Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA MADAKTARI WA CHAMA CHA WAPATHOLIJIA TANZANIA IKULU ZANZIBAR LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na wageni wake Ujumbe wa Madaktari wa Chama Cha Wapatholojia Tanzania (APT) walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 1/11/2019 wakiwa Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Chama Cha Wapatholojia Tanzania (APT) walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo,( kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Chama Cha Wapatholijia Tanzania Dkt. Charles Massambura akiwa na ujumbe wake. wakiwa Zanzibar kwa ziara ya siku mbili hafla imefanyika leo 1/11/2019 Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA MAWAZIRI, WAKUU WA MIKOA NA WILAYA PAMOJA NA KAIMU MKURUGENZI WA TAKUKURU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kikao cha viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi
za Serikali zinazohusika na mazao ya Korosho na Ufuta alipokutana nao
Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 1, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiagana na viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi za Serikali
zinazohusika na mazao ya Korosho na Ufuta baada ya kukutana nao
Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi za Serikali zinazohusika
na mazao ya Korosho na Ufuta baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar
es salaam leo Novemba 1, 2019.PICHA NA IKULU

DKT.BASHIRU AMETEMBELEWA NA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

$
0
0
Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

“Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika.” Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

BENKI YA AFDB YAONGEZA MTAJI, YAJADILI ONGEZEKO HILO

$
0
0
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza mara baada ya kumaliza mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika nchini Ivory Cost.
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeongeza mtaji wa Benki hiyo kutoka dola za kimarekani bilioni 90 hadi dola za kimarekani 283 kutokana na uwepo wa majadiliano juu ya kiwango cha ongezeko la mtaji wa Benki.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mkutano maalum wa tano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, uliofanyika Abidjan Nchini Ivory Coast na kuhudhuriwa na Rais wa nchi ya Ivory Coast, Alassane Ouattara, amesema kuwa enki ya maendeleo ya Kilimo imeongeza mtaji wake kwa lengo la kukuza kilimo.

Prof. Kabudi amesema kuwa maamuzi yaliyopitishwa na magavana wa benki hiyo waliohudhuria mkutano huo ni ya kihistoria ambapo sasa inaifanya Benki ya Maendeleo ya Afrika kushika nafasi ya pili duniani baada ya Benki ya Dunia.

Amesema kuwa uamuzi huo unaifanya Benki ya Maendeleo Afrika kuwa na uwezo mkubwa wa kufadhili na kuhisani miradi mbalimbali na mikubwa ya kimkakati katika Bara la Afrika Tanzania ikiwemo na hivyo kuliwezesha bara hilo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Prof. Kabudi amezitaja faida ambazo nchi za Afrika itazipata kutokana na kuongezeka kwa mtaji wa Benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa mikopo mikubwa na ufadhili kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ajili ya kuliendeleza bara hilo husani katika miundo mbinu, nishati na hudumu muhimu za kijamii ambayo nchi nyingi za kiafrika ambazo ni wanachama wa benki hiyo walishindwa kuitekeleza kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila kwa upande wake amesema kutokana na Bara la Afrika kuwa na Nchi nyingi masikini uwepo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika inatoa ahueni kwa Nchi hizo na kutoa wito pia kwa taasisi binafsi kutoka nchi za Kiafrika kuchangamkia fursa ya ongezeko la mtaji wa Benki hiyo kutokana na ukweli kuwa AfDB inakopesha pia taasisi binafsi.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo ilianzishwa kwa lengo la kuchochea maendeleo ya Bara hilo ikiwa na jukumu la kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya kiuchumi ya Afrika inamilikiwa kwa asilimia 60 na nchi za kiafrika na asilimia nyingine 40 zilizosalia zinamilikiwa na nchi waalikwa kutoka katika mabara mengine duniani Marekani ikiwemo.

RAIS MAGUFULI KUUFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI MAMBO YA NJE WA NCHI 29 BARANI AFRIKA NOVEMBA 8,2019 JIJINI DAR

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza na Wanahabari  leo katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar,kuhusu kufunguliwa kwa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao unatarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. 
 Balozi wa Swedeni nchini Tanzania Bi.Elisabeth Jacobsen akifafanua jambo mbele ya Wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja K. Mnyepe.Picha na Michuzi JR (MMG).
  Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Anders Sjoberg akizungumza na Wanahabari katika mkutano uliofanyika leo kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki  wa Nchi tano za Nordic katika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 unaotarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. pichani kati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe na kushoto ni  Balozi wa Swedeni nchini Tanzania Bi.Elisabeth Jacobsen 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza na Wanahabari  leo katika mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar leo,kuhusu kufunguliwa kwa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao unatarajiwa kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. 
 Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Anders Sjoberg akifafanua jambo kwa Wanahabari katika mkutano uliofanyika leo kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki  wa Nchi tano za Nordic kushiriki katika mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 unaotarajiwa kuanza kuanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania,ambapo Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Picha na Michuzi JR (MMG).




Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kufungua mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje 34 wa nchi za Afrika 29 na nchi tano za Nordic ambao utaanza Novemba 8 mwaka huu nchini Tanzania.

Katika mkutano huo unatarajiwa kuwa na wageni zaidi ya 250 huku Watanzania wakishauriwa kuendeleza utamaduni wao kwa kuwakaribisha wageni wote watakaoshiriki na kwamba watumie fursa zitokanazo na uwepo wa mkutano huo kwa kufanya shughuli halali zitakazowanufaisha  kiuchumi.

Akizungumza kuhusu mkutano huo leo Novemba 1,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam Katibu Mjuu Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Faraja Mnyepe amesema kwa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na masuala ya amani na usalama.

Amefafanua mkutano huo utajadili fursa za Uwekezaji, biashara,amani na usalama na masuala mengine mtambuka kama vile athari za mabadiliko ya tabianchi .Pia mawaziri hao watazungumza kuhusu uhusiano baina ya nchi yetu na nchi moja moja na hasa ubia wa kimaendeleo.

"Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano ,wenzetu wa Afrika na Nordoc watapenda pia kusikia uzoefu wa mafanikio ya Tanzania kwenye sekta za afya, elimu, nishati, miundombinu, kilimo ,utalii ,ukusanyaji wa kodi , mafanikio ya vuta dhidi ya rushwa, ujangili ,dawa za kulevya na maeneo mengine,"amesema Dk.Mnyepe.

Akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo amesema utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNICC) jijini Dar es Salaam na utafunguliwa na Rais Magufuli.

Amesema mkutano huo utajumuisha jumla ya mawaziri 34 wa mambo ya nje wa nchi za Afrika na Nordic pamoja na washiriki wengine ambao idadi yao inatarajiwa kufika milioni 250.Mawaziri ambao watakuja kutoka nchi za Nordic ni wa nchi za Sweden, Norway, Denmark, Finland, na Iceland.

Wakati nchi za kutoka Afrika ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso Burundi, Comoros, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) Misri, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho ,Mali, Malawi, Morocco, Msumbiji , Namibia, Nigeria, Niger, Rwanda, Senegal, Somalia, Afrika Kusini, ,Tunisia, Uganda, Zambia, Zimbwabwe, na Tanzania ambayo ndio mwenyeji.


Dk.Mnyepe amesema mkutano huo utajumuisha mawaziri, mabalozi, wa nchi shiriki za Afrika katika nchi za Nordic ,mabalozi wa nchi za Nordic pamoja na watendaji wa Serikali .Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu inasema " Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu".

Ameeleza ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Nordic ni wa kihistoria na wa pekee na kwamba ushirikiano huo ulianza hata kabla ya Uhuru wa Tanganyika ambapo Wamisionari kutoka nchi hizo walikuja kufanya kazi hapa nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu.

Pia amesema ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa  vinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika,urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika.

Dk.Mnyepe amesema katika nchi za Afrika ,Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi za Nordic kuliko nchi nyingine yoyote.Kwa mfano kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2013 mpaka 2018 Tanzania imepokea takribani Sh.bilioni 900 kutoka nchi za Nordic na kwamba nchi hizo zimekuwa zikisaidia sekta mbalimbali.

Pia amesema wazo la kuanzishwa mkutano huo ulianza mwaka 2000 ambapo kwa mara ya kwanza uliofanyika nchini Sweden mwaka 2001.Baada ya hapo mikutano kama hiyo inafanyika kwa kupokezana kutoka Bara la Afrika na upande wa Nordic.

Dk.Mnyepe amesema kutokana na ushirikiano huo wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi hizo ,nchi hizo ziliiomba Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na uhusiano mzuri uliopo na kasi za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dk.Magufuli.

Hata hivyo alipoulizwa iwapo Tanzania itatumia nafasi hiyo kuomba  nchi ya Zimbabwe kuondolew vikwazo kama ambavyo wakuu wa nchi za SADC wamekubaliana ambapo Dk.Mnyepe amesema ajenda hiyo itakuwepo kwani dhamira ya dhati.iliyopo kwa Serikali ni kuona Zimbabwe inaondolew vikwazo ilivyowekewa.

" Moja ya ajenda yetu ni kuhakikisha kila tunapopata nafasi tunaomba Zimbabwe iondolewe vikwazo, ndio msimamo wetu na  ndio msimamo wa nchi za SADC.Hivyo katika mkutano huo tutazungumza na kutoa ujumbe wetu,"amesema.

Pia aliulizwa kuhusu suala la amani ambapo kuna baadhi ya nchi za Afrika usalama si wa uhakika sana, ambapo amejibu kwa sasa nchi nyingi ziko salama zikiwemo nchi jirani lakini bado iko nafasi ya kuendelea kujadiliana na ndio maana katika mkutano huo kuna nchi za Afrika ambazo haziko salama wameaalikwa na zitapata nafasi ya kusikilizwa .

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA MABORESHO YA HUDUMA MLIMA KILIMANJARO.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.


Na. Aron Msigwa – WMU, ARUSHA.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) lifanye maboresho ya miundombinu ya huduma za dharula na uokoaji ndani ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro ili kuogeza usalama wa watalii wanaokweda 2kupanda mlima huo.

Pia, amelitaka shirika hilo liedelee kuboresha miudombinu ya malazi katika hifadhi hiyo ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa ya wapanda mlima na kuangalia uwezekano wa kutafuta wawekezaji watakaojenga hoteli za kisasa kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.

Dkt.Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati akipada mlima Kilimanjaro Septemba, 28 mwaka huu, akiwa ameambatana na kundi la Wasanii na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi.

Dkt. Kigwangalla ameieleza Menejimenti hiyo kuwa katika zoezi lake la kupanda mlima Kilimanjaro kuna changamoto alizibaini zikiwemo za kukosekana kwa miudombinu ya kutosha ya huduma za uokoaji na malazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuongeza ufanisi na idadi ya watalii wanaopanda mlima huo.

Kufuatia hali hiyo ameiagiza TANAPA ianze kuboresha huduma za dharula na uokoaji pia ijenge vituo vya kutolea tiba na huduma ya kwanza mlimani vitakavyokuwa na wataalam wa kuhudumia watalii wanaopata matatizo wakiwa mlimani pia kuboresha huduma za malazi katika baadhi njia za mlima huo.

Dkt.Kigwangalla amesema changamoto hizo zikitatuliwa kwa haraka zitauwezesha mlima huo kupata idadi kubwa ya watalii kuliko ilivyo sasa na kuiogezea serikali mapato.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za uokoaji (Rescue services) kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro ameiagiza TANAPA ifanye utaratibu wa kuazisha huduma ya viberege maalum (Zip line) vitakavyokua vinatumika kushusha wapada mlima watakaokua wakipata matatizo ya kiafya kwa haraka hata wakati wa hali mbaya ya hewa.

“Suala la matumizi ya “Zip line” mliongezee nguvu ya kulitekeleza, hii itakua njia rahisi ya uokoaji na itawajengea ujasiri wapada mlima waelewe kwamba hata kama watapata shida yoyote ya kiafya wakati wa kupanda mlima wanajua wana uhakika wa usalama wa maisha yao hata pale ambapo hali ya hewa ni mbaya na helikopta haiwezi kutua mlimani” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Amesema uwepo wa huduma hiyo ya kisasa ya kushusha watalii wanaopata chagamoto za kiafya itawezesha watalii kupata huduma mlimani kupitia vituo vya kutolea huduma ya kwanza vitakavyojegwa mlimani ambavyo vitakua na wataalam wenye mafumzo watakaokuwa na jukumu la kutoa huduma muda wote.

Kuhusu uboreshaji wa huduma ya malazi mlimani Dkt. Kigwangalla ameonesha kuridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na TANAPA kuboresha miundombinu ya malazi mlimani na kuitaka iangalie uwezekano wa kuhamasisha wawekezaji wakubwa kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa. 

Amesema uwepo wa hoteli hizo pamoja na mambo mengine utaongeza siku za watalii kukaa mlimani akitoa mfano wa hoteli nzuri na za kisasa zilizojengwa katika milima ya Alaps ambazo zinatembelewa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Kufuatia maagizo hayo, Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi amesema kuwa TANAPA inaendelea kufanya maboresho kwenye maeneo ya kulala wageni ili yaweze kwenda na wakati pia yawe na uwezo wa kupokea wageni wengi pia kuishirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma mlimani.

Amesema kazi ya kuainisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kisasa inaendelea na kwa kuanzia maeneo manne yamekwishaainishwa kwa ajili ya uwekezaji na kuongeza kuwa baadhi ya wawekezaji wamekwishajitokeza na kuonesha nia ya kujenga hoteli za kisasa katika mlima huo.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za ukoaji mlimani amesema kwa sasa kuna maeneo yana miundombinu ya barabara zinazowezwsha magari ya kubebea wagonjwa kufika katika baadhi ya maeneo na kutoa huduma ya uokoaji.

Pia amesema wamekua wakitumia helikopta kutoa huduma za uokoaji licha ya huduma hiyo kushindwa kufanyika kazi wakati wa hali mbaya ya hewa na hivyo kulazimika kutumia machela za matairi zinazoendeshwa na watu kuhudumia watalii wanaopata matatizo ya kiafya.

Aidha, Dkt. Kijazi amesema TANAPA inaendelea kufanya maboresho ya huduma za dharula na uokoaji na itawasilisha kwake taarifa ya utekelezaji itakayoainisha mpango wa ujenzi wa njia za kisasa zitakazotumia viberenge maalum vya uokoaji vitakavyokua vikipita kwenye waya (Zip line) ili kazi ya ujenzi wa njia hizo ianze mara moja. 

Miezi 15 ya mradi wa elimu kwa vishikwambi wakamilika

$
0
0
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (kulia) akimkabidhi Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (wa pili kulia) ripoti ya utekelezaji wa mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Hilary Bitwaye (kushoto), Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Michael Amos (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi Odilia Mushi.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi Odilia Mushi (wa pili kulia) ripoti ya utekelezaji wa mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Michael Amos (kushoto).
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (kulia) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Hilary Bitwaye (katikati) ripoti ya utekelezaji wa mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi Odilia Mushi.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (wa pili kulia) akimkabidhi Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (katikati) funguo za gari la mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kulia), Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi (kushoto) pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Michael Amos (wa pili kushoto).
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos (katikati) akimkabidhi Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (wa pili kushoto) gari la mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi (kushoto), Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia), Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Michael Amos (kulia).
Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (aliyeshika usukani) na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Odilia Mushi wakiwa ndani ya gari la mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP mara baada ya kupokea gari hilo kutoka UNESCO wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa halmashauri ya Korogwe walionufaika na mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Zena Said akitoa hotuba wakati wa kufunga wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi wa XPRIZE- uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos akitoa salamu za UNESCO wakati wa kufunga wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo akifafanua jambo wakati wa kufunga wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli , Bi Odilia Mushi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mtoto Habiba Athumani (13) mkazi wa kijiji cha Tabora wilayani Korogwe akitoa ushuhuda kwa wageni waalikwa kuhusu mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mtoto Ismail Adamu (13) mkazi wa kijiji cha Majengo wilayani Korogwe akitoa ushuhuda kwa wageni waalikwa kuhusu mradi wa XPRIZE- uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mmoja wa wazazi Stella Ernest ambaye mtoto wake amenufaika na mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi akitoa ushuhuda wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mmoja wa wazazi Hassan Shomari ambaye mtoto wake amenufaika na mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi akitoa ushuhuda wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wazazi ambao watoto wao wamenufaika na mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Baadhi ya watoto ambao wamenufaika na mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi wakati wa hafla fupi ya kufunga mradi huo iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika hafla fupi ya kufunga mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos wakitiliana saini na Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (kushoto) ya hati ya makabidhiano ya mradi wa XPRIZE uliokuwa ukiratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP wa kuwapatia elimu watoto walio nje ya mfumo rasmi kupitia ubunifu wa Teknolojia kwa kutumia Vishikwambi wakati wa kufunga mradi huo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, mkoani Tanga.


SERIKALI imetaka watoto wote walioshiriki katika mradi wa XPRIZE-Unesco wa kujua Kuandika, Kusoma na Kuhesabu kwa kutumia Vishikwambi katika mradi wa majaribio mkoa wa Tanga kuhakikishwa wanaendelea na elimu katika shule shirikishi za mkoa huo.

Mradi huo wa XPRIZE umekamilisha awamu yake ya miezi 15 na mafanikio yake ni makubwa.

Akizungumza mjini Korogwe wakati wa kufunga mradi huo, Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said alisema kwamba mradi huo ulilenga kupeleka elimu kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu unastahili kuingia awamu ya pili kabla ya mafanikio yake kusambazwa nchi nzima.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bi. Zena alisema kwamba kwa sasa wanafanya mchakato wa kuwa na awamu ya pili ya mradi huo ambao utaondoa changamoto zilizopo kabla ya kusambazwa nchini kote.

Mradi huo ulioanza Desemba 2017 umefikia mwisho wake Aprili mwaka huu na umeelezwa kuwezesha watoto walioshiriki kufanya vyema katika masomo hayo waliojifunza bila Mwalimu kwa kutumia michezo iliyopo kwenye Vishikwambi.

Watoto wanaohusika ni wa miaka 5 mpaka 12. Imeelezwa kuwa kwa matumizi hayo ya Vishikwambi na mafanikio yake inaonesha kuwa njia nyingine ya kurejesha watoto wengi waliokosa elimu, darasani kwa kutumia teknolojia upo sahihi.

Bi. Zena alisema hakuna shaka kwamba elimu ni muhimu na kutokana na ukweli huo, mradi umedhirisha uwezo wake wa kusaidia wasioipata kwa kawaida kuipata. Katika kuimarisha kwenye mchakato wa pili kwa kuangalia matatizo yaliyopunguza kasi, serikali inaona Vishikwambi vibaki shule kwa usalama na pia walimu kutumika kuwezesha watoto wengi zaidi kujua kwa kasi KKK huku wakiimarisha uwezo wao wa kutumia teknolojia kujilete maendeleo.

Alisema pamoja na kunufaisha watoto mradi huo pia umefanikiwa kisaikolojia kushawishi watoto zaidi kupenda kusoma na kuanza mapema kutengeneza uongozi hasa kwa vijana ambao kutokana na kujua kusoma wamekuwa maarufu katika vijiji vyao.

Alitaka pamoja na kumalizika kwa mradi huo, wasimamizi wa sola katika vitongoji 170 kuhakikisha kwamba wanatunza sola hizo ili kusaidia vijana hao na watu wengine kufanyia kuchaji.

Mafanikio ya mradi huo kunaongeza nafasi zaidi kwa mujibu wa sera ya serikali ya kuhakikisha kwamba watoto wote hata wale ambao hawakuingia katika mfumo rasmi wanaingiza katika mfumo wa elimu kwa kupitia taratibu mbalimbali. Kwa sasa taratibu hizo ni utaratibu wa Memkwa kwa elimu ya msingi na Mespa kwa sekondari

Mradi huo ambao umefungwa ni sehemu ya mradi wa majaribio wa dunia ambapo teknolojia inajaribiwa kusaidia wale waliokosa nafasi ya kuingia shule.

Wakati mradi huo unaanza mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert alisema kwamba mafanikio yake yatawezeshwa kutengenezwa kwa moduli za kufundishia watoto walio nje ya mfumo rasmi wanaotumia lugha ya Kiswahili.

Washiriki wa mradi huo wa XPRIZE chini ya uangalizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) na Kamati ya kitaifa inayohusisha pia Wizara ya Elimu imelenga kuwapata watoto ambao wanaweza kuingizwa darasa la pili na kuendelea na pia kuongeza uwezo wa kumudu masomo kwa watoto wa darasa la pili. Mradi huo ni matokeo ya mashindano Global Learning XPRIZE yaliyozinduliwa na Taasisi ya XPRIZE Septemba 2014.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos alisema katika hafla hiyo kwamba mradi huo ulisohirikisha wilaya sita za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza, na Pangani umekuwa na mafanikio kutokana na kujitoa kwa wadau wa mradi huo na wale ambao wamepelekewa.

Alishukuru serikali ya Tanzania kwua kushiriki katika shindano na pia kutekeleza malengo ya mradi huo. Alisema mradi huo ni utekelezaji wa wazo la UNESCO kwamba elimu ni tumaini jema lakufikia maendeleo.

“Mradi wa XPRIZE umedhirisha kwamba mafunzo au utoaji elimu kwa watu ambao wamekosa au wana mazingira magumu unaweza kuboreshwa kwa ubunifu wa watoto kujifunza wenyewe kwa kutumia mifumo ya komyuta kama ilivyokuwa kwa vishikwambi “ alisema Tirso.

Alisema kabla ya mradi huo washiriki wake asilimia 74 walikuw ahawajwahi kugusa jingo inaloitwa shule, asilimia 80 walikuwa wanajifunza nyumbani na asiimia 90 walikuwahawawezi kusoma hata neon moja la Kiswahili ambalo ni lugha yataifa.

“Baada ya miezi 15 namba hizo zimepunguzwa kwa zaidi ya nusu huku watoto hao wakijifunza takribani sawa na watu walioshiriki darasani kwa kipindi cha mwaka mzima” alisema.

Kutokana na mafanikio hayo UNESCO imeitaka Wizara ya Elimu kusambaza zaidi wazo la mradi huo ili kuwafikia watoto wengi zaidi waliopemnbezoni na mazingira magumu yamaisha.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli, Bi Odilia Mushi alisema kwamba mradi huo umefanikiwa na kwamba nia ya serikali kuuimarisha na kuutambua zaidi kabla ya kuutawanya nchini.

Alisema pamoja na kuibua hamasa, ushuhuda wa watoto wenyewe unaonesha kwamba teknolojia inaweza kutumika kufungua maeneo yenye matatizo ya kufikika.

Aidha Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akimkaribisha mgeni rasmi alisema kwamba watoto ambao walikuwa wamekosa elimu wamepata faida kubwa ya mradi huo hasa wa kujua kuandika kusoma na kuhesabu.

“Hawawezi kuandika kwa kutumia kalamu lakini wanaweza kuandika kwa kutumia Vishikwambi na ni hatua kubwa ya kujua teknolojia na matumizi yake” alisema.

Mmoja wa wazazi Stella Ernest, aliishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa kuwezesha kuwapo kwa programu hiyo ambayo imewatoa kimasomaso. Alisema watoto wamekuwa werevu zaidi na kutambua mambo katika hali ya kisasa kuliko awali.

Alisema hata mtoto wake mdogo siku hizi kwa kufurahishwa na michezo iliyopo katika Vishkwambi hivyo anapoamka humuuliza mama yake kama anajua kuandika Ameitaka serikali kuboresha zaidi mradi huo na kuufanya kuwa endelevu ili kusaidia watoto wengi zaidi. Aidha alitaka watoto waliobahatika kupata kujifunza wenyewe kupokewa na kuendelezwa zaidi.

Kauli hiyo pia imetolewa na mzazi mwingine Janeth Massawe ambaye alisema mradi huo ni wa mfano kwani umewasaidia kuwaondolea tatizo la elimu katika eneo lao. Alisema mradi huo umepokewa vyema na kwamba umewachagiza kutambua umuhimu wa elimu.

MRADI WA UJENZI MELI MPYA NA CHELEZO WASHIKA KASI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Bw. Eric Hamissi akimpa maelezo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi hatua iliyofikiwa ikiwemo vifaa ambavyo vimeshawasili nchini mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria ambapo Serikali imeweka Kiasi cha Shilingi Bilioni 89 katika mradi huu.



Meneja Mradi wa Chelezo na Ukarabati wa Meli za MV. Victoria na MV Butiama Mhandisi Abel Gwanafyo akimpa maelezo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Chelezo ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki meli kwa ajili ya matengenezo na marekebisho mbalimbali, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Bw. Eric Hamissi


Baadhi ya Mafundi wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria itakayofanya kazi katika ziwa victoria.


Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga meli mpya na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli alipotembelea eneo hilo ili kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa meli hiyo itakayofanya kazi katika ziwa victoria.

Muonekano wa Meli ya MV. Victoria inayokarabatiwa na Kampuni ya Huduma za Meli. 
Muonekano wa Chelezo inayojengwa na Kampuni ya Huduma za Meli ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki meli kwa ajili ya matengenezo na marekebisho mbalimbali ambayo imefikia asilimia 53 ya ujenzi na itaanza kutumika mwezi Machi 2020

…………………………………………….

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi jana (Oktoba 31) alitembelea mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ambayo ni meli kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na ujenzi wa chelezo kwa ajili ya matengenezo na marekebisho ya meli mbalimbali ikiwa ni uwekezaji unaofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Abbasi alisema kuwa ujenzi wa meli mpya ni ahadi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 23 iliyopita, ambayo imetekelezwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais . Dkt Magufuli. 

Aidha, Dkt. Abbasi aliongeza kuwa ujenzi wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1, 200 umefikia asilimia 33 ya ujenzi na utakamilika mapema mwaka 2021, ambapo Serikali imewekeza zaidi ya TZS Bilioni 150, kwenye mradi ya meli pamoja na ujenzi wa chelezo. 

Aidha, Dkt. Abbasi alishuhudia ukarabati unaoendelea katika meli ya MV. Victoria, ambayo baada ya kukamilika itasaidia kutoa huduma bora za usafiri kwenye eneo la Ziwa Victoria. 

Vilevile, akiwa ziarani hapo Dkt. Abbasi alisema kuwa ipo miradi mingi kwenye eneo la Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika, inatakayo gharimu zaidi ya TZS Bilioni 300.

Aliongeza kuwa hivi karibuni, Serikali itasaini makubaliano ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa meli katika eneo la Ziwa Tanganyika na uundaji wa meli 3 mpya na za kisasa katika eneo la Ziwa Nyasa. 

Akitaja, meli zilizokamilika kutokana na utekelezaji wa ahadi za Serikali hadi sasa kuwa ni meli za mbili za mizigo za MV. Ruvuma, na meli kubwa ya kisasa ya abiria ya MV. Mbeya II na ambayo tayari imeanza kazi. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi, alisema kuwa ujenzi wa meli hiyo mpya unaendelea vizuri, na Septemba 30, mwaka huu vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vilianza kuletwa na sasa kazi ya uunganishwaji wa vyuma imeshaanza. 

Aliongeza kuwa, ujenzi wa chelezo umefikia 53%, na ifikapo Machi mwakani chelezo itanza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya. 

Aidha, Bw. Hamissi alisema anaishukuru Serikali kwa ujenzi miradi hii miwili pamoja na ya ukarabariti wa MV. Butiama na MV. Victoria inayoendelea kwani itaigharimu Serikali TZS Bilioni 150, na hadi sasa Serikali imeshatoa TZS Bilioni 70.8, sawa na 47% ya miradi yote minne. 

Bw. Hamissi, aliongeza kuwa miradi hii imesaidia kukuza uchumi wa Mwanza kwa kutoa ajira zaidi ya watu 1,000 pamoja utumiaji wa malighafi na watoa huduma, hali inayosaidia kuboresha maisha ya wananchi. 

Alifafanua kuwa, huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ambao haujawahi kutokea tangu Uhuru na ni mapinduzi katika usafiri wa njia ya maji kwa kutekeleza miradi mikubwa minne kwa wakati mmoja, na kuwa awali meli nyingi zilijengwa kwa msaada mfano MV. Sangara.

Naye, Li Yonjee, Mtaalamu wa Meli kutoka Korea Kusini, alisema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa fursa ya kushiriki katika uundaji wa meli mpya ya kisasa, watatumia ujuzi wao wa uundaji wa meli waliofanya katika nchi za Korea ya Kusini, China na Japan, zikiwa ndio nchi kubwa za uundaji wa meli duniani, katika kuunda meli mpya ya Tanzania. 

Vilevile, Bw. Li alisema kuwa wanaahidi kutimiza matarajio ya Serikali na watanzania kwa ujumla kwa kuunda meli hiyo kwa mafanikio, pamoja kuikamilisha kwa wakati. 

Aidha, Bhoke Siguta mwanamke anayefanyakazi ya kuchomelea vyuma katika mradi wa uundaji wa meli mpya, alisema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watanzania, ikiwemo kutoa ajira. 

Bi. Siguta alisisitiza kuwa, kupitia mradi huu wa uundaji wa meli mpya ameweza kupata ajira, inayompatia kipato cha kumsaidia kutunza familia yake. 

Pia, ameshauri wanawake kujishughulisha na kazi za uchomeleaji vyuma, kwani ni kazi nzuri na zitawajengea uwezo zaidi wa kujiamini pamoja na kukuza kipato. 

Awali, Dkt. Abbasi alikutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli kuhusu mikakati na maboresho ya kampuni hiyo.

Vodacom yazindua Smart Kitochi, Simu janja ya kwanza Tanzania inayopatikana kwa bei rahisi kutoka KaiOS

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata (kushoto) akitambulisha simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi kwa waandishi wa habari jana, inayotumia KaiOS, mfumo ambao unaongoza duniani katika teknolojia ya simu janja, ni ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa kila mwezi ndani ya miezi sita ya kwanza.Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.
Mteja wa kwanza kununua simu mpya ya kitochi yenye 4G na zana za simu janja Smart Kitochi, Lydia Mtei mkazi wa Mbezi Beach akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc,George Lugata mara baada ya kuzindua simu hiyo kwenye duka la Vodashop mlimani city jana ambapo itapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano cha kampuni hiyo Jacquiline Materu na balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki.
Balozi wa Smart Kitochi, Sylvester Mujuni maarufu kama Mpoki akielezea zana zilizomo ndani ya Smart Kitochi mbele ya waandishi wa habari jana, Vodacom ni kampuni ya kwanza nchini kuleta simu ya kitochi yenye uwezo wa simu janja kwa kupata huduma za Apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi.


Baadhi ya wateja waliojitokeza kununua simu za Smart Kitochi jana kwenye duka la Vodacom Mlimani city jijini Dar Es Salaam.



Simu inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini
Wateja kupata data, muda wa maongezi na SMS bure kwa miezi 6 ya kwanza

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza uzinduzi wa simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia KaiOS, mfumo ambao unaoongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.

Uzinduzi huu unaongeza hatua kubwa si kwa kampuni hizi mbili tu, bali hata kwa nchi. Ni simu janja ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 (Dola 20 za Marekani) ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa miezi sita ya kwanza.

Smart Kitochi inatumia apps muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi zikiwapa fursa watanzania kujiunga na huduma ya inteneti. Ikiwa na sifa zote za simu janja kama vile kuwa na Wi-Fi, GPS, simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili zenye uwezo wa uhifadhi wa GB 4 + MB 512. Pia ina betri yenye nguvu ya mAh 1400 na kudumu saa sita. Ikiwa inazinduliwa leo hapa nchini, simu hii pia itaanza kupatikana katika nchi nyingine za Afrika hivi karibuni.

“Tuna furaha kuwaleteeni simu hii mpya sokoni kwa ushirikiano na mshirika wetu KaiOS Technologies,” anasema George Lugata, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Vodacom. “Pamoja na uwepo wa matumizi makubwa katika mtandao wa mawasiliano nchini, bado tunakumbana na changamoto za kidigitali kwa sababu ya uwepo mdogo wa matumizi ya simu janja, kwa kufanya hivyo tunawaletea Smart Kitochi kwa bei nafuu kwa kila mtu.

KaiOS inatumia mfumo mwepesi kabisa ambao una sifa zote za simu janja ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutosha wa uhifadhi. Pamoja na sifa hizo simu hiyo inatumia mifumo ya 3G na 4G/LTE, Wi-Fi, GPS, pamoja na NFC.

Simu ya KaiOS inakuja ikiwa na apps maarufu kama WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube, and Google Maps. Halikadhalika simu hii ina app ya KaiStore, ambayo ni kati ya apps zaidi ya 200 zinazotumiwa na watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano duniani.

KaiOS Technologies ni ya tatu kwa ukubwa duniani katika mfumo wa utoaji huduma za mawasiliano ya kidigitali, ikiwa na zaidi ya aina 100 za vifaa vinavyosambazwa katika Mabara ya Ulaya, Afrika, Asia na Marekani.

“Mgawanyiko wa matumizi ya mfumo wa kidigitali Afrika bado ni mpana. Tumejikita zaidi katika kutoa fursa pamoja na kuleta teknolojia mpya yenye utatuzi wa mambo mbambali na ndiyo maana tumeamua kufanya kazi na Vodacom. Smart Kitochi ni hatua moja muhimu katika kuuwaunganisha wale ambao walikuwa nyuma katika matumizi ya inteneti na rasilimali zote muhimu za mawasiliano nchini na kwingineko’” anasema Afisa Mtendaji Mkuu wa KaiOS Technologies, Sebastien Codeville.

“Simu ya Smart Kitochi inapatikana katika maduka yote ya Vodashop nchini na katika vituo vyote vya huduma na mauzo ya bidhaa zetu nchini kote kwa bei ya punguzo ya Tsh 48,000. Niwaombe Watanzania na hasa wateja wetu kujitokeza kununua simu hii ili waweze kufurahia huduma za Mtandao Supa na kufurahia apps kama vile Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram na nyingine nyingi zinazopatikana katika simu janja,” alihitimisha Lugata.

RC MAKONDA AZINDUA UJENZI WA BARABARA ZA MAKONGO JUU NA MADALE AMBAZO ZIMEKUWA ZIKILALAMIKIWA NA WANANCHI KWA UBOVU.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo November 01 amezindua ujenzi wa barabara za Makongo Juu na Barabara ya Madale ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikilalamikiwa kwa ubovu uliokuwa ukisababisha uharibifu wa vyombo vya usafiri, Vumbi, kupanda Gharama za usafiri na kusabbisha watu kuchelewa katika shughuli zao ambapo amewaelekeza wakandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.

RC Makonda amesema barabara ya Makongo Juu inajengwa kwa kiwango cha lami na ina urefu wa Km 4.5 ambapo ujenzi wake utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 8.9 na itachukuwa muda wa miezi 12 kukamikika ambapo ukijumuisha na gharama za fidia kwa wananchi, gharama za kuhamisha miundombinu ya umeme na maji itafikia kiasi cha shilingi Bilioni 14 ambapo amesema wananchi waliopitiwa na njia hiyo watalipwa fidia.

Akiwa kwenye Uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Barabara ya Madale yenye urefu wa Km 6 RC Makonda amesema ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.9 na mkandarasi anatakiwa kukamilisha mradi ndani ya miezi 18 kuanzia sasa.

RC Makonda amesema kukamikika kwa barabara hiyo kutawezesha watumiaji wa barabara kutumia njia ya mkato kuanzia Tegeta kutokea Wazo kuelekea Madale kutopitia Goba na hatimae kuingia Makongo na kutokea Eneo la Mlimani City jambo litakalosaidia kupunguza foleni kwenye Barabara ya Bagamoyo.

Pamoja na hayo RC Makonda ujenzi wa barabara zote hizo utajumuisha Taa za barabarani, Mitaro ya Maji ya Mvua na Sehemu ya Watembea kwa Miguu ambapo amewaomba wananchi kuwa wavumivu wakati ujenzi unaendelea.

Wananchi Tandahimba waanza kutekeleza Kampeni ya ujenzi wa matundu ya vyoo.

$
0
0
Afisa Elimu Msingi  wa Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka amesema kuwa wakazi katika vijiji  Wilayani  humo wameanza  kuchimba matundu vyoo kutekeleza Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

Mwinuka amesema wananchi wamekubaliana kuchimba matundu ya vyoo 50 kwa shule za msingi Ruvuma na Mihambwe 

Katika Kijiji Cha Chitoholi na Mkupete tayari nao wameanza ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Chitoholi na Mkupete

"Tupo pamoja  katika Kampeni ya shule ni choo ambapo wananchi  wamekubaliana kujenga matundu ya vyoo katika shule zao za msingi kwa kujitolea kwa Hali na Mali ili tatizo Hilo lisiwepo katika maeneo yao,"alisema Mwinuka

Kampeni ya shule ni choo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa  la  kuondoa tatizo la uhaba wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari ndani ya Mkoa wa Mtwara
 Ujenzi wa Matundu ya vyoo ukiendelea
 Wanakijiji wakijitolea katika maandalizi ya kujenga matundu ya vyoo 

 Wanakijiji wakijitolea katika maandalizi ya kujenga matundu ya vyoo
Wananchi wakijadiliana ili kufikia malengo yao

TAASISI YA ACHA, TRW WAZINDUA MUUNGANO WAO WA TANZANIA ELECTION ALLIANCE ILI KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA NA UCHAGUZI

$
0
0
Viongozi waandamizi wa muugano wa Tanzania Election Alliance (TanEA ) pichani, kulia Mwenyekiti wa Muungano huo Michael Kyande,Katibu wa Taasisi ya The Right Way (TRW),Gideon Mazara,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Action for Change (ACHA),Bi.Martina Kabisama pamoja na Mwenyekiti wa ACHA Justina Shauri wakionesha vijarida vya elimu ya Uraia na Uchaguzi  vitakavyosambazwa kwa Wananchi baada ya kuzindua Muungano wao leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi JR (MMG).
 Viongozi waandamizi wa muugano wa Tanzania Election Alliance (TanEA ) pichani  wakishuhudia Mwenyekiti wa Muungano huo Michael Kyande (kulia), akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Muungano huo leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Action for Change (ACHA),Bi.Martina Kabisama akizungumza leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam
 wakati wa uzinduzi wa Muungano wa Tanzania Election Alliance (TanEA ) wenye lengo la kutoa elimu ya Uraia na Uchaguzi kwa Wananchi kwa kuanza na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Action for Change (ACHA) Justina Shauri akifafanua jambo katika uzinduzi huo leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam
Mratibu wa muugano wa Tanzania Election Alliance (TanEA ) ,Rhoda Kamungu akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo,uliofanyika leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam



 Viongozi waandamizi wa Tanzania Election Alliance (TanEA ) wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi huo leo Novemba 1,2019 jijini Dar es Salaam

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii
TAASISI ya Action For Change(ACHA)  na Right Way  (TRW)  waungana kwa pamoja na kuzindua muungano wao unaofahamika kwa jina la Tanzania Election Alliance kwa lengo la kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu ya uraia na kueleza kuwa katika kutekeleza majukumu yao watashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali wanaohusika na chaguzi ukiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Muungano huo umezinduliwa leo Novemba 1, mwaka 2019 jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine viongozi wake wameeleza kuwa malengo yao, matarajio yao na ushiriki wao katika kujadili mafanikio na changamoto zilizopo katika michakato  mbalilmbali ya  uchaguzi.
Akizungumza  wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa ACHA Martina  Kabisama amesema wameona iko haja ya wao kuunganisha nguvu ya pamoja na kufanya kazi  zinazohusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
"Naomba nieleweke vizuri vibali ambavyo tumevipata ni kwa ajili ya kutoa elimu ya uraia pamoja na ile ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu mwaka 2020,"amesema  Kabisama na kuongeza muungano huo upo kihalali kwani umefuata tararibu zote na hata asasi zilizounda muugano huo zimesajiliwa na zinatambuliwa kisheria.
Amefafanua zaidi wameamua kuwa na muungano huo baada ya kuona ndani yao wamo wabobezi wa masuala ya uchaguzi ambapo waliangalia kabla ya kufikia uamuzi huo waliangalia masuala ya uchaguzi na ushiriki wa wananchi na kubaini wanayo nafasi ya wao kuunganisha nguvu ili chaguzi ziwe na mafanikio kabla na baada ya chaguzi.
"Katika kufuatilia tulibaini kuna mafanikio makubwa katika chaguzi zetu na wakati huo huo kuna changamoto, hivyo tumeona tuje na huu muunganiko kwa ajili ya uchaguzi kwani hakuna sababu ya sisi kubaki nyuma lazima tushiriki ili tuwe sehemu ya kuondoa changamoto zilizopo.
"Katika changamoto hizo zinaweza kuwa zinazohusu wananchi, sheria au vyombo vinavyosimamia uchaguzi aidha wa  Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu .Hivyo lazima tukae na kutafuta ufumbuzi kwa pamoja,"amesema.
 Hata hivyo amesema katika kuhakikisha muungano huo unakwenda vizuri waliamua kujiwekea malengo yao kwani kuungana bila kuwa a malengo ni rahisi kuvunjika. Ametumia nafasi hiyo kueleza taasisi za chaguzi zipo na zinapita  katika michakato mbalimbali hadi inapofikia hatua ya kupiga kura na kisha kuingia katika mchakato wa kuanza uchaguzi mwingine.
"Uchaguzi ni kama duara, tunapomaliza uchaguzi mmoja tunaanza safari ya uchaguzi mwingine.Hivyo muungano wetu nao tutashiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na baada ya hapo tutaendelea na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020,"amesema .
Ameongeza  taasisi ambazo zinahusika na chaguzi za Serikali za Mitaa ni Wizara ya Nchi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) , hivyo ameahidi kushirikina na TAMISEMI kuhakikisha uchaguzi huo wa mitaa unakwenda vizuri  na katika uchaguzi mkuu mwaka 2020 watashirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC).
Wakati huo huo Kabisama amezungumzia umuhimu wa Watanzania kushiriki katika chaguzi huku wakihakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na usalama na kuongeza wajibu wa kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha na siku ya kupiga kura anakwenda kuchagua kiongozi au viongozi kwa maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACHA Justina Shauri amesema vyombo vya habari vinadhamana kubwa ya kufikisha taarifa na hivyo wanategemewa sana katika kufikisha habari zinazohusu elimu kwa mpiga kura na mchakato wa kupiga kura.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shauri amesisitiza umuhimu wa uhuru wa demokrasia kwa kuhakikisha watu wanaachwa wafanya kazi za uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kama watu wanataka kuundamana basi taratibu zifuatwe.
Pia Shauri amezungumzia suala la uangalizi wa ambapo katika hilo amesema waangalizi wa uchaguzi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na hiyo itasaidia kutambua changamoto zilizopo na hatimaye zitapatiwa ufumbuzi.

"Ukiwa makini katika suala la uangalizi wa uchaguzi kuna mambo tu utayabaini aidha ya mafanikio au changamoto.Hivyo itakuwa rahisi kuboresha chaguzi zetu maana yale ambayo yatakuwa kama sababu za kukwamisha mchakato yatapata ufumbuzi,"amesema Shauri na kuongeza hivyo moja ya majukumu yao ni kutoa elimu pia kwa waangalizi nini wafanye ili kazi hiyo kufanyika kwa ufasaha.

CBE WAZINDUA KATIBA YA UMOJA WA WAHITIMU WA CHUO HICHO (ALUMNI)

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHUO cha Elimu ya Biashara nchini (CBE) kimezindua rasmi umoja wa wahitimu waliosoma katika Chuo hicho katika matawi ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya na hiyo ni pamoja na kuzindua katiba ambayo itaongoza jumuiya hasa katika kutoa mchango wao katika masuala ya elimu na maendeleo kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye Mhitimu wa chuo cha CBE, mchambuzi wa  masuala ya soka na mchambuzi wa sera wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ally  Mayay  Tembele ameupongeza uongozi wa Chuo hicho na wahitimu wa chuo hicho kwa kuona umuhimu wa umoja huo utakaoongozwa kwa katiba maalumu.

Amesema kuwa licha ya kutambulika zaidi katika soka ila elimu ya biashara anayoifanyia kazi ameipata katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) hivyo umoja huo una manufaa na mafanikio kwao na kwa taasisi hiyo.

Mayay amesema Serikali ya awamu ya tano chini uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli na wasaidizi wake wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taifa linajenga uchumi na viwanda ambao kupitia maarifa ya Elimu ya Biashara yanayotolewa na Chuo hicho yatafanikisha kwa kiasi kikubwa kuyafikia malengo hayo.

Amesema wahitimu lazima watumie fursa mpya zinazojitokeza hasa katika viwanda na hiyo ni kutokana na dira ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati kufikia mwaka 2025 na hiyo ni pamoja na kujishughulisha na masuala ya usindikaji wa mazao hasa ya kilimo ili kuweza kudhihirisha nguvu zao na maarifa yao katika kutenda kazi.

Kwa upande wake  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Mjema amesema kuwa na umoja wa wahitimu ni muhimu kwa kuwa hadhi ya Chuo hicho kipo juu kitaifa na kimataifa katika taaluma.

Aidha ameishukuru  Serikali kwa kuendelea kushiriki katika kuhakikisha kampasi zote za Chuo hicho zinapata mahitaji yote muhimu ili kuwezesha kupata elimu bora zaidi na amewashauri wahitimu hao kusaidiana hasa katika masuala ya kujiajiri na na kushirikiana na Chuo kwa kuwa mabalozi bora katika jamii.

Pia aliyekuwa Rais wa chuo hicho Jonathan  Nkwabi amesema kuwa wahitimu wa miaka iliyopita kutoka chuo hicho (Alumni) lazima washirikiane katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko na maendeleo katika chuo chao na hiyo ni pamoja na kuisaidia Serikali katika kufikia uchumi wa viwanda na hiyo ni kwa kuwa Chuo hicho ni hazina yakubwa ya masomo ya Elimu ya  Biashara.

Amesema kuwa umoja huo lazima ulete mabadiliko katika Chuo cha Biashara (CBE) na hiyo ni pamoja na kukishauri Chuo juu ya mwenendo wa ajira ili kuweza kurekebisha mitaala kulingana na mahitaji ya soko la ajira.

Nkwabi amesema kuwa umoja huo umesaidia katika kushiriki shughuli mbalimbali ya kijamii ikiwemo kutembelea wagonjwa, gereza la watoto upanga na kutembelea watoto yatima na hiyo ni pamoja na kuwa na wiki ya ubunifu pamoja na kutangaza shughuli mbalimbali wanazozifanya licha ya kupambana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wahitimu kutotambua faida ya kuwepo kwenye umoja huo.

Mmoja wa wahitimu kutoka Chuo hicho Renatha Rubaragamu aliyehitimu mwaka 1976 amesema kuwa Chuo hicho kimekuwa hazina kubwa katika masuala ya biashara na hata sasa chuo hicho kimeendelea kujiweka katika nafasi nzuri na kupitia umoja huo wanaamini watafika mbali zaidi.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mhitimu wa chuo cha CBE, mchambuzi wa  masuala ya soka na mchambuzi wa sera wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ally Mayay Tembele akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa katiba itakayoongoza umoja wa wahitimu wa Chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam. 
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mhitimu wa chuo cha CBE, mchambuzi wa  masuala ya soka na mchambuzi wa sera wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ally Mayay Tembele akiwa na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho wakionesha katiba ambayo itaongoza umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni,) leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mhitimu wa chuo cha CBE, mchambuzi wa  masuala ya soka na mchambuzi wa sera wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ally Mayay Tembele akizungumza katika hafla yaa kuzindua katiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) na kueleza kuwa maarifa yanayotolewa na Chuo hicho  yana tija kubwa katika kufikia uchumi wa kati kwaka 2025, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Mjema akizungumza katika hafla hiyo ya kuzindua katiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) ambapo amesema kuwa wahitimu lazima wawe mabalozi bora kwa Chuo hicho pamoja na kusaidiana katika masuala ya kujiajiri wenyewe, leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) anayeshughulikia masuala ya  Fedha, utawala bora na Mipango Dkt. Emmanuel Munishi akizungumza katika hafla ya kuzindua umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) ambapo ameeleza kuwa wanaamini umoja huo utaleta mapinduzi hasa katika sekta ya elimu na maendeleo kwa ujumla,  leo jijini Dar es Salaam.
 Mhitimu wa Chuo cha Biashara (CBE) mwaka 1976, Lenatha Rubaragamu akizungumza katika hafla hiyo ya kuzindua umoja wa wahitimu wa Chuo hicho (Alumni) na kueleza kuwa maarifa aliyoyapata kutoka Chuo hicho yamekuwa hazina kubwa katika utendaji kazi wake, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Leonidas Tibanga akisherehesha hafla hiyo ya uzinduzi wa katiba ya umoja wa wahitimu wa chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wahitimu (Alumni) waliohitimu kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma hadi mwaka 1965 wakichangia mada kwenye mkutano wa uzinduzi wa katiba ya umoja huo uliofanyika katika hoteli ya Peacock leo jijini Dar es Salaam


Baadhi ya wahitimu (Alumni) waliohitimu kuanzia mwaka 2018 kurudi nyuma hadi mwaka 1965 wakiwa katika hafla hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Kikundi cha sanaa cha One Star wakitumbuiza katika hafla ya kuzinduakatiba ya umoja wa wahitimu wa Chuo cha biashara (CBE), leo jijini Dar es Salaam. 

MAJALIWA AZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA BIASHARA MTWARA .

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua kongamano la Uwekezaji na Biashara Mtwara kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara, Novemba 1, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Uwekezaji na Biashara Mtwara, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Kongamano hilo kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Mtwara, Novemba 1, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


MKURUGENZI MTWARA ACHUKULIWE HATUA-MAJALIWA
* Ni baada ya kumtoza mwekezaji sh. milioni 31 za kuendesha vikao


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtu yoyote anayekwaza wawekezaji nchini atachukuliwa hatua kali, hivyo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwaamchukulie hatua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara, Bw. Maisha Selemani Mtipa baada ya kumtaka mwekezaji alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili ya gharama za vikao ili aweze kupatiwa eneo.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 01, 2019), wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Biashara mkoa wa Mtwara lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara. “Yoyote anayekwaza uwekezaji nchini kwa kuwasumbua wawekezaji tutamshughulikia kabla ya kuwasumbua wawekezaji.”

Amesema Bw. Mtipa amemwandikia barua mwekezaji wa kampuni ya MBR Internation Company Limited akimtaka alipe sh. milioni 31.6 kwa ajili y a kulipa kamati mbalimbali zikiwemo sh. milioni 1.95 kwa kamati ya Menejimenti ya Halmashauri.

Waziri Mkuu amesema “fedha nyingine sh. milioni 2.27 kwa kamati ya kugawa ardhi ya wilaya, sh. milioni 4.43 kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango sh. milioni 5.14 na sh milioni 17.79 Baraza la madiwani ili wagawane tu, huu ni utaratibu wa wapi? huku ni kufukuza na kukwaza wawekezaji.” 

Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaondoa tozo zaidi ya 150 zilizokuwa zinakwaza wawekezaji kupata uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo haitaki kusikia mahali popote panawekwa tozo zenye kuwakwaza wawekezaji. Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa Bw. Mtipa ziwe fundisho kwa halmashauri zote nchini.

Mapema, Waziri Mkuu alizungumzia uuzwaji wa korosho na kuagiza kwamba mfumo uliotumika katika mnada wa kwanza wa uuzwaji wa zao la korosho uliofanyika jana (Alhamisi, Oktoba 31, 2019) ndio unaopaswa kuendelea, hivyo ameagiza wahusika wausimamie vizuri ili usiingie dosari.

Alisema Serikali ilibaini changamoto katika uuzwaji wa mazao mengine ya pamba na kahawa ya uwepo wa watu ambao wananunua mazao nje ya mfumo kama kangomba, hivyo ni muhimu wakadhibitiwa ili fedha zote ziende kwa wakulima. 

Pia Waziri Mkuu aliagiza maandalizi yawe yanakwenda pamoja na msimu kama suala la magunia wasiachiwe watu wa ushirika pekee bali Wakuu wa Mikoa na Wilaya nao washiriki katika kutatua tatizo hilo ili minada ifanyike kikamilifu.

Pia chama kikuu cha ushirika pamoja na vyama vya msingi wazuie kuwepo kwa makato ya hovyo ambayo yalishaondolewa na Serikali ili kuhakikisha mkulima haumizwi kwa kupunguzwa kwa malipo yake. 

Amewataka viongozi hao wasimamie mtiririko wa fedha kutoka kwa wafanyabiashara kwenda kwa mkulima na wahakikishe zinaingizwa katika akaunti za wakulima. Pia sheria ya ununuzi isimamiwe baada ya mnunuzi kupewa zabuni anatakiwa alipe ndani ya siku nne. “Sheria hii itaondoa watu wa kati na kumwezesha mkulima kulipwa fedha zake kwa wakati.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa amesema amesema wanunuzi wote wametakiwa wahakikishe wakulima wanalipwa kwa wakati. “Bei ya chini katika mnada wa korosho uliofanyika Mtwara ilikuwa sh. 2,409 na bei ya juu ilikuwa 2,559 na hali inaonesha uhitaji wa korosho duniani ni mkubwa kutokana na ubora wake.”

Amesema chama cha ushirika cha TANECU waliingiza sokoni tani 13,000 huku mahitaji yakiwa ni tani 40,000 na chama cha ushirika cha MAMCU walipelela sokoni tani 7,000 na mahitaji yalikuwa tani 22,000 hivyo wafanyabiashara wengi jana walikosa korosho.

Akizungumziakuhusu kilimo cha zao la korosho, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara kuwa wasibweteke kwani mikoa mingine nayo imeanza kulima korosho, hivyo waweke mikakati mizuri ili zao la korosho liendelee kuwa zao kuu la biashara kwa mkoa.

Amesema Serikali kwa upande wake, itaendelea kuweka mazingira rafiki na miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza mkoani Mtwara.
  
“Tusisahau kuwaMkoa wa Mtwara ni korosho na korosho ndiyo mkoa. Hili linadhihirishwa na usemi wa wenyeji kuwa korosho ni dhahabu ya kijani. Mtwara ndiyo mzalishaji mkubwa wa korosho Tanzania, huzalisha zaidi ya asilimia 65 ya korosho zote nchini.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaasa wawekezaji wote kwamba waondoe hofu kuhusu kuwekeza Mtwara kwa sababu mkoa wa Mtwara wa sasa ni tofauti na Mtwara ile waliyokuwa wanaisikia zamani, uchumi wake unakuwa.

Waziri Mkuu amesema ushiriki wao kwenye kongamano hilo unaonesha utayari walionao katika kuiunga mkono Serikali kwa lengo la kuwaletea maendeleo na kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda ambayo wote wanaitamani.

Kongamano hili na mengine yaliyofanyika kwenye mikoa mbalimbali ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu alilolitoa wakati anafungua Kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi jijini Dodoma Juni 18, 2018, ambapo aliagiza mikoa yote kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa.

“Niendelee kusisitiza tena kwa mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo hili la kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji ifanye hivyo mapema.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema licha ya Serikali kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye miradi ya kijamii katika Mkoa wa Mtwara, pia imewekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inachochea kukua kwa uchumi kwa haraka. 

Waziri Mkuu ameitaja miradi hiyo ni pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege na bandari ya Mtwara; ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Nanyumbu mpakani na Msumbiji; ufufuaji na ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho.

Miradi mingine ni ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi Songea kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe kutoka Mchuchuma na chuma kutoka Liganga na kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia na vyanzo vingine.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki, Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa,Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na watendaji wengine wa Serikali.

JAJI MKUU: MSIKUBALI KUINGILIWA KATIKA MAMLAKA ZENU

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwaapisha Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Mwanzo wapya leo Novemba Mosi, mwaka huu katika ukumbi namba mbili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi na kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe Beatrice Mutungi.

Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Mwanzo wapya wakila kiapo cha kuitumia kazi yao leo Novemba Mosi, mwaka huu, katika ukumbi namba mbili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na Magreth Kinabo- Mahakama

……………..

Na Mary Gwera, Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewaasa Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Mwanzo wapya kutokubali maelekezo ya aina yoyote kutoka nje ya Mamlaka zao kuhusiana na mashauri yaliyopo mbele yao.

Akizungumza na Mahakimu Wakazi hao ,wapya 23 mara baada ya kuwaapisha rasmi, mapema Novemba 01, 2019 katika Ukumbi wa Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakimu hao wana mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri bila kuingiliwa na yeyote.

“Jaji au Hakimu lazima awe ni mtu wa kuheshimu mamlaka nyingine, vivyo hivyo msikubali maelekezo ya aina yoyote kutoka nje ya Mahakama ama iwe Jaji au mtu mwingine kuhusiana na kesi/mashauri yaliyopo mbele yenu,” alieleza Mhe. Jaji Prof. Juma.

Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kwa kuwataka Mahakimu hao kutekeleza majukumu yao bila upendeleo kwa kuwa ni jambo linalosababisha matabaka baina ya watu/wananchi.

“Upendeleo ni jambo la hatari sana, muwe wawazi, muwe wasikilizaji makini, lazima muwasaidie wananchi ambao wengi hawajui sheria kwa kuwaelimisha,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.

Hali kadhalika, Mhe. Jaji Mkuu aliwapa angalizo Mahakimu hao juu ya uandishi wa hukumu sahihi kwa kutumia lugha inayoeleweka ili wananchi/wateja waweze kuelewa kwa urahisi.Masuala mengine aliyowaeleza Mahakimu hao ni pamoja na kufanya tafiti, matumizi ya TEHAMA na kuishi viapo vyao wanapotekeleza majukumu yao. 

Jumla ya Mahakimu Wakazi wapya 23 wameapishwa na wamepangiwa kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo katika mikoa mbalimbali nchini

MAKAMU WA RAIS SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA KUAPISHWA RAIS MPYA WA BOTSWANA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Edgar Lungu wa Zambia kwenye Hafla ya kuapishwa Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi iliyofanyika leo Novemba 01, 2019 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Edgar Lungu wa Zambia na Rais Emmason Mnangagwa wa Zimbabwe wakishuhudia wakati Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi alipokuwa akila kiapo kuiongoza Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana

Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi akihutubia Viongozi wa Nchi mbalimbali na Wananchi wa Botswana Baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NAMPATIA MKANDARASI MILION 279 ILI AMALIZE MRADI WA MAJI JIBONDO -NAIBU WAZIRI AWESO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Wananchi wa Kijiji cha Jibondo Wilaya ya Mafia wamehakikishiwa kupata maji safi na salama ndani ya muda mfupi baada ya kukamilika kwa ulazaji wa mabomba chini ya bahari yatakayopeleka maji kwenye Kijiji hicho wenye thamani ya Bilion 1.9

Mradi huo wa maji unaopeleka maji Jibondo uliibuliwa na wananchi mwaka 2004 na kuwekwa katika mpango wa vijiji 10 chini ya Programu ya maendeleo ya sekta ya maji.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jibondo, Aweso amesema mradi huu umetakiwa umalizike mwishoni mwa mwaka huu ila mkandarasi ameshindwa kuendelea na kazi kutokana na madai ya malipo.

Aweso amesema, mkandarasi ameleta maombi ya milion 279 ambaoo ameahidi atakapokabidhiwa fedha hizo atafikisha maji katika Kijiji cha Jibondo.

"Ni mara tatu nafika Mafia ila mara ya pili nafika hapa Kijiji cha Jibondo na nilipokuja mara ya kwanza niliwaahidi mtapata maji na mradi ndio huo ambapo umebakia hatua ndogo ya kulaza mabomba,"amesema Aweso.

" Mkandarasi amesema, akipewa Milion 279 anamaliza mradi huu na wananchi wanaanza kupata maji safi na salama, na mimi namwambia nampatia hiyo hela kesho atapatiwa Milion 100 (mia moja) na Jumatatu aje na Mkurugenzi wake tujue tunafanyaje kumpatia fedha zingine zilizobaki,"

Aweso ameeleza kuwa, lengo la awamu ya tano inayoongozwa na serikali ya Mapinduzi chini ya  Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kumtua mama ndoo kichwani, na hilo litakamilika hivi karibuni baada ya mradi wa maji kufika katika Kijiji cha Jibondo.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini RUWASA Mhandisi Ndolimana Kijiga amesema mradi huu umejengwa na mkandarasi Elegence Developers chini ya usimamizi wa ofisi yao pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya.

Amesema, kumekuwa na changamoto za utekelezaji wa mradi huu ambapo ni pamoja na fedha kutokupatikana kwa wakati.

"Mradi huo umetekelezwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ilifanyika kati ya mwaka 2015 na 2016 na kazi iliyofanyika ni kufanya utafiti wa maji ardhinina kuchimba kisima kina cha mita 40 kwenda chini ambacho uwezo wake ni kutoa maji lita 10,000 kwa saa na pili ni kufanya usanifu wa mradi na nwisho ni ujenzi wa mradi wenyewe ulioanza kutekelezwa machi 16 2018," amesema Kijiga.

Amesema, lengo la mradi huo ni kuhakikisha wananchi wa Kijiji cha Jibondo zaidi ya 1809 wanapata majj safi na salama yenye kutosheleza na kuzuia magonjwa yanayisababishwa na ukosefu wa maji safi na salama ikiwemo na kuwapunguzia adha ya kufuata maji zaidi ya mita 400 na gharama kubwa.

"Tayari tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 75,000 kwa siku lipo katika hatua za mwisho (asilimia 90), tumeshajenga Vizimba vya kuchotea maji zaidi kilichobaki ni ulazaji wa mabomba tu,

Wananchi wa Kijiji cha Jibondo wameonesha furaha kubwa baada ya Kuhakikishiwa kupata maji safi na salama wakiwa na  adha ya muda mrefu na kuishia kununua maji kwa bei kubwa kutoka Kisiwa Kikubwa.

Naibu Waziri Aweso ameendelea na ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wanapata maji safi na salama.

Aweso aliongozana na wataalamu mbalimbali wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wanakijiji wa Jibondo katika mkutano na kuwaahidi kufanikisha kukamilika kwa mradi wa maji kwa kumlipa mkandarasi kiasi cha Shiling Milion 279 ili akamilishe mradi huo uliofikia hatua ya ulazaji wa mabomba chini ya bahari.
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipokea taarifa ya mradi wa Maji kutoka kwa Kaimu Meneja Mamlaka ya Maji Vijijini RUWASA  Wilaya ya Mafia, mradi huo una thamani Bilion 1.9 utakaoondoa kero ya maji kwa wakazi 1,809.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya kizimba kitakachotumika kuchotea maji kwa wananchi wa Jibondo pindi utakapokamilika. 
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na moja ya watendaji wa Wizara ya maji kwa njia ya simu akitoa maombi ya kupatiwa kiasi cha Shiling Milion 279 ili mkandarasi wa mradi wa maji wa Jibondo apatiwe na kukamilisha kwa haraka zaidi wananchi waanze kupata maji safi na salama
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wahandisi, watendaji wengine baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Jibondo alipotembelea kukagua mradi wa maji ulipofikia
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa katika ziara ya kukagua mradi wa maji wa Jibondo akiongozana na watalaamu mbalimbali.
 
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita 75,000 kwa siku alipotembelea mradi wa maji  wa Kijiji cha Jibondo wenye thamani ya Bilion 1.9 unaotarajia kumaliza hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisalimiana na wanakijiji wa Jibondo baada ya kutembelea kijiji hicho na kukagua mradi wa maji.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akimpa zawadi moja ya wakina mama wa Kijiji cha Jibondo baada ya kuwatembelea na kuangalia mradi wa maji ulipofikia.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa katika picha ya pamoja na Wanakijiji wa Jibondo wakifurahia ujio wake.

VOA SWAHILI: Duniani Leo November 1, 2019

WAZIRI MPINA AZINDUA VITUO VYA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MIFUGO SUMBAWANGA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akizindua kwa pamoja vituo viwili vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC) na Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Kanda ya Magharibi- Sumbawanga . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara Tanzania (TVLA), Dk. Furaha Mramba na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Maghembe Makoye 


NA MWANDISHI WETU, RUKWA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua kwa pamoja vituo viwili vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC) na Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Kanda ya Magharibi- Sumbawanga na kutangaza msimamo wa Serikali ya awamu ya tano wa kupambana na magonjwa ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake nchini.

Hivyo Serikali inawahakikishia wananchi uhakika wa upatikanaji wa chanjo kwa bei nafuu kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Chanjo (TVI) kuzalisha chanjo za kimkakati 11 ifikapo Juni mwakani na kwamba Serikali iko mbioni kutangaza bei elekezi ya Chanjo ili kuwadhibiti watu wachache waliokuwa wanawaibia wananchi.

Aliongeza kuwa hivi sasa kuna ujenzi mkubwa wa Kiwanda kipya cha kuzalisha chanjo cha Hester Bioscience Africa Limited (HBAL) ambacho kitazalisha chanjo 27 ifikapo Juni na uwekezaji wake una thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 50 na kuwezesha upatikanaji wa chanjo zote kwa wafugaji wa ndani ya nchi, Afrika na Dunia.

Akizungumza mara baada ya kuzindua vituo hivyo vitakachohudumia mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi vyenye makao yake mjini Sumbawanga, Waziri Mpina amesema kamwe Serikali haiwezi kukubali mifugo iendelee kufa kwa magonjwa na kwamba sasa magonjwa hayo hayana nafasi tena nchini.

Hivyo Serikali imeamua kuandaa Kanuni mpya za usimamizi wa uogeshaji na uchanjaji mifugo ili kudhibiti utoaji wa chanjo kwa wananchi na kwamba itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote wataokwenda kinyume na kanuni hizo.

Hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashirikiana kwa karibu na vituo vya uchunguzi wa magonjwa na wakala wa maabara ya magonjwa ya mifugo vilivyoko katika kanda zao ili kutoa huduma bora kwa wafugaji na kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake.

Waziri Mpina pia amemuagiza Katibu Mkuu Mifugo na Katibu Mkuu Tamisemi kufanya mgawanyo mpya wa maafisa mifugo ili kuweza kupelekwa kwenye maeneo ambayo hayana kabisa maafisa mifugo ukiwemo Mkoa wa Katavi ambao hauna kabisa Madaktari wa Mifugo.

Pia ameagiza ZVC na TVLA Kanda ya Magharibi Sumbawanga kuwa wasimamizi na walezi wazuri wa wafugaji na mifugo na kuhakikisha kuwa chanjo, uogeshaji na haki za mifugo zinasimamiwa kikamilifu.

Waziri Mpina pia ameiagiza Kanda kusimamia kikamilifu uingizaji wa chanjo, madawa, viuatilifu, chakula na mazao ya mifugo yanayoingizwa nchini bila vibali, bila kulipiwa ushuru, bila kukaguliwa na yaliyokwisha muda wa matumizi na feki.

Kufuatia mageuzi ya utoaji huduma za mifugo nchini, Waziri Mpina amemwagiza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kufanya ukaguzi wa maafisa wa kanda zote ili kupanga safu mpya itakayokuwa tayari kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

Waziri Mpina ameonya kuwa siku nyingine ikitokea hatua zikachelewa kuchukuliwa kwa maafisa wanaohujumu mifugo basi Mkurugenzi wa huduma za mifugo ataondolewa kwenye wadhifa wake.

Waziri Mpina alisema wafugaji walikuwa wakipata huduma za uchunguzi wa magonjwa kilichopo Iringa umbali wa zaidi ya kilomita 900 kutoka Sumbawanga hali ilisababisha ugumu kwa wafugaji na kusababisha vifo vingi vya mifugo

Hivyo Waziri Mpina amebanisha kuwa uanzishaji wa kanda hiyo utaongeza ufanisi wa kazi ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo katika mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi na kuleta ahueni kubwa kwa wafugaji.

Mpina aliongeza kuwa hadi sasa kuna Kanda 8 za Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo na Kanda 11 za Wakala wa Maabara Tanzania (TVLA) ambapo wizara inakusudia kuanzisha kanda nyingine moja katika mwaka fedha wa 2019/ 2020 itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kituo hicho kikikamilika kitasogeza huduma ya udhibiti wa magonjwa katika mikoa hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dk Hezron Nonga amesema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho kumewezesha kuongezeka kwa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo na mazao yake, shughuli za uchunguzi kimaabara zimesogezwa karibu na wananchi.

Pia upatikanaji wa chanjo kwa wafugaji kwa bei nafuu umekuwa rahisi, kuongezeka kwa upatikanaji wa taarifa za magonjwa , kuongezeka kwa majosho hamasa ya wafugaji kuongeza mifugo na idadi ya lita za kuogesha mifugo.

Pia ongezeko la maduhuli ya Serikali yatokanayo na usafirishaji wa mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi kutoka makadirio ya sh milioni 120 kwa mikoa miwili Rukwa na Katavi hapo awali na kufikia makadirio ya sh milioni 500 kwa mwaka, kufanikiwa kudhibiti ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Dk Nonga amesema pia kumeongezeka mahusiano kati ya wizara na Serikali za mitaa na hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za mifugo kwa wananchi tofauti na ilivyokuwa awali.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 2,2019

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images