Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Maadhimisho ya Tamasha la JAMAFEST 2019 Jijini Dodoma

$
0
0


Watumishi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika maadhimisho ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa (JAMAFEST) leo Septemba 21 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Vikundi vya ngoma vya Jijini Dodoma vikitumbuiza katika maadhimsho ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa (JAMAFEST) leo Septemba 21 Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi Hadija Kisubi akizungumza katika maadhimsho ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa (JAMAFEST) leo Septemba 21 Jijini Dodoma.

WAZIRI LUGOLA KUTATUA KERO ZA WAMILIKI, WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO KUPITIA BONANZA KUBWA LA VIJANA MKOANI DODOMA KESHO

$
0
0




Na Mwandishi Wetu, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bonanza kubwa la Vijana litakalofanyika Chang’ombe jijini Dodoma, kesho.

Bonanza hilo, pia litashirikisha wananchi mbalimbali wakiwemo wamiliki na waendesha vyombo vya moto kutoka Wilaya zote za Mkoa huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, jijini Dodoma leo, Waziri Lugola alisema amealikwa na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa mgeni rasmi ambao ndio waratibu wa Bonanza hilo.

Lugola alisema amepewa taarifa na uongozi wa UVCCM Mkoa, kuwa wamejipanga vizuri na pia Bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali na burudani kutoka kwa wasanii wa miondoko ya kizazi kipya.

“Kupitia mkutano huo wa Dodoma, nitalenga kuwahabarisha vijana wote na wananchi kwa ujumla hapa nchini, kuhusu mafanikio ya Serikali katika kuwasaidia vijana kupambana na umaskini, na kutatua tatizo la ajira pasipo kunyanyaswa kwa kujua au kwakutokujua kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi la polisi, pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali,” alisema Lugola.

Alisema vijana ni nguzo ya taifa, hivyo Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na inawathamini katika mazingira yao ya kujipatia kipato ikilenga kuwapa nafasi mbalimbali ili waweze kupata mafanikio zaidi.

“Mwezi uliopita nilikutana na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj zaidi ya 2000 mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, nilitoa mwarobaini wa kero zao, ambazo nyingi zaidi zilihusu Manispaa ya Moshi kutowatendea vema katika maeneo mbalimbali ya maegesho ya vyombo vyao vya moto, pamoja na kero nyingine zilizowahusu baadhi ya askari wangu wa kikosi cha usalama barabarani ambapo vijana hao waliwalalamikia,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Billy Chidagwa alisema Bonanza hilo litaacha historia katika mkoa huo kutokana na maandalizi yao waliyoyafanya katika kufanikisha vijana mkoani humo wanakutana pamoja na kero zao kutatuliwa.

Chidagwa alisema vijana mbalimbali watakuwepo katika tukio hilo, hasa wanaotumia vyombo vya moto mbalimbali vikiwemo Bajaj, Bodaboda na waendesha daladala kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.

“Tumejipanga vizuri kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Vijana, Mbunge wetu wa Jimbo, viongozi wa chama, tunaamnini uwepo wao kutakuwa na tija kufanikisha tukio hili ambalo maandalizi yake ni ya muda mrefu, na tayari yamekamilika,” alisema Chidagwa.

Alisema Bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali, ambapo kwa upande wa mpira wa miguu, timu ya bodaboda itacheza na timu ya Askari Polisi mkoani Dodoma.

“Vijana njooni kwa wingi kesho jumapili tarehe 22 mwezi huu wa tisa pale Chang’ombe ili tufurahi kwa pamoja na kumsikiliza mgeni wetu rasmi, ambaye ni Waziri Lugola atakapotatua kero zetu na kutuonyeshea njia ya mafanikio zaidi katika Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli,” alisema Chidagwa.

Waziri Lugola ambaye alikuwa mkoani Arusha kikazi, amewasili leo jijini Dodoma kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya vijana.

KATIBU MKUU MWALUKO AUNGANA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU KUMPONGEZA MKURUGEZI KWA KUSTAAFU

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi zawadi aliyekuwa Mkurugenzi, Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Cleophas Ruhumbika, ambayo ni Picha yake aliyochorwa mstaafu huyo , wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019.





Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Aristides Mbwasi, akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu)Bi. Dorothy Mwaluko, akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019.
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilila tukio la kumuuga rasmi aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma rasmi, leo, tarehe 21, Septemba, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dorothy Mwaluko akieleza jinsi aliyekuwa Mkurugenzi, Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Cleophas Ruhumbika, (kushoto kwake) anapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuchapa kazi kwa ufanisi na weledi, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019.

WAIOMBA WIZARA KUTILIA MKAZO UKATILI WA KIJINSIA KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike (kulia) akieleza namna Wizara itavyoshirikiana na kundi la watu wenye ulemavu katika kuandaa Sera, miongozi na Mikakati mbalimbali ya Wizara katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Philbert Kawemama (wa pili kulia) akieleza lengo la utaratibu wa kuzungumza na Wizara na Taasisi kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza (Kushoto) akielezea namna Wizara inavyoshugulikia masuala ya ukatili dhidi ya watoto wakiwemo wenye ulemavu katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu (SHIVYAWATA) Taifa Bi. Ummy Hamisi Nderiananga (wa tatu kulia) akitoa ombi kwa Wizara kuongeza nguvu katika kupambana na vitendo ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi (kushoto) akieleza jinsi Wizara inavyosaidia kundi la watu wenye ulemavu katika mapambano dhidi ya vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa kundi hilo katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Mwakilishi wa Shirika la ADD International Bw. Isack Idama (wa pili kushoto) akieleza jinsi Shirika lao linavyoshirikiana na kundi la watu wenye elemavu katika kuhakikisha wanapata haki zao katika kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW



Na Mwandishi Wetu Dodoma

Shirikisho la Vyama vya Walemavu (SHIVYAWATA) limeiomba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jmaii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma juu ya kupambana na manyanyaso na vitendo ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu nchini.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa Bi. Ummy Hamisi Nderiananga wakati wa kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.

Bi. Ummy ameongeza kuwa kama Wizara ilivyoweka nguvu kwenye masuala ya jinsia hasa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto basi pia waongeze nguvu katika kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika jamii.

“Vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu wawe watoto au wanawake hata wanaume pia vinatendeka katika familia zatu ila havipigiwi kelele za kutosha” alisema Bi. Ummy.

Bi. Ummy amesisitiza Wizara kupitia Mpango Mkakati wa Taifa wa kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ili uweze kuwezesha kuingiza masuala ya watu wenye ulemavu ili kuondokana na vitendo vya kikatili vinavyowapata watu wenye ulemavu nchini.

Akifafanua kuhusu Wizara kutilia Mkazo suala la Ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza amesema kuwa Wizara inalenga kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya makundi yote ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu nchini.

Bi. Mwajuma ameongeza kuwa Wizara imejikita katika Kampeni mbalimbali za kupambana na vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto likiwemo kundi la watu wenye elemavu kwa kutoa elimu kwa jamii ya kupambana na vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kuwa kikao hicho kimeisaidia Wizara kupata namna bora ya kuyafikia makundi ya watu wenye ulemavu kabla ya kuandaa miongozi na Mikakati mbalimbali ya Wizara ili katika utekelezaji wake isiache kundi la watu wenye ulemavu na makundi mengine maalum.

Bw. Golwike ameongeza kuwa Wizara itashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha watu wenye ulemavu katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu katika kapata fursa sawa kama makundi mengine katika jamii hasa katika utoaji wa mikopo na elimu ya ujasirimali.

Naye Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Philbert Kawemama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia utekelezaji wa Sheria namba 9 ya mwaka 2010 na Kanuni zake ili kuhakikisha kila Wizara na Taasisi zake zinazingatia masuala ya watu wenye ulemavu katika kuhakikisha wanapata mazingira stahiki katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameongeza kuwa pia Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia uwezeshwaji wa kundi la watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanapata fursa sawa za kimaendeleo na kusaidia kundi hilo kuondokana na vitendo vya unyanyapaa na vitendo vya kikatili dhidi yao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la ADD International Bw. Isack Idama amesema kuwa Wizara ina dhamana kubwa kwa maendeleo ya watoto na wao kama wadau wa masuala ya watu wenye ulemavu hasa watoto wangependa kuona kwa jinsi gani masuala ya watoto wenye ulemavu yanashughulikiwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania wanatembela Wizara na Taasisi za Serikali katika kufuatilia na kuona kwa jinsi gani masuala ya watu wenye ulemavu yatekelezwa.

RC MAKONDA KUWAWEKA KIKAANGONI WATENDAJI WALIOSABABISHA MIRADI YA KIMKAKATI KUTOTEKELEZWA KWA WAKATI.

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe. Paul Makonda ameitisha kikao baina yake na watendaji wa Mkoa huo wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Mamea, Wakurugenzi wa Manispaa, Makatibu tawala na wakuu wa Idara ili wamueleze ni kitu gani kinachowafanya miradi ya kimkakati ikiwemo Machinjio ya Vingunguti na Ufukwe wa Coco imechelewa kutekelezwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha za miradi hiyo lakini fedha hizo zimeishia kukaa kwenye Akaunti pasipo utekelezaji.

RC Makonda amesema katika mkutano huo utakaofanyika Jumatano ya September 25 Ukumbi wa Karimjee mtendaji atakaebainika kusababisha uzembe huo atawajibisha  hapohapo kwa mujibu wa sheria na wengine watazuiwa mishahara yao.

Aidha RC Makonda ametoa wito kwa Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutafuta njia bora ya kuwapata wakuu wa Idara wenye uwezo wa kuleta matokeo Chanya tofauti na sasa ambapo wengi wao wamepanda na kuwa wakuu wa idara kwa kigezo cha kukaa kazini Muda mrefu.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika taaluma na Michezo.

Serikali yaipongeza Haki Elimu kwa kuinua kiwango cha elimu nchini

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Haki elimu, inayojishughulisha na kutoa elimu ya usawa kwa watoto wote katika elimu, limezindua utafiti uliofanyika na kituo hicho katika mikoa mitano(5) kujua changamoto zinazowakwamisha watoto wa kike katika kupata elimu katika Jamii zetu.

Akizindua utafiti huo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt Leonard Akwilapo, amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na asasi za kiraia Kama Haki elimu, katika kuinua elimu hapa nchini na serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule.

"Sisi Kama serikali tunatambua kazi kubwa mnayoifanya asasi za kiraia, hasa ninyi haki elimu, mnasaidia kueneza elimu kwa Jamii na kuhakikisha watoto wanabaki shule, na sisi serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha watoto hasa wa kike wanabaki shule" amesema, Dkt Akwilapo.

Serikali imekuja na mpango wa elimu bure kwa shule za awali hadi kidato cha nne yote haya ni kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu, sambamba na hilo tumejenga na tunaendelea kujenga mabweni ya watoto wa kike hasa katika shule za kata.

Amesema wameweka adhabu kubwa kwa mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kumbebesha ujauzito au kuoa mtoto lakini licha ya hiyo bado wataendelea kutoa elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike na faida zake

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Haki elimu, John Karage, amesema kupitia elimu wanayoitoa kumekuwa na mafanikio makubwa kwani mpaka sasa idadi ya udahili kwa watoto wa kike umeongezeka hadi kufikia asilimia 90, na Sasa kunakuwa na uwiano Kati ya watoto wa kiume na watoto wa kike katika udahili.

Amesema utafiti huo unalenga kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kuondokana na changamoto zinazowakumba, katika kupata elimu kwa mtoto wa kike.

Nae Dkt Mugisha Lucius, ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu Cha Dar es saalam, wakati akiwasilisha utafiti huo amesema utafiti huo umefanyika katika mikoa ya Dar es saalam, Kilimanjaro, Tabora, Dodoma na Lindi, huku akibainisha moja ya vikwazo kwa mtoto wa kike kwenda shule ni tamaduni za maeneo husika.

Akatolea mfano" Mkoa wa Lindi ni kwamba mtoto wa kike akifikisha umri flani anaondolewa nyumbani kwa wazazi na kupeleka nyumba ya karibu, ambapo kule anakosa malezi ya karibu ya wazazi hivyo kushindwa kupata elimu kikamilifu" amesema Dkt Mugisha.

Pia kukosekana kwa mahitaji maalumu kwa watoto wa kike imetajwa kukosesha watoto wa kike mda wa kusoma na hatimaye kuingia katika mahusiano Jambo ambalo hufifisha ndoto zao kabisa, pia mtoto anapo kuwa kwenye mzunguko wa siku zake watoto wengi hukosa masoma kutokana na kutokuwa na visitili vinavyotakiwa kwa mtoto wa kike.

Aidha Mkoa wa Tabora imetajwa kuwa kipindi cha kilimo cha tumbaku ndipo watoto wengi hushindwa kwenda darasani na badala yake wanajiingiza katika kilimo na kukosa mda wa masomo kwa watoto.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo.
 Baadhi ya wanafunzi na wajumbe waliohudhuria hafla ya kuzindua ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo iliyofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, Dk John Kalaghe akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Dk Leonard Akwilapo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe baada ya kuzindua ripoti ya utafiti kuhusu wasichana kushindwa kuendelea na masomo. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma

Jeshi la Polisi Dodoma lakamata watuhumiwa 72 wa uhalifu

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha wanazuia uhalifu na kulinda usalama wa raia, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendesha msako na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 72 wa makosa mbalimbali.

Watuhumiwa waliokamatwa ni wahalifu wasiofuata sheria katika biashara ya mafuta ya Petroli na Diesel ambao wamekua wakisafirisha katika njia hatarishi kwenye magari ya abiria huku wengine wakikamatwa na nyara za Serikali pamoja na Dawa za kulevya.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Giles Muroto amesema wao kama chombo kinachohusika na ulinzi wa raia na mali zake pamoja na usalama hawatokubali kuruhusu uhalifu wowote ndani ya Dodoma.

Kamanda Muroto amesema kitendo cha Madereva kusafirisha mafuta kwenye gari za abiria kinaweza kusababisha maafa makubwa endapo yatalipuka.

" Sheria inakataza kabisa kusafirisha mafuta kwa kutumia vyombo vya usafiri wa abiria, hawa wanaweka madumu ya Petroli kwenye buti halafu hizi gari zinafanya safari ndefu msuguano ukitokea tu moto unalipuka.

" Tumekamata magari takribani sita ya abiria yanayosafirisha mafuta haya yote kwa ujumla wao yanabeba abiria siyo chini ya 200, hatuwezi kukubali maafa yawapate Wananchi wetu kwa tamaa za hao madereva, hivyo tumewakamata na tutawachukulia hatua," Amesema Kamanda Muroto.

Amesema Jeshi hilo pia limekamata mtuhumiwa Jonathan Temu (41) mkazi wa Dodoma akiwa na nyama ya wanyamapori aina ya Nsya wanne, Digidigi mmoja aliyoipata kutokana na uwindaji haramu

Kamanda Muroto amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kuipata silaha aliyokua anaitumia kwenye uwindaji huo sambamba na washiriki wengine na mara uchunguzi utakapokamilika atapandishwa mahakamani.

Msako huo pia uliwakamata wanawake watatu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao, pamoja na watuhumiwa wengine waliokutwa na Dawa za Kulevya aina ya Bangi, Mirungi na mitambo ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo.

Kamanda Muroto ametoa onyo kwa wote wanaovunja Katiba ya Nchi kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria na taratibu huku akiapa kuwashughulikia wahalifu wote ndani ya Mkoa wa Dodoma.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akionesha gari lililobeba madumu ya mafuta aina ya Petroli na Diesel kinyume na Sheria jambo ambalo linahatarisha usalama wa abiria
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akionesha pikipiki walizozikamata ambazo zimekua zikihusika na uhalifu sehemu mbalimbali za Mkoa wa Dodoma

WANAFUNZI ZAIDI YA 700 KUTUMIA MABWENI YALIYOKARABATIWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NOVEMBA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema mabweni mawili ya wanafunzi maarufu “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam yaliyokarabatiwa  yatachukua wanafunzi  788 . Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi katika Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.

Mabweni hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 4.5, ukarabati ukihusisha  kuweka upya mifumo ya maji safi na taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya, madirisha  uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.

Ukarabati huu unatarajiwa kukamilika, ifikapo mwezi Oktoba, 2019.  unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na  kurugenzi ya milki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ulianza 2018. Mabweni haya yalijengwa mwaka 1965 na kwa mara ya kwanza yanafanyiwa ukarabati mkubwa baada ya kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.

Waziri Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia kazi za ukarabati katika chuo hicho.

“Nimefurahishwa na kazi hii ni bora na  kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani  yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya 11,100. Naagiza uongozi mko hapa  maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya kufunguliwa Chuo Novemba  ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”

Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa  Chuo Cha Dar es salaam Profesa  Wiliam Anangisye ameishukuru Serikali ya awamu ya tano na Waziri wa Elimu kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha ili ili kuhahakikisha vijana wanapata elimu katika mazingira bora. Amemuhakikishia  Waziri Ndalichako kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika kwa wakati .

“ tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia mapato ya ndani kuyaendeleza”

Nae Dkt. Liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu shilingi bilioni  1.5  .

“ napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi unahusisha  majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi na bweni moja lililopo kitalu G.  nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba  mwaka huu“

Nae Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele, ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea  hall 5 na hall 2 na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya  wanafunzi wanaokaa chuo, kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET), Prof. Aloyce Mayo, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa mabweni mawili ya wanafunzi pamoja na mfumo wa kusambaza majisafi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua mabweni yanayokarabatiwa  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu,Sayansi  na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ukaguzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Picha mbalimbali za ukaguzi wa majengo yanayokarabatiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

KAMISHNA JENERALI PHAUSTINE KASIKE ARIDHISHWA NA KASI, UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU, GEREZA KUU ISANGA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akiangalia mbao zinazotumika katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, alipotembelea eneo hilo la ujenzi, leo Septemba 21, 2019. (Picha zote na Jeshi la Magereza).
Muonekano wa nyumba takribani 20 ambazo tayari zimejengwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga zikiwa katika hatua mbalimbali ya ujenzi.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mkoani Dodoma alipowasili kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, leo Septemba 21, 2019.


Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma;

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amekagua ujenzi unaoendelea wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga ambao unatumia nguvu kazi ya wafungwa wa gereza hilo, jijini Dodoma na ameridhika na kasi ya ujenzi huo.

Akiwa eneo hilo la ujenzi leo(Jumamosi), Kamishna Jenerali Phaustine Kasike ameelezea kufurahishwa, kuridhika na kasi ya hatua mbalimbali za ujenzi ulipofikia na ameupongeza Uongozi wa Magereza mkoani Dodoma kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

“Mmeonesha namna gani mmejipanga vizuri katika kutekeleza Mkakati wa Jeshi katika kutatua uhaba wa makazi ya Maafisa na Askari, hivyo niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya, chapeni kazi,” alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije amemshukru Kamishna Jenerali kwa kutembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ikiwemo kuwatia moyo Maofisa, askari na Wafungwa wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi huo.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije, amemhakikisha Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza kuwa wataendelea kutekeleza mkakati huo wa ujenzi wa nyumba za tofali za kuchoma ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama aliyoyatoa kwa Jeshi hilo kuhusu ujenzi wa makazi ya Maafisa na askari kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Ujenzi wa nyumba hizo za tofali za kuchoma ulianza rasmi Aprili, 2019 ambapo hadi sasa jumla ya nyumba 20 zimejengwa na zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, moja kati ya nyumba hizo tayari imekwishapauliwa, nyumba tano(05) zimekwisha fungwa lenta na nyingine 14 zinasubilia kufungwa lenta hivi karibuni.

MAJALIWA AANZA ZIARA MKOANI GEITA , AKAGUA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA CHATO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kinu cha kuchambua pamba wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato , Septemba 21, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato, Charles Nyasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika la Chato, Charles Nyasi (kulia) wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua Pamba cha Chama hicho, Septemba 21, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na wa pili kushoto ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wanachama, na Viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato pamoja na mwananchi kwenye kiwanda cha kuchambua Pamba cha chama hicho kilichopo Chato mkoani Geita, Septemba 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chato kuanza ziara ya kikazi mkoani Geita, Septemba 21, 2019.Kulia ni Mkuu wa moa wa Geita, Mhadisi Robert Gabriel na kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani. (Picha naOfisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Pamba wakati alipotembelea maghala ya Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato mkoani Geita, Septemba 21, 2019. Kushoto ni Meneja wa Chama hicho, Charles Nyasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chato kuanza ziara ya kikazi mkoani Geita, Septemba 21, 2019. Kushoto na Waziri wa Madini, Doto Biteko na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita, Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAENDELEO YA MAFUNZO KWA VIJANA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KITALU NYUMBA WILAYA YA CHAMWINO

$
0
0
Mwanagenzi mmoja wapo aliyenufaika na Mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) Bw. Fahdi Lyimo akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu bidhaa ya “Chill Source” iliyotengenezwa na Kikundi cha Vijana kiitwacho The One. Bidhaa hiyo imetumia kutengenezewa na Nyanya zilizovunwa na vijana hao katika Kitalu Nyumba kilichojengwa Halmashauri ya Chamwino. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Bw. Festo Masima ambaye ni mmoja wa vijana aliyenufaika na Mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) kuhusu ujuzi waliopata juu ya kujenga Vitalu nyumba hivyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Chamwino mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo kwa lengo la kutembelea maeneo yaliyojengwa Vitalu Nyumba “Greenhouse” na kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Wilaya ya Chamwino Septemba 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Vumilia Nyamonga akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyojengwa Vitalu Nyumba “Greenhouse” na kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.
Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Holly Green, Bw. Octavian Laswai (kushoto) akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Holly Green, Bw. Octavian Laswai (kushoto) alipokuwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House iliyojegwa katika Halmashauri ya Chamwino, Septemba 21, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

SIMBACHAWENE: MABADILIKO YA TABIANCHI HUATHIRI SHUGHULI ZA KIUCHUMI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani.
Sehemu ya washiriki wa Maadhimosho ya Siku ya Amani Duniani wakifuatiliamatukio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwa na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi Rebeca Muna, Mkurugenzi wa MashtakaBiswalo Mganga, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania AmonManyama na Clara Makanya kutoka Shirika la Mazingira.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachaweneakivishwa skafu na skauti alipowasili katika tukio hilo.
Picha ya pamoja ikiwahusisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (walioka katikati)mara baada ya kuhutubia Maadhimisho hayo.

**********************


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. GeorgeSimbachawene amesema mabadiliko ya tabianchi nchi huathiri moja kwa mojashughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii hivyo huatarisha amani.

Akizungumza kwenye kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani
yaliyofanyika Jijini Dodoma Septemba 21 Mhe. Simbachawene ambaye alikuwamgeni rasmi alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa nashughuli za kibinadamu.

Alisema kuwa shughuli hizo husababisha kuongezeka kwa halijoto, kupunguakwa kiwango cha mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji na kuongezeka kwamagonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.

"Kwa kiasi kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na shughuli zakibinadamu zikiwemo uchafuzi wa hali ya hewa, uchomaji misitu, ukataji miti bilakuotesha na shughuli za kilimo na ufugaji zisizozingatia uhifadhi wa mazingiraambazo huchangia kuongezeka kwa hali ya joto," alisema Waziri huyo.

Aliongeza kuwa pamoja na athari za mabadiliko haya kuzikumba nchi zote
duniani pia huzikumbwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hi ni kutokanana ukeli kuwa ukuaji wa uchumi wetu hutegemea zaidi shughuli za kiuchumi.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alibainisha kuwa ili kukabiliana changamotohizo kama nchi tunahitaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuhimili nakujiepusha na majanga yanayosababishwa nayo.

Alitahdharisha kuwa majanga yanayotokana na hali hiyo husababisha hasara zakiuchumi na kijamii zinazochangia kuongezeka kwa umaskini na hata migogoroya kijamii.

“Chanzo cha kupotea kwa amani kwa baadhi ya maeneo ni chanzo chake ni
mabadiliko ya tabianchi na hali ikibadili watu wakakosa mahitaji kama maji
hawawezi kukubali kufa lazima watatumia nguvu yoyote kuyapata kwa
kugombana.

“Hali ya hewa ikibadilika kusababisha kukosekana kwa maji watu watapambanana kutafuta yake kidogo yaliyopo na katika kuyatafuta lazima watagombana hivyo kusababisha vurugu hivyo amani ina uhusiano mkubwa na mabadiliko yatabianchi”alisema.

Mhe. Simbachawene alidokeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa mazingirahivyo imeendelea kufanya jitihada kubwa za kutunza na kusimamia mazingirakwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari.

Kwa upande mwingine Waziri Simbachawene alihimiza jumuiya za kimataifakuweka mkazo katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi kwakuzingatia kuwa uchumi wetu hutegemea shughuli zitokanazo na mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN)-Tanzania Amon
Manyama alipongeza Serikali kwa jiihada zake za kulinda amani hususana katikakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kuwa ni jambo jema kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na
changamoto hiyo na kuwa amani ni msingi wa kuanzishwa kwa UN hivyo
tuhakikishe jitihada hizi zinadumu.

SERIKALI KUJENGA SOKO LA SAMAKI LA KISASAKIJIJI CHA BUYUNI KIGAMBONI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sarah Msafiri akizungumza na wananchi wa kata ya Pemba Mnazi ,akileza kuhusu Serikali kujenga soko la samaki la kisasa katika kijiji cha Buyuni, ambapo amewaomba wananchi waitunze miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa na serikali.Dc Msafiri ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Emmanuel Maasaka wa Michuzi Tv)
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi John Makuri akizungumza na wananchi wa kata ya Pemba Mnazi akiwaeleza namba watavyotekeleza majukumu yao na mikakati mbalimbali katika suala zima la kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia) akisikiliza kero mbalimbli za wananchi katika ziara ya yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakikagua eneo lililotolewa na wananchi bure kwa ajili ya kujenga soko la kisasa la samaki katika kijiji cha Buyuni kata ya Pemba Mnazi jijini Dar es Salaam.
mkutano ukiendelea 
wananchi wa kijiji cha Buyuni kata ya Pemba Mnazi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri .(Picha na Emmanuel Maasaka wa Michuzi Tv)

WAKULIMA MSIUZE PAMBA CHINI YA SH. 1,200-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Pamba wakati alipotembelea maghala ya Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato mkoani Geita, Septemba 21, 2019. Kushoto ni Meneja wa Chama hicho, Charles Nyasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la pamba nchini wasikubali kuuza pamba yao chini ya bei elekezi ya sh. 1,200.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wafanyabiashara wa zao hilo waungane na kuanzisha viwanda vya kutengeneza nyuzi na nguo ili kuongeza thamani kabla ya kuuza pamoja na kuwahakikishia wakulima soko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 21, 2019) wakati akizungumza na viongozi na wananchama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato (CCU) pamoja na wananchi kwenye kiwanda cha kuchambua pamba cha Chato kinachomilikiwa na CCU mkoani Geita.

Amesema wakulima waendelee kuwa na subira kwa sababu wanunuzi hao wamepewa fedha za kutosha kununua pamba yote kwa bei ya 1,200 na si vinginevyo.

“Hata mkiwa na shida msikubali kuuza pamba yenu chini ya sh. 1,200 kwa kuwa haitachukua muda mrefu mtakuwa mmeshapata fedha zenu. Tuna taarifa kuwa kuna wanunuzi wamepata fedha na wanawatumia watu kwenda kuwalaghai wakulima kwa kutaka kununua kwa bei ya sh. 800, msikubali na mkiwaona mtupe taarifa.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema viwanda vya nyuzi na vya nguo vikijengwa nchini vitakuwa na uhakika wa soko kwani hivi sasa Tanzania haina viwanda vya kutosha vya nguo. Amesema Serikali ipo tayari kuwaunga mkono Watanzania wote au mwekezaji yeyote atakayekuwa tayari kuanzisha viwanda vya aina hiyo kwa sababu mahitaji ni makubwa. 

“Tuna shule zaidi ya 18,000 Tanzania na wanafunzi wote wanavaa sare zinatokanazo na pamba, tukisema majora ya sare yasukwe humu humu ndani na kisha kusambazwa mikoa yote bado nguo za watu wanaovaa mitaani. Watapata faida tu.”

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wote wa vyama vya ushirika katika maeneo yanayolima pamba kuwaelimisha wakulima kuhusu umuhimu wa kuzalisha pamba safi ili walinde heshima ya pamba ya Tanzania ambayo duniani inasifika kuwa ni dhahabu nyeupe.

Awali, Meneja wa CCU, Charles Nyasi alimwambia Waziri Mkuu kuwa makampuni ya METEL, KCCL na FRESHO yamejitokeza kununua pamba kupitia AMCOS na tayari kilo 9,611,860 zimenunuliwa kati ya kilo 11, 140,529 zilizokusanywa.

Alisema kampuni ya FRESHO imenunua kilo 4, 869, 960, KCCL imenunua kilo 3, 025,051 na METEL imenunua kilo 1,716, 420.

Pia Meneja huyo aliiomba Serikali isaidie kuwalipia deni la sh. 696,854,475.20 ili kumaliza tatizo la madai ya watumishi na wadai wengine. Pia aliiomba Serikali isaidie kuilipia CCU deni la sh. 102, 942,300.00 la ardhi waliyotumia kujengwa kiwanda chao.

Akijibu maombi hayo Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haiwezi kulipa deni hilo hadi itakapopewa maelezo ya kina ni nani aliyesabaisha deni, mazingira yaliyosababisha deni hilo.

RC MAKONDA ATOA TUZO NA ZAWADI KWA WANAFUNZI NA WALIMU WA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MITIHANI YA TAIFA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI DARE S SALAAM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ametoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, na walimu ambao shule zao zilifanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya msingi na sekondari mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.

Sambamba na zawadi hizo, Mhe. Makonda pia ameahidi kutoa ofa kwa walimu 30 wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na wenza wao kwenda kwenye mbuga ya wanyama ikiwa ni furaha yake baada ya shule za jiji la Dar es Salaam kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo lakini pia kwenye michezo ya Umiseta.

Kandoni na hafla hiyo, Maafisa wa Mwalimu Bank, benki ambayo ilikuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa walimu kusapoti shughuli hiyo, walikabidhi kadi za ATM kwa walimu ambao ni wateja wa benki hiyo sambamba na kuandikisha wateja wapya ambao walijitokeza kufungua akaunti.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mhe. Makonda pamoja na mambo mengine aliipongeza Benki ya Mwalimu na wadau wengine kwa kuunga mkono elimu na walimu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Bank, Bw. Richard Makungwa alisema asilimia kubwa ya wanahisa wa benki hiyo ni walimu na kuwahimiza walimu kutumia huduma za benki hiyo ili kufikia lengo la kuanzishwa kwake la kuwainua walimu kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa kutokana na benki hiyo kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa wanafunzi na walimu wa mkoa wa Dar es Salaam waliofanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Karume ulio katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam leo Septemba 21, 2019. Benki ya Mwalimu inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na walimu kote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wa shule ya sekondari iliyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake.
Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa, akitoa hotuba yake.
Afisa Uhusiano wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Michael Kachala, (kulia), akimuelimisha Mwalimu huyu ambaye ni mteja wa Mwalimu Commercial Bank, namna ya kutumia ATM card. Benki ya Mwalimu iko katika mtandao wa ATM za Umoja Switch kote nchini.
Walimu wakijaza fomu za kufungulia akaunti, kandoni mwa hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao shule zao zilifanya vizurio kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya eli mu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani), akizungumza na mmoja wa walimu ambaye alifika kwenye meza ya benki hiyo kuhudumiwa.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB)Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani) pamoja na timu yake Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi(wapili kulia) na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Bw. Michael Kachala, wakichambua ATM cards za wateja wa benki hiyo tayari kuwakabidhi.
Afisa mahusiano wa tawi la Mlimani Mwalimu Commercial Bank, Barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam wa Benki ya Mwalimu Bw. Abdulhakim Salimu (kushoto), akimwelekeza mteja namna ya kujaza fomu ya kufungulia akaunti.
Elimu ya ATM card ikiendelea kutoklewa hapa ni Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Michael Kachala (kulia), akifafanua jambo kwa mteja
Afisa wa Huduma kwa wateja wa Malimu Commercial Bank (MCB), Bi.Martha Gambosi (kulia) akimweleza jambo Mwalimu huyu (aliyeipa mgongo camera) kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo.

DKT. ASHATU KIJAJI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KIJIJI CHA MWONGOLO KONDOA VIJIJINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Mwongolo wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao walimuomba awatatulie kero ya maji ambayo imekua changamoto kubwa kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kondoa, Dodoma Alhaji Othman Gora(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya hiyo Bw. Nicholaus Kasendamila wakati wa mkutano wa hadhara kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo alipotembea Kijiji hicho.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Mwolongo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa anatolea majibu ya baadhi ya changamoto zilizotolewa na wanakijiji hao.
Bi. Khadija Irorya akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), changamoto ya ukosefu wa maji katika Kijiji hicho na kumuomba awasaidie kuitatua kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ilolo Bw. Ramadhani Bakari alipotembea Kijiji hicho.

……………………

Na Mwandishi wetu, Kondoa

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi kumaliza kero ya maji inayo wakabili wakazi wa Kijiji cha Mwongolo mkoani humo.

Ametoa ahadi hiyo alipokutana na wananchi wa kijiji hicho ambao walimweleza kuhusu changamoto yao ya muda mrefu ya kukosa huduma ya maji safi na salama pamoja na changamoto nyingine za ukosefu wa miundombinu mingine inayoweza kuchochea kasi yao ya maendeleo.

Wananchi hao walisema kero kubwa inayo waumiza ni upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wamekuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kuchota maji jambo ambalo limewafanya kuchoka na kuhatarisha usalama wa maisha yao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa amekuwa akichimba visima katika vijiji mbalimbali wilayani humo ambapo hadi sasa jumla ya visima 65 vimeshakamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

“Leo nimekamilisha kisima cha 65 Shule ya Msingi Kalamba niliposoma ndani ya miaka minne ya uongozi wangu, hapa Mwongolo ni nyumbani na kwa mapenzi niliyonayo kwa ndugu zangu wa Mwongolo, mhandisi akimaliza kuchimba kisima cha kijiji cha Mwaisanga atakuja Mwolongo katika kipindi cha mwezi huu au wa kumi kisima kitakuwa kimechimbwa” alisisitiza Dkt. Kijaji.”

Aidha ameahidi kufuatilia visima 14 vilichoahidiwa kuchimbwa kwenye sehemu ya machinjio ya kijiji hicho na Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, (DDCA), ili nao waweze kupata maji kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu hivyo itaendelea kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile Sekta ya elimu, huduma za afya, nishati, maji, miundombinu ili ziweze kuwafikia wananchi wote nchini kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwolongo Bw. Miraji Ramadhani, amemshukuru Dkt. Ashatu Kijaji kwa kutenga muda wa kwenda kutembelea kijiji hicho na kutatua baadhi ya kero zilizokuwa vinawasumbua muda mrefu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi hadi kufikia 2020 vijiji vyote 84 vya Jimbo lake la Kondoa Vijijini vitakua vimepata huduma ya maji kwa njia ya visima vya maji ili kumaliza kabisa kero ya maji Jimboni humo.

WAFANYAKAZI NMB WAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI

$
0
0

Katika kuadhimisha siku ya usafi duniani wafanyakazi wa benki ya NMB wameshiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini kote, tazama matukio ya picha katika mikoa na maeneo mbalimbali zikionesha wafanyakazi hao wakifanya usafi.
Wafanyakazi wa benki ya NMB Kanda ya Mashariki wakiendelea na usafi.


Wafanyakazi wa benki ya NMB Kanda ya Mashariki wakiendelea na usafi.
Wafayakazi wa benki ya NMB Tarime Mkoani Mara wakiendelea wakifanya usafi jana katika mji wa huo.

Wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Sengerema mkoani Mwanza nao walishiriki katika kufanya usafi kwenye mji huo.

Wafanayakazi wa benki ya NMB tawi la Kalius mkoa wa Tabora nao walishiriki katika kufanya usafi kwenye mji huo
Wafanyakazi wa NMB Kanda ya Dar es salaam nao walifanya usafi jijini Dar es salaam.

NAIBU KATIBU MKUU UWT TAIFA ATEMBELEA CHEMBA

$
0
0
Na Shani Amanzi 

Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mhe.Jesca Mbogo awataka wanawake wa Chemba wasiishi kwa kuchukiana badala yake washirikiane na wafanye kazi kwa pamoja kwani Serikali ya awamu ya tano ni ya kuchapa kazi na watumie fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi badala ya kuwa na majungu kwani majungu si mtaji. 

“kumekuwa na zana ya ujasirimali ulioanza toka zamani lakini kutokana na dunia inatanuka kiuchumi na sayansi na teknolojia ni vyema nanyi kuwa wabunifu katika kukuza ujasirimali wenu kwani lengo la kuja leo sio tuu kuwainua wakinamama kiuchumi bali pia makundi ya walemavu amnapo wapo wa jinsia zote na mtambue kuwa Chama hichi cha Mapinduzi kinawajali na kuwathamini wananchi wote kwani maendeleo yenu ni maendeleo ya nchi nzima”aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Jesca Mbogo. 

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga “ katika wilaya tunaendelea kuweka kipaumbele kwa wananchi hususani katika mambo yatayowasaidia kimaendeleo kwa kushirikiana na viongozi wa chama pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Chemba ikiwemo katika maboresho ya barabara ingawa Chemba inaendelea kukua, tunabuni njia mbalimbali za kupata mapato ya ndani ya wilaya pamoja na kutatua kero ya maji kwa wananchi” 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumeweza kutoa mkopo kwa kina mama pamoja na vijana na ile 10% 



IGP:IMARISHENI NIDHAMU MUWAPO KAZINI NA WAJIBU WENU WA KUSIMAMIA SHERIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro akizungumza na baadhi ya Askari mkoani Arusha alipowatembelea sambamba na kukabidhi nyumba kwa askari hao.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na baadhi wa Askari wa Jeshi la Polisi Njiro mkoani hapo kabla ya kukabidhi nyumba kwa askari sita
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro akisisitiza jambo kwa baadhi ya Askari katika mkoa wa Arusha
Mmoja wa kiongozi wa Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha akizungumza jambo kabla ya IGP kukabidhi nyumba kwa baadhi ya askari.
Mmoja wa Askari wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kati ya sita Arusha akikabidhiwa funguo za nyumba na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro,Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Shanna.



Na Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka jeshi la polisi nchini kuzingatia nidhamu wawapo kazini sambamba na kutojihusisha na mambo ya kisiasa badala yake wafanye kazi kwa uadilifu sambamba na kusimamia sheria kama kazi kubwa ya jeshi 

Amewasisitizia kuiheshimu kazi kujiamini na kusimamia sheria ,amesema askari ayupo upande wa siasa bali kutambua kuwa wajibu mkubwa wa askari ni kusimamia sheria na kuwatumikia watanzania,amesema aslani hapendi kumfukizisha kazi askari ila askari pia asilmazimishe kumfukuza amemtaka kila askari kutimiza wajibu wake.

"Hapa hakuna baba kanituma hiyo biashara haipo mmenipata vizuri!kila mmoja wenu atimize wajibu wake kwa mujibu nwa sheria "alisema Sirro.

Akizungumza na baadhi ya askari Mkoa wa Arusha Sirro amesema hali ya usalama wa nchi ipo vizuri, amesema changamoto waliyonayo kunaosumbua umebakia mdogomdogo,changamoto zilizopo ni dalili za ugaidi na baadhi ya askari kutoa siri za jeshi.

IGP Sirro amesema serikali ametatua changamoto iloyokuwa inawakabili ya sare kwakutoa jumla ya shilingi Bil.10 sambamba na shilingi kwaajili ya bil 3.5 kwaajili ya manunuzi ya hekopta ya jeshi


Amesema hapo miaka ya nyuma walikuwa na tatizo la sare ila kwa sasa wanakwenda vizuri kwani wameshachukua hatua ambapo kila mkoa atanunu vyerehani na kuhakikisha kila mkoa utahakikisha askari wanashonewa na watakuwa na mafundi wao.


Amesema shida kubwa inayolisumbua jeshi la polisi kwa sasa ni baadhi ya askari wachache wanaowauzia askari wenzao sare za jeshi hilo jambo ambalo linapelekea kuleta chuki miongoni mwa askari

“Kama kuna mjinga anataka aende kwa shangazi yake aendelee kuuza uniform,aendelee kununua uniform nimekwenda Zanzibar nimewaambia,na ninavyosema hivi kuna wengine wapo mahabusu kwa sasa unapomuuzia mwenzako uniform unategemea nini unapochukua fedha ya askari mwenzako unamuuzia government stoo maana yake nini’’aliuliza Sirro.

Amesema kuna baadhi ya askari wanatamaa na wanadhani zitawasaidia badala yake zitawapeleka pabaya amesema Jeshi lazima wapendane huku akiwasisitizia kwamba kama wanapendana hawawezi kuuziana sare hizo

Pia amewapongeza kwa nyumba nzuri amesema tayari zilishafanyiwa uzunduzi Geita nyumba 400 na Rais wa Jamuhuri hivyo amewataka askari 6 ambao wamekabidhiwa nyumba hizo maeneo ya njiro wazitunze ili zidumu

Ndiyo maana nikiwaona wenzetu wa bendi wanancheza naona ni kipaji wamepewa na Mungu wewe ukiona siyo kazi shauri lako na Rais Magufuli kule Geita.Kwa upande wake mkuu wa moa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Gambo amesema serikali ngazi ya mkoa wameweka mkakati endelevu wa kujenga nyumba moja ya jeshi la polisi itakayokaliwa na familia 6  u wa mkoa Mrisho Gambo amelipongeza jeshi la polisi mkoani Arusha ambapo  "Jeshi hilo ndilo limbiliao la wananchiwanyonge,wenye uwezo na wananchi wa makundi yote kayika Taifa la Tanzania"Alisema Gambo

Gambo amesema jeshi la polisi amesema kwa kupitia jeshi hilo mkoa huo umekuwa salama kwani limekuwa likilinda usalama wa raia na mali zao na linahusika na maswala ya mkoa kwa asilimia kubwa,amesema yapo majeshi yanafanya kazi kubwa na mzuri ,ila jeshi linaloonekana mara kwa mara mbele ya raia ni jeshi la polisi.

Aidha amelitaka jeshi hilo kuhakikisha raia wanakuwa salama na mali zao katika maeneo yao kipindi chote cha uchaguzi wa serikali za mtaa ,bila kujali itikadi za vyama vyao, huku wakikumbuka wajibu wa polisi ni kusimamia sheria na hawafungamani na siasa.

CCM ITAENDELEA KUONGOZA NCHI HADI MIAKA 2OO IJAYO-UVCCM

$
0
0
 Kijana wa Chipukizi, Mkoa wa Singida,  Salumu Waziri akimvika Skafu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala mara baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Mkoa wa Singida kwa ajili ya kuzindua Tamasha la Singida ya Kijani jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Dkt.Denis Nyiraha.
 Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala akisalimiana na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu baada ya kuwasili mkoani humo.
 Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aisharose Mattembe.
 Baadhi ya Wabunge Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi (kushoto) akizungumza wakati wa kikao kifupi cha ndani  na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa,  Mwalimu Raymond Mwangwala (wa pili kutoka kulia). Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba  na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Dkt.Denis Nyiraha.
 Makada wa CCM wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wabunge, Elibariki Kingu wa Singida Magharibi (katikati) na Miraji Mtaturu wa Singida Mashariki (mapacha) wakimtuza Msanii wa kuigiza sauti za watu, Oscar Nyerere wakati akitoa burudani kwenye tamasha hilo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Dkt.Kitila Mkumbo akizungumza kwenye tamasha hilo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida (NEC), Yohana Msita akizungumza katika Tamasha hilo.
 Tamasha likiendelea.
 Tamasha likiendelea.
 Mjumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Mkoa wa Singida, Rehema Zombi akizungumza.

 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Dkt. Denis Nyiraha akimkabidhi keki maalumu ya tamasha hilo, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala.
 Tamasha likiendelea. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dkt.Kitila Mkumbo, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo na Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi.
 Wana CCM wakiserebuka wakati Msanii Papi Kocha akitoa burudani.
 Mwanamuziki Papi Kocha akipagawisha katika Tamasha hilo 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba akizungumza.
 Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala akihutubia.
 Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala akiwa na baadhi ya wananchi waliojiunga na CCM wakitokea vyama vingine.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (mwenye miwani katikati nyuma) akiwa na baadhi ya Vijana wa CCM kutoka katika jimbo lake.


Na Dotto Mwaibale, Singida

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mwalimu Raymond Mwangwala amesema chama hicho kitaendelea kuongoza nchi hadi miaka 200 ijayo.

Mwangwala aliyasema hayo mjini hapa jana kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa,  Bashiru Ally wakati akizindua Tamasha la Singida ya Kijani lililofanyika viwanja vya Bombadier.

"Kutokana na chama chetu kuwa makini na kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dkt.John Magufuli ya kutekeleza miradi ya maendeleo CCM itaendelea kuongoza nchi hii hadi miaka 200 ijayo" alisema Mwangwala.

Alisema Rais Dkt.John Magufuli amefanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015/ 2020  kwani hivi sasa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari inatolewa bure baada ya kusimamia matumizi mazuri ya fedha za serikali na kodi inayolipwa.

Alitaja maeneo mengine yaliyofanywa na serikali ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji, reli, ununuaji wa ndege, barabara, umeme na sekta ya afya ambapo vituo vya afya, zahanati na hospitali zimejengwa nchi nzima akitolea mfano mkoani Singida ambako zimejengwa Hospitali mbili za wilaya ya Mkalama na Ilongero na vituo vya afya 11 vilivyogharimu zaidi ya sh.milioni 500 huko zahanati zikijengwa karibu vijiji vyote.

Mwangwala alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)  Mkoa wa Singida, Aisharose Mattembe kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika sekta ya afya kwa kununua gari la wagonjwa lenye thamani ya sh.milioni 21 na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Singida.

" Mbunge huyu hakika amefanya kazi kubwa ya kuwajali wanawake kwa kuwanunulia vifaa tiba hivyo  vitanda vya wagonjwa 16 viwili vikiwa ni vya kujifungulia wajawazito vyote thamani yake ikiwa sh.milioni 11.6, kwa utendaji wake huu wa kazi ndio unaotakiwa kuigwa na viongozi wengine katika nchi hii" alisema Mwangwala. 

Katika hatua nyingine Mwangwala aliwataka vijana wa CCM kuacha kukaa kimya badala yake wawajibu wale wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuitukana serikali na kuibeza nakueleza sasa iwe ni bampa tu bampa.

"Wewe kijana wa CCM popote pale ulipo ukiona mtu anaiponda serikali yetu mjibu papo hapo usisubiri hujibiwe na viongozi waliopo juu" alisema.

Alisema kumekuwa na maneno ya kejeri dhidi ya watu ambao wanajipendekeza na kumsifia Rais wetu ambapo alisema waendelee kumsifia ili wapate vyeo na kuachana na hao ambao wanashinda vijiweni wakilalamika.

Akizungumzia demokrasia aliyataka mataifa ya nje kutoingilia mambo yetu ya ndani na kuwa wao waendelee na yao na sisi watuache na demokrasia yetu.

Alisema katika uchaguzi ujao wa viongozi wa serikali za mitaa CCM itashinda kwa kiwango kikubwa kila maeneo na hii inatokana na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt.John Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Aliongeza kuwa hakuna kipindi cha wana CCM wanachojidai kama  kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli kwani majibu yote ya wananchi yamekwisha jibiwa.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Singida ya Kijani lililoandaliwa na UVCCM Mkoa wa Singida alisema rangi hiyo ndio inawakilisha mambo yote mazuri na kuyakataa mabaya kama rushwa, uvivu, wizi na mengine mengi ambapo aliusifia mkoa huo kwa kuwa na ushirikiano  baina ya viongozi  wa serikali na wachama na kuwa ndio unaoongoza kwa kuwa na kura nyingi wakati wa uchaguzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Dkt.Kitila Mkumbo akielezea kuhusu maji alisema serikali imetekeleza miradi mingi mikubwa ya maji nchi nzima na sasa inatarajia kutekeleza mradi wa maji kutoka ziwa Victoria ambao umepitia shinyanga na kupelekwa makao makuu ya nchi Dodoma.

Katika Tamasha hilo viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa CCM, Wabunge, Serikali na Wajumbe wa Baraza la UVCCM Taifa kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar walipata fursa ya kuelezea mambo mbalimbali ya maendeleo yaliyofanywa na kuendelea kufanywa na serikali.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images