Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

MASAUNI, TAASISI YA MISAADA YA ABDULLAH WATOA VIFAA KWA VIJANA VISIWANI ZANZIBAR VITAKAVYOWASAIDIA KUJIONGEZEA KIPATO

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),Mjumbe kutoka Shirika la Kuwawezesha Vijana la Abdullah,Rashid Ahmed(wanne kulia) wakimkabidhi Fundi Magari, Ally Saleh(wakwanza kulia),boksi maalumu la vifaa vya ufundi wakati wa kukabidhi vifaa mbalimbali kwa vijana wajasiriamali ikiwa na lengo la kuwasaidia kukuza vipato vyao na kuwaweka mbali na makundi hatarishi.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),Mjumbe kutoka Shirika la Kuwawezesha Vijana la Abdullah,Abdallah Mrusi(wanne kulia) wakimkabidhi Fundi Bodaboda,Mohammed Ally (wakwanza kulia),boksi maalumu la vifaa vya ufundi wakati wa kukabidhi vifaa mbalimbali kwa vijana wajasiriamali ikiwa na lengo la kuwasaidia kukuza vipato vyao na kuwaweka mbali na makundi hatarishi.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),akimkabidhi Mgeni Awadhi cherehani ikiwa na lengo la kumsadia kukuza kipato katika shughuli zake za ujasiriamali.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), Mjumbe kutoka Shirika la Kuwawezesha Vijana la Abdullah, Abdallah Mrusi (wanne kulia) wakimkabidhi Hussein Ally (wakwanza kulia), kifaa maalumu wakati wa kukabidhi vifaa mbalimbali kwa vijana wajasiriamali ikiwa na lengo la kuwasaidia kukuza vipato vyao na kuwaweka mbali na makundi hatarishi.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi






Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Hafla ya Utoaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujasiriamali kwa vijana ili kuwaepusha na makundi hatarishi kwa kuwawezesha katika kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya kazi za uzalishaji.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SUHULU AFUNGUA TAMASHA LA JAMAFEST 2019 JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni wa Rwanda Mhe. John Ntigengwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST lililoanza Septemba 21-28, 2019 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika nchi tatu, Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika Dar es Salaam, Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni wa Rwanda Mhe. John Ntigengwa (kulia) mara baada ya kufika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz wakati wa ufunguzi wa Tamasha la #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania kuanzia Septemba 21-28, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimia wananchi mara baada ya kufika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Tanzania katika ufunguzi wa JAMAFEST. Meza kuu... Brass Bendi ikiongoza nyimbo za Taifa za mataifa ya #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda wakati wa uzinduzi wa Tamasha la #JAMAFEST2019 #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Bendera za mataifa yanayoshiriki Tamasha la #JAMAFEST 2019
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnumz akitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la #JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Burudani ya ngoma kutoka #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda ikipamba moto katika uwanja wa Uhuru wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST.

Ngoma ya #Burundi ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ngoma ya #Kenya ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ngoma ya #Uganda ikipamba moto wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Burudani ya ngoma kutoka #Tanzania #Kenya #Uganda #Burundi #Rwanda ikipamba moto katika uwanja wa Uhuru wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST.

MAJALIWA AFUNGUA MAONESHO YA PILI YA TEKNOLOJIA YA DHAHABU MJINI GEITA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo wa Unaoonyesha Fursa za Uwekezaji wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu noti bandia na noti halali kutoka kwa Angela Kashanga (kulia) wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati alipotembelea banda la BOT katika Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na katikati ni Mkurugenzi wa BOT tawi la Mwanza, Florence Kazimoto. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtalaam wa Uchenjuaji madini, John Ngenda ( wa pili kulia) kuhusu mtambo wa kuchenjua madini wakati alipofungua Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa CCM, Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Watatu kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAMASHA LA 14 LA JINSIA KUFANYIKA VIWANJA VYA MABIBO DAR SEPTEMBA 24 -27

0
0
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia litakalofanyika Septemba 24 -27 jijini Dar es salaam



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki Tamasha la 14 la Jinsia litakalofanyika Septemba 24 hadi 27 mwaka huu katika Viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo jijini Dar es salaam.

Tamasha hilo likaloongozwa na Mada kuu 'Mwanaharakati wa Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia' limeandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia na wanaharakati binafsi. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumapili Septemba 22,2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi amesema washiriki wa tamasha hilo ni pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi,viongozi mbalimbali kutoka ngazi ya halmashauri na serikali kuu,wanaharakati na wananchi. 

"Tamasha la Jinsia la Mwaka huu lina umuhimu wa kipekee kwani kitaifa na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020.Kwa njia moja au nyingin maandalizi ya mkutano wa Beijing yalikuwa chachu kubwa ya kuanzishwa na kuimarishwa kwa asasi nyingi zinazotetea haki za wanawake ",alisema. 

"TGNP ni mojawapo ya asasi iliyoleta chachu kubwa ya kuunganisha wadau mbalimbali kutoka vikundi vya wanawake,wanazuoni na mitandao ya wanawake kupata sauti ya pamoja katika ushiriki wa mkutano wa Beijing,hivyo TGNP inaendelea kusherehekea uwepo wake kwa zaidi ya miaka 25 sambamba na maadhimisho ya mkutano wa Beijing",alieleza Liundi. 

Alisema Tamasha hilo linatoa fursa kwa asasi za kiraia zilizoshiriki katika mchakato wa Beijing kutakafari na kusherehekea uwepo wa asasi hizo kwa zaidi ya miaka 25 ambapo azimio na mpango kazi Beijing ndiyo iliyoweka misingii ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kidunia. 

"Kipekee Tanzania itakumbukwa katika historia ya kuweka misingi ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kwani katika mkutano wa Beijing,Balozi Mhe. Getrude Mongella aliibuka kidedea kwa Katibu Mkuu wa mkutano huo wa kihistoria hali iliyoiinua Tanzania katika ramani ya dunia",alisema Liundi. 

"Katika kuendelea kuenzi na kuthamini mchango wa Mama Getrude Mongella,TGNP na Tapo la Ukombozi,tumeamua kumchagua Balozi Mhe. Dr. Getrude Mongella aliyeongoza mchakato wa Beijing na pia mchakato wa 'Kuileta Beijing Nyumbani' kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Jinsia mwaka huu",alifafanua Liundi. Hata hivyo Liundi alisema mgeni maalum kutoka serikalini atakuwa Naibu Waziri- Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mhe. Dr Faustine Ndugulile. 

Alibainisha kuwa tamasha hilo litahusisha mawasilisho,mijadala ya pamoja,maonesho na warsha,kusherekea mchango wa mashujaa wanawake katika kufikia haki na usawa wa kijinsia. 
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2019 likalofanyika Septemba 24 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia. Kushoto ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Rehema Mwateba. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao Aseny Muro. 
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019. Amesema Tamasha hilo litahudhuriwa pia na wageni mbalimbali kutoka Afrika Kusini,Rwanda,Burundi,Eswatini 'Swaziland', Kenya,Uganda,Ghana na Zimbabwe. 
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema Tamasha la Jinsia 2019 litaongozwa na Mada kuu ''Mwanaharakati wa Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia' na mada ndogondogo ambazo ni 'Miaka 25 ya kujenga vuguvugu la Kifeministi 'kukabiliana na mfumo dume na utandawazi',Uongozi wa Kifeministi 'Mikakati na kujenga Tapo ka Ukombozi wa wanawake',Utengenezaji,uzalishaji na usambazaji wa maarifa ya Kifeministi ndani na nje ya tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi na kuendeleza tapo la ukombozi wa wanawake 'Ajenda yetu,mikakati yetu,mustakabali yetu'. 
Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea Tamasha la 14 la Jinsia 2019. 
Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao Aseny Muro akifafanua kuhusu Tamasha la Jinsia na masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao Agripina Mosha akielezea kuhusu masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao Rehema Mwateba akielezea kuhusu masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia.Wa kwanza kushoto ni Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana.

VIONGOZI WA DINI LINDENI AMANI YETU-DC KIGAMBONI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sarah Msafiri amewaomba viongozi wa dini wa wilaya  hiyo  kuilinda amani iliyopo nchini kwa  kuepuka kutoa matamko yanayoweza kuihatarisha.

Ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati  akizungumza katika mkutano wa hadhara katika  kata ya Kimbiji na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuilinda amani hiyo iliyodumu nchini tangu taifa lilipopata uhuru wake Mwaka 1961.

 Msafiri amewaomba  viongozi wa dini kuzidi kuwa chachu ya amani na kutumia nafasi waliyonayo katika jamii kwa kuwashawishi wananchi kudumisha amani ambayo ni tunu toka kwa mwenyezi Mungu.

Katika mkutano huo, Msafiri  amesema kuwa dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya binadamu, nakutaja kuwa hiyo ndiyo sababu ya serikali kuheshimu na kutambua mchango wa dini.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sarah Msafiri (kulia)akizungumza na wananchi wa kata ya Kimbiji kuhusu viongozi wa dini wa wilaya hiyo kuhakikisha wanailinda amani ya nchi,na kuepuka kutoa matamko ambayo hayafai, leo Jijini Dar es alaam katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kushoto) akisikiliza kero mbalimbli za wananchi katika ziara  yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

TAHLISO YAMUUNGA WAZIRI MKUU KUHUSU UBORESHAJI WA MITAALA YA ELIMU

0
0
Jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu Nchini Tanzania (TAHLISO) limeunga mkono agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyezitaka taasisi za elimu ya juu nchini kuboreshaji mitaala yake ya ufundishaji ili kuwapa fursa kuingia katika ajira binafsi hususani ujasiriamali.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa TAHLISO Peter Niboye alisema kimsingi suala hilo ni muhimu kwa kuwa litasaidia kuwaondoa maelfu ya vijana waliopo mitaani ambao wamekosa ajira licha ya kuwa na ufaulu mzuri katika masomo yao vyuoni.

Awali akifungua kongamano la kitaifa la ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa taasisi za elimu kuboresha mitaala yake ili kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri.

Akizungumzia hatua hiyo Niboye alisema agizo la Waziri Mkuu lina umuhimu mkubwa wakati huu ambao Tanzania inatekeleza sera yake ya uchumi wa viwanda  huku akiitaka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  kulisimamia suala hilo ili utekelezaji wake uweze kufanyika haraka iwezekanavyo.

“Hii siyo mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu kuligusia suala hili, alifanya hivyo pia Agosti 10 alipokuwa akifungua mkutano wetu wa kwanza mara baada ya hotuba yetu kuligusia suala hilo, kimsingi ifike mahali Wizara ya elimu ilisimamie suala hili ili kuwapa fursa vijana ya kujiajiri” alisema Niboye.

Aidha alisema uwepo wa mitaala mizuri  inayoweza kumuandaa mhitimu kujiajiri katika soko la ajira, kwa sasa lina umuhimu wa kipekee ikizingatia kuwa kwa sasa Tanzania inatekeleza sera yake ya uchumi wa viwanda iliyowezesha  vijana wengi kuona umuhimu wa kupata elimu inayoweza kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya viwanda.

“Hata ukitazama  katika vyuo mbalimbali hivi sasa utagundua kuwa vijana wengi wamekuwa wabunifu kwa kubuni mitambo inayoweza kuzalisha bidhaa mbalimbali, hii ni fursa ambayo kama Wizara ya elimu itaweza kuisimamia kikamilifi tutaweza kupiga hatua kimaendeleo” aliongeza Niboye.

Aidha akizungumza katika kongamano hilo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema sekta za elimu nchini inatakiwa kuandaa sera, sheria,kanuni na taratibu ambazo zitawawezesha watanzania kushiriki katikautekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini.

Alisema umefika wakati wakati kwa taasisi au sekta ya elimu kubadilisha mitaala ya shule ili kuwawezesha vijana kuingia katika shughuli za ujasiriamali badala ya mitaala ya sasa ambayo haitoi fursa hiyo.
Mwenykiti wa TAHLISO,Peter Niboye akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaa kuhusu  kuunga mkono agizo la Waziri Mkuu kuhusu taasisi za elimu kuboresha mitaala.

TALIRI YAJA NA TEKNOLOJIA YA MALISHO KUPUNGUZA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Dkt. Zablon Nziku akiwaonyesha waandishi wa habari majani bora yanayotumika kwa malisho ya mifugo wakati Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilipofanya ziara na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Tanga, Morogoro na pwani ya kutembelea na kujionea namna taasisi za utafiti zinavyofanya kazi zake. 
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Dkt. Zablon Nziku kushoto akiwaonyesha waandishi wa habari maharage bora yanayotumika kwa ajili ya malisho ya mifugo wakati Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilipofanya ziara na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Tanga, Morogoro na pwani ya kutembelea na kujionea namna taasisi za utafiti zinavyofanya kazi zake. 
KAIMU Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Costech Emanuel Abiner akisalimiana na mmoja wa watafiti kwenye wa Taasisi ya Mifugo Tanzania (Taliri) wakati alipowasili eneo hilo
Afisa Utafiti Mkuu Kiongozi Dkt. Bakari Msangi akiwa kwenye eneo hilo
KAIMU Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Costech Emanuel Abiner akisaini kitabu cha wageni

TAASISI ya ya utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) inayojihusisha na utafiti wa malisho bora ya mifugo imesema imekuja na teknolojia mbalimbali za malisho ili kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika kipindi cha kiangazi ili kukomesha migogoro hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi kutoka taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania Dkt. Zablon Nziku wakati tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) ilipofanya ziara na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Tanga, Morogoro na pwani ya kutembelea na kujionea namna taasisi za utafiti zinavyofanya kazi zake.

Dkt Nziku alisema kumekuwepo na migogoro mingi hususani kipindi cha malisho kuhusiana na ukosefu wa malisho katika kipindi cha kiangazi hivyo wamekuja na teknolojia ya kuhifadhi malisho ili mfugaji aweze kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula cha mifugo kwa mwaka mzima.

Alisema moja ya teknolojia waliyokuja nayo ni pamoja na kufunga aina ya malisho yakiwa makavu kwa kuhifadhi ambapo mnyama anaweza kuyatumia kama chakula kipindi cha kiangazi na hata masika kitendo
kitakachowawezesha wafugaji kupata maziwa mengi wakati wote.

Alisema kuwa mbadala wa malisho hayo utasaidia kupunguza kuvamiwa kwa mashamba ya serikali kwani kwani zipo teknolijia zinazoweza kutumika hata kwa mtu mmoja mmoja ili kuongeza ufanisi.

Dkt Nziku alisema endapo wafugaji wengi watafanikiwa kupanda aina hiyo ya malisho bora tija kwenye maziwa itaongezeka na hatimaye viwanda vitapata malighafi za kutosha hivyo ipo haja ya wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.

‘’Kiwanda chetu cha kuchakata maziwa cha Tanga fresh kinatumia maji kusafisha mitambo yao ambapo kwa siku wanalita laki moja na 20 ambapo maji wanayosafisha tumeona kuliko wayatupe wanayatrit ya kuyarudishiauhai ambapo sisi tunayatumia kumwagilia hili eneo la mfano kwajili kupata mbegu hizi,’’alibainisha Dkt Nziku.

Kwa upande wake Afisa utafiti mkuu kiongozi Dkt. Bakari Msangi alisema wao kama tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia kuanzia mwaka 2012 mpaka sasa wametoa bilioni 47 kwa taasisi mbalimbali za kitafiti kwajili ya kufanyia shughuli za kiutafiti ambapo kila mwaka wanatoa takribani bilioni 18-20 kwa miradi mbalimbali kutoka kwenye taasisi tofauti tofauti kulingana na namna walivyoshindanishwa.

Alisema matokeo chanya yanayofanywa na taasisi hiyo yanazidi kuwafanya wafadhili kuwa na motisha ya kuendelea kutoa ufadhili wao ambapo watafiti wamekuwa wakizitumia katika miradi ya kiutafiti.

Alisema jukumu la tume ni kuhakikisha wanasaidia tafiti na ubunifu kufanyika katika taasisi mbalimbali zikiwemo za utafiti na vyuo vya elimu ya juu na kati ya mambo wanayoyafanya ni pamoja na kuwajengea uwezo watafiti lakini pia kujenga vyema miundombinu ya kiutafitiikiwemo maabara lakini pia sehemu za mashamba.

Kwa upande wake Salvatory Kavishe kutoka kitengo cha malisho TALIRI alisema ni kuhakikisha wanapata mbegu za kutosha ili waweze kuwauzia wakulima ambao ni wafugaji ilin kuachana na ufugaji wa mazoea.

Alisema wametembea katika mikoa 10 Nchini kwajili ya kuchukua majani na kuyakusanya ambayo watayaboresha na kuwa mbegu bora ambapo kila mkoa wamechukua mbegu tatu tatu ili kuzifanyia utafiti ulionekana kuwa na matokeo makubwa.

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU SABA KWA WAHUJUMU UCHUMI,UTAKATISHAJI FEDHA WALIOKO MAHABUSU...SOMA ALICHOMSHAURI DPP, MAGEREZA

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambao wako mabuhusu kukubali makosa yao na kuahidi kutorudia tena ili watolewe mahabusu ambako wamekaa kwa muda mrefu.

Pia amesema baada ya kukubali makosa walipe fedha zikiwemo walizohujumu,utakatishaji,kukwepa kodi ya Serikali na aina nyingine ya hujuma, na watakaoshindwa kukubali ndani ya muda huo ambao ameutoa basi watabaki huko huko mahabusu ili sheria uendelee kuchukua mkondo wake.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Septemba 22,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapisha viongozi mbalimbali aliowateua juzi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo baada ya kuapisha viongozi hao ametumia nafasi hiyo kuonesha kusikitsha kwake na mahabusu waliokaa muda mrefu ambao wengine wanatuhumiwa kwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.

"Kwa kweli naumia sana moyo ninapoona mahubusu wanakwenda mahakamani na kurudi mahabusu ,wengine wamekonda.Najua haya mambo yanakwenda kwa mujibu wa sheria,ingekuwa uwezo wangu ningewasamehe wote wenye kesi za aina hiyo baada ya kukubali makosa na kuahidi kutorudia tena.

"Mimi natoa wazo tu,wanasheria mtaangalia kama inawezekana,binafsi napenda waondolewe mahabusu,natamani kuona mahabusu wanapungua na ikiwezekana siku moja niamke na kukuta hakuna mahabusu magerezani,'amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa DPP pamoja na wakuu wengine wa Idara zinazohusiana na mahabusu kukaa na ndani ya siku saba wale wote ambao watakiri makosa wawekewe utaratibu wa kulipa fedha."Natoa siku saba kuanzia leo".

"Kwani leo siku gani. Ni Jumapili,kumbe ni siku nzuri sasa kuanzisha kesho mkae DPP na wenzako kwa ajili ya kushughulikia hili.Huu ni ushauri wangu kwenu,niliwahi kusema huko nyuma sitaki kuongeza nchi ambayo watu wake wametawaliwa na machozi,"amesema.

Wakati anazungumzia kupunguzwa kwa mahabusu Rais Magufuli amesema Mkuu wa Magereza nchini , amemuandikia barua kwa ajili ya kuomba kuongeza askari magareza ambapo wanahitaji askari magereza 800."Nimeiangalia ile barua sijajibu na ukweli siwezi kukubali ombi lao. Badala ya kufikiria kupunguza mahabusu wanafikiria kuongeza askari."

Wakati huo huo Rais Magufuli amezungumzia suala la kuteua na kutengua teuzi ambako amesema ni kazi ngumu inayomuumiza kichwa na wala hayaendi kutengua lakini kuna wakati anavumilia mambo yanavyokwenda lakini ameamua kutengua na hasa ninapoona aliyepewa nafasi nashindwa kutimiza wajibu wake.

"Viongozi wenzangu kafanyeni kazi,sipendi kutengua lakini inabidi.Unakwenda kwenye Mkoa unakuta mambo hayaendi,tupo kwa ajili ya kuwatumikia hawa wananchi masikini. Kuna siku nitateungua kuanzia Mkuu wa Mkoa hadi Mtendaji wa kijiji tena kwa siku moja na kuteua wengine,"amesema Rais Magufuli na kusisitiza sio kwamba anawatisha lakini yeye anahimiza kufanya kazi kwa bidii.
Rais  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

VISIWA VYA ZANZIBAR VINAWEZA KUPATA MTIKISIKO MKUWA WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA-BALOZI SEIF ALI IDDI

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Visiwa vya Zanzibar vinaweza kupata mtikisiko mkubwa wa uchafuzi wa Mazingira iwapo Watu wataachiliwa kuendelea kuchimba Mchanga kiholela pamoja na matumizi yasiyo na Mpango ya Rasilmali nyengine za Mawe na Kokoto.

Alisema Serikali imelazimika kuandaa utaratibu maalum wa upatikanaji wa Rasilmali hizo muhimu katika harakati za Ujenzi wa Majengo na Miundombinu mbali mbali kufuatia athari kubwa iliyokwishajitokeza kwenye mashimo ya mchanga ambayo baadhi yake huchipuka maji ya chumvi.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo mapema asubuhi alipofanya ziara fupi ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Tangi kubwa la Kuhifadhia Maji safi na salama katika Mtaa wa Kitope Mbaleni baada ujenzi wake kusua sua kutokana na ukosefu wa nyenzo za kutekeleza Mradi huo ikiwemo Mchang, Kokoto na Mawe.

Alisema Nchi hivi sasa imeharibika kutokana na mashimo mengi yaliyochimbwa kwa ajili ya kupata Mchanga wa Ujenzi hali inayoashiria lazima zipatikane mbinu mbadala za kukabiliana na changamoto hiyo ya uchafuzi wa Kimazingira inayoweza kuleta maafa hapo baadae.

Balozi Seiif alifahamisha kwamba Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo, Wataalamu, Taasisi pamoja na Jumuiya za Kiraia zinafanya jitihada za makusudi katika kuona Ujenzi utakaobuniwa wa Majengo ya Taasisi za Umma na Binafsi yanazingatia mfumo wa kutumia Mchanga kidogo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru Taasisi ya Kiraia ya Tanzania Youth Icon {TYI} pamoja na Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} kupitia Wadau wao wa Maendleo kwa uwamuzi wao wa Kujenga Tangi hilo litakalofaidisha Wananchi waliomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Alisema Kitope ni eneo lenye usumbufu wa huduma za Maji safi na salama kwa muda mrefu tokea kuharibika kwa Tangi la zamani la kuhifadhia Maji na Wananchi wanaozunguuka eneo hilo wamekuwa wakipata changamoto ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu kwa ustawi wao.

Mapema Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Tangi hilo la kuhifadhia Maji safi na salama Kitope Mbaleni Bwana Jackson Maro alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Tangi hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji zaidi ya Lita 50,000.

Mhandisi Maro alisema kazi hiyo imeanza rasmi kwa hatua ya msingi karibu Wiki Tatu sasa, lakini imeshindwa kuendelea kama ilivyopangwa kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa wakati wa Rasilmali ya Mchanga, Kokoto pamoja na Mawe.

Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Kiraia ya Tanzania Youth Icon {TYI} Bwana Abdullah Miraji Othman alisema juhudi zimefanywa na Taasisi yake kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar{ ZAWA} za kuandika Barua katika Taasisi zinazosimamia Rasilmali zisizorejesheka lakini bado upatikanaji wa Rasilmali hizo umekuwa mdogo.

Bwana Miraji alitahadharisha kwamba Mradi wa Ujenzi huo umepangwa kukamilika ifikapo Tarehe 31 Disemba Mwaka huu vyenginevyo Wafadhili waliojitolea kuwezesha Mradi wa Ujenzi huo wataondoa Fedha zote walizozitenga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kitope Mbaleni mara baada ya kuutembelea Mradi wa Ujenzi wa Tangi la Maji safi na salama Kijiji hapo.Picha na – OMPR – ZNZ.

 Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi wa Tangi hilo la kuhifadhia Maji safi na salama Kitope Mbaleni Bwana Jackson Maro Kulia ya Balozi Seif akielezea hatua zinavyoendelea za Ujenzi wa Tangi la Kuhifadhia Maji safi katika Kijiji cha Kitope Mbaleni.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Kiraia ya Tanzania Youth Icon {TYI} Bwana Abdullah Miraji Othman akisema changamoto wanazopambana nazo kwenye Ujenzi wa Mradi huo wa Tangi la kuhifadhia Maji safi na Salama Kitope Mbaleni.

TUWAWEKEZEE WATOTO ELIMU BADALA YA KUWAPA UFAHARI ILI KUINUA TAALUMA ZAO-NDIKILO

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

WAZAZI, walezi mkoani Pwani, wametakiwa kumpa hazina ya elimu mtoto na kumwekezea elimu ikiwa ni urithi mkubwa wa maisha yake ,badala ya kumpatia vitu vya kifahari kama magari suala ambalo linachangia kurudisha nyuma maendeleo yake kitaaluma .

Aidha watoto wameaswa kuacha kujiingiza katika tabia hatarishi kama vile kutumia madawa ya kulevya ikiwemo bangi na badala yake wawe na hofu ya mungu kwa kufuata maadili mema.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitoa rai hiyo wakati wa mahafali ya 14 ,ya  darasa la saba ya shule ya msingi Kibaha Independent (KIPS )iliyopo Kibaha.

Aliwataka wazazi na walezi wenyewe kumtengeneza mtoto kwa kumuandaa  na kesho yake kwa kumfuatilia muenendo wa masomo yake .

"Muda wa kuwapa magari na simu kubwa za kiganjani utafika , ,Tuwawezeee elimu kwa manufaa yao baadae":-Wanangu safari yenu bado mbichi, elimu ni bahari ,pambaneni ,Tanzania inasubiri vijana wasomi ,msiwe na haraka na mambo ya dunia na ya ovyo ovyo kwani maisha hayataki haraka"alisisitiza Ndikilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wakurugenzi wa NJUWENI na bodi ya shule hiyo, alhaj Yusuph Mfinanga alisema, ili kuepukana na utapeli kwa malipo mbalimbali shuleni hapo wazazi wanapaswa kulipa ada na michango kupitia akaunti ya shule badala ya kukabidhi fedha mkononi .
 
Awali mkurugenzi wa shule hiyo ,Nuru Mfinanga alieleza, kwa sasa wanafanya upanuzi wa kwa kujenga shule eneo la Mwanalugali ili wanafunzi wanaojiunga shuleni hapo wasikose nafasi kutokana na ufinyu wa eneo la sasa na kuongoza mikondo.

Nuru alibainisha ,wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma kwani mwaka 2016 shule hiyo ilikuwa ya 16 kati ya shule 323, mwaka 2017 ilikuwa ya nne na mwaka 2018 ilikuwa ya nne hivyo mwaka huu wanatarajia kufanya vizuri zaidi .
 
Jumla ya wahitimu 82 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi kwa mwaka 2019 shule ya msingi KIPS.


IN MEMORY OF MWALIMU CLARA GASPAR MAREALLE

0
0

04 AUGUST 1930 – 22 SEPTEMBER 2009

Days, weeks, months and years came and gone. It is now 10 years since you left us, desolate and bereft. Mama your bountiful, unconditional and unwavering Love and support to your husband, children, grandchildren and family members gardened you unprecedented admiration from the Marealle and Lyimo Clans, then and always! You left a foot print in this earthly world of ours. We loved you Mama, and will forever Love You.
Rest in Eternal Bliss Mama.

PROF MBARAWA AMTAKA MKANDARASI KUFUATA MAKUBALIANO YA MKATABA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ameweka wazi msimamo wake wa kuunda tume maalumu itakayopitia upya mradi wa Chalinze Mboga baada ya kuukuta na mapungufu mengi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri huyo kutembelea mradi huo na kubaini mapungufu katika utekelezaji wake ikiwemo udanganyifu wa vipimo vya ulazaji mabomba.

Mradi wa Chalinze Mboga ulianza Aprili mwaka huu ukiwa chini ya mkandarasi kutoka kampuni ya Shanx aliyekabidhiwa mradi huo na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASA).

Akitoa maamuzi hayo, Mbarawa amesema kampuni ya Shanx wamwfanya udanganyifu wa vipimo vya ulazaji wa bomba pamoja na kutaka nyongeza ya gharama kulingana na kiwango cha mawe alichokuta kwenye eneo la mradi.

Mbarawa amesema, amefikia maamuzi ya kuunda tume maalaum ili kuweza kupitia upya mradi huo ikiwemo na kuwaita Dawasa na Shanx ofini kwake ili kupitia upya  maombi ya mkandarasi huyo.

"Ntawaita ofisini kwangu Dawasa pamoja na Mkandarasi ili kuweza kupitia maombi yao juu ya ongezeko la gharama za uchimbaji na ulazaji bomba, pia ntaunda tume maalumu itakayopitia upya mradi wa Chalinze Mboga," amesema Mbarawa.

Amesema, makubaliano ya awali ni kuchimba mtaro wa kulaza mabomba mita 1.8 ila wao wamechimba mita 1.6 kwenda chini tofauti na makubaliano yaliopo kwenye mkataba.

"Katika mkataba makubaliano ilikuwa kuchimba mita 1.8 kwenda chini na wanalipwa kulingana na kipimo cha uchimbaji ila kulingana na wanavyochimba ina maana malipo yao sio sahihi," amesema 

Mbarawa ameeleza kuwa Mradi huo unaenda vizuri lakini kuna mapungufu ikiwemo upande wa gharama za utandikaji bomba zina utofauti mkubwa sana ukilinganisha na mahala pengine.

Ameeleza kuwa mkandarasi wa mradi huo gharama zake za uchimbaji zipo juu ambapo anapima mita 1 kwa shilingi 49,000 wakati Arusha ni shilingi 32,000 kwa mita na wanachimba mita 2 kwenda chini. 

Mbarawa ameendelea na kusema kuwa, mkandarasi ameandika maombi ya ongezeko la gharama za uchimbaji na ulazaji bomba kulingana na kiwango cha mawe alichokuta kwenye eneo la mradi.

“Mkandarasi ameandika maombi ya ongezeko la gharama ya uchimbaji na ulazaji wa mabomba kutokana na kiwango cha mawe alichokikuta, jambo haliwezekani kwani atuwezi kuingiza pesa ya serikali kwa namna hii kilichobaki ni kuwatafuta wataalam ili waupitie upya," 

Mbarawa amesema, watalaamu hai watapitia “item by item” na kufahamu malipo anayelipwa Shanx ni sahihi na amedai kuwa kama wangemlipa malipo ya 32,000 kwa mita kazi ingefanyika.

Mbarawa amewataka Mamlaka ya Dawasa kusimamia vizuri mradi huo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na mradi.

Mradi wa Chalinze Mboga utahudumia wananchi wa Maeneo ya Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi. Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzireli ya kisasa (SGR).

Na Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na mkandarasi wa kampuni ya Shanx baada ya kutembelea mradi wa Chalinze Mboga na kukuta mapungufu mengi ikiwemo udanganyifu wa vipimo vya ulazaji mabomba na ongezeko la gharama za uchimbaji wa mtaro huo.

Mkandarasi akiwa anaendelea na kazi yake ya uchimbaji mtaro wa kulaza mabomba.

SI KILA KIJANA ANAFAA KUWA KIONGOZI KUNA MAENEO YANAPASWA KUONGOZWA NA WATU WAZIMA-LUSINDE

0
0
Imeelezwa kuwa ili vijana waweze kufanikiwa basi wanatakiwa kuwa na mambo matatu ambayo ni bidii na kujituma mbili kuaminika pamoja na kuheshimika.

Hayo yameelezwa Wilayani Mkuranga mkoa  Pwani  na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj'   ambaye pia ni  Mbunge wa Mtera  wakati wa uzinduzi wa mkuranga ya kijani uliandalia na uvccm wa   wilaya hiyo.

Lusinde amesema vijana wanapaswa kuhakikisha wanaaminika na kuheshimika kwa jamii na viongozi  kwa ujumla kwa sababu wao ndio tegemeo.

"Naomba niwaambie sio kila kijana anafaa kuwa kiongozi hapana kunamaeneo yanapaswa kuongozwa na watu wazima kwa sababu ya busara zao na vijana tuwe wa kwanza kuwaunga mkono" amesema
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalea watoto wao kwenye maadili ya dini na kuijua ili jamii iwe na kizazi chenye maadili.

"tunataka umoja wa vijana CCM  uwekimbilio la  watu panapo tokea matatizo na kusaidia jamii panapotokea matatizo, watu wasiporwe, wasiibiwe   mtoe taarifa polisi tunataka muwe mfano katika jamii."amesema
Hata hivyo ameongeza kuwa wanataka vijana wa CCM wawe wenye heshima kwa wazee wao,kuridhika na nafasi walizonazo sasa na waache tamaa.

kwa upande wake mbunge wa mkuranga Abdallah Ulega amewapongeza vijana hao kwa uzinduzi  wa huo na ametoa jezi pamoja na mipira kwa kata saba za wilaya hiyo ambazo ni Kisegese,Bupu,Mbezi,Panzuo,Beta, Njianne na Kitomondo.

Ulega amesema jenzi na mipira hiyo aliyotoa kwa ajili ya vijana wa Ccm wilaya ya mkuranga sio kwa kata hizo saba tu bali kwa kata zote 25 za wilaya hiyo.

Hata hivyo amewatoa hafu vijana kuhusiana na Ulega cup na kuwambia kuwa mwaka huu ipo na karibuni itaanza hivyo wao wajiandae.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao  amempongeza Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga  muondombuni mbalimbali na kuiongoza nchi ambayo inajulikana nchini na Duniani kote.

"sisi vijana wa mkoa wa Pwani tunamkubali na kumuunga mkono Rais kwa mambo makubwa anayoyafanya tangu taifa lilipopata uhuru wake Mwaka 1961 "alisema Mlao
 Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj'   akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga,Ally Mohammed Mbwera baada ya kuwasili leo wilaya ya Mkuranga.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)     
Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' akihutubia  katika uzinduzi wa  tamasha la Mkuranga  ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM) wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akisalimiana na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao baada ya kuwasili katika  tamasha la Mkuranga  ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)   
Kijana wa Chipukizi wa wilaya ya Mkuranga akimvika Skafu Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' mara baada ya kuwasili Ofisi ya CCM kuzindua Tamasha la Mkuranga  ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM) wilaya ya Mkuranga.
 Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao akizungumza katika uzinduzi wa  tamasha la Mkuranga  ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)
 Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj'  akisalimiana na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega   (katikati) akizungumza katika tamasha la Mkuranga  ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,(Mb)wa Mkuranga,Abdallah Ulega (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega. wakiserebuka



 Wana CCM wakiserebuka 


 Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega (kuali)




 Wana CCM wakiserebuka 






Wana CCM  wa Wialaya ya Mkuranga  wakiserebuka.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)     

CHANJO YA SURUA RUBELLA YATARAJIA KUFIKIA WATOTO 165.875 MKOANI PWANI- DKT.GUNINI

0
0




NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

KAMPENI ya chanjo ya magonjwa ya Surua Rubella kwa watoto wenye umri kati ya miezi tisa na chini ya miaka mitano , inatarajia kufikia watoto wapatao 165.875 Mkoani Pwani.

Pamoja na hilo, kampeni hiyo itahusisha utoaji wa chanjo ya polio ya sindano kwa watoto wapatao 93,546 wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba alieleza hayo ,wakati wa kikoa cha kamati ya afya ya msingi kwa ajili ya kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella na Polio ya Sindano itakayoanza septemba 26 hadi septemba 30 huku uzinduzi ukitarajiwa kufanyika Chalinze.

“Lengo kuu la kitaifa ni kufikia zaidi ya asilimia 99 ya watoto waliolengwa kupata chanjo hizo ambapo mkoa umetenga timu 156 za uchanjaji ili kufikia vituo 553 na maeneo 245 ambayo ni magumu kufikika kutokana na sababu mbalimbali”alifafanua Gunini.

Aidha alielezea, kampeni hiyo inafadhiliwa na wadau wa shirika la GAVI ambao wametoa chanjo na fedha za utekelezaji kiasi cha shilingi milioni 251.9 kupitia shirika la afya duniani (WHO) pamoja na shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF .

Gunini alisema, hadi sasa mkoa umepokea na kusambaza chanjo katika halmashauri zote na usambazaji ngazi ya vituo unaendelea.

“Vile vile mkoa umepokea na kufunga majokofu yanayotumia nguvu ya umeme wa jua 33 katika halmashauri za Bagamoyo na Chalinze ikiwa ni awamu ya kwanza na awamu ya pili majokofu 115 kwa halmashauri zilizobaki mwishoni mwa mwaka huu”:

Akizindua kampeni hiyo, mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema kiwango cha Surua Rubella kimeendelea kuwa juu ,kwa mkoa ni zaidi ya asilimia 100 idadi ya watoto wasiokamilisha chanjo na wasiochanjwa hali ambayo inaweza ikasababisha mlipuko wa ugonjwa wa surua.


“:Surua ni ugonjwa hatari na huathiri watu wa rika zote na dalili zake ni homa na vipele vidogo vidogo na ni chanzo kikuu cha maradhi,ulemavu, utapiamlo na vifo vya watoto wenye umri wa miaka mitano”

Ugonjwa wa Rubella dalili zake ni kama za Surua na madhara kwa mama mjamzito husababisha mimba kuharibika, au kuzaa mtoto mfu au njiti, ulemavu wa kimaumbile, yakiwemo matundu katika moyo, mtoto wa jicho, mtindio wa ubongo na makuzi hafifu.

TIGO TANZANIA YACHANGAMKIA fursa za Mkutano wa Mawaziri wa SADC

0
0
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tigo, Simon Karikari, akiwasilisha mada kuhusu Upatakanaji wa huduma za Mawasiliano vijijini, wakati wa Mkutano  wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC DSM, jana. Tigo ni kampuni pekee yenye internet ya kasi ya 4G+ na ndio mtoa huduma rasmi ya Wi-Fi katika wa mkutano huo.


Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Makamishna wa Tume hiyo

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mussa Lulandala kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali walioapishwa wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Loata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mtwara katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ally Possi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Mary Maganga kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Utawala katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Viongozi wengine wa Serikali Kuu katika picha ya pamoja na viongozi waliopishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Morogoro Dkt Stephen Kebwe mara baada ya hafla fupi ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AFUNGUA MAONESHO YA MADINI GEITA

0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa mjini Geita katika uzinduzi huo (hawapo pichani)
Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa hotuba kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 22 Septemba, 2019.

Mtaalam kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory (kushoto) akielezea majukumu ya TEITI kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri (kulia) kwenye Banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 22 Septemba, 2019
Mhandisi Migodi wa Wizara ya Madini, Johnbosco Karungamye (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 22 Septemba, 2019
Kutoka kushoto Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 22 Septemba, 2019.
Kutoka kushoto Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yaliyofanyika mjini Geita tarehe 22 Septemba, 2019.
Wakazi wa mjini Geita wakisikiliza hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa maonesho hayo
…………………..

Asteria Muhozya na Greyson Mwase, Geita

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo Septemba 22, 2019 amefungua Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyoanza tarehe 20 Septemba, 2019 na kutarajiwa kumalizika tarehe 29 Septemba, 2019.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi kwa Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa kuboresha shughuli za madini kupitia kuongeza ajira na vitendea kazi kama vile magari kama njia mojawapo ya kuboresha ukusanyaji wa maduhuli.

Akielezea mafanikio ya Soko la Madini Geita tangu kuanzishwa kwake Majaliwa amesema kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa dhahabu kutoka takribani kilo 100 hadi kilo 200 na zaidi kwa mwezi na kusisitiza kuwa, tangu kuanzishwa kwa soko la madini la Geita kiasi cha kilo 1,573 zimezalishwa na kuuzwa.

Katika hatua nyingine, ameitaka Tume ya Madini kuongeza kasi kwenye ukusanyaji wa maduhuli ili Sekta ya Madini iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi .

Aidha, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuyatumia vyema masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha yanalindwa.

Pia, amewataka wachimbaji wa madini kutumia tafiti zinazofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kubaini maeneo yanye madini na kuanza kuchimba ili kuepuka uchimbaji wa kubahatisha.

Amesema serikali itaendelea kuboresha Sheria na Kanuni ili kuleta tija zaidi na hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini ikiwemo kutoa taarifa kwenye vyombo vya udhibiti.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuachana na matumizi ya zebaki na badala yake watumie njia nyingine mbadala kulingana na miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya Madini pamoja na Tume ya Madini.



Akizungumzia nafasi ya sekta ya madini katika kuchochea ukuaji wa viwanda, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kwamba hadi sasa wizara kupitia Tume ya Madini imekwishatoa leseni mbili za usafishaji wa madini (Refinery Licence) moja ikiwa mkoani Dodoma na nyingine mkoani Geita

Ameongeza kuwa, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imetoa leseni nne za uyeyushaji wa madini ya Shaba na Bati ( Smelting Licence )

Kuhusu changamoto ya usafirishaji nje madini ya bati amesema Wizara kwa kushirikiana na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) zipo katika hatua ya mwisho kuwezesha upatikanaji wa Hati ya kusafirisha madini ya bati nje ya nchi na kuongeza kwamba, hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu, hati hiyo itakuwa tayari.

Akizungumzia uanzishwaji wa masoko ya madini, Waziri Biteko amesema masoko hayo yameleta matokeo chanya huku nidhamu ya watanzania kusimamia masoko na rasilimali ikiwa imeongezeka hali ambayo imepelekea baadhi ya nchi zikiwemo za Kongo, Zambia na Msumbiji kutaka kuyatumia masoko ya madini yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali nchini.

‘’ Wanaotaka kuhujumu masoko waache. Ukifanya hivyo utaambulia vitu viwili tu, kufilisiwa na kufungwa jela,’’ amesisitiza Waziri Biteko.

Pia, Waziri Biteko amebainisha kuwa, wadau wa madini nchini hawakatazwi kuingiza madini nchini kutoka nchi mbalimbali zikiwemo sampuli isipokuwa tu madini yote yanayopelekwa nje ya nchi ni lazima yazingatie sheria na taratibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko ameupongeza Mkoa wa Geita kwa kuwa kinara kwenye usimamizi wa fedha zinazotokana na mpango wa utoaji wa huduma kwa wananchi wanaozunguka kampuni za madini (CSR) na kuzitaka kuendelea kufuata sheria na taratibu zinazowekwa na serikali kwenye usimamizi wa sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa soko la madini mkoani humo, madini ya dhahabu yameanza kupatikana kwa wingi na kueleza kwamba kwa mwezi Agosti mwaka huu jumla ya kilo 504 zimeuzwa sokoni hapo, na kabla ya kuisha kwa mwezi Septemba tayari kilo 340 zimeuzwa sokoni.

Akizungumzia lengo la maonesho hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Chacha Wambura amesema kuwa ni pamoja na kukuza teknolojia ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Geita.

Katika hatua nyingine ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa maonesho hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mwongozo wa uwekezaji katika mkoa huo.

Maonesho hayo yemehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Mikoa jirani na Geita, Viongozi wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini, Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Taasisi za Kifedha, wadau mbalimbali wa madini na wananchi.

Kaulimbiu ya maonesho hayo ‘’Madini ni Chachu ya Ukuaji wa uchumi wa Viwanda. Tuwekeze kwenye Teknolojia bora ya Uzalishaji na Tuyatumie Masoko ya Madini’’

RAIS DK.SHEIN ZIARANI UMOJA WA FALME ZA KIARABU UAE

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Mwenyeji wake mmoja kati ya Viongozi wa juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (U.A.E) katika ukumbi wa watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Dubai,mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Ziara ya siku saba U.A.E.

CHINA KUMTUNUKU NISHANI YA JUU YA URAFIKI DKT. SALIM AHMED SALIM

0
0
Oktoba 1, 2019 kutakuwa na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuzaliwa taifa la Jamhuri ya Watu wa China. Maadhimisho hayo yamepewa uzito mkubwa na yatajumuisha matukio mbalimbali ikiwemo Gwaride kubwa ambalo halijawaji kutokea  nchini China. Vilevile wataonesha hatua kubwa waliyopiga ndani ya kipindi cha miaka 70 katika sayansi na teknolojia pamoja na nguvu za kijeshi. 

Katika ku revisit safari yao ya miaka 70 wameutambua mchango wa Tanzania katika maeneo mawili. Moja- mchango wa kuwawezesha kupatiwa kiti katika Umoja wa Mataifa na pili fursa waliyopata kutekeleza mradi wa kwanza wa ujenzi wa Reli nje ya nchi (TAZARA).

Katika kutambua mchango wa Tanzania kuwawezesha kuingia UN- Rais wa China Mhe Xi Jinping atamtunuku Mhe Dr. Salim Ahmed Salim Nishani ya Juu ya Urafiki ya taifa la China. Dr Salim atakuwa Mwafrika wa kwanza kupatiwa nishani hiyo na mtu wa tatu kutoka nje ya China kupatiwa nishani hiyo. 

Wengine waliokwishapatiwa nishani hiyo ni Rais wa Urusi Mhe Vladmir Putin- kutokana na mchango wa mkubwa wa Urusi kwa taifa la China katika miaka 1949-1970… waliwapa mikopo nafuu, mitaji, teknolojia na ufundi iliyowawezesha kupiga hatua. Pia nishani hiyo amewahi kupewa Kiongozi wa Khazakstan Mhe DescriptionNursultan Äbishuly Nazarbayev kutokana na ujirani mwema na ushirikiano mkubwa katika nyanja za ulinzi na uchumi. 

Khazakstan inapakana na China (mpaka wao una urefu wa kilomita 1,782.75). Mizigo ya China inayosafirishwa kwenda Ulaya kwa treni, lazima ipitie Khazakstan-,nchi hiyo ni strategic country kwa China.

Kwa upande wa mchango wa Reli ya TAZARA wachina wanaichukulia kuwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika. Hivyo katika kutambua urafiki huo- viongozi wa taasisi za China-Tanzania Friendship Association na Tanzania Zambia Friendship Association wamealikwa kuhudhuria sherehe za miaka 70 na pia watashiriki katika gwaride rasmi la Nchi Rafiki wa kweli wa China katika kipindi cha miaka 70. Kutoka Afrika ni nchi mbili tu- Tanzania na Zambia.
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images