Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

DAWASA, MAAFISA AFYA WAJA NA LENGO MOJA LA KUTOKOMEZA KIPINDUPINDU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wameweka mpango kazi wa kupambana na kutokomeza  magonjwa ya mlipuko (kipindupindu)  kwa kushirikiana na Maafisa Afya wa kata Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimefanyika leo kwa Maafisa Afya kutoka kata mbalimbali za Manispaa zote za Jiji na DAWASA kujadiliana kwa pamoja namna ya kupambana na magonjwa hayo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema katika mkakati wa muda mfupi watasaidia kutoa vidonge (dawa) kwa ajili ya kusafisha maji ya visima na kuwapatia wananchi.

Amesema, kwa kushirikiana na maafisa afya watahakikisha wanafanya vikao kila mwisho wa mwezi ili kuhakikisha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kupindupindu kisiwepo ndani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Neli amesema, kuna changamoto ya uharibifu wa mazingira kwa wale wanaotiririsha majitaka ila baada ya kikao hiki anaamini Maafisa Afya watawavumbua wale wote wanaofanya vitendo hivyo.

"Tunatambua kuna maeneo yanatabia ya kutiririsha maji taka wakati wa mvua, wanayaachia maji na kusambaa na ndio yanakuwa chanzo kikubwa cha magonjwa ya mlipuko kwahiyo mpango mkakati tuliofikia kwa pamoja ni Maafisa Afya kusimamia kwa weledi na kuhakikisha tunatokomeza tabia hiyo,"amesema Neli.

Aidha, Neli amesema kuna watoa huduma wa maji wanaouza maji kutoka kwenye visima vyao mara nyingi tumekuwa tunawashauri waweke dawa na hata hivi karibuni tumewapatia dawa kwa ajili hiyo.

Pia, baada ya sheria mpya ya maji kuanza kufanya kazi, wamiliki wote wa Visima wametakiwa kuja kujisajili na kupatiwa leseni baada ya maji yao kupimwa na kuthibitishwa kama yanafaa kwa ajili ya matumizi kwa binadamu.

Ameeleza, kuna changamoto ya visima vifupi vilivyopo kwenye maeneo yenu ambavyo kiuhalisia hamuwezi kuviweka dawa ila ninaamini mtavifanyia kazi kama tulivyokubaliana.

Akielezea mchakato wa majitaka, Charles Makoye amesema kuwa wamekuwa na mkakati wa kuendelea kujenga mabwawa ya majitaka kwenye maeneo tofauti pamoja na ujenzi wa vyoo vya jamii ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Makoye amesema, kuna baadhi ya maeneo yaliyokuwa yanaongoza kwa magonjwa ya mlipuko yamepungua kasi ikiwemo Vingunguti baada ya kujenga mfumo wa vyoo unaopeleka maji moja kwa moja kwenye mabwawa na umewasaidia wananchi kupunguza kasi ya magonjwa hayo.

Afisa Afya Mkoa Dar es salaam, Enezael Emmanuel amewataka maafisa afya kuanza kutekeleza yale waliyokubaliana kwenye kikao cha leo na kuanza kuyafanyia kazi kabla madhara hayajaanza kujitokeza.

Kwa upande wa Maafisa afya wameahidi kushirikiana na DAWASA katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kutekeleza yale waliyokubaliana pamoja na vya kila mwezi.

Maafisa Afya Wameiomba DAWASA kupeleka mifumo ya majitaka kwenye maeneo yao ambayo yana changamoto kubwa na wananchi wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa kipindi cha mvua na baadhi yao kutiririsha maji taka.
Afisa Afya Mkoa Dar es salaam, Enezael Emmanuel amewataka maafisa afya kuyafanyia kazi maazimio yote yaliyoafikiwa kwenye kikao chao pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA ya kuhakikisha wanatokomeza magonjwa ya mlipuko.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Neli Msuya akizungumza na maafisa afya wakati wa kikao cha pamoja na kufikia mpango mkakati wa muda mfupi na muda mrefu la kutokomeza magonjwa ya mlipuko.
Meneja wa Majitaka na Usafi ww Mazingira DAWASA Mhandisi Charles Makoye akielezea mkakati wa mamlaka katika kujenga miundo mbinu ya majitaka na vyoo vya jumuiya katika Mkoa wa Dar es Salaam na namna watakavyopambana na magonjwa ya mlipuko.
Maafisa afya wakiwa wanafuatilia kikao

BENKI YA CRDB YAKUTANA NA BAADHI YA MAWAKALA WAKE JIJINI DAR LEO

$
0
0
Banki ya CRDB leo imekutana na baadhi ya Watoa huduma ya Uwakala wa Benki hiyo na kufanya  nao kongamano lililoambatana na hafla fupi ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa wateja. Pichani ni baadhi wa Mawakala wa Benki hiyo, wakikata keki kama ishara ya kujipongeza kwa huduma bora za kifedha zinazotolewa na mawakala hao, wanaoshuhudia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Uwanala wa Kibenki wa Benki ya CRDB, Ericky Willy (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo (kulia).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Cornell Meseyeck akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa maalum kwa baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB, ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa wateja, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uwakala wa Kibenki wa Benki ya CRDB, Ericky Willyakizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa maalum kwa baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB, ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa wateja, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo akizungumza katika hafla hiyo.




BONDIA KIDUNDA ATINGA ROBO FAINALI MASHINDANO YA DUNIA YA MAJESHI CHINA

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu CHINA.

Bondia Koplo Selemani Kidunda maarufu ‘Mtu Mbaya’ ameendeleaza ubabe baada ya kutinga hatua ya robo fainali katika Mashindano ya Dunia ya Majeshi katika Mchezo wa Ngumi nchini China

Kidunda ameingia hatua hiyo baada ya kumtwanga kwa pointi Munkhajar BatBaatar wa Mongolia na kupata alama 10 kutoka majaji wote Watano katika mpambano huo.

Bondia huyo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alitinga hatua hiyo ya pili baada ya kwanza kumpiga kwa KO bondia Dapura Liyanage PRK kutoka Srilanka katika raundi ya pili ya mchezo.

Wakati mpinzani wake alitinga hatua hiyo baada ya kumpiga Bondia Aung ye Win kutoka Mnyamar kabla ya kukutuna na kidunda alieyemuondosha katika mashindano hayo.

Sasa Kidunda anasubiria Mpinzani atakayepambana nae mara baada ya kumalizika kwa mapambano ya leo usiku na kuamua mabondia watakaoingia katika hatua ya robo fainali ambao anaefuvu anajihakikishia medali.

Akizungumza mara baada ya Mchezo Kidunda alisema mashindano bado ni Magumu kwani kila Nchi imeajiandaa lakini dua za Watanzania zimekuwa msaada mkubwa na kuomba kuendelea kumuombea.Naye Kocha wake Hasan mzonge amesem,a amefurahishwa na hatua aliyofikia na matumaini yake atafanya vizuri katika hatua zinazofuata amabazo ni ngumu lakini ni zenye mafanikio Makubwa.

Mmoja wa Viongozi katika Msafara timu inayowakilisha Tanzania Kapteni Mohamed Kasui amesema katika mashindano makubwa kama haya kufikia hatua hiyo ni mafanikio makubwa na wanazidi kumuombea kidunda kufanya vizuri…

TPDC YAANZISHA MRADI MKAKTI KWA AJILI YA UTAFITI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA KUISADIA SERIKALI

$
0
0
VICTOR MASANGU, PWANI
SHIRILA la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) katika kukabiliana na changamoto ya uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi imekuja na mpango kabambe wa miradi mikakati mitatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa uchimbaji wa visima vya mafuta katika mikoa ya Tabora,Simiyu, pamoja na singida lengo ikiwa ni kuipunguzia serikali ya awamu ya tano kutumia gharama kubwa katika suala zima la uagizaji.

Hayo yalibainsihwa na Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya wakati wa maonyesho ya bidhaa za wawekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani, ambapo pia amebainisha kuwa lengo lao linguine ni kuweza kutanua wigo katika kuzalisha gesi asilia katika maeneo mbali mbali nchini ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kuondokana na mtumizi ya ukataji wa miti ovyo.

Kwa upande wake Afisa uhusino wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Latipher Kigoda amesema kwamba lengo kubwa ni kuwasimamia na kuwaunganisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ikiwemo kutanagaza fursa mbali mbali zilizopo kwenye kilimo pamoja na kuongeza thamani katika mazao ya biashara sambamba na kuwa na vifaa tiba ambavyo vinazalisha ndani ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye amepokea jopo la wawekezaji saba Kutoka jimbo la hebeyi kutoka nchini na kuwakabidhi mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa ambao utaweza kuonyesha fursa mbali mabli ambazo zinapatikana katika halmashauri zote tisa lengo ikiwa ni kuwapatia maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa kuzalisha chuma,nondo na saruji.
Afisa Mahusiano ya jamii wa TPDC Eugene Isaya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa maonyesho ya bidhaa kwa wawekezaji wa viwanda Mkoa wa Pwani (PICHA VICTOR MASANGU)

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA TTCL NA KITUO CHA TAIFA CHA KUHIFADHI TAARIFA

$
0
0
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Adadi Rajabu (katikati) akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC) ambacho kipo chini ya usimamizi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe, Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujionea uendeshaji wa Shirika hilo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba akielezea jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujionea uendeshaji wa Shirika hilo.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Mohammed Khamis Omar akielezea jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC).
]Mbunge wa Buhigwe na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Albert Ntabaliba akichangia jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC). PICHA NA BUNGE

BENKI YA TADB, PASS WASAINI MAKUBALIANO KUKUZA MIRADI YA KILIMO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo na Kilimo (TADB), Japhet Justine katikati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wakiingia makubaliano ya uwekezaji katika Mradi wa Ubunifu wa kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti  na Mipango, Dkt. Nyankoma Marwa na Kushoto ni  Mkurugenzi mkuu wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu Amijee.
mkuu wa Atamizi (incubator) wa PASS, Tamimu Amijee kulia akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar Es Salaam mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya PASS na Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB), kwaajili ya uanzisha huduma maalumu ya kusaidia shughuli za kilimo cha biashara kwaajili ya Vijana, wanawake na wajasiliamali.

 Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
IKIWA asilimia 35 ya watanzania ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) imedhamiria kuongeza mitaji kwa miradi mbalimbali ya vijana wanaojishughulisha na kilimo.

Benki hiyo ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali linaloshugulikia Kilimo la PASS wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika miradi ya Ubunifu ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkugenzi Mtendaji wa wa benki ya TADB, Japhet Justine amesema kuwa makubaliano ya leo ni kuwajengea uwezo wanawake na vijana katika kukuza miradi ya ubunifu ya kilimo.

"Ili kuweza kumgusa mkulima mmoja mmoja wa chini na makundi mbalimbali yanayochangia katika pato la taifa hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo ni vizuri kuingia makubaliano na kushirikiana na taasisi zenye malengo sawa na yetu". Amesema Justine.

Justine amesema kuwa ili kuongeza atamizi la vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo na kuwaongezea  huduma ya fedha ili waweze kukuza mipango na miradi yao.

Amesema kuwa Kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha katika kuongeza na kurahisha upatikanaji na kukutanisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo kutarahisha miradi ya kibunifu kuleta maendeleo chanya katika nchin kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi wa PASS, Tamim Amijee amesema kuwa taasisi ya PASS itashirikiana vyema na TADB kwa kuwekeza zaidi katika kuandaa program na rasilimali watu za kuwajengea uwezo vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo katika kukuza miradi ya kilimobiashara pamoja na kushirikiana bega kwa bega na TADB katika kufanya tathmini na kutoa misaada ya kiufundi zaidi kwa vijana, wanawake na wajasiliamali wadogo mara baada ya kumaliza program yao na kukuza miradi yao ya kibunifu.

SERIKALI YASHTUKIA KUSUASUA KWA UENDESHAJI KIWANDA CHA TANGA FRESH

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza kwenye kikao cha menejimenti ya Kiwanda cha Tanga Fresh na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akisikiliza kwa makini baadhi ya hoja kwenye kikao cha menejimenti ya Kiwanda cha Tanga Fresh na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella akizungumza kwenye kikao cha menejimenti ya Kiwanda cha Tanga Fresh na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU).

…………………..

Na. Edward Kondela

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshtukia kusuasua kwa uendeshaji wa kiwanda cha Tanga Fresh hali iliyolazimu kuundwa tume kufanya uchunguzi wa namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo kuchunguza mtambo unaotumika kusindika maziwa ya muda mrefu ambao unadaiwa umekuwa ukiongeza gharama ya uendeshaji wa kiwanda hicho.

Akizungumza jana (21.10.2019) katika kiwanda cha Tanga Fresh mjini Tanga, kwenye kikao kilichohusisha menejimenti ya kiwanda pamoja na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) kinachomiliki asilimia 43 ya kiwanda hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefafanua kuwa serikali itahakikisha inachukua hatua kunusuru kiwanda kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotembelea kiwanda hicho mwaka 2017 na kuahidiwa na menejimenti kusindika maziwa lita laki moja kwa siku ambapo katika ziara hiyo Rais Magufuli aliwasaidia kupata hati iliyokuwa imekwama kwa miaka mingi, kuondoa changamoto ya wanahisa juu ya hisa zao Tume ya Ushindani (FCC) hali iliyopelekea kiwanda kuanza kujitanua na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya muda mrefu (UHT) ingawa kiwanda kiliamua kuchukua mkopo Benki ya Biashara (NMB), unaoonekana kuwalemea na kutofanya vizuri sawa na ahadi kwa Rais Magufuli.

“Kwanza serikali imebaini manunuzi ya mtambo wa kusindika maziwa ya muda mrefu kuwa ni mtambo uliyokwishatumika na umenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni Sita, pia riba ya mkopo kuwa ni kubwa na kuwa mzigo, hivyo nimeagiza iundwe tume ambayo tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameiunda kuanzia leo kufanya uchunguzi wa mtambo ulionunuliwa ikiwemo fedha ya kununulia mtambo huo na utaratibu uliotumika kununulia mtambo.” Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega ameitaka bodi ya wakurugenzi wa kiwanda pamoja na wamiliki wakae pamoja na Benki ya Kilimo (TADB) kuitaka benki hiyo kununua deni hilo ili kutoa nafuu kwa kiwanda na kuondoa mzigo kwa wafugaji na kuinua kipato chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella amesema tayari timu ya wataalamu wakiwemo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeshaundwa ili kubaini hali ya mtambo wa kusindika maziwa. 

Bw. Shigella amefafanua kuwa serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukihujumu Kiwanda cha Tanga Fresh ikiwemo kununua mtambo wa kusindika maziwa usio na tija kwa kiwanda hicho.

Nao baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uongozi wa Mkoa wa Tanga kutafuta suluhu ya namna ya kuboresha Kiwanda cha Tanga Fresh ili kiweze kuongeza uzalishaji na kuwanufaisha wafugaji ambao wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho pamoja na kutaka kiwanda hicho kiongeze bei ya kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hao ambao hawaridhiki na bei ya Shilingi 700 kwa lita moja.

Kikao baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, uongozi wa mkoa wa Tanga, menejimenti ya kiwanda cha Tanga Fresh, bodi na wamiliki wa kiwanda kinatarajiwa kuendelea hii leo (22.10.2019) ili kutafuta suluhu ya kunusuru kiwanda hicho baada ya kupata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Waziri Mwakyembe Azindua Kamati ya Kusimamia Haki za Kazi za Wasanii

$
0
0
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mara baada ya kuizindua mapema hii leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizindua Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi. Sarah Nsangizyo Zilahulula na kushoto ni mjumbe Dkt. Dorah Mwenegoha.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati waziri alipokuwa akizindua Kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kusimamia haki za kazi za wasanii nchini wakimsikiliza Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati waziri alipokuwa akizindua kamati hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.


WATAALAM SEKTA YA MAENDELEO NCHINI WATAKIWA KUWA NA MFUMO MAALUM WA KUPATA TAKWIMU

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua mwongozo wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kushoto kwake ni Rais wa wa CODEPATA Bw. Sunday Wambura na kulia kwake ni Bw. Patrick Golwike Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara yake.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa hotuba yake kwa Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua chama cha wataalam wa maendeleo ya jamii nchini CODEPATA mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea zawadi iliyotolewa kwake na chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini CODEPATA mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua banda la Wizara yake mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wakifuatailia jambo kwa umakini wakati wa Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kujiongeza katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi za matukio ya ukatili badala ya kutegemea taarifa za Jeshi la Polisi ambazo utolewa na Mkuu wa Jeshi hilo baada ya mwaka mzima.

Waziri Ummy amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wataalam wa maendeleo ya Jamii linaloendelea kwa siku mbili kama sehemu ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa wataalam wa maendeleo ya jamii.

Waziri Ummy amesema wataalam wenzao wa afya wamekuwa wakimpatia taarifa zenye takwimu kwa wakati na kuwataka wataalam hao kuiga mfano huo kwa kuwataka kuwa wanawasiliana na vituo vya polisi mkoani kwao ili waweze kupata taarifa za waanga wa ukatili katika maeneo yao kazi.

“Kila nikienda katika ziara sipewi taarifa yoyote kutoka kwa wataalam wa maendeleo ya jamii na hata nikiwauliza unakuta hawana taarifa yoyote ile kuhusina na masuala yanayohusiana na masuala ya Maendeleo ya Jamii.’’ Aliongeza Waziri Ummy.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Nchini Bw. Patrick Golwike kuweka mfumo mzuri wa kukusanya takwimu za maendeleo ya jamii ili kuwezesha kupatikana kwa takwimu izo kwa muda na kwa haraka.

‘’Nikija katika Mkoa au Halmashauri yako nipate takwimu, ukiongea na takwimu ni rahisi kupata rasilimali fedha na misaada mingine itakayosaidia kutatua changamoto zilizopo mfano kupata takwimu za vikundi vya wajasiliamali ambao wamepokea mikopo ya Halmashauri’’. Aliongeza Waziri Ummy.

Pamoja na kutoa changamoto hizo kwa wataalam hao Waziri Ummy amewataka wataalam hao kuhamasisha jamii ili iweze kutumia teknolojia ya habari kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kuongeza kuwa kwa kutumia taarifa zinazopatikana jamii itapata taarifa za masoko ya bidhaa zao ikiwemo namna bora ya kulima kwa utaalam.

Aidha Waziri Ummy ameitaka jamii kuacha kutumia muda mwingi kufuatilia mitandao ya kijamii na badala yake wahamasishwe kutumia muda wao mwingi kwa mambo yenye tija ikiwemo ari ya kuchangia jamii kwa ajili ya maendeleo.

Waziri Ummy ameitaka jamii ya watanzania kuwa inapenda starehe sana na watu wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya kusherekea harusi, siku ya kuzaliwa bila kujiuliza kama fedha hizo zinaendana vipaumbele ambavyo mtu amejiwekea au kuchangia ada kwa ajili ya mwanafunzi. 

Waziri ummy ameitaka jamii kutumia teknolojia hiyo kufanya mambo yenye tija na akitoa mfano wa wataalam wa maendeleo ya jamii kuendelea kuhamasisha jamii kuwekeza katika elimu ya Afya ili tuweze kupata huduma bora katika jamii.

Aidha amewataka wataalam hao kufikilia kuwekeza sana katika miradi ambayo ina mashiko na kukemea tabia ya wafadhili kuweka mkazo katika masuala ya warsha na Semina ambazo hazitoi matokeo ya moja kwa moja katika jamii.

Akizungumza kwa Niaba ya katibu Mkuu Maendeleo ya jamii, Mkurugenzi wa maendeleo ya Jamii bw.Patrick Golwike amseme ajukuu kubwa la wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni kuiandaa jamii ushiriki katika shughuli za maendeelo ya nchi.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Bw. Sunday Wambura amesmea kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu umekuja na uzinduzi wa Chama chao kitakachowasaidia kupeana mbinu mbalimblia za kuhakikisha maafisa wanaisaidia jamii katika kujiletea maendeleo.

Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.

TCRA YAKUTANA NA WATU WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA KUTOA ELIMU YA HUDUMA YA MAWASILIANO

$
0
0
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Dorice Mhimbira, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
 Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), mwenye shati jeupe Sohela Mabeyo, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
 Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo Yusuph Mloli, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo David Chamila, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati wa semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa semina walipokuwa wakiwasikiliza maafisa wa TCRA wakati wa semina ya kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia, namna bora ya kutumia huduma za mawasiliano, semina iliyofanyika jijini Dodoma.

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA imekutana na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia katika mkoa wa Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kuhusu utumiaji wa huduma za mawasiliano na namna ya kukabiliana na changamoto katika kutumia huduma za mawasiliano.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick,amesema ni utaratibu wa mamlaka hiyo kutoa elimu ya mawasiliano kwa watumiaji, lakini watu hao wametoa maombi maalamu .

Kwa ajili ya kupatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kutumia bidhaa za mawasiliano, kwani watu hao wamekuwa wahanga katika kutumia mawasiliano kutokana na ulemavu walionao.

“Ni utaratibu kila wakati kutoa elimu kuhusu elimu ya kukabiliana na changamoto katika mawasiliano, lakini tumepewa ombi maalamu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu hawa wenye ulemavu wa kutokusikia, na elimu hii ni mahususi kwa sababu hawa ndio wahanga katika uhalifu wa mtandaoni”amesema Marick.

Amesema kundi hilo kama wadau wao wamekuwa na changamoto nyingi katika kutumia bidhaa za wasiliano, kwani baadhi yao hawana uelewa katika suala la changamoto za mawasiliano, hali inayopelekea kuathrika na vitendo vya wizi wa mitandaoni.

“Tumetoa tahadhari ya changamoto zilizopo katika mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli, njia mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji, mfano kapokea ujumbe wa kutakiwa kutuma fedha kwa namba usiyoifahamu usitekeleze kwanza na nini cha kufanya” amesema.

Aidha amesema na wao kama mamlaka wamesikia changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutumia mawasiliano, na wengi hawana uelewa katika kukabiliana na vitendo vya wizi mitandaoni na uhalifu mwingine mitandaoni, hasa katika kutunza siri zao za mawasiliano kuepuka na na vitendo hivyo.

“Ametolea mfano baadhi yao wanaweza kuwa amejiunga kifurushi na kabla hajakitumia wakakata, na yeye bila kuelewa kuwa anahaki ya kujua, lakini ana amua kununua vocha na kujiunga tena bila kujua kwanini, na tumewaelekeza kuwa anapokutana na kitu kama hicho, anatakiwa kuhoji na tumewaelekeza mamlaka ilipo kwa ajili ya msaada zaidi anapokuwa hajaridhika na majibu ya mtoa huduma” amesema.

Pia amesema kila kanda kuna mamlaka za mawasiliano na wanajukumu la kuhakikisha wanatoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ili kila mtumiaji atambue haki yake katika kutumia huduma ya mawasiliano na namna ya kuepuka uhalifu wa mitandaoni.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwamo Yusuph Mloli na David Chamela, wenye ulemavu wa kusikia wameshukuru kupewa mafunzo hayo kwani yamekuwa msaada mkubwa kwao, na yametusaidia katika kuwafungua na kupata uelewa juu ya huduma za mawasiliano na mamna ya kukabiliana nazo.

“Niwashukuru sana TCRA kwa sababu hapo mwanzo sikuwa na uelewa na kunavitu nilikuwa na fanyiwa na mitandao ya simu lakini sikujua kama sitendewi haki lakini kwa sasa nimeelewa vizuri, na ukizingatia sisi walemavu wa macho ndio waathirika katika vitendo vya wizi mitandaoni” amesema Chamela.

TTCL-Corporation kutoa huduma za mawasiliano nchini Burundi

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto) ya BBS kupewa huduma za mawasiliano na TTCL Corporation. Nyuma yao ni wanasheria wa pande zote mbili wakishuhudia tukio hilo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (wa pili kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe wakibadilishana nakala za makubaliano ya kibiashara mara baada ya kusainiwa leo. Katika makubaliano hayo TTCL Corporation itatoa huduma za mawasiano kwa BBS kwa muda wa miaka 10. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika tukio hilo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Dk. Jim Yonaz akishuhudia tukio hilo na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto). 
Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto) akimpa zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba kama ishara ya shukrani mara baada ya hafla hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akimpa zawadi Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe kama shukrani kwa uhusiano kibiashara kwa pande mbili. 


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Corporation) limeingia makubaliano ya kibiashara na Taasisi ya Serikali ya Nchini Burundi inayosimamia Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa wa nchi hiyo, Burundi Backbone System (BBS) ili TTCL kuwezesha mawasiliano katika taifa hilo.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo jijini Dar es Salaam na yatadumu kwa takribani miaka 10 huku yakihusisha, TTCL Corporation kutoa huduma za data na intaneti zijulikanazo kwa kitaalamukama IP TRANSIT, BACKHAULING pamoja na huduma ya IPLC.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba alisema hatua hiyo ni ya mafanikio kwani TTCL litakuwa ni Shirika pekee linalotoa huduma ya Mawasiliano ya Mkongo Nchini Burundi kupitia vituo vyake vya mpakani katika miji ya Kabanga na Manyovu, na kuiunganisha nchi ya Burundi na Dunia kupitia Mikongo mikubwa ya baharini SEACOM na EASY.

Waziri Kindamba alibainisha kuwa makubaliano hayo ya kibiashara yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.8 yatahusisha TTCL Corporation kutoa huduma za Utunzaji wa kumbukumbu mbadala kupitia kituo cha kimataifa cha kutunzia kumbukumbu 'National Internet Data center' cha jijini Dar es Salasam, pamoja na kubadilishana wataalamu kwa kujengeana uwezo kitaalamu nyanja mbalimbali za Mawasiliano.

"Mabadilishano ya wateja hasa kwa wateja wakubwa wenye matawi ya biashara au ofisi katika nchi zote mbili (Burundi na Tanzania) kwa mfano CRDB BANK, pia kupeana ushauri wa kitaalamu kuhusu watoa huduma na watengenezaji wakubwa wa vifaa vya Mawasiliano vinavyotumika kuhudumia Mawasiliano ya Mkongo (Fiber and Terminal Equipment Suppliers Advisory)."

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe aliishukuru Tanzania kupitia TTCL kwa kuendelea kushirikiana kibiashara na masuala mengine mengi ambayo Tanzania imekuwa ikiisaidia nchi ya Burundi.

Alisema mbali na makubaliano hayo ya kibiashara Burundi itanufaika kwa mengi haswa kujifunza kutokana na hatua ambazo taifa la Tanzania limepiga kwa sasa ukilinganisha na taifa la Burundi.

"...Kimsingi tunashukuru kwa uhusiano huu wa kibiashara tulioingia leo. Hata hivyo taifa letu lina mengi ya kujifunza na kunufaika kutoka Tanzania hasa kwa hatua Tanzania imepiga kwa sasa," alisema Mtendaji Mkuu wa BBS, Ntihagowumwe. 

SASA MKOA NJOMBE UMEANZA KUSHAMIRI MAJENGO YA KISASA

$
0
0
 Jengo la NSSF Njombe.

Majengo ya kisasa yameanza kushamiri katika Mkoa  mpya wa Njombe ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2012. zimeanza kujengwa majengo ya kisasa ya serikali, hoteli na ya watu binafsi. Pia imejengwa stendi mpya ya kisasa, soko la kisasa.
 Kanisa la Katoliki la ST Joseph la Njombe Mjini
 Baadhi ya majengo yanayochepuka Njombe Mjini
 Mtaa wa Mlowezi katikati ya Mji wa Njombe
 Benki ya NMB Njombe
 Jengo la CCM Mkoa wa Njombe lililopo Mjimwema

 Soko Kuu la kisasa la ghorofa  Mjini Njombe likiwa katika hatua za ujenzi

Moja ya vituo vipya  vya mafuta vilivyopo  Njombe. (PICHA ZOTE KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)

Mkoa wa Njombe ni mmojawapo kati ya mikoa mipya nchini Tanzania wenye postikodi namba 59000 [1], ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012[2]. Umepakana na mikoa ya MorogoroRuvumaMbeya na Iringa.
Kutokana na hadhi mpya, wilaya ya Njombe imegawanyika kati ya ile ya mjini na ile ya vijijini. Pia, mwezi wa Machi 2012, imeanzishwa wilaya ya Wanging'ombe.
Mwaka 2012 katika eneo hilo kulikuwa na wakazi 702,097 Census 2012. Jalada kutoka ya awali juu ya March 5, 2016. Iliwekwa mnamo 14 February 2016. katika wilaya sita zifuatazo: Njombe Mjini (wakazi 130,233), Njombe Vijijini (wakazi 85,747), Makambako (wakazi 93,827), Makete (wakazi 97,266), Ludewa (wakazi 133,218), Wanging'ombe (wakazi 161,816).
Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni WabenaWakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.
Kabila la Wabena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na wilaya ya Kilombero (Mkoa wa Morogoro), Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako katika wilaya ya Ludewa.
Yapo pia makabila madogo kama vile WawanjiWakisiWamandaWamagoma n.k. ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu Mkoani Njombe.
Karibu wakazi wote wa mkoa ni Wakristo, hasa Walutheri na Wakatoliki.


    RC MAKONDA AWAPA SIKU TANO WAKANDARASI "WABABAISHAJI" KUHAKIKISHA WANATEKELEZA MIRADI YAO, AWAONYA WATAKAOKAIDI AGIZO.

    $
    0
    0
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewapa Siku tano kuanzia leo October 22 Wakandarasi ambao miradi yao imekuwa ikisuasua kuhakikisha wanaanza kazi mara moja na kubainisha kuwa wakandarasi watakaokaidi agizo hilo Watakamatwa na Vyombo vya dola na Mikataba yao kuvunjwa.

    RC Makonda amesema wapo wakandarasi ambao Walidanganya kwenye nyaraka za kuomba tenda kuwa wana Vifaa vya Kutosha, Wataalamu na Fedha za kutosha ili waatiwe kazi lakini baada ya kupata kazi wamekuwa wakikwama kufanya kazi kutokana na uhaba wa Vifaa jambo linalopelekea miradi kutokamilika kwa wakati na kuleta Usumbufu kwa wananchi.

    Aidha RC Makonda amezionya Bodi za Manunuzi zitakazobainika kutoa tenda kwa wakandarasi kwa rushwa bila kuangalia uwezo wa Kampuni kuwa watachukuliwa hatua.

    Miongoni mwa Miradi ambayo RC Makonda amesema imekuwa ikisuasua ni Ujenzi wa Mto Ng'ombe, Mfereji wa Buguruni Kisiwani, Tabata Roman Catholic,  Barabara ya Kivule na Barabara ya Kawe




    TANZANIA KUSHAWISHI NCHI ZA SADC KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI .

    $
    0
    0
    Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi  Kemilembe Mutasa katika mkutano huo wa wataalamu kutoka nchi za SADC wamekua wakizishawishi nchi mwanachama kuridhia itifaki ya hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi  ya mifuko ya plastiki. 



    Na Vero Ignatus, Arusha.

    Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC ,wanaotekeleza mkakati wa SADC pamoja na programu ya Mazingira na Mabadiliko ya tabianchi, sambamba na sera ya mazingira ya mwaka 1997 pamoja na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.


    Katika kutekeleza programu ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika SADC, ni pamoja na kuwajengea uwezo nchi wanachama kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,kubadilishana ujuzi wa uzoefu katika masuala ya kuhifadhi mazingira, na kufanya tafiti katika vyuo vikuu ili kupata suluhisho la changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi.



    Hata hivyo Wataalaalamu wa mazingira kutoka Tanzania, wanaoshiriki mkutano wa Mawaziri wa,Maliasili na Utalii wameaswa kuanza juhudi za kuzishawishi nchi hizo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ili kudhibiti uharibifu wa mazingira katika ukanda huo.

    Akizungumza mara baada ya kuhudhuria mkutano wa wataalamu wa maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii kwa nchi za SADC, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi  Kemilembe Mutasa alisema katika mkutano huo wa wataalamu kutoka nchi za SADC wamekua wakizishawishi nchi mwanachama kuridhia itifaki ya hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi  ya mifuko ya plastiki.

    “Tanzania kuwa mwenyekiti wa SADC tunatumia fursa ya kushawishi nchi mwanachama kuhimiza agenda ya marufuku ya mifuko ya plastiki iweze kutolewa kwa nchi zote ikiwa ni mkakati wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

    Kwa upande Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Cletus Shengena alisema kuwa wataalamu wa mazingira kutoka nchi za SADC wamekua na mikutano ya kuweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiko ya tabia ya nchi ambayo ni changamoto kubwa inayokabili nchi wanachama  Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo.

    Aidha Shengena alisema kuwa mkakati huo utawasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na athari ambazo zilizoanza kujitokeza ikiwemo mafuriko na upepo mkali na vimbunga katika nchi mwanachama.

    Afisa Mazingira Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi.Emelda Teikwa Adam amesema kuwa wameangazia fursa za kukuza uchumi wa nchi za SADC kwa kutumia uchumi wa bluu unaojulikana kama uchumi wa bahari unaotumika kwa njia ya usafirishaji, uvuvi na kutoa nishati kwa maana ya uchimbaji wa mafuta na gesi kama njia za kukuza uchumi wa nchi za SADC.

    Emelda alisema kuwa ili uchumi huo uwe endelevu mazingira yanapaswa kutunza na kulindwa ili wananchi waweze kunufaika na fursa za uchumi wa bluu ambao ukitumika vizuri unaweza kupunguza umasikini.

    Jeshi la Polisi Iringa lalazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha bodaboda

    $
    0
    0
    Na Datus Mahendeka wa Jeshi la  Polisi 

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha bodaboda walioanzisha vurugu wakikaidi amri ya Jeshi la Polisi,kukamatwa kwa mwenzao ambaye alikuwa amepakia abiria sita kinyume na sheria.

    Picha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari.


    RAIA WA INDIA AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

    $
    0
    0
    Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

     RAIA wa India ambaye ni meneja wa tawi la kampuni ya Neelkani Salt Limited, Mohammed Alikhan (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili.

    Katika kesi hiyo namba 114 ya mwaka huu, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha na wizi wa katoni za chumvi 45,919 zenye thamani ya Sh413, 559,000/_

    Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa kati ya Januari Mosi, 2018 na Julai 29, mwaka huu katika mtaa wa Arusha Ilala, Jijini Dar Es Salaam, Alikhan akiwa Meneja wa tawi la kampuni hiyo aliiba katoni za chumvi 45,871 aina ya Neel Mali ya mwajiri wake zenye thamani ya Sh 412,839,000.

    Pia mshtakiwa huyo anadaiwa katika kipindi hicho aliiba kilo moja ya chumvi aina ya Neel Gold yenye thamani ya Sh 720,000. Mshtakiwa huyo anadaiwa pia kuiba jumla ya chumvi 45,919 zenye thamani ya Sh 413,559,000.

    Aidha, imedaiwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Alikhan  alitakatisha kiasi cha Sh 413,559,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana  na zao la makosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wizi akiwa mwajiliwa.

    Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi za Uhujumu Uchumi napi shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

    Kwa mujibu wa upande wa mashtaka  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa amerudishwa rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 5, mwaka huu.

    Epukeni Matumizi ya Dawa zinazotangazwa Mitandaoni Ummy Mwalimu

    $
    0
    0
    Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.


    Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa baadhi ya Watendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo Bungeni Jijini Dodoma baada ya wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma baada ya kikao na Kamati hiyo.
    Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu hoja mbalimbali za wajumbe hao leo wakati wa kikao cha Kamati hiyo Bungeni leo Oktoba 23, 2019 Jijini
    Dodoma.
    Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa Naibu wake Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.(Picha zote na MAELEZO)


    Serikali imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa zinazotangazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa hazijadhibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

    Akizungumza Jijini Dodoma mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu mbalimbali wanaotoa kiholela matangazo ya kuuza dawa za aina mbalimbali kupitia mitandao husika.

    “Jamii itambue kuwa kuuza dawa ambazo hazijazidhitishwa ni kosa kisheria naniwatake wahusika kuacha mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao”Alisisitiza Mhe Ummy.

    Akifafanua, Mhe. Ummy amesema kuwa ifahamike kuwa dawa siyo kama nguo,viatu ama bidhaa nyingine kama hizo ambazo mtumiaji anaweza kununua kadiri utakavyo kutokana na mahitaji au uwezo wake,lakini dawa isiyothibitishwa na mamlaka ni sumu na kwamba inaweza kumgharimu maisha mtumiaji anayetumia bila maelekezo ama ushauri wa daktari.

    Aliongeza kuwa, Kamati hiyo imeitaka Wizara yake kuongeza jitihada katika kuzuia matangazo yanayotolewa kupitia mitandao ya kijamii yakinadi dawa za aina mbalimbali ikiwemo kuhusu masuala ya uzazi na magonjwa mengine.

    Aidha Mheshimiwa Ummy Mwalimu,amesema,tayari Wizara yake imeshaanza kuchukua hatua kupambana na vitendo vya kutangaza dawa na chakula mitandaoni bila kusajiliwa na kwamba tayari mtu mmoja ameshakamatwa na wakati wowote anatarajiwa kufikishwa mahakamani kufutia kitendo chake cha kutangaza dawa ya kuongeza viungo vya wanaume na kudai kuwa Waziri Ummy,alifungua duka husika lililoko Kariakoo,jijini Dar Es Salaam wakati taarifa hizo zikiwa si za kweli.

    Katika hatua nyingine, aliwataka wale wote wanaotaka kuuza dawa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria kuepuka kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

    Kikao Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

    Balozi Seif azindua Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio

    $
    0
    0
     Makamu wa Pili wa Raius wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizindua Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
     Baadhi ya Washiriki wa Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
     Mkaazi wa Shirika hilo Nchini Tanzania Bibi Jacquiline Mahon akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA} kwenye Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu.
     Baadhi ya Viongozi wa Serikali walioshiriki kwenye Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
     Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman akitoa salamu za Wizara ya Afya katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
     Baadhi ya Watendaji wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa waliobahatika kushuhudia Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu.
     Balozi Seif akimpongeza Mmoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Al – Ahzar cha Nchini Misri kutokana na uamuzi wao wa kusaidia kufanyika kwa Mjadala huo wa Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu. Kati kati yao anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman. Picha na – OMPR – ZNZ.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al - Hajj Dr. Ali Mohamed Shein alisema maradhi mengi yanayowakumba Watoto yakikosa kushughulikiwa kwa Tiba sahihi katika hatua za awali huendelea kubakia kuwa matatizo ya kudumu katika maisha yao ya baadae.

    Alitanabahisha kwamba Mtoto asiye na afya njema kamwe hawezi kukua vizuri jambo ambalo huathiri ustawi wa maisha yake na baadhi ya wakati hushindwa kufanya vizuri katika masomo na kukosa ushirikiano mwema na wanafunzi wenzake.

    Dr. Ali Mohamed Shein alitoa kauli hiyo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Raius wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizindua Mjadala wa Kitaifa kuhusu Uzazi wa Mpangilio katika Mtazamo wa Kiislamu hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

    Alisema Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 90% ya Watoto walio na umri wa chini ya Mwaka Mmoja hunyonyeshwa, lakini ni Watoto 37 kati ya Watoto 100 walio na umri kati ya Mwaka Mmoja hadi Miwili ndio wanaonyonyeshwa kabla ya Mama zao kubeba ujauzito mwengine.

    Dr. Shein alisema hali hiyo inaonyesha wazi kwamba Jamii inahitaji kuimarisha Utamaduni muhimu kwa Wanawake wananyonyesha kwa kipindi kinachokubalika kama wanavyoifanya kina Mama walio wengi hivi sasa ili kuimarisha Afya za Watoto.

    Alisema asilimia 30% ya vifo vinavyotokana na Uzazi vinaweza kupungua kama Jamii itakuwa na matumizi mazuri ya huduma za Uzazi wa Mpangilio, na hii inajionyesha wazi elimu ya mpango huu kuanza kuwafikia Wananchi kutokana na Takwimu zinazothibitisha Wanawake 28 kati ya 100 hutaka kutumia huduma hizo.

    Rais wa Zanzibar alieleza kwamba njia hizo hawazipati kutokana na sababu tofauti ikiwemo ukosefu wa Taarifa sahihi za Afya ya Uzazi dhana zisizokuwa sahihi kuhusu njia ya Uzazi wa Mpangilio pamoja na ufahamu mdogo wa Elimu ya Dini juu ya suala la zima la uzazi wa mpangilio katika Uislamu.

    Alifahamisha kwamba wapo baadhi ya Watu wanaopotosha maana halisi ya Uzazi wa mpangilio kwa kuvihusisha vitendo vya utoaji wa mimba bila ya sababu zilizoruhusiwa za afya.

    Alisema hali hii imewafanya baadhi ya watu hasa akina Mama wakose hamu ya kutafuta na kupata taaluma sahihi juu ya suala hilo ambalo hata dhamira ya Serikali Kuu haihusiani na njia yoyote ya utoaji mimba kwa njia ye yote ile.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitahadharisha na kuonya kwamba ni kosa la jinai kufuatana na Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mwaka 2017. Hivyo Serikali inapinga vikali utoaji Mimba na vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya Watoto wa rika zote.

    Akigusia suala la unyonyeshwaji kwa Watoto, Dr. Ali Mohamed Shein alisema tafiti nyingi zimethibitisha kwamba Mama anaponyonyesha uwezo wake wa kuchukuwa mimba unapungua kutokana na mabadiliko ya kemikali zinazofanya kazi ya kusaidia mfumo wa kiwiliwili ufanye kazi vyema.

    Alisema hayo ni masuala muhimu yanayopaswa Jamii hasa Kina Baba kuyafahamu iwapo kutafanyika Mijadala itayotoa elimu itakayohusiana na masuala mazima ya mfumo wa uzazi wa mpangilio unaokubalika Kisayansi sambamba na Kidini.

    Dr. Ali Mohamed Shein aliwaeleza washiriki wa Mjadala huo wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpangilio katika Uislamu kwamba Serikali inatambua mafanikio makubwa katika uimarishaji wa Afya za Wananchi yanategemea usimamizi mzuri wa Mipango ya Taifa.

    Alisema juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Afya ya akina Mama na Watoto zimelenga katika kupunguza idadi ya Vifo vya Mama na Watoto vinayotokana na masuala yote ya uzazi.

    Hata Hivyo Dr. Shein alifahamisha kwamba Sera, Maendeleo na Sheria zilizopo za Nchi zimetoa uhuru kwa Wananchi kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu namna bora ya kupanga Uzazi kwa kutegemea Imani za Kidini, Utamaduni na Mipango ya Maendeleo ya Familia.

    Alisisitiza kwamba suala la Uzazi wa Mpangilo bado linaendelea kuwa ni suala la hiari kwa Wanafamilia kadri watakavyo, wanandoa kufuatana na Imani za Dini na Mitazamo yao.

    Dr. Shein alitanabahisha kwamba bado wapo baadhi ya Wananchi wenye hitilafu ya mawazo inayowapa taabu ya kutofautisha kati ya Uzazi na Mpango na uhuru wa kuzaa hasa pale Serikali inapoweka Mikakati ya kutekeleza Uzazi huo ambapo Watu hao hufikiria kuzuiwa kuzaa.

    “ Serikali ni Watu, walioichagua kwa ajili yao , kwa maslahi yao na kwa madhumuni yao. Serikali si ya Mtu Mmoja, bali ya Watu wote. Hivyo suala la uzazi ni la lazima kwa Maendeleo yetu” Alisisitiza Rais wa Zanzibar.

    Alisema Taifa linahitaji kuwa na kiazi kipya kitakacho chukuwa urithi wa kile chilichopo hivi sasa kwa lengo la kuimarisha nguvu kazi kadri ya Uchumi wake unavyoendelea kukua.

    “ Tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba tunazaa , ili pawe na warithi wa Taifa letu. Imani hii haipingani hata chembe na mafundisho na miongozo ya Dini”. Alifafanua Dr. Shein.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alieleza kwamba Serikali Kuu imeweka utaratibu mzuri wa kuzitambua na kuzikubali ndoa zote zilizofungwa kwa misingi ya Kiislamu na kwa taratibu za Dini Nyengine zinazojuilikana na kutambuliwa katika Sheria za Nchi.

    Alisema kinachofanyika kwa Serikali ni kufanya jitihada kubwa katika kutoa Elimu ya Uzazi wa Mpangilio unaozingatia mafundisho ya Dini zote zilizopo pamoja na maadili na Utamaduni wa Watu wa Zanzibar.

    Mapema kitoa Taarifa ya Mjadala huo wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpangilio katika Uislamu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Asha Ali Abdullah alisema asilimia 14% ya Wananchi wote Visiwani Zanzibar ndio wanaotumia Uzazi wa Mpangilio hali inayotoa mwana kwa Akina Mama wengi kuendelea na uzazi wa papo kwa papo unaoleta athari kwa afya za Mama na Mtoto.

    Bibi Asha alisema changamoto hiyo inatokana na mtazamo wa Jamii katika kuihusisha Dini na masuala ya Uzazi wa Mpangilio.

    Alisema juhudi za kushirikisha Viongozi wa Kidini zimesaidia kwa kiasi kikubwa kampeni ya kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vinavyosababisha maambukizo ya Ukimwi Nchini.

    Bibi Asha Ali Abdullah alisema ni vyema Kampeni hiyo iliyohusisha Viongozi wa Kidini kwa sasa ikaelekezwa katika kampeni ya kupunguza vifo vya Akina Mama kwa kuzingatia zaidi Uzazi wa Mpangilio.

    Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alilipongeza na kulishuruku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA},Taasisi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan pamoja na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al - Azhar cha Nchini Misri kwa moyo wao wa kusaidia Taaluma juu ya uzazi wa Mpangilio.

    Akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA}, Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo Nchini Tanzania Bibi Jacquiline Mahon alisema mchango mkubwa uliotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mufti Mkuu na Wizara ya Afya Zanzibar umesaidia kufanikisha Mjadala wa Kitaifa wa Uzazi wa Mpangilio katika Uislamu.

    Bibi Jacquiline alisema kitendo cha kufanywa mjadala huo kitatoa fursa kwa Wananchi walio wengi kupata Taaluma ya uelewa juu ya uhumimu wa kuimarisha Uzazi wa Mpangilio hasa ikizingatiwa kwamba hadi sasa Zanzibar ina asilimia 14% ya Watu wanaotumia Uzazi huo.

    Alisema asilimia hiyo ndogo ikiachiwa kuendelea upo uwezekano wa kutoa mwanya wa kukaribisha vifo vya papo kwa papo vya Akina Mama na Watoto vitavyoendelea kutokea kutokana na kutokuwa na mipango madhubuti ya kuwapa haki yao Akina Mama na Watoto ya kubeba Mimba na Kunyonyeshwa kwa mpangilio unaokubalika Kiafya.

    “ Kwa tafiti zilizowazi ni thuluthi Moja tu ya Akina Mama Visiwani Zanzibar wanaozingatia umuhimu wa Uzazi wa Mpangilio kwa kuchelewesha Mimba moja hadi kutunga Mimba nyengine”. Alisisitiza Bibi Jacquiline.

    Mwakilishi Mkaazi huyo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA}, Nchini Tanzania Bibi Jacquiline Mahon aliupongeza Uongozi wa Vyuo Vikuu vya Aga Khan na Al – Azhar ya Misri kwa ushirikiano wao na Taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Idadi ya Watu.

    Alisema Ushirikiano huo umesaidia kuchapisha vitabu mbali mbali vinavyosaidia kutoa elimu inayohusiana na Uzazi wa Mpangilio ambayo hutoa muelekeo wa kuzingatia maisha bora yanayofaa kuendelezwa na wana Familia .

    Bibi Jacquiline aliithibitishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Shirika hilo litaendelea kushirikiana nayo katika Mipango na Miradi yake ya Maendeleo hasa Dira ya 2020 pamoja na mapambano ya vita dhidi ya kupunguza vifo vya Akina Mama na Watoto.

    KORTI YAAMURU WASHTAKIWA TISA KESI YA WIZI WA KATONI 700 ZA KOROSHO KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 125

    $
    0
    0
    Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

    MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru  washitakiwa tisa wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa katoni 700 za korosho kulipa fidia ya Sh.milioni 125 kama hasara waliyoisababisha kwa Serikali.

    Washitakiwa hao ni  Robert Slaa, Isihaka Ngubi, Cathbert Mlugu, Mrisho Mindu, Mauridi Haji, Hamza Bunda, Kelvin Ngwandu, Joseph Robert na Joseph Mihayo wamesomewa adhabu hiyo leo Oktoba 23,mwaka 2019 baada ya kuomba msamaha na kukiri makosa yao.

    Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema washitakiwa wote wataachiwa huru kwa sharti la kutofanya kosa lolote kwa muda wa mwaka mmoja pia amewataka watimize masharti ya  makubaliano yanayowataka kulipa hasara ya korosho walizoiba.

    Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari 26 hadi Februari 6, 2018 katika yadi ya Kampuni ya Zambia Cargo and Logistics Limited, waliiba katoni 700 za Korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya Dola za Marekani 54,180 sawa  na zaidi ya Sh.milioni 125.

    Ilielezwa kuwa korosho hizo zilikuwa mali ya Barabara Trading Tanzania Limited na zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Vietnam.

    Ilidaiwa washitakiwa waliiba katoni hizo za korosho zilizokuwa katika kontena na kisha kuyajaza mchanga na mengine kuyaacha matupu.

    MSANII BARNABA ATOA SOMO KWA WASANII WANAENDA KINYUME NA MAADILI

    $
    0
    0



    NA RIPOTA WETU, BAGAMOYO

    MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya, Elias Barnabas ‘Barnaba’ amewapa somo wasanii wenzake na kuwaeleza watenganishe Ustaa na Umaarufu.

    Akizungumza akiwa katika jukwaa la tamasha la 38 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Barnaba alisema kuna baadhi ya wasanii wanachanganya mambo hayo mawili, jambo ambalo linasababisha baadhi ya wasanii kufanya mambo ambayo yanachafua kazi hiyo.

    Barnaba alisema baadhi ya wanaofanya mambo machafu kwa kutumia sanaa, wanakuwa hawana muda mrefu katika fani kwa sababu ya kutafuta ‘kiki’ badala ya kusaka namna ya kuboresha kazi zao.

    “Sitaki kuwasema wanaochafua taswira ya sanaa, lakini mnawajua, msifanye siasa za namna hiyo ambazo hazileti maana katika kuelimisha jamii,”alisema Barnaba.

    Alisema msanii ili afikishe ujumbe kwa jamii sio lazima afanye mambo ya ajabu kama yanayotendeka, mambo mengine ni baadhi ya wasanii kuvaa mavazi ambayo yanavuruga maadili.

    Aidha kabla ya Barnaba kupanda jukwaani, walioanza kufikisha ujumbe kwa jamii katika tamasha hilo ni kundi la Mazingaombwe la Ngome la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliogawa soda na kuonesha uwezo wa kutafuna nyembe sita.

    Burudani nyingine iliyooneshwa katika tamasha hilo linaloendelea ni maigizo ya kundi la Magic Bean Theatre Company la nchini Zimbabwe ambalo lilijikita katika utoaji elimu wa ulinzi kwa wanyama pori wakiwemo Tembo.

    Pia kulikuwa na maonesho mengine kama igizo la kulinda ngoma zetu, lililotolewa na wanafunzi wa shule ya msingi Mwambao.
    Viewing all 109996 articles
    Browse latest View live




    Latest Images