Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 319 | 320 | (Page 321) | 322 | 323 | .... | 3284 | newer

  0 0  0 0

  NA ABDULAZIZ VIDEO,Kilwa 
  Halmashauri ya wilaya ya Kilwa imeomba kuidhinishiwa jumla ya Tshs 28,729,895,535 kwa ajili ya Uendeshaji wa shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo Mishahara Tshs 14,016,723,484 huku mapato ya ndani ni Tshs 268,112,400 na matumizi mengineyo (OC)ni 1,567,578,000 toka serikali kuu na mapato ya ndani 2,054,184,359 
  Aidha Miradi ya maendeleo tshs 2,994,804,988 toka serikali kuu na wahisani 409,817.075 na mapato ya ndani Tshs 10,823,297,292 Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha Baraza maalum la bajeti kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo,Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Daniel Lusingu alibainisha kuwa Bajeti hiyo ina ongezeko la jumla ya Tshs 8.866,528,435 sawa na asilimia 44.63 ya bajeti ya mwaka 2013/2014 
  Pamoja na maombi hayo ya kuidhinishiwa mapato na matumizi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kuhakikisha inaongeza mapato kutoka katika vyanzo vya ndani imejipanga kuongeza wigo baada ya kubuni vyanzo vipya ikiwemo kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi mbalimbali, Kuimarisha Uagizaji na utunzaji wa nyaraka za kukusanyia mapato na kuimarisha rejesta ya vyanzo vya mapato Sambamba na kuongeza wigo wa ubinafsishaji wa vyanzo na kufanya uhakiki kila mara pamoja na kutoa elimu kwa walipa kodi na kuongeza nguvu kwenye kudhibiti mazao yatokanayo na bahari,kilimo na misitu kwa kusimamia kwa karibu vizuizi katika maeneo ya Singino,Migeregere,Mbwemkuru,mihangalaya na Nanjirinji 
  Akichangia bajeti hiyo,Diwani wa kata ya Songosongo,Mhe Hassan Swaleh pamoja na kuunga mkono Bajeti hiyo aliiomba Halmashauri hiyo kuona umuhimu wa kuthamini wavuvi kwa kupatiwa zana bora za uvuvi Ili kuongeza wigo katika makusanyo ya baharini
  Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani Kilwa
  Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani Kilwa
  Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa ,Daniel Lusingu akiwasilisha makisio ya bajeti ya Halmashauri hiyo
  Wakuu wa Idara wa Halmashauri wakihudhuria kikao hicho

  Meza Kuu. Picha zote na Abdulaziz Video

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitambulishwa  kwa mshauri wa Ujenzi wa kampuni ya Hab Consult Bw.Habib Nuru,Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dkt.Khalid Salum,alipofika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja, kuweka Jiwe la Msingi  Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar leo asubuhi
   
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameongozana na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi   Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuweka jiwe la msingi Ujenzi   wa Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, katika viwanja vya Kisonge,Michenzani  Mjini Unguja leo asubuhi
   Baadhi ya wananchi na Viongozi wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika viwanja vya Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi,(kulia) Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Bw. Habib Nuru mshauri wa Ujenzi wa kampuni ya Hab Consult ya Dar es Salaam,baada ya kuweka jiwe la msingi Mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi. 
  Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


   
   
  KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwa nini limeamua kuuchagua mji wa Morogoro 
  kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia nyimbo zao mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo.
  Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwa ajili ya kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
  Kiongozi wa Jahazi Modern Taraab, Mohamed Mauji, jana alifanya mahojiano na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na mtangazaji Hawa Hassan (kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo alitoa sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho kitaruka hewani tena Jumamosi hii saa 11 jioni.
  Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo, alisema  miongoni mwa sababu nyingi  ni pamoja na kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa (ukiondoa Dar es Salaam)  hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee.
  Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya jijini Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndipo wanazipeleka nyimbo mpya mikoani.
  Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya kukakabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.

  0 0

  Wafanyabiashara  jijini Dar es salaam  leo wamefunga maduka yao kwa kile kinachodaiwa kugomea  mashine za risit za EFD toka TRA. Taswira hizi ni sehemu ya maduka hayo maeneo ya Kariakoo  0 0

  MASHAHIDI wa Jamhuri katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege (pichani) ya matumizi mabaya ya madaraka  kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani, wamedai kwa nyakati tofauti kwamba mshtakiwa alitoa msamaha huo bila kibali cha Baraza la Utendaji (kwa sasa Bodi ya Wakurugenzi). 
   Mashahidi hao wa kwanza Mwansheria Batista Bitao na wa pili ni Mhandisi Joshua Katabwa walitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. 
   Akiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machulya shahidi huyo alidai kuwa katika kipindi cha mwaka 2007 na 2009, kwa mujibu wa mikataba ya TBS na Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage ya nchini Dubai na Quality Motors ya Hongkong walipaswa kulilipa shirika hilo asilimia 25 baada ya kufanya ukaguzi. 
   Alidai kuwa kati ya mwaka 2007 na 2009, Baraza la Utendaji (kwa sasa Bodi ya Wakurugenzi) ni chombo pekee chenye dhamana ya kusimamia shirika hilo. 
   “Mwaka 2007 na 2009 nilikuwa naalikwa katika baraza la utendaji (Bodi ya Wakirugenzi) lakini hatukuwahi kujadili suala la kusitisha tozo ya ada ya utawala… suala hilo liliibuka mwaka 2011 baada ya menejimenti kuwasilisha taarifa ya kutolewa msamaha kwa kampuni hizo mbili na iliambatanisha na maelezo ya kuomba radhi kuhusu kosa la kutoa msamaha huo bila kibali cha baraza hilo na kwamba halitajirudia,” alidai Bitao. 
  Akifafanua zaidi alidai kuwa baraza hilo lilitoa maelezo yake kwamba kosa hilo sijirudie tena na kwamba menejimenti baada ya kupitia maombi hayo ilipaswa kuyawasilisha katika baraza hilo ili liweze kutoa uamuzi wa kukubali au la. 
  Naye shahidi wa pili, Katabwa alidai kuwa kampuni hizo ziliingia mkataba na shirika lake kwa mkataba wa kulilipa asilimia 25 na kampuni hizo kubaki na asilimia 75 kama wakala wao. Alidai kuwa Machi 28, mwaka 2008 aliagizwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS (wakati huo, Ekerege) kuandaa barua ya kutoa msamaha wa asilimia 50 kwa kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage. 
   “Ekerege aliniagiza niandae barua ya kuwakubalia msamaha huo na aliisaini tarehe hiyo waliyowasilisha maombi yao… utaratibu huo ulitumika kwa kampuni ya Quality Motors kupokea majibu ya msamaha huo” alidai Katabwa. 
   Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Machi 28 mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009, katika ofisi za TBS iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake vibaya. 
   Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la asilimia 50 ya ada ya utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la utendaji la TBS kinyume cha sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS ya mwaka 2005. 
   Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za Kimarekani sawa na (kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800. 
   Upande huo wa Jamhuri ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alilisababishia shirika kupata hasara ya fedha hizo. 
   Mshtakiwa alikana mashitaka yote mawili na yuko nje kwa dhamana na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mfululizo Februari 5,6 na 7, mwaka huu.

  0 0

  Ratiba ya mazishi ya aliyekua Mkurugenzi mstaafu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Fredrick S. H. Mmbaga (pichani). Marehemu Mmbaga alifariki nchini India mwishoni mwa wiki alikokua akipata matibabu.
  Mwenyezi Mungu aiweke roho 
  yake mahali pema peponi. 
  AMIN.

  0 0

  Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubili hatima yao huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.(Picha na John Banda)


   Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na Mzaganza.
   Abiria waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuliko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.
   Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada train hiyo kukwama kuondoka Dodoma.

   Abiria hao wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.


  0 0

  The Institute of Accountancy Arusha (IAA) and the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) have today signed an  Memorandum of Understanding  to equip military personnel with necessary skills and knowledge in Strategic Studies. 

  The IAA Rector Prof. Johannes Monyo said in his speech that the move was beneficial for his institution and  TPDF's Command and Staff College (CSC ) which he added deserved a special mention for initiating it.
  “It is our understanding that many institutions in Tanzania are not used to working closely with Military personnel. TPDF and Command and Staff College realized that members of military forces are good partners in development. It is true that once good partnership is established the country tends to prosper faster”, Prof Monyo Said. 
   He also noted that the  CSC had enjoyed good working relationship with the IAA that has lasted for eight years and that in 2006 a special CSC tailored programme was developed and this was the beginning of a close working relationship between the two institutions. 
  The Rector said in this relationship the academic staff from IAA were invited to facilitate in a number of other related programmes conducted by CSC. But the target of CSC was to have long term programmes and academic partner with a capacity to run the new targeted programmes. CSC initially, consulted several institutions and universities in the country to establish long term courses in strategic studies but this effort was unsuccessful. 
  It is the flexibility of IAA management and the IAA Governing Council that authorized the commitment of resources in the year 2011 and allowed the development of Strategic Studies programmes at CSC- Monduli. 
   “Two curricula were developed in the area of Strategic Studies and these included the Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma in Strategic Studies. These curricula were developed following NACTE standards. The Ordinary Diploma curricula comprising of NTA levels 5 and 6 were submitted to NACTE for validation and were approved. Furthermore, IAA developed Postgraduate Diploma in Strategic Studies Programme. 
  These programmes are currently in progress and have a total of 52 participants from EAC and SADC countries” he said He revealed that both programmes are aimed at equipping Military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies that are needed at their workplace and elsewhere in the world. 
  The programmes, which commenced in May 2013, are expected to produce the first graduands by March this year (2014). Although this is the first collaborative arrangement with a partner from within the country IAA has two other collaborations with partners from foreign countries. IAA signed a MoU with Coventry University of UK way back in 2009 to run four masters degree programmes (MBA – ITM, MBA – LM, MBA – PSM and MSc. FI). 
  These programmes have been running for last four years. In 2013 IAA signed another MoU with Galgotias University of India to run three masters degree programmes namely; Master in Information Security, Master in Software Engineering and Master in Computer Application. These programmes started in November 2013. 
   In the same vein we are working with TMA to establish a Bachelor Degree in Military Science. This degree is expected to be run effective 2015 if the accreditation processes will be completed in time. Today we are here to officially sign the MoU between IAA and TPDF and inform Tanzanians in particular and the world at large that Military staff are good partners in development. 
   I would also like to take a moment of personal privilege to acknowledge some of those who helped to make this day and the event surrounding possible. 
  I wish to thank members of IAA Academic staff, members of CSC staff, TPDF headquarters, members of the Governing Council, NACTE, TMA and all others not mentioned above but helped in one way or the other to make this day possible.
   IAA Rector Prof. Johannes Monyo signs the Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.

   The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Kyunga signs the Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA

   The Institute of Accountancy Arusha (IAA) Rector Prof. Prof. Johannes Monyo (2nd from R) exchange the MoU documents  with The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Ezekiel-Elias Kyunga (1st from L). The MoU signed today in Arusha will equip military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.

  A group photo of members of military and IAA staff members after the signing ceremony early today.


  0 0
 • 01/09/14--05:38: Article 7


 • 0 0

  JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA MAREHEMU MAULIDI HAMID ABDALLA MAARUFU KWA JINA LA KIDISHI.

  Kidishi amefariki siku ya jumanne ya tarehe 7/01/2014 usiku . Marehemu amefariki katika hospitali ya COTUGNO mjini Napoli, baada ya kulazwa kwa muda wa wiki tatu.

  Marehemu katika uhai wake amewahi kucheza mpitra timu ya Black Fighters na hata Timu ya taifa zote za Zanzibar katika miaka ya themanini.

  Mipango ya mazishi inafanywa na tayari yameshafanyika mawasiliano na familia ya marehemu.

  TUNAPENDA KUWATANGAZI WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWA MAZISHI , MKUTANO UTAFANYIKA PALEPALE ULIPOFANYIKA MKUTANO WA KWANZA WA MAREHEMU JUMA KIJUU.

  MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA.. AMIN!

  0 0
 • 01/09/14--06:20: NYUMBA INAUZWA
 •  Nyumba hii ipo Mbezi juu njia ya kuelekea Goba,Kilometa 4 kutoka Masana Hospital eneo la Mbezi Samaki,jijini Dar es Salaam.

  Eneo lina SQM 1000 na Nyuma ina Vyumba vitatu vya kulala vyote ni self,Chumba cha kujisomea,Jiko,Stoo,Dinning pamoja na Sebule.

  Bei ni sh. Milion 200 na hati ipo kwenye taratibu ya kupatikana.

  KWA MAWASILIANO
  0718 687 575
  0786 444 000

   Sehemu ya nje ya nyumba hiyo
   geti na fensi ya kisasa
   sehemu ya ndani ya nyumba hiyo
  Sehemu ya maegezo ya magari.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akikabidhi moja ya vifaa tiba kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.Noman Sigalla.
  Naibu waziri wa Afya Dk Seif Rashid akimkabidhi moja ya mashine ya kusaidia watoto wachanga matroni Mary Mlay aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga katika hafla hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyotumika katika vituo vya kutolea huduma vinavyohudumia wanufaika wa mradi wa akina mama wajawazito unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Watu wa Ujerumani (KfW) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akitoa maelezo ya Mradi wa KfW unaoendeshwa kwa ushirikiano wa Benki wa Watu wa Ujerumani na NHIF.


  0 0

  Katika kuhakikisha inaendelea kupanua wigo na kusogeza huduma zake za kibenki karibu na wateja wake benki ya Covernant imezindua huduma za kibenki kwa njia ya simu inayojulikana kama”Benki Mtaani kwako” 
  Huduma hii ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kupitia simu za Mkononi. 
  Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi Salome Sijaona,amesema kuwa benki yake inawalenga watu wa kawaida kabisa ambao wengi wao wanaishi maeneo ya nje ya mji wengi wao wakiwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo hivyo kuanzisha huduma hii ni faraja kubwa kwa wateja wetu ambao hawatapata tabu tena ya kutoka sehemu waliko kuja katika tawi la benki hiyo kupata huduma.
   “Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka ikiwa ni sehemu muhimu ya kuendelea kuboresha na kusogeza huduma zetu kwa wateja wetu, tuna wateja maeneo mengi ya mjini na vijijini, tumeona ni jambo jema kuwaanzishia huduma hii ambayo haita walazimu wao kuja katika tawi letu kupata huduma, aliongeza Balozi Sijaona. 
  “Tunawajali na kuwathamini wateja wetu na sasa tumewaletea huduma hii ya kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia simu za kiganjani wakiwa mahala popote pale, wote tunatambua kuwa dunia ya sasa teknolojia ndio kila kitu, mtu anapoweza kupata kila kitu kupitia simu yake ya mkononi ni jambo jema kwetu, natoa wito kwa wateja wetu kutumia huduma hii ambayo naamini ni suluhisho kwao watakapo kuwa na uhitaji wa kuweka au kutoa fedha katika benki yetu.” 
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Sabetha Mwambenja amesema amefurahi kwa benki yake kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake na kuhakikisha wanafikia malengo ya huduma bora kwa wateja wake.
  Pia alizitaja sifa muhimu za huduma hiyo kuwa ni kulipia Ankara mbalimbali,kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote uliyokuwa nayo na covenant benki, kuhamisha fedha kupitia mtandao wowote wa simu za viganjani nchini,kutuma na kuchukua fedha ATM bila kadi ya benki hata kama aliyekutumia hana akaunti na Covenant benki,kupata miamala uliyofanyika kwenye akaunti yako na kusajili huduma hii mwenyewe kupitia simu yako na usajili unakamilika papo hapo. 
  “Tunamipango mingi ya kuendelea kupanua na kuboresha huduma zetu, hadi kufikia sasa tunashukuru namna ambavyo wateja wetu wameendelea kutuunga mkono siku hadi siku, tunawaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kuhakikisha tunatimiza ndoto zao za kuwa na maisha bora.
  ” Tunaendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujiunga na huduma zetu ambazo zinafaida nyingi kwani wateja wanaweza kutumia akaunti zao wakati wowote,kuondoa adha ya kusafiri/kutembealea tawi la benki,kuhamisha fedha kwa uwapendao kwa urahisi zaidi,wanaweza kuwalipa washiriki wa biashara na wagavi bila wasiwasi.
  Pia hadi sasa tunazo akaunti za aina mbalimbali ambazo ni akaunti za akiba inayojumuisha akaunti ya Ahadi, Jerusalem, Tausi Women Entrepreneurs Account, Winner Junior account, Vikundi, Akaunti ya Akiba ya Bajaj, Akaunti ya Muda Maalum na nyinginezo na akaunti za biashara ni pamoja na akaunti binafsi na nyinginezo. Ili kujiunga na huduma hiyo Mteja wa benki hiyo atatakiwa kupiga namba *150*27#
   Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(katikati)akibonyeza kitufe cha kopyuta kuashiaria uzinduzi rasmi wa huduma ya” benki mtaani kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao.Anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.

    
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant Bi.Sabetha Mwambenja(katikati)akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao,pamoja nae katika picha ni  Mwenyekiti wa Bodi wa benki  hiyo Balozi.Salome Sijaona(watatu kutoka kushoto) pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.

   Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(kulia)akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako” ambayo inawawezesha wananchi na wateja wa benki hiyo kutumia simu zao za kiganjani kupata huduma za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao.kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja.

  0 0

                              
                     SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,250 
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,750 
  SALOON CARS TO DAR/MOMBASA NOW £700
  4 X 4 CARS TO DAR MOMBASA NOW £780
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  FREE COLLECTION FROM EASE LONDON 
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO+255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND DELIVERED TO PORT FOR YOU!

  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477


  0 0

  Leo asubuhi basi la abiria  la kampuni ya Mtei Express likitoka Sindida kwenda Arusha limechomwa moto na wananchi wenye hasira maeneo ya Njia panda Mnadani, mkoani Singida baada ya bus hilo kugonga pikipiki yaani bodaboda na kuua watu watatu hapo hapo. Zifuatazo ni taswira za basi hilo lililokuwa wakati na baada ya kuchomwa moto. 
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
 • 01/09/14--19:37: Article 24

 • For more information please follow us on here.

  0 0

  VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 051Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Mwamoyo Hamza akijichukulia maakuli wakati wa sherehe za mwaka mpya siku ya Jumatano huko VOA Washington Dc.VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 005Heather akifurahi mbele ya kamera ya Mdau Sunday Shomari mara baada ya kujipakulia msosi. VOA HOLIDAY PARTY A.DIV. 024Intern wa VOA na mmiliki wa Bongovibez Bi.Mariam akiwa kwenye mkao wa kung'aa. 
  Fatou Kalala prodyuza akifurahia kilaji chake.
  Mdau Sunday Shomari akiwa na dada Ndimyake wa VOA -TV 
  Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com

  0 0


older | 1 | .... | 319 | 320 | (Page 321) | 322 | 323 | .... | 3284 | newer