Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DC MBONEKO AONGOZA WADAU KUSHEREHEKEA SIKU YA WAZEE KWA KUTOA MSAADA WA MAHITAJI KITUO CHA WAZEE BUSANDA

$
0
0



Wadau wa Maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wamesherehekea Siku ya Wazee Duniani kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 2.5 kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Wadau hao wamefika katika kituo hicho leo Jumamosi Oktoba 5,2019 kusherehekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 1.

Akizungumza katika kituo kinachohudumia kaya 20 za wazee akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM),Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta amesema wameamua kusherekea siku ya wazee duniani katika kituo hicho kwa kuwapatia mahitaji muhimu yanayotakiwa ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili wazee hao.

Mboneko alivitaja vitu vilivyotolewa na wadau kuwa ni magodoro 20,shuka 40,vyandarua 20,mchele kilo 200,sukari kilo 50,unga wa sembe kilo 225,maharage kilo 20,sabuni za miche boksi moja, sabuni ya unga kilo 15,mafuta ya kupaka katoni 2,mafuta ya kupikia lita 20,dagaa debe 2 ,dawa za meno katoni mbili,viberiti katoni 2,chumvi katoni 1,juisi katoni 2 na nyanya debe moja. 

Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru wadau waliojitokeza kutoa msaada wa vitu hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni mbili,laki tano na elfu ambao ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll Seif Said Seif aliyetoa msaada wa magodoro 20,vyandarua na shuka vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na laki nne. 

"Kwa namna ya pekee niwashukuru wadau walioguswa kutoa mchango kusaidia wazee wetu hawa.Wadau hawa ni pamoja Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,Watumishi na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hoja Mahiba na watumishi wa benki ya NBC",alisema Mboneko. 

"Wadau wengine ni Kwaya ya Malaika Wakuu Kanisa Katoliki Ngokolo,Familia ya Richard Male,Familia ya mama Shine,Mama Mihambo na marafiki zake,Gilitu,Said Makilagi (Musoma Food),Dada Scola na Lightness,waandishi wa habari na wadau wengine ambao sijawataja ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa mahitaji haya kwa ajili ya wazee wetu",aliongeza Mboneko. 

Mkuu huyo wa wilaya alisema kila mtu ni mzee mtarajiwa hivyo ni vyema tukawapenda na kuwapatia mahitaji wazee huku akisisitiza msaada huo ni kwa ajili ya walengwa tu hivyo kuwataka watu wenye uwezo wafanye kazi ili kujipatia mahitaji yao. 

Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad aliahidi kuwalipia Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) wazee 11 waliopo katika kituo cha Busanda ili wapate huduma za afya bila usumbufu. 

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kujitokeza kugombea na kuchagua viongozi wenye kusaidia jamii. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wazee katika kituo hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nganganulwa kilipo kituo hicho,George Charles akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad. Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akielezea kuhusu msaada wa vitu mbalimbali pichani vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Paroko wa Parokia ya Busanda,Padri Josephat Mahalu. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad. 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Wazee cha Busanda, Elias Shilanga akielezea kuhusu kituo cha Busanda. 
Sehemu ya vitu vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda. 
Wadau wakijiandaa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi unga wa sembe bi Mary Barabara katika kituo cha kulelea Wazee cha Busanda kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kila mzee alipokea msaada wa unga wa sembe,mchele,sukari,mafuta ya kupaka,mafuta ya kupikia,sabuni,godoro,shuka 2,vyandarua,maharage n.k 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akikabidhi godoro,shuka,chandarua kwa bibi (kulia). 
Zoezi la kukabidhi godoro,shuka na chandarua likiendelea. 
Bibi akifurahia baada ya kupokea mahitaji mbalimbali. 
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga akisaidiana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kubeba mfuko wa nyanya wakati wa kugawa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee katika kituo cha Busanda. 
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea. 
Mdau Said Nassoro akigawa sabuni ya unga. 
Mzee Zacharia Makaranga akiwashukuru wadau waliotoa msaada kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Bibi akishukuru kwa msaada uliotolewa na wadau.Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

RC MAKONDA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, DKT. BASHIRU ATOA NENO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally akizungumza katika mkutano wa viongozi wa CCM ngazi zote mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makondaakizungumza katika mkutano wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam ngazi zote uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi zote mkoa wa Dar es salaam wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizunguza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

 


 
 
 
…………………………………………

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 05 amewasilisha kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa,Wilaya, Kata na Mashina taarifa ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano kwenye Mkoa huo kwa mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya Utekekelezaji wa Ilani ya CCM inayolenga kutatua kero za Wananchi.

RC Makonda amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwenye mkoa huo ni Ujenzi wa Barabara chini ya TANROAD, TARURA na DMDP zenye urefu wa Km 5,153, Ujenzi wa Miundombinu ya upatikanaji wa Maji, Ujenzi wa Mejengo ya Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati na Vifaa Tiba ambavyo vimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto kwa wananchi.

Aidha RC Makonda ameitaja miradi mingine inayotekelezwa ni sekta ya Elimu kupitia ujenzi wa Vyumba vya madarasa, ofisi za walimu na matundu ya Vyoo, Sekta ya Nishati ya Umeme, Ujenzi wa Viwanda, Sekta ya Ardhi, Usafiri pamoja na suala la Ulinzi na usalama.

Kwa Upande wake katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally amepongeza mkoa wa Dar es salaam kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwaonyesha wananchi kwa vitendo kile kinachofanywa na Serikali yao ya Awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Aidha Dkt. Bashiru amepongeza Mkoa huo kwa kuwa kinara wa kusimamia makusanyo ya kodi, kusimamia kikamilifu suala la ulinzi na usalama, kusimamia Usafi wa Mazingira pamoja na kuwa na utamaduni mzuri wa kushirikiana na Wasanii na vyombo vya habari.

NAIBU WAZIRI STELLAH MANYANYA AZINDUA KITABU CHA MAFANIKIO YA SIRI ZA NDOA

$
0
0

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya akikata utepe kuashiria kuzindua Kitabu cha Siri za Mafanikio ya Ndoa katika hafla iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtunzi wa Kitabu hicho, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick na kushoto ni mke wake Mariam Sako.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya akionesha kitabu hicho baada ya kukizindua.
 Washiriki wa hafla hiyo wakipatiwa nakala ya kitabu hicho.
Washiriki wa hafla hiyo wakipatiwa nakala ya kitabu hicho.



Na Kulwa Mwaibale


NAIBU  Waziri wa Viwanda na Biashara, Injinia Stella  Manyanya, amesema  watanzania wengi wanachangamoto za kindoa hali inayosababisha msongo wa mawazo, mdororo wa kiuchumi na jamii isiyo na malezi bora.

Ameongeza kuwa asilimia 90 ya ndoa hizo zimekufa na wenza wake wanaishi kwa maonyesho na dhana ya kuvumiliana wakiona aibu kutengana hivyo ipo haja kufanyika kwa tafiti na kuwekeza nguvu katika elimu ya ndoa.

Injinia Manyanya aliyasema hayo jana  akizindua Kitabu cha Siri za mafanikio ya Ndoa kilichoandaliwa na mtunzi ambaye ni Mchungaji na Mkurugenzi wa Fedha  wa Bohari ya Dawa  
(MSD), Dk. Sako Mayrick.

Naibu Waziri huyo alisema  watanzania wengi wanachangamoto za kindoa hali inayosababisha 
msongo wa mawazo, mdororo wa kiuchumi na jamii isiyo na malezi bora.

“ Ni  kawaida watu kufanya sherehe za ndoa na kutumia gharama kubwa lakini ndoa zinazoishi na hai ni chache huku nyingi kuvunjika  kwake ni kimyakimya kwa dhana ya kuona 
aibu,”alisema.

Alisema changamoto hizo ndio zinazochangia ongezeko la wagonjwa wa akili,  baadhi ya watu kuwa na msongo wa mawazo uliopitiliza hadi kupasuka mishipa ya fahamu, gharama kubwa ikitumika kusafirisha baadhi ya wagonjwa nje ya nchi huku kiini cha matatizo ikiwemo ni 
migogoro iliyokithiri ya kifamilia.

“Imefika wakati wasomi wetu kutumia uwezo wao katika kutoa elimu ya ndoa na familia, na kujua  ndoa si fasheni tu, vitabu vya aina hii vinasahaulika hivyo iwe chachu ya  kupambana na matatizo yaliyopo kwakuwa vita ya uimarishaji wa ndoa katika jamii  inahitaji watu  wa kiroho na kitaalamu wakiwemu wa ustawi ya jamii kushirikiana,” alisema.

Alisema utunzi wa vitabu hivyo pia ni fursa ya kuufikia uchumi wa kati wa viwanda hivyo  alimpongeza Sako kuandika kitabu hicho alichosema kitaisadia kurejesha amani na upendo kwa watu wengi hususani vijana kutokana na mafunzo yaliyomo.

“Kama kitabu hiki kingeandikwa siku nyingi huko nyuma huenda nami kingenisaidia,” alisema.Alisema, kufuatia fursa zilizopo, uandishi wa vitabu ni  ajira na uwekezaji katika viwanda vya uchapishaji hivyo amewashauri Watanzania kuandika kwa wingi vitabu vilivyosahaulika na vyenye uhitaji  kwa jamii   ili kuweza kuufikia uchumi wa kati wa viwanda.

Aliongeza kuwa ndoa zinapokuwa na amani familia zitakuwa na furaha hivyo kuweza kufanya kazi zenye tija jambo litakaloinua uchumi wa Taifa.
Naye Profesa Amos Mwakigonja kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), alimpongeza Sako ambaye licha ya kuwa mtumishi wa serikali ni mchungaji wa Kanisa la Mafanikio la Kikristo ambaye anatumia muda mwingi  kuandika vitabu.

“Sisi wataalamu wa afya tunakutana na changamoto nyingi za watu waliothirika na matatizo ya kindoa, Sako ni mpambanaji, mwenye kutumia elimu yake ya uhasibu, sheria na huduma za kiroho kwa ajili ya jamii ni muhimu kuungwa mkono,” alisema.Kwa upande wake muandishi wa Kitabu hicho Dk.  Sako alisema jamii imekuwa na changamoto nyingi za kindoa zinazosababishwa na mfumo dume.

Alisema ni muhimu kuelewa kuwa mwanamke katika ndoa si mtu aliyepo kwa ajili ya kuzaa, kufanya kazi za nyumbani na kulea familia  pekee kwakuwa ana nguvu na uwezo wa kuharibu maisha iwapo wawili hao hawatathaminiana na kuishi kwa makubaliano.

“ Maisha ya ndoa bora ni muhimu sana hivyo wenza hawana budi kukubaliana baadhi ya mambo, ilichukua miaka kumi kujifunza kupitia vitabu, kufanya utafiti, semina na maandiko 
matakatifu kuweza kuelewa maana ya ndoa na kusudio la Mungu katika kuishi kwa amani,” alisema.

Alieleza kuwa imefika wakati wa kujua tofauti kati ya ngono, mapenzi na tendo la ndoa kuwa inaweza leta  mapinduzi makubwa katika jamii na uchumi.Alisema kupitia kitabu hicho watu watajifunza namna ya kupata mchumba bora, sifa 15 za mke na mume aliyebora, misingi 21 ya maisha ya wanandoa, heshima ya tendo la ndoa, nguvu na mamlaka ya mwanamke na  athari za mitandao.

Mambo mengine alisema ni misingi ya sheria ya ndoa, miiko ya wanandoa katika uhusiano na maombi 100 kwa ajili ya uchumba hadi ndoa.


MAONESHO YA PILI YA SIDO KITAIFA 2019 YAFANA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageluka (mwenye suti waliokaa) akiwa pamoja na Wafanyakazi wa Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye banda lao katika Maonesho ya Pili ya Sido Kitaifa 2019 yanayofanyika mkoani Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Edwin Rutageluka akizungumza na wafanyakazi wa Sido katika maonesho hayo.
Muonekano wa sehemu ya mabanda katika maonesho hayo.
Mjasiriamali Prudent Sulle (kushoto) kutoka Kampuni ya Rose Products ya Jijini Mwanza, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao kuhusu bidhaa zao wanazo zizalisha. Kutoka kulia ni Kapande Noni, Ambros Msimbe na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Rose Stephen.
Frank Lyakurwa kutoka Dar es Salaam (kulia) akielekezwa jambo na Afisa Mauzo wa Benki ya NMB, Michael Mwangamila baada ya kufungua akaunti ya chapuchapu katika maonesho hayo. Kutoka kushoto ni Wakala wa Benki hiyo, Nathan Nzolo na Afisa wa Benki hiyo Suzan Peter.
Mkaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB Mkoa wa Singida, Eliazary Lwanji akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho hayo.
Afisa Vipimo Mwandamizi wa Wakala wa Vipimo, Wilue Amos akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao kuhusu kifaa cha kupimia pampu za mafuta kinavyofanya kazi. Wa pili kulia ni Katibu Mahsusi (PS) wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Singida, Grace Severe.
Afisa kutoka Kampuni ya Helvetas Tanzania, John Mabagalu (kulia) akitoa maelezo kwa Mkazi wa Magu Mwanza, Juma Kisinza kuhusu mchele unaozalishwa na kampuni hiyo ambao unatumiwa na watu wenye kisukari.
Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Tume ya Ushindani ( FCC) Adefrida Ilomo akionesha bidhaa zisizo na ubora zilizotengenezwa kinyume cha sheria.
Mwelimishaji Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida, Japhary Hamisi akitoa maelezo kwa Mjasiriamali Nancy Kimalila aliyetembelea banda lao.
Joseph Kavishe, akijieleza kwa Afisa wa Benki ya CRDB, Evance Makundi (kushoto) alipotembelea banda la Benki hiyo katika maonesho hayo. Katikati ni wakala wa CRDB, Maria Kitima.
Wafanyakazi wa Kituo cha Radio cha Standard FM cha Mjini Singida, Ally Juma na Faida Adam wakiwa mbele ya banda lao katika maonesho hayo.
Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Irene Njovu akimuelekeza Mzee Joseph Hoyanga jinsi mashine ya kupima ubora wa vyakula inavyofanyakazi. Kulia ni Afisa wa Kampuni hiyo, Peter Charles.
Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Lazaro Mnkumbu (katikati) akitoa maelekezo jinsi ya kutumia mashine ya kupandia mbegu zinazosambazwa na kampuni hiyo. Kulia ni Mzee Masegense Masegense na Ramadhani Makenya.
Afisa wa Benki ya Tpb Bank, Lilian Rutha akitoa maelezo kwa Mtaalamu wa Kilimo, Mashaka Mlangi alipotembelea banda la Benki hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kijiji cha Mpandangendo Mkoa wa Ruvuma kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Ryuta Okamoto akionesha wananchi jinsi ya kutumia kibao maalumu cha kufulia nguo pamoja na kifaa cha kupukuchulia mahindi kilichotengenezwa na vijana kutoka katika kijiji hicho waliopatiwa mafunzo na shirika hilo.
Watoto wakipata burudani ya kubembea katika maonesho hayo kwa gharama ya sh.1000 kwa dakika nane.

Maafisa Lishe Waaswa Kuelimisha Wananchi Umuhimu wa Chakula Bora

$
0
0
Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa wadau wa lishe Jijini Dodoma Oktoba 4,2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa wadau wa lishe Oktoba 4, 2019 Jijini Dodoma.
Katibu mkuu, Ofisi ya Waziri mkuu, Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu wa mkutano wa wadau wa lishe uliofanyika Jijini Dodoma Oktoba 3 na 4, 2019 wakati akifunga mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa lishe wakifuatilia hafla ya kufungwa kwa mkutano huo Oktoba 4, Jijini Dodoma, mkutano huo ulifungwa na Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa lishe wakifuatilia hafla ya kufungwa kwa mkutano huo Oktoba 4, Jijini Dodoma, mkutano huo ulifungwa na Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.

…………………………………………………….

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Maafisa lishe nchini wametakiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora ili kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu katika jamii.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa lishe uliofanyika Jijini Dodoma Oktoba 4, 2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi Waziri mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama, Katibu mkuu Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa maafisa lishe wanapaswa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau kuhusu umuhimu wa lishe bora.

“ Kipaumbele lazima kiwekwe katika makundi maalum kama wazee, watoto, akinamama wanajawazito na wale wanaonyonyesha ili kufanikisha azma ya Serikali kuondoa Changamoto ya utapiamlo na udumavu hapa nchini”; Alisisitiza Bi. Mwaluko

Akifafanua amesema kuwa Serikali inasisitiza matumizi ya sanaa, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge katika kuelimisha umma kuhusu athari za utapimlo na udumavu hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Afya) Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa maazimio ya kikao hicho yanapaswa kutoa majawabu yatakayowezesha kuondokana na utapiamlo na udumavu hapa nchini.

Aliongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi na wadau katika kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu katika maeneo yote nchini ili kujenga jamii yenye afya bora.

Aidha, Dkt. Chaula aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu hapa nchini ili kujenga jamii yenye afya bora hasa wakati huu Taifa linapojenga uchumi wa Viwanda na kutekeleza azma ya kuleta ustawi kwa wananchi.

Kikao kazi cha wadau wa lishe kimefanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma kikiwashirikisha wadau wa maendeleo, Maafisa lishe, Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Makatibu wakuu, Wabunge na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali.

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Maafisa lishe nchini wametakiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora ili kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu katika jamii.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa lishe uliofanyika Jijini Dodoma Oktoba 4, 2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi Waziri mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama, Katibu mkuu Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa maafisa lishe wanapaswa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau kuhusu umuhimu wa lishe bora.

“ Kipaumbele lazima kiwekwe katika makundi maalum kama wazee, watoto, akinamama wanajawazito na wale wanaonyonyesha ili kufanikisha azma ya Serikali kuondoa Changamoto ya utapiamlo na udumavu hapa nchini”; Alisisitiza Bi. Mwaluko

Akifafanua amesema kuwa Serikali inasisitiza matumizi ya sanaa, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge katika kuelimisha umma kuhusu athari za utapimlo na udumavu hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Afya) Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa maazimio ya kikao hicho yanapaswa kutoa majawabu yatakayowezesha kuondokana na utapiamlo na udumavu hapa nchini.

Aliongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi na wadau katika kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu katika maeneo yote nchini ili kujenga jamii yenye afya bora.

Aidha, Dkt. Chaula aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu hapa nchini ili kujenga jamii yenye afya bora hasa wakati huu Taifa linapojenga uchumi wa Viwanda na kutekeleza azma ya kuleta ustawi kwa wananchi.

Kikao kazi cha wadau wa lishe kimefanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma kikiwashirikisha wadau wa maendeleo, Maafisa lishe, Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Makatibu wakuu, Wabunge na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali.

Teknolojia inavyoleta mapinduzi katika sekta ya bima ya afya

$
0
0

Mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akihutubia Bunge aliwasihi Watanzania kujiunga na mifumo ya bima za afya.

Katika maelezo yake Waziri alisisitiza kuwa, endapo wananchi watajiunga na mifumo hii na kupata bima za afya, wataweza kupata matibabu wakati wowote pasi na kuhofia uwepo wa fedha.

Inafahamika kuwa upatikanaji wa huduma za afya za msingi kwa kila Mtanzania  ni lengo moja la Mpango wa Maendeleo wa Taifa kufikia mwaka 2025.

Serikali imekuwa ikifanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa watu katika pande zote za nchi wanapata huduma za afya zenye unafuu.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watoa huduma za afya binafsi nchini Tanzania. Kampuni kutoka sekta binafsi wametumia fursa ya teknolojia ya kidijitali kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuepuka changamoto mbalimbali.

Uwekezaji kwenye huduma za afya kupitia simu za mkononi umekuwa na matokeo chanya kwa watu, na hivyo kuimarisha nguvu kazi ambayo imekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

Tigo Tanzania ni moja ya kampuni ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma za afya kwa mifumo ya kielektroniki.
Huduma ya Tigo Bima inawasaidia watu kutoka maeneo mbalimbali nchini kuweza kupata huduma za afya zilizo bora bila kuathiri mipango yao mingine ya kifedha.

Mtu yeyote anayetumia laini ya Tigo anaweza kujiunga na huduma mbalimbali kama vile, Maisha, ajali, na bima ya kulazwa hospitali, kwa ajili ya kujigharamia wao wenyewe pamoja na familia zao.

Pia, endapo mteja wa Tigo atalazwa hospitali, watapatiwa fedha kwa siku zote ambazo atakuwa amelazwa. Huduma kama hii inawasaidia wateja wa Tigo kuwa na mpango wa muda mrefu wa huduma za afya kuliko kushtukizwa au huduma za gharama kubwa.

Kampuni kama Tigo inaonesha kuwa teknolojia ina nafasi kubwa sana katika kuimarisha huduma za afya. Huduma kama hizi kwa kushirikiana na serikali zinaweza kuwasaidia wananchi wengi kupata huduma bora na kuimarisha mifumo ya afya.

Nafasi kama hizi zinaweza kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya Tanzania na kuhakikisha inafanikisha lengo lake la mwaka 2025.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA TUNDUMA –SUMBAWANGA KM 223.21 KATIKA ENEO LA LAELA MKOANI RUKWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia aliyeshika utepe, viongozi wa mkoa wa Rukwa, Mawaziri, viongozi wa Dini pamoja na Chama, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
 Sehemu ya Barabara ya Tunduma –Sumbawanga km 223.21 iliyofunguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Laela mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Laela mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chiwanda Tunduma mkoani Songwe mara baada ya kusimama wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
 Wananchi wa Ikana wakisangilia mara baada ya kumuona  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye eneo hilo wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na maaskari wa Jeshi la Polisi wakati akielekea kukagua kituo cha polisi cha Laela mkoani Rukwa mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga. PICHA NA IKULU

COMMUNITY’S FINANCIAL STATUS WORRYING- ASSEMBLY STATES, CALLS ON COUNCIL OF MINISTERS TO FASTRACK REMITTANCES TO REMEDY SITUATION

$
0
0

Hon Abdikadir Aden, Chairman of the General Purpose Committee presents the report of the Committee on the petition received from EACSOF
Hon Wanjiku Muhia makes her submission to the House yesterday.
The EACSOF petitioners (from left) – Ms Lilian Alex, Programme Officer, Mr Jonas Ndunguru, Communication Officer and Mrs Martha Makenge, Chief Executive Officer, EACSOF were among the parties that attended the Session yesterday.

***********************************

East African Legislative Assembly; October 4th, 2019: Arusha, Tanzania: The East African Legislative Assembly once again wants the East African Community Council of Ministers to address the dire financial crisis, the regional bloc is in. Critical to the matter is the need for all Partner States to duly remit their financial obligations in a timely manner and fashion. Particularly, the Assembly has recommended that the Council of Ministers should consider invoking Article 143 or 146 to impose sanctions against Partner States that default on payment. Particularly, one Partner State, the Republic of South Sudan is been urged to comply by end of October 2019.



As the matter came under scrutiny, the House commended the Republic of Uganda for honouring its contribution for the Financial Year 2019/20 to the tune on 72% as at October 2nd 2019. EALA urged other Partner States to emulate the Republic of Uganda by complying with regulation 23(5) of EAC Financial Rules and Regulations. Consequently, EALA also wants the Alternative Financing Mechanism finalized and effected and a reconsideration and removal of the zero budget increase ceilings.

The Assembly’s debate follows a petition filed by the regional Civil Society Organizations under the aegis of the East African Civil Society Organizations Forum (EACSOF). EACSOF had in the petition made a number of prayers for consideration by the Assembly on matters it deemed of concern to itself and citizens of the region. 

 The petition signed by acting Executive Director, Martha Makenge, avers two critical matters; on the implementation of the budget of the EAC after being passed by EALA and assented to by the Summit and on the implementation of the Customs Union and the Common Market Protocols with specific focus on implementation of Article 24 of the Customs Union Protocol (on the EAC Trade Remedies Committee).

Chief among the prayers of the petition signed by the Acting Executive Director, Martha Makenge, was for Council of Ministers to recommend to the Summit of EAC Heads of State to invoke article 143 and 146 on Partner States that have met the criteria of activation of that particular article. The EACSOF is further considering filing a legal suit with the East African Court of Justice (EACJ) on interpretation of Article 143 of the Treaty and why it has not been invoked in such circumstances that are detrimental to EAC”, the petition reads in part.

EACSOF further tasked the Assembly in its petition to question the Council of Ministers as to why some Partner States had not cleared the arrears of 2018/19 and that until the first quarter of 2019/20, there were yet to be any remittances. The petitioners therefore sought clarification to know if the failures to pay were tantamount to display of no commitment to the integration process.

The EACSOF Chief Executive further remarked that as the first quarter of 2019/20, only the Republics of Rwanda and Uganda had remitted their dues for the Financial Year 2019/20. The petitioners are therefore concerned if the inaction of the other Partner States, whose remittances were yet to be received as at today, was an indication of less commitment to the integration process. 

The petition also questions the Office of the EAC Secretary General on the actions taken with regards to remittances and implementation of Article 24 of the Customs Union Protocol; and why no public statement(s) with regards to those two matters have been undertaken.

The petitioners informed the Assembly of their constant follow-up of issues of interest to themselves.On implementation of the Customs Union and Common Market Protocols, the EACSOF raised the fact the sustained existence of Technical Barriers to Trade (TBTs) and Non-Tariff Barriers (NTBs) was duly affecting trade.

“EACSOF has been constantly following up the integration process of the EAC, with particular interest of observing the implementation of the EAC Treaty, Protocols, Laws developed in EALA as well as Policies, Strategies, Plans and Programs”, Mrs Makenge said in the petition.

Upon receipt of the petition, EALA Speaker, Rt Hon Ngoga, forwarded the same to the Committee on General Purpose as stipulated by the Rules of the House. The Committee thereafter interacted with the officials of the EACSOF and the EAC Council of Ministers. The Chairperson of the GPC, Hon Abdikadir Aden then presented the report of the General Purpose Committee on the subject matter as the House got underway.

At debate time today, Hon Makame said the matter of elimination of NTBs was critical and is provided for under the EAC Treaty and the Customs Union Protocol. “The issue of elimination of NTBs and trade disputes are provided for and the matter is crucial for East Africans to trade and matters to do with trade disputes are resolved”, Hon Makame said. I am convinced the Council of Ministers has agreed to take remedial measures”, he added.

Hon Maryam Ussi had sought an answer if there was a substantive Council Member from Republic of South Sudan given the prolonged absence of the Minister from the Assembly. In response, the Speaker declared the matter not applicable for determination as the Minister from South Sudan, was yet to be sworn -in and therefore not subjected to the Rules of the House at this point in time.

Hon Kasamba Mathias said whereas the Community appreciates the remittances of funds due by the Partner States, the consistent delay was worrisome. He said the current budget performance stands at 59% and wondered whether it was prudent to continue planning for support of 100% of all activities. “We need to find out why the Republic of South Sudan is not paying”, Hon Kasamba said. “I support the motion to give them the month-long deadline to show commitment to the integration process. What timelines should we give the Minister for EAC from Republic of South Sudan to be sworn in? he posed.

Hon Rose Akol said the Community had done a lot to bring peace to the Republic of South Sudan. “I want to commend the South Sudan Chapter of EALA for attempts they have made to make follow-up on the issue of remittances, she said. “Due to no funds the Community is failing to honour its obligations”, the legislator said, adding that the Court (East African Court of Justice) was unable to hold its cases – thereby delaying justice.

 “With all the provisions of the EAC Treaty, why is there failure on the part of the Council of Ministers to take any course of action? Hon Akol wondered. “If the sanctions are to be in place, then I see a situation where Republic of South Sudan citizens in the Partner States may be in a precarious place with regards to enjoying the accrued benefits.

Hon Kennedy Mukulia appreciated the courtesies so far extended by the EAC to the Republic of South Sudan and said sanctioning was not an option citing the case of Greece crisis in the European Union. “The Country should be urged to comply”, he said.

Hon Wanjiku Muhia sought to be informed about the level of commitment of the Republic of South Sudan in the Community. “The matter is nothing personal – but for the good of the EAC”, she said. The legislator rallied the EALA to continue with its debate and oversight mandate to ensure the EAC realizes its objectives. “I plead with the front-bench (Council of Ministers) to give us the answer to unlock the impasse”, she said.

Hom Kim Ghai, said sanctioning the Republic of South Sudan would jeopardise the country’s gains including the quest for peace. He further mentioned that it was important for Members to give South Sudan time. “While South Sudan rejected the option to join the League of Arab nations, it is interested in remaining within the EAC fold. “Sanctioning the country will not solve the problem”, he said. 

 He recommended that the Chair of the Summit and the Summit Members reach out to the President of the Republic of South Sudan and sort the issue. The legislator also asked the Council of Ministers to hold the next meeting in Juba and emphasise the need for remittances.

Others who supported the motion were Hon Fancy Nkuhi, Hon George Odongo, Hon Mary Mugyenyi, Hon Fatuma Ibrahim.

In response, Hon Adan Mohamed, Cabinet Secretary, Ministry of EAC Kenya said the Council of Ministers would study the recommendations of the House. He maintained that Council of Ministers expects that a report on the Alternative Funding mechanism shall be on its agenda before the next Summit of EAC Heads of State in November, 2019. The report is also expected to address the current policy of zero budget increase ceiling. “The Council is aware that once concluded, the alternative funding mechanism will be a solution to the financial challenges. Council will continue directing Partner States to remit the finances in a timely manner”, CS Mohammed said. 

The Hon Minister informed the House the Sectoral Council of Ministers responsible for EAC Affairs and Planning at its 24th Meeting directed the EAC Secretary General to make proposals on sanctions that can be imposed on EAC Partner States that breach the Treaty in line with Article 143.

“The Secretariat has already prepared a draft Schedule of Sanctions to be applied automatically which are still under consideration. The draft Schedule of Sanctions goes beyond the non-remittance of financial contributions to other breaches of the Treaty”, the Cabinet Secretary stated.

Tigo Fiesta 2019 _SaiziYako Muleba ,burudani mwanzo mwisho

$
0
0

Msanii wa Bongo fleva Maua Sama, akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.

Wasanii wa Bongo fleva Saida Karoli na Chege Chigunda, wakitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
Wasanii wa Bongo fleva Bill Nas na Nandy wakitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
Msanii wa Bongo fleva Whozu, akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja, akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
Mashabiki wa burudani wakionyesha shangwe la levels za Saizi Yako kwenye tamasha la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.

Mrundikano wa majukumu ya wazazi kikwazo cha elimu Njombe

$
0
0

***************************

NJOMBE

Mrundikano wa majukumu ya majukumu,mila na destuli zilizopitwa na wakati pamoja na wazazi kuwashirikisha watoto katika masuala ya biashara wangali shuleni vimetajwa kuwa vikwazo vikuu vinavyokatisha ndoto za wanafunzi wengi mkoani Njombe.

Kukithiri kwa vikwazo hivyo ambavyo vimekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni hususani katika maeneo ya vijijini vinamsukuma askofu wa jimbo la Njombe Padre Elasmo Mligo pamoja na mkuu wa shule ya sekondari Josephine Damas Mwalongo kutoa rai kwa jamii za mkoa wa Njombe kuvipinga kwa kuvipiga vita ili visiweze kuendelea kutekelezwa.

Ikumbukwe maeneo mengi ya vijiji yamekuwa yakiripotiwa mikasa ya wazazi kujikita katika kilimo na biashara za mazai zaidi na kupunguza uangalizi wa watoto huku wengine wakiwataka kufanya vibaya katika mitihani ili wasiweze kuendelea na masomo hatua za juu zaidi kwa lengo la kupata usaidizi katika kazi zao.

Wakati rai hiyo ikitolewa kwa jamii baadhi ya watahiniwa akiwemo Betrice Msovela na Joyce Eugen wanaelezea maandalizi na matarajio yao katika mtihani wao wa mwisho wa kidato cha nne huku pia wakitoa rai kwa wazazi ambao wanajikita zaidi kwenye kutafuta maisha na kujikuta wakisahau jukumu la malezi kwa watoto hususani wanaosoma.

Jacklin Nziku na Heronius Mswata ni wazazi ambao wameshindwa kuzuia hisia zao kwa watoto ambao wamekuwa wakitumbukia kwenye mahusiano ya kimapenzi wangali wanafunzi na kuharibu ndoto zao baada ya kupata ujauzito huku pia wakikiri mzigo wa majukumu waliyo nayo unavyo athiri malezi katika familia.

Shule ya sekondari ya wasichana ya Josephine imefanikiwa kuwatunuku vyeti wahitimu 47 wa kidato cha nne katika mahafali ya 5 tangu ianzishwe.

NAIBU SPIKA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA RED CROSS

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Mkutano Mkuu wa Taifa wa Shirika la Msalaba Mwekundu (TRCS) uliofanyika katika Ukumbi wa Royal Village wa Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Rais wa Shirika la Msalaba Mwekundu (TRCS), Ndugu David Kihevile wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Taifa wa Shirika hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Royal Village wa Jijini Dodoma.

***********************

Debora Sanja, BUNGE.

Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amelishauri Shirika la Msalaba Mwekundu (TRCS) kufungua matawi mengi zaidi na imara yenye wanachama wa kutosha ili huduma wanazozitoa ziwafikie watu wengi zaidi.

Naibu Spika alitoa ushauri huo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Taifa uliofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma.

Alisema matawi hayo yatasaidia kutoa elimu khusiana na Shirika hilo kwa wananchi wengi zaidi ili waweze kujua majukumu ya Shirika na vilevile kuwajengea uzalendo na jinsi ya kufanya shughuli za kujitolea.

“Niwapongeze pia kwa kuanzisha Baraza la Vijana , niwatie moyo wa kuendelea na mkakakti wenu wa kuwashawishi vijana wengi zaidi wajiunge na taasisi yenu kupitia klabu za vijana mashuleni, vijana ndiyo nguvu kazi ambayo ikitumiwa vizuri basi mtachangia kujenga jamii bora yenye kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

Aidha, alilitaka Shirika hilo kuzingatia Kanuni zao za kibinadamu, uadilifu, kutopendelea, uhuru, kujitolea, umoja na ushirikiano.

“Kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga Taasisi imara ambayo inaaminiwa na kuheshimika mbele ya Serikali, wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla,” alisema

Alisema Bunge limeifanyia marekebisho mara kwa mara sheria iliyoanzisha Shirika hilo ili kuipa nguvu na kuliwezesha kutimiza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kwamba Bunge lipo tayari kuendelea kushirikiana na Shirika hilo.

Katika Mkutano huo Naibu Spika alikubali ombi la kuwa Balozi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania na kuahidi kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na unyenyekevu mkubwa.

Awali Rais wa Shirika hilo, Ndugu David Kihevile alimshukuru Naibu Spika kwa kukubali kuwafungulia Mkutano wao .

Alieleza majukumu ya Shirika hilo kwamba ni kutoa huduma mbalimbali za kibinadamu na kwamba Shirika hilo lingetamani kila Mtanzania awe na moyo wa ubinadamu wa kusaidia jamii ya watu wanyonge.

Katika Mkutano huo Naibu Spika alitunikiwa uanachama wa Shirika la Msalaba Mwekundu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atembelea kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mbegu za pamba katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Dkt. Riyaz Haider. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa zawadi ya cheti, fedha,na baiskeli, mkulima wa zao la pamba kutoka Ikungi, Juma Shabani, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mtego wa molasis, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, kilichopo Mandewa katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Dkt. Riyaz Haider. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, Dkt. Riyaz Haider, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia pamba katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU AKASIRISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NDAGO WILAYANI IRAMBA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Ndago, wilayani Iramba mkoani Singida kwa sababu uko chini ya kiwango.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ndago mara baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

“Nimepita kote nchini kukagua vituo hivi lakini hapa wamenikasirisha. Wamenileta kwenye jengo nilikaguem nikajua ni jipya kumbe ni la zamani. Lazima nikiri kwamba fedha yetu hapa haijakamilika, jengo la mama na mtoto halijakamilika. Nilipouliza linakamilika lini, wananijibu tuko kwenye final touches (tuko hatua za mwisho),” amesema.

“Jengo lile halivutii kabisa, wanaotoa maelezo hakuna kinachoeleweka. Sijaridhishwa kabisa na hali hii. Jengo la upasuaji nalo pia nimeona ni la zamani. Hii ina maana hamjajenga jengo jipya. Mimi nataka nione jengo jipya hapa,” amesisitiza.

Alipomuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw, Leno Mwageni amebakiza kiasi gani cha fedha katika sh. milioni 400 ambazo zililetwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo, Mkurugenzi huyo alijibu kwamba hakuna kiasi cha fedha kilichobakia.

Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao kwamba Mheshimiwa Rais John Magufuli anatambua wao hawana uwezo, na tena wanaugua na kuna watu ambao wanapoteza maisha kwa sababu hawawezi kufika kwenye tiba kwa wakati.

“Vituo vya afya vinajengwa kila mahali nchini ili wewe mwananchi usilipe nauli kwenda Iramba mjini au Singida mjini kutafuta tiba, bali upate vipimo vyote hapa hapa ulipo. Vipimo vya magonjwa yote vinapatikana hapa hapa.”

“Fedha hizi zikiletwa zinataka pajengwe maabara, chumba cha upasuaji mdogo na mkubwa, chumba cha huduma ya mama na mtoto, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mkuu wa kituo, lakini hapa Ndago fedha yetu imeharibika,” amesema.

Alipoenda kukagua chumba cha kuhifadhia maiti, Waziri Mkuu alikuta limewekwa mlango wa mbele tu na vyumba vingine vyote havina milango wala mabomba na masinki hayajakamilika tofauti na taarifa aliyopewa kwamba jengo hilo liko tayari.

“Mkurugenzi nimekuta wagonjwa wamelazwa katika baadhi ya vyumba na kazi haijakamilika. Huwezi kupanga vifaa wakati ujenzi unaoendelea ili kumdanganya Waziri Mkuu. Na wala hunidanganyi mimi bali unawadanganya wananchi.”

“Ninazo taarifa kwamba jana mlikesha kupanga vitu ndani. Nenda kaondoe vifaa vyote hadi ujenzi utakapokamilika ndipo madaktari warudi kuendelea na kazi. Serikali hii haiwezi kuvumilia vitu vya hovyo. Hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.

Mapema, Mbunge wa jimbo hilo, Bw. Mwigulu Nchemba alimweleza Waziri Mkuu kwamba alichangia mifuko 400 ya saruji na wananchi wa kata hiyo walichangia mawe na ujenzi wa msingi.

Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa vituo vya afya. “Tunashukuru kwa sababu fedha hizi zimekuja kamili, na siyo kwa mafungu. Wananchi wamechangia nguvu zao na mimi mwenyewe nilitoa mifuko 400 ya saruji,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu awasaidie wananchi wa kata ya Ndago wapate barabara ya lami ya kutoka Singida-Sepuka-Ndago-Kizaga yenye urefu wa kilometa 76. “Hii ni tarafa kubwa kuliko zote na huku ndiko uzalishaji mkubwa uliko. Hii barabara imeshafanyiwa upembuzi yakinifu, kilio na furaha ya wana-Ndago ni barabara hii kuwekwa lami,” alisema.

WAZIRI MKUU AKASIRISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NDAGO WILAYANI IRAMBA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na mtaalam wa maabara, Bahati Ipunda, wakati akikagua kituo cha afya cha Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Oktoba 6.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua kituo cha afya cha Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Oktoba 6.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha afya cha Ndago, kilichopo katika Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Oktoba 6.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika kipande cha tofali, kilichobomoka, wakati akikagua kituo cha afya cha Ndago, wilayani Iramba, katika Mkoa wa Singida, na kutoridhishwa na ujenzi wa kituo hicho, Oktoba 6.2019.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu




WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Ndago, wilayani Iramba mkoani Singida kwa sababu uko chini ya kiwango.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ndago mara baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

“Nimepita kote nchini kukagua vituo hivi lakini hapa wamenikasirisha. Wamenileta kwenye jengo nilikaguem nikajua ni jipya kumbe ni la zamani. Lazima nikiri kwamba fedha yetu hapa haijakamilika, jengo la mama na mtoto halijakamilika. Nilipouliza linakamilika lini, wananijibu tuko kwenye final touches (tuko hatua za mwisho),” amesema.

“Jengo lile halivutii kabisa, wanaotoa maelezo hakuna kinachoeleweka. Sijaridhishwa kabisa na hali hii. Jengo la upasuaji nalo pia nimeona ni la zamani. Hii ina maana hamjajenga jengo jipya. Mimi nataka nione jengo jipya hapa,” amesisitiza.

Alipomuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw, Leno Mwageni amebakiza kiasi gani cha fedha katika sh. milioni 400 ambazo zililetwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo, Mkurugenzi huyo alijibu kwamba hakuna kiasi cha fedha kilichobakia.

Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao kwamba Mheshimiwa Rais John Magufuli anatambua wao hawana uwezo, na tena wanaugua na kuna watu ambao wanapoteza maisha kwa sababu hawawezi kufika kwenye tiba kwa wakati.

“Vituo vya afya vinajengwa kila mahali nchini ili wewe mwananchi usilipe nauli kwenda Iramba mjini au Singida mjini kutafuta tiba, bali upate vipimo vyote hapa hapa ulipo. Vipimo vya magonjwa yote vinapatikana hapa hapa.”

“Fedha hizi zikiletwa zinataka pajengwe maabara, chumba cha upasuaji mdogo na mkubwa, chumba cha huduma ya mama na mtoto, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mkuu wa kituo, lakini hapa Ndago fedha yetu imeharibika,” amesema.

Alipoenda kukagua chumba cha kuhifadhia maiti, Waziri Mkuu alikuta limewekwa mlango wa mbele tu na vyumba vingine vyote havina milango wala mabomba na masinki hayajakamilika tofauti na taarifa aliyopewa kwamba jengo hilo liko tayari.

“Mkurugenzi nimekuta wagonjwa wamelazwa katika baadhi ya vyumba na kazi haijakamilika. Huwezi kupanga vifaa wakati ujenzi unaoendelea ili kumdanganya Waziri Mkuu. Na wala hunidanganyi mimi bali unawadanganya wananchi.”

“Ninazo taarifa kwamba jana mlikesha kupanga vitu ndani. Nenda kaondoe vifaa vyote hadi ujenzi utakapokamilika ndipo madaktari warudi kuendelea na kazi. Serikali hii haiwezi kuvumilia vitu vya hovyo. Hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.Mapema, Mbunge wa jimbo hilo, Bw. Mwigulu Nchemba alimweleza Waziri Mkuu kwamba alichangia mifuko 400 ya saruji na wananchi wa kata hiyo walichangia mawe na ujenzi wa msingi.

Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa vituo vya afya. “Tunashukuru kwa sababu fedha hizi zimekuja kamili, na siyo kwa mafungu. Wananchi wamechangia nguvu zao na mimi mwenyewe nilitoa mifuko 400 ya saruji,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu awasaidie wananchi wa kata ya Ndago wapate barabara ya lami ya kutoka Singida-Sepuka-Ndago-Kizaga yenye urefu wa kilometa 76. “Hii ni tarafa kubwa kuliko zote na huku ndiko uzalishaji mkubwa uliko. Hii barabara imeshafanyiwa upembuzi yakinifu, kilio na furaha ya wana-Ndago ni barabara hii kuwekwa lami,” alisema.

TAKUKURU ICHUNGUZE WATUMISHI 48 IRAMBA KWA UPOTEVU WA FEDHA

$
0
0

*Asema ikithibitika ni kweli, lazima warudishe fedha hizo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda achunguze watumishi 48 waliojihusisha na upotevu wa fedha kwa njia za udanganyifu.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri hiyo.

Waziri Mkuu ametoa maeneo saba ambayo ametaka yafanyiwe uchunguzi wa kina ili kubaini upotevu huo. Eneo la kwanza ni upotevu wa makusanyo ya ndani kupitia mawakala wa ukusanyaji mapato (POS) ambapo mawakala wanaokusanya fedha wanashirikiana na watumishi wa Halmashauri na kuzitumia bila kuziingiza benki.

Kuna kundi la watumishi 10 wakiongozwa na mtu wa TEHAMA, wameshirikiana kupata password na fedha zikishakusanywa wanazitoa na kuzitumia bila kuzipelekea benki. Wamesahau kwamba malipo yalipoingizwa mara ya kwanza, data ilirekodiwa kwenye mfumo wa malipo na sisi tunaona ni kiasi gani kimekusanywa.”

Watumishi hao ni Salum Omari (Mtaalamu wa TEHAMA); Adam Mzengi (Mhasibu kahamishiwa Gairo); Rafaeli Nasari; Caroline Makundi (kahamishiwa Singida Manispaa), Edson S. Ally (Afisa Biashara); Martin Kimisho (Mhasibu Msaidizi); Prosper Banzi (Afisa Biashara); Hassan Ponda (Mhasibu kituo cha afya Ndago); Hafidh Ngayunda (Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya) na Muhidin Mohammed (Mweka Hazina wa Wilaya) ambaye tayari amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma hizo.

Kutokana na upotevu huo, Waziri Mkuu ameagiza Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya akae pembeni hadi uchunguzi wa TAKUKURU utakapokamilika.

Akibainisha mchezo mwingine uliochezwa na watumishi wa Halmashauri hiyo, Waziri Mkuu amesema kuna watumishi 38 ambao walilipwa kiasi cha sh milioni 46 ambazo zilikuwa sehemu ya sh. milioni 400 za kujenga vituo vya afya vya Ndago na Kinampanda wilayani humo.

“Hapa nina vocha zote za malipo walipeana fedha watu hawa akiwemo Mkurugenzi wao. Lakini ni kazi gani ambayo kundi lote hili lilikuwa likiisimamia na kustahili kupata malipo hayo? Kutoka makao makuu ya wilaya hadi Ndago au Kinampanda kuna umbali gani?” alihoji Waziri Mkuu.

“Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi, fuatilia wote waliohusika sababu majina tunayo, kama hawastahili kulipwa ni lazima warudishe fedha yetu. Hii ni sehemu ya sh. milioni 90 ambazo hazijulikani ziliko na zilikuja kujenga kituo cha afya. Fedha hizi zimekuja na maelekezo rasmi, ni kwa nini zilibadilishwa matumizi,” alihoji.

Waziri Mkuu alisema kuna fedha ya walimu sh. milioni 29 ambayo ilitumwa na TAMISEMI ili kulipa likizo zao lakini Mkurugenzi alitumia kulipia usafirishaji wa makontena ya vifaa vya tiba kutoka Sweden hadi Singida wakati mkataba wa malipo unasema Halmashauri ilipaswa kulipia kutoka bandari ya Tanga hadi Singida.

“Hii fedha ya walimu ya likizo nataka irudishwe mara moja. Pia kuna shilingi milioni 6.86 ambazo mmedai ni malipo ya kukomboa mizigo bandarini wakati vifaa hivyo vilipata msamaha wa kodi. Tena kuna sh. milioni 34 ambazo zililetwa kurekebisha Ikama za walimu lakini hadi leo hazijalipwa. “Kamanda wa TAKUKURU nataka uniambie nafasi ya Afisa Elimu ikoje kwenye suala hili,” alisema.

Pia alisema kuna fedha kujenga machinjio ya kisasa ambayo ililetwa lakini machinjio hayajakamilika hadi sasa. “Tumeleta sh. milioni 100 za machinjio lakini Afisa Mifugo anasema wametumi sh. milioni 20 tu, nataka sh. milioni 80 zimeenda wapi.”

Waziri Mkuu alisema kuna sh. 18,090,000 za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutoka vituo vya afya 13 ambazo zimetumika kusafirisha hayo makontena nayo pia irudishwe. “Hivi mnachangisha watu sh. 30,000 kwa ajili ya kupata dawa wakienda kutibiwa lakini leo hawana dawa kwa sababu mmezitumia ndivyo sivyo na wao hawana dawa kwenye vituo hivyo kwa sababu hamjazirejesha.”

“Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi kwenye fedha ya mikopo ya akinamama, vijana na wenye ulemavu ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri. Fedha hii haijatoka tangu mwaka 2017/2018 na 2018/2019.

WAZIRI MPINA ATANGAZA MAGEUZI USHIRIKA WAVUVI,VYAMA 20 KUANZISHWA DESEMBA MWAKA HUU

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kuzindua Ushirika wa Wavuvi Igombe jijini Mwanza, Kulia ni Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula. Kushoto ni Mwenyekiti wa ushirika huo, Paul Ngwegwe. Picha na Mpiga Wetu

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Ushirika wa Wavuvi katika Mwalo wa Igombe jijini Mwanza na kumuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha ifikapo Disemba 31 mwaka huu  kuwepo na vyama imara vya ushirika visivyopungua 20 kwenye maeneo yote nchini ambako shughuli za uvuvi zinafanyika ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya tano kuwainua wavuvi kutoka kwenye uvuvi wa kujikimu kwenda kwenye uwekezaji mkubwa utakaowezesha kubadilisha maisha yao na kukuza uchumi wa nchi.

Hatua hiyo ya Serikali inakuja baada wavuvi kudharauliwa kwa muda miaka mingi  kutokana na shughuli wanayoifanya ambapo  taasisi za fedha ziliwadharau kwamba shughuli zao hazikopesheki na wala hawawezi kupewa mikopo huku wachuuzi wa mazao ya uvuvi wakiwa ni matajiri wakubwa lakini wale wanaoingia majini kuvua wameendelea kuwa masikini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Igombe Limited Ilemela jijini Mwanza, Waziri Mpina amesema Serikali ya awamu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imekataa wavuvi na shughuli za uvuvi kudhauriwa tena ndio maana inatilia mkazo suala la ushirika na kuwaunganisha na taasisi za kifedha na kuanza kukopeshwa.

Hivyo Waziri Mpina akasisitiza kuwa sasa Wavuvi wanatoka kwenye kupuuzwa na kudhauliwa wanaingia kwenye kundi la kuheshimiwa na kupewa heshima inayostahili kulingana na shughuli yao ambayo Taifa inaitegemea kukuza uchumi na kuipatia nchi fedha za kigeni ambapo mauzo ya samaki nje ya nchi yamefikia shilingi bilioni 691 kutoka sh bilioni 379 mwaka 2018 na kulifanya zao la samaki kuongoza kwa kuipatia nchi fedha za kigeni.

Pia kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya kukuza sekta ya uvuvi na kuwaendeleza wavuvi uagizaji wa samaki kutoka nje ya nchi umeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka wastani wa  sh. Bilioni 56 mwaka 2017 hadi kufikia sh bilioni 17 mwaka 2019.

“Mwaka huu wa fedha hatutarajii kutumia hata senti moja ya kununua samaki kutoka kwa sababu samaki hao sasa mnavua ninyi na soko lote mnalihudumia hatuna sababu ya kuagiza tena samaki kutoka nje ya nchi, Sisi Wizara na wavuvi wangu tunaishukuru sana  Benki ya Posta kwa kuunga mkono jitihada za wizara hii na jitihada za wavuvi na kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwafungulia akaunti maalumu bila masharti yoyote”alisema Mpina.

Waziri Mpina alisema ushirika huo wa Igombe kwa sasa una mtaji wa shilingi milioni 20 ambazo zimetokana na mchango wa wanachama wenyewe sh milioni 7.5, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi imewachangia sh. milioni 10 na Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula amechangia sh.  milioni 2.5.

Waziri Mpina ameunga mkono mpango  wa ushirika huo wa kujenga kiwanda cha kutengeza barafu na kumuagiza Mratibu wa Dawati la Sekta ya Binafsi Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutengeza mkakati wa haraka na kwamba ifikapo Disemba 31 kiwanda cha barafu kizinduliwe rasmi ili uwe ushirika wa mfano wa wavuvi Tanzania. Pia Mpina amemuomba Mbunge wa Ilemela, Mabula aweke jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanda hicho Novemba mwaka huu kwani na yeye anamchango mkubwa katika kufanikisha uanzishwaji wa ushirika huo.

Waziri Mpina alisema sasa kuna jumla ya vyama 7 vya ushirika wa wavuvi ambavyo ni Igombe Mwanza, Ikumbaitale Chato, Kigangama Magu, Ihale Magu, Bukombe Fishing Corperative Society Sengerema, Zilangula Fishing Cooperative Sengerema, Umamiki Fishing Cooperative Society Sengerema.

“Kampeni ya ushirika sio maagizo ya Mpina ni maagizo ya Ilani ya Chama  cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ibara ya 27 (a-b) ambayo ilitaka Serikali kuhakikisha inaanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika “alisema Mpina.

Kuhusu mabadiliko ya sheria, Waziri Mpina alisema tayari Serikali imeruhusu matumizi ya leseni moja ya uvuvi kila maji na kuondoa ukomo sangara sentimita 85 sasa kuanzia sentimita 50 na kuendelea huku wavuvi wakiruhusiwa kuvua kwa kutumia nyavu za kuanzia nchi  sita na kuendelea kwa Ziwa Victoria.

Katibu wa Ushirika wa Igombe, Dunia Isomba alisema ushirika huo ulianza na wanachama 22 lakini sasa wamefikia 46 na walianza na mtaji sh. Milioni 7.5 na baadae Wizara ya Mifugo na Uvuvi inawachangia milioni 10 na Mbunge Dk Mabula milioni 2.5 ambapo kwa sasa wanakusudia  kuanzisha kiwanda cha barafu, kununua gari la kubeba samaki kwenda viwandani na kuanzisha duka la kuwa na zana  za  uvuvi zinazoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kuishukuru Serikali ya Rais Dk. Magufuli kwa namna ilivyojipambanua kuwasaidia na kuwainua wavuvi.

Mbunge wa Ilemela, Dk. Mabula mbali na kuchangia milioni 2.5 pia ameahidi kuchangia tofali zitazowezesha kuanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza barafu cha ushirika huo.

TCRA YAWAJENGEA UELEWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM KUHUSU USAJILI WA LAINI ZA SIMU KWA MFUMO WA ALAMA ZA VIDOLE.

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na watu wenye mahitaji maalumu,kuilia kwake ni Philipo Meli Mwenyekiti wa watu wasioona mkoa wa Arusha ,kushoto kwake ni Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wa kwanza mulia ni Katibu wa chama cha Viziwi Tanzania tawi la Arusha .Picha na Vero Ignatus.
MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona
Julius Felix Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini kanda ya Kaskazini TCRA ,wengine ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwaajili ya kuwajengea uelewa juu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.
Jan Kaaya ni Mhandisi Mwanadamizi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA).Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus
MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA akizungumza katika uzinduzi wa semina hiyo ya siku moja ya wadau wa mawasiliano ,kutoka makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutoona.Picha na Vero Ignatus.
Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wasiku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.Pcha na Vero Ignatus
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona .Picha na Vero Ignatus.
Mmoja wa wakalimani wa lugha ya aklama akisaidia ujumbe ufike kwa waandaaji wa semina ya watu wenye mahitaji maalum (TCRA).Picha na Vero Ignatus


Na.Vero Ignatus,Arusha .
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenyenye mahitaji maalumu, wakiwa katika makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutokuona.


Lengo haswa la mkutano huo ni kutoa uelewa kwa watu wenye mahitaji maalum, kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya mfumo wa alama za vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma za Mawasiliano


 Gabriel Daqqaro ni mkuu wa wilaya ya Arusha amesema kuwa semina hiyo itasaidia ,ukizingatia kwasasa kuna changamoto nyingi za mitandao japo kuwa  zipo faida zake kama vile kupashana habari,kuelimisha,kuburudisha na kukataza yale mambo mabaya katika jamii katika maendeleo yanayokwenda kwa kasi.


Amesema kuna makosa ya uhalifu wa kimtandao ,watu wasiowaaminifu wanaotuma jumbe za kulaghai wa wananchi,kwasababu hiyo serikali imeelekeza  laini zote za simu zisajiliwe kwa alama za vidole ,hivyo ameipongeza TCRA kwa kuona watu wenye ulemavu kuwa ni sehemu ya jamii.


“Watu hawa wenye mahitaji maalumu wananchwa mara nyingine kutokana na baadhi ya watu kudhania kwa mawazo yao hasi kwamba ulemavu ni hasara,niseme hujafa huijaumbika,nisisitize hebu tubebane tonane tupo sawa.


Daqqaro amesema serikali ya awamu ya tano imeona hilo, ndipo ikaona watu wenye mahitaji maalum ,walikuwa hawajajumuishwa katika kunufaika na zile 10% za mapato ya ndani ,kuanzia mwaka 2018 imetoa maelekezo kwamba na wenyewe ni miongoni mwa kundi linalotakiwa kunufaika ,ambapo  halmashauri zote zimeelekezwa hivyo .


Amesema ni muhimu kusajili line za simu ili kuepusha makosa ya uhalifu wa kimtandao, matapeli wanao tuma jumbne

 Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha amesema serikali serikali iliagiza kuwa 10%za mapato nao watu wenye ulemavu wanufaikike na mapato ya ndani iliagiza laini zote za simu zisajiliwe kwa mfumo wa alama za vidole hivyo watu wenye uhitaji maalumu nao ni sehemu ya jamii.


MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini(TCRA) amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kwasababu wao nao ni sehemu ya jamii ,na pia wanatumia huduma ya mawasiliano hivyo .wanahaki ya kupata taarifa mbalimbali,mafunzo.


“Tunafahamu kwa namna walivyo wenzetu wana changamoto mbalimbali yumkini kuna wengine hawawezi kupata taarifa kwa wakati ,lakini kwa wenzetu wa kwa wasiosikia taarifa kwa taarifa zinazopelekwa kwa jamii kwa njia ya  radio,televisheni,asiyeona hawezi kuona kwenye televisheni,halikadhalika asiyesikia vileviel


TCRA imesema kwa kuona umuhimu wa kundi hilo wameamua kuwashirikisha Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)ili waweze kutoa huduma kwa watu hao wenye mahitaji maalum


Mkuu huyo wa  kanda ya amesema Swala la usiri na faragha kwa watu wasioona bado limekuwa ni tatizo ,mawasiliano yao yanaweza kutatuliwa tu endapo kuna vifaa maalumu ambavyo wanaweza kuvitumia zikiwemo simu za mkononi ,pale mtu anaposoma ujumbe aweze kusikia sauti ujumbe unasemaje.


''Ila mamlaka ya mawasiliano tunajitahidi kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwasaidia ,kwa wenzetu wasioona tunawapa taarifa mbalimbali kupitia vitabu ambavyo vimechapiushwa kwa zile alama zao maalum.''


Ameainisha kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kujisajili ni kwani watakaposajili kutumia alama za vidole taarifa zao zinafahamika ,sambamba na kuimarusha usalama wanapotumia mawasiliano.


Ametoa wito kwa jamii kulitilia uzito swala hili la kusajili laini,na kwa wale ambao hawajapata kitambulisho cha NIDA,Mamlaka husika itawasaidia kupata namba zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo tayari kwaajili ya kuwasaidi ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha taifa.



Philipo Meli ni mwenyekiti wa wasioona mkoani Arusha amesema wanaishukuru TCRA kwa kuwathamini na kuwapatia semina hiyo ya kuwajengea utaalamu na kuwapatia vitabu vya nykta nundu kwaajili ya kujisomea na kupata uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo ya mawasiliano.

Amesema katika mawasiliano watu wasioona changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.

"Changamoto kubwa mtu anakutumia ujumbe hata kama unataka uwe wa siri,inashindikana mpaka utafute mtu mwaninifu aweze kukusomea ujumbe wako,hiyo ndiyo changamoto inayotupata sisi watu tusioona.''Alisema Philipo.


TOURISM SECTOR VITAL FOR EAC – EALA SAYS, AS IT CALLS FOR EMBRACE OF SINGLE TOURISM VISA

$
0
0
Speaker of EALA, Rt Hon Ngoga K. martin and the Clerks at table, Charles Kadonya (left) and Victor Manzi (right) pay attention to the proceedings this morning.
A section of the Members including the EAC Ministers (front row).
Hon Dr Woda Jeremiah Odok address the Assembly.


****************************

East African Legislative Assembly, Arusha, October 3rd 2019: Despite the significant contribution of the tourism sector in region’s economic growth, provision of employment and poverty reduction, certain overriding challenges that include sector underfunding, insecurity, lack of harmonized policies and laws, among others, need to be speedily addressed, the East African Legislative Assembly has said.

A report of the Assembly on the Oversight activity on the Performance of the Tourism Sector in the region, wants the EAC to fastrack the conclusion of the EAC Protocol on Tourism and Wildlife Management, as well as in strengthening a pool of EAC Classification Assessors to ensure efficiency and effectiveness in classification of tourism establishment.

The Assembly is also reiterating creation of a well-coordinated and digitized information exchange hub for the advancement of joint tourist visa mechanism in a bid to attract tourists in the region. Hon Mary Mugyenyi who presented the report to the House further said it was necessary for the Partner States to harmonise their national laws on tourism and related sectors. The EAC Council of Ministers is further urged to follow up with the Republics of Burundi and South Sudan and the United Republic of Tanzania to join the EAC Single Tourist Visa.

According to the Report, EAC tourism arrivals have increased from 3.5 million persons in 2006 to 5.7 million persons in 2017. However, this is still substantially low given that it represents only 8.6% of the Africa market share and 0.3% of the global market share. Tourism contributed to the Gross Domestic Product of the EAC Partner States by an average of 8.8% in 2017. The percentage contribution was higher than the average in Rwanda (12.7%), Kenya (9.7%) and Tanzania (9.0%). Tourism contributes an average of 18.8% to EAC total exports, although the percentage contribution was higher, in Rwanda (30.5%) and Tanzania (26%).

In the Partner States, the report makes interesting findings – that include a number of achievements and challenges. In Burundi, the report states the country has 126 tourist sites of which 57% are tangible cultural heritage aspects and 32% are natural heritage aspects. The weather is deemed as favorable while the culture is rich. The country further portrays rich African cuisine and culinary culture. Areas to be enhanced in the tourism sector include, development of infrastructure in all provinces; re-classification of hotel and categorization of accommodation in Burundi. In Kenya, the country has instituted a number of strategies that include development of tourism policies to support expansion of the tourism sector and a provision of charter incentives to enhance travel have been instituted. 

The country’s major activities include holiday travel (68%), business travel (18%) and transit (14%). Tourism sector registered improved performance in 2018, mainly attributed to growth of aviation, investors’ confidence, withdrawal of travel advisories, visits by foreign dignitaries and revitalized marketing efforts. The challenges for the Republic of Kenya include globalization which is leading to creation of uniform standards and protocols and the heavy taxation of the sector among others.

The Republic of South Sudan on its part, is endowed with a unique and diverse tourist attraction including the massive wildlife migration at Boma and Badigilo National Parks, considered second to the annual Serengeti-Maasai Mara animal migration. The report cites challenges including; infrastructure, insecurity caused by political instability, poverty and unemployment; inadequacy of data and research and lack of relevant policies and laws to regulate the sector.

The Tourism industry is a strategic priority for Rwanda and has been fundamental in the transformation and modernization of the national economy. Tourism continues to be a leading foreign exchange earner since 2007. The tourist attractions in Rwanda include wildlife protected areas, Akagera national park, Nyungwe national park and various reserves and sanctuaries, lakes, rivers and swamps. Notable challenges include over-reliance and dependency on the gorilla product as a major source of tourism revenue and the need for enhanced marketing as a wildlife, eco-tourism, cultural and conference destination.

Republic of Uganda, the report says, has branded itself as “Gifted by Nature” with many tourist attractions including wildlife, nature, geography, culture, heritage and good weather all the year around. Tourists sites in Uganda, include the source of the Nile, the Mount Rwenzori, Mount Elgon, Mugahinga, and Kigulu hills. The Equator, Bishop Hannington site, hot springs, handicraft and souvenir development, marine tourism and sport tourism are also major tourist attractions.

Uganda witnessed a 7.4% increase in international tourist arrivals in 2018, with the numbers growing from 1,402,409 persons in 2017 to 1,506,669 persons in 2018. Direct revenue from international tourism rose from US$ 1.453 billion in 2017 to US$1.6 billion in 2018. The challenges that affect tourist sector in Uganda include weak capacity in terms of instructional infrastructure for training manpower and human resource and inadequate funding.

At debate time, Hon Dr Abdulla Makame said there was need to consolidate the tourism industry in order to spur revenue, saying the sector would promote the region and create direct and indirect employment. The legislator called for the speedy conclusion of the Protocol on Tourism and Wildlife. Hon Leontine Nzeyimana, said tourism was a major revenue earner for the region. Hon Fatuma Ndangiza said with innovation and focus, the region can truly benefit from the sector.

Hon Abdikadir Aden rallied for the implementation of the single tourism visa saying a mechanism for revenue sharing was long overdue. The legislator rallied for enhancement of local tourism saying the region needs to make it easy for East Africans to freely enjoy the tourist attractions. Hon Kennedy Mukulia said there was need to revive the East African Airlines to tap the revenue from the tourism sector. 

The Member said security was paramount for the region and called on authorities to be vigilant and ensure tourists coming in to the region abide with existing laws and regulations. Hon Dennis Namaara said intra-competition amongst the Partner States led to situation where the region loses comparative advantage through marketing.



Others who supported the report include Hon Pierre Celestin Rwigema, Hon Josephine Lemoyan, Hon Dr Woda Jeremiah, Hon Fatuma Ibrahim, Hon Jean Marie Muhirwa, Hon Marie Claire Burikukiye, Hon Dr Ngwaru Maghembe, Hon Oda Gasinzigwa, Hon Rose Akol and Hon Dr Damas Ndumbaro, Deputy Minister, Ministry of Foreign Affairs and EAC, United Republic of Tanzania.

Cabinet Secretary, Ministry of EAC, Kenya, Hon Adan Mohammed, thanked the Committee for an elaborate report and said the region needed to focus more on connectivity to spur tourism, convenience. The Minister said natural endowments were necessary – but said in other places, products can be created and marketed to spur tourism. He called for more focus on local and domestic tourism. In Kenya, the Cabinet Secretary said bed occupancy at the Coast region were significantly lower until government and private sector deliberately put efforts to market the coastline.

The Chair of Council of Ministers, Hon Olivier Nduhungirehe, said Council of Ministers will duly implement the report. He informed the House that Council of Ministers would engage the Sectoral Council on Tourism and Wildlife to address the emanating challenges. Similarly, he said all citizens of the region would as necessitated by the Community, pay same rates for hotels and national parks as nationals of the Partner States.

MAKAMISHNA WANNE WA JESHI LA POLISI WAKIONGONZWA NA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WATEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME MTO RUFIJI

$
0
0


Mhandisi Manda akitoa maelekezo juu ya Ujenzi mradi wa
uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji kulia kwake ni Kamishna wa
Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo,
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz
wa kwanza kutoka kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo
CP Liberatus Sabas (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Makamishna wa Polisi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, katikati na kulia kwake ni
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas,
Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Maabara na Uchunguzi wa
Kisayansi CP Shaban hiki na kushoto kwa CP Boaz ni Kamishna
wa Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo
wakiwa katika picha ya pamoja na Wahandisi wa Ujenzi wa mradi
wa Umeme Rufiji baada ya kufanya ziara ya siku moja katika
mradi huo.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz,
akiongoza kikao cha Maafisa na Wahandisi wa Ujenzi wa Mradi
Mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani
baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo. 

NDITIYE: WANANCHI MKIWASILIANA SERIKALI TUNAPATA HELA

$
0
0
Prisca Ulomi, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchikusajili laini za simu kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa chaNIDA na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoanihumo.

Wakati akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwamalengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma zamawasiliano zinakuwa zenye ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivumzuri wa mawasiliano kwa kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane.

“Serikali tunataka wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapatoambayo yanaendesha shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye.Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida yamawasiliano kwenye wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato yaSerikali hivyo inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wamajukumu ya kila siku ya Serikali.

“tunashida ya mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi,” amefafanua Mkupasi.

Nditiye amemweleza kuwa amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana wanapenda mtandao wa Vodacom.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Agostino Maselle amekiri kuwa wanapata huduma zamawasiliano za mitandao mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na Isesya.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza shida ya mtandao huo na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika kusafiri kwenda Ushirombo.

Akijibu malalamiko ya wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato.

Nditiye amefanunua kuwa sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni mojainatosha na sio lazima kuwa na mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA wafuatilie na kusimamia jambo hilo.

Katika ziara hiyo, Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na watoa huduma wa kampuni ya Vodacom
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita.
Mkuu wa uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) kuhusu mnara wa Ilolangulu wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano Mbogwe mkoani Geita.
Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Agostino Masele akimuonesha Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye vijiji ambavyo havina
mawasiliano ya uhakika wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGA MAFUNZO YA KIJESHI YA WATUMISHI MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO – ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride la heshima la askari wa jeshi USU alipokwenda kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi cheti cha kuhitimu mmoja wa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro aliyepatiwa mafunzo ya Jeshi USU wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.
Askari wa Jeshi USU waliohitimu mafunzo wakionesha uwezo wao wa kufuangua silaha na kuifunga ndani ya muda mfupi wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA. Askari wa Jeshi USU kikosi maalum wakionesha uwezo wao wa kukabiliana na majangili wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.





Askari wa Jeshi USU waliohitimu mafunzo wakipita kwa ukakamavu mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.

PICHA – Aron Msigwa –WMU, Arusha.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images