Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

TIMU YA MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI KUTEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME KATIKA MTO RUFIJI

0
0
 Mhandisi Steven Manda akiwatembeza sehemu mbalimbali  Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi walipotembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.(PICHA NA JESHI LA POLISI)
 Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Mohamed H. Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi baada ya kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji mkoani Pwani.
Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mohamed H. Hassan, akiongoza Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto rufiji.(PICHA NA JESHI LA POLISI)


Dk Mahiga ataka weledi upashanaji habari

0
0
 Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga akizungumza na wadau wa tasnia ya habari na waandishi kutoka vyombo vya mbalimbali vya habari jamii nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akitoa salamu za Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mshehereshaji ambaye pia ni mkufunzi wa Redio za Jamii, Rose Haji Mwalimu akitambulisha meza kuu (haipo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege akitoa salamu za UNESCO kwa niaba ya Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini, Tirso Dos Santos (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi akitoa salamu za TADIO wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Ofisa habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNIC), Didi Nafisa akiendesha majadiliano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi pamoja na Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Kutoka kushoto meza kuu ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege, Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wadau wakongwe katika tasnia ya habari nchini wakiwasilisha maoni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Redio Jamii na wadau wa tasnia ya habari nchini walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga na meza kuu katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyofanikisha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga na meza kuu katika picha ya pamoja na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Redio Jamii na wadau wa tasnia ya habari nchini walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
 Maafisa kutoka Umoja wa Mataifa Rose Mwalongo (wa pili kushoto) na Stella Vuzo (wa pili kulia) katika picha ya kumbukumbu na wadau wa tasnia ya habari nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
SERIKALI kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa taarifa imesema ipo tayari kuangalia vikwazo vinavyosababisha ukosefu wa taarifa sahihi, ikiwamo sheria ili uchakataji wa habari uboreke kwa manufaa ya taifa.
Aidha imesema kwamba inatambua matatizo mengi duniani yanayosababisha uhasama yanatokana na kukosekana taarifa sahihi miongoni mwa wanadamu.
Aidha kukosekana kwa taarifa sahihi na kuwapo kwa taarifa za uongo kumesababisha kuwapo kwa vita na usumbufu mwingine ambao ungeliweza kutatuliwa kwa kuwapo kwa taarifa zilizo sahihi.
Kauli hizo zimetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa iliyoadhimishwa mkoani Morogoro hapa nchini yakiwa na kauli mbiu “Upataji Taarifa : Asiachwe Mtu!”.
Alisema ili taifa la Tanzania lisiingie katika migogoro serikali ipo tayari kusikiliza wadau na kushirikiana nao kuweka mazingira ya upatikanaji wa taarifa kuwa bora zaidi na unaojali maslahi mapana ya nchi.
Pamoja na kuwapongeza waandazi wa hafla hiyo, UNESCO,  Dk. Mahiga pia alielezea umuhimu wa taasisi za umma na binafsi zinazohusika na upashaji habari kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na weledi mkubwa ili kuondoa matatizo yanayoambatana na kukosekana kwa habari.
Alisema uchakataji wa habari ni muhimu ili wananchi wote waweze kupata habari na kuzitumia kwa maendeleo yao.
Alisema suala la upatikanaji wa taarifa sahihi si wa taifa moja tu bali dunia nzima na hilo limehimizwa tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia ambayo kwa namna fulani ilichochewa na kukosekana kwa habari sahihi.
Alisema pamoja na dunia mataifa kuridhia haki ya kujieleza na kupata habari, mataifa na watu wengi wamekuwa wakikosa au wakinyimwa haki ya kuhabarishwa na hivyo kuzua matatizo katika jamii husika.
Alisema ndio maana Tanzania imekuwa moja ya nchi iliyotia saini mikataba uhuru na haki ya kupata habari na kutamka wazi katika katiba yake kuhusu haki za habari.
Alisema kuna manufaa makubwa kwa watu kuwa huru katika kuhabarishana kama kuongeza uelewa wa jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya afya uchumi na namna ya kuishi.
Hata hivyo alisema taarifa zinapokuwa mbaya na zisizojenga husababisha migogoro na migongano katika jamii na hivyo kuitaka jamii kuhakikisha kwamba inapata taarifa sahihi na zenye kujenga jamii husika.
Alisema kwa kuwa utawala bora unahusisha na demokrasia ni vyema kwa nchi yoyote inayojinadi kuwa na demokrasia ni lazima kuwa na jukwaa kwa wananchi wake kupata habari sahihi.
Waziri huyo alisema kwamba habari ni kama upanga wenye makali pande zote unaoweza kuleta neema au balaa .
“Habari zikitumika vyema zinaleta haki na zikitumika vibaya zinaleta migogoro na kuhatarisha usalama wa nchi“ alisema Dk. Mahiga.
Alipotolea mfano wa uchaguzi wa serikali za mitaa na kusema kwamba ili wananchi waweze kuufanya kwa ufanisi mkubwa ni lazima wawe wameelimishwa vya kutosha kutambua na kujitambua ili wapige kura zenye uhakika.
Alipongeza Mtandao wa Radio za Jamii (TADIO) kwa kuwa karibu na wananchi na kusema wanafanyakazi njema ya kuhabarisha jamii hasa kutokana na ukweli kuwa radio ya taifa haifiki kila mahali.
Alisema kazi inayofanywa na TADIO ni ya muhimu kwani inasaidia serikali katika kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na hasa mwelekeo kama taifa.
Alisema kutokana na ufanisi huo ni vyema taasisi hizo zikajikita katika kueleza ukweli kwa weledi mkubwa ili wasiingie katika mtego wa kusumbuana na sheria na hivyo kurejesha nyuma matunda muhimu ya haki za kupashana habari.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi akizungumza kabla ya Waziri Mahiga alishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuwezesha kuwepo kwa tukio hilo muhimu hapa nchini.
Aidha alishukuru kuwapo kwa makubaliano ya awali kati ya TADIO na Chuo Kikuu Huria yaliyowezesha Mtandao huo wa Redio Jamii kuwa na ofisi katika majengo ya chuo hicho.
Pia alishukuru UDOM kwa kuruhusu mifumo yake ya Tehama kutumika na kuja kuwa sehemu ya mafunzo kwa wanahabari.
Pia alishauri taasisi zote husika kuona changamoto zinazokabiliwa na redio jamii na kuzishughulikia.
Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza alisema kwamba nchi zilizoendelea zimefanikiwa kutokana na kutumia vyema haki ya upashanaji habari.
Alisema hata hivyo hali bado si nzuri kwa upande wa watumishi wa umma ambao wamekuwa wagumu kutoa taarifa mbalimbali zinazohitajika na vyombo vya habari kwa ajili ya kufikisha kwa umma.
“ Kumekuwa na usiri mkubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuleta sintofahamu” alisema Kitomari.
Alitoa wito kwa watumishi wa umma kujengewa uwezo ili waweze kushiriki kikamilifu katika suala zima la uchakataji habari.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege alisema katika hotuba aliyosoma kwa niaba ya Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos kwamba shirika hilo linaridhishwa na kasi ya TADIO na kutaka wananchi kutambua haki zao za msingi za kupashana habari na kufanya hivyo kwa weledi.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa alisisitiza umuhimu wa kutumia habari kuharakisha kasi ya maendeleo.
TADIO – Tanzania Development Information Organisation ni asasi ya habari za maendeleo Tanzania inayohusisha vyombo vya habari za kieletroniki yaani Radio zinazozalisha maudhui ya kijamii ambazo nyingi hupatikana mikoani na sehemu za vijijini ambako idadi kubwa ya Watanzania wanaishi.
TADIO ina jumla ya Radio wanachama 32 katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani isipokuwa Tabora na Singida. Uwezo wa Radio Jamii hizi kufikia watanzania waliopo mikoani na hasa vijijini hukadiriwa kufikia asilimia 70%.
TADIO ilianzishwa rasmi mwaka 2017 baada ya kuvunjika kwa asasi ya mfanano ya awali iliyojulikana kama COMNETA.

WEUSI, FID Q WATIKISA,OMMY DIMPOZ AMWAGA MACHOZI JUKWAA LA TIGO FIESTA 2019 _SAIZI YAKO MWANZA

0
0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lulu Diva akitawala jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marioo akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rich Mvoko akitawala jukwaa laTigo Fiesta 2019 _Saizi yako k katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID '' Mnyama'' akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Badman Mkali wa Ngoma ya "NIKagongee " akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Bilnass akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ;;African Princess'' akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya Sanaa(THT) wakiwa wamebeba picha ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Ruge Mutahaba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wakati wakimkumbuka na kumtakia alale mahali pema peponi.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Injili Goodluck Gozbert akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Barnaba Classic akishambulia jukwaa la TTigo Fiesta 2019 _Saizi yako k katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpozi akifuta machozi wakati akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Mkali wa HipHop Fareed Kubanda ''Fid Q'' akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Maua Sama akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Weusi wakishambulia jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza







TAMASHA la Muziki, Msimu wa Tigo Fiesta 2019 limezinduliwa jana kwa kishindo jijini Mwanza huku kundi la Weusi likifunika kwa kuwapagawisha washabiki luluki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mbali na wasanii hao kukonga vilivyo nyoyo za washabiki wa muziki wa kizazi kipya msanii mwingine machachari Farid Kubanda ‘Fid Q’ hakuwa nyuma kuwarusha wapenzi huku Omar maarufu kama Ommy Dimpoz akimwaga kukwaani.

Washabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba walishindwa kujizuia kutokana na makamuzi ya nguvu yaliyowaacha hoi yaliyofanywa na kundi la Weusi wakiongozwa na JOH Makini,Nikki wa pili na G Nako baada ya kupanda jukwaani na kutoa burudani tosha.

Aidha, katika tamasha hilo la Tigo Fiesta 2019 msanii Fid Q alipanda jukwaani akiwa kwenye Wheel Chair (kiti cha magurudumu mawili) kabla ya kuwazodoa waliomzushia kifo na kwamba hataweza kuimba kutokana na kuugua maradhi kwenye koo kasha kumwaga machozi mithili ya mtoto.

Tamasha hilo limefanyika Mwanza kwa mara ya kwanza kuasisiwa kwake lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa ambapo washabiki kutoka viunga vya jiji hilo la milima ya miamba ya mawe walisuuzika nyoyo na mara kadhaa walishiriki kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali hasa kundi la Weusi na Fid Q.

Mbali na kundi la weusi lililopagawisha vilivyo, wengine ni Barnaba, TID, Mavoko na Diva ambapo wasanii wa jiji la Mwanza nao hawakubaki nyuma.

Akizindua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela alisema waandaaji wa Tigo Fiesta 2019 kwa ubunifu na uamuzi wao wa kuzindua tamasha hilo hawakukosea ikizingatiwa jiji hilo ni kitovu cha biashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.

“Mwanza ni kisima cha burudani kutoka na kuwa na wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya hivyo niwapongeze Clouds na Tigo kwa ubunifu wao wa kuandaa na kuzindua tamasha lao hapa.Sisi kama mkoa tutaendelea kuwaunga mkono.Pia tamasha hili mbali na kutoa burudani lina umuhimu kiuchumi, linatoa ajira za muda mfupi,linaongeza kipato cha wananchi wetu na waandaaji nao wananufaika,”alisema Mongela.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Entertainment, Joseph Kusaga, alisema wana mapenzi nakubwa na Mkoa wa Mwanza na ndiyo sababu msimu huu wamezindua tamasha la Tigo Fiesta 2019 kwa kutambua mchango wa mkoa huo.

Naye Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati, kampuni hiyo ya mawasiliano itaendelea kushirikiana na kuiunga mkono Clouds ili kuhakikisha wanawapatia Watanzania burudani yenye vionjo na ladha tofauti tofauti.


Hata hivyo washabiki na wapenzi Tigo Fiesta 2019 waligubikwa na huzuni na simanzi ya muda mfupi wakati kundi la wasanii wa Tanzania House of Talent (THT) likitoa burudani huku wakionyesha picha za aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds, marehemu Ruge Mutahaba ikiwa ishara ya kumbukumbu yake.

Ikumbukwe marehemu Ruge kabla ya kufikwa na mauti alikuwa mhimili na muasisi wa tamasha hilo zamani likiitwa Fiesta kabla ya kubadilishwa na kuitwa Tigo Fiesta.

Tamasha hilo baada ya kuzinduliwa mashambulizi yataelekezwa mkoani Kagera katika Wilaya ya Muleba na hivyo wapenzi wa huko wakae mkao wa kula kwa nafasi

NMB yaboresha mfumo wa ulipaji kwa kutumia kadi

0
0
UONGOZI wa Benki ya NMB umesema kuwa unazidi kuboresha mifumo ya huduma zao za kadi ili kuhamasisha watalii pamoja wananchi wa kawaida kutumia kadi kwenye malipo na ununuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir wakati akizungumza kwenye maonesho ya Utalii visiwani Zanzibar, ambapo benki hiyo ni moja wapo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyofika tamati siku ya Jumamosi.
Alisema kutokana na ukuaji wa Teknologia Duniani, ndivyo wanavyo buni mbinu zitakazo wawezesha wateja wao kupata huduma bora na za kimataifa. Vilevile, mifumo ya Kidigitali na matumizi ya kadi za MasterCard ambazo zinatumika kitaifa na kimataifa  zimekua zikiondoa usumbufu kwani huduma hizo zinaweza kutumikaa ndani na nje ya nchi.
Benki ya NMB benki hivi sasa ipo karibu na wananchi mjini na vijijiNI  hivyo kuingia katika masauala ya utalii, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuzidi kujitangaza na kuvutia wateja wengi zaidi pamoja na wageni wanaofika nchini. 
Naye Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar- Balozi Seif Ali Iddi ameomba mashirikiano na taasisi nyingine katika kutangaza utalii wa Zanzibar ili kuongeza idadi kubwa ya watalii Zanzibar.
Alisema wananchi wa Zanzibar wananufaika na utalii kupitia sera ya Utalii kwa wote na kubainisha kuwa sera hiyo ipo wazi  kuweza kunufanisha wananchi hasa kwa kuwa na usalama wa nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale- Mahamoud Thabiti Kombo alisema kuwa maonyesho hayo ni agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ambapo lengo ni kuitanganza Zanzibar kiutalii baada ya mafanikio makubwa ya waka jana.
Alisema kuwa maonesho ya kila mwaka yanawasadia wajasiriamali wadogo wadogo kujitangza kupitia utalii ili waweze kunufanika na matunda ya utalii kwa kuuza bidhaa na kukuza biashara zao.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Zanzibar - Abdalla Duchi, amewataka wananchi wa Zanzibar kuchangamkia fursa za utalii zinazopatika  nchini ili kujikwamua na umaskini .
Amewataka wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati  kutumia fursa zinazotolewa na Benki hiyo katika maeneo mbalimbali kwa kujisajili kuwa mawakala, ambapo itafungua fursa za ajira sambamba na kutoa huduma kwa wananchi wa kawaida ikiwemo watalii wanaokuja kutembea Zanzibar.
Aliongeza kuwa benki ya NMB ina wateja zaidi ya milioni tatu huku ikiongoza kwa matawi mengi - 229 nchini, yakiwemo NMB Zanzibar, NMB Mwanakwerekwe na NMB Chakechake- Pemba, huku ikiwa na jumla ya mawakala 84 Zanzibar kwa jumla ya idadi ya  mawakala 6000 nchi nzima.
 Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Maofisa wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show'  Visiwani Zanzibar.
  Maofisa wa Benki ya NMB wakifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa udhamini wao.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (mwenye miwani) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show' Visiwania Zanzibar.

NAIBU WAZIRI MGUMBA AWATAKA WALIMU NCHINI KUACHA KUTUMIA KILIMO KAMA ADHABU YA KUWAPA WANAFUNZI

0
0

NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba akizungumza na watumishi wa Halamashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kulia akimueleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakati wa ziara yake wialayani humo
MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange 
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisialimiana na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalim Hassani Nyange wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi 
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa wanachukia kilimo.

Mgumba alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kilima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu.

Alisema kwamba hapana suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni ute wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo.

“Hivyo ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine wakati uchumi wetu unategemea kilimo”Alisema Naibu Waziri huyo.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba mkakati wa serikali ni kuimarisha kilimo hivyo wataendelea kufungamanisha elimu yao na kilimo chao.

Akizungumzia Kilimo cha Minazi wilayani humo Naibu Waziri huyo alisema kwamba kilimo cha minazi ni kweli mpaka sasa hawaapata ufumbuzi wa magonjwa yake kwa miaka zaidi ya 30 mpaka leo ambayo yanasababsihwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Alisema pia hilo linatokana na kukubali kuletewe mbegu ya kisasa ambayo haiendani na mazingira ya nchi hivyo kama Taifa  wameendelea kuimarisha vituo vyao vya utafiti hasa cha utafiti wa minazi mikocheni lengo ni kuanza kurudi kwenye kuzalisha miche kutumia minazi ya asili inayokabiliana na hali ya hewa na ikolojia ya ya nchi yetu .

“Na sasa tumeanza kuzalisha kitalu cha miche asili Bagamoyo na itasambazwa nchi nzima kwa lengo la kupanda na hatimaye kuweza kurejesha minazi hiyo”Alisema

Akizungumzia udogo wa bei ya nazi nchini Naibu Waziri huyo alisema kwamba nazi zinauzwa bei ndogo na imeendelea kuwa ndogo ni kutokana na ushindani uliopo kwenye soko la ndani, kanda na kimataifa kwa sababu ya bidhaa mbadala.

 “Hivyo kila nazi ikipanda bei watu wanakwenda kutumia mafuta lakini kila tunapoacha kutumia nazi na kutumia mafuta na kwenda kwenye chukuchuku wanapunguza mahitaji ya nazi”Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba wanakuja na mkakati wa kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza thamani bidhaa hiyo ili kupanua soko la nazi hapa nchini na mbegu za nazi ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku akieleza kwamba wakienda kuongeza thamai tatizo hilo litakwisha.

Katika hatua nyengine Naibu Waziri huyo aliwataka watanzania tuendelee kutumia nazi kwani wanapoendelea kuitumia zaidi wanatongeza mahitaji na soko la nazi litakuwa kubwa huku akisistiza kwamba watakaendelea kutumia mafuta bei ya nazi itashuka.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso alisema kwambazao la nazi limeathiriwa namaradhi kwa muda mrefu mpaka yamepatikana bado tiba yake haijapatikana miaka 30.

Alimwambia Naibu Waziri Mgumba kwamba ugonjwa huo umekuwa haupati ufumbuzi kama lilivyokuwa gonjwa la ukimwi hiyo walimuomba watafiti na watalamu wafanye utafiti ambao utafika mwisho na wenye manufaa na kuweza kurudisha uchumi wake.

“Kwa sababu nazi zinakazi nyingi unaweza kusingwa na machicha yake ukabaki hapa Pangani….lakini pia inaleta heshima kwenye ndoa na hivyo kuweza kurejesha furaha”Alisema.

Mwisho

KATIBU MKUU MWAKALINGA AMKALIA KOONI MKANDARASI

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa (wa pili kushoto), alipokagua ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa katika barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.

Muonekano wa sehemu ya lami ya prime katika ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya. Mradi huu unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.

Timu ya wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) ikiongozwa na Mhandisi Joyce Mbunju, wakikagua tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.

Kazi zikiendelea za usukaji wa nondo katika Daraja la Lupa litakalokuwa na urefu wa mita 63 katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.

…………………..

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami kuhakikisha anamaliza mradi huo ndani ya muda wa mkataba na si vinginevyo.

Aidha, ameongeza kuwa hatamuongezea mkandarasi huyo muda wa kumaliza kwani muda aliopewa ulikuwa unamtosha kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Hayo ameyasema mkoani Mbeya alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amemuelekeza mkandarasi huyo kuongeza vitendea kazi na wataalamu ili kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliobakia.

“Natarajia utaongeza vifaa na wataalamu ili kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati, pia ukumbuke kuwa sitakupa muda wa nyongeza hivyo fanya juhudi ili umalize mradi huu ndani ya muda”, amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 unajengwa na mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo zote ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.

Arch. Mwakalinga amemuelekeza pia mkandarasi kutumia muda wake wote kuwa katika eneo la mradi hata ikiwezekana kuongeza masaa ya kufanya kazi usiku na mchana.

“Fanyeni kazi usiku na mchana ili kuepukana na changamoto za vipindi vya mvua na hakikisheni barabara hii inajengwa kwa viwango vya ubora zaidi”, amesema Arch. Mwakalinga.

Naye, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 53 ukilinganisha na muda wa mkataba uliotumika ambao ni miezi 23 sawa na asilimia 85.19 ya muda wa mkataba.

Eng. Mwita ameeleza kuwa mkandarasi mpaka sasa ameshakamilisha kujenga tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, lami ya prime KM 6.78 na kazi zingine za ujenzi wa makalvati madogo na madaraja makubwa matatu zikiendelea.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ya Singida na Tabora ambapo barabara hii ikikamilika itaongeza zaidi fursa za kimaendeleo kwa wananchi kiuchumi na usafirishaji.

SUMATRA PWANI YABANA MAGARI YANAYOKATISHA RUTI

0
0

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MAGARI ya abiria kumi,yafanyayo safari zake Mbezi -Tumbi na Mbezi-Mlandizi yamekamatwa na kupigwa faini ya sh.100,000 kutokana na kukiuka kosa la kukatisha ruti.

Aidha magari yafanyayo safari zake Bagamoyo -Tegeta Nyuki na Kisarawe yametakiwa kutoza nauli zilizowekwa kisheria ili kuondoa malalamiko kwa abiria.

Akielezea kuhusu taarifa hiyo, ofisa mfawidhi SUMATRA,Mkoa wa Pwani ,Omary Ayubu alisema, wanatekeleza maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Pwani baada kupokea malalamiko na kuomba watatue tatizo la kukatisha ruti.

Alieleza , magari matatu yamekatisha ruti kutoka Mbezi – Tumbi ambayo yaligeuzia Njuweni na mengine saba yaligeuzia Kongowe.

Ayubu alisema ,wataendelea kuwachukulia hatua kali madereva na wamiliki wa magari hayo ili iwe fundisho kwa wengine ambapo mbali ya faini watapaswa kuzingatia taratibu za leseni zao pasipo kugeuza njiani.

” Zoezi hili ni endelevu ,hatuishii hapa ,licha ya mkuu wa mkoa kutoa maelekezo lakini na sisi tumejipanga kushirikiana na jeshi la polisu kupitia kikosi cha usalama barabarani.”

“Wamiliki wajieleze kwa siku saba ,kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua kali ya kufungiwa leseni au kufikishwa mahakamani.”Alibainisha Ayubu.

Akieleza kuhusu magari ya abiria yanayokwenda Bagamoyo kupitia Baobao alisema, wanaendelea kusisitiza wamiliki kuona umuhimu wa barabara hiyo.

Ayubu alifafanua, nayo magari yanayofanya safari zake Makumbusho-Tegeta Nyuki na njia ya kwenda Kisarawe waache kuzidisha nauli wafuate sheria na nauli zilizopangwa bila kuwaumiza abiria.

JIANDAENI NA MAISHA YA UZEENI ILI MSIJE KUILALAMIKIA SERIKALI – RC MTWARA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amewataka vijana ambao bado wana nguvu za kufanya kazi kujiandaa vyema na maisha ya uzeeni ili kuepuka kutoa lawama na kulalamikia Serikali katika maisha yao ya uzeeni.

Aidha Kiongozi huyo nameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kutunga Sheria ambayo itaainisha majukumu ya watoto kwa wazee, majukumu ya wazee kwa watoto pamoja na majukumu ya Serikali kwa wazee ikiwemo haki ya kulinda wazee kama ilivyo sheria ya Mtoto ya mwaka 2009.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Byakanwa  amesema hayo leo wakati wa akizindua Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wazee Duniani yanayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Mtwara  kwa Siku tatu kuanzia Septemba 29, na kufikia kiklele chake Octoba 1, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aliongeza kuwa wakati wa utunzi wa sheria ya wazee majukumu mengi yasirundikwe kwa Serikali lakini sheria hiyo iyaangazie majukumu hayo kwa jamii ili ione umuhimu wa kuwa na wajibu wa kuwatunza wazee.
 Byakanwa pia ametoa angalizo kwa viongozi walio Serikalini sasa kutambua kuwa suala hili sio la wazee peke yao bali ni suala lao  pia hivyo ni vyema wakatumia fursa waliyonayo  kuweka mazingira mazuri kwa wazee ili nao wafaidike nayo wakati wa uzee wao.

Aidha  Byakanwa amewataka vijana ambao kwa sasa  wananguvu kujiandaa kwa ajili ya uzee ili muda wao wa uzee wautumie vizuri kwa kukaa na kukumbushana masuala ambayo yatawapa faraja lakini sio kufikiria kuanza kuwekeza mitaji katika biashara.

Kiongozi huyo wa Mkoa wa Mtwara ameongeza kuwa ukatili dhidi ya wazee uko zaidi kwa jamii na sio ndani ya serikali na kwa kiasi kikubwa unafanywa kwa wazee ambao walitumia nguvu kubwa kuwatunza na kuwalea wakiwa watoto.

"Hili linalowatokea wazee ni fundisho kwa wengi kwamba sio lazima unapomtunza mtoto naye atakuja kukutunza kwasababu wazee wengi wako peke yao maana watoto wao wako sehemu mbalimbali wakitafuta maisha na wengine wamesahau kama wazee waliwalea na kuwatunza’’. Aliongeza Byakanwa.     

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika hotuba yake kwa Mgeni rasmi amesema kuwa changamoto zinazowakabili hapa Nchini ni pamoja na umasikini uanaotokana na ukosefu wa nguvu za kufanya kazi pamoja na magonjwa yanayotoka na umri kuwa mkubwa.

Aidha Dkt Jingu ameongeza kuwa changamoto nyingine inatokana na watu kushindwa kujiandaa na maisha ya uzee lakini pia akiongeza kuwa Serikali inafanya jitihada kubwa kuhakikisha inatoa huduma kwa wazee ili kuweza kupunguza changamoto zinazowakabili.

Dkt. Jingu ametaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na Sera ya matibabu bure kwa wazee, uwepo wa mabaraza ya wazee na mapitio ya Sera ya wazee ili kuhakikisha kuwa inajitosheleza lakini pia Serikali ina makao 17 ya wazee ambayo yanapokea wazee wasiokuwa na ndugu wala Jamii ya kuwahudumia.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiongea na mzee aliyefika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona kupata matibabu bure ya wazee kabla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yanayoendelea Mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akisoma bango katika viwanja vya Nangwanda Sijaona kabla ya kufungua Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yanayoendelea Mkoani Mtwara.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea na vyombo vya habari mara baada ya ufunguzi  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yanayoendelea Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wazee wakiendelea kupatiwa huduma ya matibabu bure wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yanayoendelea Mkoani Mtwara.

KATIBU MKUU MWAKALINGA AMKALIA KOONI MKANDARASI

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa (wa pili kushoto), alipokagua ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa katika barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.
 Muonekano wa sehemu ya lami ya prime katika  ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya. Mradi huu unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.
 Timu ya wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) ikiongozwa na Mhandisi Joyce Mbunju, wakikagua tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.
Kazi zikiendelea za usukaji wa nondo katika Daraja la Lupa litakalokuwa na urefu wa mita 63 katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami kuhakikisha anamaliza mradi huo ndani ya muda wa mkataba na si vinginevyo.

Aidha, ameongeza kuwa hatamuongezea mkandarasi huyo muda wa kumaliza kwani muda aliopewa ulikuwa unamtosha kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Hayo ameyasema mkoani Mbeya alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amemuelekeza mkandarasi huyo kuongeza vitendea kazi na wataalamu ili kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliobakia.

"Natarajia utaongeza vifaa na wataalamu ili kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati, pia ukumbuke kuwa sitakupa muda wa nyongeza hivyo fanya juhudi ili umalize mradi huu ndani ya muda", amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 unajengwa na mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo zote ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.

Arch. Mwakalinga amemuelekeza pia mkandarasi kutumia muda wake wote kuwa katika eneo la mradi hata ikiwezekana kuongeza masaa ya kufanya kazi usiku na mchana.

"Fanyeni kazi usiku na mchana ili kuepukana na changamoto za vipindi vya mvua na hakikisheni barabara hii inajengwa kwa viwango vya ubora zaidi", amesema Arch. Mwakalinga.

Naye, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 53 ukilinganisha na muda wa mkataba uliotumika ambao ni miezi 23 sawa na asilimia 85.19 ya muda wa mkataba.

Eng. Mwita ameeleza kuwa mkandarasi mpaka sasa ameshakamilisha kujenga tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, lami ya prime KM 6.78 na kazi zingine za ujenzi wa makalvati madogo na madaraja makubwa matatu zikiendelea.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ya Singida na Tabora ambapo barabara hii ikikamilika itaongeza zaidi fursa za kimaendeleo kwa wananchi kiuchumi na usafirishaji. 

NCHI 67 KUSHIRIKI KONGAMANO LA TATU LA MAFUTA NA GESI LITAKALOFANYIKA OKTOBA 2 NA 3 JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KONGAMANO la tatu la sekta ya mafuta na gesi litakalofanyika Oktoba 2 na 3 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es Salaam litazikutanisha nchi 67 ambazo zitawaweka pamoja wadau na viongozi muhimu wa sekta ya nishati kutoka serikalini na sekta binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Ocean Business Partners na mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini Balozi Abdulsamad Abdulrahim amesema kuwa malengo ya kongamano hilo ni pamoja na kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Joseph Magufuli ambaye daima amekuwa akihamasisha kujenga nchi ya viwanda na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

"Tutaendelea kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais na kupitia kongamano hili tunategemea kufukua ajira, bunifu mbalimbali pamoja kuweka mahusiano bora ya kibiashara baina ya wazawa na wageni" ameeleza Abdulsamad.

Amesema kuwa kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki zaidi ya 600 litachambua umuhimu wa kimkakati na nafasi ya Tanzania kama kitovu cha Afrika Mashariki katika uendelezaji mkubwa wa sekta ya nishati.

"Washiriki wa kongamano hili watapata fursa ya kufahamu hali ya sasa ya sekta ya nishati nchini, mikakati ya kufikia Tanzania ya viwanda pamoja na kujifunza namna ya kufanya makubaliano ya kibiashara baina ya makampuni ya kimataifa na yale yaliyoko nje ya nchi" ameeleza Abdulsamad.

Amesema kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mipango ya muda mfupi ya usambazaji na uhitaji wa nishati nchini,  ushiriki wa wajasiriamali wadogo katika sekta hiyo pamoja na ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kuyafikia malengo na hiyo itaenda sambamba na utoaji wa tuzo maalumu kwa baadhi ya washiriki.

" Tuzo mbalimbali zitatolewa ikiwemo tuzo kwa kampuni bora nchini, kampuni bora ya kimataifa na kampuni bora ya mfano ya wazawa pamoja na tuzo nyingine kwa wanafunzi wa vyuo walioshinda katika mashindano ya insha ambao watapata ufadhili wa masomo ili kuendeleza vyema sekta hii na pia mwanamke shupavu katika sekta hiyo na tutawasajili wanawake wote ili kutoa chachu kwa wanawake wengine" ameeleza.

Balozi Abdulsamad amesema kuwa viongozi mbalimbali wa wa Serikali wakiongozwa na waziri wa nishati Dkt. medard Kalemani watashiriki katika kongamano hilo ambalo pia limetoa fursa za kutangaza vivutio vya utalii na kutoa ajira na fursa mbalimbali za kiuchumi kwa watanzania.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watoa huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini Balozi Abdulsamad Abdulrahim na Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Ocean Business Partners Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la tatu la sekta ya mafuta na gesi na kueleza kuwa fursa zaidi ajira na uwekezaji zinategemewa kupatikana kupitia kongamano hilo, leo jijini Dar es Salaam

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA USHAURI WAKE WA KUWASAMEHE WATUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI WALIO TAYARI KUTUBU NA KURUDISHA FEDHA NA MALI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga kumkabidhi taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga akitoa muhtasari kabla ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Dkt. Moses Kusiluka.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga baada ya kupiga naye picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga katika picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019. Picha na Ikulu

WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA PENSHENI JAMII

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii  Dkt. John Jingu akifungua kongamano la wazee lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara katika mfulululizo wa maadhimisho ya Kimataifa ya Wazee.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii  Dkt. naftari Ngondi   akifafanua jambo wakati wa  kongamano la wazee lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara.
 Baadhi ya washiriki kongamano la wazee linaloendelea katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara.
Mzee Seifu Nantapika Katibu Mtandao wa Wazee Mkoa wa Mtwara akitoa salamu kwa wazee washiriki kongamano la wazee lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara

Baraza la Wazee limeiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwasaidia wazee kwa kuwapatia pensheni jamii itakayowasaidia katika mahitaji yao ya kila siku kwa wazee ambao hawakuwa katika ajira rasmi.

Hayo yamebainika leo mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wazee kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Benki ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya Kongamano hilo Katibu wa Baraza la Wazee la Halmashauri ya Mji wa Kahama Mzee Anderson Lyimo amesema kuwa wazee wamelitumikia taifa katika Nyanja mbalimbali hivyo ni suala la muhimu kwa Serikali kutafakari na kuwapatia wazee pensheni jamii itakayowasaidia kutatua changamoto ndogondogo za kimaisha.

Mzee Lyimo ameongeza kuwa pensheni ya jamii kwa wazee itawasaidia wazee kuondokana na utegemezi kwa jamii hasa kuondokana na wimbi la wazee ombaomba ambalo kwa kiasi kikubwa hutokana na wazee kukosa fedha za kujikimu kwa mahitaji yao madogo madogo.

“Tunakuomba Mhe. Rais Magufuli tukumbuke katika suala la pensheni jamii kwetu sisi wazee itatusaidia sana kwa mfano wenzetu wa Zanzibar wanapata elfu 20 angalau kupata kuliko kukosa kabisa” alisisitiza Mzee Lyimo.

Mzee Lyimo amesisitiza kuwa jamii inawajibu wa kuwalea na kuwatunza wazee kwa asilimia kubwa na kuwaasa vijana kutowatelekeza wazazi wao wakati wanapozeeka na wajue kuwa ni wajibu wao kuwalea na kuwatunza wazee kama wao walivyotunzwa wakiwa watoto.  

Akifungua Kongamano hilo Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa Kongamano hilo litumike kutafakari kwa jinsi gani taifa litafanya kuwalea na kuwatunza wazee na kupata njia sahihi za kupambana na changamoto zinazowakabili.

Dkt. Jingu ameongeza kuwa ni muhimu sana kwa taifa kujadili suala la kuwaenzi na kuwatunza wazee pamoja na kuhakikisha wanakuwa na ustawi mzuri katika maisha yao ili waendelea kutoa mchango wao katika ujenzi wa taifa.

“Naomba tujadilia pia wajibu wa jamii katika kuwatunza na kuwaenzi wazee kama wazazi wao ndugu na jamaa waliochangia nguvu zao katika ujenzi wa taifa letu” alisema Dkt. Jingu

Dkt. Jingu ametaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na Sera ya matibabu bure kwa wazee, uwepo wa mabaraza ya wazee na mapitio ya Sera ya wazee ili kuhakikisha kuwa inajitosheleza lakini pia Serikali ina makao 17 ya wazee ambayo yanapokea wazee wasiokuwa na ndugu wala jamii ya kuwahudumia.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Wazee na Wastaafu mkoa wa Arusha Bi. Miriam Urio amewataka vijana nchini kuachana na vitendo vya imani za kishirikiana kusababisha vifo kwa wazazi wao kwasababu ya uzee bali wawatunze na kuwalea wazee wao kama wao walivyowatunza wakiwa watoto. 

DKT. SALIM ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA URAFIKI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

0
0

Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, leo asubuhi tarehe 29 Septemba 2019 amemtunukia Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa. Dk. Salim Ahmed Salim, Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika jijini Beijing.  Mheshimiwa Dkt. Salim anakuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Nishani hiyo ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.

Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.

Mbali na Dk.Salim,  wengine waliotunukiwa Nishani ya Urafiki ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Kikoministi cha Cuba Jenerali Raul Castro, Dada wa Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Kiongozi wa Jumuiya ya Urafiki ya China na Urusi Ndugu Galina Kulikova, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Bi  Isabel Crook  kutoka Canada.

Vilevile  Rais Xi alitoa Nishani  ya Jamhuri na Nishani ya Heshima ya Taifa kwa raia 36 wa China kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa la China kupitia kazi zao katika fani mbalimbali.

Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim  kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.

Tukio la Kutoa Nishani limetangazwa moja kwa moja na Televisheni zote za Jamhuri ya Watu wa China na kushuhudiwa na watu zaidi ya Milioni 500.

Kwa mujibu wa maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini China Ndugu Mbelwa Kairuki Kupitia tukio la leo, mamilioni ya Wachina hususan vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa  wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.

Aidha Balozi Kairuki ameeleza kwamba maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka 55 ya urafiki na udugu kati ya China na Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964. Uhusiano wa China na Tanzania uliotokana na uhusiano mzuri wa waasisi wa mataifa haya mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Tsetung. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huu umekwenda mbali zaidi ya uhusiano kati ya Serikali na Serikali na kushamiri kwa uhusiano wa watu kwa watu.

Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa  kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.
Bi. Maryam Salim akiwa katika picha na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping baada ya kupokea nishani kwa niaba ya baba yake

 Bi Maryam Salim akiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki mara baada ya kupokea nishani.

DKT. MWANJELWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA JIJINI MWANZA

0
0


 Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akitoa ufafanuzi wa michoro ya ramani ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akielekeza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firmin Msiangi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akisoma taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Wengine ni watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA DENMARK, UFARANZA NA QATAR HAPA NCHINI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bibi.Mette Norgaard Dissing Spandet wakati Balozi Spandet alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bibi.  Mette Norgaard Dissing Spandet wakati Balozi Spandet alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019. kwa ajili ya kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bw. Frederic Clavier wakati Balozi Clavier  alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kuelezea Mipango na Mlengo ya maendeleo ya Nchi yake kwa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bw. Frederic Clavier  wakati Balozi Clavier alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kuelezea Mipango na Mlengo ya maendeleo ya Nchi yake kwa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa Nchini Bw. Abdulla Jassim Al-Maadadi wakati Balozi Al-Maadadi  alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili kuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha kazi hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Qatar hapa Nchini Bw. Abdulla Jassim Al-Maadadi wakati Balozi Al-Maadadi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili kuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha kazi hapa Nchini..(Picha na Ofisi ya Makamu ya Rais)

MAKALA KUHUSU HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUTOKA KWA MZEE PIUS MSEKWA - SPIKA WA BUNGE MSTAAFU

0
0

MWALIMU NYERERE KAMA NILIVYOMFAHAMU MIMI.
Maelezo yanayotolewa hapa kuhusu Mwalimu Nyerere, yanatoka kwangu mimi binafsi. Yanatokana na vile nilivyomfahamu kiongozi huyo nilipokuwa ninafanya naye kazi karibu sana kwa muda mrefu wa miaka ishirini na mitano, nikiwa msaidizi wake wa karibu.
        Kabla ya kueleza sifa za Mwalimu Nyerere, ni vizuri kwanza kumkumbusha msomaji kwamba, mwalimu nyerere alikuwa ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Kwa hiyo bila shaka yeye pia alikuwa na mapungufu yale ya binadamu, kama vile hasira, amabazo kwa wakati mwingine zilimsababishia kufanya makossa katika uamuzi wake kutokana na hasira iliyompata ghafla. Ipo mifano kadhaa ya kuthibitisha hilo.

Mifano ya uamuzi wake uliotokana na hasira
Mfano mmoja ni ile siku alipowavurumisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofanya maandamano ya kupinga mpango wa wanafunzi waliomaliza elimu ya Sekondari kulazimika kwenda kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Katika tukio hilo, baadhi yao walipayuka maneno ya ovyo kwa kusema “Heri wakati wa ukoloni” wakimaanisha kwamba hali ya nchi ilikuwa bora Zaidi wakati wa utawala wa Kikoloni. Maneno hayo yalimkasirisha Rais Nyerere kiasi cha kuamuru kuwafukuza Chuoni  na kuamuru Chuo hicho kifungwe, wanafunzi wote walirudishwa makwao kwa likizo ya lazima ya miaka miwili, ili watumie muda huo kutafakari kosa waliolifanya wakiwa pamoja na wazazi wao.
         Mfano mwingine unaofanana na huo, ni wakati wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam walipofanya maandamano ya kupinga tukio la kulaani Sertikali ya Uingereza, wakati koloni lake la Rhodesia ya Kusini lilipojitangazia uhuru wake kinyemela mwezi Novemba 1965; na serikali ya Uingereza haikuchukua hatua yoyote dhidi ya viongozi waasi wa koloni hilo.
         Maandamano hayo yaliwafikisha kwenye jengo la Ubalozi wa Uingereza mjini Dar Es Salaam, ambapo waliharibu baadhi ya mali zilizokuwemo katika jengo hilo. Kutokana na kitendo hicho, vijana waliohusika walikamatwa na polisi na kuzuiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi. Baada ya hapo, Mwalimu Nyerere aliagiza vijana hao wapelekwe Ikulu ili azungumze nao. Walipofika huko, aliwapokea vizuri na kuwaeleza ubaya wa kosa lao la kufanya maandamano bila kibali cha Polisi; pamoja na kosa jingine la kuharibu mali katika jengo la Ubalozi wa Uingereza.
Hatimaye aliwataka waende kuomba radhi kwa Balozi wa Uingereza kwa kosa hilo la kuharibu mali ya Ubalozi huo. Baada ya kusema hivyo, Rais Nyerere aliuliza kama kulikuwa na yeyote miongoni  mwao ambaye alikuwa anapinga wazo hillo la kwenda kuomba radhi. Mwanafunzi mmoja akajitokeza na kusema kuwa yeye analipinga. Papo hapo Rais Nyerere alimwamuru kamishina wa polisi amkamate kijana huyo na kumpeleka akachapwe viboko sita. Siku moja baada ya tukio hilo; Rais Nyerere alimwita kijana huyo aende Ikulu, ambapo alimweleza kwamba alikuwa ametoa adhabu hiyo kutokana na hasira iliyompanda ghafla, na kwamba hasira hiyo ilimrejesha kwenye hulka za ualimu wake wa darasani, ambapo wanafunzi hupewa adhabu za kuchapwa viboko. Kitendo hicho kinadhihirisha uungwana wa Mwalimu Nyerere alidhihirisha kuwa tayari kukiri kosa, bila kujali wadhifa mzito aliokuwa nao kama Raisi wa Nchi.
           Mfano mwingine ni pale alipomfukuza kazi ghafla aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati huo. Hii ilitokana na waziri huyo kushindwa kutekeleza maagizo ya Rais ya kukataa shinikizo la kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania; ambalo lilitolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwanzoni mwa mwaka 1981. Kilichotokea kwa Waziri huyo ni kwamba badala ya kutekeleza maagizo ya Rais, Yeye aliunga mkono shinikizo la IMF kwa kushabikia kushushwa kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. Rais Nyerere alikasirika sana alipopata habari hizo. Alimwita Waziri huyo na kumtaka awasilishe kwake mara moja barua ya kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Fedha.
             Mfano mwingine ni siku alipoulizwa maswali ya kipuuzi na mwandishi mmoja wa habari wa Kenya, swali ambalo lilimpandisha hasira. Waandishi wa habari wa Kenya, walikuwa wamesikia maneno yaliyosemwa na mwanasiasa uchwara mmoja wa Tanzania, aliyelopoka kwamba eti  Mwalimu Nyerere hakuwa Mtanzania wa kuzaliwa hapa, bali ni mtu aliyetoka Burundi. Upuuzi huo uliandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya hapa nchini. Siku moja baadaye, Mwalimu Nyerere akiwa katika safari zake za kawaida, alipita katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi. Mwandishi mmoja wa habari wa Kenya aliyekuwepo hapo uwanjani akamuuliza Mwalimu Nyerere swali, “Mwalimu , tumesikia tuhuma kuwa wewe siyo Mtanzania, bali ni Mrundi. Je, tuhuma hizo zina ukweli?” swali hilo lilimuudhi sana Mwalimu Nyerere, akamjibu kwa hasira na kejeli, “Umesema kuwa umesikia tuhuma hizo. Je, ukisikia tuhuma nyingine kwmba mimi ndiye baba yako niliyezaa na mama yako, utakuja kuniuliza kama tuhuma hiuzo ni kweli?”Jibu hilo liliwafanya waandishi wenzake wote  watambue kwamba swali la mwenzao huyo lilikuwa la kijinga na halikustahili kuulizwa, kwani jibu lake lilikuwa wazi kabisa kuwa siyo kweli.




SIFA ZA MWALIMU NYERERE
Ukiondoa mapungufu ya aina hiyo ambayo ni ya ;kila binadamu, mwonekano wa jumla wa tabia ya Mwalimu Nyerere kwa watu mbalimbali, ulikuwa ni wa kuheshimika sana, hususani katika maeneo yafuatayo:

Alikuwa na ujasiri wa kukiri makosa aliyoyafanya
Hapo juu tumetaja mfano mmojawapo wa sifa yake hii. Yaani sifa ya kuwa na ujasiri, pamoja na unyenyekevu wa kukiri makosa ambayo alifanya katika uongozi wake. Si viongozi wengi duniani walio na ujasiri wa aina hiyo.
           Kuna mifano mingine miwili ambayo inadhihirisha sifa yake hii. Kwanza, ni uamuzi wa kufuta Serikali za Mitaa mnamo mwaka 1975. Kama tutakavyoona baadaye, yeye mwnyewe baadaye alitoa kauli bungeni, ya kukiri kosa hilo. Alisema hivi: ‘kufikia mwaka 1982, tukatambua kwamba tulifanya kosa kubwa kwa kufuta Serikali za Mitaa. Kwa hiyo, tukaliomba Bunge kupitisha sheria ya kuzizindua tena wilayani na mijini”. Kosa la pili alilokiri ni kufutwa kwa vyama vya ushirika. Katika kukiri kosa hilo, Mwalimu Nyerere alisema “Vyama vya Ushirika vimeanzishwa tena. Kufutwa kwa vyama hivyo lilikuwa kosa jingine kubwa tulilolifanya katika miaka iliyopita”. 

Alitumia elimu yake kwa faida ya wote
Sifa yake nyingine ni kwamba Mwalimu Nyerere alitumia elimu yake vizuri sana kulingana na ahadi ya mwanachama wa CCM, inayosema kuwa “Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu, na nitatumia elimu yangu kwa faida ya wote”.
            Kwa hakika Mwalimu Nyerere alitumia elimu yake kwa faida ya wote. Kila hotuba aliyoitoa, ilikuwa ni darasa tosha kwa wasikilizaji wake. Aidha, Makala zake nyingi na za aina mbalimbali alizoziandika, vilevile zilitosha  kabisa kuwa ni Makala za kufundishia.
              Kwa bahati nzuri, hotuba zake nyingi zimechapishwa kwenye vitabu vyake vyenye majina ya : Uhuru na Umoja; Uhuru na Ujamaa; pamoja na vitabu vingine vingi alivyoviandika yeye mwenyewe, kama vile  vya Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania 
               Pia, Mwalimu Nyerere alikuwa na kipaji maalumu cha kubuni vidokezo vinavyoeleza  jambo kubwa katika maneno machache . mifano yake ni kama vile , “Uhuru na Kazi” ; “Inawezekana, timiza wajibu wako” ; “We must run while others walk” (Sisi lazima tukimbie wakati wenzetu wanatembea);  “Linalowezekana leo, lisingoje kesho”; “Kupanga ni kuchagua” n.k

Alikuwa na kipaji cha kufundisha kwa kutumia mifano na methali
Kwa mfano, katika moja ya hotuba zake za mwanzo baada ya kuzaliwa kwa CCM, Mwalimu Nyerere alizungumzia suala lililokuwa linamkera sana, la uchafu unaosababishwa na takataka nyingi zinazotupwa ovyo katika mitaa yetu. Katika kuwatahadharisha wananchi wasipuuzie kuwepo kwa tatizo hilo, kwani linaweza kuleta mlipuko wa magonjwa; alitumia methali ya Kizanaki, ambayo tafasiri yake ni, “Mfichaficha maradhi, kilio kitamuumbua”.
              Aidha katika utaratibu wake wa kusimamia maadili ya viongozi, mara nyingi alitumia methali hii, “Mtoto akichezea wembe, utamkata papo hapo”. Akimaanisha kwamba, Kiongozi anayekiuka maadili sharti achukuliwe hatua mara moja, bila kumchelewesha.
Siku moja, Mwalimu Nyerere alipokuwa akisisitiza umuhimu wa mafunzo kwa viongozi na watendaji wa Chama cha Mapinduzi, aliamua kutumia hadithi ya mtoto wa jongoo, ambayo aliihadithia mwenyewe kama ifuatavyo:
“Mama jongoo alizaa mtoto. Mtoto huyo alipojikuta ana miguu mingi sana, akamuuliza mamaye; Je, mama, katika miguu yote hii, nikitaka kutembea nitangulize mguu gani? Mama jongoo akamjibu: wewe tembea tu, miguu itajua yenyewe itakavyojipanga”.
Alikuwa akizungumzia umuhimu wa kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kwa ajili ya viongozi na watendaji wa chama chetu. Alisema kuwa mahitaji ya mafunzo kwao hayawezi kupewa majibu kama hayo ya mama jongoo; kwamba eti wakisha chaguliwa au kuteuliwa, tuwaambie tu. “fanyeni kazi mliyopewa. Jinsimtakavyofanya mtajua wenyewe” (Mtajiju). Alituasa kuwa “Hiyo haifai kabisa”.
Katika utaratibu wake huo wa kufundisha kwa kutumia mifano, alipochukua hatua ya kumwajibisha kiongozi kwa kosa ambalo angependa liwe ni mfano kwa viongozi wengine wote, aliwapelekea taarifa juu ya hatua aliyokuwa amemchukulia kiongozi aliyemwajibisha ili wajue.
Siku moja katika miezi  ya mwanzo yam waka 1981, Mwalimu Nyerere alikuwa katika ziara mkoani Mwanza. Kulikuwa na tukio moja la kujaribu kumdanganya, ambalo lilisababisha Mkuu wa Mkoa achukuliwe hatua ya kufutwa kazi. Mkuu huyo wa Mkoa alimpeleka Rais Nyerere kumwonesha shamba la mbogamboga, ambalo alidai kuwa ni shamba la Ujamaa, kwa madhumuni ya kumthibitishia Rais kuwa alikuwa msitari wa mbele katika kutekeleza Azimio la Arusha.
             Inasemekana kuwa Mwalimu Nyerere alidokezwa mapema na wasaidizi wake, kwamba shamba hilo lilikuwa limepandwa usiku wa kuamukia siku hiyo ya ziara yake, kwa madhumuni ya kumdanganya Rais. Kwa hiyo alipofika hapo shambani, alishika mmea mmojawapo na kuutikisa ili kuona uimara wake. Mmea huo uling’oka, kwa kuwa mizizi ilikuwa bado haijashika vizuri.
              Aliporejea Ikulu baada ya ziara hiyo, Rais Nyerere aliandika barua ya kumfukuza kazi mara moja Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ili kumwajibisha kwa kosa hilo kubwa alilokuwa amelifanya. Lakini Rais Nyerere hakuishia hapo, bali aliandika maelezo marefu ya kufafanua kwanini alichukua hatua hiyo; na aliagiza maelezo hayo yakapelekwa kwa wakuu wote wa Mikoa yote, ili liwe ni fundisho kwao.
              Mfano  mwingine ni mwaka 1977, Rais Nyerere alipowawajibisha mawaziri wawili wa Serikali yake na Wakuu wa Mikoa wawili, kwa kuwataka waandike barua mara moja za kujiuzulu nafasi zao za uongozi walizokuwa nazo. 
Sababu yake ya kuwachukulia hatua hiyo ilikuiwa ni kuwawajibisha kutokana na mauuaji yaliyokuwa yamefanywa na vyombo vya usalama vya Serikali katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Mawaziri wawili waliowajibishwa ni Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, wakati huo akiwa ndugu Ali Hassan Mwinyi pamoja na Waziri mwenye dhamana ya Usalama wa Taifa. Wakuu wa Mikoa waliohusika ni wa Mikoa ya Shinyanga na Mwanza.
Kwa hiyo, aliagiza nakala za barua hiyo wapelekewe viongozi wote wa Serikali, hususan Mawaziri na Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya, ili suala hili la Kiongozi kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na watendaji walio chini ya dhamana yake ya uongozi, liwe fundisho kwao, na wajifunze kuiga mfano huo wa ndugu Ali Hassan Mwinyi.

Alihamasisha watu kwa kutumia “nguvu ya hoja”
Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuridhisha watu kwa kutumia nguvu ya hoja zake. Kwa kingereza uwezo huo unaitwa “power ofpersuasion”. Uwezo huo ndio uliomuwezesha kupata mafanikio makubwa katika malengo yake mengi ya kisiasa; kama inavyodhihirishwa na matukio yafuatayo:
               Kwanza, ni pale alipofanikiwa kuwaridhisha kwa nguvu za hoja  zake, wanachama wa iliyokuwa asasi ya kupigania maslahi ya wafanyakazi wa Kiafrika katika Serikali ya Kikoloni, iliyokuwa inaitwa “Tanganyika African Association” (TAA). Alifanikiwa kuwashawishi wanachama wa asasi hiyo kukubali wenyewe kuvunja chama chao hicho, na badala yake kuunda chama kipya cha siasa cha “Tanganyika African National Union” (TANU), mnamo mwezi Julai, 1954, ili kiwe ni chombo cha kisiasa cha kupigania Uhuru wa Tanganyika.
            Mfano wa pili ni pale alipofanikiwa kuwaridhisha kwa kutumia nguvu ya hoja zake, wanachama wa chama hicho cha TANU, wakakubali kukivunja chama chao hicho  na kukiunganisha na chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar, ili kuunda chama kipya, Chama cha Mapinduzi (CCM); ili kiwe ni chombo chenye uwezo na nguvu kubwa Zaidi ya kuongoza nchi yetu.Mfano wa tatu ni pale alipofanikiwa kuwaridhisha kwa kutumia nguvu ya hoja zake, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TANU uliofanyika Tabora mwaka 1958, wakakubali sheria ya, “kura tatu” iliyokuwa imetungwa na Serikali ya Kikoloni wakati huo. Nguvu ya hoja yake ilikuwa ni kwamba kama mkutano huo ungeamua kukataa sharia hiyo, chama cha TANU kisingeruhusiwa kushiriki katika uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi September mwaka huo; na matokeo yake yangekuwa ni kuchelesha kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika. Hali halisi iliyokuwepo ni kwamba wajumbe walio wengi katika mkutano huo, walikuwa wamejiandaa kuikataa sheria hiyo ya “kura tatu” Mwalimu Nyerere aliarifiwa mapema kabla ya mkutano kuhusu msimamo huo wa wajumbe, kwa hiyo yeye pia akaandaa mkakati wake mapema. Kwanza aliomba mkutano uchague mwenyekiti mwingine (wa muda) wa mkutano huo, ili yeye aweze kutoa hoja zake mkutanoni akiwa kama mjumbe wa kawaida, ili kuepuka kishawishi cha kutumia mamlaka ya “kiti” kulazimisha wajumbe kukubali mawazo yake.
                  Kutokana na uwezo wake huo wa kuridhisha watu kwa kutumia “nguvu ya hoja” ulivyo mkubwa, ingawa katika mkutano huo kazi hiyo ilikuwa ngumu sana, lakini bado  aliweza kuwaridhisha wajumbe, wakaikubali sheria hiyo. Uamuzi huo ulibadilisha kabisa historia ya Tanganyika , kwani ulisababisha Uhuru wa Tanganyika kupatikana katika muda mfupi sana wa miaka saba tu baada ya chama cha TANU kuundwa, mwaka 1954.
              Halikadhalika, ni uwezo wake wa kuridhisha watu kwa “nguvu ya hoja” zake, ndio uliofanikisha harakati zake  za kuunganisha maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Tanganyika katika kudai Uhuru wa Tanganyika. Alifanikiwa kufanya hivyo kwa hotuba zake zilizoweza kuwafanya wananchi wabaini ubaya na aibu ya kutawaliwa na wakoloni; na kuwafanya wawe tayari kujitolea na kujituma  kushiriki katika harakati hizo. Ilibidi watu wajitole, kwa sababu TANU wakati huo haikuwa na vitendea kazi kama magari wala fedha za kufanyia kazi hiyo.

Maoni ya watu wengine kuhusu sifa za Mwalimu Nyerere
Sifa za Mwalimu Nyerere zimeelezwa kwa namna tofauti na watu wengi wengine waliomfahamu. Kwa mfano, katika kumkaribisha kuhutubia mkutano ulioandaliwa na “African American Institute” ya huko Marekani tarehe 10 Feburuari, 1960; mshehereshaji wa hafla hiyo alimtambulisha Mwalimu Nyerere kwa maneno yafuatayo:
“Mr. Nyerere has won the confidence of all groups in Tanganyika by his wisdom, modesty and humour”.
(Bwana Nyerere ameaminiwa na makundi yote ya huko Tanganyika kutokana na busara zake, unyenyekevu wake na ucheshi wake).

Naye mwandishi Peter Haussler, katika kitabu chake kiitwacho, “Leadership for Democratic Development in Tanzania,” aliandika kuwa:
“The leadership style of Nyerere is also referred to as “charismatic” and “visionary”. Charismatic leadership is the ability to influence followers based on supernatural gifts and attractive powers. Followers enjoy being with the charismatic leader because they fell inspired, correct and important”.
(Uongozi wa Mwalimu Nyerere umeelezwa mara nyingi kuwa ni wenye haiba kubwa, wa mtu mwenye kuona mbali. Kiongozi mwenye haiba ni yule mwenye uwezo wa ajabu wa kuwawishi na kuvutia watu, aina ya uwezo ambao si wa dunia hii. Wafuasi wake wanafurahia kuwa karibu naye kwa sababu anawatia moyo, wanajiona kuwa wako sahihi, na ni watu wenye maana).
Vilevile, katika kijitabu kinachoitwa, “Memories of Julius Nyerere”, kilichochapishwa mwaka 2009 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya kifo chake, ambacho kilichangiwa na waandishi kadhaa, mwandishi mmoja alimweleza kuwa:
“Nyerere was an iconic leder, a man of principle, intelligence, and integrity”. 
(Nyerere alikuwa ni kiongozi mwenye taswira ya pekee, mwenye kusimamia misingi na maadili mema, na mwenye akili nyingi).
Mwndishi mwingine alimweleza Mwalimu Nyerere kuwa:
“He was considered a political prophet by many, and a man of intelligence, humour and honesty’
(Wengi walimwona kuwa ni kama nabii wa kisiasa, na mtu mwenye maadili mema, mchangamfu mwenye ucheshi, na mkweli).

Mimi mwenyewe vilevile nilipewa nafasi ya kuchangia Makala katika kijitabu hicho ambapo nilisema hivi:
“Nyerere has been variously described as a humanist, politician, thinker, and statesman. Indeed, Nyerere was all of those things and much more. He was an ardent believer in peace, and a unque mobilizer of people. He was a devout catholic, but a strong believer in the separation of religion from politics. He was 
a modest man in his personal life, and hated pomposity in his official life”
(Nyerere ameelezwa na watu wengi mbalimbali kwamba alikuwa ni mpenda watu, mwenye kufikiri sana, na mwanasiasa mweledi. Ni kweli kabisa kwamba, Nyerere alikuwa na sifa zote hizo, pamoja na nyingine Zaidi. Kwani alikuwa ni muumini mkubwa katika suala la Amani, na hodari sana wa kuandaa watu. Alikuwa ni mfuasi mwaminifu sana wa dini Katoliki, lakini hakupenda kabisa kuchanganya dini na mambo ya siasa. Alikuwa ni mtu mwenye staha katika maisha yake binafsi, na alichukia sana ufahari katika maisha yake kama kiongozi).
Katika dondoo la kueleza sifa za Nyerere lililosomwa na Waziri Mkuu wa India, Bibi Indira Gandhi, katika sherehe za kumkabidhi tuzo ya, “Jawaharlal Nehru Award for International Understanding” tarehe 17 Januari, 1976, Mwalimu Nyerere alitajwa kuwa :
“A man of vision, a man of action, and a man of compassion”.
(Mtu mwenye kuona mbali, mtu wa vitendo, na mtu mwenye huruma).
Kabla ya hapo, katika sherehe hiyohiyo, Rais wa India alimweleza Mwalimu Nyerere kuwa:
“He is one of the foremost champions of human rights. He is a man of the people, gifted with great commonsense”
(Mwalimu Nyerere ni mmoja wa watu walioko mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu. Ni mtu wa watu, na amejaliwa kuwa na kiwango kikubwa mno cha maarifa na busara za kawaida).
Kwa ujumla, katika maisha yake yote, Mwalimu Nyerere alidhihirisha kwamba alikuwa na sifa zote hizo, kwani alitekeleza ipasavyo misingi yote ya maadili mema, siyo tu katika maisha yake binafsi, bali pia katika maisha yake ya uongozi. Na alifanya hivyo katika kipindi chote cha uhai wake, kama inavyobainishwa katika maelezo yanayofuatia hapa chini:

MAISHA BINAFSI YA MWALIMU NYERERE
Kuhusu maisha yake binafsi, Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa zifuatazo:
  1. Alikuwa ni mtu mwadilifu sana, asiyekuwa na makuu, mtu mwenye staha, mtu aliyetosheka; na asuyekuwa n ahata chembe ya majivuno.
Kwa mfano, alipoanza kushika wadhifa wa Rais, hakupenda hata kidogo kujihusisha na zile mbwembwe ambazo kwa kawaida huambatana na wadhifa huo. Ifuatavyo ni mifano michache inayothibitisha tabia yake hiyo:
             Baadhi ya watu waliomfahamu alipokuwa mwanafunzi katika shule ya sekondari Tabora, wameeleza kwamba hata wakati huo akiwa bado mwanafunzi, tayari alikwisha kujenga tabia ya kuchukia marupurupu ya upendeleo (privileges) yaliyokuwa yakitolewa kwa wanfunzi wenye  nafasi za uongozi, yaani viranja. Hatimaye msimamo wake huo ulidhihirika wakati yeye mwenyewe alipochaguliwa kuwa kiranja, ambapo alitumia kipaji chake cha ushawishi, kupunguza marupurupu ya cheo hicho cha viranja wa wanafunzi katika shule hiyo.
            Mfano mwingine nilioushuhudia mimi mwenyewe, ni kwamba alipokwisha kuchaguliwa na kuapishwa kuwa Rais wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1962, shughuli yake ya kwanza ilikuwa ni kulifungua na kulihutubia Bunge la Kwanza la Jamhuri ya Tanganyika siku ya kesho yake tarehe 10 Desemba, 1962. Mimi wakati huo nikiwa Katibu wa Bunge, ndiye nilikuwa mwandalizi wa ratiba ya shughuli hiyo kubwa.




Nilijaribu kuiga   ratiba ambayo hutumika katika Bunge la Uingereza (House of Commons) wakati Malkia wao anapokwenda kuhutubia Bunge hilo mwanzoni mwa kila mwaka wa shughuli zake. Katika sherehe hizo huwa anasindikizwa na Afisa mmoja wa kike ambaye cheo chake kinaitwa, “Lady-in-Waiting”. Kwa kuwa nilikuwa nimesomeshwa kazi za Ukatibu wa Bunge katika Bunge hilo la Uingereza, niliamini kuwa huo ndio utaratibu unaofaa kutumiwa pia katika Bunge jipya la Tanganyika. Kwa hiyo nikapanga kuweka ndani ya ukumbi wa Bunge sambamba na kiti cha Rais mwenyewe, kiti cha mke wa Rais Mama Maria Nyerere, na kiti cha msindikizaji wake wa kike, ambaye nilimwonyesha katika ratiba yangu ya shughuli hiyo kwa cheo hicho nilichokijua cha “Lady-in- Waiting”.

         Kumbe Rais Nyerere hakupendezwa na mbwembwe hizo. Aliziona kuwa ni za Kisultani, zinazofaa kwa Masultani tu. Kwa hiyo baada ya tukio hilo alituagiza tuachane kabisa na mbwembwe hizo, alizoziita ni za kijinga.
        Wakati huo, vilevile watu walikuwa wameanza kutumia maneno, “Mtukufu Rais” katika hotuba zilizomtaja yeye, au katika barua zilizokwenda kwake. Kuzuia hilo, aliandika waraka wa kuagiza kwamba asiitwe, “Mtukufu Rais” wakati wowote na mahali popote; iwe ni katika mazungumzo ya kawaida, ama katika hotuba, au hata katika maandishi yoyote. Akaelekeza kwamba, maneno rasimi katika mawasiliano ya aina hiyo yawe ni “Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Tanganyika” na si vinginevyo. Aidha katika utaratibu wake wa kukataa mbwembwe, Rais Nyerere pia aliwaagiza polisi waache tabia yao ya kufunga kila barabara anayopita Rais, kwa muda usiojulikana, hadi hapo Rais atakapokuwa amepita. “Hii inanifanya niwe kero kubwa kwa watu wa Dar Es Salaam”, alisema.





  1. Alikuwa ni mtu asiyependa kujilimbikizia mali
Hii ni tabia yake nyingine ambayo inamtofautisha na viongozi wengine wengi duniani wa ngazi hiyo kubwa katika Mataifa yao.
           Kwa mfano, Mwalimu Nyerere hakuwahi kununua gari lake mwenyewe binafsi na kwa ajili hiyo, hakuwahi hata kujifunza kuendesha gari.
         Wakati alipokuwa mwalimu katika shule ya sekondari Pugu, sisi wanafunzi tulishuhudia siku moja akipanda nyuma ya gari la shule aina ya pick-up single cabin. Alikuwa anakwenda mjini Dar Es Salaam, bila shaka kwenye shughuli zake za kisiasa alizokuwa amezianza wakati huo. Katika kiti cha mbele walikuwa wamekaa walimu wenzake Mapadre wawili Wazungu wa Shirika la “Holy Ghost Fathers”. Sisi wanafunzi tulidhani alikuwa amefanyiwa dharau ya ubaguzi wa rangi na Mapadre hao wazungu.
          Baadaye katika mazungumzo naye nje ya darasa, mwanafunzi mwenzetu mmoja allimweleza Mwalimu Nyerere hisia zetu hizo, tulipomwona akipanda nyuma ya gari la shule “kama mzigo”. Majibu ya Mwalimu Nyerere yalikuwa kwamba Mapadre walikuwa wamemwambia akae pamoja nao katika kiti cha mbele. Lakini yeye alikataa kwa sababu hakuona haja ya kubanana kwenye kiti hicho, wakati nyuma ya gari palikuwa na nafasi kubwa ya kukaa. Ndiyo sababu aliamua kukaa nyuma ya gari. Kwa hakika, Mwalimu Nyerere hakuwa na makuu.
         Mfano mwingine wa tabia yake ni kwamba mnamo mwezi Januari mwaka 1976, Mwalimu Nyerere alitunukiwa tuzo maarufu ya “Jawahrlal Nehru Award for International Understanding”. Tuzo hiyo inaambatana na zawadi ya kiasi kikubwa cha dola za Kimarekani, kama dola laki moja. Yeye baada ya kuzipokea fedha hizo alizikabidhi zote kwa Chuo cha TANU cha Kivukoni ili zitumike kanunulia vitabu vya maktaba ya chuo hicho. Ni Dhahiri kwamba hakuwa na tabia ya kujilimbikizia mali.
         Ukiacha mifano hiyo, Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kutusimulia hadithi moja, kwamba katika safari zake za kwenda kudai uhuru kwenye Umoja wa Mataifa huko New York – Marekani, safari moja alikutana na rafiki yake ambaye alikuwa anaishi huko. Rafiki yake huyo akamwambia kuwa angependa kumununulia zawadi ya viatu lakini kwa kuwa alikuwa hajui saizi yake ya viatu, akamshauri waende wote dukani ili akamnunulie viatu vya saizi inayomfaa.
        Mwalimu Nyerere akakubali kupokea zawadi hiyo, wakaenda duka la viatu ambako alichagua jozi moja ya viatu vya rangi nyeusi. Rafiki yake huyo akamshawishi achague jozi ya pili, lakini Mwalimu Nyerere alikataa. Rafiki yake akamuuliza kwanini hataki jozi ya pili, Mwalimu akamjibu hivi; si kwa  sababu ninayo jozi moja tu ya miguu! (I have only one pair of feet!) kwa hakika hakutaka kujilimbikizia mali hata kama mali, hiyo ni viatu tu.

  1. Alikuwa ni mtu mwenye kumtegemea sana Mungu
Jambo hilo lilikuja kudhihirika miaka kumi baada ya kifo chake, ambapo kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, lilipoanzisha mchakato wa kumfanya hayati Mwalimu Nyerere kuwa ni “Mtakatifu wa Mungu”. Hatua ya kwanza muhimu katika safari ya kuelekea kwenye daraja la Mtakatifu wa Mungu ni kutangazwa kuwa “mtumishi wa Mungu”, ngazi ambayo Mwalimu Nyerere tayari amekwishaifikia. Baada ya kuanza kwa mchakato huo. Kanisa Katoliki nchini Uganda, lilishirikiana na Rais Museveni wan chi hiyo; limeshiriki kwa nguvu katika kuendeleza mchakato huo. Kwani kuanzia mwaka 2007, kanisa  hilo la Uganda lilitenga tarehe 1 Juni ya kila mwaka kuwa ni siku ya kuombea mafanikio ya mchakato huo. Maadhimisho hayo hufanyika mahali panapoitwa “Namugongo” huko Kampala Uganda. Katika maadhimisho ya mwaka 2011, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitangaza kuwa;
“We shall continue comimg back here every June 1 to pray for the beatification of our beloved father, which is the next stage. Then we will always pray for him to be canonized.”
(Tutaendelea kuja hapa Namugongo kila tarehe 1 ya mwezi Juni, kuombea mafanikio ya mchakato huu wa kumfikisha baba yetu mpendwa kwenye Daraja la “Mwenye Heri” ambayo ndiyo hatua inayo fuatia baada ya hapo tutaendelea kumwombea afikishwe kwenye daraja la juu zaidi la Utakatifu).
Kwa hakika Mwalimu Nyerere alikuwa ni mcha Mungu sana, kutokana na tabia yake ya kuhudhuria Ibada ya Misa Takatifu kila siku asubuhi, katika kanisa la Mt. Petro Oysterbay, ambalo lilikuwa la karibu Zaidi na nyumbani kwake Msasani. Lakini vilevile alikuwa na tabia nzuri ya kuomba uongozi na msaada wa Mwenyezi Mungu wa kumuwezesha kufikia uamuzi wa busara katika masuala yaliyokuwa nyeti na magumu kwake.
          Mfano mmoja ambao unadhihirisha tabia yake hiyo, ni jinsi alivyofikia uamuzi mgumu wa kuruhusu majeshi ya Tanzania yavuke mpaka na kwenda Kampala kumwadhibu vikali aliyekuwa Mtawala wa Uganda wakati huo, Iddi Amin Dada, aliyekuwa maefanya uvamizi wan chi yetu katika mkoa wa Kagera, Nitasimulia habari hii zaidi hapo baadaye.





  1. Hata alipokuwa Rais aliishi maisha ya mtu wa kawaida.
Ingawa alikuwa na nafasi ya juu kabisa na yenye heshima kubwa katika jamii, ya kuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; lakini bado Mwalimu Nyerere alichagua kuishi maisha ya mwananchi wa kawaida. Kwani aliishi maisha yake yote kama wanavyoishi wananchi wa kawaida, wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kifedha. Katika hilo, kaulimbiu yake ilikuwa ni “Kiongozi wa watu lazima afanane na watu anaowaongoza”.
           Kwa mfano nyumba yake aliyokuwa akiishi pale kijijini kwake Butiama, ni iliile aliyoijenga akiwa bado kijana, katika maandalizi ya kufunga ndoa na Mama Maria Nyerere. Lakini hata baada ya kuwa Rais wan chi, bado aliendelea kuishi katika nyumba hiyo ndogo ya chumba kimoja tu cha kulala. Kwa sababu hiyo, alipotangaza katika Mkutano Mkuu wa Tanu wa kumteua kuwa mgombea Urais mwezi September 1975, kwamba angestaafu kazi ya urais ifikapo mwaka 1980; chama cha Tanu kilipitisha azimio la kumpatia zawadi ya kumjengea nyumba bora Zaidi katika kijiji chake cha Butiama, ambayo ataitumia kama makazi yake baada ya kustaafu.
          Nyumba hiyo aliyohaidiwa ilianza kujengwa mwaka 1977, mara baada ya kuzaliwa kwa CCM, ujenzi ambao ulikamilika mwaka 1980. Mimi nikiwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM wakati huo, ndiye niliyepewa heshima ya kuikabidhi nyumba hiyo mpya kwake na familia yake, katika sherehe fupi iliyofanyika hapo Butiama mwezi Desemba 1980.
        Aidha, kwa upande wa makazi yake ya Dar Es Salaam, Mwalimu Nyerere alijijengea mwenyewe nyumba hiyo alipokuwa tayari amekwisha kushika wadhifa wa Rais wan chi yetu, kwa kutumia mkopo wa Benki. Ujenzi wake ulipokamilika tu, alihama kutoka Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba yake hiyo ya Msasani, ambako aliendelea kuishi hadi mwisho wa maisha yake hapa duniani.
          Mfano mwingine tena wa uadilifu wake, ni wakati alipopelekewa pendekezo la kujengewa barabara ya lami kutoka kijijini kwake Butiama hadi sehemu inayoitwa Makutano, ili kuiunganisha na barabara ya lami inayotoka Musoma kwenda Mwanza, kwa lengo la kufanya makazi ya Rais kule Butiama yaweze kufikika kwa barabara ya lami. Lakini Mwalimu Nyerere alikataa kuidhinisha pendekezo hilo, kwa maelezo kwamba hakutaka fedha za umma zitumike katika kumpendelea yeye kutokana na Urais wake, wakati mahitaji ya wananchi wengine yalikuwa ni makubwa Zaidi.

  1. Alikuwa ni msomi ambaye ni mfano wa kuigwa
Mwalimu Nyerere alikuwa na tabia nzuri sana ya kusoma vitabu. Kwa ajili hiyo alikuwa na maktaba yake binafsi yenye vitabu vingi sana nyumbani kwake Msasani, na vilevile nyumbani kwake Butiama.
          Ni kutokana na kutambua tabia yake hiyo ya kupenda kusoma vitabu, ndiyo sababu alipostaafu wadhifa wa Urais wa nchi mwaka 1985, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliamua kumzawadia seti nzima ya vitabu 33, vinavyoitwa Encyclopaedia Britanica. Watu wengi wanakumbuka jinsi makundi mbalimbali ya wananchi wa Tanzania, pamoja na baadhi ya watu binafsi; walivyojipanga kumpatia Mwalimu Nyerere zawadi nyingi za aina mbalimbali wakati alipostaafu Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wengine walitoa zawadi ya ng’ombe, wengine walitoa matrekta ya kulimia na kadhalika. Zawadi ya Chama cha Mapinduzi ilikuwa ni kumjengea nyumba ya kuishi Kijijini kwake Butiama. Halikadhalika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), vilevile ilimjengea nyumba ya kuishi Butiama. Lakini Bunge liliamua kumuzawadia vitabu.
       Pamoja na kupenda kusoma vitabu, Mwalimu Nyerere pia alikuwa ni mwandishi hodari wa vitabu, pamoja na Makala fasaha za aina mbalimbali, zikielezea mambo tofautitofauti. Baadhi ya hizo aliziandika kwa lugha ya Kiswahili, na nyingine akiziandika kwa lugha ya Kingereza, hususani zile zilizolenga wasomaji wake wa Kimataifa. Miongoni mwa hizo ni, “Principles and development”; “Stability and Change in Africa”; “The Honour of Africa” na “The South-South Option”
Lakini juhudi zake za kisomi zinazozoshangaza zaidi, ni pale alipofanya kazi ya kutafsiri vitabu maarufu vilivyoandikwa kwa kingereza, na kuviweka katika Lugha ya Kiswahili. Vitabu hivyo maarufu ni pamoja na sehemu ya Agano jipya la Biblia Takatifu, ambayo ni injili zote nne, kama zilivyoandikwa na watakatifu MATHAYO; MARKO; LUKA; YOHANA. Tafsiri yake inaitwa TENZI ZA BIBLIA, vitabu hivyo vilichapishwa na Peramiho Mission Press, Songea). Vitabu vingine alivyovitafsiri kwa Kiswahili ni vile vilivyoandikwa na mwandishi maarufu wa fasihi za kingereza Wiliam Shakespeare, ambavyo ni JILIUS CAESAR na THE MERCHANT OF VENICE
Kuhusiana na juhudi zake hizo, jambo kubwa zaidi na la kushgangaza kabisa, ni je, alipata wapi muida wa lutosha kufanya kazi hiyo? Ikizingatiwa kwamba Toleo la kwanza la Tafsiri ya Julius Caeser ( kwa Kiswahili: Julias Kaizari) lililochapishwa na shirika la Oxford University Press, lilitoka mwaka 1967;  miaka ambayo ni dhahiri mwalimu Nyerere alikuwa katika harakati nzito za kuijenga nchi yetu changa, mara baada ya kupatikana na uhuru mwishoni mwa mwaka 1961; pamoja na harakati nyingine za ukombozi wan chi zingine za Bara la Afrika kutoka  katika kutawaliwa na wakoloni; inashangaza kuona kwamba mwalimu Nyerere, aliyekuwa mtumishi wa umma nambari moja, aliweza kupata muda wa kufanya hivyo, inakuwaje wengine, wenye majukumu madogo zaidi kuliko aliyokuwa nayo yeye, wanashindwa?
Mchango  wa mwalimu Nyerere katika kustawisha Kiswahili
Juhudi za mwalimu Nyerere za kutafsiri vitabu hivyo na kuviweka katika lugha ya Kiswahili, zilikuwa na sababu nyingine kubwa  ambayo yafaa pia kuifahamu. Sababu yake ilikuwa ni kuonesha utajiri wa lugha ya Kiswahili ulivyo mkubwa, kiasi kwamba kinayo maneno ya kutosha, sawa na fasihi za Lugha ya kingereza, kilichokuwa kinatumika mashuleni kama lugha ya kufundishia.
Lakini siyo hilo tu. Jitihada za Mwalimu Nyerere za  kutukuza Kiswahili zilianza mapema zaidi, mara tu baada ya kupatikana uhuru wa nchi yetu; ambapo Mwalimu Nyerere, (akiwa ndiye kiongozi Mkuu wa nchi), alitangaza Kiswahili kuwa ndiyo lugha rasmi ya taifa letu. Maana ya tanzazo hilo ilikuwa ni kwamba shughuli zote za serikali (ambazo ilikuwa inawezekana kuziendesha kwa kiswahili), ilibidi sasa ziendeshwe kwa lugha hiyo ya Taifa. Na papo hapo iliamliwa pia kwamba shughuli za mijadala ya Bunge  zianze mara moja kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili. Na ndipo neno ‘Bunge’ lilipobuniwa, kutokana na neno la Kiganda “BULANGE”; lenye maana ya ‘Bunge la Buganda’ (inayotawaliwa na Mfalume Kabaka ndani ya Jamuhuri ya Uganda)
Kwa upande wa Elimu yake ya darasani, mbali na shahada yake ya M.A. aliyotunukiwa baada ya kufaulu masomo katika chuo Kikuu cha Edinburgh, Uingereza;  vile vile alitunukiwa shahada nyingine nyingi za heshima (honorary Degrees) na vyuo vikuu mbalimbali duaniani; ambavyo ni pamoja na Edinburgh (uingereza); Duquesne (marekani); Cairo (Misri); Nsukka (Nigeria); Ibadan (Nigeria); Harare (Zimbabwe); Monrovia (Liberia); Toronto (Canada); Howard (Marekani); Jawahral Nehru (India); Havana (Cuba); Lesotho  (Lesotho); The Philipines (Ufilipino); na Fort Hare (Afrika Kusini).
MAISHA YA MWALIMU NYERERE KAMA KIONGOZI
Katika maisha yake kama kiongozi wa nchi, Mwalimu alitawaliwa kwa kiwango kikubwa sana na Imani thibiti aliyokuwa nayo; kwamba “binadamu wote ni sawa”, na kwamba “kila mtu anastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake”.
Mifano michache iliyotolewa hapo juu inasaidia kuthibitisha kwamba imani yake hiyo ndiyo ilikuwa msingi mkubwa wa uamuzi wake mwingi aliokuwa akiufanya katika kipindi cha uongozi wake. Vielelezo vya utekelezaji wa imani yake hiyo, ni kama ifuatavyo:-
  1. Alichukizwa sana na dhuluma, uonevu, na upendeleo
Kuhusu juhudi zake za kupambana na dhuluma na uonevu katika jamii, ipo mifano kadhaa ya vitendo vyake vinavyodhihirisha mapambano hayo. Kwanza, mapema mwaka 1963, muda mfupi tu baada ya kushika madaraka ya Rais wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya kufuta Kodi iliyokuwa inaitwa ‘kodi ya kichwa’. Kodi hii ilikuwa ikitozwa kwa  kila mtu mzima, bila kujali uwezo wake wa kulipa. Alifuta kodi hiyo kutokana na kitendo kilichomuudhi sana cha kukamatwa kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wameshindwa kuilipa. Walioswekwa ndani katika mahabusu moja katika kijiji cha ilemela, Karibu na mji wa Mwanza
Kutokana na msongamano ulivyokuwa mkubwa katika mahabusu hiyo, baadhi ya watu hao walifariki dunia. Habari hizo zilipomfikia Rais Nyerere, aliamuru kufutwa kwa kodi hiyo mara moja, kwani aliona kuwa ilikuwa inasababisha dhuluma na uonevu kwa wananchi walio wengi
Baadaye tutaona mifano mingine ya vitendo vyake vilivyotokana na tabia yake hiyo ya kuchukia dhuluma, unyanyasaji, ubaguzi, Uonevu,  na hata upendeleo usiofaa.
  1. Alikuwa ni jasiri wa kufanya uamuzi mgumu na nyeti
Ujasiri wake wa kufanya uamuzi mzito na mgumu, ulitokana na msimamo wake imara na usiotetereka wa kutetea misingi aliyokuwa  anaiamini kwa dhati. Msimamo huo ulidhihirika tangu mwanzoni kabisa mwa kipindi cha uongozi wake, hata kabla ya kupata uhuru, Baadhi ya mifano ya vitendo vyake katika kipindi hicho ni hii ifuatayo:
Kama sehemu ya mapambano aliyokuwa akiyaongoza dhidi ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukifanywa na Serikali za makaburu wa Afrika Kusini, pamoja na udhalimu wa serikali ya Ureno iliyokuwa inatawala Msumbiji, mara tu alipopata madaraka ya kumwezesha kufanya hivyo, alifanya uamuzi wa kijasiri sana  unaoelezwa katika kifungu hiki. Ulikuwa uamuzi wa kijasiri kwa sababu, kwa kiasi Fulani, aliathiri uchumi wa Tanganyika. Bila shaka, Rais Nyerere alitambua kuwapo kwa athari hizo, lakini alitetea uamuzi wake huo kwa maelezo kwamba hizo zilikuwa ni gharama za kusimama kwenye misingi (the cost of principle); ambazo ilikuwa ni lazima kuzibeba kwa ajiri ya kutetea misingi hiyo:

  1. Alisusia bidhaa za Afrika Kusini
kuhusu Afrika Kusini, Mwalimu Nyerere alifanya mambo yafuatayo:
kwanza, alipiga marufuku uingizaji nchini Tanganyika wa bidhaa zozote kutoka Afrika Kusini.
Pili, alitangazia ulimwengu kwamba endapo Afrika kusini itaendelea kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, basi Tanganyika itakapopata uhuru wake haitajiunga na Jumuiya hiyo. Alieleza kuwa yeye, kama kiongozi wa Tanganyika huru, asingeweza kukaa meza moja na kiongozi wa serikali inayoendesha sera za ubaguzi kama hiyo ya Afika Kusini, katika vikao vya Jumuiya hiyo ya Madola.
Alifanya hivyo akijua athari zake kwa uchumi wa Tanganyika, ambao zingetokana na kutojiunga na Jumuiya ya Madola, kwani nchi hii ingekosa nisaada kutoka katika mataifa kama Uingereza na Canada, pamoja na kukosa nafuu za kibiashara (trade preferences) zilizokuwa zikitolewa kwa wanachama wa jumuiya hiyo. Lakini bado akawa na ujasiri wa kutoa kauli hiyo nzito.
Ilitokea bahati njema kwamba, kauli yake hiyo ilizaa matunda mazuri. Kwani tangazo lake hilo liligeuka kuwa shinikizo la kutosha kusababisha Serikali ya Afrika Kusini ijiondoe yenyewe katika uanachama wa Jumuiya hiyo. Baadaye Mwalimu Nyerere alitusimulia kuwa yeye mwenyewe hakuwa na matumaini kwamba kauli yake hiyo ingesikilizwa na wahusika, na kwamba yeye alikuwa hajapata habari ya matokeo hayo mpaka waziri wake Amir Jamal alipokwenda nyumbani kwake kumpasha habari hizo alizokuwa amezisikia kwenye matangazo ya BBC, kuwa serikali ya Afrika Kusini imejiondoa yenyewe katika Jumuiya ya Madola. Alituambia jinsi alivyopata mshangao wa furaha, kwani hakuwa ametegemea kupata matokeo mazuri na kwa haraka kiasi hicho.
  1. Alivunja uhusiano na Ureno
Mwalimu nyerere alivunja uhusiano wa kibihashara na Ureno, kwa sababu ya vitendo vya udhalimu alivyokuwa vikifanywa na nchi hiyo katika koloni lake la Msumbiji. Alifanya hivyo huku akijua kwamba uhusiano huo ungeendelea kuwepo, pengine angeweza kusaidia katika kuweka msimao wa pamoja wa kibihashara katika Nyanja za kimataifa, hususan bei za korosho na Mkonge, mazao ambayo yanalimwa katika Nchi zote mbili. Lakini kwa msingi wa kupambna ma udhalimu, bado alikataa uhusiano huo usiwepo.

  1. Alijitolea  kuunga mkono harakati za ukombozi wan chi za kusini mwa Afrika
Msimamo wake wa kusaidia kwa hali na mali juhudi za ukombozi wa nchi za kusini mwa afrika, ziliiweka nchi yetu katika hatari kubwa ya kushambuliwa kijeshi na nchi ambazo wapigania uhuru wake walihifadhiwa na kulindwa katika kambi kadhaa zilizokuwepo hapa nchini. Hatari hiyo ilizidi kuwa kubwa baada ya kukubali nchi yetu kuwa mwenyeji wa kamati ya ukombozi ya umoja wa Afrika (OAU Liberation Committee), ambayo ofisi zake ziliwekwa mjini Dar es salaam. Huo ulikuwa ni mchango mahususi wa Mwalimu Nyerere katika jitihada zake za kupinga dhuluma ya nchi hizo kutawaliwa na wakoloni. Lakini ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kuufanya katika mazingira ya wakati huo yalivyokuwa.

  1. Alikataa misaada ya Ujerumani
Mara baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kulitokea mgogoro wa kidplomasia ambao ulimsababisha Mwalimu Nyerere kufanya uamuzi mwingine mgumu, wa kuikataa misaada yote ya Ujerumani iliyokuwa imepanga kuitoa kwa nchi yetu. Wakati huo, ujerumani ilikuwa ni nchi mbili tofauti: Ujerumani ya mashariki na Ujerumani ya Magharibi. Ujerumani ya magharibi peke yake ndiyo ilikuwa na uhusiano wa kibalozi na Tanganyika kabla ya Muungano, na ilikuwa ikitoa misaada mingi kwetu.
Mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ujerumani ya Mashariki ilifungua uhusiano wa kibalozi na Zanzibar. Tukio hilo lilisababisha Ujerumani ya Magharibi kudai kwa nguvu,  kwamba Tanzania isiruhusu kuwapo kwa ubalozi wa Ujerumani ya Mashariki hapa nchini, kwa maana ya Zanzibar. Mashinikizo hayo yalitokana na msimamo wao wakati huo, uliojikita kwenye dhana iliyojulikana kwa jina la ‘Halshtein Doctrine’, dhana ambayo haikuruhusu kuwapo kwa uwakilishi wan chi zote mbili za Ujerumani katika nchi moja yoyote ya kigeni. Sababu yake ilikuwa kwamba Ujerumani ya Magharibi ilikuwa haitambui kabisa kuwepo kwa nchi inayoitwa Ujerumani ya Mashariki.
Katika kutafuta ufumbuzi  wa mgogoro huo, Rais Nyerere, kwa kutumia utaratibu wake wa kushawishi kwa kutumia “nguvu ya huja”, alishauri Ujerumani ya magharibi ikubali utumike utaratibu ambao tayari ulikuwa umekubaliwa utumike katika nchi ya Misri, ambapo Ujerumani ya Magharibi ilikuwa Ubalozi kamili, na ujerumani Mashariki pia alikubaliwa kuwa na uwakilishi katika ngazi ndogo zaidi ya ‘Consulate –General’.
Lakini Ujerumani ya Magharibi haikuuafiki ushauri huo, na wala haikuishia hapo; bali ilichukua hatua ya kuvunja mkataba wa miaka mitano uliokuwepo wa nchi hiyo kutoa msaada wa mafunzo ya kijeshi kwa wanajeshi wetu wa anga. Vilevile walitoa pia tishio kwamba hata misaada yao mingine vilevile itaondolewa kama Serikali ya Tanzania haitabadili msimamo wake juu ya suala hilo. Rais Nyerere hakuwa ni mtu wa kuyumbishwa kwa vitisho kama hivyo. Kwa hiyo, akaamuru Serikali ya Ujerumani Magharibi iondoe mara moja misaada yake mingine yote.
Kwa hakika, alikuwa ni uamuzi mgumu, kwa sababu uliathiri nchi yetu kiuchumi. Kwa mfano, ulifuta kabisa uwezekano wa kupata msaada wa Ujerumani katika mpango wa kuendeleza Bonde la mto Kilombero, ambao tayari Serikali ya Ujerumani ilikwisha kuukubali pamoja na kusimamisha ujenzi wa jingo la Nkurumah Hall katika chuo kikuu cha Dar es Salaam
  1. Alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza
Mnamo mwaka 1965, koloni la Uingereza lililokuwa likiitwa ‘southern Rhodesia’, lilijitangazia uhuru wake, bila idhini ya mwenye koloni lake hilo, yaani Serikali ya Uingereza. Kufuatia tukio hilo, Mawaziri wa nchi zote ambazo ni wanachama wa OAU, walifanya mkutano wa dharura mjini Addis Ababa,  kwa madhumuni ya kuzingatia tukio hilo, na kukubaliana juu ya hatua inayofaa kuchukuliwa na nchi za Afrika katika hali hiyo.
Tarehe 2 desemba, 1965, mkutano huo ulipitisha azimio la kuipatia Serikali ya Uingereza muda maalumu wa kuchukua hatua za kuzima uasi huo wa koloni lake hilo la ‘Southern Rhodesia’. Azimio hilo lilisema wazi kwamba endapo hadi kufikia tarehe 15 ya mwezi huo, serikali ya Uingereza haitakuwa imechukua hatua zozote za dhati kufanya hivyo basi nchi zote za umoja wa Afrika zitavunja uhusiano wa kidplomasia na Uingereza siku hiyo.
Serikali ya Uingereza haikuchukua hatua zozote zile. Kwa hiyo, bila kusita wala kuchelewa, ilipofika tarehe hiyo 15 Desemba, 1965, Rais Nyerere alitangaza kuvunjwa kwa uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Uingereza, katika kutekeleza uamuzi huo OAU.
Vilevile, huo ulikuwa ni uamuzi mgumu, kwa sababu uliathiri uchumi wetu. Kwa mfano, kulikuwa na makubaliano ambayo tayari yalikwisha kufikiwa, ingawa mkataba wake ulikuwa bado haujasainiwa, ya kupata mkopo usiokuwa na riba kutoka Serikali ya Uingereza, wa paundi za kiingereza milioni 7.5. Fedha ambazo zingetumika kutekeleza baadhi ya miradi iliyokuwa imewekwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano, uliokuwa unaanza kutekelezwa mwaka huo. Kutokana na tukio hilo, fedha hizo zilisitishwa  kutolewa (frozen) Ni vizuri kueleza hapa pia kwamba ulikuwa ni uamuzi mgumu kutokana na sababu nyingine, kwani ni nchi mbili tu jasiri za Tanzania na Ghana ndizo peke yake zilizochukua hatua ya kutekeleza uamuzi huo wa OAU. Nchi nyingine zote zilizobaki za Afrika hazikufanya hivyo, pamoja na kwamba zilikuwa zimeshiriki katika kupitisha Azimio hilo la Addis Ababa.
Inawezekana kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa amehisi kuwa usaliti huo ungetokea kwani jana yake tarehe 14 desemba, 1965, alikwenda kulihutubia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tena alifanya hivyo kwa lugha ya Kiingereza badala ya Kiswahili, kuashirikisha kwamba alikusudia nchi hizo nyingine ziweze kumsikia moja kwa moja bila kusubiri tafsiri.
Hotuba hiyo ya mwalimu Nyerere baadaye ilichapishwa katika kijitabu maalumu kilichopewa jina la, ‘The Honour of Africa’, (Heshima ya Afrika) ambacho kinaeleza umuhimu wa Afrika kuheshimu uamuzi wake mwenyewe. Miongoni mwa mambo mengi ya msingi aliyoyasema katika hotuba yake hiyo, ni pamoja na kuuliza maswali ya msingi kabisa yafuatayo:
“Can Africa fail to implement its own resolution? Do Africa states meet in solemn conclave merely to make a noise? Or do they mean what they say? The purpose of that resolution was to show that, Africa requires action to be taken against smith. If that action is not taken, do we just shrug our shoulders and do nothing about it? Can we – the African states – honourably do nothing to implement our own resolution?”
(Hivi kweli Afrika inaweza kushindwa kutekeleza uamuzi wake yenyewe? Nchi za Afrika zinaweza kweli kukaa katika kikao rasmi, kwa madhumuni ya kupiga kelele tu? Siyo kwamba yale watakayoyasema yana maana? Madhumuni ya azimio hilo yalikuwa ni kuonesha kwamba Afrika inadai hatua zichukuliwe dhidi ya Smith (Waziri Mkuu wa Rhodesia ya Kusini aliyejitangazia uhuru). Kama hatua hizo hazitachukuliwa, je, tunakunja mikono tu na kusema kwamba hatuna la kufanya? Hivi kweli nchi za Afrika zitakuwa zimelinda heshima yake kama hazitachukuwa hatua za kutekeleza azimio letu wenyewe?)
Mifano yote hiyo inadhihirisha msimamo wake ulivyokuwa imara sana katika kusimamia na kutetea kwa gharama yoyote, misingi ambayo aliiamini kwa dhati.
UAMUZI MWINGINE MGUMU WA MWALIMU NYERERE
  1. Uamuzi wa kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika 
Katika kumsaidia msomaji wa kitabu hiki aweze kumwelewa vizuri zaidi Mwalimu Nyerere, pamoja na sababu halisi za baadhi ya Uamuzi mwingine alikuwa akiufanya, tunaongeza mifano mingine ifuatayo.
Kwanza, ni uamuzi wake alioutangaza kwamba yuko tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kusubiri uhuru wa Kenya na Uganda, ili kuziwezesha nchi hizo tatu kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki (East Africa Federation) baada ya zote kuwa zimepata uhuru. Ni wazi kwamba baadhi ya viongozi wenzake katika TANU, hawakupendezwa na uamuzi wake huo, na wangeweza kumletea matatizo makubwa kama nguvu yake ya kukubalika katika jamii isingekuwa ni kubwa kama ilivyokuwa.
  1. Uamuzi wa kuitambua Biafra
Kutokana na imani yake kubwa kuhusu usawa wa binadamu, Mwalimu Nyerere alichukizwa sana kila alipoona binadamu Fulani wanaonewa au wanadhulumiwa na watawala wao.
            Ndiyo sababu alichukia sana utawala wa makaburu wa Afrika Kusini, kwa jinsi ulivyokuwa ukiwadhulumu na kuwanyanyasa watu weusi wa nchi hiyo. Ni sababu hiyo hiyo ya kuchukia dhuluma, ndiyo pia iliyomfanya atangaze kuitambua Biafra kama nchi inayopigania haki yake ya kujitawala wenyewe. Uamuzi huo ulikuwa ni mgumu kwa sababu Biafra ilikuwa ni sehemu ya Jamuhuri ya Shirikisho la Nigeria; pamoja na Umoja wa nchi huru za Afrika ulikuwa umepisha Azimio la kutambua mipaka ya nchi za Afrika iliyoachwa na wakoloni. Kwa hiyo, Biafra kupigania kujitenga kutoka shirikisho la Nigeria ilikuwa ni kitendo cha kukiuka azimio hilo la OAU.
Lakini pamoja na hayo, baada ya kuona jinsi watu wa sehemu hiyo ya Biafra walivyokuwa wanaonewa na kudhulumiwa na utawala wa Shirikisho la Nchi hiyo, hali ambayo ilifanya waamue kuanzisha mapigano ya kutaka wajiondoe kwenye shirikisho hilo. Mwalimu Nyerere aliamua kuunga mkono juhudi zao hizo, ili waondokane na dhuluma zilizokuwa zinawakabili kutoka kwa watawala wa Shirikisho la Nigeria.
Kwake yeye Mwalimu Nyerere, dhambi ya ubaguzi au dhuluma kwa watu kama ile iliyokuwa ikifanywa na makaburu wa Afrika kusini, inabaki kuwa ni dhambi ileile hata inapofanywa na watawala Nigeria, ambao ni wazawa. Ni lazima ilaaniwe
Mimi nilibahatika  kuwa miongoni mwa wageni waliokuwepo Ikulu kuhudhuria mkutano wake na waandishi wa habari wakati wa kuwatangazia uamuzi  wake huo, na niliweza kushuhudia hisia zake zilivyokuwa kali dhidi ya uonevu wa serikali ya shirikisho la Nigeria kwa wananchi wa Biafra, wakati alipokuwa akitoa maelezo yake. Hata hivyo, hatimaye Biafra ilishindwa katika vita vyake hivyo vya kujitenga. Kwa hiyo, iliendelea kuwa ni sehemu ya Shirikisho la Nigeria. Lakini kwa kitendo chake hicho, yeye alikwisha kuonesha msimamo wake wa kupinga dhuluma na maonevu yanaofanywa na Serikali yoyote dhidi ya raia wake.

MWISHO WA MAISHA YAKE.

Ugonjwa na kifo cha Mwalimu Nyerere
Kabla ya kifo chake, mimi, wakati huo nikiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiye nilipewa jukumu la kumpelekea Mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama, vile vitabu vya zawadi iliyotolewa kwake na Bunge, name nilifanya hivyo kwa heshima kubwa na taadhima.
        Zawadi hizo zilichelewa kupelekwa, kwa sababu vitabu hivyo vya Encyclopaedia Britanica, havikuweza kupatikana madukani vikiwa tayari vimekwisha kuchapishwa. Kwa hiyo, ilibidi vichapishwe upya huko Uingereza, na kusafirishwa kuletwa hapa nchini. Mchakato huo haukukamilika mapema. Hatimaye vilipowasili, ilikuwa ni wakati wa Mkutano wa Bunge bajeti ya mwaka 1999/2000; ndipo tukapanga utaratibu wa kuvipeleka Butiama baada ya kumalizika kwa Mkutano huo wa Bajeti.
          Ni bahati mbaya sana kwamba Mwalimu Nyerere hakupata nafasi ya kuvisoma na kuvitumia vitabu hivyo. Hii ni kwa sababu siku nilipofika Butiama kumkabidhi zawadi yake hiyo, nilimkuta akiwa tayari ni mgonjwa, amelala kitandani. Alikuwa ameanza kuumwa yale maradhi ambayo baadaye, mwezi huohuo, ilibidi apelekwe kutibiwa katika hospitali ya St. Thomas mjini London. Pamoja na jitihada kubwa za madaktari wa huko, bado hakuweza kupona. Mwenyezi Mungu alimwondoa duniani alfajiri ya tarehe 14 Oktoba, 1999.

Nilipata bahati ya kumwona huko London kabla hajafariki.
Mimi nilipata fursa ya kwenda kumjulia hali Mwalimu Nyerere wakati alipokuwa mgonjwa huko London. Ilikuwa  ni tarehe 25 Septemba, 1999, nilipokuwa njiani nikirudi kutoka nchi ya Trinidad and Tobago iliyopo katika visiwa vya Carribean; ambako nilikuwa nimekwenda kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association), nikiwa Spika wa Bunge la Tanzania. Katika mkutano huo, mimi nilipata bahati ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya utendaji (Executive Committee) ya chama hicho cha wabunge wa Jumuiya ya Madola; baada ya kuwashinda wagombea wenzangu wawili mmoja kutoka Canada na mwingine kutoka Cyprus.
          Kwa mujibu wa katiba yake, mwenyekiti wa Kamati hiyo ndiye kiongozi Mkuu wa Chama hicho. Kwa hiyo, nilitaka kumpelekea Mwalimu nyerere habari njema ya ushindi wangu huo, kwani ratiba ya ndege ilikuwa inanipitisha London ili kuunganisha na ndege zinazokuja Dar ES Salaam. Nilipangiwa na ubalozi wetu wa London utaratibu wa kumwona mahali alipokuwa amelazwa, na nikapata nafasi ya kuongea naye vizuri kwa muda usiopungua saa moja na nusu hivi, kuanzia saa sita mchana. Kutoka hapo nilikwenda moja kwa moja uwanja wa ndege wa Gatwick, kupanda ndege ya kurejea Dar Es Salaam.

Nilivyopokea taarifa ya kifo chake.
Kesho yake asubuhi, nilikwenda kwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, kwa lengo la kumpelekea habari njema za kuchaguliwa kwangu kuongoza chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola; pamoja na kumueleza nilivyopitia London kumjulia hali Mwalimu Nyerere, kwamba nilivyomwona na kuongea naye, alikuwa anaendelea vizuri na matibabu yake. Vilevile nilimjulisha Waziri Mkuu Mwalimu mwenyewe alivyokuwa ameniambia, kwamba alikuwa tayari amemwagiza Balozi wetu aliyepo London, amwandalie safari ya kurejea nyumbani wiki iliyokuwa inafuata; ili aweze kuja kukamilisha jukumu lake la kusuluhisha mgogoro wa Burundi. Lakini kumbe Mungu alikuwa na mpango tofauti kwake kwani baadaye siku hiyo hiyo, Balozi akaleta taarifa Serikalini kwamba hali ya Mwalimu Nyerere ilikuwa imebadilika ghafla jana yake jioni, na kwamba alikuwa amekata kauli, na hawezi tena kuongea. Taarifa za baadaye zilisema kwamba aliendelea katika hali hiyo ya kutoweza kuongea hadi alipoaga dunia, siku ya tano baadaye.
       Kumbe mimi ndiye niliyekuwa Kiongozi wa mwisho wa ngazi ya Taifa kuongea naye katika uhai wake! Kutokana na hali hiyo, ndiyo sababu mshituko wangu nilipopata taarifa ya kifo chake, ulikuwa ni mkubwa Zaidi.
      Hata hivyo nilifarijika nilipopewa heshima kubwa ya kuandika na baadaye kuusoma, wasifu (eulogy) wa marehemu Mwalimu Nyerere, katika mkusanyiko wa kitaifa wa maombolezo, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kabla mwili wake hujasafirishwa kwenda Butiama kwa mazishi.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Julius Nyerere,
mahali pema peponi.







DAWASA UBUNGO WAMKAMATA MWANANCHI AKIUZA MAJI KWENYE MAGARI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendelea na ukaguzi wa miundo mbinu ya maji inayohujumiwa na Wananchi wasio waaminifu.



Wananchi hao wamekuwa wanasababisha Mamlaka kupata hasara kubwa kwa kujiunganishia maji kwa njia ya wizi.

Zoezi la kuwabaini wahujumu wa miundo mbinu ya maji linaendelea kwa mikoa ya kihuduma DAWASA ambapo Mkoa wa Ubungo umeweza kubaini wizi wa maji kwa mteja asiye mwaminifu.

Akizungumzia zoezi hilo, Mwenyekiti wa kampeni maalum ya kupambana na wahujumu wa huduma na miundombinu Ubungo Frank Sulley amesema zoezi hilo limekua endelevu kwa Mkoa wa kihuduma Ubungo na wameweza kuwabaini wananchi wasio waaminifu wanaosababisha hasara kwa Mamlaka.

Amesema, wameweza kupata taarifa za kiintelijensia usiku wa kuamkia tarehe 27 Septemba 2019, na kufanikiwa kugundua wizi wa Maji eneo la Mbezi Inn alfajiri ya kuamkia tarehe 28 Septemba.

"Tuliweza kugundua hujuma iliyokua ikifanyika na Mteja asiye mwaminifu kwa kujaza maji kwenye kisima nyakati za usiku na na kuuza kwa Magari yanayofanya biashara ya kuuza maji,"amesema Sulley.

Amesema, ni kosa kisheria kwa mwananchi kujiunganishia maji na kuuza maji kwani hupunguzia Mamlaka Mapato na Serikali kwa ujumla.

Sulley ameeleza, mwananchi atakapokamatwa itapelekea kulipa faini isiyopungua milion 5 hadi milion 50 na ata kufikishwa Mahakamani.


Ofisi ya kihuduma Mkoa wa Ubungo inapenda kuwatahadharisha wananchi kuacha mara moja hujuma kwani hii ni hatari kwa ustawi wa Dawasa na Serikali kwa ujumla.
Mwenyekiti wa kampeni maalum ya kupambana na wahujumu wa huduma na miundombinu Mkoa wa Kihuduma Ubungo DAWASA, Frank Sulley akiwa na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa miundo mbinu na kubaini mwananchi akihujumu kwa kujaza maji kwenhe kisima na kuuza kwenye magari.
Mwenyekiti wa kampeni maalum ya kupambana na wahujumu wa huduma na miundombinu Mkoa wa Kihuduma Ubungo DAWASA, Frank Sulley akifungua kisima kinachodaiwa kujazwa maji na mwananchi na kisha kuyauza kwenye magari. Wakati wa ukaguzi wa miundo mbinu ya DAWASA ikiwa ni katika kupambana na wananchi wanaolihujumu Mamlaka.
Kisima kinachotumika na Mwananchi kujaza maji na kuyauza kwenye magari.

ACT- Wazalendo yawasilisha maombi ya kujiunga na kesi ya kikatiba

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

CHAMA cha ACT- Wazalendo kupitia bodi yake ya dhamini, wamewasilisha maombi ya kujiunga katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mkulima Dezydelius Patrick Mgoya, ambaye anahoji kuwepo kwa kikomo cha urais nchini.

Maombi hayo yamebainishwa leo Septemba 30, 2019 na Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo, Dk Eliezer Feleshi, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na maelekezo maalumu ya namna ya usikilizwaji wa pingamizi la awali la Seriali dhidi ya kesi ji Kiongozi Dk Feleshi ndiye kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo. Wengine katika kesi hiyo ni Dk. Benhajj Masoud na Seif Kulita.

Katika maombi hayo, ACT inayowakilishwa na kampuni ya uwakili ya Law Guards Advocates wamewasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura, wakiomba maombi yao yasikilizwe haraka.

Kufuatia maombi hayo, mahakama imesimamisha usikilizwaji wa kesi ya msingi na kuamua kusikiliza kwanza maombi hayo ya ACT-Wazalendo.

Jaji Feleshi ambae anaongoza jopo la majaji watau wakiwemo Dk. Benhajj Masoud na Seif Kulita amesema, maombi hayo ya ACT- Wazalendo yatasikilizwa na jaji mmoja ambaye atalitaarifu jopo hilo kuhusu uamuzi utakaofikiwa na kesi hiyo sasa itatajwa Oktoba 25 kwa ajili ya maelekezo muhimu.

Wakili wa ACT- Wazalendo, Jebra Kambole ameeleza kuwa maombi ya wateja wake yamepangwa kusikilizwa na jaji Benhajj na kwamba yamepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza keshokutwa, Jumatano, Oktoba 2, 2019.

Katika maombi hayo pamoja na mambo mengine, chama hicho kinadai kuwa ikiwa uamuzi wa kesi hiyo utapitishwa bila wao kushirikishwa kitaathirika na kwamba kina haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkulima huyo mkazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, Patrick Dezydelius Mgoya amefungua kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya ibara ya katiba inayoweka ukomo huo wa urais.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo namba 19 ya mwaka 2019 Mgoya anahoji Ibara ya 40 (2) ya Katiba ambayo inaweka ukomo wa mihula miwili tu ya miaka mitano mitano (10) ya uongozi katika nafasi hiyo ya urais.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itoe tamko na tafsiri ya maana sahihi na athari za masharti ya ibara hiyo.

Pia anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana dhahiri ya masharti ya Ibara ya 42(2) ya Katiba, kwa kuhusianisha na na masharti ya Ibara za 13, 21 na 22 za Katibahiyo.

Vilevile anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana ya Ibara hiyo ya 40(2) kwa kuhusianisha na Ibara ya 39 ya Katiba.

Katika hati yake ya kiapo kinachounga mkono kesi hiyo, Mgoya anadai kuwa lakini Ibara ya 40(2) ya Katiba inaweka ukomo wa muda wa mtu kuchaguliwa kuwa rais, kwamba mtu hawezi kuchaguli zaidi ya mara mbili kushikilia wadhifa wa uraisi

Hivyo anadai kuwa masharti ya ibara hiyo ya 40(2) yanakiuka haki za kikatiba za Ibara za 13, 21 na 22(2) za Katiba hiyohiyo kwa kutoa mihula miwili tu ya raia kuchaguliwa kuwa rais kwa ukomo wa miaka 10 tu.

Mgoya anadai kuwa ukomo uliowekwa chini ya Ibara ya 40(2) ya Katiba yanakinzana na haki ya kikatiba ya uhuru wa kushiriki katika shughuli za umma kwa kuchagua au kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na usawa mbele ya sheria chini ya Ibara ya 21 na 13

PUMA ENERGY TANZANIA YAMCHANGIA RC MAKONDA SHILINGI MILIONI 40 KUFANIKISHA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO 20 DAR

0
0
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy imeunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya  kuokoa maisha maisha watoto wanaogua ugonjwa wa moyo kwa kuchangia Shilingi milioni 40 ili kufanikisha upasuaji kwa watoto 20.

Mbali na kutoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia matibabu ya moyo kwa watoto hao, Kampuni hiyo ya mafuta ya Puma Tanzania imetoa zawadi kwa shule ya Msingi Kibamba pamoja na mwanafunzi wa shule hiyo kwa kushinda mchoro wa elimu ya usalama barabarani.

Akizungumza leo Septemba 30, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kikabidhi fedha hizo Mkurugenzi wa Puma Energy Dominic Dhanah, amesema hatua ya kuunga mkono kampeni hiyo ni kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu.

Amesema kampuni hiyo inatambua dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kusadia makundi yenye mahitaji maalum na ndio maana wameona kuna kila sababu ya kumuunga mkono Makonda katika kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo ambao wanahitaji kufanyiwa operesheni.

Kuhusu mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto wa shule za msingi, amesema yamesaidia kupunguza ajali katika maeneo ambayo wametoa mafunzo hivyo wanaamini kwa kufanya hivyo wanaokoa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora ya barabara inaendelea kusambaa.

Ameongeza kuwa lengo kubwa la mpango huu ni kuwafanya watoto hao kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara wakiwa bado wadogo. "Tunaamini kwa kufanya hivyo tunawaongezea uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa wa Tanzania wengi zaidi,” amesema Dhanah.

Amesema kazi hiyo kwa mwaka huu imefanyika katika mikoa ya Dodoma na visiwani Zanzibar ambapo jumla ya shule 34 zitafikiwa kwa mpango huu kwa mwaka 2019.

“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi Zaidi nchi nzima. Pia tutaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya Watanzania,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa  Kampuni ya Puma, imetoa kiasi cha Sh milioni 40 kwa ajili ya kugharamia matibabu ya watoto 20 ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo lakini wazazi mwao hawana uwezo wa kulipia matibabu.

“Puma wameonesha njia ya kujali na kutusaidia kwenye moyo. Niliomba msaada huo katika mkutano wa SADC. Nina watoto 500 pale Muhimbili wanaumwa moyo.

“Mimi nikialikwa mahali ninaomba msaada kwa wananchi wangu. Dominic wa Puma nilimuomba na gharama za matibabu kwa kila mtoto ni Shilingi milioni mbili kwa kiasi hiki cha fedha Shilingi milioni 40 sasa tunakwenda kurudisha tabasabu kwa watoto 20.

“Watapata operesheni kwakuwa sehemu ya faraja na mafanikio kwa mtoto atakayefanyiwa opesheni. Hata nilipokutana na Balozi wa Dubai baada ya kumueleza hili, yeye alikwenda kuleta madaktari ambao walifanya upasuaji wa matibabu kwa watoto 50.

"Mwezi ujao nitaunda kamati ya watu saba kwa ajili ya kusaka Shilingi bilioni moja, ili mpaka tukifika Desemba mwaka huu watoto wote wawe wamefanyiwa upasuaji,” amesema Makonda

Kuhusu idadi ya watu wanaopata ajali za barabarani, alisema kuwa kwa sasa imepungua kutokana na elimu ya usalama barabarani.

“Tuna imani watoto 1m atakuwa na uelewa iwapo wataelimishwa na wenzao. Watumia vyombo vya moto watambue kila mmoja ana jukumu la kufuata usalama barabarani. Kabla ya Desemba kutakuwa na check up ya bure kwa wanaotaka kwenda likizo.

“Mafundi wa bure watakuwapo, nataka waende vizuri kula likizo na warejee tena Dar wakiwa salama. Trafiki kwenye mwendokasi inafanya vibaya,” amesisitiza.

Hata hivyo Makonda aliagiza kukamatwa kwa madereva wanaotumia barabara za mwendokasi.

“Wanatumia barabara ya mwendokasi wakamatwe hakuna gari, pikipiki wala mtu anayepaswa kuitumia, Mwakyoma (RTO),  apeleke trafiki hapo,” ameongeza.

Kwa kukumbusha tu mpaka sasa wanafunzi zaidi ya 20,000 shule za msingi katika shule tisa  za Jiji la Dar essalaam  wamepata mafunzo ya usalama barabarani ambapo katika mashindano hayo Shule ya Msingi Kibamba iliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadiwa Sh.milioni nne.
 MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea mfao wa hundi wa Sh.milioni 40 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah kwa lengo la kusaidia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20 wenye maradhi ya moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa michoro ya alama za usalama Barabarani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu ya Usalama wa barabarani Amend Tom Bishop.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhi zawadi kwa mshindi wa shindano la michoro ya alama za usalama Barabarani kutoka Shule ya Msingi Kibamba, Emmanuel Massawe wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Puma Tanzania, Domonic Dhanah
 Mshindi wa shindano la michoro ya alama za usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam kutoka Shule ya Msingi Kibamba , Emmanuel Massawe (katikati) akishangilia pamoja na wanafunzi wenzake wa shule hiyo mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya mafuta ya Puma kwa kushirikiana na shirika la Amend na kufanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah wakiangalia kwa pamoja moja ya mchoro wa usalama barabarani uliochorwa na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibamba ambaye ndio umeshinda mashinda katika mashindano hayo.

MFUMO UTOAJI TAARIFA ZA BIASHARA NCHINI KUPUNGUZA VISHOKA, KUONGEZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI-NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
NAIBU Waziri wa  Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema Mfumo wa utoaji taarifa za biashara nchini utasaidia kupunguza vishoka na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa taasisi za umma.

Akizungumza na wadau wa biashara leo Septemba 30,2019,  Manyanya amesema mfumo huo ukitumiwa vizuri utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya biashara nchini.

Amesema mfumo huo utasaidia wafanyabishara kujua hatua kwa hatua namna ya kupata kibali cha biashara anapotaka kupeleka bidhaa zake nje ya nchi, kuingiza na kuzipitisha nchini.

Manyanya amesema utekelezaji wa mfumo huo ni hatua kubwa kwa nchi katika kutimiza makubaliano ya utekelezaji wa kipengele cha Mkataba wa Uwezeshaji Biashara nchini ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ulioanza kutekelezwa Februari 2017.

"Kwa ujumla mfumo huu utaboresha mazingira ya biashara nchini hivyo, kuchangia uchumi wa nchi kukua kwa sababu biashara zitakua na uzalishaji kuongezeka kutokana na urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko ya nje," amesema Manyanya.

Ameeleza kuwa pamoja na mfumo huo, serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Pia amesema jitihada hizo zinajumuisha mipango mbalimbali ya maboresho iliyoanza mwaka 2000 ambayo inajumuisha Mpango wa Maboresho kwenye Mfumo wa Udhibiti wa biashara Tanzania ulioridhiwa Mei 2018.

Amesema  tayari wizara na taasisi za serikali zimeanza kufanya maboresho katika maeneo ambayo ni rahisi kutrkelezwa bila kufanya mabadiliko ya sheria na matokeo yake yameanza kuonekana ndani ya muda mfupi.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara (Brela), Andrew Mkapa amesema mfumo huo unafaida nyingi kwa mfanyabiashara kujua anapataje kibali au leseni mbalimbali kwa njia ya kielektroniki.

Amesema taarifa za taasisi zote na vibali zitawekwa kwenye mfumo huo wa tovuti hivyo, mfanyabiashara anaweza kuomba vibali bila kuzunguuka.

Ameeleza kuwa mfumo huo pia unapunguza gharama kwa wafanyabiashara  ambao wanahitaji kuingiza, kusafirisha au kupitisha biashara mbalimbali.

"Tunategemea kuchukua maoni kwa watu wengi zaidi ili kuboresha mfumo huo uweze kuwa na manufaa hivyo, mpaka Desemba mwaka huu tutakuwa tumepata maoni kwa wadau wengi na tutazindua awamu ya kwanza," amesema Mkapa.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya akizungumza  katika mkutano wa wadau kuhusu mfumo wa utoaji wa taarifa za kibiashara nchini (Trade information  Module), uliofanyika leo Septemba 30,2019 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Afisa Mtendaji, Wakala  wa Usajili wa Biashara (Brela) na Kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya maendeleo Biashara Tanzania (Tantrade).
Baadhi ya wadau mbali mbali wa mfumo wa utoaji taarifa za kibiashara nchini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya (hayupo pichani)  katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images