Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

DAWASA YAKESHA USIKU NA MCHANA KUREJESHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA KEREGE,AMANI

$
0
0
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imejikuta ikikekesha usiku na mchana katika kuhakikisha inarejesha maji kwa wakazi wa maeneo ya Kerege hadi Amani, Bagamoyo kufuatia kukatika kwa bomba kuu la inchi 54 linalosafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Meneja usambazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Eng. Tyson Mkindi amesema kuwa maji yalikuwa yamekatika kwa siku tatu mfululizo.

"Jitihada za kuwarejeshea maji wakazi wa maeneo mbalimbali zipo katika hatua za mwisho ingawa  kazi ya kurekebisha bomba hilo imechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kuwepo kwa maji mengi katika mto Rufijii". Amesema Eng. Mkindi.

Eng. Mkindi amesema kuwa, chanzo cha kukatika kwa bomba hilo kuu na kushindwa kusafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini inasababishwa na uchimbaji holela wa mchanga katika mto Rufiji na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

Hata hivyo Dawasa imechukua hatua ya dharura kwa kuchepusha maji kutoka katika bomba jipya la inchi 72 na kuyaingiza katika bomba la zamani la zege ambalo litazibwa kabla na baada ya mto ili kuruhusu wananchi walio kosa maji kutoka maeneo hayo kupata huduma hiyo kama awali. Amesema Eng. Mkindi

Aidha maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa bomba hilo ni Kerege, Mapinga, Kiharaka, Kiembeni, Mingo, Kilemela, Kimele, Vikawe, na Amani.
 Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Said Leonard(kushoto) akitoa maelekezo kwa dereva wa Tingatiga lililokuwa linaweka bomba vizuri wakati wa matengenezo ya bomba  na kuchepusha maji kutoka katika bomba jipya la inchi 72 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo ili kuweza kupatikana kwa maji katika maeneo yalipokatika kwa muda. Wa kwanza kulia ni Kaimu Meneja usamabazaji maji wa Dawasa, Eng. Tyson Mkindi.
 Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam(DAWASA), Steven Kirigo akichomelea bomba la  inchi 72 ili kuchepusha maji kwa ajili ya upatikanaji wa maji haraka kwa wateja ili kuendelea kutengeneza bomba la zamani wakati wateja wanapata maji. 
  Kaimu Meneja usamabazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Eng. Tyson Mkindi akitoa maelekezo wa mafundi wa waliokuwa wanatengeneza bomba hilo katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo usiku wa kuamkia leo ili wananchi waweze kupata maji kwa haraka.
 Tingatinga likiweka Chuma kwenye maungio ya bomba ili kuweza kuunganishwa.
Picha na Michuzi Blog.

Kilindi yaingia mradi wa Xprize Unesco yakabidhiwa vishikwambi 64

$
0
0
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi Vishikwambi 64 kwa shule ya msingi ya Kwamwande iliyopo wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.
Kukabidhiwa kwa Vishikwambi hivyo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kutumia teknolojia ya kisasa kunafanya wilaya za mkoa wa Tanga zinazofundisha kwa vishikwambi kufikia 7.
Vishikwambi hivyo vipo katika mradi wa kimataifa wa XPRIZE kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirkiana na WFP.
Wilaya ambazo mradi umeshafika kwa mwaka mzima na zaidi sasa ni Mkinga, Muheza, Handeni, Korogwe, Lushoto na Pangani.
Mradi huo ambao ulikadiriwa kuwafikia watoto 2,060 ambao hawako shuleni tayari umeelezwa kuwa na mafanikio makubwa kwani umefikia watoto 2,700 na taarifa zilizopo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na UNESCO umefanya vyema pamoja na kuwapo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo kupotea, kuharibika kwa vifaa au kuibiwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO, Dar es Salaam, Bi. Faith Shayo, kuingizwa kwa wilaya ya Kilindi kumetokana na kuonekana  kwamba mradi huo wanaouratibu ulifadhiliwa na XPRIZE na kuendeshwa na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kuwa na mafanikio makubwa.
Alisema kwamba mradi huo umeleta utofauti mkubwa na sasa wameupeleka katika shule 7 za wilaya ya Kilindi.
Alisema japokuwa katika wilaya zingine watoto walipewa kwa ajili ya kujifunza wao wenyewe na ikaonekana kwamba baada ya miezi  15 walipopimwa waliweza kujua kuandika kusoma na kuhesabu, kwa wilaya ya Kilindi mradi huo unakwenda katika shule 7 na teknolojia hiyo itabaki kulindwa katika shule husika.
Alisema kama katika wilaya nyingine matokeo yalikuwa mazuri pamoja na kukosa walimu wa kuwasimamia, ni matumaini yake kuwa wilaya ya Kilindi itakwenda kasi zaidi kutokana na kuwapo na usimamizi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Hamisi Athumani alisema kwamba uwapo wa teknolojia hiyo utasaidia sana kuboresha elimu kwakuzingatia ukweli kwamba dunia iliyopo sasa ni ya ubunifu na watoto lazima kuanza kuendana na ubunifu huo kwa kujifunza kwa njia ya teknolojia.
Diwani wa kata ya Bokwa ambapo shule hiyo ipo, Idrisa Mgaza alisema kwamba kata yake inashukuru kwa mradi huo ambao wanauona ni wa neema kubwa.
Aliahidi kuulinda mradi huo ambao ulipelekwa Julai mwaka huu kwa kujengwa mifumo ya nishati jua kwa ajili ya kuchaji vishikwambi.
Alisema umuhimu wa teknolojia hiyo haupo katika elimu pekee bali na kuanza kumiliki uendeshaji wake hasa kutokana na kuwapo wa somo la Tehama.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu alisema mradi huo mkoani Tanga unaenda vyema na kuitaka jamii kuendelea kuenzi mchango huo wa UNESCO katika kukiinua kizazi kijacho.
Alitaka vifaa vya mradi huo kutunzwa na kulindwa ili viweze kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
Alisema uzuri wa mradi huo ni kuwezesha kusaidia watoto wa mazingira magumu nao kupata haki zao za msingi za kieleimu.
Naye Mgeni rasmi katika shughuli ya makabidhiano shuleni  Kwamwande, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula alishukuru UNESCO kwa mradi huo.
Aidha aliitaka jamii kutambua umuhimu wa elimu na kuikumbatia teknolojia iliyopelekwa eneo hilo kwa manufaa ya Taifa.
“Naomba tutoe ushirikiano kuwezesha kuipokea na kuikumbatia teknolojia ili isaidie ubunifu” alisema Mkurugenzi huyo.
Alitaka teknolojia hiyo kutumika kwa malengo yake ya kufunza watoto na si vinginevyo, hata kama teknolojia hiyo inaweza kufanya ya ziada.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (wa pili kulia) Vishkwambi 64 kwa ajili ya kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia ubunifu wa teknolojia vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota (kushoto) na Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza (kulia).
 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (katikati) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwamwande, Hamisi Athumani Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa juma wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
 Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza akitoa neno la shukrani kwa UNESCO na WFP wakati wa hafla  ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Kwamwande wakitoa burudani wakati wa hafla  ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kulia) na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula (kushoto) wakiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga walipokuwa wakitumia Vishkwambi hivyo viliyotolewa mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi hivyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (wa pili kulia), Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Mathias Mvula (kushoto) wakiwaangalia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga walipokuwa wakitumia Vishkwambi hivyo viliyotolewa mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kuwezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia bila ya kuwapo kwa walimu jirani nao wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi hivyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
 Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo (katikati kushoto) wakijitambulisha ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota (katikati) walipofika wilayani hapo kabla ya kuelekea kwenye eneo la tukio katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo Kilindi mkoani Tanga kukabidhi Viskwambi kwa ufadhili wa mradi wa kimataifa wa XPRIZE.
 Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo pamoja na Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu wakiwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga katika hafla ya kuabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP.
 Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Shabani Gwandu akiitambulisha meza kuu kutoka kushoto kwake Mratibu wa mradi wa kimataifa wa XPRIZE Unesco, Bi. Levira Basilina, Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu, Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo, Mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota pamoja na Diwani wa Kata ya Bokwa halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga, Bw. Idirisa Mgaza wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Bw. Gracian Makota akitoa neno la ukaribisho wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.

 Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.

 Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo akitoa salamu za Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika hilo wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
 Ofisa Elimu mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule wa Wizara hiyo Bw. Mathias Mvula wakati wa hafla ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP kwa shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi, mkoani Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bi. Faith Shayo katika picha ya pamoja na kikundi cha burudani kilichotumbuiza wakati wa hafla  ya kukabidhi Vishkwambi 64 vilivyotolewa na mradi wa kimataifa wa XPRIZE unaoratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na WFP iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi Kwamwande iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI AKABIDHI OFISI YA MWAUWASA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (aliyekaa kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati kulia) akimkabidhi nyaraka za makabidhiano ya Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto). Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA, Christopher Gachuma (wa pili kushoto) na Makamu wake, Edith Mudogo (wa kwanza kulia).
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) mara baada ya kumkabidhi Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA na Mhandisi Msenyele alikuwa Meneja Miradi MWAUWASA. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (nyuma katikati) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na wafanyakazi wa MWAUWASA (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi Ofisi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (katikati) na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA.
Baadhi ya wafanyakazi wa MWAUWASA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukabidhi Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA. 

LIGI YA EPL YATOA WACHEZAJI 15 KUWANIA BALLON D'OR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ww Ulaya Virgil van Dijk ni mmoja wa wachezaji saba wa Liverpool waliotajwa kwenye orodha fupi ya wanaume 30 tuzo ya mchezaji bora wa Dunia  Ballon d'Or ya 2019.

Tuzo hizo zitatolewa Desemba 2 mwaka huu na wa timu ya Liverpool jumla ya wachezaji saba wametajwa na kufanya timu kutoka Ligi ya England kuingiza wachezaji wengi.

Wachezaji hao ni Mohamed Salah, Sadio Mane, Roberto Firmino, Trent Alexander-Arnold, Georginio Wijnaldum na Alisson pia wamechaguliwa kutoka kwa Reds.

Timu ya Manchester City imeingiza wachezaji watano ambao ni Raheem Sterling, Riyad Mahrez, Kevin de Bruyne, Bernardo Silva na Sergio Aguero , Wengine ni  Tugoham Hugo Lloris na Son Heung-min pia wamejumuishw kutoka Tottenham Spurs.

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo na Mshambuliaji wa Barcelona  Lionel Messi, ambao wameshinda tuzo hiyo mara 10 kati yao, wanaonekana tena kati ya wagombea huku Mshambuliaji Paris St-Germain na Brazil Kylian Mbappe.

Barcelona wana wachezaji wanne ambao wengine ni  Frenkie de Jong, Marc-Andre ter Stegen na Antoine Griezman.

Walinda milango  ni Alisson wa Liverpool, Ederson wa Manchester City, Kepa Arrizabalaga wa Chelsea na Lloris wa Tottenham.

Walioteuliwa pia ni Manuel Neuer wa Bayern Munich, Samir Handanovic wa Inter Milan, Jan wa Oblak wa Atletico, Ajax's Andre Onana, Juventus 'Wojciech Szczesny na Ter Stegen wa Barcelona.

Mchezaji bora chini ya miaka 21 na huchaguliwa na washindi wa zamani wa Ballon d'Or  na mwaka 2018, Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain aliweza kuchukua tuzo hiyo.

Waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo kwa mwaka huu ni pamoja na Jadon Sancho  19 kutoka  Borussia Dortmund na England Moise Kean, 19 Everton, Italia na kiungo wa Ufaransa wa Matteo Guendouzi, 20.

Wengine ni mlinzi wa Uholanzi wa Juventus Matthijs de Ligt, 20, beki wa Real Madrid, Vinicius Junior, 19, Valladolid na beki wa Ukraine Andriy Lunin, 20, Bayer Leverkusen na kiungo wa Ujerumani Kai Havertz, 20, Atletico Madrid na  Joao Felix , 19, Ureno  Villarreal na mshindi Samuel Chukwueze, 20, Nigeria na Lee Kang-in, 18 Valencia na Korea Kusini.

Orodha ya wachezaji wote ni kama ifuatavyo.
Virgil van Dijk (Liverpool)

Bernardo Silva (Manchester City)

Son Heung-min (Tottenham)

Robert Lewandowski (Bayern Munich)

Roberto Firmino (Liverpool)

Alisson (Liverpool)

Matthijs de Ligt (Juventus)

Karim Benzema (Real Madrid)

Georginio Wijnaldum (Liverpool)

Sergio Aguero (Manchester City)

Frenkie de Jong (Barcelona)

Hugo Lloris (Tottenham)

Dusan Tadic (Ajax)

Cristiano Ronaldo (Juventus)

Kylian Mbappe (Paris St-Germain)

Trent Alexander-Arnold (Liverpool)󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

Donny van de Beek (Ajax)

Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal)

Marc-Andre ter Stegen (Barcelona)

Sadio Mane (Liverpool)

Lionel Messi (Barcelona)

Riyad Mahrez (Manchester City)

Kevin de Bruyne (Manchester City)

Kalidou Koulibaly (Napoli)

Antoine Griezmann (Barcelona)

Mohammed Salah (Liverpool)

Eden Hazard (Real Madrid)

Marquinhos (Paris St-Germain)

Raheem Sterling (Manchester City)

Joao Felix (Atletico Madrid)

WAZIRI JAFO AZINDUA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU "TEKNOLOJIA HAIEPUKIKI"

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WALIMU nchini wametakiwa kutambua kuwa matumizi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wakati wa sasa ni muhimu na si jambo la hiyari kulifahamu.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo wakati akizindua mafunzo ya TEHAMA kwa walimu kutoka Mikoa mbalimbali nchini iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Waziri Jafo amesema katika wakati huu teknolojia ni suala la lazima hivyo ni vema kutengeneza vijana ambao ni wabobezi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili waweze kuajiriwa katika mamlaka za serikali za mitaa na maeneo mengine ambayo kwa sasa yanatumia mifumo hiyo hasa katika eneo la ukusanyaji wa mapato.

Jafo amefafanua kuwa, awali mifumo ya analojia ilikuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa upotevu wa mapato katika mamlaka za serikali za mitaa, lakini kwa sasa mapato ya serikali yameongezeka mara dufu.

Amesema tangu mwaka 2016 walipoanza kutumia mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwenye mamlaka za serikali za mitaa mianya ya wizi na upotevu wa mapato umekwisha.

“Nyinyi washiriki ambao ni walimu kutoka mikoa mbalimbali 1044 ni wawakilishi wa wengi waliobaki huko mashuleni, hivyo hakikisheni mnawwakilisha vyema na nitahitaji kuiona mitihani yenu nione kama kuna tofauti ya kabla ya mafunzo na baada,” Amesema Waziri Jafo.

Pia alitangaza kufanya ziara katika shule za sekondari na msingi nchi nzima kukagua kama mafunzo hayo yanatumika na kama shule zilizopatiwa kompyuta zinazitumia ama walimu wakuu wamezifungia kwenye mabox mana kunatabia hiyo.

Naye Mkurugenzi TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, George Mbijima, amesema washiriki hao 1044 wametoka katika mikoa ambayo ni pamoja na Shinyanga, Tabora, Kigoma, Mwanza, Kagera, Geita Singida, Dodoma, ambapo walimu 1000 wanatoka katika shule za Sekondari na walimu 44 wanatoka katika shule za Msingi.

Naye wakilishi wa mfuko wa UCSAF , Justina Mashimba alisema, wamekuwa wakitoa mafunzo kuhusu TEHAMA pamopja na kugawa Kompyuta kwa walimu ambapo awamu hii watatoa kwa walimu 2000.

Amesema kundi la kwanza litahusu walimu 1044 na kundi la pili litahusu idadi ya walimu watakaokuwa wamebaki, na kwamba kundi la kwanza lina vituo 3 ambavyo ni DIT Jijini Dar Es Salaam, Dodoma na Mbeya.

Justina ameeleza kuwa mafunzo hayo walianza kutoa baada ya kubaini kuwa baadhi ya shule walimu na wanafunzi hawana uelewa kuhusu masula ya TEHAMA.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza na walimu kutoka Mikoa mbalimbali ambao wameanza mafunzo ya siku tano ya TEHAMA jijini Dodoma.
Walimu kutoka Mikoa mbalimbali nchini ambao wameanza mafunzo ya TEHAMA ya siku tano yanayoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo

CHUO KIKUU CHA UDSM KUANZA KUTOA MITIHANI YA KIMATAIFA YA UJUZI WA KISWAHILI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

KATIKA kukuza lugha adhimu ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinatarajia kuanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili (MKUKi) kuanzia Januari mwakani.

Mitihani hiyo itafanyika mara sita kwa mwaka ikiendana na kipindi cha masomo ya Kiswahili kwa kila ngazi na itafanyika kwa njia za kielektroniki katika vyuo na vituo vya Kiswahili duniani ambavyo tayari kuna makubaliano maalumu kuhusu mitihani hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo jijini Dodoma leo alipokua akizungumza na Wandishi wa habari.

" Lengo letu ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kukieneza Kiswahili na kusimamia ubora wake ambapo sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimechukua jukumu la kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu ili lugha ya kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili wanaojifunza lugha hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti," Amesema Dk Akwilapo.

Amesema katika lugha kuu za dunia mitihani hiyo hufanyika ikiwa na majina mbalimbali kama mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kichina inajulikana kama HSK na HSKK, Kihispaniola inajulikana kama DELE, Kiingereza inajulikana kama TOEFL na ya Kiarabu inajulikana kama ALPT.

Dk Akwilapo amesema Chuo Kikuu cha CKD kinakua chuo cha kwanza duniani kutunga mitihani hii na kusimamia utahinj wake na mwisho hutoa cheti cha kimataifa kuonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa.

Ameeleza kuwa tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa CKD na walimu wanaofundisha Kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hiyo ambayo itaanza kutolewa mwakani.

”CKD kimejiandaa kuhakikisha kuwa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iko madhubuti kuwezesha mitihani hii kufanyika kwa ufanisi na kwa viwango vya kimataifa. Kwani kuna wahitaji ambao watafanyia mitihani hii wakiwa katika nchi zao, sio lazima wasafiri na kuja kufanyia mitihani yao hapa Tanzania,” Amesema.

Amebainisha kuwa walengwa wa mitihani hiyo ni watu wote ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili au lugha ngeni katika ngazi mbalimbali ikilenga kupima usanifu katika kusoma, kuandika, kuongea na kusiukichangia ambapo amesema wanaamini wanapaswa kuongeza juhudi za kukuza Kiswahili ili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifanya jitihada kubwa za kueneza na kukuza lugha hiyo katika Nchi za Afrika na duniani kwa ujumla.

" Serikali ya awamu ya tano imekua mstari katika kukuza lugha yetu hii adhimu ya Kiswahili. Tumeona hata wakuu wa Nchi za SADC walikubaliana kutumia lugha yetu, sasa ni jukumu letu kuongeza juhudi ili Kiswahili kiweze kuenea sehemu mbalimbali duniani," Amesema Dk Akwilapo.

Aidha Dk Akwilapo akizungumzia mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu nchini (UMISAVUTA) yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 25 ya mwaka huu mkoani Mtwara.

" Tunatarajia uzinduzi rasmi utafanyika Oktoba 27 ambapo mgeni rasmi atakua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye atamuakilisha Waziri Mkuu ambapo yatafanyika kwa siku Sita na kushirikisha washiriki wapatao 5,600 kutoka vyuo vya ualimu vya Serikali, " Amesema Dk Akwilapo.

Ameitaja michezo itakayoshindaniwa kuwa ni Mpira wa Pete, Miguu, Wavu, Kikapu, Riadha na mashindano ya kuchora ambapo amesema lengo ni kukuza vipaji na kuwafanya walimu wawe na weledi wa kufundishia.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, DK Leonard Akwilapo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma wakati alipokua akitangaza kuhusiana na mitihani ya kimataifa ya Kiswahili ambayo itaanza kutolewa na Chuo Kikuu cha UDSM. Dk Akwilapo pia alizungumzia mashindano ya Michezo kwa Walimu Nchini yatakayoanza kutimua vumbi Oktoba 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Profesa Aldin Mutembei akifafanua jambo kuhusiana na mitihani hiyo ya Kiswahili ambayo itakua ikitolewa na Chuo Kikuu cha UDSM.

WAZIRI LUGOLA APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA WATUMISHI WALIOKUWA NIDA KUUZIWA MAGARI YA SERIKALI, AIPONGEZA KAMATI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akipokea taarifa ya Uchunguzi wa Watumishi waliokuwa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuuziwa magari ya Serikali, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wamoja Ayubu, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kamati hiyo iliteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (hayupo pichani), Septemba 16, 2019 na ilipewa hadidu za rejea 13 kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akizungumza katika kikao cha kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa Watumishi waliokuwa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuuziwa magari ya Serikali, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kamati hiyo iliteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), Septemba 16, 2019 na ilipewa hadidu za rejea 13 kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wamoja Ayubu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (meza kuu kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa Watumishi waliokuwa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuuziwa magari ya Serikali, Wamoja Ayubu (watatu kushoto), alipokuwa anaiwasilisha taarifa hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kamati hiyo iliteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia meza kuu), Septemba 16, 2019 na ilipewa hadidu za rejea 13 kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni, na kulia Mkurugenzi Msaidizi Utawala, Subira Sawasawa, pamoja na wajumbe wa kamati hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa Watumishi waliokuwa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuuziwa magari ya Serikali, Wamoja Ayubu, akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), wakati alipokuwa anaiwasilisha taarifa yake ya uchunguzi kwa Waziri huyo pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola (wapili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa Watumishi waliokuwa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuuziwa magari ya Serikali, Wamoja Ayubu (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo. Mstari wa nyumba kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni, na kulia Mkurugenzi Msaidizi Utawala, Subira Sawasawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

UONGO, UMBEA NA HUSUDA VIMESHUSHA VIWANGO VYA UBUNIFU -RC MAKONDA

$
0
0
* Awataka wanasiasa kuacha kubeza imani za watu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MATUMIZI mabaya ya mitandao ya kijamii yameelezwa kuzorotesha bunifu zenye tija katika jamii badala yake watu wamejikita katika kueneza, kusambaza, na kujaribu kuthibitisha taarifa za uongo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Makonda amesema kuwa upotoshaji katika mitandao ya kijamii umezidi kushamiri na kuwataka wakazi wa jiji hilo na wanajamii kwa ujumla kujihadhari na maneno wasiyoyafahamu na yasiyo na ukweli.

"Mtu akisema akisema uongo mara moja akabainika atengwe katika jamii, kueneza habari za uongo katika mitandao ya kijamii ambayo inatumiwa na idadi kubwa ya watu ni kuendelea kuathiri watu kwa kuwafanya kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kibunifu zenye tija badala yake wanapambana na masuala ya uongo kwa kujaribu kutafuta ukweli" ameeleza Makonda.

Kuhusiana na kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ya kuwataka wananchi kushiriki shughuli za kimaendeleo na kuabudu kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili sio kushinda kwenye nyumba za ibada kila siku Makonda ametengua kauli hiyo na kusema kuwa, Serikali haina dini na amewataka wananchi kuendelea na ibada bila kuathiri shughuli za kiserikali.

Amesema kuwa wanasiasa wawe makini wanapoongea kuhusiana na dini;
" Tuwe na kiasi tunapoongelea imani za watu, Mungu anaabudiwa kila siku wana Ilala endeleeni kuabudu na si vyema kupanga siku za kuabudu" amesema Makonda.

RC Paul Makonda


RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA MAHAKIMU NA MAJAJI ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatil Bahar Mbweni Zanzibar.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hotuba na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatil Bahar Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatil Bahar Mbweni Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein   katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatil Bahar Mbweni Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI UUZWAJI WA NYAMAPORI WAKATI IKIENDELEA NA UPITIAJI WA KANUNI ZA UANZISHWAJI WA MABUCHA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus Arusha.

Wizara ya maliasili na utalii imepiga marufuku wananchi kuuza nyama pori wakati ikiendelea na kupitia kanuni na rasimu,ambapo ifikapo desemba mwaka 2019, kanuni hizo zitakuwa zimekamilika na watatangaza kwa umma ,maeneo yatakapokuwepo mabucha hayo ,na serikali itaendelea kudhibiti biashara hiyo ,ili mwananchi aweze kununua nyama hiyo kwa njia halali.

“Haitachukua muda mrefu kanuni hizi zitatoka na tutatoa maelekezo watu wanaotaka kufungua hayo mabucha watayafungua kwa utaratibu gani”

Hayo yamekuja baada ya Mhe.Rais Magufuli akiwa mkoani Katavi alitoa maagizo kwa Wizara hiyo, huku akikumbushia maagizo ambayo alikwisha yatoa kwamba, ihakikishe inaanzisha mabucha ya kuuza nyama pori ili kuondoa na kudhibiti vitendo vya ujangili na kuwapa fursa wananchi waishi pembezoni mwa hifadhi kupata kitoweo kwa kuwa ni chakula chao cha asili.

Akizungumza jana Jijini Arusha na vyombo vya habari Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolfu Mkenda alisema kuwa wizara itaendelea kudhibiti na kuhakikisha hakuna mwananchi hata mmoja atakayeruhusiwa kuuza nyama pori hadi pale serikali itakaporidhia.

“Sasa hivi tunapambana sana na ujangili wawanyama pori ambao wanakamatwa kwa mitego kaskazini mwa Serengeti,imeanza kuingia kidogo maeneo ya seluu,tunakamata watu sana lakini baadhi ya wenyeji wa kule nyama pori ni chakula chao cha asili”Alisema Profesa Mkenda.

Alisema kuwa wanyama wote watakaowindwa kwaajili ya kuuzwa kwenye mabucha lazima wapimwe na waganga/Madaktari kwasababu wanyamapori wanamagonjwa mengi ambayo yamnaweza kuleta athari kwa afya ya binadamu.

“Wanyama pori wana magonjwa kuliko mifugio ya kawaida ni lazima wapimwe,wajulikane wajulikane wale wanaotakiwa kitaalamu kwaajili ya kuliwa ili kuondoa changamoto ya wananchi kupata maradhi yatokanayo na wanyama pori.Alisema Profesa Mkenda.

Agizo hilo limekuja baada ya waandishi wa habari kutaka kujua mchakato wa uanzishaji wa mabucha ya nyama pori utaanza lini na vilevile wizara imejipangaje kuhakikisha zoezi hilo linaepuka ujangili wawanyama.

Profesa Mkenda akijibu maswali hayo amesema kuwa Wizara lazima ipitie Kanuni na rasimu kwani tayari imekamilika vizuri na imeshawasilishwa kwa Waziri,zitajadiliwa,zikishapita zitatolewa rasmi kama kanuni,kisha waanze kufungua mabucha, ili wananchi wanaoishi kando ya hifadhi waweze kupata fursa ya kupata kitoweo hicho kwa bei inayoendana na hali zao kama yalivyo maagizo ya Mhe.Rais.

Ametanabaisha kuwa baada ya kupitishwa na waziri hiyo itakuwa fursa ya kununua nyama pori ndiyo maana hadi sasa wamekuwa wakipeleka maeneo mbalimbali yakiwemo kwenye matamasha ya urithi wetu na wamekuwa wakitoa bure kwasababu hakuna kanuni ya uuuzwaji wa nyama pori.

Alisema wananchi ambao wananishi pembezoni mwa hifadhi ambapo nyama pori ni chakula chao cha asili ,hivyo watahakikisha kuwa kunakuwepo na usawa wa bei ambayo mtu atanunua kwa njia halali,zisijeuzwa mijini mijini peke yake.

Pia alisema kanuni hiyo itatoa mwongozo aina ya wanyama watakaowindwa ,bei na utaratibu mzima wa uwindaji wao na namna ya kufungua mabucha hayo kwa haraka zaidi kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla. 

“Mfano mnyama mbogo anatembea na magojwa ambayo yanaweza kumuathiri binadamu ,Yule atakayeruhusiwa kuuza nyama piori lazima apate kibali cha wagani ,hatuwindi wanyama majike,watoto bali wale wqanaokubalika kitaalamu, yanaweza kumwambukiza hatutakuruhu nyama pori kiholela tutakukamata .Alisema Profesa Mkenda.

WAGANGA WA KIENYEJI NCHINI WAONYWA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga leo kulia ni Mjumbe wa Chama hicho Taifa Oscar Changala
 OFISA Habari wa Mkoa wa Tanga Zuberi akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 SEHEMU ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania 
 MWENYEKITI wa Klabu ya Waaandishi wa Habari Mkoani Tanga Hassan Hashim akichangia jambo kwenye mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph akiuliza swali kwenye mkutano huo.

WAGANGA wa Kinyeji hapa nchini wametakiwa kuacha kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wawahimiza wazazi kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo.


Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.


Alisema kwani kumezuka tabia ya baadhi ya waganga wa kienyeji kuwapokea wagonjwa hao huku wakijua kwamba hawawezi kuwatibia matatizo waliokuwa nayo jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa wengi wao kuzidiwa na ugonjwa walinao.


“Ndugu zangu waganga wa kienyeji achani kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wazazi wahakikishe mnawapaleka kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo”Alisema.


“Lakini pia acheni kusema kwamba watoto wenu wamerogwa, balaa wala mikosi bali wapelekeni hospitalini wapate tiba ya magonjwa yanayowakabili “Alisema


Hata hivyo aliwataka pia wasiende kwenye maombi,makanisani wale misikitini badala yake waende hospitalini kwenda kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kuondokana na matatizo yanayowakabili.


“Wananchi achaneni na imani potofu juu ya ugonjwa huo huku akitaka waupige vita kwani baadhi yao wana imani kuwa ni mizimu jambo ambalo halina ukweli wowote.


Awali akizungumza katika mkutano huo Afisa Ustawi wa Jamii Mmasa Malugu aliwataka waandishi wa habari kutumia vema kalamu zao ili kuweza kusaidia kuwafichukua watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi waliopo kwenye jamii.


Alisema kwamba lazima jamii ibadilike na kuondokana na fikra potovu kuhusiana na kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke hospitali ili waweze kupatiwa matibabu.

Nafasi ya sekta ya mawasiliano katika kulipeleka taifa letu kwenye uchumi wa kati

$
0
0
LENGO la Taifa lolote duniani kufikia uchumi wa kati huwa na changamoto nyingi. Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa nchini Tanzania tunayo bahati kwamba kwa muongo mmoja uliopita tumekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa wa wastani wa asilimia 8. 

Sambamba na hilo takwimu hizo zinaonyesha pia kuwa Tanzania imehakikisha kuwa ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri, kikiwa kwenye wastani wa asilimia 1.9.

Mafanikio haya makubwa ya kiuchumi na soko la ajira yamechangiwa kwa kiasi fulani na sekta binafsi na biashara mihimili katika sekta hiyo ikijumuisha teknolojia, ujenzi na mawasiliano. Kwa pamoja makampuni katika maeneo hayo matatu yametoa ajira kwa idadi kubwa ya Watanzania. 

Mojawapo ya sababu ya makampuni katika eneo hilo kufanikiwa katika suala la kutoa nafasi za ajira ni kwa sababu huduma zake zinahitajika katika sekta nyingine zote za uchumi. 

Kusisitiza hilo, kwa mfano tuitazame sekta ya mawasiliano ya simu. Aina ya ajira ambazo sekta hii inatoa zinakwenda mbali ya namna ambavyo awali ilitazamwa. Mfano sekta hii ina mawakala wa fedha, wasambazaji na wauzaji wa huduma za simu, wataalamu wa huduma kwa wateja na wengineo. 

Zaidi ya hiyo, sekta hiyo pia inahitaji wataalamu toka maeneo mengine mengi mfano wahandishi wa mitambo ya mawasiliano na wachambuzi wa takwimu. 

Wapo wataalamu lukuki wa fani mbalimbali ambao wanahakikisha masaa 24 mitambo iko sawa kutuwezesha kupata huduma na kutumia simu zetu bila tatizo mfano kuperuzi mtandaoni, kununua bando, kutuma na kupokea pesa, SMS, na nyingine nyingi. 

Tigo Tanzania ni mfano mmojawapo wa kampuni hizo. Kampuni hii inatajwa kama mwajiri muhimu nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 115,000 wenye ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.  

Nchi yetu haina budi kuendelea kuunga mkono sekta hii na wadau wake wa namna hiyo ili kusukuma mbali zaidi gurudumu la maendeleo ya uchumi wetu.

MWEKEZAJI TOKA SWEDEN ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine akiwa katika kikao cha pamoja na Wageni kutoka  Sweden waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais,  katika mji wa Serikali jijini Dodoma. Madhumuni ya ugeni huo ni kuelezea nia ya Kampuni ya ECO Sysytem International ya kusambaza teknolojia ya kisasa ya kupunguza uchafuzi wa hewa unaosababishwa na magari .
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Catherine Bamwenzaki akiangalia mfano wa kifaa kitakachotumika kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa hewa unaosababishwa na magari ya aina yote anyemuangalia ni Injinia Julius Enock kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na   Wajumbe Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Mwekezaji kutoka Sweden waliohudhuria kikao hiko jijini Dodoma.

WANANCHI WA KATA YA MOSHONO WAMUANGUKIA RAIS MAGUFULI

$
0
0

Na Woinde Shizza,Michuzi Tv Arusha

WANANCHI wa kata za Moshono jijini Arusha na Mlangarini wilayani Arumeru wamemuomba Rais, Dkt John Magufuli kuingilia kati na kuumaliza mgogoro wa ardhi baina yao na Jeshi la Wananchi, (JWTZ) kikosi cha 977 kwenye eneo la mita 100 kuzunguka mlima Lesurwai.

Wamemuomba Rais Magufuli awasaidie kama alivyowasaidia wananchi wa mkoani Katavi ambao aliamuru wasiondolewe kwenye ardhi yao ambayo tayari mahakama ilikuwa imeshaamuru wananchi hao zaidi ya 1,200 waondolewe.Aidha wamemuomba awanusuru kwa kuamuru wanaostahili fidia walipwe kwa thamani halisi ya mali na wale walio maeneo nje ya mita 100 wasibugudhiwe.

Wananchi hao waliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati walipokusanyika pembezoni mwa mlima Lesurwai yalipo makazi yao kujadili hatma yao.

Akisoma maazimio ya kikao hicho, Jeremea Jacob alisema kuwa kwa pamoja hawakubaliani na namna zoezi la kulipa fidia linaloendelea kwa sasa kwa kile walichodai kuwa limetawaliwa na utata mkubwa kwani tathmini hiyo ilifanyika mwaka 2012 na kutokana na jeshi kuchelewa kurudi kulipa fidia kwa miaka mingi waliamua yaendeleza maeneo hayo na mengine kuwapa watoto wao wakayaendeleza jambo ambalo halijazingatiwa kwenye fidia inayolipwa.

Aidha wamedai kuwa kuna mkanganyiko umejitokeza kwenye orodha ya fidia ambapo kuna baadhi ya wananchi wa kata ya Mlangarini majina yao yanaonekana kwenye orodha ya wakazi wa Moshono hivyo kutakiwa kwenda kulipwa kwenye halmashauri ya jiji la Arusha wakati kiuhalisia hawako jiji.
 
Alisema hali hiyo ilimlazimu aliyekuwa mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya ya Arusha, Dk  Wilson Mahera ambaye kwa sasa ameteuliwa kuaa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusitisha zoezi la ulipaji fidia.

Jacob alisema kuwa kwa upande wa jiji la Arusha zoezi la ulipaji fidia limetawaliwa na urasimu wa hali ya juu kwa kile alichodai kuwa  mwananchi akifika kwenye chumba namba 52 ambacho kinashughulika na kulipa fidia akiuliza kiwango anachopaswa kulipwa haambiwi zaidi anaambiwa atoe namba za akaunti ya benki atakuta hela zake.

Alidai  kuwa kuna wananchi ambao wamejenga nyumba kwenye maeneo hayo lakini wamejikuta wakilipwa fidia ya shilingi laki tatu ambayo haimtoshelezi hata kulipia kodi ya pango ya nyumba ya kuishi na familia yake kwa mwaka mzima kulingana na kodi za pango zinazotozwa kwenye jiji la Arusha kwa sasa.

MATAIFA 16 BARANI AFRIKA YAFANIKIWA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WACHEZAJI WA LIGI ZA NDANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MATAIFA 16 Barani Afrika  yamefanikiwa kutinga Fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) 2020 nchini Cameroon.

Mechi za mwisho zilipigwa siku ya Jumapili na kwa timu 16 kukamilika, huku vigogo wa soka Wakitupwa nje ya fainali hizo.Timu ya Ghana 'Black Stars' imeshindwa kuifunga timu ya Burkina Faso katika  mji wa Ouagadougou.

Senegal, pia ni timu kubwa iliyoondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penati.Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijitutumua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0.

Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza na kuondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .Tanzania ilikuwa ni nchi ya pili kufuzu fainali hizo baada ya kuwaondoa Sudan kwa wingi wa mabao  baada ya kutoka sare ya 2-2.

Zimbabwe imejitakatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.DR Congo iliichapa Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushindi ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.

Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Libya.
Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0.

Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria.

Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN) yatakayoandaliwa na Cameroon:

Cameroon (mwenyeji)
Tanzania
Uganda
Rwanda
Zambia
Namibia
Togo
Morocco
Zimbabwe
DR Congo
Congo
Tunisia
Burkina Faso
Guinea
Niger
Mali


WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA MABORESHO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI NCHINI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo akitoa maelekezo alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Pwani.
 Afisa Uwekezaji Mwandamizi Bw. Michael Semiono akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Pwani.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Pwani.

Afisa Uwekezaji Mwandamizi Bw. Michael Semiono akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo machapisho ya WCF alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Pwani.

Na. Sarah Reuben
WANANCHI waliotembelea Maonesho ya Pili ya Viwanda mkoani Pwani wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maboresho makubwa ya fidia kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na umma. 

Akizungumza alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Eng. Evarist Ndikilo amesema tangu kuanzishwa kwake Mfuko huu umekuwa faraja kwa wafanyakazi wengi hususan wafanyakazi wa viwandani.

“Binafsi niwapongeze sana WCF kwa kuwa mnafanya kazi nzuri sana na hata wananchi wameendelea kuipongeza sana Serikali kwa kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii hususan malipo ya fidia kwa wafanyakazi. Hali hii imechangia kuongeza motisha kazini na  kuimarisha mahusiano kati ya mwajiri na wafanyakazi wake,” alisema Eng. Ndikilo.

Eng. Ndikilo aliwaalika wananchi kutembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ili kuongeza uelewa kuhusu majukumu ya Mfuko huo ikiwemo taratibu za madai ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza pindi mfanyakazi atakapopata ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi. 

Nao baadhi ya wajiri walipotembelea banda la WCF wamesema wameongeza uelewa kuhusu masuala ya fidia na mafao yanayotolewa na WCF. 

“Mimi binafsi nilidhani bima ya afya inagharamia matibu yoyote ya mgonjwa hata yale yanayotokana na ajali au ugonjwa unaotokana na kazi lakini leo nimefahamu WCF ndiye mwenye kulipa gharama za matibabu hayo,” alisema Dkt. Aden Mpangile alipotembelea banda la Mfuko huo. Aliongeza kuwa, “Hapo awali sikufahamu kuwa kiwango cha fidia anachostahili kulipwa mfanyakazi hujulikana baada ya tathmini kufanyika kwa mfanyakazi aliyekamilisha huduma za matibu ambayo kimsingi matibabu hayo hugharamiwa na Mfuko”. 

Naye Afisa Uwekezaji Mwandamizi Bw. Michael Semiono amesema WCF ni mdau mkubwa wa maonesho ya viwanda ndio sababu Mfuko umeamua kushiriki kwenye maonesho haya ili kukutana na wadau wake ikiwemo wafanyakazi na wamiliki wa viwanda nchini. Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda, Mfuko umejielekeza kwenye miradi ya viwanda nchini iliyopo mkoa wa Dodoma, Morogoro, Tanga na Simiyu alisema Afisa huyo.  

Kuhusu mafao yatolewayo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Semiono amesema Mfuko unatoa mafao kadha wa kadha ikiwemo huduma ya matibabu yanayotolewa kwa mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa utokanao na kazi. Aliongeza kuwa Mfuko hugharamia huduma za ukarabati na ushauri nasaha pamoja na malipo ya ulemavu wa muda au ulemavu wa kudumu kwa mfanyakazi aliyekamilisha matibabu na kugundulika ana ulemavu huo.

Mafao mengine ni malipo kwa mtu anayemhudumia mgonjwa iwapo daktari watathibitisha mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa kazini hawezi kujihudumia, msaada wa mazishi na malipo kwa wategemezi iwapo mfanyakazi atafariki kutokana na kazi. 

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki kwa mara ya pili kwenye maonesho hayo kwa lengo la kuwafikia wadau wengi zaidi ili kutoa elimu kuhusu taratibu za madai kwa mfanyakazi aliyepata ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi pamoja na majukumu ya Mfuko kwa ujumla. 

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambao umeanzishwakwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka 2008.

WAFANYABIASHARA WA HOTELI NA VITUO VYA MAFUTA WAITEGA BONDE KATIKA ULIPAJI WA TOZO ZA MAJI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
BONDE la Wami/ Ruvu limesema kuwa baada ya Waziri wa Maji kutangaza tozo za visima vya majumbani kumefanya baadhi ya wafanyabiashara wa Hoteli na Vituo vya Mafuta wametumia fursa hiyo ya Waziri wa Maji kutolipa tozo za visima ambapo Bonde hilo linatarajia kuwafikisha mahakamani kwa kukiuka ulipaji wa tozo wa visima. 

Hata hivyo bonde la Wami/Ruvu linashangazwa baadhi ya wafanyabiashara wenye hoteli na vituo vya mafuta walikubali kulipa tozo za visima vya maji kidogo kidogo lakini baada ya Waziri wa Maji kutangaza kuondoa tozo za visima vya maji ya majumbani wafanyabiashara hao wametumia mwanya huo wa kutolipa tozo hizo. 

Akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema kuwa bonde limeweka mkakati kwa wote kuwapeleka mahakamani na waliokuwa wanalipa kidogo kidogo nao watalipia mahakamani huko. 

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa watu wasipolipa tozo vyanzo vya maji hiaviwezi kuendelea kutokana baadhi ya watu kufanya ukaidi wa kulipa tozo ambazo ziko kwa mujibu wa sheria. 

‘’Hawa tutapewapeleka mahakamani nasubiri mwanasheria afanye upembuzi wa wadaiwa kutokana na tozo hizo ndizo zinafanya bonde liendelee kulinda vyanzo vya maji sasa tutawezaje kupanda miti katika vyanzo hivyo wakati watu wanakaidi kwa makusudi kulipa tozo ambazo zimewekwa kisheria’’amesema Mhnadisi Ngonyani. 

Amesema kuwa serikali inataka kuchimba bwawa la maji kwa ajili ya dharula pale inapotokea vyanzo vya maji vimekuwa havina maji basi bwawa hilo lifanye kazi ya kupeleka katika mitambo na kazi hiyo ya uchimbaji inatokana na tozo za watu mbalimbali. 

Aidha amesema kuwa katazo la ulipaji wa tozo za visima vya majumbani hakufanyi sasa uchimbaji wa visima kwenda bila tozo hili halikubariki watu wote wanaotaka visima lazima wapate kibali pamoja na kulipa tozo na maji yatakayopatikana lazima yalipiwe tozo kwa ajili ya maabara ya kufanya uchunguzi wa maji hayo. 

Baadhi ya wadaiwa Wafanyabiashara ya Vituo vya Mafuta hawa hapa TSN Oil (T)LTD ,Simba Oil ,World Oil,OKOD International, Kobil.Mantrack pamoja na Gapco na Baadhi Wafanyabiashara wa Wamiliki wa Hoteli hizi hapa Dar Live ,Ice Land Hotel, Grand Villa. 

Tozo kwa wadaiwa hao ni zaidi ya milioni 328 huku wakiwa wamepata tozo hizo ni sh.milioni 149 tu huku Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) ikiwa haina deni ambapo Bonde limeipongza Dawasa. 
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza na waandishi haari kuhusiana na wadaiwa tozo za maji katika bonde hilo hatua watazozichukua kutokana na kukaidi ulipaji wa tozo ,jijini Dar es Salaam. 

Wafanyabishara Wahamasishwa Kuthibitisha Ubora wa bidhaa

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Pwani
WITO umetolewa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali mkoani Pwani kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuondokana na vikwazo vya kibiashara ndani na nje ya nchi.

Ushauri huo ulitolewa jana Ofisa Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Neema Mtemvu, wakati akizungumza washiriki wa Wiki ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara mkoani Pwani iliyoanza Oktoba 17, mwaka huu ikitarajiwa kufikia kilele chake kesho (Oktoba 23).

Mtemvu, alisema shirika hilo limeshiriki wiki hiyo Viwanda, Uwekezaji na Biashara kwa ajili ya kutoa elimu ya viwango kwa wafanyabiashara na wajasiriamali hasa kuhusiana na umuhimu wa kupata alama ya ubora.

Alisema kwa wajasiriamali gharama za kupata alama za ubora ni bure, kwani tayari zinalipwa na Serikali.

Alifafanua kwamba kinachotakiwa ni wajasiriamali kupata barua ya utambulisho kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na kuipeleka TBS, ambapo mchakato wa kuwapatia alama ya ubora unaanza mara moja.
 
Mtemvu, alisema shirika hilo inatambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi  wengi, ndiyo maana kuna mchakato endelevu wa kutoa elimu kwa wajasiriamali kwa kuwa na hilo ni sehemu ya majukumu ya shirika ili waweze kupata alama ya ubora.

Alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima kuzingatia viwango, ndiyo maana wamekuwa wakishiriki maonesho mbalimbali ikiwemo wiki ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara mkoani Pwani
kwa ajili ya kutoa elimu.

Mtemvu alitoa wito kwa wajasiriamali akisema suala la wao kukidhi matakwa ya viwango vya kitaifa kwa bidhaa wanazozalisha na zinazosindikwa ni la msingi kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

"Kwa hiyo uwepo wetu hapa ni fursa muhimu ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji aweza kushindana na kuuza bidhaa zake bila woga," alisema Mtemvu.

Alitoa mwito kwa wananchi wa Pwani na nchini kote kwa ujumla kuhakikisha wanatumia bidhaa zenye ubora.

Wakati huo huo, Mtemvu alisema wiki hiyo ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara wameitumia kama fursa kuwapa taarifa washiriki kuwa baadhi ya majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ya chakula na vipodozi sasa hivi yamehamia TBS.

"Serikali ya Awamu ya Tano imeliona hilo na kwa hatua hiyo sasa inakuwa ni rahisi mno kupata alama ya ubora, kwani ukishapata alama ya ubora utaweza kufanya biashara na vile vile ule mzunguko uliokuwepo awali wa kuzunguka wa kwenda TFDA halafu urudi TBS utakuwa umepungua," alisema Mtemvu

KORTI YAELEZWA MBUNGE WA KIGOMA MJINI ZITTO KABWE ALIKATAA KUANDIKA MAELEZO POLISI

$
0
0
Na Karama Kenyunko. Globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alikataa kuandika maelezo polisi kuhusu watu anaodai waliuliwa na Jeshi la Polisi huko kwenye operesheni mkoani Kigoma.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, SP Albert Kitundu (49) ameeleza hayo leo Oktoba 22, mwaka huu, alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas simba.

Amedai katika upelelezi uliofanywa wakati huo yeye akiwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Kinondoni, alibaini kuwa kilichosemwa na Zitto hakikuwa na ukweli kwani watu waliofariki si 100 kama ilivyodaiwa bali ni wanne ikiwemo askari polisi wawili.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, shahidi huyo amedai Zitto alikamatwa na maofisa wa jeshi hilo baada ya kutoa maneno ya uchochezi na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay na  kumuhoji kawaida ambapo alipoulizwa nafasi yake katika chama cha ACT Wazalendo, historia ya maisha yake na elimu aliyaeleza kwa kirefu.

Aliendelea kudai kuwa, alipomuuliza kuhusu tuhuma alizozitoa kwa jeshi hilo, alikiri kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu watu 100 aliodai wameuliwa.

"Baada ya kueleza hayo nilimwambia Zitto nataka kumuhoji kama mtuhumiwa ili maelezo yake yaweze kutumika kama kielelezo mahakamani. Nilimpa haki zake lakini alisema hayuko tayari kutoa maelezo yake polisi na kudai atayatoa mahakamani," alidai SP Kitundu.

Hats hivyo shahidi Katundu alidai uwa walimuomba taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwapatia.

Shahidi huyo alidai aliongoza upelelezi wa tukio hilo kwa kupitia hotuba ya Zitto ambayo mmoja wa maofisa wa polisi aliichukua kwenye mkutano wake ambayo walikuta maneno ya kichochezi yaliyokuwa yanatakiwa kutolewa ufafanuzi na mshitakiwa huyo.

Amedai maneno yaliyotakiwa kutolewa ufafanuzi ni kwamba "jeshi la polisi limeuwa wananchi wapatao 100 na waliokwenda kutibiwa katika Zahanati ya Nguruka, polisi walichukua majeruhi na kuwaua."

Pia alidai aliwasiliana na RCO wa Kigoma na kutaka awapatie taarifa kuhusu tuhuma zilizotolewa na Zitto ambaye aliwapa maelezo ya watu mbalimbali aliowahoji ndipo akagundua kilichosemwa hakikuwa na ukweli kwani watu wanne ndio waliopoteza maisha kati yao wawili ni askari polisi na wawili ni wananchi. 

Ameendele kudai kuwa, hakuna majeruhi aliyechukuliwa na polisi na kuuawa isipokuwa waliwachukua ili kuwahoji kuhusu operesheni iliyotokea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.

Katika kesi hiyo, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 Zitto akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Inadaiwa alisema " Watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua".

CRDB yatumia AALCO kujitangaza

$
0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano huo Benki ya CRDB.

Na Suleiman Msuya

BENKI ya CRDB ambayo ni mdhamini wa Mkutano Mkuu wa 58 wa mwaka wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria ya nchi za Afrika na Asia (AALCO) imesema itautumia mkutano huo kujitanga na kutanua soko la biashara.

Hayo yamesemwa na Meneja Mwandamizi Idara ya Serikali za Mitaa CRDB, Suzan Shuma, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo unafanyika.

Shuma alisema benki hiyo inatembea na kauli mbiu yao ya ulipo tupo hivyo inaamini ushiriki wake katika mkutano huo wataweza kujitangaza kwa nchi shiriki.

Alisema kwa sasa CRDB inapatikana Tanzania na nchini Burundi hivyo ni wazi kuwa siku chache zijazo wataweza kufikia nchi nyingine.

“Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo ambapo inashiriki miradi mingi ya Serikali hivyo kupitia mkutano huu wa AALCO tunatarajia kujitangaza zaidi kibiashara,” alisema.

Shuma alisema katika mkutano huo wa AALCO benki hiyo itakuwa inatoa huduma ya kutoa na kubadilisha fedha na kutoa kadi.

Alisema mikakati ya benki hiyo ni kuendelea kuwa kinara wa kutoa huduma za kibenki nchini na nje ya nchi.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome alisema CCDB ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

Alisema Serikali inaipongeza benki hiyo kujitokeza kudhamini mkutano huo na kwamba haijakosea kufanya hivyo kwa kuwa mkutano huo ni fursa ya kujitangaza kimataifa.

Mkutano wa AALCO unashirikisha nchi 49 za Bara la Asia na Afrika ambapo viongozi katika Sekta ya Sheria hukutana na kujadiliana namna ya kutatua changamoto za kisheria na haki za kibinadamu kwenye nchi wanachama.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akifungua rasmi Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) uliofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.
Washiriki wa mkutano.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo. 
Washiriki.
Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa pili kulia) akifuatilia mkutano huo pamoja na wafanyakazi wenzake.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akizungumza katika mkutano huo.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya CRDB.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB, Suzan Shuma.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa, Suzan Shuma, akizungumza na waandishi wa habari.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images