Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MKOA DODOMA, MZAKWE MAKUTOPORA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimsikiliza Imakulata Yoram (36) Mkazi wa Nkuhungu Dodoma aliyejifunguwa mtoto wa kike katika Hospitali ya Mkoa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuangalia Changamoto mbali mbali ziliopo kwenye Hospitali hiyo leo Octoba 10,20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimsikiliza Mtoto Ernest Michael (6) Mkazi wa Nkuhungu Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma kwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuangalia Changamoto mbali mbali ziliopo kwenye Hospitali hiyo leo Octoba 10,2019. kulia Michael Yohana Baba wa Mtoto huyo.










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiangalia Mti wa Mkeshia alioupanda kwenye eneo la Mzakwe Makotopora Jijini Dodoma wakati alipofanya Ziara ya Kustukiza kuangalia maendeleo ya Ukuaji wa Miti 276 iliyopandwa katika eneo hilo leo Octoba 10,2019 ambapo ameridhika na utunzaji wa Miti hiyo unaofanywa na Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT. Kulia Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi Kushoto Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhandisi Geoseph Malongo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza na Vijana wa Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT Makutopora wanaohusika na Utunzaji wa Miti iliyopandwa katika eneo la Mzakwe Makutopora Jijini Dodboma, wakati alipofanya Ziara ya Kushtukiza kuangalia maendeleo ya Ukuaji wa Miti 276 iliyopandwa katika eneo hilo leo Octoba 10,2019 ambapo ameridhika na utunzaji wa Miti hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amemuagiza Meneja Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu TFS Kanda ya kati Dodoma Bibi Tebby Yoramu kufuatilia Utafiti wa Udongo kwenye eneo la Mzakwe Makutopora Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipofanya Ziara ya kushtukiza kuona maendeleo ya ukuaji wa Miti ya aina mbalimbali iliyopandwa katika eneo lindwa la Hifadhi ya Chanzo cha Maji linalotunzwa na Jeshi la kujenda Taifa JKT Makutopora ambapo amesema kuwa azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani ipo pale pale.

Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora, Wakala wa Misitu Tanzania na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti iliyopandwa mwezi Desemba 2017 inastawi Vizuri.

“Vitabu vya dini vinasema Moja kati ya sadaka endelevu ni kupanda miti, miti hii imekuwa na kustawi kwasababu ya jitihada zenu za kuimwagilia na kuitunza, msikate tamaa, endeleeni na kazi hii njema ambayo matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mifumo ya hali ya hewa ambayo huimarisha shughuli za kilimo na maendeleo ya viwanda.” Alisisitiza Makamu wa Rais

Nae Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kuwa miti 2300 ilipandwa tarehe 21/12/2017 na kati ya hiyo miti 2076 imekuwa na kustawi ikiwa ni sawa na asilimia 90.3 ya miti yote iliyopandwa.

“Katika miti iliyooteshwa awali baadhi haikuota, hivyo tumefanya jitihada za kuirudishia, tumepanda takriban miti 300 ya ziada” alisema Luteni Kanali Mbanga.Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha tafiti zinakamilika mapema kutoka katika sampuli ya udongo iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika eneo hilo na Jiji la Dodoma kwa Ujumla.

Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 21/12/2017 katika eneo la Mzakwe Jijini Dodoma ambapo miti 2300 ilipandwa siku hiyo.

Hayo yamesemwa leo mara baada ya kutembelea shamba la miti lililopo katika eneo la Mzakwe katika Kambi ya Jeshi la Makutupora Jijini Dodoma, ikiwa ni ufuatiliaji wa Kampeni aliyozindua mwaka 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya Ziara ya Kushtukiza katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuangalia Changamoto mbalimbali ziliopo kwenye Hospitali hiyo, na kuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo kushuhulikia na kusimamia vizuri matumizi ya fedha kwa ajili ya mahitaji yaliyopangwa.

Tanzania kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka Israel

0
0
Na Mwandishi wetu,

Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe, kundi la kwanza la watalii hao lililokuwa na zaidi ya watalii 200 wamewasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 mwezi Oktoba.

Kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya makampuni ya uwakala wa utalii kukamilisha taratibu za safari zao.

“Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi” Taarifa inasomeka.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kuwa, Tanzania imejipanga
kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini.

“Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda”. Taarifa inasomeka.

Mwezi Aprili 2019, Serikali ilipokea watalii 1,000 kutoka Israel. Aidha, mwezi Mei,2019 serikali pia ilipokea watalii 330 wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji kutoka jimbo la Zhejiang, China ambao waliwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, KIA. Watalii hao walikuwa ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 ambao wanatarajiwa kutembelea Tanzania mwaka huu 2019.

TIB CORPORATE BANK YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Benki ya TIB Corpotare wamekata keki na kusherehekea kwa pamoja na wateja wao katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Hayo yamefanyika leo katika matawi tofauti ya benki hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.



Akizungumza baada ya kumaliza kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja,Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka amesema kwa mwaka huu wameleta huduma ya JIPANGE inayomwezesha mteja kuweka akiba na kujipatia faida.



Amesema, mbali na hilo jukumu lao ni kuona wateja wao wanapata huduma bora za kibenki na sio bora katika mlengo mbalimbali.



Theresia amesema, huduma ya JIPANGE inamuhusu mzazi, mtoto, Kijana, Mzee na hata kama kampuni inayotoa huduma kwa jamii.

ATE YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUPATA MREJESHO WA WANACHAMA WAKE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) imeanzisha wiki ya huduma kwa wanachama ili kuwapatia fursa kwa wanachama kutoka sekta mbalimbali kuwapatia mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na chama hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema Mwezi wa Oktoba ni maalumu kwa wiki ya huduma kwa wateja kimataifa, nao kwa mara ya kwanza wameamua kuanzisha wiki ya mwanachama ili kufahamu kwa undani shughuli mbalimbali zinazofanywa na ATE kwa niaba yao.

Amesema, Wiki hii ya huduma kwa Wanachama imeanza rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 7 Oktoba 2019 na itahitimishwa siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Oktoba 2019 ambapo dhamira ya kufanya uwepo wa wiki hii ni
Kutoa fursa kwa wanachama wetu kutupatia mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na ATE 

Aidha, Mlimuka amesema wiki hii wataitumia kwa Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama wao ya nini kifanyike au kipi kiboreshwe ili kuifanya ATE kuendelea kuwa Sauti ya Waajiri nchini mwetu.

Mlimuka ameongeza kuwa, watatumia pia kusikiliza na kutoa ushauri kwa wanachama Na rasmi kutakuwa na utaratibu wa kila wiki kutoa Taarifa Muhimu kuhusu masuala ya Sheria za Kazi na Mahusiano sehemu za kazi lengo ni kuwaelimisha waajiri kuhusiana na sheria hizi.

Amesema, dhumuni la kutoa raatifa hizo ni ikiwemo na kuepuka migogoro ya mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi na kujenga mahusiano sehemu za kazi mambo ambayo yataleta tija na kuongeza uzalishaji na hatimaye kukuza ustawi wa uchumi wetu. 

Mlimuka ameeleza, taarifa hiyo muhimu itakuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za kupeana taarifa kama vile barua pepe (emails), Tovuti ya ATE (website) pamoja na njia nyingine kama mitandao ya kijamii lengo ni kuwafikia wanachama wengi zaidi.

"Napenda kutumia muda huu kupitia vyombo vyenu vya habari kuwashukuru wanachama wote wa ATE waliopo nchi nzima kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakitupatia katika kutekeleza mambo mbalimbali yaliyo kwenye kalenda ya Chama Chetu," amesema mlimuka.

"Niwaombe tu waweze kutumia wiki hii ya Huduma kwa Wanachama kuwasiliana nasi au kufika kwa wingi moja kwa moja kwenye ofisi zetu za makao makuu zilizopo Mikocheni barabara ya Coca-Cola pamoja na ofisi zetu za kanda zilizopo Rock City Mall Mwanza na AICC Arusha ili wataalamu na watoa huduma wetu waweze kuwahudumia,"

Wiki ya huduma kwa wateja imekuwa ikiadhimishwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chama chao kuanzisha wiki ya mwamachama itakayowawezesha Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama wao ya nini kifanyike au kipi kiboreshwe ili kuifanya ATE kuendelea kuwa Sauti ya Waajiri nchini mwetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa chama hicho.

TMA yatoa utabiri wa msimu wa mvua, yatoa taadhari kuepusha majanga

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini(TMA),mvua zinazotarajia kunyesha katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka zinatarajia kuwa za wastani hadi juu ya wastani zinazoweza kusababisha athari mbali mbali yakiwemo magonjwa ya mlipuko.

Mkurugenzi wa TMA, Dkt. Agness Kijazi, ameyasema hayo wakati akitoa utabiri wa muelekeo wa mvua za msimu Novemba hadi Aprili 2019/2020 na kusema kuwa mvua nyingi inatarajia kunyesha katika nusu ya kwanza ya msimu kutokana na uwezekano wa uwepo wa upepo kuvuma kutoka upande wa magharibi.

Amesema upepo huo unatarajia kubeba unyevunyevu Kutoka misitu ya Kongo kuelekea katika maeneo ya nchi yetu huku kwa upande wa kipindi cha nusu ya pili cha msimu mvua zinatarajiwa kupungua katika baadhi ya maeneo kutokana na joto la bahari sehemu ya kati ya bahari ya Hindi kuendelea kuongezeka ikilinganishwa na maeneo mengine ya bahari ya Hindi.

"Mvua za msimu ni mahsusi katika maeneo ya magharibu mwa nchi ,kanda ya kati ,nyanda za juu kusini magharibi,kusini mwa nchi,ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambapo maeneo haya yanapata msimu mmoja wa mvua ambazo zinaanza mwezi Novemba hadi Aprili ya mwaka unaofuata," amesema Dk.Kijazi

Amesema, katika mkoa wa Tabora mvua inatarajia kunyesha juu ya wastani hadi wastani  huku mkoa wa Kigoma na Katavi ikitarajiwa kunyesha mvua za wastani hadi juu ya wastani  na kutarajia kuanza wiki ya nne ya mwezi Oktoba 2019katika mkoa wa kigoma na kusambaa Kwa mikoa ya Katavi na Tabora katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.

"Mvua katika maeneo ya Singida na Dodoma zinatarajia kuanza katika wiki ya Kwanza hadi wiki ya pili ya mwezi Novemba 2019na maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani hadi wastani," alisema na kuongeza

"Katika mikoa ya Rukwa,Songwe,Mbeya,Iringa,Njombe,Ruvuma pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro mvua zinatarajia kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba 2019 na kutarajia kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi," alisema

Aidha alisema katika mikoa ya Lindi na Mtwara mvua zinatarajia kunyesha kati ya wiki ya kwanza na wiki ya pili ya mwezi Novemba 2019 na zinatarajia kuwa za juu ya wastani hadi wastani.

Dkt.Kijazi amesema, matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani.

Alisema migandamizo midogo ya hewa pamoja na vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi inatarajiwa kuvuta upepo wenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na hivyo kusababisha mvua katika maeneo mengi hapa nchini.

Aidha Dk. Kijazi amesema mvua hizo zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko, yanayohusiana na Maji hivyo ni vema tahadhari ikachukuliwa mapema kwa kumwaga madawa ya kinga na hatua zingine stahiki ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Pia mamlaka za maji na jiji zimeshauriwa kuchukua tahadhari hasa katika kuhakikisha miundombinu inabaki salama ili kuepusha kutuwama kwa maji na kusababisha mafuriko uharibifu wa miundombinu na upotevu wa maisha na mali.

TMA pia wamewashauri menejimenti ya afya kutoa taarifa Mapema kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni na miundombinu iwapo kutatokea uharibifu wowote ili kupunguza athari na hasara zinazoweza kutokea.

Aidha Dk. Kijazi ametoa ushauri Kwa watumiaji wote wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima,wafugaji,mamlaka za wanyamapori,sekta za maji na afya kuendelea kufuatilia na kutumia ushauri wa kitaalam katika shughuli zao za kila siku.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Dkt. Agnes Kijazi akizungumza wakati alipotangaza utabiri wa hali ya hewa kuhusu uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka katika makao mkuu ya mamlaka hiyo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam leo
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza utabiri wa hali ya hewa kuhusu uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka katika makao mkuu ya mamlaka hiyo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni , Bw. Samwel Mbuya Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri TMA na kushoto ni Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.



DAWASA Kinondoni yanogesha Wiki ya Huduma kwa Wateja

0
0
Ofisi ya Mkoa wa Kihuduma wa Kinondoni wa Mamlaka ya majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kukata keki na wateja wao.

Maadhimisho hayo ni katika kuhakikisha  wiki ya huduma kwa wateja inaenda sambamba na kuwasogeza wateja karibu zaidi.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza Oktoba 7 na Kumalizika Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yake ni kila mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka. 
 Meneja wa Dawasa mkoa wa Kinondoni, Christian Kaoneka  akikata keki pamoja na wateja wa Mamlaka hiyo wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yamefanyika katika ofisi za DAWASA Kinondoni leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango akishuhudia ukataji wa keki.
 Meneja wa Dawasa mkoa wa Kinondoni, Christian Kaoneka(kulia) akimpa kipende cha keki Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kushoto) wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yamefanyika katika ofisi za DAWASA Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
 Meneja wa Dawasa mkoa wa Kinondoni, Christian Kaoneka(kulia)  akiwagawia vipande vya keki wateja waliofika ofisini hapo kwa ajili ya kupata huduma wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yamefanyika katika ofisi za DAWASA Kinondoni leo jijini Dar es Salaam. 
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kulia) akiwalisha baadhi ya wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kinondoni wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango na Meneja wa Dawasa mkoa wa Kinondoni, Christian Kaoneka(walioshika keki)wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kinondoni wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.

ASKARI POLISI SITA KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA MKOANI TABORA

0
0
Na, Editha Edward, Globu ya Jamii - Tabora 

Askari polisi sita wa kituo cha polisi Igunga pamoja na Mwenyekiti wa kitongoji cha Isakamaliwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani na Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU  mkoani Tabora kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa zaidi ya Shilingi milioni nane na laki nne kwa wananchi wawili ili wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria 

Kwa mujibu wa kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora Mussa Chaulo amesema Askari hao wote sita kwa kushirikiana  na viongozi hao wawili wa serikali ya kijiji hicho cha Isakamaliwa kwa pamoja walishirikiana kuomba na kupokea rushwa hiyo kwa wananchi wawili akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 95 ili wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria wakiwatuhumu kwa kujihusisha na Imani za kishirikina na kumiliki silaha ya moto pamoja na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo
Katika mwendelezo wa jitihada hizo za kupambana na rushwa taasisi hiyo imefuatilia miradi 14 ya maendeleo katika kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2019 yenye thamani ya Shilingi bilioni moja milioni thelathini na nne laki saba tisini na nane elfu miambili sabini na tisa katika Sekta za afya, elimu, maji na Ujenzi wa masoko ambapo ufuatiliaji wa miradi hiyo ulibaini kuwepo na viashiria vya ukiukwaji kwa utaratibu kwenye utekelezaji wa mradi mmoja wa Ujenzi wa soko hivyo imeanzisha uchunguzi kuona kama kuna vitendo vya rushwa katika mradi huo

Aidha taasisi hiyo ya kupambana na rushwa imeendelea kusisitiza kuwa imejipanga vyema kuwashughulikia wale wote watakao jihusisha na vitendo vya rushwa katika Uchaguzi wa serikali za mitaa na hata utendaji Mzima wa Shughuli za uma

"hatuta mvumilia mtu yeyote atakae jihusisha na vitendo vya rushwa hatua sitahiki za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae jihusisha katika Uchaguzi ni fursa tunayopata kwa ajili ya kuwachagua viongozi, wananchi tutumie fursa hii ya Uchaguzi kuchagua viongozi waadilifu "Amesema Chaulo.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI WA MPANDA KATAVI MKOANI RUKWA

0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mpanda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya kuwahutubia.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga mara baada ya kuhutubia katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi
 Wanakwaya ya Agape wakitumbuiza katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili uwanjani hapo.
  Kwaya ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpanda Girls wakitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili uwanjani hapo.
Kwaya ya Manispaa ya Sumbawanga ikitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika uwanja wa Azimio mkoani Katavi. PICHA NA IKULU

DAWASA Kawe yasherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja

0
0
 Ofisi ya Mkoa wa Kihuduma wa Kawe wa Mamlaka ya majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kukata keki na wateja wao.

Maadhimisho hayo ni katika kuhakikisha  wiki ya huduma kwa wateja inaenda sambamba na kuwasogeza wateja karibu zaidi.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza Oktoba 7 na Kumalizika Oktoba 11 na maadhimisho yake ni kila mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka. 
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango akikata keki na wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kawe wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yamefanyika katika ofisi za DAWASA  Kawe leo jijini Dar es Salaam.
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kushoto) akilisha keki Afisa Biashara DAWASA mkoa wa Kawe Jimmy Chuma(kulia) wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kushoto) akilisha keki Afisa wa DAWASA mkoa wa Kawe, Violet Mgeta(kulia) wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.

Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kushoto) akilishwa keki na Afisa wa DAWASA mkoa wa Kawe, Peresy Mzonya(kulia) wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.
Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango(kushoto) akiwalisha keki wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kawe wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.
 Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Doreen Kiwango akiwa kwenye icha ya pamoja na wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kawe wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika Oktoba 11, 2019.
Wafanyakazi wa DAWASA mkoa wa Kawe wakijipiga "selfie"  kwa furaha ya kuwahudumia wateja wao.

AFISA TARAFA ITISO ATOA ONYO KWA WANANCHI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

0
0

AFISA Tarafa wa Itiso, wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Remidius Emmanuel amewataka wananchi waishio katika Kijiji cha Chenene wilayani humo, kutunza miundombinu ya maji na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini wananchi wachache wanao hujumu miundombinu hiyo.

Remidius ameyasema hayo katika mkutano wa Wananchi wa Kijiji hicho walipokuwa wakitoa mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini hapo. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo pia ulilenga kuhamasisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika orodha ya Daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Pia mkutano huo ulilenga kutoa mrejesho wa hatua mbalimbali za utekelezaji na utatuzi wa kero zinazowakabili wanakijiji hicho.

Mapema Remidius amesema uwepo wa Meneja wa RUWASA mkoa wa Dodoma Dk. Godfrey Mbabaye, viongozi wenzake na wataalamu wengine kutoma RUWASA katika mkutano huo ni hatua muhimu ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, .Binilth Mahenge kuhakikisha mkanganyiko uliopo katika mradi wa maji kijijini hapo unatatuliwa.

Julai 9, .2019 Dk. mahenge akiwa katika ziara ya Kijazi Wilayani Chamwino katika kata ya Haneti aliagiza uongozi wa RUWASA kufika kijijini hapo kusikiliza madai ya wananchi juu ya mfumo wa kisima cha maji ili watoe majibu na ufafanuzi wa kitaalam na kutatua kero zote zinazojitokeza katika mradi wa maji kijijini hapo.

Dk. mahenge alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mmoja wa wananchi waliohitaji kujua ni lini kero yao hiyo itapatiwa ufumbuzi.

Akizungumza baada ya kutembelea kisima cha maji kijijini hapo,Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk. Godfrey amesema tatizo kubwa lililoleta mkanganyiko kwa wananchi hao ni kutokana na ukosefu wa taarifa za uhakika juu ya mradi huo hatua iliyoleta sintofahamu miongoni mwa wananchi hao.

" Hatuwezi kupuuza malalamiko ya wananchi hawa, wataalamu wetu watapiga kambi kupitia upya mfumo wa mashine na kisima chenu, tunasisitiza sana pale mnapobaini tatizo katika mradi huu hakikisheni mnatoa taarifa kwa wataalam wetu na kuepuka kutumia watu ambao hawana ujuzi na mifumo ya miundombinu ya visima vyenu. " Amesema Dk. Mbabaye.

Akifafanua juu ya dhana ya ongezeko la matumizi ya mafuta katika mashine ya maji amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa pump unaoendeshwa na mashine kwenda mfumo wa Umeme (Submersible Pump) mabadiliko hayo yanaendana na ongezeko la mafuta ingawa amesema kufuatia matarajio ya umeme katika Kijiji hicho kutasaidia kumaliza kabisa utumiaji wa mafuta.

"Viongozi hawa wanaposhindwa kutimiza wajibu wao na mimi kama kiongozi wa Tarafa ninakuwa sehemu ya tatizo, kwa hiyo niombe radhi kwa makosa yaliyofanywa na uongozi wa kijiji.Lakini naleta masikitiko yangu kwenu.

Kabla ya uongozi wa kijiji kusoma mapato na matumizi ya kijiji hicho, Diwani wa kata hiyo Mhe. Peter Chidawali amewahakikishia wananchi wa Chenene kwamba kero zote zote zinazokabili kijiji hicho tayari zimetatuliwa na nyingine zikiendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi ikiwa ni pamoja na Malipo ya miezi tisa (9) mnara wa TTCL kwa kijiji hicho jambo ambalo lipo katika hatua za mwisho na hii ni baada ya kuwasiliana na Uongozi wa TTCL mkoa wa Dodoma,Alisema Chidawali.

Kwa upande wake Mkaguzi wa polisi wa Tarafa ya Itiso Insp.Makweba Misana amewataka wananchi hao kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu na amesema watahakikisha wanawatia nguvuni wale wote walioshiriki kuhujumu miundombinu ya maji kijijini hapo.

Mbali na kijiji cha Chenene, ujumbe wa RUWASA ulitembelea kijiji cha Haneti na kufika katika Kisima cha maji baada ya kupokea taarifa za kuharibika kwa pampu ya maji iliyopelekea sehemu ya kijiji hicho kukosa maji.
 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Chenene  wakati wa kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini hicho kilichopo Tarafa ya Itiso
 Mkaguzi wa Polisi Tarafa ya Itiso Insp.Makweba Misana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chenene wakati wa kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini hicho kilichopo Tarafa ya Itiso
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dr.Godfrey Mbabaye akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chenene (Tarafa ya Itiso)  wakati wa kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini hicho kilichopo Tarafa ya Itiso
 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akiteta jambo na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Chamwino Mhandisi Christina Msengi  wakati wa kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini Chenene kilichopo Tarafa ya Itiso
 
 Baadhi ya Wanachi walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Chenene ili kupata mrejesho wa utekelezaji wa kero za wananchi kijijini Chenene kilichopo Tarafa ya Itiso
 Afisa Tarafa itiso Remidius Emmanuel Akifafanua jambo katika kisima cha kijiji cha Haneti baada ya Meneja wa RUWASA Mkoa we Dodoma Dr.Godfrey Mbabaye  akiongozana na ujumbe wake kufika katika eneo la kisima.

NDITIYE AZINDUA UUNGANISHAJI WA SHULE ZA SIMIYU KWENYE INTANETI

0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akibonyeza kitufe kuzindua uunganishaji wa mtandao wa intaneti kwenye kompyuta zilizotolewa na UCSAF na Vodacom kwenye shule za sekondari za mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akimkabidhi mwalimu wa shule ya sekondari Itilima, Flora Shimbi kompyuta mpakato na kifaa maalumu kwa ajili ya kuunganisha shule za sekondari za mkoa wa Simiyu kwenye mtandao wa intaneti. Tukio hilo limefanyika sekondari ya Simiyu mkoani humo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa huo kabla ya uzinduzi wa uunganishaji wa shule kwenye mtandao wa intaneti na kompyuta walizopewa na UCSAF na Vodacom. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.


Na Prisca Ulomi, Simiyu

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amezindua uunganishaji wa shule za sekondari za Mkoa wa Simiyu kwenye mtandao wa intaneti kwa kuzifunga kompyuta mia moja zilizotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kompyuta za mpakato ishirini zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kwenye mtandao wa intaneti ili wanafunzi waweze kutumia huduma ya mtandao kujifunza na waalimu kufundishia kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Nditiye amesema kuwa mradi huu ni mwendelezo wa kazi ya UCSAF kwa kupanua wigo wa mtandao wa intaneti mashuleni ili kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanatumia mtandao wa intaneti kusoma, kupata maarifa na kujiendeleza.

“Leo tunazindua uunganishaji huu kwa shule kumi za sekondari za mkoa wa Simiyu ambazo zilipewa kompyuta hizo na UCSAF na Vodacom watakabidhi kompyuta mpakato mbili kwa kila shule pamoja na kifaa maalumu cha kuunganisha huduma ya intaneti kwa shule zote kumi,” amesema Nditiye.

Nditiye amewapongeza waalimu kwa kuwa wamekuwa wakikaa na wanafunzi kwa muda mrefu kwa siku nzima hata kwa wanafunzi wanaosoma shule za kutwa kuliko hata sisi wazazi.

“Niwaombe waalimu mtumie vifaa hivi kufundishia wanafunzi nanyi waalimu kujifunza badala ya kuviweka kwa kuogopa vinapata vumbi, mvitunze ili visiharibike kwa kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kununua,” amesisitiza Nditiye.

Vile vile, ametoa rai kwa kampuni nyingine za simu za mkononi kutoa vifaa vyaTEHAMA kwa shule ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya intaneti ili waweze kujifunza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema kuwa kompyuta
zilizogawiwa hazitakaa stoo, zitatumika na kompyuta hizo zitakuwa enki ya mitihani yote na itawezesha wanafunzi wa mkoa kufaulu a wanufaike na intaneti na TEHAMA.

“Tuna amini kuwa kila halmashauri kuna Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano nah iiitatusaidia kwa wanafunzi wetu kupata mafunzo kwa kuwa tayari nchi ipo kwenye kiganja na tuna intaneti ya Vodacom ambayo tutaitumia bure kwa mwaka mmoja” amesema Mtaka.

Naye Mbunge wa Maswa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameishukuru UCSAF kwa kuupatia Mkoa wa Simiyu kompyuta 100 ili wanafunzi waweze kusoma kwa njia ya mtandao ambapo itawaongezea kiwango cha ufaulu“Tumeona juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe.

Magufuli kusema elimu bure zinasaidia watoto wetu kufaulu, nawapongeza waalimu, mnakaa na watoto wetu, kazi yenu ni ya wito, mnawajua watoto wetu, mimi ni motto wa mwalimu na mjukuu wa mwalimu, watoto wetu tukiwafundisha vizuri TEHAMA tutawapeleka mbele zaidi, na dunia ya sasa ni tofauti na wakati wetu tuliosoma, hivyo mna mazingira mazuri nah ii ni fursa ya ninyi kusoma zaidi,” amesisitiza Nyongo.

Akizungumza kabla hajakabidhi kompyuta mpakato 20 na vifaa vya kuunganishaintaneti kwa shule za sekondari 10 mkoani humo, Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, Roselyn Mworia amesema kuwa Vodacom imetengeneza tovuti ambayo itawasaidia kujifunza zaidi ili wanafunzi waweze kufaulu kwa kuwa ina masomo tofauti na mitaala tofauti na tovuti hii ni bure itawasaidia kusoma na kufanya marejeo ya masomo yao.

Naye mwalimu wa shule ya sekondari ya Mkodilana mkoani humo, Joseph Kazimoto amesema kuwa wanamshukuru Mkuu wa Mkoa wao, Mataka kwa kuanzisha kambi ya kuwakusanya wanafunzi kutoka shule mbali mbali mkoani humo na huduma ya intaneti itawawezesha kuongeza ufaulu na wana amini watashika namba moja kitaifa kwa kuwa mwaka jana walishika nafasi ya tisa kitaifa kwa matokeo ya kidato cha nne.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Meatu, Daudi Mussa amemshukuru Mataka na wageni waliofika shuleni kwa kuwa wamehamasika kusoma na kufaulu zaidi na wameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwaweka kambi wanafunzi wote wa mkoa huo kwa kuwa wanawasaidia kuandaa maisha yao na kupata mbinu za kujibu maswali na sio kukariri.

Huduma hiyo ya mtandao wa intaneti imetolewa na kampuni ya Vodacom kwa muda wa mwaka mmoja kwa kuzipatia shule za sekondari kumi za Mkoa wa Simiyu kifaa maalumu cha kutoa huduma hiyo kwenye shule hizo. Shule za sekondari ambazo kompyuta zake zitaunganishwa kwenye huduma ya intaneti ni shule ya sekondari ya Simiyu, Maswa, Dutwa, Binzwa, Anthony Mtaka, Meatu, Nasa, Mwandoya, Itilima na Kanadi.

MISITU YA TFS YAONGEZA UZALISHAJI WA ASALI NCHINI

0
0
 Afisa Nyuki wa wakala wa huduma za misitu(TSF) wilaya ya Shinyanga,Franael Sumari akionesha asali na nta waliyozalisha mwaka huu

Afisa habari na uenezi wa TFS kanda ya Magharibi,Karimu Solyambingu akionesha mtambo wa kutengeneza Nta katika misitu ya TFS Shinyanga.
Mlinzi ofisi za TFS nzega akionesha baadhi ya mizinga ambayo inaendelea kusambazwa katika wilaya hiyo.
 *************

Na Mwandishi wetu, Arusha
Uzalishaji wa Asali na nta  chini, umeongezeka katika Misitu inayosimamia na Wakala wa huduma za  Misitu Tanzania(TFS) kutokana na kuboresha uhifadhi wa mazingira na  wananchi wengi kupata elimu ya kufuga nyuki.

Afisa Habari na uenezi wa TFS Kanda ya Magharibi, Karimu Solyambingu akizungumza na waandishi wa habari, alisema ongezeko la uzalishaji huo wa asali pia limechangia udhibiti wa uhabifu wa mazingira  katika hifadhi za  misitu unaendelea kufanywa na TFS maeneo mbalimbali nchini.

"katika misitu ya hifadhi inayosimamiwa na TFS kanda ya Magharibi,  katika wilaya za Sikonge, Shinyanga,  Nzega  na hata eneo la Manyoni uzalishaji wa asali na nta umeongezeka sana"alisema

Ramadhani mzirai Meneja wa TSF wilaya ya Shinyanga alisema,uzalishaji wa asali katika misitu ya TFS katika wilaya hiyo, umeongezeka kutoka  kilo 130 mwaka 2017/19 hadi kufikia kilom 700 mwaka 2018/19.

"ongezeko hili halijawahi kutokea katika misitu yetu kwani pia tumepata zaidi ya kilo 15 za nta na tumeweza kuwa na mizinga 140 ambayo inazalisha lakini pia wananchi 264 kutoka vijiji 13 tuliwapa elimu na wanafuga nyuki kisasa"alisema

Bibi nyuki wa  kituo cha TFS wilaya ya Manyoni, Jackline Leshabari alisema alisema  uzalishaji wa asali umeongezeka wilayani Manyoni,kutoka tani  1.7 mwaka 2017/18 hadi kufikia tangi 3.2 mwaka 2018/19.

"ongezeko hilo limetokana pia na kiasi cha mvua cha wastani ambacho kilinyesha msimu uliopita ambacho kiliwezesha nyuki kupata maua kwa wingi na maji kwa ajili ya kutengeneza asali "alisema

Mkuu wa TFS wilaya ya Sikonge, Haji Abdalah alisema  kumekuwepo  na ongezeko kubwa la uzalishaji wa asali katika misitu iliyohifadhiwa katika wilaya hiyo na mwaka 2018/19 hadi kufikia tani 100.

"katika misitu hii sasa kuna zaidi ya wafugaji 1000 wanaendesha ufugaji wa kisasa lakini pia sisi kama TFS tumekuwa tukishirikiana nao katika kuandaa mizinga na kuwapa elimu ya ufugaji nyuki "alisema

Yuda Zebedayo ambaye ni mmoja wa wafugaji wakubwa wa nyuki wilaya ya Sokonge alisema mwaka huu anatarajia kuwa na asali  zaidi ya 120  kutokana na kuwepo msimu mzuri katika misitu ya wilaya hiyo.

Katika wilaya ya Nzega Katibu wa mbunge wa jimbo la Nzega vijijini, Basirio Lazaro alisema uzalishaji wa wilaya hiyo, inaendelea kuongezeka hasa baada ya TFS kuwapa  mizinga mipya 300 katika vikundi vya ufugaji nyuki.

Lazaro alisema kila kikundi kimepewa mizinga 20 na sasa wameanza kuvuna asali na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu, kuwa na mavuno makubwa.

"tunapongeza TSF na Waziri wa Maliasili na Utalii, ambaye ni mbunge wetu, Dk Hamis Kigwangalla kwa kazi nzuri ambayo wanafanya hapa nzega kuwahakikisha maisha bora wananchi kupitia asali badala ya kutegemea kilimo pekee"alisema.

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu.

0
0
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano katika ngazi hiyo ulikuwa wa siku mbili na umemalizika leo.

Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.

Pichani; wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Rwanda, Balozi Richard Masozera akiongoza mkutano huo, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara inayoshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Bw. Rafael Kanoth. 
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini taarifa ya mapendekezo mbalimbali katika mkutano huo kwaajili ya kuwasilisha taarifa hiyo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akishuhudia zoezi la utiaji saini. 
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban pamoja na Dkt. Ndumbaro na Prof. Mchome wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. 
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen P. Mbundi pamoja na wajumbe wengine wa mkutano wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. 
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kushoto) pamoja na sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wakifuatilia majadiliano. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano katika mkutano. 
Viongozi wa ujumbe wa mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wakikamilisha zoezi la utiaji saini wa taarifa ya mapendekezo ya mkutano huo. 

RAIS DKT MAGUFULI AWAFUTA MACHOZI WAFUGAJI

0
0
RAIS Dk. John Pombe Magufuli amewafuta machozi wafugaji wa Tanzania baada ya kuamuru wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji 920 vilivyokuwa ndani ya Hifadhi kutoondolewa na kuendelea shughuli zao za ufugaji na kilimo na kuondokana na kadhia ya kukamatwa , kuchomewa nyumba zao na kupigwa faini kubwa kila siku na Maafisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara yake inayoendelea Mikoa ya Rukwa na Katavi, Rais Magufuli amesema kwa miaka mingi wafugaji Tanzania wamekuwa wakiishi kwa manyanyaso makubwa jambo ambalo Serikali anayoiongoza kamwe haitakubali liendelee.

Rais Magufuli amesema asilimia 32.5 ya nchi ya Tanzania ni hifadhi huku idadi ya wananchi na shughuli za ufugaji na kilimo zikiendelea kuongezeka siku hadi siku na kutumia eneo lilibaki la asilimia 68 tu huku maeneo mengine ya nchi yakiwa ni mito, maziwa hivyo eneo lililokuwa limebaki kwa ajili ya matumizi ya binadamu lilikuwa dogo na ndio maana kumekuwepo na migogoro baina ya wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa ardhi.

“Mtu ukienda kwenye shamba fulani umevamiwa, wananyanyaswa wananchi saa nyingine na kupigwa faini za ajabu ajabu umeingiza ng’ombe zako kuchunga zinashikwa..unataka ukachungie wapi ng’ombe wanaoshika ..nyama wanataka na maziwa wanataka lakini ng’ombe wanakupiga faini imekuwa ni nchi yenye migogoro”alisema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli akabainisha kuwa watu waliopewa dhamana ya uongozi kwa bahati mbaya hawakutumia nafasi zao kutafuta suluhu ya migogoro hiyo badala yake wakawa wanatumia nguvu katika kutatua na kusababisha manyanyaso makubwa kwa wananchi .

“Bahati mbaya sisi hatukutumika kama njia mbadala ya kutatua migogoro tukawa tunatumia nguvu katika kutatua migogoro tunaenda porini mle tunawafyeka watu kwa kuchoma mazao yao wakinamama wanalia hawa ni watanzania ni wazalishaji wazuri ni wafugaji na wakulima hapakuwa na sababu ya kuwa tunaenda tunawafukuza kila mahali kwa sababu....sababu za msingi zingine zipo kwamba ardhi haitoshi”alisema Rais Magufuli.

Dk. Magufuli akafafanua kuwa ndio maana ilimlazimu kuunda timu ya mawaziri 8 kwani aliapa kuwatumikia watanzania masikini wakiwemo hata hao waliovamia maeneo na kamwe hatokubali watu waonewe na kusisitiza kuwa timu hiyo ya mawaziri imefanya kazi nzuri sana kwa kuzngukia maeneo mbalimbali nchini yaliyokuwa na migogoro wakaja na mapendezo vijiji 920 vilivyokuwa ndani ya hifadhi tukaamua vibaki.

“Tukaamua vijiji vibaki humo wala wasiondolewe humo, tukaamua mapori tengefu 12 tuyafute, misitu ya hifadhi 7 iliyokuwa imepoteza sifa zibaki kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za makazi , kilimo na mifugo tukaamua kumega hifadhi za misitu 14 kwa ajili ya kilimo na kufuta mashamba 16 ambayo yalikuwa hayaendelezwi na hayo ndio yalikuwa maelekezo yangu”alisema Rais Magufuli.

Hivyo wananchi wa vijiji hivyo wataendelea kuishi humo na sio hifadhi tena na kuwaonya watu wa hifadhi waliokuwa waenda kuwasumbua wananchi wasisogee kabisa katika vijiji hivyo na kusisitiza kuwa uamuzi huo umefanywa kwa kutambua shida za wananchi.

Pia ameonya kuwa uamuzi uliofanywa na Serikali wa kuvibakiza vijiji hivyo isiwe chanzo cha wananchi kuvamia tena hifadhi na kutaka kuongezewa vijiji vipya kwa Serikali yake haitaongeza tena kijiji kingine.

“Msije mkasema na huku tukivamia tutaachiwa mkivamia utatolewa kwa nguvu , utatolewa kwa kuvamiwa hivyo hivyo ni lazima tusemezane ukweli, msema kweli ni mpenzi wa Mungu ..uongozi wa Mkoa na Wizara ya Ardhi ikapange vizuri matumizi ya ardhi ili isiwe sababu tena ya kwenda kugombanisha watu wale watu wenye maeneo yao waendelee kubaki na maeneo yao kama alikuwa na eneo kubwa basi ni bahati yake imemkuta huko asitokee tena mtu alikuwa na ekari 20 ukampunguzia akawa na ekari 5 hapana aliyewahi kawahi, aliyechelewa shauri yake”alisema Dk. Magufuli

Hivyo aliwataka wananchi walionufaika na ardhi hiyo kuitumia vizuri kwa ajili ya shughuli za uzalishaji wa mifugo na kilimo ili waweze kupata manufaa makubwa na kutajirika kwani Serikali ya awamu ya tano sio ya kutesa watu.

‘Mkatajirike ndugu zangu huu ndio wakati wa kutajirika, awamu hii ya tano si awamu ya kutesa watu ni awamu ya kuwatajirisha watu”alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwa kiongozi pekee wa Tanzania aliyekubali kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na kumhakikishia kuwa kazi ya kulinda soko la ndani la bidhaa za mifugo na uvuvi inafanyika vizuri na kwamba mianya yote imezibwa na makufuli na hakuna tena mtu atakayechezea soko la Tanzania.

Waziri Mpina amesema pia wafugaji wengi wa mikoa ya Rukwa na Katavi wamekuwa wakiteseka kwa kukosa soko la mifugo yao kutokana na kiwanda cha SAAFI kilichopo mkoani Rukwa kutofanya kazi ipasavyo na kumthibitishia Rais Magufuli kuwa Serikali itafanya jitihada zote kuhakikishia kiwanda hicho kinafanya kazi vizuri ili wafugaji wa mikoa hiyo wapate soko la uhakika la mifugo yao.

AMSHURUKU RAIS MAGUFULI KWA KURUDISHIWA SHAMBA LAKE

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Losinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Martha Kuzilwa (94) ambaye ameporwa shamba lake. 

*****************************

Mkazi wa Kijiji cha Losinyai Kata ya Oljoro Namba 5 Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Martha Kuzilwa (94) amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuingilia kati mgogoro wa shamba lake lenye ukubwa wa ekari 300 iliyoporwa na vigogo wa kijiji hicho na kuagiza arudishiwe. 

Kuzilwa amemshukuru Rais Magufuli baada ya Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kufika nyumbani kwake na kumpa maagizo ya Rais Magufuli kuwa atapewa eneo lake lililoporwa.

Awali, Mnyeti alisema amefika nyumbani kwa Kuzilwa baada ya Rais Magufuli kumuagiza amsikilize na kumpa haki yake. Mnyeti alisema baada ya kuwepo mgogoro wa muda mrefu baina ya Kuzilwa na wavamizi hao wa ardhi alipeleka kilio chake kwa Rais Magufuli ambaye ameagiza apatiwe shamba lake. 

“Nimefika hapa nimemsikiliza huyu mama na viongozi wa kijiji wamekiri shamba ni lake hivyo namuagiza mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula, ikifika ili jumamosi ijayo akamkabidhi rasmi shamba lake,” alisema Mnyeti. 

Hata hivyo Kuzilwa alimshukuru Rais Magufuli kwa kuagiza arejeshewe shamba lake ekari 300 alilokuwa analimiliki tangu mwaka 1990 kisha akaporwa na kutishiwa maisha.

Alisema kila mara amekuwa akitishiwa maisha yake na watu watatu waliopora eneo lake la ekari 300 na kumuachia ekari 50 pekee. 

Pia, alimshukuru Mnyeti kwa kufika eneo hili na kumsaidia baada ya agizo la Rais Magufuli kwani hati zote anazo za kuhakikisha shamba hilo ni lake kihalali. “Mimi ni mwanachama wa CCM tangu enzi ya TANU hawa watu walikuwa wanataka kuniua sababu ya kunidhulumu shamba langu ambalo nimepata kihalali japokuwa kuna vigogo walikuwa wanawasaidia,” alisema. 

Alisema baadhi ya wavamizi wamejenga nyumba kwenye shamba hilo ambalo alilipata kihalali na ana hati halali za umiliki wake. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula aliahidi kutekeleza agizo hilo kwa kumkabidhi shamba hilo jumamosi ijayo baada ya kumalizika kwa ziara ya mkuu huyo wa Mkoa. 


NITARUDI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KWA MBWEMBWE-PROFESA KABUDI

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa akimaliza muda wa kuitumikia nafasi aliyochaguliwa na Rais Dkt. John Joseph Magufuli hatapata tabu kurudi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuendelea kufundisha masomo ya sheria kama awali. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na Uongozi Institute kwa kushirikiana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kabudi amesema kuwa katika awamu hii ya tano cheo ni dhamana na yeye hatapata tabu kurudi chuoni hapo wakati ukifika . 

"Mwenda tezi na omo....Marejeo ngamani, sitapata tabu kurudi chuoni hapa kwa kuwa katika awamu hii cheo ni dhamana na sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho. Chuo cha Dar es Salaam ni nyumbani, nikimaliza ngwe hii nitarudi kwa mbwembwe" ameeleza Prof. Kabudi. 

amesema kuwa wakati tukimuenzi baba wa taifa lazima tukumbuke tunu alizotuachia ambazo zilikuwa katika mfumo wa kiitikadi na uadilifu, amesema kuwa masuala ya utu, usawa, uwajibikaji, uadilifu, uzalendo, maadili na umoja ndio mambo yanayoendelea kuliweka taifa letu kuwa kisiwa cha amani na utulivu na ni vitu ambavyo Mwalimu Nyerere ametuachia. 

vilevile amesema kuwa miaka 20 bila Mwalimu Nyerere taifa limeendelea kumuenzi hasa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali kwa ujumla wameendelea kuthamini na kusimamia misingi aliyoiweka Mwalimu ili kuhakikisha taifa linabaki salama na kuwa maendeleo endelevu. 

"Miaka 20 baada ya Mwalimu kifo cha Mwalimu tunu zimeendelea kuimarishwa kupitia Serikali ya Rais Magufuli, masuala kama maji, elimu, afya na uimarishwaji wa miundombinu mbalimbali umeendelea kuimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini" ameeleza. 

Prof. Kabudi amesema kuwa viongozi lazima wafuate miiko na maadili katika kuwatumika wananchi bila kujali vyeo vyao bali kwa kuzingatia maadili, uwajibikaji ili kuweza kumuenzi Mwalimu kwa vitendo zaidi. 

kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya Siasa akiwemo katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Anna Makinda, Jaji Damiani Lubuva na viongozi wa dini na taasisi mbalimbali. 

HAKUNA WA KUBADILI UKOMO WA URAIS-PROFESA KABUDI

0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kubadili ukomo wa urais wa awamu mbili huku akisisitiza hilo haliwezekani katu.

Profesa Kabudi amesema hayo leo wakati akifungua kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere ambapo mada kuu ilikuwa inasema miaka 20 baada ya Mwalimu.Profesa Kabudi alikuwa amemuwakilisha Rais Dk.John Magufuli ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Wakati anatoa hotuba yake Profesa Kabudi amesema kuwa hakuna wa kubadili awamu mbili za uongozi wa urais."Tutaendelea na vipindi viwili vya ukomo wa urais, na kesi iliyofungulia na moja ya raia wa Tanzania kuhusu ukomo wa Rais, isihusishwe na Rais wa sasa."

Amefafanua kwamba vipindi vya urais ni sehemu ya tunu iliyoachwa na Mwalimu Nyerere na hivyo kila mmoja wetu analojukumu la kuilinda tunu hiyo ambayo imeweka utaratibu mzuri kuhusu ukomo wa Rais.

Profesa Kabudi ametumia nafasi hiyo kuelezea pia uamuzi wa Mwalimu Nyerere katika mfumo wa vyama vingi ambao aliuruhu lakini katika mfumo wa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na umoja, amani na mshikamano.

Ambapo katika eneo hilo la vyama vingi mbali ya kuwa sehemu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere, ametumia kuhimiza Watanzania wa kada mbalimbali kusoma sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo kwa sehemu kubwa imefanyiwa marekebisho.

"Moja ya marekebisho ndani ya sheria ya vyama vingi, inazungumzia umuhimu wa vyama vya siasa kufanya uchaguzi za ndani kwa ajili ya kubadilishana uongozi na wanawake kushirikishwa.

"Pia katika sheria hiyo imezungumza kwa kina suala la uwazi kuhusu vyanzo vya fedha pamoja na matumizi yake ambayo yanatakiwa kuwa wazi na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.Pia sheria hiyo inapiga marufuku kuwa na vyama vya siasa vyenye muelekeo wa udini, kuligawa taifa na fujo na kueneza chuki miongoni mwetu,"amesema Profesa Kabudi.

Ameongeza kuwa sheria hiyo pia inatoa maelekezo mafunzo na itikadi zinazofundishwa ndani ya vyama vya siasa lazima Msajili wa Vyama vya Siasa apewe taarifa na kushiriki kwenye mafunzo hayo.

Profesa Kabudi wakati anazungumzia mambo ya kumuenzi Mwalimu Nyerere amegusia suala la utaifa na hasa katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaunganisha wananchi wote bila kujali makabila zaidi ya 120 yaliyopo nchini.

"Kuna mambo mengi ambayo nchi yetu inaendelea kufanya kama sehemu ya kuenzi misingi ambayo wengine wanaita tunu iliyoachwa na Mwalimu Nyerere.Hata hivyo Rais wetu Dk.Magufuli kuna mambo mengi anafanya kwa ajili ya kumuenzi kwa vitendo Mwalimu Nyerere,"amesema Profesa Kabudi.

Ametaja baadhi ya mambo ya hayo ni utekelezwaji wa miradi mikubwa nchini ambayo inafahamika kama miradi ya kimkakati ukiwemo uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia rasmi Dodoma kwani huo ulikuwa mpango wa Mwalimu lakini hakufanikiwa kuutekeleza.Pia ujenzi wa mradi wa umeme katika bwawa la Mto Rufiji ambalo kwa sasa linafahamika kama Mwalimu Nyerere Hydro Power Project utakaozalisha megawati 2115 na utagharimu zaidi ya Sh.trilioni 7 fedha ambazo ni za ndani.

Pamoja na hayo Profesa Kabudi amezungumzia ujenzi wa reli ya kisasa ambayo awamu ya kwanza ya ujenzi imeanza Dar es Salaam hadi Dodoma."Mwalimu Nyerere aliwapenda sana Watanzania na hivyo alikuwa na ndoto ya kuona wanakuwa na uchumi wa kati , hivyo Rais Magufuli ameibeba ajenda hiyo kwa vitendo ambapo ndani ya miaka minne ya uongozi wake amehakikisha amejenga na anaendelea kujenga miradi mbalimbali ya kimandeleo.

"Na katika hilo Serikali imeamua kwa vitendo kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo 352 na kwa ujenzi wa kila kituo umegharimu Sh.milioni 500 tofauti na hapo awali ambapo gharama za ujenzi zilikuwa kubwa sana na mkapaka sasa kuna maombi ya ujenzi wa viwanda nane vya dawa nchini,"amesema.

Ameongeza kuwa katika kumuenzi Mwalimu Nyerere ambaye alihakikisha watu wake wanapata elimu, Rais Magufuli ameamua kutoa elimu bure huku akifafanua kuwa kama Watanzania wanakumbuka Rais baada ya kuapishwa alikaa miezi mitatu bila ya kuwa na baraza la mawaziri ili fedha za kuwalipa zitumike kusomesha watoto.

"Uamuzi wa Rais kutoa elimu bure, umeongeza idadi ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa asilimia 20.1 .Hali hiyo imeongeza pia idadi ya watoto wanaojiunga na masomo ya sekondari,"amesema Profesa Kabudi.

Katika eneo la maji Profesa Kabudi amesema kuwa ni moja ya changamoto kubwa lakini Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wananchi wake wanapata maji safi na salama.

"Nilikuwa kwenye ziara ya Rais, tukiwa huki tumekutana na changamoto ya uhaba wa maji.Nakumbuka siku za karibuni nilikuwa Marekani ambako huko nilikuwa nalala kwenye hoteli ya hadhi ya nyota tano lakini baada ya kurudi na kuungana na Rais kwenye ziara nimelala gesti ya kawaida ambayo maji ya kuoga tunateka kwa ndoo,"amesema.

Kuhusu mikataba Profesa Kabudi amesema kuwa iliyopo sio kwamba haikuwa halali lakini Rais Magufuli kwa mapenzi mema aliyonayo kwa wananchi wake ameona ni vema ikapitiwa ili kuleta tija kwa watu wote tofauti na awali.

"Ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kupitia upya mikataba ya madini na leo hii wote tunaona faida yake.Pia mkataba wa Kampuni ya simu ya Airtel ambao umepitiwa upya na sasa tunanufaika na uwepo wa kampuni hiyo.Niwaambie tu pamoja na Serikali kuwa na hisa bado kila mwezi tunapata Sh.bilioni moja kutoka kampuni hiyo na itakuwa hivyo kwa kipindi cha miezi 60,"amesema Profesa Kabudi.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuenzi mambo ya msingi ambayo yameachwa na Mwalimu Nyerere kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA MPANDA KM 342.9, AFUNGUA BARABARA YA STALIKE MPANDA KM 36.9 PAMOJA NA STAND YA MABASI YA MIZENGO PINDA MPANDA MKOANI KATAVI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora- Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia,Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi
wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea nje ya lango kuu ya Stendi hio ya mabasi kuzungumza na wananchi mara baada ya kuifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufungua stendi hio ya mabasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakandarasi, Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara ya Tabora- Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe mara baada ya kuzindua na kufungua miradi ya barabara mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika
kujengwa kwa kiwango cha lami.

PICHA NA IKULU

'TUMEGOMA KUAMINI KAMA MWALIMU NYERERE AMEKUFA'

0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba kabudi amesema kuwa Mwalimu Julius Nyerere amegoma kufa na sisi tumegoma kuamini kama Mwalimu amekufa kutokana na hotuba zake kuishi kizazi hadi kizazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kabudi amesema kuwa mawazo ya Mwalimu yanaishi karne hadi karne.

" Mwalimu amefariki dunia ila amegoma kufa na amegoma kuacha kusimamia misingi ya nchi hii na sisi tumegoma kuamini kama amekufa na hiyo ni kupitia hotuba zake za muda mrefu ambazo zimekuwa zikiishi kila siku" ameeleza Prof. Kabudi.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kuthamini na kusimamia misingi aliyoiweka Mwalimu ili kuweza kulijenga taifa katika misingi ya maadili na kiitikadi.

"Tunu zinazotutambulisha ambazo Mwalimu alituachia lazima tuzitunze na hiyo ukiwepo muungano, haki, utu na usawa ili kuendelea kuliweka taifa letu katika nafasi njema zaidi" ameeleza.

Kuhusiana na lugha ya Kiswahili Prof. Kabudi amesema kuwa, lugha ya Kiswahili ni lugha ya ukombozi nchini na kusini mwa Afrika na nchi nyingi zimeeleza uhitaji wa walimu wa lugha hiyo nchini mwao hivyo amevitaka vyuo vinavyofundisha lugha ya Kiswahili kutumia nafasi hiyo katika kuieneza lugha hiyo ya ukombozi.

Amesema kuwa Chuo cha Dar es Salaam kimekuwa kikifundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni kutoka bara la Afrika kwa gharama sawa na wazawa,na kueleza kuwa jambo hilo ni jema na litasaidiakuipeleka mbele lugha adhimu ya Kiswahili.

Benki UBA yatoa ushauri kwa taasisi za fedha nchini

0
0

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

TAASISI za fedha nchini, zimeshauriwa kubadilika katika kuwahudumia wateaja wao na kuacha kutoa huduma kwa mazoea wakati wanapotoa huduma kwa wateja wao, ili kuendana na kasi pamoja na ushindani uliopo kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko la ushindani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA-Tanzania, wakati benki hiyo ilipoungana pamoja na wateja wake katika kusherehekea wiki ya wateja duniani iliyofanyika tawi la Nyerere.

“Nashauri taasisi zinazotoa huduma za kifedha lazima zibadilike na kuacha kutoa huduma kwa mazoea badala yake ziwe na ubunifu unaoendana na kipindi hiki cha ushindani wa soko la teknolojia kwani usipofanya hivyo ushindani ni mkubwa sana,” alisema Isiaka

Alisema UBA wanayo furaha kuungana na wateja wao kusherekea siku ya huduma kwa mteja duniani kwa kuwa wao ndio wanafanya benki hiyo kuwepo na kuendelea kutoa huduma stahiki na zenye ubora kwa wateja wao kwenye matawi yao yote nchini . 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ledgewood Investiment, Raymond Mubayiwa, alisema kuwa katika kipindi hiki cha kusherekea wiki ya huduma kwa wateja wamejifunza mengi ikiwamo kupata fursa ya kukutana na watoa huduma wao na kuzungumza nao kwa kina kuhusu masuala mbalimbali jambo ambalo kwao limewapa faraja kubwa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akizungumza na wateja wa benki tawi la Nyerere jijini Dar es Salaam, ikiwani ni maadhimisho ya wiki ya wateja duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akiwagawia wateja wa benki hiyo keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Dar es Salaam 
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live


Latest Images