Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 318 | 319 | (Page 320) | 321 | 322 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akiongea kwenye kisomo cha mpendwa wetu Zainab Buzohera kulichofanyika jana Jumanne Jan 7, 2013 katika ukumbi wa mirage uliopo Langeley Park, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania wa DMV na majimbo mengine kama New York, New Jersey, Massachusetts, Georgia, Ohio, Pennsylvania na kwingineko. Mwili utaondoka leo Jumatano Jan 8, 2014 na kufika Ijumaa Dar ses Salaam, Tanzania siku ya Ijumaa na utaambatana na dada ya marehemu Jasmine Bernett na Mume wa marehemu Dullah wakiwemo Watanzania kadhaa hapa Maryland na majimbo mengine.
  Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Colonel Adolph Mutta akiongea kwa niaba ya Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula ambaye yupo Tanzania.
  Wafiwa mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera (wapili toka kushoto baibui nyeusi) na Dada wa narehemu Jasmine Bernett (watatu toka kushoto) wakifuatilia kisomo cha mpendwa wao kilichofanyika jana Jumanne Jan 7, 2014 Langeley Park Maryland.
  Juu na chini ni Jopo la Watanzania wakiwemo maafisa Ubalozi wakiongoza kisomo cha kumuombea mpendwa wao kilichofanyika jana Jumanne jan 7, 2014 Langley Park, Maryland.
  Umati wa Watanzania wa DMV na majimbo mengine waliohudhuria kisomo cha mpendwa wetu Zainab Buzohera kilichofanyika Jumanne Jan 7, 2014 Langeley Park, Maryland katika ukumbi wa Mirage.

  0 0

  Hon. Dr. Mahadhi Juma Maalim, Deputy Minister for Foreign Affairs and International Co-operation greets Ms. Virginia Blaser, Chargé d'Affaires of the Embassy of the United States of America to the United Republic of Tanzania.  Ms. Blaser had paid a courtesy visit in his office today to discuss areas of cooperation between the two countries. 
  Also in attendance during the meeting were Mr. Adam Issara (2nd right), Private Assistant to the Deputy Minister and Ms. Elizabeth Rwitunga, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs. 
  During their discussion, Ms. Blaser also expressed her Government sadness for the passing of the Finance Minister Dr. William Mgimwa, while sending condolences to the Widow and Family of the Late Mgimwa.All photos by Tagie Daisy Mwakawago 

  0 0

  FRANCIS DASTAN BENDERA
  Ndugu Allan Dastan Bendera mwana Diaspora wa Italy na mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Italy anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake pichani Francis Dastan Bendera, kilichotokea jana tarehe 6/01/2014 katika hospitali ya Muhimbili Dar Es Salaam Tanzania.

  Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili baada ya kupata ajali ya bus la BURUDANI lililokuwa likitokea Korogwe kwenda Dar Es Salaam .

  Ajali hiyo ilitokea  Disemba 12 mwaka huu majira ya saa 1.30 asubuhi  katika Barabara Kuu ya Segera Chalinze  eneo la Kwaluguru Kata ya Kwedizinga  wilayani ya Handeni.

  Mazishi yatafanyika kesho tarehe 08/01/2014 nyumbani kwao Korogwe.
  Basi la Burudani alilopata nalo ajali marehemu Francis Dastan Bendera

  0 0

  DSC05524

  Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika halmshauri ya manispaa ya Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
  DSC05509
  Meneja msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Singida, Isaya Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salumu Mahami.
  DSC05559
  Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akitoa mada yake iliyohusu mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya Singida.


  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,alipohudhuria katika Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel jana,ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi Ya zanzibar (katikati) Bibi Nasra Mohamed Halal Mwenyekiti wa Taasisi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na kumpongeza Dk.Amina Ameir,baada ya kutoa Historia ya Harakati za wanawake katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(akiyesimama) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuizindua taasisi hiyo katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi na wananchi wakati alipozindua Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Shati la Kitenge) akifanya ukaguzi wa ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea jana Januari 07, 2014 Mjini Dodoma. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limepewa jukumu la kukarabati jengo hilo na kukamilisha kazi hiyo mapema mwezi Februari, 2014 kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza.

  Msimamizi wa mradi wa ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Injinia. Salum Omary(kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Shati la Kitenge) hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ukarabati wa Jengo hilo unaoendelea(kulia shati la drafti) ni Kamishna wa Magereza, Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Injinia. Deonice Chamulesile ambaye ameongozana na Kamishna Jenerali Minja katika ukaguzi huo.
  Muonekano wa juu wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hivi sasa linafanyiwa ukarabati na Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Magereza kilicho chini ya Shirika la Magereza. Ukarabati wa jengo hilo kama linavyoonekana katika picha unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Februari 07, 2014 kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza.
  Baadhi ya Wafungwa wa Gereza Kuu Isanga, Dodoma wakisaidiana na mafundi kutoa nguvu kazi ya kusogeza vifaa vya ujenzi kama wanavyoonekana katika picha. Shughuli za ujenzi ni moja ya programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa wakati wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao magerezani hivyo kuwapatia ujuzi mbalimbali pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia wanapokuwa wamerejea katika jamii zao( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi , Askari na watumishi raia wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya Jeshi la Polisi (hawapo pichani) katika kikao chake cha kwanza na watendaji hao baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.Kikao hicho kilifanyika jana katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Ostarbay jijini Dar es Salaam.(Kushoto) ni Naibu IGP Abdulrahman Kaniki na (kulia) ni Kamishna wa fedha na Usafirishaji wa watu na vifaa Clodwing Mtweve.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi , Askari na watumishi raia wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya Jeshi la Polisi (hawapo pichani) katika kikao chake cha kwanza na watendaji hao baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.Kikao hicho kilifanyika jana katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Ostarbay jijini Dar es Salaam.(Kushoto) ni Naibu IGP Abdulrahman Kaniki, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja na Kamishna wa Kanda Maalumu Suleman Kova (kulia) ni Kamishna wa fedha na Usafirishaji wa watu na vifaa Clodwing Mtweve, DCI Issaya Mngulu na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).

  Na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi.

  Maofisa na Askari Polisi kote nchini wametakiwa kuendelea kufanya  kazi kwa kufuata misingi na maadili ya kazi za Polisi ili kuweza kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii jambo ambalo litafanya mapambano ya uhalifu na wahalifu kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini.

  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa akizungumza na Maofisa, Wakaguzi, Askari na Watumishi raia ndani ya jeshi la Polisi kutoka Makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya Polisi,  kikao ambacho ni cha kwanza kuzungumza na Askari tangu ateuliwe na Mh.Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.

  Alisema kazi za Polisi zinafanywa kwa kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa hivyo kila Askari akifuata misingi hiyo na ushirikiano wa pamoja ukiimarishwa mapambano dhidi ya uhalifu yatafanikiwa.

   “Wananchi wanaimani kubwa na sisi hivyo ili tuweze kuboresha uhusiano na ushirikiano uliopo kati yetu na jamii hatuna budi kutoa huduma bora bila upendeleo” Alisema IGP Mangu.

  Kwa Upande wake Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki alisema muundo mpya wa utawala ndani ya Jeshi la Polisi wa kuwa na Kamisheni mpya lengo lake ni kuboresha utendaji wa kazi za Polisi hivyo Watendaji wa Jeshi la Polisi hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Alisema lengo la Muundo huo ni muendelezo wa utekelezaji wa Maboresho ya Jeshi la Polisi yanayoendelea kutekelezwa ambayo yanahitaji kufanya kazi kwa weledi, usasa na Polisi Jamii ambapo katika kipindi cha utawala wao wataendelea kuyatekeleza.


  Naye Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa alisema atahakikisha elimu ya Polisi jamii inawafikia Wananchi wote kwa kasi kubwa ili kuendelea kuboresha uhusiano uliopo kati ya Wananchi na Jeshi la Polisi ambapo atahakikisha Askari Kata na Wakaguzi wa Tarafa wanafanya kazi kwa ukaribu na wananchi ili kutokomeza uhalifu kuanzia ngazi ya familia.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali nchini. Kulia ni Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei.
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es salaam.

   Imeelezwa kuwa Tanzania inapiga hatua nzuri katika maendeleo ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana  na  kupungua kwa mfumuko wa bei  wa taifa  hali inayoleta unafuu wa maisha kwa mlaji.

  Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka 2013 kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Desemba umepungua hadi kufikia asilimia 7.9 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 16.0  iliyofikiwa mwaka katika mwaka 2012.


  0 0

  Mwanafunzi wa Shule ya Msingi katika moja ya Shule za Msingi zilizopo kwenye kijiji cha Ipunga,Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya,akionekana kuvuka daraja la mto unaokatika kwenye Kijiji hicho ambalo limekatika Upande mmoja.hali inayopelekea kuhatarisha usalama wake na usalama wawakazi wa eneo hilo kwa Ujumla.Picha na Mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog.

  0 0


  0 0

  JANUARI 2, mwaka huu Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutojadili uanachama wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe Zitto Kabwe katika kikao cha chake cha Januari 3, mwaka huu. 
  Januari 3, mwaka huu mahakama hiyo ilisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo mbele ya Jaji John Utamwa. 
  Januari 7, mwaka 2014, mahakama hiyo pia ilitoa amri kwamba Zitto asijadiliwe uana chama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. 
  Mhe Zitto alikuwa anatetewa na wakili Mhe Albert Msando na Chadema walikuwa wanawakilishwa na Mhe Tundu Lisu na Mhe Peter Kibatala. 
   Katika kesi ya msingi, Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo. 
   Katika maombi yake, Zitto anaiomba mahakama kuiamuru kamati kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama. 
   Kadhalika, anaoimba mahakama imwamuru, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa kumkabidhi nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho. 
  Mhe. Zitto kupitia wakili wake Msando aliomba mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. 
   Akiwasilisha hoja zake wakili Msando aliomba zuio hilo litolewe hadi Zitto atakapopata nafasi ya kuwasilisha rufaa yake ya kupinga uamuzi wa kumvua uongozi katika chama, uliotolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 12 mwaka 2013. 
   Wakili Huyo alidai endapo amri hiyo haitatolewa na Kamati Kuu ikamvua uanachama, Zitto atapata athari kubwa kuliko chama chenyewe kwa kuwa atapoteza nafasi yake ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua. 
   Pia, mwanasheria huyo alidai athari nyingine ni kwamba iwapo atafukuzwa uanachama, Zitto atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). 
   Alisisitiza kuwa, Zitto haizuii Chadema kufanyakazi zake za kisiasa kama wao wanavyodai katika hati ya kiapo kinzani, bali anaomba Kamati Kuu isijadili suala lake la uanachama mpaka uamuzi utakapotolewa. 
   Akijibu hoja hizo Wakili wa Chadema, Mhe Lissu alidai kuwa katika kutoa zuio la muda mahakama inatakiwa iangalie maslahi ya walio wengi na si faida ya watu wachache. 
   Alidai katika hati ya kiapo, Mhe Zitto anadai hakuna tarehe ya kikao cha Baraza Kuu la chama kilichopangwa, pia asipokata rufaa hatotendewa haki na atapata madhara lakini dawa ya woga na hofu yake ni kuomba mahakama iamuru kikao cha Baraza Kuu kifanyike na siyo kuomba zuio. 
  Mhe Lissu alidai kuvuliwa uanachama kwa Zitto hakutakuwa na athari kubwa kama anavyodai, na kwamba athari atayoipata yeye ni kukosa posho na mishahara.
  Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya sheria, kanuni, amri na uamuzi wa kesi mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na za nje, Jaji Utamwa alisema anakubaliana mtoa maombi.
  “Kwa hiyo ninatoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chadema na au chombo chake chochote cha uamuzi kwamba kisimjadili na kutoa uamuzi wowote dhidi ya mleta maombi kuhusiana na uanachama wake kusubiri kusikilizwa na kuamuriwa kwa kesi yake ya msingi,” alisema Jaji Utamwa.
  Kesi ya msingi inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.

  0 0
 • 01/08/14--13:03: HAPPY BIRTHDAY MY SON PREZZO
 • 09th JANUARY 2014   ……. Happy Birthday my SON.  
  No matter how old you are, to me you will always be my little and special SON! You are the best SON in the whole wide world! I love and adore you very much, you are my reason to live and I pray to God to grant every mother in this world a SON as loving, caring, charming, and above all special as you and I believe the world would be a better place for all.

  May you be blessed with all the good things you deserve; you have always by my side and made me STRONG and PROUD.

  I wish you to love life and never stop dreaming big! May beauty and happiness surround you today and always!
  Happy Birthday NGECHU,

  From Malaika Mama.

  0 0

  Na Abdulaziz Lindi

  Shule Nne za kata kati ya shule 115 za sekondari zilizopo mkoani Lindi zimekosa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo.

  Hayo yameelezwa na Afisa elimu wa mkoa wa Lindi Silas Samaluku wakati alipokuwa anatoa taarifa ya maendeleo kwa wajumbe wa kikao cha wadau wa elimu Mkoani Lindi.

  Samaluku alisema kuwa Mkoa wa lindi una jumla ya shule za sekondari 115 na wanategemea wanafunzi wote waliofaulu watajiunga katika na shule hizo lakini shule nne za sekondari kati ya hizo Namapwia na Kilimarondo za wilayani Nachingwea ,Madangwa wilayani Lindi na Nandanga wilayani Kilwa zitakuwa hazina wanafunzi wa kuanza kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo

  Alieleza kuwa wanafunzi 17,249 walisajiliwa kuhitimu elimu ya msingi kati ya hao wavulana ni 7,981 na wasichana 9,448 lakini kati yao waliofanya mtihani ni 16,682 na wasichana 9,150 sawa na asilimia 95.71.

  Wanafunzi waliofaulu na kupata alama 100 hadi 250 walikuwa 6,857 kati ya hao wavulana 3,644 na wasichana 3,213 sawa na asilimia 41.1 ambayo imepanda ukilinganishwa na mwaka 2012 ambapo ilikuwa asilimia 22.60 .

  Aidha Samaluku alibainisha kuwa kipindi cha miaka miwili mfululizo wanafunzi wa wilaya ya liwale wanaongoza kwa kufanya vizuri mitihani ya darasa la saba kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.

  " mwaka 2013 Liwale imeongoza kwa kufaulisha kwa asilimia 53.37 ikifuatiwa na wilaya ya Nachingea kwa asilimia 50.05 ,Lindi manispaa kwa asilimia 42.42 wilaya ya Ruangwa kwa asilimia 42.34 ,Kilwa asilimia 33.74 ,wakati huo Lindi vijijini ikiendelea kushika mkia kwa muda wa miaka miwili mfululizokwa kuwa ya mwisho kupata asilimia 31.45

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya sukari Tanzania, Bw. Henry Semwaza (kushoto) wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau wa sukari nchini uliofanyika jana Mkoani Morogoro. Wengine ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha TPC Moshi, Bw. Robert Baissac.
  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza (katikati) muda mfupi mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa sukari uliofanyika jana mkoani Morogoro. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha TPC Moshi, Bw. Robert Baissac.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya kina juu ya umuhimu wa taarifa za hali ya hewa katika banda la TMA kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Meneja Kituo cha Zanzibar Bw. Said Khamis akimwelezea mwananchi njia mbalimbali za ukusanyaji wa takwimu za hali ya hewa kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Ofisa Uhusiano wa TMA Bi.Monica Mutoni akitoa elimu kwa umma jinsi ya kupata taarifa za hali ya hewa kupitia njia mbalimbali za usambazaji wa taarifa hizo kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Mkurugenzi wa ofisi ya Zanzibar, Bw Mohamed Ngwali akitoa maelezo ya takwimu za hali mbaya ya hewa iliyowahi kutokea kwa kipindi cha miaka 50 katika visiwa vya Unguja na Pemba, akisisitiza wananchi kutopuuza tahadhari zitolewazo.

  0 0

   Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Alhamisi   Januari 09, 2014 saa 3 usiku kwenda bara  imeahirishwa  hadi kesho siku ya  Ijumaa   Januari 10, 2014, saa 10 jioni.
  Taarifa imefafanua kuwa dharura hiyo imetokana na eneo la reli kati ya  stesheni za Godegode na Gulwe  mkoani Dodoma kukumbwa na mafuriko usiku wa kuamkia leo.


  Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio tokea jana  usiku na taarifa za uhakika zinaeleza kuwa  zoezi la kukarabati litakamilika saa 10 leo jioni ( Alhamis Januari 09, 2014).


  Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..


  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.

  TRL Makao Makuu,

  Dar es Salaam.

  Januari 09, 2014


  0 0
 • 01/09/14--03:04: bei ya madafu leo


 • 0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu  na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi  (DIGP) Abdulrahman Kaniki (kulia)  akizungumza  na waandishi wa habari  Makao Makuu ya Jeshi la Polisi . IGP Mangu aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kukabiliana na uhalifu na wahalifu.  Picha na Hassani Mndeme -Jeshi la Polisi


  0 0


  UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Uamuzi huo ulifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA  kilichofanyika Dar es Salaam jana kujadili masuala mbalimbali ya chama na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.

  Kikao kilikubaliana kuwa uchaguzi ufanyike kwa katiba ya zamani, kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua muda mrefu, hivyo kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia viti kinyume cha katiba, jambo ambalo si sahihi.

  Kutokana na hali hiyo viongozi wapya watakaochaguliwa moja ya kazi yao kubwa itakuwa kuifanyia marekebisho makubwa katiba ya chama chetu ili iende na wakati.

  Kikao kimekubaliana kuwa wanachama wote walipie ada zao zote wanazodaiwa kuanzia mwaka 2011, hadi mwaka 2013, na mwisho wa kufanya hivyo ni Januari 31 mwaka huu na yule atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo atapoteza haki ya kupiga kura na atahesabika si mwanachama hai.

  Malipo yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na hakuna mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu.

  Pia Kamati ya Utendaji imeunda Kamati ya Uchaguzi na kumteua Mwenyekiti wa zamani wa TASWA, ambaye kwa sasa ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uchaguzi Mkuu wa TASWA, ambapo pia kutakuwa na wajumbe wengine wanne

  Wajumbe hao ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Mwina Kaduguda, aliyepata kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Peter Mwenda na wanahabari Isakwisa Mwaifuge na Mbonile Burton ambao wote ni wanachama wa TASWA.

  Pia Kamati ya Utendaji imekubaliana tuombe wawakilishi wawili wawe waangalizi wa uchaguzi huo kuhakikisha haki sio tu inatendeka bali pia ionekane inatendeka, ambapo mmoja atatoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na mwingine Idara ya Habari (MAELEZO), utaratibu wa kuwasiliana na taasisi hizo mbili unaendelea.

  Fomu za kuwania uongozi zitaanza kutolewa Februari 10 hadi Februari 14 mwaka huu saa kumi alasiri, masuala mengine yahusiyo uchaguzi huo, ikiwemo mahali utakapofanyika yatatangazwa baada ya kikao cha sekretarieti ya TASWA na Kamati ya Uchaguzi kitakachofanyika Februari 3.

  Si dhambi wanaotaka kuongoza kutangaza nia zao mapema wakiona inafaa.
  Nawasilisha.
  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  09/01/2014.

older | 1 | .... | 318 | 319 | (Page 320) | 321 | 322 | .... | 3285 | newer