Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA SOKO LA MADINI KATORO

$
0
0
WAFANYABIASHARA wa Madini katika Soko Dogo la Madini Katoro wameiomba Serikali iwaruhusu kuwa na Wasaidizi watakaowasaidia kununua madini maeneo yenye mialo ya uchenjuaji na kuwauzia kwenye vituo vya ununuzi.

Wafanyabiashara hao wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea soko hilo kwa lengo la kujifunza na kuangalia namna masoko ya madini yanavyoendeshwa.

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa, Sheria na Kanuni za biashara ya madini zinaelekeza kuwa shughuli za uuzaji na ununuzi wa madini zinapaswa kufanyika kwenye vituo maalum vya manunuzi hivyo suala la kuwa na wasaidizi kwenye mialo wa kuwauzia wafanyabiashara hao linakinzana na Sheria ya Madini na Kanuni za madini kwenye masoko.

‘’ Kamati ndiyo inaishauri Serikali, ndiyo Bunge na Wawakilishi wa wananchi. Tutaendelea kutatua changamoto tunazokutana nazo kwenye masoko. Sote tunajua Masoko ni Mapya, Sheria Mpya, Kanuni Mpya, hivyo tutaendelea kutatua changamoto hizo yakiwemo masuala ya vifaa na watumishi,’’ amesema Naibu Waziri Nyongo.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo amewataka wafanyabiashara wa madini na wachimbaji kuyatumia masoko ya madini na kueleza kuwa, kufanya biashara ya madini nje ya masoko ni kujiweka kwenye matatizo. Pia, amewasisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya zebaki na kueleza kuwa, serikali itaendelea kuangalia njia mbadala za teknolojia ili kuweza kuachana na matumizi ya zebaki.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mariam Mzuzuri amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu wakati Serikali na Kamati zikiangalia namna ya kuzifanyia kazi changamoto zilizowasilishwa kwao.

‘’ Kwa kuwa masoko haya yanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ni vyema suala hili mtuachie kwanza sisi na serikali ili tuliangalie,’’ amesema Mzuzuri. Kufuatia hali hiyo, Mzuzuri ameitaka wizara kuendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara na wachimbaji wa madini ili wajue namna ya kuyatumia masoko ya madini na kujua mwenendo mzima wa shughuli za madini na biashara ya madini inavyofanyika. 

Katika hatua nyingine, kamati imeitaka Serikali kuhakikisha suala la Ulinzi kwenye masoko ya Madini halisubiri michakato bali linatakiwa kufanyiwa kazi haraka kutokana na rasilimali zilizopo katika masoko hayo.

Makamu Mwenyekiti amesema hayo kufuatia ombi la kuimarishwa kwa Ulinzi katika Soko la Katoro lililotolewa na Wafanyabiashara wa Madini sokoni hapo wakati wa ziara yake mkoani Geita. 

Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo Fred Mwakajoka ametaka taasisi zote za serikali zinazoshirikiana na Tume ya Madini kuendesha masoko hayo ziwepo katika masoko hayo ili kurahisisha utendaji wa majukumu ya masoko .

Baada ya kutembelea soko la Katoro, Kamati hiyo pia imetembelea Soko la Madini Kahama na baadaye itatembelea Nzega. Ziara ya kamati kutembelea masoko imefanywa na kamati hiyo baada ya kutembelea Soko Kuu la Madini Geita na Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwasikiliza Wafanyabiashara wa Madini katika Soko dogo la Madini Katoro wakati kamati hiyo ilipotembelea soko hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mariam Mzuzuri (kushoto) akifuatilia hoja zilizokuwa zikitolewa na Wafanyabiashara wa Soko la Madini Katoro. Katikati ni Mjumbe wa Kamati hiyo Fred Mwakajoka na kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Felister Mgonja.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akifuatilia jambo wakati Kamati ya Bunge ikiwasikiliza wafanyabishara wa madini , kamati hiyo ilipotembelea soko la madini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mariam Msabaha na Kushoto ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza jambo na wafanyabiashara wa soko la Madini Katoro wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

SERIKALI KUVUNA MABILIONI KUPITIA USAMBAZAJI GESI ASILIA VIWANDANI

$
0
0

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, Septemba 24, 2019.

Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa wamiliki wa kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Pwani, kabla ya kuzindua rasmi matumizi ya gesi asilia katika kiwanda hicho, Septemba 24, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, kabla ya kuzindua matumizi ya gesi asilia kiwandani hapo, Septemba 24, 2019.

Na Veronica Simba – Pwani
WAZIRI ya Nishati kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),  inatarajia kukusanya kati ya shilingi milioni 85 hadi 120 kwa mwezi, sawa  na shilingi bilioni 1.02 hadi 1.4 kwa mwaka kutokana na matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga, ambayo hadi sasa ni futi za ujazo laki mbili kwa siku.

Hayo yamebainishwa Septemba 24, 2019 wakati Waziri wa Nishati Dk.  Medard Kalemani, alipozindua matumizi ya gesi asilia katika kiwanda hicho  cha kufua vyuma ambacho awali kilikuwa kikitumia mafuta mazito.

Mbali na makusanyo hayo kwa serikali; kwa upande wa kiwanda, kupitia matumizi ya gesi asilia, kimeweza kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa zake kwa zaidi ya asilimia 40 ikilinganishwa na gharama zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya mafuta mazito.

Akizungumza baada ya kukagua shughuli za kiwanda hicho pamoja na kufanya uzinduzi husika, Waziri alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) pamoja na wataalamu wa Wizara, kufanya mapitio ya bei za gesi viwandani ili ziwawezeshe wawekezaji kuzalisha kwa tija.

“Mje na bei muafaka ambazo haziathiri uwekezaji wa TPDC na haziathiri uwekezaji wa wenye viwanda lakini pia zisiathiri mapato ya serikali,” alisisitiza.

Akifafanua zaidi, Waziri alisema bei ya sasa inaanzia Dola 4.7 hadi 7.72 kwa uniti moja, ambayo imekuwa kikwazo kwa wawekezaji.

Aidha, Waziri aliiagiza TPDC na kampuni yake tanzu ya GASCO, kukamilisha zoezi la ukusanyaji takwimu kwa ajili ya usambazaji wa gesi wilayani Mkuranga ndani ya kipindi cha miezi miwili ili ziwezeshe kubaini mahitaji ya gesi viwandani katika wilaya hiyo na kuvisambazia nishati hiyo
 kwani manufaa yake ni makubwa.

Waziri pia alieleza kuwa serikali inafanya mapitio ya bei za umeme ili kuzirekebisha na kwamba bei hizo zitapungua, hususan baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya uzalishaji umeme, ukiwemo wa Julius Nyerere, Rufiji.

Aidha, aliwataka wadau wa sekta za gesi na mafuta, kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la kupitisha mabomba ya gesi katika maeneo yao. “Msidai fidia kwakuwa nasi hatutozi gharama za kuunganisha. Hivyo nanyi, msilete vikwazo.”

Katika hatua nyingine, Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO wa Wilaya, Mkoa na Makao Makuu, kukipatia kiwanda cha Lodhia megawati nane zaidi za umeme kama kilivyoomba ili zifike 14 kufikia mwisho wa mwezi huu.

Alisema hakuna sababu ya kushindwa kutekeleza agizo hilo maana kuna umeme wa kutosha. Sambamba na hilo, aliagiza pia kusiwe na mgao wa umeme wilayani humo kwani kuna umeme wa ziada.

Kuhusu usambazaji umeme katika mitaa na vijiji vya wilaya hiyo, Waziri aliitaka TANESCO kuhakikisha vijiji vyote 88 vya wilaya hiyo vinaunganishiwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mkuranga, Mkuu wa Wilaya hiyo, Filberto Sanga aliishukuru serikali na kupongeza jitihada za wizara ya nishati katika kusambaza nishati ya umeme na gesi kwa wananchi.

Aliomba wilaya yake ipewe kipaumbele kwa kupatiwa umeme zaidi kutokana na uwepo wa viwanda vingi. Mkurugenzi Mtendaji wa Lodhia, Sailesh Pandit, alisema Wizara ya Nishati, kupitia TPDC na TANESCO imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika

kuongeza tija ya uzalishaji wao kwa kuwapatia nishati wanayoihitaji pasipo vikwazo. Aliwaasa wamiliki wengine wa viwanda, kutumia gesi asilia kwani inapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji.

Kiwanda kingine ambacho kimeunganishiwa gesi asilia wilayani humo ni cha Goodwill Ceramics kilichopo kijiji cha Njopeka. Zoezi la kuunganisha wateja wengine linaendelea.

WAGONJWA WALIOPELEKWA NA POLISI MUHIMBILI WATAFUTA NDUGUZAO

BENKI YAFURAHIA KUTOA FURSA KWA WATANZANIA KUWAWEZESHA KUBORESHA MAISHA NA UCHUMI

$
0
0

Mkurugenzi wa Biashara ya DCB , James Ngaluko (katikati)akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati benki hiyo benki hiyo ikitangaza kutangaza kumaliza kampeni ya bidhaa yake ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ kwa mafanikio makubwa. Kampeni ya DCB Lamba Kwanza ilizinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MKAKATI wa Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha taasisi za fedha ikiwemo sekta ya kibenki umeendelea kuungwa na Benki ya Biashara ya DCB kwa kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za mikopo na zenye riba nafuu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa benki hiyo James Ngaluko amesema pamoja na mambo mengine wanatambua jitihada za Serikali za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora na zenye gharama nafuu ikiwemo mikopo na wao wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwahudumia Watanzania.

"Tunatambua ambavyo Serikali inazungumzia umuhimu wa kuboreshwa kwa huduma za kibenki ikiwemo ya kutoa mikopo kwa haraka na yenye riba nafuu.

"Serikali imekuwa ikihimiza riba kupungua nasi tumepunguza riba zetu kwa kiwango kikubwa, nia yetu ni kuona kila Mtanzania anajenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,"amesema.

Wakati huo huo Ngaluko amesema kampeni ya bidhaa yao ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ imekuwa na mafanikio makubwa kwani imevuka malengo yake iliyojiwekea ya Sh.bilioni 15 na kuongeza amana kwa Sh.bilioni 18.5 ambayo ni zaidi ya asilimia 123.

"DCB Lamba Kwanza ilizinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu huku ikiwa na lengo la kukusanya amana za kiasi cha Sh.bilioni 15, iliwawezesha wateja wetu kupata riba ya hadi asilimia 14 ya amana wanayowekeza  ambapo mteja alianza kupokea riba yake ya mwezi  papo hapo,"amesema.

Ngaluko amesema wanatoa shukrani kwa wateja wao kwa kuipokea bidhaa hiyo na kuweza kunufaika nayo kwani kila mwezi umekua ni wa faida.Mteja anafurahia riba yake inayolipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi.
Amesema malipo ya riba ni rafiki kuwa kuwa mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu mpaka miaka miwili na ni jambo la fahari kuona benki ya kitanzania inatoa fursa kwa Watanzania na kuwawezesha kuboresha maisha na uchumi.

Hata hivyo amesema DCB Lamba Kwanza imepokewa kwa mikono miwili na wateja wetu na kufanikiwa kuvuka malengo kwa kukusanya amana ya zaidi ya Sh.bilioni 18.5 ambapo awali Benki ilikusudia kuuza kiasi cha Sh. bilioni 15.

"Tunawashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila bidhaa tunayoiingiza sokoni na kutuwezesha kuvuka malengo hii inaonyesha ni jinsi gani DCB inavyo aminika kwenye soko.Tupo imara na tumejidhatiti katika kubuni na kuingiza bidhaa zitakazokidhi kiu ya mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wetu,"amesema.

Pia amesema benki hiyo imeendelea kufanya maboresho katika baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 15 kwa mikopo ya ujenzi na ununuaji wa nyumba za makazi kwa wateja wetu wote hususan wafanyabiashara na waajiriwa. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa wajasiriamali wote na wafanyakazi wenye lengo la kununua au kujenga nyumba kuwahi fursa hii. Pia amesema benki inatoa huduma za kidigitali kupitia DCB DIGITAL inayomuwezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi.

Pamoja na hayo,Ngaluko amesema kuwa  benki hiyo imeendelea kupata faida, na kufikia kipindi cha nusu ya kwanza ya  mwaka huu imeweza kupata faida ya Sh.bilioni 1.2 ikiwakilisha ongezeko la asilimia 118  kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2018.

UHABA WA MAJI WAWALIZA WANANCHI WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akimtwika ndoo ya maji mwanafunzi wa Sekondari ya Mwaru, Zafarani Selemani baada ya kukagua mradi wa maji shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
 DC Mpogolo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwaru.
 DC Mpogolo akiwa na viongozi wa Kata ya Mwaru baada ya kukagua jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwaru.
 DC Mpogolo akizungumza na viongozi baada ya kukagua ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu katika  Shule ya Msingi Mtakuja.
 Mkutano wa ndani ukiendelea.
 Afisa Tarafa ya Sepuka Cornel Nyoni akiwatambulisha viongozi mbalimbali mbele ya DC Mpogolo kabla ya kuanza kwa mkutano wa ndani.
 DC Mpogolo akizungumza na viongozi wa Kata ya Mwaru katika mkutano wa ndani. Kutoka kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu wa Tarafa ya Sepuka, Theresia Masinjisa, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Sepuka, Halima Athumani Ng'ura na Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale.
 Hapa DC Mpogolo akizungumza na viongozi baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mlandala.
 Wananchi na wanafunzi wakisubiri kuteka maji kwenye bomba la Kijiji cha Mlandala.
 Wakazi wa Kijiji cha Mlandala, Moshi Mohamed (kulia) na Salma Athumani wakitoka kuteka maji katika bomba la Kijiji cha Mlandala.
 Mkazi wa Kijiji cha Mlandala, Ramadhani Kamata akizungumzia changamoto ya maji katika kijiji hicho.
DC Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Mwaru baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi 


Na Dotto Mwaibale, Singida
KUKOSEKANA kwa  maji ya uhakika katika Kijiji cha Mlandala Wilayani Ikungi mkoani Singida baada ya tenki kupasuka kumesababisha wananchi kuwa na changamoto ya maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Mkuu wa Wilaya  Edward Mpogolo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi katika kata za Sepuka, Mwaru na Irisya pamoja na kujitambusha baada ya kuteuliwa kuongoza wilaya hiyo waliiomba serikali kuwasaidia kuondoa changamoto hiyo.

Wamesema wanatumia muda mwingi kusubiria kupata maji na kushindwa kufanya shughuli zingine za maendele.

" Hapa kijijini kwetu mwaka 2016 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  ilituletea mradi wa maji lakini unaendeshwa kwa hasara kwani maji yote yanaishia njiani baada ya tenki kupasuka " alisema Ramadhani Kamata.

Kamata amesema mbali ya hasara hiyo ya kumwagika maji changamoto nyingine ni matumizi ya jenereta kwa ajili ya kusukuma maji kwenda kwenye tenki ambapo kila siku wanatumia lita mbili za dizeli ambazo ni sh.5000.

Kamata amesema kuwa awali halmashauri hiyo iliwaambia itawanunulia betri litakalo kuwa likisukuma jenereta hilo lakini hadi leo hii hawajapata.

 Salma Athumani amesema kupasuka kwa tenki hilo kunasababisha wananchi kutumia muda mrefu kusubiri maji katika bomba hilo moja linalo hudumia wananchi wa kijiji hicho.

Amesema katika bomba hilo kila ndoo moja wanachangia sh.50 hela aliyodai ni nyingi kwa wananchi kutokana na matumizi makubwa ya maji.

" Kutokana na maji kutoka kidogo wanafunzi wa shule yetu ya msingi ya Mlandala wanalazimika kutembea umbali wa kilometa mbili kuchota maji ya kisima kwa ajili ya matumizi ya shuleni" alisema Moshi Mohamed.

Mohamed amesema muda huo wanao tumia wanafunzi hao kwenda kuchota maji unaweza kuwaathiri katika masomo yao na kujikuta wakishuka kitaaluma.

Hata hivyo foleni ya kusubiri maji ikiwa kubwa wanalazimika kwenda kutafuta maji ya visima katika vitongoji vya Idodoma na Uzelela ambavyo vipo nje kidogo ya Kijiji cha Mlandala.

Mkuu wa wilaya  Edward Mpogolo baada ya kusikia changamoto hiyo aliahidi kuonana na mhandisi wa ujenzi wa wilaya ili kufika katika kijiji hicho kwa ajili ya kulifanyia ukarabati tenki hilo au kununua tenki kubwa la plastiki litakalotumika kwa muda ili kupunguza makali ya changamoto hiyo.

Ameongeza kuwa Serikali imekwisha toa sh. 1.5 bilioni kwa ajili ya uchimbaji wa visima 28 na sh. 2 bilioni kwa ajili ya usambazaji wa maji na ujenzi wa matenki kwa majimbo yote mawili ya Singida Mashariki na Magharibi na pindi mradi huo utakapo kamilika utamaliza kabisa changamoto ya maji katika wilaya hiyo.

SIMBA YAWASILI BUKOBA KIMYAKIMYA

$
0
0


 Wachezaji wa Timu ya Simba wakipanda gari kuelekea Hotelimara baada ya kuwasili Bukoba.
Kocha wa Timu ya Simba Patrick Aussem.

Anaadika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.
WEKUNDU wa msimbazi Timu ya Simba Sports Club wamewasili salama Mjini Bukoba Majira ya Saa  tatu kwa usafiri wa anga, tayari kuziwinda pointi tatu muhimu dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar.

Katika hali ya isiyo ya kawaida Timu hii ya Simba imewasili kimya kimya Mjini Bukoba tofauti na miaka iliyopita, ambapo hali ya mapokezi imeonekana kuwa hafifu bila kushuhudia zile mbwembwe, shamra shamra za mashabiki licha ya baadhi ya mashabiki ndaki ndaki wa boda boda kujitokeza kuipokea Timu na kisha kuisindikiza hadi Hotelini.

Akizungumza Mara baada ya kutua katika kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Kocha wa Timu ya Simba Patrick Aussems amesema "..Timu imekuwa kambini takribani siku tatu, na tayari imewasili salama Bukoba, tutakuwa na mazoezi mepesi mchana tayari kwa mchezo wa kesho, ingawa Kagera Sugar imekuwa ikimpiga Simba, lakini Mara hii tumejiandaa.." Amesema Aussems

RC MAKONDA AWATOLEA UVIVU WATENDAJI WANAOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO DAR

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na watendaji wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo wanafanya miradi ya jijini lake lisiendelee na kusababisha kukwama kwa miradi ya kimaendeleo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akiteta jambo na kipongozi mwenzie.

Baadhi ya watu waliohudhulia mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza.

Na Leandra Gabriel, MICHUZI TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewajia juu viongozi wanaofanya kazi bila kufuata mifumo ya kiutawala katika ngazi ya Mkoa na kusababisha kukwama kwa miradi ya kimaendeleo.

Akizungumza katika kikao maalumu kilichowakutanisha, wakuu wa Wilaya, wakuu wa idara, wakurugenzi, wakandarasi, washauri wa miradi na viongozi wa sekta mbalimbali Makonda amewataka viongozi hao kutoa taarifa katika ofisi husika kuhusiana na changamoto za utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Aidha Makonda ameishangaa  wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kurudisha nyuma kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka zaidi ya shilingi bilioni moja hadi kufikia shilingi milioni 600 hadi 700.

"TARURA mnakusanya mapato hadi kwenye maegesho ya kwenye nyumba za watu kweli?? na bado kasi ya ukusanyaji imeshuka kutoka zaidi ya bilioni moja hadi kufika milioni mia sita Mia saba uko sijui" ameeleza Makonda.

Makonda amesema kuwa jana Katibu mkuu TAMISEMI  na Katibu tawala wa Mkoa walikutana na baadhi ya watendaji ambapo alishiriki sehemu ya kikao hicho na walikubaliana kuwachukulia hatua watendaji ambao hawatendei kazi majukumu yao.

Kuhusiana na ujenzi unaosuasua wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti na ujenzi katika fukwe za Coco Beach Makonda amesema kuwa alikutana na viongozi wa Wilaya hizo na walipewa muda wa kukamilisha miradi hiyo.

"Tarehe 22 mwezi wa 3 nilikutana na viongozi wa  Kinondoni na niliwapa siku 3 kuanza ujenzi Coco cha kushangaza mkataba umesainiwa mwezi wa 7 au 8, hata Ilala nao nilikutana nao tarehe hiyo lakini mkataba ulisainiwa mwezi wa 9 baada ya kauli ya pili au ya tatu ya Rais" ameeleza Makonda.

Katika kikao hicho Makonda amewakataa watendaji wawili na kushauri wahamishwe vituo vya kazi baada ya kusuasua katika utendaji kazi.

MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA MAJI MKWAWA

$
0
0


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua kiwanda cha maji – Mkwawa  kilichopo mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Mary Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Ali Happy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Ahmed Huwel, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga, Naibu wa Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iri ga, Richard Kassera. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha maji – Mkwawa, Ahmed Huwel  baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji-Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kuhusu ujazaji maji katika chupa wakati alipozindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maji – Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kutembelea kiwanda baada ya Waziri Mkuu kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji- Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel (wa tatu kulia) kutembelea mitambo ya kuzalisha maji baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa  wa Iringa, Ally Happy na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji- Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
 Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji – Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA CHA ASAS MJINI IRINGA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Septemba 25, 2019.  Kushoto ni Mkugenzi Mtendaji wa Makampni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda hicho, Fuad Abri.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia) wakitazama maziwa yaliyofungashwa wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjni Iringa, Septemba 25, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  wakitazama mitambo ya kusindika maziwa na bidhaa zake   wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri,  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Fuad Abri na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Balozi wa bidhaa za maziwa za ASAS na Msanii maarufu nchini, Mai Zumo wakati walipotemblea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MASHEIKHE WAWASHUKIA WANAOTAKA KUVURUGA MAULIDI YA MTUME S.A.W

$
0
0
 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akizungumza jambo kwenye kikao cha masheikhe wa mikoa saba ya Kanda ya Ziwa na Magharibi wakiwemo wa wilaya za mkoa huo, kuhusu maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhhamad S.A.W.
Masheikh wa mikoa saba ya Kanda ya Ziwa na Magharibi pamoja na masheikhe wa wilaya za Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao cha maandalizi ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhhamad S.A.W.

Na Baltazar Mashaka Mwanza
SHEIKH wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta ametoa onyo kwa watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii ili kuwakatisha tamaa na kuwavunja moyo waumini wa dini ya Kiislamu wasichangie maulidi, waache kufungua mijadala isiyo na tija,badala yake wahamasishe waumini kuchangia sherehe hizo.

Sherehe hizo za Maulid kitaifa zitafanyika jijini Mwanza, Novemba 9, mwaka huu ambapo wageni mbalimbali kutoka nchi jirani za Burundi,Kenya, Uganda watahudhuria.

Sheikh Kichwabuta alita onyo hilo jana baada ya kumalizika kwa kikao cha maandalizi ya sherehe hizo za kuzaliwa kwa Mtume Muhhamad S.A.W kilichofanyika jijini Mwanza na kuwatanisha masheikhe wa mikoa saba ya Kanda ya Ziwa na Magharibi.

Alisema watu wenye nia mbaya wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufungua mijadala ya kuwakatisha tamaa na kuwavunja moyo waumini wa dini ya Kiislamu ili wasichangie sherehe hizo wasipewe nafasi.

Sheikhe Kichwabuta, alisema ikibainika kuwa watu wanaotaka kuwarudisha nyuma na kukwamisha shughuli hiyo yenye thawabu ni waislamu wenyewe, basi wasipewe nafasi na wawekwe pembeni hadi mwisho wa maulid hayo.

“Tuhamasishe maulidi ili watu wachangie na tusiweke vitu ama mambo ya kuwavunja moyo waumini.Tusifungue mijadala isiyo na tija kwenye ma-group WhatsApp (makundi) ili kuweza kufanikisha shughuli hii muhimu,”alisema.

Sheikhe huyo wa Mkoa wa Kagera, alishauri kuwa watu wa kuwarudisha nyuma wasipewe nafasi hadi shughuli hiyo iishe ili wasiwavuruge watu wenye fikra nzuri.

Awali Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke alisema maulid ya mwaka huu yatafanyika jijini humu ikiwa ni baada ya miaka 40 tangu yafanyike mwaka 1990, yataambatana na shughuli za kijamii ambapo mada mbalimbali zikiwemo za mauaji ya wazee,uhusiano wa watu wa dini zingine na elimu ya dawa zitatolewa. 

“Tumekutana hapa kwa ridhaa ya Mufti, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Bin Zuberi kujadili ili kufanikisha jambo hili la maulid ya kuzaliwa Mtume Muhhamd S.A.W.Wito wangu kwa waislamu na wasio waislamu, ni heshima kwa wanajamii wote kujitokeza kushiriki kwa hali na mali kuchangia na si lazima hadi wafuatwe, wafanye kwa hiari an uungwana wa mtu,”alisema.

Sheikh Kabeke alisema kwenye sherehe hizo kutakuwa na maonyesho ya shughuli za kijamii,zinazofanywa na waumini wa dini ya kiislamu pamoja na kuchangia damu.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Bakwata Mkoa wa Mwanza, Hamis Mwagao, alisema mambo mengi ya kuleta mabdiliko katika sekta za elimu na afya kwa waislamu na jamii yatafanyika hivyo ni fursa pia kwa Watanzania waishio nje ya nchi kuchangia vyakula na fedha za kufanikisha maulidi hiyo hapa kwani wageni kutoka nchi jirani za Burundi,Kenya, Uganda na Rwanda wahudhuria. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maulid hayo, Hamidu Selema  kiasi cha zaidi ya sh. milioni 100 zinahitajika.ssss

RAIS MSTAAFU WA KISIWA CHA MAYOTTE AHUDHURIA KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto waliokaa) akiwa amekaa wakiangalia burudani ya ngoma na Rais Mstaafu wa Kisiwa Cha Mayotte (wa pili toka kushoto) Mhe. Ahmed Ahoomani Douchina na wageni aliombatana nao kuhudhuria Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto waliokaa) akiteta jambo.
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Kenya kikiburudhisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Kwaya ya Kinondoni Revival ya Tanzania ikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Ngoma ya Kibati kutoka Zanzibar, Tanzania ikirindima katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Kikundi kutoka nchini Rwanda kikiburudisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Kikundi cha taarabu kutoka Zanzibar, Tanzania kikiburudisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam Septemba 21 - 28, 2019.
Kikundi cha watoto cha ngoma kutoka Tanzania kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Kikundi cha ngoma toka Uganda kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Wananchi wakipata burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.
Wasanii wa Kenya wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam, Tanzania  Septemba 21 - 28, 2019.

Fatma Mbaraka Salum azikwa leo asubuhi katika Makaburi ya Mwanakwerekwe

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili Mtaa wa Malindi kuhudhuria Mazishi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka Salum.
 Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiisamu wakimsalia aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka katika Msiki wa Malindi Mjini Zanzibar.
Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiisamu wakiishindikiza Maiti ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka kuipeleka kwenye malazi yake ya kudumu Mwanakwerekwe.
Picha na OMPR -ZNZ.
     
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Tekelezaji ya Mkoa Mjini Magharibi Mwishoni mwa Miaka ya 90 Bibi Fatma Mbaraka Salum aliyefariki Dunia Jana amezikwa leo asubuhi katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B”.

Bibi Fatma Mbaraka ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Mwaka1998 na kujiuzulu Mwaka 1999 alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya Kisukari na shindikizo la Damu.

Mamia ya Waumini wa Dini ya Kislamu, Wananchi pamoja na Wanachama wa Vyama vya Kisiasa kutoka maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Unguja wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Serikali walihudhuria Mazishi hayo yaliyofanyika Mtaani kwake Malindi Mjini Zanzibar.


Marehemu Bibi Ftma Mbaraka Salum alizaliwa Mnamo Tarehe 01 Oktoba Mwaka 1943 na baadae kupata Elimu yake ya Dini na Dunia kama ulivyo utaratibu wa Utamaduni wa Watoto wa Taifa hili.

Mnamo Mwaka 1964 Bibi Fatma alijiunga rasmi na Chama cha Afro Shirazy Party na kuteuliwa kufanya Kazi ya Katibu Muhtasi wa Aliyekuwa Meya wa Mji wa Zanzibar Makao Makuu ya ASP kuanzia Mwaka 1966.

Katika maisha yake kwenye Ulingo wa Kisiasa Marehemu Bibi Ftma Mbaraka Salum alikuwa Kamanda wa Jimbo la Malindi na baadae akiwa Mwanake pekee Zanzibar kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM Malindi kati ya Mwaka 2002 hadi 2007.

Mwaka 2007 hadi 2015 Marehemu Bibi Ftma Mbaraka alikuwa Balozi Nambari Moja Tawi la Chama cha Mapinduzi Malindi ambapo baadae alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee Tawi la Malindi.

Wana Mtaa wa Malindi wataendelea kumkumbuka Bibi Ftma Mbaraka Salum kama Mama Mlezi wa Mtaa huo kutokana na sifa ya ukarimu na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Jamii yote iliyomzunguuka hasa Vijana na Watoto.

Kila Nafsi itaonja Mauti kama alivyoagiza Mwenyezi Muungu Muumba wa Mbingu na Ardhi na hivyo ndivyo ilivyomkuta Bibi Fatma Mbaraka akirejea kwa Muumba wake akituacha sisi kwenye foleni ya kurejea wakati wowote kuanzia sasa kuipata haki hiyo isiyokimbilika.

Marehemu Bibi Fatma Mbaraka Salum aliyefariki Dunia akiwa na Umri wa Miaka 76 ameacha Mtoto Mmoja. Mwenyezi Muungu ampe hatma njema alikotambukia. Amin.Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/09/2019.

WITOWAKUJIUNGANAMAFUNZOYAIDARAYAUHAMIAJI

$
0
0
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linatangaza orodha ya majina ya nyongeza ya vijana Operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya askari wa Idaraya Uhamiaji.

Vijana hao idadi16 wanatakiwa kuripoti katika Chuo Cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa, kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam ifikapo tarehe 26 Septemba 2019 tayari kwa kuungana na vijana wenzao waliochanguliwa awali.

Uteuzi huo unafuatia usaili uliofanywa na Idara ya Uhamiaji mwezi Agosti 2019 kwenye Kambi ya Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na aina ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, inapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

Imetolewana:
Kurugenziya Habarina Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 24 Septemba 2019


ORODHA YA MAJINA YA NYONGEZA YA VIJANA WA JKT OPS KIKWETE NA OPS MAGUFULI WANAOTAKIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI WA UHAMIAJI

UONGOZI WA MKOA SIMIYU WABAINI UBADHILIFU WA SHILINGI MILIONI 55 BUSEGA

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani, Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akifungua kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Na Stella Kalinga, Simiyu
UONGOZI  wa Mkoa wa Simiyu umebaini Ubadhilifu wa kiasi cha shilingi  55,580,000/= ambazo ni sehemu ya mkopo uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji wa makazi (Viwanja) 3700 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega uliofanywa na Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya  fedha za mradi huo katika kikao cha  Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba 06,2019 Nyashimo Busega.

Sagini amewataja watumishi waliohusika katika ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Anderson Njiginya, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa mradi Raymond Mahendeka na mhasibu wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Sagini ameongeza kuwa timu ya uchunguzi imebaini mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo ikiwa ni pamoja na ukikwaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha, ukiukwaji wa masharti ya mkataba, ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma, udanganyifu na uzembe na usimamizi dhaifu wa Mradi.

“Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza watumishi waliohusika warejeshe fedha hizo haraka ili mradi utekelezwe kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za nidhamu zichukue hatua stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi wa Umma,” alisema Sagini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma wataalam wa Mkoa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi waliohusika walio chini  ya mamlaka yake kama  viongozi wa mkoa walivyoelekeza.

Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe, Goodluck Nkalango amesema madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ardhi hawakushirikishwa katika utekelelezaji wa mradi wa urasimishaji, makazi jambo ambalo lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa sahihi za mradi ikiwemo utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa waliohusika.

“Tumeipokea taarifa ya uchunguzi kupitia kikao cha baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi tutaanzia pale walipoishia kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema Mpemba.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega ilipokea mkopo wa shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi kutekeleza Mradi wa urasimishaji wa makazi viwanja 3700 katika kata za Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi; kwa mujibu wa taarifa ya Uchunguzi hadi kufikia Septemba  06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni  asilimia 98.

MAKAMU WA RAIS SAMIA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MTOTO WA MKUU WA MAJESHI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mkuu wa Majeshi Nchini, Jenerali Vennas Mabeyo kutokana na kufiwa na Mtoto wake aliyepatata ajali ya ndege wakati Makamu wa Rais alipofika Nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam leo sept 25,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mke wa Mkuu wa Majeshi Nchini, Tina Mabeyo kutokana na kufiwa na Mtoto wake aliyepatata ajali ya ndege wakati Makamu wa Rais alipofika Nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam leo sept 25,2019.
Baadhi ya waombolezaji.
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira, Georhe Simbachawene akimfariji Mkuu wa Majeshi Nchini, Venacne Mabeyo kutokana na kufiwa na Mtoto wake aliyepatata ajali ya ndege Nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam leo sept 25,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini saini kitabu cha maombolezo mkufuatia kifo cha mtoto wa Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Mabeyo kutokana na kufiwa na Mtoto wake aliyepatata ajali ya ndege wakati Makamu wa Rais alipofika Nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam leo sept 25,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Nelson Vennas Mabeyo Mtoto wa Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Vennas Mabeyo aliyefariki kutokana na ajali ya Ndege, Hafla hiyo imefanyika leo Sept 25,2019 nyumbani kwa Jenerali Mabeyo Msasani Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakitoka katika Msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi aliyefariki dunia kwa ajali ya ndege.

Majina ya nyongeza ya kujiunga na mafunzo ya idara ya uhamiaji haya hapa

Mloganzila kuendelea kushirikiana na Korea kutoa huduma za afya

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (katikati) Prof. Lawrence Museru akiwa na baadhi ya viongozi wa Muhimbili pamoja na viongozi kutoka Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) wakijadiliana juu ya hati ya makubalino kati ya KOFIN na Muhimbili.
 Prof. Museru akipitia hati ya makubaliano ambayo itasainiwa kesho.
 Kim Hyunkyong kutoka KOFIH akifafanua jambo kuhusu uboreshaji wa huduma za afya.
Baadhi ya viongozi wa MNH wakiwa kaika picha ya pamoja na viongozi kutoka KOFIH mara baada ya kumaliza majadiliano yaliyofanyika leo Muhimbili-Mloganzila.
UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo umekutana na uongozi kutoka Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) kwa lengo la kupitia na kujadiliana juu ya hati ya makubaliano kati ya KOFIH na MNH ili kuimarisha masuala ya uongozi wa hospitali pamoja na kuwajengea uwezo watumishi katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla.
Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema makubaliano hayo yatahusisha wataalam kutoka Korea kuja Tanzania ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa watalaam wa Hospitali ya Mloganzila.
Kupitia makubaliano hayo wataalam wa Mloganzila watapata fursa kwenda nchini Korea kwa ajili ya kupata mafunzo ya fani mbalimbali za huduma ya afya.
“Wataalam kutoka Korea tumekua tukishirikiana nao katika kutoa huduma za afya ikiwemo za kibingwa na hatua hii ni fursa nzuri kwa wataalam wazalendo kuendelea kujengewa uwezo zaidi na kubadilishana uzoefu” amesema Prof. Museru.
Hati ya makubaliano (Memorandum of Understanding) inatarajiwa kusainiwa kesho.

BREAKING NEWZZZZZZZZ....... AFYA YA ASKOFU MKUU RWA'ICHI YAIMARIKA, ARUHUSIWA

$
0
0
Baada ya kukaa ya Muhimbili kwa muda wa wiki mbili, Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Yude Ruwa'ichi ameruhusiwa kutoka katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amefanyiwa upasuaji wa kichwa.

KUNA WATUMISHI WATATOKEA POLISI KWENDA KWENYE KAZI ZAO HADI MIRADI IKAMILIKE- RC MAKONDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watendaji wa Manispaa zote za Jiji Dar es Salaam wakiongozwa na wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wakandarasi jijini Dar es Salaam leo.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na watendaji wa Manispaa zote za Jiji hilo wakiongozwa na wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wakandarasi wanaosimamia miradi mbalimbali ambapo amesikiliza ripoti za utekelezaji wa miradi katika halmashauri zote.

Baada ya kusikiliza miradi inayotekelezwa katika kila Wilaya na changamoto zake Makonda amesema kuwa lazima watendaji wajenge timu ya matokeo chanya na washirikiane katika kutatua changamoto.

Akizungumza leo Septemba 25,2019 jijini Dar es Salaam Makonda amesema kuwa.

"Isifike hatua hadi kiongozi mkubwa anakuja na kukuta mapungufu wakati kuna viongozi wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo, aliyekuwa ananielewa ni Hapi aliyekuwa Dc wa Kinondoni wengine wanaambiwa hivi wanafanya vile, nawahakikishia kuna watu watatokea Central kwenda kwenye kazi zao na kuna watu watahama nyumbani kwao hadi miradi ikamilike nitaongozana na RAS na kamanda Mambosasa muda wowote kuanzia leo kukagua miradi."

Aidha Makonda amewataka watendaji wa manispaa zote kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia gharama za miradi pamoja na kutumia vya ndani katika kutumia malighafi zinazozalishwa nchini.

MAHAKAMA YA KISUTU YATUPILIA MBALI OMBI LA KATIBU MKUU CHADEMA

$
0
0





Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freiman Mbowe akisalimiana na Naibu katibu Mkuu Tanzania bara na Mbunge wa jimbo la Kibamba,John Mnyika leo akiwa katika mahaka ya mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.

 Viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo wakiwa katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko waliokuwa wanaiomba mahakama hiyo kusafiri kwenda nje ya nchi kwa nyakati tofauti. 

Pia mahakama imewataka washitakiwa hao bila kujali nyadhifa zao kuwepo mahakamani kama washitakiwa wengine.

Imeelezwa kuwa, washitakiwa hao sasa watatakiwa kujitetea kwa siku  tano mfululizo kuanzia Oktoba 7 hadi 11,2019 na mahakama inategemea kuwa hakutakuwepo na sababu zingine zozote zitakazosababisha kesi hiyo isianze kusikilizwa.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema, safari hizo ni mambo yao wenyewe na hayahusiani na ratiba ya mahakama.

Amesema kuwa, iwapo mahakama itaruhusu maombi ya washtakiwa hao kusafiri, itakuwa imefungua mwanya kwa washtakiwa wengine kwani tukiruhusu haya leo hatutaweza kukataa kwa mwingine ukizingatia kuwa washtakiwa hawa wote ni wabunge.

"Maombi haya hayana msingi, hii kesi sasa hivi haiko kwenye hatua ya kutajwa, washtakiwa walikutwa na kesi ya kujibu na sasa wanatakiwa kujitetea" amesema Hakimu Simba.

Ameongeza kuwa, kesi hiyo ni ya muda mrefu, inalalamikiwa sana, inatakiwa kusikilizwa na kufika mwisho na Profesa Safari alisema wanamashahidi wengi sana hivyo kesi hii inahitaji kupangwa mara kwa mara kwa ajili ya kusikilizwa upande wa utetezi.

Jana, Wakili Profesa Abdallah Safari aliwasilisha maombi mawili mahakamani hapo ya kuahirisha  kesi hiyo hadi Oktoba 7 na 8 mwaka huu kwa sababu wanahitaji kupata muda wa kutosha kujiandaa na utetezi.

Amedai kuwa wanahitaji muda wa kutosha wa kujiandaa na utetezi kwa kuwa wana mashahidi wengi ambao wanahitajika kutafutwa na kuandaliwa. 

Pia ameomba ruhusa ya kusafiri kwa mshtakiwa Mashinji  kuanzia Septemba 26 mpaka Oktoba 6 mwaka huu kwenda Uingereza huku mshitakiwa Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, kuanzia Septemba 25 hadi 28, mwaka huu anatakiwa kwenda Kigali nchini Rwanda na Oktoba 13 hadi 18 atakwenda kuiwakilisha nchi barani Ulaya. 

Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi walipinga maombi hayo yote kwa kuwasilisha hoja mbali mbali. 

Barua ya maombi ya kusafiri Mashinji haijitoshelezi kwani haielezi anakwenda huko kufanya nini na kwanini aende mshitakiwa huyo ambaye tarehe hizo shauri lake litatajwa mahakamani, " alidai Nchimbi. 

Kuhusu mshitakiwa Matiko,  Nchimbi alidai barua ya mshitakiwa huyo inaonesha imetoka Chama cha Wanasheria Wanawake (Tawla)  kwenda kwa Katibu wa Bunge wakiomba uwakilishi wa wabunge sita nchini Kigali. 

Ameidai hayo yanabaki kuwa maombi ambayo yanaweza kukubaliwa au kukataliwa na kuongeza kuwa hakuna sababu ya mshitakiwa huyo kwenda safari hiyo kwa kuwa kuna uwakilishi wa wabunge wengine watano. 

"Ni vema ikafahamika kwamba mtuhumiwa anapokuwa na kesi mahakamani ni wazi ratiba yake kiasi fulani itaingiliwa na taratibu za mahakama,  kama itakuwa kila mshtakiwa akijisikia kusafiri anapatiwa ruhusa kwa vyovyote vile shauri hili halitafikia mwisho," alidai Nchimbi. 

Mbali na Mashinji na Matiko,  washitakiwa wengine ni Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Mbunge wa Kawe  Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images