Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Mwili wa Dkt. Willium Mgimwa Wawasili Kutoka Nchini Afrika Kusini.

$
0
0

Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.
Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini
Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.

                                                            Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

JAHAZI KUPELEKA NYIMBO MPYA MORO MWISHO WA MWEZI HUU

$
0
0
KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo.

Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex.

Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla.


Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.

UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA SHIGONGO

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Hiki ndicho ninachokifahamu mimi ndugu yenu.
Maisha ni vita, maisha ni mapambano na mtindo pekee wa kukusogeza mbele ni kupigana! Hata uwe mwema kiasi gani utakuwa na maadui, Yesu alikuwa nao, Mtume Muhammad alikuwa nao, Mandela alikuwa nao na hata Mahatma Gandhi alikuwa nao.
Hata ufanyeje maadui watakuwepo tu, utapingwa, utapuuzwa, hivyo basi kamwe usijaribu kuwafurahisha watu, eti unafanya vitu ili watu wakupende, utapoteza muda wako bure.
Kumbuka kuwafurahisha watu ndio barabara kuelekea kwenye umasikini, siku zote fanya kitu ambacho moyo wako unaridhishwa nacho. Watu watakucheka, watakutukana matusi yote lakini mwisho wa siku kama ukiendelea mbele hao ndio watakuja kukupa mkono wa hongera pale utakapoibuka mshindi.
USHUHUDA WANGU; Kwa miaka yote kumi na tano ambayo nimeishi na kufanya kazi Dar es Salaam, nimetukanwa sana, nimeitwa majina yote mabaya, nimehukumiwa sana. Badala ya kuwachukia walionitukana na wanaonitukana (hivi sasa wakisoma ) ambacho mimi hufanya ni kuziba masikio na kuyachukua matusi yao kama hamasa kisha kusonga mbele.
Najua wapo watakaolia pindi nitakapokufa, lakini pia wapo watakaofurahi na kufanya sherehe kwamba nimekufa, cha muhimu kwangu ni urithi nitakaouacha hapa duniani baada ya mimi kuondoka, si urithi wa mali bali idadi ya watu ambao Mungu atasikia sauti zao wakisema "Mtu yule alikuwa mwenye dhambi lakini alisaidia kutupa tumaini na maisha yetu yakabadilika." Hao wakiwa wengi itanitosha, yawezekana sauti zao zitamfanya Mungu aniangalie kwa jicho la huruma na kusema “KARIBU MWANANGU.”
Nawatakia mwaka mpya wenye mafanikio, kumbukeni katika nchi hii ukifanya kazi kwa nguvu na ukiwa na malengo nafasi ya kufanikiwa ipo bila kujali historia ya maisha yako. 
NAMUOMBA MUNGU MWAKA HUU 
UWE WA MPENYO KWA KILA MMOJA WETU.
Asanteni Mungu awabariki
Eric Shigongo James
Mkurungenzi Global Publishers Ltd

WAZEE WA FEVA HAMJALIONA HILI KWENYE BARABARA YA MANDELA JIJINI DAR ES SALAAM?

$
0
0
 Magari makubwa yakiwa yamepaki kwenye barabara ya Mandela jijini Dar es salaam kuanzia TOT  mpaka Mwananchi ambapo imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hii.
Hii imekuwa kero kwa watu wengi wanaoitumia barabara ya Mandela kwani magari haya yachukua nafasi kubwa ya barabara
Pia kuna magari mengine yamepaki kwenye service roads 

CHANZO: PAMOJA BLOG

MAALIM SEIF ATEMBELEA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
Na Hassan Hamad, OMKR. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Sharif Hamad, amesema serikali imepata moyo kuona taasisi, mashirika na wananchi jinsi walivyojitokeza katika maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Amesema kujitokeza kwao kwa wingi kunaashiria jinsi wananchi walivyohamasika kuonyesha na kutangaza huduma zao kwa wengine, kwa lengo la kuzitambulisha na kutafuta soko ndani na nje ya nchi. 
Mhe. Maalim Seif ameeleza hayo baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi yaliyoko Beit- el- Raas, mjini Zanzibar. 
Amesema wananchi wameonesha kuyapenda maonyesho hayo ya bidhaa na huduma, na kwamba ni vyema yakaandaliwa kila baada ya muda, bila ya kusubiri miaka 50 mengine. 
Maonyesho hayo ya kwanza ya aina yake kufanyika Zanzibar, yamekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni, yanazishirikisha taasisi mbali mbali zikiwemo taasisi binafsi, mashirika ya umma na wajasiriamali. 
Katika ziara hiyo Mhe. Maalim Seif ametembelea mabanda ya maonesho kwa taasisi tofauti zikiwemo Jumuiya ya Wafanyabiashara, Chuo Cha usimamizi wa fedha, mafunzo ya amali, polisi na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 Askari wa kikosi cha zimamoto na uokozi Zanzibar, akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea banda la kikosi hicho kwenye maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Beit-el-Raas.
 Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Rashid Omar, akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Beit-el-Raas.
Mwanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha Zanzibar, akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonyesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Beit-el-Raas.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia bidhaa za wajasiriamali, alipotembelea mabanda ya maonyesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Beit-el-Raas.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa kwenye banda la Ofisi ya Makamu wa Rais, kuangalia huduma za Ofisi hiyo, alipotembelea mabanda ya maonyesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Beit-el-Raas. 
Picha na Salmin Said, OMKR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. WILLIAM MGIMWA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
Baadhi ya Mawaziri na wabunge waliofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, leo.Picha na OMR

News alert: Moto wateketeza Nyumba 14 katika Kijiji cha Shumba Mjini Wilaya ya Micheweni, Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameiagiza Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kufanya tathmini mara moja nyumba zote zilizoathirika kutokana na moto mkubwa uliokikumba Kijiji cha Shumba Mjini leo majira ya saa 5.00 za asubuhi. 
Nyumba zipatazo 14 zikiwa na wakaazi 100 zimeathirika vibaya kutokana na moto huo na nyengine 24 kuezuliwa mapaa yake kwa hofu ya kuathirika na moto huo ambao hadi sasa kwa mujibu wa taarifa za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shehani Mohamed Shehani kwamba chanzo chake bado hakijafahamika. Uchunguzi wa jeshi la polisi pamoja na vikosi vyengine vya ulinzi ukiendelea.
Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar akiwa kisiwani Pemba kwa shughuli mbali mbali za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar alitoa agizo hilo muda mfupi baada ya kuwafariji wananchi wa Kijiji cha Shumba Mjini kutokana na maafa waliyoyapata ya janga la moto. 
Akiwapa pole wananchi hao 100 waliohifadhiwa kwenye madrasa mmoja Kijijini humo na baadaye kupelekwa Skuli ya Kijiji hicho Balozi Seif aliwataka kuwa na subra katika kipindi hichi cha mitihani na Serikali inajipanga kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao. 
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaandaa kikao maalum cha dharura keshokutwa jumatatu ili kulijadili suala hili na kuona jinsi itakavyoweza kukusanya nguvu za kuwasaidia wananchi walioathirika na janga hili. 
“ Wakati nimeshamuagiza Mkuu wenu wa Mkoa kufanya tathmini ya janga hili mimi kama mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar nitawajibika kuitisha kikao cha dharuura Jumatatu kulitafakari suala hilo “. Alisema Balozi Seif. 
Alisisitiza kwamba ni wajibu wa Serikali Kuu kutafuta mbinu na utaratibu utakaoweza kutoa fursa nzuri ya kujaribu kusaidiana Wananchi walioathirika na Maafa hayo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru wananachi na baadhi ya Taasisi zilizojitokeza kwa njia mbali mbali kusaidia wananchi hao ikiwemo vyakula, vifaa na baadhi ya huduma muhimu kama nguo kwa wale wananchi 100 waliokuwa wakiishi kwenye zile nyumba 14 zilizounguwa na kuteketeza vitu mbali mbali. 
Aidha Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Wilaya ya Micheweni pamoja na Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa hatua iliyochukuwa ya kuandaa mazingira ya kuwahifadhi wale wananachi watakaokosa hifadhi na kuwapeleka katika Skuli ya Kijiji hicho cha Shumba Mjini. 
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananci wa Kijiji cha Shumba Mjini Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Mh. Subeit Juma Khamis amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa hatua aliyochukuwa ya kuwafariji wananchi hao katika muda mfupi baada ya kutokea tukio hilo, Mh. Subeit alimuelezea Balozi Seif kuwa ni kiongozi mwenye moyo unaomuelekeza kujali wananchi wake. 
Moto huo mkubwa uliokuwa ukivuma kutokana na upepo mkali licha ya taarifa za awali za kutotambulikana chanzo chake ulianzia kwenye Nyumba ya Bwana Masoud Ali Khamis na naadhi ya wananchi walisikika wakisema chanzo chake kimesababishwa na watoto waliokuwa wakijiandaa kupika mlo wa mchana.
 Moja kati ya nyumba 14 katika Kijiji cha Shumba Mjini Wilaya ya Micheweni zilizotoathirika kwa moto mkubwa ulitokea majira ya saa 5.00 asubuhi Jumapili hii huku wakaazi wake wakichanganyikiwa kutokana na maafa hayo.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Afande Shehani Mohamed Shehani akitoa tathmini ya awali ya uchunguzi wa moto uliotokea Shumba Mjini mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyefika kijijini hapo kuwapa pole wananchi walioathirika na maafa hayo.Kulia ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Mh. Subeit Juma Khamis na kushotoni kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini pemba Mh. Dadi Faki Dadi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa.
 Baadhi ya wananchi 100 ambao nyumba zao 14 zimeathirika na vibaya na moto katika Kijiji cha Shumba Mjini wakipata hifadhi kwenye madrasa moja Kijijini hapo.
Moja kati ya nyumba 14 zilizoathirika na moto katika kijiji cha Shumba Mjini ambapo wakaazi wake wakiwa wamechanganyikiwa kutokana na janga hilo. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ. 

BURIANI NDUGU YANGU TONNY BARETTO

$
0
0

Familia, ndugu, jamaa na marafiki asubuhi leo wamememiminika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam kutoa heshima zamwisho kwa  mwili wa Tonny Baretto. kabla ya kuelekea mazikoni katika Kijitonyama Crematorium, jijini Dar es salaam, ambako mwili wake utachomwa moto kama alivyousia kabla ya kuaga dunia.

 Marehemu alikuwa ni mmoja wa wanataaluma wa habari wakongwe aliyewahi kufanya kazi Tanzania Standard Newspapers (TSN) IPP Media na sehemu mbalimbali katika vitengo vya matangazo. Marehemu Baretto alifariki ghafla December 31, 2013 na kustua kila mtu.

Globu ya Jamii inaitakia familia ya Baretto Rambirambi na kwamba wakati huu tunasherehekea nao maisha ya Tonny ambaye alikuwa rafiki wa kila mtu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AFUNGUA HOSPITALI YA KMKM KIBWENI, ZANZIBAR LEO

$
0
0
 : Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo Desemba 4, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo Desemba 4, 2014 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kufungua rasmi Hospitali ya KMKIM Kibweni mjini Zanzibar leo  

Askari wakakamavu wa kike wa KMKM wakiwa wamesimama kumlaki Rais Jakaya Kikwete alipowasili kufungua rasmi Hospitali ya KMKM Kibweni leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Salamu za rambirambi toka ubalozi wa Tanzaniia marekani

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Bryan Adams anakwambia 'Please Forgive Me'

Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi chapata viongozi wapya,Steve Nyerere aibuka Mwenyekiti.

$
0
0
Pichani ni Uongozi wa juu wa  Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven Mengere a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka hazina Mkuu, Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa hapo jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana kwenye viwanja vya Lidaz club,jijini Dar.
Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa Uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na  kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama hicho
Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha inaendelea kukua siku hadi siku.
Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.

NEWZ ALERT:MELI YA KILIMANJARO II YAKUMBWA NA DHORUBA,WATU 10 WADAIWA KUJIRUSHA BAHARINI

$
0
0
 DHORUBA:MELI YA KILIMANJARO II,ILIYOKUWA IKITOKA PEMBA KWENDA UNGUJA ILIPATWA NA DHORUBA MAPEMA LEO ENEO LA NUNGWI BAADA YA INJINI KUZIMA,HAKUNA ALIYEKUFA.INAAMINIKA ABIRIA WAPATAO 10 WALIPANIKI NA KUJIRUSHA BAHARINI ILI KUJINUSURU NA WANAENDELEA KUTAFUTWA.

 HABARI ZAIDI ZITAENDELEA KULETWA HAPA JAMVINI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIINGIA.

MSIBA DMV NA TANZANIA

$
0
0
Jumuiya ya watanzania Washington Dc inasikitika kutangaza kifo mpendwa wao Zainab Buzohera Dullah au maarufu kwa jina la Zay B aliyefariki dunia saa mbili za usiku wa Jumamosi Januari 4 ,2014. Kwa mujibu wa mume wa marehemu  Zainab alikutwa na umauti huko Doctors Community hospital Lanham Maryland baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

Msiba upo  nyumbani kwa marehemu  5030 57th Ave Apt 303 Bladensburg Md 20710. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania inaendelea. Harambee itafanyika Jumapili January 5, 2014 saa 10 jioni katika anuani ifuatayo:5401 Annapolis Rd Bladensburg Md 20710.
Gharama ni $15, 000.

Tunakuomba tuma mchango wako kwenda CITI BANK. ATT: Ms. Ngalu Buzohera AC no.50070000.
Routing 9106834936
Shukran.

HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA

$
0
0
 Meneja wa kituo cha  Redio Nuru Fm, Victor Chakudika cha mkoani Iringa akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe moja ya viti vinavyotumiwa na walemavu , makabidhiano hayo yalifanyika katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki.'
 baadhi ya viti vya walemavu na fimbo za kutembelea vilivyotolewa na redio  Nuru Fm ya mkoani Iringa kwa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa(picha na Denis Mlowe).
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Nuru FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa
=========  =======  ==========
HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA 
Na Denis Mlowe,Iringa

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Children care (IDYDC) kwa kushirikiana na Redio Nuru Fm ya mjini Iringa wametoa misaada ya viti 5 vya kubebea wagonjwa na fimbo 20 za kutembelea kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.5

Sambamba na kuisadia hospitali hiyo radio hiyo ilivisaidia vituo vya watoto ya yatima vilivyoko mkoani hapa vya Huruma Center,Sabasaba Center na kituo cha wazee Iringa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya usafi, sabuni na mipira kwa watoto hao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wakati wakitimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa kituo hicho, meneja wa radio Victor Chakudika,aliitaka jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii inayoishi katika mazingira magumu  kwa lengo la kuisaidia serikali majukumu ambayo wadau wenye uwezo wanaweza kuyatatua.

Alisema lengo la redio kuwa jirani na jamii inayowahudumia katika kuwapatia matangazo yao ya kila siku hivyo misaada iliyotolewa ni kurudisha faida kwa jamii hiyo na itakuwa inafanyika kila mwaka kwa kutoa misaada kwa wanaohitaji hasa kwa wanaoishi katika  mazingira magumu na vituo mbalimbli vya afya vilivyoko mkoani hapa.

Chakudika alisema radio hiyo inatambua umuhimu wa kuchangia huduma za afya, kwani bila wananchi husika kutokuwa na afya njema ina maana hata maendeleo hayatakuwepo hivyo ni wajibu wao kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha sekta ya afya inafanya kazi ipasavyo na kuwahudumia watu wote kwa usawa.

Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Rustica Tung’ombe kwa niaba ya Mganga mkuu aliishukuru radio hiyo kwa kujali na kuthamini maisha ya Watanzania, kwa kuamini kuwa mchango huo si tu ni kusaidia shughuli za hospitali bali pia utasaidia kuongeza viti katika hospitali hiyo na kuwasaidia wagonjwa walemavu  katika kufanya mazoezi pindi wanapohitaji huduma ya vifaa hivyo.

Alisema kushirikiana kujenga jamii ya Iringa ni jukumu la kila mwananchi hivyo vifaa vilivyoyolewa vitakuwa faida kwa kila mwanajamii na kuwataka kuendelea kutoa misaada katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

WAZIRI MKUU PINDA AENDE NYUMBANI KWA MAREHEMU MGIMWA KUKAGUA MAANDALIZI YA MAZISHI NA KUWAPA POLE WAFIWA

$
0
0
 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Bibi Jane Katingo, Mama Mzazi wa Aliekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu huyo katika kijiji cha Magunga, Iringa  kutoa pole na kuangalia maandalizi ya mazishi  
 Waziri mkuu, Mizengo  Pinda  akizungumza na   jamaa wa karibu wa aliyekuwa waziri wa Fedha, Dr. WilliamMgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu katika kijiiji cha Magunga, Iringa kuwapa pole  wafiwa  na kukagua maadalizi ya  mazishi 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwafariji  wanafamilia wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha  Magungua, Iringa kuwapa pole na kukagua maandalizi ya mazishi  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MKUU WA MKOA WA DODOMA AWASISITIZA WALEMAVU KUANZISHA MIRADI YA UFUGAJI NYUKI KUPATA KIPATO CHA KUENDESHEA SHUGHULI ZA CHAMA CHAO NA KUJIKIMU

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasisitiza wanajumbe wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki ili kujiongezea kipato wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.Kuanzisha.
 Katibu wa chama  cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma Ndg. John Mlabu akielezea changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu mkoani Dodoma wakati akiwasilisha risala ya chama hicho kwa Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (watatu) wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma.
 Baadhi ya wanachama wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma wakisikiliza salamu za mkuu wa mkoa Dodoma (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma.
 Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi na wanachama wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dodoma mud mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.
 Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa Dodoma  Dr. Rehema Nchimbi ( wapili kutoka kushoto waliochuchumaa) na wajnachama wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.
 ===========  =======  =========
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi ameziagiza wilaya zote za mkoa wa Dodoma kuhakikisha zinatenga ardhi kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kusisitiza kuwa ardhi hiyo ni lazima iipimwe na kutolewa hatimiliki. Aidha ametaka ardhi hiyo itakayotengwa kwenye kila wilaya itumike kujengea ofisi za chama cha walemavu Tanzania Ngazi za wilaya na kufanyia miradi ya uzalishaji illi kujipatia kipato.
Vilevile Dr. Nchimbi alitoa Rai kwa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanaanzisha miradi ya ufugaji nyuki ambayo wataifanyia kwenye ardhi watakazopatiwa na wilaya.

Dr. Nchimbi aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa CHAWATA mkoa wa Dodoma ambapo aliwatia moyo walemavu kwa kuwaeleza kuwa miradi ya ufugaji nyuki katika mkoa wa Dodoma imeonesha kufanya vizuri na soko zuri lipo ndani na nje ya Nchi. Aidha, Alieleza kuwa ufugaji nyuki hauhitaji fedha nyingi na wala haumuhitaji mtu kwenda kushinda kwenye mradi kila siku akifanya kazi badala yake nyuki wenyewe ndio wanafanya kazi ya uzalishaji, hivyo mradi huu wa ufugaji nyuki utakuwa wa manufaa sana kwa watu wenye ulemavu.

Aliahidi serikali kutoa msaada wa usimamizi na utaalamu katika miradi hiyo ya nyuki ambapo ameagiza maafisa ustawi wa jamii mkoa na wilaya kusimamia miradi itakayoanzishwa na maafisa nyuki wa wilaya wahakikishe wanahudumia miradi hiyo upande wa utaalamu na amezitaka halmashauri za wilaya wahakikishe wanaweka mkundombinu ya usimamizi ikiwa ni pamoja na kugharamia gharama za wasimamizi wa hiyo miradi.Hiyo

Dr. Nchimbi alimaliza kwa kuwaasa CHAWATA kuwa mapato ya miradi hiyo ya nyuki yatumike kugharamia gharama za uendeshaji wa shughuli za CHAWATA ili walemavu waendeshe shughuli zao bila kutegemea kuomba misaada, vilevile mapato hayo yanaweza kutumika miradi mingine zaidi ya uzalishaji na hivyo kuwanyanua walemavu mkoaniDodoma.

Nae katibu wa CHAWATA mkoa wa Dodoma Ndg. John Mlabu akiwasilisha taarifa ya chama chake Ameeleza kuwa wanakumbana na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu vyumba vya ofisi za wilayani, halmashauri nyingi hazitengi bajeti kwa ajili ya walemavu,  walemavu kutotengewa maeneo ya biashara kwenye maeneo yanayoainishwa kufanyia biashara na gharama za visaidizi mwendo (magongo, wheelchairs na tricycle) kuwa juu.

Nyingine ni bei kubwa za viwanja vinavyouzwa na mamlaka ya uendelezaji makao makuu CDA ambapo walemavu hawawezi kuzimudu na vilevile majengo mengi hasa maghorofa na baadhi ya ofisi nyeti hayajazingatia miundombinu ya watumiaji walemavu.

(HABARI NA PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA - OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA)

MWENYEKITI WA BONGO MUVI STEVE NYERERE AWEKA WAZI MIKAKATI YAKE YA KAZI

EAUSEBIO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Inline images 1
mwanasoka Eusebio, ambaye alikuwa mfungaji bora katika Kombe la Dunia mwaka 1966, amefariki dunia akiwa na  umri wa miaka 71 kutokana na matatizo ya moyo
Akiwa kazaliwa nchini  Msumbiji mwaka 1942 wakati ilikuwa bado koloni ya Ureno, Eusebio da Silva Ferreira amechezea timu ya Taifa ya Ureno  mara 64 na kuifungia mabao 41.

RAIS KIKWETE APOKEA MATEMBEZI YA UVCCM ZANZIBAR LEO

$
0
0
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua Brass Band ya  Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014. 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wana UVCCM baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014.PICHA NA IKULU
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Mwenyekiwa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar  Dkt Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine waki imba wimbo wa mashujaa wakati wa  ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images