Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

OSHA YATOA NENO KWA KAMPUNI ZA GESI, MAFUTA ZINAZOTAKA KUWEKEZA NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi(OSHA)umezitaka kampuni za mafuta na gesi ambazo ziko nchini kuhakikisha zinasajiliwa na wakala huo kwa lengo la kuhakikisha zinafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama kwa viwanda na nchi kwa ujumla.

Akizungumza leo Oktoba 2,2019 katika kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi lililoanza leo jijini Dar es Salaam Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya Umeme kutoka OSHA Mhandisi Maria Ndasikoy amesema tunapsema Tanzania iko kwenye uchumi wa viwanda lazima viwanda hivyo viwe salama wakati wote.

"Tupo kwenye kongamano hili la wadau wa mafuta na gesi kwa ajili ya kuwaeleza umuhimu wa kujisajili OSHA.Lazima kampuni au kiwanda kinachojihusisha na gesi na mafuta ziwe salama wakati wote.

"Tunafahamu katika shughuli za gesi na mafuta kuna vihatarishi vingi na kwa maana hiyo OSHA lazima tusimame imara kwa kusimamia majukumu yetu kikamilifu,"amesema Mhandisi Ndasikoy.

Ameongeza kwa kampuni za mafuta na gesi ambazo hazijasajiliwa watatumia nafasi hiyo kuzisajili na baada ya hapo watakwenda kukagua kwa kutumia vifaa malumu walivyonavyo ili kuangalia usalama kuanzia wa wafanyakazi, kiwanda chenyewe na usalama wa nchi kwa ujumla.

"Kwa kutumia vifaa vyetu tunaweza kukagua kiwanda cha gesi na gesi yenyewe kwa hatua mbalimbali.Pia kwa kutumia vifaa vyetu lazima tukague na mfumo wa umeme maana kama kutakuwa na tatizo ni rahisi kiwanda kuungua na kuleta madhara kwa Watanzania,"amesema.

Ameongeza OSHA ni jukumu lao pia kuangalia mazingira kwa wafanyakazi , hivyo kama gesi inavuja inaweza kuleta athari kwa mfanyakazi na uharibu wa mazingira.

"Hivyo wakati mkakati wa nchi yetu ni kuelekea Tanzania ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati maana yake lazima twende huko tukiwa salama,"amesema Mhandisi Ndasikoy.

Kuhusu hali ilivyo kwa sasa amesema kuna muamko mkubwa sana kwani wawekezaji wengi wamejisajili OSHA na wao wanakwenda kuwakagua. Hata hivyo ametoa rai kwa kampuni zinazokuja nchini kuwekeza katika gesi na mafuta ni vema zikahakikisha zinajisajili OSHA.

"Wakumbuke kufika katika ofisi zetu kujisajili ili watambulike wao wa akina nani na wanatumia vifaa gani katika kampuni zao.Wakikaguliwa itakuwa rasihi kukabiliana na madhara ambayo yanaweza kujitokeza.Pia TIC kuna ofisi zetu za OSHA, hivyo wanaweza kwenda hapo kujisajili,"amesema.
 Mmoja ya wadau akitoa maoni yake baada ya kutembelea banda la OSHA lililopo kwenye kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi lililoanza Leo jijini Dar es Salaam
 Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya  Umeme kutoka OSHA Mhandisi Maria Ndasikoy akimsikiliza mmoja ya wadau wa mafuta na gesi ambao wapo kwenye kongamano la tatu la wadau wa mafuta na gesi linaloendelea jijini Dar es Salaam
Mkaguzi wa Usalama wa Mifumo ya Umeme kutoka OSHA akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam wakati anatoa rai kwa kampuni za gesi na mafuta ambazo bado hazijasajiliwa OSHA kuhakikisha zinajisajili

WAUGUZI WAOMBA ADA YA LESENI ZA UUGUZI ZIPUNGUZWE

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wameomba Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini(TNMC) kupunguza gharama za ada ya leseni za uuguzi ambazo wamedai kuwa ni kubwa na zinaathiri vipato vyao.

Ombi hilo limetolewa na Katibu wa Chama cha wauguzi Tanzania Bara(TANNA) Bw. Sebastian Luziga wakati akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipofungua Kongamano la kisayansi na Mkutano wa 47 wa wauguzi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Oktoba 01, 2019 Mjini Bariadi.

Luziga amesema awali ada hiyo kwa ngazi ya astashahada ilikuwa 20,000/= stashahada na shahada na shahada ya uzamili ilikuwa shilingi 40,000/=, hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la ada ambapo astashahada wanapaswa kulipa shilingi 40,000/=, stashada 60,000/=shahada 80,000 na shahada ya uzamili na uzamivu ni 120,000/=.

“Ongezeko hili ni kubwa na linaathiri sana kipato cha wauguzi kwani hakuna uwiano kati ya kupanda huko kwa ada na ongezeko la mshahara; kupitia Wizara ya Afya tunaomba lishughulikiwe upya kwa kufuata utaratibu wa kushirikisha wadau,” alisema Luziga

Akizungumza mara baada ya kupokea risala hiyo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameahidi kulifikisha suala hilo pamoja na mengine yaliyowasilishwa kwa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, huku akiwaomba viongozi kulitafakari kwa upya ongezeko la ada wakizingatia hali halisi ya mishahara ya wauguzi, kodi na makato na waone busara kama ipo haja na hoja ya kuongeza ada hiyo.

“Suala hili ni hoja ya walio wengi, ninyi nyote mmemuona Mhe. Rais akizungumzia kuondolewa kwa tozo nyingi zisizo na sababu kwenye kilimo, mifugo, uvuvi; hata hili la kwenu linaweza kusababisha serikali iwe na nia ya kufahamu mabaraza yake yote na tozo zao, nawaomba viongozi mlitafakari muone kama ipo hoja na haja ya kuongeza gharama za ada,” alisema Mtaka.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema mkoa unatambua kazi inayofanywa na wauguzi ya kutoa elimu kwa wajawazito na kuhamasisha wajifungulie kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo mwaka 2017 wanawake waliojifungulia kwenye vituo vya afya ni asilimia 55 na mwaka 2018 ikapanda kufikia asilimia 70.

Naye Afisa Muuguzi kutoka Halmashauri ya Ubungo Bi. Aliho Ngeregenza amesema wauguzi walio wengi vipato vyao wanavyopata haviendani na gharama za leseni wanazolipia hivyo ombi lao wapunguziwe gharama hizo

Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara ambalo linahusisha wauguzi zaidi ya 800 litafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
 Baadhi ya wauguzi wakishangilia wakati Mgeni rasmi akiingia ukumbi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Baadhi ya wauguzi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifungua Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Rais wa Chama cha Wauguzi nchini, Bw. Paulo Magesa akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu(kushoto) na viongozi wa Chama cha Wauguzi Tanzania bara wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Katibu wa Chama cha Wauguzi nchini, Bw. Sebastian Luziga akisoma risala ya wanachama kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu
 Baadhi ya wauguzi wakiwa katika maandamano ya amani 01 Oktoba, 2019 kuelekea ukumbi wa Shule ya Sekondari Kumbukumbu ya Kusekwa mjini Bariadi, mahali ambapo Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, ambao unafanyika kwa siku nne Mkoani Simiyu.
Wauguzi wakicheza wakati muuguzi mwezao akitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

SGR – YATOA KIPAUMBELE KWA WAHANDISI WA KIKE 20 NAFASI ZA MAFUNZO KWA VITENDO KATIKA UJENZI WA RELI UNAOENDELEA TANZANIA

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania nchini – TRC limetoa nafasi 20 za mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi miwili katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kwa wahandisi wanawake katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya makao makuu TRC Dar es Salaam hivi karibuni Oktoba 01, 2019.

Lengo la kutoa nafasi hizo kwa wahandisi wanawake ni kuwaongezea ujuzi lakini pia kuongeza idadi ya wahandisi wanawake katika Miradi ya Shirika hususani mradi wa SGR ili waweze kujenga na kubuni miundombinu ya reli nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa Shirika limetoa nafasi hizo ili kuhamasisha wanawake na kuondoa dhana ya kwamba shughuli za uhandisi zinafanywa na wanaume na si wanawake, pia amewaasa kuwa na moyo wa kulitumikia taifa lao na kuwa na uthubutu wa kufanya vitu kwa maendeleo ya taifa.

“Watu wanapopata nafasi ya mafunzo kama haya, ni dhahiri wanapaswa kuyafanyia kazi” alisema Ndugu Kadogosa.

Aidha Ndugu Kadogosa alisema kuwa TRC ni sehemu nzuri ya kupata mafunzo kwa vitendo kwa wahandisi wa nyanja tofauti na pia kuwasihi wahandisi hao kujenga tabia ya kufuatilia miradi ya reli katika nchi za nje kupitia mtandao ili kupata ujuzi zaidi.

Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi kutoka Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania – ERB, Mhandisi Patric Balozi amesema mafunzo haya ya vitendo kwa kundi hili maalumu la wahandisi wanawake yatasaidia kuongeza wingi wa wataalamu hapa nchini na kuacha kutegemea wataalamu wa nje.

“Watanzinia wawe wazalendo kwaajili ya kutumikia nchi yao wenyewe”, alisema Mhandisi Balozi

Mhandisi Balozi ametoa shukurani kwa Shirika la Reli Tanzania – TRC kwa kutoa nafasi hii na kusema kuwa wanawake wanapopata nafasi kama hizi wanatakiwa kujituma hali hii itawafanya kuwa wakakamavu na kushirikiana kwa pamoja katika maendeleo ya kujenga taifa.

“Tunawahamasisha wahandisi wa kike ili tusiwapoteze, watumie nafasi hii kujifunza waweze kuwa katika historia ya mradi mkubwa wa SGR” alisema Mhandisi Balozi.

Meneja Mradi ujenzi wa Reli ya SGR kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro Mhandisi Machibya Masanja amesema kuwa kikubwa ni juhudi katika kazi na kujifunza, pia amewakaribisha wahandisi hao kujifunza ili kuweza kuendesha miradi ya reli itakayoendelea .

UPEPO MKALI ULITOKEA ARUSHA WAZAMISHA WATU WATATU, WAKIWEMO WATALII WAWILI

$
0
0


Picha ikionyesha Mkuu Wilaya ya Arumeru Jerry Muro  pamoja na kamati ya usalama ya Wilaya wakiendelea na kazi ya kumtafuta ,kijana mmoja alietambuliwa kwa jina la Samwel Gildati Mhina anaejishughulisha na kazi za kuongoza watalii anahofiwa kuzama katika ziwa momela.

Na  Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha 

UPEPO uliovuma ghafla katika Mkoa wa Arusha umesababisha kuzama kwa watu watatu wakiwemo watalii wawili huku mtu mmoja akihofiwa kupoteza maisha katika Ziwa Momela lililopo Hifadhi ya Taifa ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru.

Kwa mujibu wa Mkuu Wilaya Arumeru Jerry Muro amesema kutokana na upepo huo mkali uliotokea jana saa nane mchana mtumbwi waliokuwa wanautumia watalii hao kutalii katika ziwa Momela ulipigwa na dhoruba ya upepo na kupinduka.

Amesema katika halmashauri ya Meru eneo la Momela watu watatu waliokolewa baada ya mitumbwi miwili waliokuwa wanautumia kupigwa na uppep mkali na kupinduka, ambapo kijana Samwel Mhina anaejishughulisha na kazi za kuongoza watalii anahofiwa kuzama katika ziwa hilo pamoja.Mtumbwi aliokuwa anaitumia haujapatikana mpaka.

Murro amesema Jeshi la Polisi pomoja na vikosi  vya zimamoto na uokoaji kutoka mkoani na wilaya ya Arumeru vinaendelea na kazi ya kuwatafuta

"Mtakumbuka jana Oktoba 1,2019 mchana Mkoa wetu wa Arusha ulikumbwa na dhoruba ya upepo mkali, ambao pamoja na maeneo mengine upepo huo ulienea mpaka katika maeneo ya Wilaya ya Arumeru.Umeleta madhara katika maeneo kadhaa,"amesema.

Amebainisha kuwa katika tukio hilo raia wawili wa nje waliokolewa mara baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba ya upepo na kupinduka waliokolewa wametambuliwa kwa majina ya Dk.Tuemper Bern John na Dk. Rosenberger ambao ni wa Ujerumani

Muro amesema kuwa katika kijiji cha Kimundo kata ya Nkoarisambu nyumba moja imeezuliwa paa , ambapo pia katika kijiji cha Ulong’aa kata ya Nkwandrua paa la choo cha shule ya msingi nalo liliezuliwa.

Amesema mpaka sasa baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Dk. John Danielson pallangyo wako katika maeneo yaliyokumbwa na changamoto

UBINAFSISHAJI WA KIWANDA CHA NYUZI TABORA BAADA YA KUBAINI HAKIFANYI VIZURI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI itapitia mkataba wa ubinafsishaji wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora (New Tabora Textile Tanzania Limited) baada ya kutoridhishwa utendaji wa uzalishaji ili kuchukua hatua mapema ambazo zitasaidia kufanyakazi kwa kiwango chake endapo itabainikiwa wawekwenda kinyume kwa masharti yaliyomo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Viwanda na Bisahara Innocent Bashungwa wakati wa ukaguzi wa viwanda mbalimbali mkoani Tabora na kukuta kiwanda cha Nyuzi Tabora kikiwa katika uzalishaji mdogo wakati pamba ya wananchi imejaa mitaani.

Alisema kiwanda hicho kingekuwa kinafanyakazi kulingana na uwezo wake kingesaidia sana kupunguza tatizo la ununuzi wa pamba ya wakulima kususua na kingeongeza uzalishaji wa zao hilo na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa.

Bashungwa alisema kwa kuwa Mmiliki wa Kiwanda hicho ameonekana kuwa na uwezo mdogo na hivyo awe tayari na maamuzi ambayo yatafikiwa baada ya kuangalia mkataba na vigezo alivyopewa wakati ubinafishaji na ikibainika amekiuka Serikali itachukua hatua ili kuongeza tija na utendaji kazi wake.

Alisema wakati wa Mwekezaji huyo na wengine kuendelea kukalia viwanda ambavyo vilitarajiwa kuzalisha kwa ajili ya kukuza uchumi na kutengeza ajira umekwisha na Serikali itachukua hatua.

“Tutangalia Sheria inasemaje na mkataba mlioingia …ili kuangalia njia bora ya kukifanya kiwanda hiki kifanye kazi kwa ajili ya mustakabali mzuri wa wakazi wa Tabora na nchi kwa ujumla” alisema.

Aidha Waziri huyo alivitaja Viwanda vingine ambavyo uzalishaji na utendaji wake sio mzuri ni pamoja na Mwatex na Mutex ambavyo navyo mikataba ya ubinifsishaji wake itachunguzwa kwa ajili ya kuchukua hatua kuvinusuru.

Awali Mbunge wa Tabora Mjini Emmenuel Mwakasaka alisema toka mwaka jana alipotembelea Kiwanda hicho hakuna maendeleo yoyote ambayo yamefanyika na kukifanya kutokuwa na tija kwa vijana na wakazi wa Tabora.

Alisema toka mwaka jana hakuna ajira hata moja iliyoongezeka zaidi ya mfanyakazi mmoja.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (aliyeshika uzi) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Pascal Jotham (mwenye shati nyeusi) leo alipokuwa Mkoani Tabora kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (katikati ) akiwa ameshika mmoja ya kitambaa kilichozalishwa na Kiwanda cha Nyuzi Tabora wakati wa ziara yake Mkoani Tabora jana ya kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa(kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(kulia) wakati wa ziara yake Mkoani Tabora jana ya kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda cha Nyuzi Tabora na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (mwenye shati nyeupe) akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Pascal Jotham (mwenye shati nyeusi) leo alipokuwa Mkoani Tabora kukagua viwanda mbalimbali. Waziri huyo hauridhishwa na utendaji wa kiwanda hicho na kuahidi kupitia Mkataba wa Ubinafishaji wake. PICHA NA TIGANYA VINCENT

WADAU WAKUTANA KUKAMILISHA MWONGOZO WA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI,

$
0
0
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Mashirika ya TNC pamoja na PELUM-Tanzania imekutana na wadau wa uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini kwa ajili ya kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini (Guideline for participatory village land use planning, administration and management in Tanzania) 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kazi hiyo, M kurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen Nindi amewataka wadau hao kuhakikisha Mwongozo huo unakuja na majibu ya kisayansi katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya tabianchi kwa malengo ya kuwasaidia wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua kikao cha kikao kazi kuhusu kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, Morogoro, Octoba 2, 2019
Bw. Peter Lorri, Meneja Uhifadhi nchi kavu kutoka Asasi ya kiraia ya The Nature Conservancy (TNC), akieleza ushiriki wao katika uwezeshaji wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bw. Angolile Rayson Afisa Programu kutoka PELUM Tanzania akielezea ushiriki wao katika Mwongozo wa mpango wa matumizi ya ardhi na namna walivyoshiriki katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja uandaaji wa matumizi ya ardhi katika baadhi ya vijiji nchini Tanzania
Bw. Joseph Osena Kaimu Mkurugenzi, mipango ya matumizi ya ardhi, usimamizi na uratibu akiwapitisha wana kikosi kazi aina 14 za ramani ambazo zinatakiwa kuandaliwa wakati wa upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ambazo zitaifanya mipango hiyo kuwa ya kisayansi zaidi.
Bw. Paulo Tarimo Mkurugenzi wa Mipango ya ya Matumizi ya ardhi Wizara ya Kilimo, akichangia jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bw. Zakaria Faustin Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TNRF akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bi. Albina Burra kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) akijibu na kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau katika mjadala wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Kikao kazi cha kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, kikiendelea.

Elimu ya Mpiga Kura yatua mkoani Tabora

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tabora Boys (Tabora School) wakati Gari la Matangazo la NEC lilipotembelea shule hiyo iliyopo Mjini Tabora kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019. 
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola, akieleza jambo mbele ya mwanafunzi mwenye ulemavu wa macho wa Shule ya Sekondari Tabora Boys Elisha John kuhusu kipaumbele ambacho NEC inakitoa kwa makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu.
 Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likiwa kwenye Shule ya Sekondari ya Tabora Boys (Tabora School) iliyopo Mjini Tabora kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.
 Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Moshi Makuka akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Soko la Isevia lililopo Mjini Tabora kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019. 
 Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Monica Wabukundi (kushoto) akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wafanyabiashara wa Soko la Isevia la Mjini Tabora kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019. 
 Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likiwa kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Tabora  kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019. 
Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likipita mitaa ya Manispaa ya Tabora kuhamasisha wakazi wa manispaa hiyo kujitokeza kuandikishwa au kuboresha tarifa zao ifikapo Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoratajiwa kufanyika mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kuanzia Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.  Picha na Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura-NEC

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YATILIANA SAINI UJENZI WA MJI MPYA KWAHANI ZANZIBAR

$
0
0
Na Rahma Khamis Maelezo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Iddi Haji Makame amewataka wananchi wa Kwahani kutokua na wasiwasi kwa kuvunjiwa nyumba zao kwani Serekali ina dhamira ya dhati ya kuwajengea nyumba bora na za kisasa

Ameyasema katika eneo litakalojengwa mji mpya wa nyumba za kisasa Kwahani wakati wa hafla ya kutiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo Estim Construction LTD ya Dar es salaam .

Amesema kuanza kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya nyumba tano za ghorofa nne kila moja na maduka eneo eneo la chini ni uamuzi wa Serekali wa kuwaondoshea wananchi mazingira ya zamani na kuwawekea ya kisasa.

Aliwaeleza wananchi wa Kwahani kwamba Kampuni iliyopewa kazi za ujenzi wa mji mpya Kwahani inauwezo mkubwa na wamekubaliana watakamilisha kazi hiyokwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amewashauri kuendelea kuvuta subira katika kipindi hicho cha mpito huku wakiweka matumaini ya kuishi katika mazingira bora na yakisasa.

MsimamizI wa ujenzi wa nyumba hizo Lazaro Peter amewataka wnanchi wa eneo la Kwahani kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi ili kazi ziweze kwenda kwa kasi na zikamilike kwa muda uliopangwa.

Aliwapa matumaini makubwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwamba watapata nyumba bora na za kisasa katika kipindi cha muda mfupi ujao.

Sheha wa Shehia ya Kwahani Machano Mwadini Omar ameishauri Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo kuwatumia vijana wa eneo hilo katika kazi zisizohitaji utaalamu ili nao waweze kufaidika na mradi huo.

Alieleza kuwa nyumba zilizovunjwa kwa ajili ya kupisha ujenzi mpya zilikuwa na vijana wengi waliokuwa wakiendesha shughuli zao za maisha na hivi sasa hawana kazi maalum hivyo iwapo watapatiwa kazi wakati wa ujenzi zitawasaidia kimaisha

Baadhi ya wananchi waliovunjiwa nyumba Ali Hamad Haji na Hija Sudi Juma wamesema kuwa kuvunjiwa kwa nyumba zao imeleta shida kidogo lakini wataendelea kuvuta subira na kuitaka Serekali ifanye uadilifu wakati ujenzi utakapokamilika.

Aidha wameipongeza Serekali kwa hatua waliochukua ya kupatiwa mtaji wa kutafuta makazi ya muda huku wakisubiri makazi mapya ya kisasa yatakayowatoa katika hali ya unyonge.

Katika utiaji saini Serikali iliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Iddi Haji Makame na Kampuni ya Estim Construction Co. LTD LTD iliwakilishwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Girdhar Pindolia
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)akitiliana saini na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia kuhusiana na Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)wakikabidhiana hati ya saini na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia kuhusiana na Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)akimkabidhi Ramani ya Ujenzi wa Mji Mpya kwahani Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
 Ramani ya Nyumba za Mji mpya kwahani utakaogharimu kiasi cha Shil,Bilioni miambili hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Benki Ya Exim Yazindua Akaunti Mpya za Akiba

$
0
0
Katika kuboresha huduma zake kwa wateja, Benki ya Exim Tanzania leo imezindua huduma mpya zinazolenga kuhamasisha wateja wake na jamii kwa ujumla kuhusu uwepo wa akaunti zake mpya tatu zinazofahamika kama Akaunti ya ‘Haba na Haba', Akaunti ya ‘Haba na Haba Plus’ pamoja na Akaunti ya ‘Mzalendo’ zote zikilenga kuwawezesha wateja hao kuhifadhi fedha bila makato ya mwezi kwa matumizi ya kuweka akiba na kwa shughuli za kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja jijini Dar es salaam mapema leo, Mkuu wa Idara ya Amana wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda alisema kuwa huduma hizo zinalenga wateja wote  ikiwemo wenye kipato cha chini, kati na kipato kikubwa.

"Akaunti hizi za Haba na Haba zinalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo. Huduma zote zimelenga kutatua changamoto ya ukosefu wa namna iliyo bora ya kuhifadhi fedha miongoni mwa watanzania walio wengi bila kuwa na akiba isiyopungua pitia makato ya kila mwezi,’’ alisema.

Aidha, akifafanua kuhusu akaunti ya Haba na Haba, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye nia ya kuweka akiba kwa ajili ya malengo ya baadae huku akitaja faida zinazombatana na ufunguaji wa akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha riba, hakuna makato ya mwezi na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo,

“Pia inatoa fursa ya kuweka kiwango chochote cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda wowote ambao wateja wataona ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Wateja wataweza dunduliza akiba zao kupitia simu za mikononi kutoka Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye akaunti ya Haba na Haba.’’ alitaja


Ili kufungua akaunti hiyo Bi Agnes Kaganda alisema mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa pamoja na fedha kiasi cha Tsh 50,000 kama kiasi cha kuanzia.

Akizungumza kuhusiana na akaunti ya Haba na Haba Plus, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye kipato cha juu ambao pia kupitia akaunti hiyo wataweza kunufaika na viwango vikubwa vya riba.

 “ Akaunti hii pia inalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo.’’ Alisema huku akitaja faida zitokanazo na ufunguaji wa akaunti hizo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha riba na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo.
“Pia inatoa fursa ya kuweka kiwango chochote cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda wowote ambao wateja wataona ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Kunufaika na riba kubwa jinsi akiba yako inavoongezeka ikiwa sambamba na huduma zilizoongezwa thamani kutoka kwa Mameneja wanaohusika na mahusiano ya wateja. Wateja wataweza dunduliza akiba zao kupitia simu za mikononi kutoka Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye akaunti ya Haba na Haba.’’ alitaja
“Pia ili kufungua akaunti hii mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa pamoja na fedha kiasi cha Tsh 10,000,000 kama kiasi cha kuanzia.,’’ alitaja

Alitaja akaunti ya tatu kuwa ni Mzalendo akaunti ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya kufanya mihamala ya kila siku kupitia benki hiyo masaa 24 na siku saba za wiki bila kukatwa malipo ya kila mwezi  na pamoja na kupatiwa ATM kadi ya malipo bure.

Bi Agnes Kaganda alizitaja faida za akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa mmiliki wake kuweza kuindesha bila kuwekewa kiwango cha chini cha salio, haina ada ya uendeshaji,kupatiwa kadi ya malipo bure pamoja na manunuzi kwenye maduka yote yenye huduma ya POS (merchant Point of Sale) bila gharama yoyote.


‘Pia ili kufungua akaunti hii mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa’’ alisema.

MAABARA BUBU 13 ZAFUNGIWA, HUKU 48 ZIKIPEWA ONYO KALI

$
0
0


Msajili wa maabara binafsi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Dominic Fwiling’afu akikagua hali ya utoaji huduma za upimaji wa sampuli katika moja ya Maabara Binafsi iliyopo Jijini Dodoma.
Timu ya Wakaguzi ikiongozwa na Msajili wa Maabara binafsi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Dominic Fwiling’afu (wakwanza kushoto) wakikagua leseni na miongozo ili kutambua uhalali wa uwepo wa Maabara hiyo binafsi iliyoko Jijini Dodoma.
Moja kati ya Maabara binafsi iliyofungwa kutokana na kutokidhi viwango vya kutoa huduma za upimaji, ikiwemo kutofuata Sheria na miongozo ya uendeshaji wa maabara, Jijini Dodoma.
Mkaguzi wa maabara binafsi kutoka Wizara ya Afya Bi. Mayasa Rico akiongozana na Mtaalamu wa maabara kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Janeth Mkoba Mtaalamu wa Maabara kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Janeth Mkoba wakati wa ziara ya kukagua utoaji huduma za upimaji Jijini Dodoma.
Mkaguzi wa maabara binafsi kutoka Wizara ya Afya Bi. Mayasa Rico akiongozana na Mtaalamu wa maabara kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Janeth Mkoba Mtaalamu wa Maabara kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Janeth Mkoba wakati wa ziara ya kukagua utoaji huduma za upimaji Jijini Dodoma.

………………………………………………

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imezifungia jumla ya maabara 13, ambazo ni sawa na asilimia 21% kati ya Maabara 61 zilizokaguliwa, huku ikitoa onyo kali kwa Maabara 48 kutokana na baadhi ya Maabara hizo kutokidhi viwango vya kutoa huduma za upimaji.

Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi kutoka Wizara ya Afya Bw. Dominic John Fwiling’afu wakati wa ziara ya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma za upimaji katika maabara zilizopo Jiji la Dodoma.

“Tuliweza kufunga Maabara 13, kati ya maabara 61 tulizozikagua, na hizo maabara 13 ni sawa na asilimia 21% ambazo tuliweza kuzifungia, huku Maabara 8 sawa na asilimia 20% ni Maabara zilizo ndani ya vituo vya kutolea huduma kama vile zahanati, na maabara zinazojitegemea ni 5 sawa na asilimia 24%” amesema Bw. Dominic Fwiling’afu

Amesema kuwa Bodi ya Maabara Binafsi katika kutekeleza majukumu yake, inaendeleza mpango wake wa kukagua Maabara Binafsi zote nchini ili kuhakikisha zinatoa huduma kulingana na miongozo ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Aliendelea kusema kuwa zoezi hilo limeanza Jijini Dodoma, huku lengo likiwa kukagua jumla ya Maabara 106 ili kujiridhisha utoaji huduma sahihi kwa wananchi, ikiwemo kukagua kama Wataalamu waliopo wanakidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria.

Pia, Bw. Dominic Fwiling’afu amesema kuwa licha ya kukagua ili kujiridhisha na ubora wa huduma zinazotolewa na Maabara hizo, Bodi hiyo inajukumu la kuangalia ulipaji wa tozo mbali mbali uliowekwa kwa mujibu wa Sheria na kujiridhisha kama Maabara hizo zimetimiza masharti wakati wa uanzishwaji wake.

“Sambamba na hiyo Bodi ya Maabara Binafsi inajukumu la kuangalia ulipwaji wa tozo mbali mbali katika uendeshwaji wa Maabara hizo, kama zote zinafuata miongozo kwa mujibu wa Sheria na kuangalia utendaji na utoaji huduma katika Maabara hizo kama ni salama na sahihi” amesema Bw. Dominic Fwiling’afu

Aidha, Bw. Dominic Fwiling’afu ameongeza kuwa, mbali na kuzifungia baadhi ya Maabara hizo ambazo hazijakidhi vigezo kulingana na Sheria na miongozo, Bodi imeendelea kutoa ushauri kwa wamiliki na Wataalamu wa Maabara ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Mbali na hayo, Bw. Dominic Fwiling’afu ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma kwenye Maabara zilizosajiliwa na kutambulika kwa mujibu wa Sheria, huku akiwaagiza Wamiliki wa Maabara binafsi kuhakikisha wanabandika leseni ya usajili wa Maabara hizo katika eneo la mapokezi ili kiweze kuonekana.

Akielezea sababu za kuzifungia baadhi ya Maabara, Mkaguzi kutoka Bodi ya Maabara Binafsi Wizara ya Afya Bi. Mayasa Rico amesema kuwa kukosekana kwa Wataalamu wa Maabara wenye sifa, kuendesha Maabara hizo bila ya kuwa na vibali, kutokuwa na miongozo na kanuni ya Bodi, miundombinu kutokidhi viwango, kutoa huduma za matibabu na kutoa huduma baadhi ya huduma bila kibali.

“Kukosekana kwa Wataalamu wenye sifa, kuendesha Maabara bila kuwa na vibali,kutokuwa na miongozo na kanuni ya Bodi,majengo kutokidhi viwango kulingana na taratibu, kupima vipimo visivyoruhusiwa bila ya vibali na kutoa huduma za matibabu ndani ya Maabara ni baadhi ya sababu zinazopelekea kufungwa kwa Maabara hizo” amesema Bi. Mayasa.

Kwa upande wake, Mkaguzi kutoka Bodi ya Maabara Binafsi Wizara ya Afya Edinanth Ģareba, amedai kuwa jumla ya maabara 42 tu ndio zimesajiliwa na kutambulika kisheria kati ya Maabara 61 zilizo kaguliwa, ambazo ni sawa na asilimia 69%, huku akisisitiza kusajili Maabara hizo jambo litalosaidia kuzifuatilia Maabara hizo kwa ukaribu na kuzisa idia namna bora ya kutoa huduma ya vipimo kwa wananchi.

Aidha, Edinanth Ģareba aliendelea kutoa onyo kali kwa wauguzi na tabibu wanaopima sampuli za wagonjwa, na kusisitiza kuwa shughuli zote za maabara zinapaswa kufanywa na Mtaalamu wa Maabara tu na si vinginevyo.

HASUNGA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA,MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MITAMBO YA KUBANGUA KOROSHO YA ITALIA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo ya kikazi leo tarehe 2 Octoba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke katika na ujumbe wake mara baada ya mzungumzo ya kikazi katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2 Octoba 2019. Wengine pichani ni Dkt Maurizio Papaleo kutoka kampuni ya Oltremare na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya T Masasi Agro Bi Sarah Masasi
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2 Octoba 2019. Wengine pichani ni Dkt Maurizio Papaleo kutoka kampuni ya Oltremare na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya T Masasi Agro Bi Sarah Masasi


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 2 Octoba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Kilimo Mhe Japahet Hasunga ameeleza kuwa mazungumzo hayo yalijikita zaidi kwenye namna ya kuimarisha zaidi mahusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ambayo yanaendelea kudumu na kuwa na mafanikio makubwa.

Majadiliano hayo yamehusu pia miradi mbalimbali mahususi ambayo inaweza kuibuliwa kwa pamoja na kushirikiana wa pamoja ili kufikisha adhma ya serikali ya awamu ya tano kuwa na maendeleo endelevu kupitia sekta ya viwanda.

Pia majadiliano hayo yalijikita kwenye upanuzi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mkoani Morogoro kwani moja ya kampuni za Uingereza ni wawekezaji katika kiwanda hicho.

Alisema kuwa dhamira ya majadiliano ya kiwanda hicho cha sukari ni kuona namna ya kuongeza uzalishaji mara dufu ya huu wa sasa.Kadhalika, katika majadiliano hayo Waziri Hasunga amesema kuwa wamezungumzia namna ya kuondoa vikwazo vya mashirikiano na vya kufanya biashara au kufanya uwekezaji nchini na hususani vile ambavyo serikali ya Tanzania imeviweka katika mkakati wa kuondoa dosari na vipingamizi katika kufanya biashara nchini vijulikanavyo kama “Blue Print”.

Pia majadiliano kuhusu namna ambavyo serikali imeamua kuja na sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019 na namna ambavyo sheria itatungwa hivyo kupelekea kuwa na sheria ya kulinda kilimo itakayokuwa na vipaumbele mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke amesema kuwa mkutano wake na Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga umekuwa na mafanikio makubwa ukiwa na mtazamo wa mbali wa kuendeleza sekta ya kilimo.

Cooke alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi kwa kipindi kifupi. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili ASDP II.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari.

Mhe Hasunga amesema kuwa Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari kwa ushirikianio ya wazawa amemuahidi kuleta mitambo ya kisasa ili kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kubangua Tani 30,000 kwa mwaka.

Amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utapelekea kufikia lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho zote zinazozalishwa zinabanguliwa hapa hapa nchini.

“Na tukifanya hivyo tayari tutakuwa tumefanikiwa kuitangaza nchi yetu vizuri kwani tutakuwa tunauza korosho ambazo zimebanguliwa hapa hapa nchini”

UJENZI BWAWA LA KUFUA UMEME LA JULIUS NYERERE LIMEZINGATIA MASUALA YA USALAMA WA UHIFADHI – NAIBU WAZIRI KANYASU

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya jarida la Utalii la ” Tanzania Unforgettable” mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani, Mhe. Stewrar Genejip mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wajumbe Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani wakati wa kikao c ha kujadili masuala ya Uhifadhi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodom. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya jarida la Utalii la ” Tanzania Unforgettable” kwa Kiongozi wa ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani, Mhe. Sylvia Kotting- Uhl mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe waKamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani Wengine ni baadhi ya watumishi wa wizara ya maliasili na Utalii.(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

********************************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema nia ya Serikali ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere iko pale pale na ujenzi wake unaendelea kwa kasi huku ukizingatia masuala ya Uhifadhi katika Pori la Akiba la Selous.

Akizungumza leo na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani Mhe. Kanyasu amesema Tathmini ya Athari kwa Mazingira imefanyika na kuonyesha kuwa ujenzi huo ni salama katika shughuli za Uhifadhi.

“Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza mradi huu kwa kutumia fedha zake kutoka vyanzo vya ndani. Mradi huu utachukua eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 1,250 ambalo ni sawa na asilimia tatu (3%) tu ya eneo lote la pori la akiba selous lenye ukubwa wa kilomita za mraba 50,000.” Mhe. Kanyasu alisisitiza.

Mhe. Kanyasu amesema kiwango cha umeme cha megawati 2,100 kitakachozalishwa katika gridi ya Taifa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa misitu inayokatwa kwa kasi kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni.

Aidha, Mhe. Kanyasu amewaeleza Wabunge hao kuwa ujio wa Bwawa hilo la Umeme limepelekea sehemu ya Pori la Akiba la Selous kupandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Tiafa ya Julius Nyerere ambapo kufuatia hali hiyo ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi hiyo utakuwa madhubuti zaidi na ilivyokuwa mwanzo.

Katika hatua nyingine Mhe. Kanyasu amewaeleza Wabunge hao kuwa Serikali ya Tanzania imelichukua suala la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa uzito unaostahili na kwa kutambua athari zake kwa mwaka huu imepandisha hadhi mapori ya akiba manne na kuwa Hifadhi za Taifa na hivyo ulinzi wake wa Hifadhi hizo umeongezeka maradufu

Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe huo Mhe. Sylvia Kotting- Uhl ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa mageuzi makubwa yanayofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala ya Uhifadhi na kuahidi ushirikiano na nchi yake katika kujenga uwezo katika nyanja za kusimamia na kudhibiti taka za kielektroniki, Uzalishaji wa Umeme wa jua na kutoa mwaliko kwa ujumbe wa Tanzania kutembelea Ujerumani

Aidha, Mhe.Sylvia amesema licha ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere bado wataendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika masuala ya Uhifadhi kufuatia juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya tano ya kuendelea kutunza na kuhifadhi maeneo yasiweze kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

TUSIRUHUSU MFUMO MPYA UNUNUZI WA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin cha Mtwara, Oktoba 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo Mtwara, Oktoba 2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



WAZIRI MKUU amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima korosho nchini wahakikishe wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa wadau na wanunuzi.

“Mabadiliko ya mifumo yalitolewa na baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu, Serikali iko macho itawachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu. Tunataka mfumo wenye manufaa ndio utumike.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 2, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mtwara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo, wilayani Mtwara.

Waziri Mkuu amesema msimu wa korosho kwa mwaka huu unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, hivyo ni lazima kwa wakuu wa mikoa inayolima korosho wakajiandaa vizuri ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Waziri Mkuu ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi wa korosho kwa njia ya kangomba.”Kangomba imepigwa marufuku, watakaojihusisha moto utawawakia huko huko . Tunataka wakulima wenyewe ndio wanufaike”

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakulima wa zao la korosho kuendelea kujiimarisha na wahakikishe wanajiwekea akiba kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo kwa sababu. “Serikali itaendelea kusimamia zao hili ili wakulima wapate tija.”

Mapema, Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini na kukagua kazi ujenzi inayoendelea hospitalini hapo, ambapo amesema itakapomalizika itawapunguzia wananchi safari ya kwenda Muhimbili kufuata huduma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imejikita katika kuboresha huduma mbalimbali za wananchi zikiwemo za afya, hivyo wananchi wa Kanda ya Kusini watapata matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Hakuna mashaka wala wasiwasi wa kupata huduma bora za afya kuanzia sasa na kuendelea kwa sababu Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwezesha utaratibu mzuri wa kupata huduma za afya nchini.”

Ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda ya Kusini unatarajiwa kukamilika Agosti 2020 na kwa sasa inajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 15 na tayari Serikali imeshatoa zaidi y ash. bilioni sita.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. Bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya

Alisema historia ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa Mkoani Mtwara ilianzia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi cha Mkoa cha tarehe 16 Januari 1979. Halmashauri Kuu ilijadili na kuazimia kuishawishi Serikali kujenga hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Waziri Ummy aliongeza kuwa hospitali hiyo inajengwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza ilianza mwaka wa fedha 2005/2006 kwa kazi ya upimaji wa mipaka na mwinuko wa ardhi kupitia kampuni ya Beacon Consult Ltd kwa gharama ya sh. 26,000,000 na ilikamilika ndani ya siku 30 za mkataba. Kwa sasa ujenzi huo upo katika awamu ya nne.

Awali,Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo katika eneo la Msijute mkoani Mtwara na kukagua kazi ya ubanguaji pamoja na kuzungumza na watumishi wa kiwanda hicho ambao waliishukuru Serikali kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda.

WAZIRI LUGOLA AAGIZA POLISI KUWASAKA WABAKAJI WALIOKIMBILIA NCHINI ZAMBIA, ASISITIZA DHAMANA ZITOLEWE SAA 24 BILA KUOMBWA RUSHWA WANANCHI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola Akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Matai, Wilayani Kalambo, Mkoa wa Rukwa, jana. Lugola ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, kuwasaka na kuwatia mbaroni wabakaji wanne waliokimbilia nchini Zambia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuhoji Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kalambo, Mkoani Rukwa, Deokresi Mkandala, kuhusu watuhumiwa wanne wa ubakaji waliokimbilia nchi jirani ya Zambia. Lugola alitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, kuwasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola Akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Matai, Wilayani Kalambo, Mkoa wa Rukwa, jana. Lugola ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoani humo, kuwasaka na kuwatia mbaroni wabakaji wanne waliokimbilia nchini Zambia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

…………………….

Na Felix Mwagara, MOHA, Rukwa.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa, kuwasaka na kuwatia mbaroni wabakaji wanne waliokimbilia nchini Zambia.

Lugola alisema wabakaji hao lazima wakamatwe na waletwe nchini kwasababu Jeshi hilo lina mbinu zote za kuwasaka wahalifu hao wanaodaiwa kukimbia kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kubainika kufanya uhalifu huo Wilayani Kalambo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Matai wilayani Kalambo Mkoani humo, Lugola alisema Wilaya hiyo inakabiliwa na matukio mengi ya ubakaji ambapo mpaka sasa Polisi tayari imewatia mbaroni wabakaji 11 na bado hao wanne wanaendelee kutafutwa ili wakamatwe.

Lugola alisema kero alizopewa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara zikiwemo ubakaji kuwa juu pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi kuachishwa masomo kwa ajili ya kufanyishwa kazi wakiwa na umri mdogo, pamoja na wanafunzi kubakwa na kupewa mimba.

“Haiwezekani wahalifu waichezee Serikali ya Rais Dkt. Magufuli, lazima wakamatwe, wasakwe kwa nguvu zote, na mnipe taarifa mtakapowatia mbaroni watuhumiwa hao,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, wahalifu mbalimbali wakiwemo majambazi, kutokana na uimara wa Jeshi la Polisi wamesambaratishwa na wanaendelea kusakwa katika kona zote nchini mpaka jambazi wa mwisho atakapotiwa mbaroni.

Aidha, Lugola aliwataka wananchi kutoa taarifa kwake na kwa viongozi wa Polisi wa Wilaya na Mkoa endapo kuna mwananchi atabambikiziwa kesi au kuombwa rushwa wakati anamuombea dhamana ndugu yake.

Lugola alikiri kuwepo kwa baadhi ya polisi wanaoendelea kuwaomba rushwa wananchi ili wapate dhamana pamoja na kubambikiwa kesi.

“Ndugu wananchi, hili nilishaliagiza na pia naendelea kuliagiza, ni marufuku kwa askari polisi yeyote atakaye muomba rushwa mwananchi ili ndugu yake apewe dhamana, dhamana ni haki ya mwananchi, na uikiingia polisi bure na kutoka ni bure,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola alisisitiza kuwa, dhamana zitolewe saa 24 nchini bila wananchi kuombwa rushwa ya aina yoyote, na kuonya kuwa askari atakayepuuza agizo hilo, ataondolewa ndani ya Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kalambo, Deokresi Mkandala alipokea maagizo ya Waziri Lugola likiwemo la kuwasaka wahalifu hao waliokimbilia nchini Zambia na kuahidi kuyafanyia kazi.

Waziri Lugola anaendelea na ziara yake Mkoani Rukwa kutatua kero mbalimbali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Wilaya zote mkoani humo.

NDITIYE AKATAA TAARIFA YA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mwanza, Godwin Barongo akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye waakti wa ziara yake Wilayani humo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mwanza, Godwin Barongo wakati wa ziara yake wilayani Sengerema, Mwanza
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Silvanus Bulapilo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake wilayani humo mkoani Mwanza
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Sengerema kuhusu utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi wakati wa ziara yake mkoani Mwanza 

…………………

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiiano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameikataa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wakati wa ziara yake wilayani Sengerema mkoani Mwanza 

Nditiye ameikataa taarifa hiyo ya utekelezaji iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Godwin Barongo wakati akiwasilisha taarifa yake kwa kuwa haina utekelezaji wowote uliofanyika wa kuchagua majina ya mitaa ili Serikali iweze kuweka namba za nyumba, vibao kwa maelengo ya kukamilisha anwani za makazi na postikodi ili kila mwananchi apate anwani yake na atambulike mahali anapoishi

Amefafanua kuwa mapema mwanzoni mwa mwaka huu aliambatana na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara na kuwa na kikao cha pamoja baina ya madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa ambapo wataalamu wa Wizarani na wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) waliendesha mafunzo ya kujenga uelewa kwa madiwani na watendaji kwa malengo ya kuwawezesha kufanikisha kazi ya kuchagua majina ya mitaa ili kuweza kukamilisha anwani ya makazi kwa wananchi kwa kuwa tayari nchi nzima kila kata ina postikodi ambapo tangu wakati huo hakuna utekelezaji wowote uliofanyika

“Tunachohitaji ni majina ya mitaa, ninasikitishwa na suala la madiwani wanapopata ugumu wa kuchagua majina ya mitaa, ni lazima madiwani wakae tupate majina ya mitaa na ulikuwa na taarifa kuwa tunakuja ila hukufanya jitihada zozote kutekeleza,” amesema Nditiye

Amesema kuwa Serikali itafikiria upya na kuamua kuchukua madaraka ya madiwani ili kuweka majina ya mitaa kwa kuwa sasa hivi simu zinatumika kufanya miamala mbali mbali na hii itasaidia huduma na bidhaa zifikishwe kwa wananchi kwa kuwa anwani za makazi na postikodi ni muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi yetu na tunataka kila mwananchi atambulike anapoishi na tunahitaji utekelezaji kwa vitendo wa mpango huu kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla

Afisa Masoko wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Rose Kavemba amesema kuwa kinachohitajika ni kurasimisha mitaa, kupata majina kutoka kwa viongozi wa vijiji, mitaa na kwa madiwani kisha kutenga itakayowaongoza kufanya utekelezaji kwa kuwa kuna changamoto mkiwaachia madiwani wanavutana

Naye Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Makazi na Postikodi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Jampyon Mbugi amesema kuwa ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa mpango huo, kila halmashauri inatakiwa iunde kamati kuendana na mwongozo wa mpango huo na kurasimisha mitaa ili kupata majina ya mitaa na barabara amabpo yanatakiwa yatoke kwa wakazi husika na kuridhiwa na mamlaka husika kisha kazi ya kuweka nguzo na namba za nyumba inaanza na taarifa zinakusanywa ili kuwekwa kwenye kanzi data na baadae anwani hizo zinaanza kutumika mathalani kwa kufanya biashara mtandao

Barongo ameomba radhi na kuahidi kwa Nditiye kuwa watakaa kikao na kukubaliana majina ya mitaa. Vile vile, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Silvanus Bulapilo amesema kuwa majina ya mitaa yapo na mitaa ipo ila anashangaa ugumu unatokea wapi wa kutekeleza mpango huo

“Nashangaa ugumu unatoka unatoka wapi wa kutekeleza hili, nikuahidi tutatekeleza, niombe nikuahidi kuwa tutafanya hivyo,” amesisitiza Bulapilo

Nditiye amewataka viongozi na watendahi wote kushirikiana na madiwani wote kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kuhakikisha kuwa wanatekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi ili Serikali iweze kuwahudumia wananchi wake

MABARAZA YA ARDHI YA KATA NA VIJIJI YASIYOTENDA HAKI MAFIA YAVUNJWE-DKT MABULA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Baleni wilayani Mafia mkoa wa Pwani alipokwenda kusikiliza kero za ardhi katika eneo hilo akiwa katika ziara yake ya siku mbili katika wilaya hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
Mwananchi Hassan Omar maarufu mzee wa Lumbesa mkazi wa Dagoni Mafia akimuonesha nyaraka Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuhusiana na mgogoro wa ardhi wakati Dkt Mabula alipofanya ziara wilaya ya Mafia kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua Majalada ya Ardhi katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia jana wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnenduma na Kulia ni Afisa Ardhi Chuchu Ochere.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia baadhi ya Nyaraka za umiliki wa ardhi kutoka kwa Hassan Mohamed (Kushoto) na Mwanangano Mohamed wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya ya Mafia jana (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

…………………………


Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda kuyavunja Mabaraza yote ya Kata na Vijiji ya ardhi yasiyotenda haki wakati wa kutoa maamuzi katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana akiwa katika ziara yake ya siku mbili wilayani Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi.

Alisema, kutokana na kero nyingi za ardhi alizozipokea katika ziara yake hiyo wilayani Mafia amebaini Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya hiyo hayafanyi kazi zake vizuri na wajumbe wake wamekuwa wakiyatumia kutoa maamuzi yasiyotenda haki.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kadri Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia yanavyofanya vibaya katika utoaji maamuzi yake basi hata uanzishwaji Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya hiyo halitafanya vizuri katika utendaji wake.

‘’Ukiwa na watu wasioweza kusimamamia haki itakuwa shida sana, Mkurugenzi hakikisha Mabaraza ya Ardhi katika Kata na Vijiji yasiyofuata taratibu na kutoa haki kwa walalamikaji unayavunja na kuteua wajumbe wapya’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi alitaka kupitiwa upya Mabaraza yote ya ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia hasa yale yanayolalamikiwa na kubainisha kuwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko tayari kutoa Msajili wa Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba nchini ili atoe elimu katika Mabaraza hayo kwa lengo la kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Alisema, Mabaraza ya ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia hayatendi haki na wakati mwingine Baraza la Kata linachukua kesi ya Baraza la Kijiji lengo likiwa kutotenda haki kwa walalamikaji.

Baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi kuwa wajumbe wake hawatendi haki wakati wa kutoa maamuzi na hivyo kuonesha dhahiri uwepo dalili za rushwa.

Mohamed Shaban alimueleza Dkt Mabula kuwa, Mabaraza ya ardhi ya Kata wakati mwingine hayatendi haki na kumtaka anayeshindwa kesi kwenda Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya la Mkuranga huku wakijua mlalamikaji atashindwa kwenda Mkuranga kutokana na changamoto za usafiri na hivyo kupoteza haki yake.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda alieleza kuwa Mabaraza ya ardhi ya Kata na Kijiji katika wilaya hiyo yapo na yanafanya kazi na wajumbe wake wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ingawa alieleza changamoto iliyopo Baraza katika kata ya Kilindoni ambalo alilileleza kuwa badala ya kuatatua matatizo limekuwa chanzo cha migogoro kwa kuwa wakati mwingine hufanya mashauri yaliyo nje ya kata yake na suala hilo tayari alishalitolea agizo la kuvunjwa kwa baraza

NDITIYE ASHUHUDIA KUWASILI KWA VIFAA VYA UJENZI WA MELI MPYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitoka kukagua ukarabati wa meli ya MV Victoria wakati wa ziara yake mkoani Mwanza. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akisikiliza kwa makini maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV Victoria (inayoonekana nyuma yao) kutoka kwa Meneja wa Ujenzi wa Miradi, Mhandisi Abel Gwanafyo wakati wa ziara yake mkoani Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli, Erick Hamisi akitoa taarifa ya kuwasili kwa shehena ya kwanza ya vifaa vya ujenzi wa meli mpya ya Ziwa Victoria kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia mbele) wakati wakisubiri kupokea vifaa hivyo, Mwanza
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo wakati wa ziara yake mkoani Mwanza. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiwashukuru madereva wanajeshi wa Tanzania na wakandarasi wa Korea walioleta shehena ya kontena 17 (zinazoonekana nyuma yake) za vifaa vya kujenga meli mpya ya Ziwa Victoria baada ya kuwasili kutoka bandari ya Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
…………………………

Na Prisca Ulomi, Mwanza

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameshuhudia kuwasili kwa shehena ya kwanza ya kontena 17 kati ya 300 zenye vifaa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya ya Ziwa Victoria mkoani Mwanza itakayogharimu shilingi bilioni 89

Nditiye amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametimiza ahadi yake aliyoitoa miaka minne iliyopita kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa ya kuwajengea meli mpya baada ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba miaka 23 iliyopita

Ameongeza kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeleta wataalamu watakaoshirikiana na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na mkandarasi kutoa Korea ambayo ni Kampuni ya Gasentec Ltd wanayojenga meli hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa meli hiyo unakamilika kwa wakati ili watanzania watumie huduma ya usafiri huo katika kuhakikisha kuwa wanasimamia na kutekeleza malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwatumikia watanzania

Nditiye amempongeza Kanali A. Fuko, Mkuu wa Msafara wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa niaba ya madereva wanajeshi kwa kazi kubwa wanayoifanya siyo tu ya kulinda usalama wa nchi yetu bali hata ya kushiriki shughuli za maendeleo kwa kusafirisha shehena ya awali ya kontena 17 kati ya 300 kutoka banadari ya Dar es Salaam na kuleta Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya ambapo wametumia siku tatu tu badala ya siku saba ambazo huwa zinatumika kusafirisha mizigo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Erick Hamisi amesema kuwa ujenzi wa meli hiyo utagharimu shilingi bilioni 89 ambapo hadi sasa tayari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelipa shilingi bilioni 30 kwa mkandarasi wa kujenga meli hiyo ambayo ni kampuni ya Gasentec Ltd kutoka Korea

Hamisi amefafanua kuwa mell hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 mizigo tani 400 na magari 20 ambapo itakuwa na urefu wa mita 92.6, urefu wa kwenda juu mita 11.2 ambazo ni sawa na ghorofa nne, upana wa mita 17 na itakuwa ni meli kubwa kwa ukanda wa Ziwa na itachukua muda wa miezi 24 kukamilika ambapo hadi sasa tayari miezi 12 imeisha na inatarajiwa kuajiri watanzania 250

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gasentec Ltd, Donganyang Kwak amesema kuwa kila mwezi wanategemea kupokea shehena ya kontena 20 hadi 30 kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo na malengo yao ni kuhakikisha kuwa ujenzi unakamilika na watajitahidi kwa juhudi zao zote ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya meli hiyo itakapokamilika

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema kuwa ujenzi wa meli hiyo utakapokamilika na kuanza kutoa huduma kwenye kanda ya Ziwa utaongeza chachu ya maendeleo ya Mkoa wa Mwanza na utafungua fursa mbali mbali na kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa letu

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Salumu Mkalli amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeamua kuwatumikia watanzania hivyo tumuunge mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa ameamua na anatekeleza ambapo mradi huu wa ujenzi wa meli utakapokamilika hautanufaisha watu wa Mwanza tu bali na wa sehemu nyingine

Katika hatua nyingine, Nditiye amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV. Victoria na ujenzi wa chelezo. Aidha, amewataka wakandarasi wanaohusika kuhakikisha kuwa wanakamilisha kazi hizo kwa wakati na wafanye kazi usiku na mchana ili kuendana na muda waliopewa na Serikali wa kukamilisha kazi

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TAASISI MBALIMBALI KUBORESHA AFYA YA WANYAMA

$
0
0
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha inaboresha afya za mifugo na upatikanaji wa madawa kwa wakati ili wafugaji waweze kunufaika na mifugo yao.

Akizungumza mara baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya ZOETIS A.L.P.H.A katika Bara la Afrika Dkt. Gabriel Varga ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema ili kufuga kisasa ni muhimu kwa wafugaji kushirikishwa na wataalamu katika kutambua magonjwa ya mifugo yao na kupatiwa elimu ya namna ya kuwahudumia mifugo.

Ameongeza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga vyema katika katika kutekeleza majukumu yake kwa vitendo ili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana katika sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akiwa katika mazungumzo na Dkt. Varga amesema taasisi hiyo ambayo katika bara la Afrika inafanya kazi na taasisi ya Bill and Melinda Gates (BMGF), malengo yao yanafanana na mikakati ya wizara katika kuhudumia ukuzaji viumbe kwenye maji hivyo wizara inatarajia katika kipindi cha miaka miwili au mitatu itafanya kazi na taasisi hiyo ya ZOETIS A.L.P.H.A. katika sekta ya uvuvi.

Dkt. Tamatamah amefafanua kuwa ufugaji samaki kwa sasa hapa nchini unawekewa kipaumbele katika kuendeleza na kuongeza uzalishaji wa samaki kwa kuwa mahitaji ya ulaji wa samaki yameongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ongezeko la idadi ya watu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya ZOETIS A.L.P.H.A katika Bara la Afrika Dkt. Gabriel Varga amewaambia makatibu wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel anayeshughulikia Mifugo na Dkt. Rashid Tamatamah anayeshughulikia Uvuvi, kuwa taasisi yake inatarajia kuanzisha maabara hivi karibuni katika mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Mwanza na Morogoro ili kuboresha afya ya wanyama.

Aidha. Dkt. Varga amefafanua kuwa taasisi hiyo ambayo kwa sasa inahudumia nchi zaidi ya 100 kote ulimwenguni imekuwa ikiwasaidia wafugaji wa bara la Afrika kwa kuwapatia elimu ya huduma ya wanyama ili waweze kufuga kwa tija.

Mazungumzo hayo yamehudhuiriwa pia na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Hezron Nonga, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madala na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt. Bedan Masuruli wote kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

SERIKALI YATAJA MAENEO YANAYOASHIRIA KUVUMBULIWA RASILIMALI YA MAFUTA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.  Kongamano hilo linawakutanisha wadau zaidi ya 592 kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo Austaralia, Brazili, Canada, China, Visiwa Vya Comoro, Ghana. Mengine ni Itali, India, Japani, Kenya, Msumbiji, Netherand, Nigeria, Afrika Kusini, Oman, Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Nishati na Madini Meldard Kalemani akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea. 

 Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2. Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora. 

 Dk Kalemali ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi. “Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani. 

 Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi. "Tunawakaribisha wawekezaji zaidi wajitokeze katika sekta hii ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na kuzidi kutoa ajira wa jamii," amesema. Meza kuu: Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim, Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na Bi. Irene Batete aliyemwakilisha waziri wa Nishati Nchini Uganda. Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Bi. Irene Batete aliyemwakilisha Waziri wa Nishati Nchini Uganda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim ambao ndiyo waandaaji akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. 
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.

CHADEMA MBEYA WAPONGEZA HARAKATI ZA NAIBU SPIKA DR. TULIA ACKSON

$
0
0
Naibu Spika Dr. Tulia Ackon kwa kushirikiana na taasisi yake ya Tulia Trust amefanya ziara katika Shule ya Sekondari Ivumwe iliyopo mkoani Mbeya ambapo ametoa msaada wa Shilingi Milion mbili na laki tano (Tsh. 2,500,000/-) aliyokuwa ameahidi katika shule hiyo ili kusaidia uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo ikiwemo uchakavu wa madarasa, maabara pamoja na bweni la watoto wa kike.
Aidha, Dr. Tulia amesisitiza kwamba kupitia taasisi hiyo ya Tulia Trust ambayo inajikita katika kusaidia sekta mbalimbali nchini ikiwemo Elimu na Afya ataendelea kutoa misaada mbalimbali katika Shule ikiwa ni sehemu ya kushiriki kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Akizungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo Dr. Tulia amesema “Mimi nimetembelea shule nyingi sana hapa nchini, watoto wa shule hii ya Ivumwe mazingira yenu ni mazuri mno ukilinganisha na shule nyingine, kwamaana hiyo hakuna sababu yoyote ya kufeli, natamani sana kuzisikia hadhithi nzuri za ufaulu. Niwaombe sana watoto wazuri msome kwa bidii ili muweze kulisaidia taifa, hata mimi hapa mnaponiona na huu Udaktari wangu sio kanakwamba nimepewa tu, hapana, ni Udaktari wa kisomo hivyo na nyie mkazane kusoma ili kutimiza ndoto zenu”-Dr. Tulia
Katika hafla ya kukabishi fedha hizo Diwani wa Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki (CHADEMA) amesema maendeleo hayana itikadi hivyo anampongeza Dr. Tulia kwa kuchangia maendeleo katika Kata yake kwani ni mara ya tatu sasa Naibu Spika anachangia shughuli za maendeleo katika Kata hiyo. “Nakushukuru Naibu Spika kwa shughuli unazozifanya kwani katika shule hii inayosimamiwa na CCM mimi nina ndugu zangu 52 wanaosoma hapa na sifa inayopatikana ni ya Mwakibete na Mbeya kwa ujumla” alisema Mwampiki



Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images