Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MAJALIWA AZUNGUMZA BAADA YA KUKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA KUSINI INAYOJENGWA MTWARA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo, Mtwara Oktoba 2, 2019.
Viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini kwenye eneo la Mitenga, Mtwara, Oktoba 2, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa (wa tatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia) wakati Waziri Mkuu alipokagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, eneo la Mitengo Mtwara, Oktoba 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali Kutoridhishwa na Utendaji Kazi kiwanda Cha Nyuzi Tabora

0
0
Na, Editha Edward -Tabora

Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amefanya Ziara yake mkoani Tabora na kukagua maendeleo ya viwanda vilivyopo mjini hapo ambapo ameonesha Kutoridhishwa na utendaji kazi pamoja na uzalishaji wa kiwanda cha nyuzi TABOTEX

Waziri bashungwa amefika katika kiwanda cha nyuzi ambapo amejionea uzalishaji Katika kiwanda hicho ambacho kilibinafisishwa kwa muwekezaji Rajan tangu mwaka 2004 kutoka kwenye Mikono ya Serikali kikiwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya Mia mbili ambapo uzalishaji wa nyuzi ulikuwa ni wastani wa tani elfu tatu na Mia sita kwa mwaka 

Akiwa katika kiwanda hicho waziri bashungwa ametembelea na kushuhudia kushuka kwa uzalishaji pia na kuwa na idadi ndogo ya wafanyakazi katika kiwanda hicho

Naye mbunge wa Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka ameonesha Kutoridhishwa juu ya kiwanda hicho kwamba hakioneshi matumaini kwani tangu mwaka jana hadi leo hakijabadilika kitu chochote kwenye kuongeza wafanyakazi na kuongeza uzalishaji wa bidhaa

"Nimekuja mara ya mwisho hapa ila cha kushangaza hadi sasa sijaona mabadiliko wa sipidi ambayo inayotakiwa sasa hivi kwa viwanda sijaona pamoja na sasa tunaenda na kwa teknolojia lakini kiwanda kama kingekuwa kinaendeshwa vizuri kisingekuwa na wafanyakazi wachache kama hawa waliopo''Amesema Mwakasaka

Katika hatua nyingine waziri bashungwa amebainisha msimamo wa Serikali ya Awamu wa Tano ambayo dhamira yake ni kukuza uchumi wa Taifa kupitia viwanda vya hapa nchini 

"Wamiliki wa viwanda mnaniangusha sana serikali, mnatakiwa mboreshe utendaji wenu wa kazi panueni wigo wa masoko na muongeze uzalishaji wa bidhaa zenu"Amesema Bashungwa

Aidha katika Ziara yake waziri bashungwa pia ametembelea kiwanda cha mazao ya misitu Tabora pamoja na kiwanda cha maziwa ambapo akiwa Katika kiwanda cha maziwa ameagiza shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO kuwaunganisha wawekezaji wadogo na kampuni kubwa ili waweze kuimarika zaidi.
 Pichani ni Waziri wa Viwanda na biashara  Innocent Bashungwa (Katikati)  akiwa katika kiwanda cha nyuzi  TABOTEX,  Tabora.
Pichani ni Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa akipewa maelekezo na meneja wa kiwanda cha maziwa cha Tabora.

OFISA USALAMA SHIRIKA LA POSTA NA MWENZAKE WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AIN YA HEROIN

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin. 

Mbali na Mwamgabe, mshtakiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani hapo ni Abrahamani Msimu (54) dereva na mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam. 

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Aldolf Lema amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando kuwa Agosti 25 mwaka jana katika eneo la Posta jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 124.55.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa, Agosti 25, 2018 katika eneo la Posta, walisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa gramu 1.55.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kutenda makosa hayo na wako huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama iliwataka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja kutoka ofisi za umma watakaosaini bondi ya Sh. Milioni tano kila mmoja. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Washtakiwa hao wametimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Oktoba 16 mwaka huu.
 OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin. 

UPEPO WAZUA SINTOFAHAMU ARUSHA MTUMBWI WAZAMA ZIWANI,MTALII ANUSURIKA,JUHUDI ZA KUMTAFUTA NAHODHA ZAENDELEA.

0
0
Zoezi la kuutafuta mwili wa Samwel Gilda Mhina( 29)anayesadikiwa kupotea katika ziwa Momela mara baada ya kuzama kwa mtumbwi Katika kijiji cha Olkungwando ,kitongoji cha Momela kata ya Ngarenanyuki ,Tarafa ya King’ori wilyani Arumeru.
Zoezi la kuutafuta mwili wa Samwel Gilda Mhina( 29)anayesadikiwa kupotea katika ziwa Momela mara baada ya kuzama kwa mtumbwi Katika kijiji cha Olkungwando ,kitongoji cha Momela kata ya Ngarenanyuki ,Tarafa ya King’ori wilayani Arumeru.
Zoezi la kutafuta mwili likiendelea kama linavyoonekama katika picha katika ziwa Momela



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mtalii raia wa Ujerumani aliyefahamika kwa jina la Rosenbever Heike,pamoja na nahodha wa mtubwi Samwel Gelda Mhina( 29)wamezama katika Ziwa Momela ambapo mtalii huyo alifanikiwa kujiokoa huku juhudi za kutafuta mwili wa nahodha huyo zikiendelea.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:45 mchana jana Katika kijiji cha Olkungwando ,kitongoji cha Momela kata ya Ngarenanyuki ,Tarafa ya King’ori wilayani Arumeru.

Kamanda Moita amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali,ambapo nahodha wa mtumbwi huo ni muongoza watalii katika kampuni ya Africa .

Aidha Kamanda Moita ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya majini kuwa na tahadhari pindi kunapotokea mabadiliko ya hali ya hewa,na wawe na vifaa vyote vya uokoaji wawapo majini ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza.

Akitolea ufafanuzi wa kimbunga kilichotokea siku ya jana tarehe 1/10/2019 mkoani Arusha,majira ya saa 14:00 amesema kiliambatana na upepo mkali ambao uliweza kuezua vitu mbalimbali zikiwemo nyumba za ibada ,maduka pamoja na nyumba za watu binafsi.

MKANDARASI AAGIZWA KUMALIZA UJENZI WA MADARASA YA GHOROFA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA

0
0
Na Jusline Marco -Arusha

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Bw.Joseph Masawe amemuagiza mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa madarasa 4 ya Ghorofa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema ndani ya muda wa nyongeza aliopewa kwani ameonekana akichelewesha ujenzi kinyume na mkataba unavyoelekeza.

Masawe ametoa agizo hilo wakati alipokuwa kwenye ziara iliyoongozwa na kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu wilaya ya Arusha ya ukaguzi wa miradi ambayo imetekelezwa na ilani ya chama hicho kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Tarehe 1 Octoba 2019 Mkoani Arusha.

Akizungumzia miradi jiuo Masawe amesema kuwa ziara hiyo ni ya kawaida na ina lengo la kuhakikisha yale ambayo yaliahidiwa chini ya ilani ya Chama cha mapinduzi kupitia Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanatekelezwa kwa wakati.

Aidha miradi 10 iliweza kutembelewa ni pamoja na mradi wa Tenki la maji ESAMI, Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi hospitali ya wilaya, Matundu ya vyoo 20 shule ya msingi Murriet Darajani, Matundu ya vyoo 10 shule ya msingi sokoni I, Ujenzi wa Daraja la Shaulalu kata ya Sokon 1.

Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa 4 ya ghorofa shule ya Sekondari Sombetini,ujenzi wa uzio katika kituo cha afya daraja II,ujenzi wa barabara ya Masjid Quba na barabara ya Sanawari pamoja na Vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo kata ya Ngarenaro.

Pamoja na hayo amesema chama cha mapinduzi kiko makini katika kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa pamoja na yale waliyoahidi kupitia serikali ya awamu ya tano yanatekelezwa ikiwemo suala la Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara pamoja na maji.

Hata hivyo Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa matundu 30 ya vyoo katika shule mbili za msingi Murriet na Sokon 1 ambayo yako katika hatua za umaliziwaji.

Pia kamati hiyo ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kimewapongeza watendaji wa serikali ambao wamekuwa makini kusimamia miradi ya maendeleo hasa katika kuelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi na wakandarasi ili kupelekea miradi kutekelezwe kwa wakati na kuepusha vikwazo pindi inapoanza.
Kamati ya Siasa ya halmashauri kuu wilaya ya Arusha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Bwana Joseph Masawe wakitembelea baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa na ilani ya chama hicho.

SERIKALI KUHAKIKI TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KANDA YA ZIWA

NEWS ALERT: BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA MAJI MOROGORO YAVUNJWA

0
0
Dodoma: 03 Oktoba, 2019 
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA)imevunjwa. Hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2019.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imeainisha kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo ni kwa mamlaka aliyo nayo Waziri wa Maji kwa mujibu wa kifungu Namba 14 cha Jedwali la kwanza la Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya Mwaka 2019, kikisomwa pamoja na Kanuni Na. 14 ya Kanuni za Usambazaji wa Maji  (Tangazo la Serikali Na. 90 la tarehe 26/04/2019).

Taarifa hiyo imefafanua kuwa bodi ya MORUWASA imevunjwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia mamlaka ya maji hivyo kuathiri utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira  katika manispaa ya Morogoro.

Aidha, wakati huo huo Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) ametaka kuanza kwa  utaratibu utakaowezesha kuundwa kwa bodi mpya.


Kitengo cha Mawasiliano

EAC Secretariat​ EU-EAC MARKET ACCESS UPGRADE PROGRAMME (MARKUP) WEBSITE LAUNCHED

0
0
 

The web site of the EU-EAC Market Access Upgrade Programme was officially launched at a festive event during the EAC High Level Trade Integration Conference held from 25th to 27th September, 2019 in Nairobi, Kenya.
The Principal Secretary in the Ministry of East African Community and Regional Development, Kenya, Dr. Margret Mwakima, and Amb Jean Rigi, the Permanent Secretary at the Ministry of EAC Affairs, Burundi jointly launched the EAC MARKUP website.
Speaking at the event, Mr Kenneth Bagamuhunda, the EAC Director General for Customs and Trade, underscored the importance of supporting regional value chains in the agriculture sector and improving product quality and competitiveness.
Dr Kirsten Focken, the Programme Manager at GIZ, the German Technical Cooperation Agency, said that the website was important for purposes of visibility, sharing experiences and showcasing interventions, results and impact.
Mr Jocelin Cornet, Team Leader, Regional Cooperation of the European Union Delegation to Tanzania hailed all players for the achievements recorded so and thanked the EAC Secretariat for steering and guiding the implementation of the project.
“EU EAC MARKUP is part of the EU’s efforts towards integration in Africa and this new website is of great importance for the exchange of information and coordination of MARKUP, said Mr. Cornet.
Jointly designed by the European Union (EU), the EAC Secretariat and the governments of Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi and Kenya, the initiative is implemented by the Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ), the International Trade Centre (ITC), the United Nations Industrial Development Organization (UNIDO), the Uganda Coffee Development Authority (UCDA) and other national partners. This four-year programme is funded from the Regional Indicative Programme for EAC under the 11th European Development Fund.
EU-EAC MARKUP aims at eliminating trade barriers for East African small and medium companies and expanding their markets for coffee, tea, cocoa, selected spices and horticultural products in East Africa as well as in European markets. This will be achieved through supporting the private sector, business support institutions and policy makers in the Partner States and at the EAC Secretariat.
EU-EAC MARKUP was inaugurated on 20th of June 2018 in a signing ceremony at the EAC Headquarters in Arusha. It is now on the ground in the five Partner States of Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania and Uganda, strengthening SMEs and sector associations, supporting harmonisation of standards and SPS measures, and equipping trade support institutions to deliver better quality services.
Kenya’s EAC Affairs Principal Secretary, Dr. Margret Mwakima (centre), and her Burundian counterpart Amb. Jean Rigi (second left) toast to the launch of the EU-EAC MARKUP website. Also in the photo are (from left) the EAC Director General Customs and Trade, Mr. Kenneth Bagamuhunda, GIZ Programme Manager, Dr. Kirsten Focken and Mr. Jocelin Cornet, the Team Leader-Regional Cooperation at the EU Delegation in Tanzania.

More information is available at: www.eacmarkup.org

WATENDAJI SERIKALINI WATAKIWA KUTENDA HAKI WANAPOWAHUDUMIA WATUMISHI ILI KUPUNGUZA IDADI YA RUFAA NA MALALAMIKO YANAYOWASILISHWA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Na Happiness Shayo, Mwanza
Serikali imewataka watendaji katika taasisi za umma nchini kutenda haki wanapowahudumia watumishi wa umma ili kupunguza mlundikano wa rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma yanayowasilishwa Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya waajiri.

Wito huo umetolewa jijini Mwanza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi chake na Watendaji wa Serikali mkoani Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

“Serikali inaamini katika haki na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anataka haki itendeke hususani kwa wanyonge, hivyo mtendaji yeyote atakaebainika kumuonea mtumishi kwa kumnyima stahiki yake ni wazi kuwa serikali itamchukulia hatua za kinidhamu” Dkt. Mwanjelwa amesema.
Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, Tume ya Utumishi wa Umma imekuwa ikipokea malalamiko mengidhidi ya watendaji kuwaonea  watumishi wa umma na kuwataka watendaji hao kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao ili kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewaasa watendaji haokutumia muda wao kuwaelimisha watumishi kuhusu Kanuni, Sheria, Taratibu,Nyaraka na miongozo ya kiutumishi iliyopo ili watumishi wapate uelewa wa kutosha kuhusiana na stahiki za kiutumishi wanazostahili kupata.
“Mtumishi anapokuja ofisini kwako tumia muda wako kumuelewesha mtumishi huyo juu ya suala lake, kwa sababu ni sehemu yako ya kazi” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza

Akizungumzia kuhusu malalamiko ya watumishi kutobadilishiwa kazi(recategorization) baada ya kujiendeleza, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji amewataka Watendaji hao kuwashauri watumishi walio chini yao kujiendeleza kitaaluma katika kada zao walizopatia ajira(first appointment).

Bw. Muhoji ametoa wito kwa waajiri nchinikuwaingiza watumishi katika mpango wa mafunzo na kuwataka kuwapa ushirikiano wa kutosha watumishi wanaotaka kujiendeleza wenyewe kupitia vyanzo vyao vya mapato, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wametoa fursa kwa watumishi hao kujijengea uwezo kiutendaji” Bw. Muhoji amesema.

Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela, Bw.Said Raphael Kitinga akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho, ameishukuru serikali kwa elimu ya masuala ya kiutumishi waliyoipata kupitia mada zilizowasilishwa.
Bw. Kitinga ameongeza kuwa, kupitia kikao kazi hicho Watendaji wa Serikali mkoani Mwanza kwa kiasi kikubwa wametatuliwa changamoto zao kiutumishi zilizokuwa zikiwakabili katika maeneo yao ya kazi.

“Tumepata fursa za kutatua matatizo yetu kutokana na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi uliofanyika ’’ Bw. Kitinga amesema.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Watendaji wa Serikali Kuu, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakala za Serikali, Makatibu Tawala wa Wilaya, Watendaji wa Taasisi za Umma na Wakuu wa Sehemu/Vitengo kutoka Mkoa wa Mwanza lengo likiwa ni kubaini changamoto zinazowakabili, kusikiliza kero zilizopo na kuzipatia ufumbuzi ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa Mwanza (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Mwanza.

Baadhi ya Watendaji kutoka Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Mwanza.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji akijibu hoja wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watendaji wa Mkoa wa Mwanza kilichofanyika jijini Mwanza.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) akiteta jambo na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe.John Haule wakati wa kikao kazi kati yake na Watendaji wa Mkoa wa Mwanza kilichofanyika jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Bw. Said Raphael Kitinga.

DKT. KIJAJI AITAKA TRA KUONGEZA WIGO WA WALIPA KODI

0
0
Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kuandaa Mkakati mahsusi utakaosaidia kuongeza wigo wa walipa kodi nchini kutoka idadi ya zaidi ya walipa kodi milioni mbili nukta 7 (2.7m) waliosajiliwa na Mamlaka mpaka sasa.

Dkt. Kijaji aliyasema hayo alipofanya ziara ya kawaida ili kukagua utendaji kazi wa Mamlaka hiyo katika Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ya Mkoa wa kikodi wa Kinondoni.

Mhe.Naibu Waziri alisema ili kuwaondolea mzigo walipa kodi waliopo sasa, jitihada za makusudi zinahitajika ili kuongeza idadi ya walipa kodi.

Dkt. Kijaji ameitaka TRA kuandaa mpango mkakati utakaoonyesha kuwa baada ya miaka miwili Mamlaka hiyo itakuwa imeongeza idadi ya walipa kodi zaidi ya milioni mbili,kwa kufanya hivyo Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania watakuwa wamejibu hoja iliyotolewa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaondolea mzigo walipa kodi waliopo sasa.

Aidha Mhe. Kijaji ameitaka TRA kumuandalia na kuwasilisha kwake takwimu ya ongezeko la walipa kodi lililotokana na zoezi la kugawa vitambulisho vya wajasiriamali nchini. 

“Lengo la kugawa vitambulisho hivyo lilikuwa ni kuongeza wigo wa walipa kodi, hivyo ni vyema kujua tumeongeza walipa kodi wangapi waliotokana na zoezi hilo” alisisitiza Dkt. Kijaji

Kwa upande wa kodi ya majengo, Dkt. Kijaji ameitaka Mamalaka ya Mapato Tanzania kuhakikisha inapata orodha ya nyumba zote nchini kwa kuorodhesha wamiliki wa nyumba hizo na mawasiliano yao na kisha kuandaa kanzi data itakayosaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo. 

Dkt. Kijaji amesema ili kudhibiti upotevu mapato yanayotokana na kodi ya majengo ni lazima TRA wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kanzidata ‘database’ hiyo inakamilika ambayo itatumika kuwakumbusha walipa kodi kupitia ujumbe mfupi wa simu ambapo itasaidia katika ukusanyaji wa kodi hiyo.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Meneja wa Mkoa wa kodi wa Kinondoni Bw. Massawe Masatu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazopitia, Ofisi ya Mkoa wa kodi wa Kinondoni kwa mwaka 2018/19 ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 713ikilinganishwa na makadirio ya kukusanya shilingi bilioni 794, sawa na asilimia 86 ya lengo.

Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kuwatumia vizuri watumishi hao katika kuongeza mapato ili kuwezesha Serikali kuwahudumia vyema wananchi. 

Dkt. Kijaji ameuagiza Uongozi wa Mamlaka hiyo kuwapa ushirikiano watumishi wanaofanya kazi zao kwa weledi, na kutosita kuwachukulia hatua wale wote watakaonekana wana nia ya kuirudisha nyuma Mamlaka hiyo.
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi wa Kinodoni Bw. Massawe Masatu, akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za Mamlaka hiyo katika mkoa wake kwa Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea ofisi hiyo, Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kinondoni, Bw. Massawe Masatu wakati wa ziara yake aliyofanya katika ofisi hizo.
 Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akitoa maagizo kwa Naibu Kamishina wa Mamalaka ya Mapato Tanzania, Nd. Albert Kingu wakati wa mkutano wake na viongozi wa Mamlaka hiyo wa Mkoa wa kodi wa Kinondoni.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kinondoni.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa viongozi wa Ofisi ya Mkoa wa kodi wa Kinondoni wakati alipotembelea na kukagua utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji akiwasikiliza walipa kodi waliokuwa wakisubiri kupatiwa huduma katika Ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Millenium Tower, Jijini Dar es Salaam.

MAFIA YATAKIWA KUJIPANGA UWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoa wa Pwani kuandaa mazingira kupokea uwekezaji wa utalii kwa kupanga na kupima maeneo yake kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii.

Dkt Mabula alisema hayo kwa nyakati tofauti aliposikiliza kero za migogoro ya ardhi kwa wananchi wa kata za Baleni na Kilindoni wilayani Mafia mkoa wa Pawani wakati wa ziara yake ya siku mbili kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua masijala ya ardhi pamoja na mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, eneo la Mafia limekaa kimkakati na yasipofanyika maandalizi mapema kama vile kupima maeneo ya uwekezaji basi migogoro ya ardhi haitaisha na hivyo kuwafanya wawekezaji kushindwa kuwekeza katika wilaya hiyo.

Ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia kukusaidia kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya vijiji na kubainisha kuwa mpango huo unaweza pia kugharimiwa na vijiji husika kwa kuwa gharama yake haizidi shilingi milioni saba kwa kila kijiji na mpango huo utawezesha kuandaliwa maeneo ya kilimo, ufugaji na uwekezaji.

‘’Huu ni mwaka wa uwekezaji Wizara ya Ardhi ni wizara wezeshi tutafanya kila jitihada kupima viwanja katika eneeo la mafia na Kila anayetaka kuwekeza anataka Mafia lakini Mafia yenyewe haijawa tayari alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wizara yake iko tayari kuleta timu maalum ya wapimaji kutoka Wizarani kwa ajili ya zoezi la kupima maeneo mbalimbali katika wilaya hiyo pale ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia atakuwa tayari kugharimia fedha ya kujikimu kwa watumishi watakaofanya kazi hiyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alibainisha kuwa, halmashauri ya Wilaya ya Mafia inaweza pia kuandika Andiko litakalowezesha halmashauri hiyo kupata mkopo kwa ajili ya zoezi la upimaji katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Awali baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia halmashauri ya Mafia kwa kushindwa kupima maeneo mengi ya wilaya hiyo jambo walilolieleza limechangia kuwepo migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo. Hata hivyo changamoto kubwa inayoikabili wilaya ya Mafia ni kuwa na Mtumishi mmoja wa sekta ya Ardhi.

Maulid Mjenga alimueleza Dkt Mabula kuwa tatizo la upimaji katika wilaya hiyo mbali na mambo mengine lakini limesababisha mipaka ya Shule ya Msingi Kilindoni kutofahamika jambo lililochangia mfadhili aliyejitokeza kujenga ukuta wa shule kushindwa kufanya hivyo kutokana na kutojulikana kwa mipaka ya shule.

Migogoro mikubwa ya ardhi aliyokumbana nayo Dkt Mabula katika ziara yake wilayani Mafia ni pamoja na mgogoro wa wananchi wenye maeneo na kampuni ya Bronkhorst International Contractors Limited unaohusu fidia eneo la Ras Kisimani Mafia, mgogoro wa fidia kati ya kampuni ya Kinasi Lodge na familia ya Mwanahafsa na Bi Lawiya eneo la Utende pamoja pamoja na ule wa fidia katika shamba la Utumaini.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kulia) akikagua eneo la ufukwe la Bondeni Pwani kata ya Kilindoni ambalo baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamika kuzuiwa na mmiliki wake. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Shaib Nnunduma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa nne kulia) akikagua eneo la ufukwe la Bondeni Pwani kata ya Kilindoni ambalo baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamika kuzuiwa na mmiliki wake. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Shaib Nnunduma na wa tatu kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mafia Mbaraka Dau.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi aliowakuta katika ufukwe wa Bondeni Pwani kata ya Kilindoni wakati wa kukagua eneo hilo linalolalamikiwa kuwa mmiliki wake amekuwa akiwazuia kupita wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani Mafia.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Kampuni ya Bima ya Britam yaibuka kidedea kwenye tuzo za bima mwaka 2019

0
0
Meneja Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya(NHIF)-Kanda ya Ziwa,Jarlath Mushashu(kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Ltd, Raymond Komanga wakionyesha cheti baada ya Britam kutangazwa mshindi wa kampeni bora ya mwaka 2019.Wengine ni wafanyakazi wa kampuni ya Britam.


 Kampuni ya bima yaBritam Insurance Ltd, imeng’ara kwenye tuzo za bima zamwaka 2019 baada ya kutangazwa mshindi wa kampenibora ya mwaka katika tuzo zilizotolewa na Mamlaka yausmamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Tuzo hizo za bima zilizotolewa na TIRA kwakushirikianana Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) na kuzinduliwa Mei 21 ikiwa na lengo la kuhamasisha Ubunifu kwenye sekta yabima pamoja na kuchochea ukuaji endelevu.

Tuzo hizo zilizofanyika mapema wiki iliyopitazilihusishavipengele saba huku kampuni ya Britam iking’ara katikakipengele cha kampeni bora ya mwaka.

Akizungumzia ushindi huoMkurugenzi Mtendaji waBritam, Raymond Komanga alisema unatoa hamasa kwakampuni hiyo kuendelea kutoa huduma zenye viwango vyakimataifa pamoja na kukuza huduma hapa nchini.

Tunafurahi kupata ushindi huu na hii inaonyesha jinsigani tunatambulika katika sekta hii ya bima hivyo niwakati muafaka kwetu kuendelea kutoa elimu nakuhamasisha watanzania wengi zaidi kujiunga na hudumahii muhimu,” alisema Komanga.

Kampeni hiyo ijulikanayo kama “Tupo na Wewe” ilianzaAprili hadi Julai mwaka 2019 na imekuwa kampeniiliyoonesha mafanikio kwa jamii kutokana na kutumia njiambalimbali za mawasiliano kuelimisha wananchi juu yaumuhimu wa bima.

Tuzo hizo zilihusisha pia vipengele vingine ikiwamo tuzoya mjasiriamali kijanaTuzo ya kampuni inayosaidia jamiiKampuni bora ya mwaka, tuzo ya bidhaa bora ya kibunifuya bimapamoja na tuzo ya kijana aliyefanikiwa katikatafiti.

Komanga alisema kampeni hiyo ililenga kuelimisha ummajuu ya uwepo wa bima za aina mbalimbali zinazowezakukidhi mahitaji ya mteja katika kila hatua ya maishaikiwamo nyumbagariafya pamoja na bima kwaajili yataasisi na makampuni.
Aidhaalisema ilitumia njia mbalimbali ikiwamo redio namitandao ya kijamii pamoja na kuwahimiza wafanyakaziwake kujikita katika kuwahudumia wateja kwa wakati nakwa ufanisi ili kuleta muamko wa kujiunga na bimanchini. 
Kampeni hiyo ni moja ya mkakati wa kuunga mkonojitihada za Serikali katika kuhakikiha inafikia asilimia 45 ya watu wenye bima ifikapo mwaka 2021.
Huu ni mwendelezo wa kuwa sehemu ya maisha yawateja wetu na kuhakikisha tunawapa haki stahiki wakatiwa maafa kwa haraka na kwa ufanisi,” alisema Komanga.

Hadi mwaka huu kampuni ya Britam Insurance Tanzania ina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya pamoja na Mtwara hukuikitarajia kupanua wigo wa huduma katika siku zijazo.

Waziri Biteko awataka Mantra Tanzania kuipa muda Serikali kushughulikia ombi lao

0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko, ameitaka kampuni ya Mantra Tanzania kuipa nafasi ofisi yake ili kuweza kujiridhisha endapo maombi ya kusitisha kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa madini hayo una tija kwa kampuni na Taifa.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo wakati wa kikao baina ya Wizara na uongozi wa Kampuni hiyo ulioitaka wizara kuridhia ombi la kusogeza mbele shughuli za uzalishaji wa madini hayo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020 mpaka 2024.

Akizungumza hoja hiyo iliyowasilishwa katika kikao hicho, Waziri Biteko alihoji uhakika bei ya madini hayo ifikapo mwaka 2024 katika soko la dunia la endapo utakuwa wakuridhisha na kuwataka kuwasilisha data zao ili ofisi yake iweze kuzifanyia kazi.

“Ni kiashira gani kinachowaonesha kuwa ifikapo 2024 kutakuwa na ongezeko la thamani kwa madini ya urani?” Biteko alihoji.
Aidha, Biteko aliutaka uongozi wa Kampuni hiyo kuwasilisha mchanganuo unaoonesha ongezeko la thamani ya madini ya urani ifikapo 2024 ili wataalamu wa wizara wafanyie kazi na kuishauri wizara juu ya kuridhia au kutoridhia maombi hayo.

Akizungumzia juu ya maamuzi yaliyofikiwa na kampuni hiyo, Rais wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Vasiliy Konstantinov alisema bei ya kuuza madini hayo  kwenye soko la dunia imeshuka jambo ambalo litapelekea kampuni na serikali kutokunufaika na uwekezaji huo kutokana na kuwekeza kwa hasara.
Konstantinov alisema kuwa kampuni imeamua kufika na kukaa na wizara ili kupata msaada na kuhakikishiwa uhakika wa kuendelea na uwekezaji huo mara baada ya thamani ya madini hayo kuongezeka ili kuwawezesha kuwekeza kwa faida.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa leseni na Tehama kutoka Tume ya Madini, Yahya Samamba alihoji uamuzi wa Kampuni hiyo kuendelea na uwekezaji ifikapo 2024 endapo hakutokuwa na mabadiliko ya kuridhisha katika soko la dunia. 

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Alexander Ryabchenko alisema kwa sasa kampuni hiyo iko katika utafiti wa kutafuta njia rahisi isiyotumia gharama kubwa za uwekezaji ili kuifanya kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji mara baada ya muda huo kufika hata kama bei ya madini hiyo haitabadilika. 

Mantra Tanzania ni kampuni ya uchimbaji mkubwa wa Madini nchini iliyotolewa na Wizara ya Madini mwaka 2013.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwakaribisha wajumbe kutoka Kampuni ya Mantra Tanzania na wataalamu wa Wizara katika kikao kilichojadili juu ya uchimbaji wa madini ya uranium nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal akihoji jambo wakati wa kikao baina ya wizara na Kampuni ya Mantra Tanzania kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra nchini Frederick Kibodya akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya kampuni hiyo na wizara kilichoongozwa na Waziri wa Madini Doto Biteko.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uranium One Alexander Ryabchenko akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya wizara na kampuni hiyo.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko na wajumbe walioshiriki kikao baina ya wizara na kampuni ya Mantra Tanzania wakifurahia jambo wakati kikao hicho kikiendelea.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwa simu  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini(Jina halikupatikana) kuomba nafasi kwa ajili ya uongozi wa kampuni ya Mantra Tanzania kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania Alexander Ryabchenko akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Wizara na kampuni hiyo.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiagana kwa kushikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uranium One Alexander Ryabchenko mara baada ya kumaliza kikao baina ya wizara na kampuni hiyo. Katikati ni Rais wa kampuni hiyo Vasiliy Konstantinov
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa kampuni ya Uranium One Vasiliy Konstantinov.

MKUU WA MKOA WA KAGERA BRIGEDIA JENERALI GAGUTI AONGELEA MAFANIKIO YA ZAO LA KAHAWA MKOANI HUMO

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Chalinze katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

0
0
 Mwananchi akiweka taarifa za usajili katika Mnada wa Chalinze wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA ikiwa imepita kwa ajili ya kutoa Elimu ya usajili wa laini kwa alama za vidole.
 Afisa wa TCRA akitoa elimu kwa Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja  vya Bwilingu , Chalinze mkoani Pwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja. Vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.



Picha mbali za matukio katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.

WAKAZI wa Chalinze  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu ianzishwe imeenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA  Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Chalinze na vyunga brake   katika Uwanja wa Bwilingu wajitokeze ya kujisajili laini za simu kwa alama za vidole na  huduma nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa mnyororo   wadau wa  mawasiliano. 

Mhandisi Odiero amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa zinazohitajika katika kujisajili laini za simu  kwa alama  za vidole.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Odiero  amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Hata hivyo Kanda ya Mashariki itapita katika wilaya zote katika mikoa mitano ya kanda hiyo ambayo Morogoro,Pwani Dar es Salaam, Lindi pamoja  Mtwara.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Kavishe.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.

TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA MAGONJWA YA MILIPUKO NCHINI KWA MWEZI SEPTEMBA NA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUZUIA NA KUDHIBITI MAGONJWA

0
0
Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikitoa taarifa kwa wananchi mara kwa mara kuhusiana na mwenendo wa magonjwa ikiwemo magonjwa ya milipuko (epidemic diseases) nchini na hatua zinazochukuliwa kuzuia na kudhibiti magonjwa haya. 

Magonjwa yanayofuatiliwa kwa karibu na kutolewa taarifa mara moja pindi yakitokea ni, kumi na nne (14) ambayo ni pamoja na Kipindupindu, Polio, Kimeta, Kuhara Damu, Homa ya Uti wa Mgongo, Mafua makali ya ndege, Surua, Pepopunda ya watoto wachanga, Kichaa cha Mbwa, Ndui, Magonjwa yanayosababishwa na Virusi na Homa yanayosababisha damu kuvuja (Ebola, Marburg, RVF, Homa ya Dengue, Chikungunya), Macho mekundu, Tauni, na Homa ya Virusi ya Manjano. 

Utoaji wa taarifa za magonjwa haya zimerahisishwa, ambapo vituo vyote vya kutoa huduma za Afya nchini kuanzia ngazi ya chini hutoa taarifa hizi kwa kupitia mfumo maalum kwa njia ya simu (Integrated Disease Surveillance and Response - IDSR). Hii hupelekea taarifa zote muhimu kuhusu magonjwa kupatikana kwa haraka na hatua kuchukulia mapema na wizara ili kudhibiti magonjwa haya. 

Kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019, Wizara imeendelea kufuatilia magonjwa haya na matukio hatarishi kwa afya, kutoka kwenye mikoa yote nchini. Katika mwezi Septemba, ugonjwa wa Dengue na Surua tu ndio magonjwa ya milipuko yaliyotokea hapa nchini. 

Mwenendo wa Homa ya Dengue nchini. 

Kwa Kipindi cha mwezi Septemba 2019, jumla ya wagonjwa 10 walithibishwa kuwa na Homa ya Dengue na hakukuwa na kifo. Wagonjwa hawa walitolewa taarifa kutoka mikoa 2 ambayo ni Dar es salaam – wagonjwa 4 (Hospitali ya Taifa Muhimbili - 4) na Tanga – wagonjwa 6 (Tanga jiji - 6). Ugonjwa huu umeendelea kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa nchini na umeendelea kupungua mwezi hadi mwezi. Takwimu za miezi mitatu (Julai, Agosti na Septemba, 2019) zimeonyesha kupungua kwa ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa ambapo mwezi Julai 2019 kulikuwa na wagonjwa waliothibishwa 732, mwezi Agosti wagonjwa 92 na mwezi Septemba wagonjwa - 10. Aidha tangu mlipuko huu uanze mwezi Januari 2019 hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2019 kumekuwa na jumla ya wagonjwa waliohisiwa kuwa na Dengue 14,369 na kati yao waliothibishwa ni 6,785 na vifo 13 (Dar-6259, Tanga-365, Pwani-115, Morogoro-22, Lindi-8, Arusha-5, Singida-3, Dodoma-3, Ruvuma-2, Kagera-2 na Kilimanjaro-1). 

Ili kukabiliana na magonjwa yaenezwayo na wadudu dhurifu wakiwemo mbu, Wizara ilizindua mpango mkakati wa kukabiliana na wadudu dhurifu na mbu (National Vector control strategy 2019 - 2023) tarehe 27 Julai 2019, Dar es Salaam. Uzinduzi huu uliambatana na uzinduzi wa kitaifa wa zoezi la upuliziaji wa dawa kupambana na mbu wapevu na unyunyiziaji wa dawa za kuua viluwiluwi wa mbu waenezao magonjwa kama vile Malaria, Dengue na nk,. Dawa za kuangamiza wadudu zilinunuliwa pamoja na mashine kubwa (4) za kupulizia dawa (Fogging Machine) ambazo zilisambazwa katika mikoa iliyoathirika na ugonjwa wa Dengue yaani Dar es Salaam, Tanga pamoja na Dodoma. Wizara imeshaagiza mashine nyingine 4 ili kuweka mkakati endelevu wa zoezi hili. 

Mikoa hii pia (Dar es salaam, Dodoma, Tanga) ilishafanya uzinduzi wa Mkakati wa Kudhibiti Mbu na Wadudu wadhurifu pamoja na kuendesha zoezi la kuangamiza mbu. Hatua hii imesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Dengue nchini kama inavyoonyeshwa katika takwimu. Aidha, zoezi hili la uzinduzi linaendelea kufanyika katika Mikoa yote ili kutokomeza magonjwa yaenezwayo na wadudu hao. Elimu endelevu pia inaendelea kutolewa kwa wananchi juu ya namna kujikinga na kudhibiti ugonjwa huu 

Mwenendo wa Ugonjwa wa Kipindupindu nchini. 

Ugonjwa wa Kipindupindu umedhibitiwa, na kwa sasa HATUNA KABISA mgonjwa wa Kipindupindu nchini. Mara ya mwisho kupata mgonjwa wa Kipindupindu nchini ilikuwa tarehe 14 mwezi Julai 2019. 

Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Januari hadi Julai 2019, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 424 na vifo 8 vya ugonjwa wa Kipindupindu. Wizara inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja kufuatilia hatua zinazochukuliwa za kuzuia ugonjwa huu na timu ya Mkoa na Halmashauri ambazo ni pamoja na; Kutoa elimu ya afya kwa wananchi ya namna kujikinga kupata ugonjwa huu, Ufuatiliaji wa usafi wa mazingira. 

Wizara inakamilisha Mpango Mkakati wa Kipindupindu wa mwaka 2019 hadi 2023 ambao utekelezaji wake utajikita katika maeneo yanayotoa wagonjwa mara kwa mara (Hotspot areas) ambayo ni Dar es Salaam (Halmashauri zote), Ngorongoro (Arusha), Simanjiro (Manyara), Handeni na Mkinga (Tanga), Kilwa (Lindi), Ulanga (Morogoro), Mbarali na Chunya (Mbeya), Songwe, Sumbawanga DC (Rukwa), Mpanda (Katavi), Nyasa (Ruvuma) na Iringa DC (Iringa). 

Mpango huu, unalenga kutokomeza Kipindupindu kabisa. Katika mpango huu maeneo yalijikita ni pamoja na: Uratibu na ushirikishwaji wa wadau katika ngazi zote katika kudhibiti ugonjwa, kuimarisha ufuatiliaji na upimaji wa wagonjwa, Kuimarisha utoaji wa matibabu sahihi na mapema kwa wagonjwa, ushirikishwaji wa jamii katika kudhibiti na ugonjwa, kuweka mazingira ya kuwepo kwa maji safi na salama na masuala ya matumizi ya vyoo na vilevile kuimarisha utoaji wa chanjo kwa maeneo sugu na vigezo vitakavyotumika. 

Wizara imeendelea pia na utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira yenye kaulimbiu isemayo “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO”, ikiwa ni moja ya mikakati ya kutokomeza Kipindupindu na magonjwa ya kuhara. Kampeni hii ambayo ipo katika awamu ya pili, ilizinduliwa rasmi Disemba, 2017 na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Uanzishwaji wa Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za serikali kujielekeza katika kutekeleza lengo namba 6.2 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals) pamoja na lengo namba 3 linahusu kuboresha Afya. Katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji (2016-2019), jumla ya kaya 2,464,225 zimejenga au kuboresha vyoo kufikia kiwango cha ubora kati ya lengo la kaya 3,360,000. Hii ni sawa na asilimia 73.3. Kwa upande wa taasisi, shule 1,670 kati ya lengo la shule 2,520 zimejenga vyoo bora kwa kuzingatia uwiano. 

Kwa ujumla kaya zenye vyoo bora katika ngazi ya kaya zimeongezeka kutoka asilimia 46 Julai, 2016 hadi asilimia 57.2 Juni, 2019, na kaya zisizokuwa na vyoo zimepungua kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 2.5 katika kipindi hicho. 


Mwenendo wa Ugonjwa wa Surua nchni. 

Katika kipindi cha mwezi Septemba 2019, mlipuko wa ugonjwa Surua ulitokea katika kitongoji cha Kashasha, Kakoma na kijiji cha Kibare wilayani Kyerwa mkoa wa Kagera. Jumla ya wagonjwa 17 walipatikana na ugonjwa wa surua ambapo kati yao; wagonjwa saba walithibitishwa kwa kipimo cha maabara. Mgonjwa wa mwisho kupatwa na dalili za surua katika eneo la Kibare ilikuwa tarehe 14/09/2019. 

Kwa takribani wiki mbili sasa hakuna mgonjwa mwingine aliyepatikana. Wagonjwa wote wamepona na elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa surua imetolewa na pia kuhamasisha kuwaleta watoto katika kampeni ya kitaifa shirikishi ya chanjo ya surua na rubella, watoto wote chini ya miaka mitano. 

Katika ufuatiliaji wa ugonjwa surua nchini wagonjwa wenye dalili za homa na vipele hufuatiliwa na kuchukuliwa sampuli kupima kubaini kama wana ugonjwa wa surua. Kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019, jumla ya sampuli 222 za wagonjwa waliokuwa na dalili ya homa na vipele zilipokelewa na kufangashwa na kuwasishwa maabara ya Taifa kutoka kwenye mikoa 23 ya Tanzania bara. 


Mwenendo wa Ugonjwa wa Polio nchini. 

Hadi sasa hakuna mgonjwa wa Polio aliyethibika hapa nchini tangu mwaka 1996. Hii inatokana na jitihada kubwa za Serikali katika kutoa chanjo na kufuatilia dalili za wagonjwa wenye ugonjwa huu na pia kwa kununua chanjo za Polio ambazo zimeweza kuwafikia watoto wote chini ya miaka mitano (5) kwa zaidi ya asilimia 90%. 

Katika ufuatiliaji wa ugonjwa huu, wagonjwa wote wa dalili za kupooza ghafla (Acute Flaccid Paralysis - AFP) hufuatiliwa na sampuli kuchukuliwa na kupimwa kujua kama wana ugonjwa wa Polio. Kwa mwezi Septemba 2019, jumla ya sampuli 63 za AFP 63 zilifungashwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo. Aidha katika ufuatiliaji wa virusi vya polio katika mazingira, ambapo kirusi hiki pia hukaa kwa muda nao unaendelea na hadi sasa kirusi hiki kimeonekana kuwa hakipo katika mazingira yetu. Ufuatiliaji wa mara kwa mara unaendelea. . 

Katika mpango wa kutokomeza vifo na ulemavu kutokana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo na kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, itaendesha kampeni ya chanjo dhidi ya Magonjwa ya Surua, Rubella na Polio mnamo tarehe 17 hadi 21 mwezi Octoba 2019. Kampeni hii itafanyika nchi nzima kwa watoto wote lengwa walio na umri wa chini ya miaka mitano. Nawasihi wananchi wote washiriki ili Serikali ifikie lengo la kampeni hii. 


Mwenendo wa Ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuripotiwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 

Wizara imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuripotiwa nchini DRC na kuchukua hatua za tahadhari za kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa kuwa kwa sasa ugonjwa huu unaendelea kusambaa na kuingia kusini mwa DRC. Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2019, jumla ya wagonjwa 3,194 walithibitishwa kuwa na ugonjwa huu, na vifo 2133 (CFR 66.8%). Kutokana na ukaribu wa nchi hii na Tanzania, Wizara imeendelea kuchukua hatua za utayari kuzuia na kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu 

Hatua za utayari na kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu nchini ni pamoja na kuimarisha uchunguzi wa Wasafiri kwenye mipaka yetu yote. Kuimarisha utambuzi katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za Afya; Kuhakikisha uwepo vya Vifaa Kinga hususani kwa watumishi wa Afya; Kuimarisha utambuzi wa Ugonjwa na kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga ugonjwa huu. 

Wizara inayo namba ambayo hutumika bila malipo na wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa tetesi za ugonjwa huu ambazo ni 0800110124 au 0800110125. Kuanzia 2018 hadi sasa, tetesi 28 za wagonjwa wanaohisiwa kuwa na Ebola (washukiwa 2 kwa mwezi Septemba), zimekwisha kutolewa taarifa na uchunguzi kufanyika kwa ukamilifu na kuthibitisha wagonjwa hawa hawakuwa na Ebola, na taarifa zake kupelekwa pia katika Shirika la Afya Duniani. Aidha Wizara imeendelea kufanya pia mazoezi ya kujinoa na kijipima utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu (Simulation Exercises) katika mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha. 


NAPENDA KUSISITIZA KUWA HADI SASA HAKUNA MGONJWA ALIYETHIBITISHWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA HAPA NCHINI. WIZARA INAWASIHI WANANCHI KUTOKUWA NA HOFU NA KUPUUZA TAARIFA ZINAZOTOLEWA KILA KUKICHA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII. 


Katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola na magonjwa mengine ya milipuko yenye madhara makubwa duniani, nchi yetu kila wakati imekuwa mstari wa mbele ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa ukamilifu na kutekeleza Kanuni za Kimataifa za Afya (International Health Regulation - IHR 2005). Mnamo mwaka 2016, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kukubali bila kipingamizi kuleta wataalam duniani kuja kupima utayari wa nchi yetu katika kukabiliana na magonjwa haya hatarishi (Joint external evaluation). Hatua hii kubwa na ya uwazi ilifanywa kwa mara ya kwanza Duniani, kama moja ya njia ya kuhakikisha nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani, wanatekeleza Kanuni hizi za Kimataifa (IHR 2005). Aidha nchi nyingine zenye uwezo mkubwa duniani zilisita kufanyiwa tathmini hadi miaka miwili baadae, na nyingine hadi sasa hazijafanya zoezi hili. Hivyo basi, taarifa zinazoenea kuelezea kuhusu Tanzania kutokuweka wazi taarifa za magonjwa hususan uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini, si za kweli na hivyo ziendelee kupuuzwa. Taratibu za utoaji wa taarifa za magonjwa ya milipuko zinajulikana na ninatoa rai kwa sote tuzingatie sheria na taratibu za nchi husika na za kimataifa. 

Ikumbukwe kuwa, ugonjwa wa Ebola ambao unaweza kusambaa kwa haraka, na ambao madhara yake ni makubwa na yanajulikana duniani kote, kamwe hauwezi kufichwa na nchi yetu. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua madhara makubwa ya kuficha ugonjwa kama huu kwa wananchi. Narudia tena na kuwataka wananchi kutulia na kupuuza taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, maana HAKUNA UGONJWA WA EBOLA NCHINI TANZANIA. Inaonekana kuna njama ovu za kueneza taarifa hasi dhidi ya nchi yetu. Ninaendelea kuwasihi Wananchi kuwa watulivu na kushikamana kwa pamoja katika kuzuia ugonjwa huu usiiingie nchini. 

Aidha, Serikali inapenda kuwahakikishia Mataifa yote kuwa nchi yetu ni SALAMA na HATUNA UGONJWA WA EBOLA. Nirudie tena kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirika la Afya Duniani katika kujenga utayari wa kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola. Na endapo kutatokea mtu atakaethibishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini tutaendelea kuzingatia miongozo na taratibu za kimataifa ikiwemo kutoa Taarifa WHO kwa mujibu wa Kanuni za Kimataifa za udhibiti wa magonjwa hatari ya kuambukiza (IHR 2005). 

Kipaumbele cha Wizara kwa sasa ni kuendelea kuimarisha utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu usiingie nchini na endapo kutatokea kisa cha ugonjwa huu nchini tuweze kukabiliana nao na kuudhibiti mara moja. 

Asanteni sana

WAKULIMA WAPATA NEEMA, BEI YA MBOLEA YASHUKA

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Kilimo Japheth Hasunga amesema bei elekezi ya mbolea ya kupandia na kukuzia kwa msimu wa mwaka 2019/2020  imeshatolewa ambapo imeanza kutumika kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na hiyo ni katika kuhakikisha kunakuwa na utoshelevu wa chakula nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hasunga amesema kuwa mbolea zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na Serikali na si vinginevyo na mbolea aina nyingine zitapangiwa bei na wafanyabiashara kwa kuangalia mahitaji na hali ya soko ilivyo.

Aidha amesema baada ya kuanza kwa mfumo wa kuagiza mbolea kwa pamoja bei imeshuka kwa asilimia kati ya sita hadi 17 kwa kuangalia umbali uliopo (Mkoa ambapo mbolea inakwenda.)

Kuhusu gharama za usafirishaji wa mbolea Waziri Hasunga amesema kuwa;
"Tukumbuke kuwa kabla ya mfumo wa uagizaji wa pamoja haujaanza ilikua inafikia sh. 23,000 na sasa imepungua hadi kufika sh. 3500, hivyo ina manufaa na kwa sasa tumekuja na mifuko ya kilo tano, 10 na 25  ili wakulima wanunue kwa wanachohitaji," ameeleza.

Kuhusu bei ya mbolea katika msimu huu Hasunga amesema kuwa asilimia 90 ya mbolea inayotumika nchini imeagizwa kutoka nje ukitoa kiwanda pekee cha mbolea cha Minjingu kilichopo mkoani Manyara.

" Asilimia 90 ya mbolea tunayotumia nchini inayoagizwa kutoka nje hivyo wadau na watanzania wenye uwezo wajitokeze kuwekeza kwenye sekta ya mbolea ili gharama za mbolea zizidi kushuka zaidi," amesema.

Amesema kuwa bei iliyopangwa ni ya juu zaidi hivyo wanunuzi wanunue kwa kuzingatia bei hiyo bila kuvuka;

"Mbolea ya kukuzia (UREA) imepungua kutoka sh.57,482 hadi kufikia shi. 53,997 kwa mfuko wa kilo hamsini ambapo kuna punguzo la sh. 3485 sawa na asilimia sita," amesema.

Amesema kuwa mbolea ya kukuzia katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa mfuko wa kilo hamsini bei imeshuka kutoka sh. 48,500 hadi kufikia sh.45,280 Manyara ikishuka kutoka sh.58,339 hadi kufikia sh. 54, 830 huku Mkoa wa Iringa bei ikishuka kufikia sh. 53,934 kutoka 56,443.

Pia Mkoa wa Geita bei ya mfuko wa kilo hamsini imeshuka kutoka sh. 60,124 hadi 56,683,  Arusha bei ikishuka kutoka sh. 57,236 hadi 53,722, Songwe bei ikiwa ni shilingi 55,851 kutoka 59,360, Shinyanga bei ikiwa ni sh. 55,903 kutoka 58,996 na Rukwa bei ikiwa ni sh. 58,378 kutoka 61,102.

Amesema bei hizo zimeshuka kwa mifuko ya kilo zote huku bei ya rejareja ya mbolea hiyo ya kukuzia kwa mikoa ya Mashariki, Kati, Kusini na Kaskazini ikiwa ni kati ya sh. 45,800 hadi 47,100 na kwa Mikoa ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini bei ni kati ya sh. 52,400 hadi 59, 700.

Waziri Hasunga ametumia nafasi hiyo kuzionya Kampuni zinazouza mbolea feki na kutorosha mbolea kabla ya kuanza kutumika nchini kuacha mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kunyang'anywa leseni zao.

Vodacom Tanzania yasogeza huduma zake kwa wakazi wa Bariadi

0
0

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka kuwa mgeni rasmi, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Duka maalum la huduma za Vodacom (Vodacom Shop) mjini Bariadi – Simiyu, jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. Antony Mtaka akiongea na wananchi katika uzinduzi wa Duka la VODACOM SHOP mjini Bariadi.
 
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya Bariadi Festo Kiswaga akimlisha keki Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo kanda ya Ziwa – Vodacom, Bw. Ayubu Kalufya mara baada ya uzinduzi rasmi wa Vodacom Shop mjini Bariadi.
Meneja wa Vodacom Mkoa wa Simiyu, Chanila akimimina kinywaji cha Champagne kwa Mgeni rasmi na kiongozi mkuu kanda ya ziwa kampuni ya Vodacom ikiwa ni ishara ya kufurahia uzinduzi wa duka jipya
Meneja wa Vodacom Mkoa wa Simiyu, Chanila akimimina kinywaji cha Champagne kwa Mgeni rasmi na kiongozi mkuu kanda ya ziwa kampuni ya Vodacom ikiwa ni ishara ya kufurahia uzinduzi wa duka jipya 



Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga ambaye ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo na wadau mbali mbali wa Vodacom wakitoa zawadi kwa wasanii maarufu kutoka mjini Bariadi.

Baadhi ya wananchi wilayani Bariadi wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa duka maalum la Vodacom.
Baadhi ya watumishi na wadau wa kampuni ya Vodacom wakiwa katika maandamano ya furaha ya uzinduzi wa Duka maalum la Vodacom mjini Bariadi mkoani Simiyu. 
 

Umoja wa Mataifa waipongeza Tanzania kwa ulinzi wa amani ukanda wa maziwa makuu

0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed katika ofisi za Umoja huo New York Marekani
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) hayupo pichani, wakati akimkaribisha katika ofisi za Umoja huo zilizopo New York Marekani
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed (Hayupo pichani) wakati alipokwenda katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na baadhi ya wajumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na wajumbe wake (hawapo pichani) katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na wajumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York,Marekani.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed ameisihi Tanzania kuendelea kuimarisha amani katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na kuendelea kuchangia kutoa askari wa vikosi vya ulinzi wa amani duniani.

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Amina Mohammed ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiorikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Jijini New York nchini Marekani na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unatambua mchango wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani na kwamba Umoja huo uko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza jitihada hizo ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

“Tanzania imekuwa muhimili muhimu katika kuhimiza amani katika ukanda wa maziwa makuu ikiwa ni pamoja na kuhifadhi wakimbizi kutoka ukanda huo kwa miaka mingi bila kuchoka” alisema Dkt. Amina

Kwa upande wake waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa Tanzania inatambua nafasi ya Umoja wa Mataifa na kwamba itasalia kuwa mwanachama wa umoja huo.
“Napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wake katika vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani,” alisema Prof. Kabudi

Waziri Kabudi aliendelea kumueleza Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepiga katika masuala ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni pamoja na afya,maji, ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi pamoja na masuala ya kuimarika kwa demokrasia nchini.

Prof. Kabudi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani alipokuwa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu na kuchagua Viongozi

0
0
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa uchaguzi mjini Aschaffenburg Ujerumani jumamosi 28.09.19. Katika uchaguzi huo watanzania wanaoishi ujerumani walichagua viongozi wapya, nafasi ya mwenyekiti alichaguliwa Mwl. Bi Upendo Vanessa Lymo kuwa mwenyekiti wa UTU e.V, baada ya mwenyekiti mstaafu Bw. Mfundo Peter Mfundo kukataa kugombea nafasi hio, ambayo amekaa kwa muda wa miaka 9, na kukitumikia chama hicho kwa muda wote huo, hata hivyo kamati ilimuomba achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamati, mshauri, mlezi wa UTU e.V na kiongozi muandamizi katika shughuli za UTU e.V

Watanzania wanaoishi ujerumani waliwachagua viongozi wafuatao.

Mwenyekiti: Mwl. Bi Upendo Vanessa Lymo

Makamo Mwenyekiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo

Katibu: Bi. Petrida Karch

Muweka hazina: Bw. Mngoya Lukuta

Wanakamati:
Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw. Ebrahim Makunja (aka Kamanda Ras Makunja)
Bw. Sudi Mnette
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live


Latest Images