Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live

KIASI CHA SHILINGI BILIONI 3.417 ZINAHITAJIKA KUBORESHA CHUO CHA UHAZILI NA TIGANYA VINCENT

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa akiwahutubia watumishi na wanachuo wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora wakati wa ziara ya siku moja jana chuoni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maneno ya utangulizi wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Balozi wa Sweden Nchini Anders Sjober walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkaribisha Balozi wa Sweden nchin Anders Sjober wakati wa ziara ya Balozi huyo Mkoani Tabora jana.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akimkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Ututumishi na Utawala bora Dkt. Mary Mwanjelwa (kulia) wakati alipoongozana na Balozi wa Sweden nchini alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora jana
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey , Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Balozi wa Sweden Nchini Anders Sjober na viongozi mbalimbali na wanachuo wa Uhazili wakicheza wimbo maalumu wakati wa ziara yao ya siku moja ya kukagua Chuo cha Utumishi wa Umma.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey , Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Balozi wa Sweden Nchini Anders Sjober na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jana mbele ya jengo la Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yao ya siku moja ya kukagua Chuo cha Utumishi wa Umma.

*****************************



KIASI cha shilingi bilioni 3.417 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa miundo mbinu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora(Uhazili)

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa wakati wa ziara ya Balozi wa Sweden Nchi Anders Sjober alipotembelea Chuo hicho.

Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ukarabati wa majengo kama vile Mabweni , madarasa, jengo la utawala , uboreshaji wa miundo mingine , ukakamilishaji wa jengo jipya na ununuzi vifaa vya kujifunzia.

Dkt. Mwanjelwa alisema hatua hiyo itasaidia kukirejesha chuo hicho katika ubora wake wa awali na kukifanya kuendelea kuwa sehemu nzuri ya kuwaandaa watumishi kwa ajili ya kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka watumishi wa umma kuhakikisha watoa huduma nzuri kwa wananchi ambayo itakwenda sanjari na maendeleo ya tekonolojia yaliyo hivi sasa.

Kwa upande wa Balozi wa Sweden Nchini Sjober alisema Tanzania na nchi yake zina uhusiano mzuri wa muda mrefu na ndio maana walishiriki kujenga chuo hicho kwa asilimia 80.

Aidha aliipongeza Serikali kwa jitihada zake kujenga jengo jipya ambalo limeshagharimu shilingi bilioni 2.7 ambazo zinatokana na fedha za ndani za mapato ya Tanzania.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kinaomchango mkubwa katika utumishi ndani na nje ya Tanzania kwa kuzalisha viongozi mbalimbali. 

Aliwataja baadhi ya viongozi wakubwa ambao wamepita katika Chuo hicho ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mke wa Rais wa kwanza wa Zimbabwe mama Mugabe.


TAMASHA LA 38 LA SANAA BAGAMOYO,KUANZA KURINDIMA KESHO VIWANJA VYA CHUO

$
0
0
Wasanii zaidi ya 100 kushiriki, wamo Mwana FA, Juma Nature, Dullah Makabila, Gigy Money, Vitalis Maembe,Pia wapo Mashauzi Classic, Malkia Khadija Kopa, Msondo Ngoma, Sisi Tambala, Sinaubi Zawose

TAMASHA la 38 la Sanaa Bagamoyo linaanza rasmi kesho Oktoba 19-26 katika mji wa kihistoria Bagamoyo mkoani Pwani litatemesha mji wa Bagamoyo na mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Mwaka huu tamasha hilo litaanza kwa mtindo wa tofauti na ilivyozoeleka, litaanza kwa kuzunguka mitaa mbalimbali ya wilaya hiyo, lengo likiwa ni hamasa kwa tukio hilo muhimu.

Wasanii wa kazi mbalimbali watazunguka mji huo kwa ngoma mbalimbali ili kuwachochea wadau kujitokeza katika ukumbi ulioko chuoni hapo.

Zoezi hilo la kuzunguka maeneo ya Bagamoyo, litaanza asubuhi likishirikisha wadau mbalimbali.

Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo yenye urithi na utajiri mkubwa wa kiutamaduni Ulimwenguni, ambako Tamasha hilo la kimataifa, kwa mara nyingine tena litawakutanisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ambao wataonesha kazi zao za sanaa na utamaduni.

Dk. Hebert Makoye, ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), ambao ni waandaaji wa tamasha hilo linalozidi kujizolea umaarufu kila mwaka, anasema lengo ni kuendeleza na kudumisha Utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine kupitia warsha, kongamano na maonyesho mbalimbali.

Dk. Makoye, anasema tamasha la 38 linatarajiwa kushirikisha wasanii zaidi ya 100 ya hapa nchini na nje, likiwa na dhamira ya kubadilishana uzoefu katika sanaa, hivyo ni nafasi ya wadau mbalimbali wa sanaa kujitokeza na kushuhudia elimu kutoka kwa wasanii watakaopanda jukwaani.

Anasema, tamasha la mwaka huu litashirikisha vijana wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Bagamoyo, Vyuo na Vyuo Vikuu.

“Mwaka huu, tamasha linatarajiwa kuhudhuriwa na jumla ya watazamaji 60,000 kutoka maeneo ya Bagamoyo, Dar es Salaam na sehemu zingine za Tanzania pamoja na nje ya nchi,” anasema Dk. Makoye na kuongeza.

Kusudi la Tamasha hili ni kutoa fursa kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi, pamoja na watazamaji kukutana na kuuenzi utajiri wa utamaduni wao unaowatofautisha na mataifa mengine, ambao unaonyesha utofauti wao katika muktadha wa maadili na mshikamano, pamoja na ubunifu.

Malengo maalum ya Tamasha

Dk. Makoye, anasema ni jukwaa kwa wanafunzi wa TaSUBa na wa kutoka taasisi zingine za mafunzo, kuonesha kazi zao na stadi walizopata katika mafunzo yao ya sanaa na utamaduni.

Anasema, pia ni kukuza na kubadilishana tamaduni kati ya wasanii wa ndani na wa kimataifa, ni jukwaa la wasanii wachanga kuonesha vipaji na ustadi wao kwenye sanaa na utamaduni, kuongeza uhamasishaji miongoni mwa vijana na wasanii juu ya masuala yanayohusu sanaa, michezo na utamaduni wa Kitanzania.

Dk. Makoye, anasema Kauli mbiu ya Tamasha la mwaka huu ni ‘Sanaa na Utamaduni Ajira Yangu’.Aidha, anasema katika tamasha la mwaka huu, kutakuwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali za sanaa na za kiutamaduni, vyakula mbalimbali kama vile nyama choma, samaki, pamoja na vyakula vya baharini.Pia, anasema wageni watapata fursa ya kutembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

TaSUBa, Clouds Plus kuboresha tamasha

Mapema mwaka huu, TaSUBa imeingia makubaliano na Kampuni ya Clouds Plus Production yenye lengo la kushirikiana katika kusaka rasilimali za uendeshaji wa Tamasha hilo la Kimataifa la 38.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano iliyofanyika ukumbi mkubwa wa maonesho wa TaSUBa, Dk. Makoye, anasema lengo kuu la makubaliano hayo ni kutafuta rasilimali zitazowezesha kuendesha tamasha hilo lenye lengo la kuenzi, kudumisha na kutunza utamaduni wa Mtanzania.

Anasema tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982, tamasha limekuwa likifanyika kila mwaka bila kukosa mbali na kukumbwa na uhaba wa fedha, lakini anaamini kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya biashara ya Clouds Plus Production, tamasha linaweza kuvutia wawekezaji mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Uendeshaji wa Clouds Plus Production, Ramadhani Bukini, anasema kampuni yake inayomiliki runinga na redio, itatumia mbinu mbalimbali kulitangaza tamasha hilo Duniani ili kufanya lifikie malengo yake ya kuenzi na kudumisha utamaduni wa Mtanzania na pia kuvutia wawekezaji wengi.

Ratiba mahsusi

Dk. Makoye, anasema katika wiki ya tamasha zipo siku zitakuwa maalum kwa ajili ya ratiba mahsusi, ambako Jumatatu itakuwa ni ‘Usiku wa Filamu’, Jumatano ‘Usiku wa Muziki wa Dansi’ na Jumapili ‘Usiku wa Taarabu’.

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani mwaka huu ni Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, Juma Kassim ‘Juma Nature’, Barnaba Elias ‘Barnaba’, Dullah Makabila, Gigy Money na Vitalis Maembe.

Wengine ni Mashauzi Classic, Malkia Khadija Kopa, Thabit Abdul, Bendi ya Msondo Ngoma, John Kitime na bendi yake, Sisi Tambala, Sinaubi Zawose, Shada Acrobatics na Baldreda kutoka Marekani.

Dk. Makoye, anabainisha kuwa pia makundi ya hapa nchini yatashiriki, ambapo Bagamoyo itatoa 37, Dar es Salaam 28, Zanzibar mawili huku mikoa ya Mwanza, Ruvuma, Morogoro, Kilimanjaro, Njombe yatatoa kundi moja moja, Arusha mawili na Dodoma 10.

Makundi kutoka nje ya Tanzania, Marekani yatakuwa mawili, Botswana, Korea Kusini, Zimbabwe, Uganda, Zambia na Finland kundi moja moja huku kutoka Kenya yakiwa nane.


Mgeni rasmi ufunguzi/ufungaji

Dk. Makoye, anaweka wazi mgeni rasmi wakati wa ufunguzi katika tamasha la mwaka huu, anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe huku wakati wa kufunga atakuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza.
 Kikundi cha Sanaa cha Kisonge cha TPS-Moshi kikitoa burudani ya aina yake katika tamasha hilo
 Kundi la walimu wa Taasisi hiyo wakionesha umahiri katika tamasha la mwaka jana
 mojawapo ya makundi kutoka nje yaliyoshiriki tamasha la mwaka jana
 Watazamaji waliofika katika ukumbi wa taasisi hiyo
 Waziri Mwakye akijaribu fulana katika tamasha la mwaka jana huku Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dk Herbert Makoye akifurahia hatua hiyo
 Waziri Mwakyembe alipowasili kwenye viwanja vya TaSUBa mwaka jana
Waziri Mwakyembe katika tamasha la mwaka jana 
Waziri Shonza akiangalia mojawapo ya sanaa za ufundi katika tamasha la mwaka jana

WARNING: FRAUDULENT USE OF THE AFRICAN DEVELOPMENT BANK GROUP'S (AFDB) NAME

ONYO:MATUMIZI MABAYA YA JINA LA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KWA UDANGANYIFU

TANDAHIMBA YAJIPANGA KUONDOA TATIZO LA WATOTO KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

$
0
0

 Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka akifafanua jambo 
  shule ya msingi Amani iliyopo Tandahimba mjini
Afisa Elimu Msingi  wa Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka amesema anajipanga kuondoa tatizo la watoto kutojua kusoma na kuandika wanapomaliza elimu ya msingi.

Amesema hayo wakati akizindua mashindano ya Wilaya ya Kusoma,Kuandika,Kuhesabu na Kuchora   ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Amani iliyopo Tandahimba mjini

" Wanafunzi ambao wamemaliza mwaka huu 34 walikuwa hawawezi Kusoma wala kuandika hii ni changamoto,lakini lengo letu ni kutokuwa na wanafunzi wa namna hii ndani ya Wilaya yetu,"amesemaMwinuka

Amesema wanafunzi 54 wa darasa la Kwanza na la pili wanashindana na wanatarajia kupata wanafunzi 8 ambao watakwenda kwenye mashindano ya Mkoa na baadaye Kitaifa



ZAHANATI YA DUCE WABORESHA HUDUMA YA AFYA KWA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es  Salaam (DUCE) kimezindua jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo limezinduliwa na Mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko litakalokuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za Afya ya uzazi na mtoto.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo, Aimbora amesema DUCE wamefanya jambo kubwa sana kwani afya ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo katika taifa letu.

Aimbora amesema, zahanati ya DUCE imekuwa inatoa huduma nzuri sana kwa jamii inayowazunguka na hata yeye ni mmoja wa watu wanaofika kupata huduma hapo.

Amesema, kutanua wigo kwa kuweka huduma ya Afya ya uzazi na Mtoto itawasaidia kuanzia watumishi wa Chuo, wanafunzi na hata wananchi wanaokaa kwenye mazingira yanayowazunguka.

"Mmefanya jambo kubwa kutanua wigo wa huduma kwani ni jambo kubwa na la muhimu, kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya tunawapongeza sana na mmesema mnataka kuongeza hadhi ya Zahanati ninaamini hilo litafanikiwa kwa juhudi kubwa mnazofanya,"amesema Aimbora.

"Niwapongeze zaidi kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli za kutekeleza na kujenga Zahanati ili wananchi wapate huduma nzuri, pia madaktari na waaguzi mnafanya kazi kubwa ya kutoa huduma bora ya Afya,"


Naye Mkuu wa Chuo Kishiriki RASI Prof Bernadeta Killian amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2019, zahanati ya DUCE imeweza kuwahudumia wagonjwa 15,138 wakiwemo wanafunzu, watumishi na wakaazi wanaozunguka maeneo hayo.

Amesema, kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya ya uzazi na mtoto kwa wana DUCE na wanajamii wanaoishi jirani imewasukuma kujenga jengi hilo ili kuwezesha huduma inapatikana na kuongeza wigo na kipato kwa chuo.

"Jumla ya Milion 59 zimetumika kukamilisha jengo, Milion 41.7 zimetumika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo na Milioni 17.3 kwa ajili ya kununulia thamani na zote zimetokana na mapato ya ndani ya chuo, "amesema Rasi Bernadeta.

"Chuo kina mikakati endelevu ya kuiboresha Zahanati ili iweze kutoa huduma bora zaidi ksa wanajumuiya ya DUCE na wananchi kwa ujumla na mikakati hiyo ikiwa ni kupandisha hadhi Zahanati kuwa kituo cha Afya, kuanzisha kamati ya Afya ya Chuo, kuifanya zahanati kuwa kliniki ya huduma za kibingwa na kutangaza huduma kwa watu wengi zaidi," 

Katika jengo hilo, Kumepatikana chumba kimoja cha Daktari kitakachotumika kutolea huduma za matibabu kwa wagonjwa wote, na itasaidia kupunguza changamoto ya vyumba.

Pia, kutakuwa na huduma ya ufuatiliaji wa ukuaji bora na wenye afya kwa watoto chini ya miaka mitano sambamba na utoaji wa chanjo kwa watoto hao hali kadhakika kutakuwepo na utoaji wa huduma rafiki kwa vijana.
Mkuu wa Chuo Kishiriki (DUCE) RASI Prof Bernadeta Killian akisoma hotuba kwa mgeni rasmi yw uzinduzi wa jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akitoa pongezi kwa Chuo Kishiriki DUCE kwa hatua kubwa waliyoifanya ya kujenga jengo jipya litakalokuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za Afya ya uzazi na mtoto.
Mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akizindua jengo jipya la afya ya Mama na Mtoto litakalotoa huduma kwa watumishi wa Chuo Kishirikishi DUCE, wanafunzi na wakazi wa maeneo hayo.
Mwakilishi  wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Aimbora Aminiel Nnko akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya DUCE Dr Saning'o Sangeti baada ya kuzindua jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Rasi (Utawala)  Dkt  Method Semiono akitoa neno la Shukrani kwa Mwakilishi wa Mkuu ws Wilaya baada ya kuzindua jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Jengo jipya la Afya ya uzazi na mtoto katika zahanati ya Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

TAIFA STARS YAFUZU CHAN, YAIMALIZA SUDAN NYUMBANI

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu Michuano ya Mataifa Bingwa barani Afrika kwa Wachezaji wa Ndani maarufu kama CHAN baada yakuondoka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sudan katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la El Merriekh Omdurman nchini Sudan

Taifa Stars inafuzu Fainali za Michuano hiyo itakayofanyika nchini Cameroon mwakani kwa faida ya bao la ugenini licha ya matokeo ya jumla ya bao 2-2.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi zaidi kutokana na shinikizo la timu zote mbili, Stars ilitumia nafasi zake vizuri licha yakuruhusu bao la mapema dakika ya 30 ya mchezo lililofungwa na Mchezaji wa Sudan, Amr Suleiman.

Dakika ya 49 ya mchezo, bao safi lililotokana na faulo ya Erasto Nyoni liliirudisha Stars mchezoni pamoja na mabadiliko yaliyofanywa Benchi la Ufundi katika kipindi cha pili.

Mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda zaidi kwa Kocha Etienne Ndayiragije kuingiza Washambuliaji na Viungo ilikutawala mchezo nakupata mabao ya ushindi. Wachezaji walioingia kuongeza nguvu kwa upande wa Stars, Mshambuliaji, Shaaban Iddi 'Chilunda', Ayoub Lyanga na Kiungo Salum Aboubakar 'Sure Boy'.

Benchi la Ufundi la Stars likiongozwa na Ndayiragije lilipata faida zaidi kupelekea kupata bao la pili dakika ya 78 lililofungwa na Mshambuliaji, Ditram Nchimbi.


Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Septemba 22, 2019 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Taifa Stars ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwao, Sudan.
Mshambuliaji wa Stars, Iddi Suleiman 'Nado' akichuana na Mchezaji wa Sudan katika Mchezo wakuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), uliopigwa katika dimba la El Merreikh Omdurman nchini Sudan, Stars imefuzu Michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini licha ya matokeo ya jumla ya 2-2.
Kikosi cha Sudan
Kikosi cha Taifa Stars
Mashabiki

Tigo yatoa msaada wa Sh110 Milioni Hospitali ya CCBRT kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya mguu kifundo (clubfoot).

$
0
0

Mkurugenzi mtendaji (Tigo) Bw. Simon Karikari akimkabidhi mfano wa hundi ya Mil 110/- Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi.Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT

  Kampuni ya mawasiliano ya Tigo leo imetoa msaada wa Sh110 milioni kwa Hospitali ya CCBRT kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma za afya hasa kwa wagonjwa wenye matatizo ya mguu kifundo (clubfoot) utakaowanufaisha wagonjwa zaidi ya 400 hapa nchini. Msaada huu unatolewa ikiwa ni njia ya kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa matibabu ili kuwawezesha wagonjwa kupatiwa matibabu stahiki na ya wakati ili kuhakiksha ugonjwa huo unatokomezwa hapa nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema “Upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa mguu kifundo hasa watoto imekuwa ni changamoto kubwa hivyo tatizo hili linatakiwa kupewa kipaumbele na kwa kuona hilo Tigo tunahakikisha tunabadili historia,” alisema. Karikari alisema pia msada huo utaongeza ushiriki wa jamii na utayari wa wadau katika kuhakiksiha matibabu ya uhakika kwa watoto wenye tatizo hilo yanapatikana ili kutoa fursa kwa wao kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Aidha, Karikari alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Tigo katika kuboresha maisha ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa miguu kifundo kwakuwa ugonjwa huo unaweza kutibika. “Kupitia mchango huu tunaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kusaidia kujenga Taifa la watu wenye afya ambao wataweza kuchangia katika shughuli za kimaendeleo na pia nitoe wito kwa wadau wengine kuungana na CCBRT ili kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii yetu,” alisema. Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi aliishukuru Tigo kuwa sehemu ya maendeleo ya hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wagonjwa hasa watoto. 
“Tigo imeonyesha mfano wa kazi ya sekta binafsi katika kutoa suluhuhisho kwa matatizo yanayozikumba jamii zetu.Kwa miaka kadhaa, CCBRT imefanikiwa kutatua changamoto ya matibabu ya ugonjwa huu wa miguu kifundo kwa kuhakikisha wagonjwa wanapatiwa huduma endelevu pamoja na ufuatiliaji wa mara kwa mara,” alisema Msangi. 
Aliongeza “Kupitia Tigo tumeweza kuja na mfumo wa kuwakumbusha wateja wao kwa njia ya SMS juu ya ufuatiliaji wa matibabu kwa wagonjwa ili kuhakikisha wanamaliza matibabu kikamilifu, hivyo napenda kutoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono hatua hii.
” Kwa kutambua umuhimu wa teknolojia ya meseji (SMS) katika kurahisisha mawasiliano kwa wagonjwa wake, CCBRT imeungana na Tigo na kuanzisha mfumo wa kuwakumbusha wagonjwa kufuatilia matibabu mara kwa mara. Mfumo huo ambao ulizinduliwa mwaka 2013, ni hatua muhimu katika kuhakikisha wagonjwa wanafuatilia matibabu kwa wakati hadi pale wanapopona kikamilifu.Mgonjwa anaweza kutumiwa ujumbe wa kumkumbusha ndani ya siku nne na siku moja kabla ya siku ya kuonana na daktari. 

 Tangu ulipoanza kutumiwa na CCBRT, mfumo huo umeweza kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokatisha matibabu kabla ya wakati ambapo zaidi ya watoto 1,500 wameshanufaika na njia ya matibabu ya Ponseti (bila upasuaji) ya kutibu mguu kifundo. Aidha, zaidi ya wagonjwa 400 wamepata matibabu ya upasuaji kwa miaka minne iliyopita na ikitegemea kuongeza idadi hiyo mara mbili baada ya Tigo kutoa fedha hizo. //Mwisho//

Serikali Yatangaza Msako wa Wahujumu wa Benki ya NJOCOBA na Vyama Vya Ushirika

$
0
0

Mkuu wa mkoani Njombe Christopher Olesendeka 


NJOMBE

Mkuu wa mkoani Njombe Christopher Olesendeka ametoa siku mbili kwa wadaiwa sugu waliosababisha kufilisika kwa benki ya wananchi Njombe NJOCOBA kujisalimisha wenyewe octoba 22 saa nne asubuhi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ili kuweka maridhiano ya lini watazirejesha fedha hizo huku pia akitoa onyo kwa yeyote atakae puuza wito huo kukumba na nguvu ya vyombo vya dola.

Akizungumza katika kikao cha ushauri wa barabara RCC mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema Benki ya Njocoba ambayo ilikuwa tegemeo kubwa kwa wakazi mkoani humo haiwezi kufia mikononi mwake na kuwakosesha huduma wananchi hivyo ameanza msako wa watu waliohusika kuifilisi ili waweze kuweka makubaliano ya lini watarejesha fedha walikopeshana kienyeji na kwa kujuana bila kuzingatia taratibu.

Wakati akitangaza siku ya jumanne kukutana na wadaiwa sugu wa benki ya NJOCOBA, Olesendeka pia ametangaza octoba 24 kukutana na viongozi wa vyama vyote vya ushirika ambavyo vimekufa kutokana na utaratibu mbovu wa ukopeshaji fedha pamoja na matumizi mabovu ya fedha na kwamba kiongozi ambaye hataona umuhimu wa kufanya hivyo jeshi la polisi limkamate na kumtia mbaroni kwa masaa kadhaa.

Kwa upande wao wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Odilo Mathias wanasema uamuzi uliochukuliwa na serikali ni uamuzi mzuri na wenye tija kwa wananchi kwa kuwa ilikuwa ikitoa huduma za pembejeo za kilimo, elimu ya fedha pamoja na kuweka na kukopa.

Aidha wamesema kufungwa kwake kumeathiri mzunguko kwa fedha kwa kuwa imefungwa na fedha nyingi za wateja wake.

Hatua hiyo inapokelewaje na wakazi wa mji wa Njombe , hapa ni baadhi yao akiwemo Odilo Mathias na Rozana ngimbuzi wanaeleza hisia zao.

Benki ya wananchi Njombe ilifungwa na BOT mwaka 2017 baada ya kubainika kuwa imeshindwa kujiendesha.

WAZIRI BITEKO ATATUA MGOGORO WA WACHIMBAJI MISUNGWI

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye mkutano wa hadhara katika machimbo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mkutano wa hadhara katika machimbo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhulia katika mkutano wa hadhara ulio ongozwa na Waziri wa Madini Doto Biteko.


…………………

Na Tito Mselem Mwanza,

Waziri wa Madini Doto Biteko ametatua mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu na kuruhusu wachimbaji waendelee na shughuli za uchimbaji katika Machimbo ya wachimbaji wadogo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Mgogoro huo ulisababisha shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu kusitishwa kutokana na sababu za kimaslahi katika madura 38 kati ya 57 yaliyoko kwenye Machimbo hayo.

Shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilisitishwa Oktoba 7 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwa muda usiojulikana kutokana na mgogoro wa umiliki wa eneo yalipo mashimo hayo ili kuweka utaratibu wa usimamizi wa mapato.

Akizungumza na wachimbaji wadogo katika mkutano wa hadhara Waziri Biteko aliwataka waache fitina, majungu na makundi huku akiwataka kufanya kazi na kushirikiana kwa pamoja kwani lengo la Serikali ni kuwafanya wanufaike na uchumi wa madini.

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli alituteuwa tufanye kazi kubwa mbili katika sekta ya madini, tuwapatie wachimbaji wadogo maeneo ya kuchimba ili mshiriki kuinua uchumi wa nchi na tuhakikishe mnalipa kodi za Serikali ili fedha hizo zisaidie kuboresha maeneo mbalimbali kwa maslahi ya wananchi wote ikiwemo afya na elimu”.

“Lazima mfanye shughuli zenu kwa usalama lakini mtakapokuwa na migogoro hicho ni kiashiria cha uvunjifu wa amani, Serikali hatuwezi kuruhusu watu wake wakaumizana ndiyo maana Mkuu wa Mkoa alichukua jukumu la kusitisha shughuli za uchimbaji kwa muda, tumeshirikiana tumetatua mgogoro huo hivyo ninawasisitiza wachimbaji wote muachane na siasa zisizo na maana badala yake mfanye kazi na mlipe kodi ya serikali,” alisema Biteko. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliwataka wachimbaji na wamiliki wa eneo hilo kuweka utaratibu wa usimamizi wa mapato ili kila mtu apate haki yake anayostahili na anufaike kutokana na mapato yanayopatikana katika machimbo hayo.

Aidha, Mmiliki wa eneo hilo Wilbert Kukwanja, alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mongella kwa kuwakutanisha na Waziri Biteko na kumaliza mgogoro huo kwa sababu kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika machimbo hayo kuliwaathiri kiuchumi ambapo aliahidi kulinda amani katika eneo hilo na kutoruhusu migogoro kutokea tena.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga aliwataka wachimbaji katika eneo hilo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia usalama wao kwanza pamoja na kuepuka migogoro ambayo itawaletea hasara wao na familia zao endapo serikali itasitisha shughuli za uchimbaji huku akiwasisitiza kulipa kodi za serikali kila wanapozalisha.

Baadhi ya wachimbaji katika eneo hilo akiwemo Ally Bushiri na Maige Gaude, walimshukuru Rais Magufuli kwa kuteuwa viongozi wachapa kazi kama Biteko ambae ametatua mgogoro huo kwani walikuwa wamekwishakata tamaa walidhani tatizo hilo litadumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.

Ifikapo 2030 matumizi ya zebaki mwisho- Stanslaus Nyongo

$
0
0
Na Nuru Ikupa, DSM 

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amesema Tanzania inaungana na mataifa mbalimbali duniani katika kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahala salama pa kuishi na ili kufiki athma hiyo Tanzania inashirikiana na nchi nyingine duniani kuweka juhudi za pamoja katika udhibiti wa uharibifu wa mazingira na matumizi ya kemikali hatarishi. 

Naibu Waziri Nyongo alisema, Tanzania imesaini Mkataba ujulikanao kama Minemata wenye lengo la kudhibiti matumizi ya kemikali ya zebaki inayotumika kukamata dhahabu kutokana na athari ya kemikali hiyo kwa jamii na mazingira kwa ujumla. 

Alisema mkataba huo unawataka nchi wanachama kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 matumizi ya zebaki katika kukamata dhahabu yanafikia mwisho na njia mbadala inapatikana. 

Nyongo aliyasema hayo jana tarehe 18 Oktoba, 2019 alipokuwa katika mahojiano ya moja kwa moja katika studio za TBC Taifa jijini Dares Salaam alipoalikwa ili kuzungumzia dhana ya usimamizi wa sekta ya madini wenye kuleta tija na manufaa kwa jamii na taifa. 

Nyongo aliendelea kusema zebaki iliyopo sasa nchini itaendelea kutumiwa na wachimbaji wadogo wakati huohuo Serikali ikiendelea na juhudi ya kupata teknolojia mbadala na isiyokuwa na madhara kwa mazingira na wananchi itakayo wasaidia wachimbaji wadogo katika uchenjuaji wa madini. 

Amesema, serikali inafanya tafiti mbalimbali ili kupata teknolojia mbadala ya uchenjuaji wa dhahabu na pindi itakapopatikana Serikali kupitia vituo vya mfano vilivyopo nchini itatoa elimu ya uchenjuaji kwa njia hiyo ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini nchini kupata uelewa wa njia hiyo na hivyo kuachana na matumizi ya zebaki. 

Naibu Waziri Nyongo aliongeza kuwa kutokana na utegemezi wa wachimbaji wadogo kwa kemikali hiyo, haiwezekani kusimamisha matumizi yake kwa haraka kwani wengi hujikita kwenye uchenjuaji kwa kutumia kemikali hiyo kunakowawezesha kujipatia kipato na kutunza familia zao. 

Aidha, amewaasa wachimbaji wadogo kutumia kemikali hiyo kwa njia salama ili kuepusha athari zitokanazo na kemikali hiyo. Amesema serikali ipo macho kuhakikisha inawaelimisha wachimbaji wadogo namna bora ya matumizi ya kemikali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwashauri kutomwaga maji ya zebaki karibu na mito na makazi ya watu ili kuepusha athari zake. 

Pamoja na kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri Nyongo alisema ili kuhakikisha kuwa madini yanatutoa watanzania na kukuza uchumi wa nchi na wananchi sharti wafuate taratibu na sheria za nchi. 

“Chimba madini, uza madini yako kwenye masoko ya madini, acha kuuza kwa njia za panya, sheria itachukua mkondo wake, tutakukamata, tutataifisha madini, na utapata hasara”. Alisisitiza. 

“Ukipata madini lipa kodi lipa tozo fedha hizo ziende kwenye mfuko wa Serikali, Serikali iwekeze kwenye miradi mikubwa ya maendeleo, ijenge shule, ijenge hospitali na barabara, ipende nchi yako. Ukichimba ukashindwa kulipa kodi umeisaliti nchi yako umeusaliti uchumi wa nchi yako”. Alikazia. 

Alimalizia mahojiano hayo kwa kuueleza umma wa watanzania kuwa fasheni ya utoroshaji wa madini imepitwa na wakati kwani serikali ina wigo na mkono mrefu hivyo hivyo hakuna atakayejaribu kutorosha madini hayo atakayefanikiwa kwani atakamatwa na atafilisika.

RC MNYETI AWAFAGILIA DC MAGESSA NA DED KAMBONA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Magessa anaongoza kwa utendaji mzuri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamim Kambona ndiye Mkurugenzi anayeongoza Mkoani humo kwa uchapakazi ikiwemo kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo. 

Mnyeti aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Kibaya kwenye ziara yake ya siku tano wilayani Kiteto. Alisema mkuu wa wilaya ya Kiteto mhandisi Magessa ni mchapakazi mzuri katika mkoa huo akishirikiana na Mkurugenzi wake Kambona hivyo wapewe ushirikiano. 

Alisema japokuwa baadhi ya watu wanamlalamikia mkuu huyo wa wilaya lakini maeneo mengine wanatamani kuwa na mkuu wa wilaya kama mhandisi Magessa. 

"Pamoja na changamoto zilizopo hapa Kiteto ningekuwa natoa maksi ningewapa asilimia 95 kati ya 100 na hiyo ni kutokana na utendaji mzuri wa viongozi wa Kiteto wakiongozwa na Magessa na Kambona," alisema Mnyeti na kuongeza:

"Naomba mnisikilize vizuri mimi ndiye mkuu wa mkoa wenu nawahakikishia kuwa halmashauri inayofanywa vizuri kwenye mambo mengi katika mkoa huu ni Kiteto."

Alisema ubora wao unatokana na kusimamia vyema miradi mbalimbali ya maendeleo usimamizi mzuri hivyo wanapaswa kupongezwa kutokana na hayo. Alisema viongozi wengine wa wilaya na halmashauri za mkoa wa Manyara wanapaswa kwenda Kiteto ili wakajifunze namna ya kusimamia miradi yao ya maendeleo. 

"Ukifika Kiteto unakuta miradi bora yenye kiwango ambayo imejengwa kwa fedha pungufu na huwezi kuacha kuizindua kama baadhi ya maeneo ambapo nimepita na kukuta uchakachuaji," alisema Mnyeti. 

Alisema amefika Kiteto ameshuhudia ujenzi wa baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo madarasa ambapo wamepatiwa fedha za ujenzi wa madarasa matatu lakini wao kwa fedha hizo hizo wamejenga madarasa manne yenye ubora. 

"Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wengine waliopo katika mkoa wa Manyara wanapaswa kuja Kiteto kuiga maendeleo mazuri yanayofanyika hapa," alisema Mnyeti. 

Mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa alishukuru kwa pongezi hizo na kuahidi hawatarudi nyuma katika kuhakikisha wanasimamia maendeleo kwa manufaa ya wananchi. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Tamim Kambona alisema lengo lao ni kuhakikisha miradi ya maendeleo inasimamiwa ipasavyo ili mwisho wa siku mwananchi afaidike. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Alexander Pastory Mnyeti, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kiteto katika Mji mdogo wa Kibaya. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mhandisi Tumaini Chaula akimsikiliza Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayaya Kiteto, Tamimu Kambona akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti. 

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAMSHUKURU RAIS DKT MAGUFULI KWA KUDUMISHA MAWAZO YA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania – TRC pamoja na ‘Clouds Media Group’ (CMG) wameadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya safari ya kihistoria kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kwa kutumia treni ya Deluxe kwa lengo la kuenzi mawazo ya Baba wa taifa ya kuhamasisha watanzania kuhamia makao makuu ya nchi jijini Dodoma kwa kutumia usafiri wa treni hivi karibuni, Oktoba 2019.

Katika safari hiyo Menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa  iliungana na timu kutoka ‘Cloud Media Group’, timu ya Tigo Fiesta pamoja na wasanii zaidi ya 200 kuelekea Dodoma kuadhimisha miaka 20 ya Baba wa Taifa lakini pia kutoa burudani na hamasa kwa  wananchi wa mkoa wa Dodoma.

Licha ya kujionea Vivutio kibao vya nchi yetu ikiwemo maajabu ya mto Ruvu kwenye Safari ya kihistoria kati ya CMG na TRC, timu ya Tigo Fiesta 2019 imefanikiwa kujionea utendaji kazi wa wakandarasi waliopewa dhamana na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kujenga Reli ya Kisasa – SGR kuanzia Dar e Salaam hadi Makutupora mkoani Singida ambapo wasanii walitembelea Kilosa katika eneo ambalo handaki refu zaidi nchini linajengwa.

Katika safari hii ya kuadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, TRC na  CMG walihakikisha uwepo wa Mwl. Nyerere ndani ya treni ambapo vitu kadhaa ambavyo vilipendwa na Baba wa Taifa vilienziwa ikiwemo mchezo wa Bao ambao alikuwa akiupenda, hotuba zake pamoja na vyakula pendwa vya Mwl. Nyerere navyo vilipikwa katika safari hiyo.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli alionekana akifurahia mchezo wa Bao na baadhi ya wafanyakazi wa CMG, naye ACP S.K Kulyamo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Reli pia ni moja kati ya watu ambao siku ya leo alikuwa kwenye safari ya treni kutoka Dar mpaka Dodoma kuhakikisha usalama wa wasafiri, kubwa ni kuweza kuandika historia kwa kumuenzi Baba wa taifa na kuweza kukumbuka kifo cha Baba wa Taifa ndani ya treni ikiwa ni miaka 20 toka atangulie mbele za haki.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa mapinduzi makubwa yaliyofanyika katika kipindi kifupi pia amefurahi kuona wasanii wengi wameingia Dodoma kwa kutumia usafiri wa treni na anaamini kwamba wasanii wamefurahi, wamejifunza mengi na watakuwa mabalozi wazuri kuhusu usafiri wa reli pamoja na Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa kwa niaba ya Shirika amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kudumisha mawazo ya Mwalimu kwa kuhamisha serikali mjini Dodoma na kuboresha miundombinu ya reli ambayo ndio msingi mkuu wa usafirishaji nchini, pia amewashukuru Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi, timu ya CMG na wasanii kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 20 ya Baba wa Taifa na amesema kuwa ana imani kwamba safari hiyo iimesaidia kutunza historia kuhusu maisha ya Baba wa taifa. 

UKARABATI MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA WAENDELEA KWA KASI

$
0
0

Ukarabati wa Meli ya Mv.Victoria na Mv Butiama katika Ziwa Victoria unaendelea kwa kufunga vifaa vipya na Vyakisasa,Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na makandarasi anayefanya ukarabati wa meli hizo,na kusema kuwa kwasasa wanaendelea na kazi ya kufunga genereta mpya na kupaka rangi.

 

 
Taarifa Zaidi.


Ukarabati unaofanywa na kampuni ya KTMI ya Korea Kusini  kwa kushirikiana  Kampuni ya Songoro Marine ya Tanzania unaendelea kwa kufunga vifaa vipya na vya kisasa ili meli hizo ziweze kutoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria..

Mkurugenzi anayesimamia Miundombinu ya Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Thomasi Ngulika amesema kuwa ukarabati wa meli hizo umefikia asilimia Hamsini na kazi hiyo ni yamiezi kumi na Mbili..

Nae Meneja Mradi wa kampuni ya KTMI  kutoka Korea Kusini Chang Hwan  Lee amesema kuwa mradi huo utakamilika mapema mwezi wa tatu mwaka 2020.

Baadhi ya vijana wanofanyakazi katika meli hiyo akiwemo kijana Raymond Msuya ambaye anafanya kazi katika ukarabati wa meli ya Mv Victoria,wameiomba Serikali kuwapatia Ajira ya kudumu kwani wamepata elimu ya kukarabati meli kutoka kwa wakorea ambao wanafanya nao kazi.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI VIONGOZI MBALIMBALI


MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MKOA WA PWANI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mwongozo wa uwekezaji Mkoani Pwani baada ya kuuzindua katika Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani alilolifungua kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mjini Kibaha, Oktoba 19, 2019. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angela Kairuki na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mwongozo wa uwekezaji Mkoani Pwani katika Kongamano la Uwekezaji Mkoani Pwani alilolifungua kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mjini Kibaha, Oktoba 19, 2019. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angela Kairuki na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani kwenye ukumbi wa Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha, Oktoba 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo wakitazama malighafi ya Pazolana inayotumika kutengeneza Saruji wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la kampuni ya saruji ya Tanga katika Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lililofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha, Oktoba 19, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji), Angela Kairuki na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mhandisi Benedict Lema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Elibariki Parsalam kuhusu utengenezaji wa chakula cha kuku wakati alipotembelea banda la kampuni ya Hill Feeds katika Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani alilolifungua kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Oktoba 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani mjini Kibaha, Oktoba 19, 2019
………………….

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo lake la kuandaa makongamano ya uwekezaji ihakikishe inafanya hivyo mara moja.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Oktoba 19, 2019) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa mkoa wa Pwani kwa kutekeleza agizo nililolitoa Juni 18, 2018 wakati wa kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi la kuhakikisha mikoa yote inaandaa kongamano la uwekezaji na inakuwa na mwongozo wa uwekezaji wa mkoa. Mikoa ambayo haijatekeleza agizo hilo, ifanye hivyo mara moja,” amesema.

Waziri Mkuu amesema mkoa huo umeweza kubaini fursa zilizopo katika mkoa wa Pwani na kuzitangaza kupitia mwongozo wa uwekezaji ambao pia ameuzindua leo.

Amesema kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo: ‘‘Ijenge Tanzania, wekeza Pwani mahali sahihi kwa uwekezaji (Build Tanzania, Invest in Pwani, the Best Place for Investment)” ina maana kuwa, licha ya mkoa wa Pwani kubainisha na kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo, unajipambanua vizuri na kuonyesha kuwa ni kwa namna gani umejiandaa na umetengeneza mazingira bora yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje.

“Ili kudhihirisha dhamira ya dhati ya kukuza uchumi kupitia viwanda, nimeelezwa kuwa mkoa umetenga hekta 53,016 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambavyo vitatumia rasilmali zilizopo ndani ya mkoa na maeneo mengine ya nchi kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wanachi,” amesema. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanasimamia miundombinu inayoelekea kwenye viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao.

“Kila mmoja ahakikishe maji, umeme na barabara vinafika kila eneo ambalo mwekezaji anataka kujenga kiwanda. Nitumie fursa hii kuwaomba mlete mabadiliko chanya yanayotokana na maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano.” 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Bibi Angella Kairuki alisema kwamba Serikali imeanza kutekeleza mapendekezo ya mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Improving Business Environment Regulatory Licensing in Tanzania) kwa kuondoa tozo 163 zilizokuwa zikilalamikiwa na wawekezaji.

“Pia tumetenganisha majukumu ya TBS ya TFDA ambayo sasa ni TMDA. TBS itashughulika na vyakula na TMDA itashughulika na dawa na vifaatiba. Vilevile, tumeondoa ada za usajili sehemu za kazi ambazo zamani ilikuwa ni sh. 28,000 na sasa hivi zinatolewa bure,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikillo aliwataka watu wote wanaotaka kuwekeza nchini waufikirie kwanza mkoa wa Pwani kwa sasabu uko kimkakati na una fursa nyingi ikiwemo hali nzuri ya usalama na kwa maana hiyo mitaji yao italindwa.

“Mkoa wetu uko kwenye eneo la kimkakati la kuwezesha biashara kwa kuwa uko karibu na bandari ya Dar es Salaam na uwanja wa ndege; uko karibu na soko kubwa ambalo ni Dar es Salaam; unapitiwa na reli zote kwenda mikoani na nchi jirani; unapitiwa na barabara kuu itokayo Dar es Salaam na pia una bandari kavu ya Kwala.”

Mbali ya hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema faida nyingine ambayo mkoa huo unayo ni uwepo wa miundombinu ya maji, umeme na nishati ya gesi asilia ambayo imeanza kutumiwa na baadhi ya viwanda kama Goodwill na Lodhia Steel.

Naye Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi ya Kijamii (ESRF) ambayo ilisimamia uandaaji wa mwongozo wa uwekezaji kwa mkoa wa Pwani, alisema taasisi yao inasaidia kuandaa na kuchambua fursa zilizopo kwenye mikoa mbalimbali. “Hadi sasa tumekwishaisadia mikoa 17 kuandaa miongozo ya uwekezaji na kwa sasa mikoa 12 imeshakamilisha na mikoa mitano iko kwenye hatua mbalimbali,” alisema.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela ambao ni wadhamini wakuu, Afisa Mkuu wa Biashara, Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema benki hiyo imeendelea kugusa sekta zote za uchumi na hivyo kuongeza tija kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji.

Alisema huduma zao zimelenga kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya viwanda nchini ikiwemo utoaji wa mikopo ya biashara kwa ajili ya kuongeza mikopo ya uendeshaji (working capita loans) na mikopo ya uwekezaji (investment loans).

“Benki yetu inatoa mikopo ya biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo mikopo ya kilimo ni shilingi bilioni 357, uzalishaji wa viwanda (shilingi bilioni 214), biashara (shilingi bilioni 347), mahoteli (shilingi bilioni 87) na sekta ya madini (shilingi bilioni 91),” alisema.

MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO WA AALCO NCHINI TANZANIA

$
0
0


Eric Msuya – MAELEZO

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatarajia kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) utako anza Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo pamoja na Masharika mbalimbali ya Kitaifa.

“Mkutano huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na Viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe. Mahiga

Mkutano huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria za Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili Mataifa Wanachama na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hizo ili kuwa na Dunia yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

Sambamba na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa Sheria ya Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Amani, Matumizi ya Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya Kimataifa.

Tanzania ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation (AALCO) mwaka 1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika

“Kwa mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika mkutano huu … Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi, mafaniko ni mengi na maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata katika chama hiki” Amesema Mhe. Mahiga

Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The Asian-African Legal Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung, Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).

Wazazi mkoani Mwanza watakiwa kuwapeleka watoto kupata chanjo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano kwenye Vituo vya Afya kupata chanjo bure hidi ya magonjwa ya Surua, Rubella na Polio kuanzia tarehe 17-21 Oktoba 2019.

Kwa Mkoa Mwanza, zaidi ya watoto laki sita (watoto 637,579) wanatarajiwa kupewa chanjo ya Rubella na Polio huku watakaopewa chanjo ya Surua wakitarajiwa kuwa zaidi ya elfu sitini (watoto 266,140) hivyo kufanya jumla ya watoto wanaotarajiwa kuchanjwa kuwa laki tisa elfu tatu  mia saba kumi na tisa (watoto 903,719). Kitaifa uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika mkoani Morogoro, Oktoba 17, 2019.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Surua, Rubella na Polio.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akitoa salamu za Wizara kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo mkoani Mwanza.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AFANYA UKAGUZI GEREZA LINDI NA KINGURUNGUNDWA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akikagua Bustani ya Gereza Kingurungundwa alipotembelea jana Oktoba 18, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto)akikagua mifuko ya saruji ambayo imenunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Jeshi hilo sambamba na ujenzi wa Ofisi ya Magereza Mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, ACP. Josephine Semwenda.
Mradi wa tofali za “interlock” katika gereza la Lindi. Tofali hizo zinatumika katika ujenzi wa nyumba za Maafisa na Askari katika gereza hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais kuhusu kutatua tatizo la nyumba za watumishi wa Jeshi hilo kwa kutumia wafungwa pamoja na fursa zilizopo.







Msafara wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, ukipita katika Gadi maalum ya heshima iliyoandaliwa na askari wa Jeshi hilo alipofanya ziara yake ya kikazi katika Magereza mawili ya Mkoa wa Lindi, jana Oktoba 18, 2019 kabla ya kurejea jijini Dar e salaam kuendelea na majukumu mengine ya Kitaifa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Gereza Lindi, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Leonard Chintowa alipowasili jana Oktoba 18, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza Kingurungundwa(waliosimama)alipotembelea gereza hilo jana Oktoba 18, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, ACP. Josephine Semwenda na kulia aliyeketi ni Mkuu wa Gereza hilo SP. Eden Bilalo (Picha zote na Jeshi la Magereza).

SIMIYU KUANZISHA MFUMO WA UKUSANYAJI, UTUNZAJI TAKWIMU ZA WAKULIMA WA PAMBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.Oktoba 18, 2019.
Baadhi ya wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za Chama, wakati wa uuzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.

……………….

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkoa wa Simiyu umeanzisha mfumo rasmi wa ukusanyaji takwimu na utunzaji wa kumbukumbu za wakulima wa pamba uitwao ‘Kilimo Maendeleo’ utakaowawezesha wakulima kusajiliwa katika Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS), kuuza pamba yao kwa njia ya mtandao na kupata pembejeo zote kutoka kwa wauzaji wa pembejeo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo juu ya mfumo huo, Meneja wa huduma za ugani kutoka GATSBY AFRICA, Bw. Sunday Mtaki amesema Mfumo huo utaanza kutekelezwa katika AMCOS 24 zilizoteuliwa kwa kuanzia.

“Katika utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano ya mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, eneo la usajili wa wakulima na matumizi ya TEHAMA kwenye kilimo ni muhimu sana, tumeileta kampuni inaitwa LITENGA ambayo ina mtandao unaitwa Kilimo Maendeleo kazi yake ni kuwaunganisha wakulima kupitia AMCOS na taarifa zote za mkulima zitapatikana kupitia simu za mkononi,” alisema Mtaki.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa kilimo cha zao la pamba ulioandaliwa na Mkoa kwa kushirikiana na wadau, kwa lengo la kuboresha kilimo cha pamba, huku akiwataka Maafisa Kilimo na Maafisa ushirika kutimiza wajibu wao.

“Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika timizeni wajibu wenu msisubiri mgombane na mtu hii kazi ndiyo inayowapa heshima, Serikali ya Rais Magufuli imeweka mkakati wa kuhakikisha zao la pamba linakuwa zao muhimili kwenye nchi yetu, ndiyo maana sisi kama Mkoa tumeanza utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano wa kilimo cha zao la pamba,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ameongeza kuwa dhamira ya mkoa ni kufanya mapinduzi katika kilimo cha pamba ili wakulima walime kilimo cha kisasa chenye tija na kuwa na ushirika imara, ambapo amesema viongozi wa AMCOS wasio waaminifu watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Charles Madata amewaonya viongozi wa AMCOS kuwa waaminifu na kuhakikisha kila mmoja anakuwa na nidhamu ya fedha ili mali za wakulima ziweze kuwa salama.

Kwa upande wake Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu amesema viongozi wote wasio waaminifu watachukuliwa hatua, ambapo amebainisha kuwa takribani viongozi 107 wa AMCOS wilayani Maswa waliohusika na ubadhilifu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema kupitia mkakati wa miaka mitano ya mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, mkoa wa huo unatarajia kuongeza tija ya uzalishaji wa pamba kutoka kilo 200 kwa ekari hadi kufikia kilo 600 hadi 1000 au zaidi kwa ekari.
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live




Latest Images