Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA AFYA AZINDUA BOTI YA DHARURA NA KAMPENI YA KUZUIA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI ZANZIBAR

0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Boti mpya ya kisasa ya dharura (AMBULANCE BOT)kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaopata matatizo ya kujifungua katika Visiwa vya Pemba hafla iliofanyika hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitiliana saini na Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Tanzania Jacklin Mahon kuhusu makabidhiano ya Boti ya kisasa ya dharura (AMBULANCE BOT)kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaopata matatizo ya kujifungua katika Visiwa vya Pemba hafla iliofanyika hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Jackline Mahon akizungumza machache katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na Uzazi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na Uzazi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis akitoa hotuba katika Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na Uzazi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na Uzazi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanziba.kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis na kushoto ni Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Tanzania Jacklin Mahon.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed wakikabidhiana hati ya saini na Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Tanzania Jacklin Mahon katika hafla ya makabidhiano ya Boti ya kisasa ya dharura (AMBULANCE BOT)kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaopata matatizo ya kujifungua katika Visiwa vya Pemba hafla iliofanyika hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Boti mpya ya kisasa ya dharura (AMBULANCE BOT) iliozinduliwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaopata matatizo ya kujifungua katika Visiwa vya Pemba hafla iliofanyika hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KANAZI-KIZI-KIBAONI KM 76.6, DARAJA LA KAVUU MITA 85.3 PIA AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAONI MKOANI KATAVI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni km 76.6 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Kavuu M 85.3 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kibaoni mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Kibaoni mkoani Katavi mara baada ya kuwasili wakati akitokea wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Sehemu ya barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni km 76.6 iliyokamila kujengwa kwa lami na kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kibaoni mkoani Katavi mara baada ya kufungua barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni km 76.6 iliyokamila kujengwa kwa lami pamoja na Daraja la Kavuu M 85.3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kizi mkoani Rukwa wakati akielekea Kibaoni mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mulele wakati akielekea kufungua barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni km 76.6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wanyama aina ya viboko katika hifadhi ya Taifa ya Katavi mara baada ya kusimama wakati akielekea Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nsimbo mkoani Katavi mara baada ya kuwasili akitokea Kibaoni.

PICHA NA IKULU

MAADHIMISHO YA MIAKA 145 YA SIKU YA POSTA DUNIANI, SHIRIKA LA POSTA LAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA BARUA KIMATAIFA NCHINI

0
0
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo, walimu, wazazi pamoja na wageni wengine waliohudhuria kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la uandishi wa barua Kimataifa nchini, Joan John Erasto (wapili kushoto), wa Shule ya Sekondari Binza, mkoani Simiyu. Hafla ya maadhimisho ya miaka 145 ya Siku ya Posta Duniani imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni mwalimu wa shule hiyo, Japhet Kilela.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi akitoa maelezo katika hafla hiyo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dkt. Haruni Kondo.

Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifuatilia hotuba mbalimbali katika maadhimisho hayo. 

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika, Mwanaisha Said, akizungumza katika hafla ya maadhimisho hayo. 

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu-Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa uandishi wa barua, Hasnein Rizwan kutoka shule ya Sekondari ya Almuntazir Boys Seminary ya jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi akimkabidhi cheti mshindi wa pili wa shindano hilo, Grace Kahimba wa Shule ya Msingi ya St. Ann’s ya Morogoro. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu Mwanaisha Said na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dkt. Haruni Kondo. 

Mshindi wa kwanza nchini katika shindano la Kimataifa la uandishi wa barua, Joan John Erasto, akiisoma barua yake iliyompatia ushindi wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akizungumza katika maadhimisho hayo, leo jijini.Kaimu Postamasta Mkuu Mwanaisha Said, akimkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Jim Yonazi (katikati), kuzungumza katika hafla hayo.





Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano), Dkt. Yonazi akizungumza katika maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Usafiri wa ndege nchini (MAUFU), Maua Katandula, ambao ni mmoja wa wadhamini wa shindano la kimataifa la Uandishi wa Barua nchini, akizungumza katika maadhimisho hayo.

KWAYA YA GETHMANE YATOA MSAADA KWA WAGONJWA WA FISTULA CCBRT

0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Tv


Mmoja ya wanakwaya ya Gethmane ya Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabidhi zawadi kwa mgonjwa wa Fistula ambaye anatakiwa matibabu katika Hospitali ya CCBRT .Kwaya hiyo unaotarajia kuzindua DVD mbili Oktoba 13 mwaka huu ambapo tukio la leo ni sehemu ya kuelekea katika uzinduzi huo


WAIMBAJI wa kwaya ya Gethmane ya Kanisa la SDA(Wasabato) Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wametoa misaada kwa wagonjwa Fistula waliopo katika Hospitali ya CCBRT ikiwa ni sehemu ya kuonesha matendo ya huruma kwa wenye uhitaji.

Kwaya hiyo ikiongozwa na Masunya Anthony ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni, Mzee wa Kanisa Emmanuel Mgonja pamoja na Mlezi wa kwaya hiyo wametoa msaada huo leo hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuelekea Oktoba 13 mwaka huu ambapo kwaya hiyo inatarajia kuzindua DVD mbili katika ukumbi wa Uhuru JKT Mwenge jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza mbele ya wagonjwa hao wa fistula, madaktari na wauguzi, waimbaji wa kwaya hiyo wamesema wanatambua umuhimu wa kutoa msaada kwa jamii yenye uhitaji na ndio maana wamefika katika hospitali hiyo na kutoa japo kidogo ambacho wamejaaliwa kuwa nacho.

Akizungumzia msaada huo, Mwalimu wa kwaya hiyo Stella Malingoza amesema kuwa, mwaka huu kwaya hiyo imetimiza miaka 10 na wanajiandaa kuzindua DVD zao mbili Oktoba 13 mwaka huu hivyo wameona ni vema kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wakatoa msaada huo ambao ni sabuni, mafuta ya kupakaa, dawa ya meno na miswaki.

"Kwaya yetu ya Gethmane tumekuwa na utamaduni wa muda mrefu wa kujitoa kwa misaada ya aina mbalimbali, tunaweza tusiwe tumetoa msaada mkubwa lakini kile ambacho tunakipata huwa tunakipeleka kwenye jamii ambayo ina uhitaji.Hivyo tumekuja CCBRT kwa ajili kuwaona mama zetu na dada zetu wenye kusumbuliwa na ugonjwa fistula na kadri tutakavyopata tutarudi kwao na kwa wengine.

"Thamani ya msaada wote ambao tumeutoa katika wodi hii ya wagonjwa fistula una thamani ya zaidi ya Sh.milioni 2.4.Tunajua wanakabiliwa na changamoto nyingi na wanamahitaji mengi lakini hiki kidogo ambacho tunacho tumeona tuwaletee na kuwakabidhi,"amesema Stella.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Watanzania bila kujadili itikadi za dini kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Oktoba 13 ambayo itakuwa siku maalumu ya uzinduzi wa nyimbo zao mpya ambapo watazindua DVD na hakutakuwa na kiingilio.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa hilo Masunya Athony ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa watu wanapokuwa wagonjwa wakati mwingine inakuwa ngumu kupata neno la Mungu kwa usahihi, hivyo kwa kutambua hilo wameona Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni linawajibu wa kuwafikia wagonjwa na kuzungumza nao ikiwa pamoja na kufanya maombi.

Amesema wanachokifanya hata Bwana Yesu amewahi kuyafanya na hivyo wao wameona ni vema wakahusika katika kusaidia mahitaji ya watu na hasa wenye kusumbuliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za maradhi na kuongeza kuwa kwaya hiyo kwa nyakati tofauti imekuwa karibu na jamii kwa kufanya matendo yaliyo mema.

Wakati huo huo Mzee wa Kanisa hilo Emmanuel Mgonja amesema kuwa wanapokwenda kutimiza miaka 10 ifikapo Oktoba 13 mwaka huu ambapo wameona ni vema wakashiriki kuwaona wagonjwa na kuwasaidia kwa kile kidogo walichonacho.

"Kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa DVD mbili siku hiyo ya Oktoba 13 mwaka huu tumeona ni vema tukaja hapa kwa ajili ya kuwasalimia wagonjwa hawa wa fistula, kushirikiana nao kwa kufanya maombi na kisha kutoa msaada huu ambao tumekuja nao,"amesema Mgonja.

Awali Muuguzi katika Hospitali ya CCBRT ambaye anahudumia wagonjwa wa Fistula Theodora Masako amesema kuwa ugonjwa huo unatibika lakini changamoto iliyopo wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa huo wamekuwa wagumu kufika hospitali kupata matibabu kwasababu mbalimbali ikiwemo kuhofia gharama za matibabu na wengine kuamini wamepata tatizo kwasababu ya imani za kishirikina.

"Tumekuwa tukitoa elimu kuhusu ugonjwa huu ambao hauna uhusiano na ushirikina, na wala matibabu yake hayana gharama yoyote ile na hapa kwetu tunatoa matibabu bila malipo.Hata hivyo tutumie nafasi hii kuishukuru kwaya hii ya Gethmane kwa kutambua umuhimu wa kutoa msaada wao kwa ajili ya wagonjwa hawa ambao tunawahudumia hapa hospitalini kwetu,"amesema Masako.

Amesema wagonjwa wanapoona wanatambelewa wanafarijika na kupata moyo kuwa wapo watu ambao wanawathamini na kuwajali kwani moja ya changamoto ya ugonjwa huo, wengi wao wamekuwa wakitengwa na jamii na wakati mwingine hata na familia zao.
 Mmoja ya wanakwaya ya Gethmane akikabidhi Zawadi kwa mgonjwa wa fistula katika Hospitali ya CCBRT leo baada ya kwaya hiyo kufika kwa ajili ya kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa hao
 Mmoja ya mlezi wa Kwaya ya Gethmane ya Kanisa ya SDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam akitoa msaada kwa mgonjwa wa Fistula katika Hospital ya CCBR leo jijini
 Muuguzi katika Hospitali ya CCBRT Theodora Masako akizungumza na wagonjwa wa fistula baada ya Kwaya ya Gethmane kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada kwa wagonjwa hao ikiwa ni muendelezo wa matukio kuelekea Oktoba 13,mwaka huu ambapo watafanya uzinduzi wa DVD mbili katika Ukumbu wa Uhuru JKT Mwenge
 Baadhi ya wagonjwa wa fistula katika Hospitali ya CCBRT wakiwasikiliza viongozi na wana kwaya wa Gethmane ya Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam
 Wanakwaya wa Gethman kutoka Kanisa la CDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam  wakiimba moja ya nyimbo zao wakati walipowatembelea wagonjwa wa Fistula waliopo Hospitali ya CCBRT .Kwaya hiyo pamoja na kuimba mbele ya wagonjwa hao wametoa msaada wa vitu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 2.4
 Mchungaji wa Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Masunya Anthony akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya Kwaya ya kanisa hilo inayofahamika kwa jina la Gethmane kutembelea wodi ya wagonjwa fistula katika Hospitali ya CCBRT na kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 2.4.Wengine kwenye picha hiyo ni baadhi ya waimbaji wa kwaya hiyo ambayo inatarajia kuzindua albam zake mbili Oktoba 13 mwaka huu katika Ukumbu wa Uhuru JKT Mwenge

AIRTEL YAUNGANA NA SERIKALI MAANDALIZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIM JULIUS .K. NYERERE

0
0
 Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (pili kushoto) akipokea miamvuli zaidi ya 1000 kutoka kwa Meneja wa mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Zephania Ludigiji kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu  ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati), Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde na wafanyakazi wengine wa Airtel.
 Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (pili kushoto) akipokea miamvuli Zaidi ya 1000 kutoka kwa Meneja wa mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Zephania Ludigiji kwa ajili ya maandalizi ya  maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya  kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati), Menjeja matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto)


   Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati)akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa  miamvuli Zaidi ya 1000 kwa Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama na wawakilishi wa Airtel kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (tatu kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Massawe (wa pili kushoto). 
Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (kati) akijaribisha mwamvuli aliokabidhiwa na timu ya Airtel, Maalum kama maandalizi  ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kumkumbuka ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo mwaka huu kitaifa yatafanyika Lindi, huku wakishuhudiwa na wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (pili kulia), Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (pili kushoto na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Massawe (kushoto).


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeungana na Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenye matayarisho ya kumbukumbu  ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itafanyika Lindi katika viwanja vya Mpilipili.

Miamvuli hiyo zaidi ya 1000 iliyotolewa na Airtel itatumiwa na watoto watakaendesha halaiki siku ya kilele cha maadhimisho hayo katika viwanja vya mpilipili Lindi.

Posta mnawajibu wa kurahisisha utoaji wa huduma kidigitali -Dkt.Yonazi

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa Shirika la Posta Tanzania linawajibu wa kuisaidia Serikali katika kuharakisha maendeleo kwa kurahisisha utoaji wa huduma za barua, nyaraka, vipeto na vifurushi ndani na nje ya nchi kwa kwenda kidigitali ambako dunia ndio iko huko. duma

Hayo ameyasema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano -Mawasiliano Dkt.Jimmy Yonazi wakati alipomwakilisha Waziri wa Wizara hiyo katika siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 145 ya Umoja wa Posta duniani.

Dkt. Yonazi amesema kuwa shirika hilo limekuwa likirahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha za uwakala hasa maeneo ambayo hayafikiwi kirahisi na Kampuni pamoja na taasisi zinazotoa huduma za kibiashara.

Dkt. Yonazi amesema shirika linajukumu la msingi la kutoa huduma za posta kwa watu wote hivyo ni muhimu likaendelea kuboresha mikakati yao ili liweze kuwafikia watanzania kote nchini ikienda sambamba na huduma bora.

"Tupo Serikali ya awamu ya tano inayowataka watu kufanya kazi, shirika hili ambalo linamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 lina wajibu wa kufuata kauli mbiu hiyo kwa vitendo, kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa ni bora kwa wateja mnaowahudumia " amesema.

Amesema shirika hilo haliwezi kukwepa kuwa moja ya watumiaji wakuu wa mifumo ya kompyuta na mitandao kwani ndiko dunia ilipo kwa sasa na biashara inafanyika katika mitandao .

Naye Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo, Mwanaisha Said amesema wamejizatiti na kuboresha baadhi ya huduma zao ambazo nyingi kwa sasa zinafanyika kidigitali katika kufanikisha maendeleo endelevu.

Said amesema kwa mwaka huu wamepata mwitikio mkubwa kutoka Tanzania bara na visiwani katika kushiriki shindano ambapo jumla ya wanafunzi 1881 walijitokeza ikilinganishwa na 850 walioshiriki mwaka jana ikiwa na kutaka wanafunzi washiriki Shindano la Afrika la uandishi wa habari.

Washindi katika shindano hili wa kwanza ni Joan Erasto kutoka shule ya Sekondari ya Binza iliyopo Simiyu, wa pili ni Grace Kahimba kutoka Shule ya msingi ya St Ann's ya Morogoro na mshindi wa tatu ni Hasnein Rizwan wa Shule ya Almuntazir Boys Seminari ya jiji Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika hilo, Dk. Harun Kondo amesema shirika hilo limesimama na kuzalisha faida kwa sasa kutokana na mshikamano uliyopo kati ya bodi na wafanyakazi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano -Mawasiliano Dkt.Jimmy Yonazi akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 145 ya Umoja wa Posta Duniani ambapo ilikwenda sambamba na utoaji zawadi walioshiriki shindano la uandishi wa Barua hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

BENKI YA DCB YAZINDUA DCB AKAUNTI YENYE KUMHAKIKISHIA MTEJA KUWEKA AKIBA NA UHAKIKA WA ELIMU YA MTOTO WAKE HADI CHUO KIKUU.

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB,Godfrey Ndalahwa akizungumza mbele ya Waandishi wa habari na Wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akaunti maalum ya akiba ya mpango wa elimu ijulikanayo kwa jina la DCB Skonga,leo jijini Dar.Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ,James Ngaluko na kushoto ni Balozi wa benki hiyo kupitia akaunti ya DCB Skonga,Zamaradi Mketema.


Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB,James Ngaluko akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu akaunti ya DCB Skonga,amesema kuwa kupitia bidhaa ya DCB Skonga mteja anaweza kuchagua mpango wa aina mbalimbali wa kuweka akiba pamoja na muda wa uwekezaji kulingana na umri,gharama na muda wa masomo ya mtoto wake, "hiyo ndiyo njia salama ya kuweka akiba yako huku ukihakikishiwa elimu ya mtoto wako na mwisho wa muda uliochagua (mwaka 1 hadi 17) benki itakupa akiba yako yote ambayo pia itakusaidia kutimiza malengo yako mengine mbalimbali ya kimaisha",alisema Ngaluko.
Balozi wa benki ya DCB kupitia bidhaa ya DCB Skonga,Zamaradi Mketema akieleza namna gani akaunti hiyo inavyoweza kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali,amefafanua pia kuwa akaunti hiyo haijakaa kibiashara,imekaa katika mtindo wa kumsaidia mtu kuzifanikisha ndoto zake za kimaeendeleo ikiwemo elimu katika familia. "kwa hiyo akaunti hii imekuja kwa wakati muafaka kabisa,imekuja kutuokoa na kutuhakikishia kwamba hata jambo lolote likitokea ntaitumia akaunti hiyo kuhakikisha mtoto wangu anamaliza elimu yake bila tatizo lolote",alisema na kuongeza kuwa kupitia akaunti hiyo mtu anaweza kupata mkopo mpaka asilimia 50

Baadhi wageni waalikwa wakiwemo wafanyakazi wa beki ya DCB wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa akaunti maalum ya akiba ya mpango wa elimu ijulikanayo kwa jina la DCB Skonga,leo jijini Dar.
 
 
Benki ya Biashara ya DCB leo imezindua akaunti maalum ya akiba ya Mpango wa elimu ijulikanayo DCB Skonga,ikilenga kumhakikishia mteja akiba na uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo Kikuu.
 
Akizungumza katika uzinduzi wa akaunti hiyo leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB,Godfrey Ndalahwa amesema kuwa DCB Skonga ni akaunti maalum ya akiba inayo mpa mteja fursa ya kuweka akiba kila mwezi ili kutimiza malengo aliyo jiwekea huku mteja akihakikishiwa elimu ya mtoto  wake hadi chuo kikuu
 
Ndalahawa amesema benki ya DCB inaamini katika kutoa fursa zenye tija kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla,kwa kuwaletea bidhaa nzuri zinazowapa tija na faida lukuki."Kwa mara nyingine tena leo DCB inaandika historia nyingine kwa kuzindua bidhaa mpya ya mpano wa elimu ijulikanayo DCB SKONGA AKAUNTI,",alisema Ndalahwa.
 
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB,James Ngaluko alisema kwa kupitia bidhaa hiyo ya DCB Skonga mteja anaweza kuchagua mpango wa aina mbalimbali wa kuweka akiba pamoja na muda wa uwekezaji kulingana na umri,gharama na muda wa masomo ya mtoto wake.

"Hii ni njia salama ya kuweka akiba yako huku ukihakikishiwa elimu ya mtoto wako na mwisho wa muda ulio chagua (mwaka mmoja hadi 17 ) benki itakupa akiba yako yote ambayo itakusaidia kutimiza malengo yako mengine mbalimbali ya kimaisha",alisema Ngaluko.

Alisema kuwa akaunti hiyo inampa fursa mteja kuchagua muda wa kuweka akiba kutoka mwaka 1 hadi 17 na endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda kuisha,tegemezi wake watarudishiwa kiasi cha fedha alichowekeza kuanzia mwanzo wa mpango na vile vile mtoto atalipwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.
 
Aidha Balozi wa benki ya DCB kupitia bidhaa ya DCB Skonga,Zamaradi Mketema amesema akaunti hiyo ina umuhimu mkubwa kwa jamii,kwani inaweza kumsaidia mtu katika maeneo mbalimbali katika kutatua changamoto zake ikiwemo sula la elimu kwa familia yake.
 
"Akaunti hiio haijakaa kibiashara,imekaa katika mtindo wa kumsaidia mtu kuzifanikisha ndoto zake za kimaeendeleo ikiwemo elimu katika familia,kwa maana hiyo akaunti hii imekuja katika wakati muafaka kabisa,imekuja kutuokoa na kutuhakikishia kwamba hata jambo lolote likitokea ntaitumia akaunti hiyo kuhakikisha mtoto wangu anamaliza elimu yake bila tatizo lolote",alisema Zamaradi.

WAZIRI MKUU KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA MAFUNZO KWA VIJANA YA KILIMO CHA KISASA KWAKUTUMIA KITALU NYUMBA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa kamati ya maandalizi alipotembelea viwanja vya Mpilipili kwa ajili ya kukagua eneo hilo utakapofanyika Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia Kitalu Nyumba (Greenhouse) pamoja na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Lindi. (Kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi (wa tatu kutoka kushoto) akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walipotembelea eneo la Ngongo mahali kilipo Kitalu Nyumba. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (wa pili kutoka kulia).

**************************

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia Kitalu Nyumba (Greenhouse) pamoja na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyikia Mkoani Lindi siku ya Alhamisi tarehe 10 Oktoba, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 9, 2019 kuhusu Uzinduzi wa Mafunzo kwa vijana ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia Kitalu Nyumba (Greenhouse) pamoja na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Mhagama alisema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu Programu ya ukuzaji ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kuondokana na tatizo la ajira, kukuza ujuzi wao na kuwasaidia waweze kushiriki kwa wingi kwenye ujenzi wa taifa kwa uzalendo.

“Tumeamua kutoa mafunzo haya kwa vijana wasiopungua 18,000 katika kila halmashauri ili vijana waweze kunufaika na mradi huu kwa kujihusisha na kilimo cha Kisasa chenye tija kwao,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa matokeo haya chanya yameletwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwawezesha vijana nchini.

“Tunaamini teknolojia hii itakapoenea kwenye maeneo mbalimbali nchini vijana watakuwa na uwezo wa kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii chenye tija kwao, kwani wataweza kupata mazao mengi kwenye eneo dogo,” alifafanua Mhagama.

Aidha amewasihi wananchi kufuatilia matangazo ya uzinduzi huo yatakayorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya Taifa (TBC) ili waweze kuona juhudi za Serikali katika kuwawezesha vijana kupitia Mafunzo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia Kitalu Nyumba (Greenhouse).

Wakati huo huo aliwahimiza wakazi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nanenane, Ngongo ambapo uzinduzi wa mafunzo hayo yatafanyika na pia kutembelea viwanja vya Mpilipili ambapo Maadhimisho ya 17 ya wiki ya Vijana yatafanyika.

MFANYABIASHA YUSUFU ALLY ALMAARUFU 'MPEMBA WA MAGUFULI' NA WENZAKE WAANDIKA BARUA KUKIRI MASHITKA YAO KWA DPP

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MFANYABIASHARA Yusufu Ally, maarufu kwa jina la mpemba wa Magufuli na wenzake,wanaokabiliwa na mashitaka ya  uhujumu uchumi ikiwemo kujihusisha na biashara ya meno ya tembo, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka yao hayo.

Mpemba, katika kesi hiyo anashtakiwa pamoja na Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba kesi hiyo leo Oktoba 9,2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini amepata taarifa kuwa washtakiwa wameaandika barua kwa DPP ya kuomba msamaha , hivyo ameomba mahakama iwape muda kwa ajili ya kufuatilia makubaliano hayo.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 .

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh  milioni 392.8  bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Oktoba 26, mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye   uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya Dola za Marekani 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Wanadaiwa kuwa  Oktoba 27, mwaka huu, wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya Dola za Marekani 15,000  sawa na Sh milioni 32.7 .

Aidha, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh  milioni 294.6   bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

DC MTATIRO ATATUA MGOGORO ULIODUMU MIAKA MINNE

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru , Julius Mtatiro ametatua mgogoro wa muda mrefu kati ya Wananchi wa kijiji cha Chemchem katika kata ya Tuwemacho dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambao ulianza mwaka 2014.

Mgogoro huo unahusisha madai ya kijiji cha Tuwemacho katika ujenzi wa Barabara Kuu ya Tunduru Songea na Tunduru Masasi miaka 5 iliyopita ambapo kokoto zilizokidhi vigezo na viwango zilichimbwa kwenye mgodi wa mawe wa kijiji hicho kwa ahadi kuwa halmashauri ingelilipa asilimia 20 ya mapato ya ushuru wa kokoto hizo kwa kijiji husika ambazo ni sawa na shs milioni 48 ambazo kama wangelizipata wangelianza ujenzi wa zahanati kijijini hapo.

Mtatiro amemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru kuanza mara moja ujenzi wa zahanati ya kisasa ya shilingi milioni 84 katika kijiji cha Chemchem kama ishara ya kuwalipa wananchi fedha zao ambazo wamezidai bila mafanikio, na kwamba fedha hizo zina riba ambayo ni haki ya wananchi hao.

Pamoja na hatua hizo, Mtatiro ameelekeza Ofisi ya Mkurugenzi na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tunduru, waendelee kufanya mawasiliano na TANROAD ili fedha hizo zipatikane na ameelekeza zitakapotolewa zipelekwe katika kijiji husika moja kwa moja.

Aidha, Mtatiro kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini, Mhe. Mpakate, wameamua kuanzisha ujenzi wa Ofisi ya kisasa ya kijiji ambapo Mtatiro atatoa mifuko 25 ya Simenti, Mbunge atatoa bati 60 na mifuko 25 ya Simenti na wananchi watachangia nguvu zao.

Katika mkutano huo, Mtatiro amesisitiza umuhimu wa kuwatendea haki wananchi na kupambana na shida na kero zao kama anavyofanya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

SHINDANO LA MISS UNIVERSE TANZANIA LARUDI KWA KISHINDO

0
0


Baada ya kimya cha mwaka mmoja, kampuni ya Compass Communication imeandaa tena mwaka huu, shindano la Miss Universe Tanzania.

Baada ya kufanya usaili na warembo takriban 90 kutoka mikoa tofauti nchini, shindano hili la kitaifa la mwaka huu linahusisha warembo 10 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es salaam linatarajiwa kufanyika tarehe 12 mwezi wa kumi katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kuanzia saa 1 jioni.

Katika miaka ya nyuma shindano hili limeweza kuibua vipaji vya wengi na wameendelea kufanya vyema katika ulimwengu wa urembo na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu. Baadhi yao ni pamoja na Flaviana Matata, Nelly Kamwelu pamoja na Hellen Dausen.

“Urembo ni sanaa na urembo ni kazi, na ndio maana sisi kama Compass Communications tumeona fursa na kuamua kuendeleza vipaji vya wasichana wengi wenye ndoto na wenye kuamini kuzifikia kupitia tasnia hii ya urembo” ameeleza mkurugenzi wa kitaifa wa shindano hili, Maria Sarungi Tsehai

Pia kwa Mwaka 2019 mashindano haya yanaadhimisha miaka 12 tangu kuanza kufanyika hapa nchini mwaka 2007. Kama ilivyo adha mshindi wa Miss Universe hapa nchini ataenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia hapo baadae mwaka huu.

Maria Sarungi Tsehai ameeleza kuwa mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri na wadau wote wa tasnia,. “Tunaishukuru sana Serikali, Wizara husika pamoja na Baraza la Sanaa (BASATA) kwa kutupatia ushirikiano kwa miaka yote na ni matumaini yetu kuzidi kupata ushirikiano kutoka kwenu na kusongesha kwa pamoja hili gurudumu la sanaa”, ameongezea Bi Sarungi

Miss Universe kwa mwaka 2019, imedhaminiwa na Precision Air, Serena Hotel, Sea Cliff Luxury apartments , Kwanza TV, Pepsi , Samaki Samaki Fish and More pamoja na Timeless Saloon.
Imetolewa, Dar es Salaam 09/October/2019

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Saddam Khalfan
+255 712 785 161
saddam@compass-tz.com

PIA TUNAPENDA KUUTARIFU UMA KUHUSU  MABADILIKO YA VENUE KUTOKA SEA CLIFF KWENDA SERENA SABABU YA HALI YA HEWA.

MVUA YAUA WATU SITA KOROGWE,TANGA

0
0
JUMLA ya watu sita wakiwemo watoto wanne na watu wazima wawili wamefariki dunia katika vijiji vya Bungu na Dindila wilayani Korogwe mkoani Tanga kutokana kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia saa 2 usiku wa Oktoba 8 hadi majira ya saa 9 alasiri Oktoba 9.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga SACP Edward Bukombe alisema kuwa mvua hiyo iliyonyesha katika vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe katika milima ya Usambara ilisababisha barabara kuu ya Arusha -Segera -Dar eneo la Msambiazi Korogwe mjini kutopitika na kufungwa kwa muda kwa tahadhari za kiusalama.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa alithibitisha kwa barabara hiyo kufungwa kwa muda na hadi kwa muda wa saa mbili na baadae kuendelea na safari zake kati ya Tanga, Dar es salam, Lushoto, Moshi, Arusha na Nairobi kupitia Namanga mkoani Arusha yaliruhisiwa.

Akizungumzia vifo vya watu sita, Kamanda Bukombe amesema kuwa watu hao ambao majina yao bado hayajulikana ni katika kijiji cha Dindira mwanamke mmoja na watoto wake wawili waliangukiwa na nyumba usiku mkubwa wakati katika kijiji cha Bungu msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Asha Yahaya Ambanyonge alikuwa kalala na wadogo zake wawili ambapo nao wameangukiwa na nyumba na kufariki papo hapo.

Mkazi wa Kijiji cha Mgila kata ya Kwashemshi tarafa ya Bungu Korogwe Vijijini Jabir Hamisi Titu (66) alisema kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa mbili usiku Oktoba 8 hadi majira ya saa 9 alasiri mbali na maafa pia imeharibu miundombinu ya barabara ya Kwashemshi-Mgila yenye urefu wa kilometa 5,imesomba mazao, imesomba matanuri ya matofali ya kuchoma na kuangusha mawe kutoka milimani.

Ameongeza kuwa katika kijiji cha Vingo kata ya Kerenge Mremwa kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amesombwa na maji na hajulikani alipo alikuwa akijaribu kuangalia bustani yake iliyokuwa bondeni.

"Hii mvua imeleta maafa, imeharibu miundombinu,mazao yamesombwa na maji hakupitiki " alisema.Wilayani Muheza katika barabara ya Amani -Muheza kata ya Mbaramo eneo la Msangazi mawasiliano ya barabara yalifungwa kwa muda kutokana na mafuriko yaliyoziba njia.

eneo hilo ni sumbufu kwa muda mrefu kutokana na mkondo wa maji uanoanzia vijiji vya Kibanda, Semngano na Kerenge unaokatisha barabara kuu ya Tanga -Segera ambapo mwaka 1997 palitokea mafuriko yaliyosomba basi la Kampuni ya No Challenge na kusababisha vifo vingi. 

KLABU YA ROTARY YA MZIZIMA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE

0
0


Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Dkt. Emeria Mugonzibwa akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani jana jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule hiyo.
Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Dkt. Emeria Mugonzibwa akikabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule Sekondari Jangwani jana  jijini Dar es Salaam.


KHADIJA KOPA ALIVYOZUSHIWA KUMUUA MWANAWE OMAR KOPA ILI KUJIONGEA UMAARUFU

0
0
‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa

Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Sifa za ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa zimezagaa kila kona katika nchi zilizo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na nchi za Falme za Kiarabu, kufuatia uimbaji wake mwanana wa taarab.

Mama huyu ni mwimbaji, mtunzi na mtayarishaji wa rekodi nyimbo za taarabu pia ni mfanyabiashara maarufu.

Khadija Kopa amejizolea sifa lukuki akiwa na kikosi hicho kwa kuimba nyimbo zenye mipasho, inayopendwa na wapenzi na washabiki wa muziki wa taarab humu nchini.

Mara baada ya kuzaliwa mwaka 1963, Kisiwani Zanzibar, alipewa jina la Khadija, akiwa ni mtoto wa kipekee katika familia ya Omar Abdallah Kopa.

Alivyojiunga Culture Musical Club.

Siku moja alikuwa amekaa nyumbani kwao huku akiiga kuimba wimbo, akapita babu yake aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Babu huyo akamsifia ya kwamba anajuwa kuimba.

Baada ya sifa hizo, Kopa akajiona anatosha kujiunga katika kundi kubwa la muziki huo, akachukuwa hatua ya kuandika barua pasipo kumshauri babu yake, akaipeleka kwenye uongozi wa Culture Musical Club akiomba ajiunge nao.

Alikubaliwa na kuweza kufanya kazi ya kuimba nyimbo za taarab tangu mwaka 1990, katika kundi lake la kwanza la Culture Musical Club ya mjini Zanzibar.

Wakati akiwa Culture Musical Club, umaarufu wake ulionekana baada ya kuimbaji kwa mahiri mkubwa kupitia sauti yake maridhawa.

Kopa aliimba vibao vya kama vile “Kadandie”, “Daktari” na “Wahoi”, alivyoviimba akiwa katika kikundi cha Culture Musical Club, ambavyo vilimpa umaarufu mkubwa visiwani Zanzibar na Pemba.

Sifa zake zikatambaa hadi Tanzania bara, ambako uongozi wa TOT Plus, ulifanya mchakato wa kumfuata Khadija Kopa visiwani Zanzibar, wakamuomba ajiunge na kikundi hicho.

Sababu kubwa ilikuwa ni kukipa sura na mwonekano mpya, tofauti na tasnia ya taarab iliyozoweleka Tanzania Bara.

Khadija Omar Kopa aliamua kuhamia jijini Dar es Salaam baada ya kushawishiwa na uongozi wa Tanzania One Theatre (TOT), kujiunga nacho, kikiongozwa na Kapteni mstaafu John Damian Komba mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Awali baadhi ya washabiki wa muziki huo hususan katika jiji la Dar es Salaam, hawakuwa wakifahamu uwezo wake katika kuimba. Waliomuona kama mwimbaji wa kawaida, tofauti na mashabiki wa taarab wa visiwa vya Zanzibar, jina la Khadija Kopa lilikuwa kubwa mno.

Kopa licha ya kuimba taarab, amekuwa mstari mbele katika uimbaji wa kwaya ya TOT, akishirikiana vyema na Kapteni mstaafu John Komba (marehemu) pamoja na waimbaji wengine wa TOT wakiwamo akina Abdull Misambano, Mwanamtama Amir na Gasper Mapunda.

Nguli huyu hujichanganya kupiga muziki na baadhi ya bendi za muziki wa dansi, ambazo humualika kuongeza sauti nyororo katika nyimbo zao.

Mfano wa karibu ni pale aliposhirikiana vyema na wanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu, wakatengeneza video ya wimbo wa ‘Chanzo ni Wanaume’. Kopa ameonekana akiimba kwa kupokezana na waimbaji wa bendi hiyo Jose Mara na Kharid Chokoraa.

Adiha aliwahi kushirikiana na msanii wa Bongo fleva, Diamond Platnumz, aliyekuwa kiongozi wa kundi la taarab la Jahazi, Alhaj Mzee Yusuph.

Khadija pia amepata kushirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir, marehemu Leila Khatib na wanaume kama akina Abdul Misambano na Ali Star ‘Sharo Babu’.

Waliporomosha nyimbo ambazo zilitamba miaka hiyo kupitia mashairi maridadi yaliyotungwa na kuimbwa na nguli hao.

Kopa ni mama mwenye watoto wanne na wajukuu wawili, pia hujishughulisha masuala ya siasa ambapo alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM.

Historia ya Khadija Kopa katika muziki inaeleza kuwa alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo. Kopa alisoma masomo ya Koraan kwenye madrasa mjini Zanzibar, ambako alikuwa akighani sana Kaswida.

Mambo ya siasa aliyaanza wakati alipokuwa akiandaliwa katika kundi la watoto Young Pioneer, upande wa kwaya.

Kopa alipokuwa shule ya msingi, alikuwa akiimba na kucheza kwenye kundi la ngoma za utamaduni na kwaya. Shule yao ilikuwa bingwa kwa kwaya visiwani humo.

Muonekano wa Kopa

Kwa umbo, Khadija Omar Kopa ni mnene ‘Shibonge’ mwenye rangi nyeusi yenye mng’ao wa kumeremeta.

Licha ya kuwa na umbile hilo, ni mwepesi wa kuzunguusha maungo yake atakavyo awapo jukwaani.

Kopa anaweza kuwashukia washabiki, akanengua nao huku akiwaachia vibwagizo kemkem ukumbini.

Sauti ya Khadija Kopa haiigiki kwamwe, ni ya aina yake yenye mikwaruso fulani, wakati akiimba.

Aidha macho yake yenye mvuto yaliyotulia kwenye paji lake la uso ukiwa na tabasamu tele muda wote utadhani hajui kitu kinachoitwa kukasirika.

Khadija Kopa anao uwezo mkubwa wa kujibu ‘mapigo’ kwenye nyimbo zake dhidi ya mahasimu wake. Pia anaweza kuongeza vionjo vya ‘mipasho’ katika wimbo, kufuatia tukio lililopo ukumbini pasipo kuwaarifu wasanii wenzake jukwaani

Sifa hizo ndizo zilizomfanya mwanamama huyo apachikwe jina la ‘Malkia wa Mipasho’ nchini, ambapo yaelezwa kuwa waliompa jina hilo hawakubahatisha, walitambua vyema kwamba uwezo wake katika tasnia hiyo ni mkubwa.

Kopa akiwa TOT Plus mwaka 1992, alidhihirisha kwamba hawakukosea kumfungia safari hadi Visiwani humo, baada ya kung’ara kwa vibao kama “TX mpenzi”, “Ngwinji”, “Wrong Namba”, “Mtie kamba mumeo” na nyinginezo.

Miaka miwili baadaye, Khadija Kopa alikorofishana na uongozi wa TOT Plus, baada ya yeye na mwimbaji mwenzake, Othman Soud wakaamua kuondoka kinyemela na kwenda Dubai ambako walishiriki kuanzisha kundi la East African Melody.

Baada ya kurejea nchini kutoka Dubai, Khadija Kopa alilazimika kujiunga na kikundi cha Muungano Cultural Troupe kwa kuwa uongozi wa TOT uligoma kumpokea.

Kujiunga kwa Khadija na Othman Soud katika kikundi cha Muungano, kulisababisha kuwepo kwa ushindani mkali kati ya vikundi hivyo viwili.

Baadaye vikundi hivyo vikawa vikifanya maonyesho kadhaa ya pamoja kwa ajili ya kuonyeshana nani mkali.

Akiwa Muungano, Khadija aling’ara kwa vibao vyake murua kama vile “Homa ya Jiji”, “Kiduhushi” na “Umeishiwa”.

Pia kulizuka ushindani mkali kati yake na marehemu Nasma Khamis ‘Kidogo’, ambaye alichukuliwa na TOT, kutoka Muungano Cultural Troupe kwa lengo la kuziba pengo lake.

Akizungumza mjini Dar es Salaam hivi karibuni, Khadija Kopa alikiri kwamba asingeweza kufika mahali alipo bila ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa Othman Soud.

“Othman ndiye aliyekuwa mtunzi wa nyimbo zote nilizokuwa nikimba tangu nikiwa Culture na TOT.

Hata TOT waliponifuata Zanzibar, niliwaambia kwamba nisingeweza kujiunga na kikundi hicho bila ya Othman Soud, bila yeye nisingeweza kufanya lolote la maana,” alisema Khadija Kopa.

Kwa sasa, Othman ni askari wa Jeshi la Magereza visiwani Zanzibar.

Uamuzi Othman Soud kuacha kujihusisha na muziki wa taarab, kulimuathiri kwa kiasi kikubwa Khadija Kopa, ambapo alilazimika aanze kuchacharika na kutunga nyimbo zake mwenyewe.

Khadija Kopa alikiri kuwa ushindani wa kimuziki uliokuwepo kati ya TOT na Muungano Cultural Troupe, ulisaidia kwa kiasi kikubwa kuinua hadhi ya muziki huo.

Alisema haitatokea kwa vikundi viwili vya taarab nchini kuwa na ushindani kama huo.

“Kila tulipofanya maonyesho ya pamoja, kumbi zilifurika, iwe Dar es Salaam, Morogoro au Mwanza, mashabiki walikuwa wakifurika ukumbini kutushuhudia.

“Ni ushindani uliosababisha mashabiki wetu wajenge uhasama mkubwa, lakini sisi wasanii tulikuwa kitu kimoja. Wengine walidhani mimi na Nasma tulikuwa na uadui kutokana na nyimbo tulizoimba, kumbe tulikuwa marafiki wakubwa na tulisaidiana kwa kila hali,”alisisitiza Khadija Kopa.

Amekiri kuwa ushindani wa taarab umepungua katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo kwa utitiri wa vikundi vya muziki huo.

Aidha, alisema maonyesho ya vikundi hivyo vimekuwa vikifanyika muziki kuanzia Jumatatu hadi Jumapili, hivyo kuwafanya wasanii wake kuchoka na kukosa ubunifu.

“Kinachosikitisha zaidi ni kuona kuwa baadhi ya vikundi vya mitaani vimekuwa vikiimba nyimbo za vikundi vingine katika maonyesho yao, ambayo yamekuwa yakifanyika bure hadi mashabiki wanachoka.

“Utakuta kikundi kimoja kinafanya onyesho mtaa huu, kingine kinafanya onyesho mtaa wa pili. Huyu akisikia mwenzake amekwenda kufanya maonyesho Lindi na mwingine naye anakwenda huko huko”, alifafanua Khadija Kopa.



Ushoga na taarab.

Akizungumzia madai ya kuwepo kwa uhusiano kati ya muziki wa taarab na Ushoga, Khadija alisema si kweli kwa sababu kumjua shoga kunahitaji ushahidi wa uhakika.

“Ushoga ni nafsi ya mtu kupenda kitu, si maumbile au mwonekano wake,”alisisitiza mwanamama huyo.

Mwimbaji huyo alieleza kusikitishwa kwake kwa tabia ya baadhi ya mashabiki wa muziki huo, hasa wanawake, kucheza kwa kukata viuno na pia kuvaa mavazi yanayowaonesha wakiwa nusu uchi.

Alisema japokuwa kukata viuno ni asili ya Mwafrika, lakini uvaaji wa mavazi ya nusu uchi si wa kistaarabu, umepitiliza na unachangia kushusha hadhi ya muziki huo na kuufanya uonekane kuwa wa kihuni.

“Tatizo hili halipo kwenye muziki wa taarab pekee, hata hip hop muziki wa dansi na bongo fleva, utakuta wacheza shoo wa kike wamevalishwa nguo za nusu uchi. Mbona wanaume hawavai nguo za aina hiyo”. Alihoji msanii huyo.

Amesema imefikia hatua hivi sasa, mzazi hawezi kutazama televisheni akiwa na watoto wake, vinginevyo analazimika kuwa na ‘remote’ mkononi ili kukitokea tukio la aibu, aweze kuzima televisheni mara moja ama kukimbilia nje ili kuepuka aibu.

Khadija amekiri kuwa umaarufu kwa wasanii ni mzuri, lakini wakati mwingine umekuwa ukiwasababishia madhara ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa mambo ya uongo.

“Binafsi niliwahi kuzushiwa kwamba nilimuua mwanangu Omar Kopa, eti nijiongezee umaarufu baada ya kuonekana amenizima.

Hata Leila Khatib alipokufa, niliambiwa kwamba mimi ndiye niliyemuua!”alizungumza kwa uchungu Khadija Kopa.

Aliongeza kuwa, mbaya zaidi siku ambayo Leila alizikwa, hakuweza kuhudhuria kwenye mazishi kutokana na yeye kufiwa na bibi yake, hali iliyozidisha uvumi huo.

“Ukiwa msanii mzuri, unageuzwa kama Malaika mtoa roho. Msanii mwenzako akiumwa, unaogopa hata kwenda kumuangalia,” alisema.

Khadija amekielezea kifo cha aliyekuwa mkurugenzi wa kikundi cha TOT Plus, Kepteni mstaafu, John Komba kuwa ni pigo kubwa katika fani ya sanaa nchini.

Amesema si rahisi kwa pengo la Kepteni Komba kuzibika kutokana na vipaji alivyokuwa navyo, isipokuwa anaweza kutokea msanii atakayeleta ahuni.

“Kuziba pengo lake si rahisi, litabaki kama lilivyo,”alisisitiza msanii huyo, ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa TOT.

Kopa alisema kinyume na uvumi kuwa kundi la TOT taarab limesambaratika, siyo kweli bado lipo na linaendelea kuwakonga nyoyo za wapenzi mashabiki wake.

Amesema TOT ni kikundi kikubwa kinachokuwa katika shughuli nyingi zikiwemo siasa wakati mwingine hata za serikali.

Mwimbaji Khadija Kopa ametamka kuwa anao mipango ya kutoa albamu yake ya kibinafsi, tayari wimbo wake “Mji ni Chuo Kikuu” unachezwa na vituo vingi vye redio.

“Katika TOT tumetoa albamu hivi juzi juzi. Hii yaitwa Fullstop, tunajitayarisha kufanya mkanda wa video. Lakini mimi mwenyewe nataka kutoa albamu yangu Mji ni Chuo Kikuu. Itakuwa na nyimbo nne ambazo baadhi nimewashirikisha Fatma Issa na Saada Mohamed” alisema Khadija Kopa.

Aidha amewataka wapenzi wa muziki wa taarab wasiwe wepesi wa kutaka kusikiza nyimbo zilizotengezwa vichochoroni na watu wasiowajali waimbaji halisi.

Kila kazi ina mafanikio, miongoni mwa mafanikio aliyoyapata Khadija kutokana na muziki huo, ni pamoja na kutembelea nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani.

Pia amefanikiwa kuanzisha kundi lake linalojulikana kwa jina la Ogopa Kopa Classic Music.

Kundi hilo linaundwa na wasanii wasiozidi 10, akiwemo mtoto wake wa mwisho wa kiume, anayefahamika zaidi kwa jina la Black Kopa.

Moja ya malengo yake ni kurekodi upya nyimbo zake zote alizowahi kuziimba akiwa katika vikundi mbalimbali.

Khadija iwapo mipango yake hiyo itafanikiwa, anatarajia kuanzisha miradi mbalimbali ya kikundi kwa lengo la kuwaongezea wasanii mapato.

Pia amepanga kuwashawishi wasanii wake wajiunge na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kujiwekea akiba kwa maisha yao ya baadaye.

Khadija hakuwa tayari kuzungumzia kwa kirefu ndoa yake na mumewe, aliyefariki mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, ambaye inadaiwa alikuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Ndoa yake

Alisema halikuwa jambo la ajabu kwake kuolewa na mwanaume mwenye umri mdogo kwa sababu hata Mtume Muhammad SAW na mkewe Khadija, walifunga ndoa wakiwa wanatofautiana umri kwa miaka mingi.

“Mume wangu alikuwa anajuwa kunitunza, nikienda kwenye maonyesho alikuwa akinifuata, tunarudi nyumbani pamoja, sijui kama naweza kumpata mume mwingine bora kama yeye. Kama atajitokeza, itabidi nimchunguze sana,”alisema Khadija huku akitabasamu.

Khadija ametoa mwito kwa wasanii wa muziki wa taarab kuwa na umoja kama ilivyo kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ikiwa ni pamoja na kurekodi nyimbo pamoja.

“Inasikitisha kuona sisi wasanii wa muziki wa taarab, hatuna uwezo wa kufanya hivyo. Bongo fleva wanaungana na kuimba pamoja, lakini sisi hatuna uwezo huo. Mbaya zaidi hatuna mapromota na mameneja wa kutuvusha kutoka hapa tulipo,”alilalamika.

Taarab Nairobi.

Licha ya kuhusishwa kuwa muziki wa taarab ni mhsusi kwa wakazi wa Pwani, miaka ya hivi karibuni muziki huo umeibuka kuwa maarufu mno jijini Nairobi nchini Kenya.

Unapotaja taarab jijini humo, mtaje pia Khadija Kopa ambaye mashairi yake huwaacha mashabiki wake wakipagawa.

‘Malkia wa Mipasho’ anashabikiwa mno kwa nyimbo zake za kuwapa vidonge vyao, kila anapotangaza kuandaa shoo jijini Nairobi, tiketi huuzwa na kuisha kabla ya siku ya tamasha.

Alipokuwa na tamasha jijini Nairobi hivi karibuni, mama huyo alivutia mno na mashabiki wa rika tofauti ambao si kawaida kwao kufika katika matamasha. Tamasha hilo lililodhaniwa na Wakongwe hasa wale wa Pwani.



Ulanguzi wa kazi zao.

Mwimbaji huyu mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, amelalamikia kuhusu ukosefu wa ushirikano wa kutosha kutoka kwa mashabiki ambao kwa kawaida wanapenda kununua kanda zilizo kughushiwa, zile zilizonaswa na walanguzi na badala yake kuziacha za wasanii halisi.

“Tunatengeneza nyimbo zetu halafu sisi wenyewe hatufaidiki, watu wanaingilia kazi zetu. Kwa mfano mimi nimeanza kuimba muda mrefu sasa, lakini bado kazi zangu hazijaniletea faida”, alilalamika Kopa.

Khadija Omar Kopa ndiye aliyeviporomosha vibao kadhaa vikiwamo vya “Y2K”, “Utaishia Kunawa”, “Top In Town”, “Full Stop”, “Full Kujiachilia”, “Gendaeka”, “Mambo iko Huku”, “Nalijua Jiji” ni miongoni mwa zingine nyingi.

Mwisho.

Mwandaaji wa makala hii anapatikana kwa namba: 0784331200, 0736331200, 0767331200 na 0713331200.





MKURUGENZI WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) AFUNGUA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI LEO

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu wa Rais wa Tatu wa shirika la Hali ya Hewa (WMO) Duniani Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambo kuhusu utabiri wa mvua za vuli ambao utatangazwa kesho mara baada ya kufungua semina ya wanahabari inayofanyika leo kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .
Bw. Samwel Mbuya Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri TMA akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes Kijazi kufungua semina kuhusu utabiri wa mvua za vuli ambao utatangazwa kesho kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .
Abubakar Lungo Mchambuzi wa Utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari inayofanyika Makao makuu ya TMA Ubungo Plaza, kuhusu utabiri wa mvua za vuli unaotarajiwa kutolewa kesho na mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambo kuhusu utabiri wa mvua za vuli ambao utatangazwa kesho mara baada ya kufungua semina ya wanahabari iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .

RUGEMALILA, SETHI WAANDIKA BARUA KWA DPP YA KUOMBA MSAMAHA NA KUKIRI MASHITAKA YA UHUJUMU UCHUMI

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WAMILIKI wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi na James Buchard Rugemalira, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuomba msamaha na kukiri mashitaka ya uhujumu uchumi yanayowakabili mahakamani hapo.

Hata hivyo imebainika kuwa,  Seth aliandika barua yake hiyo iliyopitia kwa mkuu wa Gereza Mapema Mwezi huu baada ya msamaha huo kutangazwa na Rais Dk John Magufuli ambaye alimuelekeza DPP kuwa washtakiwa wenye mashtaka ya uhujumu uchumi ambao wako tayari kukiri makosa yao waandike barua ya kuomba msamaha ili kurejesha hasara waliyosababisha. 

Mapema leo asubuhi Oktoba 10, 2019  Wakili Michael Ngaro anayemtetea Rugemalira amedai kuwa mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi yanayomkabili na kwamba mpaka sasa hawajapata majibu.

Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, 2017. 
wanakabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya USD 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27 

Kufuatia taarifa hiyo Ngaro ameuomba upande wa mashitaka kufanya mchakato ili wapate majibu ya barua hiyo haraka

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa, ni kweli wamepokea barua za washtakiwa wote wawili na kwamba zinafanyiwa kazi na watapatiwa majibu.

Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa imeahirishwa hadi Oktoba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena

Seth na Rugemalira wako gerezani kwa mwaka wa tatu sasa kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Washitakiwa hao wanadaiwa, kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Aidha, katika mashtaka ya kujipatia fedha inadaiwa, kati ya  Novemba 28 na 29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la Mtakatifu Joseph,  kwa ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27.  

Pia washtakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ambapo inadaiwa, Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la  kati kinondoni, kwa vitendo vyao waliisababishia serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Kati ya Novemba 29,2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT ambazo ni USD milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4  wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

KLABU YA ROTARY YA MZIZIMA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE

0
0
 Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam,Dkt. Emeria Mugonzibwa  akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani  leo jijini Dar es salaam kabla  ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule hiyo.

Rais Mstaafu wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Dkt. Emeria Mugonzibwa akikabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam kwa wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum wa Shule  Sekondari Jangwani  leo jijini Dar es Salaam.

WALENGWA WA TASAF WILAYANI RUNGWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWAKUMBUKA.

0
0
Na Estom Sanga- RUNGWE. 

Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko huo na kuonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini . 

Kabla ya kutembelea halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi ya Taifa ya TASAF,walikutana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya ,Bw. Albert Chalamila ambaye amewaeleza wajumbe hao kuwa utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo imeleta hamasa kubwa kwa wananchi kuuchukia umaskini kwa kufanyakazi kwa bidii. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya amesema licha ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutotekelezwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo,mafanikio yake yamesababisha wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za Mpango huo kuomba wajumuishwe ili nao waweze kunufaika na utaratibu huo wa serikali wa kuzifikia kaya maskini. 

Aidha Bw. Chalamila amesema sekta za elimu, afya,na shughuli za uzalishaji mali vimepata msukumo mkubwa kwa kaya za Walengwa wa TASAF ambao kabla ya kuanza kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini waliishi katika hali ya unyonge uliosababishwa na umaskini wa kipato jambo ambalo amesema limepungua kwa kiwango kikubwa baada ya Serikali kupitia TASAF kuanza kutekeleza Mpango huo. 

Wakiwa Katika halmashauri ya wilaya Rungwe,Wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi ya taifa ya TASAF wamepata fursa ya kukutana na baadhi ya Wananchi wanaonufaika na huduma za Mfuko huo ambao wameonyesha baadhi ya mafanikio waliyopata hususani katika sekta ya uboreshaji wa makazi, elimu,afya na huduma ya maji ambayo wamesema umewasaidia kuboresha maisha yao na kuwapa hamasa kubwa ya kukabiliana na umaskini. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo,Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Naftal Ng’ondi amewahimiza walengwa wa TASAF kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuunga mkono jitihada za serikali za kuondoa kero ya umaskini miongoni mwao,kwani amesema mkakati huo unapaswa kuwa wa muda ili waweze kupisha wananchi wengine waweze kunufaika nao. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akijibu hoja ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi katika maeneo ambayo hayakujumuishwa kwenye huduma za Mpango, amesema serikali imeamua katika sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini maeneo yote nchini yajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo. 

Bwana Mwamanga amesema uamuzi huo wa serikali ambao unaweka msisitizo kwa Wananchi watakaojumuishwa kwenye Mpango kufanyakazi za maendeleo watakazozibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kwa kazi hizo jambo ambalo amesema litachangia kuboresha maisha yao. Hata hivyo amefafanua kuwa Walengwa ambao ni wazee , wagongwa wa muda mrefu, watoto yatima na walemavu ambao hawana msaada wataendelea kupata huduma za uhawilishaji fedha ili waweze kujikimu .
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF wakipata maelezo ya namna chanzo cha maji kilichojengwa katika eneo la Bulyaga Juu ,nje kidogo ya mji wa Tukuyu kilivyojengwa kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF.Maji hayo hayakauki katika kipindi chote cha mwaka.

 Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya TASAF,Dkt. Naftal Ng’ondi (mwenye kote cheupe) akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa Walengwa wa TASAF katika chanzo cha maji kilichojengwa wa TASAF katika eneo la Bulyaga juu ,halmashauri ya Rungwe kwa utaratibu wa Ajira ya Muda.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyeinama) akigusa maji kwenye chanzo cha maji kilichojengwa na Walengwa wa TASAF katika eneo la Bulyaga juu, nje kidogo ya mji wa Tukuyu kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Albert Chalamila (aliyevaa suti ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya uongozi waTaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF na menejimenti ya Mfuko huo baada ya kukamilisha mazungumzo ofisini kwake. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga.

WAZALISHAJI WA CHUMVI MKOANI TANGA WAJENGEWA UWEZO KUONGEZA UZALISHAJI BORA

0
0
 MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha Neelkanth Salt Ahmed Liemba akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur
 Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha  Neelkanth Salt Ahmed Liemba
 MKURUGENZI wa  Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi cha  Neelkanth Salt Liemba akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur
 Sehemu ya wachimbaji wa madini ya chumvi wakiwa kwenye mkutano huo


MENEJA wa Kiwanda cha Kuzalisha Chumvi  cha Neelkanth Salt Ahmed Liemba amesema kwamba wamelazimika kuwajengea uwezo wazalishaji wa ndani namna ya kuongeza uzalishaji bora ili malighafi wanazozalisha iweze kuwa na ubora ambao utakuwa na tija kubwa.

Ahmed aliyasema hayo wakati wa kikao cha kujadili changamoto za wazalishaji chumvi mkoani Tanga ambapo alisema kwamba licha ya kuwa hapa nchini kuna maeneo mengi makubwa ya uzalishaji wa malighafi hiyo lakini bado haina ubora ambao unahitajika kwenye viwanda vya ndani.


Alisema kwa kuliona hilo wao kama kiwanda wamelazimika kukutana na wazalishaji hao ili kuweza kuwapa maelekezo ni aina gani ya chumvi ambayo wanahitaji kwa sasa ili waweze kujipanga kuongeza uzalishaji huo ambapo pia walipatiwa elimu kutoka kwa wataalamu wa kiwanda hicho.


Meneja huyo alisema pia kwamba uwepo wa uhaba wa Chumvi yenye ubora nchini umesababiosha wenye viwanda kulazimika kuagiza malighafi hiyo kutoka nje ya nchi ili kuweza kukidhi mahitajio ya soko la ndani jambo ambalo wamelazimika kutumia gharama kubwa.


“Sisi kwenye kiwanda chetu kwa siku tunahitaji tani 300 za malighafi huku uzalishaji ukiwa ni tani 250 kwa siku huku zaidi ya tani 50 ikipotea kutokana na ubora duni wa malighafi hivyo mkutano huu utakuwa chachu kubwa ya kuweza kuondosha changamoto za namna hiyo “Alisema


Aidha alisema kwamba changamoto kubwa ilikuwa ni kwamba wazalishaji wengi hasa watanzania wanazalisha chumvi ambao haina ubora kutokana na kwamba hawana elimu licha ya kwamba Tanzania kuna maeneo mengi ya ukanda wa bahari hivi sasa wameamua kushirikiana nao ili kukuza sekta ya chumvi nchini.


Meneja huyo alisema kwamba malengo yao soko la Tanzania  ni kuweza kukamata soko la ndani na nje  ikiwemo kuendelea kutoa elimu ikiwa ni msisitiza wa Rais Dkr John Magufuli ya serikali ya viwanda hivyo wao kama wazawa wameamua kuingia kwenye sekta hiyo na wataweza.


Awali akizungumza Mwenyekit wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi mkoa wa Tanga Abdul Nuur-alisema kwamba lazima wachimbaji wawe wazi kulipa kodi zao zinavyotakiwa ili waweze kuonekana wanachangia kwa serikali kwani hilo ndilo jambo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo.


Naye kwa upande wake Afisa Mkazi wa Madini mkoa wa Tanga Zabibu Napacho alisema ili wachimbaji wa chumvi wazalishe lazima waweze kukidhi vigezo vya uzalishaji huku akiwaeleza kwamba wao kama ofisi ya madini watakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwao wawekezaji ili waweze kuendeleza zao hilo la chumvi na madini hayo.


Hata hivyo alisema pia changamoto kubwa ni ukosekanaji wa masoko lakini wanaishukuru kampuni ya Neelkat kuja Tanga na kuwawezesha wachimbaji kupata soko la uhakika.


“Lakini naomba mapato ya serikali kila mmoja awe mfanyabiashara hai mwenye leseni ya uchimbaji wa madini ya chumvi…wale ambao hawana leseni wahakikishe wanakuwa nazo “Alisema

KADI YA MPIGA KURA HAITATUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0
0
Na. Idara ya Habari-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya mazoezi mawili tofauti yanayoendelea Nchini ya kuandikisha wapiga kura na kuwatahadharisha kwamba Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume haitatumika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwenzi ujao.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo (10.10.2019), Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kwamba uandikishaji unaoendelea ambao ulianza tarehe 08, Oktoba 2019 unahusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019 ambao hausimamiwi na Tume.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu wananchi kuwa uandikishaji unaofanyika kuanzia tarehe 08, Oktoba 2019 hadi tarehe 14, Oktoba 2019 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) kupitia Halmashauri mbalimbali kote Nchini unahusika na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019. Mwananchi asipojiandikisha hataweza kupiga kura katika uchaguzi huo,” amesema Dkt. Mahera.

Aliongeza kwamba mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye uandikishaji unaofanywa na OR-TAMISEMI hatapata fursa ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24 mwaka huu, hata kama atakuwa na Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume na kwamba uchaguzi huo hausimamiwi na Tume bali unasimamiwa na OR-TAMISEMI

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo la kujiandikisha ili wapaete fursa ya kuwachagua viongozi wa mitaa yao siku hiyo ya tarehe 24 Novembe 2019.

Aidha, Dkt. Mahera amesema kwamba Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ina jukumu la kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara.

“Uandikishaji huo (wa OR-TAMISEMI) ni tofauti na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaofanywa na Tume kwenye mikoa mbalimbali Nchini. Uboreshaji huu unahusu Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara utakaofanyika mwakani 2020,” amesema.

Dkt. Mahera ameeleza kwamba zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaendelea kwa sasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ambako uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 14 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba mwaka huu.

Ameongeza kwamba zoezi hilo litaendelea kwenye mikoa ya Songwe, Dodoma na Singida kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi tarehe 01 Novemba 2019.

“Wanaostahili kujiandikisha ni wale ambao wana miaka 18 na wale ambao watafikisha miaka 18 mwakani (2020) kabla ya uchaguzi, lakini pia zoezi linawahusu wale ambao kadi zao zimeharibika au zimepotea ili wapate fursa tena ya kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” alismema Dkt. Mahera.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images