Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi yako lafana Sumbawanga

0
0

Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Joriii akiitawala jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia laeo
Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga

Msanii wa bongoflava Jay Melody akiwa jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo mjini Sumbawanga
Msanii Badest akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta sumbawanga jana
Mtangazaji wa kipindi cha Double XXL kinachorushwa na radio ya crouds fm ambaye alikuwa moja washereheshaji katika tamasha la Tigo Fiesta Sumbawanga akiwa na wapenzi wa kipndi hicho kutoka Sumbawanga
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiburudika na mziki katika jukwaa la Tigo Fiesta.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiwa na mtangazaji wa Double XXL katika jukwaa la Tigo Fiesta mwisho wa wiki .
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akimtambulisha mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini mh Aeshi Hilaly na kuchemza muziki jukwaani usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
Mbunge wa Sumbawanga mjini akiongea na wananchi walio hudhulia kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga.
Msanii Marioo akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
Msanii wa muziki wa injili Goodluck Gozbeth akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
Msanii wa bongo fleva Joh Makini akiwa jukwaani akitumbuiza kwenye Tigo Fiest 2019 sumbawanga usiku wa kuamkia leo
Msanii Mr Blue akitumbuIza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
Maelfu ya wapenda burudani wa mkoa wa Rukwa na Mikoa ya karibu wakifurahia burudani mbali mbali zinazotolewa katika jukwaa la Tigo Fiesta saizi yako Mjini Sumbawanga

VOA Swahili: Miaka 20 yatimia tangu Mwalimu Nyerere afariki dunia

VOA Swahili: Duniani Leo October 14, 2019

TAIFA STARS YAWALAZIMISHA SARE RWANDA NYUMBANI KWAO

0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameilazimisha suluhu  ya 0-0 timu ya Taifa ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Nchini Rwanda.

Mchezo huo wa Kirafiki wa Kalenda ya FIFA ulizikutanisha timu hizo Ambapo kila mmoja kushindwa kuona lango la mwenzake.Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa, timu zote mbili zikisaka ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya viwango vya FIFA.

Rwanda waliokuwa nyumbani, walionesha uhai mkubwa katika kulisakama lango la Tanzania ila umahiri wa golikipa Metacha Mnata uliweza kuhakikisha lango lake linakuwa salama.

Uwepo wa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika safu ya ushambuliaji ya Rwanda ulikua ni mwiba mkali, ila mpaka dakika tisini zimekamilika kwa timu zote kutoka sare ya 0-0.

Wachezaji hao Meddie Kagere, Patrick Sibomana na Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa anacheza As Kigali ambapo kabla ya kwenda huko alicheza timu ya Yanga na Simba.Kocha msaidizi wa Stars, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji walipambana kupata matokeo ila bahati haikuwa yao.

Matola amesema wachezaji wake walicheza vizuri katika dakika zote 90 wameonesha kiwango kizuri, ila mpira una matokeo matatu kupata sare sio jambo baya ila kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa Sudan wa kufuzu kwenda CHAN.

Stars watashuka tena dimbani kucheza dhidi ya Sudan mchezo unaotarajiwa kuwa wa kufa na kupona ambapo Tanzania wanatakiwa wapate ushindi wa goli 2-0 ugenini baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kupoteza kwa goli 1-0.

WASANII WAASWA KUJITAMBUA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII,

0
0

Charles James, Michuzi TV

WASANII mkoani Dodoma wametakiwa kutambua thamani yao, kuwa na nidhamu na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufanikiwa kwenye safari yao ya kisanii kuanzia ndani mpaka nje ya Nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi wakati akizindua rasmi mchakato wa Tuzo za Nyambago ambazo zimekua zikitolewa kwa wasanii wa Kanda ya Kati.

Amesema Mkoa wa Dodoma una kipaji vingi sana lakini vinashindwa kuonekana Kitaifa kutokana na kukosekana kwa ushirikiano baina ya wasanii wenyewe kwa wenyewe, vyombo vya habari na wadau Kwa ujumla.

" Mkoa wa Dodoma una wasanii wazuri na wenye vipaji pengine kuwashinda hata ambao wameshatoka, muhimu ni kuongeza juhudi katika kazi, ushirikiano na nidhamu.

Wasanii wote wakubwa mnaowaona wamefanikiwa kwa sababu ya nidhamu na kujituma. Niwaombe mshirikiane wote hasa ndugu zetu wa Media tunaomba sana muwe msaada kwa vijana wetu hawa maana wakifanikiwa yanakua ni mafanikio yetu wote kama Mkoa," Amesema.

Akizungumzia Tuzo hizo DC Katambi amewapongeza waandaji wa Tuzo hizo kwa namna ambavyo wameendelea kujitoa kusapoti kazi kubwa inayofanywa na wasanii wa Kanda ya Kati kwani zimekua msaada wa kuwainua na kuwatambulisha zaidi kwenye sanaa.

Amesema kama wasanii wa Dodoma watatumia vizuri jukwaa la Tuzo za Nyambago wataonekana na kukua kisanii kwa haraka zaidi.

" Hizi tuzo ni kubwa ndugu zangu, kwa muda mrefu kumekua hakuna tuzo za Sanaa hapa nchini, nyie Nyambago mmeonesha uthubutu mkubwa. Hongereni na niwaambie Serikali yetu inathamini sana michezo na sanaa tutaendelea kuwaunga mkono.

" Leo siku ya uzinduzi mmenipa ugeni rasmi lakini nataka siku yenyewe ya Tukio mgeni rasmi aje mwingine lazima Wizara itambue hiki kitu kikubwa mnachokifanya kwenye sanaa yetu. Suala la mgeni rasmi siku ya kilele chenyewe niachieni mimi nitamleta," Amesema DC Katambi.

Aidha amewataka wasanii hao kutumia sanaa zao kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye daftari la orodha ya wapiga kura waweze kujiandikisha ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka ifikapo Novemba 24 mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tuzo hizo, Anna Kimpa amemshukuru DC Katambi kwa kuendelea kuwa karibu nao toka walivyoanzisha Tuzo hizo ikiwa sasa ni mwaka wa pili na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwaunga mkono.

Amesema Tuzo hizo zitafanyika Desemba 13 na zinashirikisha wasanii wa fani mbalimbali, wapiga picha, washereheshaji wa masherehe pamoja na watangazaji wa Radio lengo likiwa ni kuongeza ushindani na kukuza tasnia hizo Kanda ya Kati.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akizungumza na wasanii wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa Tuzo za Nyambago zinazotolewa kwa wasanii wa Kanda ya Kati. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tuzo hizo, Anna Kimpa.
 Mwenyekiti wa Tuzo za Nyambago zinazoshirikisha wasanii kutoka Kanda ya Kati, Anna Kimpa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo.

 Wasanii na Wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Tuzo za Nyambago ambazo hutolewa kwa wasanii kutoka Kanda ya Kati

WAZIRI LUKUVI AWATAKA WAKAZI WA JIMBO LA ISMANI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0
0

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani akiwa anajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura katika kituo cha Msindi kilichopo katika kijiji cha Idodi kata ya Idodi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani akiwa yupo kwenye mstari kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani  amewataka wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa siku tatu ambazo zimebakia kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 24-11-2019 na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati ukifika.

Akizungumza wakati alipokuwa anajiandikisha kwenye daftari za mpiga kura katika kituo cha Msindi kilichopo katika kijiji cha Idodi kata ya Idodi, lukuvi alisema kuwa kila mkazi wa jimbo la Ismani wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.

“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema lukuvi

Aidha lukuvi aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha,kupiga kura na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.

Lukuvi aliupongeza uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kuhamasisisha vilivyo zoezi hili la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura na kufanikiwa kuongoza kitaifa.

Nao baadhi ya wakazi wa jimbo la Ismani waliojitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura walimpongeza mbunge huyo kwa kujitokeza na kupanga kwenye mstari kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari hilo la mpiga kura.

OSHA YAPONGEZWA KWA KUONDOA URASIMU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA)  kwa kubadili mfumo wa utendeji kazi wake na kuondoa urasimu wa utendaji kazi, kwani urasimu hupelekea shughuli nyingi kukwama kupelekea wawekezaji wengi kukimbia nchini kutokana na vikwazo. 

Mwaisumbe aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, amesema hayo jiji Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF, amesema juhudi za kupunguza tozo kumeisaidia OSHA kuweza kuwafikia Wawekezaji wengi zaidi na hivyo suala la Usalama na Afya Mahali Pa kazi kuanza kutekelezwa na kuzingatiwa  na Waajiri wengi hapa nchi.

“Nimefarajika kusikia kwamba, mmeendelea kuboresha huduma zenu, hilo ni jambo jema. Waajiri wengi nchini hawatapendi kuona urasimu, wengi wao wawekezaji wakiona kuna urasimu huondoka na kutafuta sehemu zingine ili waweze kuwekeza” amesema Mhe. Mwaisumbe .

Mhe. Mwaisumbe amesema juhudi hizi ambazo zimefanywa na OSHA zimekuja kipindi kizuri hasa kipindi hiki nchi inapotekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Miradi ya Umeme, Ujenzi wa Barabara, Madaraja, ambapo watu wengi huajiri.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo watumishi wa Umma kwa lengo la kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi. Amesema Wakala unaendelea kuboresha huduma zake, hivyo mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wakaguzi wawapo kazini.

Khadija amesema yakuwa wakati nchi inaendelea kupiga hatua mbalimbali za kiuchumi na mabadiliko mbalimbali ya Kiteknolojia duniani, mafunzo kama haya yatakuwa muafaka, yataenda sambasamba na kuwafunza wakaguzi mbinu mpya za kukabiliana na mabadiliko hayo pamoja na changamoto.

“Wenzetu hawa huko kwao masuala ya usalama na Afya yanazingatiwa na yanapewa kipaumbele, sasa ujuzi ambao wakaguzi wataupata kutoka kwa wataalamu hawa yatasaidida kuboresha utendaji kazi wetu, na mbinu mpya za kuweza kufanikisha zoezi zima la kufanya kaguzi za usalama na Afya,” amesema Bi Mwenda.

Naye, Mjumbe wa Shirika la Workplace Health without Borders (WHWB), Aristides Medard kutoka Tanzania ambao ni Waratibu wa Mafunzo hayo kwa kushirikiana na OSHA kwa upande wa Tanzania amesema lengo kubwa la taasisi hiyo ni kuhakikisha linatoa mafunzo  yanayolenga kuondoa changamoto mbalimbali za usalama na Afya Mahali pa kazi duniani ambazo hujitokeza.

Mafunzo haya ya wiki moja yameandaliwa na OSHA kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wakaguzi wa OSHA pamoja na WCF, namna bora ya kufanya kaguzi, na yanaendeshwa na wakufunzi kutoka CANADA,MAREKANI na UBELGIJI kutoka shirika la kimataifa la Workplace health without Border (WHWB).
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda akizungumza na Wakaguzi wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi hao jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe akizungumza na Wakaguzi kutoka OSHA wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakaguzi hao ambapo amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA).
 Baadhi ya Wakaguzi wa OSHA wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo jijini Arusha.

RC SINGIDA AKUTANA NA MAMA MASHUJAA WA CHAKULA WA OXFAM KATIKA MAONESHO YA CHAKULA

0
0
 Mama Shujaa wa chakula kutoka Shirika la Oxfam, Stella Masulya akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi namna ya anavyohofadhi samaki wake kwa kutumia moshi na anavyoandaa dagaa kwa njia ya asili katika maonesho ya kuadhimisha siku ya chakula duniani yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Singida.
 Dkt.Nchimbi akisaini katika kitabu cha wageni katika banda la Oxfam kwenye maonesho hayo.
 Mama Shujaa wa chakula kutoka Arusha, Elinuru Moses akimuelezea Dkt. Nchimbi umuhimu wa kutumia vyakula asilia na namna ya kuvihifadhi.
 Wakina mama Shujaa wa chakula kutoka mikoa mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya siku ya chakula duniani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
 Dkt.Nchimbi akipokea zawadi ya viazi lishe vinavyozalishwa na wakulima wadogo wadogo kutoka Mbongwe.
 Mama Shujaa wa chakula kutoka mkoani Mtwara akimuuzia vikapu Dkt. Nchimbi alivyotengeneza kama mjasiriamali mdogo ili kukuza kipato cha familia yake.
Mama Shujaa wa chakula, Elinuru Moses akimuelekeza Dkt. Nchimbi umuhimu wa chakula asilia  katika kuboresha afya.

UMOJA WA WANAWAKE WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (UWAMITA) WAZINDULIWA JIJINI DAR E SALAAM

0
0
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (mwenye suti) ambaye alikuwa mgeni maalum akiungana na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) kuonyesha katiba ya umoja wao mara baada ya kufanya uzinduzi  wa umoja huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kushoto). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia) ambaye alikuwa mgeni maalum akisoma katiba kabla ya kukata utepe ikiwa ishara ya kuzindua Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kwa mgeni maalum).
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia) ambaye alikuwa mgeni maalum akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kwa mgeni maalum).
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) wakati wa hafla ya kuzindua Umoja huo iliofanyika katika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWAMITA Bi. Frida Kundy na kutoka kushoto ni Bi. Lilian Patrick na Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba.
Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) wakimsikiliza mgeni maalum wakati wa hafla ya kuzindua Umoja huo iliofanyika katika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akionyesha katiba ya Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) mara baada ya kuzindua umoja huo, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWAMITA Bi. Frida Kundy na kushoto ni Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) Bi. Frida Kundy akizungumza na wanachama wa Umoja huo wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Akina mama wastaafu waliokuwa wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakipiga makofi ambapo mbali na uzinduzi huo, akina mama hao waliagwa rasmi.
Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba akitoa nasaha zake.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akigongeana glasi (Cheers) na viongozi wa UWAMITA na akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akiongoza zoezi la ukataji keki na viongozi wa UWAMITA na akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akilishwa keki na mmoja akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akiwagawia keshi akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) Bi. Frida Kundy akicheza muziki na akinamama waliostaafu wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo akiburudika na akina mama ambao ni wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) mara baada ya umoja huo kuzinduliwa. Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UWAMITA pamoja na akina mama waliostaafu wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa UWAMITA wakifurahi katika picha ya pamoja.
Wanachama wa UWAMITA na viongozi wao wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

DIRA YA DUNIA JUMATATU 14.10.2019

TUSICHANGANYE MADESA

0
0

Picha Hii ilitumika kwa mara ya kwanza April 17,2015  na mtandao wa New times.Picha hii imetumika sana katika kipindi cha vurugu zilizokuwa zikifanyika Afrika kusini mwanzoni mwa Septemba mwaka huu ikilinganishwa na matukio hasa ya vurugu.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KUTOKUJUA sheria sio kinga ya kuvunja sheria, hivyo basi tusichanganye madesa wakati wa matukio mbalimbali yanapotokea duniani kote.

Katika Vurugu za Afrika Kusini zilizoanza mwanzoni mwa septemba, 2019 msanii na mzazi mweza wa msaani wa Bongo freva Nasib Abdul maarufu kama Diamond, Zarina Hassani kwenye akaunti yake ya Instragram aliweka picha iliyounganishwa na kuhusisha picha hiyo na vurugu zilizotokea mwanzoni mwa Septemba mwaka huu nchini Afrika Kusini

Hat hivyo picha hiyo  kwa mara ya kwanza ilipostiwa 17Aprili 2015 saa 12:26 ikiwa na kichwa cha habari  cha Why are South Africans attacking fellow Africans? ambapo picha iliyowekwa ni kipindi cha mwaka 2015 na watu kuchukua kuitumia kwa vurugu za 2019.

Baada ya hapo picha hiyohiyo ililudiwa kupostiwa na mtandao wa 
nehandaradio.com Novemba 2,2017 mwandishi wa aliandika makala kuelezea matatizo ya mapigano ya Afrika kusini.

Hata hivyo habari za uongo zimekuwa kikitamaraki katika mitandao ya kijamii bila kujua chanzo cha picha pamoja na video ambazo hazihusiani na matukio na kuhusisha ma tukio linalokuwa linaendelea kwa kuchochea hisia za hasira za watu kufanya vitendo ambavyo hawakuvitegemea kutokana na picha tuu ambazo haziendani na mazingira husika.

Hata hivyo picha hiyo imeweza kutumika na mitandao mbalimbali kama The new times ilitumika 2015, Zambianobserver.com walitumia Machi, 29,2018, Afrigue.le360.ma walitumia picha hiyohiyo Oktoba 27,2019 wakihusisha picha hiyo na vurugu zilizokuwa zikiendelea Afrika Kusini mwanzoni mwa Septemba Mwaka huu.

Basi sasa kama mtu akiwa anatuma picha kwenye mitandao ya kijamii awe na uhakika na picha anayotuma ili kuondokana na kupunguza kabisa habari za uzushi(Fake News).

Taasisi ya Kipinet kukutanisha wajasiriamali zaidi ya 400

0
0
TAASISI ya Wajasiriamali ya Kipinet imekutana na wajasiriamali 400 kwa ajili kuboresha biashara ili ziweze kuleta tija ya kujikwamua na umasikini  .

Akizungumza na wajasiriamali hao Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Charles Sabiniani amesema kuwa fursa za biashara no nyingi sana hivyo kunahitaji kujitoa katika kufanya biashara.

Amesema kuwa jamii ina mahitaji mengi ambayo kwa wajasiriamali in fursa katika kubuni vitu ambavyo vitasaidia jamii hiyo kuondokana  na ukosefu wa bidhaa.

Sabiniani amesema kuwa Kipinet iko katika kushika bega wasariamali katika kutoa mafunzo ya biashara mbalimbali zikiwemo za ubunifu bidhaa mbalimbali katika kutafuta masoko.

Aidha amesema kuwa wanawake ndio walezi wa familia hivyo ni lazima mjitume katika kupiga vita umasikini ndani ya familia.

"Kipinet tutahakikisha  biashara zinasimama na kuleta mafanikio kutoka wajasiriamali wadogo mpaka wakubwa na taifa kuweza kupata maendeleo kutokana na kodi" amesema Sabiniani.

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kipinet Charles Sabiniani akizungumza na wajasiriamali kwa ajili ya maonesho ya  Biashara yatakayofanyika Novemba 7 hadi 10 katika Hoteli ya Travertine Magomeni Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika mkutano kuhusiana  maandalizi ya maonesho ya biashara.
Wajasirimali wa Taasisi ya  Kipinet  wakipata  maelezo kutoka  kwa  Mkurugenzi  wa Taasisi hiyo  Charles sabiniani kuhusiana na elimu ya vifungashio kuelekea maonyesho ya wajasiriamali yatayofanyika Novemba  7 hadi 10 katika vya Hotel ya Travertine Magomeni jijini Dar es Salaam.

NECTA YA TANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019

NBC yatoa wito kwa wazazi kuwafungulia watoto wao Chanua Akaunti ya NBC

0
0

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imetoa wito kwa wazazi kote nchini kufungua akaunti maalumu ya watoto ya Chanua pamoja na bima ya elimu ya Educare za benki hiyo ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao pindi wawapo hai ama wasipokuwepo.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo,  Benjamin Nkaka katika hafla waliyoiandaa kwa ajili ya watoto wa wateja wao ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.

Mkurugenzi huyo alisema akaunti ya watoto ya Chanua ya NBC pamoja na bima ya elimu ya educare vitamuwezesha mzazi kuanza kuwekeza kidogodogo kwa ajili ya mtoto wake hivyo kuondoa hofu ya watoto kupata elimu  bora pindi  mzazi  anapoondoka duniani.

“Akaunti ya Chanua na bima ya Educare za NBC ni suluhisho la uhakika kwa elimu ya watoto, wakati mzazi awapo duniani,asipokuwepo au atakapotapa ulemavu wa kudumu, nawashauri wazazi kuwafungulia watoto wenu akaunti hii na kuanza kuwekeza pamoja na bima ya educare zote kutoka NBC,” alisema.

Kuhusu hafla hiyo Bwana Nkaka alisema NBC imekuwa na desturi ya kukutana na wateja wao mara kwa mara ikiwa ni moja ya azma yao ya kusogeza huduma zao karibu na wateja wao hivyo licha ya kuwaeleza watoto  walioambata na wazazi wao bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki hususan zinazowalenga watoto, lakini pia watoto walishiriki burudani za aina mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika malezi ya watoto.

“NBC imekuwa ikibadilika siku hadi siku tukitumia njia mbalimbali katika kuwafikia wateja wetu, licha ya kuwa na mtandao mpana wa matawi lakini pia tumeanzisha NBC Kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa kupitia simu yake ya mkononi.

“Lakini hii haitoshi NBC inao mtandao mkubwa wa mawakala wake wakitoa huduma mbalimbali za kibenki nchini kote, lakini hivi karibuni tumeingia ushirika na Shirika la Posta ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zetu za kibenki katika ofisi zote za shirika hilo mahali kote nchini,” aliongeza mkurugenzi hiuyo.

 Ofisa Malipo ya Ndani wa NBC, Suzyo Gwebe Nyirenda akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya watoto waliohudhuria katika hafla hiyo wakichorwa picha ikiwa ni sehemu ya shamra shamra zilizokuwepo katika kuadhimisha moja ya matukio ya mwezi wa huduma kwa wateja ambapo NBC iliandaa sherehe hiyo kwa watoto wa wateja wao.
 Baadhi ya watoto walihudhuria hafla hiyo wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwepo katika siku hiyo ikiwa ni moja ya matukio ya NBC kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
  Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akiwawekea chakula baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki ya NBC, Benjamin Nkaka akizungumza na watoto wa wateja wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa wazazi kuwafungulioa watoto wao akaunti ya Chanua na pia bima ya elimu ya educare ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao wakati wawapo hai ama wasipokuwepo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi yako lafana Sumbawanga

0
0

Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Joriii akiitawala jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia laeo
Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga

Msanii wa bongoflava Jay Melody akiwa jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo mjini Sumbawanga
Msanii Badest akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta sumbawanga jana
Mtangazaji wa kipindi cha Double XXL kinachorushwa na radio ya crouds fm ambaye alikuwa moja washereheshaji katika tamasha la Tigo Fiesta Sumbawanga akiwa na wapenzi wa kipndi hicho kutoka Sumbawanga
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiburudika na mziki katika jukwaa la Tigo Fiesta.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiwa na mtangazaji wa Double XXL katika jukwaa la Tigo Fiesta mwisho wa wiki .
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akimtambulisha mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini mh Aeshi Hilaly na kuchemza muziki jukwaani usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
Mbunge wa Sumbawanga mjini akiongea na wananchi walio hudhulia kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga.
Msanii Marioo akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
Msanii wa muziki wa injili Goodluck Gozbeth akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
Msanii wa bongo fleva Joh Makini akiwa jukwaani akitumbuiza kwenye Tigo Fiest 2019 sumbawanga usiku wa kuamkia leo
Msanii Mr Blue akitumbuIza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
Maelfu ya wapenda burudani wa mkoa wa Rukwa na Mikoa ya karibu wakifurahia burudani mbali mbali zinazotolewa katika jukwaa la Tigo Fiesta saizi yako Mjini Sumbawanga

BENKI YA CRDB YAPELEKA WATEJA 70 KUJIFUNZA MAONYESHO YA BIASHARA CHINA

0
0
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa TWCC, Mwajuma Hamza, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam muda mufupi kabla ya kwenda China katika Maonesho ya Biashara ya Canton. Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara Tanzania (TCCIA) imeandaa ziara ya wateja wake 70 kutembelea hayo.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, akibadilishana mawazo na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Jacqueline Maleko (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi TWCC, Mwajuma Hamza, (katikati).

Kaimu Mkurugenzi TWCC, Mwajuma Hamza (katikati), akibadilishana mawazo na Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe (kulia) na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Jacqueline Maleko (kushoto).
Meneja Uhusiano wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Elizaberth Mgaya (kulia), akisalimiana na wateja wa benki hiyo.
 
 Meneja Uhusiano wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Elizaberth Mgaya (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya safari kwenda China kutembelea maonesho ya biashara ya Canton.
Mfanyabiashara Samweli Mchome, akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa safari yao.
Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Jacqueline Maleko, akizungumzia namna Benki ya CRDB ilivyofanikisha safari yao.
Kaimu Mkurugenzi TWCC, Mwajuma Hamz, akizungumza na waandishi wa habari.
Kaimu Mkurugenzi TWCC, Mwajuma Hamz, akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wafanyabiashara wakikabidhiwa hati za kusafiria.
Viongozi wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) wakiwa katika picha ya pamoja na  wafanyabiashara wanaokwenda kutembelea maonesho ya biashara ya Canton nchini China.

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara Tanzania (TCCIA) imeandaa ziara ya wateja wake 70 kutembelea maonesho ya biashara ya Canton nchini China.

Akizungumza wakati wa kuanza safari hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, amesema ziara hiyo ni sehemu ya mkakati wa Benki ya CRDB katika kuwajengea uwezo wateja wake
wajasiriamali jambo litakalosaidia kuongeza ufanisi katika biashara zao.

“Pamoja na huduma ambazo tumekuwa tukiwapatia ikiwamo mikopo ya uwekezaji na uendeshaji biashara zao, bado tunaona kuna umuhimu kwao kujifunza kwa wenzetu nchi zilizoendelea wanafanyaje ili na wao waweze kuboresha zaidi biashara zao. Ni matarajio yetu watajifunza vitu vingi na sisi tutakuwa nao kuwasaidia kufikia lengo,” alisema Bi. Shambwe.

Pia alizungumzia utayari wa Benki ya CRDB katika kusaidia wajasiriamali nchini Bi. Shambwe alisema mwaka 2005 Benki ya CRDB ilikuwa Benki ya kwanza nchini kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali ambapo mpaka sasa zaidi ya wajasiriamali 30,000 nchini wameweza kunufaika na mikopo kwa ajili ya kuendeleza na kukuza biashara zao.

“Pamoja na dawati la Wajasiriamali tuna madawati maalum kwa ajili ya biashara, tuna dawati la China na India kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara kufanya biashara kwa urahisi zaidi,” aliongezea Bi Shambwe huku akisema kuwa Benki hiyo inatoa fursa za kipekee kwa wakinamama kupitia mikopo ya wakina mama wajasiriamali ijulikanayo kama WAFI.

Naye Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko ambaye pia ni mmoja wa wateja walionufaika na mpango huo wa Benki ya CRDB aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwathamini na kuwajengea wajasiriamali uwezo, huku akiwataka wafanyabiashara wengine katika ziara hiyo kutumia fursa hiyo kujifunza vitu ambavyo vitakwenda kuboresha biashara zao.

Ziara hii inakuja katika kipindi ambacho Benki ya CRDB imezindua kampeni maalum ijulikanayo kama “Ulipo Tupo” ikielezea ni jinsi gani Benki hiyo imejipanga viliyo
kuwahudumia Watanzania katika kila hatua ya maisha yao ili kufikia lengo lakuboresha maisha ya kila Mtanzania.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA KATIKA KITUO CHA POLISI CHA RUANGWA MKOANI LINDI

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu kutoka kwa CPL Zurith baada ya kuwasili katika kituo cha Polisi cha Ruangwa alipopitia akiwa katika ziara ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Joseph Magufuli. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Kituo cha Polisi cha Ruangwa kilichopo mkoani Lindi.( PICHA NA JESHI LA POLISI)
Maafisa na wakaguzi wakimpokea Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro baada ya kuwasili katika kituo cha Polisi cha Ruangwa kilichopo wilayani Ruangwa mkoani Lindi kwaajili ya kusikiliza changamoto za askari wa kituo hicho. (PICHA NA JESHI LA POLISI)

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA CRDB AWAHAMASISHA WAZAZI KUWAFUNGULIA WATOTO AKAUNTI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akimkabidhi cheti Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Helasita, Ibrahim Sylvester Tati ambaye amekuwa kinara katika masomo, wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Amulyke Ngeliama akifuatia na Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Sekondari Helasita, Joseph Sanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amewahamasisha wazazi kuwafungulia watoto wao akaunti kwani husaidia kuwajengea uelewa juu ya masuala ya fedha. Nsekela ameeleza hayo wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Helasita yaliyofanyika wikiendi hii.

Nsekela alisema wazazi wanapaswa kuelewa kuwa pamoja na elimu ambayo watoto wanaipata shule, wanatakiwa kupata elimu na uelewa juu ya masuala ya fedha hususani katika kujiwekea akiba. 

“Hii itawasaidia watoto kujijengea uwezo mkubwa katika masuala ya fedha na kujua namna bora ya kutimiza malengo yake,” alisema Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo ya mfumo wa binadamu kutoka kwa Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari Helasita, Andebwise Mwambaya, wakati alipotembelea kazi mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi hao, wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Nsekela alisema Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya Ulipo Tupo imefanikiwa kubuni akaunti maalum kwa ajili ya watoto yaani “Junior Jumbo” na “Teens Account” pamoja na akaunti ya “Scholar” maalum kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu. “Ni wahakikishie tu, Benki ya CRDB ipo Tayari kuwahudumia,” aliongezea Nsekela.

Akitoa hotuba yake katika mahafali hayo, Nsekela aliupongeza uongozi wa shule ya sekondari Helasita kwa kuweza kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na kuifanya shule hiyo kuwa kinara katika masomo katika wilaya ya temeke.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo ya mfumo wa kompyuta kutoka kwa wafunzi.

Nsekela pia aliwaasa wanafunzi wanaohitimu kuendelea kusoma kwa badii ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho. “Napenda kuwakumbusha vijana wetu mnaohitimu leo kuwa bado safari yenu kimasomo inaendelea kwani tunaimani ya kuwa wote mtafaulu katika daraja la kwanza na kujiunga na kidato cha tano,” alisema Nsekela.

Nsekela alihitimisha kwa kusema kuwa vijana wanapaswa kufahamu kuwa wao ndio wamebeba mstakabali wa Taifa la Tanzania, kwani taifa lina nafasi ya kuwa endelevu likipata watendaji walio na viwango bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Sekondari Helasita, Joseph Sanga wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya Helasita, iliyipo Kijichi jijini Dar es salaam, akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Neema Machali, kupitia mchoro wa shule hiyo.
Picha ya pamoja.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Latest Images