalimbali, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano na maoni ya wadau.

Haya yameelezwa leo mkoani Singida na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango sehemu ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sophina Mjangu wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa maendeleo ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Singida, Dodoma na Tabora na Wizara.

Bi. Sophina amesema kuwa madhumuni ya Sera iliyopo yalikuwa ni kutoa mwelekeo ambao ungehakikisha kuwa mipango, Mikakati na shughuli mbalimbali za uongozi na maendeleo katika kila Sekta na Taasisi inazingatia usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa lengo kuu la kupitia Sera hiyo ni kuifanya iendane na wakati na iwezi kubeba mabadiliko yaliyojitokeza katika miaka kumi na tisa tangu kandaliwa kwake mwaka 2000 ikiwemo changamoto katika utekelezaji wa Sera hii ikiwemo mapungufu yake na nini kifanyike ili kuiboresha Sera ili kueandana na wakati husika.

“Hii itatokana na maoni ya wadau tutakayoyapata inawezekana ikawa mpya au tukabadilisha na jina la Sera ili tunawasikiliza wadau ili nadhani yote yanawezekana” alisema Bi. Sophina

Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Bw. Stanslaus Choaji amesema kuwa Kikao hicho kinatarajia kufikia malengo ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususan katika Sekta ya Afya, Elimu, Kilimo na Masuala ya kifedha, uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira na Uzazi na Afya ya Mtoto na kukusanya Taarifa na Takwimu zitakazowezesha kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia.

Ameongeza kuwa kikao kazi hicho kitawezesha kukusanya maoni yatayowezesha kuwa na Sera Shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu na kupata uelewa wa pamoja kuhusu wajibu wa Serikali na wadau katika uwepo wa Sera ya maendeleo ya Wanawake na Jinsia .

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Singida Bw. Jonathan Simiti amesema kuwa Sera hiyo inatakiwa kufanyiwa maboresho ingawa kuna juhudi za Serikali katika kuondokana na Unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi kwa hivyo Sera isaidie wanawake kuwezeshwa katika kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.

“Nimesikia kwenye redio kuwa wanawake sasa wanaendesha magari makubwa kama malori na mabasi ya abiria masuala ya kijinsia yamekuwa kwa kiasi kikubwa nchini ukilinganisha na wakati uliopita” alisema Bw. Simiti.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Singida Bi. Shukranui Mbago amesema kuwa Sera iliyopo ni nzuri na inatekelezeka ingawa kuna mambo muhimu yanatakiwa kuingizwa ikiwemo umiliki wa mali na kutoa maamuzi kwa watoto wa kike na wanawake katika ngazi ya Kata.

“Unakuta Mwanamke au mtoto wa kike anatafuta pesa lakini kwa asilimia kubwa zinamilikiwa na wanaume na watoto wa kiume tunahitaji Sera isisitize umiliki wa mali na utoaji wa maamuzi hasa katika Kaya kwa mtoto wa kike na mwanamke” alisema Bi. Shukrani.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo katika machakato wa kukusanya maoni kwa wadau kutoka Kanda saba za Tanzania Bara ili kuwezesha maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000.

Tigo inavyorejesha tabasamu kwa wagonjwa wa mguu kifundo.

$
0
0





Mkurugenzi mtendaji (Tigo) Bw. Simon Karikari akimkabidhi mfano wa hundi ya Mil 110/- Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi.Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT

Siku zote ni furaha pale mwanamke anapopata mtoto ambaye alimtarajia kwa takribani miezi tisa ya ujauzito.Hii ilidhihirika kwa Salma Hajj (29) baada ya kujifungua salama mtoto wake wa kwanza wa kiume miezi kumi iliyopita.


Hatahivyo, furaha ya Salma haikudumu.Baada ya muda mfupi, Salma ambaye ni mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam furaha yake ilitokweka baada ya kugundua kuwa mwanae wa huyo alikuwa na tatizo la miguu kujikunja pasipo kujua ni nini tatizo.

Tatizo hilo linajulikana kama ‘mguu kifundo’ au kwa kiingereza linafahamika kama ‘Clubfoot’ ambalo kisayansi linalotokea hata kabla ya mtoto kuzaliwa.

Kila mwaka zaidi ya watoto 100,000 duniani huzaliwa na ugonjwa huu ambao humfanya mtoto kushindwa kutembea kwa kutumia unyayo na badala yake hutumia kifundo cha mguu.

Kwa Tanzania,inakadiriwa kuwa karibuni watoto 2,800 wanazaliwa na ugonjwa huu kila mwaka.Kati yao asilimia 50 wana athirika mguu mmoja huku waliobaki wakiathirwa miguu yote miwili.


Asilimia 80 ya wagonjwa wasiopata matibabu yake wanapatikana kwenye nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania.Kama ugonjwa huu usipotibika unaweza kusababisha maumivu makali wakati wa kutembea na hatimaye husababisha ulemavu wa muda mrefu.

“Kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu.Nilijisikia vibaya kwamba mwanangu hataweza kutembea vizuri na hatahivyo sikujua anasumbuliwa na tatizo gani kwa kipindi kile,” anasema Salma.

“Nilihisi kama ilikuwa mwisho wa dunia kwangu na mwanangu; nilijiuliza maswali mengi bila majibu kwamba atawezaje kutembea? ataonekanaje kwa watu? atasoma katika shule gani? nilichanganyikiwa sana,” anasema Salma.

Mmoja wa mtoa huduma (nesi) alimjulisha kuwa tatizo hilo linaweza kutibika katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam bila malipo.Kilichofuata ilikuwa ni kutembelea hospitalini hapo ambapo madaktari walianza kutoa matibabu kwa mtoto wake kwa miezi michache tu.

Kwa mujibu wa daktari wa mifupa (Orthopedic) wa CCBRT, Dk. Zainab Ilonga, anasema chanzo cha ugonjwa huo bado hakijulikani.

Anasema hadi sasa sababu yake bado haijathibitika lakini wanaamini kuwa moja ya sababu ni matumizi ya pombe na matumizi mabaya ya madawa wakati wa ujazuzito au urithi wa vinasaba (genetic) na kwamba tafiti zaidi zitasaidia kutambua chanzo halisi cha tatizo hilo.

“Kuna njia mbili za kutibu ugonjwa huu wa mguu kifundo;moja ni kutumia njia ya Ponseti ambayo haihitaji kufanya upasuaji na nyingine ya kufanya upasuaji,” Dk Ilonga anasema na kuongeza

“Kwa Tanzania tunatibu watoto takribani 400 kwa mwaka sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wote na hii inatokana na baadhi ya wazazi kuwanawaficha watoto wenye tatizo hili.”

Ignacio V. Ponseti ni njia ambayo imekuwa ikitumia kutibu mguu kifundo tangu miaka ya 1940.Moja ya kanuni ya njia hii ni kwamba tishu za mtoto ikiwamo tendoni, ligamenti na maungio yake yapo katika hatua ya ukuaji hivyo kufanya mguu kuungana baada ya kila wiki moja.

Kwa kutumia njia hii ndani ya wiki kadhaa hali ya mgonjwa inaweza kubadilika na kufanikisha kurekebisha mguu bila uhitaji wa kufanya upasuaji.Mtoto wa Salma alipitia hatua hiyo maarufu kama ‘gentle bone manipulations’ na ufuatiliaji (castings) ili kujua mabadiliko ya kibaolojia hasa misuli yake, maungio na tishu kwa lengo la kutibu tatizo alilokuwa nalo.

“Kuna wakati alikuwa anapitia wakati mgumu kwani alikuwa analia sana jambo lililonifanya na mimi kulia.Nilikuwa na wasiwasi juu ya maisha ya mwanangu siku za mbeleni,” anasema kwa huzuni.

“Nawashukuru sana Tigo na madaktari wa CCBRT kwa msaada wao mkubwa kwasababu saizi mtoto wangu ana miezi kumi na amepona kabisa,” anasema Salma huku akiwa na uso wa furaha.

Afisa wa Uwajibikaji kwa Jamii wa Tigo, Halima Okash anasema “Tuliona kuna umuhimu wa kusaidia wahitaji hawa kwasabau CCBRT inahudumia jamii yenye uhitaji na wasiojiweza katika kuwasaidia kupata huduma za matibabu.Tumeunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na CCBRT kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata nafasi ya kutibiwa kwa gharama ndogo au bure kabisa,” anasema Okash.

Kupitia huduma za upasuaji kutoka hospitali ya CCBRT jumla ya watoto 1,509 wamenufaika katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

“Haya ni mafanikio yanayotufanya sisi Tigo kujisikia faraja kwa kiasi kikubwa kwani kwa kutoa matibabu kwa watu wenye ulemavu,Tigo na CCBRT tunaleta matokeo chanya kwa maisha ya mtu mmoja mmoja, familia na jamii ya Tanzania kwa ujumla,” anasema Okash.

Tangu mwaka 2013, Tigo iliingia ubia na hospitali ya CCBRT kutoa matibabu kwa wagonjwa wa midomo sungura, kwa kutumia njia ya jumbe (SMS) zinazotumwa kwa wagonjwa wa CCBRT kuwakumumbusha kufuatilia matibabu na kutoa uelewa kuhusu huduma kwa umma.

Kupitia mpango huu, wagonjwa wanaweza kupata jumbe za matibabu kwa siku nne na siku moja kabla ya siku ya matibabu na hii imeisaidia CCBRT kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokatisha matibabu.

Kwa msaada wa Sh110, 0000,000 kwa mwaka kutoka Tigo, CCBRT inaweza kutoa huduma za matibabu kwa njia Ponseti (bila upasuaji) kwa wagonjwa wapya zaidi ya 400 na wengine wanaoendelea na matibabu hospitalini hapo.

Mhandisi Nyamhanga: Simamieni Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019

$
0
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga 


Na. Angela Msambira Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka viongozi na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu Kanuni, Sheria, na Miongozo mbalimbali iliyowekwa ili uchaguzi huo ufanyike katika mazingira ya amani na uwe huru na haki.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akielezea hatua inayofuata baada ya zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kukamilika hapo jana ambapo amesema zoezi linaloendelea kwa tarehe 5 Novemba, 2019 ni Uteuzi wa Wagombea katika nafasi za Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa na nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.

Amesema kuwa kuanzia tarehe 5 hadi 6 Novemba, 2019 ni kipindi cha watu walioomba kuteuliwa kuwa wagombea au wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ambao hawajaridhika na uteuzi uliofanywa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuwasilisha pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea.

“Nitoe maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kusimamia kwa weledi zoezi la uwasilishaji wa pingamizi na kutoa uamuzi wa haki kuhusu pingamizi hizo za uteuzi wa wagombea” amesisitiza Katibu mkuu.

Mhandisi Nyamhanga ameseama kwamba baada ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kupokea pingamizi na kutoa uamuzi, waombaji au wagombea ambao hawataridhika na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watakuwa na haki ya kukata rufaa kati ya tarehe 5 hadi 8 Novemba, 2019 kwenye Kamati za Rufani zilizoanzishwa katika kila Wilaya nchini.

Aidha, Kamati za Rufani zitatoa uamuzi kuhusu rufaa mbalimbali zilizowasilishwa kwake kati ya tarehe 5 na 9 Novemba, 2019. Vilevile, mtu yeyote ambaye ameomba kuteuliwa kuwa mgombea au mgombea ambaye hajaridhika na uamuzi wa Kamati ya Rufani atakuwa na haki ya kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ndani ya muda wa siku 30 baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Mhandisi Nyamhanga amevikumbusha Vyama vya Siasa ambavyo vitashiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 kuhakikisha vinawasilisha ratiba za mikutano ya kampeni kwa Wasimamizi wa Uchaguzi tarehe 10 Novemba, 2019 kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA YAKE MZEE BAKARI MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika mazishi ya marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa , Novemba 6, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIKAO KAZI CHA WADAU KUHUSU TATHMINI NA MAPITIO YA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA 2000 NA MKAKATI WA UTEKELEZAJI 2005 CHAFANYIKA SINGIDA

$
0
0
Katibu Tawala Msaidizi Uzalishaji, Beatus Choata (katikati), akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu tathimini na mapitio ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya 2000 na mkakati wa utekelezaji 2005 kilichoanza mkoani Singida leo kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa . Kutoka kulia ni Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Emmanuel Achayo, Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Profesa Lindah Mhando, Mkugenzi Msaidizi Sehemu ya Sera Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sophina Mjangu na Mratibu wa kikao hicho, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa wizara hiyo, Hanifa Selengu.
Wadau wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Sera Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sophina Mjangu, akizungumza katika kikao hicho.
Wadau wakiwa katika kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wadau wakiwa katika kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Profesa Lindah Mhando, akizungumza.
Mtaalamu Muelekezi wa Sera, Emmanuel Achayo, akizungumza.
Mratibu wa kikao hicho, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa wizara hiyo, Hanifa Selengu, akizungumza.
Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washiriki wa kikao hicho kutoka Mkoa wa Tabora wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.



Na Dotto Mwaibale, Singida 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeanza kufanya kikao cha tathmini kwa kupitia upya sera ya usawa wa wanawake na jinsia ili kuangalia utekelezwaji wa sera hiyo hapa nchini ambapo kikao hicho kimeanza kwa mikoa ya kanda ya kati, Singida, Tabora na Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu tathmini na mapitio ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia, Katibu Tawala Msaidizi Uzalishaji Mkoa wa Singida, Choata Beatus kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa huo, alisema wizara iko katika mchakato wa kufanya tathimini na mapitio ya sera ya maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2000 na mkakati wa utekelezaji wa 2005 .

Beatus alisema mchakato huo unahusisha na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika ngazi zote ili kuwezesha kuwa na sera shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu. 

"Mchakato huu utafanyika katika kanda saba, kanda hizo ni kanda ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini, Mashariki, Kanda ya Ziwa, Kusini, Magharibi na Kanda ya Kati ambapo tumeufungua rasmi leo hii ".alisema Beatus. 

Alisema lengo la kikao hicho ni kupata taarifa na takwimu kuhusu utekelezaji wa masuala ya usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususani katika sekta ya afya, elimu, kilimo, masuala ya kifedha, pamoja na uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira, uzazi na afya ya mtoto.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Jonathan Semiti alisema licha ya mkoa kutekeleza sera hiyo bado kuna haja ya wadau kutoa mapendekezo pale ambapo mwanamke hajapatiwa nafasi katika jamii. 

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Jane Chalamila alisema mwanamke bado hajapewa nafasi ya kushiriki katika uongozi, kutoa maamuzi ngazi za kijamii hivyo kupitia kikao hicho cha wadau kitaibua masuala mbalimbali yatakayomwezesha kushirikishwa.

18 KORTINI KWA KUFANYA KAZI BILA KUSAJILIWA NA PSPTB

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
WATU 18 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na shitaka moja la kufanya kazi za ununuzi na ugavi bila ya kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na  Mwanasheria wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Suleiman Mnzava amewataja washtakiwa hao kuwa ni Jema Mbugi, Julieth Daniel, Jeremiah Mafuru, Lucy Wanne, Odillo Benedict, Bibiana Romanus, Bahati Wonnandi, Raphael Waryana, Joseph Mhere na Victor Kilonzo, Moshi Mohamed, Avitus Rutayuga, Esther Reyemamu, Ruth Mwaipyana, Beatrice Mushi, Julieth Mwihambi, Geogre Lyimo na Estonia Kalokola.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Hudi Hudi imedaiwa kuwa kati ya Februari 11 na 15, 2019, katika ofisi mbalimbali jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walikutwa wakifanya kazi za ununuzi na ugavi bila ya kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Aidha, upande wa mashtaka umeiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa washtakiwa Mehere, Mohamed, Mwaipyana na Mwihambi ambao hawakuwepo mahakamani hapo leo. Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai kuwa hauna pingamizi la dhamana dhidi ya washtakiwa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo ameiomba mahakama ipange tarehe nyingine ili washtakiwa hao waweze kusomewe maelezo ya awali.

Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama iliwataka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa na awe na kitambulisho cha Taifa. Pia ametakiwa kusaini bondi ya Shilingi Milioni 5 kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 21, 2019 kwa ajili ya kutajwa.
  Baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wanafanyakazi za ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakitoka kwenye chumba cha mahakama ya Kinondoni mara baada ya kufikishwa na Bodi hiyo.
Mwanasheria wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Suleiman Mnzava akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapandisha kizimbani wafanyakazi waliokuwa wanafanyakazi za ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na bodi hiyo leo katika mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images