Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUBADILISHA KILIMO CHA KUJIKIMU KWENYE KAHAWA KUWA KILIMO CHA BIASHARA-MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la mfano la kahawa wakati alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisaini kitabu cha wageni tarehe 26 Septemba 2019 mara baada ya kutembelea Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe, Mwingine pichani ni Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma (Kulia).
Meneja wa kituo cha utafiti wa Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi akimuelezea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kuhusu kilimo bora cha kahawa wakati akikagua shamba la mfano la kahawa alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele.

Miongoni mwa mazao hayo ya kipaumbele ni kahawa ambapo katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Kahawa imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000. Aidha bodi imepanga kuzalisha na kusambaza miche milioni 10 ya kahawa katika wilaya 42.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 26 Septemba 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) alipotembelea taasisi hiyo Mkoani Songwe.

Alisema kuwa zao hilo lina mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa na kwa maendeleo ya jamii lakini katika miaka ya karibuni lilionekana kuzorota kutokana na kuwapo kwa changamoto mbalimbali. 

Kutokana na hali hiyo Serikali imeendelea kubuni mikakati mipya ya taratibu za usimamizi wa sekta hiyo ili kuleta ufanisi katika uzalishaji wa zao hilo.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuongeza uzalishaji wenye tija katika zao la kahawa serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa miche bora kwa ajili ya kuzisambaza kwa wakulima nchini.Pia ameipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbegu bora za kahawa huku akisisitiza taasisi hiyo kuongeza weledi katika utoaji elimu kwa wakulima.

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma ameiomba wizara ya Kilimo kwa ushrikiano na wataalamu mbalimbali wa TaCRI kuongeza juhudi ili kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa.

Pia amesema kuwa uwezo wa Taasisi hiyo katika kuzalisha mbegu bora bado ni mdogo hivyo ameiomba serikali kuongeza uwezekano ili kuzalisha mbegu nyingi ambazo zitawafikia wakulima wengi.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha utafiti wa Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi ameeleza kuwa jukumu kuu la TaCRI ni kurudisha matumaini ya tasnia ya kahawa kwa kutoa na kusambaza teknolojia za kuendeleza zao la kahawa kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji na ubora.

Nyingine ni kupunguza gharama za uzalishaji, kuboresha kipato na riziki kwa wakulima wote wa kahawa na kuongeza mchango wa sekta ya kahawa kwenye pato la Taifa.

WASANII GNAKO, MBOSSO NA MARIOO WAZIDI KUPENYA SOKO LA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI KUPITIA JAMAFEST

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya GNAKO wa kundi la Weusi akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
   Msanii Mbosso akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
 Msanii Marioo akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Dj Ommy Crazy nae hakuwa nyuma kuwapagawisha wanajumuiya wa Afrika Mashariki waliofika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.

Balozi wa Italia nchini Roberto Mengoni atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimwelezea Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni namna wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo ilivyoongeza ufanisi wa matibabu kwa watoto wakati wa ziara iliyofanywa na balozi huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka JKCI na wenzao wa Shirika la Mending Kids International.
Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni akizungumza na mama Khayraty Suleiman ambaye mtoto wake anasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa ziara iliyofanywa na balozi huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Mending Kids International.
Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akimwelezea Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni maendeleo ya hali za wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wakati wa ziara fupi iliyofanywa na balozi huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Mending Kids International.

Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akimwelezea Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni maendeleo ya hali za wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wakati wa ziara fupi iliyofanywa na balozi huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Mending Kids International. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji Dkt. Angela Muhozya.


Timu ya wataalamu wa afya kutoka nchini Italia na Marekani wa Shirika la Mending Kids International lenye wataalamu wa afya kutoka nchini Italia na Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni wakati wa ziara fupi iliyofanywa na balozi huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Mending Kids International.


Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa shirika la Mending Kids International mara baada ya kumalizika kwa huyo ya kutembelea kambi maalum inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Mending Kids International mara baada ya kumalizika kwa ziara yake fupi ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na JKCI.

SHILATU AAGIZA “FEDHA ZA NIDA” ZIRUDISHWE NDANI YA SAA 24

$
0
0
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Chikongo kilichopo kata ya Mkoreha kwenye mkutano wake wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi

…………………….
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameagiza Wananchi kurudishiwa fedha zao walizolazimishwa kutoa ili wapatiwe huduma za kupewa fomu, kugongewa muhuri na kusaidiwa kujaza fomu za kuomba kitambulisho cha Taifa.

Hayo yamejitokeza kwenye mkutano na Wanakijiji wa kijiji cha Chikongo kilichopo kata ya Mkoreha ambapo Wanakijiji hao walilalamika mbele ya Gavana Shilatu kutozwa fedha hizo kinyume na utaratibu na ambao waliokataa kutoa hawakupatiwa fomu ama huduma yeyote ile.

“Hakuna utaratibu wa fomu ya kuomba kitambulisho cha Taifa kulipiwa; ama kulipia kugongewa muhuri; au kuomba msaada wa kusaidiwa kujaza fomu mpaka utoe fedha Shilingi elfu moja, hakuna bali Mwananchi anatakiwa ahudumiwe bure. Naagiza ndani ya saa 24 Wananchi wote waliochukuliwa fedha zao kurudishiwa mara moja fedha zao, Mtendaji Kata na Mtendaji Kijiji simamieni utekelezaji wa agizo langu. Serikali inatoa huduma ya kuwapatia vitambulisho vya Taifa Wananchi bure kabisa na huduma iendelee kutolewa bure na pasisikike tena malalamiko ya Wananchi kutozwa fedha.” Alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo walijitokeza Watu 18 na wengineo zaidi ambao hawakufika mkutanoni wakitajwa kuchukuliwa Shilingi elfu moja moja zao ili wapatiwe huduma, Gavana Shilatu ameagiza wote waliotozwa elfu moja warejeshewe fedha zao.

Wakizungumzia uamuzi wa Gavana Shilatu wamefurahishwa kuona fedha zao zinarudi na huduma kuagizwa itolewe bure kabisa.

“Sie tunajua huduma inatolewa bure na tulikuwa tunashangaa kuona tunatozwa fedha. Tunamshukuru Afisa Tarafa Mihambwe kuingilia Kati Mara moja tulivyomfikishia kero yetu hii. Tunafurahi kuona Viongozi wetu wanaposimama nasi Wananchi” alisema Mwanakijiji Ndevu.

Wakati huo huo Gavana Shilatu ametumia mkutano huo wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru 2019 utakao kuwa wilayani Oktoba 4; Pia Kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura Novemba 24, 2019.

Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mtendaji Kata Mkoreha, Mtendaji Kijiji Chikongo, Mwenyekiti Kijiji Chikongo pamoja na Wajumbe Halmashauri ya Kijiji Chikongo na Wananchi.

Wateja wa Tigo jijini Mwanza kufikiwa na huduma kwa urahisi baada ya ufunguzi wa duka jipya

$
0
0



Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika, akikata utepe kuzindua duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza, kushoto ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati wakishuhudia.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthman Madati akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza,

Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika, akitoa hotuba wakati wa kuzindua duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza
wageni waalikwa wakifuatilia hotuba kwa makini uzinduzi wa duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza
Muonekano wa Duka jipya la Tigo Mwenye Jengo la Rock City Jijini Mwanza

Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika(wa pili kulia) na Msimamizi wa duka la Tigo Rock city Neema Mossama, wakikata keki wakati wa uzinduzi duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza, kushoto ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati(wa kwanza kulia) wakishuhudia.

Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika(kulia) akizungumza na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo(kushoto) Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati, baada ya kuzindua duka la Tigo kwenye jengo la Rock city.
Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika, akiangalia simu kwenye duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza baada ya kulizindua.



Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidijitali Tanzania,Tigo, leo imefungua duka jipya jijini Mwanza.Duka hilo litawafanya wateja wa kampuni hiyo kupata huduma zote kwa urahisi zaidi ndani ya eneo moja la Rock City Mall.

Duka hilo litatoa huduma zote muhimu kuanzia usajili wa namba za simu kwa alama za vidole, huduma za kifedha ‘Tigo Pesa’ na mauzo ya data na vifaa vya mawasiliano kama simu janja, router na modem kwaajili ya huduma yetu tuliyo zindua hivi majuzi iitwayo ‘Tigo Home internet’.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati amesema hatua ya kufungua duka hilo ni moja ya mkakati wa Tigo wa uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinawafikia wateja kwa wakati nchi nzima.

“Duka hili jipya litampa mteja wetu wasaa wa kutazama na kujaribu bidhaa mbalimbali kabla ya kuamua kufanya manunuzi.Hatua hii imekuja kufuatia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wateja wetu waliokuwa wakihitaji uwepo wa duka letu kwenye jengo hili maarufu kibiashara hivyo tumekidhi mahitaji yao,”alisema Madati.

Awali akizindua duka hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mkoani Mwanza, Dkt.Severine Lalika alipongeza juhudi za Tigo katika kuwekeza rasilimali katika uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.

“Huduma bora kwa wateja ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji katika utoaji wa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,” alisema Lalika.

Kadhalika,duka hilo linakuwa la nne kufunguliwa mkoani humo huku likiwa na huduma mpya ikiwamo simu zinazotamba kwa sasa aina ya S3 na R7 pamoja na vifaa vya huduma za intaneti kwa makampuni maarufu kama ‘Tigo business’.

Maduka mengine matatu ambayo yanatoa huduma mkoani hapa ni pamoja na Mwanza kiosk-barabara ya Nyerere, Ukerewe shop-Wilaya ya Ukerewe, Sengerema shop-Wilayani Sengerema na Airport kiosk- Uwanja wa ndege wa Mwanza.

DKT. AKWILAPO AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KIJIOGRAFIA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akizungumza na wadau wa kongamano la Kimataifa la kujadili masuala ya kijiografia(GAT)
Mtoa mada kutoka nchini Afrika Kusini akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya tabianchi na namna ya jamii unavyoweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila.


KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amefungua Kongamano la kimataifa la kijiografia, linalojulikana kama (GAT) ambao linalenga kujadili mabadiliko ya tabia nchi na namna jamii inavyoweza kukabiliana na changamoto hizo.

Akifungua mkutano huo unaofanyijka katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) jijini Dar es Salaam, Dkt. Akwilapo amesema jiografia ndiyo maisha kwa kuwa inaangalia, Kilimo, Afya, Ajira, na maisha ya kila siku.

“Elimu ndiyo mkombozi wa maisha, jiografia ni afya, Kilimo na maisha ya kila siku hivyo Jamii inavyopambana na mazingira ndivyo inavyochangia katika Kukuza uchumi wa nchi husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ameeleza kuwa pamoja na majukumu mengine ya Chuo, Chuo pia kinawajibika kufanya tafiti hivyo kupitia Kongamano la GAT wadau wanapata fursa ya pamoja ya kujadili, kuoneshana namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitikeza katika Jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto ktk sekta zote, hivyo hili ni eneo ambalo wataalamu wanatoa ushauri wanamna ya kukabiliana nalo kupitia mkutano wa namna hii wa GAT” alisema Prof. Mwakalila.

Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo ambaye ni Mhadhiri MwandamiZi wa Chuo Kikuu Nkwawa Dkt. Evaristoo Haule amesema GAT imejikita kufanya kazi na watafiti, na wanataaluma katika masuala ya Jiografia ikiwemo watunzaji wa wanyama, utunzaji wa Maliasili, uchumi wa viwanda na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kongamano hilo la siku tatu ambalo limeanza leo linashirikisha wadau kutoka nchi zaidi ya tano ikiwemo Afrika Kusini, Ethiopia, Nigeria, Zambia na wenyeji Tanzania.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano,
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE.

VIONGOZI WAELEZA HATUA AMBAZO ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI, TIC KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI

$
0
0


Na Ripoti Wetu, Michuzi TV

KATIKA kutambua umuhimu wa biashara na uwekezaji nchini, viongozi wa ngazi mbalimbali wamezungumza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha huduma kwa wawekezaji na umuhimu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika kufanikishwa uwekezaji wa wawekezaji watarajiwa nchini

Viongozi hao wamezungumza hayo hivi karibuni waliposhiriki mkutano wa kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki amesema kwa sasa wanafanya maboresho katika sera na sheria ya uwekezaji ili kuwa na mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya sheria ya uwekezaji yanalenga kuvutia uwekezaji zaidi na itasaidia kupunguza kiwango kinachotakiwa ili kujisajili na TIC.Pia itasaidia au kuwezesha wawekezaji wa kada ya chini na kati pia kusajiliwa na TIC.

" Usajili utawasaidia kunufaika na faida zinazotokana na kujisajili ikiwamo vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi,"amesema Waziri Kairuki na kuongeza wanategemea mapendekezo hayo yawasilishwe Bungeni Novemba, mwaka 2019.

Aidha Kairuki ameshukuru juu ya matamko mabaya ya viongozi na vitisho kwa wawekezaji na wafanyabiashara kwamba kwa sasa yamepungua na wanaomba viongozi wenye tabia hiyo waache mara moja. Pia amesema Serikali ipo kwa ajili ya kuhudumia na kufanikisha malengo ya wafanyabiashara na wawekezaji maana ndio wanatoa fedha ya maendeleo ya nchi.

"Niwapongeze Mkoa wa Ruvuma, sijawahi kusikia wala sijapokea taarifa yakuwepo kwa matamko wala vitisho dhidi ya wawekezaji bali mmekuwa wakaribishaji na wasaidizi wa wawekezaji,"amesema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla amesema wawekezaji wote wanaohitaji ardhi lazima wapite TIC hasa wawekezaji wa kigeni.

Amesema lengo ni kutengenezewa hati pacha ya umiliki yaani 'Deriverrive Right' itakayompa uwezo wa kuimiliki. Ametoa mwito kwa kwa halmashauri zote kuhimiza wawekezaji wote hasa wa kigeni wanaohitaji ardhi ya uwekezaji kupitia TIC.

"Mnapopata ardhi kwa ajili ya uwekezaji msimpe mwekezaji moja kwa moja bali fuateni taratibu na sheria za kupitia TIC ili kujiepusha na migogoro inayoweza kujitokeza pasipo na sababu.Hili lizingatiwe,"amesema.

Hata hivyo amesema Novemba 19 mwaka huu Wizara itafungua ofisi kila mkoa ili kurahisisha upatiknaji wa ardhi ikiwamo ya uwekezaji, upimaji na upatikanaji wa hati ngazi ya kila mkoa. Amesema hiyo itapunguza usumbufu kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufuatilia hati mikoa jirani (Kanda) au Dar es Salaam.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha Dk.Ashatu Kijaji amesema hakuna nchi inayoendelea bila wafanyabiashara na wawekezaji. Na ili nchi iendelee tunahitaji kodi kwa maendeleo na kodi inatokana na wafanyabiashara na wawekezaji hivyo tushirikiane nao vizuri.

"Katika kuboresha na kuweka mazingira mazuri mwa wafanyabiashara na mwekezaji inashauriwa wapewe miezi sita(6) kabla ya kuanza kulipa kodi pale wanapoanza utekelezaji wa miradi yao,"amesema.

Ameongeza kuwa hiyo itawapa muda wa kujifunza, kujitathmini na kujipanga kwa ajili ya kulipa kodi na kuongeza malipo yafanyike kupitia mashine za EFD zinazotolewa na TRA na sio vinginevyo.

Pia amesisitiza kodi kulipwa kwa utaratibu wa sheria husika na si vinginevyo, hivyo maofisa wazingatie hilo na wafuate sheria wanapokusanya kodi.

Kwa upande wa Wizara ya Mazingira imeeleza kuna uhusiano mkubwa kati ya uwekezaji na mazingira na kwamba uwekezaji wowote unaofanyika lazima uwe endelevu kwa maana ya uzingatie sheria za kutunza uhifadhi mazingira kwa matumizi ya leo na hata vizazi vinavyokuja.

Wizara hiyo imetoa mwito kwa wawekezaji wote kuwasiliana na NEMC ili kupata miongozo ya mazingira wanapotarajia kutekeleza miradi yao nchini. Aidha NEMC pia inafanya maboresho ili kumwezesha mwekezaji kupata kibali cha kuendelelea na mradi wake. 

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika Mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina  Mabula akifafanua jambo kuhusu uombaji wa ardhi kwa wanaohitaji ardhi kwa ajili ya uwekezaji
 Naibu Waziri wa Fedha Dk.Ashatu Kijaji akizungumza katika mkutano huo ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa kukufanya kodi kwa mujibu wa sheria
 

TAHADHARI YA UTAPELI


NGOMA YA KINYARWANDA YAWA GUMZO KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wachezaji ngoma wa Kinyarwanda wamesimamisha kwa muda shughuli nyingine zilizokuwa zikiendelea kwenye maonyesho ya Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST) jijini Dar es Salaam nchini Tanzania baada ya kupanda jukwaani. 

 Watazamaji mbalimbali kwenye maonyesho wameacha shughuli zao kwa muda na kusogea kushuhudia ngoma hiyo iliyoshirikisha wanaume na wanawake. Wadada wa Kinyarwanda walikuwa kivutio zaidi huku baadhi ya watazamaji wakiwashangilia na wengine wakionyesha kuwakubali kwa kuchukua video kwa simu na wengine wakijadiliana kuhusu urembo wa wanawake wa Kinyarwanda.

 “Huwa nashangaa hawa kina dada kutoka nchini Rwanda ni warembo jamani “Halafu hawatumii mavitu vitu lakini kama wananyumbulika.” “Nikiwaona kwenye picha huwa nahisi wamejiumba wenyewe jinsi wanavyovutia kama wamezaliwa na mama mmoja..” walisikia vijana wawili waliokuwa wakizungumza uwanja hapo wakati ngoma hiyo ikiendelea kutumbuiza Walisikika baadhi ya watu uwanjani hapo kila mmoja akisema lake kuhusu urembo wa wanawake hao ambao umekuwa gumzo.

SERIKALI KUBADILISHA KILIMO CHA KUJIKIMU KWENYE KAHAWA KUWA KILIMO CHA BIASHARA-HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la mfano la kahawa wakati alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisaini kitabu cha wageni tarehe 26 Septemba 2019 mara baada ya kutembelea Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe, Mwingine pichani ni Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma (Kulia).
Meneja wa kituo cha utafiti wa Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi akimuelezea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kuhusu kilimo bora cha kahawa wakati akikagua shamba la mfano la kahawa alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele.

Miongoni mwa mazao hayo ya kipaumbele ni kahawa ambapo katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Kahawa imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000. Aidha bodi imepanga kuzalisha na kusambaza miche milioni 10 ya kahawa katika wilaya 42.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 26 Septemba 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) alipotembelea taasisi hiyo Mkoani Songwe.

Alisema kuwa zao hilo lina mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa na kwa maendeleo ya jamii lakini katika miaka ya karibuni lilionekana kuzorota kutokana na kuwapo kwa changamoto mbalimbali. 

Kutokana na hali hiyo Serikali imeendelea kubuni mikakati mipya ya taratibu za usimamizi wa sekta hiyo ili kuleta ufanisi katika uzalishaji wa zao hilo.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuongeza uzalishaji wenye tija katika zao la kahawa serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa miche bora kwa ajili ya kuzisambaza kwa wakulima nchini.

Pia ameipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbegu bora za kahawa huku akisisitiza taasisi hiyo kuongeza weledi katika utoaji elimu kwa wakulima.

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma ameiomba wizara ya Kilimo kwa ushrikiano na wataalamu mbalimbali wa TaCRI kuongeza juhudi ili kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa.

Pia amesema kuwa uwezo wa Taasisi hiyo katika kuzalisha mbegu bora bado ni mdogo hivyo ameiomba serikali kuongeza uwezekano ili kuzalisha mbegu nyingi ambazo zitawafikia wakulima wengi.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha utafiti wa Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi ameeleza kuwa jukumu kuu la TaCRI ni kurudisha matumaini ya tasnia ya kahawa kwa kutoa na kusambaza teknolojia za kuendeleza zao la kahawa kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji na ubora.

Nyingine ni kupunguza gharama za uzalishaji, kuboresha kipato na riziki kwa wakulima wote wa kahawa na kuongeza mchango wa sekta ya kahawa kwenye pato la Taifa.

WATAFITI WA DAWA ZA BINADAMU WAMEHIMIZWA KUFANYA TAFITI AMBAZO ZITAMLINDA MTUMIAJI-DKT.PAUL KAZYOBA

$
0
0
WATAFITI wa dawa za binadamu wamehimizwa kufanya tafiti ambazo zitasaidia uzalishaji wa dawa ambazo zitamlinda mtumiaji na kuepusha athari zinazoweza kujitokeza baada ya matumizi.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Kuratibu na kukuza utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Paul Kazyoba katika mkutano wa mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Dkt.Kazyoba amewataka Wananchi kujijengea utaratibu wa kuuliza kama tafiti za afya zimepitia utaratibu hivyo taasisi ndogondogo zinazofanya utafiti wa afya zijijengee uwezo wa kuweza kutathimini maadili ya tafiti zenyewe.



Lengo kubwa la kuwa na Smert project ni kuhakikisha Mwananchi analindwa katika usalama wake kwenye matumizi ya dawa.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha NIMR_Mbeya, Mtafiti Mkuu wa Mradi wa Smert (Tanzania_Uk) Dkt.Nyanda Ntinginya amesema kuwa mradi huo ulianzishwa kwa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa kamati za naadili za taasisi pamoja na utendaji kasi wa kamati za kikanda za utafiti.



“Kabla ya mradi huu hatujafanya kulikuwa na changamoto ya muda mrefu kutumiwa kabla ya mradi kuruhusiwa kwenda kufanyiwa utafiti”.Amesema Dkt.Ntinginya,
Mkurugenzi wa Kuratibu na kukuza utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Paul Kazyoba (kulia) akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za (TMDA) leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurungenzi wa Dawa na vifaa tiba wa Mamlaka wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Akida Khea (kulia) akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa  mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za (TMDA) leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akizungumza wakati alipokuwa akitambulisha sehemu ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika ufunguzi wa mkutano wa  mwaka wa pili wa Smert project uliofanyika katika ofisi za TMDA leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Mkurungenzi wa Dawa na Wifaa tiba wa Mamlaka wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Akida Khea (kulia).
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

UANDISHI VITABU KUWA KIGEZO WAKUFUNZI KUPANDA VYEO MLALE

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu pichani katikati akiongea na wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale kilichopo kata ya Magagula Wilaya Songea Mkoani Ruvuma mapema jana mara baada ya kutembelea miradi inayoendelea chuoni hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Bi. Luciana Mvula kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mabweni ya wanafunzi alipotembelea Chuo hicho jana Mkoani Ruvuma

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ameagiza uongozi na wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale kilichopo Kata ya Magugula Wilaya Songea Mkoani Ruvuma kuanza kutumia kutumia vitabu kwa njia ya mtandao ili kuweza kutoa taaluma inayoendana na wakati.

Dkt. Jingu amesema hayo wakati wa ziara yake Chuoni hapo kwa lengo la kujiona maendeleo ya Chuo hicho lakini pia kusikiliza wafanyakazi ili kuangalia namna bora ya utendaji kazi kati ya Wizara yake na Chuo hicho ambayo inasimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii.

Dkt. Jingu pamoja na kuwataka wakufunzi hao kutumia elimu ya mtandao kuboresha taaluma zao lakini pia amewataka wakufunzi hao kuanza kutumia Maktaba ya Kimtandao ili waweze kupata vitabu mbalimbali vilivyoandikwa kuhusiana na taaluma ya Maendeleo ya Jamii.

Dkt. Jingu pia amewataka wakufunzi Chuoni hapo kuanza kuandika vitabu ili kuweza kutoa taaluma inayoendana na wakati akionya kuwa inabidi upandaji vyeo wa wakufunzi ubadilishwe ili uandishi wa vitabu uwe moja ya kigezo muhimu cha kupandisha vyeo kwa wakufunzi wanaofundisha taaluma ya Maendeleo ya Jamii.

‘’Mnaona mnatoa welimu sahihi kumbe mnatumia elimu ya miaka 47 iliyopita hivyo nawataka muandike vitabu kwa lengo la kutoa elimu inayoendana na wakati ingawa najua kuwa pamoja na uandishi wa vitabu hivyo haviwezi kutosha ila kwasasa mnaweza kutumia Maktaba ya Mtandao itakayowaezesha kupata vitabu kutoka vyanzo mbalimbali mtandaoni.’’ Alisisitiza Dkt. Jingu

Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Bi. Luciana Mvula amezitaja changamoto zinazokabili chuo hicho kuwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa chuoni hapo lakini pia upungufu wa vitendea kazi kama compyuta na gari kwa ajili ya huduma za dharula kama vile ugonjwa kwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.

Bi .Mvula pia imeitaja changamoto ya upungufu vitabu katika Maktaba ya Chuo hicho na kumuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya kuangalia namna bora ya kuwezesha chuo kuboresha Maktaba hiyo lakini pia kukarabati majengo ya zamani ya chuo hicho ambayo imeanza kuchakaa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu anaendelea na Ziara ya Siku Tano katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutembelea vyuo vya Maendeleo ya Jamii na pia Makazi ya Wazee yaliyoko katika Mikoa hiyo.

FEDHA ZA NDANI ZIJENGE MIRADI YA KIMKAKATI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Mji wa Mafinga wahakikishe wanajenga mradi wa kimkakati kwa kutumia fedha za mapato ya ndani na si kusubiri miradi kutoka Serikali Kuu wakati wanakusanya zaidi ya sh. bilioni saba kwa mwaka.

Amesema halmashauri hizo licha ya kukusanya fedha nyingi kwa mwaka lakini matumizi yake si mazuri kwa sababu hawana mradi wowote wa kimkakati wanaoutekeleza, mfano ujenzi wa maeneo ya kuegeshea magari makubwa au hata ujenzi wa kituo cha mabasi, miradi ambayo ingewaongezea mapato.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Septemba 26, 2019) wakati akihutubia na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Wambi wilayani Mufindi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.”Nataka kuona mradi wa kimkakati ukitekelezwa kwa fedha mnazokusanya kutoka kwa wananchi.”

Alisema viongozi hao wanaweza kutenga kiasi cha sh. bilioni moja kwa mwaka na kujenga hospitali au wakatenga fedha na kujenga barabara za lami kwa awamu katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa kuwa ujenzi wa barabara za lami mijini ni sh. milioni 300 kwa kilomita moja, hivyo wangeweza kutekeleza ujenzi huyo kutokana na fedha wanazokusanya.

“Msitegemee fedha kutoka Serikali Kuu tu jengeni wenyewe barabara zenu kuzunguka Mji wa Mafinga kwa kiwango cha lami kwa sababu mna fedha za kutosha tena mnaweza kutumia fedha za mapato ya ndani mnazokusanya kutoka kwa wananchi badala ya kuzitumia kwa kulipana posho tu.” 

Awali,Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya kata ya Mdabulo na kupokea taarifa fupi ya ujenzi wa bwalo, bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike pamoja na ujenzi wa madarasa na kisha alizungumza na wananchi na kuwaeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao.

Waziri Mkuu alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na maeneo yao ya makazi, Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya afya katika kila kata pamoja na ujenzi wa hospitali za wilaya ikiwemo na wilaya yao ya Mufindi ambayo ipo katika hatua mwisho kukamilika.

Kwa upande wao, wabunge wa mkoa wa Iringa wakiwemo wa majimbo na wa viti Maalumu kwa nyakati tofauti waliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye mkoa wao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, SEPTEMBA 27, 2019.

SIKU YA HEAMEDA YAWAALIKA KUUNGANA NAO

Wakaguzi wa ndani wapunguza ubadhilifu nchini

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha
WAKAGUZI hapa nchini wameeleza mafanikio ya kupungua kwa ubadhilifu wa Mali za umma kwa kiwango kikubwa katika sekta mbalimbali za serikali na binafsi baada ya serikali kuridhia ukaguzi wa aina moja.

Wameeleza hayo jijini Arusha kwenye mkutano wa sita  wa wakaguzi wakuu wa hesabu za ndani, ulioandaliwa na taaisisi ya ukaguzi wa ndani (IIA)wakidai kuwa mafanikio ni baada ya serikali kupitia bodi ya wahasibu NBAA kuridhia viwango vya kimataifà vya ukaguzi wa ndani mwaka 2011.

Mkaguzi wa ndani na Mkuu wa serikali msaidizi upande wa ubora wa Ukaguzi wa ndani AIAG(QA),Chotto Sendo amesema kuwa  mafanikio hayo yametokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika ikiwemo wakaguzi wa ndani kutumia ufumo mmoja wa ukaguzi.

Amesema mabadiliko yaliyofanyika yamewezesha wakaguzi wa ndani kuimarika zaidi katika kuibua ubadhilifu unaoendelea na hivyo kupunguza mianya ya hiyo katika taasisi mbalimbali.

"Changamoto kubwa kwa sasa tupo katika hatua ya kuelekea kwenye viwanda lakini tulikuwa hatujajiandaa kulingana na viashiria hatarishi vilivyokuwepo ndio maana tunaendesha haya mafunzo kukabikiana na vihatarishi" Alisema.

Naye Mkurugenzi katika taasisi ya ukaguzi wa ndani,(IIA),Zelia Njeza amesema kuwa wamejikita kutoa elimu kwa wadau na kujielimisha kupitia mafunzo mbalimbali kuhakikisha kwamba wanatoa huduma inayotakiwa kwa maendeleo chanya.

Amesema kuwa kumekuwepo namwamko mkubwa kwa wakaguzi wa ndani katika kusimamia kazi yao na kuongeza usimamizi katika udhibiti wa viashiria hatarishi ,utawala bora na mifumo ya udhibiti.

Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa ndani wa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar, Safia Abdulhamid amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wakaguzi wa ndani ni kushindwa  kutekelezwa kwa mapendekezo yao baada ya kukamikisha ukaguzi.

Pia amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakiogopeka na kutazamwa  kama Askari Polisi jambo ambalo linawafanya kupata ugumu katika kutekeleza majukumu yao.

TBS Yashiriki Mikutano ya Mashauriano, yatoa Elimu

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji (hawapo pichani). Lengo la mikutano hiyo iliyofanyika mikoa ya kusini ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kuanzia Septemba 24 hadi jana Septemba 26, mwaka huu ilikuwa ni kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kutatua changamoto hizo. Miongoni mwa waliotoa mada ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Yusuf Ngenya. Na na Chalila Chbuda


Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kuhusu fursa wanazopata wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi viwango, kuhamasisha wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure pamoja na kuzipatia majibu changamoto wanazokumbana wadau wake mbalimbali.

Shirika hilo limetoa elimu hiyo wakati wa mikutano ya mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili kwenye mikoa ya Kusini ambayo ni Ruvuma, Mtwara na Lindi kuanzia Septemba 24, mwaka huu. Mikutano hiyo ilimalizika jana mkoani Lindi.

Ufunguzi wa mkutano Songea, ulifanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Ndeme na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Sima, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Anjellah Kairuki na wakuu wa wilaya zote.

Akitoa mada kwa nyakati tofauti kwenye mikutano hiyo, Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, aliwaeleza washiriki hao kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo yameleta mabadiliko katika Sheria ya Viwango Na: 2 ya mwaka 2009.

Kufuatia mabadiliko hayo, Dkt. Ngenya alisema shirika hilo kwa sasa inatekeleza baadhi ya majukumu ambayo awali yalikuwa chini ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo kwa sasa inajulikana kama TMDA.

Alisema kufuatia mabadiliko hayo majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi yanafanywa na TBS. 

Akieleza fursa zinazotolewa na shirika hilo kwa wajasiriamali nchini, Dkt. Ngenya, alisema ni pamoja kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha bila malipo kwa miaka mitatu lengo likiwa ni kuwawezesha kupanua soko la bidhaa zao na kuwaondolea vikwazo vya kibiashara. 

Alisema Serikali imeanzisha utaratibu huo ili kuwasaidia
wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Alitoa wito kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla 
kuichangamkia fursa hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inasisitiza uchumi wa viwanda.

“TBS kama taasisi wezeshi inatoa huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa bure kwa wajasiriamali wadogo na wakati, lengo likiwa ni kuendeleza viwanda vya Tanzania, hivyo ni vyema wakathibitisha ubora wa bidhaa zao ili wasipate vikwazo vyovyote katika kupata soko ndani na nje ya nchi,” alisema Dkt. Ngenya.

Alisema kuwa endapo wajasiriamali hao watathibitisha bidhaa zao
itawasaidia kuzalisha bidhaa endelevu ambazo zitakuwa na soko kila
mahali ikiwemo masoko ya kikanda.

Dkt. Ngenya, alifafanua kuwa lengo la TBS ni kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zenye tija kwa taifa, bila kuathiri taratibu na sheria za nchi. Kutokana na umuhimu huo, alisema ndiyo maana shirika hilo limeshiriki mikutano hiyo kama taasisi wezeshi.

TAFADHALI USISOME UJINGA HUU, HAUNA MAANA YOYOTE KWAKO WALA KWA KWAKE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Tv
KUNA siku huwa najikuta nawaza ujinga tu, tena ujinga ambao hauna maana yoyote ile kwa yoyote.

Ndio! Sijui akili yangu ikoje? Nashindwa kuilewa kabisa na kwa nini mimi tu ndio niwaze ujinga? Nimekuwa nikijiuliza nakosa majibu.

Ipo siku Mungu wangu ambaye naamini kwa kila jambo atanipa utimamu wa akili. Nitakuwa na akili nambari moja, nitakuwa na akili ambayo itanifanya nichambue na kueleza mambo kwa kina. Hii akili ya kuwaza ujinga iko siku sitakuwa nayo. Najua nitaimisi lakini huenda Mungu anataka kunitoa nilipo na kuniweka kwenye daraja la wenye akili.

Bahati nzuri katika nchi yetu hii ya Tanzania, wajinga tunayo nafasi ya kusikilizwa. Hata kama tunapuuza lakini angalau ujinga wangu utapata nafasi ya kusikika au kuonekana hata kwa bahati mbaya.

Nikiri tu, ujinga wangu ndani yake umechanganyikana na baadhi ya mambo. Pata picha sina elimu halafu mjinga. Yaani kichwani huko nakujua mwenyewe tu.

Kwanza hata wewe ambaye umesoma hadi hapa nilipofika umenivumilia kweli. Najiuliza unaweza kusoma maneno yaliyoandikwa na mjinga mimi.

Kwa kuwa sina ambaye nimemlazimisha kusoma hapa haya twende. Fuatilia tu kusoma ujinga wangu. Hutapata dhambi lakini naamini utakuwa tu unafahamu mjinga nawaza nini.

Hata hivyo, najua changamoto ya msomi anapokutana na vitu vya kijinga. Nahisi anaweza kuwaza huyu mtu ni wa wapi? Ni wa dunia hii hii inayoishi binadamu. Ndio naishi duniani hapa hapa, unataka nikaishi wapi? Nani amekwambia mjinga hana nafasi duniani? Mjinga mimi nafasi ninayo na nitaendelea hadi hapo Muumba wa mbingu na ardhi atakapochukua pumzi yake.

Kwa ujinga wangu huu huu na akili yangu ndogo, jana nimepata nafasi ya kufuatilia mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa (jina nimelisahau) ambao ameuitisha kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wake na wakuu wa wilaya. Kwa ujinga wangu sikumbuki hata ilikuwa mkoa gani. Ila nilikuwa nasikiliza tu.

Ukweli ni kwamba licha ya ujinga wangu, kuna baadhi ya kauli ambazo zimenifurahisha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huyo. Kwa mfano, wakati anazungumza na watendaji na wakuu wa wilaya ya mkoa wake huo akazungumzia ushirikiano ili kufanikisha miradi ya maendeleo.

Hongera, kauli za kushirikiana ni za msingi sana mahali popote iwe kazini, iwe nyumbani, iwe mtaani, iwe kwenye mambo ya familia na kokote kule lazima ushirikiano uwepo.

Kote ambako wamefanikiwa, msingi wake ni ushirikiano. Ndio maana hata katika ngazi ya familia tunaambiwa kwenye maendeleo ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke. Huo ndio ukweli na maana yake mume na mke wanashirikiana vema.

Hivyo, Mkuu wa Mkoa alipozungumzia ushirikiano kwanza ikanipa faraja, pili ikanipa matumaini sasa baada ya kikao hicho watendaji, wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa watakuwa wamoja na kushirikiana. Narudia tena hongera kwa kukumbusha ushirikiano.

Kwa ujinga wangu wakati naendelea kupongeza kauli ya ushirikiano, ghafla masikio yangu yakasikia tena kauli nyingine. Hii sasa inahusu kuhujumiwa. Mkuu wa Mkoa anasema anahujumiwa sana. Kuna watendaji na viongozi wa kisiasa ndani ya Mkoa wake wamekuwa sehemu ya kukwamisha mambo.

Nikawa nawaza nani anamhujumu Mkuu wa Mkoa? Kwanini anahujumiwa? Wanamhujumu wanataka kupata nini baada ya hujuma zao kufanikiwa? Kuna tatizo kati ya Mkuu wa Mkoa na watendaji wake au wakuu wa mikoa?

Kwa ujinga wangu nikawa naendelea kuwaza na kujiuliza mawali ya kijinga. Eti nawaza najiuliza kwa nini Mkuu wa Mkoa ahujumiwe na wanaomhujumu hawana wasiwasi. Hivi kukwama kwa miradi ya maendeleo katika Mkoa huo ni sababu za hujuma?

Katika maswali yooooote hayo nimekosa majibu ya moja kwa moja. Kwa bahati mbaya ujinga nilionao ninaweza kuuliza tu maswali lakini kupata majibu siwezi. Iko siku nitakuwa na akili timamu iliyochanganyika na elimu nitakuwa na majibu.

Hata hivyo, katika mazingira ya kawaida sikutaratajia watendaji (si wote) na wakuu wa wilaya (nao si wote) kufanya hujuma kwa Mkuu wa Mkoa. Ukweli maendeleo ya Mkoa wenu na kufanikisha kila lililo ndani ya mikakati yenu ni jukumu letu sote.

Natambua mamlaka ya Mkuu wa Mkoa, natambua mamlaka ya wakuu wa wilaya na wakati huo huo natambua nafasi ya watendaji kila mmoja kwa nafasi yake na majukumu yake. Ili mambo yaende lazima muwe wamoja.

Katika maisha ya dhana ya kuhujumiana ukweli nawaambia hamtafika. Mtakuwa na vikao vya kila mara kujadiliana nani anamhujumu nani. Hata hivyo, huu ni ujinga wangu tu.

Wakati naendelea kuwaza ujinga eti nimetamani na kikombe cha chai rangi ambacho ndani yake kuna harufu ya hiliki. Achana na habari ya kikombe cha chai.

Naomba nieleze kitu hapa kidogo. Tena weka akilini, kweli nawaza ujinga lakini kuna wakati akili inakaa sawa. Hapa naona angalau akili imetulia. Hivyo hiki ambacho nitaandika nacho weka akilini. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nyote ni wateule wa rais, nyote mnajenga nchi moja na nyote ni Watanzania.

Msikubali kutenganishwa na hizo nafasi, kwamba nani mkubwa nani mdogo dhidi yangu. Unachotakiwa kuweka kichwani mmepata nafasi hiyo kwa lengo la kuhakikisha nchi yetu inapata maendeleo. Nchi yetu inapiga hatua.

Ndiyo maana halisi, tabia ya baadhi ya wakuu wa wilaya kuwadharau wakuu wa mikoa si sahihi hata kidogo. Mkuu wa Wilaya unayo nafasi ya kutambua nafasi yako na majukumu yako kimamlaka. Huo ndio ukweli. Mnayo nafasi ya kusikiliza na kupokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa ilimradi yawe yanaheshimu Katiba, utu na utanzania wetu.

Vivyo hivyo kwa wakuu wa mikoa nanyi mnayo nafasi ya kuheshimu wakuu wa wilaya. Bila wao Mkuu wa Mkoa si chochote wala si lolote. Unakuwa Mkuu wa Mkoa kwa sababu kuna wakuu wa Wilaya ambazo kwa pamoja zinaunganisha Mkoa wenu.

Hivyo, wakuu wa mikoa mkijiona ninyi ni zaidi ya wakuu wa wilaya mtakosea.Tena mtakosea sana. Fuatilia kote ambako kuna kutoelewana kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya mambo hayaendi.


Ukitaka kuthibitisha hilo muulize Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakwambia.Tena hivi karibuni alikuwa Mkoa wa Morogoro. Amekuta na mauza mauza huko.

Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi picha haziendi. Kila mmoja anafanya mambo yake kwa namna anavyotoka.

Mkuu wa Mkoa ukijiona uko juu sana kuliko wengine kwenye mkoa wako, lazima kuna mahali mtatofautiana na hapo ndipo mtaanza kutafutana uchawi. Badilikeni, kuweni kitu kimoja kwa maslahi ya nchi yetu na wananchi wake.

Ngoja nirudi kwenye kuwaza ujinga, iko hivi kwa akili yangu hii ya kijinga nikiri nimekuwa nikifuatilia kwa karibu baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Nilichojifunza kuna wakati aidha wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa kila mmoja anatafuta sifa binafsi badala ya sifa ya pamoja katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Hili la kila mmoja kutafuta sifa ndipo changamoto inapoanzia. Ndio maana inakuwa rahisi miradi kukwama. Maana huyu anadhani hili likifanikiwa basi sifa itakwenda kwa fulani. Japo huu ni ujinga lakini nashauri jengeni tabia ya kutafuta sifa ya pamoja kama mnadhani sifa zina umuhimu katika maisha ya leo.

Kama kuna mradi wa maendeleo wote muwe wamoja, zungumzeni kauli moja ambayo mtaona ndio chachu ya mafanikio yenu. Kinyume na hapo mtabaki mkinyoosheana vidole. Kuna mikoa inaleta raha. Watu hawana maneno zaidi ya kuchapa kazi kwa uadilifu na uaminifu. Hongereni mlioko kwenye mikoa hiyo.

Wale wanaobaki kujibizana na kurushiana maneno wasiwape tabu. Iko siku tena si nyingi watakuwa wamoja tu na kuchapa kazi. Maana angalau wanaweza kuitana na kuambiana ukweli.

Pamoja na yote hayo bado naamini kuwa rais wangu mpenda Dk. John Magufuli amewapa nafasi hizo kwa kuamini mtatekeleza yale yote ambayo amewaagiza. Mtatekeleza ambayo mnakubaliana katika Mkoa au Wilaya zenu.

Nimekumbuka kitu. Wakuu wa Wilaya (si wote) acheni dharau na kiburi. Kuna mambo mengi yanakwama na mnashindwa kufanikisha kwa sababu tu ya dharau mlizonazo kisha mnachanganya na kiburi.

Sijui kiburi kinatokana na nini au ndio cheo tena. Yetu macho tu. Mjifunze kama unataka kuheshimiwa lazima uheshimu waliopo au wanaokuzunguka. Kama unataka kufanikisha shirikiana na wenzako kufanikisha. Kama unataka usilete kiburi basi nawe acha kiburi.

Na kwa wakuu wa mikoa, nanyi naomba niwaambie hivi mamlaka mliyonayo ni makubwa katika ngazi ya mkoa. Tumieni mamlaka hayo vizuri. Mamlaka hayo yasiwe fimbo kwa walio chini yenu.

Mamlaka mliyonayo yasiwatie kiburi na kujenga dharau. Mamlaka mliyonayo yasiwe sehemu ya kujiona mnaweza kufanya chochote na kwa yoyote.

Pamoja na mamlaka yenu jitahidi kuheshimu wengine. waheshimu mliowakuta kwenye utumishi, wahehimu waliowakuta ofisini.

Waheshimu wananchi wenu na kubwa zaidi heshimu mawazo ya wengine. Unaweza kuwa kwenye nafasi lakini baadhi ya maamuzi yako yakawa si sahihi. Ukipingwa kubali, rekebisha kisha songa mbele.

Ukweli nawaambieni kuna wakuu wa mikoa ni hazina kwa taifa letu na wakuu wa mikoa hao lazima washikiliwe kwa mikono miwili. Najua pia wakuu wa mikoa hao ambao ni hazina kwa nchi wana kasoro ndogo ndogo ambazo zikifanyiwa kazi hakika sina shaka kabisa na utumishi wao. Waache sifa, waache dharau. waache kujiona wao ndio kila kitu na hakuna zaidi yao.

Nihitimishe kwa kueleza tu, yooote hayo ambayo nimeandika ni ujinga.Tena ujinga ambao unapaswa kupuuzwa na hauna sababu ya kuweka akilini. Iko siku nikiwa na akili nitaandika mambo ya msingi kwa ajili ya nchi yangu kama ambavyo wanafanya wengine.

Angalizo; ujinga wangu una nia njema, isitafsiriwe vibaya. Sina ugomvi na mtu. Najua mamlaka ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. Ndio wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama, aidha ya Wilaya au ya Mkoa. Nitafurahi nikibaki kuwa rafiki badala ya kuwa adui. Nitaishi wapi mie maisha yenyewe ndio haya pangu pakavu tia mchuzi.

Mie ambaye nimepewa akili tu za kuvukia barabara naomba mniache, maana si amri yangu. Naamini nitakuwa sawa. Hata hivyo, kwa kumaliza jambo linalonipa faraja nchi yangu iko kwenye mikono salama ya Rais wangu Dk. John Magufuli.

Hapa sasa kwa akili zangu timamu naomba niseme hivi mwakani ni Uchaguzi Mkuu, na kupiga kura ni siri ya mpiga kura. Hata hivyo kura yangu sitaki iwe siri tena.

Kwanini iwe siri wakati yanayofanywa na Rais Magufuli nayaona tena kwa macho. Kura yangu katika uchaguzi mkuu mwaka 2020 inakwenda kwa Rais Magufuli.

Iko siku nitaeleza kwa nini kura yangu kwa Rais Magufuli. Kubwa tuombe uzima tu. Nakukumbusha ujinga ambao nimeuandika achana nao kabisa. Tubaki kujadili mambo ya maana.

Mwisho kabisa kabisa maandiko ya vitabu vitakatifu yanasema; Neno lililooza lisitoke kinywani mwenu, bali neno lolote ambalo ni jema kwa ajili ya kujenga -Kitabu cha WAEFESO 4:29
Simu 0713833822.

ENGEN YAZIDI KUWASOGEZEA HUDUMA WATEJA WAKE,YYAZINDUA KITUO KIPYA JIJINI DODOMA

$
0
0


Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited, imezidundua kituo kipya cha mafuta jijini Dodoma,ikiwa ni sehemu ya kujitanua na kuongeza wigo wa kibiashara kwa kuwafikia Wateja wake walioko katika maeneo mbalimbali nchini,

Akizungumza jana katika uzinduzi rasmi wa kituo hicho kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza),Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Paul Muhato aliuhakikishia umma kuhusu upatikanaji wa soko la bidhaa za Kampuni hiyo,ikiwa ni sehemu ya uchangiaji wa kukuza uchumi jijini Dodoma na miji mingine nchini Tanzania ambako kampuni hiyo imekuwa ikijitanua .

Alisema Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited ni kampuni yenye mafanikiyo, iliyojidhatiti vilivyo na yenye ubunifu mkubwa,hasa katika utoaji wa huduma na bidhaa zake bora za mafuta,pamoja na maduka yanayorahisisha upatikanaji wa bidhaa bora za kampuni hiyo.

"ENGEN imekuwa mshirika katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 20 sasa,hivyo kama sehemu ya kuendeleza mkakati wake wa kujitanua kibiashara,nauhakikishia umma kuhusu uwepo wa soko la bidhaa za kampuni ya Engen zipo za kutosha,zilizo na kiwango cha ubora wa Kimataifa na usiotia shaka kabisa'',alisema Muhato.

Amesema upanuzi wa vituo katika maeno mbalimbali ni hatua ya asili katika mpango wa ukuaji wa kampuni kwa sasa,na pia wanaendelea kuangalia maeneo ya kimkakati nchini kote kwa ajili ya maendeleo na ununuzi wa vituo vya rejareja ili kutumikia vyema soko la Tanzania.

"Hivi sasa tuna vituo 10 vinavyopatikana katika mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha na Mwanza - lakini idadi hii itaongezeka katika kipindi cha miaka michache ijayo,

Tukiwa tunakusudia kuweka mteja kama kipaumbele cha kwanza, tunatarajia angalau vituo vinne zaidi katika maeneo ya kimkakati mwishoni mwa mwaka,huku tukisisitiza umuhimu wa kuwa na mafuta bora kwa wateja wetu poote pale'', alisema Muhato .

Amesema katika suala la utoaji huduma,Wana wahudumu Waliofundishwa vizuri kawahudimia wateja kwa saa 24 kila siku, lakini pia upatikaji wa malipo ya bidhaa zao,unaweza kutumia njia nyingi ikiwemo ya kwa njia ya kadi ya Mafuta ya Engen.

"Wateja pia watafurahia huduma zingine kadhaa kama vile maduka, migahawa ya hali ya juu, Sehemu ya matengenezo ya magari, mahali pa kuosha gari na huduma zingine, zote zikiwa chini ya paa moja. "alimaliza kusema Muhato.

Muoenekano wa Kituo kipya cha mafuta Engen kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza)jijin Dodoma mjini
Madereva wa pikipiki wakisubiri kupata ofa ya kujaziwa mafuta kila mmoja waliohudhuria katika siku ya uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Engen jijini Dodoma.

ILANI YA UCHAGUZI YA WANAWAKE YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2020 YAZINDULIWA

$
0
0
Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.


Ilani hiyo inayojumuisha sauti za wanawake kutoka sauti za wanawake kutoka makundi mbalimbali chini ya Uongozi wa TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania na Mtandao wa Wanawake na Katiba,Uchaguzi na Uongozi imezinduliwa na Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro.

Awali akizungumza,Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena alisema ilani hiyo imebeba masuala muhimu yanayohusu wanawake kwenye uchaguzi.

“Ilani hii imebeba ajenda ya mwanamke,turufu ya ushindi 2019/2020 imewalenga wanawake,serikali,vyama vya siasa,wagombea nafasi za uongozi,vyombo vya habari na wapiga kura”,alisema Muro.

Alisema ilani hiyo inaendeleza madai ya wanawake watetezi wa haki za ushiriki katika uongozi wa kisiasa tangu taifa lipate uhuru mpaka leo.

“Hii ni ilani ya tano iliyobeba madai ya wanawake tukiwa wadau na washiriki wakuu katika michakato mbalimbali ya uchaguzi.Ilani ya kwanza ilikuwa ya mwaka 2000 ikijulikana kama ilani ya wapiga kura,ilani ya pili ni ya mwaka 2005,ya tatu ni ya mwaka 2015 na ya nne ni ilani ya mwaka 2015”,alieleza Muro.

“Sisi wanawake wapiga kura tunatambua ni wadau muhimu kwenye shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii.Tunatambua na kudai haki za kushiriki katika uchaguzi kama wapiga kura na wanaowania nafasi za uongozi,walioteuliwa na kugombea hatimaye kushinda nafasi za uongozi kupitia uchaguzi”,aliongeza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema madai yaliyomo kwenye ilani ya uchaguzi ya wanawake yanahusu masuala ya wanawake wote nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena akielezea kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ambayo imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakionesha mabango yenye ujumbe wa ‘Uongozi sio misuli ni hekima na busara kila mtu anao’.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 .
Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020,Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi.
Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ukiendelea.
Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

RC FUATILIA UTENDAJI KAZI OFISI YA DC KILOLO-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happy na Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah (wa pili kushoto) kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo , Septemba 27, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019.
Muonekano wa sehemu ya hospitali ya wilaya ya Kilolo ambayo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi huo Septemba 27, 2019 na kusema kuwa amefurahishwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada kukagua na kufurahishwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi afuatilie utendaji kazi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo kufuatia watumishi 14 wa ofisi hiyo wakiwemo madereva 10 kuhamishwa baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdallah kudai kuwa hawafanyi kazi ipasavyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ni mhuimu kwa viongozi wakatambua dhamana zao katika utekelezaji wa shughuli zao pamoja na kuwatambua, kuwajali na kuwathamini watumishi wa kada zote wakiwemo madereva, hivyo ni vizuri wawaandae kwa kuwapa maelekezo kwa wakati kwa kuwa nao ni binadamu na wanafamilia.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 27, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kilolo, Halmashauri ya wilaya ya Kilolo pamoja na Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesisitiza umuhimu wa watumishi hao kushirikiana.

Waziri Mkuu amesema pamoja na shughuli za maendeleo wanazofanya katika wilaya hiyo lakini hawana mshikamano, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya ahakikishe anashirikiana vizuri na wenzake kwa sababu watumishi wengi wamehamishwa tangu aingie katika ofisi hiyo na hata wanaoletwa wanalalamika na wanaomba wahamishwe.

Amesema watumishi wengi katika ofisi hiyo anawaona hawana uwezo wakiwemo wasaidizi wake kama madereva, watunza kumbukumbu na makatibu muhtasi. “Hata aliyekuwa Katibu Tawala wa wilaya hii alihamishwa kwa sababu na kutoelewana na DC, na hata huyu Katibu Tawala wa Wilaya aliyepo sasa hana raha anataka kuhama kwa sababu hizo hizo.”

“Lazima tuwatambue wasaidizi wetu na majukumu yao. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haiwezekani ikawa hivi, lazima kuna shida kuwaondoa watumishi wote, Mkuu wa Mkoa fuatilia hii ni mpya. Hapa tujue mbovu ni nani Mkuu wa Mkoa tunataka tujue DC wako anataka dereva wa aina gani, tangu amefika hapa madereva 10 wote hawafai? 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “ili mfanye kazi vizuri mnatakiwa mshikamane mfanye kazi kama timu moja kwani pamoja na shughuli mnazofanya hamna ushirikiano. DC (mkuu wa wilaya) sasa utabaki peke yako utakuwa unaandika mwenyewe, unaendesha gari mwenyewe maana wote hawafai. Mkuu Mkoa nakukabidhi majina ya watumishi hao ushughulikie suala hili. Na Katibu Tawala wa Mkoa usilete watumishi wengine hapa mpaka suala hili litakapopatiwa ufumbuzi”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga kiasi cha fedha katika makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwenye maeneo yao kama ujenzi wa vituo vya afya, barabara za halmashauri na masoko badala ya kutegemea fedha kutoka Serikali Kuu pekee.

Amesema wilaya ya Kilolo ambayo haina kituo cha mabasi inatakiwa itenge fedha kutoka kwenye makusanyo yao na kuanzisha mradi wa kituo hicho ambao utekelezaji wake utaboresha huduma kwa wananchi pia, mradi huo utasaidia katika kuongeza mapato ya halmashauri. Halmashauri ya wilaya ya Kilolo inakusanya sh. bilioni nne kwa mwaka.

Waziri Mkuu amesema watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani wananchi wanahitaji waone matokeo ya uwepo wao kutokana na dhamana waliyotewa na Serikali katika wilaya hiyo. “Madiwani nanyi simamieni halmashauri yenu vizuri kwa sababu nyie ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri.”

Awali, Mbunge wa jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya yao ikiwemo ya umeme, ambapo kati ya vijiji 94 vilivyoko vijiji 54 vimeunganishiwa huduma hiyo na vilivyosalia vitakuwa viunganishiwa umeme ifikapo Desemba mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu miradi ya maji mbunge huyo alisema kati ya vijiji 94 vya wilaya hiyo vijiji 15 tu ndio bado havina maji ya uhakika lakini wanaendelea na mchakato wa ufuatiliaji ili kuhakikisha navyo vipata maji safi na salama.”Kuhusu sekta ya elimu tatizo tulilonalo ni madai ya walimu waliohama na waliopandishwa madaraja.” Waziri Mkuu amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Mapema, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo ambapo alisema ameridhishwa na ujenzi huo uliogharimu sh. bilioni nne na alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mkurugenzi pamoja na mkandarasi anayenga.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images