Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

WALEMAVU 200 WATUNUKIWA VYETI VYA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

$
0
0
Charles James,Michuzi TV

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa watu wenye uhitaji maalum ili kuweza kuwanasua katika kundi la ombaomba na kuwafanya wawe tegemezi kwa kuwa na miradi yenye kuwapa kipato.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella Ikupa wakati alipokua akifunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mafunzo hayo yalianza toka Novemba 29 ambapo yaliandaliwa na Taasisi ya NAKUA NA TAIFA LANGU kwa kushirikiana na Diwani wa Kata hiyo Mhe Kenneth Lindi ambapo yalihusisha watu wenye ulemavu na wanawake.

Elimu iliyotolewa ni Elimu ya kujitambua, Elimu ya usindikaji bidhaa kwa vitendo, Elimu ya masoko, Athari ya matumizi ya rushwa katika upatikanaji wa huduma, Umuhimu na utaratibu wa kuunda vikundi vya walemavu na wanawake pamoja na Elimu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo.

Akizungumza na wahitimu hao, Naibu Waziri Ikupa amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya NAKUA NA TAIFA LANGU, Jessica Mshama kwa uzalendo aliouonesha kwa kuamua kutoa elimu kwa watanzania wenzake ambayo itawaondoa kwenye lindi la umaskini.

" Nikupongeze sana Jessica umefanya jambo kubwa siyo tu kwa Wananchi wa Buigiri bali kwa Taifa lako kwa ujumla. Elimu hii uliyowapa ina manufaa makubwa kwao wenyewe na hata kwa kizazi chao. Niwaahidi Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa maendeleo katika kuwakomboa watu wetu," Amesema Mhe Ikupa.

Amesema ili kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ni lazima kila kundi nchini lihusike katika uzalishaji na kuwapongeza wahitimu hao kwa kuelewa mafunzo vizuri na kuanza kutengeneza bidhaa zao ikiwemo Ubuyu, Siagi ya Karanga pamoja na Sabuni.

Nae Mkurugenzi wa NAKUA NA TAIFA LANGU, Jessica Mshama amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu ya kujitegemea watu wenye ulemavu ili kuepukana na dhana ya kwamba walemavu wote ni ombaomba.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imepiga hatua kwenye maendeleo hivyo wao kama wadau wana kila sababu ya kusaidia Rais Magufuli katika kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

" Mhe Waziri tunashukuru kwa kufungua na kufunga mafunzo haya. Tunakuahidi kuwa Taasisi yetu itaendelea kutoa mafunzo haya Nchi nzima lakini pia kuwatafutia masoko ya bidhaa wanazotengeneza hawa wahitimu.

 Tayari Dodoma tushatoa elimu kwa watu 300 hapa Chamwino na Wilaya ya Chemba, tutaenda Kongwa, Mpwapwa na Wilaya zingine. Lakini lengo letu ni kuona tunawainua kiuchumi walemavu na wanawake nchini," Amesema Jessica.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Kenneth Yindi ameishukuru Serikali na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo hayo ambayo anaamini yataenda kubadilisha mtazamo na fikra za wananchi wa Kata ya Buigiri.

Amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuweza kujitambua na kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zitakua na nembo ya Buigiri jambo ambalo litasaidia Kata yao kukua kimaendeleo na kuvutia watu kuja kuwekeza na hivyo kuongeza mapato ndani ya Halmashauri yao.

" Hakika tunaipongeza Taasisi ya NAKUA NA TAIFA LANGU kwa kuendesha mafunzo haya, wametoa kiasi cha Sh Milioni Tatu za ueneshaji sambamba na walimu wawili, huu ni uzalendo mkubwa waliouonesha kwetu na tuwaombe waendelee kushirikiana na Serikali yetu ili kufikia kundi kubwa la watu wenye uhitaji," Amesema Yindi.

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, John Masaka ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo katika kufanikisha inawakomboa wananchi wake na kuahidi kutumia mafunzo hayo vizuri ili kujipatia kipato na kuepukana na dhana ya kwamba watu wa Dodoma ni ombaomba.

Pamoja na kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu Naibu Waziri Ikupa alifungua pia Soko la Buigiri kwa ajili ya walemavu hao na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino kuwaongezea kiasi cha Sh Milioni Tatu ili waweze kukuza mitaji yao.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe Stella Ikupa akikata utepe kuashiria kufungua Soko la Buigiri ambapo litatumika na watu wenye ulemavu waliomaliza mafunzo ya Ujasiriamali.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya NAKUA NA TAIFA LANGU, Jessica Mshama akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo ambayo Taasisi yake imekua ikiendesha. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe Stella Ikupa akisikiliza maelezo ya mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali katika Kata ya Buigiri wilayani Chamwino ambalo baadhi ya bidhaa wanazozitengeneza ni pamoja na Siagi ya Karanga na Ubuyu.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya Ujasiriamali wilayani Chamwino, Dodoma.
 Diwani wa Kata ya Buigiri, Kenneth Yindi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo ya Ujasiriamali wapatao 200 ambao ni Walemavu na Wanawake.
 Naibu Waziri Stella Ikupa akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali yaliyotolewa na Taasisi ya NAKUA NA TAIFA LANGU katika Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino.

KOCHA MKUU TAIFA STARS ATAJA MAMBO MATATU TANZANIA KUFANIKIWA KATIKA SOKA

$
0
0
Kocha Mkuu wa Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije

Na Said Mwishehe, Michuzi Tv
KOCHA Mkuu wa Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije ametaja mambo matatu ya kufuatwa iwapo tunahitaji kuinua soka letu nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kocha Ndayiragije ameeleza kwa kina mambo ya msingi ambayo nchi yetu inatakiwa kufanya ambayo ni kuwekeza katika soka la vijana, pili viwanja vizuri vya soka na tatu kila mdau wa soka atimiwe wajibu wake.

Akifafanua zaidi amesema kuwa ili kuwa na timu nzuri kwenye vilabu vya Tanzania na kukuza soka, ni vema eneo la kuweka kwa vijana likapewa kipaumbele kwani ndioko ambako wachezaji wazuri wanaandaliwa vya kutosha na hatimaye kupata timu bora kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Kuhsuu viwanja vizuri, Kocha huyo amesema ili kuwa na wachezaji wazuri na walioandaliwa lazima wapate viwanja vilivyokuwa na viwango vya soka."Uzuri wa kiwanja cha soka ni eneo muhimu sana, hivyo ni vema kwa vilabu vya soka nchini Tanzania kuona ni namna gani wanaweza kuwa na viwanja vizuri kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka.Kwangu ubora wa kiwanja ni jambo muhimu katika kukuza soka la nchi husika."

Pia amesema jambo la tatu ili kufanikiwa katika soka ni kuhakikisha wadau na wapenda soka wanatimiza wajibu wao kikamilifu ambapo amesema waandishi wa habari za michezo na wachambuzi wa soka wanatakiwa kutimiza wajibu wao, Shirikisho la Mpira wa Miguu nao watimize wajibu wao na makocha nao wafanye kazi yao kikamilifu.

"Kila mmoja akitimiza majukumu yake nina uhakika tutapiga hatua sana katika medani ya soka.Hivyo nishauri kila mmoja awe na jukumu la kuhakikisha anakuwa sehemu ya kufanikisha wajibu wake kwa ajili ya nchi,"amesema Kocha Ndayiragije.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza katika kazi yake ya ukocha amefundisha katika nchi tisa za Bara la Afrika lakini alichobaini Tanzania kuna vipaji vya hali ya juu vya soka, hivyo kikubwa ni kuwekwa mikakati thabiti kuendeleza vipaji hivyo.

Pamoja na uwepo wa vipaji vya soka, ameonesha hofu kutokana na vilabu vingi kukosa uwezo wa kutosha katika kuendeleza vipaji hivyo akitoa mfano kuwa mchezaji anaweza kuwa na kipaji na yuko katika klabu ambayo haina uwezo mkubwa kifedha, hivyo ikitokea klabu yenye uwezo inamchukua na akifka hapati nafasi, hivyo matokeo yake kipaji kinapotea.

WAZIRI DOTO BITEKO AELEZEA MAFANIKIO YA SEKTA YA MADINI KATIKA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

ONYO KALI LATOLEWA KWA WATU WENYE KUTAKA KUVURUGA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA , KUVUNJA AMANI ILIYOPO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Kangi Lugola akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Uhalifu na matumizi mabaya ya silaha na  mitandao ya kijamii.

WIZARA ya Mambo ya Ndani pamoja na Jeshi la Polisi wametoa onyo kali kwa watu ambao watabainika kutaka kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kutoa lugha za kuchonganisha au kupotosha.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na wote ambao wanatarajia kufanya matukio ya uvunjifu wa amani na kwamba mbali ya kutiwa nguvuni wajiandae kudumbukizwa kwenye maji ya washawasha na si kumwagiwa maji hayo kama ilivyozoeleka.

Akizungumza  leo Novemba 2,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema kuwa ole wao wenye mipango ya kuvuruga uchaguzi kwani watashughulikiwa na kwamba vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri.

"Kuna watu wamekuwa na tabia ya kutoa lugha za kuchonganisha wananchi kwa kisingizo cha kufanya kampeni wakati wa mikutano ya kampeni. Wale wenye tabia ya kupotosha au kuvunja amani safari hii hawana nafasi,anayebisha ajaribu hata sasa aone .Washawasha watamwagiwa na sio tu kumwagiwa bali tutawatumbukiza katika maji yenyewe,"amesema Waziri Lugola.

Ameongeza kuwa Polisi wameandaa mpango kazi kuhakikisha UCHAGUZI wa Serikali za Mtaa unakwenda vizuri ,hivyo atakayethubutu kujaribu kuuvuruga atakiona cha moto chini ya yeye(Waziri) , IGP Sirro na Rais Dk.John Magufuli wamedhamiria kuhakikisha amani iliyopo nchini inaendelea kuwepo na hakuna anaeweza kuivuruga kwa kigezo cha uchaguzi.

Wakati huo huo Waziri Lugola amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kushughulikia matatizo ya wananchi na kwamba ametoa maagizo kwa IGP Sirro kuhakikisha makamanda wa Polisi katika Mikoa yote na Makamanda wa Polisi wa Wilaya wanapanga ratiba ya kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia kazi.

Amesema katika ziara za viongozi wakuu wa nchi, wamekuwa wakipokea malalamiko na hivyo wamekubaliana makamanda hao watoke na ameahidi kufuatilia utendaji wao na wale ambao watafanya kazi kwa kusuasua wajiangalie kwani hatawavumilia .

TAKUKURU NA POLISI WAASWA KUFANYIA KAZI TAARIFA ZA RUSHWA ZINAZOTOLEWA NA WANANCHI ILI WAENDELEE KUTOA TAARIFA HIZO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akikata utepe
kuzindua rasmi Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya
barabarani inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau
mbalimbali, uzinduzi huo uliofanyika jana katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza
na wananchi na wadau (Hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi wa
Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani inayohusisha
TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali, uliofanyika jana katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akitoa neno la utangulizi kuhusu
uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani
kabla ya kumaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H.
Mkuchika (Mb) kuzindua rasmi kampeni hiyo kwa niaba Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Kuzuia Rushwa wa TAKUKURU Bi. Sabina Seja
akizungumza kwa niaba Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuhusu
uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani
inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali ulifanyika
jana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

*******************************

Na James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Novemba 02, 2019

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi
nchini zimetakiwa kufanyia kazi taarifa za rushwa zinazotolewa na wananchi na wadau ili kuwajengea imani kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa zitakazowezesha vyombo hivyo kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa barabarani kwani kumekuwa na malalamiko ya uwepo wa rushwa hiyo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) wakati akizindua Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani na Mfumo wa Kuchukua Taarifa (TAKUKURU Mobile App) inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na usalama barabarani na hatimaye kupunguza ajali za barabarani.

Mhe. Mkuchika amewataka wananchi kutenda haki kwa kutoa taarifa za ukweli zinazojitosheleza na kuongeza kuwa fursa hii isitumike kuwakomoa wasimamizi wa Sheria za Barabarani ambao kwa namna moja au nyingine tumekwaruzana nao katika shughuli zetu za kila siku.

Pia, Mhe Mkuchika ametoa wito kwa wadau kushiriki kikamilifu katika kampeni hii na kumtaka kila mdau kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa atakavyokutana navyo pindi anapotumia barabara.

“Serikali inamtaka kila mdau kujenga tabia ya kuhoji na kutoa taarifa pale
ambapo mazingira yanaonyesha au kuashiria uwepo wa rushwa barabarani na kwa kufanya hivyo tutakuwa na uzalendo kwa nchi yetu”, Mhe.Mkuchika
amehimiza.

Kabla ya Kumkaribisha Mhe. Mkuchika kuzindua Kampeni ya UTATU, Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael amesema vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumiaji wa barabara vinachafua tasw ira ya nchi na kupunguza sifa tunazopatakatika vita dhidi ya rushwa, hivyo kunahitajika ushirikiano wa dhati wa wadau wote ili kupambana kikamilifu katika vita hii ya rushwa barabarani.

Dkt. Michael amesema siku hii ya Uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ni maalum katika kuhakikisha wadau wanashiriki kikamilifu kusimamia utekelezwaji usalama wa barabarani na ndio maana Serikali itazindua mfumo rasmi wa TAKUKURU

Mobile App utakaowezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
barabarani ili kuepusha ajali zinazosababishwa na vitendo vya rushwa.

Awali, Mkurugenzi wa Kuzuia Rushwa wa TAKUKURU Bi. Sabina Seja
akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amesema, lengo la kujumuika pamoja ni kuendeleza msukumo katika mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na kupata nafasi ya kuielimisha na  kuishirikisha jamii kuhusu tatizo la vitendo vya rushwa barabarani ambalo tafiti nyingi zilizofanyika zinaonesha kuwa wananchi wanalalamikia vitendo hivyo.

Bi. Seja amesema, Kampeni inayohusu UTATU itawawezesha wadau kutafakari kwa pamoja hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na tatizo la rushwa barabarani.

Bi. Seja ameyataja malengo ya Kampeni ya UTATU kuwa, ni kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa wasimamizi wa sheria za barabarani, kuandaa mkakati wa kuzuia vitendo vya rushwa barabarani, kushirikisha umma kuzuia vitendo vya rushwa barabarani na kutumia TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani ambapo tayari TAKUKURU imeshatengeneza mfumo wa TAKUKURU App ambao utakaowawezesha wananchi kuchukua matukio ya vitendo vya rushwa kwa kutumia simu za mkononi kupiga picha za video, mnato na kurekodi sauti na kutuma katika mfumo huo ili kufanyiwa kazi.

Naye, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema
mkakati wa Kampeni ya UTATU ni sehemu ya matakwa ya kihistoria na kitaasisi katika jitihada za kupambana na rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ambayo ilitungwa baada ya kufutwa Sheria ya Kuzuia Rushwa ya TAKUKURU Sura 329 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kauli mbiu ya Kampeni hii UTATU iliyozinduliwa na Serikali kwa Ushirikiano wa TAKUKURU, Jeshi la Polisi na wadau mbalimbali inasema ‘KWA USALAMA WAKO KATAA RUSHWA BARABARANI’.

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA WILAYANI HANDENI KUONA NAMNA YA KUWANUSURU WANANCHI ELFU 55

$
0
0


Moja ya mabwawa ya maji yaliyoharibika wilayani Handeni na kupelekea wananchi kukosa huduma ya maji kutokana na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na kusababisha mafuriko 
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakioangalia maeneo mbalimbali ya mabwawa hayo ambayo yameathirika
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kulia katikati ni Mbunge wa Jimbo la Handeni mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliyevaa kofia na miwani 
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akiwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni William Makufwe
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa  katikati akisisitiza jambo kwa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembela eneo la mabwawa hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni (CCM) Omari Kigoda 
 muonekano wa moja ya mabwawa ya maji wilayani Handeni
WAZIRI wa Maji Pro,Makame Mbarawa amelazimika kufanya ziara ya  wilayani Handeni Mkoani Tanga ili kuona namna ya kuweza kuwanusuru zaidi wananchi elfu 55 waliokumbwa na tatizo la kukosa huduma ya maji safi na salama kutokana na mabwawa 12 yaliyokuwa yakitumika kutoa huduma hiyo kuathirikawa na mvua zilizonyesha Mkoani hapa.


Mvua hizo ambazo zilisababisha athari kubwa ya kusomba mabwawa hayo ya maji na kupelekea wananchi hao kukosa maji wilayani humo jambo lililomlazimu Waziri huyo kuambatana na viongozi Mamlaka mbalimbali za maji ili kuweza kurudisha huduma hiyo na kuwanasuru wananchi hao na ukata wa maji.


Akizungumza mara baada ya kutembelea mabwawa hayo yaliyobomolewa na na mvua hizo, Waziri Mbarawa alisema kwamba hilo ni janga ambalo linaweza kutokea wakati wowote hivyo kupitia Mamlaka zilizopo watahakikisha mji huo unapata maji kwa kuunganisha na mradi wa maji wa htm Korogwe ambao utaleta maji Handeni ambapo kunatakiwa bomba la mita 300 wataalamu wataletwa ili kuweza kufanikisha suala hilo.


 “Leo Bomba litafika kwa sababu kuna miradi mingi inaendelea kwenye mamlaka zote nchini watatoa bomba haraka lije hapa na tuna timu ya wataalamu kutoka mikoa ya Moruwasa, Tanga Uwasa na Dawasa lakini bomba likifika haraka lifungwe kuondosha changamoto hiyo haraka “Alisema  


Waziri Mbarawa alisema kwamba wataalamu wanapaswa kufanya kazi kwa kipindi cha wiki moja ili huduma ya maji iweze kujerejea Wilayani hapa huku maeneo ya vijiji yaliyoathirika wataalamu wa bonde la mto Pangani wanatakiwa kuchimba visima harakaharaka na kwa kutumia gari lililopo  Wilayani Pangani namba 83 kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.


“Tunachokifanya hapa ni jambo la dharura hawa watu watakao kuwa na shughuli za uchimbaji wa visima natambua watu wa Tanga-Uwasa wapo hapa mtawapatia fedha kwa ajili ya shughuli hiyo na ianze mapema iwezekanavyo”Alisema Prof,Mbarawa.


Akizungumzia mipango ya muda mrefu alisema ili kuondoa tatizo hilo watahakikisha wanaona namna ya kujenga miundombinu imara ikiwemo kuongeza nguvu kwa lengo la kuweza kuyaangalia upya mabwawa yote yanakuwa salama zaidi ili zinaponyesha mvua zisiweze kuleta athari kama iliyojitokeza na kupelekea wananchi kukosa huduma hiyo muhimu.


“Lakini pia tutahakikisha tunayalinda mabwawa hayo kwasababu bwawa ni jambo kubwa sana na kama tusipifanya hivyo yanaweza kupasuka na kuleta athari kwa wananchi pia tutaangalia mipango yake ya kupitia na sisi wizara tutaongeza nguvu na utaratibu mpya kuweka ulinzi kwenye sehemu ya mipango yake ya kupitia kama yanaweza kupita na yanakuwa salama na wananchi waweze kuepukana na athari”Alisema


Akieleza namna walivyopambana na suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema baada ya kuwepo kwa tatizo hilo  alikutana na Meneja wa Ruwasa Mkoa ambaye alieleza namna alivyoandika mapendekezo yake na na kuyawasilisha wizarani ambpo waziri huyo ulimuelekeza Naibu Kati bu Mkuu ufike eneo hilo na aweze kujionea hali halisi.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba jambo hilo liliwapa faraja kubwa kutokana na kwamba serikali kuwakimbia wakati wa tatizo hilo ambalo lilikuwa limeshawavuka uwezo wao lakini kwa ujio wake wanamatuimani wanaweza kupata ufumbuzi wa mji huo kupata maji ya kutosha.


“Ninaishukuru wizara imefanya jambo kubwa muhimu kufanya kuhakikisha Handeni inapata maji ya kutosha ambayo miaka ya nyuma haikuwahi kupata na changamoto hiyo imepeleka kubomoka madaraja na barabara kwa maana presha ya maji ikawa kubwa hivyo niishukuru sana “Alisema RC Shigella.

Takwimu Rasmi Zatajwa Kuchochea Ufanisi wa Miradi

$
0
0
Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia Bw. Rob Swinkels akisisitiza kuhusu faida za ushirikiano ulipo kati ya Tanzania na Benki hiyo hali iliyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya pili Barani Afrika kwa ubora wa Takwimu baada ya Afrika ya Kusini, hayo yamejiri Oktoba 31, 2019 Jijini Dodoma wakati wa kikao kati ya ujumbe huo na menejimenti ya NBS ili kufanikisha Mpango Kambambe wa Taifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu (TSMP) awamu ya pili.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wale wa kutoka Benki ya Dunia wakiwa kwenye mkutano wa pamoja leo kwa lengo la kujenga uwezo kwa menejimenti ya NBS ili kufanikisha Mpango Kambambe wa Taifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu (TSMP) awamu ya pili.

Na; Mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano imetajwa kufanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na matumizi bora ya takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mtakwimu mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa Ofisi hiyo imefanikiwa kuzalisha takwimu zenye ubora wa viwango vinavyokubalika kimataifa hali inayochochea mafanikio ya miradi inayotekelezwa ikilenga kuchochea ustawi wa wananchi.

“Tunatarajia kujenga Ofisi katika mikoa yote hapa nchini ili kuboresha zaidi mfumo wa ukusanyaji takwimu kuiwezesha Serikali kupanga mipango yake kwa ufanisi mkubwa zaidi” Alisisitiza Dkt. Chuwa.

Akifafanua amesema kuwa takwimu bora ni msingi wa maendeleo yaliyofikiwa hapa nchini katika sekta zote zinazolenga kuleta ustawi wa wananchi. Akizungumzia utekelezaji wa mpango Kabambe wa Taifa wa Kuboresha na Kuimarisha.

Takwimu (TSMP) awamu ya pili Dkt. Chuwa amesema kuwa unalenga kufanya maboresho zaidi katika ukusanyaji na uchakataji wa takwimu kwa kujenga miundombinu bora zaidi hadi ngazi ya mikoa ikiwemo majengo.

“Lengo namba 17 la Malengo ya Millenia linasisitiza ushirikiano kati ya Serikali na wadau ili kuchochea maendeleo ya wananchi ndio maana tumekuwa na ushirikiano huu na Benki ya Dunia” Alisisitiza Dkt Chuwa.

Kwa upande wake mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi. Bi Nadia Belhaj Hassine Belghith amesema kuwa Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na nyingine kutokana na matumizi ya takwimu zenye viwango na ubora unaotakiwa.

“Takwimu zinawawezesha wakulima kujua wapi yalipo masoko ya mazao yao hivyo kuchochea maendeleo yao na nchi kwa haraka zaidi” Alisisitiza Bi. Belghith.

Akifafanua amesema kuwa takwimu ni msingi na kichocheo cha maendeleo katika Taifa lolote kama ilivyo kwa Tanzania ambayo katika Afrika ni ya pili kwa kuzalisha Takwimu Bora.

Ujumbe wa Benki ya Dunia na Ofisi ya NBS wamekutana Jijini Dodoma kwa wiki moja katika mkutano wa mashauriano wa kuimarisha ushirikiano wao. Katika mkutano huo moja ya masuala yaliyozungumziwa ni kufanikisha utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Pili wa Taifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu (TSMP II) unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2019/ 2020 hadi 2024/ 2025 baada ya kumalizika kwa mpango kama huo mwezi Juni mwaka jana.

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA USAFIRISHAJI:WAZIRI MHAGAMA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika Novemba 1, 2019 Dodoma.


Katibu Mkuu wa TABOA Bw. Enea Mrutu akichangia jambo wakati wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Baadhi ya washiriki wa Kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.
Viongozi wa vyama vya wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama na Naibu wake Mhe Antony Mavunde wakishuhudia zoezi la utiaji saini wa maazimio ya kikao cha pamoja kati ya wadau wa sekta ya uchukuzi na Serikali kilichofanyika Novemnba 1, 2019 Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

******************************


Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi.

Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

“Moja ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama

Kutolewa kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.

Alifafanua kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali, wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona namna sheria za kazi zinavyozingatiwa.

Azimio jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.

“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.

CHADEMA WALALAMIKA WAGOMBEA WAO KUNYANG'ANYWA FOMU NA KUCHANWA WAKATI WAKIREJESHA

$
0
0
Na Woinde Shizza globu ya jamii ,Arusha




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha kimekutana na kujadili changamoto za urejeshwaji wa fomu za wagombea wake Katika nafasi ya serikali ya Mtaa kitongoji na vijiji.

Aidha chama hicho kimebaini kuwa zoezi hilo lilifanyika bila kuwepo kwa demokrasia kwani wagombea wake walikuwa wananyanganywa fomu na kuchanwa kwa kutumia mabavu huku wakitishiwa kwa bastola kupitia kwa makada Wa ccm

Akizungumza na vyombo vya habari Katibu wa Chadema Arusha Innocent Kisanyage Amesema kwamba makada wa chama chamapinduzi Ccm wamekua wakitumia nguvu kubwa kunyanganya Fomu za wagombea na kuchana kwa kushirikiana na wasimamizi wa vituo huku watendaji wa Kata wakikimbia vituo vyao vya kazi .

Amesema kitendo hicho kinaonyesha kwamba Chadema Mkoa Wa Arusha bado ni tishio kubwa kwakua inatumika nguvu nyingi kuhakikisha kwamba wanashindwa kuwaweka wagombea.

Aidha Baadhi ya wagombea walio nyanganywa fomu zao na kupigwa mapanga na wengine kunyooshewa bastola wamesema walifika kituo kikuu cha Polisi jijini Arusha lakini walijibiwa watoe fomu za kugombea ndio wapate P 3 ili waweze kupatiwa matibabu.

Sakata la urudishwaji wa fomu kwa wagombea wa vyama vya siasa limebubujikwa na sintofahamu kwani watendaji wamekua wakiwarudisha wagombea wa upinzani kwa kile wanacho Dai kwamba hawana sifa za kugombea nafasi hizo 

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini God Bless Lema amesema kwamba kitendo hicho nicha kiuni kwani Ccm wanatumia nguvu kubwa kuaharibu uchaguzi na kama wanataka upinzani wajitoe waseme kwamba uchaguzi ni wa chama kimoja tu 

Lema ameeleza kwamba awapo tayari kuona uchaguzi mdogo unatumika nguvu kubwa kuwaumiza wagombea kwa kunyooshewa bastola mapanga kwani nchi hii ni ya kila Mtanzania na sio mtu mmoja peke yake 

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure amesema mpaka sasa vijiji vyote katika jimbo la Arumeru Magharibi na mashariki Munduli akuna mgombea aliyefanikiwa kurejesha fomu na kumekuwepo na huuni mkubwa kwa kutishiwa na wengine kukimbiwa na watendaji wa kata

Uchaguzi huo Mdogo kabla kuelekea uchaguzi mkuu mwakani tayari umeonyesha kwamba Ccm aikubaliki ndio maana wanatumia jeshi la Polisi kuvuruga uchaguzi huo 

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha Msena Bina amesema akuna malalamiko yoyote walio pokea kutoka kwa Chadema wala wagombea wa nafasi hizo . 

Wananchi Mbeya Wanufaika na Ujenzi wa Miundombu Sekta za Afya, Elimu na Maji

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa MbeyaMhe.Albert Chalamila 

Serikali ya Awamu ya Tano imeuwezesha mkoa wa Mbeya kujenga miundombinu ya kisasa katika sekta zinazochangia kuleta ustawi kwa wananchi ikiwemo afya.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila amesema kuwa mkoa huo umepiga hatua kubwa katika kuleta mageuzi kupitia miundombinu iliyojengwa katika sekta za afya, elimu, maji, uchukuzi na kilimo.

“Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika mkoa wetu na ziko katika hatua za mwisho kukamilika ili ziweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali kuboresha sekta hiyo” Alisisitiza Chalamila.

Akifafanua, mhe. Chalamila amesema kuwa mkoa huo umefakiwa katika ujenzi wa Vituo vya Afya hali inayoboresha huduma zinazotolewa katika sekta hiyo katika Halmashauri za Wilaya mkoani huo.

Sehemu ya Halmashauri za Wilaya zilizonufaika na ujenzi wa Hospitali za Wilaya ni; Rungwe,Busokelo na Kyela,pamoja na upanuzi na ujenzi wa Vituo vya Afya ili
kutimiza lengo la Serikali kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wote.

Katika sekta ya Elimu Mhe. Chalamila amesema kuwa Shilingi Bilioni 18 zimetolewa katika kuboresha sekta hiyo hivyo kukuza kiwango cha elimu na ubora kutokana na uwekezaji huo uliofanywa na Serikali.

“Tumejipanga katika kukuza sekta ya viwanda na tumetenga eneo maalum la
uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na tayari baadhi ya wajasiriamali wa mkoa huo wamepata fursa ya kwenda nchini China kujifunza namna ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vya usindikaji mbogamboga na matunda,” Aliongeza Chalamila.

Akieleza zaidi, amesema kuwa mkoa huo umeweka mkazo katika kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta mbalimbali ili kuboresha hali ya maisha.

Aidha, Katika Halmashuri ya Wilaya ya Busokelo, Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo utakaogharimu shilingi Bilioni 5.3 ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Rungwe Bi Rehema Peter amesema kuwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 5 utawanufaisha wananchi zaidi ya elfu ishirini.

“Kukamilika kwa mradi huu wa maji kutaongeza wananchi wanaofikiwa na huduma ya maji kutoka asilimia 65 hapo awali hadi kufikia asilimia 80 hali itakayochochea kukua kwa shughuli za kiuchumi na ustawi wa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. James Kasusura amesema kuwa wamefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo katika robo ya kwanza ya mwaka 2019/2020 kwa kukusanya shilingi Bilioni 3.1 sawa na zaidi ya asilimia 26 ya lengo walilojiwekea.

Tumeweza kukarabati nyumba 25 za walimu katika Jiji letu na pia tumejenga kituo cha afya Nzowe kwa shilingi milioni 700 zilizotolewa na Serikali.
Kipindi cha TUNATEKELEZA kinaratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO na kurushwa na Shrika la Utangazaji Tanzania, Awamu hii ikiwashirikisha Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara.

NAIBU WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI BASEKI KWA KUIHUJUMU SERIKALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Mhandisi Leonard Baseki kwa kuihujumu serikali na kushindwa kukamilisha mradi wa maji Mkuranga.

Akizungumza baada ya kupata taarifa ya mradi wa maji Mkuranga, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara kufuatilia suala hilo na kumsimamisha kazi mhandisi huyo kwa kuihujumu serikali.

Aweso amesema, mhandisi wa maji Baseka ameshindwa kutekeleza mradi huo na kuishia kuihujumu serikali zaidi ya Bilion 2 kwa kujenga mradi ambao hauna chanzo cha maji.

" Haiwezekani mhandisi tena wa serikali anaharibu hapa Mkuranga halafu anahamishiwa sehemu nyingine na kule anaenda Kuharibu pia kwahiyo nimemuagiza Katibu Mkuu amsimamishe kazi na apelekwe kwenye bodi ya wahandisi," amesema.

Aweso amesema, tayari wahandisi 95 wameshaondolewa kutokana na kutokukamilisha miradi na kuiingiza serikali  hasara na kuchelewesha adhma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani

"Nawaonya wahandisi wengine kuwa hatutafumbia.macho pindi wanapohujumu Serikali tutawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka mbele ya kamati ya maadili," amesema

Akizungumzia mradi wa maji wa Mkuranga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA, Aweso amemtaka Mkandarasi wa mradi huu kwenda kwa haraka ili wananchi wapate maji kwa wakati kama makubaliano yalivyo kwenye mkataba.

Zaidi, Aweso amesema amewaagiza  DAWASA kufanya kikao cha pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Mkuranga na kufanya usanifu wa mradi wa Maji ili wakazi wote wa Mkuranga wapate maji.

"Nawapongeza DAWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendesha miradi, kwa fedha zao za ndani hili ni jambo kubwa sana tumeona Dar es Salaam wamefanya kazi na sasa wameamua kuja Mkuranga ili wananchi mpate maji safi na salama," amesem Aweso.

Aweso ameendelea na ziara yake ndani ya Mkoa wa Pwani wa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuweza kumtua mama ndoo kichwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Bakari Mgaya alipofika kulikagua tanki la maji lililopo kwenye hatua ya ujenzi litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion 1.5 na kuhuhudumia wakazi 25,000 kwa siku Mkuranga Mkoani Pwani

 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Mhandisi Bakari Mgaya wakati alipotembelea miradi ya maji Mkuranga Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisalimiana na Katibu wa Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, Omar Kisatu baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkuranga leo.
Vifaa na mabomba yanayotumika kulaza kwa ajili ya usambazaji wa maji Mradi wa Mkuranga.
Msimamizi wa  Mradi wa Mkuranga kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA  Mhandisi Bakari Mgaya akisoma taarifa ya mradi ws Mkuranga ambao umefikia hatua ya ujenzi wa tanki la Lita Milion 1.5 wenye thamani ya Bilion 5.5 wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso leo Mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati alipotembelea miradi ya maji ya Wilaya hiyo leo Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na watendaji mbalimbali wa Mamlaka za Maji, watendaji wa serikali wakati alipotembelea miradi ya maji Mkuranga leo Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiyaonja maji yanayotoka katika chanzo cha maji asilia kitakachopeleka maji kwenye tanki linalohifadhi maji Lita Milion 1.5 lililopo kwenye hatua ya ujenzi litakalohudumia wakazi 25,000.

MAHOJIANO YA RAIS .DK.SHEIN NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR ZBC

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akijibu suala wakati wa mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Ndg,Chande Omar Omar yanayohusu miaka tisa ya Uongozi wake,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]02/11/2019.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Ndg,Chande Omar Omar akiuliza suala wakati wa mahojiano yanayohusu miaka tisa ya Uongozi wake,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]02/11/2019.

MHE.MALEMBEKA ATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KWA UWT.

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa ndugu Thuwayba Edington Kisasi(kushoto), akikabidhi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo ndugu Mariam Shomari( wa pili kutoka kulia), iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa huo Mhe.Angelina Adam Malembeka.
SHEHA wa Shehia ya Kitope ndugu Khamis Ndende(wa pili kutoka kulia), akimkabidhi Afisa Takwimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘B’ ndugu Shaibu Hambal( kushoto) Mifuko 50 ya Saruji iliyotolewa na Mbunge huyo Mhe.Angelina Malembeka kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Kichungwani.
*******************************

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) kimewataka wanachama wa jumuiya hiyo kuwaruhusu viongozi kutoa michango mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya ujenzi wa majengo ya jumuiya kwa mujibu wa utaratibu.
Imesema si viongozi tu bali hata wanachama wowote wanaruhusiwa kutoa michango hiyo ili mradi wapitie katika utaratibu ambao umewekwa ili kutoa sitofahamu.
Kauli hiyo ameitoa Makamu wa Mwenyekiti UWT Taifa, Thuwayba Kisasi,wakati akipokea mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za jumuiya hiyo katika mkoa wa Kaskazini Unguja wenye thamani ya sh.milioni tatu ambao imetolewa na Mbunge wa viti maalum wa mkoa huo Angelina Malembeka.
Makamu huyo wa UWT alisema hazuiliwi mwanachama yeyote wa jumuiya hiyo katika kuchangia maendeleo ya UWT kwa dhamira ya kuijenga jumuiya ili mladi kamati za utekelezaji za jumiya na Chama kifahamu suala hilo.
“Chama si wanachama tu bali pia majengo ya kisasa kutokana na kuwa chama hichi kinahadhi yake hivyo lazima jumuiya hii iwe na majengo ya hadhi yake hivyo ninampongeza Mbunge kutoa mchango huu kwa ajili ya kukijenga chama hivyo ametoa fursa kwa wengine kutoa mchango wao,”alisema Makamu Mwenyekiti huyo
Aliongeza kuwa kinachotakiwa kwa kipindi hichi ni kuongeza kasi ya kuzitatua changamoto za wananchi kama CCM ilivyoelekeza ili kukipatia ushindi chama katika uchaguzi mkuu na kwamba si muda wa kurumbana.
Alisema kinachotakiwa wanajumuiya wa UWT kutambua ni muda wa kukijenga chama na jumuiya kwa pamoja na kuachana na tofauti zilizopo kati yao na kwamba hali hiyo ya mivutano haipendezi.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Kaskazini Unguja,Angelina Malembeka alisema mchango huo ameutoa kutokana na kuunga mkono chama katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa vitendo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya UWT ya kisasa.
Alisema UWT mkoa wa Kaskazini imejenga jengo la ofisi yake lakini imeishia hatua ya mwanzo na kwamba mchango wake huo utasaidia kuendeleza ujenzi huo ambao umesimama kwa muda.
“Nimefanya haya kwa ajili ya kukijenga chama pamoja na UWT na mchango huu wa mifuko ya saruji ina thamani ya sh.milioni tatu na kwamba ninatekeleza ilani kwa vitendo kwa kuhakikisha UWT mkoa ina kuwa na jengo lake la kisasa,”alisema

Wachimbaji wa Madini watakiwa kuhakikisha wana leseni za madini

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amewataka wachimbaji wa madini ya ujenzi nchini kuhakikisha wanapata leseni za madini kama Sheria ya Madini na Kanuni zake inavyofafanua.

Profesa Kikula aliyasema hayo leo tarehe 02 Novemba, 2019 katika machimbo ya mchanga katika maeneo ya Mgongo na Igingilanyi yaliyopo Wilayani Iringa Mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini hayo.

Ninawasilisha kwenu story, picha pamoja na captions ambazo zimeambatishwa pamoja na email hii. Captions zinapatikana mwishoni mwa story iliyoambatishwa.

WANANCHI WA MAGUNGUMKA WALA KIAPO KUWACHAGUA WAGOMBEA WA CCM SINGIDA

$
0
0
Wananchi wa Kitongoji cha Magungumka Kata ya Mgungila wilayani Ikungi Mkoani Singida wakila kiapo jana katika mkutano wa hadhara mbele ya Mbunge wao Elibariki Kingu cha kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 24 mwezi huu.
Mbunge Kingu akihutubia kwenye mkutano huo. 

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Wilaya ya Ikungi, Sanka Pius akizungumza.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo.
DC wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza.
Watoto wakiwa kwenye mkutano huo.
DC Mpogolo akifurahi na Diwani wa eneo hilo, Hussein Ng'enyi.
Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano.
Mkutano ukiendelea.




Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kitongoji cha Magungumka Kata ya Mgungila Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamekula kiapo mbele ya mbunge wao Elibariki Kingu na kusema watahakikisha kura zote za wagombea nafasi ya uenyekiti wa vijiji, vitongoji na mitaa katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 24 mwezi huu kuwa zitakwenda kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge wa jimbo hilo, Elibariki Kingu wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo wananchi hao walisema hawaoni sababu itakayowafanya wasiwachague viongozi hao kutoka CCM.

" Hiki kitongoji chetu cha Magungumka hakikuwa na maendeleo kabisa hatukuwa na huduma muhimu kama zahanati, barabara, shule na maji lakini serikali yetu kupitia huyu mbunge wetu Kingu tumepata vitu hivyo sasa kwanini tusiwachague viongozi kutoka CCM" alisema mkazi wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Shija.

Shija alisema walikuwa na changamoto kubwa ya barabara kwani wakati wa mvua za masika walikuwa wakitembea kwenye maji kutafuta usafiri wa kwenda Singida mjini lakini hivi sasa kero hiyo haipo tena baada ya Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli kupitia Mbunge Kingu kuwajengea barabara.

Kingu akizungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM wa wilaya hiyo, Sanka Pius alisema Serikali imetenga sh.300 milioni kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji hicho pia imetoa sh.47 milioni kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya kitongoji hicho.

Alisema tangu Rais Dkt. John Magufuli aingie madarakani katika kipindi cha miaka minne tu amefanya mambo makubwa ameweza kusambaza miradi ya maji 24 katika jimbo hilo, kujenga barabara, zahanati, vituo vya afya na shule na maeneo mengine yamekwisha pata umeme.

" Ndugu wananchi heshima pekee ya kumpa Rais wetu kwa kutuletea miradi hii ni kuhakikisha tunakipa ushindi mkubwa chama chetu naombeni twendeni tukajiandikishe kwa wingi na siku ikifika ya kupiga kura basi tuwachague viongozi watakaounda serikali kupitia CCM" alisema Kingu.

Kingu katika mkutano huo alitoa mabati 117 na saruji mifuko 110 kwa ajili ya ujenzi wa nadarasa ya shule ya kitongoji hicho chenye wananchi wengi pamoja na choo.

DC Mpogolo akizungumza katika mkutano huo alisema amesikia ombi la kuongeza mda wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura kutokana na watu wengi kushindwa kujiandikisha kwa sababu ya wingi wao na mashine kukorofisha na kueleza suala hilo atalipeleka kwa wahusika ili lifanyiwe kazi.

Katika hatua nyingine Mpogolo amewahakikishia usalama wananchi hao wakati wa upigaji wa kura katika uchaguzi wa viongozi wa vijiji na vitongoji utakaofanyika tarehe 24 mwezi huu na kuwa serikali imejipanga na mtu yeyote atakayejaribu kuleta vurugu atakiona cha moto.

RC MAKONDA APIGA MARUFUKU KAMPUNI YA UJENZI YA NYANZA KUPEWA MRADI DAR ES SALAAM, NI BAADA YA KAMPUNI HIYO KUZIDISHA "UBABAISHAJI".

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Novemba 02 amewataka TANROAD kuhakikisha Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza haipatiwi mradi wowote wa ujenzi ndani ya mkoa huo baada ya kampuni hiyo kuendelea kusuasua kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Kivule licha ya Kupewa fedha za ujenzi.

RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo akiwa kwenye barabara ya Kivule ameshuhudia Mkandarasi huyo akiwa na uhaba wa Vifaa licha ya kudanganya kwenye mikataba kuwa anavyo vifaa vya kutosha ili apatiwe tenda.

Aidha RC Makonda amezionya bodi za manunuzi zinazotoa tenda Kwa kuendekeza Rushwa na kujuana jambo linalowafanya kushindwa kumuonya mkandarasi kwakuwa tayari wamefungwa midomo Kwa rushwa.

Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao kwa sasa upo kwenye hatua ya kufunika gorofa ya kwanza huku akieleza kuwa anaamini ujenzi utakabidhiwa Mwezi Disemba.

Katika hatua nyingine RC Makonda ametembelea ujenzi wa Mto Sinza na Mto Ng'ombe wenye urefu wa Km 7.5 ambao baada ya kuwakamata wakandarasi hatimae ujenzi sasa umeanza huku akimtaka mkandarasi wa kampuni hiyo kumaliza mradi kwa wakati.

Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya NAMIS Corporate LTD inayojenga Soko la Tandale kukamilisha ujenzi huo haraka ili wafanyabiashara wauze bidhaa katika sehemu nzuri.


Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) waangamiza bidhaa mbali mbali zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu

$
0
0
Wafanyakazi kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) wakiangamiza bidhaa mbali mbali za Chakula na Vipodozi katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Maryam Kidiko – Habari Maelezo Zanzibar.
Mfanya Biashara wa Bidhaa ya Mchele ulioangamizwa tani 105 kutoka Kampuni ya Ahmed Khelef, Ibrahim Omar Awesu akitoa maelezo kuhusu kuharibika kwa bidhaa hiyo huko Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa athari zitokanazo na Chakula kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) Aisha Suleiman akitoa maelezo kuhusu bidhaa mbali mbali za Chakula tani 133.5 zilizoharibika na kuangamizwa huko Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
******************************

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 02/11/2019

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imeteketeza zaidi ya tani 130 za bidhaa za chakula na tani tano za vipodozi zilizoharibika katika jaa la Kibele wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha uchambuzi wa Athari zitokanazo na Chakula wa ZFDA Aisha Suleiman amesema bidhaa hizo zilikaguliwa na kuonekana hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Alisema kuwa bidhaa hizo ambazo baadhi yake zikiwa zimeharibika na nyengine zikiwa zimeingia nchini bila kufuata utaratibu wa uingizaji bidhaa zilikamatwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Alizitaja bidhaa zilizoangamizwa kuwa ni mchele tani 105 ulioingizwa na kampuni ya Ahmed Khelef, majani ya chai tani 24 kutoka kampuni ZATEPA, bidhaa mchanganyiko tani moja, pipi tani moja na nusu kutoka kampuni Basil Cook pamoja na soda za kopo tani mbili kutoka kampuni ya Ahmed Salim.

Amefahamisha bidhaa zinazoingia nchini zinatakiwa kufuata taratibu zote za uingizaji ikiwa pamoja na kufanyiwa ukaguzi na maafisa wa Wakala wa Chakula na Dawa ili kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zipo salama na hazina madhara kwa mtumiaji.

Aidha Mkuu huyo amewataka wafanya biashara na wananchi kuwa waangalifu wakati wanapnunua na kusafirisha bidhaa ili kuhakikisha zinaingia nchini zikiwa bado hazijaharibika.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Dawa na Vipodozi wa ZFDA Nassir Buheti amesema vipodozi vilivyotekezwa baadhi yake vina sumu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu.

Amefahamisha kuwa vipodozi hivyo vimeingia nchini kinyume na utaratibu havijaisha muda wake wa matumizi bali vimeonekana kuwa vinaviambato vyenye sumu havipo salama kwa mtumiaji.

Kwa upande wake Mfanyabiashara Ibrahim Omar Awesu kutoka Kampuni ya Ahmed Khelef alisema walinunua mchele huo ukiwa katika hali nzuri kwa matumizi lakini uliharibika kutokana na kampuni ya usafirishaji kuchelewa kuusafirisha na kusababisha na hatimae kuharibika ukiwa njiani kuja Zanzibar.

Aidha ameomba wakala wa Chakula wa Dawa kufanya mapema ukaguzi wa bidhaa zinazoingia nchini pamoja na makampuni ya usafirishaji kuingiza bidhaa hizo kwa wakati ili kuepuka hasara. 

LIPULI YAIKUNG'UTA MWADUI BAO 2-0 UWANJA WA SAMORA, IRINGA

$
0
0
 Hekahela langoni mwa timu ya Timu la Lipuli ya Mjini Iringa katika mchezo wa Ligi kuu uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Samora dhidi ya Timu ya Mwadui ya Shinyanga. Mchezo huo umemalizika kwa Timu ya Lipuli kuibugiza mabao mawili kwa nunge (2-0) yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Daruesh Saliboko.
 Beki wa Timu ya Lipuli, Novart Lufunga akiwania mpira wa juu ya Mshambuliaji wa Timu ya Mwadui, Raphael Aloba, katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Samora, Mkoani Iringa. Lipuli imeshinda 2-0.
 "...ukitua tu, naondoka nao..."






WAZIRI MAMBO YA NDANI ATUMA SALAMU KWA KIGOGO2014 WA MTANDAONI,AMWAMBIA SIKU ZAKE ZINAHESABIKA KAMA KALENDA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema siku za mtu anayejiita Kigogo anayetumia mtandao wa kijamii na hasa Twitter kutukana,kukejeli na kuikashfu Serikali ya Awamu ya Tano anatakiwa kufahamu siku zake zinahesabika.

Kwa muda sasa mtu anayejiita Kigogo2014 amekuwa akitumia mtandao wa kijamii kutoa taarifa mbalimbali ambazo nyingi zimekuwa zikilalamikiwa na nyingine zimekuwa  zikisababisha mjadala mtaani na mitandaoni kiasi cha baadhi ya Watanzania kuhoji huyo Kigogo ndio nani,maana haijafahamika kwa jina zaidi ya kutumia sura kama  ya mwanamuziki maarufu wa Marekani Jay Z ingawa alichokifanya ni kuuurefusha mdomo.

Waziri Lugola ameyasema hayo leo Novemba 2,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam  wakati anazungumzia utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini ambapo ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa jeshi hilo chini ya uongozi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi ,IGP Simon Sirro.

Hata hivyo waandishi walitaka kufahamu hatua ambazo zinachukuliwa kukabiliana na baadhi ya watu wenye kutumia mitandao ya kijamii kutoa lugha za kukejeli,kashfa,kuzusha na dhihaka dhidi ya wengine na hasa Kigogo2014, ambapo Waziri Ligola amesema kila mtu anafahamu kalenda inavyohesabiwa ,hivyo Kigogo atambue siku zake zinahesabika na siku si nyingi atpatikana.

" Huyo anayejiita Kigogo afahamu kwamba siku zake zinahesabika , ni kama vile kuhesabu kalenda unaanza moja hadi 31 ,hivyo tutampata tu, "amesema Waziri wakati akijibu swali kuhusu mtu huyo na kuongeza Watanzania wanatakiwa kutumia mitandao vizuri na sio kuitumia kwa ajili ya kupotosha, kuchonganisha au kutukana wengine kwani sheria itachukua mkondo wake.

Mbali ya kuzumzungumzia Kigogo, Waziri Lugola ameeleza kutokana na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi chini ya Serikali  ya Awamu ya Tano ya Rais Dk.John Magufuli, usalama wa raia na mali zao umeimarika na hata matukio ya ujambazi yamepungua kwa asilimia kubwa .

Amesema kuwa Jeshi la Polisi liko imara wakati wote,hivyo amesema wenye tabia ya kujihusisha na uhalifu watambue kuwa hawako salama na wasithubutu kutenda uhalifu kwani watakamatwa na watakaokuwa wabishi kwa Kupambana na Polisi watashughulikiwa.

Pia amesema kuna majambazi ambao wamekuwa wakifanya ujambazi na kisha kukimbilia Mkoa wa Kigoma na Kagera, hata hivyo ameeleza Polisi wameizingira Mikoa hiyo na hivyo majambazi walioko huko muda wowote watakuwa mikononi mwa jeshi hilo.

Kuhusu vitendo vya rushwa, Waziri huyo amesema kwa sehemu kubwa rushwa imepungua lakini ametoa rai kwa kila Mtanzania kuchukia rushwa kwani hakuna rushwa kama hakuna anaetoa,hivyo mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wakosefu mbele ya sheria.

Pia amezungumzia wa watu kutoa malalamika iwapo watakuwa nayo dhidi ya Jeshi la Polisi lakini ni vema wakafuata utaratibu kwa kuonana na wakuu wa vituo vya Polisi na wakaona hawajaridhika wanakwenda kwa wakubwa zaidi na hata kwa IGP au Wizara ya Mambo ya Ndani.

Amesema kwa kufanya hivyo anaamini malalamiko dhidi ya Polisi kama yapo badi yatapata ufumbuzi kwani kuendelea kulalamika bila kufuata utaratibu huo inaweza kuonekana kama majungu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Kangi Lugola akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Novemba 2,2019 jijini Dar  es Salaam,kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Uhalifu na matumizi mabaya ya silaha na  mitandao ya kijamii.
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Kangi Lugola akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Uhalifu na matumizi mabaya ya silaha na mitandao ya kijamii.Pichani kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Jacob Kingu na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi ,IGP Simon Sirro.Picha na Michuzi JR.(MMG).

Glitters Car wash washerehekea mwaka moja wa kazi

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kuosha Magari ya Glitters Car Grooming Bays ya jijini Dar es Salaam wakishangilia wakati wa kutoa huduma ya uoshaji magari bure leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo. 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Glitters Abdallah Motto amesema changamoto kubwa wanazozipitia ni kukimbiwa na wafanya kazi ambao kabla huwapa elimu ya namna ya uoshaji magari lakini baadaye hukimbia.

Aidha katika sherehe hiyo kulikua na utoaji wa elimu kwa namna ya uendeshaji magari kwa kuzingatia usalama wa muendeshaji na abiria wawapo barabarani.
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images