Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

UONGOZI TANGA CEMENT WAJIVUNIA MAFANIKIO,WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUONGEZEWA MABAHEWA KUSAFIRISHA SARUJI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Tanga

UONGOZI wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Tanga Cement mkoani Tanga kimesema kinajivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, uongozi huo umesema pamoja na kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania(TRC), kuna changamoto ya uchache wa mabehewa kwa ajili ya kusafirisha saruji jambo ,hivyo wametoa rai ya kuongeza mabehewa japo 300.

Hayo yameelezwa wakati ziara ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambao wamepata fursa ya kutembelea kiwanda hicho kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji, kupata taarifa za mafanikio na changamoto.

Akizungumza jana mkoani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Reinhardt Swart amewaambia waandishi wa habari kiwanda kinajivunia kuendelea kuzalisha saruji iliyo bora ukilinganisha na washindani wao kwa kuwa na viwango vya ubora wa Kimataifa na hivyo kuwa na soko la uhakika.

"Mkakati wetu siku zote ni kuendelea kuzalisha saruji inayokidhi viwango vya ubora wa kimataifa.Gharama tunazotumia ni kubwa katika uzalishaji ambazo zinatokana na umeme, mafuta na klinka ambayo inatumika wakati wa kutengeneza saruji kiwandani,"amesema Swart.

Alipoulizwa kuhusu usafiri wa kutumia reli kusafirisha saruji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mara nyingi wamekuwa wakipata changamoto ya kutokuwepo kwa mabehewa ya kutosha ambapo hali hiyo inasababisha kiwanda kushindwa kufikisha sokoni zaidi ya tani 10,000 - 15,000 kwa mwezi.

Amefafanua kwamba changamoto hiyo inasababisha kuongezeka kwa bei ya saruji kutokana na kukosekana kwa bidhaa sokoni.Hata hivyo amesema ni nafuu na rahisi sana kusafirisha saruji kwa kutumia reli na kuongeza kuwa inakuwa nafuu zaidi endapo unasafirisha mzigo maeneo ya mbali zaidi. 

"Ni rahisi kwa upande wa kampuni na kwa upande wa serikali pia kwani matumizi ya reli yanapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa barabara hivyo kufanya miundombinu ya umma kubaki salama. Ukweli uliopo kama kampuni tunapendelea zaidi matumizi ya reli,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mwezi kiwanda kinahitaji zaidi ya mabehewa 455, hivyo kama watapata mabehewa 300 yatakayojikita kwao itakuwa heri zaidi na kilio cha kutokuwepo kwa mabehewa kitapungua.

"Tunaweza kupeleka mabehewa 40 kutoka Tanga mpaka Arusha ndani ya wiki moja. Kila behewa linaweza kubeba tan 40 za saruji,"amesema wakati anafafanua kwa waandishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart akiwaeleza Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda chicho mwishoni mwa wiki,namna wanavyojivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.Picha na Michuzi JR.

Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda cha Tanga Cement wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart alipokuwa akiwaeleza shughuli mbalimbali zifanywazo na Kiwanda hicho,mwishoni mwa wiki.


Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart wakati alipokuwa akizungumza.
Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart.

Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.Picha na Michuzi JR.
Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Tanga Cement,Diana Malambugi akifafanua ni namna gani Kampuni hiyo imekuwa ikitoa ajira katika ngazi mbalimbali za Idara za Kiwanda hicho,ikiwemo na namna ya kuhakikisha mambo ya jinsia yanazingatiwa huku akibainisha kuwa Katika kiwanda hicho suala hilo limezingatiwa vilivyo.
Mhandisi Gadiel Benjamin wa Kiwanda cha Tanga Cement akionesha sampuli za udongo na madini ya aina ya Limestone yanayotumika kutengenezea Saruji. katika kiwanda hicho wakati alipotoa mada kuhusu uzalishaji wa Saruji,mbele ya Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Kiwanda cha Tanga Cement ,Nuru Mtanga akifafanua jambo na kuwashukuru wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kutokana na namna wanavyotoa ushirikiano kwa kiwanda hicho.

Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Tanga Cement ,Logolieki Mollel akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nama saruji inavyochanganywa kitaalamu na hatimae kuipata Saruji iliyo bora na yeye kiwango cha Kimataifa

JAMAFEST 2019 YAZIDI KUNOGA, WASANII MBALI MBALI WAJITOKEZA KUSHIRIKI

$
0
0
Tamasha la Jamafest 2019 linazidi kunoga huku wasanii na vikundi mbali mbali vya ngoma vikijitokeza kushiriki kwa ufasaha kwa nchi za Tanzania ambao ni wenyeji, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Tamsaha hilo lililoanza Sepetemba 21 linatarajiwa kumalizika Septemba 28, 2019.

KARIBU UJIONEE URITHI WA UTAMADUNI NA SANAA ZA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0


UTAMADUNI ni mfumo wa maisha ya watu jinsi wanavyoishi na maendeleo yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na hivi ndivyo Tanzania inavyotunza utamaduni wake katika tamasha la utamaduni na Sanaa za jumuiya ya Afrika Mashariki linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mambo yanayofanya Tanzania kutunza utamaduni wake ni heshima iliyopo miongoni mwa jamii na husaidia watu kuwa na maendeleo kwa sababu ya heshima hiyo.

Tamasha la nne la JAMAFEST linaipamba Tanzania kwa kuwa nchi yenye utamaduni imara ndio maana Tamasha la utamaduni na Sanaa la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanyika hapa nchini.

Tamasha hili la JAMAFEST linaunganisha nchi za Afrika Mahariki ili kila nchi ioneshe utamatuni wake kwa nchi mwanachama katika utamaduni na sanaa zake.

Tamasha la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili kuzunguka nchi wanachama ambalo hufanyika kwa muda wa siku nane huku likionesha kivutio vya nchi mbalimbali.


 Wasanii wakitumuiza katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam. Ikiwa Tanzania ni mwenyeji wa Tamasha hili.




 Kikundi cha Ngoma za asili hapa nchini ngoma ya unzinza kutoka Buchosa Sengerema jijini Mwanza wakitumbuiza katika tamasha la Jumuia ya Afrika Mashariki la JAMAFEST linaloendele kufanyika jijini Dar  es Salaam katika Uwanja wa Taifa. 
 Baadhi ya banda la utamaduni na sanaa katika maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za jumuia ya Afrika Mashariki linalofanyika jijini Dar es Salaam Septema 21 hadi 28.
 Picha ya Kuchorwa.
 Kikundi cha Ngoma za asili kutoka Kukoba.


 Kikundi cha Ngoma ya asili kutoka Rwanda wakijiaanda kwa kutumbuiza.
 

 Kikundi cha Ngoma ya asili kutoka Mkoani Mbeya wakitumuiza katika tamasha la nchi za Juia ya Afrika Mshariki la Utamaduni na Sanaa la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


 Uremo uliotengenezwa na karatasi za kalenda katika banda la watu wa nchini Uganda. Hii ni katika Tamasha la Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki la JAMAFEST linalofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



Mabanda ya kuonesha bidhaa za kiutamaduni na sanaa za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika jijini Dar es Salaama katika uwanja wa Taifa.

MABINGWA WAPYA ANGELA KAIRUKI CUP 2019 WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO.

$
0
0
Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu ,Uwekezaji ,Angela Kairuki akizungumza wakati wa mchezo wa fainali ya Mashindano ya Angela Kairuki Cup 2019 alipoalikwa kama mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhi zawadi kwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Katibu wa Cha soka wilaya ya Same,Nathaniel Msuya akisoma taarifa fupi ya mashindano ya Angela Kairuki Cup wakati wa kuhitimisha ligi hiyi iliyodumu kwa muda wa miezi miwili ikishirikisha jumla ya timu 54 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Same. 
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji Angela Kairuki akisalimiana na waamuzi wa mchezo huo.
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Ujamaa fc Kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali. 
Waziri Kairuki akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kisiwani United kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali baina ya timu hizo mbili.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kisiwani united kabla ya kuanza kwa mchezo huo. 
Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Ujamaa fc kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kwa timu hizo ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Isaya Mungulu. 
Baadhi ya Mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mchezo wa fainali baina ya timu za Kisiwani united na Ujamaa fc zikimenyana kuwania ubingwa wa mashindano ya Angela KAiruki Cup 2019 .
Mashabiki wa timu ya Kisiwani United wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa na kutangazwa mabingwa wapya baada ya kuchapa timu ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi Hedaru.
Sehemu ya zawadi zilizotolewa kwa Mshindi wa kwanza na wa pili katika Mashindano hayo .
 Mgeni rasmi ,Waziri Kairuki akikabidhi Kombe kwa nahodha wa timu ya Kisiwani united mara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya soka ya Ujamaa fc bao 2 kwa 1.
 Waziri Kairuki akikabidhi fedha taslimu ,kiasi cha Sh Milioni 1.5 kwa nahodha wa timu ya Kisiwani United mara baada ya kuibuka Mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Waziri Kairuki aikabidhi pipikipi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Kisiwani United baada ya kuibuka mapbingwa wapya wa mashindano hayo. 

Na Dixon Busagaga ,Moshi.
 
Mabingwa wapya wa mshindano ya Angela Kairuki Cup 2019 timu ya Kisiwani united  wamekabidhiwa zawadi zao ambapo wamefanikiwa kijinyakulia zawadi ya Ng'ombe pesa taslimu kiasi cha sh Mil 1.5,Pikipiki moja, na Medali 25 kwa Wachezaji.


Zawadi kwa mabingwa hao wapya zimekabidhi na Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji ,Angela Kairuki mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kisiwani United   kutoka kata ya Kisiwani dhidi ya  timu ya Ujamaa fc ,ambapo Kisiwani walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa moja.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo,timu ya Ujamaa fc wamejinyakulia kitita Cha sh Mil moja,Medali na pikipiki huku mshindi wa tatu,timu ya Kiwanja fc akiambulia kiasi Cha sh laki tano pamoja na medali.

Katika mchezo huo mabao ya washindi yalipachikwa na Wachezaji Ally Rajab kunako dakika 35 ya kipindi cha kwanza huku mchezaji Juma Makumbi  akipigilia msumari wa pili uliowapatia ubingwa timu ya kisiwani fc.

Bao kwa upande wa timu ya soka ya Ujamaa fc iliyokuwa imesheheni wakongwe limefungwa na mchezaji Ezekiel Ombeni kunako dakika ya 40.

Katika mchezo huo ilishuhudiwa mchezaji Ally Mbaga akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa pembeni wakati akilalamikia maamuzi yake dhidi ya bao lililofungwa n timu ya Ujamaa fc.

 
Mashindano ya Angela Kairuki Cup yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika wilaya ya Same na kushirikisha timu kutoka kata 32 za wilaya hiyo huku mdhamini Mkuu wa mashindano hayo ,Wazxiri wan chi,ofisi ya Waziri Mkuu ,uwekezaji ,Angela Kairuki akiahidi kuendelea kuyadhamini kwa miaka mitano.

MWISHO.


DC IKUNGI AWAONDOLEA HOFU WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANDALA MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mlandala katika mkutano wa hadhara alipofanya ziara ya kikazi juzi kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.
 DC Mpogolo akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kijijini hapo.
 DC Mpogolo akisalimiana na Mzee Ramadhan Ginza ambaye ni Chifu wa kijiji hicho.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanawake wakiwa kwenye mkutano huo.
 DC Mpogolo akiserebuka sanjari na wasanii wa kijiji hicho.
 Diwani wa Viti Maalumu (CCM) kutoka Tarafa ya Sepuka, Theresia Masinjisa akizungumza kwenye mkutano huo.
 Diwani wa Viti Maalumu (CCM) wa Kata ya Sepuka,  Halima Ng'ura akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hobela Kwilasa akizungumza.
Diwani wa Kata ya Mwaru,  Iddi Makangale.
 Mwananchi wa kijiji hicho, Musa Kamata akiuliza swali kuhusu sekta ya elimu.
 Asha Hassan akiuliza swali kuhusu afya.
 Hamza Ntandu akiuliza swali kuhusu vitambulicho vya Nida.
 Mzee Iddi Juma akiuliza swali kuhusu malisho ya ng'ombe.
 DC Mpogolo akiwa na Mzee Iddi Juma.
 DC Mpogolo akipitia nyaraka za ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Mdughuyu hapo alikuwa akipiga kazi bila ya kujali giza lililokuwepo.
 'Wazee ni dawa" DC Mpogolo akiteta jambo na wazee wa kijiji hicho. Kulia ni Mzee Ramadhani Ginza ambaye ni Chifu na Iddi Juma.
 DC Mpogolo akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mlandala.
Hapa DC Mpogolo, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Mwaru baada ya kumaliza riaza yake katika kijiji hicho.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo amewataka wananchi wa Kijiji cha Mlandala mkoani Singida kuondoa hofu waliyokuwa nayo kutokana na matukio ya kihalifu yaliyojitokeza 
katika kijiji hicho.

Mpogolo alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa katika ziara ya kikazi  Kata ya Mwaru ya kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha kwao baada ya kuteuliwa na Rais Dkt.John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.

"Nimesikia kuhusu vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika kijiji hiki yakiwemo mauaji nitawasiliana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ili kuzungumzia  suala hilo ikibidi mkuu wa polisi wa wilaya afanye utaratibu wa ulinzi" alisema Mpogolo.

Mpogolo alisema serikali haiwezi kuvumilia kuona watu wachache wakiharibu amani ya wananchi huku wakiishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.Mkuu huyo wa wilaya alifikia hatua ya kutoa kauli hiyo baada ya wananchi wa kijiji hicho kumueleza kuhusu wasiwasi wa usalama wao kufuatia matukio hayo ya kihalifu na mauaji.

Wananchi hao wakizungumzia matukio hayo walisema yanafanywa na baadhi ya watu kijijini hapo kwa kushirikiana na wageni.

"Watu wanaofanya matukio haya kwa kushirikiana na wageni wanafahamika tunakuomba mkuu wetu wa wilaya utusaidie katika changamoto hii kwani tumefikia hatua ya kuogopa kwenda 
kwenye shuguli zetu za maendeleo na kutembea peke yetu nyakati za usiku kuhofia usalama wetu" alisema mkazi wa kijiji hicho Ramadhani Tumbo.

TAARIFA KWA UMMA

OFISA USALAMA SHIRIKA LA POSTA ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv

OFISA usalama wa shirika la Posta Tanzania  George Mwamgabe  anashikiliwa na  mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kutumia shirika hilo.

Mbali na ofisa huyo, mamlaka hiyo pia inawashikilia watuhumiwa wengine watano ambao nao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza leo Septemba 23, 2019 Kaimu Kamishina Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya James Kaji amesema katika kipindi cha mwezi huu mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroine katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza pamoja na zaidi ya kilo 215 za vifurushi vya dawa za kulevya mirungi zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza ameongeza.

Kuhusu kukamatwa kwa Ofisa wa usalama wa shirika la Posta, Kaimu Kamishina Jenerali James amesema, mtuhumiwa huyo awali alitoweka kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake na Sasa yupo mikononi mwa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Akizungumzia kuhusiana na mirungi iliyokamatwa amesema uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa mkemia mkuu wa serikali ulithibitisha majani hayo yana kemikali aina ya Cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea wa mirungi.

Taarifa za awali zilibaini kuwepo kwa kasi kubwa ya usafirishwaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya hasa Uingereza, Canada na Ufaransa kwa njia ya Posta ambapo awali vifurushi hivyo vilikuwa vikisafirishwa kupitia Posta ya Dar es Salaam na sasa vimekamatwa vikisafirishwa kupitia Posta jijini Arusha.

Mamlaka hiyo imetoa rai kwa wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha mara moja na kutafuta kazi halali za kufanya kwa kuwa mkono wa sheria utawafikia popote walipo.

Waziri Kabudi aipongeza Airtel kwa kupanua huduma za kifedha Afrika Mashariki

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ameipongeza Airtel Tanzania kwa kushirikiana na makampuni dada ya Afrika Mashariki ili kuanzisha huduma ya pamoja ya kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.

Waziri Kabudi alitoa pongezi hizo ofisini kwake wakati akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw Suni Colaso Kuhusu huduma mpya za Airtel Money ambapo watumiaji wa huduma ya Airtel Money kutoka nchi hizo sasa wanaweza kufanya malipo katika nchi tajwa kwa kutumia simu zao wakiwa popote kwani huduma hii imeshazinduliwa tayari.

“Ushirikiano huu kati ya Airtel Tanzania na watoa huduma wengine wa Airtel kutoka Kenya, Uganda na Rwanda utasaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo nne kwani itakuwa rahisi kutuma na kupokea pesa, kulipia bidhaa au huduma mbalimbali kwa kupitia huduma hii ya pamoja ya Airtel Money,” alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, wafanya biashara sasa hawatalazimika tena kubeba fedha nyingi mifukoni wanaposafiri katika nchi hizi na pia ujumbe wanaopokea baada ya kutuma pesa ni ushahidi tosha wa malipo kwa kupitia Airtel Money.

“Sisi kama Serikali tunaunga mkono hatua hii ya Airtel kwa sababu itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza biashara katia ya nchi hizi za Afrika mashariki na pia kuendeleza ushirikiano mzuri ambao upo baina ya nchi hizi,” alisema huku akitoa wito kwa Watanzania watumie huduma hiyo kwa wingi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso alisema wao wanaamini uanzishwaji wa njia hii ya malipo na utumaji fedha katika nchi hizi za Afrika Mashariki utarahisisha biashara baina ya wananchi wa mataifa haya na kuifanya hii iwe ni njia ya kipekee ya malipo kati ya nchi na nchi nyingine.

“Huduma hii pia ni nafuu kwani ada au malipo yake ni nafuu mno ikilinganishwa na huduma nyingine za fedha kimataifa,” alimuambia Waziri.

Alisema kwa sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye simu zao kutoka mitandao mingine ya Airtel kutoka Zambia na Malawi na watoa huduma wengine duniani ikiwemo Qatar, Oman, Afrika Kusini, Uingereza, Ushelisheli na UAE na wanaweza kutuma na kupokea fedha kutoka Rwanda. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso ambaye alimpa taarifa kuhusu huduma mpya ya kulipia kwa Airtel Money kwa nchi za Afrika Mashariki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano.

NEC YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI MKOANI KAGERA.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera na kutoa semina juu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano huo mapema Septemba 23, Mwaka huu Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Asina Omari ametaja lengo la Semina hiyo kuwa ni kutoa taarifa juu ya kukamilika kwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura hivyo kuwaomba wadau hao kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi na jamii ili kufanikisha zoezi.

Bi Asina ameongeza kuwa mpaka sasa Tume imekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ya Uboreshaji ikiwa ni pamoja na uhakiki wa vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi ya Vifaa vya Uboreshaji wa Daftari, Mkakati wa Elimu ya mpiga kura, uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura n.k uboreshaji huo utafanyika kwa kutumia mashine  ya kielektroniki ya Biometriki (BVR).

Mkutano huo umehusisha Viongozi wa vyama Siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za kiraia, wawakilishi wa makundi maalum ya watu wenye Ulemavu, Vijana na wanawake na wanahabari.
 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Asina Omari akitoa hotuba yake kwa wadau (hawapo pichani)  wa Uchaguzi Mkoani Kagera wakati akitoa taarifa juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Daftari la kudumu la wapiga kura.
 Pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Daftari Bw. Frank Muhando akiwasilisha mada katika Mkutano na wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera.
Pichani ni Mwenyekiti wa Watu wenye ulemavu Mkoa wa Kagera SHIVYAWATA Bwn Novati Joseph akiuliza swali juu ya Kundi la watu wenye ulemavu kutopewa makabrasha yenye nukta nundu.

 Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera.

KAGERA SUGAR WAWASILI SALAMA NYUMBANI, WAAHIDI MAKUBWA KWA MASHABIKI .

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Timu ya Mpira wa Miguu ya Kagera Sugar FC inayocheza Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imewasili salama Nyumbani Mkoani Kagera Baada ya Kucheza Mechi tatu za Ugenini,  na kuibuka na Ushindi mfululizo.

Timu hiyo imewasili Wilayani Missenyi ilipo kambi yao usiku, na Kisha kuelekea Bukoba Manispaa na kufanya mazoezi mepesi tayari kuziwinda pointi tatu muhimu dhidi ya mechi yao na wekundu wa msimbazi, klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam.

Mwalimu wa Timu hiyo ya wakata Miwa wa Kagera Mecky Maxime amesema kuwa Timu ipo katika hali mzuri na wako tayari kwa mapambano huku akiongeza kuwa Simba ni Timu kubwa hivyo maandalizi lazima yawe mazuri kuikabili akisistiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu Timu yao Iendeleze ushindi.


Kagera sugar inaingia tena kuwanjani Alhamisi hii kutafuta pointi tatu dhidi ya Simba huku rekodi zikionesha Timu hiyo kuifunga klabu ya Simba Mara tatu mfululizo kwa mechi waluzokutana, kubwa zaidi ni Timu ya Kagera imeanza msimu wa Ligi bila kufungwa na mechi zote ikiwa imecheza Ugenini, hivyo inaongoza Ligi kwa jumla ya Pointi tisa mpaka sasa.
Mwalimu wa Timu ya Kagera Mecky Maxime

KKKT KIMARA YAADHIMISHA MIAKA 10 BARAKA NA UTUMISHI

$
0
0
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Joyce Ndalichako (wapili kulia) na Askofu Thomas Skrenes (wapili kushoto) wakikata utepe wa uzinduzi wa jengo la kulelea watoto Yatima katika kanisa la KKKT Kimara. Wengine pichani ni Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kimara Wilbroad Mastai (kushoto) na Askofu Msaidizi, Chadiel Lwiza (kulia).

Usharika wa K.K.K.T. – Kimara ambao ni sehemu ya Jimbo la Magharibi, Dayosisi ya Mashariki na Pwani umetimiza miaka 10 ya Baraka na Utumishi kwa kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi  kwa washarika wake.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya kuadhimisha miaka 10 tangu Mchungaji (Mch.) Wilbroad Mastai alipopewa dhamana ya kuwa Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kimara, Kanisa hilo limeweza kupitia mafundisho imara kuhusu uchumi Kibiblia kuwajengea maarifa washarika namna ya kumiliki na kutawala uchumi wao.

Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa Kanisa limeweza kufungua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kwa shule ya awali na msingi inayotambulika kwa jina la Jerusalem Pre & Primary School na kununua shule ya Sekondari inayotambulika kwa jina la Bunju Boys.

Mafanikio mengine ni pamoja na kujenga kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Usharikani hapo, kujenga Hospitali pitakayokuwa chini ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani na kumiliki hisa Mendeleo Benki.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mch. Mastai alisema: “Fadhili za huyu Mungu kwetu sisi hazihesabiki wala hazielezeki. Hata kwa vitu vya mwilini tu, ndani ya hii miaka kumi, Mungu ametuongeza na kutuzidisha.”

 “Wapendwa tulioko hapa leo hii, sisi wa usharika wa Kimara tumetafakari, tumejipima na kujitathimini, tukajiridhisha kuwa katika kipindi cha muongo mzima, mimi pamoja na waumini wa usharika huu, tukimwabudu Mungu na kutumika hapa usharikani, tumepewa neema na upendeleo mwingi sana, kwa Baraka za Rohoni na za mwilini,”

Mch. Mastai aliongeza kuwa “Mungu ameyagusa maisha yetu kwa mtu mmoja mmoja na pia kama Usharika. Na hata watu wengine wengi tusiowajua na wale wasiotujua, walisikia habari za Mungu wetu anayerehemu, wakakimbilia mahali hapa. Wengi wana neno la kusema juu ya wema wa Bwana. Fadhili za huyu Mungu kwetu sisi hazihesabiki wala hazielezeki. Hata kwa vitu vya mwilini tu, ndani ya hii miaka kumi, Mungu ametuongeza na kutuzidisha.”

Mch. Mastai alitoa shukran kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi njema anayoendelea kuifanyia nchi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanyika hapa nchini.

“Tunamshukuru, tunampongeza na kumtakia Baraka za Mungu Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Kazi yake ni njema sana. Tanzania inajengwa na inajengeka. Tanzania inajua hilo, Dunia inatambua hilo, Kuzimu nayo inajua hilo, hata Mbingu za Mungu wetu kwa kuwa ndiko yatokapo mema yote.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akitoa ujumbe kwa waumini walioshiriki ibada maalumu ya shukrani kwa baraka na utumishi katika kanisa la KKKT Kimara.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Joyce Ndalichako akiongea na waumini waliohudhuria ibada maalumu ya shukrani kwa baraka na utumishi katika kanisa la KKKT Kimara.
Mchungaji wa Kanisa la KKKT Kimara Wilbroad Mastai (aliyesimama) akifafanua jambo katika ibada maalum ya shukrani kwa baraka na utumishi katika kanisa hilo.
Mwalimu wa neno la Mungu Christoher Mwakasege akiongoza maombi kwa waumini walioshiriki ibada maalumu ya shukrani kwa baraka na utumishi katika kanisa la KKKT Kimara.
Washarika wa KKKT Kimara wakisikiliza mafundisho ya Mwalimu Christopher Mwakasege (hayupo pichani) alipohudhuria ibada maalumu ya baraka na utumishi kwa washarika wa Kimara.

PROF. KABUDI AMEFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MSAIDIZI WA RAIS WA MAREKANI NA MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA BI ERIN WALSH

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Aidhaa, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa baina ya Tanzania na Marekani. Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha mahusiano yaliyopo katika nyanja mbalimbali kwa faida ya Nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh. Pamoja nao ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero (katikati) akifuatilia mazungumza ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiagana na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.

SIJARIDHISHWA NA UTENDAJI WA OFISI YA MKURUGENZI KONDOA-DKT. KIJAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Kalamba wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao walimuomba awahimize Watendaji wake ili jengo la Kituo cha Afya Kalamba likamilike na kuanza kutoa huduma kwa Wanakijiji hao. 
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kalamba wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent (hayupo pichani) kuhusu umaliziaji wa Kituo cha Afya cha Kalamba ambacho kitakuwa kikihudumia zaidi ya Wanakijiji 13,000 wa Kalamba na Haubi.
Dkt. Alpha Kwilasa wa Kituo cha Afya cha Busi akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji huduma zinazotolewa katika kituo hicho cha afya wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua chumba cha kuhifadhia maiti alipotembelea miradi ya Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua chumba cha kuhifadhia maiti alipotembelea miradi ya Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa maagizo kwa uongozi wa kijiji hukakikisha wanafuatilia kila hatua ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika vijiji vyao ili viweze kumalizika kwa wakati alipotembelea wilayani humo.



Na Josephine Majura, Kondoa


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa muda wa siku 37 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha kuwa ujenzi wa vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba vinakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa vituo vya afya vinavyojengwa kwa fedha za Serikali katika vijiji mbalimbali Wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, ambapo alibaini kuna uzembe katika umaliziaji wa ujenzi wa baadhi ya vituo hivyo kikiwemo Kituo cha Afya Kalamba.

Alielezea kutoridhika na utendajikazi wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo katika usimamizi wa miradi hiyo muhimu kwa wananchi wakati Serikali ilikwishatoa fedha zote za kukamilisha miradi hiyo na kuagiza hadi Oktoba 30 mwaka huu miradi hiyo iwe imekamilika.

“Dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli yakuleta milioni 400 kwenye kituo hichi cha Afya ni kupata huduma lakini hatujaanza kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa”, alisema Dkt. Kijaji. 

Aliiagiza Ofisi ya Mkoa na Wilaya hukakikisha wanafuatilia vizuri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayofadhiliwa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa sababu Serikali haianzishi mradi mpya bila kutoa fedha zote za miradi husika. 

Serikali ilitoa fedha kwa nyakati tofauti kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa vituo vya afya vitano wilayani Kondoa kati ya vituo hivyo, vituo viwili vya Mauno na Busi vimekamilika, huku vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba havijakamilika. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent alimuahidi Dkt. Kijaji kutekeleza magizo yote aliyoyatoa hasa ya kulipwa kwa watumishi waliofanya kazi mbalimbali kwenye vituo hivyo vya afya ndani ya siku 14. 

Naye Mwanakijiji wa Mauno Bw. Haji Selemani, ameishukuru Serikali kwa juhudi mbalimbali inayofanya katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa huduma za jamii na kusifia huduma inayotolewa na Watumishi wa Kituo cha Afya Busi. 

Kwa upande wake Mwanakijiji cha Bereko Bw. Juma Saidi amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kwa kazi kubwa anayoifanya jimboni huko na kumuombea afya njema ili awe na nguvu yakufanya kazi na zaidi. 

Dkt. Ashatu Kijaji alikuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani Kondoa, mkoani Dodoma ambapo ametembelea mradi wa Ujenzi wa vituo vitano vya afya wilayani huyo ambavyo vinajengwa kwa fedha za Serikali na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakazi wa Wilaya ya Kondoa.

PHOENIX TANZANIA ASSURANCE WAFURAHI PAMOJA NA WATOTO YATIMA

$
0
0
 
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Phoenix Tanzania (Assurance Co. Ltd) Mubaraka Kibarabara (kushoto) amkimkabidhi sehemu ya msaada wa Chakula, Nguo, Vifaa vya Shule na Fedha Taslimu, Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatimba cha Hisani, Hidaya Mtalemwa, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kutembelea kituo hicho kilichopo Mbagala Maji Matitu, Dar es Salaam, juzi kutoa msaada. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya. (Picha Zote na Mafoto Media)

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Phoenix Tanzania (Assurance Co. Ltd) Mubaraka Kibarabara (kushoto) amkimkabidhi sehemu ya msaada wa Chakula, Nguo, Vifaa vya Shule na Fedha Taslimu, Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatimba cha Hisani, Hidaya Mtalemwa, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kutembelea kituo hicho kilichopo Mbagala Maji Matitu, Dar es Salaam, juzi kutoa msaada. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya. (kushoto) ni Meneja wa Phoenix, Robert Kalegeya.



Meneja akizungumza na watoto

Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya, akizungumza

Mfanyakazi wa Phoenix Tanzania Assurance Co. Ltd, akipiga picha na mtoto wa Kituo cha watoto Yatima Hisani, wakati walipowatembelea na kutoa msaada wa Chakula, Vifaa vya Shule, Nguo na Pesa Taslimu, ambapo pia walikula nao chakula cha mchana na kufurahi pamoja.

Na Mafoto Media

KAMPUI ya Bima ya Phoenix of Tanzania Assurance Co. Ltd, imejiwekea mkakati wa kusadia watoto Yatima kila mwaka ili kuweza kusaidia na kuendeleza vipaji vya watoto waweze kufikia malengo yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Rasilimali watu wa Kampuni hiyo, Mubaraka

Kabarabara, wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya Elimu, Chakula, Nguo na Pesa taslimu, walipotembelea katika Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Hisani kilichopo Mbagala Maji Matitu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Kabarabara alisema kuwa msaada huo uliokabidhiwa katika Kituo hicho, ulichangwa na wafanyakazi wa Kampuni hiyo baada ya mmoja wao kuwasilisha wazo na kujadiliwa kwa pamoja na kisha kufanyiwa kazi mpaka kukamilika kwa zoezi hilo.

''Lilikuwa ni wazo la mmoja wetu aliyewasilisha kwetu na baada ya kujadiliana ni jinsi gani tufanye ili kulifanyia kazi, tulikubaliana na kuweza kupata michango ya wafanyakazi na kujadili vitu muhimu vya kuwasaidia watoto hawa na kuwa na makubariano ya pamoja na ndiyo maana hii leo tumeweza kulifanikisha zoezi hili,

Lakini pia baada ya kujionea na kutambua mahitaji ya watoto hawa bado ni mengi na muhimu tumejiwekea utaratibu wa angalau kila mwaka tuwe tukifanya zoezi kama hili hata mara moja ila tukifanikisha zaidi angalau tuweze kufanya hivi kula na kufurahi na watoto mara mbili kwa mwaka. alisema Kabarabara

Mwishoni mwa wiki Wafanyakazi wa Kampuni ya Phoenix walifika katika Kituo hicho na kukabidhi msaada, ambapo pia walipata fursa ya kula chakula cha mchana pamoja na watoto wa kituo hicho cha Hisani chenye jumla ya watoto 40 wa kike wakiwa ni 19 na wa kiume 21.

Akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Phoenix, Mkuu wa Kituo hicho, Hidaya Mutalemwa, aliwashukuru wadau wa Kampuni ya Phoenix waliojitolea kufika na kutoa msaada kwa watoto wa kituo hicho chenye changamoto nyingi ambazo kuisha kwake kunategemea wadau mbalimbali.

''Hatuna neno zuri la kusema ili mtuelewe tunawashukuru kwa kiasi gani, ila mungu awabari kwa hiki mlichokitoa kwa watoto wetu leo wamefurahi kiasi wengine wanawalilia msiondoke muendelee tu kubaki nao, Changamoto ni nyingi katika kituo hiki ambazo nyingi zinategemea wadau kama ninyi ili watoto waendelee kuishi kwa amani na furaha kama hii leo''. alisema Hidaya.

Picha ya pamoja....

RUBANI NA ABIRIA MMOJA WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA NDEGE YA AURIC AIR KUANGUKA SERONERA,SERENGETI MKOANI MARA

$
0
0
Watu wawili wamepoza maisha katika ajali ya Ndege iliyotokea mapema leo huko Seronera, Serengeti mkoani Mara. Ndege hiyo mali ya Kampuni ya Auric Air inayodaiwa ilikuwa ikiruka kutokea uwanja mdogo wa Seronera kuelekea eneo la Grumet ilianguka wakati ikitaka kuruka. 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema, ndege hiyo yenye namba ya kuruka 5H-AAM ,Shelutete amebainisha kuwa ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuanguka ilipokuwa ikitaka kuruka kuelekea Grumet ikiwa na abiria mmoja. 

soma hapa chini kwa taarifa .


TAMASHA LA JAMAFEST BILA VAZI UTAMADUNI LA TAIFA

$
0
0
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akimsikiliza mmoja wa maafisa BASATA mara baada ya kutembelea banda la baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) katika Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afrika Mashariki  la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.

KUTUNZA utamaduni wa Taifa ni pamoja na mavazi na lugha hii ni tofauti kwa Tamasha la JAMAFEST linalounganisha nchini za Afrika Mashariki linalotangaza utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki na mwenyeji wa tamasha hilo hana vazi linalotambulisha utamaduni wa Tanzania.



Kwa upande wa Lugha Tanzania imekuwa mstari wa mbele kutangaza Lugha ya kiswahili na kuenea nchini nyingi za Afrika na hata mashariki ya mbali, hata hivyo imeonekana kwenye mitandao ya kijamii watu kutoka mabara mengine kuongea na kuimba kwa kutumia lugha ya kiswahili.

Tangu mwaka 2004 kumekuwa na harakati za Tanzania kutaka kuwa na vazi lake la taifa, lakini juhudi hizo zinaonekana kushindikana, huku sababu za msingi zikishindwa kuwekwa wazi na wahusika. 

Suala la vazi la taifa ni muhimu sana kwa lengo la kujenga utaifa na kutambulika kwa haraka kwa raia wa Tanzania, hasa anapokuwa nje ya nchi na pia kutangaza utamaduni wa Mtanzania.

Mwandishi wa MICHUZI BLOG ametembelea banda la Baraza la sanaa la Tanzania (BASATA) katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutaka kujua vipi mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi kutokana na kuwa tupo kwenye tamasha la utamaduni na sanaa kwa nchi za Afrika Mashariki?

Hata hivyo Afisa Tehama wa Baraza la sanaa Tanzania, Rajau Sorro amesema kuwa mchakato wa kupatikana kwa vazi la Taifa punaendelea na ifikapo mapema mwakani (2020) mchakato huo utakuwa umeisha na tutakuwa na vazi rasmi la Taifa.

Nae Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema kuwa watanzania watumie tamasha la JAMAFEST kutangaza lugha ya Kiswahili pamoja na utamaduni wa Tanzania.

Matumaini ni kuwa Tamasha la JAMAFEST litakapofanyika kwa maranyingine hapa nchini tutakuwa na vazi rasmi la taifa bila shaka kwani mchakato wake umebakia miezi michache.










 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afika Mashariki linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiangalia bidhaa mbalimbali wakati alipotembelea Tamasha la Utamaduni na sanaa la JAMAFEST linalohusisha nchi sita za Afrika Mashariki linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akimsikiliza mfanyakazi wa TBC amaye alikuwa akielezea chaneli ya utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyopewa jina la Tanzania Safari Channel mara baada ya kutembelea Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afrika Mashariki  la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.


 Kikundi cha Sanaa cha Lumumba Threatre wakitumuiza katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Vikundi vya sanaa vikijiandaa kutumbuiza.

MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA STAND MPYA YA MABASI MBEZI LUIS, AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI KABLA YA MEI 2020.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo September 23 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Stand mpya ya kisasa ya Mabasi ya Mikoani na Nchi za Jirani ya Mbezi Luis ambayo ujenzi wake umefikia 35% hadi sasa na Kumtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.

RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambapo ndani yake kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya mabasi 500, Shopping Mall, Hotel, Maegesho ya Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo, Kituo cha Polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.

Aidha RC Makonda amemuelekeza katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda Kamati ya kufuatilia Maslahi ya wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika miradi ya kimkakati ili kuhakikisha wanapata stahiki zao zote ikiwemo mishahara na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Pamoja na hayo RC Makonda ameendelea kuwataka wakandarasi wa miradi mbalimbali kuhakikisha wananunua vifaa kutoka kwenye Viwanda vya wazawa jambo litakalosaidia kuinua uchumi wa Viwanda na Taifa kwa ujumla.


Katika Ziara hiyo RC Makonda ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam.


WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATANGAZA UTARATIBU MAALUM KWA LENGO LA KUHUDUMIA WAFANYABIASHARA WA MIPAKANI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi madhubuti wa Rais John Magufuli, imedhamiria kuhakikisha kuwa biashara za mipakani zinaimarishwa na kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuondoa vikwazo vyote vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi na kuwezesha Wananchi na Taifa kwa ujumla kunufaika na kukuza biashara.

Hayo yamesemwa leo Septemba 23 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya ambapo amerumia nafasi hiyo kuutaarifu umma na wafanyabiashara wote nchini hususan wale wanaofanya biashara mipakani.

"Wizara kwa niaba ya Serikal imeweka utaratibu maalum utakaowezesha kutoa taarifa juu ya vikwazo, changamoto au kero za kibiashara hasa zile zisizokuwa za kikodi (NTBs) wanazokumbana nazo. 

"Lengo la kuweka utaratibu huu ni kuwezesha wafanyabiashara kupata huduma haraka kupitia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma mipakani. Kwa kuanzia, Wizara imetoa anuani maalumu za barua pepe na namba za simu za watendaji ambazo tutapenda kila mfanyabiashara anayepata vikwazo aweze kutoa taarifa kupitia namba hizo,"amesema.

Mhandisi Manyanya aidha amesema Wizara inawataka wakuu wa taasisi hizo walioko kwenye vituo vya mipakani kubandika orodha hiyo kwenye mbao za matangazo ili kurahisha mawasiliano

Ameongeza kuwa vikwazo visivyokuwa vya kikodi ni pamoja na rushwa ya kifedha na isiyo ya kifedha, urasimu na kutotoa miongozo ya taratibu zinazohitajika, kukosa taarifa muhimu na kutojua fursa zilizopo.

Amefafanua kwa upande wa Wizara, taarifa hizo zinapaswa kutumwa kwa Mratibu wa Vikwazo Visivyo vya Kiushuru (NTB’s) Aneth Simwela kupitia barua pepe tanzania@tradebarriers.org au kupiga simu katika namba +255622259341.

Amesema kwa changamoto za masuala ya Viwanda na Masoko, Wafanyabiashara na Wadau wanaweza kuwasilisha changamoto zao kupitia barua pepe dawatilamsaada@mit.go.tz au kuwasiliana na Andrew Shirima wa Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia namba ya simu +255713500532.

Pia Wizara na Taasisi ambazo zinazotoa huduma mipakani ni Mamlaka ya Mapato (TRA); Idara ya Uhamiaji, Wakala wa Vipimo (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Mkemia Mkuu wa Serikali; Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Kitengo ya Huduma za Afya ya Mimea, Idara za Maliasili na Utalii, Idara za Mifugo na Uvuvi Halmashauri za Wilaya na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Mhandisi Manyanya amesema kiwa prodha yenye majina ya Taasisi/Mamlaka na mawasiliano ya Maafisa Wasimamizi wa Taasisi hizo kwa huduma za mipakani inapatikana kwenye tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) www.tantrade.go.tz au kupitia barua pepe: info@tantrade.go.tz au feedback@tantrade.go.tz au wasiliana na Bw. John Fwalo kupitia namba ya simu +255767285252.

"Endapo hutaridhika na huduma kutoka Taasisi yeyote tajwa hapo juu, wasilisha malalamiko yako kwa barua pepe minister@mit.go.tz au ps@mit.go.tz. Unaombwa pia kutumia barua pepe tajwa endapo utaridhika na huduma zilizotolewa,"amesema Manyanya kwa niaba ya Wizara hiyo ya viwanda na biashara. 

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA MTAWALA WA RAS KHAIMAH LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mlango wa Zanzibar mwenyeji wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Alqasimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi yake Ras Al Khaimah,leo 23/9/2019.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh.Saud Bin Saqr Alqasimi, alipofika katika makaazi yake Al Dhait Raa Al Khaimah, akiwa katika ziara yake leo 23/9/2019.
UJUMBE wa Mtawala wa Ras Al Khaimah wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati wa mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na mwenyeji wake Mtawala waRas Al Khaimah. Sheikh Saud Bin Alqasimi, mazungumzo hayo yamefanyika katika makazi yake Al Dhait Raa Al Khaimah

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA GEITA NA KUFUNGUA NYUMBA ZA WATUMISHI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Nyumba za Makazi za Wakuu wa Idara na Vitengo wa Secretarieti ya Mkoa wa Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Nyumba za Makazi za Wakuu wa Idara na Vitengo wa Secretarieti ya Mkoa wa Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, Mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata na dulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Geita, Septemba 22, 2019. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wa Mkoa wa Geita wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo, Septemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Geita baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita Septemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images