Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

MBUNGE KINGU AKUTANA NA MABALOZI JIMBONI NA KUZUNGUMZA NAO

$
0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akizungumza na mabalozi wa Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi hao.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ameendelea na ziara ya kukutana na wajumbe wa nyumba kumi (Mabalozi) katika jimbo hilo kwa ajili ya kuzungumza nao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Katika ziara hiyo Kingu amekuwa akikutana na mabalozi, wazee na wajumbe wa jumuia zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya nao mazungumzo ya kuimarisha chama hicho na kusikiliza changamoto zilizopo na kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungunza na mabalozi wa Kata ya Minyughe aliwataka kudumisha mshikamano na kuondoa tofauti zao kama zipo ili kukipa ushindi mnono chama hicho katika uchaguzi huo.

" Sina wasiwasi kwa hapa Minyughe najua mpo vizuri hamna migogoro kama ilivyo katika maeneo mengine ninawaamini na viongozi wenu wamejipanga kukupigania chama chetu" alisema Kingu.

Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Issa Mussa Mkuki alitoa onyo kwa wanachama wa chama hicho ambao watabainika kukisaliti katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi." Mwanachama wetu yeyote atakaye tusaliti hatuta mvumilia tutamchukulia hatua za kinidhamu" alisema Mkuki.

Kingu ameendelea kufanya ziara katika jimbo hilo ambapo jana alikutana na wazee pamoja na vijana wa Kata ya Puma na kuzungumza nao.

NANDY ALIPEWA ‘SHAVU’ NIGERIA AKAKATAA.

$
0
0

Anyakua tunzo Marekani

Na: Moshy Kiyungi,Tabora

Novemba, 2019.

Kama Nandy angelikuwa limbukeni katika maisha, leo hii asingelikuwepo katika ardhi ya Tanzania. Alikataa ofa ya kubakia nchini Nigeria ambako aliahidiwa kuingia mkataba katika lebo ya Chocolate City na kufanya kazi nchini humo.

Tukio hilo lilijiri baada ya kuwa mshindi wa pili katika Shindano la Karaoke Barani Afrika la Tecno Own The Stage, lililofanyika Februari 2016 Lagos nchini Nigeria.

Katika shindano hilo Nandy, alijizolea shilingi milioni 36, pia kuahidiwa kuingia katika lebo kubwa nchini Nigeria ya Chocolate City na kufanya kazi huko lakini alikataa.

Kwa Uzalendo wake uliotukuka, aliamua kurudi nyumbani na kwenda kujiunga katika Jumba la Vipaji Tanzania House of Talents (THT) ambako yupo nao hadi sasa.

Nandy amedhihirisha kuwa kipaji chake siyo cha kubahatisha, Oktoba 2019 ameshinda tena tuzo nyingine kupitia kipengele cha The Best Female in East, South and North Africa, iliyotolewa Oktoba 20, 2019 na African Entertainment Awards USA (AEAUSA) nchini Marekani.

Nandy anaendelea kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva pamoja na uigizaji, ambapo yaelezwa kuwa ni miongoni mwa wasanii wa kike waliopo kwenye chati kwa sasa.

Mara baada ya kuzaliwa mjini Moshi, wazazi wake Bi. Mary Charles, ambaye ni fundi wa kushona na Mzee Charles Mfinanga, ambaye ni fundi makenika, walimpa jina la Faustina.

Lakini kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, wanamtambua kama Nandy a.k.a African Princess.Jina la Nandy ni kifupi cha jina lake halisi Nandera.

Alianza kutumbuiza muziki akiwa na umri mdogo kabisa wa miaka mitano.
Nandy alikuwa mwanachama hai wa kwaya ya mafunzo ya Jumapili ya Kanisa la KKKT huko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mawenzi, baadaye kajiunga Lomwe High School ambako huko alikuwa mwanakwaya mkuu katika shule hiyo.Baada ya kumaliza elimu ya juu alijiunga na Chuo cha Biashara (CBE), jijini Dar es Salaam.

Ngoma iliyomtambulisha mapema ilikuwa ni ya ‘Nagusa Gusa’ ambayo remix yake alimshirikisha msanii Mr. Blue.Msanii huyo licha ya kuimba, ni mwigizaji anayekuja juu katika anga za filamu.

Hivi sasa anaonekana akiigiza katika tamthiria ya Huba, inayooneshwa katika kituo kimojawapo cha luninga nchini.Licha ya kufanya muziki na kuigiza, Nandy ni bonge la dizaina. Ameweza kuwavalisha mastaa wengi wa Bongo Movie.

Yaelezwa kuwa mavazi yake yote anayoonekana amevaa ya asili, huwa anayabuni mwenyewe na kushona.Miongoni mwa watu maarufu aliyewahi kupata ofa ya kubuniwa mavazi ni Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.


Milioni 36 zamtoa.

Kati ya vitu anavyojivunia kupitia kipaji chake ni pale alipokuwa mshindi wa pili katika shindano la Karaoke, akajipatia shilingi milioni 36.

Nusu ya pesa hizo zilimuwezesha kumiliki kampuni yake ya kubuni na kutengeneza mavazi ya asili na magauni ya harusi, iitwayo Nandy African Print.

Ilikuwa atoke kwa Akili the Brain?

Kipaji chake kilikuwa kitoke kwa mara ya kwanza katika kampuni ya Akili Records, chini ya Akili The Brain.

Nandy alisema katika kuhangaika kwake kutoka kimuziki, alishawahi kufika kwenye studio ya Akili Records na kutengeneza ngoma nne.

Lakini hazikufanikiwa kutoka mpaka alipopata nafasi ya kwenda Nigeria kwenye Karaoke ya Tecno.

Mwaka wa 2017 alishinda tuzo ya All Africa Music Awards, katika kundi la wasanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.
Maisha ya awali

Nandy kazi zake zilianza kujulikana baada ya rafiki yake kumtambulisha kwa Ruge Mutahaba, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT), sasa ni marehemu.

Hako ndiko alikokutana na Ema the Boy, ambaye alimtayarishia kibao chake maarufu cha ‘Nagusagusa’, kilichotamba mno wiki tu tangu kutolewa kwake.

Mwanzoni mwa mwaka wa 2016, Nandy alishiriki kwenye mashindano ya kuimba yaliyoandaliwa na Tecno.

Shindano lilishirikisha washiriki wengine kutoka nchi nyingi za Afrika. Kipindi cha fainali kilichofanyika huko Lagos, Nigeria, Nandy aliibuka kama mshindi wa pili.

Shindano hilo lilimkuza kimuziki, hasa katika suala zima la utumbuizaji jukwaani, alipata maarifa ya muhimu kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile akina M.I Abaga, Yemi Alade na Bien wa Sauti Sol.

Mwaka wa 2017 alitoa kibao cha ‘One Day’ ambacho kilisukuma kazi yake na hatimaye kumpa nafasi kadhaa zilizomfanya kushiriki kwenye Coke Studio Africa 2017.

Mwaka huohuo Nandy akachaguliwa kwenye Tuzo za All Africa Music Awards, katika kundi la wanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki, ambapo aliibuka mshindi.

Aidha Nandy alishirikishwa na Willy Paul kutoka Kenya kutengeneza wimbo wa mwingine wa ‘Hallelujah’, ambao unapendwa na idadi kubwa ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva.

Mwaka 2018 alitoa albam ya African Princess, akafuatia kuporomosha singo zake za I'm Confident ya mwaka 2013, Nagusa gusa ya 2017, One Day ya mwaka 2017, Wasikudanye ya mwaka 2017, Kivuruge ya 2017 na Ninogeshe ya mwaka 2018.

Aidha mwanadada huyo alishirikishwa vilivyo na Nassor Isihaka a.k.a Aslay katika wimbo wa Subalkheri Mpenzi ambao ni remix.

Msanii huyo alishinda tuzo ya AFRIMA za nchini Nigeria, ambako yeye na Ali Kiba walitia fora.



Matarajio yake

Hivi karibu alitoa kibao kinanachokwenda kwa jina Mahabuba, ambacho amemshirikisha msanii mwenzake Isihaka Nassor ‘Aslay’.

Msanii huyo wa Bongo Fleva, mtunzi wa wimbo One Day, amemtaja mshindi wa tuzo ya BET kutoka label ya WCB, Rayvanny kama msanii anayetamani kufanya naye kazi kutoka ndani ya label hiyo.

Mwimbaji huyo ameeleza kuwa kwa namna anavyotazama aina ya muziki anaofanya Rayvanny na wake anaona unaendana.

“Nawaelewa wote lakini kwa haraka haraka nikipewa chance kwa mtu wa WCB kufanya naye ngoma nitafanya na Rayvanny.

Nahisi kama tuna Chemistry ile, ambayo tunaweza tukaendana, yaani ukiwasikiliza mashairi yao wewe ndio unajua unafiti wapi, kwa hiyo mimi naona kwa Rayvanny nafiti,” alitamka Nandy.

Msanii huyo Nandy ambaye kwa sasa anafanya vizuri kwa wimbo wake mpya ‘Wasikudanganye’, hajawahi kumshrikisha msanii yeyote katika nyimbo zake tangu alipotoka na ngoma yake ‘Nagusagusa’ kisha kufuatiwa na One Day.


Kwa upande wa Saida Karoli, amemtaja kuwa ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao pia anatamani kurudia nyimbo zao.

Kuhusu kufanya kazi na Saida Karoli, Nandy amesema, “natamani sana hata anipe ngoma yake ya zamani niifanyie remix na sijui ni ipi kwa sababu kafumua!, sijui nitaimbaje.

Natamani anipe nifanye verse na kama alifanya chorus ibaki pale pale, halafu mimi nirudie zile verse, I hope atakubali” amesisitiza.

Iwapo utapata kuiona Baadhi ya nyimbo za Saida Karoli ni pamoja na Kasimile Katonda, Nsenene, Karibatano na Mapenzi Kizunguzungu uliouachia Juni 2003.


Saida alitoka na albamu nyingine nzuri iliyokwenda kwa jina la Salome Maria.


Nandy alitarajia kuolewa na Ruge Mutahaba wa Clouds FM. Mpaka sasa anamkumbuka sana kwani alimtolea mahari kabla hajafa. Pole sana Nandy, Mungu atakujaalia kumpata mume mwingine.

Mwisho.

Makala hii imeandaliwa toka vyanzo mbalimbali vya habari.

Mwandaaji anapatikana kwa namba:

0784331200, 0767331200, 0736331200 na 0713331200.

RC MONGELLA AZINDUA MAADHIMISHO YA MAULID KITAIFA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) amezindua rasmi wiki ya maadhimisho ya sikukuu ya Maulid inayofanyika kitaifa jijini Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika Novemba 04, 2019 katika uwanja wa Furahisha ambapo Sikukuu ya Maulidi inatarajiwa kufanyika Novemba 09, 2019.


Sikukuu ya Maulid mara ya mwisho ilifanyika mkoani Mwanza zaidi ya miaka 20 iliyopita hivyo kufanyika mwaka huu 2019 (1441) ni neema kubwa huku jambo jema zaidi likiwa ni ushirikiano baina ya dini zote.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionesha kanga zenye ujumbe wa Maulid 2019 kama ishara ya uzinduzi wa sikukuu hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maulid.
Sheikh Issa Othuman Issa kutoka Baraza la U'lamaa BAKWATA akitoa salamu zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua Maulid 2019.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maulid kitaifa jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza (wa pili kushoto) akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI ambalo ni miongoni mwa wadau walioshiriki maonesho ya wiki ya Maulid 2019.
Tazama Video hapa chini

Nakwenda kufanya Kilimo ,Watu wa mjini wakinihitaji nitakuja- CAG Mstaafu Profesa Assad

$
0
0
CAG mpya Kichere- kazi yangu ni kulinda kihenge cha mapato ya serikali


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad amesema kuwa anakwenda kufanya kilimo kutokana na uwekezaji alioufanya katika siku hivi karibuni baada ya kustaafu nafasi hiyo watu mjini wakinihitaji nitakuja .

Profesa Assad ameyasema hayo wakati wa makabidhiano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),leo  jijini Dar es Salaam.

Profesa amesema kuwa katika kufanya kazi amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi na kumtaka CAG mpya afanye ushirikiano nao kwani watu hao wamejengwa kwa muda mrefu na sifa zote .

Assad amesema kuwa katika kufanya kazi tumejenga mahusiano na wadau mbalimbali wa nje ambao ndio watu wa kujengeana uwezo na sio kwa ndani

“Changamoto ni nyingi tumepitia lakini siwezi kutia ukakasi katika hili na watu  niliowakosea, naomba wanisamehe kwani sisi ni binadamu”amesema Profesa Assad

Kwa upande wa CAG Charles Kichere mpya amesema kuwa kazi kubwa ni kulinda kihenge anajua kazi ngumu ya ukusanyaji wa mapato.

Kichere amesema ataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu kwa kushirikiana na timu yake ya ofisi ya Taifa ya mkaguzi ikiwa na kuangalia mapato ya nchi yanatumikaje kwa kuangalia ripoti sambamba na kujenga timu imara na sio watu walisambaratika.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za ofisi CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere akizungumza mara baada ya kukabidhiwa na aliyekuwa CAG Profesa Mussa Assad katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Mpya Charles Kichere akiwa na maua mara baada ya kupokewa wakati akiwasili katika ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi ya aliyekuwa CAG Profesa Assad jijini Dar es Salaam.

BREAKING NEWZZZZZZ: ALIYEKUWA RAIS WA SIMBA AVEVA NA MAKAMU WAKE KABURU WAACHIWA HURU KWA DHAMANA

$
0
0
ALIYEKUWA  rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu, wameachiwa huru kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kutupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali kupinga 
Wasipate dhamana.

Mwakyembe akumbusha vyombo vya habari kulinda wanahabari

$
0
0
Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa kuhakikisha kuwa maisha ya wanahabari yapo salama.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akifungua kongamano la wanahabari kuhusu usalama, ikiwa ni sehemu ya siku ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari.
Alisema katika kongamano hilo linalofanyika mjini hapa kuwa Usalama kwa mwanahabari unaanzia katika chumba cha habari na chombo chake cha habari. Alisema mwanahabari anapoandika habari, ipo haja ya kuelewa kama familia yake iko vyema kiasi gani.
“Unapokaa unaandika stori, watoto kama wanaumwa … “ alisema Waziri Mwakyembe na kuongeza kuwa  ni lazima chombo cha habari kuhakikisha kwamba huyu hana shida katika kazi zake. Aidha alisema usalama huo maana yake ni mshahara wake na bima kwani hivyo viwili ndivyo vinamfanya awe na uhakika wa maisha yake na usalama wake na familia yake.
Alisema kukosekana kwa mishahara au mishahara kuwa midogo kunadhalilisha taaluma kwani mwandishi huyo anaweza kukengeuka katika kazi zake kwa sababu za bahasha. Alisema mwanahabari anapolazimika kumuomba mtoa habari fedha ni kudhalilisha taaluma.
“Mwanhabaari ambaye anaenda kazini bila uhakika wa mshahara ni tatizo. Mtu aandika habari za uchunguzi akiwa karibu ya kukamilisha ,…. Anampa kitu anachukua”  alisema Mwakyembe na kuongeza kuwa akishachukua habari ile iliyokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi inakufa.
Waziri Mwakyembe alisema mazingira hayo ya kukosekana kwa bima na mshahara kunatengeneza mazingira ya wanahabari kutokuwa wazuri katika taaluma yao.
“Mwanahabari wa leo lazima awekewe bima. Anayebisha ni nani. Si lazima kutokee machafuko. Mwanahabari huyu anaweza kusubiri kitu katika mvua mpaka akipate halafu anapata nyumonia” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kusibiri michango wakati wa kufa.
Aidha akizungumzia sheria ya habari, alisema kwamba sheria hiyo ipo kumlinda mwanahabari na kwamba zaidi ya mambo manne yanatajwa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo ambayo mpaka sasa hayajafanywa.
Alisema sheria hiyo haiwezi kuchambuliwa bila mambo manne yanayohusiana na sheria hiyo kutekelezwa.

Mambo hayo ni pamoja na uwapo wa Baraza Huru la Vyombo vya Habari, Baraza la Ithibati ambalo linatambua nani mwanahabari na kupanga kanuni, Kuanzishwa kwa kamati ya mamalalamiko ambayo ina maamuzi sawa na mahakama na kuwapo kwa mfuko wa mafunzo kwa wanahabari.
Alisema sheria imelenga taaluma ya habari kujiendesha yenyewe na bado mambo hayajakaa sawa na ikiendelea hivi lazima serikali ichukue hatua.
Aidha alisema haiwezekani kubadilishwa kwa kiwango cha elimu kwa kuwa waandishi wa habari ni walimu wa taifa na haikubaliki kuwa na walimu wasiojua kufundisha.
Alitaka kukomeshwa kwa tabia ya vyombo vya habari kutafuta makanjanja kwa kuwa wanawalipa fedha kidogo. Mwandishi wa habari mwandamizi Jesse Kwayu akitoa shukurani kwenye ufunguzi huo aliitahadharisha jamii ya wanahabari kuhusu uzingatiaji wa maadili ya taifa hili.
Pia alitioa tafakari ya mahusiano kati ya wanahabari na serikali na kusema ni vyema washirkiane kumtumikia mwananchi lakini wasiwe na urafiki wa mashaka kama kuwapo kwa shamba na mwanakondooo wakinywa maji katika kisima kimoja. Aidha alitaka usimamizi wa sheria wa umakini na usiodhuru watu wengine au kuwakandamiza.
Kila Novemba 2 ya kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari ikiwa ni kuikumbusha dunia haki ya upatikanaji wa habari na kuwalinda watoaji habari.
Sherehe hizo ambazo huadhimishwa kimataifa zina lengo la kukumbusha uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari huru kwa kuwa ni muhimu katika kukuza uelewa na kuboresha demokrasi, ikiwa ni sehemu moja muhimu ya utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia.
Katika miaka ya karibuni, kumekuwepo na matukio yanayotishia usalama wa wanahabari na vyombo vya habari na hivyo kutishia utendaji kazi wao.
Taarifa zilizopo zinaonesha kwamba wanahabari na vyombo vya habari na wale wanaosaidia wanahabari kufanyakazi zao wamekuwa wakitishiwa maisha, kushambuliwa, kufungwa, kutishiwa kukamatwa, kunyimwa haki za kukusanya habari na kushindwa kupatiwa ufumbuzi wa matukio mabaya yanayofanywa dhidi yao na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO)  Audrey Azoulay katika kipindi cha muongo mmoja (miaka 10) wanahabari 851 wameuawa na kwa mwaka huu pekee (2019) wameuawa wanahabari 44.
Pia alisema katika taarifa yake ya siku hii ya kupinga ukatili dhidi ya wanahabari, kwamba katika kila mashauri 10 ya ukatili, mashauri 9 yanayogusa wanahabari hayajapatiwa ufumbuzi.
Alisema wakati wanahabari wanahenyeka katika matukio hayo ya dhuluma jamii pia hulipa gharama kubwa kwa mateso yao. Bila kuwa na uwezo wa kulinda wanahabari hali ya jamii kuendelea kukosa taarifa muhimu zitakazowezesha kufanya maamuzi yenye  weledi hutibuka.
Bila waandishi wa habari kuwa na nafasi ya kufanyakazi zao kwa usalama, ipo hatari dunia kukosa taarifa na hivyo kuleta sintofahamu katika mambo muhimu.
Katika siku hii ni vyema dunia ikasimama na kuungana na wanahabari kwa ukweli na haki.
Kutokana na mazingira yalivyo duniani kote, UNESCO Tanzania imeandaa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania.
Kongamano hilo linalofanyika huku kauli mbiu ikiwa kuuweka ukweli hai (Keep Truith Alive) limelenga kuwezesha jamii na taifa kwa ujumla kuwa na uwezo wa kuhakikisha usalama wa wanahabari wake kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu ya dunia 16.10.1 na 10.2 yanayohusiana na usalama wa wanahabari na upatikanaji wa habari.
Kongamano hilo pia litatumika kuangalia hatua zilizofikiwa hadi sasa nchini Tanzania kufuatia maazimio ya mwaka jana; ikiwamo kujua na kuangalia na kuupitisha mfumo wa kuangalia usalama wa wanahabari nchini unaozingatia makubaliano ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
Kongamano hilo la wanahabari limewezeshwa na UNESCO kutokana na ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC) kwenye akaunti maalumu ya mradi wa uimarishaji wa mchango wa vyombo vya habari kwa maendeleo endelevu.
Mradi huo umelenga kuimarisha maarifa na uwezo wa kuangalia usalama wa wanahabari Tanzania ikiwamo ufuatiliaji wa kisheria wa matishio yaliyoripotiwa.
Washiriki wa kongamano hilo ni pamoja na Idara ya Habari (MAELEZO), Tume ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG), Jeshi la Polisi Tanzania, Jukwaa la Wahariri (TEF), Baraza la Habari (MCT), MISA Tanzania, Chama cha wanahabari wanawake Tanzania (Tamwa), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Muungano wa Radio za jamii (TADIO), Uhuru Media (public media), Mwananchi Communications (private media), Millard Ayo (online media), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) na maofisa habari wa mikoa.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akifurahi jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati walipowasili kwenye kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos wakati alipowasili kwenye kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche. 
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto).
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Nancy Kaizilege (hawapo pichani) akiitambulisha meza kuu wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
  Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jesse Kwayu akitoa neno la shukrani wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mwezeshaji wa kongamano kutoka Kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC), Mwanasheria Harold Sungusia akiwapitisha washiriki kwenye ratiba wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwapongeza Hype Interactive LTD, Mtendaji Mkuu, Bw. Michael Kimollo pamoja na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Kampuni hiyo Mussa Kalokola vijana ambao wametengeneza ‘App’ ya kuangalia usalama wa wanahabari wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (kushoto).
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime akizungumza jambo wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Nancy Kaizilege akifafanua jambo wakati wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha. 
 Washiriki wa kongamano hilo kutoka Idara ya Habari (MAELEZO), Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), Jeshi la Polisi Tanzania, Jukwaa la Wahariri (TEF), Baraza la Habari (MCT), MISA Tanzania, Chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Muungano wa Radio za jamii (TADIO), Uhuru Media (public media), Mwananchi Communications (private media), Millard Ayo (online media), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) na maofisa habari wa mikoa.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe na meza kuu katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la wiki moja kuhusu uangalizi na utoaji taarifa juu ya usalama wa wanahabari Tanzania lilioenda sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanahabari lililowezeshwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la misaada la Sweden (SIDA) katika mchango wake kwenye Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Mawasiliano (IPDC)linalofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton ya jijini Arusha.

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA,WAGOMBEA 110 CCM WAPITA BILA KUPINGWA JIMBO LA HAI

$
0
0
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya wilaya ya Hai,Juma Massatu amesema wanachama 110 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji wamepita bila kupingwa.

Idadi hiyo ni Kati ya vitongoji 294 ambavyo wanachama wa vyama mbalimbali walijitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi hizo ambapo hawakuweza kuchukua na kurejesha fomu hizo.

Tayari Msimamizi huyo was uchaguzi amewatangaza rasmi wagombea hao kuwa ndio washindi katika vitongoji hivyo.

WAZIRI KALEMANI AZINDUA RASMI BODI YA PBPA

$
0
0

Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na kuitaka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni.

Tukio hilo lilifanyika Novemba 4, 2019 katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo Kikuyu, Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt Hamisi Mwinyimvua na viongozi wengine wa Wizara, ambapo Waziri alimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi husika, Dkt Lutengano Mwakahesya, Kanuni zitakazomwongoza yeyé na Wajumbe wa Bodi, katika kutekeleza majukumu yao.

“Nakukabidhi Kanuni mtakazotumia kutekeleza majukumu yenu ili kazi zenu zikawe zenye ufanisi. Fanyeni kazi zenu zote kwa kuzingatia sheria na kanuni.”

Akizungumzia majukumu makuu ya Bodi hiyo, Waziri Kalemani alisema jukumu kubwa ni kuhakikisha shughuli za kuingiza mafuta kwa pamoja zinaratibiwa ipasavyo ili yapatikane kwa muda wote.

“Mnatakiwa kuhakikisha uratibu unakuwa ni sahihi, usiosababisha migogoro kati ya waagizaji wa mafuta kwa pamoja na watoa huduma wengine,” alisisitiza.

Vilevile, Waziri alieleza jukumu lingine ni kwa Bodi kuhakikisha kuwa mafuta yanayopatikana yana viwango vinavyokidhi ubora na mahitaji ya sekta ya mafuta hapa nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri alielezea hali ya upatikanaji mafuta nchini, ambapo alisema katika kipindi cha miaka minne iliyopita, hali hiyo imeimarika kwa kiasi kikubwa.

Akitoa takwimu, Waziri alisema hadi kufikia mwaka 2015, nchi ilikuwa na Bandari moja tu ya Dar es Salaam iliyokuwa na uwezo wa kupokea Meli za Mafuta tani 165,000. “Sasa zimeongezeka Bandari mbili, Mtwara na Tanga, zenye uwezo wa kupokea mafuta tani 90,000 hivyo uwezo wetu wa jumla wa kupokea mafuta kwa sasa ni tani 255,000.”

Waziri aliendelea kueleza kuwa, uwezo wa nchi kuingiza mafuta kwa sasa ni lita milioni 265 kwa siku wakati mahitaji ni lita milioni 9.4 tu. “Hivyo tuna ziada ya lita milioni 255.3 kwa siku.”

Akidadavua zaidi, Waziri alieleza kuwa, nchi ina ziada ya mafuta ya dizeli kiasi cha lita milioni 151.2 ambazo zinatosha kwa matumizi ya siku 32; aidha, kuna ziada ya lita milioni 85.3 za petroli ambazo zinatosha kwa matumizi ya siku 26.

Kwa upande wa mafuta ya ndege, alisema kuwa, ipo ziada ya lita milioni 22.9 ambazo zinatosha kwa siku 41 na ziada ya lita milioni 5.7 za mafuta ya taa ambayo yanatosheleza mahitaji ya siku 40.

Hata hivyo, Waziri alibainisha kuwa, katika kipindi cha miaka minne, mahitaji ya mafuta ya taa kwa nchi yamepungua kutokana na kuenea kwa umeme katika maeneo mengi.

Alisema, takwimu zinaonesha mwaka 2015 mahitaji ya mafuta ya taa kwa siku yalikuwa lita 1,070,000 ambapo yamepungua hadi kufikia lita 1,045,000 kwa siku kwa sasa.

Waziri Kalemani alitumia jukwaa hilo kutoa onyo kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa na tabia ya kuficha mafuta wakisubiri bei ipande ndipo wayatoe na kuuza. Aliitaka Bodi kuwafikishia salamu kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria na atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufungiwa kituo chake.

Waziri pia, alitoa maelekezo kwa Bodi hiyo kufanyia kazi suala la kuhakikisha wananchi wa vijijini wanaondokana na changamoto ya upatikanaji wa mafuta. Aliwataka kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ili wafanye tathmini itakayowezesha uanzishwaji wa vituo vya kuuzia mafuta vijijini.

Alisema, wananchi vijijini wamekuwa wakihangaika kupata mafuta na wakilazimika kununua nishati hiyo kwenye madumu kutoka kwa wauzaji holela mabarabarani jambo ambalo siyo salama.

“Tunavyopeleka umeme vijijini, tupeleke pia na mafuta ili kuwaondolea adha wananchi. Hii itawasaidia sana wahitaji, hususan wamiliki wa taxi, bodaboda na bajaji,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Mwinyimvua, pamoja na kuwapongeza wajumbe wa Bodi kwa kuteuliwa kwao, aliwataka pia kufanya kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yao kama alivyoelekeza Waziri.

Naye Mwenyekiti wa Bodi, aliahidi kwa niaba ya wenzake kuwa watafanyia kazi yale yote waliyoelekezwa.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia), akimkabidhi Kanuni za Kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Dkt Lutengano Mwakahesya (kushoto). Anayeshuhudia (katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua. Waziri aliizindua rasmi Bodi hiyo Novemba 4, 2019 jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia), akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) (hawapo pichani), wakati alipokuwa akiizindua rasmi Bodi hiyo Novemba 4, 2019 jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (Meza Kuu-kulia), akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) (kushoto), wakati alipokuwa akiizindua rasmi Bodi hiyo Novemba 4, 2019 jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na walioketi upande wa kulia ni viongozi mbalimbali wa Wizara pamoja na wataalamu kutoka Wakala hiyo.
 Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akiizindua rasmi Bodi hiyo, Novemba 4, 2019 jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo Novemba 4, 2019 jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hamisi Mwinyimvua na kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi husika, Dkt Lutengano Mwakahesya.
 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Nishati wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Novemba 4, 2019 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi; Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Raphael Nombo na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Maseke Mabiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala huo, Novemba 4, 2019 jijini Dodoma.

Rais Xi atembelea Banda la Tanzania Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Nje.

$
0
0
Dar Es Salaam, 05 Novemba 2019
Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje (China International Importation Expo) yamefunguliwa na Rais wa China, Mhe Xi Jinping tarehe 05 Novemba 2019.  Maonesho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa Mataifa 64 akiwemo Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron, Mawaziri Wakuu wa Jamaica; Serbia na Greece. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.


Baada ya kufungua maonesho hayo Rais wa China ametembelea Mabanda ya nchi tano likiwemo Banda la Tanzania.  Nchi nyingine ambazo Rais Xi ametembelea mabanda yao ni Ufaransa; Ugiriki; Serbia na Jamaica.


Katika ziara ya kutembelea Banda la Tanzania, Rais Xi Jinping alifuatana na Waziri Mkuu wa Jamaica; Greece na Serbia na kupokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Innocent Bashungwa na alitumia muda wa dakika 10 katika banda la Tanzania.  Rais Xi na wageni wake walipata maelezo kuhusu bidhaa mbalimbali za kilimo na madini zinazopatikana nchini Tanzania na vivutio vya utalii. Vile vile, Rais Xi alipokea salamu salaamu za  Mhe Rais Dk John Pombe Magufuli.


Kwa upande wake Rais wa China ameipongeza Tanzania kwa kushiriki katika maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje na ametuma salaamu za pongezi kwa Mhe Rais Magufuli kwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na China.  Aidha, Rais Xi alivutiwa zaidi na bidhaa ya korosho za Tanzania na madini ya Tanzanite ambapo alitaka kufahamu zaidi juu ya upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko la China na bei ya Tanzanite. Alipewa majibu ya kutosha.


Maonesho ya Kimataifa yataendelea hadi tarehe 10 Novemba 2019.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Banda la Tanzania
Banda la Tanzania lilivyopendeza

Bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje nchini China
Bidhaa za Tanzania zikiwa katika vifungashio bora kabisa zilivutia watu wengi katika maonesho hayo.

 



NEWS FLASH: Precision Air Yamtangaza Patrick Mwanri kuwa Mkurugenzi Wake Mpya

$
0
0
Shirika la ndege la Precision Air limemteua Bw. Patrick Mwanri (44) kuwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wake mpya kuanzia tarehe Mosi Novemba 2019. Bwana Mwanri amekuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Aprili 2019.

Bw. Mwanri ana uzoefu wa takribani miaka 15 katika tasnia ya usafiri wa anga tangu alipojiunga na shirika la ndege la Precision Air mwaka 2004 akiwa kama Mratibu wa safari,  pia amekishika nyadhifa mbali mbali katika shirika hilo ikiwemo Afisa Utawala na Wahudumu wa Ndege, Meneja Ubora na Mkuu wa Kitengo cha Ubora, Usalama na Mazingira, Mkuu wa Ubora Usalama na Ulinzi, nafasi ambayo alikuwa akishikilia kabla ya kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Mkurungenzi mpya huyo amehitimu Shahada ya Uzamili ya Biashara ya Utawala wa Mambo ya Anga kutoka katika Chuo Kikuu cha Biashara cha Toulouse nchini Ufaransa. Hali kadhalika alipata Shahada yake ya kwanza ya Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Kompyuta kutoka katika chuo cha Teknikali cha St. Petersberg nchini Urusi, Astashahada ya Mifumo ya Usimamizi wa Ubora wa Ndege kutoka Shirikisho la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA) na Astashahada ya Usamizi wa  Uongozaji Ndege kutoka Chuo cha Anga cha Skypath, Kenya.
Bwana Mwanri anachukua majukumu yake mapya kutoka kwa mkurugenzi, aliyemtangulia Bi. Sauda Rajab ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha mwezi Machi 2019. Sauda alijiunga na Precision Air mnamo mwaka 2013 kutoka shirika la ndege la Kenya Airways  na kuiongoza kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka 6. Bi Sauda atakumbukwa kwa uongozi wake hususani miaka ya 2013 na 2014 kipindi kilichokuwa na wakati mgumu kwa shirika hilo. 
Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa shirika la ndege la Precision Air Bw.Michael Shirima, amempongeza Mkurugenzi mpya na kumtakia kila lenye kheri katika majukumu yake mapya.
“Bodi inayo imani na bwana Mwanri na ndiyo maana imethibitisha uteuzi wake, tunategemea atatumia ipasavyo uzoefu wake wa masuala ya anga katika kushamirisha biashara na kufikia malengo ya shirika.” 
“Tunashauku kubwa kufuatia kuteuliwa kwa mzawa kuliendesha shirika letu, tunaimani kuwa vijana wengi watahamasika kujiamini zaidi na kuona kuwa wanaweza kufikia malengo kwa kufanya juhudi na kujituma, kama alivyoonyesha Bw.Mwanri.Hii pia ni katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua vijana na vipaji vya wazawa kwa kuwafungulia fursa katika nyadhifa za juu.” Aliongeza.
Akizungumzia uteuzi wake, bwana Patrick amesema kuwa anamshukuru Mwenyekiti na bodi nzima kwa kumuamini na kuahidi kuwa atarudisha heshima hiyo kwa kuliendeleza shirika kuwa chaguo la wasafiri na chachu ya maendeleo.
‘’Nitaendelea kufanya kazi bega kwa bega na timu yangu ili kuhakikisha kuwa Precision Air inaendelea kuwa tegemeo katika  usafiri wa anga nchini Tanzania na tunaendelea kuishi kauli mbiu yetu ya kuunganisha jamii kupitia huduma zetu, Aliongeza.”
Kuhusu Shirika la Ndege la Precision Air

Precision Air ni shirika la umma lililoanzishwa mnamo mwaka 1993 na linatoa huduma za usafiri  wa anga kwenda sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi jumala yake ikiwa ni maeneo 13. Safari zake huanzia makao yake yaliyoko makuu Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Serengeti, Mtwara, Kahama, Bukoba, Mwanza, Zanzibar, Tabora, Serengeti, Nairobi, Entebbe na makao makuu ya nchi Dodoma. Huduma nyingine zinazotolewa na shirika ni pamoja na huduma za ubebaji mizigo kwa njia ya anga. Hali kadhalika shirika la Precision Air limewahi kupokea tuzo kadha wa kadha kutoka Tanzania Society of Travel Agents, Africa Aviation News Port, Tanzania Leadership Awards, TASOTA, na pia kampuni ni mshirika wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.

CAG MSTAAFU PROF ASSAD AKABIDHI OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI KWA CAG MPYA,KICHERE LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mkaguzi na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Bw. Charles Kichere amesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu ambayo yameachwa na CAG aliyemaliza muda wake Prof.Mussa Assad kwani Ofisi hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya watanzania.

Akizungumza katika makabidhiano Kichere alisema kuwa Ofisi ya CAG ni nguzo muhimu kwa watanzani kwani ndiyo ofisi inayolinda na kuangalia matumizi sahihi ya kodi yao wanayolipa kila siku.

“Tutaendelea kuifanyakazi ambayo imefanywa na Prof.Assad na timu yake, nitahakikisha kushirikiana na wafanyakazi wa Ofisi hii kuifanya kazi hii ya kulinda mapato ya kodi ya watanzania”, Alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo mapya atahakikisha kuwa atalinda Kodi ya watanzania wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wafanyakazi ili fedha inayopataikana kwenye kodi iweze kuwanufaisha wote.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hakuna kodi inayotolewa na watanzania ambayo itapotea kwa hiyo ataangalia na kuilinda  kwaajili ya kuwaletea maendeleo.

“Nataka kufanya kazi kulinda maslahi ya watanzania nimefanyakazi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA najua ugumu wa kukusanya kodi na kupata mapato, kwa hiyo nitahakikisha kuwa nailinda kodi ya wananchi kwa wivu mkubwa sana”, Alisisitiza Kichere.

Kwa upande wake CAG aliyemaliza muda wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad amesema kuwa anakwenda kufanya kilimo kutokana na uwekezaji alioufanya katika siku hivi karibuni baada ya kustaafu nafasi hiyo, akinadi kwamba  watu mjini wakinihitaji nitakuja .

Profesa Assad ameyasema hayo wakati wa makabidhiano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),leo  jijini Dar es Salaam.

Profesa amesema kuwa katika kufanya kazi amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi na kumtaka CAG mpya afanye ushirikiano nao kwani watu hao wamejengwa kwa muda mrefu na sifa zote .

Assad amesema kuwa katika kufanya kazi tumejenga mahusiano na wadau mbalimbali wa nje ambao ndio watu wa kujengeana uwezo na sio kwa ndani

“Changamoto ni nyingi tumepitia lakini siwezi kutia ukakasi katika hili na watu  niliowakosea, naomba wanisamehe kwani sisi ni binadamu”amesema Profesa Assad

Kwa upande wa CAG Charles Kichere mpya amesema kuwa kazi kubwa ni kulinda kihenge anajua kazi ngumu ya ukusanyaji wa mapato.

Kichere amesema ataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu kwa kushirikiana na timu yake ya ofisi ya Taifa ya mkaguzi ikiwa na kuangalia mapato ya nchi yanatumikaje kwa kuangalia ripoti sambamba na kujenga timu imara na sio watu walisambaratika.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za ofisi CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere akizungumza mara baada ya kukabidhiwa na aliyekuwa CAG Profesa Mussa Assad katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Mpya Charles Kichere akiwa na maua mara baada ya kupokewa wakati akiwasili katika ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi ya aliyekuwa CAG Profesa Assad jijini Dar es Salaam.

RAIS WA CHINA XI JINPING AFUNGUA MAONESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA NJE,AAHIDI NCHI YAKE KUFUNGUA MILANGO ZAIDI

$
0
0


Rais wa China Mhe Xi Jinping afungua rasmi maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za nje na kuahidi kwamba Nchi yake itafungua milango zaidi kwa bidhaa za nje kuingia katika soko la China. Katika hafla hiyo viongozi wa Mataifa 64 walihudhuria akiwemo Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron, Mawaziri Wakuu wa Jamaica; Serbia na Greece. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.

‪Aidha baada ya kufungua maonesho hayo Rais wa China  ametembelea Mabanda ya nchi (5) yakiwemo mabanda ya Ufaransa; Ugiriki; Serbia; Jamaica na Tanzania.

Katika ziara ya kutembelea Banda la Tanzania Rais Xi Jinping alifuatana na Waziri Mkuu wa Jamaica; Greece na Serbia na kupokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa. 

Balozi wa Tanzania Ndugu Mbelwa Kairuki alitoa maelezo juu ya bidhaa mbalimbali za kilimo na madini zinazopatikana nchini Tanzania na vivutio vya utalii. Aidha, Balozi Kairuki aliwasilisha salaam za Rais wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Magufuli kwa Rais wa China.

Kwa upande wake Rais wa China ameipongeza Tanzania kwa kushiriki katika maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Bidhaa za Nje na ametuma salaam za pongezi kwa Mhe Rais Magufuli kwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na China.  Aidha, Rais Xi alivutiwa zaidi na bidhaa ya korosho za Tanzania na madini ya Tanzanite ambapo alitaka kufahamu zaidi juu ya upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko la China.

Maonesho ya Kimataifa yataendelea hadi tarehe 10 Novemba 2019.

Habari picha kwa hisani ya Mdau Phelister Wegessa .


 



NEWS ALERT: Precision Air Announces Patrick Mwanri as Its New CEO

$
0
0

Precision Air Services Plc, has announced Mr. Patrick Mwanri(44) as its new Group Managing Director and C.E.O. Mr.Mwanri who was sitting as Ag. Group Managing Director and CEO from April 2019, assumed his new role effective from 1st November 2019. 
Mr.Mwanri has a wealth of experience of over 15 years in aviation having joined Precision Air in 2004 as a Flight Operations Officer and has risen up the ranks holding various positions in the airline including Crew Scheduling & Administration Manager, Quality Manager and Head of Quality, Safety and Environment, Head of Quality, safety and security a position he was holding prior to his acting appointment as Group Managing Director & CEO in April 2019. 
He holds an Executive MBA in Aerospace Management from Toulouse Business School in France Bsc. in Engineering & Technology- Informatics and Computer Science from the St. Petersburg Electro-technical University, Russia, Diploma in Airline Quality Management Systems by IATA as well as Diploma in flight Operations and Dispatch from Skypath Aviation College in Kenya.
Mr Mwanri is taking over the stewardship of the airline from former CEO Ms. Sauda Rajab whom her contract expired back in March 2019. Sauda joined Precision Air in 2013 from Kenya Airways  and led the company for 6 years. She will be remembered for managing the company through the tough times in 2013-2014. 
Addressing the media, Precision Air’s Chairman Mr. Michael Shirima, congratulated the new CEO and wished him all the best in his new role.   
“The board believes in Mr. Mwanri and that's why it has approved his appointment, we expect he will use his rich experience in the aviation business to propel the business and achieve our corporate goals.” 
“ We are also excited that we have given a home grown young Tanzanian to run our company, we believe this will inspire youth to believe in themselves that they can achieve anything if they work hard and show commitment, as it was shown by Mr.Mwanri. This also is to support the government efforts to promote youth and local talents by giving them the opportunity to take up top management posts.” He added
Commenting on his appointment, Mr. Patrick Mwanri said he thanked the Board and the Chairman for trusting him and promised to return the trust by leading the company to become the airline of choice and the catalyst of change. 
“I will continue working with my team to make sure that Precision Air continues to be the back born of air transport in Tanzania and that we stay true to our course of connecting community through our services.” He added 
About Precision Air

Established in 1993, Precision Air has been in operations for 25 years, providing key connections for tourist and economic travel within and beyond the country. Currently Precision Air provides scheduled flights to over 13 destinations within and outside Tanzania from its main hub in Dar es Salaam, including Arusha, Kilimanjaro, Serengeti, Mtwara, Kahama, Bukoba, Mwanza, Zanzibar, Tabora, Seronera, Nairobi, Entebbe and most recently route Tanzania’s capital of Dodoma. Other services provided by Precision Air include chartered, courier and, cargo air services.  The Airline is also a recipient of multiple awards from Tanzania Society of Travel Agents, Africa Aviation News Port, Tanzania Leadership Awards, TASOTA, among others and a listed company at the Dar es Salaam Stock Exchange.

ASASI ZA KIRAIA 16 ZACHANGIA BILIONI 236 KWENYE UCHUMI NCHINI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

ASASI 16 za Kiraia nchini zimetajwa kutoa mchango wa Bilioni 236 kwenye uchumi nchini ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016-2018.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze ambaye amesema licha ya kuwepo Asasi nyingi nchini lakini waliamua kufanya utafiti wa Asasi 16 tu ambazo zimefanyiwa uhakiki.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mada ya mchango wa Azaki kwenye uchumi wa Nchi katika mkutano wa kwanza wa majadiliano ya Wiki ya Azaki jijini Dodoma 

Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kutokana na Asasi za kiraia kwa kipindi cha miaka mitatu ni sawa na kilo 2,181 za dhahabu zinazosafirishwa na kuuzwa nje ya Nchi.

“Lakini pia kiasi hicho cha fedha ambacho kimechangiwa na Asasi hizi 16, kwa kipindi hicho cha miaka mitatu ni sawa na serikali kuingiza watalii 42,316 na kukaa nchini kwa muda wa wiki moja au ni sawa lita 247 milioni za petrol,dezeli na mafuta ya taa” Amesema Eyakuze.

Pia Eyakuze amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu 2016/18 kiasi cha kodi ambazo zimelipwa na Azaki hizo 16 kwa serikali ni kiasi cha Sh. Bilioni 19.

Amefafanua kuwa kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa kwa kipindi hicho ni sawa na mapato yatokanayo na maji ya kunywa, vinywaji laini na sigara ya mwaka 2018/19 ambayo yalikuwa ni bilioni 18.8.

“Au kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa unaweza kulinganisha kabisa na kodi iliyokusanywa na Mamalaka ya maopato nchini TRA 2018/19 katika mikoa ya Rukwa, Lindi, Simiyu, Songwe na Katavi kwa pamoja ambayo makusayo yao ni Sh. Bilioni 21," Amesema Eyakuze.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Francis Kiwanga, amesema katika wiki hiyo ya Azaki moja kati ya shuguli zitakazofanyika ni pamoja na kuwa na kongamano linalojumuisha wadau wengine ikiwemo serikali.

Amesema katika kongamano hilo wanajadiliana namna ya kushirikiana na kuweka mikakati ili mchango wa Asasi za kiraia uweze kutambulika na serikali.

Naye Mratibu wa Asasi za kiraia nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali a mitaa (Tamisemi) Denis Londo amesema Asasi la Kirai zinamchango mkubwa kwa Taifa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa wiki ya Azaki jijini Dodoma leo.
 Mratibu wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dennis Londo akizungumza wakati wa uchangiaji wa mada mbalimbali katika mkutano wa kwanza wa majadiliano wa wiki ya Azaki jijini Dodoma.
 Mmoja wa watoa mada wa mada ya haki na sheria akizungumza katika mkutano wa majadiliano kwenye ufunguzi wa wiki ya Azaki leo Dodoma.
Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini waliojitokeza katika mkutano wa wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma. Asasi za Kiraia zipatazo 500 na Taasisi 100 zinashiriki mikutano hiyo.

Benki ya NBC yaendeleza jitihada zake katika kusaidia huduma za jamii

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo (katikati) akipokea cheti  kutoka kwa Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Mshindano ya Gofu ya Hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari, Hemaly Jethwa kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika mshindani hayo yaliyofanyika katika Viwanja cha gofu vya Gymkhana jijini Dar es Salaam hivi karibuni yakiwa na lengo la kukusanya fedha kusaidia wenye mahitaji maaalumu ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. . Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC, Joseph Lema. Mashindano hayo yaliwashirikisha zaidi ya wacheza gofu 104.  
 Picha mbalimbali za tukio la mashindano ya gofu ya hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari na kudhaminiwa na          Benki ya NBC. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kukusanya fedha na kusaidia wenye mahitaji maaalumu katika jamii ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliwashirikiosha zaidi ya wacheza gofu 104. 

 Picha mbalimbali za tukio la mashindano ya gofu ya hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari na kudhaminiwa na          Benki ya NBC. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kukusanya fedha na kusaidia wenye mahitaji maaalumu katika jamii ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliwashirikiosha zaidi ya wacheza gofu 104.    
Maofisa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), wakipiga picha ambapo pamoja na kutoka huduma za maji na kofia kwa wakimbiaji, washiriki pia walipata nafasi ya kujulishwa huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na benki hiyo. 


KATIKA kuendeleza jitihada zake za kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii, Benki ya NBC imedhamini hafla maalumu ya kuchangisha fedha  iliyoandaliwa  na Klabu ya Rotari ya Bahari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Hafla hiyo iliandaliwa na klabu hiyo ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wenye mahitaji maalumu katika jamii ya watanzania ikiwemo mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na ujenzi wa kituo cha kufundishia kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
 Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa NBC, Evance Luhimbo alisema NBC kwa miaka kadhaa imekuwa ikishughulisha katika kusaidia shughuli za jamii katika maeneo  mbalimbali kama vile elimu, afya na masuala ya ujasiriamali,
 “Sisi ni jukumu letu kama benki kurudisha katika jamii sehemu ya faida tuipotayo katika biashara yetu, NBC ni benki kongwe yenye uzoefu katika kutoa huduma bora za kibenki kwa zaidi ya miaka 52, hivyo tutaendelea kusapoti miradi kama hii yenye kuleta tija katika jamii”, alisema.
 Pamoja na hayo alisema mara baada ya kupokea maombi ya kuchangia hafla hiyo kutoka Klabu ya Rotari, benki yao haikusita kuitikia wito kwani ni imani jamii ikiwezeshwa kiuchumi na kielimu na jamii ikiwa na afya bora inaweza kuchangia vizuri katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.    
 Aidha Bwana Lhimbo aliitaja baadhi ya shughuli za kujamii ambayo NBC imefaya ikiwa ni  pamoja na kutoa vifaa vya  ujenzi wa madarasa katika shule za mkoani Lindi, Zanzibar, msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa Morogoro pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kifedha na ujasiriamali katika shule mbalimbali nchini.

 Baadhi ya miradi ambayo imeshafanikishwa na Klabu ya Rotari ya Bahari ni pamoja na matibabu ya moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ukarabati wa maktaba katika shule ya msingi buyuni, upanuzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi stadi katika kituo cha masista cha Carmel, Kurasini, ukarabati wa maktaba katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja  pamoja na kutoa misaada ya aina tofauti katika vituo vingine vya walemavu na wasiojiweza.

WALIMU NCHINI KULETEWA MWONGOZO WA PROGRAMU ZA MAFUNZO ENDELEVU KAZINI

$
0
0

Serikali imeaandaa mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa Programu za Mafunzo Endelevu ya Walimu kazini ambazo zitakua na tija na pia kuongeza motisha kwa walimu.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kushirikishana uzoefu wa uendeshaji wa programu za mafunzo endelevu ya walimu kazini. 

Amesema  pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kuboresha elimu kumekuwepo na changamoto hivyo mwongozo huo utasaidia kuondoa changamoto zinazojitokeza katika programu za mafunzo kazini kwa walimu ikiwemo kutokuwa na mwendelezo  na kukosekana kwa mfumo wa uratibu wa uendeshaji wa mafunzo.

Dkt. Akwilapo amewataka wajumbe wa mkutano kushiriki kikamilifu  kwa kutoa maoni ili kuandaa  miongozo ya utekelezaji wa Programu za Mafunzo Endelevu ya walimu kazini nchini. 

"Wizara ya Elimu imeona  ni muhimu kupata uzoefu kutoka kwa wadau na washirika wetu kutoka ndani na nje ya nchi kuhusu namna Programu za Mafunzo endelevu ya walimu kazini zinavyoendeshwa, naamini ushiriki wenu utasaidia kubaini maeneo muhimu katika kuratibu kazi zilizobaki," Amesema Dkt Akwilapo

Dk Akwilapo amesema kwa miaka mingi Serikali imekuwa ikitekeleza programu za mafunzo kazi kwa walimu ikiwepo Mpango wa Tanzania UNESCO na UNICEF (MTUU)  na Programu ya Kutegemeza Elimu ya Msingi Kiwilaya (DBSPE) hivyo uwepo wa muongozo huo ni  muendelezo juhudi hizo katika kuhakikisha mafunzo kazini kwa walimu yanafanyika kwa ufanisi.

Nae Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema  wazo la kuwa na muongozo kuhusu mafunzo endelevu ya walimu kazini ni wazo ambalo nchi yoyote iliyo makini ambayo inayotaka kuwa na walimu bora katika elimu inapaswa kuzingatia kwani mafunzo ya awali ya walimu pasipo mafunzo endelevu kazini ni mafunzo yasiyo kuwa na tija na kwamba vitu hivi viwili vinategemeana.

" Katika kipindi hiki tumeamua kwa dhati kwamba baada ya mafunzo ya awali ya walimu watakapokwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi huko wakute wabobezi ambao watawapokea na kuendeleza kuwapa utaalamu siku kwa siku ili waweze kukua na kuendelea kitaalamu," Amesema Dkt. Mutahabwa

Kwa upande wake Msahauri wa Elimu Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID)John Lusingu amesema uamuzi wa Serikali kuitisha kikao hicho cha wadau ni jambo jema kwa kuwa wadau wanapata nafasi ya kuchangia katika kuboresha badala ya mtu mmoja kuja na wazo na kutakiwa kufanyiwa kazi.

Mkutano wa wadau katika kushirikishana uzoefu wa uendeshaji wa programu za mafunzo endelevu ya walimu kazini  unafanyika kwa siku mbili  kuanzia Novemba 5, 2019 na unashirikisha wadau mbalimbali kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa DFID, Watafiti wa Elimu kutoka Marekani (RISE), EQUIP-T, Tusome Pamoja,  TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwa wenyeji.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa kushirikishana uzoefu wa undeshaji wa programu za mafunzo endelevu ya walimu kazini jijini Dodoma
Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamojana wadau wa elimu baada ya kufungua mkutano wa wadau wa kushirikishana uzoefu wa uendeshaji wa programu za mafunzo endelevu ya walimu kazini.

Former President Mkapa’s Autobiography to be launched on 12thNovember, 2019

$
0
0
The autobiography by the former President of the United Republic of Tanzania,H.E. Benjamin William Mkapa, titled “My Life, My Purpose: A Tanzanian President Remembers”, is set to be released on 12th November, 2019 at Julius Nyerere International Convention Centre, in Dar es Salaam, Tanzania.

The launching ceremony will be officiated by the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Two former Tanzanian Presidents, H.E. Ali Hassan Mwinyi and H.E. Jakaya Mrisho Kikwete will be in attendance. The event will also include current and former high-level government officials, business leaders, development partners, academia, representatives from book stores, libraries, civil society and youth.

The book, published by Mkuki na Nyota with support of UONGOZI Institute,
contains H.E. Mkapa’s personal account of his unique memories. The memoirs range from his childhood, time as president, and his continuing post-retirement involvement at the domestic and international stages. They are enriched by his views on leadership and advice for aspiring leaders.

“Writing these memoirs required me to take a reflective journey through my life. Some memories were painful to recall and write about; some gave me pride in what we Tanzanians have achieved. While the world may have changed somewhat since I was president, most challenges and concerns remain the same for our leaders,” said H.E. Mkapa.

“I appreciate the opportunity to pay tribute to those who contributed to my personal growth, to the liberation of African States and to leadership in Africa. I am especially grateful that I can provide another perspective of Mwalimu Julius Nyerere,” he added. H.E. Mkapa hopes that the book will enrich the history of Tanzania, inform and inspire a new generation of African leaders, as well as those who want to know more
about Tanzania’s development.

Participation in the launching ceremony will be by invitation only. The book will be available in various book stores and libraries in Tanzania, and online through Amazon and African Books Collective after November 12th.
Issued by:

Office of the Former President of the United Republic of Tanzania
His Excellency Benjamin William Mkapa

KAMPUNI YA MONMAR AND SONS YAKATALIWA KUPEWA MKATABA WA UJENZI WA MTANDAO WA MAJI SIKONGE

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imepiga marufuku Kampuni ya Monmar and Sons ya Mkoani Tabora kupewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa usambazaji wa miundombinu ya maji katika Vijiji vinne vya Kata ya Kitunda wilayani Sikonge kutokana na kutoridhishwa na ubora wa kazi zake katika baadhi ya maeneo nchini.

Mradi huo ambao ulikuwa ni kujenga chujio la maji, ujenzi wa tenki la maji na ujenzi wa mtandao wa usambazaji wa maji , kwa gharama za awali ulikuwa ugharimu shilingi milioni 900 lakini baada ya Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kufanya hesabu unatakiwa kutumia milioni 700.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Sikonge wakati wa ziara yake ya siku moja ya kusikilizia matatizo ya maji ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema katika maeneo mengi ambayo Kampuni hiyo ilipopewa miradi katika Mkoa wa Tabora na Katavi  ukakamilishaji wake umekuwa sio wa kuridhisha kwa kuwa imekuwa ikijengwa kwa kiwango cha chini na kuonekana na dosari muda mfupi baada ya kuzinduliwa.

Makame alisema mfano mzuri ni ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Songambele wilayani Sikonge ambalo linavuja na kusababisha upotevu wa maji.

Aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumtaka kujenga upya tenki hilo na kumpa taarifa ndani ya wiki moja.

Aidha Profesa Makame alisema Wizara ya Maji itatoa shilingi milioni 250 za awali  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mtandao wa kusambaza maji kutoka katika Bwawa la Igumila kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wa Kata ya Kitunda.

Aliwataka kutumia mafundi jamii wakati wa utekelezaji wa mardi huo ili kupunguza gharama za awali ambazo walikisia kutumia milioni 900.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alisema ni lazima ndani ya kipindi alichoagiza Waziri wa Maji kuhusu kufanyia marekebisho kasoro katika mradi wa Kijiji cha Songambele yanafanyika la sivyo atalazimika kumkamata la kumweka ndani.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri akitoa taarifa ya maendeleo ya upatikanaji wa  maji kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara yake jana
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo  kwa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya maji katika Bwawa la Utyatya  wakati wa ziara ya Waziri huyo  jana
 Bwawa la Utyatya ambalo ni chanzo cha maji kwa wakazi wa Sikonge Mjini



ZAHERA "OUT" YANGA, BENCHI LA UFUNDI NA KAMATI YA MASHINDANO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


UONGOZI wa Yanga umevunja mkataba na kocha wake Mwinyi Zahera, benchi la ufundi  na kuvunja kamati ya mashindano.

Kwa habari za Uhakika, Zahera anadai takribani Dola 60,000 sawa na Milion 130 za Kitanzania zikiwa ni za Malipo ya mkataba unaoisha Septemba 2020,  akidai mshahara na marupurupu mengine.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Klabu.

Akielezea maamuzi hayo, Msolla amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya kufikia makubaliano na Kocha Mkuu na benchi la ufundi la kuamua kuvunja mkataba.

Amesema, kwa sasa timu itakuwa chini ya Kaimu Kocha Charles Boniface Mkwasa mpaka pale kocha Mkuu atakapotangazwa tena

Aidha, Zahera hakuwa anafahamu kama kibarua chake kimeota nyasi na mpaka kufikia asubuhi ya leo amefika mazoezini kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini na kuendelea na majukumu yake wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda ya Mtwara.

Yanga inasafiri kesho kuelekea Mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda utakaopigwa siku ya Ijumaa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Timu hiyo itasafiri na benchi jipya la  ufundi likiongozwa na Mkwasa, akisaidiwa na Said Maulid na wengineo.

MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO NA BAJETI YA SERIKALI 2020/21 WAWASILISHWA BUNGENI

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu swali Bungeni kabla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Bungeni Jijini Dodoma.
 Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga (kushoto) na  Bw. Adlof Ndunguru,  wakifuatilia uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia  uwasilishwaji wa  Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, yaliyokuwa yakiwasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani,  bungeni Jijini Dodoma.
 Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Bi Mary Maganga baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto),  Manaibu  Katibu Wakuu wa Wizara hiyo. Bi Mary Maganga (kushoto) na Bw. Adlof Ndunguru (kulia)  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bw. Benny Mwaipaja, wakijadili jambo baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Bungeni Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images