Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Malipo hewa yarudiwa Hai

$
0
0
AGIZO la Rais Magufuli la kutaka kurejeshwa kwa fedha za Chuo cha Ualimu cha Mongere kilichopo wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro cha kiasi  shilingi million 76 .9 zilizo tafunwa na  aliyekua Mhasibu wa Chuo Cha uwalimu Sarafina Mbwambo na Melkizedek Mchau karani Wa Miamala Wa ELCT ND Sacco's Zimezaa Matunda .  

Watuhumiwa hao wameanza kurejesha  fedha kiasi cha Shilingi Million  54 .8 kati ya fedha kiasi cha shilingi Million 76.9 walio zitumia kupitia  Miamala hewa.

Akipokea Malipo hayo Mara baada ya kutoa wiki mbili fedha hizo kurejeshwa katika Account ya Chuo, Mkuu Wa Wilaya Lengai Ole Sabaya amesema kwamba Fedha Hizo zililipwa na wazazi kwa lengo la wanafunzi kupata Elimu ya kufundisha kozi ya Ualimu na ndipo watumishi hao kujichotea fedha hizo kutumia Account hewa.

Amesema kutokana na watumishi hao kuchota fedha hizo bila huruma wakijua kwamba wazazi wa wanafunzi waliofika chuoni hapo kupata elimu ni watoto wa maskini alitoa wiki mbili fedha hizo kurudishwa katika Account ya Chuo na wanafunzi kuendelea na Masomo. 

Fedha hizo zilileta Mgogoro Mkubwa baina ya uongozi cha chuo pamoja na wazazi Mara baada ya wanafunzi kuingiwa hofu ya kurudi Nyumbani kwa kukosa masomo na ndipo mkuu wa wilaya kuingilia kati na kutoa maagizo ya kukamatwa kwa Muhasibu pamoja na karani wa Miamala hewa.

Sabaya amezitaja taasisi zingine zilizo tafuna fedha hizo ni pamoja na  benki ya Crdb wilani Hai taasisi ya ELCT ND pamoja na chuo cha Ualimu Mongare kwa uzembe wa kuacha kufanya ukaguzi wa mahesabu kwa mwaka mzima Chuoni hapo kiasi cha shilingi million 36.9 

Mkurugenzi wa Chuo hicho  Joseph Mongare Msaki akisoma taharifa ya urejeshwa Fedha amesema kwamba fedha hizo zimeingizwa katika account ya Chuo Mara baada ya utapeli uliofanyika na mhasibu kwa kushirikiana  na wakala wa Sacco's. 

Joseph amesema kwa mujibu wa Maagizo ya Rais kuhagiza fedha hizo kurejeshwa Mara moja katika accounti ya Chuo ndipo kupitia  mkuu wa wilaya kutoa amri ya wiki mbili fedha hizo ziwe zimerejeshwa chuoni.

Mkurugenzi amemshukuru Mkuu wa wilaya pamoja na Rais John Pombe Magufuli kwa fedha hizo kurejeshwa na wanafunzi kuendelea na masomo yao kama hapo awali.

Mkuu wa wilaya Lengai Ole Sabaya toka kukabidhiwa wilaya Hai Amekua mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuondoa changamoto ya ubadhirifu wa Mali za umma pamoja na kutatua migogoro ya Ardhi .

CRDB wameomba kuzilipa kwa utaratibu wao ili kumaliza changamoto hiyo jambo ambalo amewakubalia.

Aidha amewataka wanachuo hao pamoja na taasisi zilizo husika katika upotevu wa fedha hizo kuacha uhasama badala yake washirikiane kwakua tatizo limesha malizika.

"Hakuna sababu ya kuchukiana na hizi taasisi tunashukuru Mungu tumemaliza hilo pamoja na Kumshukuru Rais Magufuli kwa kuingilia katika 
 Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu cha Mongere kilichopo wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wakiwa na mabango ya kushukuru Rais.
Mkurugenzi wa Chuo hicho  Joseph Mongare Msaki  akizungumza  Mbele ya Mkuu wa Wilaya 

Mkuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya akionyesha risiti za malipo ya baadhi ya aliekuwa muhasibu wa chuo hicho kwa wanafunzi.

RC MAKONDA, MKURUGENZI PUMA ENERGY TANZANIA WAWATEMBELEA WATOTO WANAOTARAJIWA KUFANYIWA OPARASHENI YA MOYO JKCI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto ambao wametibiwa kwa ufadhili wa wadau waliomchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imechangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimsikiliza Mama wa mtoto Aidan Mfunya mkazi wa Kigoma ambaye mtoto wake anasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo ambaye wadau wake mbalimbali walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji kwa ufadhili wa Mhe. Makonda na wadau wake na hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimjulia hali mtoto Jasin Ally mkazi wa Arusha ambaye anasubiri kufanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo ambaye wadau wake walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kampuni ya PUMA Energy imemuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimjulia hali mtoto Doreen Likweri ambaye anasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ambaye wadau wake walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania imemuunga mkono mkuu wa mkoa huyo kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah huduma zinazotolewa katika chumba cha wagonjwa watoto walioko katika uangalizi maalum (JKCI) wakati ugeni huo ulipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto waliotibiwa kwa ufadhili wa wadau waliomchangia fedha mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimfundisha jinsi ya kupiga picha mtoto Jovin Muniko ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo na wadau wake kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imemuunga mkono Mhe. Makonda na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), wazazi na Watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo mara baada ya kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania kukabidhi mfano wa hundi ya shilinngi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.

Zainabu Mundera mkazi wa Kyela mkoani Mbeya akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda kwa kumfadhili mtoto wake kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji kwa ufadhili wa Mhe. Makonda pamoja na wadau wake na hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na baadhi wa wafanyakazi wa chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto ambao wamefanyiwa na wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo pamoja na wadau wake.Picha na JKCI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimfundisha jinsi ya kupiga picha mtoto Jovin Muniko ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo na wadau wake kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imemuunga mkono Mhe. Makonda na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.

DPP AWAONYA MAWAKILI WANAOCHOKUA FEDHA ZA WATUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI WANAOMBA MSAMAHA, KUKIRI MAKOSA YAO

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Michuzi TV

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini Tanzania, Biswalo Mganga, amewaonya mawakili wa kujitegemea wanaochukua fedha kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wanaoomba msamaha na kukiri makosa yao kwa kudanganya kuwa wanazipeleka fedha hizo kwa DPP au Ofisi ya DPP kuacha tabia hiyo mara moja kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria

DPP Mganga ameyasema hayo leo Oktoba 3,mwaka 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambapo pia ametumia nafasi hiyo kueleza wakati wanaendelea na zoezi la watu walioloomba msamaha na kwenda mahakamani kukiri na kuamriwa aidha walipe fedha au amri nyingine yoyote ile kwa nafuu ambayo watakayokuwa wamekubaliana imebainika kuna baadhi ya watu wakiwemo mawakili ambao wamekuwa wakitumika kutaka kukwamisha mchakato huo.

"Tumepata taarifa kuna baadhi ya mawakili wamekuwa wanachukua fedha kwa washtakiwa wanasema wanazipeleka kwa DPP au katika ofisi ya DP, naomba niwakanye au niwaonye wasirudie, wanaofanya hivyo, wanatafuta ugomvi na tayari nimeishaanzisha uchunguzi wasije tukalaumiana", amesema.

Pia amewewataka mawakili kufanya shughuli zao za ki uwakili bila kuathiri heshima ya watu wengine au ofisi anayoiongoza. Amesema utaratibu wa mshtakiwa kukiri uko pale pale, utaratibu wa kulipa malipo atapewa mahakamani si kwa Wakili ama mtu yeyote atoke na kwenda gerezani au kuwafuata ndugu na kuwaambia wampatie fedha akidai kwa madai anazipeleke banki, utaratibu huo haupo, ni vizuri watu wakajiepusha.

Aidha ameongeza kwa kuliangalia hilo, Serikali imefungua akaunti maalumu BOT, ambako fedha zote zitakazokuwa zinalipwa kwenye zoezi hilo zitapelekwa, na wala si kwenye akaunti ya Mahakamaha au viongozi wa juu wa Mahakama pamoja na viongozi wengine serikalini na wote wamejulishwa.

"Hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya Mahakama ya ofisi ya DPP wala TRA zaidi ya hiyo ya BOT, hivyo atakayelipa kwingine huko tusilaumiane. Niwaombe tena, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote yule atakayefanya vitendo vya namna hii nikamvumilia, hatutamvumilia mla rushwa," amesema DPP.

Alipoulizwa kuhusu watu ambao siyo washtakiwa lakini wametangaza kwamba wanataka kurudisha fedha ambazo walipewa na washtakiwa kwake. Amesema, mtu kama anajua alifanya makosa huko na anaona hataki kuendelea kuwa na uchafu, kitu kinachomkereketa rohoni na amegundua unamzuaje asirudishe hizo fedha.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA LISHE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Wadau wa Lishe kwenye ukumbi wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma, Oktoba 3, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma kufungua Mkutano wa Wadau wa Lishe, Oktoba 3, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema utapiamlo ni miongoni mwa vikwazo vya kutimiza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda ambao utawezesha Taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 

Amesema bila ya kuwa na lishe bora na afya njema, vinavyosaidia kuongeza uwezo wa kuelewa na ubunifu ili kuhimili ushindani wa kiuchumi nchi haitafika kwa wakati kwenye uchumi wa kati na wa viwanda uliokusudiwa. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 3, 2019) wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wadau wa Lishe uliofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Amesema ni muhimu elimu ya lishe ikatolewa kwa wananchi wote.

“Pamoja na tafiti kuonesha kwamba tumepunguza viwango vya udumavu na upungufu wa damu bado viwango vyake havikubaliki kimataifa. Vilevile, tuna viwango vya utapiamlo ambavyo vimezidi kuongezeka na havikubaliki kimataifa ikiwemo uzito uliozidi kwa wanawake wenye umri wa kuzaa.”

Amesema hali hiyo ni hatari kwa nchi ambayo inayokabiliwa na aina nyingine za utapiamlo unaosababishwa na lishe duni kama udumavu, utapiamlo mkali na wa kadiri ambapo athari zake ni kubwa katika ukuaji wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. “Hii ni ishara tosha kwamba tunatakiwa kuongeza juhudi katika kupambana na aina zote za utapiamlo ili kufikia viwango vinavyokubalika Kimataifa.” 

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutoa kipaumbele kwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na ambayo yanatekeleza miradi inayolenga kupunguza udumavu kwa watoto, matatizo ya upungufu wa vitamin na madini.

Kipaumbele kitatolewa katika kuimarisha matibabu ya utapiamlo mkali na wa kadiri, kupunguza tatizo la uzito uliokithiri na viriba tumbo na tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake na watoto ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inaleta matokeo chanya katika maeneo hayo.

Amesema kuwa mipango yoyote wanayojiwekea haiwezi kuleta matokeo chanya bila kuitengenezea mikakati thabiti ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kutenga rasilimali za kutosha, ambapo wataalamu hao waibue mikakati itakayoweza kutumika katika kupunguza tatizo la utapiamlo. 

Pia, Waziri Mkuu amewataka waajiri wote waandae fursa na kuwaalika mahala pa kazi maafisa lishe ili kuongeza ufahamu wa watumishi kuhusu lishe bora. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zimetakiwa ziweke mipango ya kuhakikisha maafisa lishe wanaalikwa kutoa elimu sambamba na ufundishaji shuleni.

Kwa upande wake,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema bila kuwa na nguvu kazi yenye lishe na afya bora Taifa haliwezi kufanikiwa kwenye masuala ya elimu, kilimo, viwanda hivyo kukwamisha jitihada za Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.

“Kwa hali iliyopo sasa ni wazi kuwa bado tuna kazi kubwa ya kufanya ili kuondokana na utapiamlo nchini. Juhudi za pamoja zinahitajika ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea katika Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe (2016/17 – 2020/21), ambayo ni pamoja na kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kufikia asilimia 28 na uzito uliozidi kufikia asilimia 30.”

Amesema Serikali inatambua kuwa lishe ni suala mtambuka linalotegemea jitihada za sekta mbalimbali, ambapo waliandaa Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa miaka mitano kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2020/21 ili kutoa muongozo katika utekelezaji wa afua mbalimbali za masuala ya lishe. 

Naye, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema katika jitihada za kupambana na umasikini ni vema elimu ya lishe bora ikatolewa kwa wananchi wote, ambapo amemshauri Waziri Mkuu aibebe agenda ya lishe, ambapo Waziri Mkuu amekubali.

Waziri Mkuu huyo Mstaafu ameongeza kuwa, mila potofu nazo zimechangia suala la utapiamlo nchini kwa sababu katika familia nyingi nchini vyakula vingi vizuri wanapewa wanaume na vyakula vibovu wanakula wanawake na Watoto.

Awali, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile amesema udumavu umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 31.5 mwaka huu.

Dkt. Ndungulile alisema licha kupungua kwa udumavu, changamoto iliyopo kwa sasa ni suala la unyonyeshaji kwa watoto walio na umri wa chini ya miezi sita, wanaonyenyeshwa ni asilimia 58 tu, huku asilimia 30 ya Watoto wenye umri wa zaidi ya miezi sita hawalishwi vizuri.”Theruthi moja ya wanawake nchini wana viribatumbo na utapiamlo wa lishe iliyopitiliza

WACHEZAJI CHIPUKIZI WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA AFRIKA WALIODHAMINIWA NA QNET WAHADITHIA MAMBO WALIOYAONA MANCHESHTER CITY

$
0
0
Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Mkurugenzi wa Masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Ivory Coast, Mashabiki 3 wa mpira wa miguu waliodhaminiwa na QNET, Meneja wa PR wa QNET – SSA na Meneger wa Mambo ya Sheria wa QNET – SSA.


Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Watoto wamewakilishwa na mwandishi wa habari na Meneja wa PR wa QNET bwana Akoua Maxime.
………..

Wachezaji wa mpira wa miguu chipukizi wa Afrika waliochaguliwa kutoka nchi za Ghana, Ivory Coast na Cameroun tarehe 31 August 2019, wameeleza fursa hiyo ya pekee na yenye kuhamasisha wakati wa mahojiano na vyombo vya habari jijini Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast. QNET iliwaalika waandishi wa habari katika mechi ya kupeana uzoefu kati ya Manchester City FC na Brighton & Hove Albion; Waandishi hao walitazama ligi ya mabingwa na kuzungumza na wachezaji chipukizi kutoka Afrika. 

QNET kampuni ya biashara ya mtandao inayoongoza ulimwenguni, kama sehemu ya jitihada zake za kuendeleza vipaji na kama namna ya kurudisha fadhila kwa jamii ambako inafanyia kazi, imedhamini wachezaji watatu vijana wa kiafrika kwenda kuhudhuria programu ya Lugha na Mpira wa Miguu ya kipindi cha msimu wa joto katika shule ya mpira wa miguu cha Manchester City jijini Manchester. 

Programu hii ilikua ya wiki mbili yenye lengo la kuhamasisha na kufundisha mpira wa miguu na kozi ya Lugha ya Kiingereza kwa wachezaji chipukizi wenye umri kati ya miaka 12-17. Programu hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 28 Julai mpaka tarehe 12 Agosti, 2019 katikati ya viwanja vya mafunzo vya timu ya Manchester City katika shule ya Mpira wa Miguu ya klabu ya City. 

Kwa mujibu wa Hamza Gaveh, wachezaji chipukizi kutoka Ghana walisema: “Ilikuwa ni moja kati ya wakati mzuri sana katika maisha yangu. Nimepata fursa ya kupata mafunzo pamoja na klabu bora zaidi ya mpira wa miguu katika mashindano ya ligi za uingereza. 

Nimejifunza mengi kutoka katika vipindi vya mpira na kutoka katika vipindi vya Lugha ya Kiingereza. Nilikuwa kinara katika darasa langu la lugha ya kiingereza na katika michezo, nimejifunza zaidi kuhusu kufanya kazi kwa pamoja katika timu na mikakati ya kijihami. Nimepata marafiki wapya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Urusi na katika nchi za Sacandinavia.”

Baba Ndiaye kutoka Ivory Cost amesema: “Japo kuwa nimesafiri sehemu kadhaa kucheza mpira wa miguu, Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City ni sehemu bora zaidi kati ya zote nilizowahi kwenda. Baada ya vipindi vya kuhamasisha tulivyovipata, sasa ninajihisi kwa kiasi kikubwa kwamba siku moja nataka kuchezea klabu ya manchester City. Ninafanya vizuri sana darasani na natumaini kufanya vizuri katika mpira wa miguu na kuchezea Ligi ya Maibingwa uingereza. 

Na Yvan Noh Nafeng kutoka Cameroun kwa furaha kubwa alisimulia: “Sikuwahi kusafiri kwa ndege hapo awali na ilikuwa ni mara ya kwanza kupata hati ya kusafiria ya kimataifa. Tukio zima hili lilikuwa ni kitu kikubwa sana ambacho hakijawahi kutokea maishani mwangu. Nawafahamu wachezaji wengi chipukizi kutoka katika klabu yangu ya mpira wa miguu nchini Cameroun wanaotaka kuwa kama mimi, nimepanga kubakia na tabia njema na kuwa makini. Vile vile ninapanga kuwafundisha wenzangu baadhi ya masomo ya mpira wa miguu niliyojifunza”.

Akiongea katika sherehe, Bwana Rajesh Rao, Mkurugenzi wa Mkuu wa QNET wa Mahusiano ya Kimataifa, alisema. “Programu hii ni sehemu ya jitihada za QNET za kuendeleza vipaji, kurudisha kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu pamoja na jamii kwa ujumla. Tunaamini kwamba fursa waliyopata kutoka Klabu ya Manchester City FC imewahamasisha vijana hawa kutafuta viwango vya juu katika maisha yao”.

Akiongea kuhusu ushirikiano kati ya Manchester City, QNET na programu ya mpira wa miguu, Bwana Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kanda ya Afrika, amesema “QNET ni biashara ambayo inaamini na kudumisha uendelevu. Tunaamini katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja na mdhamini wa lebo za mikononi (Sleeve Sponsor) ni moja kati ya jitihada zetu katika mpira wa miguu pamoja na hamasa ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. Kupitia Ushirikiano huu, tumepata fursa ya kupeleka watoto wanaotokea katika familia zenye kipato cha chini Afrika kwenda katika klabu za mpira wa miguu na shule ya lugha ya kiingereza jijini Manchester; jambo hili kweli limebadilisha maisha ya watoto hawa, Watoto tunaowasherehekea leo ni matunda ya ushirikiano huu. Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia wadau wetu wote.”

QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambako inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtando kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)

ASKARI POLISI SITA, WAFANYABIASHARA WAWILI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHA YA MIL 200/-, KUTAKATISHA FEDHA MILIONI 50/-

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

ASKARI Polisi sita na wafanyabiashara wawili wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali likiwemo la kushawishi rushwa ya Sh. milioni 200 na kutakatishaji Sh.milioni 50.

Washitakiwa hao ambao wamefikishwa mahakamani hapo leo Septemba 30,mwaka 2019 wamesomewa mashitaka yao mbele ya mahakimu wawili tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon mbele ya Hakimu Shaidi imewataja washtakiwa waliofikishwa hapo ni Sajenti Swedy Swedy (34), Koplo Mohamed (33), Koplo Jonas Lwezimula (38), wengine ni dereva Erick Kumburu (39) na mfanyabiashara Patrick Kumburu (40).

Imedaiwa, kati ya Julai 3 na 5 mwaka huu, maeneo ya Jamhuri na Indra Ghandi wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, washitakiwa Kumburu, Erick, Lwezimula, Mohamed na Swedy walikula njama kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa Julai 3, mwaka huu katika maeneo hayo hayo, walipokea Sh milioni 48 kutoka kwa Aisha Gote kwa niaba ya dada yake Nazima Khambiye. Pia Julai 5, mwaka huu maeneo hayo, walipokea Sh milioni mbili kutoka kwa Khambiye kwa lengo la kutompeleka kito cha polisi.

Katika mashitaka la nne, inadaiwa kati ya Julai 3 na 5, mwaka huu kwa lengo la kudanganya, mshtakiwa Kumbuku alijifanya Ofisa wa Benki ya Tanzania (BOT) kitu ambacho alijua si kweli.

Aidha washtakiwa hao wanadaiwa wakiwa maeneo hayo, walijihusisha na muamala wa Sh milioni 50 huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la makosa tangulizi ya wizi na kulazimisha kupata fedha.

Hata hivyo, washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo na haina mamlaka ya kutoa dhamana.

Aidha, wapelelezi, kutoka jeshi la polisi Shaban Shillah, Emmanuel Njegele, Joyce Kitta na Ulimwengu Rashidi nao ambao wamefikishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wakidaiwa kushawishi rushwa ya Sh milioni

Akisoma ya mashtaka, wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo amedai Desemba 17, 2018 huko Rainbow Social Club, Kinondoni, washtakiwa hao wakiwa maofisa wa uchunguzi, waliomba rushwa ya Sh milioni 200 kutoka kwa Diana Naivasha kama kishawishi cha kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Pia washitakiwa hao wanadaiwa, wakiwa waajiriwa wa Jeshi la Polisi, wakiwa katika Kituo cha Polisi Kawe walipokea rushwa ya Sh. milioni sita kutoka kwa Naivasha.

Alidai Desemba 18, mwaka 2018 washitakiwa hao walipokea rushwa ya Sh milioni sita kutoka kwa Naivasha na Desemba 19, 2018 washitakiwa hao wakiwa Kituo cha Polisi Kawe, walipokea Sh milioni mbili kutoka kwa Naivasha. Pia inadaiwa Desemba 23, 2018 washitakiwa walipokea rushwa ya Sh milioni mbili huku Januari 3, mwaka huu maeneo ya Tamarind Restaurant wilayani Kinondoni, walipokea rushwa ya Sh milioni mbili.

Aprili 13, mwaka huu maeneo ya Tripple 7 Bar and Restaurant, maofisa hao wa jeshi la polisi Idara ya Upelelezi inadaiwa walipokea rushwa ya Sh. milioni moja kutoka kwa Naivasha kama kishawishi cha kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Imeendelea kudaiwa kati ya Desemba 17,2018 na Aprili 13, mwaka huu maeneo yasiyojulikana jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kitta alighushi maelezo ya Naivasha ya Desemba 17, 2018 ili kuonesha kuwa maelezo hayo ni ya kweli na yalisainiwa na Naivasha wakati si kweli.

Pia mshitakiwa Shillah na Njegele ambaye hakuwepo mahakamani, Aprili 13, mwaka huu wakiwa maeneo ya Triple 7 walikiuka amri halali ya kukamatwa na Mpelelezi wa Takukuru, Colman Lubis. Hata hivyo, washtakiwa wamekana mashitaka na upande wa mashitaka umedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Washtakiwa wameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo Hakimu Rwizile aliwataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya taifa ambapo kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni 10.

Pia aliwataka kuwasilisha mahakamani hapo hati za kusafiria na mmoja kati ya wadhamini hao ametakiwa kuwa na hati au uthibitisho wa mali isiyohamishika. Mshitakiwa Shillah peke yake ametiza masharti na wengine walirudishwa rumande hadi Oktoba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

DKT.KALEMANI AMSIMAMISHA KAZI ALIYESABABISHA UMEME KUKATIKA KWA UZEMBE

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akielezwa namna Mfumo wa Gridi ya Taifa,unavyofanya kazi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto)akitoa maelezo kwa baadhi ya watendaji katika kituo cha umeme cha umbongo, huku akiwa ameshika kifaa kilichokatika baada ya kuungua na kusababisha kukatika kwa umeme usiku wa octoba, 03,2019.
Transifoma kubwa namba sita( T6) inayozalisha umeme wa Megawati 120 iliyopata hitilafu baada ya kifunga stimu(Fuse) kuungua na kukatika.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kufunga mtambo mkubwa mpya wa umeme wa Megawati 240, utakaoimarisha huduma ya umeme kwa Mikoa wa Dar es salaam na Pwani.
Mmoja wa wasimamizi wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Ubungo akimuonyesha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, sehemu ambayo kifunga stimu( fuse)iliyoungua na kukatika ilipokuwa imekaa.

………………..


Na Zuena Msuya, Dar es salaam,

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amemsimamisha kazi kwa uzembe, Mhandisi Samson Mwangulume wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) baada ya umeme kukatika kutokana na hitilafu iliyotokea katika Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Ubungo, Jijini Dar es salaam.

Umeme huo ulikatika usiku wa Octoba 03, 2019 na kusababisha Mkoa wa Dar es salaam na Zanzibar kukosa huduma ya umeme kwa muda.

Aidha aliwataka watumishi 6 wa TANESCO, wanaosimamia Mifumo ya Gridi ya Taifa kuhamia katika nyumba zilizojengwa na Serikali katika Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo, hadi kufikia saa nane mchana ya Octoba 03,2019 akiwemo Mkuu wa mfumo huo.

Dkt. Kalemani alisema hayo baada ya kufanya ziara ya kutaka kujua tatizo lililosababisha umeme kukatika, pamoja na laini ya kusafirisha umeme kutoka katika Gridi ya Taifa juzi, octoba 1,2019, katika sehemu ya Ubungo umbali wa kilometa 22 kuelekea mkoani Morogoro.

Baada kutembelea kituo hicho na kuona mfumo mzima wa kusafirisha umeme kwa njia ya Kieletroniki( SCADER) na kupata maelezo kutoka kwa wataalam, imebainika kuwa chanzo cha hitilafu hiyo ni uchafu katika vikombe(Broker) katika Transifoma kubwa namba sita( T6) inayozalisha umeme wa Megawati 120 hivyo kusababisha kifunga stimu( Fuse)kuungua na kukatika.

Dkt.Kalemani, alisema kutokea kwa tatizo hilo ni uzembe uliofanywa na msimamizi aliyekuwa zamu siku hiyo pia kutofanya kazi yake kwa ufanisi, pamoja na kutofanyika kwa ukaguzi na matengenezo ya mitambo hiyo mara kwa mara.

“ Wataalamu wangu wamenambia kuwa kuna fyuzi ilikatika, lakini nimetaka kujiridhisha, nimetembelea mfumo wa usafirisha nimeona, nimekuja katika transifoma nimeona,sababu kubwa waliyonieleza ni uchafu, sasa hili swala la uchafu ni uzembe uliofanywa na aliyekuwa zamu kushindwa kubadilisha na kufanya usafi katika vikombe hivyo, nimetoa maelekezo huyu Samsoni aliyekuwa zamu namsimamisha kazi kutokana na uzembe wake, atupishe watasimamia wengine,” alisema Dkt. Kalemani.

Akizungumzia wasimamizi wa mfumo wa gridi ya taifa kuishi katika nyumba zilizopo katika kituo cha ubungo, Dkt.Kalemani alisema kuwa dhimuni la watumishi hao kuishi katika nyumba hizo, ni kuweza kutatua kwa haraka na kwa wakati tatizo lolote linaloweza kutokea katika mitambo hiyo, badala ya kuanza kutafutwa na kutembea umbali mrefu kuja kutatua tatizo.

Vilevile kuimarisha na kuongeza udhibiti na usimamizi katika Gridi ya Taifa.

Pia ametoa onyo kwa msimamizi wa mfumo wa Gridi ya Taifa kutoka Ubungo hadi Kidato mkoani Morogoro, kuhakikisha changamoto ya kukatika umeme kwa wakazi wa Kimara na maeneo jirani halitokei tena na endapo litatokea aache kazi mwenyewe.

Dkt.Kalemani alilazimika kutoa ovyo hilo, baada ya msimamizi huyo kusema kuwa tayari ameweza kudhibiti tatizo lililokuwa likitokea mara kwa mara na kuleta adha kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema kwa sasa umeme upo mwingi nawa kutosha hivyo hakuna sababu ya kukatika, na hitilafu zinazotokea ni kutokana na uzembe wa wahusika kutosimamia mitambo vizuri na kusababisha uharibufu .

Kuhusu kuimarisha huduma ya umeme kwa Jijini la Dar es salaam, na Mkoa wa Pwani, Dkt. Kalemani alisema kuwa tangu mwezi uliopita wameanza kufunga mtambo mpya mkubwa wa megawati 240 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Mtambo huo utakuwa mbadala wa mitambo miwili ya zamani iliyoanza kufanya kazi tangu mwaka 1975, hivyo kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme Dar es salaam na Pwani kwa kiasi kikubwa.

Vile vile amemuagiza Kaimu Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Ubungo pamoja na usambazaji wahakikishe wanasimamia zoezi la kutoa mizigo yote iliyopo bandarini ili kuweza kurahisisha ukamilishwaji wa ufungaji wa mtambo huo mpya ambao umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 16.

UBALOZI WA TANZANIA, UHOLANZI WASHIRIKI KWA MAFANIKIO TAMASHA LIJULIKANALO KAMA “EMBASSY FESTIVAL – THE HAGUE”

$
0
0
Balozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea Banda la Tanzania wakati wa Tamasha maarufu kama Embassy Festival lililofanyika hivi karibuni. Tamasha hilo huandaliwa na Manispaa ya The Hague kwa kushirikiana na Balozi za nchi mbalimbali zenye Ofisi zake The Hague kwa lengo la kutangaza tamaduni za nchi hizo. 
Balozi Irene Kasyanju (mwenye fulana kulia) pamoja na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Bibi Naomi Zegezege Mpemba (wa pili kushoto) wakitoa maelezo kuhusu Tanzania kwa wageni

waliotembelea Banda la Tanzania, huku Bw. Denis Baraka (wa kwanza kushoto) ambaye ni Mtanzania na mdau wa shughuli za utalii ambaye kwa sasa anasoma nchini Ujerumani na ambaye kutokana na kupenda kutangaza utalii wa Nchi yake alisafiri kutoka Kiel, Ujerumani kuja Uholanzi kuungana na Ubalozi pamoja na Watanzania wengine kwenye Embassy Festival. 
Mwonekano wa Banda la Tanzania na wageni waliotembelea. 
Balozi Irene Kasyanju (wa tatu kushoto) akiwa na walishiriki wa maonesho ya mavazi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wakiwa wamevaa fulana za kuitangaza Tanzania ambao ni Bw. Issa Lupatu, Mwambata Fedha wa Ubalozi (wa pili kulia aliyevaa miwani) na Bw. John Appolo Kilasara,Katibu wa Chama cha Watanzania wanaoishi Uholanzi (Tanzanians in the Netherlands – TANE) ambaye pia ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha ISS nchini Uholanzi 
Balozi Irene Kasyanju akiwa na Bi. Bahia Kihondo, Mtanzania aliyeandaa maonesho ya mavazi
pamoja na watoto ambao walifungua maonyesho hayo kwa kusoma shairi fupi kwa lugha ya Kidachi na Kiswahili. 
Watazamaji wa maonesho ya mavazi yaliyotangaza utamaduni wa Mtanzania walikusanyika kwa 
wingi kutazama maonesho hayo 
Mwonekano wa Banda la Tanzania kwa sehemu ya ndani, likiwa limefurika Diaspora waliofika
kulitembelea na kupata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Uholanzi, Bi Linda Mkony (aliyevaa koti katikati) na Bw. Denis Baraka, wakiwa pia wamevaa 
na fulana maalum za kuitangaza Tanzania 
Washiriki wakionesha vazi lenye michoro ya wanyama “animal prints” wanaopatikana kwenye mbuga za Tanzania kwa mtindo wa kisasa 
Maonesho ya mavazi yakiendelea– vazi la khanga. 
Washiriki wa maonyesho ya mavazi wakiwa katika vazi la Kimasaai.


Ubalozi wa Tanzania The Hague, Uholanzi umeshiriki katika Tamasha maarufu la Embassy Festival lililofanyika mwezi Septemba, 2019. Tamasha hili huandaliwa na Manispaa ya The Hague kwa kushirikiana na Balozi za nchi mbalimbali zenye Ofisi zake nchini humo kwa lengo la kutangaza utamaduni wa nchi hizo.

Kama ilivyokuwa kwa balozi nyingine, Ubalozi wa Tanzania ulikuwa na banda lake kwa ajili ya kuonesha utamaduni wa Tanzania. Kwa kushirikiana na Watanzania wanaoishi Uholanzi (Diaspora), Ubalozi ulitumia fursa hiyo kutangaza utamaduni pamoja na vivutio vya utalii zikiwemo mbuga za wanyama. 

Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi (fashion show) kwa kuonesha vazi la Kimasai (shuka na shanga, n.k.), pamoja na khanga. Aidha, Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi na vitambaa vyenye animal prints za Simba, Chui (The big five), Twiga na Pundamilia na kuvionesha kwa mtindo wa kisasa na hivyo kuvutia watu wengi. 

Diaspora wajasiriamali walipata fursa ya kuuza bidhaa zao mbali mbali za asili kama vile khanga, chai, kahawa ya Tanzania, shanga, hereni, viatu na bangili. Watu wengi waliotembelea Banda la Tanzania walifurahia korosho, chai na kahawa vyote kutoka Tanzania vilivyokuwa vimeandaliwa mahsusi kwa ajili yao.

Ubalozi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangazaTanzania kupitia tamasha hilo ambapo idadi kubwa ya watu walishiriki na kuchukua vipeperushi vya kutangaza utalii wa nchi. 


MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AKUTANA NA BALOZI WA COMORO NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekema (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Comoro nchini, Dk. Ahamada El Badaoul Mohamed aliyemtembelea ofisini kwake jana. 

WAZIRI HASUNGA ATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MBOLEA YA KUKUZIA (UREA) KWA MSIMU WA KILIMO 2019/2020

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo tarehe 3 Octoba 2019 kwa ajili ya kutangaza bei elekezi ya mbolea ya kukuzia (UREA) kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo tarehe 3 Octoba 2019 kwa ajili ya kutangaza bei elekezi ya mbolea ya kukuzia (UREA) kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Katika kuhakikisha kuwa tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo inaongezeka ili kujitosheleza kwa chakula na malighafi za viwandani; serikali imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na wakuu wa nchi za Afrika kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2006. Ili kufikia lengo hilo Wizara ya Kilimo ilianzisha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS - Bulk Procurement System), kufuta tozo mbalimbali za mbolea, kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa mbolea na kuweka bei elekezi za mbolea kwa mkulima. 

Uingizaji wa mbolea kupitia BPS unahusu mbolea za Urea, DAP, NPK, CAN na SA. Hata hivyo, kwa sasa BPS inatumika kuingiza mbolea za DAP na Urea ambazo zinazotumika kwa zaidi ya asilimia 50.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 3 Octoba 2019 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo.

Alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 4(1)(u) cha Sheria ya Mbolea ya Na. 9 ya mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea, 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2017 (The Fertilizer (Amendment) Regulations, 2017), mbolea aina zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na Serikali. Hata hivyo, bei elekezi zinazotangazwa ni kwa mbolea zinazoagizwa kupitia BPS ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (Urea).

1. Zabuni za Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS)

Waziri Hasunga amesema kuwa Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) umeanzishwa kwa lengo la kupata punguzo la bei litokanalo na kununua na kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja (Economies of scale). Tangu kuanza kwa BPS mwaka 2017, huu ni msimu wa tatu wa kilimo wa utekelezaji wake ambapo mbolea zimeingizwa nchini kwa punguzo la bei katika chanzo (FOB – Free on Board) kwa asilimia 6 – 17 ikilinganishwa na bei katika soko la Dunia inayosimamiwa na taasisi inayofuatilia bei ya mbolea katika soko la Dunia iitwayo Argus Gmbh. Aidha, BPS imefanya gharama za usafirishaji wa mbolea baharini kushuka kwa kiasi kikubwa kutoka Tshs 23,000/= hadi Tshs 3,500/= kwa mfuko mmoja wa kilo 50. Kutokana na BPS, matumizi ya mbolea yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.

2. Mjengeko wa bei elekezi

Ikumbukwe kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya mbolea zinazotumika nchini kwa sasa huagizwa kutoka nje ya nchi. Hivyo, katika kutengeneza mjengeko wa bei, gharama mbalimbali huzingatiwa hususan bei ya ununuzi katika chanzo, usafirishaji wa mbolea baharini, bima, tozo za Mamlaka ya Bandari (TPA) na taasisi mbalimbali za udhibiti, gharama za vifungashio, kufungasha, usafirishaji hadi kwa muuzaji wa rejareja na faida ya mfanyabiashara.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa bei elekezi za mbolea hutegemea umbali wa sehemu inakopelekwa kutokea bandarini. Maeneo yote itakapopelekwa mbolea yana umbali kati ya kilometa 1 na 1,600 kutoka bandari ya Dar es salaam. Kwa Wastani, gharama ya kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea wa Kilo 50 kwa barabara kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi makao makuu ya Halmashauri kwa barabara ni Sh. 5,500/= kwa kilometa 1,000. Gharama hii hupanda na kushuka kutegemeana na hali ya barabara na hali ya hewa (masika au kiangazi). Aidha, usafiri kwa njia ya Reli ni nafuu zaidi kwa sababu gharama za kusafirisha mbolea kwa kilometa 1,000 kwa mfuko wa kilo 50 ni Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA).

3. Mwenendo na mchanganuo wa bei elekezi za mbolea ya kukuzia (Urea)

4.1.Mwenendo wa bei elekezi katika soko la ndani ya nchi


Ushindani wa zabuni za BPS zilizofunguliwa Julai 04, 2019 ulifanya bei za mbolea aina ya Urea kununuliwa kwenye chanzo kwa punguzo la dola saba (7) za kimarekani ikililinganishwa na bei za zabuni ya Julai, 2018.

Sambamba na punguzo lililotokana na zabuni hizo, Wizara ya kilimo ilifanya utafiti kati ya Juni na Julai, 2019 wenye lengo la kufanya marejeo ya kikokotoo cha bei elekezi ambacho kimetumika kwa misimu ya kilimo 2017/2018 na 2018/2019. Utafiti huo ulishirikisha wadau wa mbolea wakiwemo wauzaji (waingizaji, wasambazaji, wauzaji wa jumla na rejareja), wanunuzi (wakulima wadogo kupitia vyama vyao vya ushirika, wakulima wakubwa, viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na wanunuzi wa mazao).

Ushindani wa zabuni za BPS pamoja pamoja na utafiti wa kupitia upya kikokotoo umefanya bei ya mkulima kupungua kwa wastani kimkoa kutoka Tshs 57,482 hadi wastani wa Tshs 53,997/=. Hili ni punguzo la wastani wa Tshs 3,485/= au asilimia 6 kwa mfuko wenye uzito wa kilo 50.

MKUTANO WA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za Serikali, katika mkutano wake na Waandishi wa Habari ulifanyika leo Oktoba 3, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za Serikali, Mkutano huo ulifanyika leo Oktoba 3, 2019 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za Serikali, Mkutano huo ulifanyika leo Oktoba 3, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, akikaribisha swali kutoka kwa Mwandishi wa Habari (hayupo pichani), wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za Serikali, ulifanyika leo Oktoba 3, 2019 Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki kuzungumzia matumizi ya vitambulisho vya Taifa katika kufungulia akaunti

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anold Kihaule (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake na kujadili jinsi ya kuweza kuunganisha nguvu za upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa urahisi ili vitumike kwenye utambulisho wa kufungulia akaunti za Benki. Kwa mujibu wa Bwana Nsekela, vitambulisho vya Taifa ni nguzo muhimu sana katika zoezi la ufunguaji akaunti kwa wateja kwani vinabeba taarifa zote za utambuzi zinazohitajika na mabenki. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Tuse Joune (kushoto) na Mkurugenzi wa Tehama wa NIDA, Gideon Ndalu.

MHE IKUPA: WENYE ULEMAVU CHANGAMKIENI FURSA ZA MIKOPO

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Bw. Kayanda Ibrahim alipowasili wilaya ya Pangani kwa ajili ya ziara kukgua utekelezaji wa masuala ya UKIMWI na wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya pangani Mhe. Zainab Abdallah akieleza jambo kuhusu wilaya yake wakati wa kikao hicho.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akizungumza masuala ya watu wenye ulemavu wakati wa kipindi maalum cha elimu kwa umma katika studio za radio Pangani iliyopo Wilaya ya Pangani mkoani Tanga alipofanya ziara yake katika Taasisi ya UZIKWASA Mkoani humo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo wakati wa kikao chake na watendaji wa Taasisi ya UZIKWASA (hawapo pichani) alipokutana nao Oktoba 3, 2019 ili kukagua kazi wanazotekeleza.
Katibu Tawala wa Pangani, Mwalimu Hassan Nyange akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa za Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Taasisi ya UZIKWASA Bw. Novatus Urassa akieleza jambo wakati wa kikao hicho.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


NA.MWANDISHI WETU

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masualaya ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amewaasa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ili ziwasaidie kuboresha maisha yao.

Ametoa wito huo hii leo (oktoba 3, 2019) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kipindi maalum kinachorushwa na radio Pangani alipotembelea kituoni hapo Mkoani Tanga ili kujionea jitihada zinazofanya na radio hiyo katika kuhabarisha umma juu ya masuala mtambuka ikiwemo vipindi maalum vya elimu ya jamii kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu nchini.

Mhe.Ikupa alieleza kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha inatekeleza sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayohusu haki na ulinzi kwa watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapatiwa haki hizo ikiwemo masuala ya ajira, elimu, afya na utengamao wa maisha yao ili kuondokana na dhana potofu ya utegemezi kwa kundi hilo.

“Kwa muda mrefu sasa watu wenye ulemavu nchini wamekuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao za ajira, elimu, afya na kufikia wakati jamii kuwaficha badala ya kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao na kuweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujikwamua kiuchumi kuondokana na hali ya utegemezi.”alisema Mhe. Ikupa.

Aliongezea kuwa tayari Serikali imeendelea na jitihada za kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwatengea asilimia 2 katika kila Halmashauri nchini ambazo zinatumika katika kuwapatia mikopo kwa kupitia uundwaji wa vikundi na kujisajili ili kupewa mikopi hiyo isiyokuwa na riba na kujikwamua kiuchumi.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Zainab Abdallah alieleza kuwa Wilaya yake inatekeleza hilo na kuwataka vijana wenye ulemavu kutumia fursa za mikopo ili kuwezeshwa na kujiendeleza weneywe.

Akiongezea kuwa, jitihada za Wilaya yake ni kuhakikisha wanawafikia wenye ulemaviu katika kuwapatia mahitaji yao ikiwemo, elimu na kuwapa nafasi katika fursa mbalimbali zinazojitokeaza katika Wilaya yake.

“Niwaombe muendelee kujiunga kwenye vikundi kwani kasi iliyopo hairidhishi kwa kuwa hadi sasa kuna vikundi vitatu tu ambavyo vimesajiliwa Halmashauri na ili uweze kupata mikopo hiyo ni lazima vikundi vitambulike,”alieleza Zainab.

Aliongezea kuwa, ipo haja ya kila mwenye ulemavu kujitahidi kujishughulisha katika shughuli ya kumuongezea kipato kwa kuzingatia uwezo aina ya ulemavu wake kwa kuwa serikali imeendelea kuweka mkazo katika kuliangalia kundi hili.

“Hadi sasa Wilaya yetu ina watu wenye ulemavu zaidi ya 700 hivyo ni wakati sahihi kuona namna kundi hili linaangaliwa na kupatiwa elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikimu katika mahitaji yao na familia zao kwa ujumla’”alifafanua Mhe. Zainab

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Hassani Nyange alimpongeza Naibu waziri huyo kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha kundi la wenye ulemavu linapatiwa huduma kwa usawa na haki ili kuendelea kuboresha mazingira ya kundi hilo.

“Binafsi ninafuraha kwa ujio wako Pangani tunaahidi kuendelea kuunga jitihada za serikali vya vitendo kwa kuzingatia awamu hii ya tano imejikita kuinua uchumi kuanzia mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla hivyo tutaendela kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika shughuli za uzalishaji mali na kufikia Taifa la uchumi wa kati,”aliongezea Nyange.

JAJI MKUU AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BARAZA LA USULUHISHI TANZANIA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Taasisi ya Usuluhishi Tanzania( Tanzania Institute of Arbitrators) waliofika ofisini kwake leo, iliyopo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania kwa lengo la kujitambulisha.
Mjumbe wa Baraza la Taasisi ya Usuluhishi Tanzania, Frank Mwalongo akizungumza jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Mjumbe wa Baraza la Taasisi ya Usuluhishi Tanzania, Larissa Leach (wa pili kulia)akizungumza jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi ya Usuluhishi Tanzania(Tanzania Institute of Arbitrators). Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa wajumbe wa Baraza la Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania, Gabriel Malata (kulia).(Picha na Magreth Kinabo)

AMENDMENT TO EAC CUSTOMS MANAGEMENT ACT IN THE OFFING

$
0
0
Hon Dr Abdullah H. Makame who seconded the Motion presented by Hon Abdikadir Aden to introduce an amendment to the EAC Customs Management Act, 2014.






A section of the legislators pay attention to the proceedings yesterday.
Hon Abdikadir Aden, mover of the Motion seeking leave to introduce amendment to the EAC Customs Management Act, 2014,

***************************

East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: 2nd October, 2019: A proposal to amend the EAC Customs Management Act, 2014, to extend the time for removal of bulk containerized goods from the port(s) of discharge, is in the offing, in a move likely to reduce the cost of doing business in the region. In the regard, the Assembly has granted Hon Abdikadir Omar Aden, leave to introduce a Bill to amend section 34 (5) of the existing Customs Management Act, 2014, to realise the above objective. With it, the Assembly further adopted a motion to amend the Act, when it received support yesterday.


The Motion moved by Hon Aden, Chair of the General Purpose Committee and seconded by Hon Dr Abdullah Makame, was moved under Article 49(1), 59(1) and Rule 26 of the Rules of Procedure of the House.

At the moment, under the existing Act, the entry of cargo is required to be made within twenty-one days from the date of discharge of the vessel failing which the goods contained in the cargo begin to attract a charge or demurrage.

However, Hon Aden avers that extending the time for removal of large consignments from the port of entry would eliminate demurrage charges and hence goods more affordable and allow for longer storage period to facilitate clearance.

In the EAC, all cargo coming in to the region enters through the designated ports but mainly through the ports of Dar es Salaam in the United Republic of Tanzania and Mombasa in the Republic of Kenya.

“I am concerned that the limited time provided for entering and clearing bulk consignments is increasing the cost of doing business for East Africans engaged in the business of importing goods who are passing on the cost of the consumer of the imported goods”, Hon Aden said.

Under Article 59(1) of the Treaty, any Member may propose any motion or introduce any Bill in the Assembly. The Rules of Procedure of the Assembly also requires that a Private Members Bill shall be introduced first by way of Motion to which the proposed draft of the Bill shall be attached.

EAC CLIMATE CHANGE PROGRAMME LAUNCHED

$
0
0
The intra-Global Climate Alliance Plus (GCCA+) Programme on supporting Climate Change Adaptation and Mitigation Actions in the East African Community has been launched at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. 

The European Union (EU) is providing funding to the tune of 1.6 million Euros for the four-year project which commenced in July 2019 and runs up to June 2023.

The project which was launched by the EAC Secretariat in collaboration with the EU will, among other things: support EAC Partner States in addressing different climate change challenges; reviewing and updating their Nationally Determined Contributions (NDCs) for the effective implementation, and; developing community based climate change initiatives that will have tangible impacts on local communities.

In his opening remarks, the Chairperson of the Meeting, Eng. John B. Kizito, on behalf of the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Rwanda thanked the EU for its support in enhancing the capacity of the EAC region on climate change, strengthening the implementation of climate change actions, the Paris Agreement and regional capacity to access climate change funding.

Eng. Kizito cited some of the challenges posed by climate change in the region and echoed the need to take concerted measures in strengthening resilience while adopting low carbon and sustainable development pathways.

The EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, who represented the Secretary General, reiterated the EAC’s commitment to mitigate the impacts of climate change, adding that the Community had developed EAC Climate Change Master Plan (2011-2031), which is due for review.

Mr. Massimo Bonannini, the Programme Manager at the EU Delegation Office in Dar es Salaam, expressed concern that financial resources allocated to climate change actions were not enough and the NDCs which are the core of the Paris Agreement, altogether do not meet the expected targets.

Mr. Bonannini said that the EU would give more emphasis to climate change, adding that in the period 2021-2027, some 25% of the budget will be linked to climate change actions.He said that the EU was ready to increase its future engagement in order to support developing countries in their actions to reduce emissions and adapt to climate change.

He disclosed that the EU considers technical and political dialogues at national and regional levels as crucial to pursue relevant adaptation and mitigation strategies.

He said that the GCCA+ was one of the instruments that that the EU was implementing to help climate change mitigation actions in developing countries, adding that since 2008, GCCA+ had supported some 80 projects with a total allocation of more than 800 million Euros.

RICE FARMERS IN EAST AFRICA TO BENEFIT FROM US$3 MILLION GRANT

$
0
0
 Rice farmers in East Africa are set to benefit from a US$3.1 million dollar grant to a rice sector promotion project which will be implemented over a period of three years.

The Competitive African Rice Initiative in East Africa (CARI-EA), which is being implemented jointly by the East African Community (EAC) and Kilimo Trust (KT) seeks to improve the rice sub-sector in the region.The project was approved for funding by Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) in April 2019 and is now at the initial stage of implementation.

The project targets to reach 660,000 farming households (220,000 directly and 440,000 indirectly impacted). It aims to contribute to inclusive transformation of the rice sector in East Africa for sustainable increase in incomes of women, men and young people employed in the value chain of locally produced rice.

The 13th Meeting of the Sectoral Council on Agriculture and Food Security held in Arusha, Tanzania was informed that the project will be implemented over a period of 36 months (April 15th, 2019 – April 14th, 2022).

The project funding is worth US$3,133,378 courtesy of the US Agency for International Development (USAID) and the German International Cooperation Agency (GIZ) through the Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), whereby EAC will receive a grant of USD 322,600.

CARI-EA will support the EAC Secretariat to address the most critical bottlenecks in creating an enabling environment for structured trade in rice at both national and regional levels.

Key activities will include supporting EAC Partner States governments to develop clear rice development plans and mobilize private sector investments in rice mills as well as public sector investments in irrigated rice schemes.

CARI-EA will also support private sector millers to utilize opportunities at the national, regional and extra-regional levels through strengthened market linkages to ensure sustainable rice supply. The project will also carry out assessment of supply chain and logistical constraints and opportunities that hinder processors from attaining desired quality and quantity of paddy from smallholder farmers.

To ensure that farmers sustainably increase productivity to supply the contracted volumes of paddy agreed with SMEs and large traders, CARI-EA will promote the use of irrigation technologies and use of residual moisture during the dry season for a second crop e.g. vegetables or beans so as to enable income continuity for farmers over the year while increasing household food security and reduction in vulnerability.

On its part, the EAC Secretariat will aim to develop an EAC rice trade strategy involving all Partner States, establish the EAC Regional rice platform and increase the membership of private sector processors and rice value chain actors in the industry platform, and undertake research into the issues affecting rice regional trade.

The Secretariat will also establish a rice traceability and certification mechanism for locally produced rice in the EAC and promote the Sanitary and Phytosanitary (SPS) protocol already developed by the Community.

The ultimate aim of the project is to unlock constraints that hinder regional rice trade and thus catalyse growth by stimulating investment, create competitiveness and inclusiveness in the rice industry.

Furthermore, CARI-EA will partner with National Agricultural Research Centres and seed agencies in Partner States to ensure that enough breeder seed is available for multiplication by commercial rice seed companies.

The 13th Sectoral Council on Agriculture and Food Security consequently noted the introduction of a new programme on rice sector development and urged Partner States to support its implementation.

On aflatoxin control and management, the Sectoral Council urged Partner States to address the issue of aflatoxin as serious matter by putting in place measures to address contamination and disposal challenges along the food and feeds value chains.

The Community adopted the EAC Aflatoxin Prevention and Control Strategy, Action Plan and Results Framework adopted by the 36th Council of Ministers in February 2018.

Speaking at the opening session of the meeting, the Chairperson, Hon. Dr. Gerardine Mukeshimana, said that the agricultural sector contributes between 24 and 44% of Partner States’ GDPs. Dr. Mukeshimana, who is also Rwanda’s Minister of Agriculture and Animal Resources, further noted that agriculture employs between 70 - 80% of the population in the region. She added that it was a key sector in the transformation and development of EAC Partner States, particularly in employment creation and increasing national agriculture export earnings.

Dr. Mukeshimana underscored the need for Partner States to prioritize and invest in livestock and fisheries value chains taking cognizance of their important role in the food and nutrition security.In his remarks, EAC Deputy Secretary General in charge of the Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, said that the EAC has a huge potential for agricultural production, but the sector was facing challenges related to food insecurity, climate change, and trade.

“The sector supports over 80% of the population and is the main source of raw materials for industries in the region. More than 70% of the industries in the region are agro-based and agricultural commodities and products constitute about 65% of the volume of intra-regional trade,” said Hon. Bazivamo.

He noted that region has been experiencing a decline in intra-regional trade over the last five years yet trade was essential for the promotion of agricultural production and industrial development.

Also in attendance at the meeting were Kenya’s Minister for Agriculture, Livestock and Fisheries, Hon. Mwangi Kiunjuri; Hon. Dr. Rurema Déo-Guide, Minister of Environment, Agriculture and Livestock (Burundi); Hon. Kibazanga Mbalibula Christopher, Minister of State for Agriculture, Animal Industry and Fisheries (Uganda), and Hon. Luhaga Joelson Mpina, Minister for Livestock and Fisheries (Tanzania).

*TAARIFA MUHIMU KWA UMMA* : KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA NDANI YA SIKU 90

**TAARIFA MUHIMU KWA UMMA**: UPATIKANAJI WA NIN KWA AJILI YA USAJILI WA KUHUISHA KAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA

Washtakiwa Raia wa Kigeni wahukumiwa kulipa faini ya sh.Milioni 100 au kwenda jela miezi 12

$
0
0
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Arusha Rose Ngoka amewahukumu washitakiwa kumi ambao ni raia wa kigeni, kulipa Sh.milioni 100 au kwenda jela miezi 12, kwa kosa kufanya kazi kampuni ya uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC) bila kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.

Ametaja majina ya raia hao kuwa ni Darweshi Jumma, Riaz Aziz Khan, Mohammad Tayyab, Ali Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta, Imtiaz Feyaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali.

Hakimu Ngoka amesema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao kwa kukiri kufanya kosa hilo nchini na kuamuru kila mmoja kulipa faini ya Sh.milioni 10 au kwenda jela miezi 12.

"Kwa kuzingatia maombi ya Wakili wenu wa utetezi Steven Mosha na kwa kuangalia mazingira ya kesi na madhara ya kijamii kama alivyosema mahakama imekata hatiani na kuwapa adabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine,"alisema

Amesema mbali na kuwapa adhabu ya kulipa faini,pia aliwaonya washitakiwa hao na kuwataka kutii sheria,kanuni na taratibu za nchi pindi wanapoingia nchini.

Steven Mosha ni wakili wa utetezi kabla ya hukumu hiyo kutolewa ameiomba Mahakama hiyo kuwapa adhabu ndogo washitakiwa hao kwa sababu ni kosa lao la kwanza kufanya.

" Naomba Mahakama iwapunguzie adhabu sababu wamekiri na kuokoa muda wa mahakama,lakini pia washitakiwa wawili wana utaifa wa nchi ya India na nane raia wa Pakstani na walishitakiwa miezi mingi nyuma na kutumia gharama kubwa za kuishi,"alisema

Amesema kutokana na kushitakiwa wamelazimika kutumia fedha nyingi katika kuishi nchini na wengi wao vijana wanahitajika katika taifa lao kujenga taifa." Hakimu naomba wape adhabu ndogo sababu wengine umri wao mkubwa wanahitaji kukaa wanafamiliya zao,"alisema

Aidha amesema kuwapa adhabu kubwa itasababisha ugumu wa maisha kwa familia zao,hivyo aliomba wapewa adhabu ya kulipa fedha kwa sababu wapo tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ambacho mahakama hiyo itaamuru.

Kabla ya Wakili wa utetezi kutoa maombi hayo Wakili Mkuu wa Serikali Maritenus Marandu amesema kabla ya jana washitakiwa hao waliandika barua iliyowasilishwa na Wakili wao Steven Mosha ikionyesha washitakiwa hao kukiri makosa yao.

Pia aliiambia mahakamani hiyo kuwa, upande wa Jamuhuri hauna kumbukumbu za makosa ya nyuma,ila aliomba mahakama iwape adhabu inayostahili kulingana na kosa walilofanya.

Akiwakumbusha washitakiwa hao makosa yao Wakili Mwandamizi wa serikali Mkoa wa Arusha Abdallah Chavula akiwa na Wakili Idara ya Kazi Arusha Emmanuel Mweta amesema washitakiwa hao walifanya kosa la kufanya kazi nchini bila vibali vya kazi kati ya Novemba 2018 na Januari 2019.

Washitakiwa hao wenye taaluma mbalimbali walikamatwa wakiwa na hatia zao zà kusafiria wakijiandaa kuondoka nchini.

Washitakiwa hao walikamatwa Januari mwaka huu na Septemba 2 mwaka huu kesi hiyo ilifutwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Arusha Niku Mwakatobe kutokana na Wakili wa serikali kutokuwa tayari kuwasomea hoja za awali ili kesi iendelee.

Wakati huo huo mshitakiwa wa kwanza Isaya Mollel katika kesi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa OBC anayekabiliwa na kosa la kuajiri raia hao wa kigeni, bila ya kuwa na vibali kwa mujibu wa sheria za nchi za kutoa ajira kwa wageni hajakiri kosa na amepangiwa kesi yake Oktoba 16 mwaka huu.

Washitakiwa hao walifanikiwa kulipa faini hiyo na kuachwa huru.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>