Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA KIJIJI CHA NYUKI KISAKI MKOANI SINGIDA

$
0
0

Mwalimu wa Chuo cha Ufugaji Nyuki cha International Beekeeping Open School & IPPE, Salvatory Millinga (wa pili kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa chuo hicho namna ya kulina asali kutoka kwenye mzinga wakiwa katika mavazi maalumu wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika Kijiji cha Nyuki cha Kisaki mkoani Singida juzi.
Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.


Kiwanda cha kuchakata asali kilichopo katika kijiji hicho cha nyuki.



Mafundi wakichimba shimo la maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakipanga chupa zenye asali kabla ya kupelekwa sokoni.


Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akiweka asali iliyochakatwa kwenye chupa ya nusu lita tayari kwa kuwekwa lebo na kupelekwa sokoni.


Kiemi akiwaonesha waandishi mashine ya kuchakata asali jinsi inavyofanya kazi.


Kiemi akizungumza na mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha ufugaji nyuki kilichopo kwenye kijiji hicho cha nyuki aliyetokea mkoani Ruvuma.
Fundi mkuu wa kutengeneza mizinga ya nyuki akionesha moja ya mizinga ya kisasa ya nyuki ambayo inatengenezwa katika kijiji hicho.
Moja ya bweni la kulala wanafunzi 12 linaloendelea kujengwa katika kijiji hicho cha nyuki.
Mizinga ya nyuki ikiwa katika kijiji hicho cha nyuki.
Baadhi ya magari yanayotoa huduma ya usafiri katika kijiji hicho.
Jengo la ofisi kuu ya kijiji hicho likiendelea kujengwa.
Kiemi akiwaonesha wanahabari shamba la kijiji hicho.
Kiemi akionesha namna ya mizinga ya nyuki inavyotakiwa kuwekwa kwa mpangilio.
Hapa Kiemi akitoka kukagua moja ya ofisi inayojengwa kwenye kijiji hicho.

Mzinga ukiwa umening'inizwa kwenye mti.
Madaraja ya reli ni moja ya kivutio cha utalii kwenye kijiji hicho cha nyuki.
Muonekano wa jengo la Utawala katika kijiji hicho.
Wanafunzi na Mwalimu wa chuo cha ufugaji nyuki katika kijiji hicho Salvatory Millinga (wa pili kushoto) wakionesha uvaaji wa vazi maalumu la kulinia asali.


Na Dotto Mwaibale, Singida

WAFUGAJI wa nyuki nchini wametakiwa kuacha dhana ya kuelewa kuwa nyuki wanamazao mawili tu za asali na nta wakati wanamengine matano yenye thamani kubwa.

Hayo yalisema juzi na Rais wa Umoja wa Vijana wa Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS), Philemon Kiemi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

" Pengine kutokana na uelewa mdogo wa wakufunzi wa ufugaji nyuki ndio uliosababisha wafugaji wa nyuki hapa nchini kubaki na dhana ya kuwa mazao ya asali na nta ndiyo yenye thamani kubwa katika ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Kiemi alisema nyuki wana mazao mengine matano ukiondoa nta na asali yaliyozoeleka na wananchi na wafugaji ambayo yanathamani ndogo sana.

Aliyataja mazao hayo mengine yatokayo na nyuki na bei zake kuwa ni Gundi ambayo bei yake kwa kilo ni sh.150,000, maziwa sh.milioni 4 kwa lita, chamvua sh.300, 000 kwa kilo,supu ya nyuki sh.50,000 kwa lita na sumu ya nyuki sh.400,000 kwa gramu.

Alisema mkulima aliyedhamiria kufuga nyuki kiukweli hawezi kutamani kufanya biashara nyingine kutokana na kipato kikubwa anachoweza kukipata ambapo hata akiuza gunia moja tu la mahindi haliwezi kufikia thamani ya kilo moja ya zao la gundi litokanalo na nyuki.

" Ufugaji nyuki hauhitaji madawa mvua wala gharama yoyote zaidi ya kuwa na mizinga yako lakini kilimo cha mahindi, alizeti na mazao mengine kinahitaji mahitaji mengi kama mbolea, madawa, mvua na mambo mengine yanayo mgharimu mkulima tofauti na ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Akifafanua zaidi Kiemi alisema ana ndoto ya kuwabadilisha asilimia 70 ya wakulima hapa nchini ili wawe wafugaji wa nyuki kwa sababu ufugaji wa nyuki unatunza mazingira, unatoa ajira nyingi na soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi akitolea mfano wa bei ya gunia moja la mahindi na mbuzi mmoja ni sawa na lita moja ya asali ya nyuki wadogo.

Kiemi ambaye ana vijiji vitatu vya nyuki mkoani Singida vyote vikiwa na ekari 7000 ni mfugaji wa nyuki wa kwanza Barani Afrika kwa kuwa na mizinga zaidi ya 13,000 akizidiwa na raia mmoja wa Mexico aitwaye Miel Carlota ambaye wanakampuni ya watu watatu wenye mizinga makundi 50,000 na anamashamba 318 ambapo alisema mpaka ifikapo mwaka 2021 anataka kuwa na mizinga 20,000 na kuwa mfugaji wa nyuki namba moja duniani.

WAFUGAJI NA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WATAKIWA KUUNGA MKONO UUZAJI NG'OMBE KWA KILO

$
0
0
Na woinde shizza Michuzi Tv, Arusha 

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi ABDALLAH ULEGA Amewataka wafugaji na wafanya biashara wa mifugo  kuunga mkono uuzaji ng’ombe kwa kilo na kuondokana na uuzaji mifugo kwa makisio, kwani litaleta thamani kwa mifugo pia maendeleo kwa mfugaji  na tija kwa serikali kuweza kukusanya mapato yake  

Akizungumza na wafugaji pamoja na wafanya biashara wakati akifunga mafunzo ya elimu kwa mfugaji na mfanya biashara juu ya uuzaji ng’ombe kwa kutumia mizani wilayani longido Mkoani Arusha  Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah ulega amesema Minada yote nchi nzima lazima ng’ombe auzwe kwa kilo ili kuwe na kiwango maalumu cha uuzaji wa ng’ombe

 ULEGA   Amesema mfanya biashara yeyote atakaebainika kuhusika  kununua au kuuza mifugo nje ya eneo lilotengwa kwa ajili ya uuzaji na ununuzi wa mifugo [MINADA] watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwaita wahujumu uchumi 

"mtu yeyote mfugaji ambaye atakutwa anauza Mifugo nje ya Mnada tutamchukulia hatua kali na siokulipa faini tu bali tutampeleka Mahakamani na tutamfungulia kesi ya uhujumu uchumi "alisema Ulega

ULEGA Akiwa katika moja ya viwanda vya kusindika maziwa kijulikanacho kwa jina la Kilimanjaro Freshi  Amesema ameridhishwa na uendeshaji wa kiwanda hicho kwa kununua maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo na kuanzisha kitengo maalumu cha   kutoa  elimu kwa wafugaji  jinsi gani ya kuweza kuwapa chakula bora ili waweze kutoa maziwa ya kutosha

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido Jumaa Muhina Aliwataka wafugaji hao  kuachana na dhana yakufuga Mifugo mingi ambayo awanatija badala yake wafuge mifugo michache yenye tija

"nibora mfuge Mifugo mitatu au miwili yenye tija kuliko kufuga lundo la Mifugo ambayo aina faida yeyote, unakuta mtu anamifugo rundo na mungine ana mmoja lakini unakuta ukipima kwenye mizani unakuta uzito nisawa sasa sasahivi fugeni mifugo michache yenye tija "Alisema Muhina

Mmoja wa Mfugaji huyo aliyetambulika kwa jina la  Olisienda Sadalla alishukuru kwa mafunzo aliyoyapata na kuhaidi kuwa watafuata sheria na kanuni zote zinazotakiwa na serikali ili wasiingie kwenye matatizo. 
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji na wafanya biashara wa wilaya ya Longido (hawapo Pichani) wakati alipokuwa Kufuga mafunzo ya siku moja walikuwa wakifanya katika ukumbi wa St. Theresia uliopo Namanga mkoani Arusha, ambapo aliwataka wafugaji hao kutotorosha mifugo na kwenda kuuza nje ya nchi badala yake wafaate sheria na kanuni huku akibainisha kuwa atakae Kusuka hatua kali itachukuliwa dhidi yake ikiwepokufugwa(picha na woinde shizza, Arusha). 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja maziwawyanatengenezwa na kamanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na Woinde shizza ,Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda  cha  KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea  kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la  Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Woinde shizza, Arusha). 

WAZIRI HASUNGA AVIAGIZA VYAMA VYA USHIRIKA KUSHIRIKI KATIKA UNUNUZI WA MBOLEA KWA PAMOJA (BPS)

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera wakikagua ghala la mbolea kujionea kiasi kilichopo katika ghala la Tarimo lililopo Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 13 Octoba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akitoa tathmini ya hali ya uzalishaji wa chakula katika mkoa huo kadhalika kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea wakati wa maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera wakikagua mabehewa ya kubeba mazao mbalimbali kwa ajili ya kuyasafirisha katika kituo cha reli Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 13 Octoba 2019.

Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania Dkt Steven Ngailo akitoa taarifa kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea wakati wa maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Katavi

Kutokana na kuwepo kwa mfumo wa ununzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) serikali imeviagiza Vyama vya ushirika vya msingi (AMCOs) na vyama vikuu (FCU) kuanza kushiriki kwenye ununzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) ili kuhakikisha upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika leo tarehe 13 Octoba 2019 katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Amesema kuwa ili kuongeza matumizi ya mbolea nchini, Wizara ya kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati na kwa bei nafuu ikiwemo mfumo wa unuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS).

Pia, imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoa elimu kwa njia tofauti kwa lengo la kuongeza uelewa wa umuhimu na kuongeza matumizi ya mbolea nchini hivyo ili tija na uzalishaji viongezeke vyama vya ushirika havina budi kushiriki kwenye ununuzi wa mbolea ili kuwarahisishia wanachama wao ambao ni wakulima kupata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.

Mhe Hasunga ametoa mwito kwa wafanyabiashara wa mbolea kuuza mbolea kwa bei elekezi iliyopangwa na serikali na wazingatia bei hizo kwa mbolea za kupandia (DAP) na kukuzia (UREA) ambazo zinaingizwa nchini kwa mfumo wa Uingizaji wa Mbolea kwa Pamoja yaani Bulk Procurement System BPS.

“Kama mnavyofahamu, Serikali imeendelea kuratibu utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (Tanzania Agriculture Development Bank-TADB), Benki ya Uwekezaji (Tanzania Investment Bank TIB) na Mfuko wa Pembejeo wa Taifa. Hivyo, nitoe wito kwa wakulima wote wa Mkoa wa Katavi na Mikoa mingine kujiunga katika ushirika ili kuweze kutumia fursa zinazotolewa na taasisi hizi ili kujiletea maendeleo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri Hasunga amesema kuwa ili kuwa na matumizi sahihi ya mbolea, ufahamu juu afya ya udongo ni muhimu; hivyo, ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoa taarifa ya afya ya udongo kwa wakulima na wadau wengine ili matumizi ya mbolea yaendane na mahitaji ya zao na udongo husika.

Niwakumbusha wafanyabiashara wakubwa kuwa mbolea zinahitajika zaidi mikoani; hivyo ni wakati muafaka wa kuanza kusambaza mbolea mikoani haraka iwezekanavyo. Pia ni wakati sahihi wa kufungua matawi ya mauzo na maghala mikoani badala ya mbolea nyingi kurundikana kwenye maghala yaliyoko Dar es salaam ambako mahitaji yake ni madogo.

Ameongeza kwa kusema kuwa ili mbolea iweze kuwafikia wakulima kwa wakati, amelitaka shirika la reli Tanzania (TRC) kutoa kipaumbele katika usafirishaji wa mbolea kwa mikoa ya Tabora, kigoma na Katavi huku akiitaka Mamlaka ya udhibiti wa mbolea (TFRA) kuhakikisha inasimamia ubora wa mbolea kuanzia bandarini inapoingia hadi kwa muuzaji anayemuuzia mkulima.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni ‘matumizi sahihi ya mbolea kwa uhakika wa chakula na uchumi wa viwanda’. Ambapo lengo la maadhimisho ya siku ya mbolea duniani nchini Tanzania ni kupata wigo mpana zaidi kwa Wadau kuelezea masuala mbalimbali katika tasnia ya mbolea. 

Masuala hayo ni pamoja na mafaniko ya tasnia ya mbolea nchini, kuwahabarisha wadau wa mbolea hususani wakulima na wafanyabiashara wa mbolea mifumo mbalimbali ya upatikanaji na usambazaji wa mbolea; pia kutoa elimu kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia tasnia ya mbolea.

Siku ya mbolea duniani ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Oktoba, 2016 huko nchini Uingereza. Siku hii ilianzishwa mahsusi kwa lengo la kuhamasisha Wadau wa tasnia ya mbolea duniani kote kutambua jukumu kubwa walilonalo la kuhakikisha kuwa wakulima wanatumia mbolea bora na sahihi ili kuleta mapinduzi ya kijani kwa uhakika wa chakula.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera amesema kuwa tayari serikali imetangaza bei elekezi ya mbolea hivyo wafanyabiashara watakaokiuka na kuanza kuuza kwa bei zaidi ya hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuwanufaisha wakulima kwenye sekta ya kilimo hivyo kukiuka maelekezo ya serikali kwa wafanyabiashara wa mbolea hawana tofauti na wahujumu uchumi.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mazao ya chakula amesema kuwa mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo utahamasisha wakulima kulima mazao mengi kwa tija ili kuongeza uzalishaji utakaoimarisha usalama wa chakula nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Steven Ngailo amesema kuwa mbolea kwa ajili ya kukuzia na kupandia tayari imewasili nchini hivyo wakulima wana fursa mahususi kabisa ya kujitokeza na kuendeleza sekta ya kilimo katika kuongeza uzalishaji wa chakula kwa ajili ya biashara.

Ameitaja kuwa siku ya mbolea Duniani ni kumbukizi ya maadhimisho ya uvumbuzi wa mbolea aina ya Amonia uliofanywa na Bwana Fritz Haber mwaka 1908. Uvumbuzi huo ulichochea mapinduzi ya kijani katika karne ya 20 yaliyowezesha kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao kutokana na matumizi ya mbolea yaliyosaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa janga la njaa na kuleta uhakika wa chakula katika nchi nyingi duniani.

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA NA DC KOROGWE WATEMBELEA ENEO LA MANDERA KUONA MAFURIKO YALIYOSABABISHA BARABARA KUFUNGWA KWA MUDA

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa wametembelea eneo la Mandera linalounganisha wilaya za Korogwe na Handeni na kujionea mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi (aliyesimama mbele kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi alipotembelea kuona athari za mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda, kulia mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa. Octoba 13,2019
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa.(Kulia mbele) akiwapa pole wakazi wa wilaya ya Korogwe pamoja na wananchi wote walioshindwa kuendelea na Safari kutokana na maji kujaa katika eneo hilo la Mandera kushoto mbele ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Hili ndilo eneo la Mandera ambapo daraja lilifungwa kwa muda 
Maji yakiwa yamezidi daraja , ingawa hapa maji yanaonekana kupungua kiasi 
Hali ya mafuriko ilivyokuwa katika eneo la Mandera
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe (wa tatu kutoka kushoto) akimonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi walipotembelea eneo la mafuriko.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akisisitiza jambo walipotembelea eneo la mafuriko.Picha na Fredy Njeje - Korogwe 

NAIBU WAZIRI MABULA AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA ZOEZI LA URASIMISHAJI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa amemshika Mbuzi kabla ya kukabidhi kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya MAGA NDONDO CUP ambapo timu ya Warrious iliibuka mshindi wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya Best kwa mikwaju ya penati 3-1.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa amemshika Mbuzi kabla ya kukabidhi kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya MAGA NDONDO CUP ambapo timu ya Warrious iliibuka mshindi wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya Best kwa mikwaju ya penati 3-1.

…………………….


Na Munir Shemweta, WANMM ILEMELA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi kuchangamkia zoezi la urasimishaji linaloendelea nchini ili waweze kuwa na umiliki halali wa ardhi yao watakayoweza kuitumia kujiletea maendeleo.

Dkt Mabula ambaye ni Mbunge la Ilemela mkoani Mwanza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipozungumza na wananchi wa jimbo lake katika Mtaa wa Kabanganya kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa.

Alisema, Rais wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli ameelekeza maeneo yote yaliyokuwa katika ujenzi holela yarasimishwe kwa kupimwa ili wananchi wake wawe na umiliki halali kwa kuwa walitumia nguvu nyingi wakati wa kuyaendeleza.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupimiwa pekee katika maeneo yaliyorasimishwa hakutoshi na kushauri wananchi kuhakikisha wanapata hati za umiliki ili waweze kuzitumia katika kujipatia mikopo na shughuli nyingine za kimaendeleo.

‘’Wananchi walijenga kwa nguvu zao, serikali haikuwa makini katika kupanga maeneo ili watu wakae katika mpangilio mzuri hivyo Rais aliagiza wananchi warasimishiwe ili waweze kuwezeshwe kiuchumi na kutumia ardhi yao na majengo kuendelea katika shughuli za uchumi na kuweka dhamana na zoezi hili linafanyika kwa miaka kumi na kumalizika 2023’’ alisema Dkt Mabula.

Akizungumzia shughuli za maendeleo katika jimbo lake la Ilemela, Dkt Mabula alisema tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa jimbo hilo amefanya mambo makubwa katika sekta ya elimu kwa kuwezesha ujenzi wa shule za msingi na sekondari sambamba na kuongeza vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule hizo tofauti na miaka ya nyuma.

WASTAAFU WASHAURIWA KUFUGA SAMAKI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kulia) akizungumza alipotembelea banda la ufugaji wa samaki katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida. Wa pili kulia ni Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi mfugaji mkubwa wa samaki mkoani Singida.
 Wafanyakazi wa Mzee Juma Mkhofoi wakiyafanyia usafi mabwawa ya ufugaji wa samaki yanayomilikiwa na mzee huyo.

Mzee Mkhofoi (kulia) akiwa katika banda la kufugia samaki kwenye maonesho hayo. Samaki hao wametoka katika moja ya mabwawa yake.
Mfugaji Mzee Mkhofoi akiangalia kibao cha tarehe aliyopandikiza vifaranga vya samaki katika bwawa hilo.
Mzee Juma Ibrahim Mkhofoi (wa pili kulia) akielekeza wananchi jinsi ya ufugaji samaki katika maonesho hayo.

 Hapa akiwapa samaki chakula.
 Mzee Mkhofoi akitoka kwenye ofisi ya mda iliyopo kwenye mabwawa yake ya samaki.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.
 Usafi kwenye mabwawa hayo ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WASTAAFU wameshauriwa kufuga samaki ili waweze kupata chakula chenye lishe bora na kuinuka kiuchumi badala ya kutegemea fedha za kiinua mgongo pekee.

Wito huo umetolewa na Juma  Ikhofoi mfugaji mkubwa wa samani  mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Uwanja wa Bombadia mjini hapa.

" Niwaombe wastaafu wenzangu wasikae bure na kutegemea kiinua mgongo pekee kuendesha maisha yao bali wafuge samaki kwani watapata kitoweo chenye lishe bora na fedha za kujikimu  " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema gharama za ufugaji wa samaki ni ndogo  na soko lake ni kubwa tofauti na kilimo ambacho kinahitaji mambo mengi.

Aliongeza kuwa mabwawa ya samaki yanaweza kuchimbwa eneo lolote na chakula chao ni pumba ya mpunga na mahindi ambayo haizidi sh. 5000 kwa gunia na udavi ni sh.250,000 ambapo 
samaki kwa bwawa moja kwa siku wanakula kilo moja tu.

Alisema yeye baada ya kustaafu Wizara ya Maji na Umwagiliaji aliamua kuchimba mabwawa 67 kwa ajili ya kufuga samaki ambapo kila bwawa alitumia sh. milioni moja na sasa anafurahia 
ufugaji huo.

Alisema mabwawa hayo aliyachimba mwaka jana na sasa ameanza kupata matunda ya ufugaji huo kwani kuanzia mwaka jana mwishoni hadi mwaka huu mwanzoni ameweza kupata zaidi ya 
sh.milioni sita baada ya kuvua samaki  na kuwauza.

" Nimeanza kupata pesa kwa kuwauza samaki aina ya sato ninaowafuga pamoja na kitoweo chenye lishe ambacho kinakubalika kwa afya tofauti na nyama zingine " alisema Mkhofoi.

Mkhofoi alisema lengo lake ni kuwa na mabwawa zaidi ya 80 na kila wiki awe ana zalisha kilo kuanzia 1000 hadi 2000 na kuwa soko lake kubwa litakuwa hapa hapa mkoani Singida na 
hapendi kuwauzia wafanyabiashara kwa kuwa wanaenda kuwalangua walaji ambao watashindwa kupata chakula chenye lishe bora.

Mkhofoi ametumia fursa hiyo ya maonesho hayo kuwaomba wananchi wa mkoa wa Singida ambao watahitaji kupata mbegu ya samaki hao kwa ajili ya kufuga na kwa  kitoweo  kwa ajili ya 
matumizi ya nyumbani wawasiliane naye kwa namba ya simu 0755 735441 na 0655 735441.

WAZIRI MPINA ASHIRIKI ZOEZI LA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KIJIJINI ISANGIJO,MEATU MKOANI SIMIYU

$
0
0
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Afisa Mwandikishaji Sospeter Mseya.(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia kwenye kituo cha kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019)
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na Waasisi wa Chama cha TANU muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. .(13. 10.2019
 MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Maswa, Constantine Sement Shillingi  (13. 10.2019)
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora watakaoweza kusimamia mipango ya Serikali kwenye vitongoji na vijiji muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Mwamhuge, Kijiji cha  Isangijo Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu (13. 10.2019)

WANAFUNZI UGANDA WAFANYA MDAHALO KUHUSU MWALIMU NYERERE

$
0
0

Sanjari na Mdahalo huo, uongozi mpya wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma vyuo vikuu nchini Uganda walitumia hafla hiyo kuapishwa rasmi kushika madaraka waliyochaguliwa.




Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima (katikati), Mwambata Jeshi, Brig. Gen. Stephen Mkumbo na Afisa anayesimamia masuala ya Utawala Ubalozini wakiwa katika hafla ya Kumbukizi ya Miaka 20 ya Siku ya Mwalimu Nyerere iliyofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda tarehe 13 Oktoba 2019. Hafla hiyo ilifanyika kwa kufanya mdahalo kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere ambapo wanafunzi mbalimbali kutoka Tanzania wanaosoma elimu ya juu nchini Uganda walishiriki mdahalo huo.
Wanafunzi walioshiriki wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zinawasilishwa katika mdahalo huo kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere.
Balozi Mlima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Uganda. 


Uongozi wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Uganda wakiwa katika picha ya pamoja. 












RC SINGIDA AFUNGUA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt.Bedan Masuruli akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi katika banda la wizara hiyo kwenye maonesho hayo.
 Afisa Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mary Yongolo (kushoto) akimpa zawadi ya maziwa Dkt.Rehema Nchimbi baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Tanga Fresh. Kulia ni Kaimu 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mifugo, Dkt. Bedan Masuruli.
 Mtafiti wa Zao la Maharage kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Arusha Edith Kadege akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi kuhusu maharage lishe yaliyofanyiwa utafiti na kituo hicho.
 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)  wa Taasisi ya Promised Eden Environmental care (PEEC) Ascarlyon Lufurano (kushoto) akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi kuhusu kilimo cha mapapai yanayo zalishwa na Taasisi  hiyo.
 Afisa Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Dodoma, Deograsias Ruzangi, akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhusu machapisho mbalimbali yanayohusu kilimo na uvuvi.
 Wanakwaya ya Kanisa la AICT mkoani Singida wakitoa burudani.
 Hafla ya ufunguzi maonesho hayo ikiendelea.
 Hafla ya ufunguzi maonesho hayo ikiendelea.
 Msanii wa muziki wa Sengeli Mzee wa Bwax akipagawisha katika hafla hiyo.
 Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Chima Mbuwa akizungumza katika mkutano huo.
 Taswira ya mkutano huo.
 Wasanii wa kikundi cha Mbaramwezi wakitoa burudani.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Honest Kessy akizungumza.
 Wasanii kutoka Singida Mjini wakitumbuiza.



Afisa Masoko wa Kampuni ya Hughes Agricultural (T) Ltd, Lawrence Kisoka akizungumzia 
ubora wa matrekta aina ya New Holland Agriculture yanayosambazwa na kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mikalu Mapunda akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge waliotembelea banda la NFRA.
Afasa Manunuzi na Ugavi Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge waliotembelea banda la bodi hiyo.


Dotto Mwaibale na Boniphace Jilili Singida. 

HALMASHAURI za mkoa wa Singida zimetakiwa kuviwezesha kupata pembejeo bora za kilimo vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia asilimia kumi zinazotengwa na 
halmashauri kote nchini kwa ajili ya makundi hayo. 

Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakati akifungua rasmi maonesho ya kitaifa Mkoani humo ya maadhimisho ya siku ya Chakula duniani.

Alisema zile asilimia kumi zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya akinamama,vijana na watu wenye ulemavu ni vyema halmashauri zikawatafutia matrekta 
kwa kuwakopesha ili kuinua kwa haraka kipato chao.

Hata hivyo alisema kupitia elimu inayoendelea kutolewa kwenye maonesho hayo viongozi waichukue na kuwapelekea wananchi kwenye maeneo yao,huku akiziagiza halmashauri za wilaya 
za mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya malisho, na kuziagiza kila shule za mkoa huo kutenga nusu hekari ili kulima maharage yatakayo tumika kutengenezea uji wa lishe kwa ajili ya wanafunzi.

Dkt Nchimbi alisema taifa lolote lililo simama imara watu wake wana lishe bora na hivyo ili kufikia uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda ni lazima watu wawe na lishe bora.

Aidha kaimu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Berdan Nasuruli alisema ujumbe wa Wizara ni kutaka raslimali nyingi ilizonazo Tanzania ziwasaidie wananchi kupata lishe bora.

Amesema licha ya Tanzania kuwa ya pili barani afya kwa ufugaji wa ng'ombe lakini watu wake hawatumii maziwa,hivyo viongozi wahimize watu kunywa maziwa na kula Samaki ili kuwa na lishe bora,na maadhimisho hayo yatakuwa na maana endapo watu watabadilika kwa kuanza kutumia vyakula vyenye lishe bora. 

Naye kaimu katibu Mkuu Wizara ya kilimo Honest Kessy alisema maadhimisho hayo ni ya 39 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1981,na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Lishe bora kwa ulimwengu usio na njaa" ambapo mwaka huu kitaifa yanaadhimishwa mkoani hapa.

Kessy aliwataka wananchi wa mkoa huo na wote wanaoweza kufika kwenye maonesho hayo kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo lishe bora ili kuboresha afya zao kwa 
maendeleo yao na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Tanga Fresh Mkoa wa Singida, Alfred Masawe aliwashauri wananchi kutumia Maziwa ya kampuni hiyo ambapo kuna Maziwa fresh, Maziwa mtindi, Loghurt,Cheese pamoja na Unsal



.

KKKT YAIPONGEZA SERIKALI KULETA MAENDELEO NA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA HUDUMAZA KIJAMII NCHINI

$
0
0
Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango akiipongeza Serikali kwa kuleta maendeleo nchini mara baada ya kusimikwa kuwa askofu wa Dayosisi hiyo katika Ibada takatifu iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani)
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na madhehebu mengine wakishiriki ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani)
Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo akimpongeza Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuwaletea watanzania maendeleo, pongezi hizo amezitoa mbele ya waumini wa KKKT na madhehebu mengine wakati wa ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika mjini Njombe.

……………………..

Na James K. Mwanamyoto – Njombe

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeipongeza Serikali kwa kuleta maendeleo katika miundombinu ya barabara, reli na anga, kuhimiza maendeleo ya viwanda ili kuwawezesha watanzania kuuza bidhaa zilizoandaliwa, ikiwa ni pamoja na kutoa uhuru wa kila mtanzania kuabudu. 

Pongezi hizo zimetolewa na Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango mara baada ya kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Ibada Takatifu iliyofanyika jana Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Baba Askofu Dkt. Frederick Shoo.

Askofu Fihavango amesema, Kanisa linaishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Dayosisi yake hususani katika sekta ya afya.

Dayosisi yangu ina ubia na Serikali wa kutoa huduma za afya kupitia Hospitali Teule ya Kilutheri Ilembula iliyopo Wangingombe ambapo kati ya watumishi 182 waliopo, Serikali inalipa mishahara watumishi 110 kupitia mfuko wa ruzuku, amefafanua Dkt. Fihavango.

Askofu Fihavango ameongeza kuwa, Serikali imekuwa ikitoa fedha na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo ili kuwezesha utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi, akitoa mfano katika mwaka wa fedha 2018/19 hospitali imepokea jumla ya shilingi 187,421,791/= na ruzuku ya mishahara ya watumishi kiasi cha shilingi 1,056,168,000/=.

Kama haitoshi, Askofu Fihavango ameeleza kuwa, Serikali imetoa gari la wagonjwa kwa Hospitali ya Kilutheri Ilembula na Kituo cha Afya Kidugala ambalo limesaidia kuboresha huduma za afya hasa za mama na mtoto hivyo inaonyesha dhahiri kuwa kanisa na Serikali ni washirika katika kuleta maendeleo ya taifa.

Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ibada hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametoa pongezi kwa KKKT kwa kushirikiana na Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Mhe. Mkuchika amesema, Serikali inatambua mchango wa kanisa hilo katika kutoa huduma za kiroho, afya, elimu na uchumi bila kubagua wananchi kwa kigezo cha utofauti wa dini, hivyo limekuwa na mchango katika maendeleo ya taifa na kulitaka kuwahimiza waumini wake kutokwepa kulipa kodi ili Serikali ipate fedha za kuendesha shughuli za maendeleo.

“Katika kutoa huduma za afya, Serikali inaendelea kushirikiana na kanisa kutoa huduma hiyo kupitia Hospitali Teule ya Ilembula na Kituo cha Afya Kidugalo na zahanati nyinginezo ambazo ni mali ya KKKT Dayosisi ya Kusini” Mhe. Mkuchika ameongeza.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa Serikali inatoa vifaa tiba na mishahara kwa watumishi wa Hospitali Teule ya Ilembula ambao 110 ni wa kanisa na 37 wa Serikali ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za matibabu.

Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa wito kwa KKKT kuendelea kushirikiana na Serikali katika kushauriana na kudumisha utamaduni wa kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ustawi na maendeleo ya wananchi kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Kwa upande wake, Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo amempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuwaletea watanzania maendeleo katika sekta ya afya, elimu na nishati.

Askofu Dkt. Shoo, pia hakusita kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kurejesha nidhamu ya utendaji kazi katika utumishi wa umma kwani nidhamu ya watumishi wa umma imekuwa ni chachu ya maendeleo katika taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibada ya kumsimika Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini, Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika Njombe, Oktoba 13, 2019.

NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA VIJANA KUJIFUNZA MAISHA YA NYERERE KWA VITENDO

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM BUTIAMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula amewataka vijana kujifunza maisha ya baba wa Taifa Mwalimu Julius kwa vitendo ili matendo ya kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania yaendelee kukumbukwa.
Akiwa katika Maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya Mwl.  Nyerere katika kanisa Katoliki la Bikira Maria jimbo la Musoma Parokia ya Butiama mkoani Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019 Dkt Mabula alisema, ni vyema vijana wa watanzania wakatumia hazina ya wazee kama Mwl Nyerere Julius Nyerere kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo.
"Niwaombe vijana kutumia hazina ya wazee wetu na kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo" alisema Dkt Mabula.
Dkt Mabula ambaye alikuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya Butiama mkoani Mara  alihitimisha salamu zake za miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wilayani Butiama kwa kuwataka wananchi kuishi pia kwa kumcha Mungu kwa kuwa wakati wa uhai wake baba wa taifa aliishi kwa kumcha Mungu. 
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba alimueleza Mwl Nyerere kuwa alikuwa ni mtu wa maisha ya Mungu aliyejitahidi kujenga umoja na mshikamano kwa nchi yake na Bara la Afrika kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula alimuelezea Mwl Nyerere kama mtu aliyepigania haki na aliyesisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja.
Maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere katika kanisa katoliki Parokia ya Butiama mkoani Mara  yalihudhuriwa pia na  Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Steven Wasira, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Sospeter Muhongo,  Chief Wanzagi,  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt Maulid Banyani na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania  Masanja Kadogosa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasha mshumaa katika kaburi la Baba wa Taifa Mawalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo Butiama mkoa wa Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakiwa mbele ya kaburi la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Maadhimisho ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo Butiama mkoa wa Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019. Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba na wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Phillip Mangula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa nje ya Kanisa Katoliki Parokia ya Butiama mara baada ya Misa ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo Butiama mkoa wa Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019. Wa kwanza kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba na wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Phillip Mangula. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Sospeter Muhongo na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)



RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, WIKI YA VIJANA NA KUMBUKIZI YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE MKOANI LINDI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu  Ndugu Mzee Mkongea Ally kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi
leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Jukwaa kuu na viongozi wengine wa kitaifa  sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alizoongoza katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019

 Wabunge wa Lindi na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama "Harmonize" ama "Konde Boy"  kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ama Konde Boy kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
 Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo
Jumatatu Oktoba 14, 2019


 Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo
Jumatatu Oktoba 14, 2019

 Vijana wa Halaiki katika sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu
Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
 Kikundi cha utamaduni cha Dege la Jeshi kikitumbuiza kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14,2019
 Wanewnguaji wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) wakitumbuiza kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
 Msanii wa Kizazi Kipya Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.PICHA NA IKULU

Washindi wa kwanza wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon watangazwa..

$
0
0


Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kansai Plascon (T) Ltd, FloraMapunda,akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi, Robson Majura, mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon .Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha shilingi,!1,000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Jijini Dares Salaam.
Muwakilishi kutoka kampuni ya Plascon Mkoani Mwanza Subodh Issar akimkabidhi Frank Silver mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon .Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha shilingi 1000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni Jijini Mwanza.


Washindi kujishindia zawadi za pesa taslimu 

Dar es Salaam: Promosheni ya Paka Rangi ya Plascon na Ushinde imerejea, na sasa inakuja na toleo maalumu la rangi, maarufu kama Rangi ya Pesa kwa nia njema ili kuwanifaisha wateja wake. Mwaka huu washindi watajishindia na zawadi za pesa taslimu.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Hussein Jamal, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo kipya cha mauzo ya rangi ya Plascon, jijini Dar es Salaam.

Jamal alisema, “Kibiashara tunafurahi kuwa na kampeni kama hii ambapo kupitia katika promosheni yetu , tuna uhakika kwamba, kuwapo na ushindi wa pesa taslimu kutaleta nyuso za furaha kwa washindi katika kipindi chote cha msimu wa kampeni hii.

Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde inatupatia fursa, siyo tu kuwazadia wateja wetu muhimu, watumiaji wa rangi na wauzaji, lakini pia kujenga msingi wa mafanikio ambayo tumeyapata kupitia bidhaa yetu ya hii ya Plascon, tangu tulipoizindua mwaka 2017,”

Kadhalika, Jamal alifafanua kuwa, promosheni hiyo ni ushahidi tosha wa kuonesha jinsi ambavyo Plascon imeamua kutoa huduma kwa watanzania na namna biashara yake inavyolenga kuongeza thamani katika uzalishaji wa rangi bora, zenye viwango, utafiti na wenye lengo la kukidhi haja ya mahitaji ya rangi na kutoa ushauri bora kwa watanzania na watumiaji wa rangi kwa ujumla.

Promosheni iliyopewa jina la ‘Colour of Money’ itaendeshwa kuanzia Otoba 7 hadi Desemba 14, 2019, na inatarajia kushirikisha mamia na maelfu huku kila mshiriki akiwa na uhakika wa kutotoka mikono mitupu .

Meneja Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Tyron Immelmann, alisema kuwa, mwaka huu , Plascon itatoa zawadi za pesa taslimu shilingi milioni tano kila wiki, ambapo kila siku kutakuwa na mshindi wa Sh 1,000,000 taslimu.

Washiriki watatakiwa kununua lita 20 za rangi ya Plascon, na kupewa kadi ambayo mteja ataisugua na na kutuma namba zake za bahati kwenda 15054, baada ya hapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi.

Matangazo ya Msimu huu wa Promosheni ya Paka Rangi Ushinde na Rangi ya Pesa, yatatangazwa kupitia vipeperushi kutoka kwa wauzaji, halikadhalika kupitia katika radio na televisheni.

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA NYERERE DAY,BEIJING NCHINI CHINA

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafuu Mh Mizengo Pinda akizungumza wakati wa siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoadhimishwa leo jijini Beijing katika Chuo Kikuu cha Peking na kuhudhuriwa na viongozi mbalimali wa Serikali,Chama cha Kikomunisti, wanadiplomasia, wanazuoni na wanafunzi.
 Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki akizungumza jambo kwenye Siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoadhimishwa leo jijini Beijing katika Chuo Kikuu cha Peking na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda na viongozi wa Serikali,Chama cha Kikomunisti, wanadiplomasia, wanazuoni na wanafunzi.
Baadhi ya viongozi wa Serikali,Chama cha Kikomunisti, wanadiplomasia, wanazuoni na wanafunzi wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri  leo kwenye siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoadhimishwa jijini Beijing katika Chuo Kikuu cha Peking .
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza jambo  katika siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoadhimishwa leo jijini Beijing katika Chuo Kikuu cha Peking na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda na viongozi wa Serikali,Chama cha Kikomunisti, wanadiplomasia, wanazuoni na wanafunzi.
 
Baadhi ya Wawakilishi kutoka katika Chama cha Kikomunisti cha China wakieleza namna walivyomfahamu Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere,yote hayo yamefanyika leo katika siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoadhimishwa leo jijini Beijing katika Chuo Kikuu cha Peking na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda na viongozi wa Serikali,Chama cha Kikomunisti, wanadiplomasia, wanazuoni na wanafunzi.
 Picha ya pamoja.Picha kwa hisani ya Mdau Phelista Wegessa-Beijing,China.


NYIMBO ZINAZOHIMIZA AMANI, UPENDO ZA KWAYA YA GETHMANE ZAMKOSHA WAZIRI ANGELLA KAIRUKI...ATOA NENO

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki ameipongeza Kwaya ya Gethmane ya Kanisa Wasaabato Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kutunga na kuimba nyimbo za Injili zinazozungumzia umuhimu wa Watanzania kuendelea kudumisha amani,umoja na upendo.

Kairuki ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua DVD mbili za Sikiliza na Petro za Kwaya ya Gethmane ambapo kabla ya kuzizindua alipata nafasi ya kusikiliza nyimbo kadhaa na kukoshwa na aina ya ujumbe uliopo katika nyimbo zao.

"Kwa kweli nimefurahishwa na ujumbe ambao uko kwenye nyimbo za kwaya hii.Ni jambo nzuri kuona na kusikia Watanzania tukihamasishana kudumisha amani, umoja na mshikamano.Kwaya ya Gethmane ambayo sasa inatumiza miaka 10 tangu kuanza kwake kwa kutumia nafasi yao wametambua jukumu hilo na hivyo wametunga nyimbo mahususi kuzungumzia amani ,upendo na mshikamano.

"Hili ni jambo la kupongeza na kutoa rai kwa waimbaji wa nyimbo mbalimbali zikiwemo nyimbo za Injili kuimba nyimbo za kuhamasisha amani na mshikamano. Tunafahamu Oktoba 14 tunaadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.Tunakumbuka alivyosimama imara kusimamia amani na kuwafanya Watanzania kuwa wamoja, ni jukumu letu kumuenzi kwa kukumbusha umuhimu wa kuwa wamoja ,",amesema Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki aliyekuwa mgeni rasmi pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna kila sababu ya Watanzania kuendelea kuheshimu uhuru wa kuabudi kwa kila mtu na dini yake au dhehebu lake na hakuna aliyebora zaidi ya mwingine.

Pia Waziri Kairuki ameongeza Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na watanzania wa kulinda amani iliyopo na wao kama Serikali wataendelea kuilinda amani hiyo kwa gharama yeyote ile. "Ni jambo la muhimu sana kila mtu kuheshimu dini ya mwingine,"amesema.

Wakati huo huo Waziri Kairuki ameongeza harambe ya kuchangia kwaya hiyo kwa ajili ya kuendeleza malengo na mipango ya maendeleo na kuitumia jamii kupitia nyimbo za Injili ambapo fedha na ahadi zaidi ya Sh.milioni 25 zimepatikana kutoka kwa waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa DVD hizo.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa hilo la Wasabato Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Masanya Anthony amesema kuwa Kanisa wanatambua umuhimu wa nchi ya Tanzania kuendelea kuwa yenye amani na hivyo wataendelea kuliombea Taifa na viongozi wake wakati wote.

"Kanisa letu tunalojukumu la kuliombea Taifa na tutaendelea kufanya hivyo siku zote.Waziri Kairuki tunaomba ufikishe salami zetu kwa Rais wetu Dk.John Magufuli na mueleze kuwa Kanisa la Wasabato Kinondoni tunatambua kazi kubwa unavyofanya Rais ya kuijenga nchi yetu.Kwaya yetu pamoja na nyimbo nyingine za injili imeamua kuwa na nyimbo za kuzungumzia amani na kuisifu nchi yetu nzuri,"amesema Mchungaji Anthony.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki(katikati) akiwa ameshika DVD mbili za Petro na Sikiliza baada ya kuzizindua rasmi katika Ukumbu wa Uhuru jijini Dar es Salaam. DVD hizo ni za kwaya ya Gethmane ya Kanisa la Wasabato Mtaa wa Kinondoni .Kulia ni Mchungaji wa Kanisa hilo Masanywa Anthony pamoja na waalikwa wengine wakishuhuhudia uzinduzi huo
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki akijiandaa kuzindia DVD mbili za nyimbo za Injili ambazo ni za Kwaya ya Gethmane ya Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni Dar es Salaam
 Wanakwaya wa Gethsemane kutoka Kanisa la Wasabato Mtaa wa Kinondoni wakiimba  moja ya wimbo wao mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki (hayuko pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa DVD mbili za kwaya hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki akishiriki kuimba na kucheza wimbo wa Injili wa Kanisa Sabato wakati wa uzinduzi wa DVD mbili za kwaya ya Gethmane uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Mmoja ya waalikwa Profesa Philemo  Sarungi(kulia) akisaliamiana na mwalikwa mwingine wakati wa uzinduzi wa DVD mbili za kwaya ya Gethmane uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Moja ya kwaya ya ambao waalikwa kwenye uzinduzi wa DVD mbili za kwaya ya Gethmane wakitumbiza ukumbini kabla ya kufanyika kuzinduliwa rasmi DVD hizo
Wanakwaya wakiwa jukwaaani wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa DVD mbili za Kwaya ya Gethmane ya Kanisa Wasabato Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam

SERIKALI KULIPA MIL 315.1 ZA WAKULIMA WA MUZIA AMCOS MKOANI RUKWA – MHE HASUNGA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo na mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe Julieth Binyura. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Sehemu ya wawakilishi wa Wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitatua kadhia za chama hicho kuhusu kutapeliwa fedha na Mwenyekiti wa chama hicho Ndg Linus Kalandamwazye kiasi cha Shilingi Milioni 315.1 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe Julieth Binyura wakijadili jambo mara baada ya kumalizika kikao kazi kuzungumza na wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa
Sehemu ya wawakilishi wa Wanachama wa Muzia Amcos ya Wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitatua kadhia za chama hicho kuhusu kutapeliwa fedha na Mwenyekiti wa chama hicho Ndg Linus Kalandamwazye kiasi cha Shilingi Milioni 315.1 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.






Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Rukwa

Serikali imetangaza dhamira yake ya kuwalipa wakulima 156 wa mahindi jumla ya Shilingi 315,118,510 kutokana na kuzulumiwa na mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ndg Linus Kalandamwazye.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo jana tarehe 13 Octoba 2019 wakati akizungumza na wanachama wa Muzia Amcos Wilayani Kalambo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.

Malipo hayo yatawahusu wakulima wa Tarafa ya Mwimbi yenye kata nne ambazo ni Mambwe Kenya, Ulumi, Mkombo na Mwazye kutokana na kupima mahindi yao zaidi ya Tani 622.679 kwenye Chama cha Muzia Amcos kilichopewa uwakala na serikali wa kununua mazao kwa wakulima tarehe 8 Agosti 2017 kwa makubaliano ya kulipwa ndani ya wiki tatu kutoka tarehe ya kupimwa lakini hawakulipwa mpaka sasa.

“Kesi ikiwa mahakamani serikali haiwezi kuingilia badala yake wakati tunaendelea na kesi hiyo ninaziagiza taasisi zangu tatu kuchanga fedha kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema wanaotakiwa kuchanga fedha hizo kwanza ni Wizara ya Kilimo kwa kushindwa kulishughulikia jambo hilo kwa wakati ili wakulima hao waweze kulipwa fedha zao.Ameiagiza pia Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuchanga fedha hizo kwani wao ndio wasimamizi wa Vyama vya Ushirika lakini kwa kipindi chote wameshindwa kushughulikia changamoto hiyo ya wakulima.

Kadhalika, Mhe Hasunga Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuchangia fedha hizo.Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haina dhamira ya kuwadunisha na kuwafedhehesha wananchi badala yake imejipambanua kuwanufaisha wakulima katika kilimo.

Alisema kuwa serikali imeamua kuwalipa fedha hizo wakulima ili kuendelea na uzalishaji bora wa mazao ya kilimo lakini kesi itakapomalizika serikali itazidai fedha hizo.Mhe Hasunga amemuagiza Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Rukwa kupanga vizuri madai ya wakulima hao huku akisisitiza kutoingizwa majina mapya (Majina Hewa) yasiyohusika na madai ya fedha hizo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwa kukubali kulivalia njuga jambo hilo kwa kuwalipa fedha hizo wakulima kwani kufanya hivyo kutarahisisha wakulima hao kuendelea na uzalishaji wa mazao katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020.

Amesema kuwa maamuzi hayo ya wizara kuamua kuwalipa wakulima huku taratibu zingine za kisheria ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua Mwenyekiti huyo zikiwa zinaendelea zimeibua ari na nguvu mpya katika kilimo.

Awali, akisoma taarifa ya malalamiko ya kutapeliwa fedha hizo katibu wa chama cha MUZIA AMCOS Ndg Geofrey Mbati amesema kuwa pamoja na kupeleka malalamiko katika maeneo mengi lakini ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wa karibu katika kipindi chote cha kutafuta muarobaini wa malipo ya wakulima.

Alisema kuwa miongoni mwa maoni ya wakulima ilikuwa ni ombi la kupatiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwanusuru kutokana na kadhia hiyo ya muda mrefu iliyopelekea kushindwa kulipa ada za wanafunzi shuleni, kushindwa kuwekeza tena kwenye kilimo pamoja na kushindwa kumudu gharama za maisha hali iliyopelekea kuishi maisha ya kifukara.

Tekinolojia Kuleta Ufanisi Mkubwa Katika Sensa ya Mwaka 2022- Mtakwimu Mkuu wa Serikali.

$
0
0
 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akizungumza na Afisa Mtendaji, Kata ya Kondoa Mjini Samson Mtui alipofika Ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kuanza ziara ya kukagua maendeleo na ubora wa kazi ya kutenga maeneo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akitoa maelekezo kwa timu ya warasimu ramani wanafanya kazi ya kutenga maeneo huko wilayani Kondoa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrasimu ramani Emmanuel Mahemba wakati wa ziara ya kukagua kazi ya utengaji maeneo katika Mtaa wa Mnarani, Kata ya Kondoa Mjini mkoani Dodoma.  Kulia ni Mrasimu Ramani Galos Mbedule.

Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Taarifa za Kijiografia Ofisi ya Taifa ya Takwimu Benedict Mugambi akitoa maelezo namna maeneo ya kuhesabia watu yanavyotengwa na taarifa za taarifa za kijiografia zinavyokusanywa. Wengine ni warasimu ramani na kwa nyuma ni Meneja wa Takwimu Mkoa wa Dodoama Iddi Mruke.



Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa amesema matumizi ya tekinolojia za kisasa zitaleta ufanisi mkubwa katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 hivyo kuipatia nchi Takwimu za uhakika zaidi na kwa wakati kuliko Sensa zilizopita.


Dk. Chuwa alieleza hayo jana wakati alipotembelea wilaya ya Kondoa kukagua maendeleo na ubora wa kazi katika zoezi ya kutenga maeneo katika mtaa wa Mnarani wilayani Kondoa ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.


“Lengo letu ni kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Ufanisi mkubwa na nimekuja hapa kukagua na kutathmini ubora wa kazi ya kutenga maeneo katika wilaya yenu” Dk. Chuwa alimueleza Afisa Mtendaji, Kata ya Kondoa Mjini Samson Mtui alipofika Ofisini kwake kujitambulisha.


Wakati wa ukaguzi huo Dk. Chuwa alioneshwa namna maeneo hayo yanavyopimwa na kuwekewa mipaka pamoja na namna taarifa zinavyohifadhiwa katika Kishikwabi (tablet) ambazo zitatumika wakati wa kuhesabu watu tofauti na Sensa zilizopita ambapo Wadadisi walikuwa wakitumia ramani zilizochorwa katika karatasi.


Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Taarifa za Kijiografia katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Benedict Mugambi alimueleza Mtakwimu Mkuu kuwa kwa kutumia Kishikwambi Mdadisi atafanya kazi yake ya kuhesabu watu katika eneo lake tu na hataweza kuingia eneo la mwenzake.


“Mdadisi akitoka nje ya eneo lake Kishikwambwi kitamuonesha alama kuwa anaingia eneo silo lakini zaidi Dodoso halitaweza kufunguka hivyo hataweza kufanya kazi” alieleza Mugambi.


Dk. Chuwa alibainisha kuwa matumizi hayo ya tekinolojia yatapunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha watu wanaosahaulika kuhesabiwa wakati wa zoezi la kuhesabu watu.Katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kiwango cha watu waliosahaulika kuhesabiwa kilikuwa asilimia 5 ambacho hata hivyo ni cha chini ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.

Kwa mfano, katika Sensa iliyopita nchini Afrika Kusini kiwango cha watu waliosahaulika kuhesabuwa kiliwa zaidi ya asilimia kumi.


 “Tunataka kile kiwango cha asilimia 5 cha waliosahauliwa kuhesabiwa mwaka 2012 kiondoke katika Sensa ijayo ili tupate takwimu halisi na kuongeza ufanisi katika upangaji wa mipango yetu ya maendeleo” Dk. Chuwa alisisitiza.


Awali, akitoa taarifa ya kazi, kiongozi wa timu hiyo Mrasimu Ramani Jerve Gasto wa NBS alieleza kuwa hadi sasa vijiji vyote 84 katika Halmashauri ya Kondoa Vijijni tayari vimetengewa maeneo ya kuhesabia watu na taarifa zote muhimu zimeshachukuliwa na kuweka katika ramani.


Kwa upande wa Halmashauri ya Kondoa Mjini, Gasto alieleza kuwa kazi imeanza na wamekamilisha mtaa mmoja wa Mnarani kati ya mitaa 36 na kuongeza kuwa kazi hiyo inatarajiwa kumalizika baada ya siku kumi.


Kuhusu taarifa zilizokusanywa alieleza kuwa ni za huduma za jamii kama elimu, maji na afya, shughuli za uzalishaji kama viwanda na ofisi za serikali na huduma za kiroho.Gasto alieleza kuwa mwitikio wa wananchi ni mzuri na wamekuwa wakiwapa ushirikiano wakati wote wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao na kuwashukuru viongozi wa wilaya kwa kuwa nao bega kwa bega tangu walipoanza kazi hiyo wilayani humo. 

Hata hiyo alieleza kuna changamoto kadhaa wanazopambana nazo wakiwa kazini ikiwemo baadhi ya wananchi kuingia katika mapori ya hifadhi na utata wa mipaka katika baadhi ya vijiji.


Kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu wilayani Kondoa ilianza tarehe 16 Septemba, 2019 na kushirikisha warasimu ramani kutoka NBS, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) na wataalamu wa mipango miji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.


Watalamu hao wamegawanyika katika timu tano zenye watu watatu kila moja na kwa mujibu wa Gasto timu ya sita inatarajiwa kujiunga nao sasa kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa. 

VIJANA WA SKAUTI WAADHIMISHA KUMBUKIZI YA KIFO CHA MWL NYERERE KWENYE MNARA WA BUGOYI “A” SHINYANGA

$
0
0

Chama cha Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, kimeadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwenye Mnara wa Shule ya Msingi Bugoyi A Mjini humo, ambapo siku anafariki dunia Mwenge wa uhuru ulikuwa shuleni hapo.


Maadhimisho hayo yamefanyika leo Oktoba 14, 2019, siku ambayo alifariki Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999, akiwa nchini London akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Mtakatifu Thomas ambapo imepita miaka 20 sasa. Akizungumza mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu, amewataka vijana hao wa Skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo, kwa kuwa wazalendo kuipenda nchi yao pamoja na kudumisha amani na upendo.

 Amesema zawadi pekee ambayo vijana hao wanapaswa kumpatia Mwalimu Nyerere, ni kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani ya nchi ambayo aliiacha Baba wa Taifa, na siyo kumuenzi kwa kutenda mambo mabaya ikiwamo kujiingiza kwenye madawa ya kulevya. “Vijana ni taifa la kesho hivyo nyie kama Skauti ambao mnapitia mafunzo mengi, mnapaswa kwenda kueneza elimu kwa vijana wenzenu ya kuwa wazalendo na kuipenda nchi, pamoja na kudumisha amani na upendo vitu ambavyo ametuachia Baba yetu wa Taifa,”amesema Mkadamu. 

“Pia na waomba na wanafunzi kote nchi mumuenzi Baba yetu wa Taifa kwa kusoma kwa bidii na kumfukuza Adui ujinga, moja ya maadui watatu aliokuwa akiwapinga, na kuachana na tabia ya kwenda na simu shuleni na kuanza kuchati na kuwasababishia kufanya vibaya kimasomo,”ameongeza. 

Naye Katibu wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini Vicent Kanyogoto, amesema wamedhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwenye mnara huo, ambapo wamekaa muda wa siku nne kwa wakifanya shughuli za usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti na kuwapatia vijana elimu ya uzalendo pamoja na kudumisha amani na upendo. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu akizungumza kwenye kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, maadhimisho yaliyofanyika kwenye Mnara wa Shule ya Msingi Bugoyi A, na kuwataka vijana kumuze Nyerere kwa kuwa wazalendo katika nchi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu, akitoa wito kwa wanafunzi kumenzi Mwalimu Nyerere kwa kusoma kwa bidii na kumfukuza adui ujinga. Mjumbe wa Kamati ya Ufuatiliaji na Hamasa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Eric Daudi akiwaasa vijana wa Skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kudumisha amani na upendo. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Ndembezi Pendo John akitoa nasaha kwa vijana hao wa skauti kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kutenda mambo mazuri . Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akipongeza vijana hao wa Skauti namna walivyoboresha mazingira ya usafi shuleni hapo ukiwamo na mnara huo wa Mwalimu Nyerere pamoja na kupanda miti. Mwanafunzi Emmanuel Barnaba anayesoma Shule ya Msingi Bugoyi A akisoma risala ameiomba Serikali kuboresha miundo mbinu ya Shule hiyo, ilikuendana na hadhi ya Mnara wa kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Katibu wa Chama cha Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini Vicent Kanyogota akizungumza kwenye maaadhimisho hayo ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere uliopo shule ya Msingi Bugoyi A. Skauti wakiwa kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A, ambapo siku Mwl .Nyerere anafariki Mwenge wa uhuru ulikuwa Shuleni hapo. Skauti wakiwa kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwenye Mnara wa Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A. Mafundi wakiendelea kujenga Mnara wa kumbukumbu wa Mwalimu Nyerere katika shule ya Msingi Bugoyi A, ambapo siku anafariki dunia, Mwenge wa Uhuru ulikuwa shuleni hapo na ulizimwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo chake na kupelekwa kanisani. Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mukadamu akipanda mti kwenye Shule ya Msingi Bugoyi A, MahaLi ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere. Kamishina wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, Peter Mgalula akipanda Mti kwenye shule ya Msingi Bugoyi A, Mahari ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere. Katibu wa Skauti wilaya ya Shinyanga Mjini, Vicent Kanyogoto akipanda Mti kwenye shule ya Msingi Bugoyi A, Mahari ulipo Mnara wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A, Anna Alute akipanda mti. Vijana wa Skauti nao wakipanda miti. Vijana wa Skauti wakijipanga tayari kwa kufanya maandamano kuzunguka mjini Shinyanga huku wakiwa wameshika picha ya Mwalimu Nyerere. Vijana wa Skauti wakijiandaa kufanya maandamano huku pia wakibeba picha ya Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli. Vijana wa Skauti wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwa kuzunguka mitaa ya mji wa Shinyanga. Maandamano yakiendelea. Maandamano yakiendelea na burudani ikiendelea. Awali Mgeni Rasmi Kwenye maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Nyerere Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga akivalishwa skafu mara baada ya kuwasili kwenye Mnara wa Mwalimu Nyerere katika Shule ya Msingi Bugoyi A. Skauti wakitoa burudani ya kucheza Kwaito wimbo wa Tanzania Tanzania. Vijana kutoka kundi la The Fire mjini Shinyanga nao wakitoa burudani. Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Hafeez Mkadamu akihitimisha maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwa kugawa vyeti kwa wahitimu wa Skauti. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti. Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa hitimu wa Skauti. Skauti wakipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwamo Afisa elimu wa shule za msingi manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga katikati mwenye kilemba kichwani pamoja na viongozi wao wa Skauti. Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

NDITIYE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA GHATI YA NYEMIREMBE, CHATO

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa Mhandisi George Mmpini wa kampuni ya V. J. Mistry (wa pili kulia) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ghati ya Nyemirembe wilayani Chato moani Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa ghati ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato mkoani Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (mbele) akitoka kukagua nyumba zilizojengwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria na mizigo kwenye ghati ya Nyemirembe, Chato mkoani Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeinua mkono) akisisitiza jambo kwa mhandisi George Mmpini wa kampuni ya V. J. Mistry wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ghati ya Nyemirembe, Chato mkoani Geita

RC Makonda afurahishwa na kasi ya ujenzi wa Machinjio

$
0
0
TANGU Rais Dkt John Pombe Magufuli, alipotembelea ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti hivi karibuni na kuangiza ujenzi huo uwe umekamilika ndani ya miezi mitatu ijayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea kusimamia ujenzi huo usiku na mchana.

Usimamizi huo unaonekana kuanzaa kuzaa matunda ya haraka jambo ambalo sasa anadai kufurahishwa na kasi ya ujenzi huo kiasi cha kumpa matumaini ya kukamilika ndani ya miezi mitatu iliyotolewa.

Akizungumzia ujenzi huo, Makonda amesema kuwa, katika jambo ambalo Watanzania walifanya kwa isahihi na kwamba hawatakuja kujuta kufuatia maendeleo yake, ni pamoja na kumchagua Rais Magufuli kuwa rais wa nchi hii.

Kwa maana hiyo uamuzi wa kufanya hivyo hakika wanatakiwa kutambua kuwa walichagua maendeleo ya ujenzi wa miundombuni sahihi kama, mabarabara,Hospitali,shule na sasa machinjio makubwa na ya kisasa kabisa ya vingunguti.

Kwa maana hiyo anawaomba watanzania waendelee kuunga mkono juhudi zake kwani yeye na viongozi wengine hawatachoka kumsaidia ili kufikia malengo bora aliyokusuhudia kuwafanyia watanzania wote kipindi chote cha uongozi wake. 
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images