Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WATUMISI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI NA HALMASHAURI YA MAFINGA MJI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Mafinga Mji na Mufindi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mafinga Mji, Septemba 26,2019. Yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UJENZI WA DARAJA LA MTO SIBITI WAANZA KUHUJUMIWA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly MKALAMA
UJENZI wa daraja la Mto Sibiti uliopo Kijiji cha Nyahaa,Kata ya Mpambala,wilayani Mkalama,Mkoani Singida lenye urefu wa mita 82 umeanza kuhujumiwa na watu wasiojulikana kwa kuondoa kifaa kinachotambulika kitaalamu kwa jina la EXPANSION JOINT kinachosaidia kuzuai daraja hilo lisitanuke.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kaimu meneja wa Wakala wa Barabara (TANROAD) Mkoa wa Singida,Mhandisi Matare Masige alifafanua kwamba pamoja na serikali kutumia mabilioni ya fedha kugharamia ujenzi wa daraja hilo,lakini baadhi ya wananchi wameanza kufanya hujuma kwa kuiba baadhi ya vifaa vilivyowekwa katika daraja hilo.

Alibainisha kaimu meneja huyo kwamba licha ya serikali kupeleka askari kwa ajili ya kulinda daraja hilo lisihujumiwe lakini katika hali ya kushangaza,kusikitisha na kuleta sintofahamu,kwani katika kipindi cha mwaka mmoja tangu Raisi Dkt.John Pombe Magufuli alipoweka jiwe la msingi uharibifu umeanza kujitokeza.

Alipotakiwa kuzungumzia hujuma zilizoanza kujitokeza huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo lilipeleka askari kwa ajili ya kulinda daraja hilo,akizungumza kwa njia ya simu akiwa katika safari za kikazi,Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida,ASP.Sweetbert Njewike alikiri kupeleka askari kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa adaraja hilo.

Hata hivyo ACP Njewike alisisitiza kwamba daraja hilo limekuwa likilindwa kwa zamu kati ya askari wa Mkoa wa Singida na Mkoa wa Simiyu na anaamini kwamba Mkuu wa polisi wilaya ya Mkalama alikuwa akaisimamia zoezi hilo kikamilifu ili madhara yeyote yale yasiweze kutokea.

Aidha Kamanda huyo wa jeshi la polisi aliweka bayana kwamba kwa amujibu wa maelezo ya kitaalamu aliyopewa na Kaimu Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida ni kwamba kifaa kilichohujumiwa hakiwezi kuleta madhara yeyote ile kwenye daraja hilo wakati vyombo vya moto vitakapoanza rasmi kutumia barabara hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye daraja hilo,baadhi ya wananchi na viongozi wa kata ya Mpambala walionyesha kusikitishwa na hujuma zilizofanywa za kuiba kifaa hicho chenye umuhimu mkubwa katika daraja hilo.

 Diwani wa kata ya Mpambala,Boazi Hasani Ndandutwa akizungumzia tuhuma za askari waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda daraja hilo kufanyakazi za kukamata vyombo vya moto siku yam nada wa Bukundi alikiri kuwakuta askari hao kila siku ya jumatano kunapokuwa na mnada.

“Kwa akweli kila wakati nilikuwa anapita kwenda Bukundi nilikuwa nawakuta askari wapo hapa darajani,lakini kwa siku za katikati mwa wiki au mwanzoni mwa wiki kiukweli mara nyingi nilikuwa sipiti lakini siku ya jumatano ni kila jumatano wanakuwa huku kwenye daraja,”alifafanua diwani huyo.

Hata hivyo Boazi alionekana kushangazwa na uharibifu huo ulioanza kutokea katika daraja hilo alishindwa kufahamu iwapo uharibifu huo unafanyika wakati wa usiku au mchana na hivyo kuahidi kwamba atalazimika kuwatafuta na kuwasisitiza askari ili waweze kuona uharibifu unaotokea ili nao waweze kuchukua nafasi yao kwa kuimaraisha ulinzi zaidi.

Naye mkazi wa Kijiji cha Mwanga Jasia Jacksoni Shabani alisisitiza kwamba iwapo kuna askari waliopelekwa kulinda daraja na wao kuamua kufanya kazi nyingine serikali isisite kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kuzembea hadi daraja limeanza kuhujumiwa.

“Sawa askari wanatakiwa wachukuliwe sheria kwa sababu kama wamepewa dhamana ya kulinda hili daraja na sasa hivi hawajafanikiwa kufika hapa ni mojawapo ya makosa askari wanayoyafanya,cha msingi inatakiwa hawa maaskari watafutwe sheria ambazo zinahitajika kuchukuliwa juu yao ili wasije tena wakakosa kufanya ulinzi katika hili daraja.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Mhandis Jacksoni Masaka licha ya kukiri kupata taarifa za kuhujumiwa kwa daraja hilo kutoka kwa meneja wa tanroad mkoa wa singida lakini alibainisha kuwa kamati ya ulinzi na usalama ilishamwagiza kamanda wa polisi wa wilaya kupeleka askari kwa ajili ya ulinzi wa daraja hilo.

“Daraja hili linalindwa na polisi wanafanya patro mara kwa mara kwa hiyo kamati ya ulinzi na usalama ilishamwagiza ocd ahakikishe anapeleka kule askari,tatizo lake ocd wakati mwingine anakuwa hana gari la uhakika,gari lake ni bovu wakati mwingine linakuwa lina shida ya matairi na kule kituo cha Ibaga hawana gari la kituo,kwa hiyo wanalazimika kutumia pikipiki mara kwa mara kwenda Sibiti kitu ambacho kinakuwa kina gharama fulani kwa askari.”alisisitiza mkuu wa wilaya huyo.
 Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Mhandisi Jacksobi Masaka(aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa hujuma zinafanywa kwenye daraja la mto Sibiti kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imemwagiza OCD kuhakikisha anapeleka askari kulinda daraja hilo.



 Daraja lililojengwa katika mto Sibiti ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa mbali mbali kupeleka kwenye masoko ya biashara ya ndani na nje ya nchi.


 maeneo ya daraja la mto Sibiti yaliyoanza kuhujumiwa na watu wasiojulikana kwa kuchukua kifaa kinachojulikana kwa jina la kitaalamu la "EXPANSION JOINT" kinachosaidia daraja kutotanuka.

TAMISEMI FUATILIENI MIKOA YA NJOMBE NA TANGA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) afuatilie sababu za mikoa ya Tanga na Njombe kutotekeleza sheria ya kutoza asilimia tano ya ushuru unaotokana na mazao ya misitu.

Amesema makampuni yanayonunua nguzo lazima yahakikishe yanazingatia sheria ya nchi ikiwemo ulipaji wa kodi zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kampuni zote zilizonunua nguzo bila ya kulipa kodi zifuatiliwe na zilipe kodi yote waliyoikwepa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 26, 2019) wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme cha Qwihaya kilichoko Mafinga wilayani Mufindi akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

“Naibu Waziri TAMISEMI hakikisha unakwenda mkoani Njombe na uaanze kuzungumza na mkuu wa mkoa, tunataka kujua kwa nini hawajaanza kutekeleza sheria ya kutoza asilimia tano ya ushuru unaotokana na mazao ya misitu hali iliyosababisha wanunuzi kumbilia huko na kuacha kununua mazao hao katika mkoa wa Iringa.”

“Tunataka tujue ni nani huyo anayewakataza wasilipe kodi na tuangalie anamahusiano gani na viongozi wa mkoa huo. Ukaangalie makampuni hayo yanamahusiano gani na viongozi hao hadi wasilipe kodi na tutajua kama kampuni hizi ni zao au za ndugu zao.”

Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inawabana wafanyabiashara wote walionunua nguzo kwenye mikoa hiyo ambao hajalipa asilimia tano ya ushuru unaotokana na mazao ya misitu ili waweze kulipa kiasi chote walichokikwepa..

Amesema Serikali inahitaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na haoni sababu ya mikoa hiyo kushindwa kutoza kodi iliyowekwa kwa mujibu wa sheria. Kitendo cha mikoa hiyo kutotoza kodi hakikubaliki na wafanyabiashara wote waliochukua nguzo bila ya kulipa kodi hiyo watalipa kodi yote kuanzia walipioanza kuchukua nguzo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mikakati ya wafanyabiashara wafanye biashara zao katika mazingira bora na kwa kuzingatia sheria za nchi na pia Rais Dkt. John Magufuli amezuia nguzo zote za umeme kuagizwa kutoka nje ili kuwawezesha wafanuyabiashara wa ndani kuuza nguzo pamoja na wananchi kupata ajira. 

“Hata tulipokuwa tunanunua nguzo kutoka nje zilikuwa zinatoka hukuhuku na walichokuwa wakifanya ni kuzichukua huku na kuzipeleka nchi jirani na kuziweka kwa wiki kisha wanabadilisha vibao na kuzirudisha tena nchini.”

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi alimweleza Waziri Mkuu kwamba wateja wa mazao ya misiti wameanza kupungua na kwenda mikoa ya Tanga na Njombe kwa kuwa katika mikoa hiyo haijaanza kutekeleza sheria ya kutoza asilimia tano ya ushuru unaotokana na mazao ya misitu, hivyo ameiomba Serikali iwasaidie.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme cha Qwihaya, Benedicto Mahenda alisema kiwanda hicho kilianzishwa 2007 kwa ajili ya uchakataji wa mbao na 2016 kilianza kuzalisha nguzo za umeme wakiwa na mtambo wenye kuzalisha nguzo 100 kwa siku. Kiwanda kimeajiri watumishi 350.

Meneja huyo alisema katika kuitikia wito wa Rais Dkt. Magufuli wa kujenga uchumi kupitia sekta ya viwanda, walifanya mabadiliko kwa kujenga kiwanda kikubwa na cha kisasa cha kuzalisha nguzo za umeme chenye uwezo wa kuzalisha nguzo 1,500 kwa siku.

Alisema malighafi za kiwanda hicho wanazipata kutoka katika shamba la miti la Sao Hill lililoko chini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na kwenye mashamba ya wakulima wadogo. Soko kubwa la bidhaa zao ni TANESCO kupitia utekelezaji wa miradi ya REA.

Pia, Meneja huyo alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake wa kuzuia nguzo zisitoke tena nje ya nchi na kutumia nguzo zinazozalishwa na viwanda vya ndani. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutuamini na kututia moyo wawekezaji wa ndani na kutuonyesha soko la kuuza bidhaa zetu.”



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua nguzo za umeme zilizorundikana kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company LTD cha Mafinga zikisubiri wanunuzi. Kiwanda hicho cha nguzo kilitembelewa na Waziri Mkuu, Septemba 26, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Leonard Mahenda,  wa tatu kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Fred Ngwega  na wa nne kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Nguzo za umeme zikiwa kwenye mtambo wa kuziwekea dawa maalum ya kuzifanya zisishambuliwe na wadudu au kuungua moto zikiwa katika kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, September 26, 2019.

 Baadhi ya  nguzo za umeme zilizorundikana  zikisubiri wanunuzi kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 26, 2019. {Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIMAMOTO NCHINI YAPOKEA MSAADA WA BOTI YA MAOKOZI MAJINI

$
0
0
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada wa boti ya maokozi uliotolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Mjini wa Hamburg. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 
 Kiongozi wa Kikosi cha Wazamiaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Stesheni Sajini  Saidi Sekibojo, akitoa maelezo jinsi vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na wazamiaji wanapotekeleza majukumu yao katika uokoaji majini, wakati wa kupokea msaada wa boti ya maokozi uliotolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Mjini wa Hamburg. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akiwa kwenye picha ya pamoja na askari wa kikosi cha uzamiaji majini cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kinachoongozwa na Stesheni Sajini  Saidi Sekibojo, wakati wa kupokea msaada wa boti ya maokozi uliotolewa na Serikali ya Ujerumani kupitia Mjini wa Hamburg. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 
Boti ya maokozi iliyotolewa msaada na Nchi ya Ujerumani kupitia Mji wa Hamberg kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji itakayo saidia katika shughuli ya uokoaji majini. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MAKAO MAKUU

SIJAWAHI KUMSAIDIA MALINZI KUPATA FEDHA YOYOTE - ALIYEKUWA MHASIBU WA TFF

$
0
0
ALIYEKUWA Mhasibu wa Shirikisho la Soka  Tanzania (TFF), Nsiande Mwanga (29) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa hakuwahi kumsaidia Jamal Malinzi kupata fedha yoyote kwa sababu fedha zilizokuwa zikitolewa ni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za shirikisho hilo.

Mwanga amedai hayo leo Septemba 26, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi wake wa kujitetea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akiongozwa na Wakili Richard Rweyongeza, Mwanga amedai alianza kazi TFF Aprili Mosi 2016 na kabla ya kujiunga na shirika hilo hakuwa anawafahamu Malinzi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa.

Alidai alipojiunga na shirikisho hilo hakuwa anafahamu kwamba walikuwa wanamtafuta mtu anayehusika na kodi na kwamba katika barua yake ya ajira ilimuelekeza poa kufanya kazi atakazopewa na mwajiri wake.

Amesema, hajawahi kuhusika na malipo ya Malinzi katika benki nyingine yoyote kwa sababu alikuwa mtia saini wa benki za Stanbic pekee na katika hundi zilizoletwa mahakamani ameweka saini hundi mbili na nyingine sijui nani aliyesaini," amedai Mwanga.

Pia amedai kuwa, anatambua Malinzi anaidai TFF kwa sababu wafanyakazi waliopo kwenye kitengo cha uhasibu wanajua kwamba Malinzi anadai ingawa yeye hajawahi kupata maelekezo yoyote kutoka kwa Malinzi akimuomba ampatie fedha na kwamba hakuwahi kuandika hundi ya kumlipa.

Pia amedai, Hellen Adam ambaye ni mhasibu wa TFF ndio alikuwa mtu wa kwanza kumpeleka benki ya Stanbic na kumtambulisha kama mtia saini na sio washitakiwa Mwesigwa na Malinzi.

Mwanga ameiomba mahakama imuachie huru kwa sababu hakuwahi kushirikiana na Mwesigwa kumsaidia Malinzi kujipatia fedha yoyote kama mashitaka ya utakatishaji fedha yanavyoeleza.

Mbali na Malinzi na Mwesigwa  washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Katika kesi  hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

WATU LAKI NANE DUNIANI HUPOTEZA MAISHA KWA KUJIUA KILA MWAKA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
IMEELEZWA kuwa watu wapatao laki nane duniani hupoteza maisha kwa kujiua kunakosababishwa na matatizo mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo, matumizi ya pombe na dawa za kulevya pamoja na kukaa na magonjwa sugu kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa afya ya magonjwa akili kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Praxeda Swai amesema kuwa  shirika la afya duniani (WHO) limekuja na kauli mbiu ya kuzuia matukio ya kujiua na hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa matukio hayo kote duniani.

"Kila mwaka duniani kote watu laki nane hupoteza maisha kwa kujiua wakitumia njia hatarishi na kufanya kati ya vifo laki moja vifo kumi na mbili hutokana na kujiua kwa mwaka" ameeleza Praxeda.

Aidha amesema kuwa kwa sekunde 40 mtu mmoja hupoteza maisha kwa kujiua na kwa saa moja pekee watu 90 hupoteza maisha kwa kujiua wakiwa wamedhamiria licha ya wengine kuokolewa.

Akieleza sababu ya watu kujiua Dkt. Praxeda amesema kuwa matatizo msongo wa mawazo, kuishi na magonjwa sugu, matumizi ya pombe na dawa za kulevya huweza kumpelekea mtu kujiua huku akitolea mfano kuwa mtu akiwa amelewa hakuna kitu kinachomzuia kufanya chochote.

Kuhusiana na wimbi la watoto wenye umri mdogo kujiua amesema kuwa;

" Wimbi la watoto wadogo kujiua husababishwa na kutekelezwa, kunyanyasika kingono, kiakili, kimwili, kutosikilizwa katika familia pamoja na kunyanyaswa na watoto wenzao hali inayowapelekea kushindwa kuhimili misongo hiyo na kuamua kujiua" ameeleza.

Ameeleza kuwa viashiria vya mtu kutaka kujiua ni pamoja na kufanya majaribio ya kutaka kujiua kama vile kujikata kwa wembe, vyupa na kisu na hata kutuma jumbe za kukata tamaa, kuaga watu wake wa karibu, kugawa mali au vitu anavyomiliki pamoja na kuandika wosia na amewashauri wanajamii kushiriki kukomesha suala hilo kwa kuongea na watu wenye viashiria hivyo pamoja na kuonesha upendo kwao.

Kwa upande wake Msaikolojia tiba na mwenyekiti wa chama Cha wataalamu wa afya ya akili (MEHATA)  Dkt. Isaack Lema amesema kuwa wameendelea kuhamasisha wanajamii kuhusiana afya ya akili ili kujenga ustawi wa kutambua na kukabiliana na msongo wa mawazo, kufanya maamuzi na kufurahia maisha.

"Kati ya watu wanne mmoja ana tatizo la akili na kama kunafanyika mawasiliano baina yao hayatafanikiwa kwa kuwa mmoja ana tatizo la akili, na pia katika wafanyakazi watano mmoja ana tatizo la akili hivyo lazima jamii itambue kuwa suala la afya ya akili ni la watu wote." Ameeleza.

Vilevile amesema kuwa vifo vya  vijana wa kati ya miaka 15 hadi 29  sababu ya kujiua hushika nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikiwa ni ajali huku sababu vifo kwa wazee wa miaka 75 na kuendelea sababu ya kujiua imeendelea kuwa juu.

Amesema kuwa afya ya akili ni kwa watu wote na mpango wa kuzuia kutokea kwa matukio ya kujiua unaofanywa na hospitali ya taifa Muhimbili, Chama cha wataalamu wa afya ya akili (MEHATA) na sekta nyingine utafanikiwa kwa kushirikiana na wanajamii hasa kwa kuwaunganisha na huduma watu wenye viashiria vya kutaka kujiua.
  Msaikolojia tiba na mwenyekiti wa chama Cha wataalamu wa afya ya akili Dkt. Isaack Lema akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mpango wa kupambana na vitendo kujiua ambapo amesema kuwa jamii ishiriki kuwasaidia watu wenye viashiria vya kutaka kujiua kwa kuwaunganisha na huduma katika hospitali kote nchini, leo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa afya ya magonjwa ya akili Praxeda Swai akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wimbi la watu kujiua kunakosababishwa na matatizo mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo ambapo amewashauri wanajamii kushiriki kuwasaidia watu wenye viashiria vinavyopelekea kujiua, leo jijini Dar es Salaam.

INTRODUCING NIKAGONGEE REMIX - BADDEST 47 X SHILOLE (Official Music Video)

VOA: Duniani September 25, 2019


PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI KATIKA PICHA YA PAMOJA NA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP NA MKEWE, AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA NAIBU WAZIRI WA AFYA WA NCHI HIYO, TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 120 KUPAMBANA NA SELI MUNDU

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump na Mkewe Melania. Prof. Palamagamba John Kabudi yuko New York Marekani kuhudhuria mutano wa 74 wa Baraza la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo Pichani) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika  
Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika  Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

MAREKANI KUTOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 120 KUPANDA NA UGONJWA WA SELI MUNDU (SICKLE CELL)

Tanzania ni miongoni mwa baadhi ya Nchi zinazotarajiwa kunufaika na kiasi cha dola za Kimarekani milioni 120 zilizotengwa na Serikali ya Marekani kwa ajili ya utafiti wa kupambana na ugonjwa wa  seli mundi (sickle cell).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi jijini New York Nchini Marekani.

Admiral Brett ameutaja mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kama mwanzo mpya wa ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani na kuongeza kuwa Nchi yake ina nyenzo zote ikiwemo teknolojia ya kuoambana na maradhi ya seli mundu ili kuboresha Maisha ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa katika siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua chanya katika kuimarisha masuala mbalimbali ya afya za wananchi wake na kwamba ni azma ya Marekani kuona kuwa ugonjwa wa seli mundo unapata tiba.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema utafiti na hatimae tiba ya maradhi hayo ya seli mundu kwa kiasi kikubwa itainufaisha Tanzania kutokana na kushika nafasi ya tatu katika Bara la Afrika na ya nne duniani kwa kuwa na wagonjwa wengi wa seli Mundu.

Ameongeza kuwa Tanzania na Marekani zitashirikiana katika kufundisha na kujengeana uwezo wa namna ya kupambana na maradhi ya seli mundu lakini pia kutafuta fedha zitakazowezesha upatikanaji wa dawa ya seli mundu kutokana na ukweli kuwa dawa za ugonjwa huo kwa Tanzania ni miongoni mwa dawa muhimu yaani essential drugs ili iweze kuwafikia wananchi wengi na kwa bei nafuu.

Amezitaja Nchi zilizo na idadi ya watoto wengi wanaozaliwa na ugonjwa wa seli mundu ambapo kwa Afrika Tanzania ni ya tatu baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nigeria nay a nne duniani baada ya India.

Stanbic Bank Tanzania commits TZS 177 billion to infrastructure projects in Tanzania

$
0
0

Stanbic Bank Tanzania today reaffirmed its commitment to the development of Tanzania and announced that in 2019 it provided TZS 177 billion in funding to various infrastructure development projects in the country. Providing finance and financial expertise to the private and public sector in Tanzania is a key focus for the bank.

Stanbic Chief Executive Mr. Ken Cockerill said, “Stanbic Bank is well positioned to play an important role in supporting Tanzania’s second Five Year Development Plan, which seeks to encourage industrialization and promote economic growth and social development.”

Mr Cockerill also mentioned that, “Infrastructure development is the cornerstone for sustainable long-term economic growth and competitiveness. With that in mind we are proud to be at the forefront of bridging the infrastructure funding gap to accelerate socioeconomic transformation in Tanzania.”

Unlocking private sector funding will create solutions to bridge Tanzania’s and the continent's infrastructure deficit and challenging business environment by developing and financing infrastructure, natural resources and industrial assets with a view to enhancing productivity and generating economic growth across Africa.

The Government of Tanzania has in 2019 dedicated over TZS 12.2 trillion (USD 5.3 billion) towards key development projects that include Africa’s longest Standard Gauge Railway (SGR), the Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline and Julius Nyerere International Airport Terminal 3.On his part, Stanbic’s Head of Corporate & Investment Banking, Mr. Manzi Rwegasira said, “Tanzania is well on its way to bridging the infrastructure gap which is critical to Tanzania becoming a middle-income country by 2025.”

Tanzania’s population is also growing at a rate of 1.6 million people per year and this is projected to reach 67 million people by 2025 and 77 million by 2030, hence the importance for modern infrastructure for an upcoming middle-income country.Mr. Rwegasira added that, “It is through collaboration between the private and public sector, spearheaded by corporates such as Stanbic Bank Tanzania, that will drive inclusive development in our economy.”

Official data from the Bank of Tanzania shows that the country’s economy grew at an average GDP growth rate of 6.6% in 2018 with the infrastructure sector significantly contributing to this growth. This year, the economy is projected to grow by 7.1 % with infrastructure projects such as roads, ports and rail expected to drive Tanzania’s GDP growth.

Since, 2018 Stanbic has raised over TZS 300 billion in financing for Tanzanian companies and institutions across the agricultural, consumer, industrial, natural resources and government sectors.

The bank is committed to working with the government and key stakeholders to improve the investment and resource mobilization climate in order to ensure that Tanzania realizes its socio-economic aspirations by 2025.


TANZANIA KATIKA MKAKATI WA MPYA WA FEDHA KWA MFUMO USIO WA KIBENKI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.



Katika kufikia azma ya kuwa na uchumi jumuishi Tanzania iko katika utekelezaji wa mkakati mpya wa matumizi ya fedha kwa mfumo usio wa kibenki ambao umewalenga wakulima wadogo na wakati hususani wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia Nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa juu kuhusu masuala ya uchumi jumuishi kwa maendeleo uliondaliwa kwa pamoja na Tazania na Uholanzi.

Akizungumza katika Mkutano huo, kando ya mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea New York MarekaniProf. Kabudi ameelezea mafanikio ambayo Tanzania imefikia katika mpango wake wa kwanza kuongeza watu katika mfumo wa fedha usio wa kibenki na sasa iko katika mpango wa pili ambapo watumiaji wa mfumo wa fedha usio wa kibenki wameongezeka maradufu.

Aidha ameongeza kuwa matumizi ya kidijitali katika kutoa huduma za kilimo,kutafuta masoko ya bidhaa pamoja na kuwawezesha wananchi kupata fedha ikiwa ni pamoja na vicoba kwa kiasi kikubwa imeongeza pia idadi ya wanawake katika kuleta usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake Balozi na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Malkia Maxima amesema kwa kiasi kikubwa anaridhishwa na hatua ambazo Tanzania inazichukua kwa nia ya kupunguza umasikini,na kutengeneza ajira na kuleta usawa wa kijinsia kwa kuwawezesha wananchi wake kuwa na njia ya kujiongezea kipato kupitia mfumo wa kifedha usio wa kibenki.

Malkia Maxima amezisisitiza serikali na sekta binafsi kuona umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa huduma kupitia mfumo wa fedha usio wa kibenki hususani kwa wakulima ili tija ionekane zaidi kwa wananchi hususani kwa wakulima wa kipato cha chini na kati.

Kwa mara ya kwanza upasuaji wa moyo wa kukamilisha kuunganisha mfumo wa mzunguko wa damu iliyokwisha kutumika mwilini

$
0
0



Na Ales Mbilinyi – JKCI

26/9/2019 Kwa mara ya kwanza hapa nchini umefanyika upasuaji wa moyo wa kukamilisha kuunganisha mfumo wa mzunguko wa damu iliyokwisha kutumika mwilini kwa kuunganisha mishipa hiyo ya damu kwenda moja kwa moja kwenye mapafu ili ikasafishwe bila kupitia mfumo wa usukumaji wa upande wa kulia wa moyo (Fontan operation).

Upasuaji huo ambao ulichukuwa muda wa masaa sita ulifanyika kwa mafanikio makubwa umefanywa jana katika kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikia na wenzao wa shirika la Mending’s Kids International lenye wataalamu wa afya kutoka nchini Italia na Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anjela Mhozya alisema mtoto aliyefanyiwa upasuaji huo anaumri wa miaka minne alikuwa na tatizo la kutokuwepo kwa valvu ya kulia ya tricuspid na mfumo wa moyo wa kulia ambao ulikuwa mdogo kuliko kawaida (tricuspid atresia).

“Tangu kuanza kwa kambi hii siku ya jumatatu jumla ya watoto 35 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kutokuwa katika mpangilio maalum wamefanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wamesharuhusiwa kutoka katika chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na dawa pamoja na mazoezi”,.

“Kati ya watoto 35 waliofanyiwa upasuaji watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab na 15 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua”, alisema Dkt. Anjela ambaye pia ni daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko ICU.

Dkt. Anjela alisema ujio wa madaktari hao kutoka nchini Italia na Marekani umekuwa ni neema kwao kwani kumewasaidia kuongeza ujuzi wa kazi na mara baada ya kumalizika kwa kambi hiyo watautumia ujuzi huo katika kazi zao za kila siku.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni ambaye alitembelea Taasisi hiyo ili kuangalia maendeleo ya kambi hiyo aliipongeza JKCI kwa huduma za matibabu ya moyo inazozitoa hasa kwa watoto ambao ni taifa la kesho.

“Nafahamu kuwa Taasisi hii inategemewa na watanzania pamoja na nchi jirani na ndiyo maana katika kambi hii kuna watoto kutoka nchini Ethiopia na Malawi ambao wamekuja kutibiwa na kama nilivyowaona hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu”,.

“Hongereni sana kwa kazi mnayoifanya ya kuokoa maisha ya watanzania wenye matatizo ya moyo. Tanzania inafanya vizuri katika sekta ya afya nampongeza Waziri wenu Mhe. Ummy Mwalimu mara kwa mara nimekuwa nikimuona akifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya”, alisema Mhe. Mengoni.

Nao wazazi ambao watoto wao wametibiwa katika kambi hiyo waliishukuru Serikali kwa Kuboresha huduma za matibabu ya moyo hapa nchini na kuwataka wazazi wengine ambao watoto wao wanamatatizo ya moyo kwenda kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)ambako kuna wataalamu wa kutosha.

Upendo Samweli kutoka Iringa ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua alisema mtoto wake alikuwa anapata tabu ya kupumua vizuri, kukohoa mara kwa mara na kupungua uzito lakini baada ya kufika JKCI na kufanyiwa vipimo alikutwa na tundu kwenye moyo.

Upendo aliomba, “Ninawaomba madaktari walioko mikoani wanaowatibu watoto kama wataona wanamtibu mtoto kwa muda mrefu hapati naafuu wampe rufaa ili aweze kutibiwa katika Hospitali zenye utaalamu wa juu zaidi. Mimi mwanangu kabla hajagundulika kuwa na matatizo ya moyo niliambiwa mtoto hapati lishe ya kutosha, kanywa maji ya uzazi lakini baada ya kuona anatibiwa muda mrefu bila ya kupata naafuu niliomba rufaa ya kuja kutibiwa JKCI”,.

Naye Rachel Anton mkazi wa Kibaha ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kuziba tundu kwenye moyo na kurekebishwa mishipa ya damu ya moyo alishukuru kwa huduma ya matibabu aliyoipata na kuwasihi wazazi wanapoona mtoto hakui vizuri na anaumwa mara kwa mara wawahi Hospitali mapema ili aweze kutibiwa kwa wakati.

Wakusanya mapato wapewa siku sita kurudisha shilingi Bilioni 1.2

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo. 

********************************

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku sita kwa wakusanya mapato wa halmashauri nne za mkoa huo ambao hawajawasilisha makunsanyo yao benki ili kuweza kusomeka katika mfumo wa kukusanya mapato ngazi ya halmashauri (Local Government Revenue Collection Information System – LGRCIS).

Amesema kuwa wadaiwa hao wanatakiwa kurudisha shilingi 1,217,350,090.85 ya mapato ambapo hadi tarehe 23.9.2019 fedha hizo zinasomeka kwenye mfumo lakini bado hazijapelekwa benki na hivyo kuhisiwa kuwa zimo kwenye mifuko ya wadaiwa hao huku halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiongoza kwa kuwa na deni kubwa la shilingi 695,288,837.45.

Ameyasema hayo katika kikao maalum cha kuwasilishiwa taarifa ya hali ya mapato Mkoani humo iliyofanywa na timu ya uhakiki na ufuatiliaji wa mapato ya ndani kwenye mfumo iliyoongozwa na Katibu Tawala msaidizi seksheni ya serikali za Mitaa, kikao ambacho kimehudhuriwa na wakurugenzi, wakaguzi wa ndani pamoja na maafisa TEHAMA wa halmashauri.

“Hawa wadaiwa wote hawa ambao majina yao ninayo hapa, wako wengi, wengi sana, ninawapa siku sita, wadaiwa wote wawe wamerudisha fedha hizi, zote zirudi na siku kama hii wiki ijayo jumanne wote waje hapa, ntakaa nao kikao, wawe wamemaliza madeni yao yote na mifumo yenu yote muwe mmeikamilisha na katika kikao hicho kutakuwa na kamati ya ulinzi na usalama wote tutakuwa hapa, sina mchezo na upande wa kukusanya mapato, tusipokusanya vizuri inamaana hata ile 10% ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu haitatolewa vizuri,” Alisisitiza.

Aidha, Alimuagiza Katibu Tawala wa mkoa kuhakikisha anawalinda wakaguzi wa ndani ambao ndio jicho la kwanza ndani ya halmashauri kabla ya kuingia kwa mkaguzi wa nje na kuwataka wakaguzi hao kutokatishwa tamaa na mtu yeyote mwenye lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa na kuongeza kuwa mapendekezo yanayotolewa na wakaguzi hao ni wajibu kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuepukana na hoja za ukaguzi kutoka kwa wakaguzi wa nje.

Awali akitoa taarifa ya uhakiki na ufuatiliaji wa mapato ya ndani kwenye mfumo wa kielektroniki, Katibu Tawala msaidizi seksheni ya Serikali za Mitaa Albinus Mgonya alisema kuwa miongoni mwa masuala yaliyobainika katika ukaguzi huo ilionekana kuwa kuna tatizo kubwa la kuwepo kwa matumizi ya fedha kabla ya kupelekwa benki na mapato mengine kuwepo kwenye mikono ya watu kwa muda mrefu hali ianyopelekea kujikopesha na kushindwa kurudisha.

“Upo udanganyifu kwenye baadhi ya vituo vya kukusanya mapato kama vile stendi za mabasi, Minada, maegesho ya magari n.k ambapo watoa ushuru kwa maana ya wateja hawana uhitaji wa risiti kulingana na uharaka wao kwenye kazi zao, pia kuna udhaifu kwenye usajili wa POS (Point Of Sales Machine) ambapo baadhi ya halmashauri zimebainika kusajili kwa jina la sehemu au cheo mfano VEO au WEO badala ya jina la mhusika na kusababisha mdaiwa halisi kutojulikana na kuwajibishwa kisheria,” Alisema.

Kwa upande wake mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Sigridi Mapunda alioroddhesha changamoto kadhaa ikiwemo udhaifu wa utekelezwaji wa hoja anazoziibua katika kazi yake ya ukaguzi, udhaifu katika ofisi ya mweka hazina pamoja na afisa TEHAMA wa halmashauri kushindwa kushughulikia miamala iliyolipwa ili kuweza kufutwa katika mfumo.

“Wale wakusanya mapato, watendaji wa kata huwa hawawashi zile mashine na hivyo hufanya kazi ‘offline’ wanapokuja kuchukua bili huwa wanawasha muda mfupi mara ile miamala inapofunguka wanapewa bili ambayo ni ndogo kwasababu miamala mingine inakuwa bado haijafunguka lakini baadae katika mfumo madeni ya wale wakusanyaji yanapanda kutokana na kufunguka kwa ile mialamala,” Alisema.

Hadi kufikia tarehe 23.9.2019 mapato ambayo hayajawasilishwa (defaulters) kwa Manispaa ya Sumbawanga ni shilingi 45,454,992,68, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni Shilingi 695,288,837.45, Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ni Shilingi 255,883,853.32 na Halmashuri ya Wilaya ya Nkasi ni Shilingi 220,722,407.40.

Naibu Waziri Ikupa Aipongeza JAMAFEST Kushirikisha Wenye Ulemavu

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye
Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).

Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu),
Mhe. Stella Ikupa, Akikabidhi baiskeli ya watu wenye mahitaji maalum kwa Bw.
Martine Vicent Mkazi wa Wilaya ya Kigamboni mara baada ya kumaliza kutembelea
mabanda katika Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).

Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye
Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akizungumza na Waandishi Wa Habari (hawapo pichani) Mara baada ya kutenmbelea mabanda katika Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).

Eric Msuya – MAELEZO, Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amelipongeza Tamasha la Utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) kwa kuwazingatiaa watu wote wenye mahitaji Maalumu kwa kuwapa kipaumbele katika Tamasha hilo.

Ameseyasema hayo leo, mbele ya Waandishi wa Habari, mara ya baada ya kutembelea Mabanda na kujionea ubufunifu mbalimbali ya maonyesho ya Tamasha la JAMAFEST, linaloendelea kufanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Amewapongeza Waandaji wa Tamasha la JAMAFEST kwa kuwapa kipaumbele watu wenye Ulemavu katika kuwapatia mabanda, kwa ajili ya kuuza na kuonyesha bidhaa zao katika Tamasha hilo na kuweza kutangaza biashara zao

“Nitoe Pongezi kwa Waandaji wa Tamasha hili la JAMAFEST, Muitikio wa watu umekuwa mkubwa hasa kwa kundi la watu wenye ulemavu, nimejionea vitu vingi vinavyotengenezwa na walemavu, bidhaa zao ni nzuri kabisa na zipo kwa viwango vya juu sana” Alisema Mhe. Stella Ikupa

Sambamba na hilo Mhe Ikupa Amewataka Watanzania kufika katika Viwanja vya Taifa kujionea bidhaa mbalimbali za kiutamaduni zinazo tengezwa na Watanzania ili waweze kujua Utamaduni wa Watanzania na Wanaafrika Masharikikwa ujumla.

Pia Mhe. Ikupa amewasisistiza Watanzania kutumia muda wao mwingi kujionea mambo mbalimbali ya Utamaduni yanayo fanyika katika Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST

“Ukifika kwenye Tamasha hili la JAMAFEST hautajuta kupoteza huo muda wako, ila utakuwa umepata kitu kikubwa cha kujifunza juu ya Utamaduni wa Muafrika” Alisema Mhe. Stella Ikupa

Aidha katika Ziara hiyo Mhe. Ikupa amewakabidhi baiskeli za watu wenye mahitaji maalum ndugu Martini Vicente mkazi wa Kigamboni na Ndugu Rajabu Ismail mkazi wa Magomeni- Mwembe Chai ambao wote ni Walemavu wa Miguu.

Mashindano ya kuogelea ya Masters kufanyika Jumamosi

$
0
0

Mashindano ya Taifa ya kuogoelea kwa waogeleaji wakubwa (Masters swimming championships) yatafanyika Jumamosi (Septemba 28) kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Sekondari ya Shaaban Robert.

Mashindano hayo yatajumisha waogeleaji wenye umri kuanzia miaka 25 na zaidi yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji mbalimbali wa mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), Asham Hilal alisema jana kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na kumalizika saa 11.00 jioni na leo ndiyo mwisho wa kuthibitisha.

Asmah alisema kuwa kila muogeleaji anatakiwa kulipa ada ya ushiriki kwa mujibu wa sheria ambapo waogeleaji ambao watafanya vyema watapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kanda ya tatu hapo baadaye.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na kuna mwitikio mkubwa kutoka kwa waogeleaji mbalimbali. Ni mashindano ya wazi ambapo mtu, au klabu zinaruhusiwa kushiriki,” alisema Asmah.

Alisema kuwa katika mashindano yaliyopita, klabu ya Taliss-IST illibuka katika nafasi ya kwanza. Mpaka sasa klabu hiyo imethibitisha kuwakilishwa na jumla ya waogeleaji 24 ambao kwa sasa po mazoezini chini ya kocha, Alexander Mwaipasi.

Alisema kuwa sheria za shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) zitatumika katika mashindano hayo ambapo waoegeaji wamegawanywa katika makundi ya miaka tofauti.

Makundi ya miaka hiyo ni 25 mpaka 29, 30 – 34, 35 – 39, 40 – 44, 45 – 49, 50 – 54, 55 – 59, 60 – 64, 65 – 69, 70 – 74, 75 – 79, 80 – 84, 85 – 89 na waogeaji wenye miaka kati ya 90 mpaka 94.

Mbali ya staili za butterfly, backstroke, Individual Medley, freestyle, breaststroke, waogeleaji pia watashindana katika ‘relay’ mbalimbali.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NGUZO ZA UMEME CHA QWIHAYA MJINI MAFINGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua nguzo za umeme zilizorundikana kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company LTD cha Mafinga zikisubiri wanunuzi. Kiwanda hicho cha nguzo kilitembelewa na Waziri Mkuu, Septemba 26, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Leonard Mahenda, wa tatu kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Fred Ngwega na wa nne kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
Nguzo za umeme zikiwa kwenye mtambo wa kuziwekea dawa maalum ya kuzifanya zisishambuliwe na wadudu au kuungua moto zikiwa katika kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, September 26, 2019
Baadhi ya nguzo za umeme zilizorundikana zikisubiri wanunuzi kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 26, 2019. {Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA TAASISI YA UTAFITI NA SERA YA SHEIKH SAUD AL QASIMI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi Ndg,Natasha Ridge (kushoto) akimkabidhi kitabu Maalumu cha Mitaala ya Elimu utoaji wa mafunzo ya kitaalamu ya kuwajengea uwezo walimu kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati ujumbe wa Taasisi hiyo ulipofanya mazungumzo na Rais Dk.Shein na Ujumbe wake katika Hotel ya Waldorf Astoria Ras Al Khaimah.
Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika Mkutano maalumu na Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi nchini Ras Al Khaimah (U.A.E) ambapo wapo nchini humo na Mheshimiwa Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa Ziara maalumu ya siku saba (kuyshoto) Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh.Mohamed Ramia Abdiwawa,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi Gavu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh.Said Hassan Said na Waziri wa Ardhi,Ujenzi,Maji na Nishati Mh.Salama Aboud Talib
Washiriki wa Mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh.Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) wakiwa katika mkutano ambao ulijadili kwa kina Masuala ya Elimu kwa pande zote mbili katika Ukumbi wa Hotel ya Waldorf Astoria Ras Al Khaimah.
Washiriki wa Mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi ya Sera na Utafiti ya Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh.Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakiwa katika mkutano ambao ulijadili kwa kina Masuala ya Elimu kwa pande zote mbili katika Ukumbi wa Hotel ya Waldorf Astoria Ras Al Khaimah.

Picha na Ikulu

MTENDAJI MKUU MAHAKAMA AKAGUA MIRADI YA UJENZI MAHAKAMA LINDI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga(wa pili kulia) akimweleza jambo Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Bw. Joseph Chota wa (kwanza kulia).
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga ( wa kwanza ) na kulia ni Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi , Mhe. James Karayemaha na kushoto (aliyevaa kofia) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha, wakikagua kiwanja cha ambacho kinatarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (aliyenyoosha mkono) akiwa na wahandisi, wakiwemo viongozi wengine wakikagua ramani ya kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Kushoto ni Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. James Karayemaha.


Muonekano wa mbele wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga(kulia) akikagua ramani ya Mahakama ya Wilaya Kilwa.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (katikati) akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akikagua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kilwa.

(Picha na Hillary Rory – Lindi)

MATUKIO KATIKA PICHA: MKUTANO WA WAWEKEZAJI, WAFANYABIASHARA – MTWARA, LINDI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (katikati) na Waziri wa Madini Doto Biteko wakielekea kwenye mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa (katikati) na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (kushoto) wakifuatilia hoja mbalimbali za wafanyabiashara na wawekezaji wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Lindi. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mbunge wa Mtwara vijijini Hawa Ghasia akichangia jambo wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. Lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao.
Mfanyabiashara wa matunda mkoani Mtwara Hamis Mfaume akieleza changamoto zinazomkabili katika biashara yake wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani humo.
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoani Lindi, Mariam Mfunda akieleza changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu katika shughuli zao za uzalishaji wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani humo.
Meneja wa Usajili wa Walipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu, Rehema Shao akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

BODI YA NYAMA:NI MARUFUKU MAGARI YENYE KUTU KUBEBA NYAMA.

$
0
0



Imani Sichalwe Kaimu Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania akizungumza katika Maonyesho ya Teknolojia za Uchakataji wa nyama Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus Arusha.

Bodi ya Nyama nchini imepiga marufuku matumizi ya magari yenye kutu katika kubeba nyama kwani kutu ni hatari kwa afya ya binadamu hivyo amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa watakaokahidi agizo hilo.

Imani Sichalwe ni Kaimu Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania akizungumza katika Maonyesho ya Teknolojia za Uchakataji wa nyama yaliyohudhuriwa na Wanachama wa Chama cha Wachinjaji na Wafanyabiashara wa nyama jijini Arusha ,amesema wamechukua hatua hiyo ili kulinda ubora wa nyama na kulinda afya za walaji kwa kihakikisha magari yenye kutu hayataruhusiwa kubeba nyama pamoja na ubebaji wa nyama mgongoni.

Alex Lasiki ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachinjaji ameiomba serikali isogeze mbele katazo hilo la kutumia vigogo vya miti kukata nyama na kuweka mashine za kukata nyama kwani wachinjaji wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji midogo ili waweze kujipanga kununua mashine za kisasa.


Ismail Kulanga ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha amesema kuwa jiji la Arusha litashirikiana na machinjio ya Arusha Meat ili kuboresha mazingira ya machinjio hayo na kuhakikisha huduma bora zinatolewa.
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images