Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live

DC. JOKATE AWAPONGEZA DAWASA KWA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI KISARAWE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa  mradi mkubwa wa maji wa Kisarawe unaojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Mradi huo ulioanza kujengwa Julai 2018 ulizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu baada ya agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kuitaka Dawasa kupeleka maji Kisarawe wakitumia mtambo wa Ruvu Juu.

Jokate amekagua mradi huo ambao umekamilika na upo katika hatua za majaribio na usawazishaji wa mandhari. 

Aidha, baada ya kujionea hatua ya mradi ilipofikia Jokate amewapongeza Dawasa kwa jitihada walizozifanya na ndani ya mwaka mmoja mradi huo kukamilika.

Wananchi wa Kisarawe wako mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 20,000 mwishoni mwa mwezi huu.


Mradi huo wenye thamani ya Bilion 10.6 ukijengwa na fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) umeanza kufanyiwa majaribio Oktoba 20 ikiwa ni kwa ajili ya kusafisha tanki la maji na mabomba.

Dawasa wametumia kipindi cha mwaka mmoja kukamilisha kwa mradi huo wakifuata maagizo ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kupeleka maji Kisarawe wakitumia Mtambo wa Ruvu Juu.


SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA PILI KATIKA JESHI LA MAGEREZA ZAFANA MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akikagua Paredi Maalum lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza lililofanyika Oktoba 25, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akiwa katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
 Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza  wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika Sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike(kushoto) akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi minne.
 Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza wakiwa tayari wamevishwa vyeo vipya kama wanavyoonekana katika picha.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP Phaustine Kasike akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza(hawapo pichani).
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
 Mhitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza akisoma risala mbele ya mgeni rasmi. 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wakaguzi Wasaidizi wa Magereza waliosimama mstari wa nyuma(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Kamati ya Bunge yaipongeza PURA kwa kuokoa Tshs Bilioni 10 za PSAs

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA)  kwa kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni 10.08 kutokana na kaguzi za gharama na mapato ya mikataba ya  Mafuta na Gesi Asilia nchini (PSAs).

Pongezi hizo wamezitoa tarehe 25 Oktoba, 2019 wakati wa kikao baina ya Kamati hiyo na Wizara ya Nishati  pamoja na PURA ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliiongoza Wizara ya Nishati katika uwasilishaji wa taarifa hiyo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Menejimenti ya Wizara, PURA na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Charles Sangweni alisema kuwa  kama kaguzi hizo zisingefanyika, wawekezaji wangeweza kujirudishia fedha hizo (cost recovery) kulingana na mkataba hivyo kiasi hicho kilichookolewa kitafanya mapato ya Serikali kuongezeka wakati wa ugawanaji wa faida itokanayo na mauzo ya Gesi Asilia.

“ PURA ilianza kutekeleza jukumu hili kwa kufanya kaguzi za gharama na mapato kuanzia mwaka 2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 10.08 zimeokolewa hadi sasa.” Alisema Sangweni

Sangweni alieleza kuwa Mamlaka hiyo pia imeendelea kufanya kaguzi katika maeneo ya uzalishaji wa Gesi Asilia kwa lengo la kuhakiki usalama wa mazingira na wafanyakazi pamoja na kupata uhalisia wa shughuli zinazotekelezwa katika uzalishaji wa Gesi Asilia nchini.

Alisema kuwa, katika kipindi cha robo mwaka wa 2019/2020, masuala mbalimbali yaliangaliwa na kuhakikiwa na kaguzi hizo zilibaini  kuongezeka kwa uzalishaji wa Gesi Asilia ambapo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2018/19  uzalishaji ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 15.73 na kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2019/20 uzalishaji ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 16.05.

Alisema kuwa, kwa ujumla Gesi iliyogunduliwa nchini hadi sasa ni takriban futi za ujazo Trilioni 57.54 ambapo kati ya kiasi hicho, Gesi iliyogunduliwa nchi kavu (onshore) ni futi za ujazo Trilioni 10.41 na kwa upande wa Bahari Kuu (offshore) ni futi za ujazo Trilioni 47.13.

Aidha alisema kuwa, kaguzi za PURA zilibaini kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi wazawa katika kampuni zinazozalisha Gesi Asilia huku akitolea mfano kampuni ya PanAfrican Energy na Maurel et Prom ambapo idadi ya wafanyakazi wazawa imefikia zaidi ya asilimia 90.

Sangweni pia aliieleza Kamati ya Bunge kuhusu kazi inayofanywa na Mamlaka hiyo katika kusimamia shughuli za utafutaji na uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya kusimamia shughuli ya uchukuaji wa data na uchorongaji katika Kitalu cha Eyasi Wembere  kilicho chini ya TPDC ambapo visima vifupi vitatu vya utafiti wa awali vimeanza kuchorongwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alieleza kuhusu faida mbalimbali za uwepo wa Gesi Asilia nchini ikiwemo kuwa kama chanzo cha kuzalisha umeme nchini kwani zaidi ya asilimia 57 ya umeme unaozalishwa unatokana na Gesi Asilia.

Aidha alieleza kuhusu juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa PURA inatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kuongeza bajeti ya Taasisi hiyo, kukamilisha muundo wa Taasisi hiyo na kuipatia fedha kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mbele kulia) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (mbele kushoto) wakiwa katika kikao na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara mara baada ya kumaliza kikao chao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
 Wataalam kutoka Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi
 Watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Charles Sangweni.

SHIRIKA LA LIFEWATER INTERNATIONAL LAZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Shirika la Lifewater International lenye makao yake makuu nchini Marekani limezindua mradi wa maji mkoani Shinyanga, ambapo katika awamu ya kwanza utatekelezwa katika kata tatu za Mwantini, Mwamala pamoja na Mwalukwa zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Uzinduzi wa mradi huo wa maji umefanyika leo, Oktoba 25, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo,Mboneko  amelipongeza Shirika la Lifewater International, kwa kuanzisha mradi wa maji mkoani Shinyanga ambao utaanza kutekelezwa kwenye kata hizo tatu za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji safi na salama. Amesema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli inasisitiza sana upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi ili wananchi waweze kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama, pamoja na kuugua magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji ambayo siyo salama kiafya, na kubainisha mradi huo upo sehemu sahihi. 

“Tunalishukuru sana Shirika hili la Lifewater International kwa kutuletea mradi huu wa maji mkoani Shinyanga, na kuanza kutekelezwa kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo tunaomba mradi huu pia ufike na kwenye maeneo mengine ambayo yana shida ya maji safi na salama ikiwemo wilaya ya Kishapu,”amesema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Lifewater International Tanzania Devocatus Kamara, amesema mradi huo kwa kuanza utatekelezwa kwenye kata hizo tatu za halmshauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo ni Mwantini, Mwamala na Mwalukwa , na baada ya hapo utapanuka kwenye maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine, ambayo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na usafi wa mazingira. 

Amesema mradi huo utadumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 na utagharimu kiasi cha Shilingi za kitanzania 4,286,070,528, ambao utajenga visima vipya virefu vya maji safi na salama na kuvikarabati vibovu, kujenga na kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora, kuboresha usafi wa mazingira, na utahamasisha na kuhimiza ushiriki wa jamii kikamilifu ili kuhakikisha uendelevu wa mradi.

Kwa upande wake,Meneja wa Shirika  Lifewater International mkoa wa Shinyanga Benety Malima, amesema kuwa katika maeneo  ambapo maji ya ziwa Victoria yamekwishafika, watafanya utaratibu wa kuendelea kuyasambaza katika maeneo yanayokusudiwa.Pia amesema maeneo ambayo yatapitiwa na mradi huo wa maji, ni sehemu za shule, zahanati, pamoja na kwenye makazi ya watu, ambapo mradi huo umelenga kufikia watu 100,000.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizindua mradi wa maji wa Shirika la Lifewater ambao utatekelezwa mkoani Shinyanga na kuanza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika Kata tatu za Mwantini, Mwamala na Mwalukwa, ambao utadumu ndani ya miaka mitatu (2020-2024). Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mkurugenzi wa Shirika  la Lifewater International Tanzania Devocatus Kamara, akielezea namna mradi huo wa maji utakavyofanya kazi Mkoani Shinyanga. Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akiwataka watumishi wa Serikali kutoa ushirikiano kwenye utekelezaji wa mradi huo wa maji.Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Uzinduzi ukiendelea.Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Kushoto ni Meneja wa Lifewater International mkoa wa Shinyanga Benety Malima akiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi wao wa maji.Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akichangia mada kwenye kikao cha uzinduzi wa mradi wa maji kutoka Shirika la Lifewater Internationali.Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini mkoa wa Shinyanga (Ruwasa) Malwa Kisibo,akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji.Kaimu meneja wa wakala wa maji vijijini wilaya ya Shinyanga (Ruwasa) Emaeli Nkopi, akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji.Kaimu Afisa afya mkoa Mussa Makungu akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi huo wa maji kutoka Shirika la Lifewater International.Kaimu Afisa afya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Gibril Mongi akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Kaimu mganga mkuu wa halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Bashiri Salumu akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa maji.Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, akichangia mada kwenye uzinduzi wa mradi maji kutoka Shirika la Lifewater Intenational.Wajumbe wakipiga picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko aliyekaa kwenye kiti katikati mara baada ya kumaliza kuzindua mradi wa maji kutoka Shirika la Lifewater International. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

JAJI MKUU: KEMEENI MAAHIRISHO YA KESI BILA SABABU ZA MSINGI

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Naibu Wasajili na Mahakimu kutoruhusu maahirisho ya mashauri ya mara kwa mara bila ya sababu za msingi.
Akizungumza na Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya mara baada ya kuwaapisha Naibu Wasajili na kuwakabidhi nyenzo za kazi Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya mapema Oktoba 25, 2019 katika Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa wana nguvu/mamlaka ya kuhakikisha kuwa mashauri yanakwisha kwa muda unaotakiwa.

“Nyie mna mamlaka ya kuwadhibiti Wapelelezi, Waendesha mashtaka kuhakikisha wanaharakisha kufanya upelelezi na kufuata sheria na taratibu zilizopo,” alisisitiza Mhe. Jaji Prof. Juma. 
Aidha; Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kwa kuwataka Maafisa hao wa Mahakama kuhakikisha suala la upelelezi unaofanywa na Polisi linafanyika kwa kutumia ‘video’ kama sheria inavyotaka.

Hali kadhalika, Mhe. Jaji Mkuu amewataka pia Maafisa hao kutumia sheria ya Makubaliano katika kesi za jinai ‘Plea-bargain’ ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.
“Sheria hii ya makubaliano katika kesi za jinai kati ya upande wa mashtaka na mshtakiwa inatumika pia nchini Marekani na imeleta mafanikio katika kupunguza msongamano, hivyo sheria hii isiishie kutumika makao makuu pekee bali itumike katika Mahakama zote nchini,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.

Kwa upande mwingine, Mhe. Jaji Mkuu aliwataka Maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi na taratibu za Kimahakama na Taifa kwa kuwa Taasisi imewaamini.
“Ninyi ni viongozi na mtambue kwamba ni injini ya Mahakama kwa aina ya kazi mnazofanya, ni muhimu kufanya kazi kwa kufuata kanuni za Maafisa Mahakama na vilevile ni wajibu wenu kuwaelimisha watumishi mnaowaongoza kujua maadili ya utumishi,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Katika hafla hiyo, Mhe. Jaji Mkuu amewakabidhi nyenzo za kazi jumla ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya 10 naye Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewaapisha jumla ya Naibu Wasajili wapya 10 ambao wote wameteuliwa kwa lengo la kuongeza nguvu kazi ya utoaji haki nchini. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza na Naibu Wasajili wa Mahakama walioapishwa leo pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi waliokabidhiwa nyenzo za kazi. Aliwataka  kuzingatia maadili ya kazi zao. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. (Kushoto) ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi na kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akionesha kitabu cha maadili , wakati akizungumza na Naibu Wasajili wa Mahakama, walioapishwa leo  na Mahakimu Wakazi Wafawidhi waliokabidhiwa Nyenzo za kazi kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi, likiwemo suala la kuzingatia maadili ya kazi zao. (Kushoto) ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi na kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi.
 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za Kimahakama wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happyness Ndesamburo akiapishwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Naibu Msajili.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe Silvia Lushashi nyenzo za kazi.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe Daniel Malik nyenzo za kazi.
 Baadhi ya Naibu Wasajili wa Mahakama waliapishwa leo na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu (ambaye hayupo pichani).
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (wa kwanza (kushoto) akiwa katika hafla hiyo na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania.

WATOTO 1000 WANAOZALIWA NCHINI, WATATU HUZALIWA NA ULEMAVU WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI

$
0
0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Jonathan Budemu akizungumza wakati wa maadhimisho hayo 
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimkabidhi cheti Mfanyakazi wa Benki ya NMB Jeniffer Mtey kwa ajili ya udhamini wa maadhimisho hayo 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga kushoto akimpongeza mtoto mwenye ulemavu wa kichwa kikubwa Joaly Salehe  ambaye aliimba wimbo wakati wa maadhimisho hayo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari

 WATOTO 1000 wanaozaliwa kila siku nchini watatu wanazaliwa wakiwa na matatizo ya ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi idadi ambayo imeelezwa kwa mwaka inafikia watoto 4800.

Takwimu hizo zilitolewa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani.

Maadhimisho hayo yalifanyika Kitaifa kwenye viwanja wa Tangamano mjini Tanga ambapo alisema kwamba serikali imekuwa ikiweka juhudi kubwa kuweza kuhakikisha inatokomeza suala hilo.

Alisema kwamba wakati umefika jamii kuacha kuwa na mila potofu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na dhana hiyo ianze kwa wazazi, walezi na familia inayowazunguka.

“Kwani imani potufu ndio zimepelekea wazazi na walezi wa watoto hao kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji bila mafaanikio na kusababisha ongezeko la vifo vya watoto wao”Alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliitaka jamii kutambua kwamba mtoto akizaliwa na kichwa kikubwa sio laana,mkosi wala balaa huku akiwataka kuachana na imani potufu kwani wameambiwa na wataalamu chanzo cha watoto kuzaliwa hivyo ni kutokana na upungufu wa madini ya foliki Acidi na virutubisho muhimu vinavyotokana na kwenye vyakula nyingi vilivyopo hapa nchini,.

“Lakini pia niwaase wakina mama wajawaziti kutumia vitamin hiyo kabla ya kupata ujazito huku akitoa wito kwa wanawake wenye umri wa kuzaa miaka 15 hadi 49 kuzingatia ulaji bora wa vyakula vyenye vitamin ya aina ya foliki acidi ikiwemo mbogamboga na matunda”Alisema Waziri Ummy

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa kila mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa wajawazito kwenda kliniki mapema mara wanapogundua ni wajawazito ili waweze kupatiwa huduma za afya ikiwemo vidonge vyenye vitamini ya foliki acid.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema kwamba tatizo hilo linazuilika na kumalizika kabisa kwenye jamii kwa kutoa elimu namna ya kuepukana nalo.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka viongozi wa dini kushirkiana na wadau katika kutoa elimu kwa jamii kwani tatizo hilo linaweza kuwa historia kama elimu sahihi inaweza kupatikana kwa wakati.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Watu Wenye ulemavu Joyce Maongezi alisema kwamba jamii inapaswa kutambua mapema watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Alisema kwamba ofisi yao itaendelea kutoa vifaa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuielimisha jamii pamoja na kuzindua mfuko wa Taifa wa watu wenye ulemavu ambao utaweza kuwasaidia.

“Lakini pia Halmashauri zitekeleze agizo la Serikali za kutaka watenge asimilia 2 ya mapato yake kwa ajili ya watu wenye ulemavu “Alisema

RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE WATOA POLE KWA FAMILIA YA MMOJA WA WAASISI WA VYAMA VINGI NCHINI MAREHEMU MZEE JAMES MAPALALA OSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Marehemu James Mapalala Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Bi. Hannah Mapalala Mke wa Marehemu James Mapalala alipokwenda na Mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali Sala maalumu ya kumuombea pamoja na Familia ya Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Marehemu James Mapalala walipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es salaam. Marehemu James Mapalala alifariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Benard James  Mapalala (Mtoto wa Marehemu James Mapalala) alipokwenda na Mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Osterbay jijini Dar es salaam, aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na waombolezaji wengine walipokwenda kutoa pole kwa familia ya Marehemu James Mapalala ambaye ni Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini, nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
PICHA NA IKULU

Kizimbani kwa kuiba Tausi wa Ikulu

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

WATU watatu wakazi wa jijini Dar es Slaam, leo Oktoba 25, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matano yakiwemo ya kukutwa na ndege aina ya Tausi wa Ikulu na kujihusisha na mtandao wa uhalifu.

wenye thamani ya Dola za Marekani 1,500 sawa na Sh 3,44 4,150.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amewataja washitakiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 116/2019 kuwa ni, David Graha, Mohammed Hatibu na Mohammed Ally.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo imedaiwa,  Juni Mosi 2015 na Oktoba 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa walijihusisha na mtandao wa uharifu ambapo wanadaiwa kuratibu genge la uhalifu wakijihusisha na biashara ya ndege aina ya Tausi bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Katika shitaka la pili, Nchimbi amedai katika tarehe hizo washitakiwa walikutwa na ndege watatu aina ya tausi wenye thamani ya USD 1,500 ambazo ni sawa na Sh milioni 3.4 mali ya serikali bila kuwa na kibali.

Pia Oktoba 14, mwaka huu maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Ally alikutwa na ndege watatu aina ya Tausi wanaopatikana Ikulu, ambao aliwapata kwa njia zisizo halali huku katika shtaka la tano, washtakiwa i Graha na Hatibu katika tarehe hizo hizo walijipatia Sh 300,000 huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la wizi.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuzingatia kwamba mashitaka hayo hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 7 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walirudishwa rumande kwa sababu mashitaka hayo hayana dhamana.


SADC KUWA NA VISA MOJA KUPUNGUZA URASIMU

$
0
0
Ahmed Mahmoud/Arusha

Naibu Ktibu Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya hiyo

Hayo yameelezwa leo na Naibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa wenye dhamana na Wizara za Maingira,Maliasi na Utalii katika nchi hiyo za Ukanda wa Kusini mwa bara la Afrika za SADC

Dkt Mhilongo pia amesema nchi za SADC zimejipanga kuangalia kwa kina suala la Viumbe na Mimea Vamizi katika nchi hizi wananchama za SADC pamoja na Wanyama ambao wakati katika hatari ya kutoweka katika nchi hizi

Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao wenye dhamana hii ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha wanangalia kwa kina Itifaki na Mikataba inayohusu Sekta hizi tatu katika nchi Wanachama za SADC

Amesema Mkutano wa Mawaziri haw ani muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mataifa ya SADC.

Hivyo amewataka wakati wa Mkutano huo wanapaswa kupima na kuangalia kwa kina Sera na Itifaki zinazosimamia Sekta hizi tau ambazo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa mapataifa haya

Mbali na kungalia masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao kuhakikisha wanangalia kwa Kina Hima Sheri azote zinazosimamia na kuongoza Sekta hizi katika Jumuiya hii. Amesisitiza Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC Dkt Mhilongo

Amesisitiza kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama za SADC na mbadiliko ya tabianchi

Amesisitiza umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yalenge katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika nchi za SADC

Ameeleza kwamba mkutano wa mwisho kufanyika kwa Mawaziri wa SADC ulifanyika Novemba 2017 Mjini Pretoria Afrika ya Kusini

Nchi za SADC imebahatika kuwa na raslimali lukuki zikiwemo zaWanyamapori, misitu, Uvuvi raslimali ambazo ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya nchi wanachama za SADC.Amesisitiza Dkt Mhilongo

Mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuathiri mataifa haya ya kusini mwa Afrika na kuathiri hali ya uzalishaji katika Sekta za Kilimo, ufugaji na maendeleo ya ukanda huu.Amesisitiza Dkt Mhilongo

Amewataka Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki ya SADC inayohusu umuhimu wa kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori

Pia amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika

Naibu Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba historia kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita

Amesema SADC iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Keneth Kaunda wa Zambia, Rais Somora Machel wa Msumboji na Rais Austino Neto wa Angola na Rasi Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyi iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC

Aidha Mkataba wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia kwa ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gabron Botswana

Aidha kukosekana kwa Visa moja kwa Watalii ulaya wanapokuja katika ukanda huu wa kusini mswa nchi za kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa

Ndege ya pili Boeing 787-8 Dreamliner yaondoka Marekani,kutua kesho mchana nchini.

$
0
0

25 Oktoba, 2019.

Ndege mpya ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeondoka nchini Marekani kuja Dar es Salaam Tanzania.

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kesho mchana (26 Oktoba, 2019).

Ndege hiyo itapokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Hii inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na uchumi.



Ligi kuu ya Serengeti Lite Kuanza hivi karibuni

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake (TWFA) Amina Karuma (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa Ligi ya Wanawake inayodhaminiwa na Kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite. Kulia nini Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo na kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewerieas (SBL) George Mango
Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo (kati kati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kuanza kwa Ligi ya Wanawake inayodhaminiwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL)kupitia bia yake ya Serengeti Lite. Kushoto ni Afisa Masoko wa SBL George Mango na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake (TWFA) Amina Karuma
Afisa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewerieas (SBL) George Mango (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa Ligi ya Wanawake inayodhaminiwa na Kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake (TWFA) Amina Karuma na kulia ni Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo
Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia mkutano wa kutangaz kuanza kwa Ligi ya Wanawake inayodhaminiwa na Kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite itakayoanza kesho ikishirikisha timu 12 zitakazocheza ugenini na nyumbani.

PROFESA KITILA AFUNGA WARSHA YA MRADI WA MAJI MAARUFU 'P for R' MKOANI SINGIDA

$
0
0

 Katibu  Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo (katikati) akizungumza na Mameneja wa RUWASA wa Wilaya, Waganga Wakuu wa Wilaya, Maofisa Afya, Maofisa Elimu (SWASH), Maofisa Ustawi wa Jamii, TAMISEMI na Maofisa Wakaguzi wa Ndani wakati akifunga warsha ya mafunzo ya uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa .mradi wa maji utakaokwenda sambamba na malipo kulingana na matokeo ya kazi (PforR) mjini Singida leo. Kulia ni Kiongozi  wa Timu ya  mradi huo kutoka Benki ya Dunia  (Task Team Leader), Iain Menzies na kushoto ni Mratibu wa mradi huo, Mhandisi Mashaka Sitta. 
 Mratibu wa mradi huo, Mhandisi Mashaka Sitta, akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo.
 Kiongozi  wa Timu ya  mradi huo kutoka Benki ya Dunia ( Task Team Leader), Iain Menzies akizungumza mbele ya washiriki wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Agnela Nyoni akizungumza kwenye ufungaji wa warsha hiyo.
 Washiriki  wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo (hayupo pichani) wakati akifunga warsha hiyo.
Washiriki  wakiwa kwenye warsha hiyo.

RC MNYETI AFAGILIA MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amefagilia miaka minne ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli kuwa ni ya maendeleo makubwa kwa wananchi wa Tanzania. 

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maghagh Wilayani Mbulu, Mnyeti alisema miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli imekuwa na mafanikio makubwa ya maendeleo. 

Alisema miaka minne ya Rais Magufuli imekuwa faraja kwa watanzania wengi ikiwemo miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo imebadili maisha ya Watanzania. 

Alisema maendeleo mengi yamefanyika nchini ikiwemo vituo vya afya, hospitali za wilaya, kuboresha elimu, maji, ujenzi wa barabara na ununuzi wa ndege. 

“Kwa maendeleo haya ya miradi mbalimbali ya maendeleo hivi tutamsahau Rais Magufuli, tunachopaswa kufanya ni kumpa zawadi ya ushirikiano na kumuombea kwa Mungu,” alisema Mnyeti. 

Alisema wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yao ya maendeleo binafsi na kwa jamii kwa ujumla. 

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Simbalimile Mofuga alisema miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli yamefanyika maendeleo mengi mithili ya miaka 40.

Mofuga alisema Rais Magufuli amekaa madarakani miaka minne pekee lakini maendeleo yaliyofanyika kwenye utawala wake utadhani ametawala miaka 40.

Diwani wa kata ya Endamilay, Gesso Bajuta alisema maendeleo mengi yamefanyika wilayani Mbulu kipindi cha Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya. 

“Majengo makubwa ya hospitali mpya kwa shilingi bilioni 1.5 ni maendeleo makubwa mno yamefanyika tunamshukuru sana Rais Magufuli,” alisema Bajuta

NCHI ZA SADC KUWA NA VISA MOJA KUPUNGUZA URASIMU

$
0
0

Ahmed Mahmoud/Arusha
Naibu Ktibu Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya hiyo.

Hayo yameelezwa leo na Naibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa  wenye dhamana na Wizara za Maingira,Maliasi  na Utalii katika nchi hiyo za Ukanda wa Kusini mwa bara la Afrika za SADC.

Dkt Mhilongo pia amesema nchi za SADC zimejipanga  kuangalia kwa kina   suala la Viumbe na Mimea Vamizi katika nchi  hizi wananchama za SADC pamoja na Wanyama ambao wakati katika hatari ya kutoweka katika nchi hizi.

Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri  hao wenye dhamana hii ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha  wanangalia kwa kina Itifaki na Mikataba  inayohusu Sekta hizi tatu katika nchi Wanachama za SADC
Amesema Mkutano wa Mawaziri hawa ni muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mataifa ya SADC.
Hivyo amewataka wakati wa Mkutano huo wanapaswa kupima na kuangalia kwa kina  Sera na Itifaki zinazosimamia  Sekta hizi tau ambazo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa mapataifa haya.

Mbali na kungalia masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao kuhakikisha wanangalia  kwa Kina Hima Sheri azote zinazosimamia  na kuongoza Sekta hizi katika Jumuiya hii, amesisitiza Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC Dkt  Mhilongo

Amesisitiza kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama za SADC na mbadiliko ya tabianchi

Amesisitiza umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yalenge katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika nchi za SADC

Ameeleza kwamba mkutano wa mwisho kufanyika kwa Mawaziri wa SADC  ulifanyika  Novemba 2017 Mjini Pretoria Afrika ya Kusini
Nchi za SADC imebahatika kuwa na raslimali  lukuki zikiwemo zaWanyamapori, misitu, Uvuvi  raslimali ambazo  ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya  nchi wanachama za SADC, amesisitiza Dkt Mhilongo

Amesema mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuathiri mataifa haya ya kusini mwa Afrika  na kuathiri hali ya uzalishaji katika Sekta za Kilimo, ufugaji na maendeleo  ya ukanda huu.

Amewataka Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki  ya SADC  inayohusu umuhimu wa kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na  Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori.

Pia amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Naibu Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba  historia  kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita.

Amesema SADC iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Keneth Kaunda wa Zambia, Rais Somora Machel wa Msumboji na Rais Austino Neto wa Angola na Rasi Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyi iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC.

Aidha Mkataba wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia  kwa ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gabron Botswana
Aidha kukosekana kwa Visa moja  kwa Watalii  ulaya wanapokuja  katika ukanda huu wa kusini mswa nchi za kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa

MAKAMISHNA WA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA HAWATEKELEZI MAJUKUMU YAO IPASAVYO, UBADHILIFU UMEKITHIRI- MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.(Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiongoza kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) (Wa Pili kulia) akiongoza kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Tume y maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kanani (Wa Pili kulia), Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bi Elizabeth Makwabe (Wa Kwanza Kushoto) na Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Benson Ndiege.
 Mwenyekiti wa Tume y maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kanani  akizungumza wakati wa kikao kazi cha Tume hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na Menejimenti ya tume hiyo mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.


Amesema kuwa Mali zinaibiwa za wananchi, watu wanauziana viwanda huku Ubadhilifu ukiwa umekithiri kuliko kawaida lakini bado kuna tume ya Maendeleo ya Ushirika.


Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Makamishna wa Tume hiyo katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 25 Octoba 2019.


Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya Bilioni 124 zimeibiwa kwenye vyama vya ushirika lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, "Mnataka mpaka kuwe na posho ndipo kamati ikutane kuona ulazima wa kusimamia fedha na Mali za ushirika" Alihoji Mhe Hasunga


Aliongeza kuwa wizi wa mali na fedha hizo za ushirika ni ishara ya makamishna kutofanya majukumu yao ipasavyo hivyo jambo hilo linapelekea Wanachama kuendelea kuteseka.


"Nasikitika sana Watu walioaminiwa na kupewa dhamana wameshindwa kutekeleza majukumu yao, kwenye zao la ufuta pekee zimeibiwa Bilioni 2.5 lakini wahusika wanadunda mtaani kadhalika mazao kama ya korosho na Pamba ambapo hakuna Ushirika badala yake kuna madalali tu" Alisema


Mhe Hasunga ameongeza kuwa hakuna sababu ya kuwa na Tume ya Ushirika isiyotekeleza majukumu yake ipasavyo huku akiongeza kuwa serikali inataka kujenga ushirika lakini kuna watu kazi yao ni kubomoa, na kuweka urasimu katika utendaji.


Waziri Hasunga amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya ushirika Dkt Titus Kanani kuchukua hatua za haraka kwa watendaji wote wa Tume hiyo ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.


Mhe Hasunga amesema kuwa endapo ushirika utasimamiwa vizuri wananchi watakuwa na maendeleo maradufu yatakayopelekea Taifa kuendelea mbele kiuchumi.


Kadhalika ametoa nafasi ya ziada kwa Tume hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha matokeo makubwa ya uwajibikaji vinginevyo ametishia kuivunja tume hiyo.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kamani amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kukubali kushiriki katika kikao hicho huku Kamishna wa Tume hiyo Mudhihir M. Mudhihir akizungumza kwa niaba ya Makamishna wengine amehakikisha kuwa Tume hiyo itatekleza majukumu yake kwa weledi mkubwa.

MWISHO.

STARTIMES YAJA NA TAMTHILIA YA THE LOST HEARTS

$
0
0
Startimes wanakuletea Tamthilia nzuri ambayo itavutia macho ya watazamaji wengi iitwayo THE LOST HEARTS, itaanza kurushwa siku ya Jumapili tarehe 27 mwezi oktoba  kwenye chaneli ya ST Novela Eplus saa 3:45 Usiku. Tamthilia hii itakuja baada ya Tamthilia ya Blood Sisters  kuisha.

Hivi utafanya nini endapo rafiki yako mpendwa kakuchukulia mpenzi wako? Hiki ni kionjo tu ndani ya Tamthilia ya The Lost Hearts, ambapo waigizaji nguli na wahusika wakuu wa tamthilia  hii Tessa na Magra ambao ni marafiki wakaribu sana wanakuja kua maadau kwa sababu tu ya mmoja wao anamsaliti mwenzake kwa kutembea na mpenzi wa mwenzie,hii tamthilia itatuonyesha namna inavyotesa kwa rafiki yako mpendwa kukuchukulia mpenzi wako.

Tamthilia kwa Ufupi
Tessa,ambaye ni  mbunifu wa mitindo na Marga ambaye ni malkia wa urembo na model, ni marafiki wa karibu wanaoshirikiana kutimiza ndoto zao licha ya ugumu wa maisha yao. Walakini, dhamana yao inapimwa wakati Caloy anaingia katika maisha yao. Caloy ana uhusiano wa kihistoria na Marga, lakini anapendelea kuweka mahusiano ya siri.
 Kisha Caloy akakutana na Tessa na wakapendana, ambapo wakasababisha Marga abadilishe uamuzi  wa kumrudisha kwake. Wakati huo huo, mahusiano ya Caloy na Tessa yanajaribiwa wakati Jaime, bosi wa Tessa na mjane wa marehemu ya Tessa, anapoanza kumpendelea.

Pamoja na hali ya wasiwasi kati ya marafiki na wapenzi inakua, bila kutarajia, maisha ya Caloy, Marga, Tessa na Jaime yanageuka ghafla na kua mwelekeo tofauti kutokana na kosa moja la ulevi. Baada ya hayo, kizazi chao kinaendelea kuchochea uhusiano bila kujua.
Kuendelea kupata uhondo huu wa Tamthilia ya The Lots Hearts Lipia kifurushi cha Mambo Tsh 14,000 Tu!

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NCHINI AZERBAIJAN KUMWAKILISHA JPM MKUTANO WA NCHI ZISIZOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan,  Ali Ahmadov wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Heydar Aliyev, Oktoba 25, 2019 amabako atamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote unaofanyika  Baku nchini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA AWASILI NCHINI AZERBAIJAN KUMWAKILISHA JPM KATIKA MKUTANO WA NCHI ZISIZOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan,  Ali Ahmadov wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Heydar Aliyev, Oktoba 25, 2019 amabako atamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote unaofanyika  Baku nchini humo. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PYRAMIDS YA MISRI YATUA MWANZA TAYARI KUPAMBANA NA YANGA

$
0
0
 Kikosi cha Timu ya Pyramids kutoka Misri kimewasili salama jijini Mwanza tayari kwa mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

TANZANIA YATAKA ZIMBABWE KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIUCHUMI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka Zimbabwe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (Mb) akitoa hotuba ya majumuisho na kufunga kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu, akihutubia hadhara wakati alipowasilisha mada iliyolenga hali ya utawala na diplomasia ya uchumi Afrika katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu lililojadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka zimbabwe.

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa pili kutoka kulia) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali, vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu

Baadhi ya mabalozi wateule pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe.

Vingozi, Mabalozi na wananchi wakifuatilia mdahalo wa kujadili jinsi ya kuiwezesha Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.


Viewing all 110149 articles
Browse latest View live




Latest Images