Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN YAADHIMISHA WIKI YA USALAMA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Paul Muhato (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wakikagua moja ya kisima cha mafuta ikiwa ni sehemu ya kilele cha Wiki ya Usalama ambayo huadhimishwa kati ya tarehe 21 mpaka 25, Oktoba Duniani kote, ambapo kwa upande wa Engen wamefanya kilele hicho kwa kutembele na kukagua sehemu za usalama katika Kituo chao cha Mikocheni Jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Paul Muhato akikagua moja ya mitundi ya kuzimia moto, katika Kituo cha mafuta cha Engen Mikocheni ikiwa ni sehemu ya kilele cha Wiki ya Usalama ambayo huadhimishwa kati ya tarehe 21 mpaka 25, Oktoba Duniani kote, ambapo kwa upande wa Engen wamefanya kilele hicho kwa kutembele na kukagua sehemu za usalama katika Kituo chao cha Mikocheni Jijini Dar es salaam leo. 










Mabalozi wa SADC, Qatar watoa wito kuiondolea vikwazo Zimbabwe.

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Eswatini na Afrika Kusini ambao wanaunda kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini Qatar. Waheshimiwa Mabalozi walikuwa wanakamilisha mpango mkakati wa kutumia siku ya tarehe 25 Oktoba kama ilivyoamuliwa na Viongozi wa Nchi za SADC kupaza sauti kwa njia mbalimbali kutoa wito kwa nchi za Magharibi kuiondolea vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe. 

Mabalozi hao wamepanga kupeleka Waraka wa Kidiplomasia Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Balozi za EU na Ubalozi wa Marekani pamoja na kutoa makala kwenye vyombo vya habari kuelezea athari za vikwazo katika uchumi wa Zimbabwe. 
Waheshimiwa Mabalozi wakiwa wanaendelea kutekeleza jukumu lao.
Baada ya kumaliza kazi wanapongezena kwa kushikana mikono ikiwa ni kiashiria cha mshikamamo hadi Zimbabwe inaondolewa vikwazo. 

ALAMA YA DHARULA....

$
0
0
Katika pita pita za kamera man wa Globu ya Jamii, akiwa katika barabaraba ya Rose Garden na kukutana na Lori hili la kuchanganya zege likiwa limekata wese, mara akashuka utingo cha kifaa cha kutahadhalisha kuwa mchuma huo hauko poa na kukiweka kama kionekanavyo hapo na kulekea kuchukua zake wese. 

BIASHARA KATI YA TANZANIA NA URUSI IRATIBIWE-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwwa ameutaka ubalozi wa Tanzania nchini Urusi uratibu mipango ya wafanyabiashara wa Urusi wanaokusudia kuja nchini kuwekeza kwa kuwaunganisha na Taasisi na Wizara husika ili waweze kuwekeza mitaji yao kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Ametoa agizo hilo jana (Alhamisi, Oktoba 24, 2019) baada ya kugundua uwepo wa wafanyabiashara wengi wa Urusi wanakusudia kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji pamoja na kutafuta wafanyabiashara wa Kitanzania watakaoungana nao katika uwekezaji wanaokusudia kuufanya.

“Tayari miadi imekwishawekwa ya kuwakaribiasha wawekezaji wa Urusi kuja Tanzania kwa ushawishi wa kwangu mwenyewe pamoja na ushawishi wa wafanyabiashara wa Tanzania, hivyo nisingependa wafanyabiashara hao wasumbuliwe au kukatishwa tamaa katika kutimiza nia yao hiyo.” Waziri Mkuu alisisitiza.

Alisema Mkutano baina ya Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi uliomalizika jana Oktoba 24, 2019 ulilenga kujenga uhusiano mzuri zaidi katika nyanja mbalimbali hususani za kiuchumi.

Akizungumza baada kumalizika mkutano huo kwenye ukumbi wa Olympic Park wa Sochi nchini Urusi, Waziri Mkuu alisema Urusi imeutumia mkutano huo kueleza bayana maeneo ambayo wako tayari kushirikiana na Afrika katika kuwekeza kwa faida ya pande zote mbili.

Waziri Mkuu aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na uuzaji wa zana za kilimo kama vile matrekta, sekta ya mafuta na gesi pamoja na madini, Ujenzi wa miundombinu hasa reli, masuala ya elimu hasa utoaji wa nafasi za mafunzo nchini humo.

Alisema kwa upande wake Tanzania imejinadi vizuri ikIngozwa na yeye mwenyewe kwani alifanya mazungumzo na viongozi wa makampuni zaidi ya manane ya Urusi ili kuyashawishi yawekeze nchini na yote yalikubali kufika Tanzania mapema iwezekanavyo.

“Viongozi wa makapuni yote niliyopata nafasi ya kuzungumza nao wamesema wako tayari kuja nchini ili waweze kufanya mazungumzo na Serikali pamoja na wafanyabiashara wazalendo ambao wako tayari kuungana na wafanyabiashara hao katika kuwekeza nchini Tanzania.”

Waziri Mkuu alisema viongozi hao walimueleza maeneo ambayo wao wanaamini kuwa wanafanya vizuri na wangependa kupata kibali cha kuwekeza Tanzania baada ya mazungumzo yao na Serikali. Pia walieleza ni kwa namna gani Taifa litanufaika na uwekezaji wao.

Alisema, tayari wafanyabiashara binafsi 18 wa Tanzania walijitokeza kushiriki katika Mkutano huo na walifanya kazi kubwa na nzuri ya kuwahabarisha wenzao wa Urusi kuhusu mazingira mazuri ya kuwekeza yaliyopo nchini hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuondoa kero, kanuni na taratibu ziliokuwa zikiyafanya mazingira ya uwekezaji kuwa magumu.

Awali, akizungumza kwenye Mkutano baina ya Wakuu wa nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Tanzania ni nchi sahihi kwa uwekezaji kwa wanaotaka kuwekeza barani Afrika kwani imedhamiria kukuza uchumi wake na kufikia wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda. Pia ni nchi yenye amani na utulivu.

 “Nchi yetu imejaliwa kuwa na maliasili nyingi ambazo vilele ni malighafi kwa viwanda kama vile mazao ya kilimo, misitu, bahari, maziwa, madini na mbuga za wanyama ambazo ni kivutio cha watalii,” alifafanua Waziri Mkuu.

Leo Oktoba 25, 2019 Mheshimiwa Majaliwa ataondoka nchini Urusi kwenda nchi ya Azerbaijan ambako pia atamwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote. Mkutano huo ni wa siku mbili.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA, MALIASILI WA SADC

$
0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaojadili kuhusu Mkakati wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo umefunguliwa leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha.
Mawaziri pamoja na Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa SADC unaojadili kuhusu Mkakati wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. wakimsikilioza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akifungua Mkutano huo leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa SADC unaojadili kuhusu Mkakati wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Baada ya kufungua Mkutano huo leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

BEI ZA MATUNDA KATIKA SOKO LA MAPINDUZI MWANANYAMALA LEO

$
0
0
Leo kamera man wetu katia maguu katika soko la Mapinduzi Mwananyamala, jijini Dar es salaam ili kukujuza wewe Mdau Bei za matunda ya aina mbalimbali kama zilivyoainishwa na wenyewe kupitia vibao vyao hapo pichani. (Picha na Emmanuel Massaka)



MKURABITA YATAKIWA KUHAKIKISHA HATIMILIKI ZA KIMILA ZINATUMIKA KUWAPATIA MIKOPO WANUFAIKA WA MPANGO HUO

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi, Bw. Kelvin Joseph alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuwaunganisha wanufaika wa MKURABITA na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na kujiinua kiuchumi wakati Naibu Waziri huyo aliposimama kukagua utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango huo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Tunduma mkoani Songwe jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)na kuzungumza na watumishi. 



Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika mkoa wake jana kabla ya Naibu Waziri huyo kuanza ziara ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) 
Aaron Mrikaria-Songwe 

Tarehe 25 Oktoba, 2019 

Watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wametakiwa kuratibu taasisi za fedha
zenye utayari wa kuwapatia mikopo wanufaika wa Mpango huo wenye
hatimiliki za kimila ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi
zitakazowawezesha kuinua kipato na kuboresha maisha yao. 

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa
Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA). 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanufaika
wa Mpango huo katika Kijiji cha Naming’ongo ambao wamesema
wanashindwa kutumia hatimiliki za kimila kupata mikopo kutokana na
kukosa mwongozo na utaratibu wa upatikanaji wa mikopo kwenye taasisi
za fedha, licha ya hatimiliki hizo kupunguza migogoro ya ardhi. 

“Nawapa wiki mbili mnipe majibu ya taasisi za fedha zitakazokubaliana na
Serikali kutoa mikopo kwa kutumia hatimiliki za kimila, na kuongeza kuwa
elimu kwa umma itolewe ili wananchi waliorasimishiwa mashamba na
maeneo ya biashara wajue taratibu za kupata mikopo kwenye taasisi za
fedha zilizo tayari kutoa mikopo hiyo,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Watendaji wa MKURABITA
kuharakisha zoezi la kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi
waliorasimishiwa ardhi, ikizingatiwa kuwa mchakato wa zoezi hilo huishia
wilayani hivyo hakuna sababu ya ucheleweshaji. 

“Kama mwananchi ameshatekeleza taratibu zote za urasimishaji, kuna haja
gani ya kusumbuliwa wakati upatikanaji wa hatimiliki za kimila ni
makubaliano ambayo yanakamilika katika ngazi ya kijiji na si wizarani,”
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kuona mashamba ya mpunga
ya wanufaika wa MKURABITA wa Kijiji cha Naming’ongo na kuwapongeza kwa kilimo cha kisasa. 

Jumla ya mashamba 776 yamerasimishwa katika Halmashauri ya Wilaya
ya Momba mkoani Songwe ambapo kati ya hayo, hatimiliki za kimila 527
zimeshatolewa.

RC MNYETI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA GHAFLA HOSPITALI YA MBULU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akimpa pole mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye hospitali ya Mji wa Mbulu alipofanya ziara ya ghafla. 

**************************************** 

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti katika hali isiyo ya kawaida amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mji wa Mbulu kwa lengo la kubaini namna wagonjwa wanavyohudumiwa. 

RC Mnyeti alifika kwenye hospitali hiyo mara mbili jana alasiri na saa tisa usiku bila uongozi wa hospitali wala wagonjwa kutambua kuwa ni mkuu wa mkoa amewatembelea ghafla. 

Awali, alifika alasiri na gari lake bila bendera na kutembelea wodi walikolazwa wagonjwa na kuzungumza nao ili kutambua namna wanavyopatiwa huduma. Alizungumza pia na wauguzi waliokuwepo ambapo aliwahoji namna wanavyotoa huduma ikiwemo lugha nzuri kwa wagonjwa ili wapate faraja wakati wakitibiwa. 

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gedamar alisema lengo lake lilikuwa ni kujua namna wagonjwa wanavyohudumiwa kuliko kusubiri kuambiwa. 
“Nimefika hospitali na kukuta baadhi ya mapungufu yafanyiwe kazi, wauguzi usiku inakuwa shida kuhudumia wagonjwa, nimeshuhudia mwenyewe,” alisema Mnyeti. 

Alisema dirisha la wazee inaonyesha wameweka karatasi muda siyo mrefu baada ya kupata taarifa ya yeye kuanza ziara wilayani Mbulu. Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga alisema wanayapokea mapungufu hayo na kuhakikisha watayafanyia kazi. 

“Tunakuahidi kuwa mapungufu hayo madogo tumeyachukua na tunakuhakikishia kuwa yatafanyiwa kazi ili yasijirudie tena,” alisema Mnyeti. Mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa kwenye hospitali hiyo John Tsere alisema kitendo cha mkuu wa mkoa kutembelea kwa kushtukiza hospitalini hapo kitaongeza uwajibikaji kwa wauguzi na madaktari. 

“Amefika bila polisi wala viongozi wa wilaya na amevaa nguo za kawaida yaani huwezi kubaini kama ni mkuu wa mkoa wakati mwingine ni vizuri kufanya hivyo ili uone mwenyewe kuliko kusomewa taarifa,” alisema Tsere. 

Mnyeti yupo kwenye ziara ya siku nne wilayani Mbulu ya kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na kusikiliza changamoto na kero zao ili kuyapatia majawabu.

PUMA ENERGY, SELCOM NA MASTERCARD WAUNGANA KUHAMASISHA MALIPO YA KIELEKTRONIKI

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dominic Dhanah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bomba Weekend katika kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Sameer Hirji, akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya BombaWeekend kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dominic Dhanah.

Baadhi ya wateja wakikaribishwa na wafanyakazi wa Puma Energy kwa ajili ya kujaza mafuta kwa kutumia kadi ya Master Card kwenye kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga.
Bw. Modestus Chambu mmoja wa wateja wa kampuni ya Puma Energy akijaziwa mafuta kwa kadi ya Master Card kwenye kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.
Wateja wakiendelea kuhudumiwa na wafanyakazi wa Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.
Bw. Modestus Chambu mmoja wa wateja wa kampuni ya Puma Energy akiwaelezea waandishi wa habari faida anazozipata kwa kujaza mafuta kutumia mfumo wa Kielektroniki Master Card.


KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo BombaWeekend yenye lengo la kurejeshea asilimia tano ya fedha watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar s Salaam na itaendeshwa kwa wiki 11, kila Ijumaa hadi Jumapili kuanzia saa 10 hadi 12 jioni kupitia mtandao wa Puma wenye vituo 52 nchi nzima. Pamoja na dhumuni la kuzawadia watumiaji wa huduma hiyo, Bomba Weekends ina dhamira ya kuchangia katika juhudi za serikali za kurasimisha malipo na kuhamasisha uchumi wa malipo ya kieletroniki ili kufikia malengo ujumuishaji wa kifedha wa nchini Tanzania.

Pia imeelezwa kwamba mchakato mzima wa kurudishia pesa wakati wa Bomba Weekends unaendeshwa kupitia huduma ya zawadi kwa wateja ya Qwikrewards iliyoundwa na Selcom Paytech LTD mahususi kwa watumiaji wa Mastercard QR.

Na kwamba Qwikrewards inamuwezesha mtu yeyote kukusanya pointi au kupata pesa taslim kupitia akaunti iliyounganishwa na namba yake ya simu kila afanyapo malipo kutumia Mastercard QR. Watumiaji Qwikrewards wanaweza kukomboa pointi walizokusanya kwa kupiga 150*15 na kuzitumia katika maeneo zaidi ya 30,000 nchini ambapo Mastercard QR inakubalika kama njia ya malipo.

Aidha Mastercard QR imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake nchini mwaka 2018 hadi sasa kupelekea kukubalika na watoa huduma mbali mbali zaidi ya 30,000 kuwa na uwezo wa kupokea malipo kutoka mitandao yote 7 ya simu na benki 15 nchini.

Akizungumza kwa kina kuhusu kampeni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema "Bomba Weekends inahamasisha wateja we kulipia mafuta katika vituo vyao kwa kutumia njia rahisi, haraka na salama zaidi na kunufaika papo hapo kupitia Qwikrewards kutoka Puma.

Amesema ushirikiano huu unadhahiri kwamba Puma ni kiongozi wa katika sekta ya mafuta inapofikia kujiunga na suluhisho bunifu za malipo ambazo hurahisisha malipo kwa wateja wetu na kutuwezesha kutoa huduma bora zaidi katika vitu vyetu."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Nd. Sameer Hirji, alionyesha matumaini makubwa kuelekea uchumi wa malipo ya kielektroniki akisisitiza kuwa ni lazima taasisi ambazo zinaongoza mchakato huo kuongeza thamani kwa wateja ili kuwapa hamasa zaidi kutumia malipo ya elektroniki.

"Kupitia Bomba Weekends tukishirikaina Puma Energy pamoja na Mastercard QR tumedhamiria kuwazawadia wateja watakaolipa kielektroniki katika matumizi yao ya kila siku, mafuta yakiwa sehemu kubwa ya matumizi hayo.

" Tunaamini kwamba tunavyozidi kurahisisha na kuimarisha upatikanaji na upokeaji wa malipo ya kieletroniki ndivyo tutazidi kuwajengea Watanzania imani ya kutoka nyumbani bila pesa taslim. Tukiwa na Qwikreward na maeneo zaidi ya 30,000 ambapo Mastercard QR inakubali kitaifa tunaamini tunaongoza mabadiliko kuelekea malipo ya kielektroniki na malengo ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania,”amesema .

Wakati huo huo wadau mbalimbali wanatumia mfumo wa malipo kwa njia ya kieletroniki wamesema wamefurahishwa na uamuzi wa kampuni hizo kuungana kuhakikisha wanahamasisha ulipaji wa fedha kwa njia hiyo ambayo ni salama na yenye kurahisisha malipo.

Wamesema katika kipindi hiki cha kampeni hiyo wataitumia vema ili kupata asilimia tano ambayo imetolewa kama sehemu ya kupata fedha ambayo Puma wameamua kuirejesha kwa Watanzania.

MKUU WA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY,KIJITONYAMA WAITIKIA MWITO WA MAHAKAMA YA KISUTU

$
0
0
Na Karama Kenyunko,  globu ya jamii

WAKUU wa vituo vya Polisi  Oysterbay na  Kijitonyama wameitikia wito na kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kueleza kwa nini mshtakiwa Elizabeth Balali (54) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi hakupelekwa gerezani kama amri ya mahakama ilivyotaka badala yake wakakaa nae kituoni.

Wakuu hao ASP Kazwenge wa Osterbay na ASP Rujuo wa Kijitonyama walifika mahakamani hapo leo Oktoba 25,2019 kama mahakama ilivyowaagiza jana na majira ya saa tano na nusu iliingia katika chumba cha Hakimu  Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina ambapo walikaa  kwa dakika kadhaa wakiwa pamoja na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon kisha wakatoka nje ndipo mahakama ikamuita mshtakiwa.

Mshtakiwa Elizabeth Balali alifikishwa mahakamani hapo ambapo Wakili Wankyo aliieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika hivyo akaomba tarehe  nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua yà upelelezi.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na akasisitiza kuwa mshtakiwa apelekwe rumande."Kesi itatajwa tena tarehe 11, mwaka huu mshtakiwa apelekwe rumande, nasisitiza mshtakiwa apelekwe rumande" amesema Hakimu Mhina.

Jana jioni, Mahakama iliamuru wakuu hao wa vituo kufika mahakamani hapo kueleza  kwanini wamekaa na mshitakiwa kituo cha polisi badala ya kumpeleka gerezani.Oktoba 10, mwaka huu mahakama ilitoa amri kwa mshitakiwa ambaye ni msimamizi wa mirathi wa mke wa marehemu, Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) kwenda gereza la Segerea kwa sababu anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana.

Hata hivyo, kesi hiyo ambayo ilipaswa kuendelea jana haikuweza kusikilizwa kutokana na mkanganyiko uliokuwepo baada ya mshitakiwa huyo kubainika hakuwepo gereza la Segerea na kwamba alikuwa kituo cha polisi.

Mshitakiwa huyo aliletwa mahakamani akitokea Kituo cha Polisi Kijitonyama alikokuwa amekaa kwa siku saba na Kituo cha Oysterbay alikaa siku saba.Katika kesi hiyo, Elizabeth ambaye ni Mkazi wa Boko Magengeni,  anakabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh milioni 25 kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Awali wakili Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai  kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk Roderick Kisenge kwa ulaghai.Mshitakiwa anadaiwa  kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambalo halijapimwa lililopo eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Wankyo alidai katika kipindi hicho  mshitakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Katika Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka, Elizabeth hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya Uhujumu Uchumi na Hakimu Mhina alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana kisheria.

Hivyo alielekeza mshitakiwa huyo kurudishwa rumande katika gereza la segerea hadi leo kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

KAZI YA KUHIFADHI NA KULINDA MAZINGIRA YETI NI YETU WENYEWE-MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu amefungua mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo amezitaka nchi za Sadc kuweka mikakati na kuridhia itifaki ya mazingira ili kutunza mazingira na kuweka jitihada za pamoja za kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira .

“Kazi ya Kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ni yetu Wenyewe “ Anaeleza Makamu wa Raisi akifafanua umuhimu wa kutunza mazingira.

Makamu wa Raisi amesema kuwa serikali zinasubiri mapendekezo yanayotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji kwa maslahi mapana ya SADC na nchi wanachama .

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala amesema kuwa Mawaziri hao watapitisha mapendekezo ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana na ujangili na kuhakikish kunakua na utalii endelevu.

Pia tutaangalia itifaki ya SADC Kuhusu usimamizi wa misitu ,itifaki ya mpango wa maendeleo ya utalii kwa nchi zote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC Unaojadili kuhusu mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na Hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii baada ya kufungua Mkutano huo leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Mawaziri pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii wa Nchi Wanachama wa SADC wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Mkutano huo leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa mikutano AICC Jijini Arusha .

DK.SHEIN AKUATANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na mgeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) Nd,Guo Yezhou akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu] 25/10/2019. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP)Nd,Guo Yezhou (wa tatu kulia) akiwa na Ujme aliofuatana nao wakati walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza mgeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP)Nd,Guo Yezhou (kushoto) wakati wa mazungumzo yao leo akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar ,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP)Nd,Guo Yezhou wakati wa mazungumzo yao leo akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar ,[Picha na Ikulu] 25/10/2019. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) Nd,Guo Yezhou (kushoto) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe wake,[Picha na Ikulu] 25/10/2019.

IGP SIMON SIRRO AKUTANA NA WANANCHI WA IGOGO JIJINI MWANZA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro, akizungumza na wananchi wa kata ya Igogo mkoani Mwanza ambapo amesikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wanapotafuta huduma za kipolisi sambamba na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo

MAKAMU WA RAIS ASIKITISHWA NA KASI YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NCHI ZA SADC

$
0
0

Na Vero Ignatus,Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amefungua mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika jijini Arusha .

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Mhe,Samia Suluhu ameeleza kusikitishwa na uharibifu wa mazingira katika nchi wanachama wa jumuiya Ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).

Amesema anaimani mkutano huu utaweka mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kuzuia kuingia kwa viumbe vamizi,ambapo viumbe hivyo vinaweza kuhatarisha ustawi wa sekta za kilimo,uvuvi,mifugo na utalii pamoja na hifadhi ya bioanuia

''Nafahamu kuwa kunajuhudi mbalimbali za kudhibiti viumbe vamizi nikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mpango mkakati na mpango kazi kudhibiti viumbe hivi"Alisema Mhe.Samia.Amesema ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni muhimu kuwa na mikakati ya pamoja ya uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa Sekta ya utalii imekuwa na mchango mkubwa katika nchi za SADC kwani inachangia dola 56.3 bilioni sawa na asilimia 8.2 ya pato ghafi,ambapo imechangia ajira ya watu 6.3 milioni,ambapo mwaka 2018 sekta hiyo ilichangia dola bilioni 2.4sawa na asilimia 25 fedha za kigeni.

Amezitaka nchi wananchama kuweka mikakati na kuridhia itifaki ya mazingira ili kutunza mazingira na kuweka jitihada za pamoja za kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira .

“Kazi ya Kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ni yetu Wenyewe “ Anaeleza Makamu wa Raisi akifafanua umuhimu wa kutunza mazingira.Makamu wa Raisi amesema kuwa serikali zinasubiri mapendekezo yanayotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji kwa maslahi mapana ya SADC na nchi wanachama .

Aidha amesema kuwa ili kuweza kuwa na utalii endelevu ni lazima kuhifadhi mifumo ya ikolojia ya misitu wanyamapori,viumbe vya majini, fukwe,mabonde ya asili,kutokana na ukweli kuwa rasilimali mbalimbali zilizopo za kimazingira,maliasili na utalii,hazitambui mipaka ya kijiografia. 

Waziri waMaliasili na Utalii, Dk Hamis Kingwangala amesema majukumu ya mkutano wa leo ni kuridhia mapendekezo mbalimbali ya kulinda maslahi ya nchi wanachama,ambapo wanatarajia kuangalia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

"Pia tutajadili utekelezaji itifaki ya kuwalida wanyamapori nausimamizi na utunzwaji wa misitu" amesema Kigwangala.Mhe.Kigwangala amesema kuwa Mawiziri hao watapitisha mapendekezo ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana na ujangili na kuhakikisha kunakua na utalii endelevu.

Pia tutaangalia itifaki ya SADC Kuhusu usimamizi wa misitu ,itifaki ya mpango wa maendeleo ya utalii kwa nchi zote.Wanachama wa SADC ni nchi 16 ambazo ni Angola, Botswana, Comoros,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar,Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania,Zambia na Zimbabwe .
Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu akizungumza katika mkutano wa mkutano wa Mawaziri sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara SADC(SADC) uliofanyika jijini Arusha .
Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara SADC(SADC) uliofanyika jijini Arusha .
Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) .


HUKUMU DHIDI YA ALIYEKUWA RAIS TFF JAMALI MALINZI , WENZAKE WATATU KUJULIKANA NOVEMBA 7 MWAKA HUU

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi Blog 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Novemba 7, mwaka 2019 unatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi ya ya inayomkabili aliyekuwa  Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu.

Mbali na Malinzi washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu  Mtendaji wa zamani wa Shirikisho hilo, Celestine Mwesigwa,aliyekuwa mhasibu  Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Mapema leo Oktoba 25, Wakili wa Serikali Ester Martin alidai Mahakani hapo kuwa kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde imekuja kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya hukumu lakini hakimu Kasonde amepata udhuru wa kikazi hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi amesema hukumu dhidi ya washtakiwa hao itasomwa Novemba 7 mwaka huu.

Hukumu hiyo imepangwa kutolewa baada ya washtakiwa hao kumaliza kutoa utetezi wao ambapo walijitetea wenyewe huku upande wa mashtaka ulikuwa na jumla ya mashahidi 15 pamoja na vielelezo 9.

Julai 23 mwaka huu washtakiwa hao walikutwa na kesi ya kujibu aada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi.

Katika kesi  hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa dola za Marekani  173,335.



WANAWAKE WAPEWA MBINU ZA KUSHINDA UCHAGUZI

$
0
0
WANAWAKE wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma waliotia nia ya kugombea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini Tanzania, Novemba 24, 2019 toka vyama vya siasa wamepewa mbinu za kushinda uchaguzi huo kwa wingi na kishindo.

Wanawake 64 wamepewa mafunzo na Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) la Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake waliotia nia katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwa na moto wao wa “Wanawake wakati wa kuongoza ni sasa.’
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (MB), maandalizi ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa yamekamilika kwa kuzingatia kanuni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 Ibara ya 4 (1-3). 

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo toka TGNP, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Bw. Henry Kigodi amesema: TGNP imejikita kusaidia wanawake ambao wametia nia katika kugombea nafasi mbalimbali ili kukidhi hitaji la kupata viongozi wanawake wengi ambao kwa kipindi kirefu hushindwa kufanikiwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa mbinu za kampeni na kukabiliana na mfumo dume. 

Bw. Kigodi alisema wanawake wakipata uongozi huwa makini katika maamuzi, kutekeleza na kusimamia shughuli za kimaendeleo kwakuwa wanawake huwa wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleo katika vitongoji, vijijiji na mitaa yao. “Wanawake ndio wanaohangaika na changamoto za ukosefu wa maji, huduma za afya na Malezi lakini wao ndio hushiriki kwa kiwango kikubwa katika shughuli za uzalishaji mali kama kilimo na hawafaidi matunda yake,” alisema Kigodi.
Mwezeshaji wa Mafunzo Bw. Henry Kigodi akifafanua jambo katika mafunzo 

Naye, mwezeshaji Mwenza Gratiana Rwakibarila, alisema ni vema wanawake wakatambua kuwa wana uwezo mkubwa katika kuongoza jamii na hivyo wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha wanapata mbinu za kushinda nafasi walizoziomba kwa kupewa mafunzo ya kujijengea uelewa wa pamoja juu ya ushiriki katika uchaguzi.
Mwezeshaji Gratiana Rwakibarila akiwa anaeleza namna ya kuboresha mbinu za kampeni 

Vilevile alisema, wanawake lazima wajengewe uelewa wa dhana za jinsia ili kuwawezesha watia nia kuzihusisha na maswala ya uchaguzi, kujadili umuhimu katika ushiriki wa wanawake katika kampeni na uchaguzi. Aidha, Gratiana alisema mafunzo hayo yatawaboreshea mbinu zao za mikakati na mbinu za kampeni wakati wa uchaguzi.

Jumla ya vyama vitano vya siasa vinashiriki mafunzo hayo, vyama hivyo ni ADA- TADEA, CCM, CHADEMA, CUF na TLP. Washiriki wamesisitizwa kuwa wakishinda wayaangalie maendeleo kwa mtazamo wa kijinsia na kupambana na sera potofu za kijinsia.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika vikundi vya mijadala 

EAC SECRETARY GENERAL PARTICIPATES IN RUSSIA-AFRICA ECONOMIC SUMMIT IN SOCHI, RUSSIA

$
0
0
East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko, is participating in the inaugural Russia-Africa Economic Summit which is being held in Sochi, Russia from 23rd to 24th October, 2019. 

During the Summit, Amb. Mfumukeko was a panelist in a session which explored potential cooperation ties between Russia and Regional Economic blocs. 

The Secretary General engaged the participants on the status of integration in the EAC. He informed the forum that EAC has a population of 168.2 million and a combined GDP of US$155.2 billion making it one of the Africa’s fastest growing regional blocs in Africa. 

Amb. Mfumukeko highlighted the key potential areas of cooperation between Russia and EAC saying that there was need for both parties to examine the trading landscape between themselves and optimise what each party can produce for the others’ market. 

“One potential area where the EAC is deficient is the provision of critical services for business and investment in areas like transport, logistics and technicians. Both parties need to explore the existing gaps,” he said. 

The SG said that the EAC economies were still virgin and quite endowed with massive natural resources, adding that Russian investors ought to come to the EAC and explore how to exploit this potential. 

“There is need to organise periodic bilateral traders/investors interactions through visits and trade and investment fairs,” said the SG, adding that the EAC Partner States and Russia should explore the possibility of removing travel restrictions such as travel visas to enhance the movement of persons between both parties. 

Amb. Mfumukeko said that there was need for the EAC Partner States to develop education and youth exchange programmes in addition to exploring the development of the respective languages of each party in the education curricula of the other party. 

The Forum is the first where the rich history of cooperation between Africa and Russia is being re-examined. 

Among those attending the two-day Summit are government officials and members of the business community from both Russia and Africa. The delegates aim to substantively discuss the current status and prospects of cooperation and a wide range of topical issues of the World Economy. 

Russia acknowledges the fact that today African countries are well on their way towards social, economic, scientific and technological development and are playing a significant role in international affairs. Russia further appreciates that African countries are strengthening mutually beneficial integration processes within the African Union which has eight (8) Regional Economic blocs among them the EAC. 

The EAC Partner States’ led by their Heads of State also also participated in the Summit.

RELI TV: SAFARI YA KIHISTORIA YA WASANII YA DAR -DODOMA

WALIMU 1029 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WAHITIMU MAFUNZO YA TEHAMA NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali imeendelea kuwajengea walimu uwezo katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kuimarisha maeneo ya kujifunzia na kuhakikisha shule zinakuwa na vifaa vya kutosha.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika Mikoa yote 31 nchini na Mikoa 5 ya Tanzania bara Profesa. Ndalichako amesema kuwa anathamini sana mchango wa TEHAMA kwa kuwa sayansi na teknolojia kwa sasa vimekuwa chachu ya maendeleo hivyo ubunifu kwa sasa ni lazima utiliwe mkazo zaidi.

" Kwa washiriki 1029 waliopata mafunzo haya katika vituo vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo cha Teknolojia Mbeya wakawe mabalozi kwa walimu katika maeneo yao ya kazi na Serikali imeanza kuwekeza katika vifaa na walimu na wakawe chachu kwa wanafunzi ili somo hilo liwe la lazima mashuleni kutokana na umuhimu wake" ameeleza Prof. Ndalichako.

Aidha amewapongeza Taasisi ya Mawasiliano kwa Wote kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI na Wizara ya Elimu wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu katika kuhakikisha walimu kutoka maeneo mbalimbali wanapata mafunzo hayo.

Pia ameishukuru Serikali ya India kupitia ubalozi wake nchini kwa kujenga kituo cha umahiri cha TEHAMA katika taasisi ya teknolojia (DIT) na katika Chuo cha Nelson Mandela jijini Arusha na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali ili kuwezesha mafunzo kwa walimu laki moja na themanini kote nchini.

Awali akizunguza kuhusu mafunzo hayo Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa. Preksedia Ndomba amesema; huu ni mwaka wa 62 tangu taasisi hiyo ianzishwe na wamekuwa wakitoa wataalamu na mafunzo kwa viongozi wa taasisi mbalimbali wakiwemo maafisa wa jeshi.

Prof. Ndomba amesema kuwa baada ya kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamehitimishwa kwa mtihani wa upimaji matokeo yatatumwa Wizara ya Elimu na Ofisi ya TAMISEMI ambako walipendekeza walimu hao kushiriki mafunzo hayo.

Pia mwakilishi wa walimu 534 katika kituo cha Taasisi ya Teknolojia (DIT) Mwalimu. Anzawe Chaula amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa wamejifunza mada tano ambazo wanaamini zitawasaidia katika taasisi zao wanazofanyia kazi.

" Tumepata ziada ya chaki, tumejifunza kutumia vifaa vya TEHAMA pamoja na kuvifanyia marekebisho pindi vinavyoharibika tunaiomba Serikali itafute wadau zaidi ili tuweze kupata vifaa vya TEHAMA" ameeleza.

Ameeleza kuwa uelewa mdogo waliokuwa nao awali kuhusiana na TEHAMA umepata mbinu mpya ambapo amesema mahusiano bora baina ya shule za Msingi, Sekondari na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) yatazidi kuleta tija zaidi katik sekta hiyo adhimu ya Elimu.





Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na walimu wa shule ya msingi pamoja na washule za sekondali jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha umahiri wa TEHAMA, (ITCOEICT), Daudi Mboma akizungumza na walimu wa shule ya msingi na sekondari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
  Balozi India nchini Tanzania, Sanjiv Kohli akizungumza na waalimu wanafunzi wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam katika vituo mbalimbali,wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari.
Mwalimu Wanzawe Chaula, akisoma Risala wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako. Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)Profesa Preksedia Marco akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT)Profesa Apollinaria Pereka akizungumza na walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam. 


 
Baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi wakipokea vyeti
vya kufunzu kumaliza mafunzo ya TEHAMA wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam katika vituo mbalimbali.


Baadhi ya walimu wa shule za Msingi pamoja na shule za Sekondari walihudhulia mafunzo ya TEHAMA wakiwa katika mkutano wa ufungaji mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo. 

WATENDAJI SEKTA YA MAJI WAASWA KUWA WABUNIFU NA KUCHAPA KAZI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo, akizungumza na wakurugenzi wa mamlaka za maji na watendaji wakuu wa sekta hiyo wakati akifungua mkutano wa uendeshaji wa kisekta mjini Singida leo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Barnabas Ndunguru, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Ewura, Lawrence Sawe na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maji, Adam Karia.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga (kushoto),akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo baada ya kufungua mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano huo.
 Watendaji wakuu wa Sekta ya Maji nchini wakifuatilia mada katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Watendaji wakuu wa Sekta ya Maji nchini wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo amewataka watendaji  wa mamlaka za maji nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe wabunifu ili kukuza mapato ya sekta hiyo.

Aliyasema hayo  alipokutana na wakurugenzi wa mamlaka za maji na watendaji wakuu wa sekta hiyo wakati akifungua mkutano wa uendeshaji wa kisekta mjini Singida leo. 

" Zamani mamlaka za maji zilikuwa zikitoa huduma lakini sasa hivi zinaendelea kutoa huduma na pia ujenzi wa miradi ya maji haya ni mabadiliko makubwa sana kisekta hivyo zingatieni ubunifu katika utendaji wenu" alisema Mkumbo.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo kuna kila sababu ya kupitia muundo mpya wa utumishi kuanzia ngazi ya wizara na taasisi ili kuiweka katika mifumo inayoeleweka.

Alisema kupitia mfumo huo mpya itasaidia taasisi husika kuweza kuchagua wahandisi wenye viwango stahiki kukidhi matarajio ya miradi kwa ufanisi.
"Tunakusudia kuanza kuzingatia vigezo ikiwemo kuangalia ni mradi gani apewe mkandarasi kulingana na sifa na uwezo alionao kuweza kusimamia mradi husika" alisema.

Mkumbo alisisitiza kuwa yote hayo yatawezekana kama kutakuwepo na ushirikiano wa dhati baina wa watendaji wa sekta ya maji na wadau wote kwa ujumla.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images