Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MUME WA ZAMARADI AFIKISHWA KORTINI

$
0
0

Mume wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Novemba 4, 2019 akifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kusomewa shtaka la kumtishia kumuua kwa silaha aina ya Pisto, Venance John.
 Mume wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Novemba 4, 2019 akitoka   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  baada ya kukizi masharti ya dhamana.

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
MUME wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi, leo Oktoba 4, 2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kumtishia silaha aina ya Pisto, Venance John.

Hamisi amefikishwa mahakamani hapo kufuatia siku chache zilizopita kuonekana katika mitandao ya kijamii kupitia video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha anamtishia silaha John ambaye ni dereva wa roli la Mchanga.

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Frank Moshi, kuwa Oktoba 30, 2019 maeneo ya Mbezi Mabwepande katika Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Imedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa Hamisi alikutwa na Pisto aina ya Beleta yenye namba ya usajili 102969 ambapo kwa makusudi alimtishia Venance John huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria .

Hata hivyo, mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama ambapo mahakama ilimtaka kuwa na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa ambapo walisaini Bondi ya Sh. Mil 2 kwa kila mmoja.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba  13, 2019, mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.

KUFIKIA KESHO HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA KUANZA KUPATIKANA KISARAWE

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe uliokamilika kwa asilimia 99 na kufikia kesho wananchi wa Kisarawe wataanza kutumia maji safi na salama.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi wa DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange alipotembelea mradi huo uliopo kwenye hatua za mwisho
 Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili kushoto) akipanda ngazi kuelekea juu ya tanki la Kisarawe akiwa ameongozana na Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja na watendaji wengine wa Mamlaka hiyo. Picha ya chini akiwa juu ya tanki hilo.
 Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe Mhandisi Ishmael Kakwezi akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange alipofika kuangalia kazi inayofanywa ya kuziba bomba linalovuja linalopeka maji Kisarawe.
Kaimu Mkurugenzi wa Miradi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kwenye  moja ya switch inayotumika kuwasha Pampu na kusukuma maji kutoka  Kibamba itakayopeleka maji kwenye tanki la Kisarawe.
Mafundi wakiendelea na kazi ya matengenezo katika mabomba yanayopeleka maji Tanki la Kisarawe

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WANANCHI wa Kisarawe wanatarajia kuanza kutumia maji safi salama hapo kesho baada ya mradi wa Maji wa Kisarawe kukamilika kwa asilimia 99 kufikia leo. 

Mradi wa Kisarawe wenye thamani ya Bilion 10.6 ulianza kujengwa Juni 2018 baada ya agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kuzindua mtambo wa Ruvu Juu na kuwataka DAWASA kuhakikisha Kisarawe wanapata maji safi na salama.

Agizo hilo limeweza kutekelezwa kwa muda wa mwaka kwa kutumia fedha za ndani za Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Amesema, kazi kubwa imeshafanyika na palipobaki ni kidogo sana ila kuanzia kesho wananchi na wakazi wa Kisarawe wataanza kutumia maji safi na salama na kuepukana na maradhi yanayosababisha na maji yasiyo salama.

"Tumetekeleza ahadi ya Rais, kama alivyotuagiza na sisi tumeleta mradi huu hapa Kisarawe na wananchi waendelee kuleta maombi ya maji ili waweze kuunganishiwa,"amesema Mwamunyange.

" Kuna marekebisho kidogo katika mabomba yetu, ila hiyo ni kazi ndogo na mafundi wapo kazini wanaendelea na kazi ya kuhakikisha wanaimaliza haraka," amesema

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema ana furaha kubwa sana kwa kuweza kuukamilisha mradi wa maji wa Kisarawe tena kwa fedha za ndani.

Luhemeja amesema, tayari wameshapokea maombi 1200 kutoka kwa wakazi wa Kisarawe kwa ajili ya kuunganishiwa maji ila malengo ni kupita idadi hiyo ya wateja.

Aidha, amesema wakazi 25,000 watafaidika na mradi huo na anawakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza Wilaya ya Kisarawe kwani huduma ya maji safi na salama ipo na inayotoshelezw.

Mradi huo wa Mkuranga unahusisha ujenzi wa Kituo cha kusukuma maji, kulaza mabomba kwa urefu wa Kilomita 350 kutoka Kibamba hadi Kisarawe pamoja na kujenga tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhia maji Lita Miliomln sita kwa siku.

RAIS DKT. MAGUFULI AWA APISHA CAG, MAJAJI 12 WA MAHAKAMA KUU, MAKAMISHNA WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU PAMOJA NA BALOZI MMOJA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Bw. Charles Edward Kichere mara baada ya kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG). Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Joachim Chrles Tiganga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Deo John Nangela kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Angela Anthony Bahati kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Angaza Elias Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu Kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Novemba 4, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Amina Talib Ali Kuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Aisha Amour kuwa balozi wa Tanzania Nchni Kuwait. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Novemba 4, 2019.

   Viongozi walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam,  Novemba 4, 2019. 
 Viongozi walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiweka sahihi kwenye hati ya kiapo cha Maadili kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam,  Novemba 4, 2019. 




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada kuwaapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge  Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha Dkt. Isidori Mpango  pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG), Majaji 12 wa Mahakama kuu, Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG) mpya Bw. Charles Kichere, Watendaji wa Ofisi ya CAG pamoja na Makamu mwenyeki wa Kamati ya Bunge ya PAC Aesh Hilaly  Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4, 2019.

PICHA NA IKULU



MALIKIA CLEOPATRA ALIYEPOTEZA DIRA YA MISRI.

$
0
0

Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam


Mwanamuziki Zahir Alli Zorro, wakati akiwa katika bendi ya JKT Kimulimuli, alipata kuimba wimbo akimsifia mwanamke mrembo wa Misri Cleopatra.

Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza sifa zote hizo alizozipamba nguli huyu zikoje?

Cleopatra ni nani?

Cleopatra alikuwa Malkia maarufu zaidi kati ya wote waliowahi kutawala nchi ya Misri.

Alizaliwa katika mji wa Alexandria mwaka wa 69 K.K (Kabla ya Kristo), wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII.

Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa .

Cleopatra hakua Mmisri, ispokuwa asili yake alikuwa mMacedonia, familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander The Great.

Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.



Urithi wa utawala wa Ptolemy

Mfalme wa Misri, Ptolemy wa XII, wakati anafariki mnamo mwaka wa 51 K.K. akaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka 12 Ptolemy XIII. 

Lakini aliagiza kwamba, kijana huyo atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra. Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza.

Ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.Cleopatra aliyekuwa na umri wa miaka 18, mapema alithibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususan katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania.

Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Caesar na Cleopatra: 48-44 K.K

Kuwasili kwa Julius Caesar Alexandria, kulimpa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni, kwa wakati huo.

Aliiachia Misri mikononi mwa Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey akawa mtawala mwenye nguvu katika dola ya Roma.

Julius Caesar aliamua kupumzika kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyo Cleopatra hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).

Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria, Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, akadai kuwa mtoto ni wa Caesar, na pia anafanana sana na baba yake huyo.

Katika mwaka wa 46 K.K Caesar alimualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina Caesarion, “Caesar mdogo). Walikaribishwa katika jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae Caesar aliuawa.

Baada ya Caesar kuuawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

Antonius na Cleopatra, 41- 31 k.k

Misri ya Cleopatra bado ulikuwa ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterranean unajihusisha na siasa za Roma, kuna uvumi ulienea Roma kwamba Cleopatra alimsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar.

Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka wa 41, Marcus Antonius aliamuru majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na kuamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia.

Cleopatra alivuka Medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana msimanzi.

Alisafiri hadi kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia aliwasili akiwa katika Boti ya kifahari, akiwa amevaa mavazi ya kuvutia ya mahaba, yenye asili ya Kigiriki.

Hazuiliki kutamanika na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya Jenerali Marcus Antonius.


Cleopatra alimualika Antonius amtembelee Alexandria.

Antonius alikubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea. Alipowasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya baridi.

Baada ya Antonius kuondoka kurudi Roma, Cleopatra patra anajifungua mapacha, mvulana na msichana.Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius.

Antonius Alimuagiza Cleopatra kwenda Antioch, Syria ambako huko alimuoa.Sasa wakajionesha waziwazi pamoja, wakaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma.

Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki , akawa na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa Mashariki ya Kati (Syria).

Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wakawa na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja.

Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za Wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.

Mkutano katika Alexandria 44 K.K

Watu wengi wanakusanyika kwa ajili ya mkutano katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huo.

Katika jukwaa kuu aliketi Antonius na mkewe Cleopatra, akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithiri ya Mungu wa kike wa Misri.

Katika viti vingine vinne vya kifalme walikuwa wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na ‘Caesar –mdogo’, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.

Mnamo majira ya jioni katika tafrija hiyo, ambayo baadae ilijulikana kama “harambee katika Alexandria”, Antonius aliugawa utawala wa Mediterranean Mashariki kwa familia yake hiyo mpya.

Antonius alimtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar-mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus wakati huohuo tawala zingine aikatawaliwa na watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), aliwapa sehemu ya Mashariki mwa Euphratia, kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, aliwapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo, Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambae alivaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia.

Ikawa sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.

Actium na baadaye: 31-30 K.K

Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia.

Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano.

Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki.

Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda;

Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake , na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae.

Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujinyonga katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na jeshi lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tar. 12 Agosti 30 KK.


“ASP” Nyoka aliemuua Cleopatra 30 K.K

Cleopatra aliamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia ‘serious’ uwajibikaji wake kwa Misri.

Pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliyejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri.

Malikia alitambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.

Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, aliagiza sumu ndogo ya nyoka, ASP, ambayo iliingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda.

Cleopatra alivaa mavazi yake mazuri ya ki-Malikia, akalala katika kiti chake cha dhahabu. Akamu kujitoa kafara kwa “Amen-Re” Mungu wa Jua wa Misri.


Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (ASP).

Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia ulikuwa kama ‘maigizo’, na unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia unaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.

Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake.

Pia aliichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.Huyo ndiye Cleopatra aliyewababaisha baadhi ya watu nyakati hizo.

Mwisho.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.

Mwandaaji anaptikana kwa Namba: 0784331200, 0736331200, 0767331200 na 0713331200.

KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAKABILIWA NA UCHAKAVU WA BAADHI YA MAJENGO,CHAUDUMIA WAGONJWA TAKRIBAN 300 KWA SIKU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

KITUO cha afya Chalinze, wilayani Bagamoyo, Pwani, kinakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa baadhi ya majengo ,upungufu wa majengo,watumishi,kukosa uzio,huku kikiwa kinahemewa kupokea wagonjwa  takriban 300 kwa siku. 

Kituo hicho kilianza kama zahanati mwaka 1982 kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 1996 kuwa kituo cha afya, majengo yake  yamekuwa chakavu.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Sudi Msakamali, aliyasema hayo baada mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete na uongozi wa shule ya msingi Chalinze Modern Islamic kwenda kufanya usafi pamoja na kukabidhi msaada wa sabuni za maji na za unga kwa ajili ya usafi kituoni hapo.

Msakamali alisema , kituo hicho kinapokea wagonjwa 300 kwa siku, huku kikizalisha watoto kati 130 mpaka 150 kwa mwezi.

"Changamoto kubwa ni kuboreshwa miundombinu ya majengo, sababu wagonjwa wanaokuja kupatiwa matibabu ni wengi, idadi ya majengo ni ndogo hivyo kusababisha foleni na msongamano, na kutokuwepo uzio ," alisema Dkt. Msakamali.

Akizungumzia changamoto hiyo, Ridhiwani aliipongeza shule ya msingi Chalinze Modern kwa namna wanavyojitoa katika kufanikisha maendeleo, ikiwemo kutoa msaada wa mifuko kumi ya saruji na karatasi nyeupe rimu 15 kwenye shule ya msingi ya Kibiki.

Alifafanua ,serikali imeshaanza kuzitafutia ufumbuzi changamoto ya uhaba wa watumishi,madawa na kwamba TACAIDS imeshaanza ujenzi wa  maabara itayojihusisha na upimaji wa vipimo vyote ikiwemo ya damu.

Akikabidhi sabuni za maji chupa 10, miche 15 ya sabuni ya kufulia na kiroba cha sabuni ya unga, Mkurugenzi wa shule ya msingi Chalinze Modern Omary Swed alibainisha shule yao imejitoa kwa ari na mali kushiriki kusaidia shughuli za kijamii.

"Shule yetu ya Chalinze imekuwa mstari wa mbele kusaidia shughuli za kimaendeleo katika nyanja tofauti, juzi tulikwenda shule ya msingi ya Kibiki tumesaidia mifuko kumi ya saruji na rimu 15 za karatasi kwa ajili ya mitihani," alisema Swed.

BMT LAONGEZA MUDA KWA VYAMA NA MASHIRIKISHO KUKAMILISHA VIGEZO NA MASHARTI

$
0
0
Wakati wa uzinduzi wa Baraza la Kumi na nne (14) la Michezo la Taifa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe alitoa maelekezo ya kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikifanya kazi bila kufuata utaratibu na hivyo kushindwa kuleta tija katika maendeleo ya michezo nchini. 

Katika kutekeleza maagizo hayo, Baraza la Michezo la Taifa lilitoa maelekezo kwa Vyama na Mashirikisho ya Michezo ya Taifa juu ya namna bora ya kutekeleza masuala ya Michezo hapa nchini katika Mkutano wake na Vyombo vya Habari, uliofanyika tarehe 25 Julai, 2018.

Lengo la Mwongozo huo lilikuwa kutoa maelekezo ya namna bora ya kusimamia uendeshaji wa masuala yote ya Michezo katika Vyama / Mashirikisho ya Michezo nchini ambapo tuliwataka viongozi hao kuzingatia vigezo vitatu (3) muhimu katika uendeshaji wa shughuli za Vyama / Mashirikisho ya Michezo nchini kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo. Mambo hayo ni pamoja na Vyama / Mashirikisho: 1) Kumiliki Ofisi na Anuani ya Makazi; 2) Kumiliki Akaunti za Benki; pamoja na 3) Kuaandaa Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Majukumu yao na Bajeti ya shughuli zao za mwaka. Mwongozo huo uliwataka Viongozi hao kutekeleza mambo hayo ndani ya kipindi cha miezi sita (6) tangu Mwongozo ulipotolewa, tarehe 25 Julai 2018.  

Baada ya kipindi kilichotangazwa cha miezi sita kupita, Baraza la Michezo la Taifa liliendesha zoezi la kukusanya taarifa katika Vyama /Mashirikisho juu ya utekelezaji wa Mwongozo huo na kubaini upungufu mkubwa katika utekelezaji wake. Taarifa iliyokusanywa katika Vyama / Mashirikisho sabini (70) vilivyosajiliwa katika ngazi ya taifa, ilibaini kuwa;  

Vyama / Mashirikisho kumi na nane (18) tu ndiyo vilivyokidhi vigezo vyote vitatu – vya kuwa na Ofisi ama za kumiliki wenyewe au za kukodisha, kuwa na Akaunti ya Benki, na kuwa na Mpango Kazi na Bajeti;  

Vyama / Mashirikisho thelathini na saba (37) vimetekeleza kigezo kimoja au viwili kati ya vigezo vitatu vilivyoainishwa na vyama / Mashirikisho kumi na tano (15) havijakidhi kigezo hata kimoja cha mwongozo uliotolewa na wala havifanyi shughuli zinazotarajiwa kwa mujibu wa Katiba zao.

Baraza linatoa pongezi kwa Vyama/Mashirikisho kumi na nane (18) kwa utii wao na kutekeleza maagizo kama yalivyotolewa kwenye Mwongozo huo. Ni matarajio ya Baraza la Michezo la Taifa kuwa vyama hivi vitatekeleza Mipango waliyojiwekea kikamilifu na kuhakikisha hesabu zao zinakaguliwa na kuwasilishwa kwa mamlaka husika.

Aidha, vyama hivyo vinatakiwa kuhakikisha vinaendelea kuboresha utawala bora ndani ya vyama, vinatekeleza matakwa ya katiba kikamilifu, kuhakikisha ushiriki wa timu zao katika mashindano ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuwa na mipango ya kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo.
Rejea kiambatanisho (i) kwa orodha ya Vyama na Mashirikisho hayo.

BMT inatoa nyongeza ya muda wa siku tisini (90) kwa Vyama/Mashirikisho thelathini na saba (37) ambavyo vinakosa baadhi ya vigezo ambavyo vilianishwa katika Mwongozo wa Uendeshaji wa Shughuli za Michezo kama ulivyowasilishwa kwao mnamo tarehe 25 Julai, 2018.  Kutokutekeleza kwa wito huu kutavipelekea Vyama/Mashirikisho hayo kufutiwa Usajili wake kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Usimamizi wa Michezo nchini.  

Pia Baraza la Michezo la Taifa linakusudia kuvifutia usajili Vyama/Mashirikisho  kumi na tano (15) ambavyo havikidhi vigezo vyote vya mwongozo wala  kuendesha shughuli za michezo kwa kipindi kirefu. 
 Rejea kiambatanisho (iii) kwa orodha ya Vyama na Mashirikisho hayo.

Vyama na Mashirikisho ya Michezo yatafutiwa usajili wao kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Kifungu cha 16 (1) (d) na 17 (1) na (2) ambavyo vinampa mamlaka na utaratibu Msajili wa vyama vya Michezo kuvifutia usajili Vyama/Mashirikisho ya Michezo ambavyo vimeshindwa kukubaliana na masharti ya Sheria hiyo. 

Vyama/Mashirikisho ya Michezo ambayo hayajakidhi Kigezo hata kimoja cha Mwongozo (Vyama vinavyofutiwa usajili)
Chama cha Wanawake cha Michezo Tanzania (TAWSA)
Tanzania Pool Association (TPA)
Tanzania Squash Rackets Association (TSRA)
Physical Education Association (PEA)
Tanzania Karate Do-Federation Association (TKA)
Tanzania Badminton Association (TBA)
Chama cha Walimu wa Riadha Tanzania (CHAWARITA)
Tanzania Canoe Association (TACA)
Tanzania Weightlifting Federation (TWF)
Tanzania Scrabble Players Association (TSPA)
Tanzania Shooting Association (TASA)
Tanzania Rugby Union (TRU)
Tanzania Jump Rope Association
Tanzania Amateur Boxing Coaches Association
Tanzania Basketball Coaches Association

Mawaziri wa Afya,UKIMWI SADC Kujadili Ajenda 13

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akifungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC), ambao ni moja ya vikao vya Mkutano wa Mawaziri wa Wizara hiyo kwa nchi za SADC, Mkutano huo unaendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Na. Paschal Dotto

Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Sekta ya Afya umeanza rasmi Jijini Dar es Salaam kwa Kutanguliwa na Kikao cha Makatabu Wakuu wa Wizara ya Afya kutoka nchi wanachama, huku ajenda 13 zikitajwa kujadiliwa katika Mkutano huo uonafanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Akizungumza katika Ufunguzi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.Zainab Chaula amesema kuwa katika kati ya ajenda hizo 13, Kifua Kikuu itakuwa ni ajenda ambayo italengwa zaidi kwani malengo ya nchi za SADC ni kupunguza ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa au kuufuta kabisa ifikapo 2030.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula, akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Wakuu wa Sekta ya Afya Kutoka Nchi 16 za Jumuiy ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada yakufungua Mkutano wa Afya na UKIMWI unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

“Ajenda kubwa kati ya zile 13 katika Mkutano huu ni ile ya kupunguza ugonjwa wa kifua kikuu au kukomesha kabisa kwa nchi wanachama wa SADC, kwani malengo ya nchi hizi 16 ni kukomesha TB ifikapo mwaka 2030”, Alisema Dkt.Chaula.

Dkt.Chaula alisema kuwa ajenda nyingine ni pamoja na kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi, masuala ya malaria, Afya ya mama na mtoto, chanjo ya mtoto, masuala ya lishe bora, utapiamlo na viribatumbo, uimarishwaji wa mfumo wa Afya hususani upatikanaji wa dawa na upatikanaji wa takwimu za Afya, rasilimali watu, rasilimali fedha na masuala ya ununuzi wa dawa ambapo Bohari Kuu ya Dawa kutoka Tanzania(MSD) inafanya kazi ya ununuzi na kusambaza dawa kwenye nchi za kusini mwa Afrika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula, akiwa katika picha ya pamoja na Kamti ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI kwa nchi Wanachama wa SADC mara baada yakufungua Mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kufungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC), ambao ni moja ya vikao vya Mkutano wa Mawaziri wa Wizara hiyo kwa nchi za SADC, Mkutano huo unaendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Ili kutekeleza azma hiyo, Mawaziri wa Sekta ya Afya kwa Nchi za SADC makatibu wakuu na wajumbe mbalimbali tayari wameanza kuandaa ajenda hizo, na mwitikio wa mahudhurio kwa wajumbe umekuwa mkubwa ambapo mpaka sasa ni asilimia 95.

Aidha Dkt. Chaula alisema kuwa, Tanzania imepewa heshima ya kuwa wanunuzi na wasambazaji wa dawa kwa nchi za SADC kwa hiyo Mawaziri watapata nafasi ya kutembelea Bohari Kuu ya dawa pamoja na kiwanda Kikubwa cha viua dudu cha kibaha.

“Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa SADC watapata fursa ya kutembelea kiwanda cha viua dudu Kibaha, kwa kuwa uwezo wake sasa umekuwa ni mkubwa na mnajua sasa hivi ajenda kama nchi ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kati wenye viwanda, kwa hiyo kiwanda hiki pia kinatuwakilisha kwenye nchi hizi za SADC”, alisema Dkt. Chaula.

Makatibu Wakuu na Wajumbe wa Sekta ya Afya kutoka nchi Wanachama SADC wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Afya na UKIMWI wa Mawaziri Wizara ya Afya unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI baada ya kufanikisha kwa kiasi kikubwa tohara kwa wanaume.

“Tunaingia na ajenda tulizowekeana katika kipindi kilichopita, sisi Tanzania kuna eneo ambalo tumefanya vizuri kuliko nchi zote za ukanda huu katika kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI eneo hilo ni tohara kwa wanaume, kwa hiyo katika mkutano huu tutabadilishana uzoefu katika eneo la mafanikio kwa kila nchi kwa nchi 16 za SADC”, Alisema Dkt. Maboko.

DTB BANK YATOA MSAADA WA MAGODORO KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA DHI NUREYN, IRINGA

$
0
0
Meneja Masoko wa benki ya DTB-Tanzania,Ndg. Sylvester Bahati (kushoto) akimkabidhi Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Dhi Nureyn, Faidh Said Abri, sehemu ya Msaada wa Magodoro yaliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Kituo hicho, kilichopo Mkoani Iringa. Benki ya DTB-Tanzania imetoa Magodoro zaidi ya ishirini, yaliyokuwa yakihitajika sana kituoni hapo, mwishoni mwa wiki.
Meneja Masoko wa benki ya DTB-Tanzania, Sylvester Bahati akiwa ameambatana na baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Benki hiyo wanaoshiriki mashindano ya Ligi Daraja la pili, wakati wakizungumza na mmoja wa wasimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Dhi Nureyn, kilichopo Mkoani Iringa.
Meneja Masoko wa benki ya DTB-Tanzania, Sylvester Bahati akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya Msaada wa Magodoro kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Dhi Nureyn, kilichopo Mkoani Iringa.
Sehemu ya Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya DTB wanaoshiriki Ligi Daraja la Pili, wakiwa na baadhi ya Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Dhi Nureyn, kilichopo Mkoani Iringa.
Picha ya Pamoja ya Wafanyakazi wa Benki ya DTB pamoja na Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki hiyo, nje ya Kituo cha Watoto Yatima cha Dhi Nureyn, kilichopo Mkoani Iringa.
Picha ya Pamoja.

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTAFUTA SULUHU YA SUMU KUVU

$
0
0
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na wadau wa mkutano unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumukuvu ,wanaotoka katika Nchi 15 za Afrika katika mkutano unaofanyika katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha leo.
Washiriki wa Mkutano unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumu kuvu wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Kilimo Mhe.Josephat Hasunga.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewataka Wakulima kuchukua hatua kudhibiti sumukuvu ambayo imekua ikiathiri mazao tangu yanapokua shambani na baada ya kuvunwa ili kuondokana na sumu hiyo yenye madhara inayosababisha saratani na hata kupelekea vifo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau hao Mhe.Hasunga amesema kuwa serikali imeanza kushirikiana na wadau katika kutafuta suluhulu ya wakulima kuyakinga mazao yao na sumu kuvu na tayari wamekuja na dawa itakayowasaidia kudhibiti sumu hiyo kabla na baada ya mazao kuvunwa.

Amesema mkutano huo unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumu kuvu , lengo lake ni kukaa na kujadiliana kwa kina na kuona ni hatua gani zichukuliwe ,ili kuhakikisha kwamba wanapambana na ugonjwa huo sambamba na kutoa hamasa na elimu kwa wakulima,juu ya ugonjwa huo wa sumukuvu.

Hasunga amesema tayari Serikali imekuja na mkakati uliozinduliwa kipindi mkoani Simiyu kipindi cha sikukuu ya nanenane na umeshaanza kutekelezwa katika programu inayotambulika kama TANIPAC ,ambapo moja ya mambo yanayotekelezwa katika mradi huo ni kuhakikisha kuwa wanajenga magala,kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuepukana na sumu Kuvu 

Aidha amesema Utafiti uliofanywa na wataalamu wa nchi mbalimbali unaonyesha kwamba takribani asilimia 20%-40% ya mazao mbalimbali ya nafaka yamnaathiriwa na ugonjwa wa sumu kuvu.

Waziri amewataka Watafiti kufanya utafiti juu ya sumu kuvu na kuangalia hali halisi ya tatizo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa watafiti itakayosaidia kuchukua hatua zaidi.

Mratibu wa Utekelezaji Mradi wa Kudhibiti Sumu kuvu nchini,Clepin Josephat ,Mtaalamu amesema kuwa mwaka 2016 baadhi ya watu walifariki kutokana na sumu kuvu ,ambayo haionekani na haishikiki hivyo serikali ipo kwenye mpango wa kujenga maabara kubwa ya kilimo itakayosaidia kukabiliana na tatizo hilo.

Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya kudhibiti sumu kuvu ya Aflasafe kutoka shirika la IITA Ranajit Bandyopadhyay ,amesema kuwa baada ya utafiti wao na kupata dawa ya kudhibiti sumu kuvu wamekuja na mikakati ya kusambaza taifiti hiyo na dawa ili iweze kusaidia wakulima baada ya kukaa katika maktaba .

Kwa mujihu wa takwimu za mwaka 2017 za Shirika la chakula na Kilimo Duniani,(FAO)Tanzania ininazalisha tani milioni 6 za mahindi,ipia inazalisha zaidi ya tani milioni 1 za karanga .

WAZIRI MKUU AZINDUA WIKI YA AZAKI, AWATAKA KUENDELEA KUHUDUMIA WANANCHI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema inathamini kazi kubwa inayofanywa na Asasi za Kiraia nchini (Azaki) hasa katika kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali katika kuwaletea maendeleo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakati akizindua wiki ya Azaki ambayo inashirikisha zaidi ya Asasi za kiraia zipatazo 500 na Taasisi 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Mhe Waziri Mkuu amesema ni ukweli usiopingika kuwa Asasi za Kiraia zimekua na ushirikiano mkubwa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwahudumia wananchi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ambao umekua na tija na manufaa kwa jamii.

Amesema Asasi za Kiraia zimekua mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali kwenye vita dhidi ya ukatili wa kijinsia, mila potofu ikiwemo kupigania upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike 

" Serikali yetu chini ya Rais Dk John Magufuli kwa hakika itaendeleza ushirikiano na Azaki katika kuwatumikia wananchi wetu, tunafahamu namna ambavyo mmekua mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi wetu.

Tunafahamu mmekua mkitoa elimu kwa viongozi wetu hasa katika eneo la utawala bora lakini pia mmekua mkiwahudumia wananchi wetu kwenye sekta ya elimu, afya na hata kiuchumi kwa kuanzisha mikopo ambayo imekua na manufaa makubwa katika kukuza vipato vyao," Amesema Mhe Waziri Mkuu.

Amezitaka Azaki kuendelea kuiunga mkono Serikali katika vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu kwenye mali za umma na nidhamu katika utendaji na kuwaasa kutumia fedha wanazopata kwa wahisani kufanya miradi ambayo ina taji kwa jamii.

Amesema ili kuendana na kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema "Ubia kwa maendeleo, ushirikiano kama nguzo ya maendeleo nchini" ni muhimu Azaki kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo yote hasa wale wa kijijini.

Pia Mhe Waziri Mkuu amezitaka Azaki kuhamasisha wananchi kuchagua viongozi bora wenye uzalendo ambao watashirikiana na Asasi hizo katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Kwa wa upande wake Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na Azaki utaendelea kwaajili ya kuleta maendeleo ya Tanzania.

“Asasi zimesaidia kutoa elimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo wao wanabaki kuwa ni watu muhimu katika Taifa hili,” Amesema.

Naye Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa wapo tayari kama Wizara kukaa pamoja na kutatua changamoto wanazokumbana nazo Azaki.

Rais wa Foundation Civil for Society (FCS), Stigmata Tenga alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo ikiwemo kuwepo kwa ugumu kwa taasisi na mamlaka za serikali kutaka kuonyesha vibali hali inayosababisha miradi kuchelewa au kutofanyika kabisa.

“ Pia bado kuna changamoto ya kuaminiana kwani ili dhana iwe kweli ni lazima kuaminiana,kwani asasi zinafanya kazi kwa maendeleo ya taifa hivyo wanaomba waaminiwe ili kazi zilete tija zaidi,”Amesema Tenga.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria kufungua rasmi wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) jijini Dodoma leo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu na kulia ni Francis Kiwanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS. 
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa maendeleo na wananchi mbalimbali waliojitokeza katika ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 
 Wananchi jijini Dodoma waliojitokeza katika wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya Azaki uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiongoza wadau mbalimbali na washiriki wa Azaki katika matembezi ya amani kutoka katika viwanja vya Nyerere kwenda uwanja wa Jamhuri ikiwa ni kuashiria kuanza kwa wiki ya Azaki jijini Dodoma leo.

JAJI KIONGOZI AZUNGUMZA NA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WALIOAPISHWA LEO

$
0
0
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akizungumza na majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioapishwa leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA)-Lushoto (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa leo.(Picha na Magreth Kinabo-Mahakama)

Naibu Waziri wa Afya afungua warsha ya wadau wa Utafiti Kanda ya Ziwa

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifungua warsha ya siku mbili kwa wadau wa utafiti/ watoa huduma za afya Kanda ya Ziwa.

Warsha hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo watoa huduma za afya wakiwemo Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushirikiriki katika tafiti imefanyika Novemba 04, 2019 jijini Mwanza ikiandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mwenyekiti wa Baraza la NIMR, Dkt. Deodatus Mtasiwa akitoa salamu zake kwenye ufunguzi wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu NIMR, Prof. Yunus Mgaya akizungumza wakati wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi wa Utafiti NIMR, Dkt. Paul Kazyoba akitoa ufafanuzi kuhusiana na warsha hiyo iliyowashirika watoa huduma mbalimbali wa afya wakiwemo Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kanda ya Ziwa.
 Mkurugenzi wa NIMR Kituo cha Mwanza, Dkr. Safari Kanung'hi akitoa salamu zake kwenye warsha hiyo.
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt Philis Nyimbi akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
 Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa tano waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na washiriki mbalimbali wa warsha hiyo.
Tazama Video hapa chini
NIMR yawapiga msasa watoa huduma za afya Kanda ya Ziwa

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AKAGUA KITUO CHA AFYA NA UJENZI WA SHULE ITIGI SINGIDA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akishiriki ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Isingiwe wakati alipofanya ziara ya kukagua Kituo cha Afya cha Kata ya Mitundu na ujenzi wa vyoo vya Shule ya Sekondari ya Mitundu iliyopo wilayani Itigi mkoani Singida juzi. 
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akikagua ujenzi wa vyoo vya Shule ya Sekondari ya Mitundu.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akikagua Hosteli wanayoitumia wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Mitundu.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akizungumza na wanafunzi wa kike ambao wapo hosteli na kuwasisitizia kuzingatia masomo.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mitundu, Sister Sarah Tidias alipofika kukagua kituo hicho. Kusho ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akiingia kukagua chumba cha kuhifadhia dawa cha kituo hicho.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akikabidhi mashuka katika kituo hicho.
Mashuka yakikabidhiwa.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akikabidhi sabuni.
Madarasa mawili yaliyo kwisha kujengwa Shule ya Msingi Isingiwe. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe amekagua Kituo cha Afya cha Kata ya Mitundu na ujenzi wa Shule ya Msingi Isingiwe na ujenzi wa vyoo Shule ya 

Sekondari ya Mitundu iliyopo wilayani Itigi mkoani Singida na kuzungumza na mganga mfawidhi wa kituo hicho Sister Sarah Tidias ili kujua changamoto zilizopo.

Akizungumzia changamoto zilizopo katika kituo hicho Sister Tidias alisema wanaukosefu wa maji ambapo hutumia kutoka kwenye visima viwili ambayo huyavuta kwa kutumia mikono na 

kuwa hakina umeme mbadala baada ya wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kukatika."Umeme wa Tanesco ukikatika tunalazimika kutumia tochi kumsaidia mjamzito wakati wa kujifungua" alisema Sister Tidias.

Tidias alitaja changamoto nyingine kuwa kituo hicho kina watumishi wachache, hakina gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kuwapeleka Hospitali ya Rufaa.

Alitaja changamoto nyingine kuwa wanauhaba wa majengo kama jengo la upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wanawake na wanaume, jengo la kufulia, kuhifadhia maiti, nyumba za watumishi na uzio kuzunguka kituo hicho.

Alitaja huduma zinazotolewa katika kituo hicho kuwa ni kutibu wagonjwa wa nje ambao kwa mwezi ni hufikia 800 na zaidi, wajawazito ambao kwa mwezi uliopita walikuwa 95 na kliniki ya watoto kwa mwezi wanahudumia watoto 120.

RORYA WAMKOSHA DKT.GWAJIMA,AWAPA TANO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt.Dorothy Gwajima, akitoa maelekezo kwa Halmashuri zingine nchini kwenda kujifunza na kuiga mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ilivyofanya vizuri kwenye fedha Bil.1.5 za Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha, akimuelezea Naibu Katibu Mkuu jinsi walivyofanikisha ujenzi huo, pembeni yake ni mmoja ya Wastaafu ambaye wanamtumia kama afisa ugavi kwenye Halmashauri hiyo akisaidiana na maafisa Ugavi wa Halmashauri kutokana na umahiri wake katika kazi hiyo.
Moja ya Jengo la Hospitali hiyo kama linavyo onekana ni jengo la Utawala.
Naibu Katibu Mkuu akiwasalimia Wagonjwa katika kituo cha Afya Otegi ambacho nacho alikitembelea.
Mtaalam Mhandisi aliyeambatana na Msafara wa Naibu Katibu Mkuu, akitoa maelekezo kwa Wataalam Wahandisi wa Halmashauri wakati wa Ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha, akimuelezea Naibu Katibu Mkuu juu ya namna wananvyofanya ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya. 

……………………….
Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Mara
Halmashauri ya Wilaya ya Rorya imefanya vizuri katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unaondelea kujengwa hivi sasa, hali hiyo imepelekea Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika afya Dkt. Dorothy Gwajima, OR-TAMISEMI kutoa pongezi huku akiziagiza Halmashauri zingine kote nchini kuiga mfano wa Halmashauri hiyo. Siri ya mafanikio ya ujenzi huo uliofikia zaidi ya asilimia 80 umetokana na umoja, mshikamano na maelewano baina ya viongozi wa Halmashauri na Wilaya.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu, alisema hatua kubwa iliyofikiwa haina budi kupongezwa na kila mpenda maendeleo wa nchini, kwani yapo maeneo mengi ya nchi ambayo yalipata fedha za awamu ya kwanza shilingi bilioni 1.5 kama ilivyo Halmashauri ya Rorya, lakini mpaka hivi sasa wanabishana wapi Hospitali ijengwe huku wananchi wakiendelea kukosa huduma.

“Nikiri waziwazi kwakweli nyie mmekuwa wa mfano sana na hali hii ndio kurejesha fadhili kwa Rais wetu kipenzi cha watanzania Dkt. John Pombe Magufuli”, alisema Gwajima na kuongeza “ninatamani wengine wakaijua siri hii ya mafanikio, kwakuwa kuna Halmashauri huko sehemu zingine tulizopita ni vituko vitupu, pesa wamepelekewa toka Januari lakini hadi leo wanashindana wapi ijengwe Hospitali,” alishangazwa Dkt. Gwajima.

Kwa upande wao viongozi na Wataalam wa Halmashauri hiyo, walisema siri kubwa ni mshikamano na maelewano baina yao wenyewe lakini pia mawazo kutoka kwa wataalam.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simoni Chacha, alisema, kikubwa walichokifanya mara baada yakupokea fedha walikaa kwa pamoja na kuweka mikakati ya namna ya ujenzi utakavyo endeshwa na kwakiasi kikubwa waliwashirikisha baadhi ya wataalam wastaafu.

“Sisi Mhe. Naibu Katibu Mkuu, hatukutaka kujifungia ndani wenyewe tuliwahusisha wataalam wastaafu, lakini sisi Kamati ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yote tulikubaliana lazima tuwasikilize wataalam kwa ushauri wao na sisi kama wasimamizi hatukupuuza ushauri wao” alisema Chacha.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya hiyo Charles Chacha, alisema mara kadhaa Mhandisi na Mganga Mkuu wa Wilaya na wataalam wenzao walipokutana na jambo likawatatiza, basi waliwaomba ushauri na walijadili kwa pamoja namna yakutatua tatizo.

“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, kwakuwa hapakuwepo na muongozo wakuteua kamati baada ya mvutano niliamua kufanya maamuzi magumu ikiwapo hili lakuwashirikisha wataalam wastaafu akiwapo Afisa Ugavi wetu ambaye kila siku jukumu alilonalo ni jinsi gani anapokea vifaa na kuvitoa kwenye vitabu vyetu kwa utaratibu na kwakweli amekuwa msaada sana,” alisema Mkurugenzi.

Nao wataalama Wahandisi wanao simamia shughuli za ujenzi walisema, kufikia asilimia zaidi ya 85 ya ujenzi haikuwa kazi ndogo kwani kila mara wamekuwa wakifanya vikao eneo la kazi na kupitia kila kinachofanyika na wakifika mahali wakashindwa kuelewana wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na kwa aajili yakupata ushauri alisema Mhandisi wa Halmashauri hiyo.

Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, umefikia asilimia zaidi ya 80 kwa majengo yote yaliyo elekezwa na serikali kujengwa, Majengo hayo ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje asilimia 88, jengo la Maabara asilimia 87, jengo la Mionzi asilimia 87, na jengo la uzazi asilimia 86. Majengo mengine ni jengo la ufuaji 87 pamoja na jengo la Utawala asilimia 84, huku wakitazamia kukamilisha asilimia zilizobakia ndani ya miezi miwili ijayo ili huduma kwa wananchi zianze kutolewa.

Naibu Katibu Mkuu, yupo kwenye ziara yakukagua shughuli za Miradi ya Maendeleo hususan sekta ya afya, ambapo katika siku ya kwanza ametembelea Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya, Kituo cha Afya Otegi, Hospitali ya Mji wa Tarime , kituo cha Afya Magoma na Kituo cha Afya Nyamwaga ambacho kilisajiliwa kama zahanati lakini kwa sasa kutokana uhitaji na ukarabati mkubwa unaoendelea, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ameomba kipewe hadhi ya Hospitali ya Wilaya

WAZIRI SIMBACHAWENE, TAASISI YA SOKOINE WAKUTANA KUTAMBULISHA MRADI WA KUKABILI MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka Taasisi ya Kumbukumbu ya Sokoine waliofika ofisini kwake lwa lengo la kuutambulisha Mradi kuimarisha mfumo wa kupanga bajeti na kuhuisha masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Fasal Issa alisema Mradi huo wenye thamani ya sh. bilioni 2 utatekelezwa katika wilaya za Mpwapwa, Chamwino na Kondoa mkoani Dodoma.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kujengea uwezo wilaya hizo katika kuboresha uhimili wa mabadiliko ya tabianchi hususan katika sekta ya maji.

PROF. KABUDI AKUTANA NA MABOLOZI WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC WALIOPO NCHINI, WAANDISHI WA HABARI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza alipokutana na waandishi wa habari kuwaelezea Maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kikao cha pamoja na mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakizungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwaelezea waandishi wa habari maandalizi ya mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 – 8 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam
Baadhi ya mabalozi kutoka nchi za Afrika na Nordic wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani) wakati alipokutana nao kuzungumzia maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AZITAKA AZAKI ZIHIMIZE ULIPAJI KODI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi, kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Asasi Zisizo za Kiserikali 2019, yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma, Novemba 4.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

…………………………

*Ataka fedha wanazopata zitumike kujenga miradi mikubwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Asasi za Kiraia ziendelee kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kulipa kodi.

“Nitoe rai kwenu wana AZAKI, muendelee kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ili Serikali iweze kujenga miradi mikubwa ya kijamii,” amesema.

Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Novemba 4, 2019) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) nchini yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Maonesho hayo yatafikia kilele chake Ijumaa, Novemba 8, mwaka huu.

Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini kama vile kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Madiwani, viongozi wa vijiji na mitaa ili watambue majukumu yao.

“Niwatoe hofu tu kwamba Serikali inatambua mchango wenu wa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo; kujiongezea kipato na kupata ujuzi; utoaji wa huduma za kijamii hususan elimu, afya, upatikanaji wa maji, huduma za kisheria na huduma za mikopo midogo.

“Pia tunatambua mchango wa AZAKI wa kuleta teknolojia mpya na rahisi kwa wananchi pale mnapoona kuna uhitaji. Pia mnaisaidia Serikali kupinga mila potofu na kandamizi hasa kwa makundi yenye mahitaji maalum,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzitaka AZAKI nchini zizingatie sheria iliyofanyiwa marekebisho ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24/2002 na kanuni zake, ambayo ilipitishwa na Bunge kupitia Sheria Na. 3/2019 na kusisitiza kwamba marekebisho hayo yalilenga kuboresha sekta hiyo.

“Nipende kuwahakikishia wana-AZAKI kuwa marekebisho hayo yalilenga kuboresha sekta ya NGOs na siyo kuyabana mashirika yasiyo ya Kiserikali kama ambavyo imekuwa ikipotoshwa na baadhi ya watu. Marekebisho hayo yalizingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,” amesema.

Kuhusu mapato ya AZAKI, Waziri Mkuu amesema fedha wanazopata zinaweza kufanya miradi mikubwa ambayo itawanufaisha wananchi na akawasihi wazitumie kwenye ujenzi wa miradi mikubwa inayoonekana badala ya kuendesha semina na warsha.

“Tunajua fedha mnazopata zinaweza kusaidia kwenye miradi hii. Kwa mfano, kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu, tulifanya mapitio ya ufadhili wa fedha mnazopata. Na katika upekuzi uliofanyika kwenye taasisi 92, ilibainika kwamba zilipokea jumla ya sh. bilioni 261.059 ambazo zimeingia kwenye AZAKI hizi.”

“Vilevile, mwaka 2016 hadi 2017, tuliangalia mapato ya NGOs 51, tukagundua kuwa katika kipindi cha miaka miwili, zimepokea jumla ya shilingi trilioni 2.5. Kama fedha hizi zote zingeratibiwa vizuri kwa kupunguza matumizi yasiyo na umuhimu ni lazima tungefika mbali. Tutumie vizuri fedha hizi za ufadhili kwa miradi inayoonekana,” amesisitiza.

Akizungumzia kuhusu ajira kwa vijana, Waziri Mkuu amesema vijana ni kundi lenye umuhimu mkubwa katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo licha ya kuwa wanakabiliwa na uhaba wa ajira.

Amesema Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, inaonesha asilimia 35 ya Watanzania wote ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa nguvukazi ya Taifa wa mwaka 2014, vijana wamebainika kuwa ndio kundi kubwa la nguvukazi ya Taifa ambao ni asilimia 56 ya nguvukazi yote nchini.

“Kila mwaka, kumekuwa na ongezeko la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira. Kwa mfano, taarifa ya hali ya ajira ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa mwaka 2019 inaonesha kuwa asilimia 11.8 ya nguvukazi ya vijana duniani ambao ni takriban vijana million 59.1 hawana kazi,” amesema.

Mapema, Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Bw. Suleiman Jafo alizishukuru asasi zote za kiraia ambazo zinafanya kazi Tanzania kwa sababu zinawahudumia wananchi kwa karibu zaidi. “Ninazishukuru NGOs zote kwa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi. GTunazishukuru kwa kazi kubwa mnayoifanya Tanzania nzima kwa kushirikiana na Ofsi ya Rais TAMISEMI,”

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa maonesho hayo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu alisema mwaka huu, wizara yake imesajili mashirika yasiyo ya Kiserikali 617 ikilinganishwa na mashirika 385 yaliyosajiliwa mwaka 2017.

“Kati ya hayo mashirika 617, mashirika 44 ni ya ngazi ya kimataifa; 551 ni ngazi ya kitaifa, saba ni katika ngazi ya mikoa na mashirika 15 ni katika ngazi ya wilaya. Hadi kufikia Oktoba, 30, 2019, tumeshasajili mashirika 19,318” alisema.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 5,2019

MKUTANO WA KUMI NA SABA WA BUNGE KUANZA LEO JIJINI DODOMA

SHEHENA YA MIFUKO ISIYOKIDHI VIWANGO YAKAMATWA

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kusimamia marufuku ya katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kushirikiana na Kikosi kazi cha Kitaifa. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la uzalishaji, utengezaji na uingizaji na usambazaji wa mifuko isiyokidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki pamoja na Kamati za Mikoa na Wilaya wanaendesha oparesheni maalumu nchi nzima kwa lengo la kusaka mifuko isiyokidhi viwango.

Tarehe 30/10/2019 NEMC ilikamata marobota 21 katika Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera na marobota 7 Mkoani Arusha ambayo yanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Arusha. Upelelezi wa mashauri haya bado unaendelea.

Leo tarehe 4/11/2019 Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi kwa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza wamekamata shehena ya mifuko isiyokidhi viwango gunia 8 yenye thamani ya Shilingi 10,000,000/- Mifuko hiyo iliingia kupitia bandari bubu ya Bwiru jijini Mwanza ikitokea nchi jirani. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani na mifuko hiyo itateketezwa kwa mujibu wa sheria kama itakavyoelekezwa na NEMC.

Ofisi ya Makamu wa Rais, inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko mbadala kuhakikisha wanazingatia matakwa ya Sheria. Aidha, wafanyabiashara wanasisitizwa kuacha kuzalisha, kuingiza nchini, kuuza na kusambaza mifuko isiyokidhi viwango. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote wanaokiuka agizo hilo.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images