Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Tanzania Yasaini Mkataba wa Kupinga Matumizi ya Nyuklia

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akisaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia na kuwa mojawapo ya nchi kumi na mbili zilizosaini na kuridhia mkataba huo na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na ya 32 zilizoridhia mkataba huo. Zoezi hilo limefanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa kunakofanyika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,New York, Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri wa nchi 12 ambao wamesaini na wengine kuridhia mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia na kuwa mojawapo ya nchi kumi na mbili zilizosaini na kuridhia mkataba huo na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na ya 32 kati ya zilizoridhia mkataba huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York, Marekani. Mazungumzo ya viongozi hao yalilenga masuala ya maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki sambamba na hali ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

……………………..

Yapongezwa kwa kulinda amani ukanda wa maziwa makuu
Kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia
Yawa miongo mwa nchi 60 zilizosaini mkataba huo duniani



Na Mwandishi wetu, New York

Umoja wa Mataifa umeipongeza Serikali ya Jamhri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake wa kulinda amani katika ukanda wa maziwa makuu na kuahidi kushirikiana na Tanzania katika kuzuia matukio yanayosababishwa na misimamo mikali.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Plamagamba John Kabudi ambapo pia katika mazungumzo hayo wamegusia masuala ya maendeleo katika ukanda wa maziwa makuu, ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa ya Burundi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema umoja huo unatambua mchango na jitihada za Tanzania na kuongeza kuwa Umoja huo upo tayari kushirikiana na Tanzania katika jitihada zake za kuzuia matukio yanayosababishwa na misimamo mikali.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameuhakikishia Umoja wa Mataiafa kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja huo katika vikosi vya kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sehemu nyingine duniani ili kuufanya ukanda wa maziwa makuu, Afrika na duniani kwa ujumla kuwa mahali salama pa kuishi.

Ameongeza kuwa Tanzania inaunga mkono mabadiliko yanayofanyika ndani ya Umoja wa Mataifa na kwamba inakubaliana na mabadiliko hayo. Aidha, Waziri Kabudi ameitumia fursa hiyo kumueleza katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa hatua mbalimbali za kimaendeleo ambazo Tanzania inatekeleza katika kufikia malengo ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.

Katika tukio jingine Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia na kuwa mojawapo ya Nchi kumi na mbili zilizosaini na kuridhia Mkataba huo na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na ya 32 kati ya nchi zilizoridhia mkataba huo.

Prof. Kabudi amesema kuwa Tanzania inaunga mkono jitihada zote za kupiga kabisa marufuku matumizi ya silaha za nyuklia kama sehemu ya kuufanya ulimwengu kuwa salama ambapo chini ya mkataba huu zimefanywa kuwa silaha za maangamizi.

Hata hivyo Prof. Kabudi amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikatai na inaunga mkono matumizi ya amani ya nguvu za nyuklia kama sehemu ya dawa, kuhifadhi vyakula na uzalishaji wa nishati miongoni mwa matumizi mengine chini ya uangalizi madhubuti wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki.

Ameongeza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua hiyo ikitiliwa maanani kuwa zipo nchi zenye silaha za nyuklia takribani 14 elfu na zimetenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuimarisha silaha hizo na kutoa wito kwa mataifa hayo kujenga imani kwa mataifa mengine na kwamba matumizi ya silaha hizo si njia sahihi na salama za kuihakikishia dunia amani na usalama.

Prof. Kabudi anatarajiwa kuhutubia katika mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadae hii leo jijini New York, Marekani.

NCHI SITA ZA SADC KUSHIRIKI MAONESHO YA SIDO KITAIFA SINGIDA

0
0

Na Dotto Mwaibale, Singida

NCHI sita za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) kushiriki maonesho ya pili ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) kitaifa 2019 mkoani Singida.

Nchi zitakazo shiriki maonesho hayo ni Kenya, Burundi, Ruanda, Uganda, China, India na Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (pichani) alisema maonesho hayo yataanza kufanyika Oktoba 4 hadi 9 mwaka huu.

" Maonesho haya yatafanyika sanjari na maadhimisho ya wiki ya chakula duniani ambayo yatafanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 16 mwaka huu katika Viwanja vya Bombadier zamani Peoples" alisema Nchimbi.

Nchimbi alisema kufanyika maonesho hayo mkoani Singida ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo ambao unakuwa kiuchumi kutokana na shughuli za kilimo, ufugaji, biashara na viwanda.

Alisema Mkoa wa Singida wanajivunia kuchaguliwa kufanyika kwa maonesho hayo kitaifa na hii itawapa hamasa kubwa wananchi katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji kutokana na mazao yanayolimwa mkoani hapa pamoja na vya mafuta ya alizeti.

Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho hayo.

ZIARA YA MJUMBE WA KAMATI KUU CCM KWENYE BANDA LA WIZARA YA MADINI NA TAASISI ZAKE KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Ngemela Lupinga (kulia) akifafanua jambo kwenye Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 27 Septemba, 2019. Kushoto ni watalam kutoka Tume ya Madini, Msafiri Kussa na Monica Mkumbo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Ngemela Lupinga (kulia) akisalimiana na mtaalam kutoka Tume ya Madini, Monica Mkumbo (kushoto) mara baada ya kuwasili katika banda hilo kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 27 Septemba, 2019.
Mhandisi Mchenjuaji Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST), Priscus Kaspana (kulia) akimwonesha sampuli za madini Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Ngemela Lupinga (kushoto) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 27 Septemba, 2019
Mhandisi Migodi wa Wizara ya Madini, Johnbosco Karungamye (katikati) akielezea majukumu ya Wizara kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Ngemela Lupinga (kushoto) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 27 Septemba, 2019.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo kwa Upande wa Taaluma kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Elvanus Kapira (kushoto) akielezea kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kwa Kanali Mstaafu Ngemela Lupinga (kulia) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 27 Septemba, 2019.

NGOMA ZA MATAIFA MBALI MBALI ZAZIDI KUPAMBA TAMASHA LA JAMAFEST 2019

0
0
Kikundi cha Ngoma na Sarakasi cha Safi kutoka nchini Tanzania kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Mmoja ya kijana wa kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi kutoka Tanzania akionyesha umahili wake wa kucheza kwa kutumia shingo na mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Vijana wa Kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi wakionyesha umahili wao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wakiwaaga wanajumuiya wa Afrika Mashariki waliohudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wasanii wa Kenya wakionyesha umahili wao wa kuigiza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma toka Zanzibar, Tanzania wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma ya Kisukuma kutoka Wilaya ya Buchosa, Sengerema - Mwanza wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Akina mama wa Kigogo wanaweza, wakionyesha umahili wao wa kupiga ngoma na kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Ngoma ya kigogo toka Dodoma wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Kenya kikionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili toka kushoto) akishuhudia ngoma za mataifa toka Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kuhudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Mambo ni moto!

Wakili Tenga na wenzake wa Six telecoms, wamuandikia barua DPP

0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,

IKIWA ni siku ya tano tangu Rais John Magufuli atoe ruhusa kwa mahabusu wa kesi za uhujumu uchumi kukiri makosa yao na kulipa vigogo Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, akiwemo Wakili maarufu Dk Ringo Tenga, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) yenye maombi mbalimbali kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Mapema, wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai jmbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo leo Septemba 27, limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba katika ahirisho lililopita, upande wa utetezi uliomba kujadiliana na wateja wao.

Wakili wa Utetezi, Bryson Shayo amedai mahakamani hapo kuwa, wameshauriana na wateja wao na katika mashauriano hayo washitakiwa wameandika barua kwa DPP kuzingatia agizo hilo la Rais John Magufuli la Septemba 22, mwaka huu.

Amedai Septemba 26, mwaka huu washitakiwa hao waliandika barua kwenda kwa DPP yenye maombi mbalimbali kuhusu shauri hilo hivyo, aliomba ahirisho la siku 14 ili barua iweze kujibiwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Septemba 24 mwaka huu upande wa utetezi uliomba mahakama kuitisha shauri hilo leo (jana) kwa sababu ya mazingira ya kesi yenyewe wanaomba wazungumze na wateja wao.Dk Tenga na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza maalipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango USD 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa USD 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Pia wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti USD 466,010.07 kwa TCRA.

Vile vile ,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara USD 3,748,751.22 sawa na Sh bilioni nane .


WAKULIMA SIKONGE WAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUPATA MIKOPO KUPITIA TAASISI ZA FEDHA

0
0
 Bwala linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji Uliyanyama lenye mita za ujazo milioni mbili.

 Katika picha ni Banio linalopokea maji kutoka katika Bwawa la Umwagiliaji Ulianyama Wilayani Sikonge na kupeleka maji katika mfereji na mashamba ya kilimo cha Umwagiliaji katika Skimu hiyo.

 Katika picha ni moja ya miundombinu iliyojengwa kiufanisi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Uliyanjama iliyopo Wilayani Sikonge Mkoani Tabora ili kuweza kumudu kasi ya maji yanayoingia katika mashamba na kuzuwia upotevu wa maji na mmomonyoko wa ardhi.

 Katika Picha ni magunia ya mpunga katika moja ya ghala la kuhifadhia nafaka lililojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kayika skimu ya ka Kilimo cha Umwagiliaji Uliyanyama Mkoani Tabora.


Bw. Simon Kalosa katibu wa chama cha umwagliaji cha Uliyanyama Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, akiongea kuhusu mafanikio yaliyopatika katika skimu hiyo baada ya Uboreshaji wa Miundombinu ya umwagiliaji.



Waziri Kairuki Agawa Taulo za Kike kwa Wanafunzi Shule ya Sekondari ya Mkombozi-SAME

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Angellah Kairuki akiwakabidhi taulo za kike kwa baadi ya  wanafunzi wa shule ya sekondari Mkombozi iliyoko kijiji cha Hedaru wilaya ya Same mkoani Killimanjaro kama anavyoonekana katika picha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Angellah Kairuki akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mkombozi iliyoko kijiji cha Hedaru wilaya ya Same mkoani Killimanjaro. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Angellah Kairuki akiwakabidhi taulo za kike kwa mwalimu kwa niaba ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mkombozi iliyoko kijiji cha Hedaru wilaya ya Same mkoani Killimanjaro kama anavyoonekana katika picha.

Na Vero Ignatus,Killimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Angellah Kairuki amegawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari mkombozi iliyoko kijiji cha Hedaru wilaya ya Same mkoani Killimanjaro lengo likiwa ni  kuwawezesha wasichana kusoma bila usumbufu wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Kairuki alifika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa kike huku akiwataka kujiepusha na vishawishi pamoja na tamaa ili waweze kutimiza ndoto zao na kusaidia jamii inayowazunguka .
Aidha amesema kuwa ataendelea kushirikiana na shule hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio ,uhaba wa matundu ya vyoo ili wanafnzi hao waweze kusoma katika mazingira rafiki.
Furahini Lubuwa ni  wa shule ya sekondari ya mkombozi,hiyo amempongeza Waziri  Kairuki kwa kutembelea wanafunzi hao na kuwapatia msaada wa taulo za kike kwani zitawasaidia hasa wale ambao wanatoka katika familia zenye kipato cha chini .
Fatuma Hemed ni mmoja wa Wanafunzi wa Shule hiyo amesema kuwa msaada huo utawawezesha kusoma bila usumbufu kwani wapofikia kipindi cha hedhi huwa na hofu hasa wale ambao hawawezi kujisitiri vyem hivyo msaada huo utawasaidia.

Matukio katika Picha: Safi theatre yatia fora Jamma festival


RC FUATILIA UTENDAJI KAZI OFISI YA DC KILOLO-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi afuatilie utendaji kazi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo kufuatia watumishi 14 wa ofisi hiyo wakiwemo madereva 10 kuhamishwa baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdallah kudai kuwa hawafanyi kazi ipasavyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ni mhuimu kwa viongozi wakatambua dhamana zao katika utekelezaji wa shughuli zao pamoja na kuwatambua, kuwajali na kuwathamini watumishi wa kada zote wakiwemo madereva, hivyo ni vizuri wawaandae kwa kuwapa maelekezo kwa wakati kwa kuwa nao ni binadamu na wanafamilia.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 27, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kilolo, Halmashauri ya wilaya ya Kilolo pamoja na Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesisitiza umuhimu wa watumishi hao kushirikiana.

Waziri Mkuu amesema pamoja na shughuli za maendeleo wanazofanya katika wilaya hiyo lakini hawana mshikamano, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya ahakikishe anashirikiana vizuri na wenzake kwa sababu watumishi wengi wamehamishwa tangu aingie katika ofisi hiyo na hata wanaoletwa wanalalamika na wanaomba wahamishwe.

Amesema watumishi wengi katika ofisi hiyo anawaona hawana uwezo wakiwemo wasaidizi wake kama madereva, watunza kumbukumbu na makatibu muhtasi. “Hata aliyekuwa Katibu Tawala wa wilaya hii alihamishwa kwa sababu na kutoelewana na DC, na hata huyu Katibu Tawala wa Wilaya aliyepo sasa hana raha anataka kuhama kwa sababu hizo hizo.”

“Lazima tuwatambue wasaidizi wetu na majukumu yao. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haiwezekani ikawa hivi, lazima kuna shida kuwaondoa watumishi wote, Mkuu wa Mkoa fuatilia hii ni mpya. Hapa tujue mbovu ni nani Mkuu wa Mkoa tunataka tujue DC wako anataka dereva wa aina gani, tangu amefika hapa madereva 10 wote hawafai? 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “ili mfanye kazi vizuri mnatakiwa mshikamane mfanye kazi kama timu moja kwani pamoja na shughuli mnazofanya hamna ushirikiano. DC (mkuu wa wilaya) sasa utabaki peke yako utakuwa unaandika mwenyewe, unaendesha gari mwenyewe maana wote hawafai. Mkuu Mkoa nakukabidhi majina ya watumishi hao ushughulikie suala hili. Na Katibu Tawala wa Mkoa usilete watumishi wengine hapa mpaka suala hili litakapopatiwa ufumbuzi”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga kiasi cha fedha katika makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwenye maeneo yao kama ujenzi wa vituo vya afya, barabara za halmashauri na masoko badala ya kutegemea fedha kutoka Serikali Kuu pekee.

Amesema wilaya ya Kilolo ambayo haina kituo cha mabasi inatakiwa itenge fedha kutoka kwenye makusanyo yao na kuanzisha mradi wa kituo hicho ambao utekelezaji wake utaboresha huduma kwa wananchi pia, mradi huo utasaidia katika kuongeza mapato ya halmashauri. Halmashauri ya wilaya ya Kilolo inakusanya sh. bilioni nne kwa mwaka.

Waziri Mkuu amesema watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani wananchi wanahitaji waone matokeo ya uwepo wao kutokana na dhamana waliyotewa na Serikali katika wilaya hiyo. “Madiwani nanyi simamieni halmashauri yenu vizuri kwa sababu nyie ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri.”

Awali, Mbunge wa jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya yao ikiwemo ya umeme, ambapo kati ya vijiji 94 vilivyoko vijiji 54 vimeunganishiwa huduma hiyo na vilivyosalia vitakuwa viunganishiwa umeme ifikapo Desemba mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu miradi ya maji mbunge huyo alisema kati ya vijiji 94 vya wilaya hiyo vijiji 15 tu ndio bado havina maji ya uhakika lakini wanaendelea na mchakato wa ufuatiliaji ili kuhakikisha navyo vipata maji safi na salama.”Kuhusu sekta ya elimu tatizo tulilonalo ni madai ya walimu waliohama na waliopandishwa madaraja.” Waziri Mkuu amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Mapema, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo ambapo alisema ameridhishwa na ujenzi huo uliogharimu sh. bilioni nne na alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mkurugenzi pamoja na mkandarasi anayenga.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya watumishi wa wilaya ya Kilolo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA KILOLO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happy na Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah (wa pili kushoto) kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo , Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019.
  Muonekano wa sehemu ya hospitali ya wilaya ya Kilolo ambayo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi huo  Septemba 27, 2019 na kusema kuwa amefurahishwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada kukagua na kufurahishwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NGOMA ZA MATAIFA MBALI MBALI ZAZIDI KUPAMBA TAMASHA LA JAMAFEST 2019

0
0
Vijana wa Kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi wakionyesha umahili wao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha Ngoma na Sarakasi cha Safi kutoka nchini Tanzania kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Mmoja ya kijana wa kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi kutoka Tanzania akionyesha umahili wake wa kucheza kwa kutumia shingo na mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wakiwaaga wanajumuiya wa Afrika Mashariki waliohudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wasanii wa Kenya wakionyesha umahili wao wa kuigiza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma toka Zanzibar, Tanzania wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha ngoma ya Kisukuma kutoka Wilaya ya Buchosa, Sengerema - Mwanza wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Akina mama wa Kigogo wanaweza, wakionyesha umahili wao wa kupiga ngoma na kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Ngoma ya kigogo toka Dodoma wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Kenya kikionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili toka kushoto) akishuhudia ngoma za mataifa toka Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kuhudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Mambo ni moto!

MWENGE WAZINDUA KIWANDA CHA MAJI ASILI NA JIWE LA MSINGI BARABARA YA MBUYULA MBINGA MJI

0
0
MWENGE wa uhuru kitaifa umemaliza mbio zake kwenye Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma kwa kuzindua, kukagua, kuweka jiwe la msingi, kutembelea miradi tisa ya thamani ya shilingi 924,150,266.14 ikiwemo mradi wa maji Asili (Mdaka Five) na barabara ya lami ya Mbuyula. 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally akizungumza jana wakati akizindua kiwanda cha maji Asili cha Mdaka Five aliwataka wamiliki wake kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo. 

"Kupitia kiwanda hiki cha maji Asili hongereni sana watu wa Mbinga mji mmepiga hatua kwenye viwanda kwani Rais John Magufuli ana amini katika Tanzania ya viwanda ili kuongeza ajira na kulipa kodi," alisema Ally. 

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi la barabara ya lami ya Mbuyula, Mzee aliwapongeza Tarura kwa ubora uliotumika ikiwemo kuzingatia urefu na upana. 

"Tunatoa ushauri kuwa vipimo vyote vilivyoelekezwa vifanyiwe kazi ipasavyo ili barabara hii iweze kuwanufaisha wananchi wa eneo hili pindi ikikamilika kabisa," alisema Ally. 

Meneja wa Tarura Halmashauri ya Mji wa Mbinga, mhandisi Ismail Mafita, akisoma taarifa ya barabara ya hiyo ya lami awamu ya kwanza alisema inajengwa na mkandarasi Ovans Construction Ltd kwa gharama ya shilingi 152,570,000.00.

Mhandisi Matifa alisema barabara hiyo imetengewa shilingi 16,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa mfereji wa upande wa pili, kuweka kivuko cha waenda kwa miguu na alama za barabarani ila kilometa zilizobaki zitamalizwa baada ya fedha nyingine kuletwa. 

Alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa kata za Mbinga Mjini, Mbambi, Matarawe na wanaoenda kupata huduma za afya katika hospitali ya Mji wa Mbinga (Mbuyula). 

Mkurugenzi wa Mdaka Five Co. Ltd, Joseph Mdaka alisema mradi wa kiwanda cha maji Asili umegharimu shilingi 265,500,000. ikiwemo jengo na mashine na hadi kukamilika kwake itagharimu shilingi 485,500,000 ikiwemo ujenzi wa maghala na uzio kiwandani.

Mdaka alisema lengo la mradi huo ni uzalishaji wa maji ya kunywa ambao ni safi na salama kutoka chanzo cha maji mlima Mhekela kilichotunzwa vizuri kwa kupanda miti eneo lote linalozunguka chanzo. 

"Uwepo wa kiwanda hiki utazalisha ajira za kudumu 25 na utahudumia wananchi wa Mbinga na Ruvuma kwa ujumla kwa kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi wa kati na mkakati wa kila mkoa kuwa na viwanda visivyopungua 100," alisema. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, Grace Quintine alisema mwenge wa uhuru umeridhishwa na miradi yote tisa ya thamani ya shilingi 924,150,266.14 na hakuna hata mmoja uliokataliwa. 

Quintine alisema kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu ni "Maji ni haki ya kila Mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa". 
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally akipeana mikono na Mkurugenzi wa Mdaka Five CO. Ltd, Joseph Mdaka baada ya kuzindua kiwanda chake cha maji Asili kilichopo mtaa wa Masumuni Halmashauri ya mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma. 
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally akizindua mradi wa maji wa Maganagana, kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, Grace Quintine. 
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally na Meneja wa Tarura, Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, Ismail Mafita, wakiangalia upimaji wa upana wa barabara ya lami ya Mbuyula ambapo aliweka jiwe la msingi. 

BONDIA JUMA CHOKI SASA AWAZIA UBINGWA WA TAIFA BAADA YA KUWA KING OF THE RING

0
0
Na Mwandishi wetu
BONDIA Juma Choki Baada ya kumgalagaza bila ya huruma Emanuel Mwakyembe na kuchukua ubingwa wa King Of The Ring 2019 katika uzito wa KG 58 amesema ato bweteka kwa kuwachua ubingwa huo 

Ambapo alipewa zawadi ya pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano amesisitiza ato bweteka kwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ata hivyo ameomba kuwa andaliwe ubingwa wa taifa ndio matarajio yake kwa sasa akichukuwa ubingwa wa taifa kisha ataenda juu kuchukuwa ubingwa wa Afrika arafu ubingwa wa Dunia

Bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuchukuwa mikanda nje ya nchi na kuletea sifa Tanzania 

Akizungumza kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa choki ni bondia mzuri na malengo yake ni kufika mbali na kweli atafika anapo pataka kwani kwenye nia pana njia

Ikumbukwe kuwa mimi ndio nimewatoa mabondia mabingwa wa dunia ambao wamepita katika mikono yangu kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Sunday Kiwale Ibrahimu makubi ambaye kwa sasa yupo mazoezini akijiandaa na mpambano wake na abdallah kingolwira wa morogoro pambano litakalofanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 mwenge pale jeshini.

Hivyo nina uwakika na mabondia wangu wote ninaowafundisha na siku zoto sinaga kazi mbovu

Wakili Tenga na wenzake wa Six telecoms, wamuandikia barua DPP

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV,

IKIWA  ni siku ya tano tangu Rais John Magufuli atoe ruhusa kwa mahabusu wa kesi za uhujumu uchumi kukiri makosa yao na kulipa vigogo Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, akiwemo Wakili maarufu Dk Ringo Tenga, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)  yenye maombi mbalimbali kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili katika
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Mapema, wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai jmbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo leo Septemba 27, limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba katika ahirisho lililopita, upande wa utetezi uliomba kujadiliana na wateja wao.

Wakili wa Utetezi, Bryson Shayo amedai mahakamani hapo kuwa,  wameshauriana na wateja wao na katika mashauriano hayo washitakiwa wameandika barua kwa DPP kuzingatia agizo hilo la Rais John Magufuli la Septemba 22, mwaka huu.

Amedai Septemba 26, mwaka huu washitakiwa hao waliandika barua kwenda kwa DPP yenye maombi mbalimbali kuhusu shauri hilo hivyo, aliomba ahirisho la siku 14 ili barua iweze kujibiwa.

 Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.
 
Septemba 24 mwaka huu upande wa utetezi uliomba mahakama kuitisha shauri hilo leo (jana) kwa sababu ya mazingira ya kesi yenyewe wanaomba wazungumze na wateja wao.

Dk Tenga na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza maalipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa  chini ya kiwango USD  0.25 kwa  dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa USD 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Pia wanadaiwa  katika kipindi hicho  walishindwa kulipa ada za udhibiti USD  466,010.07 kwa TCRA.

Vile vile ,washitakiwa hao  wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara USD  3,748,751.22 sawa na Sh bilioni nane

Twanga Pepeta, Nguza, Papii kocha jukwaa moja Jumamosi

0
0
Na Mwandishi wetu
 BENDI ya muziki ya African Stars itafanya onyesho la pamoja na wanamuziki nyota nchini, Nguza Vikings na mwanaye, Papii Kocha kwenye ukumbi wa hotel ya Nefaland ya Magomeni Kagera.

Onyesho hilo limepangwa kufanyika Jumamosi ya Septemba 28  huku Nguza na Papii wakipania vilivyo kuonyesha makali yao kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi huo.

Wakati Twanga Pepeta ambayo ipo chini ya ukurugenzi wa Luizer Mbutu inatarajia kutambulisha nyimbo kadhaa mpya, Nguza na Papii  kupitia bendi yao ya Big Sound wanatarajia kuweka hadharani vibao kadhaa vipya ambavyo wamevitunga hivi karibuni.

Mratibu wa onyesho hilo, Bakari Seif amesema kuwa onyesho hilo litaanza saa 2.00 jioni ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini kupata burudani inayoendana na kiingilio chao.

Amesema kuwa wanatarajia kupata shoo yenye ubora wa aina yake kwani Twanga Pepeta ni kisima cha burudani na Nguza na Papii ni moto wa kuotea mbali katika burudani.

“Hili ni onyesho maalum kwa mashabiki wa muziki wa dansi ambao wamekuwa wakimsubiri kwa hamu Twanga Pepeta na Nguza akiwa na Papii Kocha na bendi yake ya Big Sound. Nyimbo zote zinazotamba kwa bendi na wanamuziki hao zitapigwa ,.” amesema Seif.

HATIMAYE SAA ZAHESABIKA KWA WALIOKWENDA KWA DPP KUKIRI TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA, UHUJUMU UCHUMI

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KESHO ndio kesho kwa wanaotuhumiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha!Ndivyo unavyoweza kuelezea kwani kesho ndio zinamalizika siku saba ambazo Rais Dk.Joh Magufuli amezitoa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kushughulikia kesi za watuhumiwa hao ili watakaokiri na kukubali kurudisha fedha waachiwe huru.

Rais Dk.Magufuli Septemba 23,mwaka 2019 wakati wa kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine alishauri iwapo itawezekana wale ambao wapo mahabusu kwa kesi za tuhuma za uhujumi uchumi na utakatishaji fedha, wakiri makosa yao na baada ya hapo wapewe msamaha ili warudi uraiani.

Baada ya ushauri huo wa Rais , DPP Biswalo Mganga siku iliyofuata alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kutoa utaratibu ambao utatumika kwa watuhumiwa hao ambapo alieleza wazi

jambo hilo linawezekana endapo mshtakiwa mwenyewe ataiandikia ofisi yake barua kupitia kwa Mkuu wa Gereza na kusisitiza barua hiyo inapaswa kuandikwa na mtuhumiwa mwenyewe aliye gerezani na siyo Wakili. .

Tangu kutolewa kwa ushauri wa Rais kuhusu watuhumiwa hao na kisha DPP kutoa maelekezo ambayo yanapaswa kufuatwa imeelezwa kuwa idadi kubwa ya mahabusu wa kesi hizo wamejisalimisha ofisi za DPP kwa ajili ya kuomba msamaha ili waachiwe.

Hata hivyo hadi sasa haijafahamika idadi rasmi ya watuhumiwa ambao wameandika barua kwa DPP kupata msamaha huo ingawa inaelezwa kuwa wengi wanaotuhumiwa wamejitokeza kutumia nafasi hiyo kukiri makosa yao na kuomba msamaha.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na vyombo vya habari DPP Biswalo Mganga amenukuliwa akieleza ni vema akaachwa afanye kazi yake , hata hivyo alikiri ofisini kwake ameendelea kupokea watuhumiwa hao.  Katika kuhakikisha watanzania wanafahamu kinachoendelea , Michuzi TV na Michuzi Blogu itaendelea kukujuza kuhusu watuhumiwa hao.

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA TAMASHA LA PILI LA UTALII ZANZIBAR

0
0
Sekta ya Nchini Utalii imetakiwa kushirikiana kwa pamoja na Wawekezaji na pamoja na watoa huduma ya Utalii Nchini kuweka nguvu zaidi kwenye kutoa matangazo ili kurahisisha Usafiri na kuweza kuleta Watalii kwa wingi Nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo Jana Usiku katika Tamasha la Maonesho ya pili ya Utalii Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa Park Hyatt Shangani Zanzibar.

Mhe. Samia amesema ni vizuri kushirikiana na kuongeza nguvu, Jitihada katika kufanya kazi ili kukuza suala zima la Biashara ya Utalii Nchini ambapo pia amewataka Vijana kujitokeza kwa wingi kwenda katika maonesho hayo kuona kinachofanyika na kuweza kujifunza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya Tamasha la pili ya Utalii Zanzibar lililofanyika Jana usiku Park Hyatt Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Zanzibar Bibi Hadija Bakari kwa niaba ya Wizara yake kwa kufanikisha kufanikisha Tamasha la pili ya Utalii Zanzibar lililofanyika Jana usiku Park Hyatt Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti kwa Katibu Mtendaji wa kamisheni ya Utalii Zanzibar Abdallah Mohamed kwa kuweza kufanikisha Tamasha la pili ya Utalii Zanzibar lililofanyika Jana usiku Park Hyatt Zanzibar.




RAIA WA SRI LANKA AMUANDIKIA BARUA DPP KUKIRI KOSA LA KUSAFIRISHA MADINI YA SHILINGI MILIONI 36/- KINYUME NA SHERIA

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

RAIA wa Sri Lanka AbdulAzeez Amaan (26) amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuomba kukiri kosa la kusafirisha madini yaliyokuwa na thamani zaidi ya Sh.milioni 36 kinyume na sheria.
Amaan ambaye ni mwanafunzi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 26,mwaka 2019 akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha madini hayo bila ya kuwa na kibali wala leseni.
Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa, Septemba 21 mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ambapo mshtakiwa huyo alikutwa akisafirisha madini aina ya Scapolite yenye uzito wa gramu 996.50, Sperssartite gramu 487, Tanzanite gramu 44, Quarts gramu 126, Citrine gramu 174, blue agate gramu 101.80, Toumarine gramu 16, Aquamarine gramu 14.30 na Supphire gramu 5.04 yote kwa pamoja yakiwa na jumla ya Sh.milioni 36.5 bila ya kuwa na kibali.
Hata hivyo baada ya kusomewa shtaka lake Hakimu Simba alimtaka mshtakiwa huyo kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo aina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo  hadi pale itakapopata kibali kutoka kwa DPP.
Wakili wa Utetezi Shabani Mlembe alidai mteja wake amekwishaandika barua kwa DPP la kukiri kosa hilo, hivyo wanaomba tarehe ya karibu ili kufanya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo umekamilika na hawana pingamizi na maelezo hayo ya upande wa utetezi.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na kukamilisha taratibu.
Wakati huo huo, Hassan Azizi (33),Hassan Shaban (30) na William Daraja wamefikishwa katika Mahakama hiyo wakikabiliwa tuhuma za Uhujumu Uchumi ikiwamo kusafirisha gramu 983.5 za dawa za kulevya aina heroine.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo.
Upande wa Jamhuri ulidai Septemba 4, mwaka huu eneo la Tegeta Nyaishozi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam washtakiwa walikutwa na dawa hizo za kulevya
Hakimu alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Washtakiwa kwa nyakati tofauti walidai kwamba wamekaa mahabusu ya polisi zaidi ya siku 14 na kwamba wamepigwa sana makofi kiasi hawana uwezo wa kusikia vizuri.

Hakimu Mwaikambo amesema kwa sababu wanakwenda mahabusu magereza wana utaratibu wao wa kuwapa matibabu.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu alisema kesi hiyo itatajwa Oktoba 10,mwaka huu na washtakiwa wapelekwe mahabusu.

Makala – Shiriki Bongo Star Search 2019 Uwe STAR.

0
0

Bongo Star Search ni kipindi cha kusaka vipaji kupitia Televisheni.Kipindi hiki kimelenga kumtafuta Muimbaji mahiri kupitia usaili utakaofanyika mikoa mitano hapa Tanzania. Watazamaji pia watashiriki kwenye mashindano na kumchagua mshindi kwa kupiga kura mtandaoni.

BSS 2019 inatoa fursa msimu huu wa 10 ya kutafuta vipaji mahiri vya vijana machachari wa Kitanzania. BSS 2019 inaletwa kwenu na StarTimes na itarushwa kwenye Chaneli ya StarTimes Swahili na APP ya StarTimes ON.

Bongo Star Search Inawakaribisha wale wote wenye Vipaji kushiriki Usaili kwenye Mikoa husika na kwenye Mtandao kupitia App ya StarTimes ON.

Usahili utaanza Tarehe 28 Sept katika Mikoa 5:
28 & 29 September – Arusha at the Fuzz-Pointzone Resort (Mianzini)

4 & 5 Oct – Mwanza at [Rock City Mall

10 & 11 October – Mbeya at [Mbeya City Pub & Lounge]

17 & 18 October - Dodoma [Royal Village Hotel]

23, 24 & 25 - Dar es Salaam at [National Museum]

Kutakua na Majaji Mahiri wanne watakaotoa kura za NDIO au HAPANA kwa washiriki baada ya kuangalia umahiri wao katika kuimba.Ukipata Kura Tatu za NDIO moja kwa moja utakua umeshinda kuingia mchuano wa pili,Ukipata kura Mbili za NDIYO”…..

Usaili wa Mtandaoni utafanyika kuanzia tarehe 8 mpaka 30 Oktoba.Kwa kushiriki unaweza ukajaza form kupitia Application ya StarTimes ON kisha weka Link kwenye YouTube,au Jirekodi kisha post Instagram na kuweka hashtag #bssonline audition2019 na @startimestz..Tuma walau wimbo uliokamilika na urekodi mwingine bila kuhariri(edit) na kurudiarudia. Muimbaji aonekane kabisa akiwa anajirekodi,na pia inatakiwa muimbaji aonyeshe hisia akiwa anaimba na kucheza.

Mchujo utafanyika ndani ya masaa 48 na majibu yatatangazwa katika kurasa za Bongo Star Search na StarTimes.Mwisho wa upigaji kura washindi wa 30 wa mwanzo wataingia kwenye Mchuano.

Usaili wa Bongo Star Search utarushwa hewani kuanzia tarehe 13 Oktoba kila Jumapili saa Mbili kamili kupitia Chaneli ya ST Swahili.Usiache kushiriki kwani nani ajuaye! Star wa kesho anaweza kua ni wewe.

WIKI YA ELIMU YA WATU WAZIMA YAFANA BUKOBA MANISPAA.

0
0
Anaandika Abdullatif  Yunus - Michuzi TV.
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera imeadhimisha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima yenye kauli mbiu isemayo "Elimu haina Mwisho' wakati ambapo jamii asilimia kubwa bado wana fikra potofu juu ya dhana ya Elimu hii, Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Rwamishenye Bukoba Manispaa Mkoani Kagera Septemba 27 Mwaka huu.

Akizungumza Mara baada ya Kuhitimisha sherehe za Maadhimisho hayo Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala amekiri kuwepo Kwa upotoshaji Wa dhana nzima ya Elimu ya watu wazima, wakidhani kuwa Elimu hii uhusisha wazee tu au watu wenye umri zaidi ya miaka 18, jambo ambalo sio sahihi kwani Elimu hii Kwa sasa inamgusa MTU yeyote aliyekosa Elimu na stadi za maisha kubwa ikiwa ni kujua kusoma, kuhesabu  na kuandika maarufu kama "K" tatu, Kwa utaratibu MEMKWA na MESKWA, na kuwataka wote wenye kupotosha kuacha Mara moja.
 
Kadole amesema  takwimu zinaonesha kuwa Sensa iliyofanyika  mwaka 2012 zinaonesha kuwa asilimia 22℅ ya   Watanzania  hawajui kusoma na kuandika, hivyo Serikali tayari imeanza utaratibu Wa kuwezesha programu hii kupitia mpango wa Elimu bila malipo na Kwa mara ya kwanza mwaka huu Manispaa ya Bukoba wametenga Milioni Nne kuongeza ufanisi wa Elimu hii.

Awali Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Bukoba Mwl. Frolence Kibani amefafanua kuwa Ndani ya Wiki ya maadhimisho wameweza kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kuwapatia Elimu wale walioikosa Elimu, wakiwemo watoto na watu wazima, sambamba na hilo Mwl. Kibani ameiomba jamii kuchangamkia vituo vinavyotoa Elimu ya watu wazima na ufundi stadi ambapo vituo hivi ni Zam zam, Nshambya Kibeta huku akisisitiza kuwa Elimu hii ni bila malipo.

Sherehe za kikomo cha wiki ya Elimu ya Watu wazima, iliyoanza 23 Septemba 2019, hizo zimepambwa na burudani mbalimbali ikiwemo nyimbo na maigizo, zikitanguliwa na maandamano yaliyoongozwa na kikundi cha ngoma kutoka shule za Adolph, huku sherehe hizo zikihudhuriwa na wadau wa Elimu, viongozi wa Taasisi mbalimbali wakiwemo wadau NMB, wanafunzi pamoja na wazazi.
 Katibu Tawala Manispaa ya Bukoba Bi. Kadole Kilugala wakati akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.
 Afisa Elimu ya Watu wazima Bukoba Manispaa Mwl. Frolence Kibani akisoma Risala iliyoandaliwa kwa Mgeni Rasmi, Katibu Tawala kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya Bukoba, pembeni ni Msherehedhaji Mwl. Joyce Robozi.
 Katibu Tawala Manispaa ya Bukoba Bi. Kadole Kilugala wakati akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima.
 Baadhi ya Wadau wa Elimu wakiwemo watumishi Idara ya Elimu pamoja na wazazi wakiendelea kufuatilia sherehe za maadhimisho ya kilele cha wiki ya Elimu ya watu wazima.
Kati ya burudani iliyochota hisia za waliohudhuria, kutoka kwa wanafunzi wanaolelewa na Kituo cha Tumaini Education Center, ambapo hawa ni miongoni mwa watoto waliokuwa wakiishi mazingira hatarishi.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images