Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live

MABARAZA YA ARDHI YATAKIWA KUTOA HAKI WILAYANI IKUNGI SINGIDA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akikagua ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Italala Kata ya Sepuka mkoani Singida alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi na kujitambulisha kwa wananchi baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.
DC Mpogolo akiangalia eneo la kulowanisha ngozi wakati alipokuwa akikagua Kiwanda Kidogo cha Kusindika Ngozi katika Kijiji cha Msungua.
DC Mpogolo akikagua mashine ya kutotolesha vifaranga na mayai iliyopo Kijiji cha Msungua ambayo haizalishi chochote.
DC Mpogolo akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mnang’ana.
DC Mpogolo akipata maelezo ya uchimbaji wa kisima cha maji katika Kijiji cha Mnang’ana.
Hapa DC Mpogolo akiangalia jengo la Soko la Kata ya Sepuka ambalo ujenzi wake umesimama tangu mwaka 2013. Anaye toa maelezo ni Diwani wa Kata ya Sepuka Yusuf Misanga.
Afisa Tarafa ya Sepuka, Corlinel Nyoni akiwatambulisha viongozi katika mkutano wa hadhara.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Sepuka, Halima Athumani akizungumza.
Ulinzi ukiimarishwa katika mkutano wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Sepuka, Yusuf Misanga akizungumza.
DC Mpogolo akihutubia.
Mkazi w Kata hiyo Kitiku Memba akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi.
Mzee Seleman Majilanga akizungumzia kudhurumiwa shamba lake.
Mariam Muna akizungumzia kuhusu ardhi.
Athumani Nkindu akizungumzia ujenzi wa shule.
Mzee Iddi Mwango akizungumzia kuporwa shamba.
Mkutano ukiendelea.
Wazee wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano huo.
DC Mpogolo akimkabidhi Lucas Lissu cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya usaidizi wa kisheria.
Maria Kingu akikabidhiwa cheti cha usaidizi wa kisheria.



Na Dotto Mwaibale, Singida

MABARAZA ya kata ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi yametakiwa kutenda haki na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Sepuka mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi na kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo miezi miwili iliyopita.

” Nayaomba mabaraza yote ya kata ya usuluhishi migogoro ya ardhi yawatendee haki walalamikaji na kuacha kuchukua rushwa kwa walalamikiwa na kupindisha haki” alisema Mpogolo.

Mpogolo katika mkutano huo aliwageukia wasaidizi wa msaada wa kisheria katika wilaya hiyo waliopata mafunzo kwa kuwezeshwa na Wizara ya Katiba na Sheria kufanya kazi hiyo kwa weredi bila ya kuwatoza wananchi fedha na kutoa hukumu.

Alisema kazi yao ni kuwapa msaada wa kisheria wananchi bure na sio kuhukumu na pale wanapoona mashauri yamekuwa magumu wanatakiwa kuyapeleka ngazi nyingine ya utatuzi.

Katika mkutano huo DC Mpogolo alibaini Kata ya Sepuka kuwa na migogoro mingi ya ardhi ukilinganisha na kata zingine huku ikiwahusisha ndugu na jamaa wa karibu.

Mzee Seleman Majilanga alimwambia DC Mpogolo kuwa mabaraza ya ardhi ya kata yamekuwa na changamoto katika kutatua migogoro kutokana na wajumbe kujihusisha na rushwa na kupindisha haki.

Katika ziara hiyo DC Mpogolo alikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Italala, zahanati ya Mnang’ana, kiwanda kidogo cha kusindika ngozi kilichopo Kijiji cha Msungua na jengo la soko Kata ya Sepuka ambalo ujenzi wake ulisimama tangu mwaka 2013.

DKT. MWANJELWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA JIJINI MWANZA

$
0
0
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akitoa ufafanuzi wa michoro ya ramani ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akielekeza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firmin Msiangi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akisoma taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Wengine ni watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.

*******************************

Na Happiness Shayo – Mwanza
Tarehe 28 Septemba, 2019

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameridhishwa na
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa kilichopo eneo la Pasiansi jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa
kituo hicho, Dkt. Mwanjelwa amesema ujenzi wa mradi huo uko
katika hatua nzuri hivyo, ameipongeza Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa kwa kufikia hatua hiyo.

“Hakika jengo hili ni la viwango, linaridhisha na vifaa vya ujenzi
vilivyotumika viko katika viwango bora” Mhe. Dkt. Mwanjelwa
amefafanua.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
kwa kutenga bajeti iliyowezesha ujenzi wa kituo hicho kwani mradi
huo ulianza tangu mwaka 2008.

“Matumizi ya mkandarasi na mshauri binafsi yalisababisha kuwapo
kwa gharama kubwa za ujenzi zilizosababisha kusimama kwa
ujenzi katika hatua za awali, lakini mwaka 2017/2018 Serikali ya
Awamu ya Tano ilithamini mradi na kutoa fedha zilizofanikisha
mradi kama unavyoonekana sasa” Mhe. Dkt. Mwanjelwa
amesisitiza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amesema, Serikali iliamua
kujenga kituo hicho cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kwa
lengo la kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za ofisi za
serikali zilizopo kanda ya ziwa.

Bw. Msiangi amesema, kituo kitakapokamilika kitatumika kama
kituo mbadala cha kuhifadhi mifumo ya kumbukumbu na nyaraka
iliyopo katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu cha jijini Dodoma.

Naye, Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa
Mwanza, Bw. Victor Baltazar amemthibitishia Dkt. Mwanjelwa kuwa, ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi
Novemba, 2019.

“Mpaka sasa tumejenga jengo la utawala, maghala ya kuhifadhia
nyaraka kwa asilimia 95 na pia tumejenga uzio, eneo la kuegesha
magari, eneo la bustani, banda la walinzi na madereva kwa
asilimia 60” Bw. Baltazar amefafanua.

Ziara ya Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ya kutembelea kituo cha
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Mwanza ni sehemu ya
utekelezaji wa majukumu yake la kukagua utekelezaji wa miradi
iliyo chini ya Ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi wa umma nchini.

MASHINDANO YA “HASUNGA CUP 2019” YAFIKA UKOMO, WAZIRI HASUNGA APANIA SEKTA YA MICHEZO

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi vifaa vya michezo nahodha wa timu ya Hasamba Fc Ndg Waziri Nzunda wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na waamuzi kadhalika wachezaji wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na mashabiki wa mpira wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Moja ya mshambuliaji wa timu ya Hasamba Fc akiwatoka wachezaji wa timu ya Ihanda Fc wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wachezaji kabla ya mchezo wa fainali wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.


Na Mathias Canal, Songwe


Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" Leo tarehe 29 Septemba 2019 yamefika ukomo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ambapo timu ya Hasamba Fc ndiyo iliyoibuka kidedea na kunyakua zawadi kwa kuibamiza bila huruma timu ya Ihanda Fc kwa jumla ya Penati 7 kwa 6


Timu hiyo ya Hasamba Fc imeambulia ushindi huo wa goli 7 kwa 6 mara baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu magoli yaliyofungwa na mshambuliaji Asili Mnkondya wa timu ya Ihanda mnamo dakika ya 20 huku Beny Mgonde akiisawazishia timu yake mnamo dakika ya 72 ya mchezo huo.


Michuano hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Vwawa na kuendeshwa kwa umahiri mkubwa, ilizinduliwa mwezi Machi 2019 katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe huku ikizikutanisha timu 18 zilizotokana na muunganiko wa timu za vijiji katika kata hizo 18 katika Jimbo la vwawa.


Akizungumza katika kilele cha Mashindano hayo kilichofikia ukomo katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe, Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo mahususi kwa ajili ya kubaini vipaji vya vijana kwa ajili ya kuunda timu itakayoshiriki ligi daraja la nne na hatimaye ligi kuu Tanzania bara.


Amesema kuwa mashindano hayo pia yamekuwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali ambayo yamewaimarisha vijana hususani katika kuonyesha vipaji vyao.


Katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza ambayo ni timu ya Hasamba Fc amekabidhiwa zawadi ya Seti moja ya jezi, Seti moja ya soksi na kitita cha Shilingi laki tatu.



Mshindi wa pili timu ya Ihanda Fc imepewa zawadi seti moja ya jezi, seti moja ya soksi na kitita cha shilingi 200,000, Mshindi wa tatu yeye amekabidhiwa seti moja ya jezi na kitita cha Shilingi 100,000 huku mshindi wan ne akijinyakulia seti moja ya jezi pekee.



Katika hotuba yake Mbunge huyo wa Jimbo la Vwawa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga aliwapongeza viongozi wote na timu zote zilizoshiriki ligi hiyo kwani bila wao kusingekuwa na mafanikio yenye tija.



Mhe Hasunga aliwahakikishia wananchi kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu ili kutekeleza mpango mkakati wa uimarishaji na uboreshaji wa michezo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ibara ya 161.


MWISHO.

MAJALIWA AZINDUA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA CHA IDODI NA KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi (wa tano kushoto) wakizindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi wilayani Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi baada ya kuzindua Upanuzi wa Kituo cha Afya Idodi wilayani Iringa , Septemba 28, 2019. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi Wilayani Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Iringa, Costantino Kihwele, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ismani, William Lukuvi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na Mkewe Mary wakimpongeza, Bibi Chipe Ngubi ambaye amejifungua mtoto wa kiume Greyson wakati walipozindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi wilayani Iringa na kutembelea Wodi ya Mama na Mtoto, Septemba 28, 2019. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama ngoma wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji cha Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadahara, Septemba 28, 2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji cha Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadhara, Septemba 28, 2019.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi akiwasalimia wapiga kura wake kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Idodi wilayani Iringa, Septemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (aliyekaa wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkao wa Iringa na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Idodi, Septemba 29, 2019. Kushoto (aliyekaa) ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT.KALEMANI ATOA MWEZI MMOJA NGUZO ZILIZOHIFADHIWA ZISAMBAZWE

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, akitoa maelezo kwa Mkandarasi na wasimamizi katika Ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, baada ya kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika kituo hicho.
Vibarua wakiendelea na kazi ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za ujenzi katika kituo hicho.
Moja ya Transifoma kubwa ikiwa imesimikwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida kwa lengo kukiongezea uwezo kituo hicho hadi kufikia kV 400.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani( katikati) akikagua nguzo zilizo hifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida






Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kushoto) wakibadilishana mawazo baada ya Waziri wa Nishati, kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto) akipata maelezo ya namna kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, kinavyofanya kazi, kutoka kwa Meneja wa kituo hicho, Mha. Malili Mipawa(kulia).



Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani, akikagua eneo itakaposimikwa moja ya transifoma katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida.
……………

Na Zuena Msuya , Singida

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewagiza mameneja wa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)wote nchini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wanasambaza kwa wateja nguzo zote za akiba zilizohifadhiwa katika vituo na maeneo mbalimbali nchini.

Kalemani alisema hayo, Septemba 28,2019, baada ya kuona nguzo zaidi ya Elfu mbili zikiwa zimehifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi upanuzi wa kituo hicho kinachojengewa uwezo wa kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti(kV) 400.

Dkt.Kalemani, alisema kuwa hapendezwi kuona wateja wanalalamikia suala la ukosefu wa nguzo na kushidwa kuunganishiwa umeme katika maeneo mbalimbali wakati kuna nguzo zimerundwika mahali kwa ajili ya matumizi ya akiba.

“Wananchi wanahitaji nguzo kila siku,mnawaambia hakuna nguzo, ajabu nguzo kama hizi zimehifadhiwa sehemu mbalimbali mnadai ni za matumizi ya akiba,sasa akiba ya nini wakati wananchi bado wanauhitaji , pia maeneo mengi nguzo zimeharibika zinataka kubasilishwa, nawapa Mwezi mmoja zisionekane hapa na maeneo mengine yote!”, Alisema Dkt.Kalemani. 

Katika hatua nyingine, alimtaka mkandarasi wa Kampuni ya KC International LTD inayotekeleza ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida kuongeza nguvu kazi ili kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Januari 2020.

Kazi ya ujenzi katika hatua ya awali katika kituo hicho imekamilika na kufikia 95% ambapo pia tayari wamekamilisha baadhi ya maeneo zitakaposimikwa transofoma kubwa nne ambapo mbili kati ya hizo zitakuwa na uwezo wa 125 MVA kwa kila moja na mbili nyingine zitakuwa na uwezi wa 250 MVA kila moja, pia kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kuendeshea mitambo inaendelea .

Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawat(MW) 432 ambapo kwa sasa mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Singida ni MW 15 tu, hivyo kituo hicho kitaimarisha upatikanaji wa Umeme wakutosha na wauhakika katika Mkoa huo na mikoa iliyo karibu.

Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida ndiyo kitakuwa kituo kikubwa na pia njia panda kubwa ya kusambaza umeme kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia Mkoa wa Shinyanga, Kanda ya Kaskazini kupitia Babati Mkoani Manyara, hadi Namanga Mkoani Arusha na baadaye Nchini Kenya.

Gharama za upanuzi wa kituo hicho ni Dola za Kimarekani milioni 60 sawa na Bilioni 130 za Kitanzania, fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan(JICA) pamoja na Fedha za ndani.

WAZEE WAISHIO KATIKA MAKAZI YA SERIKALI WATAKIWA KURUDI KATIKA FAMILIA ZAO

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea na Wazee wa Makazi ya Wazee Nandanga yaliyoko nje Kidogo ya Mji wa Ndanda mkoa wa Lindi alipotembelea Makazi hayo.
Baadhi ya Wazee wa Makazi ya Wazee Mkaseka yaliyoko Wilaya ya Masaki Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipotembelea Makazi hayo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na Mzee wa Makazi ya Wazee Ngehe yaliyoko Wilaya Nyasa Mkoani Songea Bi. Regina Tilya wakati alipotembelea Makazi hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na Wazee wa Makazi ya Wazee Mkaseka yaliyoko Masaki Mtwara alipotembelea Makazi hayo.


Na Mwandishi Wetu- Lindi

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewaambia wazee waishio katika Makazi ya kutunza Wazee ya Serikali nchini kuwa lengo la Serikali ni kuboresha makazi hayo lakini akawataka wazee hao kurudi kujiunga tena na familia zao ili kuishi na faraja tofauti na sasa ambapo wanaishi katika mazingira kambi.

Dkt. Jingu ameyasema hayo mkoani Lindi wakati alipoyatembelea makazi ya kutunza wazee na wasiojiweza ya Nandanga kujionea huduma zinazotolewa kwa wazee waishio katika makazi hayo.

Dkt. Jingu pia amewakumbusha wazee hao umuhimu wa kuishi na familia zao na kuwataka kutambua kuwa jukumu la kwanza la kuhudumia mzee au mtu yeyote ni la familia na jamii yake.

Dkt. Jingu pia aliwataka wazee hao kutambua kuwa serikali na wadau wengine wanachangia tu huduma lakini akawataka wazee hao kutambua umuhimu wa kuishi na familia kwani familia ni ya msingi kabisa kwa wazee hao kuishi lakini pia kutoa ushauri wao kwa familia na jamii kutokana na wao kuishi miaka mingi.

Aidha Dkt. Jingu aliwataka wazee hao kuendelea kutoa msaada kwa jamii kwa kuwa wana maarifa mengi kutokana na kuishi kwa muda mrefu na kuonya kuwa kuendelea kwao kuishi katika makazi ya Serikali ni kupunguza mchango wao kwa jamii husika.

“Watumishi wa Serikali wanahudumia makazi haya wanajitahidi kufanya kazi hapa lakini wanakitu ambacho hawawezi kukitoa hata wafanye kazi namna gani kwani hawezi kutoa upendo unaopatikana katika familia ambao ni upendo wa baba na mtoto au upendo wa mtoto kwa baba” Aliongeza Dkt. Jingu. 

Afisa Mfawidhi katika anayehudumia Makazi ya Wazee Nandanga Bw. Cleophas John alitaja changamoto wanazokabiliana nazo wazee katika Makazi hayo kuwa ni ukosefu wa umeme katika baadhi ya nyumba kituoni hapo, upungufu wa chakula, huduma ya usafiri na ukosefu wa nguo kwa wazee wasiojiweza changamoto ambazo zilijitokeza katika makazi mengine ikiwemo uchakavu wa miundobinu ya makazi. 

Dkt. Jingu kwa nyakati tofauti ametembelea Makazi ya Wazee ya Mikoa ya Songea, Lindi na Mtwara kuangalia namna bora ya kuboresha hali katika makazi ya wazee ambapo ametembela Makazi ya Wazee Nandanga yaliyoko Lindi, Makaseka Mkoani Mtwara na Makazi ya Wazee Ngehe kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Songea.

WAKANDARASI MRADI WA MAJI SAME-MWANGA WATAKIWA KUONGEZA KASI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa tatu kutoka kulia) alipotembelea eneo la chanzo cha maji (Bwawa la Nyumba ya Mungu) cha mradi wa Same- Mwanga akimsikiliza Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi Emma Magembe.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akimsikiliza Mtaalam Mshauri kutoka Kampuni ya ECG anayesimamia ujenzi wa chanzo cha maji na kituo cha tiba ya maji Mhandisi Nabil Fathy.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akitembelea kituo cha tiba ya maji cha mradi wa Same-Mwanga kinachojengwa na Kampuni ya M.A Kharafi & Sons.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kushoto) akikagua moja ya tenki la maji la mradi wa Same-Mwanga linalojengwa na Kampuni ya Badr East Africa Enterprises.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kushoto) akitembelea kituo cha tiba ya maji cha mradi wa Same-Mwanga kinachojengwa na Kampuni ya M.A Kharafi & Sons.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (mbele) akikagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (booster station) cha mradi wa Same-Mwanga kinachojengwa na Kampuni ya Badr East Africa Enterprises.

…………………


Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa maji wa Same-Mwanga wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ukamilike kwa wakati.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa maelekezo hayo Septemba 28, 2019 wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua hatua ya ujenzi iliyofikiwa na Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ambao ni kampuni ya M.A Kharafi & Sons na kampuni ya Badr East Africa Enterprises.

Mara baada ya kujionea shughuli zilizokuwa zikiendelea na kupokea taarifa ya mradi kutoka kwa wakandarasi hao, Mhandisi Sanga alieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezwaji wake na aliwasisitiza kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa wakati.

Mhandisi Sanga aliwataka Wakandarasi kuwa wepesi kwenye kufanya mawasiliano na Wizara kila wanapokutana na changamoto yoyote ambayo ipo nje ya uwezo wao ili ufumbuzi upatikane haraka bila kuchelewesha shughuli za ujenzi wa mradi.

“Sijaridhishwa na kasi yenu ya ujenzi wa mradi. Kama kuna changamoto mnakutana nazo zilizo nje ya uwezo wenu mhakikishe mnawasiliana na Wizara mapema iwezekanavyo ili tupate ufumbuzi,” alisema Mhandisi Sanga.

Aliongeza kwamba Serikali inachohitaji ni kuona matokeo na haipo tayari kumvumilia mkandarasi ambaye anachelewesha mradi bila ya kuwa na sababu za msingi.

“Wanachohitaji wananchi ni maji, Serikali haitomvumilia Mkandarasi ambaye atashindwa kwenda na kasi inayokubalika,” alibainisha Mhandisi Sanga. 

Mhandisi Sanga vilevile aliwakumbusha wakandarasi hao kuhakikisha manunuzi ya vifaa vinavyohitajika kwenye ujenzi wa mradi huo yanafanyika hapa nchini badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi hasa ikizingatiwa kwamba vingi vinapatikana hapa hapa Nchini.

Wakandarasi hao kwa nyakati tofauti walimuahidi Naibu Katibu Mkuu Sanga kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi sambamba na kuzingatia maelekezo aliyoyatoa.

Mradi wa Same-Mwanga ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa Miji ya Same na Mwanga, Mkoani Kilimanjaro na baadaye Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.



Ziara hiyo ya Naibu Katibu Mkuu Sanga kwenye mradi huo ni ya kwanza tangu ameteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo Septemba 22, 2019

Wakazi wa Bukoba waipokea Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari Oktoba 2-8, 2019

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola (katikati ya wanafunzi) akieleza jambo kuhusu watu wenye ulemavu wakati Gari la Matangazo la NEC lilipotembelea Shule ya Sekondari ya Rugambwa iliyopo Manispaa ya Bukoba kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji waDaftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Kagera, Kigoma na Wilaya ya Chato unaoanza Oktoba 2 hadi Oktoba 8, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola (katikati) akifafanua nafasi ya watu wenye ulemavu katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura akiwa na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma Shule ya Sekondari ya Rugambwa ya Manispaa ya Bukoba.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yasinta Mlula akiwaeleza jambo wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mkazi wa Manispaa ya Bukoba mwenye ulemavu akiwa na Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ibrahim Dedu wakati Gari la Matangazo la Tume (halipo pichani) lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Monica Wabukundi, akiwasiliza vijana kwenye Stendi ya mabasi ya Mjini Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye stendi hiyo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Picha na Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura-NEC

TIMU YA MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI KUTEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME KATIKA MTO RUFIJI

$
0
0
Mhandisi Steven Manda akiwatembeza sehemu mbalimbali Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi walipotembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Mohamed H. Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi baada ya kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji mkoani Pwani.
Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mohamed H. Hassan, akiongoza Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto rufiji.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

HATI FUNGANI NI FURSA YA JAMII KUITIKIA WITO WA JPM KUJIKOMBOA KIUCHUMI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa UTT AMIS, Simon Migangala.
Rais Dkt. John Magufuli Aakimkagua samaki na kumnunua kwa mfanyabiashara wa soko la Samaki Feri, jijini Dar es Salaam alipofany ziara ya kutembelea wafanyabiashara wadogo wanaotumia vitambulisho vya wajasiriamali ambao wanaweza kukuza mtaji wao kupitia uwekezaji kwenye Mfuko wa Hati Fungani.

……………………

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wengi wanatafuta mafanikio maishani mwao lakini bila kuwa na bidii, ustahimilivu, nidhamu na shauku kubwa, huwezi kupata mafanikio ya kweli.

Kuna mbinu mbalimbali ambazo kila mwananchi anayetafuta mafanikio anaweza kuzitumia ili kufikisha lengo alilonalo.

Jambo la kwanza ni kujua unataka nini, ukijua unachotaka utakuwa na msimamo wa kutaka kufikia malengo yako.

Kama hujui unachotaka, jambo la msingi, chukua kalamu na karatasi kisha jiulize unataka kufanikiwa kitu gani?Ni muhimu wakati unajiuliza, usifikirie mawazo hasi au mabaya ya kujiona kama utashindwa kufanikiwa bali kiajimi.

Ondoa wasiwasi wowote ambao utakuwa nao, orodhesha mambo yote unayotaka kufanikiwa, anza kupanga mipango kwa kujiwekea malengo, kutekeleza moja baada ya jingine.Utajiri siyo fedha ambazo mtu anakusanya bali ni fedha ambazo huwekwa na kufanya kazi.

Tamaduni zetu zimeifanya jamii kubwa kuhifadhi fedha ndani kwenye vyungu, magodoro hata vibubu. Njia hizo zimekuwa zikibadilika taratibu sawa na ukuaji wa elimu na teknolojia.Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti. Uwekaji akiba ni tabia nzuri lakini bila kuziwekeza ni bure.

Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani uwekezaji una uwiano mkubwa na muda. Muda unapozidi kuwa mrefu na uwekezaji wako unazidi kukuwa mkubwa. Mara zote pesa ndani ya uwekezaji UTT AMIS zinawekezwa katika mpango wa faida jumusihi ambapo muda huwa ni jambo la msingi kabisa.

UTT AMIS ni taasisi ya Serikali ambayo imepewa dhamana ya usimamizi wa mali kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.Nchini Tanzania unaweza kuwekeza fedha zako katika masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti za muda maalum na zisizo za muda maalum katika benki za biashara.

Pia hati fungani za Serikali za muda mfupi, mrefu, kampuni na hisa zilizo orodheswa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambazo zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri.Uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko ambayo wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezasha mtu, watu, vikundi, taasisi, kampuni kuwekeza pesa zao kwa Meneja wa UTT.

Meneja wa mfuko huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye masoko ya fedha na mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Waraka wa makubaliano ni maandiko ya kisheria yanayo zungumzia haki za pande zote mbili meneja na mwekezaji pia huanisha sehemu za kuwekeza na uwiano wa kuwekeza.

Faida inayopatikana hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika. Awali UTT ilipewa dhamana ya usimamizi wa mifuko mitano.Mifuko hiyo ni Mfuko wa Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi. Hivi sasa taasisi hiyo imeongeza mfuko mwingine wa Hati Fungani.

Mfuko wa Umoja, ulioanzishwa Mei 16, 2005 ukilenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 70, kwa sasa sh. 582.
Sifa zilizopo katika mfuko huo ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). kiwango cha chini cha kujiunga ni vipande 10 tu, malipo ya mauzo hutozwa asilimia moja ya thamani halisi, pia ni rahisi kujiunga na kutoka, manunuzi na mauzo hufanyika kila siku ya kazi.

Mfuko wa Watoto una lengo la kuwasaidia watoto katika maendeleo yao nchini. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 100, mfuko ulianzishwa Oktoba 1, 2008.

Na kwa sasa thamani ya kipande katika mfuko wa watoto ni shilingi 348 Sifa za mfuko huo ni uwekezaji kwa ajili ya mtoto mwenye umri chini ya miaka 18. Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. 10,000, unaruhusiwa kuwekeza kidogo kidogo kwa sh. 5,000.

Sifa nyingine ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga), mfuko hutoa mipango ya aina mbili, kwanza malipo ya ada, pili mpango wa kukuza mtaji.

Malipo ya ada na mauzo ya vipande yanaruhusiwa pale mtoto anapofikisha miaka 12. Mfuko huo ni miongoni mwa mifuko inayotatua changamoto za kielimu hasa katika ulipaji ada kwa wanafunzi, kutoa mtaji baada ya ukomo wa shule kufikia.

Pia mfuko una mipango miwili mikubwa, mpango wa ada za shule na mtaji kwa mwanao. Ili mzazi aweze kuchangia kupitia mfuko huo, anapaswa kuweka sh. 10,000 kima cha chini na hakuna ukomo kwenye kiwango cha juu. Mwekezaji anaweza kuwekeza mara kwa mara kadri anaweza.

Mfuko wa Jikimu una lengo la kukidhi mahitaji ya wawekezaji wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa mara, ulianzishwa Novemba 3, 2008 ukiwa na sifa za mipango ya uwekezaji, kiwango cha uwekezaji, mpango wa gawio robo mwaka.

Kiwango cha chini kuwekeza ili kupata gawio mara nne kwa mwaka yaani kila robo mwaka ni shilingi milioni 2. Mpango wa gawio wa mwaka (kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni moja), tatu mpango wa mwaka wa kukua (sh. 5,000).Vipande vinauzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga).

Mfuko wa Ukwasi unaotoa nafasi ya uwekezaji mbadala kwa wawekezaji wakubwa au taasisi ambao wangependa kuwekeza fedha zao za ziada kwa kipindi kifupi ama cha kati huku wakikuza mtaji wao.

Ulianzishwa Aprili 30, 2013, bei ya kipande ikiwa sh. 100.00, hivi sasa imepanda hadi zaidi ya sh. 219 hii ikiwa ina maana ya kuwa mfuko umekua mara 2.19 ndani ya miaka mitano au umekuwa kwa asilimia 119 huu ni ukuwaji mzuri sana kibiashara. Sifa za mfuko huo ni rahisi mwekezaji kupata fedha zake za mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya maombi ya kuuza vipande kupokelewa Makao Makuu ya UTT AMIS.



Mfuko huo hauna ada ya kujitoa wala kujiunga, una unafuu wa gharama za uwekezaji, unafaa kwa wawekezaji mmoja mmoja au taasisi, kiwago cha chini cha kuwekeza sh. 5,000,000.00.

Kuongeza uwekezaji wako sh. 1,000,000.00, pia unaruhusu uhamishaji vipande kutoka kwa mwekezaji mmoja kwenda mwingine, kuruhuusu uhamishaji vipande kwenda kwenye mifuko mingine, kuviuza kwa thamani halisi.

Mfuko wa Wekeza Maisha unamwezesha mwekezaji kupata faida pacha (mapato mazuri pamoja na mafao ya bima).

Mfuko huo ulianzishwa Mei 16,2007, wawekezaji kati ya miaka 18 na 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga. Unatoa mipango ya aina mbili, kuchangia uwekezaji awamu ya kwanza, mkupuo mmoja.

Vipande vinauzwa kwa thamani halisi, hakuna gharama za kujiunga. Kujiunga ni sh. 8,340.00 tu kwa mwezi. Mafao ya bima yanayopatikana ni bima ya maisha, ulemavu wa kudumu na bima ya ajali.

Mfuko unamwezesha mwekezaji kuwekeza kwa mpangilio, kuchangia kwa mwezi, mara mbili kwa mwaka, mara moja kwa mwaka ambapo faida za uwekezaji katika Mifukoya Uwekezaji wa Pamoja ni kukuza mtaji kwa kutoa faida nzuri ukilinganisha na mifuko mingine kwenye masoko ya fedha.

Faida nyingine ni kutawanya hatari za uwekezaji, mwekezaji hupunguza athari za uwekezaji kwa kuwekeza katika uwekezaji anuai, wawekezaji kufaidika na unafuu wa gharama za uwekezaji.

Pia wawekezaji wanaweza kufuatilia maendeleo ya masoko ya fedha kwa kufuatilia maendeleo ya mifuko.

Mfuko mpya Hati Fungani unaojulikana kama ‘Bond Fund’ ni kati ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS ulioanzishwa kwa malengo maalum.

Malengo hayo ni kubuni, kuendeleza, kuanzisha na kusimamia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja, kuwekeza, kununua, kumiliki na kuuza dhamana, kutimiza malengo, wajibu, haki na sheria.

Mengine ni kutoa huduma za usimamizi wa fedha kwa kampuni na wawekezaji binafsi, kutoa ushauri wa uwekezaji kwa taasisi na watu binafsi, kutunza taarifa za wawekezaji wa mifuko na kuhamasisha wananchi kujiwekea akiba.

Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati Fungani kumetokana na mahitaji ya wawekezaji na uchambuzi wa bidhaa za kifedha zilizoko kwenye soko la mitaji kwa sasa.

Mfuko utawawezesha wawekezaji wadogo na wa kati kuzifikia fursa za uwekezaji ambazo kwa hali ya kawaida ni wawekezaji wachache na wakubwa ndio wanaozifikia.

Pia utawekeza kwenye hati fungani zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa kwa asilimia 90 na asilimia 10 itakuwa kwenye uwekezaji wenye ukwasi mkubwa.

Lengo ni kuwawezesha wawekezaji wanaohitaji kuchukua fedha kutokana na uwekezaji wao katika mfuko wafanye hivyo.

Mfuko umeundwa ili kumwezesha kila mwekezaji kuchagua kama anapenda kukuza mtaji au kupokea gawio kwa mwezi, kila miezi sita kutokana na mahitaji yake ya kifedha.

Sheria ya Masoko ya Mitaji inataka Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kuwa na Meneja, Mdhamini, Wakaguzi wa Mahesabu, Wanasheria na Msajili.

Mfuko huo utasimamiwa na UTT AMIS kama Meneja na Benki ya CRDB kama Mdhamini. Utakaguliwa na KPMG ambayo ni taasisi ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu ya fedha.

Wanasheria watakuwa Kampuni ya Abenry and Company ambao wana uzoefu mkubwa katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na Msajili atakuwa UTT AMIS.

Akiuzungumzia mfuko huo, Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisemaumelenga kuondoa changamoto ambazo wawekezaji wanakutana nazo.

Anasema soko la fedha lina bidhaa nyingi zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji.

Baadhi ya bidhaa hizo zinaeleweka kirahisi hata namna ya kuzifikia na kuwekeza lakijni wakati mwingine hazitoi faida shindani kwa wawekezaji.

Anasema baadhi ya wawekezaji hasa wadogo ni vigumu kuwekeza kwenye baadhi ya bidhaa katika soko la fedha. Mfuko wa Hati Fungani umeratibiwa ili kuondoa changamoto hizo.

Mwekezaji anapata faida sawa na wawekezaji wakubwa, akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake kwenye mfuko kwa utaratibu rahisi bila kupoteza faida aliyoipata.

Pia mfuko huo unawafaa wawekezaji wakubwa kwa sababu ya faida shindani, gharama ndogo za kuwekeza, ukwasi wa kutosha, usalama wa mtaji, hatari ndogo za uwekezaji.

Mfuko unatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza, kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji huo.

Kwa mantiki hiyo, mfuko umeandaliwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa kipato cha chini, kati na kipato cha juu ambapo watu binafsi, kampuni, taasisi na vikundi rasmi wanaweza kushiriki katika uwekezaji kwenye mfuko huo.

Lengo kuu la mfuko ni kuwawezesha wawekezaji katika ushiriki mpana kupitia uwekezaji wa vipande na kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kupitia hati fungani, masoko ya fedha.

Mfuko huo hutoa fursa ya uwekezaji rahisi wa muda mrefu kwa wawekezaji ambao wangependa kuwekeza ili kukuza mtaji wao, kupata gawio kila mwezi au kila baada ya miezi sita kama mwekezaji anavyohitaji.

Mbaga anasema, mfuko una mipango miwili ya uwekezaji ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji. Kuna mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi na gawio kila miezi sita, mpango wa kukuza mtaji.

Gawio la mara kwa mara halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana itarudishwa kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande vitakavyonunuliwa kwa bei ya wakati huo.

Mpango huo utawafaa wawekezaji wanaohitaji kuweka akiba kwa malengo maalum mfano kujenga nyumba au wafanyakazi wenye kipato kama wangependa kuwa na fedha ya akiba.

Wawekezaji katika mpango huo wanaweza kuuza kiasi chochote cha uwekezaji wakiwa wamekidhi vigezo vinavyohusu uuzwaji wa vipande. 

Wawekezaji wanaohitaji kuchukua faida kila mwezi kama wastaafu wanaopata fedha zao za mkupuo, kuwekeza kwenye mfuko, wanashauriwa kuchagua kupokea gawio kila mwezi ili wapate kipato cha kuishi bila kupoteza fedha walizopata.

Mbaga anasema wawekezaji wengine wanaopata fedha nyingi mara moja mfano wachimba madini, wanaweza kuchagua gawio kila mwezi ili wafanye shughuli zao bila kuathiri mtaji wao.

Pia wawekezaji watakao jiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko vinavyohusu uuzwaji vipande.

Mpango wa gawio kila miezi sita, Mbaga alisema hutegemea na mahitaji ya fedha ya mwekezaji na anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya kuwekeza kwenye mfuko.

Kwa wawekezaji ambao wanahitaji kuchukua faida kila miezi sita mfano wafanyakazi wanaohitaji kuweka kiasi cha fedha ili faida inayopatikana itumike kulipa ada kusomesha watoto, wanaweza kuchagua kupokea gawio kila miezi sita.

Pia kuna wawekezaji wanaopata fedha nyingi mara moja kama wakulima wa mazao mbalimbali ya msimu, wanaweza kuchagua kupata gawio kila miezi sita.

Lengo ni kupata fedha wakati wa kutayarisha, kulima mashamba na wakati wa kuvuna ili waweze kuendesha shughuli zao kwa kufuata msimu bila kupoteza mtaji walio nao. Pia hawa wanahitaji pesa wakati wote huku kilimo kikiwa ni cha msimu mpka msimu. Wakati wanasubiri msimu mpya wana chukuwa pesa za kwa mwezi ili kukidhi mahitaji ya kila siku.



Wawekezaji watakao kujitoa kutoka mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vipande vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko.

Akizungumzia sera ya uwekezaji, Mbaga anasema muundo wa mgawanyo katika mfuko wa Hati Fungani unatoa mapato ya muda mrefu ikijumuisha hati fungani zinazotolewa na Serikali.

Uwekezaji kwenye hati fungani ili mfuko uwe na mapato ya kudumu utakuwa si chini ya asilimia 90 ya thamani ya mfuko, asilimia 10 itawekezwa kwenye rasilimali zenye ukwasi ili wawekezaji wanaohitaji kuchukua fedha wafanye hivyo.

Meneja atawekeza kwenye rasilimali zenye ukwasi ili kuhakikisha uwezo wa kulipa wawekezaji pale fedha zao zitakapohitajika unakuwa imara.

Mbaga anasema wawekezaji wote wa ndani, nje ya Tanzania kama Sheria ya Soko la Mitaji na Dhamana inavyoruhusu wanaweza kuwekeza kwenye mfuko huo.

Kuhusu ununuzi wa vipande, alisema vinanunuliwa siku yoyote ya kazi isipokuwa kipindi cha kufunga vitabu ambacho hakitazidi siku saba za kazi.

Kuanzia Septemba 16 hadi Oktoba 16, mwaka huu itakuwa kipindi cha mauzo ya awali hivyo Watanzania wachangamkea fursa hiyo kwani kiwango cha chini kitakuwa sh. 50,000 na thamani halisi ya kipande itakuwa sh. 100.

Maombi ya kununua vipande yanaweza kuwakilishwa katika tawi lolote la Benki ya CRDB, ofisi za madalali waliosajiliwa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam; Ofisi za Shirika la Posta; Wakala yoyote atakayeteuliwa na UTT AMIS.

Wawekezaji walio nje ya Tanzania anayetaka kuwekeza katika mfuko huo awasiliane na ofisi za madalali waliosajiliwa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam au kuwasiliana moja kwa moja na Ofisi za UTT AMIS ili kupata taarifa na muongozo zaidi.

Anaongeza kuwa, thamani ya mwanzo ya kipande itakuwa sh. 100. Thamani ya kuuza na kununua kipande itakuwa sawa na thamani halisi ya kipande bila gharama yoyote.

Kiwango cha chini kitakuwa sh. 50,000, hakuna ukomo kwenye kiwango cha juu ambapo hiyo ni fursa kwa kila Mtanzania.

Baada ya muda wa mauzo ya awali, mwekezaji anaweza kuwekeza kuanzia sh. 5,000, mara nyingi kadri awezavyo.

Malipo ya mauzo ya vipande yanaweza kufanywa kwa fedha taslimu au hundi ya benki itakayolipwa kwenye akaunti ya ‘Mfuko wa Hati Fungani’ iliyopo Benki ya CRDB.

Wawekezaji wanaweza kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya CRDB na kufanya malipo. Pia malipo yanaweza kufanyika kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money.

Kiwango cha chini cha uwekezaji wakati wa mauzo ya mwanzo kwa Mpango wa Kukuza Mtaji ni vipande 500. Kwa kuwa thamani ya mwanzo ya kipande ni sh. 100, thamani ya chini ya vipande katika mauzo itakuwa sh. 50,000.

Unaposema Mfuko wa Kukuza Mtaji maana yake mwekezaji atakuwa anawekeza mara kwa mara kwa malengo Fulani ili kutimiza azima fulani huko mbele. Na kila anacho wekeza kitakuwa kinakuwa kutokana na mwenendo wa soko

Kuhusu mpango wa gawio kila mwezi, kiwango cha chini cha uwekezaji wakati wa mauzo ya mwanzo kwa mpango wa gawio kila mwezi ni vipande 100,000. Kwa kuwa thamani ya mwanzo ya kipande ni sh. 100, thamani ya chini ya vipande katika mauzo itakuwa sh. 10,000,000.

Mpango wa gawio kila miezi sita, kiwango cha chini cha uwekezaji wakati wa mauzo ya mwanzo kwa mpango wa gawio kila miezi sita ni vipande 50,000. Kwa kuwa thamani ya mwanzo ya kipande ni sh. 100, thamani ya chini ya vipande katika mauzo itakuwa sh. 5,000,000. Kuhusu ununuzi na mauzo ya baadaye yatakayoanza Oktoba Mosi, mwaka huu, idadi ya chini ya vipande inayoweza kuuzwa ni vipande vyenye thamani ya sh. 5,000, vitaonekana katika mgawanyo wa desimali nne.

Maombi ya mauzo, manunuzi ya vipande yatapokelewa na kukubalika siku za kazi tu.

Mauzo ya vipande yatafanyiwa kazi baada ya kupokelewa kwa fomu ya kuuza vipande ambayo itakuwa imeambatanishwa na taarifa ya akaunti, nakala ya kitambulisho, kielelezo kingine kitakachohitajika na Meneja wa Mfuko.

Malipo ya mauzo ya vipande kwenda kwa mwekezaji yatafanyika kwa njia ya benki au kupitia Shirika la Posta ndani ya siku 10 za kazi tangu kupokelewa maombi yaliyo kamili.

Lazima mwekezaji ajaze fomu ya maombi ya kujiunga ili aweze kununua vipande na kuwekeza, fomu hiyo ipelekwe kwa wakala yeyote aliyeteuliwa na Meneja wa Mfuko.

Wakulima Sikonge wanufaika na kilimo cha umwagiliaji

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Sikonge Tabora 

UBORESHAJI wa miundombnu ya umwagiliaji katika Halmashauri ya Siikonge Mkoani Tabora umeongeza uzalishaji wa zao la mpunga, hivyo kuinua kipato cha wakulima wilayani humo. 

Akizungumza na waandishi wa habari na Maafisa toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Katibu wa Chama Cha Wamwagiliaji cha Skimu ya Ulyanyama wilayani Sikonge Bw. Simon Kalosa amesema kuwa baada ya serkali kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kutoa mafunzo ya uendeshaji na utunzaji wa skimu, uzalishaji wa mpunga umeongezeka tofauti na ilivyokuwa awali. 

Bw. Kalosa amesema kuwa wastani wa uzalishaji wa mpunga kwa sasa katika skimu ya Ulyanyama ni tani 8 kwa hecta wakati kabla ya uboreshaji wa miundombinu uzalishaji ulikuwa ni magunia sita hadi nane kwa ekari. 

Kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga katika skimu ya ulyanyama Kalosa amesema hali za maisha ya wananchi wengi zimekuwa bora na wengi wameweza kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao. 

Kalosa amesema kuwa skimu ya ulyanyama ina jumla ya wakulima 306 ambao hujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji na wengi wao wamefaidika na uwekezaji uliofanywa na serikali katika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo. 

Akizungumza awali mkulima wa kilimo cha Umwagiliaji Bi. Happiness Mpunda amesema kilimo cha umwagiliaji kimebadilisha maisha yake na familia kwa ujumla kwani sasa anajitosheleza kwa chakula na kuinua kipato cha familia. 

Bi.Mpunda amesema katika msimu wa 2018/2019 ameweza kuvuna magunia 35 kwa ekari ambapo kabla ya kupata mafunzo ya matunzo bora ya mashamba alikuwa akipata gunia sita tu kwa ekari. 

” Kuna tofauti kubwa sana ya uzalishaji kabla na baada ya mafunzo ya uendelshaji na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, tulipokuwa tunatumia mbinu za kienyeji tulitumia nguvu nyingi sana uzalishaji kidogo wakati kwa sasa ni kinyume chake”Alisema Bi. Mpunda. 

Amesema kutokana na kilimo cha umwagiliaji ameweza kusomesha watoto watano na amenunua usafiri ambao umeweza kurahisisha mizungo ya kutafuta masoko ya mazao yake. 

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Wamwagiliaji cha Ulyanyama Bwn. Dikson Simbila amesema kuwa ijapokuwa masoko ya mpunga wanaolima lipo ndani nan je ya Halmashauri ya Sikonge bado bei ziko chini kinyume na matarajiao yao. 

Bw. Simbila amesema ili kuongeza thamani ya mpunga wao, chama kilinunua kinu cha kukobolea mpunga ambao pia huweza kupanga madaraja mbalimbali ya mpunga tayari kwa kuuza. Kwenye masoko mbalimbali. 

Amesema kutokana na bei kuwa chini inawalazimu kusubiri hadi mwezi Disemba ili walau wapate bei nzuri ya mpunga ambapo hii huchelewesha maandalizi ya mashamba kwa ajili ya msimu unaofuatia. 

Akizungumza mapema, Mhandisi wa unwagiliaji wa mkoa wa Tabora Bwana Bahati Bulekele amesema kuwa a wake eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hecta 38,000 ambapo hekta 5,352 zimeshaendelezwa . 

Mhandisi Bulekele amesema Mkoa wa Tabora una jumla ya skimu za umwagiliaji 58 katika halmashauri mbalimbali na kati ya hizo 16 ndio zinazofanya kazi kwa kiwango cha juu. 

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina mamlaka ya kuratibu, kuendeleza na kusimamia maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji nchini ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali katika utekelezaji na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya umwagiliaji, mkakati wa maendeleo ya umwagiliaji. 

Tume pia inaratibu shughuli zote za umwagiliaji katika sekta ya umwagiliaji zinazotekelezwa na wadau wengine wa maendeleo, kuuhamasisha na kudumisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zenye kutekeleza majukumu yanayofanana na Tume.

Bi Happiness Mpunda mkulima katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Uliyanyama akiongea kuhusu faida alizozopata kutokana na kilimo cha Umwagiliaji.
Pichani ni ghala la kuhifadhia nafaka lililojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora.
Katika Picha ni kinu cha kuchakata zao la mpunga kinachotumiwa na wakulima wa umoja wa wakulima wa umwagiliaji Uliyanyama Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, ili kuweza kuongeza thamani ya mazao yao.

MOTORISTS URGED TO USE TOTAL EXCELLIUM FOR CLEANER ENGINES

$
0
0
Total Tanzania Limited

Dar es Salaam, September 29, 2019:TOTAL Tanzania has urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions.
The TOTAL Network Director, Marieme Sow said in a press statement that TOTAL Excellium was specially designed by the company’s researchers to clean the engine kilometer after kilometer and also prevent up to 93% of deposits build-up in comparison to non-additive fuel. TOTAL Excellium is the only fuel in Tanzania with additives which has molecules that reduce friction between metal parts, hence minimize wear and tear, to help extend engine life. Together, cleaning and friction-reduction technologies lead to reduced fuel consumption and lower CO2 emissions.
“When you drive your car, deposits build up in your engine due to direct injection and friction between metal particles.,” she added that modern engines are particularly vulnerable to this problem, an accumulation of deposits can affect the engine's operation and negatively impact performance, resulting in higher fuel consumption, more harmful emissions and less power.
She called on customers to embrace consistency and only fuel at TOTAL service stations if they want to see the results and insisted that mixing of fuel will not give the expected results to the car engine. “We recommend that they stick to TOTAL Excellium and they will experience these positive results,” she said.
Marieme added that long-distance drivers especially bus and truck drivers who use TOTAL Excellium have been testifying on how their engines record much better performance, uses less fuel and are much cleaner due to TOTAL Excellium.
Total Director of Legal and Corporate Affairs, Marsha Msuya Kilewo exclaimed that while all petroleum product imported in Tanzania through Bulk Procurement system is of the same quality, Total makes the difference by adding the additive to the fuel through an automated system at the depot before the product is transported to all Total and Gapco branded service stations. She affirmed that despite the huge investment made by Total to bring the Excellium product in the market – Total Excellium is sold at the same price as other non-additive fuel and all you have to do to get Total Excellium, is DRIVE to your nearby Gapco or Total station to enjoy the benefits of this amazing product.

TOTAL currently has more than 100 service stations countrywide and is on a mission to ensure that all motorists choose TOTAL Excellium as their fuel of choice.



About Total Tanzania

Total Tanzania Limited is a petroleum market and service company, incorporated in Tanzania since 1969. Total Business focuses on the marketing, supply, and service of petroleum products, HFO and Lubricants, which are marketed through its General Trade, service stations and specialties departments within its organization. Total Tanzania Limited extends its expertise in offering reliable, secure and convenient service through its use of the Total Card system for the purchase of Lubricants, fuels, and car service at any total service station General trade customers. As part of its diversification Total Tanzania, Limited through the Total Access to Solar (TATS) project supports the distribution of solar lanterns to Tanzania community by introducing distribution of solar lanterns through the AWANGO brand
About Total
Total is a global integrated energy producer and provider, a leading international oil and gas company, a major player in low-carbon energies. Our 98,000 employees are committed to better energy that is safer, cleaner, more efficient, more innovative and accessible to as many people as possible. As a responsible corporate citizen, we focus on ensuring that our operations in more than 130 countries worldwide consistently deliver economic, social and environmental benefits.

 The TOTAL Network Director, Marieme Sow, speaking during the launch of TOTAL Excellium Campaign urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions. The Campaign was launched in Dar es Salaam over the weekend and it will spread to more than 100 Total Service Stations nationwide and it will last for one month.
 The Total Director of Legal and Corporate Affairs, Marsha Msuya Kilewo, speaking during the launch of TOTAL Excellium Campaign urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions. The Campaign was launched in Dar es Salaam over the Weekend and it will spread to more than 100 Total Service Stations nationwide and it will last for one month.
 The Total Director of Legal and Corporate Affairs, Marsha Msuya Kilewo, speaking during the launch of TOTAL Excellium Campaign urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions. The Campaign was launched in Dar es Salaam over the Weekend and it will spread to more than 100 Total Service Stations nationwide and it will last for one month.
 The TOTAL Network Director, Marieme Sow, distributing Total T-shirts and Caps to motorists during the launch of TOTAL Excellium Campaign urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions. The Campaign was launched in Dar es Salaam over the weekend and it will spread to more than 100 Total Service Stations nationwide and it will last for one month.
The TOTAL Network Director, Marieme Sow, in a group photo with Total Excellium Ambassadors, during the launch of TOTAL Excellium Campaign urged motorists to maximize on the use of TOTAL Excellium, a high-tech fuel that cleans and provide longer-lasting protection to vehicle engines to ensure they perform better, use less fuel and produce fewer polluting emissions. The Campaign was launched in Dar es Salaam over the weekend and it will spread to more than 100 Total Service Stations nationwide and it will last for one month.

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.150 ZATEKETEZWA KWA MOTO

$
0
0




Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na wavuvi leo 29/9/2019 katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu zikiteketezwa kwa Moto leo katika bwawa la Nymba ya Mungu Kilimanjaro.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisisitiza jambo kwa wavuvi pamoja na wananchi waliojitokeza kumsikiliza leo katika eneo la Bwawa la nyumba ya Mungu Mwanga Kilimanjaro.


NA:Vero Ignatus,Mwanga Kilimanjaro.


Serikali imeteketeza kwa Moto zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Akiwa katika Oparesheni maalumu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali itaendelea kupiga Vita Uvuvi haramu kwa ajili ya kunusuru mazalia ya viumbe hai wa majini kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Waziri Mpina amewataka wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo uvuvi haramu umeshamiri kuacha mara moja ambapo zoezi hilo la kuwasaka wavuvi haramu liakuwa la nchi nzima

''Hivi sasa tunachoma nyavu hapa za ni safari tuliyoianza ya kuchoma nyavu na kukamata wavuvi haramu, na wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu nchi nzima ,kwahiyo tunaanza safari hapa mwanga ambapo safari hii itakuwa ni ya nchi nzima "Alisema Mpina

Katika Hatua nyengine Waziri Mpina ametoa miezi mitatu kwa halmashauri ya wilaya ya mwanga kuhakikisha Ujenzi wa choo Bora kwa ajili ya wavuvi na Wafanyakazi Biashara wa eneo hilo vinginevyo Marufuku halmashauri kukusanya ushuru katika eneo Hilo.

"Halmashauri inaendelea kukusanya mapatao kila uchao na wala hawachoki hawana likizo wala jumapili,lakini choo tu wakati mwingine hata milioni mbili hakifiki,kimeshindikana kujengwa,ifikapo tarehe 30/12/2019nitarudi hapa kuja kukagua,nikikuta hakuna mwalo,nikikuta hakuna vyoo,nitaifungia halmashauri ya mwanga kukusanya chochote"akisema Mpina

Samuel Kifoyo ni Mkazi wa mwanga ambae imeelezwa amekuwa akitafutwa na Baadhi ya watu wakiwemo Baadhi ya Askari kwa tuhuma mbalimbali ambapo baada ya kupata taarifa za ujio wa waziri wa uvuvi anajitokeza adharani akiwa katika mavazi ya kike kuhofia kupigwa na mahasimu wake Katika kata ya Lang'ata Kama anavyo anabainisha.

"Nimekuja hapa leo ili unilinde ,mama yangu ni mjane kazi yake anakata kuni nimeteseka nimekaa muda mrefu,watu wametoa pesa ili nikamatwe niuliwe na dada huyo yupo hapa,na leo alikuwa aseme kama alivyosema mwanga ndiyo maana nikaona bora mimi nikaona niwahi,nilikuwa nimejificha kwenye mapori nikivizia msafara wako mheshimiwa".Alisema Samweli Mkazi wa Mwanga.

Joachim Haule na Juma Waziri ni Baadhi ya wakazi wa kata hiyo wanasema eneo Hilo bado Hali ya usalama si shwari na hapa wakaeleza changamoto wanazo kabiliana nazo katika Oparesheni zinazo fanywa eneo Hilo.

Kwa mujibu wa wizara ya mifugo na uvuvi kwa sasa tanzania inasamaki wakutosha bila kuagiza nchi nyengine lakini bado suala la Uvuvi haramu limeshamiri katika Baadhi ya maeneo Kwenye maziwa na baharini, huku Oparesheni zilizo kuwa zikiendelea miaka iliyo pita zikianza upya kwa Kasi kubwa maeneo yote ya uvuvi na mifugo.

PROFESA KABUDI ASEMA NISHANI ALIYOPEWA DKT SALIM ANASTAHILI, AWATAKA WATANZANIA WANAPOPEWA MAJUKUMU YA KITAIFA KUYAFANYA KWA UAMINIFU NA UZALENDO USIOTILIWA MASHAKA.

$
0
0

Watanzania wametakiwa kuyafanya majukumu ya kitaifa wanayopewa na viongozi wa serikali kwa uzalendo usiotiliwa mashaka,uamini na ufanisi kama walivyoelekezwa wakati wa kukabidhiwa majukumu hayo kwa faida ya Nchi. 
 Hayo yamesemwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akitoa Kongole kwa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kufuatia kitendo cha kukabidhiwa Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China nishani ambayo inamfanya Dkt. Salim kuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China. 
 Prof. Kabudi ameongeza kuwa nishani aliyokabidhiwa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim imeliletea heshima kubwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nay eye mwenyewe kutokana na utendaji wake usiotiliwa mashaka baada ya kuaminiwa na kukabidhwa majukumu hayo na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwataka Watanzania wote hususani vijana kuiga mfano huo. 
 Amesema Dkt Salim Ahmed Salim ni Mtumishi mwaminifu na mzalendo kwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kuanzia na ukurugenzi katika wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki balozi katika nchi za Misri,India,China na Umoja wa Matifa lakini pia ,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Waziri wa Mambo ya Nje,Naibu waziri Mkuu kisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 
 Nishani hiyo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki. 
 Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa. 
 Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. 
Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani. 
 Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini China Balozi Mbelwa Kairuki (pichani) amesema mamilioni ya Wachina hususani vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. 
 Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. 
Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao. 
 Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.

Total Yazindua Kampeni ya Uelimishaji Madereva Faida za Mafuta ya Excellium

$
0
0
  Kampuni ya Total Tanzania imewahimiza madereva kote nchini, kutumia mafuta ya Total Excellium ili kubaini tofauti na mafuta mengine yote yasiyo na excellium, ili wakiishagundua tofauti, ndipo wafanye uamuzi ni mafuta gani ya kutumia kwenye magari yao, au vyombo vya moto.

Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow katika taarifa yake kwa vyombo vya habari katika kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa viambata mbalimbali na kuunda mafuta ya Total Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. .
Marieme Sow amesema, mafuta ya vituo vya Total, yameongezwa kiambata cha excellium kilichotengenezwa mahsusi na watafiti wa kampuni ya Total ambacho husafisha injini za gari yako kwa kadri inavyotembea, kwa kila kilomita baada ya kilomita na pia kuzuia uchakavu wa injini hadi asilimia 93% ukilinganisha na mafuta mengine yasiyo na Excellium.
Mafuta ya Total Excellium ndio mafuta pekee nchini Tanzania yenye viambata ambavyo hupunguza msuguano kwenye injini, hivyo kupunguza kuchakaa kwa injini na kuongeza maisha ya injini ambako pia huifanya injini kufanya kazi vizuri zaidi kwa kutumia mafuta kidogo na kuzalisha hewa ya ukaa kidogo hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Mariane Saw amesema, ili madereva waweze kuona faida na utofauti kati ya kutumia mafuta ya Total Excellium na mafuta mengine, inawabidi kutumia mafuta ya excellium mfululizo bila kuchanganya changanya mafuta, hivyo ametoa wito kwa madereva kufanya utafiti huo kwa kutumia mafuta ta total mfululizo na kupima utofauti wa matumizi ya mafuta na wepesi wa magari yao.  "Tunapendekeza washikamane na Total Excellium na watapata matokeo haya mazuri," alisema.
Marieme ameongeza kuwa madereva wa umbali mrefu hususan madereva wa mabasi na malori ambao hutumia mafuta ya Total Excellium wamekuwa wakishuhudia jinsi injini zao zinarekodi utendaji bora zaidi, hutumia mafuta kidogo na ni safi zaidi kwa sababu ya Total Excellium.
Mkurugenzi Sheria na Mahusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya Kilewo amesema japo uagizaji wa mafuta nchini Tanzania hufanywa kupitia mfumo wa ununuzi wa pamoja (bulk procurement) hivyo mafuta yote yanayoingizwa nchini Tanzania yanakuwa na ubora ulio sawa, lakini mafuta ya Total ni tofauti na mafuta mengine yote kwa sababu mafuta ya Total yakishapokelewa, yanaingizwa kwenye Depot ya Total, na kuongezwa ubora kwa kuongezewa viambata, hivyo mafuta yakitoka depot za Total yanakuwa yameongezewa Excellium, hivyo kuwa mafuta ya Total Excellium.
Marsha Msuya Kileo, ameongeza, licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Total kutengenezwa viambata vinavyounda mafuta ya Total Excellium, lakini mafuta hayo ya Total Excellium bado yanauzwa kwa bei zile zile bei elekezi ambazo ziko sawa na mafuta mengine, hivyo unapojaza mafuta ya Total, unalipa kiwango kile kile cha fedha, lakini kupatiwa mafuta yaliongezwa ubora. 
 Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port Access. Temeke, jijini Dar es Salaam na inaendeshwa nchi nzima katika vituo vya Total zaidi ya 100 kwa muda wa mwezi mzima.
 Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port Access. Temeke, jijini Dar es Salaam na inaendeshwa nchi nzima katika vituo vya Total zaidi ya 100 kwa muda wa mwezi mzima.
 Mkurugenzi Sheria na Mahusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya Kilewo, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port Access. Temeke, jijini Dar es Salaam na inaendeshwa nchi nzima katika vituo vya Total zaidi ya 100 kwa muda wa mwezi mzima.
 Mkurugenzi Sheria na Mahusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya Kilewo, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port Access. Temeke, jijini Dar es Salaam na inaendeshwa nchi nzima katika vituo vya Total zaidi ya 100 kwa muda wa mwezi mzima.
 Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow, akigawa zawadi ya fulana za Total Excellium wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port
 Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow, akigawa zawadi ya fulana za Total Excellium wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port

Mkurugenzi wa Mtandao wa Total, Marieme Sow, katika picha ya pamoja na mabalozi wa Total Excellium, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma, faida za matumizi ya mafuta ya TOTAL Excellium ambayo yameongezwa kiambata cha Excellium ambayo husafisha na kutoa ulinzi kwa injini za gari kufanya kazi vizuri zaidi, kudumu zaidi na kutumia mafuta kidogo zaidi na hutoa moshi msafi usiochafua mazingira. Kampeni imezinduliwa jana katika kituo cha Mafuta cha Total Port Access. Temeke, jijini Dar es Salaam na inaendeshwa nchi nzima katika vituo vya Total zaidi ya 100 kwa muda wa mwezi mzima.

Wafanya kazi Airtel wamuanga Mkurungenzi wao kwa mtindo wa kipekee, naye aagana nao akiishukuru serikali.

$
0
0
Wafanya kazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania wamemuanga Mkurungenzi wao anayeondoka kwa njia ya kipekee baada ya kuhudumu kwenye kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka sita.
Akiongea kwenye hafla hiyo, Mkurungenzi huyo anayeondoka Bw. Sunil Colaso alisema kuwa Tanzania imekuwa ni kama nyumbani na hatua hii ya kuwaanga ni ngumu kwani kwa kipindi cha miaka sita Tanzania imekuwa ni nyumbani.
“Nachukua fursa hii kuwashukuru wafanya kazi wote wa Airtel kwa muda wote tuliofanya kazi pamoja. Tumeshirikiana kufanya kazi kwa bidii na umoja wenu ulifanya kazi yangu kuwa rahisi na kufanikisha malengo yetu. Ni Imani yangu kuwa kuwa leo wakati naondoka ninaacha nyuma timu imara ambayo itaendelea kuwahudumia Watanzania kwa huduma bora za mawasiliano kila siku.
Alitoa wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya.
Colaso pia akitoa shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania, Wizara na Taasisi zake zote kwa kuiunga mkono Airtel Tanzania kwa kipindi chote cha uongozi wake. “nashukuru kwa dhati serikali kwa kutuunga mkono Airtel Tanzania, ndio maana tumefanikiwa kutoa huduma bora kimataifa na hapa nchni sana sana kwenye huduma za Airtel Money, Airtel yatosha bando inayowafaidisha wateja kwa huduma za kupiga simu pamoja na intaneti.  Nawapongeza pia wafanyakazi wote wa Airtel kwa kuwa na mafanikio ya kipekee ya kuweza kusambaza huduma za Airtel Money mpaka vijijini ambapo hadi sasa mmefungua  zaidi ya maduka ya Airtel Money Branches 900. Alisema Colaso
Mkurungenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alimpongeza Colaso huku akisema mbali ya bosi huyo kuwa ni mtu mwenye maono ya kuendeleza sekta ya mawasiliano hapa nchini, lakini pia alijipambanua katika kuifanya sekta ya mawasiliano kuleta tija katika maswala ya uchumi  hapa nchini.
“Tunamuaga leo Mkurugenzi Sunil Colaso, alikuwa ni mtu wa kupenda kazi yake, kujitolea kusaidiana na wafanyakazi  kila alipohitajika, alipenda kufanya kazi kwa Umoja,  haya ni kati  ya mambo ambayo tutamkumbuka nayo. Alikuwa ni mtu mwenye sifa zote za kiongozi na mwenye kujenga timu ya pamoja, alimpa kila mfanyakazi wa Airtel Tanzania nafasi ya kuonyesha uwezo wake.’ Singano alieleza.

 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akipokea keki kama ishara ya kuagana na wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga  ilifanyika jijini Dar es salaam  baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa zaidi ya miaka 6.
 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akikata keki kama ishara ya kuagana na wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga  ilifanyika jijini Dar es salaam  baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa zaidi ya miaka 6. 
Bw. Sunil Colaso ametoa wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya. 

Airtel Tanzania staff bid farewell to outgoing MD Sunil Colaso in style

$
0
0

Airtel Tanzania staff have bid farewell in style to their out-going Managing Director Sunil Colaso who is leaving Tanzania after serving Airtel Tanzania for over six years.
Speaking during the farewell event, the outgoing Managing Director Mr. Sunil Colaso said Tanzania has become his second home and it was difficult to bid farewell to his second Family, Airtel Tanzania were he has been working for more than six years.
“I thank my team, for all their hard work and dedication during my tenure, I must admit that you made it so easy for me as a leader to achieve our targets. Today, I am confident I leave behind a capable team that is enthusiastic enough to continue serving Tanzanians better and better every day,”
He called on staff and other stakeholders to accord all the support to the incoming Managing Director George Mathen who is expected in the country next month to lead Airtel Tanzania to even greater heights.
Mr. Colaso also thanked the Government of Tanzania, its Ministries, and Agencies for all the support accorded to Airtel during his entire time. Through the support, Airtel was able to provide world-class communication services across the country, specifically in Airtel Money, Voice and Data. Among many of his achievements, Mr. Colaso was instrumental in building one of the largest mobile money distribution network in the country with over 900 Airtel Money Branches.
The Airtel Tanzania Corporate Communications Director Beatrice Singano hailed Mr. Colaso for being a visionary leader who was not only dedicated to the growth of the industry but also supportive to the contribution of the sector in the economy. 
“His love for his work, devotion and team spirit are some of the many qualities we will remember him by. He was an inspirational and motivational leader who encouraged team spirit and gave each individual within the team space to grow,” insisted Singano.
Farewell cake for out-going Managing Director Sunil Colaso who is leaving after serving Airtel Tanzania for over six years.

KATIBU MKUU MWAKALINGA AMKALIA KOONI MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOROSI MBEYA

$
0
0
  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami kuhakikisha anamaliza mradi huo ndani ya muda wa mkataba na si vinginevyo.

Aidha, ameongeza kuwa hatamuongezea mkandarasi huyo muda wa kumaliza kwani muda aliopewa ulikuwa unamtosha kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Hayo ameyasema mkoani Mbeya alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amemuelekeza mkandarasi huyo kuongeza vitendea kazi na wataalamu ili kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliobakia.

"Natarajia utaongeza vifaa na wataalamu ili kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati, pia ukumbuke kuwa sitakupa muda wa nyongeza hivyo fanya juhudi ili umalize mradi huu ndani ya muda", amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 unajengwa na mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo zote ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.

Arch. Mwakalinga amemuelekeza pia mkandarasi kutumia muda wake wote kuwa katika eneo la mradi hata ikiwezekana kuongeza masaa ya kufanya kazi usiku na mchana.

"Fanyeni kazi usiku na mchana ili kuepukana na changamoto za vipindi vya mvua na hakikisheni barabara hii inajengwa kwa viwango vya ubora zaidi", amesema Arch. Mwakalinga.

Naye, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 53 ukilinganisha na muda wa mkataba uliotumika ambao ni miezi 23 sawa na asilimia 85.19 ya muda wa mkataba.

Eng. Mwita ameeleza kuwa mkandarasi mpaka sasa ameshakamilisha kujenga tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, lami ya prime KM 6.78 na kazi zingine za ujenzi wa makalvati madogo na madaraja makubwa matatu zikiendelea.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ya Singida na Tabora ambapo barabara hii ikikamilika itaongeza zaidi fursa za kimaendeleo kwa wananchi kiuchumi na usafirishaji. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa (wa pili kushoto), alipokagua ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.


 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa katika barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya.
 Muonekano wa sehemu ya lami ya prime katika  ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 kwa kiwango cha lami, mkoani Mbeya. Mradi huu unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.

Timu ya wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) ikiongozwa na Mhandisi Joyce Mbunju, wakikagua tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.
Kazi zikiendelea za usukaji wa nondo katika Daraja la Lupa litakalokuwa na urefu wa mita 63 katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39, mkoani Mbeya.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA UNGA WA MHOGO-CSTC LINDI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula wakisalimiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) walipotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kukagua mazingira ya kiwanda hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake mkoani Lindi ili kusikiliza na kutatucha changamoto za wawekezaji.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya ardhi kwa watendaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) kilichopo Wilaya ya Lindi Vijijini alipotembea mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (kushoto kake) pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (kulia kwake) kilichopo Lindi alipotembelea kiwandani hapo
 Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile  akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo inayotumika katika kiwanda cha CSTC kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula kilichopo Lindi Vijijini alipotembelea kiwandani hapo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) wakiangalia moja ya mfuko wa unga wa muhogo uliotengenezwa na kiwanda hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiuliza swali kwa Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile (wa kwanza kushoto mwenye kofia) wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watumishi wa kiuwanda cha kutengeneza unga wa muhogo kilichopo Lindi.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

DKT. SALIM ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA URAFIKI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, leo asubuhi tarehe 29 Septemba 2019 amemtunukia Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa. Dk. Salim Ahmed Salim, Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika jijini Beijing.  Mheshimiwa Dkt. Salim anakuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Nishani hiyo ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.


Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.


Mbali na Dk.Salim,  wengine waliotunukiwa Nishani ya Urafiki ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Kikoministi cha Cuba Jenerali Raul Castro, Dada wa Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Kiongozi wa Jumuiya ya Urafiki ya China na Urusi Ndugu Galina Kulikova, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Bi  Isabel Crook  kutoka Canada.


Vilevile  Rais Xi alitoa Nishani  ya Jamhuri na Nishani ya Heshima ya Taifa kwa raia 36 wa China kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa la China kupitia kazi zao katika fani mbalimbali.


Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim  kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.


Tukio la Kutoa Nishani limetangazwa moja kwa moja na Televisheni zote za Jamhuri ya Watu wa China na kushuhudiwa na watu zaidi ya Milioni 500.


Kwa mujibu wa maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini China Ndugu Mbelwa Kairuki Kupitia tukio la leo, mamilioni ya Wachina hususan vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa  wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.


Aidha Balozi Kairuki ameeleza kwamba maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka 55 ya urafiki na udugu kati ya China na Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964. Uhusiano wa China na Tanzania uliotokana na uhusiano mzuri wa waasisi wa mataifa haya mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Tsetung. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huu umekwenda mbali zaidi ya uhusiano kati ya Serikali na Serikali na kushamiri kwa uhusiano wa watu kwa watu.


Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa  kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


Bi. Maryam Salim akiwa katika picha na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping na picha ya chini akiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki mara baada ya kupokea nishani.
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live




Latest Images