Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUMIA KONGAMANO LA KUMKUMBUKA MWALIMU NYERERE KUZUNGUMZIA UHURU WA MAWAZO,VIONGOZI KUJISHUSHA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuna kila sababu ya Watanzania kuendeleza misingi imara iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere huku akisisitiza umuhimu wa watu kuwa huru kutoa mawazo yao badala ya kuyazuia.

Pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake licha ya kuwa Rais wa nchini bado hakujali nafasi yake kwani aliamini katika utu na hivyo alikuwa anafikika kwa urahisi na akipenda kujikweza kwa cheo chake kwa kujiona yeye ni Bora au yuko juu zaidi ya Watanzania, siku zote alijishusha na kujiweka kundi la watu wa kawaida sana.

Kikwete ameyasema hayo leo Oktoba 8,mwaka 2019 wakati anafungua Kongamano lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wastaafu na waliopo katika utumishi wamehudhuria .

Wakati Kukwete anazungumza katika kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusisha mchango wa Mwalimu Nyerere katika kujenga misingi imara ya Taifa letu ambapo amewataka Waatanzania kuendelea kuienzi na kusimamia kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

"Mwalimu Nyerere aliamini kwenye utu,hivyo cheo chake cha Rais hakikusababisha ajione yeye ni Bora zaidi ha wengine,alijishusha na kila mtu alimfikia.Unapokaa na Mwalimu Mwalimu Nyerere unakuwa huna hofu .Ukiwa na cheo bado hakukuondolei ubinadamu wako, "amesema Rais mstaafu Kikwete.

Akizungumzia zaidi Mwalimu Nyerere, Rais huyo mstaafu amesema kuwa Mwalimu hakuwa na kinyongo na mtu eti kwasababu ametoa mawazo tofauti ya na kwake kwani eliminj katika Uhuru wa mawazo na mawazo hayapigwi rungu bali yanajibiwa kwa mawazo bora zaidi na hatimaye mambo yanakwenda vizuri.

"Hata CCM ni Chama nyenye maarifa mengi sana na kinachotumia akili lakini msingi wake mkubwa Mwalimu aliruhusu Uhuru wa mawazo.Niwakumbushe mwaka 1992 uamuzi wa busara kafanyika kwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi,iliundwa tume wakati huo kukufanya maoni ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Fancis Nyarari.

"Wakati ule upepo wa vyama vingi ulikuwa unakuja.Ukafanyika utafiti kupitia tume hiyo ambapo asilimia 80 walitaka mfumo wa Chama kimoja na asilimia 20 Chama kimoja. Mimi nilikuwa wa Kamati Kuu,si haba nimekaa ...mjadala ulikuwa mkubwa na mkali, hata hivyo ikaamriwa asilimia 20 wameshinda na ilikuwa uamuzi wa kimkakati.

"Chama hiki kina maarifa mengi, na msingi mkubwa CCM wana uhuru wa mawazo.Kupoteza uhuru wa mawazo ndani ya Chama ni kwenda kukiharibu.Mwalimu alikuwa na akili sana ,yeye peke yake ni sawa na wajumbe 500.Alikuwa na uwezo wa kuchambua na anawasikiliza na kisha anakuja na samari yake ambayo inamaliza hoja zote ambazo hazikuwa na maana"amesema Kikwete.

Amesisitiza Mwalimu hakuna na kinyongo na mtu mwenye mawazo tofauti na yeye,alikuwa na moyo mzuri sana."Niwakumbushe wakati wa uhujumu uchumi tulikutana Karimjee na ajenda ikawa ajenda ya uhujumu uchumi.Kuna mjumbe mmoja alimwambia Mwalimu hawezi kuchukua zilizo ili akamwachia Sokoine kupambana na wahujumu uchumi , lakini Mwalimu alicheka tu.

'Wazee walitaka kumjua aliyeshauri vibaya...lakini aliwajibu washauri wake wa nini,kwani ni washauri wake,hivyo washughulike na yeye."Mwalimu anatufundisha kama  ulishauriwa ukakubali lawama zibaki za kwako na sio kumlaumu aliyekushauri.

Kikwete amesema kongamano ambalo limeandaliwa na Chuo hiko ni muhimu na la kupongeza kwani kinatoa fursa ya kukumbuka yale yaliyofanywa na Mwalimu na kuongeza Mwalimu kukumbukwa ni jambo ambalo anastahili, wala sio hisani na kwanini amefanya mambo mengi kwa Tanzania na Afrika na hata kwa duniani na utaamua kuyaorodhesha utakesha.

Ametaja baadhi ya mambo ambayo Mwalimu ameyafanya kwa ajili ya nchi ni kwamba Mwalimu ndio mkombozi wetu kwani ametukomboa kwa kututoa katika ukoloni.Mwalimu aliamua kuanzisha safari ya kuondoa ukoloni na ndipo Tanu ikaanza na Mwalimu akawa Rais, na baada ya uamuzi huo Serikali ya Mkoloni ikamtaka kuchagua abaki Tanu awe au Mwalim lakini yeye akaamua kubaki kuwa Mwalim.

"Ni uamuzi mgumu lakini kwa moyo wake wa upendo aliamua kujitoa yeye kwa ajili ya wengine. Hilo ni jambo kubwa sana kwa kuonesha moyo wa kujitolea, wangapi leo wanaweza kujitolea maana hata mshahara ukiwa mdogo watu wanaandamana.

"Mwalim Nyerere alikuwa na karama ya maneno na tumepata Uhuru kwa maneno, usione vyaelea ujue vimeundwa, umahiri wake ndio umetufikisha hapo. Kwa wenzetu imeshindikana hadi wanatumia nguvu. Tatu Mwalimu aliamini kwenye umoja na ndio maana kwa kushirikiana na swahiba wake mzee Karume walianzisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuweo kwenye ramani ya dunia lakini hao wazee wameweza kuanzisha nchi yetu na mafanikio yake sote tunayaona.

Jambo la nne Mwalimu amesaidia kujenga taifa lenye umoja , amani na mshikamano, nchi yetu hii ina kabila zaidi ya 120 lakini wote tumebaki kuwa wamoja.Kulikuwa wamoja.Kulikuwa watu wenye dini na wasio na dini lakini tukabaki na umoja wetu,"amesema Kikwete na kuongeza tukianza kubaguana kwa dini au kabila hatutabaki salama.

Wakati jambo la tano la kukumbuka,Kikwete amesema Mwalimu alikuwa mtu wa kawaida mbele ya watu wengine.Ukikaa na Mwalimu hupati hofu ya kuwa naye kwani alikuwa ni Rais aliyejishusha na alikuwa wa kawaida.Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa Rais haina maana wewe ni zaidi ya watu wengine.

"Ni jambo nzuri kutambua kujishusha na unapojishusha hakuondoi nafasi yako, ukiwa binadamu hakuondoi nafasi yako.Jambo la sita aliamini Uhuru wa Tanganyika hauna maana kama nchi nyingine za Afrika hazitakuwa zimejikomboa kutoka mikono ya wakoloni Mwalimu alifanya kila linalowezekana kukomboa nchi nyingine za Afrika,"amesema Kikwete kwenye kongamano hilo.

Alizungumzia pia Mwalimu Nyerere alivyokuwa anawapenda vijana na akakumbusha hata yeye(Kikwete) mwaka 1968 akiwa kidato cha tatu alikuwa kiongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Kibaha na kwamba mwaka1982 akapata nafasi ya kuingia Halmashauri Kuu ya CCM.UVCCM ndio sehemu ya kujifunza fursa ya uongozi.Nimeingia Halmashauri Kuu ya Chama mwaka huo na hapo ukawa mwanzo na mwisho wa siku nikawa Rais.

'Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa Mwalimu, niwapongeze Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuandaa kongamano hili.Baadhi ya mambo wamekuwa tunu ya taifa na lazima. hizo tunu tuzilinde.Kwa Tanzania hii sote ni wamoja pamoja na kuwa na makundi mbalimbali ya watu.

"Watanzania wenzangu, wanachama wenzangu tushikamane katika kusimamia tunu ya amani.Amani haina Chama ,dhehebu wala kabila.Umoja hauna chama,kabila wala dini.
Makongamano hayo ni muhimu kwani kukumbusha mambo ya msingi ya taifa letu,"amesema Kikwete.
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza wakati akizindua Kongamano la Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere limefanyika leo katika Chuo hicho na kuhudhuria na  watu wa kada mbalimbali
 Mgeni rasmi kwenye Kongamano la kuadhimisha miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa amesimama Meza kuu akiwa na viongozi wengine baada ya kumalizia kwa wimbo wa Taifa
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano la Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere wakiwa ukumbini kabla ya kuanza kwa kongamano hilo ambalo limefanyika leo katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akisaliamiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria Kongamano la kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 20 ya kifo ch Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.Kongamano hill ambalo  limeandaliwa  na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere limefanyika leo Oktoba  8,2019

ZAIDI YA WAKAZI MIL.1.9 ARUSHA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha akipata maelezo namna ga kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ambapo yeye ni mkazi wa eneo hilo leo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipata maelekezo namna ya kujianikisha kwenye daftari la wapiga kura katika kata ya Murieti ambapo akiwa ni mkazi wa eneo hilo.


Na Vero Ignatus,Arusha.

Zaidi ya wakazi milioni 1.9 mkoa wa Arusha wanatarajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa ili kuweza kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika Nyanja zote.

Richard Kwitega ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa wananchi hao watapiga kura watakuwa na sifa ya umri wa miaka 18 na kuendelea huku wakiwa na sifa za kuwa wakazi wa eneo husika wanakojiandikishia na kupiga kura .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefika na kujiandikisha katika daftari la kupiga kura, katika kata ya Muriet ambako ni mwenyeji wa eneo hilo, amesema kuwa serikali imeweka mazingira rafiki kwa watu wote kujiandikisha bila kujali itikadi za vyama vyao wote wanapaswa kushiriki katika zoezi hilo la kujiandikisha.

Msena Bina ni msimamizi wa Uchaguzi jiji la Arusha amesema kuwa vituo vimefunguliwa 154 kwa ajili ya wananchi kujiandikisha hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amesema kuwa jeshi hilo litaimarisha hali ya ulinzi na usalama, na kufanya kazi bila kupendelea chama chochote, kama walivyotoa maelekezo kwa Askari kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo.

JAJIMKUU: UTOAJI HABARI NI WAJIBU SI FADHILA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari (hayupo pichani) pindi ujumbe kutoka Taasisi hiyo ulipomtembelea Ofisini kwake, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
 Maafisa kutoka MISATAN-Tanzania, (kushoto), Mwenyekiti, Bi. Salome Kitomari na Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro kwa pamoja wakinukuu masuala yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Jaji Mkuu.
 Mwenyekiti wa MISATAN-Tanzania, Bi. Salome Kitomari akizungumza jambo na Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani).

Mhe. Jaji Mkuu akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Adrian Kilimi, kulia ni Maafisa kutoka MISATAN na Mahakama.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka MISATAN-Tanzania na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari, wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro na wa kwanza kulia ni Salum Tawan, Mkutubi-Mahakama ya Tanzania.


(Picha na Mary Gwera, Mahakama)



Na Mary Gwera, Mahakama


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.  Ibrahim Hamis Juma ameishauri Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISATAN) pamoja na vyombo vya habari nchini kuitekeleza ipasavyo Sheria  namba 6 ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016.


Akizungumza na Mwenyekiti wa MISATAN Tawi la Tanzania, Bi. Salome Kitomari, mapema Oktoba 08, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mhe. Jaji Mkuu alisema Sheria hii itumike ipasavyo kudai taarifa.


“Tumieni sheria hii kudai taarifa, sheria inatoa shurti ya kutoa taarifa zinazotakiwa na umma, hivyo suala la kutoa taarifa sio fadhila ni amri kwa hivyo ni vyema kuangalia ni kwa namna gani tunatumia Sheria hii kushurutisha utoaji wa taarifa,” alibainisha Mhe. Jaji Prof. Juma.

Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa ili kutekeleza sheria hii ipasavyo ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza takwa la kikatiba na kisheria.


Kwa upande mwingine, Mhe. Jaji Mkuu alizungumzia pia suala la Vyombo vya habari nchini kuandika Habari za uchunguzi ‘Investigative Journalism’badala ya kutegemea habari zitokanazo matukio mbalimbali.

“Ni muhimu pia kufanya habari za uchunguzi kwa kuchagua mada maalum ‘agenda setting’ itakayokuongoza kufanya utafiti, kwa kufanya hivi itasaidia kupunguza malalamiko na vilevile itasaidia kuwa na habari zenye usahihi zaidi ‘accurate’, alieleza Mhe. Jaji Mkuu.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISATAN-Tanzania, Bi. Salome Kitomari alimueleza Mhe. Jaji Mkuu kuwa Taasisi yake imekuwa na uhusiano mzuri na Mahakama katika maeneo mbalimbali.“MISATAN kwa kushirikiana na Mahakama tumefanikiwa kutoa mafunzo ya Huduma kwa Mteja ‘Customer Care’ kwa zaidi ya Watumishi 350 wa Mahakama,” alieleza Bi. Kitomari.
Hata hivyo; Mwenyekiti huyo alishauri mafunzo haya ni vizuri kutolewa pia kwa Watumishi wa Mahakama wa ngazi za juu wakiwemo Majaji na Mahakimu.


Aidha; Bi. Salome aliongeza kwa kupendekeza kufanyika kwa Mkutano kati ya Mahakama, MISATAN na Taasisi nyingine za Habari lengo likiwa ni kujenga imani na uwajibikaji kwa taasisi zote.Ujumbe huo wa MISATAN umemtembelea Mhe. Jaji Mkuu kwa lengo la kuitambulisha rasmi Taasisi hiyo, kuishukuru Mahakama kwa kufanya kazi kwa karibu na MISA Tanzania ikiwa ni pamoja na kujadili maeneo ya uhusiano baina ya Taasisi hizi kwa miaka ijayo.

 


VIKWAZO 174 VYA BIASHARA EAC VIMEONDOLEWA KWA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara,
Bi.Sekela Mwaisela akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kikao cha
Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya
biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia hotuba yaMkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.SekelaMwaisela, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara naKamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyikaJijini Dar es Salaam.

*****************************

Jumla ya vikwazo 174 sawa na asilimia 75 vimeondolewa ili kurahisisha ufanyajibiashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo sasaitawezesha kuwepo kwa biashara kubwa baina ya nchi hizo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Mkutano kati ya
Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.Sekela Mwaiselaalisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kanda zingine kuna sheriaambazo zinazingitia biashara.

“Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ibara ya 13(1) Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Biashara pamoja na Ibara ya 6 ya Itifaki ya Biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika (SADC) zinazitaka NchiWanachama kuondoa vikwazo vya zamani ili kuwezesha biashara kwawafanyabiashara”, Alisema Mwaisela.

Mwaisela alieleza kuwepo kwa juhudi za kuondoa kabisa vikwazo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikishirikisha kuwepo kwa vikao vya kamati za biashara, Mikutano ya Kikanda, Mikutano ya Mawaziri pamoja na Mikutano ya Nchi kwa Nchi hiyo itatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoa changamoto zao kwa utatuzi zaidi.

Katika kuteleza hilo Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wadau leo imefungua Mkutano wa wadau wa biashara ambapo agenda kubwa ni kuelimisha wafanyabiashara kuhusu kutoa taarifa iwapo watakutana na vikwazo mbalimbali wakiwa kwenye kusafirisha bidhaa zao.

“Kusudi kubwa la Mkutano huu leo ni kujadiliana kuhusu kutoa vikwazo lakini pia kuwawezesha wafanyabiashara kuwa na elimu kuhusu hivyo vikwazowanavyokutana navyo, sehemu gani ya kutoa taarifa kwa Msaada Zaidi”, alisema Mwaisela.

Alisema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kujenga miundombinu wezeshi ikiwemo Bandari, Reli, ambavyo vinaambana na ujenzi wa miradi mikubwa kama ule wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme Julias Nyerere Hydro Power Poject (JN HPP) ambao utazalisha Megawati 2,115.

Kwa upande wa wadau wa biashara wao wamesema kuwa Serikali imewezeshakuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara katika Jumuiya ya Nchi wanachama ukiachilia mbali kuwepo kwa vikwazo vidogovidogo ambavyo vinatatulika.

“Mkutano huu unaonesha nia njema ya Serikali kuweza kuwasiliana kwa karibu na wafanyabiashara ili kuweza kujua changamoto zao na mazingira ya biashara wanayokutana nayo sokoni, tumefurahi kwamba Serikali imejitahidi kupunguza changamoto za biashara” David Minja, Unilever.

RAIS MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI NKASI,RUKWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora mara baada ya kuhutubia wanachi wa Namanyere Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Namanyere Nkasi mkoani Rukwa mara baada ya kuwasili akitokea Sumbawanga.


Utabiri wa Hali ya Hewa wa Siku Tano na Athari Zinazoweza Kutokea

Wafugaji kutumia simu kuyafuata malisho na maji

$
0
0


Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet,akizungumzia juu ya mradi huo ambao wafugaji watatumia simu za mkononi kufahamu maeneo ya malisho na maji.



Na.Vero Ignatus,Monduli

Simu za mkononi zitatumika kutuma jumbe kuulizia eneo lenye maji,malisho katika wilaya tatu za mkoa wa Arusha 

Mradi huu umezinduliwa na shirika la kimataifa la PCI ,l, katika kijiji cha Arkaria wilayani Monduli na utatekelezwa pia wilaya za Longido na Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema, wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa application ya Afriscout watatuma bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.“Tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisema Jennifer

Dkt.Asimwe Rwiguza ni Kaimu mkurugenzi endeshaji wa malisho na vyakula vya mifugo,katika uzinduzi huo alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

Mfugaji John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na wakulima.John Rutabingwa ni Mkurugenzi halmashauri ya Monduli, alisema halmashauri hiyo itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

Mradi huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.

MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAAMUA KUTEKETEZA DAWA ZA KULEVYA ZA HEROINE NA COCAINE JIJINI DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini(DCEA) imetekeleza dawa za kulevya kilo 120.91 za Heroine na kilo 70.96 za Cocaine zinazohusisha kesi 35.

Aidha uzito wa  dawa hizo unajumuisha kilo 63.155 za Heroine ambazo kesi yake imehukumiwa mkoani Mtwara ikimhusisha Mwinyi Rajab na Ally Hamad na kushindwa kutekelezwa mkoani humo.

Utekelezaji wa dawa hizo umefanyika leo Oktoba 8,2019 katika kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam ambapo Mamlaka imefanya uteketezaji huo wa dawa za kulevya kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa ,Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Mazingira.

Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo wakati wa kuteketezwa dawa hizo imeeleza kuwa dawa hizo zimehusiana na kesi zilizomalizika katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mkoani Dar es Salaam na kwamba jumla ya dawa za kulevya zilzoteketezwa ni kilo 120.91 au gramu 120.919.88 za heroine na kilo 70.96 (gramu 70.967.86) za Cocaine ambazo zinahusisha kesi 35.

"Hii ni mara ya kwanza uteketezaji dawa za kulevya kufanyika tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2919 kwa Mkoa wa Dar es Salaam  ambapo mara ya mwisho uteketezaji kama huu ulifanyika mwaka 2015 katika kiwanda cha  Wazo Hill ukihusisha dawa za kulevya za aina mbalimbali.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili dawa za kulevya ziteketezwe lazima kuwepo  a  amri ya Mahakama iliyosikiliza kesi na kumalizia au ambapo kesi hiyo ipo.

"Pia uteketezaji wa dawa za kulevya hufanyika kwa utaratibu maalum ili kuepuka uharibifu wa mazingira na madhara ya kiafya kwa wananchi,hivyo viwanda vya saruji kutumika,"imesema Mamlaka hiyo kupitia Kitengo chake cha Habari na Mawasiliano.

Hata hivyo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya umetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za wazalishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya ili sheria ichukue mkondo wake.

KITABU CHA MABADILIKO YA TABIA NCHI CHAZINDULIWA, SIMBACHAWENE AWAASA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi umezinduliwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene na kuwaasa wananchi kutunza mazingira, kuacha kukata miti ovyo na kutunza vyanzo vya maji ili nchi isije kuingia kwenye uharibu wa mazingira.

Mkutano huo umeqhudhuriwa na wataalamu mbalimbali wa mazingira na kufanyika  kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ukiandaliwa na Chuo Kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha Mwalimu Nyerere upande wa Mazingira.

Waziri Simbachawene ameweza kuzindua kitabu kinachojulikana kama Climate Change and Coastal Resources in Tanzania kilichoandikwa kwa ushirikiano na wataalamu kutoka Tanzania, Norway, Marekani na zingine.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Simbachawene amesema mabadiliko ya tabia nchi ni ajenda ya dunia ambapo shughuli za kibinadamu zinasababisha ongezeko la hewa ukaa.

"Hewa ukaa imekuwa inaleta joto na majira yanabadilika na hii inatokana na shughuli za kibinadamu, kiujumla mfumo mzima unabadilika,"

Simbachawene amesema, serikali haina budi kuanza na mfumo mpya wa kutoa elimu ili kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Ameseka, hili ni kongamano la siku mbili litakalotoa mawazo na mtazamo mpya utakaosaidia kupambana na mabadiliko hayo ambapo madhara yatakapozidi kuwa makubwa duniani ongezeko la joto kuongezeka na kufikia 2 bara la Afrika litaingia gharama ya takribani dola Bilioni 530 ili kukabiliana na hali hiyo.

"Wananchi wanatakiwa kutunza mazingira, kuacha kukata miti ovyo, utunzaji wa vyanzo vya maji na hata kutumia nishati mbadala ili mazingira ya kiasili yaendelee kuwapo na kuendelea kufaidika,"

"Utoaji wa elimu ni muhimu kwa wananchi na ukiangalia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 imeweka wazi kila mmoja anahusika kwenye utunzaji wa mazingira na kuyalinda na ili yaweze kuleta tija ya kukuza uchumi kwa kutumia sekta ya viwanda," amesema Simbachawene.

Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira Profesa Pius Yanda amesema kitabu kilichozinduliwa kimeweza kufanyiwa tafiti mbalimbali kwenye ukanda wa bahari na kuandikwa na wataalamu kutoka nchi za Tanzania, Norway na Marekani.

Yanda amesema, kitabu hicho kimeweza kuzungumzia utawala bora utasaidia katika kupunguza athari za tabia nchi na pia kuna makala mbalimbali zilizoandikwa zikizungumzia utafiti wa baharini mabadiliko ya tabia nchi yanavyoweza kuongeza joto na kusababisha upatikanaji mdogo wa samaki.

Kongamano hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili na litakuwa na mada mbalimbali zinazozungumzia mabadiliko ya tabia nchi na maelezo yakitolewa na wataalamu wa ndani na nje ya nchi.

Serikali ya Tanzania imeushukuru ubalozi wa Norway kwa kuweza kuwa wadau wakubwa wa mazingira na wamekuwa na mchango mkubwa kwa serikali ya Tanzania kupitia mazingira.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  George Simbachawene akizindua kitabu kinachozungumzia mabadiliko ya tabia nchi kilichoandikwa na wataalamu kutoka Tanzania, Norway na Marekani, mkutano huo wa kimataifa umeandaliwa na Chuo kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira. Akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Ole Nasha, Makamu Mkuu wa Chuo Prof William Anangisye na Balozi wa Norway Nchini Tanzania.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  George Simbachawene( kushoto) akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira Prof Pius Yanda baada ya kuzindua kitabu kinachozungumzia mabadiliko ya tabia nchi kilichoandikwa na wataalamu kutoka Tanzania, Norway na Marekani, mkutano huo wa kimataifa umeandaliwa na Chuo kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira.
Mwenyekiti wa Kigoda ch Mwalimu Nyerere Mazingira Prof Pius Yanda akizungumzia kitabu kilichozinduliwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene kinachoelezea mabadiliko ya tabia nchini. Mkutano huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

PSPTB YAWAWEKA KIKAANGONI WAKUU WA VITENGO VYA MANUNUZI TAASISI 20 ZA SERIKALI

$
0
0
Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)  imewataka wakuu wa vitengo vya ununuzi na ugavi katika taasisi 20 nchini zikiwepo BoT, TBS, TCAA na NIMR kukaa pembeni kupisha uchunguzi.
Maamuzi hayo yametolewa leo PSPTB baada ya kupokea  ripoti ya PPRA na kuonesha taasisi hizo kukosa weledi katika manunuzi ya umma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema, taasisi kumuajiri mtu asiyesajikiwa na bodi hiyo ni kosa  la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka miwili jela au faini ya milioni mbili au vyote kwa pamoja.

Mbanyi amesema toka mwaka 2016 hadi 2019 walifanya ukaguzi kwenye mikoa tisa na katika taasisi 146 na kubaini jumla ya watumishi 268 hawajasajiliwa kwenye bodi ya ununuzi na ugavi na mpaka kufikia Septemba 2019 wataalamu 146 wamesajiliwa na 89 wakiwa bado huku 33 hawapo kazini kwa sababu mbalimbali.

Amesema, bodi kwa kutumia mamlaka iliyonayo chini ya kifungu cha 33 cha kanuni za maadili na mienendo ya wataalamu inafanya uchunguzi wa kina kwa wakuu wa vitengo vya ununuzi toka taasisi hizo na kuwapeleka mbele ya kamati ya maadili ya bodi.

Mbanyi amesema, kwa sasa inawaagiza wakuu wa taasisi hizo kuwatoa kuongoza vitengo vya idara za ununuzi mpaka shauri lao litakapokamilika na watajulishwa.

"PSPTB inawaagiza waajiri wote kwenye sekta ya umma na binafsi kuhakikisha watu wote wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi wamesajiliwa na wana sifa stahiki kwa mujibu wa sheria,"amesema Mbanyi. 

Taasisi hizo ni pamoja na wizara ya maji na umwagiliaji, Wakala wa umeme Vijijini (REA), Mamlaka ya Anga, Veta Makao Makuu, Mamlaka ya Bandari, Manispaa ya Ubungo, Manispaa ya Kahama, TANAPA, Wakala wa mbegu za Kilimo (ASA), Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira Singida, Wilaya ya Kaliua, Wilaya ya Nkasi, Wilaya ya Masasi, Shirika la Reli Nchini (TRC), Manispaa ya Kigamboni.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bodi hiyo ilivyofanya ukaguzi kwa taasisi 146 zilizopo katika mikoa tisa  na kubaini jumla ya watumishi 268 wanafanya kazi za ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano  uliofanyika katika ofisi za bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyazi pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi alipokuwa  anazungumza na waandishi wa habari  katika ofisi zaBodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

Waandishi wa redio jamii 25 wajifua kuhusu majanga

$
0
0
WAANDISHI wa habari kutoka kanda zote nchini ambao wanahudumu katika redio za jamii, wameingia katika mafunzo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki watajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.
Akizungumza mjini hapa Christophe Legay, Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari ili waweze kuelimisha jamii.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya tatu kwa waandishi wa habari na yamegusa wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo hayo.
Legay alisema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabianchi majanga ya asili yamekuwa yakijitokeza sana na kwa kasi hivyo imeonekana haja ya kuwapatia wananchi mafunzo maalumu ya kukabiliana na majanga hayo ikiwa na pamoja na kujiweka tayari.

"Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia" alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.

Alisema kwa sasa wengi wa waandishi namna yao ya kuandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali.
Legay alisema watu wakitambua namna ya kusimamia maafa na matumizi ya raslimali na nyenzo za usimamizi hasara kwa mali na watu zitapungua.

Alisema pamoja na majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, pia kuna majanga yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile milipuko ya matanki, ajali mbalimbali ambazo wananchi amekuwa wakijihudumia badala ya kuokoa mali na watu.

Naye Kevin Robert, mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka UNESCO alisema ni wajibu wa waandishi wa habari kwanza kutambua namna ya kukabiliana na majanga, elimu ambayo itawapa undani wa nini kinatokea, wafanye nini na nani asaidie wawe na taarifa sahihi za kusaidia wananchi.

Robert alisema wanahabari hao kutoka Redio 25 na Mratibu kutoka mtandao wa Redio za Jamii zilizotawanyika nchini kote ikiwamo mikoa ya Lindi,Katavi, Kilimanjaro Mara wanafundishwa mifumo ya upashanaji habari katika maafa, mifumo ya habari, kitengo cha maafa na utaratibvu wake na namna nzuri ya kusaidia waliokumbwa na mafaa.

Tanzania kwa sasa imeshakabiliwa na majanga ya asili mengi kama  mafuriko, ukame, upepo mkali, tsunami, mmomonyoko wa bahari,  mvua za mawe na upepo mkali  kama wa Kahama na mafuriko ya Mtwara, 2015 na pia kulipuka kwa lori la mafuta mjini Morogoro.
Katika ajali ya Morogoro wananchi badala ya kuokoa walikuwa wanaiba mafuta hadi lori lilipolipuka.

Kevin aliwataka waandishi hao kutambua changamoto zilizopo pamoja na kuelewa Sheria ya Uratibu wa Misaada ya Maafa Namba 9 ya 1990 (iliyofutwa na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya 2015) na kujua kazi ya kitengo cha Kuratibu Misaada ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema ni matarajio ya UNESCO kuona kwamba mafunzo hayo yanaimarisha upashanaji habari wenye tija kubwa katika kukabili majanga na maafa.
 Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO, Christophe Legay akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Kevin Robert akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mratibu wa Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), Irene Makene akitoa salamu TADIO kwa waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Washiriki kutoka redio za jamii wakichangia maoni wakati wa mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Baadhi ya ya waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.

TMA yatoa taadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa na mawimbi kwa siku tatu mfululizo

$
0
0
 
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa na mawimbi makubwa katika baadhi ya maeneo ya Kaskazini kwenye mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro, Visiwa vya Unguja na Pemba.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na TMA, ikionesha uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa mvua kubwa sambamba na mawimbi makubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 9 hadi Oktoba 12, 2019.

Angalizo hilo la mawimbi Mmakubwa limetolewa pia kwa baadhi ya maeneo Pwani ya Bahari ya Hindi na kusini mwa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mamlaka hiyo imewataka watumiaji wa bahari na maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari.

“Tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa imetolewa kwa maeneo ya ukanda wa pwani yote, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,”  imeeleza sehemu ya taarifa hiyo fupi.

Katika taarifa hiyo ya  kifurushi cha siku nne cha tahadhari za hali ya hewa, TMA imeeleza athari kuwa kiwango kikubwa cha athari kinaweza kujitokeza.

TMA pia imeeleza athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, kutawanyishwa na ucheleweshwaji wa usafiri baharini na nchi kavu na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

NAIBU SPIKA AKIONGOZA KIKAO CHA BODI YA MRADI WA KULIJENGEA BUNGE UWEZO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 
 Naibu Spika wa Bunge na Mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Mradi kulijengea Bunge Uwezo (Legislative Support Project-LSP II) Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bodi hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Naibu Spika ni Mwenyekiti mwenza wa Bodi hiyo na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Christine Musisi. Wengine katika kikao hicho ni Wajumbe wa Bodi hiyo kutoka pande zote mbili.

PICHA NA BUNGE

DC Katambi aingilia kati mgogoro kati ya wafanyakazi na mkandarasi wa miradi ya Soko na Stendi ya Mabasi

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi ameingilia kati mgogoro uliopo baina ya wafanyakazi wanaojenga miradi ya Soko, Stendi ya kisasa ya mabasi na eneo la michezo la Chinangali dhidi ya Kampuni ya Mohamed Builders inayosimamia miradi hiyo.

DC Katambi amechukua hatua hiyo baada ya wafanyakazi hao kuandamana kwenda kwenye Ofisi yake kudai haki zao za malipo kutoka kwenye Kampuni hiyo ambapo wanadai malimbikizo ya mishahara yao.

Wakizungumza na Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alifika na kuzuia maandamano hayo, wafanyakazi hao kwa pamoja wamemueleza DC Katambi kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na danadana za malipo ambazo wamekua wakipigwa na muajiri wao.

" Mheshimiwa DC sisi wananchi wako yapata mwezi wa nane huu unaenda hatujalipwa stahiki zetu, tukidai kwa nguvu wanatulipa kidogo kidogo na kututishia kutufukuza. Tunashangaa kwanini wanatufanyia hivi ilihali Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hii.

Unavyotuona hapa wengine hatuna hata fedha ya kula na Watoto wetu. Tunaomba uingilie kati na kusaidia tuweze kupata haki zetu, " Amesema mmoja wa wafanyakazi hao, Makwata Alfred.

Mfanyakazi mwingine Ramadhan Masha amesema kwa muda mrefu wamekua wakiangaika kufuatilia malipo yao lakini hakuna msaada wowote wanaoupata zaidi ya kutishiwa kufukuzwa kazi.

" Utaratibu ni sisi tulipwe fedha zetu kila siku lakini wao wamekua wakitucheleweshea wakabadilisha utaratibu tuwe tunalipwa kwa wiki na bado hiyo imekua ni tatizo. Tunaomba Mhe uingilie kati tuweze kulipwa haki zetu, " Amesema Masha.

Akijibu malalamiko hayo, DC Katambi amesema ofisi yake haijawahi kupokea kero za malipo kutoka kwa wafanyakazi hao na kuahidi kulishughulikia huku akitoa maagizo matano kwa Kampuni na kuitaka kufika ofisini kwake mara moja kueleza sababu za wafanyakazi hao kutolipwa.

" Ndugu zangu nimesikia kilio chenu, mimi siku zote niko upande wa wananchi, sitokubali kuona haki ya wananchi waliompigia kura Rais Magufuli ikipotea. Hivyo nawahakikishia nyinyi nyote mliopo hapa hakuna yeyote atakayefukuzwa kwa kudai haki yenu.

La pili kupitia viongozi wenu wa katika miradi yote mkae kwa pamoja mniletee barua inayohusiana na madai yenu, jambo la tatu madai ya NSSF nitamuita Meneja wa NSSF leo na mkandarasi kwa kuwa atakuepo wanieleze hizo fedha wanazowakata zinaenda wapi na mtazipataje ikitokea mmeacha kazi," Amesema DC Katambi.

Aidha ameahidi kusimamia ulinzi na usalama kwa wafanyakazi hao pamoja na kukaa kikao na wafanyakazi hao wote na uongozi wa Kampuni hiyo ili kujua mustakabali wao ili waweze kulipwa haki zao kwa haraka.

DC Katambi amewataka wafanyakazi hao kuacha kugomea miradi hiyo kwani kufanya hivyo siyo tu wanamkomoa mkandarasi huyo bali wanamuangusha Rais Magufuli ambaye amekua mstari wa mbele kuleta maendeleo jijini Dodoma.

" Ndugu zangu kila kazi ina changamoto yake, niwasihi msifanye migomo ya kuacha kufanya kazi. Niwaombe mkikwamisha hii miradi mjue mnaikwamisha Nchi siyo mkandarasi. Naombeni mrudi kazini mkaendelee na kazi wakati ambao Mimi nashughulikia malipo yenu," Amesema DC Katambi.

Baada ya kikao hicho wafanyakazi hao wamerudi kazini kuendelea na kazi na kumshukuru Mhe DC kwa kusikiliza kero zao huku wakimuomba aendelee kuwasimamia na kuwatetea.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiwa na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo wakizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Mohamed Builders waliokua wakiandamana kushinikiza kulipwa kwa fedha zao.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Mohamed Builders baada ya kufika kuwasikiliza kero zao za malimbikizo ya mishahara wanayodai kwa waajiri wao
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Mohamed Builders inayosimamia ujenzi wa miradi mitatu ya Soko, Stendi ya Mabasi na Eneo la Michezo la Chinangali ambao wamefanya maandamano kwenda kuonana na DC kutokana na kile walichodai kutokulipwa mishahara yao.

DC KOROGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA KIKOSI KAZI CHA KURATIBU NA KUSIMAMIA MIRADI INAYOTEKELEZWA KUPITIA MKOPO WA BENKI YA DUNIA

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akisisitiza jambo wakati wa mamzungumzo hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa wa Kujenga Uwezo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Debora Mkwemwa wakati wa mazungumzo hayoi


MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa amekutana na kufanya mazungumzo na Kikosi kazi cha kuratibu na kusimamia miradi inayotekelezwa kupitia mkopo wa benki ya Dunia ambao walifika wilayani humo kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea. 

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwake, Afisa wa Kujenga Uwezo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Debora Mkwemwa alisema kwamba wamefika wilayani humo kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa kazi zinazoendelea. 

Alisema ufuatiliaji huo ni miradi ya ujenzi wa barabara tatu,ujenzi wa soko ambao tayari umekwisha na stendi kubwa ya mabasi Korogwe ambayo imekamilika na inatumika kwa sasa hivyo kazi wanayoifanya ni kutaka kuangalia je wana Korogwe kupitia halmashauri na viongozi wanaipokeaji hiyo miradi na wanaisimamia vipi ili waweze kuwahudumia wananchi muda mrefu. 

Alisema kwamba pia watawashauri namna ya kuisimami miradi hiyo ikiwemo pia kushauriana kuhusu miradi watakayoipendekeza kwa ajili ya siku zijazo baada ya kukamilika miradi ambayo walioichagua wenyewe huku akieleza wakipata nafasi watapata miradi mingine inayoanza 2020-2021. 

Afisa huyo alisema kwamba watashauriana nao kuhusua na miradi watakaokuwa wameichagua ili iweze kuwa miradi rafiki ya kutoa huduma na pia kuwanufaisha wana Korogwe. 

Awali akizungumza baada ya mazungumzo hayo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kwamba kama kuna hitaji matokeo ya haraka sana inapaswa wawe wanaweka kwenye jamii ambayo itakuwa inanufaika zaidi 

Alisema kwamba amelichukua suala hilo na atakwenda kulifanyia kazi hasa kwaHalmashauri watu wa mipango na wachumi ambao ndio wanaibuni hiyo miradi huku akiwashukuru wao kutaka kushirikiana na viongozi hao ili fedha za miradi zisirudi na yeye kama DC ametambua kwamba huo ni uzalendo mkubwa kwani kufuatilia jambo ndio mambo yanakwenda hivyo aliwashukuru sana kwa kuwa wamefanya shirikishi hivyo kwa pamoja tutatoka na kitu kimoja. 


DC KASESELA AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA IRINGA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MPIGA KURA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akinadikisha mbele ya muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akipata maelezo kutoka kwa muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa amewataka wakazi wa wilaya ya Iringa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 24-11-2019 na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati ukifika.

Akizungumza wakati alipokuwa anajiandikisha kwenye daftari za mpiga kura katika kituo cha Kinondoni 1 manispaa ya Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa,Richard kasesela amesema kuwa kila mkazi wa wilaya ya iringa wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.

“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore amewahimiza wakazi wa mtaa huo kuendelea kufika katika kituo na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili kuja kutumia haki yao ya msingi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika Tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2019 

MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA 2019 KUFANYIKA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini hapa leo, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa 2019 yanayo tarajiwa kuanza kufanyika mkoani Singida kuanzia kesho. 
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na Waandishi wa habari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida 

MAADHIMISHO ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Singida ambapo Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika kusherehekea siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kuwa yatazinduliwa kesho katika Uwanja wa Bombadia.

" Ndugu Wananchi napenda kuwafahamisha kuwa mkoa wetu wa Singida umepewa heshima na Taifa kuwa mwenyeji wa Siku ya Chakula Duniani.Maadhimisho haya yatazinduliwa kesho Oktoba 10, 2019 natoa wito kwa wananchi wa Singida na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Bombadia ambako maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia kesho na kufikia kilele chake Oktoba 16, 2019.

Dkt. Nchimbi alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo inasema “Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa” na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote wa sekta kilimo kuchangia katika kuhakikisha nchi na dunia inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote.

Alisema Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonyesha hali ya upatikanaji chakula mwaka 2019/2020 ni nzuri, kwani nchi, ina chakula cha kutosha. Kiwango cha utoshelevu wa chakula ni asilimia 119. Uzalishaji wa mazao ya chakula ulifikia tani 16,408,309 ukilinganisha na mahitaji ambayo ni tani 13,842,536. Kati ya hizo Tani 9,007,909 ni mazao ya nafaka na tani 7,400,400 ni mazao yasiyo nafaka.Tunawapongeza watanzania kwa kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo.

MAKAMU WA RAIS ajiandikisha daftari la wapiga kura, atoa neno kwa watanzania

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandikisha kwenye Daftari la orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akitoa taarifa fupi kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani),ambaye alienda kujiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani illiyopo jijini Dodoma.



Charles James, Michuzi TV

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipoenda kujiandikisha katika daftari hilo kwenye Shule ya Kilimani jijini Dodoma leo.

Mama Samia amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi bila kujali itikadi zao za vyama kujiandikisha lakini vile vile waweze kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaowataka.

" Mimi leo nimeamua kutumia fursa hii kuja kujiandikisha katika mtaa wangu wa Salmini na najua ni haki yangu kuchagua Mwenyekiti wa Mtaa wangu na viongozi wangu kwa sababu najua makazi yangu hapo Dodoma na hawa ndio watakaosimamia mambo yangu kwenye mtaa wangu.

" Kwahiyo niwaombe sana ndugu zangu mtoke mkajiandikishe muweze kupiga kura lakini kubwa zaidi niwaombe wakati wa kuchagua mchague viongozi kweli watakaokwenda na kasi ya Serikali yetu, " Amesema Mama Samia.

Amewataka watanzania kuchagua viongozi waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi, wenye maadili ya kuwatumikia watanzania na wenye kutunza rasimali za wananchi wao na ambao watawasaidia viongozi wa ngazi za juu katika kuwatumikia watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Benelith Mahenge zoezi la uandikishaji ndani ya Mkoa huo limeanza jana na kwamba matarajio yao ni kuandikisha wananchi Laki Tisa.

" Idadi ya vituo ndani ya Mkoa wetu ni 3, 679 na toka jana tumeandikisha watu 156,000 hivyo tunaamini mpaka siku saba ziishe ambazo ni za uandikishaji tutakua tumezidi hata idadi kwa kuwa wananchi wengi pia wanaenda makazini hivyo siku za Jumamosi na Jumapili watapatikana kwa wingi," Amesema Dk Mahenge.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUPITIA UPYA MAENEO YALIYOTENGWA KWA SHUGHULI ZA JAMII

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia picha zinazoonesha maeneo yaliyovamiwa wilaya ya Ilemela wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Katikati aliyevaa Miwani ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya eneo lililovamiwa wilaya ya Ilemela jana wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia picha zinazoonesha maeneo yaliyovamiwa wilaya ya Ilemela jana wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa kupitia maeneo yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jana. Katikati aliyevaa Miwani ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo.


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kupitia upya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile makaburi, maeneo ya wazi, ujenzi wa taasisi za umma na masoko ili kujiridhisha kama bado yanafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa au yamevamiwa ili kurasimisha.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akikagua utekelezaji wa kupitia maeneo yaliyovamiwa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana linalotekelezwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizarani, Ofisi ya kanda ya Ziwa na Maafisa ardhi wa wilaya hizo.

Dkt Mabula alikemea kitendo kinachofanywa na baadhi ya halmashauri nchini kutolipa fidia katika maeneo wanayoyatwaa kunakosababisha kuzalisha migogoro isiyo ya lazima na uvamizi mpya katika maeneo hayo.

‘’Halmashauri zote nchini naziagiza kupitia upya maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii tujue maeneo hayo yamevamiwa kwa kiasi gani, tuwafanyie urasimishaji wananchi walipe kodi ya serikali na kama eneo bado halijavamiwa basi tulilinde ili lisiendelee kutumika kwa matumizi yaliyo,kusudiwa ‘’ alisema Mabula

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wataalamu wa ardhi nchini kuacha kukaa ofisini na badala yake waende kwa wananchi ili kuepuka kuitia hasara serikali kwa kutoa taarifa zisizo na uhakika.

Alitoa hofu wananchi wa mitaa ya Nyagungulu, Mwambani na Bukengwa yaliyopo kata ya Ilemela mkoani Mwanza kuwa, serikali ya awamu ya tano itaendelea kutatua migogoro ya ardhi kwa kuzingatia haki , sheria na ubinadamu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula, mbali na kumpongeza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi kubwa anayoifanya pia alimshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuunda timu ya Mawaziri kupitia maeneo yote yenye changamoto za ardhi huku akiiomba halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha ulipaji fidia kwa wananchi wenye migogoro ya ardhi unafanyika.

Naye Kmaishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alieleza kuwa, zoezi la ukaguzi maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii lilianza septemba 30, 2019 na kumalizika Oktoba 4, 2019 kabla ya kuongezwa siku nne na Naibu Waziri Dkt Mabula ambapo aliomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na viongozi ili kukamilisha zoezi hilo kwa haraka na ufanisi.

Waajiri Watakiwa kuzingatia Mpango wa Mafunzo kwa Watumishi wa Umma Ili kuwajengea Uwezo kiutendaji

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.
Afisa Utumishi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Elisha Msengi akijibu hoja wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Meatu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza alipowasili katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu katika ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo.

…………………………

Na Happiness Shayo- MEATU

Serikali imewataka waajiri nchini kuweka kipaumbele katika programu za mafunzo kwa Watumishi wa Umma ili kuwajengea uwezo kiutendaji kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya kiutendaji.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

“Waajiri hakikisheni mnatoa mafunzo kwa watumishi wenu ili kuendana na kasi ya Sayansi na Teknolojia ikiwa ni pamoja na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa ametoa wito huo baada ya kubaini kuwepo kwa uelewa mdogo wa masuala ya kiutumishi kwa baadhi ya watumishi wa umma wilayani humo.

“Nimegundua bado kuna ombwe la uelewa mdogo wa miiko ya kazi miongoni mwa watumishi wa umma unaosababisha kufanya kazi kwa mazoea, hivyo mafunzo yatawasaidia kuboresha utendaji kazi wao.” Dkt. Mwanjelwa ameongeza.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameitaka Tume ya Utumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kujiridhisha kama Waajiri wanawapeleka watumishi kupata mafunzo katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ili wawe na ufanisi kiutendaji. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kufanya ziara wilayani hapo na kuahidi kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa.

Dkt. Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za watumishi hao na kuzitatua.
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live


Latest Images