Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA YA NYASA AANZISHA “UCHAGUZI CUP”

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, ameanzisha ligi ya Mpira wa miguu ya “ Uchaguzi Cup” yenye lengo la kuhamasisha wananchi, kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, utakaofanyika novemba 24 mwaka huu. 

Ligi ya “ Uchguzi cup ” inafanyika katika viwanja vya michezo vya mbamba-bay na Kilosa Wilayani hapa na inashirikisha timu kumi na tatu (13) za mpira wa miguu za wilayani hapa. 

Akifungua Ligi hiyo, jana katika uwanja wa Polisi Mbamba-bay wilayani hapa Bi Chilumba, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kujitokeza kwa wingi katika michezo ya ligi hiyo, kwa kuwa watapata burudani ya mpira wa miguu bila kiingilio chochote. 

Alifafanua kuwa, lengo la mashindano ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, na kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu kwa kuwachagua viongozi wa Vijiji na Vitongoji. 

Bi Chilumba aliongeza kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni wa muhimu sana kwa kuwa viongozi hawa ndio wanaoishi moja kwa moja na wananchi na wanatoa maamuzi kwa ngazi za Serikali za Mitaa hivyo wananchi wanatakiwa kuhamasika, na kuwachagua vongozi wanaowafaa. 

Alitoa wito maalum kwa vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za mitaa kwa kuiga mfano wa Mh.Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli kwa kuwa Teuzi nyingi anazozifanya zinajumuisha vijana wengi. 

Mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo ulizikutanisha Timu za Likwilu fc na Linda Fc na matokeo timu hizo zilikwenda suluhu ya magoli mawili kwa mawili.


TAMASHA KUBWA LA KUMKUMBUKA MWALIMU JULIUS NYERERE KUFANYIKA BUTIAMA KUANZIA OKTOBA 8 HADI OKTOBA 14, JAJI WARIOBA MGENI RASMI

0
0





Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

KAMPUNI ya Miranda Investment kwa kushirikiana na Serengeti Media Centre, Chuo cha Utalii Serengereti na Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya Wazanaki imeandaa tamasha kubwa la Kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambalo linatajia kufanyika kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 14 Butiama Musoma mkoani Mara ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa kwanza wa Rais Joseph Warioba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanyika kwa tamasha hilo na kwamba ni miaka 20 tangu Mwalimu Julius Nyerere, hivyo wao kampuni hiyo wameona kuna umuhimu wa kufanya tamasha hilo ambalo pamoja na mambo mengine litawaleta Watanzania pamoja.

Amesema tamasha hilo ambalo limebeba kauli mbiu ya Uadilifu na Uchapakazi ni dira ya kuufikia uchumi wa viwanda na kwamba Mwalimu Nyerere alipambana sana katika ukombozi wa Taifa la Tanzania. Mgeta ameongeza wakati taifa linamkumbuka Mwalimu Nyerere, kupitia tamasha hilo wananchi kutoka Mkoa wa Mara na mikoa jirani watapata burudani za kila aina kupitia michezo mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa mwaka huu.

Kwa upande wake Mtaribu wa Tamasha hilo Kulwa Karedia amesisitiza kama Watanzania wanavyotambua kila ifikapo Oktoba 14 ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kwa mwaka huu maadhimisho hayo ni ya 20.

Amesema kuwa maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali, vikundi na watu binafsi, lengo kubwa ni kumkumbuka mwasisi wa taifa letu kutokana na kujitoa kwa kila namna dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni na hatimaye kuleta uhuru ambao tunajivunia kwa kuupata bila kumwaga damu.

"Tunatambua mwalimu Nyerere alilifanyia taifa hili mambo ambayo hayawezi kufutika kamwe machoni mwa Watanzania. Kutokana na msingi huo, tuliopo tunapaswa kumuenzi kwa kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya. Kwa kutambua uzito wa hili, Miranda Investment, Serengeti Media, Chuo cha Utalii Serengeti na Kituo cha Kuendeleza Utamaduni wa Wazanaki, tumeandaa tamasha na kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambalo litaanza kuunguruma Oktoba 8- 14 kijijini Butiama mkoani Mara,"amesema Karedia.

Pamoja na Serikali kuwa na siku ya kitaifa ambayo inaadhimishwa mwaka huu mkoani Lindi kwa shughuli mbalimbali, zikiwamo sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru ambao Mwalimu Nyerere aliuasisi, tumeona ni jambo jema na la msingi tuungane na wakazi wa kijiji cha Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla kukumbuka siku hiyo muhimu kwa kufanya tamasha la burudani kwa michezo mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine amesema kubwa ni kuwapo kwa mashindano ya riadha yaliyopewa jina la Mwalimu Nyerere Historical Marathon yakiwakilisha wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara na nje ya mkoa huo."Tamasha hili tutashirikisha pia wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara, Tarime, Bunda, Musoma, Butiama na Serengeti na mikoa ya jirani kama Mwanza, Simiyu na Arusha,"amesema.

Kuhusu matukio yatakayofanyika katika tamasha hilo Karedia amesema ni riadha, Mbio za Kilomita 10, Mbio za Kilomita Tano kwa vijana kati ya miaka 13 - 18.Pia kutakuwa na mbio za kilomita mbili na nusu , mbio za kujifurahisha
Karedia amesema mbio zote zitaanzia Uwanja wa Mwenge Butiama kupitia Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kuelekea Barabara ya Kiabakari ambayo Mwalimu Nyerere aliitumia wakati wa kuunga mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka 1967.Pia kutakuwa na mbio za baiskeli, bonanza la mpira wa miguu na kuongeza kuwa timu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara zimealikwa kushiriki, wakiwamo mabingwa watetezi Butiama Stars 

Pia kutakuwa na mpira wa pete ambapo Karedia amesema kwa mwaka huu wameboresha zaidi mashindano hayo kwa kuongeza mchezo wa mpira wa pete, maana wanaamini mwalimu alikuwa mpenzi wa kila kundi. Tunagetemea timu kutoka wilaya zote zitafika Butiama.

Amefafanua kuwa mchezo wa bao nao utakuwapo kwenye tamasha hilo hasa kwa kuzingatia Baba wa Taifa, alikuwa mchezaji hodari wa mchezo huu, kutokana na hali hiyo, tumealika timu zaidi ya sita kutoka Sengereti, Musoma, Tarime na Butiama. Hapa tunagemewa kivumbi kutimka kwa sababu kuna wazee waliobebea, wataonyeshana umwaba hapa.

Wakati huo huo kutakuwa na ngoma na kwaya ambapo vikundi vya ngoma za asili na kwaya vitashiriki. "Tunagetegea kuwa na wageni mbalimbali wa kitaifa na kitamaifa. Nasema hivi kwa sababu tumefanya mawasiliano na balozi kadhaa kama ule wa Marekani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Msumbiji,Afrika Kusini na China,"amesema Karedia .

Wakati huo huo amesema washiriki zaidi ya 1,000 kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mara na maeneo jirani wanatarajiwa kushiriki tamasha hili Tunamshukuru Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Mara, Profesa Sospter Muhongo kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mno wana Mara kujitokeza.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais Jaji Joseph Warioba. Pia wanatarajia uwapo wa wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine kutoka mikoa ya jirani.

Karedia ametoa mwito kwa kuwaomba wakazi wa Mkoa wa Mara na mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi kushiriki tamasha hili ili kumuenzi Mwalimu Nyerere wa vitendo, tukiongozwa nakauli mbiu ya mwaka huu katika tamasha hilo inasema hivi: Uadilifu na uchapakazi ni dira ya kufikia Tanzania ya Viwanda

 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi  Kumbukumbu ya Utamaduni wa Zanaki Mashaka Mgeta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu tamasha la kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere linalotarajia kufanyika Butiama wilayani Musoma mkoani Mara .Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo Kulwa Karedia.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazaki Mashaka Mgeta(kushoto) akiwa na Mratibu wa tamasha la kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajia kufanyika Butiama mkoani Mara
 Mratibu wa Tamasha la Kumbukumbu ya miaka ya 20 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Julius Nyerere, Kulwa Karedia(kulia) akizungumzia ratiba ya  shughuli zitazofanyika wakati wa tamasha hilo linalotarajia kuanza Oktoba 8 hadi Oktoba 14 mwaka huu Butiama mkoani Mara .Kushoto Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta.

MAPATO TRA YAPAA,YAKUSANYA TRILIONI 1.767 KWA MWEZI SEPTEMBA 2019.

Shindano la Kuipa jina Sayari-nje ya Tanzania

TAASISI YA TULIA TRUST YASAIDIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU MKOANI MBEYA.

0
0
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson kwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust amefanya ziara katika shule mbalimbali mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu ambapo miongoni mwa shule hizo ni pamoja na Shule ya msingi Jitegemee ambayo ameipa mchango wa Shilingi Milion mbili (Tsh 2,000,000/-) ili kusaidia ukarabati wa miundombinu mibovu katika shule hiyo.

 Pia, baada ya kusomewa changamoto nyingine zikiwemo ubovu wa madarasa, ukosefu wa uzio na ofisi za waalimu, Dkt. Tulia ameahidi kutoa msaada zaidi kwenye shule hiyo kwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust.

Katika hatua nyingine, Dkt . Tulia ametoa mchango wa Shilingi Milion moja na laki sita (Tsh 2,400,000/-) katika Shule ya Msingi Nzovwe iliyopo Jijini Mbeya ili kusaidia pia uboreshaji wa miundombinu isiyo rafiki katika shule hiyo ambapo pia alisomewa changamto zingine ikiwemo ubovu wa madarasa, uzio wa shule n.k

“Nimesomewa changamoto nyingi zilizopo katika shule zetu hizi ambapo niseme tu sisi kama Tulia Trust tumezipokea na tutaenda kuona ni namna gani basi tunaweza kuzifanyia kazi ili basi watoto wetu hawa waweze kuzoma katika mazingira yaliyo bora na salama”-Dr. Tulia


TAKUKURU Yamnasa mtuhumiwa waliemsaka tangu mwaka 2017

0
0
Charles James, Michuzi TV
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemkamata Be Emmanuel Mziwanda ambaye alikua Afisa Afya Mkuu na Mratibu wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambaye wamekua wakimsaka tangu Juali, 2017.

Mziwanda anakabiliwa na mashtaka ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri na kuisababishia hasara Serikali ya Shilingi Milioni 15 ambazo TAKUKURU inasema alizipata kwa njia ya udanganyifu.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema baada ya kufanya uchunguzi wao na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani Bw Mziwanda alitoweka hadi walipomkamata Oktoba mwaka huu akiwa msibani wilayani Mpwapwa.

" Tunapenda kuwashukuru wananchi wote na wadau walioshirikiana na Taasisi yetu kufanikishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu, tutamfikisha Mahakamani muda wowote baada ya taratatibu za kisheria kukamilika," Amesema Kibwengo.

Aidha Katika robo ya Julai hadi Septemba 2019, TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imeendelea kutekeleza majukumu yake ambapo wametoa elimu ya rushwa kwa Wananchi hasa Katika kipindi hiki ambacho uchaguzi wa Serikali za Mitaa unakaribia.

Amesema TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, imefuatilia miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 46 katika sekta za ujenzi wa miundombinu, elimu, afya, maji na kilimo ambapo wamegundua viashiria vya uwepo wa uvunjaji wa taratibu kwenye utekelezaji wa miradi minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.9.

" Tumeanzisha uchunguzi kuona iwapo kuna vitendo vya rushwa Katika miradi hiyo, Pia tumeingilia kati utekelezaji wa mkataba wa uundwaji wa Kampuni kati ya Halmashauri moja na Taasisi binafsi kwa ajili ya kununua maeneo, kuyapima na kuyauza," Amesema Kibwengo.

Amesema Katika eneo la Kupambana na rushwa kwa kipindi tajwa wamepokea jumla ya tuhuma 155 na makosa yahusianayo ambapo uwiano wa tuhuma hizo kisekta ni kama ifuatavyo.

Kata, Mitaa na Vijiji 39%, Ardhi 13.5%, Elimu 12.3%, Mahamama 7.7%, Wizara 5.8%, Polisi 5.2%, Sekta binafsi 5.2%, Maji 4.5%, ambapo tuhuma zilizobakia zinahusu sekta ya Afya, Uhamiaji, TARURA na vyama vya Siasa.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Dodoma, Sosthenes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya robo ya Julai na Septemba ambapo alieleza kukamatwa kwa mtuhumiwa ambaye wamekua wakimsaka kwa zaidi ya miaka miwili.

Serikali yazindua mafunzo ya kilimo cha Mbogamboga, kugharimu Bilioni 2.5

0
0
Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imewataka vijana nchini kutumia fursa zinazopatikana katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza changamoto ya ajira ambayo inawakabili vijana wengi.

Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako jijini Dodoma leo wakati akizindua mradi wa kuimarisha ujuzi  na uwezo wa kutoa mafunzo katika sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda uliodhaminiwa na Nchi ya Uholanzi utakaogharimu kiasi cha Sh.bilioni 2.5.

Prof Ndalichako amesema mafunzo hayo yatanufaisha vyuo vitatu ambavyo ni Chuo cha Kilimo Tengeru mkoani Arusha, Chuo cha Kilimo Uyole Mbeya na Chuo cha Kilimo Mahinya mkoani Ruvuma na baadaye vitatoa elimu ya ujuzi katika vyuo vingine vya ufundi.

Amesema hawawezi kufikia  uchumi wa viwanda kama hawana wataalamu wazuri waliobobea katika sekta ya viwanda.

"Kilimo ili kilete ufanisi ni lazima walime kisasa na kuachana na kilimo cha mazoea cha kutumia nguvu na ardhi kubwa badala ya kutumia maarifa, katika programu hii tunalenga wanachi wetu watumie maarifa zaidi na si nguvu kama ilivyo hivi sasa, tunaishukuru sana nchi ya Uholanzi kwa ufadhili na ushirikiano huo," Amesema.

Prof Ndalichako amewataka vijana kuhakikisha ujuzi wa mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kwa kuanzia katika vyuo vitatu unatumika na kutekelezwa vizuri ili kuleta tija.

Waziri Ndalichako amesema Taifa la Uholanzi limefanikiwa sana katika kilimo na inaingiza pato kubwa kwa kupitia kilimo, hivyo kupitia chuo chao na ufadhili huu Tanzania watajifunza namna wenzao walichofanya na kufanikiwa.

Nae, Kaimu Katibu Mtendaji wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Dk.Adolf Rutayunga, alisema tayari vyuo 530 vya binafsi na serikali vimesajiriwa tangu kuanzishwa kwa NACTE, na vyuo 87 vya Sayansi na teknolojia shirikishi vimesajiliwa.

"Leo pia tunapokea ufadhili mwingine wa zaidi ya Sh.bilioni 2 kwa ajili ya mafunzo katika sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda ambapo vyuo vitatu vitakwenda kunufaika," Amesema.

Akimuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la NACTE, John Kandoro, Winfrida Rutahinurwa, alisema, baraza limetoa kpmputa 400 katika vyuo mbalimbali vya elimu ya ufundi hapa nchini ili kuviwezesha kwenda ya mfumo wa sayansi na teknolojia.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako (katikati) akiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Jevoen Verheul wakionesha cheti kinachoashiria uzinduzi wa mafunzo ya kilimo cha Mbogamboga jijini Dodoma.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako (katikati) na Balozi wa Uholanzi nchini, Jevoen Verheul wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya kilimo cha Mbogamboga jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki na wadau waliojitokeza Katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo jijini Dodoma.

Stanbic Bank Tanzania drills down on the Tanzania Oil and Gas Congress

0
0
Stanbic Bank Tanzania has announced their support for the third Tanzania Oil and Gas Congress that will take place in Dar es Salaam between the 2nd and 3rd October, 2019 at the Julius Nyerere International Convention Center (JNICC).

“It’s an honour to participate and attend the congress as a panellist, Stanbic Bank is excited to be part of conversations that will further the oil and gas sector and the development of Tanzania’s economy”, said the bank’s Head of Oil and Gas, Mr. Elias Ngunangwa.”

Stanbic Bank Tanzania has vast knowledge, expertise and experience in advising and arranging capital for projects in the sector. “We believe that financial institutions have an important role in facilitating investment in sectors such as oil and gas to promote industrialization and economic growth. We are committed to being a key player in supporting the government and stakeholders to utilize the resource effectively,” he added.

Tanzania is endowed with a proven 57 trillion cubic feet of natural gas reserves, which is the highest among the East African Community (EAC) partner states. Once commercialized, the gas will have a significant impact to the economy of Tanzania through foreign revenue earned. Mr. Ngunangwa elaborated that, the sector is a game-changer in the growth of Tanzania’s economy, particularly industrialization.

The conference aims to foster partnerships and share knowledge on the investment opportunities and explore strategies to boost industrialization in the region. More than 300 Stakeholders are also expected to showcase upcoming oil and gas projects in Tanzania. The conference will provide companies with partnership opportunities and financial advisory insights to help them advance in the sector.

Wambura aandika barua kwa DPP kuomba msamaha

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
ALIYEKUWA  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa  yanayomkabili mahakamani hapo.

Wambura ambaye alifikishwa  kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Februari 11, mwaka huu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 17 yakiwemo ya kutakatisha zaidi ya Sh. Milioni 100.

Wambura amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina kuwa, ameandika barua hiyo kufuatia agizo la msamaha uliotolewa na rais hivyo ameuomba upande wa mashtaka  wafuatilie barua hiyo ili apate majibu kwa haraka.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai watafuatilia suala hilo ili wapate majibu mapema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 16,2019

Mapema, kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwani upelelezi wake bado haujakamilika.

Katika mashtaka hayo 17; shtaka moja ni la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo; mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha haramu.

Katika shtaka la kwanza ambalo ni la kughushi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 6, 2004, sehemu isiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Siku hiyo, Wambura kwa nia ya kutapeli alitengeneza barua ya kughushi ambayo haina kumbu kumbu namba akionyesha imeandikwa na E Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.

Katika shtaka la kutoa na kuwasilisha nyaraka ya uongo, mshtakiwa alitoa barua iliyokuwa haina kumbu kumbu namba ya Julai 6, 2004, akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na E. Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck System Ltd, akionyesha kuwa anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, kuanzia shtaka la tatu hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi cha zaidi Sh 95 milioni, kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na riba kutoka kwa kampuni ya Jeck System Ltd huku akijua kuwa siyo kweli.

Pia katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, Wambura anadiawa kutenda kosa hilo, Juni 17, 2015 huko katika ofisi za TFF, ambapo kwa njia ya udanganyifu, mshtakiwa alijipayia Sh 10milioni kutoka TFF kwa kuonesha kuwa ni malipo ya USD 30,000 pamoja na riba kutoka kwenye kampuni hiyo ha Jeck jambo ambalo siyo kweli.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wambura anadai, kati ya Agosti 15 na Oktoba 21, 2014, makao makuu ya Shirikisho hilo, alijipatia Sh 25milioni kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

Pia, shtaka jingine utakatishaji fedha haramu, Mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 2015, alijipatia Sh 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali na zimetokana na shtaka la kughushi.

Mkurugenzi wa zamani Mipango Takukuru, aomba aomba msamaha yuko tayari kulipa

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MKURUGENZI wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, ameandika barua kwa DPP kwa ajili ya kukiri kosa katika kesi uhujumu uchumi inayomkabili.

Akiwasilisha taarifa hiyo, mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina, wakili wa mshtakiwa huyo, Eliya Mwingira amedai, mteja wake ameishaandika barua kwa DPP hivyo ni vema wakapata majibu kwa wakati ili mshtakiwa aweze kupata haki yake ukizingatia kuwa ameishakaa gerezani kwa muda mrefu, tunaomba japo tarehe ijayo tuwe tumepata majibu.

Mapema, wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai kuwa, kesi hiyo leo Oktoba Mosi, 2019 ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi  bado haujakamilika.

Amedai watafuatilia taarifa hiyo kwa DPP na watakuja na majibu mapema.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu 4, mwaka huu

 Katika kesi hiyo, mshtakiwa Kuluthumu   anakabiliwa na mashitaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya  Agosti  13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya  ya Bagamoyo huku akijua kuwa sio kweli.

Katika shtaka la pili, inadaiwa  kati ya Januari 2012 na Mei 2017  huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja  kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Mansoor alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.


Mshtakiwa huyo pia  alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika shtaka la tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh milioni saba kutoka jwa Ekwabi Majungu  ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Pia anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika shtaka la utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa  alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa  fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

TMA yawaasa wananchi, kufuatilia utabiri wa hali ya hewa

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imewaasa wananchi wa mikoa ya Kaskazini, Kilimanjaro Arusha na Manyara  kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na mamlaka hiyo  ili kuweza kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza.

Katika Taarifa iliyotolewa na Meneja wa kituo Kikuu cha  utabiri TMA, Samwel Mbuya leo Oktoba Mosi, 2019 imesema leo majira ya mchana katika baadhi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara kulitokea na upepo mkali uliotokana na mkusanyiko wa mawingu ya radi katika eneo dogo na kutengeneza mkondo wa mawingu.

"Mawingu hayo yalisababisha dhoruba ya upepo uliokuwa na kasi ya kilomita 50 kwa saa hali ambayo  ilidumu kwa takribani dk.30 katika eneo husika kabla ya hali hiyo kurejea kawaida.

Taarifa hiyo imesema, mkondo huo wa mawingu ulianzia kusini mwa Kenya na kujielekeza katika baadhi ya mikoa hiyo na kufuatiwa na vipindi vya mvua na ngurumo kutokana na mawingu hayo.

Amesema,  matukio hayo ni hali inayoweza kujitokeza panapotokea mawingu hayo mazito kujikusanya katika mkondo, hivyo amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na kuzingatia kufuatilia hali ya hewa.

DC Katambi atoa siku tatu kwa mkandarasi aliejenga ukuta chini ya kiwango

0
0
Charles James, Michuzi TV
KUFUATIA kutoridhishwa na uzio wa ujenzi wa mradi wa upanuzi uzalishaji wa umeme jijini Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ameagiza kuvunjwa kwa ukuta huo kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

DC Katambi ametoa siku tatu kwa mkandarasi huyo kutoka Kampuni ya KEC ya nchini India kuvunja uzio wa ujenzi huo unaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 125.

Maagizo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ya kutembelea ujenzi wa mradi huo unaojengwa kwa fedha za Serikali.

Amesema matofali yaliyotumika kujenga mradi huo hayana ubora unaotakiwa hali iliyopelekea kubomoka na hata yanapondoshwa huvunjika kutokana na kukosa viwango.

“ Ukitazama matofali haya yaliyotumika kujenga uzio huu hayana ubora kutokana na kubomoka, hata ukiyashika kwa mkono tuu bila kutumia vipimo vyovyote hali hii hatuwezi kuifumbia macho ni lazima ukuta huu uvunjwe na makandarasi kwa gharama zake mwenyewe.

Fedha hizi ni za walipa kodi wa Kitanzania hatuwezi kukubali watu wachache waichafue Serikali yetu ambayo inafanya kazi usiku na mchana kuwaletea maendeleo wananchi wetu. Ndio maana nimetoa siku tatu ukuta uvunjwe na ujengwe tena, " Amesema DC Katambi

Amesema ukuta huo sio tu umejengwa chini ya kiwango lakini pia umekiuka masharti na miongozo ya mkataba wa awali kama ambavyo BOQ inaelekeza.

“Hapa leo nakuja wapo wenyewe hakuna mtu hata mmoja wa Tanesco, sasa hali hii inatishia sana kwani mradi huu unaweza kuchakachukiwa kwa kiwango kikubwa sana na fedha za watanzania zikaliwa bila kuwepo na tija yeyote” Amesema Katambi.

Kwa upande wake mhandisi Shafii Kiula, kutoka shirika la ugavi wa umeme nchini Tanesco alimesema shirika hilo tayari lilishamwandikia barua mkandarasi wa mradi huo kuuvunja ukuta kwa gharama zake na kuanza upya ujenzi kutokana na matofali yaliyotumika kukosa ubora.

MABARAZA YA ARDHI YA KATA NA VIJIJI YASIYOTENDA HAKI MAFIA YAVUNJWE-DKT MABULA

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda kuyavunja Mabaraza yote ya Kata na Vijiji ya ardhi yasiyotenda haki wakati wa kutoa maamuzi katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana akiwa katika ziara yake ya siku mbili wilayani Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi.

Alisema, kutokana na kero nyingi za ardhi alizozipokea katika ziara yake hiyo wilayani Mafia amebaini Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya hiyo hayafanyi kazi zake vizuri na wajumbe wake wamekuwa wakiyatumia kutoa maamuzi yasiyotenda haki.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kadri Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia yanavyofanya vibaya katika utoaji maamuzi yake basi hata uanzishwaji Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya hiyo halitafanya vizuri katika utendaji wake.

‘’Ukiwa na watu wasioweza kusimamamia haki itakuwa shida sana, Mkurugenzi hakikisha Mabaraza ya Ardhi katika Kata na Vijiji yasiyofuata taratibu na kutoa haki kwa walalamikaji unayavunja na kuteua wajumbe wapya’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi alitaka kupitiwa upya Mabaraza yote ya ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia hasa yale yanayolalamikiwa na kubainisha kuwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko tayari kutoa Msajili wa Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba nchini ili atoe elimu katika Mabaraza hayo kwa lengo la kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Alisema, Mabaraza ya ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia hayatendi haki na wakati mwingine Baraza la Kata linachukua kesi ya Baraza la Kijiji lengo likiwa kutotenda haki kwa walalamikaji.

Baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi kuwa wajumbe wake hawatendi haki wakati wa kutoa maamuzi na hivyo kuonesha dhahiri uwepo dalili za rushwa.

Mohamed Shaban alimueleza Dkt Mabula kuwa, Mabaraza ya ardhi ya Kata wakati mwingine hayatendi haki na kumtaka anayeshindwa kesi kwenda Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya la Mkuranga huku wakijua mlalamikaji atashindwa kwenda Mkuranga kutokana na changamoto za usafiri na hivyo kupoteza haki yake.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda alieleza kuwa Mabaraza ya ardhi ya Kata na Kijiji katika wilaya hiyo yapo na yanafanya kazi na wajumbe wake wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ingawa alieleza changamoto iliyopo Baraza katika kata ya Kilindoni ambalo alilileleza kuwa badala ya kuatatua matatizo limekuwa chanzo cha migogoro kwa kuwa wakati mwingine hufanya mashauri yaliyo nje ya kata yake na suala hilo tayari alishalitolea agizo la kuvunjwa kwa baraza hilo.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Baleni wilayani Mafia mkoa wa Pwani alipokwenda kusikiliza kero za ardhi katika eneo hilo akiwa katika ziara yake ya siku mbili katika wilaya hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
 Mwananchi Hassan Omar maarufu mzee wa Lumbesa mkazi wa Dagoni Mafia akimuonesha nyaraka Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuhusiana na mgogoro wa ardhi wakati Dkt Mabula alipofanya ziara wilaya ya Mafia  kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua Majalada ya Ardhi katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia jana wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnenduma na Kulia ni Afisa Ardhi Chuchu Ochere.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia baadhi ya Nyaraka za umiliki wa ardhi kutoka kwa Hassan Mohamed (Kushoto) na Mwanangano Mohamed wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya ya Mafia jana (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

AFISA TARAFA ITISO: TUTATUMIA MAKUNDI YA NGOMA ZA ASILI KUHAMASISHA NA KUELEZA UMUHIMU WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0
0
Afisa Tarafa Remidius Emmanuel akizungumza na baadhi ya vikundi vya Sungusungu pamoja na wananchi wa kata ya Itiso wakati wa tamasha dogo la utamaduni lililoandaliwa na viongozi wa kabila la Wagogo wa Tarafa ya Itiso na kufanyika  katika Kijiji cha Mapanga (Makulu).
 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tarafa ya Itiso A/Insp. Mohamed Ally akitoa neno kwa wananchi pamoja na baadhi ya vikundi vya Sungusungu wakati wa tamasha dogo la utamaduni lililoandaliwa na viongozi wa kabila la Wagogo wa Tarafa ya Itiso na kufanyika  katika Kijiji cha Mapanga (Makulu)
 Kiongozi wa Kabila la Wagogo Tarafa ya Itiso, Chief Mahemu Izidoli Maope akizungumza wakati wa tamasha dogo la utamaduni lililoandaliwa na viongozi wa kabila la Wagogo wa Tarafa ya Itiso na kufanyika  katika Kijiji cha Mapanga (Makulu)
Afisa Tarafa  Itiso Remidius Emmanuel akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa kabila la Wagogo  wa Tarafa ya Itiso mara baada kumalizika kwa tamasha dogo la utamaduni lililoandaliwa na viongozi wa kabila la Wagogo wa Tarafa ya Itiso na kufanyika  katika Kijiji cha Mapanga (Makulu).

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO CHA YALIN CHA MTWARA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin cha Mtwara, Oktoba 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo Mtwara, Oktoba 2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BODI YA REA YAKAGUA MRADI WA UMEME JUA UYUI

0
0
Na Veronica Simba – Tabora
Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imekagua mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika kijiji cha Tura, kilichopo Uyui, Mkoa wa Tabora; ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo katika mikoa mbalimbali nchini, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Akizungumza Oktoba Mosi, 2019 baada ya kukagua mitambo miwili ya umeme jua iliyofungwa kijijini hapo, Mwenyekiti wa Kamati husika, Mhandisi Styden Rwebangira, alisema mradi huo uliofadhiliwa na serikali kupitia mkopo wa gharama nafuu kutoka serikali ya Austria, ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi walio mbali na gridi ya Taifa.

“Kijiji hiki ni mojawapo ya wanufaika; kimepata umeme huu wakati kikisubiri umeme wa REA, maana kimeainishwa kupatiwa umeme huo katika Awamu ya Tatu ya mradi husika, Mzunguko wa Pili,” amefafanua.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, alisema Wakala huo umeshakamilisha upimaji, ambapo takwimu zinaonesha kuwa, kutoka kwenye njia iliyo na umeme mpaka kijiji husika ni takribani kilomita 98.8 za umeme wa msongo wa kati.

“Mpango wetu ni kusambaza umeme huo kwa umbali wa kilomita 10 ili kuwafikia wateja wote zaidi ya 400 waliopo katika kijiji hiki,” alisema Olotu.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Tura, Nelson Mungwila, alitoa shukrani kwa serikali kwa kubuni mradi huo ambao alisema umekuwa wa manufaa makubwa kwa wananchi husika hususan katika kuboresha hali zao kiuchumi kupitia miradi mbalimbali wanayojishughulisha nayo.

Aliiomba serikali iwasaidie kuchangia gharama za kununua betri mpya za kuendeshea mitambo hiyo ya umeme jua ili wananchi waendelee kunufaika na mradi huo, kwani zilizopo zimeharibika.

Katika ziara hiyo, Kamati husika itatembelea mikoa mbalimbali kwa takribani wiki moja, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kwa lengo la kutatua changamoto zinazochelewesha utekelezwaji na ukamilishwaji wake.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangira (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kushoto), wakikagua moja ya mitambo ya umeme jua iliyopo katika kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Oktoba 1, 2019.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangira (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kushoto), wakijadiliana jambo na Afisa Mtendaji wa Kata ya Tura, Nelson Mungwila (kulia), walipowasili kwenye kata hiyo kukagua mradi wa umeme jua, Oktoba 1, 2019.
 Shule ya Msingi iliyopo katika kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Shule hii ni miongoni mwa taasisi za umma zinazonufaika na mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
 Mashine ya kusaga nafaka iliyopo kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Mashine hii ni miongoni mwa miradi ya kijamii inayotekelezwa kijijini hapo kwa kutumia umeme unaotokana na mradi wa umeme jua, ambao umefadhiliwa na serikali.
 Taa maalum iliyowekwa kumulika moja ya mitaa ya kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora (kushoto) kwa ajili ya kuimarisha usalama. Taa hiyo inatumia nishati inayotokana na mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
 Nguzo za umeme katika moja ya mitaa ya kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Nguzo hizo zinatumika kuunganisha umeme katika makazi ya watu, miradi ya kijamii na taasisi za umma na dini kupitia mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
Matukio mbalimbali wakati Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ilipofanya ziara kukagua mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika kijiji cha Tura, kilichopo Uyui, Mkoa wa Tabora, Oktoba 1, 2019.

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA KUSINI

0
0
Na Veronica Simba – Tabora
Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imekagua mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika kijiji cha Tura, kilichopo Uyui, Mkoa wa Tabora; ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo katika mikoa mbalimbali nchini, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Akizungumza Oktoba Mosi, 2019 baada ya kukagua mitambo miwili ya umeme jua iliyofungwa kijijini hapo, Mwenyekiti wa Kamati husika, Mhandisi Styden Rwebangira, alisema mradi huo uliofadhiliwa na serikali kupitia mkopo wa gharama nafuu kutoka serikali ya Austria, ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi walio mbali na gridi ya Taifa.

“Kijiji hiki ni mojawapo ya wanufaika; kimepata umeme huu wakati kikisubiri umeme wa REA, maana kimeainishwa kupatiwa umeme huo katika Awamu ya Tatu ya mradi husika, Mzunguko wa Pili,” amefafanua.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, alisema Wakala huo umeshakamilisha upimaji, ambapo takwimu zinaonesha kuwa, kutoka kwenye njia iliyo na umeme mpaka kijiji husika ni takribani kilomita 98.8 za umeme wa msongo wa kati.

“Mpango wetu ni kusambaza umeme huo kwa umbali wa kilomita 10 ili kuwafikia wateja wote zaidi ya 400 waliopo katika kijiji hiki,” alisema Olotu.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Tura, Nelson Mungwila, alitoa shukrani kwa serikali kwa kubuni mradi huo ambao alisema umekuwa wa manufaa makubwa kwa wananchi husika hususan katika kuboresha hali zao kiuchumi kupitia miradi mbalimbali wanayojishughulisha nayo.

Aliiomba serikali iwasaidie kuchangia gharama za kununua betri mpya za kuendeshea mitambo hiyo ya umeme jua ili wananchi waendelee kunufaika na mradi huo, kwani zilizopo zimeharibika.

Katika ziara hiyo, Kamati husika itatembelea mikoa mbalimbali kwa takribani wiki moja, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kwa lengo la kutatua changamoto zinazochelewesha utekelezwaji na ukamilishwaji wake.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangira (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kushoto), wakikagua moja ya mitambo ya umeme jua iliyopo katika kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Oktoba 1, 2019.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangira (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kushoto), wakijadiliana jambo na Afisa Mtendaji wa Kata ya Tura, Nelson Mungwila (kulia), walipowasili kwenye kata hiyo kukagua mradi wa umeme jua, Oktoba 1, 2019.
 Shule ya Msingi iliyopo katika kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Shule hii ni miongoni mwa taasisi za umma zinazonufaika na mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
 Mashine ya kusaga nafaka iliyopo kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Mashine hii ni miongoni mwa miradi ya kijamii inayotekelezwa kijijini hapo kwa kutumia umeme unaotokana na mradi wa umeme jua, ambao umefadhiliwa na serikali.
 Taa maalum iliyowekwa kumulika moja ya mitaa ya kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora (kushoto) kwa ajili ya kuimarisha usalama. Taa hiyo inatumia nishati inayotokana na mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
 Nguzo za umeme katika moja ya mitaa ya kijiji cha Tura, wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora. Nguzo hizo zinatumika kuunganisha umeme katika makazi ya watu, miradi ya kijamii na taasisi za umma na dini kupitia mradi wa umeme jua unaotekelezwa kijijini hapo kwa ufadhili wa serikali.
Matukio mbalimbali wakati Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ilipofanya ziara kukagua mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika kijiji cha Tura, kilichopo Uyui, Mkoa wa Tabora, Oktoba 1, 2019.

TECNO IKISHIRIKIANA NA TIGO YAZINDUA RASMI TECNO SPARK 4

0
0
 Sasa TECNO imewapa tena wateja wake nafasi ya kurahia ladha mpya ya simu janja na hii kutokana na ujio wa simu mpya ya TECNO Spark 4 yenye sifa malukuki na kwa bei nzuri.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa TECNO Spark 4 uliofanyika katika duka jipya la TECNO ‘TECNO Smart Hub Kariakoo’ manager wa masoko wa kampuni ya TECNO, William Motta alisema, “teknolojia ya AI iliyopo ndani ya TECNO SPARK 4 imebeba uwezo mkubwa wenye kuzipa support kamera tatu za nyuma za TECNO Spark 4 kwa picha nzuri na videos zenye ubora. 

William Motta amevieleza vyombo vya habari kuwa TECNO Spark 4 imekuja na sifa zifuatazo Kasi ya mtandao wa 4G, Kamera tatu za nyuma, GB 32 za memory na kioo cha nchi 6.52 super full-view. 

Wakati huo, Mkuu wa idara ya kitengo cha bidhaa wa kampuni ya TIGO Mkumbo Mnyonga alisema, “pindi unaponunua simu ya TECNO Spark 4 basi hapo hapo utazawadiwa na ofa ya GB 18 kutoka tigo.uzinduzi wa simu hii mpya unaenda sambamba na ofa ya GB 18 kutoka tigo”. 

Mkumbo Mnyonga “lengo letu ni kuhakikisha jamii ya kitanzania inahamia katika mfumo mpya wa kijital. Na hiyo ndio sababu ya kampuni ya TIGO kushirikiana na TECNO ili kulifikia dhumuni lakuongeza wimbi la watumiaji smartphone nchini”.

DC Misungwi kuratibu zoezi la kufufua kiwanda cha Pamba Manawa

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Husseis Bashe (wa pili kulia) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda (kulia) kukagua sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata pamba Manawa kilichopo Kata ya Misasi wilayani Misungwi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Septemba 27, 2019 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alitembelea kiwanda hiki 
 Mwonekano wa baadhi ya mitambo katika kiwanda cha kuchakata pamba Manawa kilichopo wilayani Misungwi ambacho tangu mwaka 2014 kilisitisha shughuli zake.
Tazama BMG Online TV hapa chini

DC KOROGWE ATAKA WAZEE WAENDELEE KUPEWA ELIMU YA UGONJWA WA UKIMWI ILI KUEPUKANA NAO

0
0
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambapo kiwilaya ilifanyika kwenye ukumbi wa Halamshauri ya Korogwe mji wilayani Korogwe kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda 
Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda akitoa taarifa yao wakati wa maadhimisho hayo 
Mwakilishi wa Shirika la Help Age Internation Martha Kihampa akizungumza wakati wa maadhimisho hayo 
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo 
Sehemu ya wazee kutoka maeneo mbalimbali wilayani Korogwe wakiwa kwenye maadhimisho hayo 
Sehemu ya wazee wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akilakiwa na Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia akiagana na Mwakilishi wa Shirika la Help Age Internation Martha Kihampa mara baada ya kufungua maadhimisho hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua maadhimisho hayo 



MKUU wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Gwakisa ametaka wazee kuendelea kupewa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi ili kuweza kuepukana nayo ambayo ni hatari kwa ustawi wa jamii pindi wanapokumbana nayo.

Kissa aliyasema hayo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambapo kiwilaya ilianzimishwa kwenye ukumbi wa Mji wa Korogwe ambapo alisema wazee ni kama binadamu wengine hivyo lazima wapatiwe elimu hiyo ili waweze kuchukua tahadhari.

Alisema kwani wanapokuwa wakijitibu magonjwa ya namna hiyo wakiwa na umri mkubwa ni gharama na ngumu sana kwao huku akiwataka waendelee na mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

“Ndugu zangu wazee lazima tutambue kwamba kuna ugonjwa hatari wa ukimwi hivyo upo uhimu wa kuendelea kupatiwa elimu kuhusiana na ugonjwa huo kwani ni wanapojitibu ugonjwa huo mkiwa na umri mkubwa ni gharama kubwa sana “Alisema.

Aidha alisema kwamba kwenye maeneo yanatotoa huduma wananchi watambua ni jukumu lao la kutunza wazee huku akieleza kwamba serikali iliagiza wazee wanapokwenda hospitalini watibiwe kwa haraka na dawa wazipate kwa wakati.“Watumishi wa afya hakikisheni wazee wanahudumiwa vizuri mtu ambaye hataki kumuhudimua mzee vizuri kwa sababu ni mzee atoke kwenye hispitali zaserikali aende akatafute kazi nyengine ya kufanya”Alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba watanzania wamelelewa kuheshimu wazee kwani hakuna mtu ambaye hatafika kwenye uzee hivyo serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuweza kuondosha changamoto zinazowakabili.

Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Shirika la African Women Aids Working Group (AFRIWAG) mkoani Tanga Magreth Ruhinda alieleza vikwazo ambazo vimekuwa vikiwakabili wazee nchini na kujikuta wakishindwa kufikia malengo yao ambavyo vimegawanyika kwenye makundi manne.Magreth alibainisha vikwazo hivyo vinatokana na unyanyasaji wa ukiukwaji wa haki za wazee,umaskini wa kipato,huduma duni za afya na matibabu ikiwemo zinazotokana na ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Aidha alisema kutokana na uwepo wa changamoto hizo shirika hilo kwa kushirikiana na wenzao wa Kimataifa wa Help Age wamefanikiwa kutekeleza mradi wa kuboresha afya za wazee kwenye halamshauri ya wilaya ya mji wa Korogwe .Mwenyekiti huyo alisema kwamba utekelezaji huo unafanyika chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza na kisiwa cha Jersey ambao umewezesh mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa baraza Halmashauri na Mabaraza ya kata.

Alisema pia wataendelea kutoa mafunzo kwa watumishi 33 katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza uelewa kwa watumishi kuhusu namna ya kutoa huduma rafiki za afya kwa wazee, magonjwa yasiyoambukizwa, kutambua hali za uzee zinazowakabili na afya ya uzazi.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Wazee kutoka Baraza la Halmashauri ya Korogwe mji Mtafi Hassani alisema kwamba kundi hilo linakabiliwa na chanagmoto mbalimbali ambazo hazina budi kupatiwa ufumbuzi na serikali kuu na serikali za mitaa ikiwemo za kiafya,kiuchumi na sauti zao kutokusikilizwa mara kwa mara huku akieleza kwamba wanahitaji kusikilizwa kwa jicho la kipekee kwa dhati na vitendo.

“Tunaiomba serikali ya Rais Dkt John Magufuli isikie kilio chetu kama ilivyo kwa makundi mengine ...Lakini sera ya wazee ya mwaka 2003 ambayo imesheheni matamko mengi ya kisera yanayodhihirisha utashi wa kisiasa wa serikali yetu hadi sasa haijatungiwa sheria toka iliopopitishwa mwaka 2003 hivyo tunaomba serikali ya awamu hii ya tano iharakishe mchakato wa kutungiwa sheria iweze kutekelezeka”Alisema .

Mtafi ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee Mtaa wa Mtonga Kata ya Mtonga wilayani humo aliipongeza serikali kwa kutoa msamaha wa matibabu kwa wazee kila wanapokwenda kutibiwa katika hospitali za serikali na umma ikiwemo kuongeza dawa na watumishi katika vituo vya kutolea huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo hivyo.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images