Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

WAZIRI KWAMWELWE AONYA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akipata maelezo kwenye banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mda mfupi kabla ya Kufungua Mkutano  Mkuu wa  Mwaka wa Taifa, Uliohushisha Wadau wa TEHAMA  Nchini  kutoka Serikalini,  Mashirika na Makampuni binafsi Jijini Dar Es Salaam, tarehe 24 Oktoba 2019. Mhe. Kamwelwe alionya watu wenye Uelewa wa TEHAMA kutotumia vibaya ufahamu wao, kwa kuposti taarifa za uzushi na uchochezi zinaweza kuhatarisha Usalama na Amani ya nchi. Alionya, wahusika wote hawatakwepa mkondo wa sheria. (Picha na TCRA).

Wasafirishaji bidhaa za kilimo, chakula nje wapatiwa elimu

0
0
  Wafanyabiashara wasafirishaji wa bidhaa za chakula na kilimo Kanda ya pwani wakifuatilia ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na TBS, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapatie elimu ya kusafirisha mazao hayo nje ya nchi bila vikwazo vya kibiashara.
 Picha na Chalila Kibuda

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA wanaosafarisha bidhaa za mazao ya kilimo na chakula katika Kanda ya Pwani kwenda nchi za nje wamepatiwa elimu kuhusiana na taratibu za usafirishaji wa mazao hayo pasipo kukumbana na vikwazo vya aina yoyote.

Awali wafanyabiashara hao walikuwa wanapata huduma hiyo kutoka kwa iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), lakini baada ya majukumu hayo kuhamishiwa kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), shirika hilo imebidi liwaandalie semina kwa lengo la kuwapa utaratibu ambao inabidi waufuate.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, Mkurugenzi upimaji ugezi wa shirika hilo, Mhandisi Johanes Maganga, alisema madhumuni ya semina hiyo ni kuwaelimisha kuhusiana na utaratibu wa usafirishaji bidhaa hizo unavyofanyika.

Alisema mzalishaji akishazalisha mazao yake anayotaka kusafirisha nje ya nchi, wao TBS wanamsaidia aweze kufanya biashara yake kwa urahisi bila vikwazo vyovyote.

"Kwa hiyo sisi kama shirika tuna kituo cha kuwahudumia hawa wafanyabiashara wanaopeleka bidhaa nje ya nchi kwa maana kwamba tuna taarifa zote za kule ambapo bidhaa zinakwenda, hivyo msafirishaji au mfanyabiashara akija pale tunaweza kumpa taarifa za kile kinachotakiwa na kila nchi, bidhaa inatakiwa iwe na kiwango gani.

Tunampimia bidhaa yake na kumpa cheti cha ubora kwa bidhaa ile ambayo anaipeleka," alisema Mhandisi Maganga na kuongeza;

"Akifika kule anakoipeleka na bidhaa ikawa na ile nyaraka ambayo inathibitisha kwamba imeishapimwa na TBS inakuwa ni rahisi bidhaa yake kuaminiwa inakokwenda."

Alisema wanafanya hivyo kwa lengo la kumrahisishia mfanyabiashara kufanya shughuli zake, aweze kufuata taratibu za usafirishaji bidhaa nje ya nchi kiurahisi.

Alifafanua kwamba kabla ya hapo wafanyabiashara walikuwa hawajui zile taratibu zinazotakiwa, kwa hiyo walikuwa wakipata shida. 

"Kwa hiyo tumewaita hapa pamoja, tukae nao tuwaeleze ni jinsi gani ya kufanya biashara, watueleze matatizo na changamoto zinazowakabili na sisi tuwaambie jinsi ya kuweza kutatua hizo changamoto katika kusafirisha bidhaa kwenda nje," alisema Mhandisi Maganga.

Alipoulizwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo  wafanyabiashara hao, Mhandisi Maganga alijibu kuwa ni pamoja na  kutokuelewa taratibu, hivyo kama mtu anataka kusafarisha bidhaa kwenda nje kama haelewi hizo taratibu anakuwa na mkwamo fulani kwenye hiyo biashara.

"Kwa hiyo baada ya hii semina itakuwa ni rahisi sana mtu kufuata utaratibu, anaweza kusafirisha biashara zake kwenda nje kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni," alisema.

Alisisitiza kuwa kabla ya bidhaa kusafirishwa kwenda nje, lazima ipimwe na ijulikane ubora wake na wanatumia vile viwango vya nchi ambako bidhaa husika inakwenda.

Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, Mhandisi Maganga alisema wana soko la pamoja ambapo wameoanisha viwango, kwa hiyo bidhaa ikishapimwa Tanzania na ikapewa alama ya ubora na TBS, kwenye soko la Afrika Mashariki inaweza kwenda popote, hakuna anayeweza kuitilia shaka.

"Lakini ikienda nje ya Afrika Mashariki tunahitajika kuzipima hizo bidhaa kwa viwango vya nchi zinakokwenda kwa sababu taarifa zote ambako zinapelekwa tunakuwa nazo sisi," alifafanua Mhandisi Maganga na kuongeza;

"Tunaweza kumwambia mzalishaji ni kitu gani afuate ili kuondokana na vikwazo."   Kuhusu upimaji wa ubora wa asali, alisema shirika hilo linafanyakazi hiyo na kwamba zipo kampuni ambazo zimepewa leseni ya ubora na zinafanyabiashara ya kupeleka asali nje, hazipati matatizo yoyote.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa TBS, Gervas Kaisi, alisema lengo la kuwaita wasafirishaji wa bidhaa za kilimo na chakula ni baada ya mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 ambayo imeongezea TBS majukumu katika masuala ya usalama ya chakula na vipodozi kutoka iliyokuwa TFDA.

"Kwa hiyo katika miezi hii mitatu kunakuwa na hiyo sintofahamu ya wafanyabiashara wanaoshughulika na hayo mazao ya kilimo na chakula, tumeona ni vema tukaitisha semina ili tukatoa uelewa wa pamoja ili walio wengi hawa waweze kupeleka hiyo elimu namna gani iliyo rahisi kuweza kuthibitisha bidhaa zao za mazao ya chakula na kilimo na namna gani wanaweza kusafirisha mazao hayo  kwenda nje ya nchi," alisema Kaisi.

MUUZA MATUNDA AIONA NDOTO YAKE YA KUFUNGUA DUKA LA VIFAA VYA UMEME

0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya ubashiri wa Matokeo ya mechi mbalimbali Gal's sport betting nchini akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi hundi ya fedha kwa mshindi aliepatikana kwenye ubashiri wake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ubashiri wa Matokeo ya mechi Gal's sport betting nchini Hakan Aric akimkabidhi hundi ya fedha  shillingi 100,000,000 Mshindi aliebatikana kwenye ubashiri wake Juma yusuph Kadoga mkazi wa chamazi jijini Dar es salaam
       
     Na. Khadija seif, Michuzi TV
MUUZA matunda Juma  Kadoga awashauri vijana kutokata tamaa na kuwa imani juu ya matokeo chanya wakati wa kufanya ubashiri wa michezo.

Juma ambae ni kijana  mwenye miaka 30 mkazi wa chamazi jijini Dar es salaam mwenye asili ya Tanga anaeishi na mke pamoja na watoto wanne.

Aidha ,Juma ameeleza kuwa Hali ya maisha kiuchumi si nzuri sana kutokana na mahitaji mengi ya kifamilia yakiongezeka siku hadi siku.

"Watoto wanne wanahitaji chakula,mavazi pamoja na kwenda shule ambapo pia fedha kwa kiasi kikubwa hutumika ili kukidhi mahitaji yao na ya nyumbani  kwa ujumla,"

Pia ameshukuru Kampuni ya  ubashiri wa matokeo ya mechi mbalimbali  Gal sport betting kwa kubadilisha maisha yake kwa kumpatia fedha za kitanzania 100,000,000.

"Nina furaha kubwa kuwa  mshindi  wa kiwango cha fedha Kama hiko na fedha nilizozipata nitazitumia kuwasaidia wazazi wangu walioko Tanga ili nipate baraka zao Kwanza kabla ya kuanza kutafakari ni kwa namna gani nitazitumia fedha zangu za ushindi,"

Hata hivyo Juma anafafanua kuwa maisha yalimpelekea kupoteza ndoto yake ya kujishughulisha na uuzaji wa vifaa vya umeme Jambo ambalo kwa sasa ataweza kulifanikisha kupitia fedha alizozipata

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya ubashiri wa matokeo Hakan Aric amesema mshindi huyo amejishindia kitita cha shillingi Milioni mia moja za kitanzania.

''Viwango vyetu vya ubashiri ni ya Hali ya juu nchi nzima,hata hivyo tutaongeza bidhaa zaidi kwenye wasifu ili kuongeza burudani Jambo litakalo panua wigo wa ushindi kwa wateja wetu".

AFRICA'S PREMIER ANNUAL TRADE FAIR

WIZARA YA MAJI, BENKI YA DUNIA KULIPANA KWA MATOKEO YA KAZI MRADI MPYA WA MAJI

0
0
Mratibu wa Mradi Mpya wa Maji Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Doris Mulashani, akifungua warsha ya mafunzo ya uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa mradi utakaokwenda sambamba na malipo kutokana na matokeo chanya ya kazi uendelevu, usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini.
Mwakikishi wa Benki ya Dunia katika warsha hiyo, Toyoko Kodama akiwasilisha mada.
Wadau wa maji wakiwa katika warsha hiyo.
Majadiliano yakiendelea katika warsha hiyo.
Majadiliano katika makundi yakiendelea. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

BENKI ya Dunia imetenga dola za marekani milioni 350 zitakazotumika kulipia ujenzi mpya wa mradi wa maji utakaokwenda sambamba na malipo kulingana na matokeo ya kazi (PforR).

Hayo yalielezwa jana na mratibu wa mradi huo, Mhandisi Mashaka Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya mafunzo ya uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa mradi huo inayofanyika mjini Singida.

"Tayari sh.166 bilioni zimekwisha tolewa kama mbegu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu kwa mikoa 17 na halmashauri za miji 86" alisema Sitta.Alisema tayari wameanza kutoa mafunzo ya uelewa wa pamoja kwa watendaji ili kukidhi vigezo vya namna ya kupata fedha hiyo na utekelezaji wa mradi huo kwa ufanisi.

Alisema mafunzo hayo wameanza kuyatoa katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Singida na wanatarajia kwenda Mwanza lengo likiwa ni kuelewa viashiria na mahitaji ya mradi.

Sitta alisema kila wilaya wanatarajia kupeleka sh.1. 36 bilioni na kuwa kila mwaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itafanya tathmini ya utekelezaji wa mradi huo."Azma iliyopo pamoja na mambo mengine ni kutatua kabisa changamoto za maji, elimu na afya hapa nchini" alisema Sitta.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AWATAHADHARISHA WATANZANIA KUHUSU MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

0
0

Baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kubatilisha vifungu vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18. jana  October 24, 2019 Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) uliofanyika Jijini Dodoma amesihi Watanzania kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za ndoa na mimba za utotoni.

“Watu wote tungependa ile Hukumu ya ilivyotoka tu, yaani watu miaka 18 ndio waanze kufikiri ndoa. Sote tunafahamu hata miaka 18 sio kwamba ndio yupo tayari kwa ajili ya ndoa lakini niwaombe sisi tuendelee kuweka mkazo kwenye mafunzo kwa vijana wetu wenye umri mdogo kwamba hata ile miaka 18 yeye haimtoshi kuanza kubeba familia ili pamoja na haya mengine tusianze sasa tumemaliza la ndoa za utotoni tunajikuta tunaendeleza mimba za utotoni”

“Kwa maana hivi ni vitu viwili tofauti japokuwa kuna mahali huwa vinakutana. Ndoa za utotoni zinapelekea mimba za utotoni lakini sio mimba zote za utotoni zinasababishwa na ndoa za utotoni”-Dkt. Tulia Ackson

WAKANDARASI WALIOLETA "JANJAJANJA" MIRADI YA UJENZI DAR WAKAMATWA NA POLISI KWA AGIZO LA RC MAKONDA.

0
0
Wakandarasi wa Kampuni za CHICCO Engineering na Nyanza Road Work wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa kosa la Kushindwa kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Mto Ng'ombe na Barabara ya Kivule kwa wakati na kuleta usumbufu Mkubwa kwa wananchi ukiwemo wa Mafuriko, Nyumba Kubomoka, Uharibifu wa Mali, Ajali na Magari kuharibika huku wakandarasi hao wakila Maisha mitaani. 

Kwa mujibu wa RC Makonda Mkandarasi wa  Kampuni ya CHICCO amekamatwa kwa kushindwa kuanza Mradi wa ujenzi wa Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ambapo licha ya Kusaini Mkataba Mkandarasi huyo hajaanza kazi kwa zaidi ya Miezi minne na hadi sasa amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni 4.8 huku wananchi wakiteseka na kero ya Mafuriko.

RC Makonda amesema jambo hilo ni uzembe na hujuma inayoweza kuchonganisha Wananchi na Serikali yao ambayo tayari imetoa fedha za ujenzi wa Mto huo ili kuwaondolea kero lakini Mkandarasi amekuwa akisuasua kuanza kazi.

Kwa upande wa Kampuni ya Nyanza RC Makonda ameagizwa kukamatwa kwa Mkandarasi huyo kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kivule na Daraja licha ya Kupokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 800 jambo linalopelekea wakazi wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa Barabara na wakati mwingine kusababisha Ajali na Kuharibika kwa Vyombo vya usafiri.

Kwa Maelekezo ya RC Makonda Wakandarasi hao waliokamatwa watakuwa Wakilala Polisi Central na asubuhi watatokea polisi kwenda kufanya kazi ya Ujenzi hadi hapo atakapojiridhisha kuwa kazi inaenda vizuri huku akieleza kuwa zoezi hilo la ukamataji litakuwa endelevu kwa Wakandarasi wote wanaokwamisha miradi ya serikali.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO IJUMAA 25,2019


MASHINDANO YA MAJESHI YA DUNIA NCHINI CHINA: WANARIADHA FARAJA NA DAMASI WATINGA FAINALI MITA 5000, MAGDALENA AKWAMA

0
0

Wanariadha kutoka Tanzania Faraja Damas na Joseph Panga wamefuzu kuingia fainali ya Mita 5000 katika mashindano ya majeshi ya dunia yanayoendelea nchini China huku akiwapita wanariadha wengine 47.

Faraja alishika nafasi ya kwanza baada ya kukimbia kwa dakika 14:39.24 huku akiwaacha nyuma wakimbiaji wengine katika kundi la pili la wakimbiaji waliokuwa wakisaka nafasi ya kuingia fainali.
Hata hivyo siku ilikuwa Njema kwa mwanaridha Joseph Panga baada ya  kufuzu katika hatua ya Fainali baada ya kukimbia nafasi ya sita  kwa dakika 14:10.47 ambazo zilizidi mshindi wa kundi la kwanza na kupata nafasi kuingia fainali.
 Katika kundi la kwanza Mkenya Peter Ndegwa aliongoza baada ya kukimbia kwa dakika 14:04.67 na kufanikiwa kutinga fainali huku akiwa na kibarua cha kukabiliana na wanaridha wengine 14 waliofuzu mbio za Mita 5000 kOktoba 26 ili kumpata mshindi wa kwanza wa pili na watatu .

Wakati huo Mwanariadha Private Magdalena Shauri aliyeshinda mashindano ya afrika mashariki ya majeshi ameshindwa katika fainali za mbio za Mita 5000.

Sasa   huku wanariadha wa Marathoni wakiongozwa na Private Felix Simbu wakitarajiwa kukimbia tarehe 27. Wakati huo huo bondia selemani kidunda ametolewa katika hatua ya robo fainali baada mpambano mkali ambapo kidunda alipambana muda wote na kumrushia mpinzani wake makonde mazito. Hata hivyo mpaka mwisho wa Mpambano Kidunda alipata pointi 26 huku mpinzani wake Ghousoon Ahmad wa syria akipata pointi 30 na kutangazwa mshindi baada ya maamuzi ya majaji wote watano.

EAC SECRETARY GENERAL PARTICIPATES IN RUSSIA-AFRICA ECONOMIC SUMMIT IN SOCHI, RUSSIA

0
0


                                                                EAC Secretariat

East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko, is participating in the inaugural Russia-Africa Economic Summit which is being held in Sochi, Russia from 23rd to 24th October, 2019.

During the Summit, Amb. Mfumukeko was a panelist in a session which explored potential cooperation ties between Russia and Regional Economic blocs.

The Secretary General engaged the participants on the status of integration in the EAC. He informed the forum that EAC has a population of 168.2 million and a combined GDP of US$155.2 billion making it one of the Africa’s fastest growing regional blocs in Africa.

Amb. Mfumukeko highlighted the key potential areas of cooperation between Russia and EAC saying that there was need for both parties to examine the trading landscape between themselves and optimise what each party can produce for the others’ market. 

“One potential area where the EAC is deficient is the provision of critical services for business and investment in areas like transport, logistics and technicians. Both parties need to explore the existing gaps,” he said.

The SG said that the EAC economies were still virgin and quite endowed with massive natural resources, adding that Russian investors ought to come to the EAC and explore how to exploit this potential.

“There is need to organise periodic bilateral traders/investors interactions through visits and trade and investment fairs,” said the SG, adding that the EAC Partner States and Russia should explore the possibility of removing travel restrictions such as travel visas to enhance the movement of persons between both parties.

Amb. Mfumukeko said that there was need for the EAC Partner States to develop education and youth exchange programmes in addition to exploring the development of the respective languages of each party in the education curricula of the other party.
The Forum is the first where the rich history of cooperation between Africa and Russia is being re-examined.

Among those attending the two-day Summit are government officials and members of the business community from both Russia and Africa. The delegates aim to substantively discuss the current status and prospects of cooperation and a wide range of topical issues of the World Economy.

Russia acknowledges the fact that today African countries are well on their way towards social, economic, scientific and technological development and are playing a significant role in international affairs. Russia further appreciates that African countries are strengthening mutually beneficial integration processes within the African Union which has eight (8) Regional Economic blocs among them the EAC.

The EAC Partner States’ led by their Heads of State also also participated in the Summit.

 East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (right), participating in the inaugural Russia-Africa Economic Summit which  in Sochi, Russia 
 East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (right), speaks when participating in the inaugural Russia-Africa Economic Summit which  in Sochi, Russia 

WAZIRI KABUDI AONGOZA MAADHIMISHO YA 74 YA SIKU UMOJA WA MATAIFA Posted: 24 Oct 2019 03:46 PM PDT

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini alipowasili katika uwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma kushiriki maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama sehemu maalumu wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa unapigwa kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa mbele ya parede maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua parede maalumu liliondaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja Mataifa 
Sehemu ya hadhara iliyojitokeza katika uwanja wa Nyerere Square kushuhudia sherehe za maadhimisho 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) akifuatalia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akipokea zawadi kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini iliyowasilishwa na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi, kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika jijini Dodoma 
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi Wafanyakazi wa Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia  hadhira iliojitokeza kwenye maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia  hadhira iliojitokeza (hawapo pichani) kwenye amaadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square


WAKATI HUO HUO MHE. PROF. KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA  BW. MICHAEL DUNFORD KAIMU MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akiwa na Bw.Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa
Mataifa nchini, walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wengine ni Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Bi.Glory Ngaiza Afisa Mambo ya Nje.
Waziri Mhe. Prof. Kabudi akilelezea jambo wakati wa mazungumzo na Bw. Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa Mataifa nchini. Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa


VILEVILE WAZIRI MHE. PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisisitiza jambo alipokutana wakati wa mazunguzo na Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha ushiririkiano kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma

RELI YAANZA KUTANDIKWA KIPANDE CHA MOROGORO-MAKUTUPORA, HANDAKI LA SGR SASA NI ZAIDI YA MITA 700

KAMISHNA WA POLISI LIBERATUS SABAS AKISIKILIZA KERO NA MALALAMIKO YA WANANCHI KASULU

0
0
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP Liberatus Sabas, akiwa na maafisa kutoka Makao Makuu ya Polisi pamoja na Kamanda wa Mkoa wa Kigoma ACP Martin L. Otieno Wamewasili katika Wilaya ya Kasulu mkoani humo kwaajli ya kusikiliza malalamiko ya wananchi pamoja wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko la Sophia, kutokana na kuwepo na wahalifu wanaotumia wilaya kama njia ya kuvushia silaha kutoka nchi za jirani, ila wengine hushirikiana na waharifu kutoka nchi za jirani kuja wilayani hapo na kufanya uhalifu wao kisha kukimbilia  nchi za jirani kama vile Burundi na Rwanda.
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP Liberatus Sabas, akiwa na maafisa kutoka Makao Makuu ya Polisi pamoja na Kamanda wa Mkoa wa Kigoma ACP Martin L. Otieno Wamewasili katika Wilaya ya Kasulu mkoani humo kwaajli ya kusikiliza malalamiko ya wananchi pamoja wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko la Sophia, kutokana na kuwepo na wahalifu wanaotumia wilaya kama njia ya kuvushia silaha kutoka nchi za jirani, ila wengine hushirikiana na waharifu kutoka nchi za jirani kuja wilayani hapo na kufanya uhalifu wao kisha kukimbilia  nchi za jirani kama vile Burundi na Rwanda.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP Liberatus Sabas, akiwa na maafisa kutoka Makao Makuu ya Polisi pamoja na Kamanda wa Mkoa wa Kigoma ACP Martin L. Otieno Wamewasili katika Wilaya ya Kasulu mkoani humo kwaajli ya kusikiliza malalamiko ya wananchi pamoja wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko la Sophia, kutokana na kuwepo na wahalifu wanaotumia wilaya kama njia ya kuvushia silaha kutoka nchi za jirani, ila wengine hushirikiana na waharifu kutoka nchi za jirani kuja wilayani hapo na kufanya uhalifu wao kisha kukimbilia  nchi za jirani kama vile Burundi na Rwanda.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

Serikali, SIDA, Unesco waanza maandalizi ya ripoti ya kitaifa uanuai wa kitamaduni

0
0
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Utamaduni, Elimu, Utamaduni na Sayansi la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wamezindua mafunzo ya kuandaa ripoti ya kitaifa ya Mkataba wa UNESCO wa mwaka 2005.

Mkataba huo ambao serikali ya Tanzania umetia saini mwaka 2011 unazungumzia kulinda na kuendeleza uanuai wa kujieleza kiutamaduni.
Kwa mujibu wa matakwa ya mkataba huo kila baada ya miaka mine mataifa yanayotakiwa kuandika taarifa kuelezea utekelezaji wa mkataba huo. Mengi ya mataifa ikiwamo Tanzania haijawahi kuandika  taarifa hiyo.

Kwa kawaida taarifa hiyo ni mchanganyiko wa taarifa za serikali na wadau wengine wakiwemo wa taasisi zisizo za kiserikali (AZAKI).
Fedha za kufanyia mafunzo hayo na kuandika taarifa zimetolewa na Sweden kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (SIDA) chini ya uratibu wa UNESCO.
Taarifa hiyo ikishakamilika inatarajiwa kujadiliwa na wadau na kupelekwa serikalini ambako nako itapitiwa na kufikishwa UNESCO.

Akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini Dk. Kiagho Kilonzo, alisema kwa sasa Tanzania ipo tayari kwa taarifa hiyo ndio maana imeunda kamati na kuanza mafunzo.
Kamati hiyo ya kuandika Ripoti inaongozwa na Robert Mwampembwa ambaye ikisimamiwa na Doreen Sinare, Ofisa mtendaji Mkuu wa COSATA ambaye ndiye mtaalamu wa mradi.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden nchini Andres Sjoberg, ufadhili wa taifa hilo kwa nchi 16 zinazotakiwa kuandika utekelezaji wa mkataba huo umelenga kuhakikisha kuwa kuna uhuru wa wasanii kujieleza kiutamaduni na hasa wanawake.
Alisema kwa sasa dunia sio kijiji bali kutokana na mifumo ya upashanaji wa habari kuzidi kuimarika dunia imekuwa ni moja na hivyo masuala ua kujieleza yanabaki kuwa wazi kila mahali.

Naye Dk. Harrison Mwakyembe alisema kwa sasa Tanzania iko vizuri kutokana na kuridhia mkataba huo wa 2005 ambao lengo lake kubwa ni kutengeneza fursa kwa wasanii kuwa karibu na soko la dunia.
Aidha alisema kwamba nia kubwa ya makubaliano hayo ni kulinda uanuai wa kujieleza kiutamaduni na hivyo kutengeneza mazingira ya kukua kwa utamaduni kwa manufaa ya watu wote.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe ni matarajio yake kwamba ifikapo Aprili mwakani taarifa hiyo itakuwa imekamilika na tayari kutumika na tasnia ya utamaduni na ubunifu na dunia pia.
Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Dar es Salaam, Tirso Dos Santos,  alisema kwamba taarifa ya Tanzania itaunganishwa na mataifa mengine ili kuelezea dunia inavyoendelea katika kutekeleza matakwa ya mkataba.

"Sote tunajua kwamba Tanzania ni kitovu cha ubunifu na hasa kwa kuwa na matamasha mbalimbali hali inayodhirisha umuhimu wa mradi huu kwa ajili ya maendeleo maendelevu ", alisema mwakilishi huyo wa UNESCO ambapo aliyataja matamasha makubwa ya filamu nchini ikiwamo ya ZIFF na Azam kama moja ya uanuai wa utamaduni.
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos mara baada ya kuwasili kwenye warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg.
 Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA ambaye pia ni Mtaalamu wa Taifa wa mradi unaolenga kutekeleza makubaliano ya UNESCO ya mwaka  2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Tamaduni Anuwai, Bi. Doreen Sinare akitambulisha meza kuu (hawapo hewani) wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa salamu za UNESCO wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg akitoa salamu za SIDA wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA na Mtaalamu wa Taifa wa mradi unaolenga kutekeleza makubaliano ya UNESCO ya mwaka  2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Tamaduni Anuwai, Bi. Doreen Sinare cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi  Bw. Maximilian Chami kutoka Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco) cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Meneja wa Programu wa Taasisi ya Culture and Development East Africa (CDEA), Bw. Mandolin Kahindi cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi kutoka COSOTA Bw. Zephania Lyamula cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (katikati) akimkabidhi Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Mwamini Mohamed cheti cha ushiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO kwa ufadhiliwa wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa Sweden nchini Mh. Andres Sjoberg (kushoto) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kulia).
Baadhi ya washiriki wakiwasilisha kazi za vikundi wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wa sekta ya Ubinifu, Utamaduni na Sanaa katika uandaaji wa taarifa ya kitaifa ya makubaliano ya UNESCO ya mwaka 2005 ya Ulinzi na Ukuzaji wa Vielelezo vya Utamaduni Anuwai iliyoratibiwa na UNESCO na kufadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) iliyofanyika kwenye Hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.

MBUNGE DITOPILE AAHIDI MIFUKO 50 YA SARUJI KUMALIZA UJENZI WA UZIO SEKONDARI YA DODOMA

0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZAZI nchini wametakiwa kushirikiana na Walimu ili kuweza kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni na siyo kuacha kila kitu kufanywa na walimu.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Taifa anayewakilisha vijana (UVCCM), Mariam Ditopile kwenye mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.

Amesema jukumu la wazazi siyo kununua mahitaji ya mtoto tu bali anapaswa kufuatilia maendeleo yake ya kitaaluma na nidhamu na siyo kuwaachia walimu jukumu hilo peke yao.

" Ndugu zangu wazazi jukumu lenu siyo kununua tu sare za Shule na vifaa vingine, fuatilieni maendeleo ya hawa vijana hapa katikati muda ambao wanaenda na kurudi shule. 

Hakuna mtoto anaezaliwa bila akili, wote hawa wana akili tena nyingi sana. Ni jukumu letu sisi wote wazazi, wadau na walimu kulinda uwezo wa watoto wetu, tuhakikishe wanapata elimu na kufuatilia maendeleo yao. Tusiruhusu mitaa ikalea watoto wetu, tukisharuhusu hali hiyo mjue ni ngumu kupata ufaulu Mzuri," Amesema Ditopile.

Akizungumzia changamoto ya maji na uzio katika Shule hiyo Mhe Ditopile ameahidi kutoa mifuko 50 ya Saruji pamoja na Tenki kubwa la kuhifadhia Maji ndani ya Siku tatu ujenzi wa uzio uwe umeshaanza ambapo yeye mwenyewe pia atatafuta nguvu kazi ya kuja kujenga.

Amesema ni jukumu lao kama wasaidizi wa Rais Dk John Magufuli kumsaidia katika changamoto nyingine na wala siyo kukaa na kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu ilihali wao wenyewe wanaweza kuhamasishana na kumaliza changamoto hizo.

Kuhusu kiwango cha ufaulu shuleni hapo, Mbunge Ditopile ameonesha kukerwa na matokeo ya miaka mitatu ya nyuma ambapo kiwango cha daraja la nne na sifuri kilikua kikubwa kulinganisha na madaraja ya ufaulu.

" Hapa kwenye ufaulu kwa kweli siridhishwi napo, Dodoma Sekondari iko katikati ya Jiji tena Makao Makuu ya Nchi hamuoni tunajipa aibu hii? Hapa hakuna changamoto ya walimu wala vifaa ya kufundishia, kila kitu kipo sasa tatizo ni nini?

Kitendo cha kushindwa kufuta zero shuleni kwetu hapa ni kujinyima fursa za kimaendeleo ambazo Serikali inazileta Dodoma. Fursa kubwa ya elimu ipo Dodoma ni wakati wetu wa kuamka na kujipanga ili kumaliza changamoto hii," Amesema.

Amewataka wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kutuliza akili watakapoingia kwenye vyumba vya mtihani ili waweze kufanya vizuri ili kumuunga mkono Rais Magufuli ambaye amewalipia ada kwa miaka yote minne ya masomo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Father Chesko Kusaga ameishukuru Serikali kwa kuendelea kufanya uwekezaji kwenye sekta ya elimu ambapo tayari walishapokea kiasi cha Shilingi Milioni 900 kwa ajili ya maboresho ya elimu.

" Mhe mgeni rasmi tunakuahidi kuwa tutafuta hizi zero, mwaka huu tumejipana kuhakikisha Dodoma Sekondari kweli inabeba taswira ya Makao Makuu ya Nchi kwa kufanya vizuri kwenye elimu. Hatutomuangusha Rais wetu katika hili.

Lakini pia tuishukuru Wizara ya Elimu kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha maendeleo ya Shule yetu, Tulipokea kiasi cha Shilingi Milioni 195 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na mabweni mawili. Pia tunaishukuru Halmashauri ya Jiji kwa kutupatia Shilingi Milioni 120 za ujenzi wa mabweni," Amesema Father Kusaga.
 Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile akimkabidhi vyeti na kiasi cha fedha Shilingi 50,000 mwanafunzi bora katika Shule ya Sekondari Dodoma, Ludovick katika mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
 Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana, Mariam Ditopile akizungumza na wanafunzi, wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari Dodoma kwenye mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Dodoma Sekondari, Father Chesko Kusaga akizungumza katika mahafali hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma wakimsikiliza, Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile ambaye alikua Mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.

BILIONI 10 ZATENGWA KWA AJILI YA UJENZI WA CHUO CHA UFUNDI CHATO

0
0
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akicheza muziki na baadhi ya viongozi wa Chato wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa elimu(hawapo pichani) waliohudhuria sherehe za  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Chato


Wizara ya Elimu, Sayansi na  Teknolojia imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10.7 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa chuo hicho, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema ujenzi wa chuo huo unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani.

"Nawapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chato kwa usimamizi mzuri kwani mpaka sasa mradi huu umefikia asilimia 78 huku mkandarasi akiwa ameshalipwa asilimia 41 ya pesa yote  jambo linaloonyesha kwamba kuna fedha itabaki ambayo itasaidia kuongeza majengo mengine," amesema Waziri Ndalichako.

Aidha, Waziri Ndalichako amewataka Wakandarasi na Washauri Elekezi wanaofanya kazi za Wizara ya Elimu kuwa wazalendo na kuacha kuongeza gharama za miradi inayotekelezwa na wizara hiyo.

"Tumegundua katika mikataba mingi malipo ya washauri elekezi yanalipwa kulingana na kiwango anacholipwa mkandarasi hivyo kufanya mkandarasi  kuongeza gharama na kutokukagua vizuri miradi hiyo," ameelezea Profesa Ndalichako.

Waziri huyo amesema Wizara inafanya mapitio hata kwa miradi iliyoishakamilika  ili kujiridhisha na gharama halisi za utekelezaji na kuwezesha kutoa fedha zinazolingana na gharama na kuhakikisha miradi inakamika kwa viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema ujenzi wa chuo hicho cha kipekee mkoani humo ni mwendelezo wa mageuzi makubwa yanayoshuhudiwa katika sekta ya elimu kwa kipindi cha uongozi wa serikali ya Awamu ya Tano.

"Chuo cha VETA Chato kitakuwa cha kwanza chenye ubora wa juu katika kanda ya ziwa kwa kuwa ni kikubwa  na kitakuwa na  karakana zenye vifaa vya kisasa ambavyo vitawezesha vijana wa Chato kuwa na ujuzi na maarifa," amesisitiza Mhandisi Gabriel.

Aidha, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameishukuru serikaki kwa kujenga chuo hicho na kuahidi kuhakikisha anahamasisha vijana wa Chato kujiunga katika chuo hicho ili kupata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda.

Kalemani amemuomba mkandarasi wa mradi huo kuongeza vijana wa Chato katika mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na hatimaye mafunzo yaanze kutolewa Januari 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu amesema mradi wa ujenzi chuo hicho ni miongoni mwa miradi 40 ya ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi pamoja na upanuzi wa vyuo vilivyopo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya kuongeza upatikanaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi na hatimaye kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 200,000 ya mwaka 2016/17 hadi 700,000 ifikapo mwaka 2020.

"Mradi huu na mingine kama hii inayotekelezwa nchini inachangia utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kuwa vijana wanapata ujuzi stahiki utakaowawezesha kuajiriwa  au kujiajiri ili kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa viwanda," amesisitiza Bujulu.

Akitoa taarifa ya Mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya ziwa, Michael Ikongoli amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo 27 ambayo ni pamoja na madarasa, karakana, nyumba 4 za walimu, bwalo la chakula, jengo la utawala na kwamba samani zote za Chuo hicho zitatengenezwa na Chuo cha VETA Mwanza kwa gharama ya shilingi milioni 693.

MWINGEREZA AWATAKA MASHABIKI, WASANII NA WADAU KUTHAMINI VYA KWAO.

0
0
   
     Na.Khadija seif, Michuzi TV

WAANDAAJI wa filamu nchini wametakiwa kuongeza ufanisi na ujuzi katika kazi zao ili kuboresha na kuingia ushindani katika soko la kimataifa la filamu.

Akizungumza na Michuzi tv Katibu Mtendaji wa Baraza la sanaa nchini (BASATA) Godfrey Mwingereza amesema China imekua nchi yenye ushindani katika kutengeneza filamu zenye ubora kuanzia wachezaji, picha mnato,kiwango cha picha kwa ujumla .

"Ni wazi kwa sasa nchi ya China imekua ikijizolea mashabiki siku hadi siku na kutokana na tamthilia zao kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili inaleta ushawishi na chachu ya kutazama tamthilia hiyo kwa mfano Maododo ilikua ni tamthilia yenye mashabiki wengi nikiwemo mimi mwenyewe,"

Hata hivyo amewapongeza Kampuni ya startimes kwa kuandaa hafla hiyo fupi na kuwaleta nchini wasanii kutoka China waliogiza kwenye tamthilia ya ode to Joy iliyowekwa sauti kwa lugha ya sauti ikiongezwa na mwanadada Andy.

"Hafla Kama hizi ni mojawapo ya fursa kwetu ili kuendelea kujifunza vingi kutoka kwenye tamaduni za wenzetu kwani wanaonyesha jinsi gani wanavothamini wasanii wao na utamaduni wao kwa ujumla, kwani wamejitokeza wachina wengi ukumbini kuwaona wasanii hao hiyo ni dalili tosha ya kuonyesha uthamini wa vya kwao,"
 Meneja Maudhui Zamaradi Nzowa akimkaribisha Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa (BASATA) Godfrey Mwingereza ukumbi wa Kilimanjaro hotel katika hafla ya kuwakaribisha wasanii walioigiza kwenye tamthilia ya ode to Joy
 Kikundi cha ngoma kiitwacho Makumbusho kikitumbuiza katika hafla fupi ya kutambulisha msimu wa pili wa tamthilia ya ode to Joy inayorushwa na King'amuzi cha startimes.
 Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa (BASATA) Godfrey Mwingereza akiwa pamoja na wadau mbalimbali wasanaa katika hafla fupi ya kutambulisha msimu wa pili wa tamthilia ya ode to Joy
Jamii ya watu wa nchi ya China waliojitokeza kwenye hafla fupi ya kuwakaribisha wasanii walioigiza kwenye tamthilia ya ode to Joy 

JUKWAA LA MABADILIKO YA TABIANCHI WAISHAURI SERIKALI KUONGEZA FEDHA KATIKA SEKTA YA NISHATI JADIDIFU

0
0
Na Penina Malundo

JUKWAA la Mabadiliko ya Tabianchi limeishauri Serikali kutoa kipaumbele katika eneo la nishati jadidifu kwa kutengaji wa bajeti ya kutosha kwa lengo la kusaidia kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa masuala ya nishati jadidifu unaofadhiliwa na Shirika la Hivos kutoka Jukwaa la Mabadiliko Tabianchi(FORUMCC) ,Euphrasia Shayo wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali wakiwemo vijana,wanawake pamoja na kundi la watu walemavu waliokutana na kujadili masuala ya nishati jadidifu zinavyoweza kupunguza mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kila mwaka fedha nyingi zinatengwa katika nishati ambazo sio jadidifu ikiwemo nishati ya makaa ya mawev ambapo bajeti ya mwaka 2016/17 inaonyesha ilitengewa asilimia 35 huku kwa nishati jadidifu ilitengewa asilimia 5 tu ya bajeti.

“Katika bajeti ya Serikali inayowekwa kila mwaka pesa nyingi zinakwenda kwa nishati za kawaida ambazo asilimia kubwa ndo zinaleta mabadiliko ya tabianchi na sio kwenye nishati jadidifu ambapo wafadhili wanaweka fedha ili kuweza kupunguza kasi ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi,”amesema.

Ameongeza kwamba wanataka Serikali iweke kipaumbele katika masuala ya nishaji jadidifu kwani bajeti ya mwaka 2016/17 waligundua Serikali ilitenga asilimia 30 ya kupata nishati kwa kupitia makaa ya mawe ambayo yanaleta mabadiliko ya tabia nchi huku kwa nishati jadidifu ilitenga asilimia 5 tu, hivyo wanatamani katika suala la nishati jadidifu bajeti yake ifike hata asilimia 50.

Ameongeza kuwa nishati jadidifu ni nishati inayotokana na mwanga wa jua,upepo na wakati mwingine maji na nishati hiyo inachafua mazingira kwa asilimia ndogo ukilinganisha na nishari ya Mkaa,Kuni na makaa ya mawe ambapo uchafua mazingira kwa asilimia kubwa na kusababisha mabadiliko ya tabianchi.

“Tumeingia katika mradi huu wa masuala ya nishati jadidifu unaofadhiliwa na Shirika la Hivos kutoka nchini Nethaland kutokana na nishati jadidifu kuwa ni moja ya njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hivyo imeweza kutufadhili kwa kutoa elimu ipasavyo juu ya umuhimu wa nishati jadidifu,”amesema.

Aidha amefafanua kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa nishati nchini ni wakinamama, hivyo Shirika lao litaweza kutengeneza jukwaa la pamoja lenye kuzungumza sauti ya pamoja itakayotoa nafasi ya Serikali kufanya kitu cha kuweza kusaidia nishati jadidifu inatumika ipasavyo.

“Tanzania maeneo yake mengi hayana nishati ya umeme wa kutosha na hii inafanya watu wengi kutofikiwa na nishati hiyo hivyo endapo jitihada zikiwekwa na Serikali ikawezesha nishatijadidofu kutumika ipasavyo hususani vijijini itaweza kusaidia mazingira kuwa safi na salama,”amesema

Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi wa kushawishi Benki ya Maendeleo ya Afrika kuelekeza uwekezaji kwenye sekta ya nishati jadidifu unaotekelezwa katika nchi sita ambao unafadhiriwa na Christiani Aid kupitia African Climate Justice Alliance (PACJA),Msololo Onditi alisema Jukwaa lao la ForumCC kwa sasa linatekeleza mradi wa pili unaohusiana na nishati jadidifu.

Amesema matumizi makubwa yanayotumiwa na watanzania ni matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ambayo asilimia kubwa yanasababisha mabadiliko ya tabianchi hivyo uwekezaji mkubwa wa nishati jadidifu utaweza kusaidia kumudu utumiaji wa nishati safi.

“Kupitia mradi huu tunajengeana uwezo kama asasi za kiraia kupitia nishati jadidifu katika mazingira ya mabadiliko ya tabianchi na kushawishi watendaji wa Serikali kuwa na sera mikakati na mipango ambayo itavutia uwekezaji mkubwa katika upande wa nishati jadidifu,”amesema Onditi.

Amefafanua bado nchi haina sera wala mkakati unaosimama na kuongoza katika matumizi la nishati Jadidifu kwani sera iliyopo ni ile ya nishati ya jumla kwa sasa.

Hata hivyo wadau wa Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi wamezungumzia kwa kina umuhimu wa Serikali kuweka sera maalum ambayo itasimamia nishati jadidifu kwani kwa sasa kuna sera moja tu ambayo inahusu nishati kwa ujumla na hivyo kuonekana kwa usimamizi mzuri wa nishati jadidifu na hivyo wanaishauri Serikali kuweka sera inayojitegemea katika sekta hiyo.
Wadau wa Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi wakiwa makini kufuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano maalum uliowakitanisha wadau hao jijini Dar es Salaam chini ya.mwamvuli wa Jukwaa la FORUMCC

Serikali yaagiza waliokimbia na Bilioni 1.2/= za Wakulima Mtwara wakamatwe

0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Stendi ya Mabasi wilayani Newala leo, ambapo ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata Viongozi wa Vyama Vya Msingi vya Ushirika ambao wametoroka na fedha za wakulima wa korosho wilayani hapo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwananchi wa Newala,Shadrack Ntesi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika Stendi ya Mabasi wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Newala baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Aziza Mangosongo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

***************************************** 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara kuwakamata Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wanaotuhumiwa kukimbia na Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2/= za wakulima ambazo ni madeni ya Korosho. 

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Newala katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi Kuu baada ya kupokea Ripoti ya Jumla ya Madeni wanayodai wakulima katika Wilaya za Mtwara, Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba. 

“Nilivyofika hapa Mtwara jambo la kwanza lilikuwa kumuuliza Kamanda wa Polisi wa hapa juu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais alilolitoa siku za hivi karibuni alipokuwa ziara na kuagiza kukamatwa kwa viongozi wawili wa vyama vya msingi vya ushirika wanaodaiwa fedha za korosho na wakulima, ameniambia walitekeleza agizo na hao viongozi wawili tayari wameanza kulipa hizo fedha,” amesema Masauni 

Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya madeni kwa Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara Naibu Waziri Masauni amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wengine katika wilaya zilizobakia za Mtwara, Newala, Masasi, Nanyumbu na Tandahimba ambazo katika taarifa ya jumla ya mkoa inaonyesha takribani Shilingi Bilioni 1.2 bado zinadaiwa na wakulima hao kutoka kwa viongozi wa vyama hivyo. 

“Mheshimiwa Rais kwenye ziara yake aliishia wilaya ya Masasi lakini katika ripoti hapa inaonyesha katika wilaya zingine wakulima pia wanadai fedha zao ambacho ni kiasi kikubwa,nakuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara kuwakamata viongozi wengine katika wilaya zilizobakia na hakikisha kiasi hicho cha fedha cha wakulima hao kinalipwa,” amesema Masauni 

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Blasius Chitanda inaonyesha jumla ya Vyama vya Ushirika 61 bado vinadaiwa na wakulima katika wilaya za Mtwara, Masasi, Tandahimba na Newala kuanzia Msimu wa Korosho wa Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo baadhi ya wakulima wanaodai fedha zao waliiomba serikali kuhakikisha wanalipwa haki yao kwani madeni hayo yamechukua muda mrefu hali inayopelekea kuzorotesha shughuli zao za kuchumi huku familia zao zikipata taabu kutokana na fedha zao kutopatikana kwa wakati.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB wachangia damu kwa wagonjwa 240 wenye uhitaji

0
0
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam Badru Idd (wa pili kulia) akiwaongoza wenzake kuchangia damu katika Hospitali ya Ocean Road.

………………………………………………… 

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inakabiliwa na uhaba wa damu hali inayosababisha wakati mwingine huduma kushindwa kutolewa kwa ufanisi. 

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Ocean Road, Dk. Mark Mseti, amesema kwa siku za hivi karibuni hospitali hiyo imekuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa damu hali inayokwamisha utoaji huduma kwa wahitaji. 

Mseti alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kutokana na tiba zote za mionzi kuhitaji wagonjwa kuwa na damu ya kutosha ili ziweze kufanya kazi sawasawa . 

“Tunahitaji chupa za damu 40 hadi 50 kila siku, kuna wakati Mpango wa Taifa wa Damu Salama unaileta kwa kiwango kinachostahili tunapata chupa 50 au 40 na tunaweza kufanya kazi kama inavyostahili lakini hivi karibuni kwa takribani wiki mbili hivi kumetokea uhaba mkubwa wa damu kwenye taasisi yetu. Kwa mfano jana na juzi tulipata chupa zisizozidi 20 kwa siku,” amesema Dk Mseti. 

Katika kujaribu kukabiliana na changamoto hiyo wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wametumia huu mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kuchangia uniti 97 za damu. Dk. Mseti amesema kiasi hicho cha damu kitatumika kwa wagonjwa 240 wenye uhitaji wa tiba hiyo. 

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, amesema lengo la kushiriki zoezi hilo ni kuangalia jinsi ya kuokoa maisha ya watanzania wenzao wenye uhitaji. Amesema kupitia zoezi hilo walilolifanya,anatoa rai kwa Watanzania wengine kushiriki kuokoa maisha kwa kuchangia damu 

“Nimetembezwa hospitalini unakuta hata hiyo damu inayohitajika haipo au ni kidogo, watanzania tujitolee kuokoa maisha ya wenzetu,” amesema
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images