Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

TANESCO YAKUSANYA BILIONI 46 KWA WIKI

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini. Kikao hicho kilifanyika jijini Tanga.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo (wa pili kushoto) na watendaji mbalimbali kutoka TANESCO wakiimba wimbo wa ‘solidarity’ kabla ya kikao cha wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wafanyakazi hao.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kikao chake na wafanyakazi wa TANESCO wa Kanda ya kaskazini.

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wafanyakazi hao.
…………………


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa sasa linakusanya shilingi bilioni 46 kwa wiki hali inayofanya Shirika hilo kuendelea kujitegemea baada ya kuacha kupokea ruzuku kutoka serikalini ili kujiendesha.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani tarehe 18 Oktoba, 2019 wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa TANESCO wa Kanda ya kaskazini kilichofanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo na viongozi kutoka TANESCO Makao Makuu.

” Niwapongeze TANESCO kwa kuendelea kujiendesha kwani hampokei tena ruzuku kutoka Serikalini na sasa mnakusanya shilingi Bilioni 46 kwa wiki tofauti na miaka miaka miwili iliyopita mlipokuwa mkikusanya bilioni Sita hadi Tisa kwa wiki, mnao uwezo, endeleeni.”alisema Dkt Kalemani

Kuhusu mkakati wa kuongeza mapato ya Shirika alisema kuwa, kunzia mwaka huu wa fedha, Kila Ofisi ya Mkoa ya TANESCO itapewa malengo ya makusanyo na atakayefikia malengo hayo atapewa motisha, ila atakayeshindwa atachukuliwa hatua.

Kuhusu ongezeko la wateja waliounganishwa na umeme, Dkt Kalemani ameliagiza Shirika hilo kufanya kazi kama makampuni ya simu kwa kufuata wateja kule waliko ili idadi ya wateja hao iongezeke na hivyo mapato ya Shirika kuongezeka.

Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani alisema kuwa, kuanzia sasa miradi yote ya TANESCO inayotekelezwa kwa fedha za ndani itasimamiwa na wataalam wa ndani ya nchi ukiwemo mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (MW 2115).

” Niwapongeze TANESCO kwa kusimamia mradi huu mkubwa wa Julius Nyerere, zamani tulikuwa tukisimamiwa lakini sasa tunawasimamia wakandarasi na hii inaokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika kutafuta wasimamizi wa miradi kutoka nje ya nchi kuja kusimamia miradi yetu.” alisema Waziri wa Nishati

Kuhusu suala la umeme vijijini, Dkt. Kalemani alisema kuwa bei ya umeme vijijini ni shilingi 27,000 bila kujali umbali aliopo mteja hivyo kila mtumishi ahakikishe hilo linatekelezeka.

Aidha, aliagiza wataalam wa TANESCO kuacha mara moja lugha lugha ya “hakuna vifaa” ambayo mara kadhaa imekuwa ikitumika wakati wateja wanapotaka kuunganishiwa umeme na kueleza kuwa vifaa vya umeme kama vile nguzo, mita, transfoma na nyaya vinazalishwa ndani ya nchi na kupatikana kwa urahisi hivyo lugha za visingizio zisiwepo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Raphael Nombo alizungumza na wafanyakazi hao kuhusu masuala ya muundo wa TANESCO, mikataba ya wafanyakazi na suala la mishahara.

TANESCO, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa minne ambayo ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.


WAZIRI MWAKYEMBE AIPONGEZA TAIFA STARS

TAKUKURU YAKAMATA MAPAPA 99 WA AMCOS WANAODAIWA KUDHULUMU WAKULIMA LINDI, NI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI ALOTOA OKTOBA15,2019

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi blog
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema inawashikilia viongozi 99 wa vyama 10 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) pamoja na kurejesha milioni 255,598,194.00 ikiwa ni utekelezaji wa agizo walilopewa na Rais Dkt. John Pombe Joseph alilolitoa akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa Mjini, mkoani Lindi.
Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi Rais Dkt Magufuli aliiagiza TAKUKURU pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Ushiriki, Hussein Bashe, kuhakikisha kuwa Vyama 10 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vinavyodaiwa na Wakulima vinawalipa wakulima husika kabla ya msimu wa Korosho kuanza, vinginevyo wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari leo Oktoba 19, 2019, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema ofisi yake imeshatekeleza agizo hilo la Rais kwa kuwakamata Viongozi 99 wa Vyama 31 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vilivyowadhulumu Wakulima wa Ufuta kiasi cha Sh. 1,236,364,075.00.
Amesema  kiwango hicho cha fedha wanachodaiwa kukidhulumu viongozi hao ni takribani mara tatu (3) ya kiwango kilichobainika awali ambapo baada ya Viongozi hao kuhojiwa wamekubali kulipa deni lote wanalodaiwa kabla ya kuisha kwa Mwaka 2019.
 Brigedia Mbungo amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na halitokoma mpaka wahakikishe wakulima wote wamelipwa stahili zao kwa mujibu wa Sheria na kwamba fedha zote zilizorejeshwa kiasi cha Sh. 255,598,194.00 zimeshaanza kugawiwa kwa walengwa ambao ni wakulima wa Ufuta kupitia kwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza chini ya Usimamizi na uangalizi wa TAKUKURU.
Pia amesema katika zoezi la kurejesha fedha za wakulima, Takukuru imekuwa ikitambua mali za watuhumiwa, kuzipiga picha na kuzikamata mali za viongozi hao wa AMCOS ambazo zimekuwa zikidaiwa kama dhamana ya madeni wanayodaiwa kwa wakati kama walivyoahidi ili kuziuza endapo watashindwa kutimiza ahadi zao.
“Ili kuwathibitishia kuwa TAKUKURU haina utani katika zoezi hili tunaendelea na zoezi la kutambua, kuzipiga picha na kukamata mali za viongozi wa AMCOS zinazodaiwa kama dhamana ya madeni wanayodaiwa, na endapo viongozi hao watashindwa kukamilisha malipo ya madeni wanayodaiwa kwa wakati kama walivyoahidi kwa maandishi wao wenyewe kwa hiari yao basi mali husika zitataifishwa kwa mujibu wa Sheria ili wakulima wa Ufuta wapewe fedha zao.
Aidha Brigedia Mbogo amewataka Viongozi wote wa Vyama vya Ushirika nchini vinavyodaiwa na Wakulima viwalipe wakulima wao haraka iwezekanavyo kabla TAKUKURU haijawafikia na kwamba katika zoezi hilo hakuna chama cha ushirika kinachodaiwa ambacho kitabaki salama.
Amesema zoezi la ufuaitliaji wa malipo ya Wakulima kwa Vyama vya Ushirika ni endelevu na pindi litakapokamilika Takukuru itatoa taarifa kamili.

Amewataka wananchi wenye ushahidi wa dhuluma iliyofanywa kwa wakulima wa ufuta ama kwa yeye mwenyewe kudhulumiwa au kuhujumiwa kwa namna yoyote ile katika biashara ya Ufuta, wafike katika ofisi za TAKUKURU zinazopatika katika Mikoa na Wilaya zote nchi nzima.

BENKI YA CRDB YADHAMINI MAONYESHO YA UTALII YA SITE JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati akiwasilisha mada katika warsha iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Benki ya CRDB ambao ni miongozi mwa wadhamini wa maonesho hayo, imeelezea fursa mbalimbali inazozitowa kwa wateja wakena namna inavyoweza kubadilisha sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akifafanua jambo katika warsha iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu akielezea jambo juu ya mikopo ya magari ya Utalii kwa baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Automechs Limited ( HAL), Satbir Hanspaul ambaye pia ni mbia wa Benki ya CRDB anayetengeneza na kuuza magari maalumu ya Utalii nchini, akifafanua jambo juu ya namna magari hayo yanavyoweza kuwa katika warsha hiyo, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani city, jijini Dar es salaam, katika maonyesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2019 yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

MBUNGE AYSHAROSE MATTEMBE AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA SHELUI SINGIDA

$
0
0
 Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Shelui Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe akizungumza na wazazi katika mahafali hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika shule hiyo mkoani Singida.
 Mbunge Mattembe akisalimiana na mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Elly Nguma. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Shelui Kinota Hamisi, Afisa Elimu Kata,  Swetu Makula na Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo, Jenipher Miano.
 Bweni la wanafunzi wa kike ambalo ujenzi wake ukiendelea.
 Mhe. Mattembe akizungumza na viongozi wa kata hiyo wakati akikagua ujenzi wa bweni la wasichana wa shule hiyo ambalo serikali ilitoa sh. milioni 75.
 Mattembe akizungumza na viongozi wa kata hiyo wakati akikagua ujenzi wa bwalo la shule hiyo ambapo serikali ilitoa sh.milioni 100.
 Mhe.Mattembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo mbele ya bwalo hilo.
 Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo. 
Mhe.Mattembe akiwasalimia kwa kuwapungia mikono wahitimu  katika mahafali hayo. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Kasimu Maksudi akizungumza katika mahafali hayo.
 Mkuu wa shule hiyo,  Elly Nguma akizungumza.
 Afisa Mtendaji wa Kata Shelui, Geofrey Tungu akizungumza.
 Diwani wa Kata ya Shelui,  Kinota Hamisi, akizungumza.
Vijana wa Skauti wa Shule hiyo  wakiingia katika viwanja vya mahafali kwa ukakamavu.
 Vijana wa Skauti wa Shule hiyo wakionesha sarakasi.
 Skauti wakionesha umahiri wa kuvunja tofari juu ya tumbo kwa kutumia nyundo.
 Wahitimu wakiimba wimbo maalumu.
 Mhe.Mattembe akiserebuka na wanamuziki wa kizazi kipya wa shule hiyo.
 Wahitimu hao wakiigiza kuimba na kucheza muziki wa wazee wa zamani.
 Keki maalumu ya mahafali hayo.
 Mhe.Mattembe akikata keki hiyo.
 Wananchi wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wananchi wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mhe.Mattembe akilishwa keki hiyo.
 Mahafali yakiendelea. 
 Taswira ya uwanja wa mahafali hayo. 
 Mhe.Mattembe akimkabidhi cheti cha Taaluma mhitimu, Hassan Juma.
 Mhe.Mattembe akikabidhi jezi na mpira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
 Hapa Mattembe akikabidhi taulo kwa ajili ya watoto wa kike wa shule hiyo.
 Mhitimu Agnes Daudi akionesha kipaji cha kuimba.
 Wazazi wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa mchango wa ujenzi wa bwalo la shule hiyo baada ya kuhamasishwa na Mbunge Mattembe.
 Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Viongozi na wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Viti Maakumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kujitokeza kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo badala ya kuiachia serikali pekee.

Mattembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Shelui alitoa ombi hilo wakati akihutubia kwenye mahafali hayo.

"Serikali ina majukumu mengi katika nchi nawaombeni wazazi na walezi jengeni tabia ya kuchangia miradi ya maendeleo ili kuisaidia serikali" alisema Mattembe.

Mattembe alisema katika shule hiyo kuna miradi ya ujenzi wa bwalo na bweni la wanafunzi wa kike ukiendelea lakini umekuwa ukisuasua baada ya fedha zilizotolewa na serikali kumalizika hivyo aliwaomba wazazi hao kuchangia ujenzi huo ili kuwapunguzia adha watoto wao ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutawaongezea ufaulu wanafunzi wa shule hiyo kwa vile watapata muda wa kutosha wa kujisomea.

Mattembe aliwataka wazazi hao kuwa na muda wa kuzungumza na watoto wao mambo mbalimbali ya kuwajenga katika misingi mizuri ya maisha badala ya kuwaacha wakiharibikiwa kwa 
kujiingiza katika vitendo viovu.

 Katika hatua nyingine Mattembe aliwaomba wazazi hao kuviendeleza vipaji walivyo navyo watoto wao vya kuimba, kuigiza na michezo mbalimbali na kueleza kuwa vinawajenga na  kuacha kufikiria mambo yasiofaa.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Kasimu Maksudi aliwaeleza wahitimu hao kujiandaa kwa mtihani wao wa mwisho na kuwa kuhitimu kwa kidato cha nne ndio mwanzo wa kuendelea na  masomo mengine ya kidato cha tano na sita hadi elimu ya juu hivyo wasibweteke kwa kuridhika na elimu hiyo.

Kabla ya kuhutubia katika mahafali hayo Mattembe alikagua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana ambao serikali ilitoa sh. 75 milioni na sh. 100 milioni kwa ajili ya bwalo.

LITTLE TREASURES YAFANYA MAOMBI NA SHEREHE KUFURAHIA KWA MATOKEO MAZURI DARASA LA SABA 2019

$
0
0
Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imefanya sherehe ya kujipongeza na maombi ya shukrani kwa kupata matokeo mazuri katika mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2019 wakiongoza na kauli mbiu 'Tanzania Four, Shinyanga One'.

Shule ya Little Treasures imeshika nafasi ya nne katika orodha ya shule 10 bora kitaifa huku mwanafunzi Daniel Ngassa kutoka shule hiyo akishika nafasi ya saba kwenye orodha ya watahiniwa bora kitaifa na wanafunzi wengine wawili ambao ni Suzane Assenga na Scolastica Shelembi wakiingia kwenye orodha ya watahiniwa bora 10 kitaifa upande wa wasichana.

Sherehe ya Pongezi na Maombi kwa shule hiyo imefanyika leo Jumamosi Oktoba 19,2019 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi,viongozi wa dini madhehebu mbalimbali,wageni waalikwa,wazazi na walezi,walimu na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019.
Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Little Treasures Lucy Dominic amesema shule hiyo imeshika nafasi ya nne kitaifa,ya kwanza katika wilaya ya Shinyanga na ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga hivyo lengo la sherehe na maombi hayo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda na kuiinua shule hiyo. 

"Tuko hapa kwa lengo kuu la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kuiinua shule yetu. Tunaamini kuwa ni Mungu pekee anaye tuwezesha, Ni nafasi pia kuendelea kuomba neema zake azidi kutubariki zaidi na zaidi kwani Sisi kama wanadamu tunajua tulikotoka na tulipo lakini hatujui tunakokwenda na ndiyo maana tunamtanguliza mbele azidi kuwa nuru yetu",alisema Dominic.

"Tumekutana hapa ikiwa ni mwendelezo wa furaha isiyo kifani kwetu wanafamilia ya Little Treasures. Kumshukuru Mungu na kusherehekea mafanikio makubwa tuliyoyapata katika matokeo ya mtihani wa tiafa wa darasa la saba mwaka 2019",aliongeza. 

Kwa upande wake,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 na kuahidi kutoa zawadi kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani.

"Little Treasures mmefanya maajabu,tunawapongeza sana,mmeutangaza mkoa wetu,mmeuingiza mkoa wetu katika shule 10 bora kitaifa",alisema Kahundi.

"Nazipongeza Shule zetu tatu binafsi ambazo ni Little Treasures,Kwema Modern na Rocken Hill kwa kweli zimetangaza mkoa wetu kwa matokeo mazuri kitaifa.Lakini nizipongeze shule za serikali za mkoa wa Shinyanga ambazo zimefanya vizuri kwenye matokeo haya nazo ni Kinaga iliyopo Kahama,Ilobi iliyopo Kishapu na Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga",alisema Kahundi.

Alisema mbali na mkoa wa Shinyanga kushuka kutoka nafasi ya 15 mwaka 2018 hadi 17 mwaka huu akitaja sababu kuu kuwa ni wanafunzi kuacha shule ' Drop outs',shule za serikali zimeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures  Lucy Dominic akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Sehemu ya wanafunzi 91 waliomaliza darasa la saba katika shule hiyo na wote wamepata daraja A katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 na kuifanya shule hiyo kung'aa ngazi ya taifa,wilaya na mkoa wa Shinyanga.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akicheza na wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2019 na kufaulu katika shule ya msingi Little Treasures leo. Jumla ya wanafunzi 91 wamemaliza darasa la saba katika shule hiyo na wote wamepata daraja A katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 na kuifanya shule hiyo kung'aa ngazi ya taifa,wilaya na mkoa wa Shinyanga.
Sehemu ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika  sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akimuonesha mwanafunzi aliyeshika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019,Daniel Ngassa kutoka shule ya Little Treasures iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Wanafunzi wa kike waliosimama pia wamekuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019.Kushoto ni Suzane Assenga na Scolastica Shelembi (kulia).
Meza kuu wakifuatilia matukio yanayoendelea.
Wazazi wa Daniel Ngassa wakimpongeza kijana wao kwa kushika nafasi ya saba kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019.
Nabii Janeth Aminiel Kimo wa Kanisa la Uwezo wa Bwana Mwanza akiwaombea wanafunzi waliomaliza darasa la saba 2019 katika shule ya msingi Little Treasures na kufaulu vizuri katika mtihani.
Maombi yakiendelea kumshukuru Mungu kutokana na matokeo mazuri iliyopata shule ya msingi Little Treasures katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019.
Askofu Raphael Machimu kutoka kanisa la EAGT Shinyanga akiendesha maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Maombi yakiendelea kumshukuru Mungu kutokana na matokeo mazuri iliyopata shule ya msingi Little Treasures katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019.
Padre Tupendane Philemon wa Kanisa Katoliki la Mt. Yosefu Mipa (Jimbo Katoliki la Shinyanga) akiwaombea wahitimu wa shule ya msingi Little Treasures na shule hiyo kwa ujumla.
Maalim/Ustadhi Ashiraf Majaliwa akitoa salamu za Mufti wa Tanzania na Sheikh wa mkoa wa Shinyanga na kuomba dua kwa ajili ya shule ya Little Treasures.

MC Mama Sabuni akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu (kushoto).
Wagini waalikwa wakiwa eneo la tukio.
Watahiniwa bora kitaifa matokeo ya mtihani darasa la saba 2019 kutoka shule ya Msingi Little Treasures (Daniel Ngassa katikati aliyeshika nafasi ya saba kitaifa) na  Wanafunzi wa kike ambao ni miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba 2019 Suzane Assenga (kulia) na Scolastica Shelembi (kushoto) wakikata keki.
wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wahitimu darasa la saba 2019 shule ya Little Treasures wakicheza wimbo wa Yope wa Diamond na Innoss'B
Wahitimu darasa la saba 2019 shule ya Little Treasures wakicheza wimbo wa Yope wa Diamond na Innoss'B
Mwalimu Mkuu shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza wakati wa sherehe na maombi kwa shule ya Little Treasures
Walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakitoa burudani ya wimbo.
Meneja wa Shule ya msingi Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga akizungumza wakati wa sherehe ya pongezi na maombi ya shukrani kwa shule ya Msingi Little Treasures kushika nafasi ya nne kitaifa,nafasi ya kwanza wilaya ya Shinyanga na ya kwanza mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya kidato cha saba mwaka 2019. 
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akikabidhi keki maalumu kwa wahitimu wa darasa la saba mwaka 2019
Zoezi la kukabidhi keki likiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

HALMASHAURI ZATAKIWA KULINDA MAENEO YA HIFADHI YALIYOIDHINISHWA VIJIJI YASIVAMIWE

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua Mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Chato mkoa wa Kagera wakati akikagua miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Chato Charles Kabeho na kulia kwa Naibu Waziri ni Mhandisi wa ujenzi wa Mradi huo Renatus Mhada.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoa wa Kagera Charles Kabeho akielekea kukagua Mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Chato mkoa wa Kagera wakati akikagua miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Watumishi wa sekta ya ardhi wa halmashauri za Wilaya na Mji za mkoa wa Geita jana wakati wa ziara yake ya kuangalia utendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita.
……………………..

Na Munir Shemweta, WANMM GEITA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinalinda maeneo yote ya hifadhi yaliyoidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuwa vijiji ili yasiendelee kuvamiwa.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya siku moja kutembelea mkoa huo kuangalia utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na kufuatia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Machi 2019.

Alisema, ni jukumu la halmashauri za wilaya wakati zikisubiri kuletewa tarifa rasmi ya maeneo yaliyoidhinishwa kuwa vijiji na mengine yaliyobadilishiwa matumizi kuyalinda maeneo hayo yasivamiwe tena ili taarifa itakapokwenda katika halmashauri husika kuhusiana na maeneo pasiwepo uvamizi mwingine zaidi ya ule wa awali kabla ya kutembelewa na timu ya Mawaziri nane.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, halmashauri ambazo maeneo yake ya hifadhi yalivamiwa na vijiji vyake kuidhinishwa zitapelekewa taarifa sambamba na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali vijiji vilivyidhinishwa.

‘’Mna jukumu kulinda maeneo hayo yasivamiwe tena kwa sababu kamati ya mawaziri wanne walipita kwenye baadhi ya maeneo na yaliainishwa na kinachotakiwa kwenu ni kuhakikisha hakuna uvamizi unaoendelea katika hifadhi ’’ alisema Dkta Mabula.

Alisema, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ishamaliza kupanga maeneo ya vijiji yaliyoidhishwa mkoa kwa mkoa na kinachofanyika sasa ni kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili wananchi waweze kuishi kwa amani katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika wakati wa kikao hicho na watendaji wa sekta ya ardhi alisema wizara yake katika kukabiliana na upungufu wa watumishi wa sekta hiyo imejipanga kuhakikisha inawagawa watumishi wa sekta ya ardhi waliopo katika halmashauri kulingana na idadi iliyopo sasa.

Mwanyika alisema Wizara ya Ardhi ina mahitaji ya watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri zote wapatao 2900 ambapo kwa sasa kuna jumla ya watumishi 1500 hivyo kufanya kuwepo pungufu ya watumishi 1400. Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi alisema, kinachofanyika sasa sasa kwa Wizara yake ni kutambua watumishi waliopo na baadaye kuwatawanya katika mgawanyo mzuri.

Naye Kamishna Msaidzi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alisema halmashauri ambazo hazina wataalamu wa kutosha zinazoazima kutika mikoa iliyo jirani na halmashauri hizo wataalamu wake wa sekta ya ardhi wanatakiwa kufanya kwa weledi na si vinginevyo ili kazi ya sekta hiyo iweze kwenda vizuri.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) uliopo wilayani Chato mkoani Kagera.

Akiwa katika ukaguzi wa mradi huo unaogharimu Bilioni 1.2 na kusimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt Mabula alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha linakamilisha ujenzi wa mradi huo katika muda uliopangwa kwa kuwa shirika hilo sasa limeamiwa na serikali kwa kupatiwa miradi mbalimbali nchini.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUJITANGAZA

$
0
0
Muonekano wa daraja la zamani la Ruaha Mkuu linalounganisha wilaya za Kilosa na Kilombero ambalo ujenzi wake unaendelea.
Muonekano wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi M/s Reynolds Construction Company mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa (katikati) akikagua ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi M/s Reynolds Construction Company mkoani Morogoro (wapili kushoto), ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Japhet Masele.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akiteta jambo na Mhandisi Mshauri wa M/s Nicholas O’ Dwyer and Co. Ltd anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 na daraja la Ruaha Mkuu linalounganisha wilaya za Kilosa na Kilombero.
Muonekano wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 eneo la Mang’ula inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Morogoro.

……………………

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa ameutaka Wakala wa huduma za Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuongeza kasi katika mkakati wake wa kuanzisha karakana katika ngazi za wilaya ili kuwezesha taasisi nyingi za umma na watu binafsi kupata huduma hizo kwa urahisi.

Akizungumza mara baada ya kukagua karakana mpya na ya kisasa katika wilaya ya Kilombero mjini Ifakara Naibu Waziri Kwandikwa amesema huduma hiyo itawapunguzia adha wananchi wa maeneo ya Mlimba, Ulanga, Malinyi na Ifakara kutembea umbali mrefu kufuata huduma za TEMESA mjini Morogoro.

“Ongezeni wigo wa huduma zenu za ufundi wa magari, mitambo na umeme, hakikisheni zinatolewa kwa wakati, ubora na unafuu ili mjiimarishe kimapato na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi zaidi”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

Amewataka TEMESA kununua vipuri kwa bei ya jumla ili kuwawezesha kutoza bei nafuu katika huduma zao na hivyo kuwavutia wadau wengi.

Naibu Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa TEMESA kusimamia uwekaji wa mifumo ya umeme katika miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Serikali ili kuifanya iwe imara na kuepusha majanga ya moto yanayoweza kusababishwa na uunganishaji holela wa umeme katika majengo ya Serikali. 

Naye Mtendaji mkuu wa TEMESA Eng. Japhet Masele amesema Wakala huo umejipanga kujenga karakana nne za kisasa katika wilaya za Same, Kahama, Simanjiro na Chato ili kuwapunguzia wananchi na taasisi za umma kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 kwa kiwango cha lami na daraja la Ruaha Mkuu na kumtaka mkandarasi M/s Reynolds Construction Company kutoka Nigeria anayejenga barabara hiyo kujipanga upya ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Amesema kasi ya sasa hairidhishi na hivyo itachukua muda mrefu hivyo kumtaka mkandarasi huyo kujipanga upya na kuongeza nguvu kazi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

Kukamilika kwa wakati kwa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 68.9 inayopita katika eneo lenye uzalishaji mkubwa wa miwa na mpunga licha ya kurahisisha huduma za uchukuzi, kilimo na biashara pia kutakuza uchumi wa wananchi wa mkoa wa Morogoro.

VODACOM YAZINDUA HUDUMA YA LIPA KWA SIMU JIJINI DODOMA

$
0
0


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mhudumu wa Vodacom katika kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mhudumu wa Vodacom katika kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni ni Meneja wa LIpa, Luis Maro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kushoto), akionyeshwa namna meseji ya “Lipa kwa simu yako” inayoingia kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) baada ya mteja kulipa kupitia huduma hiyo wakati wa uzinduzi katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo.
Ofisa Masoko wa Vodacom, Robert Massinda, akimuelekeza mteja wa Vodacom, Fatma Haji wakati akilipia tiketi yake kwa “Lipa Kwa Simu Yako” kwenye kampuni ya mabasi ya Shabiby wakati wa uzinduzi wa huduma wa huduma hiyo Dodoma leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mfanyakazi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (katikati), akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (katikati), akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.
 

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI WANAWAKE ZANZIBAR

$
0
0
 MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Viongozi wa UWT alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Warsha ya Wajasiriamali Wanawake kushoto Mamaku Mwenyekiti wa UWT Taifa.Bi. Thuwaiba Editon Kisasi .(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika ukumbi wa mkutano wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu (SUZA) kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali Wanawake kushoto Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.Bi. Thuwaiba Editon Kisasi na Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.Bi.Hamida Mussa Khamis, wakielekea katika maonesho ya Bidhaa za Wajasiriamali Wanawake
 MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein, kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Suleiman Iddi na kushoto Makamu Mwenyekiti wa UWT.Bi. Thuwaiba Editon Kisasi, wakitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake, wakimsikiliza Kiongozi wa Kikundi cha Furaha cha Donge Mkoa wa Kuskazini Unguja.Bi. Madina Khamis Makame.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, wakitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu (SUZA)
 /MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.Bi.Thuwaiba Editon Kisasi wakitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa hafla ya Kongamano la Wajasiriamali Wanawake,lililofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia moja ya bidhaa za Wajasiriamali Wanawake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali Wanawake lililofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama.Asha Suleiman Iddi na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico na kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.Bi. Thuwaiba Edditon Kisasi 
 MKE wa Rais wa Zanzibar. Mama Mwanamwema Shein,(katikati) akimsikiliza Mfanyakazi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar.(ZSTC) Farida Othman. Akitowa maelezo za bidhaa zinazozaliwa na Shirika hilo wakati wa maonesho ya Wajasiriamali Wanawake, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Sulein Iddi na kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.Bi.Thuwaiba Editon Kisasi.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico na kushoto Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.Bi. Thuwaiba Editon Kisasi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA GUGU KAROTI NA VISUMBUFU VINGINE VYA MAZAO YAFANYIKA MKOANI ARUSHA

$
0
0

Zoezi la kung'oa gugu karoti likiendelea kama inavyoonekana katika picha,ambapo gugu hilo linakuwa kwa kasi katika mikoa mitano hapa nchini ikiwemo Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Kagera na Geita. 

Bwanashamba kutoka Taasisi ya ECHO Charles Bonaventure akiwa ameshikilia  mmea wa gugu karoti mara baada ya kuung'oa ,Kulia kwake ni Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega  akifuatiwa na Ndugu Remigius Mchunguzi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viwatilifu kwa ukanda wa Kitropiki (TPRI)

Washiriki wa siku ya gugu karoti pamoja na baadhi ya wanakamati wa uhanasishaji wakiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega wakishirikiana katika kuling'oa gugu hilo kama wanavyoonekana wakuwa wamevaa vifaa vya kujikinga na madhara yatokanayo na gugu hilo.

Mmea vamizi wa gugu karoti ukiwa tayari umeshang'olewa,ambapo baada ya kunyauka utateketezwa kwa moto ikiwa ni njia moja wapo ya kuliangamiza gugu hilo.

Ramadhani Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka TPRI, akitoa ufafanuzi wa jambo kwa mgeni rasmi mara baada ya kutembelea maonyesho ya bidhaa katika siku ya gugu karoti mkoani Arusha.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki siku ya Gugu Karoti Mkoani Arusha ambapo mkutano huo uiifanyika katika Ukumbi wa TPRI mkoani humo.

Dkt.Ester Kimaro akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na zile za binafsi katika ukumbi wa TPRI mkoani Arusha.

Ramadhani Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka TPRI, amesema kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika mikoa yote nchini Tanzania

Erwin Kinsey Mkurugenzi wa ECHO Afrika ya Mashariki akizungumza katika siku ya Gugu Karoti iliyofanyika Mkoani Arusha.

Wakwanza kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ,akifuatiwa na Dkt.Ester Kimario,aliyemuwakilisha mkurugenzi wa TPRI,wakifuatilia mijadala inayoendekea katika siku ya gugu karoti




Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizingumza na waandishi wa habari mara baada ya kuling'oa gugu hilo kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani Arusha

Ndelekwa Kaaya ni mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu karoti akiwa ameshikilia gugu hilo mara baada ya kuling'oa akiwa na vifaa vya kujikinga kama anavyoonekana katika picha.

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ,akifuatiwa na Dkt.Ester Kimario,aliyemuwakilisha mkurugenzi wa TPRI,wakishiriki katika zoezi la ung'oaji wa gugu karoti 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kamati inayoshughulikia kuhamasisha na kuondoa mimea vamizi mkoa wa Arusha.




Na.Veronica Ignatus,Arusha


Serikali mkoani Arusha imeitaka kamati inayoshughulikia kuhamasisha, na kuondoa mimea vamizi ,kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu kwa taasisi mbalimbali za serikali, ikiwemo mifugo,Kilimo,Mazingira na wizara ya Afya, mashuleni na maeneo mbalimbali ya jamii juu ya mimea vamizi wa gugu karoti.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani Arusha ,iliyofanyika wilayani Arumeru ,katika Taasisi ya Utafiti wa viwatilifu kwa ukanda wa kitropiki (TPRI)Mkoani hapa.


Kwitega amesema kuwa bila ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu, wadau wa maendeleo ,kazi hiyo haitakuwa na maana wala mafanikio ,hivyo kila mmoja analojukumu la kuhakikisha anafanyakazi kwa nafasi yake, ili elimu na uelewa iwafikie jamii kwa ujumla katika mapambano hayo.


Ametoa wito kwa Waandishi wa habari ambao ni wadau muhimu na jeshi la mianvuli, kutumia vyema kalamu zao kuhabarisha jamii juu ya gugu hilo vamizi ,kwa kutoa elimu kwa umma juu ya madhara na namana ya kuliangamiza gugu hilo.

Ndelekwa Kaaya ni mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu hilo, amesema kuwa  dhumuni la  siku hiyo ni  kuwahamasisha na kutoa Elimu ya uelewa kwa  wadau wa kilimo,mifugo,mazingira,afya ya binadamu,viongozi wa dini,viongozi wa kimila taasisi za Elimu ,makundi maalum watafiti ,wanasayansi ,wafanyabiashara viongozi wa siasa wafahamu kuhusu madhara na udhibiti wa Gugu karoti na visumbufu vamizi katika mkoa wa Arusha, na mikoa mingine ambapo kuna visumbufu vamizi.


Amesema katika siku hiyo mada mbalimbali zinazohusiana na ueneaji usambaaji na mbinu,njia za kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi zitatolewa na wataalam mbalimbali toka taasisi za serikali na sekta binafsi ili kujenga uelewa kwa jamii ya watanzania.


Amesema kuwa jitihada zilizofanywa na kamati katika harakati za kudhibiti gugu hilo ni pamoja na kushirikiana na taasisi binafsi ,zimeweza kufanya utambuzi wa visumbufu vamizi ,na kuainisha maeneo yalipovamia.


Ameinisha changamoto zinayoikabili kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, kwaajili ya kuwezesha uhamasishaji wa kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi, ikiwemo kuwafikia wadau wengi katika maeneo yaliyovamiwa mkoani Arusha .


Aidha ukosefu wa vifaa vitendea kazi ,vifaa kinga vinavyotakiwa kutumika katika zoezi la ung’oaji wa visumbufu vamizi haswa katika maeneo mbalimbali katika barabara za jiji la Arusha, ambapo ushirikiano mdogo kutoka kwa wadau wenyewe katika maeneo yaliyovamiwa na visumbufu vamizi likiwemo gugu karoti .


Ramadhani Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka (TPRI) amesema kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika mikoa yote nchini Tanzania,ambapo maeneo mengi yaliyovamiwa ni mashamba ya mazao ,malisho ya wanyama,Hifadhi za taifa ya Arusha ,Ziwa manyara , Serengeti na Ngorongoro,maeneo ya makazi ya watu ,maeneo ya kutunza na kusambaza nishati ya umeme ,mabwawa ya maji kwaajili ya matumizi ya binadamu na  wanyama. 

Kilewa ameyataja  madhara yatokanayo na gugu hilo kuwa ni pamoja na magonjwa ya aleji ya ngozi kwa binadamu na wanyama,kifua kinachobana (pumu)kwa binadamu,umasikini  katika ngazi ya familia, kata ,wilaya na mkoa.(pumu)kwa binadamu.


 Kiuchumi gugu hilo linasababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya chakula na biashara,Athari katika biashara ya utalii na wanyama kushindwa kupita kwenye baadhi ya mimea vamizi,maziwa ya wanayama wanaofugwa kuwa na uchungu kwasababu ya sumu iliyomo katika mimea vamizi,upungufu wa malishio ya wanyama pamoja madahara kwa afya ya udongo na uoto wa asili na uharibifu wa mazingira 

Aidha asili ya gugu hilo kwamba ni Amerika ya Kusini,A.kati na A.Kaskazini maeneo ya Mexico, hapa nchini Tanzania liliingia mwaka 2010  limetokea nchini Ethiopia,ambapo mmea mmoja huweza kutoa mbegu 15,000 ,25,000-100,000 na zinauwezo wa kuzaa kila baada ya  miezi 4,mmea mmoja unaweza kutoa miche kwa mara tatu,unauwezo wa kukaa ardhini kwa miaka kumi.


"Zinaene kwa njia ya upepo,utengenezaji wa barabara,upepo binadamu wenyewe,asaia ,Afrika,visiwa ,Austaralia Afrika ya kusini,nchi zote za afrika ya nmashariki kwa afrika zaidi ya 13,kwa Tanzania taarifa iliyopo ni mikoa mitano,inaathiri uoto wa asili,inazuia mbegu za mazao zisiote ,inasaidia uzaliaji wa wadudu,vimelea vya magonjwa kwenda kwenye mazao mengine,inzi weupe.Alisema Kilewa.


MWISHO
H

MAONESHO YA SITE YAZIDI KUTANUA WIGO WA BIDHAA ZA UTALII KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

WAFANYABIASHARA wadogo wa bidhaa za utalii wamefanikiwa kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa kwa kutumia mfumo wa Speed Networking .

Hayo yamefanyika kwenye maonesho ya Utalii yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Saalam.

Bodi ya Utalii Nchini (TTB) wameendelea kuandaa Maonesho ya Swahili International Tourism Expo (SiTE) 2019 kwa mara ya tano na jumla ya kampuni za waoneshaji 210 kutoka nchi 60, Jumla ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari takribani 333.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Mratibu wa Maonesho ya SiTE ambaye pia Meneja Huduma za Utalii Joseph Sendwa amesema onesho hili linawafaidisha mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.

Amesema, bodi ya utalii imekuwa inaenda sokoni kutaganza utalii na kuweza kuandaa maonesho ili kuwakutanisha wadau wa utalii kutoka pande zote duniani.

Pia, Sendwa amesema wafanyabishara wa utalii wameweza kuunganishwa na wadau wakubwa wa utalii na kufanya appointment moja kwa moja kwa kutumia  mfumo wa Speed Network ambao ni rahisi sana.

"Wafanyabiashara wa bidhaa za utalii wameweza kufanya mazungumzo na wadau wakubwa na kuweka makubaliano na hii imewasaidia kupata mazungumzo nao ya kibiashara na wanunuaji tofauti," amesema

Sendwa ametoa wito kaa watanzania hususani mawakala wa masuala ya utalii wakubwa na wadogo kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho ya SITE kujionea bidhaa mbalimbali.

Aidha, TTB imeandaa ziara kwa ajili ya mawakala wa utalii na waandishi wa habari wa kimataifa Oktoba 21, kwenda kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya asili ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Maeneo mengine ni Fukwe za Tanga na mapango ya Amboni, Misitu ya Magoroto, Mlima Kilimanjaro na miradi ya utalii wa utamaduni katika Mkoa wa Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Riaha na Mji wa Iringa. Pia Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa na Mikumi, Visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Pia, katika maonesho hayo kumekuwa na semina  zinazoendeshwa  na wataalamu waliobobea kwenye masuala ya utalii kukiwa na mada mbalimbali.
Mratibu wa Maonesho ya SiTE ambaye pia Meneja Huduma za Utalii Joseph Sendwa akizungumzia maonesho ya utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE) 2019 yanavyozidi kukua na kuvutia wadau wa utalii na fursa wanazozipata mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.
linawafaidisha mawakala wa utalii wa Tanzania kuweza kufikia masoko makubwa duniani bila kutumia gharama.

MWENYEKITI WA JUKWAA LA WANAWAKE AONGOZA WANANCHI KATIKA ZOEZI LA USAFI

$
0
0
  Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega  (wa pili kushoto) akiwa na   Mganga  Mkuu wa Wilaya Mkuranga,Dkt. Steven Mwandambo (wa kwanza kulia)wakishiriki kazi za usafi katika barabara  ya Kisiju leo  ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi. Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.

  Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega (wa kwanza kulia)akiwa na wananchi wa wilaya hiyo wakiendela na kazi ya usafi katika barabara  ya Kisiju  leo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega  akitoa maelekezo kwa wakazi wa wilaya hiyo waliojitokeza  kwa wingi kushiriki kazi za usafi katika barabara ya Kisiju  ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi.




Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akiwa na wananchi wa wilaya hiyo wakiendela na kazi ya usafi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI ... UTAWALA WA TFF YA SAFARI HII NI KIBOKO YA WOTE WA NYUMA

$
0
0

Na HAJI MANARA

Inawezekana utawala wao hauna mbwembwe kama za Haji Manara, na umekosa umaarufu kwa baadhi ya Mashabiki wa soka nchini, lakini nathubutu kuandika utawala huu wa sasa wa Shirikisho la Soka nchini TFF ndio utawala unaoonyesha mafanikio makubwa ya maendeleo ya uwanjani Kwenye mchezo huu kuliko utawala wowote huko nyuma.

Hebu tuanzie miaka ya sitini baada ya uhuru hadi sasa na tukiyatembelea maneno ya Chairman Mao ya "No research No  Data No right to Speak"

Nani anaweza kulinganisha mafanikio ya utawala huu wa sasa wa TFF na zilizopita?

Ngoja nikueleze machache kisha unijibu swali langu pendwa,
Kwa mara ya kwanza baada ya Uhuru,Tanzania imeandaa Mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF ( Afcon Under 17 ) Baada ya miaka thelathini na tisa Tanzania imeshiriki fainali za Mataifa ya Afrika,
Baada ya miaka kumi Tanzania inarejea tena Kwenye Mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ( CHAN).

Hapa sote tunajua yaani kufuzu kwetu kwa AFCON na CHAN ni ndani ya mwaka mmoja huu wa 2019,
haipo TFF yoyote huko nyuma na hata tukisema FAT iliyowahi kuiwezesha nchi hii kubwa kufuzu katika mwaka mmoja Mashindano hayo yote kwa wakati mmoja ( FACT ISIYOGUSIKA)

Kufuzu tena kwa timu Kwenye Afcon under 17
Kuchukua ubingwa wa CECAFA Kwa timu yetu ya under 20,
Kuchukua ubingwa kule Kampala
Timu yetu ya taifa ya vijana kushinda Cecafa kule Burundi,
Kushinda kikombe tena kwa timu ya vijana kule Botswana na Rwanda
Kushinda kwa timu za taifa za Wanawake kubwa na ile ya vijana Mashindano mbali mbali ya COSAFA na CECAFA kule Afrika kusini na Rwanda, lakini kuiwezesha Taifa Stars kwende Kwenye makundi ya kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2022 kule Qatar.

Niwaarifu hayo yote yamefanyika katika kipindi cha miaka miwili tu, tena mengi kati ya hayo ni mwaka huu wa 2019.

Sasa nani anaweza kunyoosha kidole juu akanitajia TFF au hata FAT ambayo ktk kipindi cha mwaka mmoja au miwili wamefanya haya?

Ndio maana nilimsafiria Chairman Mao ambapo mm nnaeandika makala hii ni muumini wa falsafa zake nilizozikalia darasani.

Haiyumkiniki kuupinga ukweli uliowazi na tutafanya dhambi kuu isiyohitaji usamehevu wowote ule.

Tanzania kwa miaka mingi tumekuwa Pombe ya ngomani, kila aliyepo anajichotea tu, al-muhimu uwe na chombo cha kunywa, iwe kikombe, glasi, kopo na hata kifuu, twende!!

Ila sasa heshma yetu inaanza kurejea taratibu na sasa tukiwa uwanjani, wenzetu Afrika wanasema Yes, nchi inacheza!!

Hapo sijaongelea mafanikio makubwa ya Simba msimu huu ya kuwa klabu ya kwanza tokea uhuru kufuzu kwa hatua ya Robo fainali kutoka ktk makundi ( Groups Stage) ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Nawezaje kuacha kuitaja TFF hii ni mafanikio ya Simba msimu uliopita ilhali wao ndio wenye mpira wao nchini?

Sisemi kwamba TFF hii haikosei na haijakosea,. mm msingi wa makala yangu ni mafanikio ya uwanjani ambayo ndio Watanzania wanayataka.

Narudia tena na tena, MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.

Sote tunajua wanazo changamoto nyingi na mapungufu yao kama Binadaam lakini katika hili la matokeo ya uwanjani wao ni namba wani kulinganisha na Nyimati za tawala zingine za TFF/FAT Huko nyuma.

Siku nyingine nikijaaliwa ntaandika changamoto na kasoro zao uongozi huu madhubuti ulio chini ya Rais Chief Wallace Karia na mtendaji mkuu Mido kisheti Wilfred Kidao.

Najua katika eneo la ukosoaji mm ni mzuri zaidi ya kusifia, hvyo nna imani ntawafurahisha sana Wakosoaji wa Tawala hii bora kabisa ya soka nchini kuwahi kutokea.

Nice weekend.

MJUE GLORY MEISEYEKI, MWANA HABARI ALIYEJIKITA KATIKA MASUALA YA UTALII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Maonesho ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SiTE) yameweza kuwavutia wadau wengi, hususani wajasiriamali wadogo wanaozalisha mazao ya utalii nchini.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Mjasiriamali mdogo ambaye pia ni muanzilishi wa Asili Style, Glory Meiseyeki amesema kuwa hii ni mara yao ya kwanA kushiriki katika maonesho hayo ya (SiTE)  na wameweza kukutana na wadau mbalimbali.

Amesema, wazo la kuanzisha kutengeneza bidhaa za utalii ni baada ya kupata wazo hilo wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya TBC Safari alipowavalisha baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho.

Glory amesema, maonesho ya mwaka huu ni mazuri na yeye ni mara yake ya kwanza kushiriki ila ameona fursa nyingi ikiwemo kuzungumza na wadau mbalimbali wa bidhaa za utalii 'Speed networking'.

"Unakutana na watoa huduma tofauti, kutoka nchini tofauti mnakutana na kufanya mazungumzo pamoja na kubadilishana mawasiliano,"amesema Glory.

"Asili style imeanzishwa mwaka huu, na imejikita katika kuzalisha na uuzaji wa bidhaa za utamaduni ambapo tumeanzia nguo za kimasai ambapo zina rangi nyingi unaziweza kuzielezea, utungaji wa shanga na vingine zaidi,"

Glory ni mwaandishi wa habari aliye mbunifu na kupenda masuala ya utalii na kuamua kujikita zaidi katika kuwa mbunifu wa mitindo mbalimbali ya kitalii kwa kutumia nguo na bidhaa za Kimasai.
Mwanahabari Glory Glory Meiseyeki, mjasiriamali mdogo na Mwanzilishi wa Asili Style akionesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza kwa kutumia utamaduni wa asili ya Kimasai katika maonesho ya tano ya Utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE)  2019.
Mwanahabari Glory Glory Meiseyeki, mjasiriamali mdogo na Mwanzilishi wa Asili Style akitoa maelezo mbalimbali kwa wateja waliofika kutembelea band lake ndani ya maonesho ya ya tano ya Utalii Swahili International Tourism Expo (SiTE)  2019




MOBILIZE4HEALTH AFYA FORUM NOVEMBER 9, WASHINGTON DC, USA

$
0
0

2019 DICOTA HEALTH FORUM: 
PRELIMINARY PROGRAM

We are pleased to share with you the preliminary agenda. We invite you to explore the agenda and also share your thoughts. Our team is working hard to assemble an exceptional group of speakers to allow for a meaningful exchange of information to propel us forward. Do you have experiences to share as part of your health venture(s)? Contact us at dicota@dicotausa.org.

8:00 am Registration and Breakfast
9:00 am Opening Keynote Address
10:00 am Navigating Tanzania Health Governance
and Regulatory System
11:00 am Human Resources for Health
12:00 pm Lunch Keynote Address
2:00 pm Diaspora Health Initiatives in Tanzania
3:00 pm Leveraging Diaspora-owned American -based
Ventures in Tanzania
4:00 pm Business and Investing in Health in Tanzania
5:00 pm Closing Keynote Address

EARLY BIRD REGISTRATION

**Register by Oct 15, 2019
and Save $25.
**Active DICOTA members
get 25% off.
REGISTER NOW

NEW PASSPORT APPLICATION OR RENEWAL FOR ALL GUESTS REGISTERED AND ATTENDING DICOTA HEALTH FORUM.

All guests, who have completed online application, made all required payments and have sent their names to dicota@dicotausa.org by October 25, 2019 will get their picture and fingerprints taken at Tanzania Embassy in Washington DC on Friday, November 8th, 2019.

PLEASE FOLLOW INSTRUCTIONS BELOW:
All guests who have registered for DICOTA Health Forum and in need of new / renew their Passports are required to FIRST complete the online application process (here) and make all required payments online as outlined here by October 25, 2019.
Please send your full name and contact information to dicota@dicotausa.org (Subject: PASSPORT) after completing the online process no later than October 25, 2019.

Please contact the Passport department at the Tanzania Embassy in Washington DC (202) 939-6125 for all questions concerning the online application process.

SOCIAL EVENT

After a full-day of exchanging, learning, and connecting, we invite you to get on our dancing shoes and head to the Serengeti Restaurant and Lounge. Prepare to let loose with music and enjoy the tantalizing Swahili dishes.

TIME: 9:00 pm to 3:00 am
MUSIC: By the Mix Master, DJ Luke
COVER CHARGE: $10 per person
LOCATION: Serengeti Restaurant & Lounge
6210 Georgia Ave, NW, Washington, DC

SPONSORSHIP OPPORTUNITIES

DICOTA welcomes you to join us as a sponsor for the Mobilze4Health Forum. As a sponsor, your organization will gain valuable exposure to a targeted audience and you will be helping to ensure the success of this forum. We have four levels to choose from, including KLUTE, MERU, MAWENZI, and KILIMANJARO. Not sure which level is right for you?

E-mail us at dicota@dicotausa.org. Let's discuss your goals. Together we'll build the appropriate sponsor package so you can effectively benefit from engaging in the forum.
 

PROF. KABUDI AKUTANA NA MABALOZI WATEULE WA EU NA RWANDA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazugumzo na Balozi  Mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti katika ofisi ndogo za Wizarajijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fantiakifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge akimkaribisha Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles katika ofisi ndogo za Wizarajijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti na Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge, pamoja Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles. Kulia ni Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge.

Prof. Kabudi akutana, kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Balozi Fanti kuwa Uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni wa Muda mrefu tangu mwaka 1975 ambao hadi sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na umoja huo.
"Ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umelenga kupunguza umasikini, kukuza maendeleo endelevu, na kusaidia ujumuishaji wa Tanzania katika uchumi wa dunia, mpango kazi wa ushirikiano huu unaundwa na nguzo kuu tatu ambazo ni maendeleo ya uchumi, biashara na uwekezaji pamoja na mazungumzo ya kisiasa. Msaada wa Umoja wa Ulaya umeweza kushughulikia changamoto mbalimbali katika ajenda za maendeleo ya kitaifa" Alisema Prof. Kabudi
 Waziri Kabudi ameongeza kuwa, kulingana na takwimu za mwaka 2017, Umoja wa Ulaya unaonekana ndiye mshirika mkubwa zaidi wa biashara ya bidhaa kwa Tanzania baada ya India, kwa asilimia 13.1. Bidhaa zinazoingizwa kutoka Umoja wa Ulaya ni pamoja na mashine, vifaa, bidhaa za kemikali na vifaa vya usafirishaji.  
 Prof. Kabudi amegusia pia mazungumzo ya kisiasa na kueleza kuwa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya. Mazungumzo ya kisiasa yanalenga kuongeza uwazi na umoja ili kukuza uelewa wa pamoja katika vyama vya siasa.
 Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti amesema kuwa Umoja huo upo tayari kusaidia Tanzania na kuhakikisha kuwa sera za nchi zinasonga mbele ili kuiwezesha Tanzania kuwa na  maendeleo endelevu na kusaidia malengo ya nchi. 
"Pia tupo tayari kuhakikisha kuwa uwekezaji na biashara unaofanywa kati ya Umoja wa Ulaya pamoja na Tanzania unakuwa wa manufaa kwa pande zote lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa Tanzania" Balozi Fanti
Katika tukio jingine Waziri wa Mamno ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule  wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Karamba Charles ambaye ameelezea uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Rwanda ni wa kiwango cha juu na kuongeza kuwa jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuongeza kiwango cha biashara na uswekezaji kati ya Nchi hizo mbili.
Meja Jenerali Karamba Charles ameyasema hayo wakati akikabidhi nakala za hati ya utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kuchukua nafasi ya  aliyekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Balozi Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania

MAHFALI KIDATO CHA NNE, SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAFANA

$
0
0
Na Karama Kenyuko, Michuzi TV

KANALI Philip Mahende wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), amewaasa wazazi nchini kuishi katika misingi bora, kushiriki katika mambo ya kijamii kwa sababu Watoto hujifunza kutokana na kile wanachofanya wazazi.

Akizungumza katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari ya Makongo ya jijini Dar es Salaam leo Oktoba 19, 2019, Kanali Mahende kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Charles Mbuge, amewaasa pia wazazi kutumia muda mwingi kukaa na familia zao hasa watoto wadogo ambao bado wanakua na kuweza kujifunza kwenye maadili.

Aidha amesema, Jeshi la Kujenga Taifa linazo shule ambapo linalea Wanafunzi kuanzia ngazi ya Shule ya Msingi hadi Sekondari, tumekuwa tukiwapa malezi ya aina zote, stadi za maisha stadi za kazi ujasiliamali pamoja na mbinu za kivita ili kiwajengea misingi imara ya maisha hata pale wanapokuwa wamemaliza masomo yao

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo, Kanali Yuda Kitinya amewataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha  Wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao hawahudhurii masomo shuleni katika kipindi kifupi kilichobakia cha kuelekea mtihani wa taifa wafike ili kuweza kufundishwa kile ambacho wamebakiza.

"Watoto wetu baadhi kwa huu muda mfupi uliobaki hawafiki shuleni, wazazi naomba tushirikiane kwa hilo, wanatafuta vituo vingine mitaani, inatuwia vigumu. Mwalimu amepanga kwa ajili ya kumalizia vile anavyoona vitakuwa vigumu, halafu mtoto ametafuta mwalimu mwingine mitaani ambae hamjui udhaifu wala uwezo wake, kwa hiyo yeye atamfundisha akimhakikishia kuwa yeye ni mwalimu bora kuliko wote hapa Da es Salaam kumbe anamlia pesa zake". Amesema Kanali Kitinya


Amewaambia wanafunzi hao kuhakikisha wanautumia muda mfupi uliobaki kujisomea ili waweze kufaulu katika mtihani wao.

Amesema wamekuwa wakitumia mbinu mbal mbali ili kuweza kuwafikisha wanafunzi hao mahali pale wakiamini kuwa wakizifuata na kizishika mbinu hizo basi wote wataweza kufaulu na kuongeza kuwa katika wiki mbili zilizobaki watahakikisha wanarekebisha pale ambapo watakuwa hawajajiweka vizuri ili kuwawezesha kufanya mitihani yao kwa ufanisi mkubwa.

Mbali na elimu pia tumewajenga kitabia na nidhamu na tumewajengea, ukakamavu na stamina ili kufanya miili yao iwe na nguvu na kutumia vizuri muda wao ndio maana kuna maeneo hapa shuleni hawaruhusiwi kutembea isipokuwa kukimbia".

Ameongeza kuwa, shule ya Makongo pia imekuwa ikishiriki katika michezo mbali mbali kwa mafanikio makubwa ambapo imekuwa ikiongoza kwenye michezo mbali mbali kwa kupitia shule yenyewe ama timu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa wanafunzi wake wame wakishiriki na mpaka sasa kwa miaka mitano mfululilzo shule hiyo imekuwa ikiongoza na kutoa wawakilishi kitaifa.

Aidha amesema kuwa, uongozi wa shulenhiyo umekuwa ukijitahidi kuboresha maeneo mbali mbali japo kazi ya kuboresha miundombinu shuleni hapo ni kazi ngumu ila

Kanali Kitinya amesema shule hiyo inajabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la ufinyu na uchakavu wa maktaba ya shule eneo ambalo ni muhimu sana kwa mahitaji ya shule kwani jengo letu ni dogo na linahitaji marekebisho.

Pia màabra zetu ni za zamani, zinahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ama kujengwa mpya. Pia madarasa yetu ni ya muda mrefu kwani kama mnavyojua Makongo ilianza zamani sana majengo yamechoka na yanahitaji ukarabati mkubwa.

Ameongeza kuwa, shule imekuwa na changamoto kubwa ya usafiri safiri hasa kwa wanafunzi wa kutwa ambao wamekuwa wakipatwa na adha mbali mbali hususani kipindi cha mvua. "Hosteli yetu ni ndogo na haitoshelezi wanafunzi wote, wanafunzi wa nje wanakuwa na changamoto ya usafiri hasa kipindi cha mvua..., tunataka wanafunzi haww waweze kufika shuleni kwa urahisi wakiwa hawajachoka na kupata muda mzuri wa kusoma na kufundishwa,amesema.

"Tunatarajia watoto hawa baada ya kumaliza mitihani yao na kwenda uraiani watakuwa mabalozi wazuri na wanajamii safi, hatutegemei mmoja akakamatwa na polisi kwamba kafanya jambo baya, ama akawekwa gerezani...,tunaamini kww elimu waliyoipata hapa basi wote watakuwa ni wazalishaji wa kutegemewa kuanzia nyumbani mpaka jamii nzima inayowazunguka" amesema Kanali Kitinya.


Kwa upande wake mwalimu wa Taaluma kapteni Rajabu Mohamed amesema, anaamini wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha nne watapata ufaulu kwa alama za juu kwa kuwa taaluma waliyokuwa wakiwapatia ni bora kwani walikuwa wakihakikisha wanajisome kwa kuwapatia mitihani mara kwa mara.

"Tunatarajia wanafunzi hawa watapata matokeo bora hivyo ninawasii wazazi wasisite kuleta watoto wao Makongo Sekondarikwani hapa mbali na kuwapatia elimu pia tunawalea kwa nudhami bora, utimamu na kuwashirikisha katika michezo mbali mbali.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (Mwenye sare za Jeshi), Kanali Yuda Kitinya akizungumza katika Mhafali hayo ya Kidato cha Nne shuleni hapo aambapo amewataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha  Wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao hawahudhurii masomo shuleni katika kipindi kifupi kilichobakia cha kuelekea mtihani wa taifa wafike ili kuweza kufundishwa kile ambacho wamebakiza.
  Vijana wa Skauti katika Shule ya Sekondari ya Makongo wakionyesha Ukomando mbele ya Mgeni rasmi.
KANALI Philip Mahende wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumza kwa niaba ya Brigedia Jenerali Charles Mbuge, amewaasa wazazi kutumia muda mwingi kukaa na familia zao hasa watoto wadogo ambao bado wanakua na kuweza kujifunza kwenye maadili. , amewaasa wazazi nchini kuishi katika misingi bora, kushiriki katika mambo ya kijamii kwa sababu Watoto hujifunza kutokana na kile wanachofanya wazazi.

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA KODI KIWANDA CHA KILIMANJARO FRESH

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Ahmed Mahmoud, Arusha)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja maziwa yanayotengenezwa na kiwanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na Ahmed Mahmoud,Arusha). 

********************************

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeaidi kutatua changamoto kubwa inayokikabili kiwanda cha usindikaji wa maziwa cha Kilimanjaro fresh cha jijini Arusha kinachokabiliwa na changamoto ya ukubwa wa kodi ya ongozeko la thamani ambalo inabidi kushindwa kufikia uzalishaji mkubwa wa maziwa kama uhitaji wake ulivyo mkubwa kwa jamii

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Freshi jijini Arusha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ullega amesema kwamba serikali kupitia wizara yake itaakikisha inaondoa changamoto hiyo ya tozo kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa usindikaji wa maziwa katika kiwanda hicho cha Kilimanjaro fresh Milk

Ullega amesema kwamba kiwanda hicho toka kuanzishwa kwake miesi 6 kimekua na mafanikio mkubwa ili mpate mafanikio zaidi lazima mnunue kwa bei kubwa zaidi kutoka kwa wafugaji ambao watapata nguvu ya kuweza kuzalisha zaidi na kuongeza thamani ya uzalishaji wenye uboira unaohitajika.

Amesema kuwa mmesema kuwa mtatoa motisha ya mitanda endeleeni na zoezi hilo kwa kuwa ni sehemu ya kuongeza motisha kwa wafugaji kuongeza uzalishaji kwenye bidhaa za maziwa hapa nchi nanyi kuweza kuongeza uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho na muendelee kufuata maagizo ya serikali kwa ajili ya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo.

Alisema kuwa kiujumla wameeza vizuri katika uzalishaji wenye tija na nimependa utoaji wenu wa elimu kwa wafugaji kuwapa elimy ya ulishaji wa chakula vizuri mrudie agizo la waziri mkuu kwa kiwanda cha maziwa Asas kwenye wiki ya maziwa Kilimanjaro muandike barua wizarani kuhusu malalamiko yenu nasi tutayafanyia kazi haraka kwa faida ya ukuaji wa tasnia

Awali akitoa maelezo ya Kiwanda hicho mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Kilimanjaro Fresh Irfhan Virjee alimweleza mh,Naibu waziri changamoto zinazo mkabili katika uzalishaji wa maziwa kua tozo ni changamoto ya kodi ya vat ambapo ameomba kuondolewa.

Alisema kuwa mwezi wa kwanza mwaka 2020 wanataraji kuzalisha lita zipatazo elfu 20 ambapo pia wanataraji kuanza kuuza maziwa nje ya nchi ambapo walianza kuzalisha kuzalisha lita elfu 3000 hadi sasa wanazalisha lita 800kwa siku.

Alisema kwamba kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa wafugaji kutoka vyama vya ushirika ambapo huwauzia maziwa kwa kiasi cha shi;lingi 800 hadi kufikia shilingi 850 ambapo pia wakulima hupatiwa motisha kwa lengo la kuendelea kutunza mifugo kwa lengo la kuboresha mifugo kupata maziwa yalio na ubora wa hali ya juu .

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR.

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa meza kuu (kulia kwa Rais) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, wakipitia makabrasha ya Kikao cha Kamati Maalum ya CCM,wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Kikao hicho.(Picha na Ikulu)MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kufungua Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kulia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.Bi. Lela Burhani Ngozi, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo 20-10-2019 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu) 


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo Tarehe Octoba 20,2019 ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho cha siku moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Kupitia Kikao hicho Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kikao hicho ni mwendelezo wa kujadili baadhi ya ajenda zilizotokana na kikao kilichopita ambazo zilitakiwa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Kikao hicho.

Kikao hicho ni maalumu kinachojadili masuala mbali mbali ya Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977 Toleo jipya la 2017.

Viongozi mbali mbali Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’.
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images