Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

NMB Yawahakikishia Wateja Wake Wakubwa Huduma Bora

0
0
BENKI ya NMB imewahakikishia wateja wakubwa nchini huduma bora na timilifu kulingana na mahitaji yao ya kifedha, uhakika unaotokana na ukubwa wa mtaji wa benki hiyo unaofikia zaidi ya Sh. Bilioni 700.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB- Aziz Chacha, wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.

Chacha alibainisha ya kwamba, uwezo wa kipesa unaotokana na ukubwa wa mtaji katika benki ya NMB ni mkubwa, unaowawezesha kuhudumia wateja wa kada zote, wakiwemo wateja wakubwa na kumudu kwa asilimia zote mahitaji yao ya kifedha.

Aliongeza ya kwamba wateja wakubwa wana mahitaji makubwa ya kihuduma, lakini wao wana nguvu ya kutosha kuyatimiza na ndio maana wakawaalika katika jukwaa hilo, ili kujadiliana kwa pamoja kujua namna ya kushughulika na changamoto zao na kuzitatua.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NMB, Amour Muro, alisema ‘NMB Executive Network’ ni jukwaa linalotumika kukutana na wateja wakubwa, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

“Hili ni moja ya majukumu yetu katika wiki hii na hii inatusaidia kuzungumza nao kujua namna ya kuongeza thamani ya huduma tunazowapatia. Kupitia Jukwaa kama hili, tunatanua uelewa na kuongeza thamani ya kupitia majadiliano tutakayofanya,” alisema Muro.

Alisema NMB kama taasisi inaamini katika huduma walizonazo, lakini njia bora na sahihi ya kuzifanyia maboresho mbalimbali ni kukutana na makundi tofauti ya wateja, kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi, ili kuwezesha upigaji hatua za maendeleo yao.

Magdalena Magali, ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Saruji ya Tanzania Potland, kwa upande wake aliishukuru NMB kwa kuwaandalia jukwaa maluum wateja wakubwa na kupokea mawazo yao chanya kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wateja na taasisi hiyo kwa ujumla.

Aliipongeza NMB kwa mabadiliko chanya ya kimfumo kutoka analogi kwenda dijitali, uliojikita katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka, wepesi na usalama na kuwataka Watanzania kuchangamkia huduma hizo ili kuokoa muda na kwenda na wakati.

Naye Steven Gideon, ambaye ni Ofisa Mipango na Bajeti wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), alisema kampuni yake inapongeza uamuzi wa NMB kukutana na kujadiliana nao, kwani njia rahisi ya kufikia malengo ni kufanyia kazi changamoto zilizopo ilikusonga mbele. 

Gideon aliwataka Watanzania kujali muda na kuendana na kasi za maendeleo kwa kuchagua kuifanya NMB kuwa mshirika sahihi wa ukuaji kiuchumi na kwamba siri ya mafanikio iko katika mapinduzi ya kiteknolojia yaliyofanywa na benki hiyo, yanayoongeza ufanisi kwa wateja.

 Kaimu Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa wa NMB- Aziz Chacha,alipokuwa akizungumza  wakati akifungua Jukwaa la Wateja Wakubwa (NMB Executive Network), lililofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma.
 Wateja wakiwa katika picha ya pamoja

HALMASHAURI ZATAKIWA KUENDELEZA VIJANA KUPITIA KILIMO CHA KISASA CHA KITALU NYUMBA

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wanachi waliyohudhuria katika Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba uliofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Mkoani Lindi Oktoba 10, 2019.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Lindi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba yaliyofanyika mkoani humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua jiwe la Msingi kuashiria kuzinduliwa rasmi Mafunzo kwa vijana kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba. 
Muonekano wa Kitalu nyumba kilichozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majiwa katika Viwanja vya Nanenane, Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia Kitabu cha Historia ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipotembelea banda la Maonesho la Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwilimu Nyerere mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Mpilipili.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na kikundi cha International Youth Fellowship alipotembelea Banda la Maonesho la kikundi hicho wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayoendelea Mkoani Lindi. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
Baadhi ya Vijana wa Skauti wakipitia na jumbe mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria kufungua maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Mkoani Lindi katika viwanja vya Mpilipili. (Wa pili kutoka kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, na Mwakilishi wa UNFPA Bi. Tausi Hassani. (Wa nne kutoka Kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na Waziri wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume.
Msanii wa Mziki wa Kizazi kipya Kala Jeremiah ambaye pia ni Balozi wa Vijana akiimba pamoja na vijana wakati wa maadhimisho ya wiki ya vijana. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Asasi za Vijana mara baada ya kuzindua wiki ya vijana Mkoani Lindi Oktoba 10, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU 

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri kuwawezesha vijana mikopo ya asilimia 4% ya mapato ya ndani wanayotenga kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujenga Vitalu Nyumba (Green House) vyao binafsi.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2019 wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa Vijana ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba katika Viwanja vya Nanenane, Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amesema vijana ni rasilimali muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika jamii, hivyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamua kuwajengea vijana mazingira wezeshi ikiwemo kupata fursa za mikopo na ujuzi unahitajika ili waweze kushiriki kikamilifu katika shunguli za kimaendeleo.

Alieleza kuwa, Serikali iliamua kuanzisha utaratibu wa kila halmashauri kutenga asilimia 10% ya mapato yake kwa lengo la kutoa mikopo isiyo na riba kwa vijana asilimia 4%, wanawake asilimia 4% na wenye ulemavu asilimia 2%.

“Halmashauri zote zihakikishe zinatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana ili waweze kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo shughuli za kilimo zitakazowasaidia kujiajiri na kujiingizia kipato,”

Alifafanua kuwa sekta ya kilimo ndiyo kimbilio la wananchi wengi na kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba vijana wengi watapata ajira katika sekta hiyo kwa kuwa ina faida kubwa sana ikiwemo kupata mazao mengi katika eneo dogo na kupata mazao bora yanayokidhi viwango katika soko la ndani nan je ya nchi.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali kupitia Ofisi yake imeendelea kuratibu programu ya ukuzaji ujuzi nchini na imeanza kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba katika Mikoa yote na Halmashauri zote nchini. 

Aidha alitoa wito kwa vijana kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa za mafunzo ya stadi mbalimbali za kazi kupata ujuzi stahiki utakaowawezesha kushindana katika soko la ajira.

“Nimefarijika kuona vijana waliopata mafunzo haya katika awamu ya kwanza wamekuwa na uwezo wa kujenga vitalu nyumba kwa ajili ya watu wengine waliotambua umuhimu wa kilimo cha aina hiyo, fursa hiyo ni ishara tosha kuwa vijana wameimarika katika mafunzo hayo,”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizindua Maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mpilipili na amewasihi vijana kuwa wazalendo na kutambua mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika kuleta maendeleo ya nchi yetu na bara la afrika kwa ujumla.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alieleza kuwa Serikali imetoa kutoa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa kwa teknolojia ya kitalu nyumba katika halmshauri zote nchini ambapo katika awamu ya kwanza mradi huo umefika katika halmashauri 83 hadi sasa lengo ni kufikisha ujuzi huo kwa vijana zaidi ya 18,000.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Gogfrey Zambi alisema kuwa vijana katika mkoa huo wamehamasika na mradi huo kwa kuwa wametambua una manufaa kwao.

“Programu hii imekuja wakati sahihi na imesaidia vijana kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija,” alisema Zambi

Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa alielezea hali ya usalama katika mkoa huo kulekea kwenye Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo.

Pia Kijana Mmoja wapo aliyenufaika na mafunzo hayo Bw. Azizi Njenje ameishukuru Serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwafanya kuwa chachu katika kushiriki kwenye shughuli za kilimo.

CCM YATOA TAARIFA YA MCHAKATO WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI 2019

TIMU YA KIKAPU YA DEEPSEA YA JIJINI TANGA YAPANIA KUTETEA TAJI LAO LA U-16

0
0
Wachezaji wa timu ya Kikapu ya Deepsea ya Jijini Tanga wakiwa mazoezini wakijiandaa na michuano ya Kikapu U -16 itakayoanza kesho kwenye uwanja wa JMK Jijini Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole kushoto akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole katikati akisisitiza jambo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wake mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

MABINGWA watetezi wa Mashindano ya Kikapu nchini U-16 timu ya Deepsea leo wamefanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kesho kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Kidonge chekundu JMK.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Ali Hassani Seknole alisema kwamba maandalizi kwa upande wake yamekamilika kwa asilimia kubwa na wachezaji wapo tayari kuweza kupambana na kutetea ubingwa wao ambao waliuchukua mwaka jana.

Alisema kwamba anashukuru kutokana na matayarisho ambayo wameyafanya kwa kipindi cha muda mrefu wanaimani kwamba watafanikisha ndoto zao za kuweza kurudi na Ubingwa wa Michuano hiyo ambayo imekuwa na upinzani mkubwa kila mwaka.

“Kwa kweli tunashukuru maandalizi yamekwenda vizuri na hatuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi lakini kubwa tunawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wametusawaidia kwa ajili ya timu yao kwenda kushiriki mashindano hayo kutoka Mwanza, Kigoma, Mtwara na Dar na Tanga”Alisema Kocha huyo

Hata hivyo alisema kwamba timu hiyo itaondoka na wachezaji 10, viongozi wawili huku akieleza kwamba wataanza mechi yao ya kwanza kesho jioni huku wakihaidi kuweza kupata matokeo mazuri.

Naye kwa upande wake Nahodha wa kikosi hicho Alex Clemence alisema wamejiandaa vizuri kwenda kupambana na adui wa aina yoyote ile ili kuweza kupata matokeo mazuri na kurudi na ubingwa

TTB YAWATEUWA CABBIES DO KILIMANJARO KUWA MABALOZI WA UTALII WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

0
0

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili na CABBIES DO KILIMANJARO 2019 ya jijini London wa kuwa mabalozi wa utalii wa hiari ukuwa ni mkakati wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza.
  Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi na John Dillane wa CABBIES Do KILIMANJAEO wakitiliana saini  ya Mkataba wa Makubaliano ambao una sharia na taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa wakati wa wakutekeleza jukumu yao ya kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia matukio mbalimbali atakayokuwa yanafanywa na mabalozi hao nchini Uingereza.
 Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi na John Dillane wa CABBIES Do KILIMANJAEO  wakipongezana mara baada ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili na CABBIES DO KILIMANJARO 2019 ya jijini London wa kuwa mabalozi wa utalii wa hiari ukuwa ni mkakati wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza.

Cabbies Do Kilimanjaro ni kampeni iliyofanywa na Timu ya Madereva Tax wanne wanaojulikana kama London Black Taxi Drivers kwa lengo la kuutangaza na kuwahamasisha wananchi wa London kuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro.


KILA PALIPO NA AMCOS PAWE NA SACCOS

0
0
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume akifafanua jambo kwa wanaushirika wakati wa kufunga maadhimisho kufunga maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Kitaifa, Jijini Arusha
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Prof. Alfred Sife akifunga rasmi maadhimisho ya ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Kitaifa, Jijini Arusha
Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Wanawake wa Karagwe mkoani Kagera Bi. Safina Amran akipokea Tuzo ya Chama chenye utendaji mzuri katika Sekta ya ushirika wa Akiba na Mikopo.
Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo waliopata tuzo za vyama vyenye utendaji mzuri wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi (katikati) Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Prof. Alfred Sife pamoja na viongozi wa Sekta ya Ushirika, Jijini Arusha

Wanaushirika wa Vyama vya Akiba na Mikopo wameshauriwa kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) katika maeneo zilipo vyama vya Ushirika wa mazao (AMCOS) kwa madhumuni ya kuwezesha ununuzi na upatikanaji wa pembejeo za kilimo kama vile mbolea, mbegu na dawa za wadudu waharibifu wa mazao ili kukuza uchumi pamoja na Sekta ya Ushirika. Ushauri huo ukitokana na azma ya Serikali katika kuhakikisha Sekta ya kilimo inaendelea kukuwa na kuongeza mchango wa Pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Prof. Alfred Sife akifunga maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Kitaifa yaliyokuwa yakifanyika Jijini Arusha yaliyoandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT)

Akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho hayo Prof. Sife ameongeza kwamba vyama vya Akiba na Mikopo ni chachu ya maendeleo katika Jamii kwani vyama hivyo vimekuwa msaada kwa wananchi wengi kutokana na upatikanaji wa mikopo yenye riba na masharti nafuu unaowawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali kama vile kuboresha makazi, kupata mitaji ya biashara za aina mbalimbali.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw.Tito Haule katika kufunga maadhimisho hayo alipata fursa ya kutoa wito kwa vyama vya Akiba na Mikopo kuendelea kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika kwa mujibu wa Sheria Namba.6 ya Mwaka 2013 ili kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinaendelea kuwa salama na wanachama wanapata huduma bora. Aidha, Mrajis alipongeza jitihada za SCCULT katika kuunganisha, kuviweka pamoja na kuhamasisha vyama kuendelea kujiunga na Chama Kikuu hicho.

“Mafanikio katika uendeshaji na usimamizi wa vyama hivi ni dhahiri kwamba unatokana na mchango mkubwa wa utendaji wa Serikali yetu ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Niwaombe wanaushirika tuendelee kushirikiana kwani Ushirika ni sauti ya pamoja, Chama cha Ushirika kinapata nguvu zaidi pale kinapoungana na vyama wenzake chini ya mwavuli wa Chama Kikuu cha Ushirika”
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Dkt. Gervas Machimu alisema vyama vya Akiba na Mikopo hivi sasa vipo 6,137 nchini ambavyo vinapatikana nchini kote mijini na vijijini. Akifafanua zaidi kwamba SCCULT inaendelea kutoa msukumo wa vyama hivi hususan maeneo ya vijijini kwa lengo la kukuza uchumi wa wananchi, kuendeleza kilimo, uvuvi hasa wakati huu tunapoelekea uchumi wa viwanda. Mwenyekiti huyo alitoa rai kwa vyama kuendelea kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi, wanachama bila kusahau wajibu wa kujali jamii katika mazingira ya vyama hivyo.

Dkt. Gervas alibainisha baadhi ya changamoto zinazozikabili vyama hivyo ni pamoja na tozo za makato ya SACCOS wanazokatwa watumishi kupitia Hazina akiomba Serikali kuangalia namna bora ya kurejea suala hili ili kukuza na kuendeleza ndoto za wanachama wa vyama vya Akiba na Mikopo. Mwenyekiti alieleza baadhi ya taasisi kutowasilisha makato ya marejesho ya mikopo ya SACCOS kwa wakati kunarudisha nyuma dhamira njema ya kukua kiuchumi kwa vyama na wanachama kujikwamua kiuchumi.

Mwenyekiti alisema SCCULT itaendelea kushirikiana kwa karibu na Vyama vya Akiba na Mikopo hivyo vyama vitumie fursa hiyo kupata ushauri, ufafanuzi, elimu na miongozo ya kuboresha utendaji wa vyama.
“Niwaombe wajumbe wa Bodi wa za Vyama vya Akiba na Mikopo, watendaji pamoja na wanachama kuendelea kushirikiana na chama chenu Kikuu cha SCCULT ili kuboresha utendaji wa vyama na kukuza Sekta ya Ushirika,”.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bi. Elizabeth Makwabe akitoa shukrani wakati wa kufunga maadhimisho hayo amesema Tume imejipanga na kujiimarisha zaidi katika kuendelea na uhamasishaji wa vyama vya Ushirika hususani kwa wanawake na vijana. Akiongeza kwamba Tume ina dhamira ya kuanzisha Jukwaa mahususi la wanawake katika Ushirika ili kuwahamasisha zaidi wanawake waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

WANACHAMA SITA WA CCM MIHUGA WATAKIWA KUJISALIMISHA BAADA YA KUFANYA VURUGU NA KUCHANA NYARAKA-NDIKILO

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WANACHAMA sita wa Chama Cha Mapinduzi ,wanaodaiwa kufanya vurugu na kuchana nyaraka baada ya majina yao kutorudi katika mchujo wa wagombea wa uchaguzi wa viongozi wa serikali za Mitaa, katika kijiji cha Mihuga ,Miono wilayani Bagamoyo wametakiwa kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi.
 Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ,mkoani Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akizungumza katika ziara yake ya kuhamasisha zoezi la uandikishaji kwenye daftari la orodha ya wapiga kura.

Alieleza ,amefikishiwa taarifa ya tukio hilo ambapo watu hao walikimbia na hawajulikani walipo.

"Kama jina lako limechujwa kazi yako sio kufanya vurugu rudi kwa viongozi wako wa kata  kaeni na angalieni taratibu ili haki yako ipatikane na sio kufanya vurugu"
"Sitokubali watu kutuharibia uchaguzi wetu ,tuchague viongozi kwa amani na utulivu, na hawa ambao wamefanya kitendo hiki cha uhalifu ,ni lazima wajitokeze kutoa ushirikiano kwa polisi"alieleza Ndikilo.

Ndikilo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Salim Mohammed, Mfumwa Ramadhani, Mwajuma Husen ,Fatuma Kazimili, Kapera Ramadhani na Furaha Zuberi .

Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa mkoa aliwataka watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika na tukio la kuweka sumu kwenye malisho ya mifugo na kusababisha ng'ombe 15 kufa,huko kijiji cha Miono kujisalimisha polisi ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Ndikilo, amesikitishwa na tukio hilo ambalo linadaiwa kuhusishwa na mmoja wa viongozi wa juu wa kata ya Miono.

Alisema, migogoro ya wakulima na wafugaji imalizwe kwa amani na sio kuwekeana visasi baina ya makundi hayo mawili.

MVIWATA MANYARA WALIA NA GMO

0
0
MTANDAO wa Wakulima Tanzania Mkoani Manyara, wameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kusitisha mpango wa matumizi ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) ili kuwaepusha kuwa tegemezi wa mbegu kutoka nje kwani teknolojia inayotumika kubadilisha vinasaba vya mbegu bado haipo nchini.

Wakulima hao waliyasema hayo mjini Babati kwenye mkutano mkuu wa mtandao wa wakulima Tanzania (Mviwata) wenye kauli mbiu ya mtetezi wa mkulima ni mkulima mwenyewe. 

Mmoja kati ya wakulima hao Lohay Langai alisema mbegu hizo zilizobadilishwa vinasaba (GMO) huwenda zisiwe na tija kulingana na mazingira na hali ya hewa ya maeneo mengi ya hapa nchini. 

Langai alisema hali hiyo itasababisha wakulima kuwa tegemezi wa mbegu kutoka nje na hata kuchelewa kupatikana lakini huwenda pia ikaporomosha uchumi wa wakulima.

Mwenyekiti wa Mviwata mkoani Manyara, Mohammed Hussein alisema anadhani serikali italeta mbegu hizo za wakulima wakijua kuwa wanakuja kuboresha kilimo kumbe watakuja kuwafanya wakulima wawe tegemezi.

Hussein alisema haoni sababu ya serikali kuingiza mbegu hizo za GMO na badala yake ingeweza kuboresha mbegu za asili zilizopo kwa sasa na zingeweza kuleta tija lakini siyo kuleta mbegu zilizobadilishwa vinasaba. 

"Hizi mbegu zilizobadilishwa vinasaba wanafikiri ndiyo wanakuja kumkomboa mkulima kumbe wanakuja kuwaandaa wakulima kuwa tegemezi wa mbegu kutoka nje ambazo wanaweza wasizipate pia kwa wakati," alisema Hussein.

Mkulima mwingine Emanuel Nuas alisema wakulima hawazihitaji mbegu hizo kabisa bora zilizopo ziboreshwe na kuwapa wakulima elimu ya masuala ya hewa hapo ndiyo inaweza kusaidia lakini siyo mbegu hizo za GMO.

Mratibu wa Mviwata mkoani Manyara, Martin Pius alisema katika kuendelea kupeana elimu ya masuala ya kilimo wakulima waliopo kwenye mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania Mviwata wanakutanika mjini Babati na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mashirikiano ya ushirika na vyama vya wakulima.

Pius aliwaasa viongozi wa  serikali kuwekeza zaidi katika kuimarisha ushirika nchini kwa kuwaajiri wataalam wengi na wenye uelewa wa masuala ya kilimo ili kuweza kutembelea na kutoa elimu hususani ya kimasoko kwa wakulima.

Mgeni rasmi wa siku hiyo, mkuu wa wilaya ya Hanang' Joseph Mkirikiti alilaumu baadhi ya mashirika na taasisi mbalimbali za kifedha ambazo zimekuwa zikieleza kuhudumia wakulima lakini kiuhalisia hawafiki kwa wakulima hao.

"Ninachotaka kusema ni kuwa kumekuwepo na baadhi ya taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayozungumza na wakulima lakini hawafiki kwa wakulima kutoa elimu ya namna ya kupata mikopo na pembejeo," alisema Mkirikiti.

Aliwaasa wakulima wa Mviwata mkoani Manyara kuweka malengo ya kukua na kutokuendelea kujiita wakulima wadogo kila wakati.

"Ninawaomba na nyie wakulima wa Mviwata Manyara msiwe mnajiita wakulima wadogo kila mwaka fikirieni sasa kukuwa, mtakuwa wadogo mpaka lini?" alihoji Mkirikiti.

Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano mkuu wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) uliofanyika mjini Babati Mkoani Manyara, ukiwa na kauli mbiu ya mtetezi wa mkulima ni mkulima mwenyewe.


NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO TIMU ZA JWTZ

0
0
  

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kulia ni Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego akishuhudia.
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya jeshi inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni, vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni 18. Kulia ni Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge.

Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi jezi Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi, Ally Ngingite pamoja na Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego (kulia) wakishuhudia.
 
Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana vifaa hivyo vya michezo

********************************

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni udhamini wao katika michezo mitatu, yaani mchezo wa ngumi, mieleka pamoja na mchezo wa riadha.

Udhamini huo wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 18, umekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati, Filbert Mponzi kwa viongozi wa JWTZ.

Aidha akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bw. Mponzi alisema Vifaa hivyo vya Michezo vilivyotolewa na NMB ni sehemu ya udhamini wa Benki ya NMB kwa Michezo ya ngumi, mieleka pamoja na riadha.

Aliongeza kuwa, Benki ya NMB inaushirikiano mkubwa na wa muda mrefu ambao umekuwa na faida kwa pande zote huku ukiendelea kuimarika siku hadi siku.

“…Kwa niaba ya NMB tunaomba mtuwakilishe vema na tutafurahi zaidi mkirudi hapa na medali za dhahabu, tutakuwa na furaha zaidi kwani si tu mmeshinda bali benki yetu itakuwa imeshiriki kufanikisha ushindi huo,” alisema Bw. Mponzi akikabidhi msaada huo.

Alibainisha kuwa NMB imekuwa ikishirikiana na JWTZ kudhamini michezo mbalimbali, jambo ambalo linaendelea kuboresha mahusiano mazuri kati ya pande zote.

Michezo ya Majeshi Duniani, World Military Games inayoshirikisha majeshi mbalimbali ulimwenguni, inatarajia kufanyika nchini China katika Jiji la Wuhan hivi karibuni

SBL yawekeza Paundi Mil 10 kupanua uzalishaji wake Dar, Moshi

0
0
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imetangaza mpango wake wa upanuzi wenye thamani ya paundi milioni 10 kwa viwanda vyake vya Dar es salaam na Moshi. 

Uwekezaji huo unapelekea kampuni hiyo kuongeza uwezo wake wa uzalishaji wa bia na hivyo kukidhi mahitaji ya wateja wa bidhaa zake yanayoongeza kila siku. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, kazi ya upanuzi tayari imeshaanza Dar es salaam, ambalo ni tawi la kwanza la uzalishaji kati ya matatu lililoanzishwa mwaka 1996. Matawi mengine ya uzalishaji ni Moshi na Mwanza 

"Upanuzi huu haumaanishi tu kupata uwezo wa ziada wa uzalishaji wa bia kwa sisi (SBL), lakini pia unaongeza fursa zaidi za ajira kwa watanzania na kuongeza uhitaji zaidi wa shayiri, mahindi na mtama ambavyo kampuni hununua kutoka kwa wakulima wa ndani," Mkurugenzi Mkuu huyo anasema. 

SBL kwa sasa imeajiri wafanyikazi wa moja kwa moja zaidi ya 800 na wengine katika viwanda vyake. Kuna maelfu ya wanufaika wengine wakiwamo wasambazaji, wasafirishaji, wakulima, wamiliki wa baa na wafanyikazi ambao hutegemea bidhaa za kampuni hiyon kama chanzo cha mapato. 

Kampuni hiyo hutegemea vyanzo vya ndani vya shayiri, mahindi na mtama kwa uzalishaji wake wa bia. Mkurugenzi huyo anafafanua kuwa, hadi kufikia mwishoni wa mwaka jana, kampuni yake ilichukua nafaka za ndani hadi kufikia tani 15,000, ambayo ni sawa na asilimia 60 ya mahitaji kamili ya malighafi ya SBL kwa uzalishaji wa bia kwa mwaka. 

SBL ina bidhaa nyingi zinazouzika na zina ubora wa hali juu kwa jina lake. Chapa yake kuu ya Serengeti Premium Lager imekuwa bia ya kwanza nchini Tanzania kufanywa kuwa malt kwa asilimia 100. Hivi karibuni SBL ilizindua bidhaa yake nyingine ya Serengeti Premium Lite, ambayo ni ya kwanza nchini Tanzania iliyoingizwa sokoni mwaka wa 2017. 

"Wateja wetu walionesha uhitaji wa bia halisi ya kitanzania na ndio maana tulizindua Serengeti Premium Lite miaka miwili iliyopita. Watanzania wameipokea vyema bidhaa hii mpya ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika soko, "Ocitti anasema na kuwashukuru wateja kwa kuunga mkono chapa hiyo. 

Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Deloitte mwaka 2018 juu ya uchangiaji wa SBL kwenye uchumi wa Tanzania ulionyesha kuwa, SBL ilichangia thamani ya shilingi bilioni 567 katika uchumi wa Tanzania kwa mwaka jana. Hii ni sawa na asilimia moja ya uchangia kwenye pato la taifa kwa bidhaa za ndani (GDP) ) ambalo kwa sasa linakadiriwa kufikia dola bilioni 55, karibia sawa na shilingi trilioni 127. 

SBL ilianzishwa na wajasiriamali wachache wa Kitanzania mwaka 1996 na kiwanda kimoja ambacho kilijengwa jijini Dar es salaam. Kati ya mwaka 2010 na 2013 muundo wa umiliki wa kampuni ulibadilika na kuja na bodi ya kampuni kubwa ya bia ya East Africa Breweries Limited (EABL), mtayarishaji wa vinywaji duniani, Diageo, ambao wamechangia ongezeko la uwekezaji zaidi kwa kufungua viunga vikuu viwili vya nyongeza vya uzalishaji katika Jiji la Mwanza na Moshi. 

Hadi sasa, kampuni imepanua wigo kwa kuzalisha bidhaa za bia zinazoongoza kama vile Pilsner Lager, Tusker Lager, Guinness na Senator Of Late - Serengeti Premium Lite. 

Halikadhalika, SBL pia inasambaza katika soko la Tanzania bidhaa zingine za kwanza za Diageo za Kimataifa kama vile Johnnie Walker, Gordons, Smirnoff Black ICE na zingininezo.

TANZIA:MKUFUNZI WA SHOTOKAN-RYU KARATE AFARIKI DUNIA

0
0
Mkufunzi na Mkuu wa Idara ya Ufundi ya JKA/WF-­‐Tanzania kitaifa, pia Mwenyekiti wa Tanzania Shotokan-­‐Ryu Karate-­‐Do Association (TASHOKA) Abdallah Kambi Sensei  amefariki dunia.

Kambi Sensei aliyeingia madarakani tarehe 27 Julai 2019, amefikwa na umautio leo alfajiri katika hospital kuu ya Taifa Muhimbili, alipokua amelazwa kufuatia kusumbuliwa na kifua na tumbo, tangu mwezi August.

Mwenyekiti, JKA/WF-­‐Tanzania Jerome G. Mhagama, amethibitisha kutokea kwa msiba huo, na ameeleza taratibu za maziko ya Kambi Sensei aambaye alijiunga na JKA/WF-­‐Tanzania mwaka 2009 na kuwa mwanafamilia hai wa JKA mpaka umauti unamkuta.
 
Katika hatua nyingine Mhagama ameeleza taarifa nyingine za msiba wa mdau huyo wa mchezo wa Karate, huku wakitarajia majibu wa kikao cha familia ya marehemu.

Ndani ya JKA Kambi Sensei alikuwa mmoja wa Wakufunzi tegemezi mwenye Black Belt 4th Dan-­‐JKA, pia alikuwa na JKA International Licence yenye viwango vya Instructor class C, Judge class D & Examiner class D.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Alale mahali pema peponi.

TUNAHITAJI TAFITI BORA ZA MBEGU-BASHE

0
0
 Naibu waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe akitembelea vipando vya mazao mbalimbali vilivyoko katika Naibu waziri Chuo Kikuu cha kilimo kilichopo Morogoro


Na Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo 

Morogoro 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe ameshauri Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine na Wakala wa Uzalishaji Mbegu Tanzania (ASA) kushirikiana kuzalisha mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya wakulima. 

Bashe ameyaesema hayo jana kuwa Taasisi za Serikali zinapasa kuwa mdau wa kwanza katika kuhakikisha mbegu bora na za kutosha zinapatikana. 

“Usalama wa Chakula utakuwa endelevu endapo hatua madhubuti zitachukuliwa kuona taifa linazalisha mbegu za kutosha na zinazohimili magonjwa” alisema Naibu Waziri 

Bashe yupo mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi kukagua shughuli za uzalishaji mbegu ambapo alifanya mikutano na wakuu wa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine,Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) pamoja na Wakala wa Mbegu (ASA) 

Bashe alisitiza kuwa uchumi hauwezi kukua kama hakutakuwa na uwekezaji mzuri kwenye kilimo kwa kutumia utaalam unaopatikana kwenye taasisi za kitaaluma. 

Naibu Waziri alibainisha kuwa ni lazima kilimo kiangaliwe kwa jicho la kibiashara ili kiweze kumvutia mkulima na wawekezaji hivyo ni wakati wa wataalamu wa kilimo kuchochea mabadiliko chanya. 

“Ni muda muafaka sasa tafiti nyingi za SUA zitokane na matatizo ya wakulima ili waweze kuzitumia na kubadilisha kilimo chao kuwa chenye tija” alisema Bashe 

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Prof Raphael Tihelwa Chibunda amesema chuo chake kipo tayari kufuata maelekezo kwa kuwa tafiti zao zote zinalenga mahitaji ya jamii ya watanzania. 

Prof Chibunda amesema pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu lakini ni muhimu kama nchi kuimarisha huduma za ugani ili kuleta matokeo mazuri pindi wakulima watakapotumia mbegu bora za kilimo 

Hata hivyo amemweleza Naibu Waziri kwamba imefika wakati nchi kuondokana na kuweka vikwazo zadili (regulatory) badala yake iwe na mikakati ya promosheni kwa kuwa bado hatujawa na utoshelevu katika mbegu. 

Madereva tax kutoka Uingereza wapanda Mlima Kilimanjaro

0
0
Timu ya madereva taxi watano kutoka Uingereza ilifanya ziara nchini kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 10 Oktoba 2019. Ziara hiyo iliratibiwa na Wizara kupitia Ubalozi wetu London kwa kushirikiana na TTB. Timu hiyo ilikuja nchini kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni zoezi la hisani ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military veterans) huko Uingereza. 

Katika kutambua uamuzi mzuri wa timu hiyo kuuchagua mlima Kilimanjaro kwa zoezi hilo la hisani na kwa malengo ya kunufaika na ujio wao katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii nchini Uingereza, Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliwaandalia timu hiyo ziara ya kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali hapa nchini zikiwemo mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro na Tarangire.

Vilevile, Timu hiyo ya madereva taxi baada ya kumaliza kutembelea vivutio vilivyotajwa hapo juu walitangazwa kuwa mabalozi wa hiari wa utalii (tourism goodwill ambassadors) wa Tanzania kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vya hapa nchini wawapo katika shughuli zao huko Uingereza. Hafla ya kuwatangaza ilifanyika Hotel ya Mount Meru Arusha. Baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa hiari, walisaini Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya timu hiyo na TTB tayari kwa kutekeleza majukumu yao.

Tukio hilo lilihudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, akimuwakilisha Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangallah (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Aidha, Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Timu ya Madereva kutoka Uingereza ikipanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military veterans) huko Uingereza. 
Timu ya Madereva wa Taxi kutoka Uingereza ikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak). 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akitoa neno katika hafla ya uwekaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Timu ya Madereva wa taxi watano kutoka Uingereza. Makubaliano hayo yalihusu timu ya madereva wa Uingereza kuwa Mabalozi wa hiari wa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza. 
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Dkt. Devota Mdachi na Kiongozi wa Madereva wa Taxi wakiweka saini MoU. 
Hati ya Makubaliano baada ya kusainiwa ikioneshwa kwa wajumbe walioshiriki hafla ya uwekaji saini. 
Madereva wa Taxi, baadhi yao wakiwa na wenza wao baada ya hafla ya uwekezaji saini MoU 

BASATA LAMUITA MSANII MENINA KUFUATIA PICHA ZAKE CHAFU KUVUJA MTANDAONI

MIAKA MINNE YA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

0
0
Na Judith Mhina-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa funzo kubwa kwa Watanzania kuwa tunahitaji kuwatengeneza watumishi aina ya Rais Magufuli ili Tanzania iweze kusonga mbele.

Sio mara moja wala mbili Rais Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa kutokana na utendaji anaokutana nao katika ziara zake mikoani, na hatma ya Tanzania huko tunakoelekea. Hii ina maana kubwa kwetu na ni vema kupata majibu hayo kwa mstakabali wa Taifa letu.

Rais Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa ambayo mimi na wewe kutoa majibu kwa haraka itakuwa ni uongo. Bali  kama Watanzania tunawajibu wa kumuahidi Rais  kuwa kutokana na utendaji wake uliotukuka, tumeona kinachojiri kwa sasa hapa Tanzania kwa kweli maendeleo makubwa yaliyopatikana  na yanayoendelea  kupatikana ni wajibu kuwatengeneza Magufuli wengi kwa mstakabali wa Taifa letu.

Baadhi ya maswali hayo ambayo kila uchweo, katika ziara zake mikoani au wakati za kuapisha viongozi mbalimbali  Rais Magufuli anajiuliza na anasema “Je nikiondoka leo  Bwawa la Umeme la Nyerere litajengwa? Nikiondoka leo reli ya kisasa (SGR) itajengwa Je Nikiondoka leo ndege zitanunuliwa? Hapa ndipo napata nguvu ya kufanya kazi.”  

Rais Magufuli nguvu anayoipata kwa ajili ya kutimiza azma yake katika kuleta maendeleo  Tanzania, ndipo anapochochea azma ya vijana na watanzania wenye uchungu na nchi hii kufikiri na kutafakari kwa nini na wao wasiwe watendaji wazuri kama Rais Magufuli?.

Maneno ya uchungu anayojiuliza Rais Magufuli yawe  chachu kwa vijana  kutafakari  na kuahidi kila mmoja nitaifanyia nini Tanzania. Kila kijana wa Tanzania ajiwekee mikakati yake binafsi  kwa kuangalia mifano hai ya utendaji wa Rais Magufuli na kuahidi kufanya vema  akiwa katika sekta binafsi hapo alipo au sekta ya Umma.

Kitabu cha Uongozi na Hatma ya Taifa la Tanzania cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kimeeleza wazi aina ya kiongozi anayepashwa kuiongoza Tanzania. Aidha miko na taratibu za uongozi ni lazima zifuatwe ili kuhakikisha ustawi wa Taifa lolote lile duniani.

Kwanza Rushwa ni Adui wa Haki suintatoa wala kupokea rushwa tuwatengeneza vijana ambao wana nia ya dhati na dhamira zao zinatuambia kwake hakika rushwa ni adui wahaki. Sifa hii Rais Magufuli ameidhibitisha kuwa ameipiga vita rushwa kwa nguvu zote, hususan kupambana na watu wenye fedha au kipato cha juu, Hakika kwa hili hongera na pongezi unastahili.

Vita dhidi ya madawa ya lulevya, ambayo ni vita kali sana duniani kwa kuwa wahusika wana uwezo wa kutoa rushwa ya kiasi chochote kilecha fedha,  kwa serikali na watendaji wake. Lakini Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa- TAKUKURU.

Pia, kuanzisha Tume ya Kuratibu Uthibiti wa Dawa za Kulevya –Drug Control Commission of Tanzania, ikiwa na kujitolea kwa vijana shupavu kama na wa mfano kama, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Mhe. Paul Makonda, hiki ni kithibitisho vijana wakuendeleza unayoaanza wapo.     
Baba wa Taifa amesema Rais tumtakaye ni yule ambaye anaweza kutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuhakikisha unadumu milele.  Kwani ndio kielelezo cha Umoja wetu, Amani Upendo na Mshikamano, ambao ndio dira yetu  na tunu ya Taifa letu.

Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ameonesha kielelezo hicho kwa uwazi na kuahidi kuudumisha Muungano huo, kwa nguvu zake zote akili na maarifa aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Nina hakika wapo vijana ambao wanautetea Muungano huu na kuenzi kwa nguvu akili maarifa na moyo wao wote.

Mfano wa mambo yanayoimarisha Muungano ni uwepo wa Wizara za Muungano ambao unafahamika, lakini wapo mawaziri kutoka upande wa pili wa Muungano ambao wanashika nyadhifa ambazo sio wizara za Muungano, ikiwemo masuala ya msamaha wa deni la Tanesco kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
Kiongozi tumtakaye ni lazima aone nyufa za Muungano na awe na uwezo wa kuziba nyufa hizo  kabla hazijaleta madhara. Rais Magufuli amelidhibitisha hilo na nachukua kila hatua ya kuhakikisha Muungano wetu unakuwa imara zaidi kuliko wakati wowote .

Baba wa Taifa amesema Tanzania inataka Rais ambaye atakuwa Mtumishi na sio Mtawala, kiongozi anayeumizwa na shida na mahangaiko  ya Watanzania. Rais Magufuli amethibitisha hili kwa kusema sipo radhi kuongoza Watanzania wanaotoa machozi.  Rais anahangaika usiku na mchana kuhakikisha anatatua shida na mahangaiko mbalimbali ya Watanzania.

Tumeshuhudia Rais akichukizwa na ulanguzi wa korosho za wakulima na kuingilia kati ili wasidhulumiwe jasho lao, lakini pia kujua haki zao kama wakulima. Amechukizwa na ufujaji wa fedha za Umma kwenye sherehe ambazo hazina tija  na kuzipeleka kufanya usafi wa mazingira na kupambana na ugonjwa wa kipindupindu na kununua dawa.

Serikali ya Awamu ya Tano inakusanya kodi kwa kila mtu bila ubaguzi, kwa mara ya kwanza katika historia  ya nchi imevunja rekodi ya kukusanya  fedha za Tanzania Trilioni 1.8 kwa mwezi  Agosti 2019. Nyerere alisema katika moja ya hotuba zake serikali corrupt haikusanyi kodi, inabaki kukimbizana na wafanya biashara wadogo wadogo.  

Rais Magufuli ameumwa na mahangaiko ya wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga ) amekuja na mfumo madhubuti ya kuwafanyia wafanye biashara zao kwa uhakika zaidi bila kubughudhiwa. Kuanzishwa kwa vitambulisho maalum vya Rais ndio kielelezo cha kuonyesha ni jinsi gani anaumizwa na mahangaiko ya watanzania.

Rais tumtakaye ni yule anayeweza kuwa mbunifu kutokana na rasilimali tulizonazo na kuhakikisha Taifa linajitegemea ili kuleta heshima. Rais Magufuli amelitekeleza kwa kutumia fedha za ndani katika kujiletea maendeleo, sasa nchi inaheshimika  ukikataa na fedha zako haijalishi nchi inasonga mbele. Vijana wanaona Rais anavyofanya wanajifunza wanakuelewa kwa kuwa wazalendo wapo.

Kuanzishwa kwa sera ya Elimu bure Tanzania kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne kila mwezi serikali inatoa jumla ya Bilioni 23. 5 kwa ajili ya Elimu bure shule za sekondari na za Msingi Tanzania Bara.

Kwa sasa kuna vijana wengi sana ambao wapo shule  na hawahangaiki tena na kukimbizana na Walimu, Wazazi wafadhili na wengineo katika kutafuta fedha za ada. Matokeo yake hata watoto wa maskini kwa sasa wapo shule.  Ndio hao hao  watakaokuja kuchukua nafasi za uongozi katika nchi hii na hakika tutambue vijana wanaona anachofanya Rais Magufuli.

Tumeshuhudia miaka mingi inapita migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji, Wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ikiwemo hifadhi za Taifa. Rais Magufuli hili limemuuma Sana na kuhakikisha jumla ya vijiji 920 kati ya 975 nchini vilivyopo maeneo ya hifadhi vimetambuliwa rasmi.  Yote haya kwa masilahi ya watanzania wanyonge vijana wanaona nina hakika watafata nyayo zako.

 Aidha, Tanzania imefuta maeneo ya akiba 12 yenye ekari 707, 659, 95 na misitu 7 yenye ekari 46,715. Pia serikali imeamua kumega eneo la hifadhi 14 ili kuwapa wananchi maeneo ya kuishi kuzalisha kilimo na ufugaji ambapo katika uamuzi huo vijiji 60 vinavyonufaika ni  vya Mkoa wa Katavi.
Kiongozi bora ni yule anaweza kutoa suluhisho la kudumu kwa watu wanaohusika badala ya kubaki na ngonjera za utafiti unafanywa, tupeni muda serikali inalifanyia kazi,  nimeagiza viongozi watatoa mustakabali wa tatizo hilo. Utasikia mchakato unaendelea miaka nenda miaka rudi.  

Kitabu cha Uongozi wa Tanzania na Hatma yake cha Baba wa Taifa Nyerere kinasema Rais tumtakaye ni yule anayeguswa na matatizo ya majirani zake Rais Magufuli ameonyesha Mfano wa kuhakikisha majirani zake waliopata dhoruba ya kimbunga cha Kenneth kilichotokea mapema mwezi April 2019 na kuadhiri Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, na kuhakikisha Tanzania inatoa msaada wa tani za mahuindi kadhaa kwa Malawi Zimbabwe na Msumbiji.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC kwa sasa imepamba moto na nchi ya Tanzania ndio Mwenyekiti, ambapo imeonyesha dira kwa kuzindua Kituo cha Huduma za Pamoja za Mpakani, Nakonde One Stop Post ili kuongeza mtengamano wa Jumuiya hiyo katika masuala mbalimbali ya Bishara, Mawasiliano, Uchukuzi na mengineyo.   

Rais wa Tanzania awe ni yule anayetaka kuwaletea maendeleo watanzania sio kujiletea maendeleo yeye mwenyewe, familia yake na marafiki zake. Rais magufuli ametia fora katika eneo hilo barabara  nyingi zimejengwa nchi nzima kwa kiwango cha lami, barabara hizi ni kichocheo kikubwa cha uchumi, Rais Magufuli  vijana wanaona na kuona ni kuamini.

Vituo vya Afya 320 Zahanati na Hospitali za Wilaya kadhaa za Rufaa Mkoa zimejengwa na kuimarishwa, Bajeti ya dawa imeongezwa na dawa zinapatikana hospitali zote za serikali kutoka Bilioni 32  mpaka Bilioni 352. Vyumba vya madarasa vingi vimejengwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Awamu ya Tano.

Rais tumtakaye ni yule anayehimiza Umoja Mshikamano Upendo kwa Watanzania na ndio maana Tanzania na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetengemaa, uanzishwaji wa Umoja wa forodha katika mipaka ya Tanzania na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Aidha, Ushirikiano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC ni kielelezo kingine ambacho kinaonyesha Tanzania imeadhimia kuhakikisha dhamira ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya Umoja wa Afrika inatimizwa.

Rais tumtakaye ni yule asiye na ubaguzi wa dini, rangi sura eneo atokalo mtu kabila au vinginevyo. Watanzania wote ni sawa na Afrika ni moja Rais Magufuli anasema “Naomba mniombee nisibadilike niwatumikie Watanzania kwa moyo wangu wote akili na maarifa, naomba nisibadilike nisiwabague Watanzania kwa kabila zao, dini zao, rangi zao maeneo wanayotoka naomba mungu anisaidie”

Rais Magufuli amesema “Siwezi kuendesha nchi ambayo watu wake wanatoa machozi”  Viongozi wetu wametimiza wajibu wao, uamuzi ni wa Watanzania kuamua kutumikia nchi yao kwa nidhamu na heshima, upendo na amani kila utendalo liwe kwa masilahi ya nchi na sio vinginevyo. Rais magufuli matendo yako yatatengeneza MAGUFULI  WENGI WAJAO MUNGU IBARIKI TANZANIA.      


NAIBU SPIKA DR. TULIA AWATEMBELEA NA KUWAPA POLE WAFIWA AJALI YA DARAJA MBEYA

0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wafiwa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya daraja linalounganisha kata za Mwasanga na Tembela Mkoani Mbeya kufuatia mvua kubwa iliyosababisha daraja hilo kuvunjika siku nne zilizopita na kusababisha vifo vya watu wanne waliokuwa wakivuka katika daraja hilo.

Akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Serikali akiwemo Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya ACP James Kasusura, Diwani wa Kata ya Mwasanga Mhe. Hokola pamoja na viongozi wa CCM, Dr. Tulia ametoa misaada mbalimbali kwa wafiwa ikiwemo kilo 100 za Mchele, kilo 40 za Maharage pamoja na pesa Taslim Shilingi 600,000/- (huku taasisi ya Tulia Trust ikichangia jumla ya Shilingi 200,000/-)
Akizungumza na Wananchi hao Dr. Tulia amesema “Tumepoteza ndugu zetu katika jambo hili baya lililotupata, nilizipata taarifa hizi nikiwa safarini, nimerejea leo na nimeona nije niwaone ndugu zangu kwa hili janga lililotupata. Niwashukuru sana Wanajamii kwa kujitoa kwenu katika kuendelea kuwafariji wenzetu hawa waliopoteza ndugu zao.”

Pia Dr. Tulia amesema “kikubwa zaidi niwapongeze na kuwashukuru Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Mhe. Albert Chalamila pamoja na Jiji kwa hatua kubwa ambazo wamekwisha chukua hadi sasa hivi. Kwa wakati huu hatua ya awali ilikuwa ni kuwahifadhi kwanza Marehemu ambao wamepoteza maisha kwenye hili janga na pia wametoa michango mingine ya chakula na fedha kwa ajili ya kuwasaidia hawa wenzetu wafiwa.”

Wakati huo huo ametoa rai kwa jamii kukaa na watoto kwa ukaribu katika kipindi hiki cha mvua. Amesema “mvua ni nyingi na maji ni mengi kwahiyo mtoto mdogo anaweza asijue maji ni mengi kiasi gani hivyo tuendelee kukaa nao karibu ili kuepukana na hizi changamoto”-Dr. Tulia

Mwimbaji Esther Kusekwa Hajakata Tamaa “Anatamani Kukutana na Rais Magufuli”

0
0
Mwimbaji wa nyimbo za injili na kijamii jijini Mwanza, Esther Kusekwa (katikati) amesema ana kiu na ndoto kubwa ya kukutana ana kwa ana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kusekwa ameyasema hayo Oktoba 11, 2019 alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) kupata Baraka zake baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2019 mkoani Lindi.

Kwa sasa Kusekwa anatamba na Albamu mbalimbali za Injili na za kuhamasisha maendeleo ikiwemo Magufuli ni Jembe.

WAZIRI MKUU AZINDUA MAFUNZO YA KILIMO KUPITIA TEKINOLOJIA YA KITALU NYUMBA

0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mradi wa mafunzo ya kilimo kupitia tekinolojia ya kitalu nyumba kwenye viwanja vya Nanenane, Ngongo mkoani Lindi, Oktoba 10, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama na  kulia ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Karume. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Tausi Hassan kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu   (UNFPA). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyanya wakati alipozindua  mradi wa mafunzo ya kilimo kupitia tekinolojia ya kitalu nyumba kwenye viwanja vya Nanenane, Ngongo, Lindi Oktoba 10, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa mafunzo ya kilimo kupitia tekinolojia ya kitalu nyumba kwenye viwanja vya Nanenane wa Ngongo, Lindi Oktoba 10, 2019. Wa tatu  kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama na  wa pili kulia ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Karume.  Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia) na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Karume (kulia) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kuzindua  Mradi wa mafunzo ya kilimo kupitia tekinolojia ya kitalu nyumba kwenye viwanja vya Nanenane, Ngongo, Lindi Oktoba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi mbalimbali na baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika kwenye  viwanja vya Mpilipili mjini Lindi, Oktoba 10, 2019. Waliokaa kutoka kushoto ni  Tausi Hassan kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA),  Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar,  Balozi Ali Karume, Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUCHIKA AWAPONGEZA WATUMISHI WA RUVUMA KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

0
0
Na James K. Mwanamyoto, Songea 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amewapongeza Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa msaada wa fedha, sabuni za kufulia na mafuta ya kula kwa watoto yatima wa kituo cha Swako kilichopo Songea mjini kwani wameonyesha taswira nzuri ya utumishi wa umma kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zitolewazo na taasisi za Serikali.

Mhe. Mkuchika ametoa pongezi hizo alipokutana na Watumishi wa Umma kwenye ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya watumishi hao, Mhe. Mkuchika amewashukuru watumishi waliochanga fedha hizo na kutoa mahitaji mengine ambayo yamekuwa ni faraja kwa watoto hao.
“Msaada mlioutoa utakuwa ni chachu ya kujenga ustawi wa watoto hao ili hapo baadae waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa, na ndio maana mmemuona mlezi wa kituo hicho amefurahi sana baada ya kupokea msaada wenu”, Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Msaada walioutoa watumishi hao ni mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya kuzitaka  taasisi za umma nchini kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa umma mwaka huu kwa kushiriki masuala ya kijamii ili kujenga uhusiano mzuri na wananchi. 

Aidha, Mhe. Mkuchika amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Prof. Riziki Shemdoe kwa kuratibu vema utekelezaji wa maelekezo ya ofisi yake katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu kwani pamoja na kutekeleza maagizo mengine wakati wa wiki hiyo ambayo huadhimishwa tarehe 16 hadi 23 Juni kila mwaka lakini waliona pia ni vema wakawasilisha msaada kwa watoto yatima .

Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Prof. Riziki Shemdoe alimueleza Mhe. Mkuchika namna watumishi wa Sekrekarieti ya Mkoa wa Ruvuma walivyojitoa kuchanga fedha hizo na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu shughuli za ustawi wa kijamii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini.

Mhe. Mkuchika anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Songea (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake kilichofanyika mjini Songea kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
 Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi chake kilichofanyika mjini Songea kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi msaada wa fedha taslimu na mahitaji kwa mlezi wa kituo cha Swako cha kulea watoto yatima, Bi. Regina Chinguku kilichopo Songea mkoani Ruvuma kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma waliochanga ili kukisaidia kituo hicho.

Mazoezi ya Familia yapigiwa chapuo.

0
0
Mbio za Marathon zimekuwa ni sehemu ya Maisha ya watu wengi hasa mijini na kwa kiwango kikubwa imechochea sana kuboresha maisha ya Watanzania wengi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Familia Marathon Balozi wa Familia Marathon Veronica Kundya alisema “ mazoezi yana mchango mkubwa wa kuboresha afya ya Familia hivyo kujenga taifa bora la lenye nguvu la kesho”.Mbio hizo za Familia Marathon zinatarajiwa kufanyika Disemba 8 2019 jijini Dar Es Salaam
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images