Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live

MAKUNDI MAKUU MANNE YA AFRIKA YAKUTANISHWA HAYDOM

0
0
Msanii Paschal Daniel wa Pamoja Central Group wa Mwanza akizungumza kwenye tamasha la nane la utamaduni Haydom.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu (katikati) akikagua maeneo ya kituo cha pembe nne za utamaduni (4CCP) Haydom. 


NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu amehitimisha tamasha la nane la utamaduni Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, lililokutanisha makundi makuu manne ya lugha za Afrika, kwa kuitaka jamii ithamini utamaduni kwani una uwezo mkubwa wa kukuza utalii. 

Kanyasu aliyasema hayo kwenye tamasha la nane la pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) lililojumuisha vikundi vya sanaa vya mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema utamaduni una nguvu kubwa ya kuongeza watalii wengi hapa nchini kwani ni kivutio ambacho hakichoshi kuangalia kila wakati hivyo fursa hiyo ichangamkiwe. 

“Kuna nchi hazina mbuga, hifadhi, wala wanyamapori lakini wanapata watalii wengi kutokana na utamaduni walionao kwani unaweza kumuona tembo na kisha usirudi tena mwakani lakini utamaduni utarudi kila mwaka,” alisema. 

Mratibu wa 4CCP Eluminatha Awet alisema Haydom ni kitovu cha Afrika kwani ni sehemu pekee inayokutanisha tamaduni nne tofauti na kuziweka mahali pamoja. 

Awet alisema jamii nne Afrika za wanailotiki (datoga), wakushiti (iraqw), wakhoisans (wahadzabe) na wabantu wamekutana kwenye tamasha hilo.

“Makundi makuu ya lugha za Afrika yamekutana mahali hapa licha ya tofauti zao za lugha, mfumo wa maisha, tamaduni na hata shughuli za kiuchumi,” alisema. 

Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema kituo hicho cha utamaduni kimeasisiwa na raia wa Norway marehemu Dk Halgrim Olsen.

Mofuga alisema marehemu Dk Olsen alifanya maendeleo mengi enzi ya uhai wake ikiwemo ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Haydom na kituo cha polisi Haydom. 

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay alisema naye ni miongoni mwa waanzilishi wa tamasha hilo akiwa msanii wa Tumaini sanaa group. 

Massay aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwapatia mizinga ya nyuki 100 ambayo waliikabidhi jamii ya wahadzabe wa bonde la Yaeda Chini.

Mkazi wa Haydom Elias Bura amepongeza hatua ya 4CCP kuandaa jambo hilo la kihistoria ambalo huu ni mwaka wa nane tangu waanzishe.

“Tumeona ngoma, kurusha mishale, mikuki, kuchapana, nyumba zao, mavazi na vyakula vya utamaduni tofauti ya jamii kubwa nne za Afrika hapa Haydom,” alisema. 

Tamasha hilo limefanyika kwa siku nne na kuhusisha vikundi 15 vya sanaa za ngoma kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Singida na Mwanza.

VILABU 40 KUSHIRIKI MASHINDANO YA DRAFT IRINGA

0
0
Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa kusukuma kete (Draft) katika kijiwe cha M.R. wakiendelea kupambana katika michezo kutafuta bingwa wa mchezo huo mkoa wa Iringa. (Picha na Denis Mlowe) .

***********************************

NA DENIS MLOWE,IRINGA

JUMLA ya Vilabu 40 vimejitokeza kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa kusukuma kete (draft) manispaa ya Iringa yanayojulikana kwa jina la Ngajilo Draft Championship 2019 yaliyozinduliwa rasmi juzi katika kijiwe cha M.r Hotel.

Mratibu wa mashindano hayo, Temihanga Kabambe alisema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwakusanya watu pamoja mara baada ya kazi za kutwa kuchwa kuweza kudumisha umoja na amani kwa manispaa ya Iringa na kukutanisha wadau wa mchezo huo na kuleta mwamko kwa jamii kushiriki mchezo huo.

Kabambe alisema kuwa mchezo wa draft ni miongoni mwa michezo inayopendwa na kila rika ambapo amewataka wachezaji hao kuungana kwa pamoja na kuutangaza mchezo huo ambao kwa manispaa ya Iringa umekuwa moja ya michezo unaotumika zaidi watu kufahamiana.

Alisema kuwa kutokana na vijiwe vingi kujitokeza katika mchezo huo tofauti na mashindano ya kwanza, mkakati moja wapo ni kukuza mchezo wa draft na kuutambulisha mchezo huo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa hivyo 

ili kuinua mchezo huo kuna kila sababu ya kuwa na mashindano ya mara kwa mara kuibua vipaji vitakavyoweza kuutangaza mchezo huo.

Alisema kuwa katika kuandaa mashindano hayo wamefanikiwa kusajili vilabu vyote katika manispaa ya Iringa ambapo vimekubali kushiriki mashindano hayo yenye msisimko mkubwa kwa kuweza kukusanya watu mbalimbali tangu yamezinduliwa katika vilabu husika kuweza kupata mwakilishi atakayeingia kwenye nafasi za kumtafuta bingwa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika Oktoba 19 mwaka huu mgeni rasmi atakuwa mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo ambapo timu alizitaja baadhi zinazoshiriki baadhi ni kutoka vilabu vya , Kihesa, Mshindo, Mlandege, M.r, Stand ya Pawaga, Mjimwema, Nduli, Isikalilo, Isoka, Mwangata, Don Bosco na Lukosi.

Alivitaka vilabu vyote kucheza kwa amani kama ambavyo lengo la mashindano hayo kujenge urafiki, amani na kufahamiana ili kuweza kupata bingwa sahihi katika mashindano hayo ambayo hadi sasa washiriki zaidi ya 6 wamejihakikishia kuingia katika fainali za kumtafuta bingwa kutoka katika vilabu wanavyotokea.

Katika mashindano hayo bingwa ataondoka na kitita cha shilingi 500,000 mshindi wa pili sh, laki 200,000 na mshindi wa tatu sh,100,000 huku bingwa wa kila Vilabu atakayeshinda nafasi za kuwakilisha katika kutafuta bingwa wa manispaa ataondoka na sh. 10,000 

Kwa upande wake, mfadhili wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo alisema kuwa mchezo wa kusukuma kete unachezwa na watu wengi katika jamii na mmoja ya michezo inayotumia sana akili katika kuucheza na hata wachezaji wake wana akili hivyo endapo wataanzisha chama chao kitakuwa na umuhimu sana katika jamii hasa kuwakutanisha watu na kubadilishana mawazo.

Ngajilo alisema kuwa mchezo huu wa jadi hauchukuliwi kipaumbele kama ilivyo kwa michezo mingine hali ambayo mkiwekeza katika mtindo wa kisasa zaidi uhakika wa wadau wengine kujitokeza na kudhamini itawezekana kwani moja ya michezo pendwa kwa sasa na rika mbalimbali.

Alisema kuwa mchezo wa draft una changamoto mbalimbali lakini endapo wadhamini wakiwekeza katika mchezo huu ndio asili ya mtanzania kwani ndipo kwenye watu ambao wanajenga uchumi, kujenga jamii iliyobora kutokana na kubadilishana mawazo katika misingi ya kiakili zaidi.

Alisema kuwa lengo la kudhamini mashindano hayo ni kuleta hamasa kubwa na kuchochea watu wengi washiriki katika mchezo wa kusukuma kete lakini pia mchezo wa draft uwe mkubwa zaidi na kuufanya wa kisasa zaidi kwa kuhakikisha kila kata wanashiriki na kutumia kumbi za kisasa zaidi kufanyika kwa mchezo huo.

“Lengo kuufanya mchezo huu kuwa wa kisasa zaidi na mchezo wa draft ni mchezo wa akili sana na kama huna akili huwezi cheza mchezo huu kwani unataka akili sana na kuwe na mahusiano ya akili na viungo aidha unaletea afya ya akili naupenda mchezo huu kwa kuwa unaleta changamoto za akili kuweza kushiriki” alisema

Alisema kuwa endapo wakiamaua kuufanya mchezo huu kisasa zaidi uhakika wa watu wengi kujitokeza zaidi kudhamini hivyo wachezaji ndio chachu ya mafanikio ya mchezo huu kuweza kudhaminiwa na makampuni mbalimbali.

Naye bingwa wa msimu uliopita, Juma Athuman ‘Bin Kulijua’ alisema kuwa anatarajia mwaka huu kuchukua tena ubingwa huo kwa kuwa washiriki wote wanaoshiriki uwezo wao uko chini sana na amejipanga vyema kujishindia sh. laki 5 ambazo zinatolewa na mdhamini wa mashindano hayo Ngajilo.

Athuman alimshukuru mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo na kwa kuweza kudhamini mashindano hayo kwani wadau wengi wako zaidi katika michezo mingine na kushindwa kuwafikia mashabiki na wachezaji wa mchezo wa jadi ambao hata mwasisi wa taifa Julias Nyerere alikuwa anaucheza na kumwahakikishia kwamba watatumia mchezo huo kuweza kuleta changamoto chanya katika jamii na kujenga mshikamano.

ML 280 KUMALIZA KERO YA MAJI TUNDURU

0
0
Na Mwandishi Wetu,Tunduru

JUMLA ya shilingi milioni 280 zinatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika vijiji vinne vya kata ya Misechela Jimbo la Tunduru Kusini mkoani Ruvuma.

Mbunge wa Jimbo hilo Daimu Mpakate amesema hayo kwa nyakati tofauti wakati akiongea na wakazi wa kijiji cha Misechela na Mkaleka katika ziara yake ya kusikiliza kero na kuongea na wananchi wa vijiji mbalimbali katika jimbo lake.

Kwa mujibu wa Mpakate,Serikali kupitia wakala wa Maji vijijini imetenga kiasi hicho cha fedha ili kutekeleza mradi wa maji ambao mara utakapokamilika utawezesha kumaliza kabisa kero ya maji iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Alisema, mbali na fedha hizo Ofisi ya Mbunge kuanzia Mwezi Novemba mwaka huu itaanza kazi ya kuchimba visima vifupi na virefu katika baadhi ya vijiji ambavyo vina tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Aidha alisema, wakala wa Bara bara mjini na vijijini(TARURA) wilaya ya Tunduru nayo imetenga shilingi milioni 118 kwa ajili ya ukarabati wa Bara bara ya Tunduru Mjini- Amani,Chiungo, Mea Mtwaro, Misechela na Bara bara ya Liwanga Misechela ambazo zimeharibika kutokana na mvua za masika.

Alisema, kazi hizo zitaanza mara baada ya kupatikana kwa Wakandarasi ambao watapewa dhamana ya kujenga miradi hiyo mikubwa katika kata ya Misechela na kata nyingine katika Jimbo la Tunduru Kusini,ambapo amewaomba wananchi wa vijiji vitakavyopitiwa na miradi hiyo kutoa ushirikiano kwa wakandarasi na kujiepusha na vitendo vya wizi ili iweze kukamilike kwa wakati.

Mpakate alisema, Ofisi ya Mbunge kupitia mfuko wa Jimbo kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano,imejipanga kuhakikisha inamaliza kero zote za wananchi ambazo zinakwamisha kuharakisha maendeleo na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Pia alisema, ili kuhakikisha wanafunzi hawapoteza muda wa masomo kwenda kutafuta huduma, yeye kama Mbunge amefunga mashine za kusaga nafaka kwenye shule za Sekondari 14 ili zitumike kusaga mahindi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi hasa baada ya kubaini kuwa wanafunzi wanatumia muda mwingi na kutembea umbali mrefu kwenda kusaga nafaka.

Alisema, katika utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo michango na nguvu za wananchi ni jambo la muhimu sana kwani fedha zinazotengwa na Serikali ni ndogo,kwa hiyo ni lazima wananchi wenyewe nao waanze kuchukua hatua ili serikali iweze kuwaunga mkono.

Katika hatua nyingine,Mpakate amewataka wenyeviti wa vitongoji,vijiji na watendaji wa vijiji kuwakamata wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika maeneo yasioruhusiwa ili kuepusha kutokea migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa Serikali ya wilaya imeshatenga vitalu maalum kwa kwa ajili ya ufugaji.

Mpakate amewaonya viongozi wa vijiji kuacha tabia ya kuuza Ardhi kwa wageni, kwa lengo la kujipatia fedha badala yake kuwaelekeza wafugaji katika maeneo waliyotengewa.

Alisema, baadhi ya viongozi hao wamejiingiza katika biashara haramu ya kuuza na kutoa Ardhi kwa wageni wakiwemo jamii ya wafugaji ambao wamevamia kwa wingi katika vijiji mbalimbali wilayani Tunduru.

Alisema, Serikali haitawavumilia viongozi wanaojihusisha na suala la kuuza Ardhi kiholela na kuwataka viongozi wa umma kujiepusha na vitendo vya ukiukaji wa Sheria za Ardhi badala yake waendelea kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma Bora.

Alisema, baadhi ya tabia ya viongozi hao wana tabia ya kuwakamata wafugaji hata wakiwa bara barani na kuwatoza fedha ambazo haziendi Serikalini jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

“ ni lazima tufuate sheria hawa wafugaji ni Watanzania wenzetu,viongozi acheni kuwanyanya badala yake mnapo wakuta bara bara wakisafirisha mifugo waelekezeni maeneo yaliyotengwa,mkifanya hivyo wafugaji watakauwa tayari kuchangia shughuli zote za maendeleo katika vitongoji na vijijini vyenu” alisema Mpakate.
 Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Daimu Mpakate kulia akiwasikiliza baadhi ya wenyeviti wa vitongoji wanaotuhumiwa kukubali kuingiza mifugo na kuuza Ardhi kwa Wageni katika maeneo yao bila kufuata sheria, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuongea na wananchi katika  jimbo lake,

MAJENGO MATATU YAKABIDHIWA KWA WIZARA YA MADINI

0
0
kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi wakijadiri jambo
kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye
Jengo la kituo cha umahiri lililopo Mkoani Simiyu.




Na Tito Mselem, Simiyu


Naibu Waziri wa Wadini Stanslaus Nyongo akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amekabidhiwa jengo la kituo cha umahiri Mkoani Simiyu.


Mpaka sasa majengo matatu ya Wizara ya Madini yamekabidhiwa baada ya
kukamilika kwa asilimia 100 ambayo yamegharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.4ambapo Wizara kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vitua vya umahiri saba nchi nzima kikiwemo kituo cha Simiyu kilicho gharimu shilingi Bilioni
1.308.

Imeelezwa kuwa kampuni ya SUMA JKT iliingia mkataba na Wizara ya
Madini ili kukamilisha Ujenzi wa Vituo vyote saba nchi nzima ambapo
Kituo cha Simiyu Ujenzi wake ulianza tarehe 5 septemba, 2018 na
kukamilika Septemba, 2019.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Naibu Waziri wa Madini Nyongo alisema Lengo la vituo hivi pamoja na mambo mengine ni kutoa mafunzo ya
kitaalam yahusuyo Madini, mafunzo haya yatahusu Utafiti wa Madini, ikiwa ni pamoja na kuonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo wake, Uchimbaji wa Madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji, pia katika majengo haya kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kutakuwa na usagaji wa mawe na kupima sampuli za madini mbalimbali.

“Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ulifanya utafiti wa kijiolojia
na kubaini maeneo saba muhimu ambayo vituo vya umahiri vitajengwa
pakiwemo Simiyu,” Nyongo alisema.


Baada ya Naibu Waziri kukabidhiwa jengo hilo nae alilikabidhi kwa Tume
ya Madini na kuwataka Ofisi ya Madini Simiyu kulitumia vizuri jengo hilo
ili lilete manufaa yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia
wachimbaji wadogo mafunzo ya namna bora ya kuendesha shughuli zao
ili wafanye shughuli zao kwa ufanisi na hatimae kuongeza makusanyo ya
Serikali.

Wakati huo huo, Naibu Waziri ametoa wito kwa wachimbaji wa madini
na wananchi kwa ujumla wakitumie kituo hicho cha Simiyu ili kujifunza na kupata taarifa kuhusiana na shughuli za utafiti na uchimbaji madini
kwa kuwa kituo hiki kimejengwa kwa ajili ya wananchi na kwa kodi za
wananchi.

Kwa upande upande wake mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka
aliipongeza Wizara ya Madini kwa ujenzi wa kituo hicho muhimu
kitakacho wasaidia wachimbaji wengi wa madini katika Mkoa wa Simiyu.

Aidha wake kaimu meneja wa mradi wa usimamizi Endelevu wa
Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis alisema kuwa mradi huo
umegawanywa katika sehemu kuu tatu ambazo ni kuongeza unufaikaji kutokana na sekta ya Madini kwa Nchi, kukuza uwazi na uwajibikaji katika Sekta ya Madini na Mafunzo na Usimamizi wa Mradi.

“Mradi ulijikita katika kutekeleza kazi mbalimbali zikiwemo ujenzi wa vituo saba vya umahiri, ujenzi wa vituo vya mfano, ukarabati wa ofisi za madini, ununuzi wa vifaa vya ofisi za madini, ununuzi wa samani za ofisi, utafiti wa kijiolojia katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uchimbaji mdogo, na kuongeza ushirikiano na serikali za mitaa zinazofanya shuguli za madini,” Veronica alisema.

“Tumeamua kujenga kituo cha umahiri Simiyu kwa kuwa utafiti wa kijiolojia umebaini kuwepo na mashapo ya kutosha katika maeneo ya Nyaranja Meatu na kuwepo na madini ujenzi, pia Mkoa kuna taarifa za awali za kijiolojia zikionesha utafiti mkubwa wa Madini ya Nickel kule Dutwa na Ngasamo,” Veronica aliongeza.

Vilevile, Wizara kupitia Mradi imejenga jengo la taaluma katika Chuo cha Madini (MRI) kwa ajili ya matumizi ya ofisi, madarasa, kumbi za mikutano na ofisi za ushirika wa wachimbaji madini wanawake Tanzania kwa ajili ya kuendeshea shuguli zao.

Kazi za ujenzi kwa baadhi ya majengo zimekamilika na mengine yapo katika hatua za ukamilishaji na Mkandarasi anatarajia kukabidhi Majengo hayo hivi karibuni kwa jumla ya gharama ya Sh.7.897 kwa majengo yote saba.

VODACOM YATOA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOUNGANISHWA KWENYE MTANDAO WA INTANETI KWA SHULE ZA MKOA WA SIMIYU

0
0


Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akimwelekeza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye jinsi mfumo wa Instant School unavyofanya kazi, tumetoa Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akizungumza na wageni waliohudhuria kwenye sherehe ya makabidhiano ya Kompyuta mpakato 20, Router 10 na uunganishaji Inteneti kwa mwaka mzima kwa shule kumi mkoani Simiyu. 

………………………….


Hii ni sehemu ya ajenda ya Vodacom ya kusaidia ukuwaji wa elimu kwa kupitia mfumo wa kidigitali nchini Tanzania.

8 Oktoba 2019, Simiyu. Kampuni inayoongoza ya Mawasiliano ya Vodacom PLC nchini Tanzania imetoa msaada wa kompyuta na kipanga njia (Router) zenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 48 pamoja na kuunganisha kwenye mtandao wa intaneti kwa shule kumi katika mkoa wa Simiyu kama sehemu ya mpango wake kusaidia ukuwaji wa sekta ya elimu.

Programu hii ni ushirikiano wa pamoja na Mfuko wa Huduma ya Mawasiliano ya (UCSAF) yenye lengo la kushinikiza ujumuishaji wa kusoma kwa mfumo wa kidigitali katika shule Tanzania. Kupitia ushirika huu shule 300 haswa vijijini zitapokea kompyuta na kuunganishiwa mtandao intaneti.

Akiongea katika shule ya Sekondari ya Simiyu mkoani Simiyu, Naibu Waziri wa Kazi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Atashasta Nditiye alisema mchango wa kompyuta unaenda mbali katika kuunga mkono agizo la serikali la kukuza maendeleo ya kijamii vijijini na mijini Tanzania kupitia mfumo wa mawasiliano.

“Vodacom imekuwa mshirika wa serikali katika maendeleo. Nina furahi kuona ushirika huu katika utekelezaji wa mradi wa serikali wa kuunganishwa kwa shule za uma nchini katika mfumo wa kidigitali. Tunashukuru sana kwa mchango huu na tunataka kampuni zingine kuiga zoezi hili katika kusaidia sekta ya elimu.”

Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Foundation, Rosalynn Mworia alisema mpango huo ni sehemu ya ajenda ya kukuza mafunzo bora nchini Tanzania ambao unaelekea kufanikiwa kwa mipango ya maendeleo ya kimataifa. Kompyuta hizo pia zitawezesha shule hizo kuunganishwa mfumo wa upatikanaji wa elimu kwa njia ya kidigitali kupitia mtandao wa Vodacom.

“Tunafurahi kusaidia sekta ya elimu kama sehemu ya mpango wetu wa uwekezaji wa kijamii. Tumeshirikiana na serikali kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayesalia katika utimiaji wa mfumo wa kidigitali. Mbali na uchangiaji wa kompyuta, pia tunasaidia kila shule na kuunganishwa kwenye mtandao wa intaneti bure”. Mworia alisema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UCSAF Justina Mashiba alisema, “Tunajivunia kufanya kazi na Vodacom kuhakikisha mpango wetu unafanikiwa kwa kuunganisha shule zote za uma na upatikanaji wa mtandao ili kutumia kikamilifu vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano”.

“Mchango huu ni kusaidia kazi yetu ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kila mahali haswa katika jamii za pembezoni”.Hafla hiyo ni sehemu ya awamu ya kwanza wa michango ya kompyuta inayotolewa na Vodacom Foundation na UCSAF kwa shule za uma nchini.

Vodacom imekuwa ikishiriki katika kusaidia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari shuleni kupitia mpango wake wa shule nzuri ambapo madawati 75 na kompyuta zilitolewa katika shule za sekondari ya Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja pamoja na shule ya sekondari ya Kinyerezi.

RC GAMBO AIASA BODI YA REA KUITENDEA HAKI NAFASI WALIYOPEWA

0
0
Na Veronica Simba – ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameiasa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), kuitendea haki nafasi waliyopewa na Mheshimiwa Rais John Magufuli; kwa kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na weledi, hususan katika sekta ya nishati ambayo wanaisimamia.

Gambo ametoa wito huo leo, Oktoba 9, 2019 wakati Kamati ya Ufundi ya Bodi hiyo, ilipomtembelea ofisini kwake, ikiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, mkoani humo.

“Itumieni nafasi mliyopewa na Rais kuhakikisha wananchi, hususan walioko vijijini, wanapata nishati ya umeme ili waweze kuboresha maisha yao.”

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa, ameishauri Bodi hiyo kushughulikia maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli, kupeleka umeme katika migodi mbalimbali ya madini ili kuwawezesha wachimbaji kuendesha kazi zao kwa tija.

“Hapa tuna Soko la Madini Karatu, nitafurahi nikisikia mmewapelekea umeme.”Katika hatua nyingine, Gambo ameipongeza REA kwa kuwapelekea umeme wananchi wa Wilaya ya Longido ambao awali hawakuwa kwenye Mpango, lakini kwa maelekezo ya Wizara, walijumuishwa na tayari walikwishaanza kuunganishiwa umeme.

Akizungumza kwa niaba ya Ujumbe huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya REA, Mhandisi Styden Rwebangila amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba watafanyia kazi maelekezo yake.

Amesema, Bodi imempa Mkandarasi NIPO Group, anayetekeleza mradi wa umeme vijijini mkoani Arusha siku 21 kuhakikisha anasimika nguzo zote zaidi ya 1,000 zilizo chini, kuvuta nyaya pamoja na kuwanganishia umeme wananchi wote waliolipia, na kwamba asipotekeleza hayo, hatua za kimkataba zitachukuliwa dhidi yake.

Akitoa takwimu za utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza, mkoani humo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA, Mhandisi Jones Olotu amesema, mkandarasi amefikia asilimia 52 kati ya 62.5 alizopaswa kuwa amefikia hadi sasa.

Aidha, alibainisha kuwa, amewasha umeme katika vijiji 39 kati ya 126 anavyotakiwa kuwasha na ameunga jumla ya wateja 1,880 kati ya 5,428 anaotakiwa kuwaunga kwa Mkoa mzima wa Arusha.

Bodi inatarajiwa kufanya maamuzi dhidi ya Mkandarasi baada ya siku 21 ilizompa kuisha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati), akizungumza na Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), ofisini kwake, Oktoba 9, 2019.

KASI YA USIKILIZAJI MASHAURI IMEMALIZA MRUNDIKANO WA KESI MAHAKAMANI

0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

KATIKA nchi inayoazimia kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi, ni lazima migogoro inayowasilishwa Mahakamani ikamilike kwa haraka ili kuwawezesha wananchi watumie muda wao mwingi katika uzalishaji mali.

Kumekuwa na dhana kuwa mashauri ya jinai na madai yanapochelewa kukamilika mahakamani, basi ni mahakama tu ndiyo inayochelewesha utoaji haki pasipo na kuelewa kuwa katika mnyororo wa utoaji haki kuna wadau muhimu wanaopaswa kutimiza wajibu wao kwa wakati.

Wadau hao ni pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Mashtaka/DPP, Jeshi la Polisi, Mkemia Mkuu wa Serikali, Jeshi la Magereza, Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Tume ya Kurekebisha Sheria (LRC).

Wengine ni pamoja na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Serikali ni wadau muhimu na wezeshi kwa Mahakama na utoaji haki ambao wamekuwa wakishirikiana kwa karibu zaidi na wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu za kimahakama za uendeshaji mashauri, wanahudhuria Mahakamani kadri wanavyoitwa pamoja na kukata rufaa ndani ya muda uliowekwa kisheria.

Hatua zote hizi zitasaidia Mahakama kuwahudumia kwa wakati, na kwa ubora zaidi pamoja na kuwahimiza wananchi kuwa na jukumu la kufahamu taratibu za sharia ikiwemo hatua za mwanzo zinazopaswa kufahamika na mwananchi katika kufungua shauri Mahakamani na kuhakikisha kuwa anafahamu hatua zote kesi yake itapitia katika ngazi ya Mahakama zote hadi Mahakama ya Rufani.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020 Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga anasema kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani ni ni moja ya vipaumbele muhimu vya Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata haki sawa na kwa wakati.

Anaongeza kuwa katika kufanikisha azma hiyo, Mahakama ya Tanzania mwaka 2018 ilianza ikiwa na jumla ya mashauri 65,223, na kusajili mashauri mapya 259,476 katika ngazi zote za Mahakama, ambapo mashauri 255,836 yalitolewa uamuzi ikiwa ni sawa na asilimia 99 ya mashauri yote yaliyofunguliwa katika kipindi hicho.

Dkt. Mahiga anaongeza kuwa mashauri yaliyobaki mahakamani ni 68,863 na kati ya hayo, mashauri yenye umri zaidi ya miaka miwili (mashauri ya mlundikano) ni 3,435 sawa na asilimia 5 tu ya mashauri yote yaliyobaki.

Kwa mujibu wa Waziri Mahiga anasema Kwa ngazi ya Mahakama ya Rufani, mwaka 2018 ulianza na mashauri 2,933 na kusajili mashauri mapya 1,499 ambapo mashauri 1,184 yalisikilizwa na kutolewa uamuzi, sawa na asilimia 79 ya mashauri yote yaliyosajiliwa katika kipindi hicho na mashauri yaliyobaki mahakamani ni 3,248.

’Bila shaka, ongezeko la idadi ya majaji wa Mahakama ya Rufani baada ya uteuzi wa hivi karibuni wa majaji 6 wa mahakama hiyo litasaidia kuharakisha usikilizaji wa mashauri ikilinganishwa na miaka iliyopita’ anasema Waziri Mahiga.

Waziri Mahiga anasema katika ngazi ya Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Kanda na Divisheni, mashauri yaliyokuwepo ni 19,207 na mashauri mapya yaliyosajiliwa ni 18,284 na mashauri yaliyoamuliwa katika kipindi hicho ni 17,046, sawa na asilimia 93 ya mashauri yaliyosajiliwa wakati mashauri yenye umri wa miaka miwili na zaidi ni 1,860 sawa na asilimia 6 ya mashauri yaliyobaki, yakiwemo mashauri 100 yenye miaka 5 na zaidi.

Akifafanua zaidi Waziri Mahiga anasema kwa upande wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya, zilianza mwaka 2018 na mashauri 24,840 na kusajili mashauri mapya 51,161 ambapo jumla ya mashauri 47,089 yalimalizika, sawa na asilimia 92 na kubakiwa na mashauri 28,912, yakiwemo mashauri 837 yenye umri wa kati ya mwaka mmoja na miaka miwili.

‘Mahakama za mwanzo nchini ndizo zinazoongoza kwa kufungua na kusikiliza idadi kubwa ya mashauri kuliko mahakama za ngazi nyingine ambapo katika mwaka 2018 mahakama hizi zilianza na mashauri 15,055 na kusajili mashauri mapya 177,566’ anasema Waziri Mahiga.

Kwa mujibu wa Waziri Mahiga anasema Mashauri yaliyomalizika ni 176,542 sawa na asilimia 99, na kubakia mashauri 16,079 tu kwa nchi nzima na kati ya mashauri 16,079 yaliyobaki, mashauri ya mlundikano yaliyokuwa na zaidi ya miezi 6 Mahakamani kwa ukomo wa Mahakama hizi ni tisa ambayo yapo katika wilaya za Babati (1), Muleba (6) na Tarime (2).

Aidha Waziri Mahiga anasema katika kuimarisha utawala bora, maadili na uwajibikaji wa watumishi, Mahakama ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa huduma za kimahakama katika kanda zote 14 za Mahakama Kuu na kuhusisha vituo 839 vya mahakama.

Anazitaja Mahakama hizo ni pmaoja na Mahakama za mwanzo, mahakama za wilaya na Mahakama Kuu kati ya vituo 980 vilivyopo nchini, sawa na asilimia 86 ikiwemo Vituo vya Mahakama za Mwanzo 717 841 sawa na asilimia 85, Mahakama za Wilaya 97 kati ya Mahakama 111, sawa na asilimia 89 na Mahakama za Hakimu Mkazi vituo 25 kati ya 28 sawa na asilimia 89.

‘Aidha, jumla ya malalamiko 1,046 ya wananchi yanayohusu kero za upatikanaji wa huduma mbalimbali za mahakama yalipokelewa ambapo malalamiko 951, sawa na asilimia 91 yalishughulikiwa’ anasema Waziri Mahiga.

Wadau wa Mahakama wakimaliza wakitimiza wajibu wao kwa wakati, wanaiwezesha mahakama kumaliza mashauri na mwanachi kupata haki yake kwa wakati sambamba na wananchi kusoma sheria ili angalau wawe na uelewa ili kutowaachia wanasheria peke yao jukumu la kufahamu taratibu za sheria.

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU – LINDI

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo kwa Wanakamati ya Maandalizi alipotembelea Uwanja wa Ilulu kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkuani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea uwanja wa Ilulu kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watoto wa halaiki alipowatembea kwa ajili ya kukagua maandalizi yao kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Sehemu ya watoto wa halaiki wakifanya mazoezi ya utayarisho kuelekea Kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Lindi Oktoba 14, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipokea mwamvuli kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania kanda ya Lindi Bw. Zephania Ludigija itakayotumiwa na Watoto wa Halaiki.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ATEMBELEA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa huduma kwa mteja aliyepiga simu katika kitengo cha huduma kwa wateja cha benki hiyo, ikiwa ni muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea hivi sasa Duniani kote. Kushoto ni Afisa wa Benki ya CRDB Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Maria Nyabitwano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifatilia maoni ya wateja mbalimbali waliyoyatuma kupitia mitandao ya kijamii, ikiwa ni muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea hivi sasa Duniani kote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiuliza jambo kwa Afisa wa Benki ya CRDB Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Emmanuel Chance kutoka kwenye moja ya barua pepe iliotumwa na mteja, ikiwa ni muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea hivi sasa Duniani kote. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Yolanda Uriyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimsikiliza Kiongozi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Marvel Kyando alipokuwa akimueleza namna huduma hiyo inavyotokewa na kitengo hicho.


DKT. KIJAJI AIPA TRA SIKU 75 KUANDAA ORODHA KAMILI YA WALIPAKODI, MAJENGO NA MABANGO

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameipa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA miezi miwili na nusu hadi ifikapo Disemba 31 mwaka 2019, kuandaa na kuwasilisha wizarani orodha ya walipakodi, idadi ya majengo na mabango yote yaliyoko katika mkoa wa Dar es Salaam ili kupata takwimu sahihi za idadi ya walipakodi. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke ili kukagua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hayo ili kubaini fursa na changamoto za masuala ya ukusanyaji kodi.

Amesema kuwa pamoja na Mamlaka hiyo kufanya vizuri katika makusanyo ya mapato Mwezi Septemba, 2019, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.78 kimekusanywa, kiasi hicho bado ni kidogo ikilinganishwa na mwamko wa wananchi uliopo hivi sasa katika kulipa kodi.

Aidha Mhe. Kijaji amerejea kuitaka TRA kuwasilisha kwake takwimu ya ongezeko la walipa kodi lililotokana na zoezi la kugawa vitambulisho vya wajasiriamali nchini kwa kuwa lengo la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kugawa vitambulisho hivyo lilikuwa ni kuongeza wigo wa walipa kodi watakao kuwa wanafuzu kwa kuongeza mitaji yao, hivyo ni vyema kujua idadi yao kamili na mahali walipo.

Kwa upande wa kodi ya majengo, Dkt. Kijaji ameitaka Mamalaka ya Mapato Tanzania kuhakikisha inapata orodha ya nyumba zote nchini kwa kuorodhesha wamiliki wa nyumba hizo na mawasiliano yao na kisha kuandaa kanzidata itakayosaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo. 

“Ili kuongeza mapato yanayotokana na kodi ya majengo ni lazima TRA wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kanzidata hiyo inakamilika ambayo itatumika kuwakumbusha walipa kodi kupitia ujumbe mfupi wa simu ambapo itasaidia katika ukusanyaji wa kodi hiyo kama ilivyo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapowakumbusha wananchi kulipa kodi a ardhi kupitia simu zao” Alisema Dkt. Kijaji

“Nataka pia mkague watumiaji wote wa mashine za utoaji risiti za kieletroniki (EFD) kwa wafanyabiashara wa Temeke ili kuhakikisha kila anayeuza anatoa risiti na anayenunua anadai risiti na kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza makusanyo ili Taifa liendelee kujitegemea kimapato” alisisitiza Dkt. Kijaji 

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Bw. Paul Walalaze, alisema mkoa wake una idadi ya walipakodi 437,539 na kwamba katika mwaka 2018/19, mkoa wake ulipanga kukusanya shilingi bilioni 395 na kufanikiwa kukusanya sh. bilioni 328.5 sawa na asilimia 85 ya lengo.

“Tumekusanya pia kodi ya majengo sh. bilioni 1.4 kati ya malengo ya kukusanya bilioni 1.6, kodi ya mabango sh. bilioni 2.2 kati ya lengo la kukusanya sh. bilioni 2.3 sawa na mafanikio ya asilimia kati ya 87 na asilimia 95" aliongeza Bw. Walalaze.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja, amemhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Kijaji kwamba watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwemo kutoa elimu kwa walipakodi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), katikati, akikagua kanzidata ya walipakodi wa majengo na mabango, katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, mkoa wa Kikodi wa Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hellen Gibbe Msimamizi Msaidizi wa Kodi na kushoto ni Msimamizi wa Kitengo cha Mapato yasiyo ya Kodi, wote kutoka TRA-Temeke.
 Mkuu wa masuala ya usimamizi wa Data na Ukaguzi wa ritani Bw. Pius Kunjumu (aliyesimama nyuma) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Hayupo pichani) alipofanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam, kusikiliza fursa na changamoto ya utendaji kazi wa Mamlaka hayo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
 Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Madeni wa TRA-Temeke, Bw. Nicholaus Migera, (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Hayupo pichani) alipofanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam, kusikiliza fursa na changamoto ya utendaji kazi wa Mamlaka hayo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
 Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi hizo za TRA Mkoa wa Kikodi wa Temeke Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Hamisi Lupenja (kulia) na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam. Bw. Paul Walalaze, wakisikiliza hoja za watumishi wa TRA-Temeke, Jijini Dar es Salaam wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi hizo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisikiliza kwa makini hoja mbalimbali za watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Ofisi ya Temeke (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam
Katibu wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Bw. Moses Dulle, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo wakati Dkt. Kijaji aliofanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mkoa wa Kikodi wa Temeke, Jijini Dar es Salaam
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

WADAU WA MASUALA YA WANAWAKE NA WATOTO WAKUTANA KUJADILI KIPEPERUSHI CHA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA

0
0
Mkurugenzi Msaidizi Wizara kutoka Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Jackson Samwel akifungua kikao kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa za hali halisi ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma Oktoba 8, 2019.
Mratibu Taifa wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Bi. Happiness Mugyabuso akizungumza jambo wakati kikao kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA walipokutana Oktoba, 8, 2019 Jijini Dodoma.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya LEDECO Adv. Clarence Kipobota akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA walipokutana Oktoba, 8, 2019 Jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bi. Rennie Gondwe akiwasilisha hoja wakati kikao cha mapitio rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA walipokutana Oktoba, 8, 2019 Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa kikao kazi cha kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa kikao kazi cha kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao kazi cha kazi cha mapitio ya rasimu ya kipeperushi cha taarifa/takwimu za hali halisi ya utekelezaji wa MTAKUWWA wakichukua nukuu wakati wa kikao kazi hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

COCA-COLA KWANZA YADHAMINI MATEMBEZI YA HISANI

0
0
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza inadhamini kwa mara ya nne mfululizo matembezi ya kilomita 5 yenye lengo la kukusanya zaidi ya Tsh 100m kuwasaidia kina mama wenye saratani ya matiti nchini Tanzania. Matembezi hayo yatafanyika Jumatatu 14/10/2019 katika viwanja vya The Green (zamani uwanja wa Farasi).

Fedha nyingine itatumika kuelimisha vijana mashuleni na kusaidia ujenzi wa hosteli ambayo itakuwa inatumiwa na akina mama wanaokuja jijini Dar es Salaam kufuatilia matibabu. Matembezi hayo vile vile yatajumuisha mbio za kilomita 9.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 9/10/2019 meneja masoko na biashara wa Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka amesema kampuni yake inaona fahari kutumia sehemu ya faida yake kudhamini matembezi hayo ya hisani kusaidia kuboresha maisha ya akina mama nchini.

Mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na asasi ya saratani Tanzania (TBCF) yanatarajia kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya elfu mbili mia tano na mgeni rasmi atakuwa John Ulanga, Mkurugenzi Mkazi wa chapa ya Afrika Mashariki.

’Siku hizi saratani ya matiti siyo tishio kwa wanawake peke yake bali hata kwa wanaume vile vile. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wanaume kujitokeza kupima ili kuona kama wana dalili za saratani ya matiti au la”, alisema Mbaraka.

Akizungumza katika mkutano huo, mratibu wa programu wa TBCF Kisa Mwakatobe amesema watatumia matembezi hayo ya hisani mbali na mazoezi ya mwili pia yatatoa elimu jamii kuhusu saratani ya matiti na haki zinazohusiana na matibabu na maisha kwa ujumla.Amesisitiza umuhimu wa kupima afya mara kwa mara kwani ugonjwa huo ukigundulika katika hatua za awali unaweza kutibiwa kirahisi.
Meneja Biashara na Masoko wa Cocacola Kwanza, Wahida Mbaraka, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu matembezi ya hisani ya Dasani Charity Walk kwa ajili ya kuchangia akina mama wanaosumbuliwa na Saratani ya Matiti yatakayofanyika Dar es Salaam Oktoba 14.Kulia ni Mratibi Miradi wa Asasi ya Saratani ya Matiti,Kisa Mwakatobe.

MAAFISA TAKUKURU WAIELEZA KORTI WALIVYOMKUTA MHADHIRI MSAIDI CHUO CHA NIT AKIJIANDAA KUFANYA NGONO NA MWANAFUNZI

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa, maafisa wa Takukuru walimkuta Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akijiandaa kufanya ngono na mwanafunzi wake.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Faraja Sambala ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati akimsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali ya mshitakiwa.

Akisoma maelezo hayo, Sambala amedai kuwa Mahimbo ni mkazi wa Makongo juu Dar es Salaam na wakati wa tukio alikuwa mwajiriwa wa NIT akifundisha somo la usimamizi wa Barabara na Usafirishaji na kwamba Victoria Faustine alikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Amedai Januari 11, mshtakiwa Mahimbo alimpigia simu mwanafunzi Huyo akimsisitiza wakutane siku iliyofuata ambapo walikutana baa iitwayo Shani iliyopo maeneo ya Mwenge.

Walipokutana , mshitakiwa alikuwa na mtihani wa marudio ambao Victoria alitakiwa kufanya, karatasi ya majibu na marking scheme ambapo alimsahihishia na kumpa alama 67 na baada ya kumaliza wakuhamia kwenye baa na nyumba ya kulala wageni inayoitwa Camp David , iliyopo Mlalakuwa Mwenge.

Amedai wakiwa pale walikunywa na kulewa kisha wakachukua chumba na kuingia ndani na kwamba mshitakiwa alianza kuvua nguo na kubaki na nguo ya ndani.

"Mshitakiwa alianza kumkumbatia Victoria na kuanza kumvua nguo zake na mara walisikia mlango ukigongwa na Victoria aliufungua na kuingia maofisa wa Takukuru, muhudumu wa baa na mjumbe. Walikuta nguo zipo juu ya meza," alidai.

Mshtakiwa alikamatwa na Januari 12, 2017 alienda kuandika maelezo Takukuru na Agosti 14, mwaka huu aliletwa mahakamani.Mshitakiwa alikana maelezo hayo na kukubali majina yake na mahali anapokaa.

Upande wa mashitaka ulidai kuwa wanamashahidi sita na vielelezo saba ili kuthibitisha mashitaka hayo huku mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi wanne.

Maimu alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa chuo hicho.Mhadhiri huyo anadaiwa akiwa mwajiriwa wa NIT alikuwa akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/16.

Anadaiwa alitenda kosa hilo Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 alitumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji uliokuwa unafanyika Januari 5 ,mwaka 2017.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na keshi itaanza kusikilizwa Novemba 11, mwaka huu.

RAIS WA ZANZIBAR DR.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA CCM WILAYA YA CHAKECHAKE PEMBA

0
0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Chakechake Pemba, katika ukumbi wa mkutano wa ZSTC kiwanda cha Makonyo Wawi, kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndg.Yussuf Ali Juma na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma MabodiMWENYEKITI wa Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chakechake Pemba.Ndg.Haji Hamad Kombo akizungumza kwa niaba wa Wazee wakati wa mkutano huo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha ZSTC Makonyo Wawi
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mzee Ali Omar Abdalla baada ya kumaliza mkutano wake na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Chakechake Pemba uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha ZSTC cha Makonyo Wawi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.Mhe. Hemed Suleiman Abdalla, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba leo kuaza ziara yake Kisiwani Pemba, kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.Mhe.Omar Othman Khamis,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi na Makamu Mwenyekiti wa UWT.Bi. Thuwaiba Editon Kisasi
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza na Wazee wa CCM Wilaya ya Chakechake Pemba, kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumza na Wazee hao katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi.(Picha na Ikulu)
WAZEE wa Wilaya ya Chakechake Pemba wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia katika ukumbi wa mkutano wa ZSTC Makonyo, wakati wa ziara yake Kisiwani Pemba na kuzungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya hiyo leo 9-10-2019

WAZIRI MKUU ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WATANZANIA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiaza Mwenge wa Uhuru,Nkwimba Madirisha Nyangogo wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiaza Mwenge wa Uhuru, Nkwimba Madirisha Nyangogo wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikimbiza Mwenge wa Uhuru wakati ulipopokelewa kijijini kwake Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 9, 2019. Kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakati mwenge huo ulipopokelea wilayani Ruangwa katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge huo wilayani Ruangwa yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Misngi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa na kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mzee Ali Mkongea.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakati aliposhiriki katika mapokezi ya Mwenge huo wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. Wa tatu kushoto ni Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea na wa nne kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea wakati alipozungumza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim, Mgandilwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea wakati mwenge huo ulipopokelewa wilayani Ruangwa katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu, Oktoba 9, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki. Katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ruangwa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Nangumbu wilayani humo, Oktoba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

*Ashiriki mbio za mwenge kijijini kwao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana na wazingatie ujumbe wa mbio za mwenge za mwaka huu unaohimiza umuhimu wa maji, uchaguzi wa Serikali za mitaa, vita dhidi ya rushwa, malaria, UKIMWI na dawa za kulevya.

Ametoa wito huo leo asubuhi (Jumatano, Oktoba 9, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri za Lindi na Ruangwa na wananchi wa kijiji cha Nangumbu kwenye uwanja wa shule ya msingi Nangumbu ambako mwenge huo ulipokelewa saa 1:44 asubuhi ukitokea Nyangao wilayani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, aliwasili wilayani Ruangwa jana jioni, ili kushiriki mbio za mwenge. Kesho (Alhamisi, Oktoba 10) mwenge huo utaelekea Nachingwea, ambapo Ijumaa (Oktoba 11) utaenda Liwale, Jumamosi (Oktoba 12) utaenda Kilwa na Jumapili (Oktoba 13) utakuwa Manispaa ya Lindi ambako utahitimisha mbio hizo na kuzimwa Oktoba 14, mwaka huu.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wajiandikishe kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Tanzania iweze kupata viongozi bora. “Tuitikie kaulimbiu ya mwaka huu kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hapa Ruangwa, hadi jana jioni watu 28,000 walikuwa tayari wamejiandikisha. Tukachague viongozi wachapakazi na waadilifu watakaoleta maendeleo kwa nchi yetu,” amesisitiza.

Mapema, akizungumza baada ya kupokea mwenge huo saa 2:21 asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Hashim Mgandilwa alisema utakimbizwa kwenye kata saba na vijiji 17 ambapo miradi mitatu mikubwa yenye thamani ya sh. bilioni 2.9 itazinduliwa.

Katika kijiji cha Nangumbu, mwenge ulizindua mradi wa mabweni na klabu ya kupiga vita rushwa kwenye shule ye sekondari ya Hawa Mchopa. Ukiwa njiani, mwenge huo ulipitishwa kijiji cha Nandagala ambako Waziri Mkuu alizaliwa. Pia aliupokea na kuukimbiza kidogo akiwa na wanakijiji wenzake, kisha mwenge huo ukaendelea kukimbizwa kuelekea kata ya Likunja ambako watazindua mradi wa maji wa Kitandi. Pia mwenge huo utazindua mradi wa barabara ya lami kwenye kata ya Nachingwea, iliyoko Ruangwa mjini.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mbio za mwenge wilayani Ruangwa, kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Bw. Mzee Ali Mkongea alimshukuru Waziri Mkuu kwa kujumuika na wananchi kushiriki ratiba ya mapokezi ya mwenge wilayani humo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano, ndani ya miaka mitatu (2015-2018) imekamilisha kwa wakati miradi 124 ya maji ambapo aliitaja baadhi yake kuwa ni miradi mikubwa ya Chalinze, Bagamoyo, Arusha, Tabora na Musoma. Pia alisema Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu na vifupi vya maji kwa gharama ya sh. bilioni 14.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeingia mkataba na Serikali ya India wa dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji kwenye miji 28 ya Tanzania. Lakini kuna changamoto nyingi kwenye miradi hii ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma na wakandarasi kujenga baadhi ya miradi chini ya kiwango.”

“Pia kumekuwa na shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji. Wananchi tusaidiane kuvilinda vyanzo hivi kwa sababu kazi ya kuvitunza si ya Serikali peke yake bali inaanza na mimi na wewe,” alisema.

Aliwasihi wananchi hao wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuchagua viongozi wazalendo ambao wana calibre ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa takwimu za ugonjwa wa malaria nchini, Bw. Mkongea alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 24, ukifuatiwa na Geita (asilimia 17), Mtwara (asilimia 15) na Lindi wenye asilimia 12.  

“Niwasihi wananchi tumieni vyandarua vinavyotolewa bure na Serikali hasa akinamama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kuna maeneo tumekuta baadhi ya watu wakivitumia kuvulia samaki na kufungia bustani ili kuku wasiingie. Haya si matumizi yake hata kidogo,” alisisitiza.


Meja Jenerali Kingu asisitiza ufanisi na uwajibikaji wa viongozi wizarani

0
0
Baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu
(hayuko pichani), wakuu wa taasisi, idara na vyombo vya ulinzi
na usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo wakichangia mada
kwenye kikao hicho kilichofanyika Mjini Dodoma jana.

*****************************************

Na Mwandishi Wetu, MOHA

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Jacob Kingu, ametoa wito kwa wakuu wa idara kwenye
taasisi, vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Wizara
hiyo, kutelekeza wajibu walionao ili kuongeza uwajibikaji.

Meja Jenerali Kingu aliyasema hayo Mjini Dodoma jana
alipofanya kikao cha pamoja na wakuu wa idara hizo.

Idara hizo ni Utawala, Wakimbizi, Jeshi la Polisi, Uhamiaji,
Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi.

Kikao hicho kilijadili mchakato wa ajira kwa watumishi wa
idara zilizopo chini ya Wizara hiyo, upandishaji vyeo, taratibu
za uteuzi na nidhamu katika vyombo vya ulinzi na usalama.

“Naipongeza Wizara kwa kuandaa mkutano huu ili kujadili
changamoto, mafanikio, idara ya utawala na rasilimali watu ina
jukumu kubwa zikishughulika na watu, watumishi.

“Pia idara hizi ndio kiungo katika uratibu, uwezeshaji kwenye
taasisi na vyombo vilivyopo chini ya Wizara ili kuleta mafanikio
zaidi kama watatekeleza wajibu wao ipasavyo,” alifafanua.

Meja Jenerali Kingu alisema idara hizo zina jukumu kubwa la
kuzishauri mamlaka ndani ya taasisi, vyombo husika kwani
kukiwa na tatizo ina maana kuna mahali hakuko sawa.
Alisisitiza suala la kutolewa mafunzo ya kitaaluma kwa
watumishi wote ambayo tatazingatia usawa.

“Suala la kuajiri watu kwa upendeleo lisipewe nafasi, tuajiri
watumishi wenye sifa kwa manufaa ya taasisi,” alisisitiza.

Alizungumzia suala la wastaafu kucheleweshewa malipo yao
akitaka wapunguziwe adha wanayoipata na kutaka yafanyike
maandalizi mapema ili kuondoa kero, kasoro zilizopo na
malalamiko ambayo si ya lazima.

Alisisitiza umuhimu wa kila mkuu wa idara kufuata sheria,
taratibu za utumishi wa umma hasa pale ambapo watumishi
wanapofanya makosa ili yasiweze kujirudia.

Akizungumzia majukumu ya viongozi hao, Meja Jenerali Kingu
aliwataka wasisubiri kukumbushwa wajibu wao, kila kiongozi
ayatambue majukumu aliyonayo na kuyatekeleza kwa ufanisi
yakiwemo ya wastaafu, nidhamu, uhamisho kwa watumishi.

Aliwataka wakuu wa idara kushirikiana na watumishi ili kuwe
na mpangilio mzuri wa kazi, kuongeza ufanisi na uwajibikaji.

“Naamini idara zote zilizopo chini ya Wizara hii zina watendaji
wazuri wanaojua wajibu wao na wachapakazi hivyo tuwatumie,
kuwepo na mpango mkakati wa kuondoa kero mbalimbali.

“Kero hizo ni pamoja na suala la kama mishahara, stahiki za
watumishi na upadishaji vyeo…utakuta mtumishi kapanda cheo
muda mrefu lakini anapata mshahara wa zamani usiolingana na
nafasi mpya aliyonayo, kuwepo mabadiliko,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimali Watu, Emanuel Kayuni, alimshukuru Meja Jenerali
Kingu kwa maagizo aliyotoa na kuahidi yatafanyiwa kazi.

KAMISHNA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI AKIWA NA KAMATI NDOGO YA VYOMBO ULINZI NA USALAMA WAKIKAGUA VIPENYO RASMI NA VISIVYORASMI VINAVYOTUMIWA NA WAHALIFU KUTOKA NCHI JIRANI YA MSUMBIJI

0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP
Liberatus Sabas akiwa na Kamati Ndogo Ya Vyombo Ulinzi Na
Usalama wakiteta jambo baada ya kumaliza kukagua moja ya
kipenyo cha Mtipesa ambacho kilichopo mkoani Mtwara mpakani
mwa Tanzania na Msumbiji. (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna Wa Operesheni Na Mafunzo Ya Jeshi La Polisi Cp
Liberatus Sabas Akizungumza Na Madereva Bodaboda waliopo
Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji eneo la Mtipesa juu ya
kukabilina na Wahalifu Watakaoingia au kutoka nchini msumbiji
ila amewaasa Madereva hao kuwa na tabia ya kutoa Taarifa
Katika Vituo Vya Polisi Vilivyo karibu yao hasa pale wanapoona
Mtu na Kumtilia shaka.(PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP
Liberatus Sabas, akiwa katika moja ya mitumbwi eneo la
Kihanga Mkoani Mtwara inayotumiwa na raia kuvusha
watanzania wanaoelekea nchini Msumbiji katika shughuli za
kujipatia kipato ila wengi wanaotumia usafiri huo ni wakulima
(PICHA NA JESHI LA POLISI)

IGELEKE FC BINGWA WA SAUTI YA SIMBA SUPER CUP 2019

0
0
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academ ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akiongea baada ya kupatikana kwa mshindi wa kombe hilo
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academ ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akionyesha jezi ambazo alizigawa kwa mshindi wa kwanza na wapili wa mashindano hayo 
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academ ambaye alikuwa ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 akitoa mpira kwa mshindi wa tatu wa mashindano hayo 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MASHINDANO ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 kata ya Mkimbizi yamefikia tamati siku ya jana baada ya kuchezwa fainali kati ya Mkimbizi FC na Igeleke FC katika viwanja vya shule ya msingi Mkimbizi na Igeleke FC kuibuka mshindi.

Mashindano haya ya mpira wa miguu yaliyokua yanahusisha zaidi ya timu nane ambazo ni Mkimbizi fc, Masoko fc,Mtwivila fc,Romanithelc Rc,Rutherana kkkt,Igereke fc,Bima fc na Vetaran fc za kata ya Mkimbizi yalikuwa yanadhamini na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Edward Chengula kwa kuwa amekuwa mdau mkubwa kwenye sekta ya michezo manispaa ya Iringa

Na ikumbukwe kuwa hivi karibuni diwani Nguvu Chengula alidhamini mashindano makubwa yaliyofanyika kata ya Kihesa yaliyokwenda kwa jina la Bidii Cup mashindano hayo yalikuwa yana msisimko na mvuto wa hali ya juu sana na vijana walionesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu kiasi kwamba wadau na viongozi wanaohusika na michezo katika mkoa wa Iringa walikunwa na uwezo uliooneshwa na vijana. 

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi mshindi wa kombe hilo Chengula alisema kuwa mpira wa miguu kwa sasa umekuwa unatoa ajira na kuwaajiri watu wengi hivyo vijana wanatakiwa kuonyesha vipaji vyao.

“Saizi mnatakiwa kuonyesha vipaji vyenu kweli kweli kwa kuwa kwa sasa mpira wa miguu umekuwa ajira ambayo wachezaji wamekuwa wanalipwa mamilioni ya fedha tofauti na miaka ya nyuma ilivyokuwa” alisema Chengula

Chengula alisema kuwa amekabidhi jezi seti moja na mpira mmoja kwa mshindi wa kwanza,mshindi wa pili alijinyakulia jezi seti moja huku mshindi wa tatu alijinyakulia mpira mmoja.

Aidha Chengula aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari za mpiga kura kwa kuwa kila mkazi wa wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.

“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema Chengula

Lakini Chengula aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.

Vilevile Chengula ndiye alikuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kusaka vipaji vya vijana wanaoweza kuimba na kucheza (dancers) mashindano hayo yalikwenda kwa jina la Mwangata House of Talent na yalikuwa na msisimko mkubwa kwa kuwa vijana waliimba na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha tasilimu laki sita,vijana wote walioonesha uwezo mkubwa katika mashindano hayo chama cha mapinduzi (CCM) Iringa waliahidi kuviendeleza vipaji hivyo.
 
Katika maswala ya soka mkurugenzi wa shule za Sun Academy amekua mstari wa mbele kabisa kuhakikisha vijana wanapata burudani, wanajenga afya zao na wanapata nafasi ya kujitengenezea ajira kupitia vipaji vyao vya kusakata soka, mpaka sasa emesaidia pia mashindano ya mpira pale kata ya Mlandege na kuwasaidia vijana kwa kuwapa vitendea kazi ikiwemo mipira na jezi katika mashindano yale.

Vijana hawahitaji mambo mengi,vijana wanahitaji kupata kile wanachokipenda. Suala la michezo kwa vijana ni suala mtambuka na linalopendwa na kila kijana. Vijana wana vipaji na uwezo mkubwa sana hasa wanapopewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao. Hivyo kama kiongozi anayejali ni lazima aliangalie kundi hili kwa umakini mkubwa. 

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya “Njoo Kesho” pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Hata RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU RAIA WAWILI WA CHINA BAADA YA KULIPA FIDIA YA SH MILIONI 70

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia wawili wa China, Li Ling na Chen Guo,  kulipa fidia ya Sh milioni 70  baada ya kukiri makosa ya kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali na  wameamriwa kuondoka nchini mara moja kwa kuwa sio raia wa Tanzania.

Pia mahakama hiyo imetaifisha gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 982 CDH  na mashine mbili za washitakiwa hao na kuwa mali ya serikali.

Akisoma adhabu hiyo Leo Oktoba 9,2019  Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alisema kuwa mshitakiwa Ling atatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 45 na mshitakiwa Guo atalipa Sh milioni 25 na faini ya Sh milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuishi nchini bila kibali.

Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka  kuwafutia washitakiwa hao  mashitaka ya utakatishaji fedha na kuwasomea mashitaka mawili  ya kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali. 

Hata hivyo, washitakiwa wengine wanne waliokuwa katika kesi hiyo  wamegoma kukiri mashitaka yao yanayowakabili hivyo wamerudishwa rumande. 

Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali, Salim Msemo  amedai hawana kumbukumbu  ya makosa ya nyuma ya washtakiwa hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe  fundisho kwao na  wengine.

Wakili Msemo amedai kuwa wameingia makubaliano na washitakiwa  hao baada ya kukiri kosa la kujihusisha na nyara za  serikali na kuishi nchini bila kibali, hivyo wameamua kuondoa kesi ya  uhujumu uchumi.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Shaidi  amewaapisha washitakiwa na kuwauliza  kama walisaini kwa hiari yao na kudai walifanya hivyo kwa hiari yao.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Misemo  amedai Julai 5,2015 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mshitakiwa Ling alisafirisha nje ya nchi kucha 25 za simba zenye thamani ya Sh 22, 500,000 bila kuwa na kibali. 

Amedai katika kosa lingine Julai 5, 2015 katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mshtakiwa Cheng Guo alisafirisha nje ya nchi meno 21 ya simba yenye thamani ya Sh 12, 500,000 bila ya kuwa na kibali. 

Msemo  amedai Januari 18, 2015 mshitakiwa Guo alikutwa akiwepo nchini kinyume na sheria. 
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live




Latest Images