Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Tanga Fresh yamwaga maziwa katika shule saba Manispaa ya Kinondoni

$
0
0
Meneja wa Ufundi wa Bodi ya Maziwa, Deogratius Mlay akitoa maelezo kuhusiana na maadhimisho ya unywaji wa maziwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Mauzo wa Tanga Fresh, Protas Kimario akitoa maelezo namna ya Tanga Fresh inavyhamasisha unywaji wa maziwa katika shule na umhimu wa maziwa hayo katika shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi. 
 Afisa Lishe wa Manispaa ya Kinondoni Emiliana, Daud akizungumza na wanafunzi katika maadhimisho ya unywaji wa maziwa shuleni duniani ambapo Tanga Fresh imegawa maziwa katika shule za msingi saba za manispaa hiyo.

Wanafunzi wakipewa maelezo katika wiki ya unywaji wa maziwa.
 Wanafunzi wakigaiwa maziwa katika maadhimisho ya unywaji wa maziwa.
 Wanafunzi wakinywa maziwa katika wiki ya unywaji wa maziwa 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SHULE za Msingi Saba katika jiji la Dar es Salaam zimeadhimisha maadhimishisho ya wiki ya unjwaji wa maziwa shule ikiwa ni kujenga watoto kuwa na afya bora.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi Meneja wa Ufundi wa Bodi ya Maziwa Deogratius Mlay amesema kuwa unywaji wa maziwa unatakiwa kuwa endelevu kwani ni shule 25 ndio zina program za unywaji wa maziwa shuleni.

Amesema kuwa bodi ya maziwa imekuwa na mikakati ya kuhakikisha jamii inatengeneza mazingira ya unjwaji wa maziwa pamoja na bidhaa za maziwa katika kujenga afya bora na kuweza kuzalisha mali kwa maendeleo ya taifa.

Aidha amesema kuwa bodi na utaratibu wa kwenda katika mabaraza ya shule katika kuweka kipaumbele cha unjyaji wa maziwa shuleni kwa kutoa fedha kwa watoto kwa ajili ya maziwa.

Amesema kuwa mtu anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka lakini unjwaji huo uko chini hivyo jamii ijenge mazingira ya kunywa maziwa hayo .

Kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh ndio imekuwa ikitoa pakiti moja kwa kila mtoto ikiwa ni kuadhimisha unywaji wa maziwa shule saba hizo.

TFS YAWASISITIZA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI KUTEMBELEA HIFADHI ZA MISITU YA ASILIA

$
0
0
 Ofisa wa Misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)John Selestine (katikati)akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Wakala huo lililopo katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam waliotembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Tamasha la JAMAFEST wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Misitu wa Wakala huo John Selestine.
 Baadhi ya mabango ya matangazo ya hifadhi za misitu ya asili iliyopo nchini yaliyopo katika Banda la TFS katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe(kulia) akizungumza katika tamasha la JAMAFEST ambapo amesisitiza wananchi kujikita kufuga nyuki ili kupata asali na mazao yake 
 Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe akisisitiza jambo wakati anazungumzia umuhimu wa wananchi kujikita katika ufugaji Nyuki nchini.
Ofisa Nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Juma Mdoe  (anayeandika) akiwa na Ofisa wa Misitu wa Wakala huo John Selestine kwenye banda lililopo katika tamasha la JAMAFEST

Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umewasisitiza Watanzani kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za mazingira ya asili yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini kwetu ambako kunavivutio vya utalii ambavyo vingine havipatikani mahali pengine kokote.

Kwa kutambua umuhimu wa kutangaza hifadhi hizo na vivutio vyake, TFS imeamua kupiga kambi katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa za Nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST)linaloendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa wa Misitu kutoka wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania John Selestin amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza rasilimali za hifadhi za misitu ya asili nchini na kuongeza katika eneo la Urithi wa dunia wao wanajivunia uwepo wa misitu ya  hifadhi ya asili ambayo ni sehemu ya urithi.

"Katika urithi wetu tunajivunia uwepo wa misitu ya hifadhi za mazingira ambayo inapatikana katika maeneo mbalimbali nchini . Katika misitu yetu ya asili kuna mimea na viumbe ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote zaidi ya kwetu Tanzania,"amesema Selestine na kuongeza kuwa uasili wa misitu hiyo unatokana na viumbe na mimea ya asili iliyomo.

Ameongeza kuwa TFS katika urithi wa dunia wapo katika tamasha hilo kwa ajili ya kuelezea na kutangaza misitu ya hifadhi ya mazingira asilia  ambayo imezaliwa kutokana na misitu ya hifadhi ambayo wanaisimamia na hiyo  misitu iliyotokana na tafiti mbalimbali kubaini kuna mimea na viumbe ambavyo havipatikani mahali kokote duniani.

"Uwepo wa viumbe na mimea ambavyo havipatikana kokote ndio imesababisha tuwe na urithi na kufanya misitu hiyo ya pekee .Tunawaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kutembelea misitu hiyo ya hifadhi ya mazingira ya asili ambayo nchini kwetu ipo 17,"amesema.

Amefafanua kuna maeneo mengi ya hifadhi ya mazingira ya asili ikiwemo, Amani, Magamba, Chome na Pugu.Ndani ya misitu hiyo kuna vivutio vya utalii kwani kuna mimea na viumbe vya asili ambavyo vipo kwenye hifadhi hizo. 

Pia kuna maporomoko ya Kalambo mkoani Rukwa pamoja na Ziwa Ngozi ambalo limetokana na kreta na ziwa hilo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika ambayo yanatokana na kreta.

"TFS ambayo ndio wasimamizi wa hifadhi za  misitu na rasilimali za misitu, ukweli misitu hiyo bado imeonekana inausili na vivutio mbalimbali ambavyo ni vya urithi.Tunatoa mwito kwa wananchi kujenge utaduni kutembelea hifadhi ya misitu ya mazingira ya asili,"amesema.

Kwa upande wake Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe ametumia tamasha hilo kuendelea kuhamasisha wananchi kujikita katika ufugaji nyuki na mazao yake kwani kuna faida nyingi ikiwemo ya kipato.

"Pamoja na kusimamia usimamizi na kuendeleza rasilimali za misitu bado wakala wetu  umejikita katika ufugaji wa nyuki na mazao yake ikiwa pamoja na kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi kufuga nyuki kwani kuna faida nyingi,"amesema.

Mdoe ametumia nafasi hiyo kueleza mazao yatokanayo na ufugaji nyuki yamekuwa yakiingiza kipato kikubwa kwa wafugaji na kwa taifa kwa ujumla, hivyo ametoa rai kwa wananchi kujihusisha na ufugaji nyuki.

NAIBU WAZIRI KANYASU ATAKA WATENDAJI TFS KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA MISITU

$
0
0
Naibu Waziri Maliasili na Utalii na Mgeni Rasmi, Costantine Kanyasu,  katika kikao cha watendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) akiwasisitiza watendaji wa TFS (hawako pichani) kushirikiana na wadau mapema leo Septemba 25, 2019 jijini Dodoma.
 Ofisa Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mariam Kobero (wa kwanza kushoto) akiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo wakifuatilia kikao Mjini Dodoma.

Ofisa Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mariam Kobero (wa kwanza kushoto) akiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo wakifuatilia kikao Mjini Dodoma.

Na Ripota Wetu, Michuzi TV- Dodoma 
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantantine Kanyasu amewataka watendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kushirikiana na mamlaka za Serikali za mitaa, sekta binafsi na jamii katika kusimamia misitu.

Kanyasu ametoa kauli hiyo leo Septemba 25, 2019 mjini Dodoma wakati akifungua kikao maalumu cha utendaji ambacho kimewakutanisha pamoja viongozi wa TFS kuanzia makao makuu hadi katika ngazi ya wilaya.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 25, 2019 wakati wa ufunguzi wa kikao maalumu cha utendaji kilichowakutanisha pamoja viongozi wa TFS kuanzia makao makuu hadi katika ngazi ya wilaya, Kanyasu amesema rasilimali za misitu zinategemewa kwa kiasi kibwa na jamii lakini usimamizi wake unahusisha mamlaka za Serikali za mitaa, sekta binafsi na jamii kwa jumla. 

“Mtawanyiko huu wa usimamizi unatoa changamoto mbalimbali ambazo zinaonesha umuhimu wa kushirikiana kiutendaji na kisera. Mathalani ushirikiano wa Maofisa misitu (DFOs) walioko katika halmashauri zetu na ninyi mameneja wa Wilaya (DFMs) ni jambo ambalo wakati wote linapaswa kutiliwa mkazo. 

“Wote mnasimamia misitu kama rasilimali ya taifa hakuna haja ya kutafuta nani aliye mkubwa wa mwenzie. Ni lazima DFMs na DFOs muheshimu mgawanyo wa majukumu yenu kama yalivyobainishwa katika mwongozo wa usimamizi wa misitu nchini, “anasema Kanyasu.

Aidha amesema Serikali ya awamo ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Magufuli imeweka msisitizo mkubwa katika uhifadhi na maendeleo ya viwanda. Msukumo ambao unalenga kuleta ukombozi wa uchumi kwa wananchi kupitia ajira za viwandani na kuongeza thamani ya mazao.

Kanyasu anasema ni vizuri jitihada za uhifadhi zikatangulia na kuungwa mkono na wananchi wote ili viwanda vipate kushamiri. “Na hii inamaanisha lazima kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake. Hapa kwenye misitu wote wenye dhamana wasimamie rasilimali misitu kwa weledi na umahiri wa hali ya juu,”. 

Naibu Waziri huyo anasisitiza kuwa bila hifadhi thabiti ya misitu viwanda vitashindwa kufanya kazi yake sawasawa kutokana na uhusiano wa misitu na upatikanaji wa maji/mvua, uhusiano wa misitu na mabadiliko ya tabia ya nchi, uhusiano wa upatikanaji wa maji na uzalishaji wa umeme unaotumika viwandani na majumbani, na uhusiano wa mvua na maendeleo ya sekta ya kilimo na mifugo nchini.

Kwa upande wake Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos Silayo anasema TFS imejengea mtandao wa usimamizi wa misitu katika maeneo yote nchini. 

Hivyo kwa kukutana mameneja wa kanda, mameneja wa mashamba, wakuu wa vitengo na Mameneja wote wa Misitu wa Wilaya (DFMs) leo kutasaidia kuleta pamoja fursa za kujadili mafanikio na changamoto za sekta ya misitu.

“Tunategemea kikao kazi hiki chenye wajumbe 210 kitatumika kama hatua muhimu ya kufikia malengo ya usimamizi wa misitu kwa kukumbushana wajibu wa kila mtumishi katika eneo lake kupokea changamoto zinazojitokeza field na kuweka mkakati wa namna ya kuimarisha utendaji wetu katika ngazi zote za wakala ili kufikia malengo yetu na ya serikali kwa jumla,” anasema Prof. Silayo.

DAWASA DAR YATAHADHALISHA WAHUJUMU WA MAJI, YASEMA ATAKAYEBAINIKA FAINI YAKE SHILINGI MILIONI TANO HADI 50

$
0
0
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) imesema watu wote waliojiunganishia maji kwa njia za panya wajitokeze kwenye mamlaka hiyo kwani wakifikiwa faini yake ni sh.milioni tano hadi sh.milioni 50.

Hayo ameyasema  Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo amesema operesheni hiyo ni endelevu kwa mikoa yote ya Dawasa kutembelea miundumbinu ya maji.

Amesema kuwa operesheni hiyo itakuwa inakwenda kila mkoa na kuwataka wananchi waliojiunganishia maji wajitokeze katika ofisi za Dawasa kufanya utaratibu wa kuunganishwa katika mfumo.

 Zawayo amesema miundombinu ya maji katika maeneo ya Kawe na Msasani wananchi wakitumia maji kwa njia ya udanganyifu na kusababisha hasara kwa wateja halali waliounganishwa na wanaolipa bili.

 Aidha  amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ni vyema wanaohujumu miundombinu hiyo wakaacha mara moja kabla ya hatua kali za kisheria dhidi yao hazijachukuliwa.

Zawayo amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa wa kuhujumu miundombinu ya maji amekamatwa na atafikishwa mahakani na sheria itafuatwa ili liwe fundisho kwa wengine na wazitumie ofisi za mamlaka hiyo kwa kupata huduma ya maji na sio kuhujumu huduma hiyo kwa wateja ambao wameshalipia huduma zao.

"Tutashughulika  na  wale wote ambao wanahujumu miundo mbinu ya maji na hatutawafumbia macho maana wanasababisha hasara kubwa kwenye mamlaka hiyo kwa kuhudumia maji ambayo hayalipiwi bili" Amesema Zawayo

Amesema kuwa adhabu kwa wahujumu wa miundombinu hiyo ya maji ipo palepale, yaani faini  kuanzia shilingi milioni tano hadi hamsini, na amewashauri wananchi kuwa waaminifu ili kutokutwa na kadhia hiyo.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa maofisa wa  DAWASA mara baada ya kupatikana kwa mambomba ya maji yaliyokuwa yameunganishwa kinyemela  wakati ukaguzi wa miundombinu ya wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila(kulia) akimuonesha sehemu ya maungio ya maji yaliyokuwa yanaunganishwa kinyemela kwa Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(wa pili kushoto) wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Fundi wa DAWASA akipasua sakafu kwa ajili ya kukagua bomba la maji ya Mamlaka hiyo kwenye moja ya nyumba iliyosemekana kuna wizi wa maji wakati wa zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Mita ya DAWASA iliyokutwa ndani ya jiko la Mteja kabla ya kuvunjwa na kujua kama kuna wizi wa maji wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Mita mara baada ya kuvunja sakafu na kujionea wizi mkubwa wa maji ya DAWASA ndani ya jiko la mteja wa Mamlaka hiyo leo wakati wa kukagua miundombinu ya maji katika maeneo ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mabomba ya maji yalivyopita kwenye kuta pamoja na sakafuni  yaliyoleta sintofahamu kwenye nyumba hiyo yakiwa yametinduliwa wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Mfanyakazi wa DAWASA akikagua mabomba yanayoingiza na kutoa maji kwenyw kisima kilichokutwa kwenye moja ya nyumba kwenye mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya DAWASA.
Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa miundo mbinu ya Mamlaka hiyo katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe jijini Dar es Salaam.

HDIF YANUFAISHA WABUNIFU ZAIDI YA SH. BILIONI 50 NCHINI

$
0
0
ILI kuwapa nguvu wabunifu nchini mfuko wa ubunifu kwa maendeleo ya watu wa Uingereza (HDIF) umetoa zaidi ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya ubunifu.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkaazi wa HDIF, Joseph Manirakiza, wakati akizungumza na wadau mbalimbali kutoka serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali.

Manirakiza amesema tangu mfuko huo uanzishwe mwaka 2014, jumla ya miradi 43 imesaidiwa ambayo gharama yake ni zaidi ya shilingi bilioni 50 za kitanzania.


“Lengo ni kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika kuwanyanyua wabunifu, zipo sekta nyingi ambazo zinatuhusu ili kuweza kushirikiana nayo,” alisema Manirakiza.


Kwa upande wake mkurugenzi wa tume ya sayansi na teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu amesema serikali imeamua kukutanisha wadau kutoka wizara nne tofauti ili kuweza kujadiliana na kuzungumzia sera.

Dk. Nungu alisema, “wadau wa sekta hizo wanakutanishwa pamoja kwa lengo la kujadiliana na kuzungumzia sera, kwani ni mara ya kwanza tangu kukutana.”


Naye mwakilishi wa baraza taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Gwakisa Bapala, alisema wao ni wadau ambao wanashirikiana na HDIF ili kuwawezesha na kuwainua wananchi kiuchumi.

Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe, alisema kupitia mradi wa HDIF wilaya yake imefanikiwa kujenga zaidi ya vyoo 20 vya ubunifu.

“Vyoo ambavyo vinajengwa wilayani kwangu kupitia mfuko huo, vinabana matumizi ya maji kwani maji yanayotumika ni kidogo na mtu anakuwa msafi….hii ni mojawapo ya ubunifu mkubwa uliofanywa wilayani kwetu,” alisema Mh. Gondwe.

 Mtaalamu wa mawasiliano wa Human Development Innovation Fund ( HDIF) bi Hannah Mwandoloma akikaribisha washiriki wa warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkurugenzi Mkazi wa HDIF Be Joseph Manirakiza akitoa mada juu ya ubunifu katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC
 Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkuubwa wilaya ya Handeni Be Godwin Gondwe akiwasilisha mada katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la Shule Direct Bi.Faraja Nyalandu akielezea jinsi ubunifu wa shirika lake lilivyo saidia wanafunzi na walimu was Tanzania katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Washiriki wakifuatilia madabzilitolewa na wawasilishaji katika Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya siku moja ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mtaalamu wa mawasiliano akiwasilisha Jambo kwa washiriki wa warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC
Washiriki toka wizara mbali mbali na taasisi za serikali pamoja na baadhi ya wagunduzi wa miradi iliyofadhiliwa na HDIF Wakisikiliza mada katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC

KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUCHANGIA UCHUMI-MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Alhaj Alfan Ally wa Darasa la Tatu katika Shule ya Msingi ya Viziwi ya mjini Iringa, zawadi ya shilingi laki moja baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa Shindano la Uandishi wa Insha kuhusu Wiki ya Maziwa wakati alipohutubia katika kilele cha wiki hiyo kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Septemba 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Mchekeshaji Mai Zumo mmoja wa Mabalozi wa wanaohamasisha unywaji wa maziwa ha kwa watoto mashuleni kupitia Kampuni ya ASAS, alipotambulishwa huku akiwa amebebwa na baba yake mzazi Zumo. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa mgeni rasmi kaaika kilelele cha wiki ya Maziwa kwenye uwanja wa Mwembetogwa mini Iringa Septemba 25, 2019. Kulia ni Mama Mzazi wa Mai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli itaendelea kuhakikisha kuwa kilimo, ufugaji na uvuvi unakuwa wa kisasa na wenye tija kwa wananchi sambamba na kutoa mchango unaostahili katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Katika kuhakikisha azma hiyo ya Serikali inafikiwa, nitoerai kwa wafugaji nchini kuunda ushirika imara utakao wawezesha kupata huduma mbalimbali za mifugo na ushirika huo pia ulenge katika kuboresha uzalishaji na ukusanyaji wa maziwa, upatikanaji wa masoko pamoja na kuongeza kiasi cha usindikaji viwandani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 25, 2019)kwenye Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa mijini Iringa. “Unywaji maziwa shuleni si tu ni muhimu lakini pia inatoa msukumo wa kuboresha afya zetu hususan za watoto shuleni kupitia unywaji wa maziwa.”

Amesema wataalamu wa lishe wanashauri kula chakula bora kinachokuwa na viini lishe vyote muhimu kama wanga, protini, vitamini, madini, mafuta na maji ya kutosha. Hata hivyo, ili kupata chakula bora, wananchi wanapaswa kuchanganya vyakula vya aina nyingi katika mlo mmoja.

Waziri Mkuu amesema kutokana na umuhimu huo, ndiyo maana watalaamu wa lishe wanashauri kuwa mtoto apate glasi moja ya maziwa katikati ya siku itakayompatia lishe ya kutosha hadi atakapomaliza masomo yake kwa siku hiyo. “Kwa bahati mbaya hapa nchini, watoto wengi huondoka asubuhi kwenda shuleni bila kupata chakula chochote. Aidha, shuleni nako mara nyingi hawapati chakula na hivyo hukosa usikivu mzuri katika masomo yao.”

Zaidi ya nchi 70 duniani ikiwemo Tanzania zinaadhimisha siku ya unywaji maziwa na tayari zilishaanzisha mpango wa unywaji maziwa shuleni kwa watoto wao, lengo ni kuhakikisha mtoto anapata lishe kamili na anakuwa na usikivu mzuri katika masomo yake. Mtoto amelengwa kwa sababu ni kundi ambalo ni muhimu katika kujenga Taifa lililo bora na anatarajiwa kurithisha vema vizazi vijavyo.

“Nimearifiwa kuwa hapa nchini programu ya unywaji maziwa shuleni ilianza kutekelezwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Dar es Salaam na Njombe ambapo shule 40 na wanafunzi 34,561wamenufaika katika kunywa maziwa lita 631,860 ambayo yamekuwa yakitolewa kwa ushirikiano na Serikali, wazazi, wafadhili mbalimbali na wasindikaji wa maziwa. Lengo kuwafikia wanafunzi wote.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia ya dhati ya kufanya mpango huu uwe wa kitaifa. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na wadau wengine itaendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa katika shule zetu hapa nchini. Juhudi hizi zitakwenda sambamba na kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 2.7 zinazozalishwa sasa kwa mwaka mpaka lita bilioni saba kwa mwaka ifikapo 2020.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafugaji wa Iringa kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika. “Nitoe wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinawezesha na zinasimamia uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia kuimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.”

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Maafisa wa Serikali, wadau wa mazima pamoja na wananchi.


ASKOFU MKUU YUDA THADEUS RUWA'ICHI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI MOI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019. Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu. Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea. PICHA NA ISSA MICHUZI

MKULIMA AISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mkulima wa Korosho mkazi wa Kata ya Michenjele Mzee Musa Chuma Ndembo ameishukuru Serikali kwa kusimama kidete hadi kuhakikisha analipwa madeni yake. 

Mzee Ndembo ameyasema hayo mara baada ya kulipwa madeni ya fedha za Korosho aliyokuwa akidai kwa chama cha msingi cha Michenjele ambacho alisumbuka nacho kwa zaidi ya miezi 5 akitafuta haki yake na kutokupata hadi pale suala lake alipolipeleka ngazi za Serikali.

*"Nimeteseka kwa zaidi ya miezi mitano nikikidai chama cha msingi pasipo mafanikio lakini ndani ya wiki moja tu tangu nilipofikisha suala langu kwa Afisa Tarafa Mihambwe nimelipwa fedha zangu. Naishukuru sana sana Serikali."* Alisema Mkulima Mzee Ndembo

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ya fedha Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ambaye alikuwa shuhuda na msimamizi wa haki ikitendeka amesema kazi ya Serikali ni kuhakikisha kuna haki na usawa ndani ya jamii na hakuna Mtu yeyote yule atakayeonewa.

*"Serikali ipo na inaendelea kusimamia haki ikitendeka kwa jamii. Natoa Rai kwa Viongozi wa vyama vya Msingi kuacha kuwasumbua, kuwanyanyasa na kutaka kuwadhulumu Wakulima. Nawasisitiza Amcos wote wenye madeni ya Wakulima mfanowe Mzee Ndembo na wengineo wawalipe mara moja kujiepusha matatizo na vyombo vya sheria."* Alisisitiza Gavana Shilatu

Makabidhiano hayo yamefanyanyika ofisi ya Mtendaji kata Michenjele na kuhudhuliwa na chama Cha Msingi, Mkulima Mzee Ndembo na Mkewe pamoja na Mtendaji kata. 
Mzee Musa Ndembo akitia saini ya dole gumba kukiri kupokea fedha zake Leo Jumatano Septemba 25, 2019 tukio likishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu, Mtendaji kata Michenjele Shazir Hamis, Mke wa Mzee Ndembo (hayupo pichani) na wa Michenjele Amcos (hawapo pichani) katika ofisi ya Mtendaji kata Michenjele.Viongozi

VIJANA JITOKEZENI KUGOMBEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA-DC KIGAMBONI

$
0
0
MKUU wa wilaya Kigamboni Sarah Msafiri amewataka vijana wa wilaya hiyo kujitokeza kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiwaeleza kuwa uchaguzi huo si wakuunda Serikali bali ni wa kumsaidia majukumu Dkt John Magufuli .

Amesema kuwa Serikali tayari ipo Madarakani ambayo imetokana na Chama cha Mapinduzi CCM hivyo nivema wakajitokeza kugombea na si kuwaachia akina Baba tu.

Sarah ameyasema hayo jana Wilayani humo wakati akizungumza na wananchi wa tarafa ya Somangila kuhusu kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kupitia Manispaa hiyo ya Kigamboni .Amewaeleza kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mtaa hivyo vijana ,na akinamama wajitokeze kugombea ili kuweza kupata nafasi za uongozi .

Kuhusu fidia kwa baadhi ya Wananchi kupitia mradi wa Temeke Sarah alisema mwenzi octoba mwaka huu Waziri wa Ardhi William Lukuvi atakuja kuzungumzia fidia hiyo.
Amesema anatambua kuwa kuna wananchi ambao walitakiwa wapatiwe fidia kutokana na maeneo yao kuchukuliwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.mbalimbali hivyo Waziri Lukuvu atakuja kutolea ufafanuzi

Akizungumzia fursa za mikopo Wilayani humo Sarah alisema Manispaa imejipanga kikamilifu kutoa fursa za mikopo nakwamba Serikali imeshatoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na akina mama.Amesema mikopo hiyo ipo na Mwezi ujao wataaza kutoa mikopo hiyo hususani kwa wale wenye vigenzo na mikopo hiyo itakuwa na riba nafuu sana kulingana na kiwango cha Fedha atakachochukuwa.ambapo hautazidi shilingi 2000.

Pia Mkuu wa wilaya Sarah akizungumzia Miundombinu ya barabara amesema Serikali inatambua changamoto hiyo na mpango kabambe upo tayari kwa ajili kutengeneza barabara.Amesema kuwa Serikali ya Wilaya nimeshaweka mpango mkakati wa muda mfupi ili kuweza kutatua sehemu ya changamoto za barabara hizo ili kuepusha kujitokeza kwa Mafuriko kama ilivyo sasa.

Pia Sarah amewaeleza wananchi hao kuwa Wilaya imetenga hekari nne kwa ajili ya Wananchi kufanya biashara mbalimbali wakiwamo mama lishe,wauza vinywaji baridi ambavyo si vileo hivyo wajitokeze kupeleka Maombi yao ili kuweza kupata nafasi hiyo.

Kwaupande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kigamboni OCD John Makuri aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali ya mitaa.

Amesema nivema wakajiepusha ma masuala ya uovu na badala yake waendelea kudumisha ,kulinda amani iliyopo na kwamba yeyote atakayejihusisha na vitendo viovu hatua Kali dhidi yake zitachukuliwa.
Mkuu wa Wilaya Kigamboni,Sarah Msafiri akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Somangila leo kuhusu vijana kujitokeza kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.hayo yalizungumzwa na Mkuu wa Wilaya katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,John Makuri akizungumaza leo na wananchi wa Tarafa ya Somangila Wilaya ya Kigamboni kuhusu kuendelea kulinda amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali ya mitaa.
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Muhando akizungumza wakati akizungumza wakati alipokuwa akitambulisha sehemu ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya hiyo katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUCHANGIA UCHUMI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli itaendelea kuhakikisha kuwa kilimo, ufugaji na uvuvi unakuwa wa kisasa na wenye tija kwa wananchi sambamba na kutoa mchango unaostahili katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Katika kuhakikisha azma hiyo ya Serikali inafikiwa, nitoerai kwa wafugaji nchini kuunda ushirika imara utakao wawezesha kupata huduma mbalimbali za mifugo na ushirika huo pia ulenge katika kuboresha uzalishaji na ukusanyaji wa maziwa, upatikanaji wa masoko pamoja na kuongeza kiasi cha usindikaji viwandani. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 25, 2019)kwenye Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa mijini Iringa. “Unywaji maziwa shuleni si tu ni muhimu lakini pia inatoa msukumo wa kuboresha afya zetu hususan za watoto shuleni kupitia unywaji wa maziwa.”

Amesema wataalamu wa lishe wanashauri kula chakula bora kinachokuwa na viini lishe vyote muhimu kama wanga, protini, vitamini, madini, mafuta na maji ya kutosha. Hata hivyo, ili kupata chakula bora, wananchi wanapaswa kuchanganya vyakula vya aina nyingi katika mlo mmoja.

Waziri Mkuu amesema kutokana na umuhimu huo, ndiyo maana watalaamu wa lishe wanashauri kuwa mtoto apate glasi moja ya maziwa katikati ya siku itakayompatia lishe ya kutosha hadi atakapomaliza masomo yake kwa siku hiyo. “Kwa bahati mbaya hapa nchini, watoto wengi huondoka asubuhi kwenda shuleni bila kupata chakula chochote. Aidha, shuleni nako mara nyingi hawapati chakula na hivyo hukosa usikivu mzuri katika masomo yao.”

Zaidi ya nchi 70 duniani ikiwemo Tanzania zinaadhimisha siku ya unywaji maziwa na tayari zilishaanzisha mpango wa unywaji maziwa shuleni kwa watoto wao, lengo ni kuhakikisha mtoto anapata lishe kamili na anakuwa na usikivu mzuri katika masomo yake. Mtoto amelengwa kwa sababu ni kundi ambalo ni muhimu katika kujenga Taifa lililo bora na anatarajiwa kurithisha vema vizazi vijavyo.

“Nimearifiwa kuwa hapa nchini programu ya unywaji maziwa shuleni ilianza kutekelezwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Dar es Salaam na Njombe ambapo shule 40 na wanafunzi 34,561wamenufaika katika kunywa maziwa lita 631,860 ambayo yamekuwa yakitolewa kwa ushirikiano na Serikali, wazazi, wafadhili mbalimbali na wasindikaji wa maziwa. Lengo kuwafikia wanafunzi wote.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia ya dhati ya kufanya mpango huu uwe wa kitaifa. Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na wadau wengine itaendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa katika shule zetu hapa nchini. Juhudi hizi zitakwenda sambamba na kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 2.7 zinazozalishwa sasa kwa mwaka mpaka lita bilioni saba kwa mwaka ifikapo 2020.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafugaji wa Iringa kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika. “Nitoe wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinawezesha na zinasimamia uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia kuimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.”

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Maafisa wa Serikali, wadau wa mazima pamoja na wananc




















Naibu Waziri Kijaji: Serikali Imedhamiria kutatua kero za Wafanyabiashara Nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji hao kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdeme akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa uwekezaji mkoani humo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki na Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mussa Sima.
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Ruvuma Wilson Nziku akieleza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara mkoani humo wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Meneja wa Usajili wa Walipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Rehema Shao akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwa lengo la kutatua changamoto hizo. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

…………………….

Na Veronica Kazimoto,Ruvuma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imedhamiria kutatua kero za wafanyabiashara ambapo kwa mwaka huu wa fedha imefanya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji uliofanyika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Dkt. Kijaji amesema kuwa moja ya sheria ya kodi iliyofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Kodi ya Mapato. 

“Miongoni mwa sheria zilizofanyiwa mabadiliko mwaka huu wa fedha wa 2019/20 ni pamoja na sheria ya kodi ya mapato ambapo tumepunguza viwango vya kodi kwa wafanyabiashara wadogo,” alisema Dkt. Kijaji. 

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa hapo awali wafanyabiashara wenye mauzo ghafi ya kuanzia shilingi 4,000,000 hadi 7,000,000 kwa mwaka walikuwa wanalipa shilingi 150,000 lakini baada ya mabadiliko ya sheria hiyo, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia shilingi 100,000 kwa mwaka. 

Kwa upande wa wafanyabiashara wenye mauzo ghafi kuanzia shilingi 7,000,000 hadi 11,000,000 walikuwa wanalipa shilingi 318,000 baada ya mabadiliko ya sheria ya kodi ya mapato kiwango hicho kimepunguzwa hadi kufikia 250,000 kwa mwaka 

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa, kwa wafanyabiashara wenye mauzo ghafi kuanzia shilingi 11,000,000 hadi 14,000,000 walikuwa wanalipa shilingi 546,000 ambapo baada ya mabadiliko ya sheria kiwango hicho kimepungua hadi shilingi 450,000 kwa mwaka. 

Vilevile, Naibu Waziri Kijaji amefafanua kuwa, kero nyingine iliyotatuliwa kupitia sheria hiyo ni ile ya wafanyabiashara kuanza kulipa kodi hata kabla ya kuanza kufanya biashara zao ambapo kwa sasa watatakiwa kulipa kodi ndani ya miezi 6 baada ya kuanza biashara.

“Nikisema serikali imedhamiria kutatua kero za wafanyabiashara mjue imedhamiria kweli. Hapo awali, wafanyabiashara wengi walililamikia kitendo cha kuanza kulipa kodi wakiwa ndio wanaanza biashara, lakini mwaka huu wa fedha yamefanyika mabadiliko na sasa wafanyabiashara wapya wataanza kulipa kodi ndani ya miezi 6 wakiwa tayari wamekwishaanza biashara zao,” alisisitiza Dkt. Kijaji.

Mkutano huu wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa mwezi Juni, 2019 alipokutana na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo aliiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wizara zote zinazohusika na wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

WASANII WA BONGOFLEVA WAWASHA MOTO KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Msanii Barnaba akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019. 
Wasanii wa muziki wa Kizazi kipya wa kundi la TMK Wanaume Family wakiongozwa na Mhe. Temba akiogoza jahazi kutoa burudani ndani ya katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Country Boy akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Country Boy akitoa burudani.
Msanii Nahreel wa kundi la Navy Kenzo akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Aika wa Navy Kenzo akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Nahreel na Aika wa kundi la Navy Kenzo wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Joh Makin akitoa burudani katika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Dj D- Ommy kwenye mashine akiendelea kuwapagawisha wanajumuiya ya Afrika Mashariki waliofika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Jux akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wasanii Jux (kushoto) na Joh Makin (kulia) wakitoa burudani. 
Aika, Nahreel na Jux wakitoa burudani kwa pamoja katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Jux akimtambulisha mpenzi wake.
Mahaba niueee...

VYAMA VYA USHIRIKA KANDA YA KUSINI VYAHIMIZWA KUCHAMKIA FURSA ZA KILIMO ZINAZOTOLEWA NA BENKI YA CRDB

$
0
0
Na Kilo Mgaya, Masasi - Mtwara

Meneja wa Kanda ya Kusini Benki ya CRDB Bi. Jeniffer Tondi amevihimiza vyama vya ushirika kanda ya kusini inayohusisha mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB katika uwezeshaji sekta ya kilimo.

Akizungumza katika kongamano la uwezeshaji sekta ya kilimo lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kuhudhuriwa  na vyama vya ushirika zaidi ya 42 katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Bi. Tondi alisema Benki ya CRDB imeweka mikakati madhubuti katika kuhakikisha inaisaidia Serikali kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini ili kusaidia kufikia malengo ya kujenga uchumi wa kati wa viwanda.

“Katika uwezeshaji wa sekta ya Kilimo Benki yetu imekuja na kauli mbiu inayosema Kilimo chetu, Viwanda vyetu, Uchumi Wetu, ambapo tumejikita katika maeneo makuu matatu ikiwamo mikopo ya pembejeo na uendeshaji, uunganishwaji na masoko pamoja na kutoa elimu ya mambo ya fedha na uwekezaji,” alisema Bi. Tondi.

Akizungumzia uwezeshaji katika zao la korosho kwa mikoa ya kanda ya kusini, Bi Tondi alisema Benki ya CRDB mwaka jana pekee ilitoa jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 16.9, huku akieleza kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika katika ununuzi wa pembejo za kilimo pamoja  ununuzi wa magunia ya kuhifadhia korosho kwa vyama vya ushirika vya msingi.

Akizungumza katika kongamano hilo Meneja wa tawi la Benki ya CRDB, Amani Madale aliwasisitiza wakulima kutumia fursa ya akaunti ya FahariKilimo katika kupokea malipo yao, huku akisema kuwa akaunti hiyo imezingatia zaidi mahitaji ya wakulima ambapo hufunguliwa pasipo kuwa na gharama zozote za uendeshaji.

“Mkulima anapofungua akaunti hii anaunganishwa moja kwa moja na huduma ya SimBanking inayomuwezesha kufanya miamala yote ya kifedha kupitia simu yake ya mkononi, lakini pia kupitia kadi yake ya TemboCard mkulima ataweza kupata huduma kupitia mawakala wetu wa CRDB Wakala ambao wapo mpaka vijijini ambapo ndipo wakulima wengi walipo,” aliongezea Madale huku akivitaka vyama vya ushirika kuchangamkia fursa ya CRDB Wakala.

Kwa upande wake Meneja wa Chama Kikuu cha Uchirika Mtwara na Masasi (MAMCU), Joseph MMole aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa kongamano hilo la uwezeshaji sekta ya kilimo huku akisema kongamano hilo litakwenda kuwahamasisha wakulima wengi kujitokeza kuchukua mikopo ya pembejeo na hivyo kuwawezesha kufanya kilimo cha kisasa zaidi.

Mbali na fursa za mikopo ya kilimo na akaunti ya FahariKilimo, wakulima pia walihamasishwa kujitokeza kuchangamkia fursa za huduma za bima, mikopo ya nyumba, pikipiki, bajaji ikilenga kuboresha maisha yao, huku pia wakihamasishwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika hisa za Benki ya CRDB ili kujiongezea kipato.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kusini, Jeniffer Tondi akizungumza na wawakilishi wa vyama vya ushirika vya msingi katika kongamano la uwezeshaji sekta ya kilimo wilayani Masasi lililofanyika katika ukimbi wa mikutano wa hoteli ya Rock City. Benki ya CRDB imewahimiza wakulima kuchangamkia fursa za mikopo ya kilimo kuboresha kilimo chao huku ikiwataka wakulima kujiunga na akaunti ya FahariKulimo ambayo haina gharama yoyote ya uendeshaji na hivyo kumpa mkulima unafuu.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Masasi, Amani Madale akizungumza na wawakilishi wa vyama vya ushirika vya msingi katika kongamano la uwezeshaji sekta ya kilimo wilayani Masasi lililofanyika katika ukimbi wa mikutano wa hoteli ya Rock City. 
Sehemu ya Washiri wa kongamano la uwezeshaji sekta ya kilimo liloandaliwa na Benki ya CRDB wilayani Masasi, wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. 
Baadhi ya Washiri wa kongamano la uwezeshaji sekta ya kilimo liloandaliwa na Benki ya CRDB wilayani Masasi, wakiuliza maswali. 


WANANCHI KATA YA RUNGEMBA WANUFAIKA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akipokewa na Kamati ya Shule ya Msingi Mnyigumba iliyoko katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akiangalia mahindi lishe wakati alipotembelea  Shule ya Msingi Mnyigumba iliyoko katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akikagua Mradi wa Kilimo cha parachichi katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akizungumza na Wanakijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi Wetu Mafinga
CHUO cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Rungemba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeleta neema kwa wananchi wanaowazunguka kwa kuhamasisha wananchi wa Vijiji wa Kata hiyo kushiriki katika miradi mbalimbali ya kuwaletea  maendeleo ikiwemo miradi ya lishe bora pamoja na elimu ya kilimo inayowataka kuzingatia kanuni bora za upandaji mazao.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Siku moja ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba mkoani Iringa kujionea kasi ya uhamasishaji wananchi kushiriki katika miradi ya kujiletea Maendeleo inayofanywa na Chuo hicho.

Dkt. Jingu amesema kuwa jamii ikishiriki katika miradi ya kiuchumi yenye matokeo chanya maisha ya wananchi yatabadilika kwa haraka sana na kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuwataka wanachi kutambua kuwa hakuna wakuwaletea maendeleo bali maendeleo yataletwa na wao wenyewe.

Aidha Dkt.Jingu ameridhishwa na kazi ya uhamasishaji wananchi kujiletea Maendeleo kwa wananchi wa vijiji vya Rungemba Itimbo na Kitelewasi ambao tayari wameanza kunufaika kiuchumi badala ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba  kuhamasisha Maendeleo ya kilimo  na lishe bora.

Dkt. Jingu aliongeza kuwa kuwa na elimu ya nadharia bila vitendo haitoshi akaongeza kuwa ni vyema vyuo vingine nchini vikatembelea chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba ili kuiga namna ambavyo Chuo hicho kinatekeleza dhana ya ushirikishaji Jamii katika maendeleo ya Jamii kwa vitendo.

Akizungumzia kuhusu miradi ya uzalishaji Mali katika vijiji vya Kata ya Rungemba Mkulima kutoka Kijiji cha Kitelewasi Bw.Augustino Mbedule amesema kutokana na mafunzo na miradi ya uhamasishaji unaofanywa na Chuo hicho tayari Jamii kijijini hapo imeanza kubadilika kimaisha.

Bw.Mbedule ameitaja miradi ilioanzishwa na Chuo hicho kuwa ni uhamasishaji kilimo cha mahindi lishe, Kilimo cha zao la parachichi, ufugaji nyuki na kampeini ya unyonyeshaji maziwa ya mama ili kupambana na udumavu wa watoto chini ya miaka mitano.


 Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba Bw. Raphael Mbiiji amesema Chuo hicho kikisaidiana na Chuo Kikuu Cha Sokoine Mjini Morogoro walifanya utafiti katika Vijiji vya Itimbo,Kitelewasi na Rungemba vilivyopo nje kidogo ya mji wa Mafinga Iringa na matokeo ya utafiti huo yalionyesha vijiji hicho kina tatizo kubwa udumavu kwa watoto wachanga.

Bw. Mbiiji aliongeza kuwa na matokeo ya utafiti huo yaliyopelekea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba pia uhamasisha Jamii za vijiji  kuhusu umuhimu wa kunyonyesha na lishe boraIli kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto na kwa sasa mwamko wa Jamii katika kilimo cha mahindi lishe na mbogamboga unazidi kuongezeka.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu anaendelea na Ziara ya Siku Tano katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutembelea vyuo vya Maendeleo ya Jamii na pia Makazi ya Wazee yaliyoko katika Mikoa hiyo.

WAZIRI KALEMANI AAGIZA BEI YA GESI ASILIA IPITIWE UPYA

$
0
0
Na Veronica Simba – Pwani
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameziagiza Mamlaka zote zinazohusika na upangaji wa bei ya gesi asilia, kufanya mapitio upya ili kuja na bei itakayozinufaisha pande zote yaani serikali na wawekezaji.

Alitoa maelekezo hayo kwa nyakati tofauti, Septemba 24 mwaka huu, alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill na kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, vilivyopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Dkt Kalemani alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia siku hiyo kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wataalamu wa Wizara, kufanya mapitio ya bei za gesi viwandani ili ziwawezeshe wawekezaji kuzalisha kwa tija.

Alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wawekezaji mbalimbali wenye viwanda, wakiwemo Goodwill na Lodhia, kuwa gharama ya gesi asilia iko juu hivyo wanaomba serikali iangalie uwezekano wa kuipunguza ili wazalishe kwa tija zaidi.

“Lengo la serikali ni kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini hivyo naagiza muanze mara moja kufanya mapitio ya bei husika. Mje na bei linganifu ili kila upande unufaike.”

Katika kufanya mapito husika, Waziri aliwataka wataalam hao, pamoja na mambo mengine, kuangalia pia uzoefu wa nchi nyingine zenye gesi asilia.

Hata hivyo, Waziri alilazimika kufafanua sababu zinazopelekea bei ya gesi kutofautiana katika maeneo mbalimbali, ambapo alieleza kuwa mojawapo ni kutokana na gharama ya kazi inayofanyika katika kuitafuta, kuichimba na hatimaye kuileta juu ya ardhi. Alisema teknolojia husika ina gharama kubwa.

Pia, alieleza sababu nyingine kuwa ni gharama ya usafirishaji wa gesi kutoka kwenye kisima kwenda kwenye Mtambo maalum wa kuchenjulia pamoja na gharama ya kufanya zoezi hilo la uchenjuaji.

“Sasa, kadri unavyokuwa mbali kutoka kwenye eneo la kuchakata gesi, ndivyo gharama inavyoongezeka. Bei ya gesi kwa yule aliye karibu na eneo la uchenjuaji haiwezi kulingana na aliye mbali.”

Bei ya sasa ya gesi asilia inaanzia Dola 4.7 hadi 7.72 kwa uniti moja.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019.

Baraza la Wafamasia linakwenda na Tehama katika utoaji wa huduma-Msajili wa Baraza

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
BARAZA la Wafamasia limesema kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) hawana budi kwenda na teknolojia hiyo kwa kuweka mfumo kwa wafamsia wote nchini kutumia kujifunza vitu mbalimbali vinavyotokea ikiwemo masuala ya dawa.

Hayo ameyasema Msajili wa Baraza hilo Elizabert Shekalaghe katika maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani kwa baraza kuzindua mfumo taarifa mbalimbali ambazo wafamasia wanatakiwa kufuata yaliyofanyika jana katika ofisi ndogo za baraza hilo jijini Dar es Salaam amesema kuwa mfumo huo utarahisisha wafamasia hao kupata taarifa kwa kila wakati pamoja na leseni zao kwa katika mfumo.

Amesema kuwa katika mfumo kutafanya wafamasia kupata huduma zote katika mtandao na hakuna sababu ya kwenda katika ofisi za baraza.

Shekalaghe amesema kukiwepo na dawa mpya imeingia basi wafamasia wote watapata taarifa katika mtandao pamoja na dawa ambayo si salama kwa binadamu.

“Dunia inakwenda kwa kasi hivyo nasi lazima twende kwa kasi hiyo katika mabadiliko ya utoaji wa huduma katika mfumo wa mtandao na kurahisisha utoaji huduma bora za afya kwa wananchi”amesema Shekalaghe.

Aidha amesema kuwa wafamasia wanatakiwa kufuata sheria,Kanuni pamoja na taratibu na wataokwenda kinyume baraza halitaweza kuvumilia kwani kuachwa kwa mtu kuna haribu taasisi na kufanya wananchi kukosa imani utendaji wa Baraza hilo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Legu Mhangwa amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa wafamasia ni muhimu sana katika maendeleo ya afya za wananchi katika utumiaji wa dawa.

Mhangwa amesema baraza limefanya kazi kubwa katika kuunda mfumo huo hivyo lazima utumike na kuleta matokeo chanya kwa wafamasia.
Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabert Shekalaghe akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani iliyofanyika katika ofisi ndogo za Baraza jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafamasia Legu Mhangwa akizungumza kuhusiana na mfumo wa mpya wa mawasiliano uliyoanzishwa na kuzinduliwa katika maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafamasia Legu Mhangwa akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa kwa mfumo wa mawasiliano kwa wafamasia.
Mkuu wa Idara ya Mafunzo wa Baraza la Wafamasia Grace Malange akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo yatakayokwepo katika mfumo wa baraza hilo.
Mkuu wa Idara ya Tehama wa Baraza la Wafamasia Yamwaka Gadi akiwapitisha wafamasia katika mfumo katika maadhimisho ya Siku wafamasia Duniani.
Baadhi ya wafamasia walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya wafamasia.
Picha ya pamoja ya katika maadhimisho ya siku wa wafamasia.

WAZIRI MKUCHIKA AZITAKA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS KUWA MFANO WA KUIGWA KIUTENDAJI NA KIMAADILI

$
0
0
Na James K. Mwanamyoto
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika amewataka watumishi wa taasisi za umma zilizo chini ya Ofisi ya Rais kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wa taasisi nyingine za umma kiutendaji na kimaadili kwa kuwa jamii inaitazama Ofisi ya Rais kama kioo cha utendaji kazi mzuri katika utumishi wa umma.

Waziri Mkuchika ametoa wito huo wakati wa kikao kazi chake na Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Mhe. Mkuchika amewaasa watumishi wa taasisi hizo kujiona kuwa ni sehemu ya kuitunza heshima ya Ofisi ya Rais kwa kufanya kazi kwa uadilifu.
Amewasisitiza watumishi wa chuo hicho kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kuharakisha maendeleo ya nchi.

“Mimi nipo kwa ajili ya kumsaidia Mhe. Rais ambaye ndiye Waziri wa Ofisi hii kusimamia utendaji kazi wa taasisi zote zilizopo chini ya ofisi yake, hivyo hatuna budi kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi kama ambavyo yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kutekeleza majukumu yake kwa vitendo”, amesisitiza Mhe. Mkuchika.

Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa rai kwa Watumishi wa Umma wote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi iliyopo ili kuepukana na vitendo vya ubaguzi wa kijinsia, dini, ukabila na  itikadi za kisiasa kwa wananchi na watumishi wenzao wanaowahudumia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel S. Shindika kwa niaba ya chuo, amemthibitishia Mhe. Mkuchika kuwa, atahakikisha maelekezo yote aliyoyatoa yanatekelezwa ili kuendana na kasi ya kiutendaji ya Mheshimiwa Rais yenye lengo la kuleta maendeleo ya Taifa. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.
 Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel S. Shindika akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) kwa kufanya ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.


Baadhi ya Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua hoja za Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATOA NENO KWA MAKAMANDA WA POLISI

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (aliyesimama) akitoa mada kwenye kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi, leo Jijini Dar es salaam, kikao ambacho kinalenga kuweka mikakati mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime (kushoto) akitoa  mada kwenye kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi,leo Jijini Dar es salaam, kikao ambacho kinalenga kuweka mikakati mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.

SERIKALI MBIONI KUJENGA MITAMBO MIPYA YA UMEME MKOANI MTWARA

$
0
0
Na Hafsa Omar, Mtwara    
Katika kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mtwara unakuwa na umeme wa uhakika kwa muda wote, Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaeleza wafanyabishara na wawekezaji wa Mkoa huo kuwa, Serikali ipo mbioni kujenga mitambo miwili mipya ya umeme.

Alisema hayo, Septemba 25, 2019 wakati alipokuwa ajibu hoja za wadau wa maendeleo katika  mkutano uliolenga kusikiliza  changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara, ambapo alisema Serikali inazifahamu changamoto zote za umeme zinazojitokeza katika mkoa huo na tayari zinafanyiwa  kazi.

“Kituo cha umeme cha Mtwara kina zaidi ya miaka 10 na baadhi ya mitambo imechakaa, hapa ninavyozungumza sasa mitambo inayofanyakazi ni ile miwili tu mipya, na mahitaji ya umeme katika mkoa wa Mtwara na Lindi yameongezeka,  kwani kwa sasa inatakiwa takriban megawati 17.7 wakati uwezo wa uzalishaji katika Kituo cha Mtwara ni megawati 18 hivyo tunafanya jitihada za kuongeza mitambo mipya.”Alisema Mgalu

Alifafanua, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), katika mwaka huu wa fedha imetenga bajeti ya kununua mitambo miwili ambayo itasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Vile vile, Naibu Waziri alisema hatua nyengine ambayo Serikali imechukua ni pamoja kuwa  na mpango wa muda mrefu utakaosaidia utapatikanaji wa umeme wa uhakika mkoani humo.

“ Tunatarajia kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi hapa hapa Mtwara wa megawati 300 na njia ya kuusafirisha, pale Somangafungu pia kuna mpango wa kujenga mtambo wa kuzalisha megawati 240 kwa  kutumia gesi  na njia ya kuusafirisha kutoka Somangafungu hadi Kinyerezi, njia zote  zitakuwa na  msongo wa kV 400 na tunategemea  kutekeleza huu mradi kati ya mwaka 21/23.”alisema Mgalu
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara (hawapo pichani) katika Mkutano uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoani Mtwara.
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia akizungumza jambo katika Mkutano uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoani Mtwara. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wanaosimamia Sekta mbalimbali.
 Baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara  wakiwa katika Mkutano uliolenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli zao. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wanaosimamia Sekta mbalimbali.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI TISA MBINGA MJI YA MILIONI 924

$
0
0
MWENGE wa uhuru umefungua, umepitia, umekagua, umezindua na kuweka jiwe la msingi la miradi tisa ya thamani ya shilingi 924,150,266.14 kwenye Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma. 

Mkurugenzi wa mji wa Mbinga, Grace Quintine akizungumza jana wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Gipson Mhagama alisema mwenge huo umekimbizwa kwenye kilomita 118.

Quintine alisema katika mradi wa kwanza, mwenge huo wa uhuru utafungua nyumba bora ya mwananchi wa kijiji cha Mpepai. 

Alisema mwenge huo umefungua zahanati ya kijiji cha Lipilipili na kukagua shamba bora la miti ya hifadhi ya mazingira. 

Alisema utazindua klabu ya wapinga rushwa ya shule ya sekondari Depaul Mbangamao na kuweka jiwe la msingi shule ya sekondari Kagugu. 

"Utazindua mradi wa maji Maganagana, kuweka jiwe la msingi mtambo wa kumenya kahawa Sepukila na kufungua kiwanda cha maji Asili (Mdaka Five) mtaa wa Masumuni na kuweka jiwe la msingi barabara ya Mbuyula," alisema Quintine. 

Alisema baada ya kukimbizwa kwenye halmashauri ya mji wa Mbinga, mwenge wa uhuru utakabidhiwa katika halmashauri ya wilaya ya Songea. 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally aliipongeza halmashauri ya mji wa Mbinga kwa kuwa na miradi mizuri yenye tija kwa jamii.

"Katika mradi wa zahanati ya Lipilipili wananchi wanapaswa kutumia huduma za afya kuliko kujitibu kwa waganga wa kienyeji kwani ni muda mrefu hamkua na zahanati," alisema Ally.


Ally alisema mradi wa maji wa Asili wa Mdaka Five umeongeza ajira na barabara ya Mbuyula nayo imejengwa kwa kiwango kinachostahili.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka 2019 ni maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 
 Mkurugenzi wa Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, Grace Quintine akipokea mwenge wa uhuru kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Gipson Mhagama ambao ulizindua miradi tisa ya Halmashauri ya mji huo yenye thamani ya shilingi 924,150,266.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu Mzee Mkongea Ally akipokewa na viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu Mzee Mkongea Ally akizungumza baada ya kuzindua mradi wa zahanati ya Kijiji cha Lipilipili Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambao awali wananchi wa eneo hilo walikuwa wanatembea umbali mrefu wa kilomita saba kufuata huduma ya afya.
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images