Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WANANCHI NYAMONGO WAFANYIWA TATHMINI YA FIDIA KUPISHA UJENZI BWAWA LA MAJI TAKA

0
0
Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha akiangalia moja ya nyumba iliyofanyiwa uthamini kwa ajili ya kulipwa fidia katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la taka sumu jana. Kulia ni Mthamini kutoka wilaya ya Serengeti Bariki Ileta.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha (Nyuma) akiwa na wataalamu wa Uthamini kutoka Serengeti Bariki Ileta (Mbele) na Bisare Charles kutoka Tarime wakati wa zoezi la Uthamini linaloendelea katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara ili kulipwa fidia kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la taka sumu jana.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa Uthamini wakati wa zoezi la Uthamini katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara ili kulipwa fidia kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la taka sumu jana.
Mkazi wa kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara Marwa Mangora Mube akiwaoongoza wataalamu wa Uthamini kukagua eneo lake kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ili kulipwa fidia kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la taka sumu jana.
Wataalamu wa Upimaji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiandaa vifaa tayari kwa upimaji wakati wa zoezi uthamini katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara ili kulipa fidia kwa wananchi kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la taka sumu jana. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

************************************ 


Na Munir Shemweta, WANMM NYAMONGO

Serikali imeanza kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Nyamongo katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa kuanza kufanya tathmini ya fidia ya kutwaa eneo la ardhi kwa ajili ya kupanua Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA North Mara ili kujenga Bwawa la Maji Taka.

Tayari timu ya wataalamu 25 kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayojumisha Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali pamoja na idara ya Upimaji na Ramani iko eneo la Nyamongo kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoani Mara kutathmini mali za wananchi ili kulipwa fidia na kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Maji Taka.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo jana katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha alisema, zoezi la uthamini linalofanyika ni kwa ajili ya kutwaa eneo la ujenzi wa Bwawa la Maji Taka katika eneo la Nyamongo lenye ukubwa wa hekta 237 ambalo linahusisha vitongoji vitatu vya Kigonga A, Kwinyunywi na Kigonga B ambapo uthamini wake ulishaanza toka mwezi julai mwaka huu.

Mugasha alisema, uthamini huo unaangalia mali inayohamishika na ile isiyohamishika na kufuata sheria ya ardhi na ile ya kijiji na kusisitiza uthamini huo umekuwa ukifanyika kwa uwazi na hauna lengo la kumnufaisha au kumpunja mtu yeyote.

‘’ Eneo la Nyamongo tunalichukulia kama eneo la mfano hasa baada ya kufanyika tathmni maeneo mbalimbali ya mgodi miaka ya nyuma na kubaini udanganyifu wa baadhi ya wananchi na Wathamni wasiowaaminifu kutumia zoezi kama hili kujinufaisha’’ alisema Mugasha.

Kwa mujibu wa Mthamini Mkuu wa Serikali, udanganyifu wowote utakaofanyika kwa nia ya mmiliki wa nyumba ama eneo kujinufaisha Ofisi yake haitamvumilia kwa kuwa baada ya uthamini wanafanya uhakiki kujiridhisha usahihi wa taarifa na mali za wananchi.

Mthamini kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu Lazaro Mayumba anayeshiriki zoezi hilo alisema, zoezi hilo linafanyika kwa kasi kwa kuwa serikali ina jukumu la kulinda mali na afya za wananchi waliokuwa wakilalamikia kwa muda mrefu kuhusu kutiririka maji yenye sumu katika Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA North Mara.

Alieleza kuwa, katika kuhakikisha wananchi wanaozunguka mgodi huo hawaathiriki na wakati huo mgodi haufungwi kutokana na madhara yanayopatikana dhidi ya taka sumu, serikali iliona iko haja kutwaa eneo litakalosaidia mgodi kupata eneo kwa ajili ya ujenzi bwawa kubwa na lenye ubora ambalo halitaleta madhara yanayodaiwa na wananchi.

”Mbali na madai ya wananchi wanaozunguka mgodi wa North Mara lakini pia athari za taka sumu zinaweza kufika mto Mara ambao uko umbali wa takriban kilometa tatu kutoka katika Mgodi na kama hatua za haraka hazitachukuliwa unaweza kuharibu uoto wa asili pamoja na mbuga za wanyama”’ alisema Mayumba.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Matongo linakofanyika zoezi la Uthamini wameonesha kufurahishwa na hatua ya serikali kuamua kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa jipya la taka sumu za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa madai kuwa wamekuwa wakiathirika sana na maji yanayotiririka katika mgodi huo.

Gaga Sita Kishashila mmoja wa wakazi wa kijiji cha Matonga alisema pamoja na zoezi la uthamini linaloendelea sasa lakini shauku kubwa ya wakazi hao ni kutaka kujua wanalipwa lini ili waweze kuondoka maeneo hayo mapema na hofu yao ni kukwama kwa zoezi hilo kama ilivyotokea huko nyuma.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Simion Kirario aliomba uthamini unaofanyika kuangalia na hali za wananchi hao kwa kuwa baadhi yao wana hofu ya kulipwa kiasi kidogo kutokana na aina ya nyumba wanazomiliki za Msonge huku wakihitaji kuwa na fedha nzuri itakayowawezesha kununua eneo lingine na kufanya maendelezo.

Mwenyekiti wa Kitongoni cha Kigonga A Kibwabwa Mwita Kibwabwa alisema kazi ya uthamni katika kitongoji chake imeenda vizuri kwa kuwa zoezi hilo linafanyika kwa kasi na wananchi wake wanataka kujua wanalipwa lini. Hata hivyo alisema baadhi ya wananchi wamelalamikia kiasi watakacholipwa na kukiona kidogo ukilinganisha na matarajio yao.

Kwa muda mrefu wananchi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa mara hasa wale wanaoishi vitongoji vinavozunguka Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA North Mara wamekuwa wakilalamikia uchafuzi wa mazingira hasa maji yanayovuja kutoka Mgodi huo kuwa yana sumu inayoathiri afya zao jambo lililomlazimu Rais John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake katika eneo hilo kuagiza kufanyika utafiti ili kubaini ukweli huo.

WATOTO WA WAFUGAJI WANUFAIKA NA ECLAT FOUNDATION

0
0

Na mwandishi wetu, Arusha

WATOTO wa jamii ya wafugaji wa Lorkisalie Wilayani Monduli na Malambo Wilayani Ngorongoro wamenufaika kielimu baada ya kampuni ya ECLAT Foundation kujenga miundombinu ya madarasa ya shule zao za msingi kwa kutumia sh236 milioni. 

Ofisa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation, Bakiri Angalia aliyasema hayo wakati akielezea ujenzi wa miundombinu ya shule hizo mbili tofauti zilizopo kwenye jamii ya wafugaji. 

Angalia alisema kwenye shule ya msingi Lengijabe ya wilayani Monduli mkoani Arusha wametumia sh102 milioni kumalizia ujenzi wa madarasa sita. 

Alisema pia kwenye shule hiyo wametoa madawati 138, ujenzi wa matundu 16 ya vyoo na kuweka mfumo wa uvunaji maji ya mvua. Alisema kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi Malambo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wametumia sh134 milioni. 

"Tumejenga madarasa matatu na ofisi ya walimu, madawati 69 na kuweka mfumo wa nishati ya umeme wa jua," alisema Angalia. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Steven Ulaya akizungumza wakati akikabidhiwa madarasa ya shule hiyo aliipongeza ECLAT Foundation kwa kufanikisha ujenzi huo. 

Ulaya alisema wanaahidi kuhakikisha walimu, wanafunzi na jamii ya eneo hilo wanatunza miundombinu ya shule hiyo iliyofanikishwa na ECLAT Foundation. Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima alisema wamekuwa wakisaidia jamii ya maeneo mbalimbali nchini katika kufanikisha maendeleo. 

"Tumefanikisha miradi mbalimbali nchini ikiwemo Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha, Simanjiro mkoani Manyara, Tandahimba mkoani Mtwara na Kakonko mkoani Kigoma," alisema Toima. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Steven Ulaya akiwakabidhi hati ya kutambua mchango wao kwa jamii Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima na Mkurugenzi wa Upendo Society Dkt Fred Heimbach.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Steven Ulaya (kushoto) kizungumza na wadau wa elimu, katikati ni Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima.

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA

0
0

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye WILLIAM MWAZEMBE [45] Mkazi wa Kijiji cha Ikukwa akiwa na bhangi gramu 300.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 17 Septemba, 2019 saa 19:30 usiku huko eneo la Chunya mjini, Kata ya Itewe, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya katika msako mkali uliofanyika maeneo hayo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye BAHATI NDELE, [28] Mkazi wa Ilemi akiwa na bhangi kilogram moja [01] na gramu 210.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2019 saa 15:30 alasiri huko eneo na Kata Ilemi, Tarafa Sisimba, Jiji la Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

 

KUJARIBU KUJIUA KWA KUNYWA SUMU.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye SILVIA SANDE[28] Mkazi wa Nsongwi kwa mauaji ya mtoto wake mwenyewe aitwaye ASIFIWE RASHIDI BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili na kwa jaribio la kujiua yeye mwenyewe kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu.

Ni kwamba mnamo tarehe 16 Septemba, 2019 saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Nsongwi Juu kilichopo Kata ya Ijombe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa alikunywa sumu ya kuulia wadudu chumbani kwake kwa lengo la kujiua kisha kumnywesha sumu hiyo mtoto wake aitwaye ASIFIWE RASHIDI BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, mkazi wa Nsongwi juu.
Mtuhumiwa na mtoto wake baada ya tukio hilo walikimbizwa kituo cha afya Igawilo ambapo mtoto alifariki. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani. Chanzo cha tukio kinachunguzwa. 
KUPATIKANA NA NISHATI YA MAFUTA BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa tisa [09] kwa tuhuma za kupatikana na kufanya biashara ya nishati ya mafuta aina ya Diesel na Petrol bila kibali.
Watuhumiwa wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tarehe 17 Septemba, 2019 katika maeneo ya Maghorofani, Uyole Jijini Mbeya, Chimala, Igawa na Igurusi Wilayani Mbarali na maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela.
Katika msako huo jumla ya lita 1,500 za Petrol na lita 2,500 za Diesel zimekamatwa. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  1. MAJALIWA EDWARD [30] Mkazi wa Mwambene
  2. EDSON KALINGA @ MANGI [32] Mkazi wa Iganzo
  3. HAMIS ANYIMIKE [32] Mkazi wa Mafiati
  4. ISSAH MWAMBELO [33] Fundi Magari na Mkazi wa Sae
  5. KAMBELA HAMAD MWIPOPO [30] Mkazi wa Makunguru
  6. GEORGE MWAKALOBO @ MWADADA [40] Mkazi wa Ipinda
  7. MAJUTO SIMONI [37] Mkazi wa Kapwili
  8. LWITIKO MWAIPOPO [38] Mkazi wa Ipinda
  9. JAKOBO MWAKILEMA [47] Mkazi wa Ipinda
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imetolewa na:
 [ULRICH OMATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Tamasha la utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Dar

0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jumafest) litalifanyika Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAZIRI wa habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Herrison Mwakyembe ameutaka Umma wa watanzania kujitokeza  kwa  kushiriki kwenye tamasha   la kimataifa la utamaduni wa Afrika mashariki (Jamafest) linalotegemea kufanyika katika Uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Septemba 21 hadi 28 mwaka huu.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Waandishi Habari kuhusiana  tamasha hilo amesema matarijio ya nchi kuwa  yetu kama mwenyeji wa  tamasha ni pamoja kuvunja rekodi ya maonesho ya  kuonyesha vipaji tulivyonavyo, kazi  mbalimbali  za mtanzania ikiwemo kuhifadhi na kulinda utamaduni wa mtu mweusi kupitia tasnia ya sanaa itakayo leta taswira ya kiushindani.

"Watanzania wote hapa nchini wahudhurie  kwenye onesho kubwa la kitamaduni ambayo lengo letu ni kuonyesha roho ya Afrika ambyo ni utamaduni  katika nyanja mbalimbali za sanaa," amsema Dkt.Mwakyembe

Dkt.Mwakyembe amesema kuwa tamasha hilo litawashirikisha wasanii na wajasiriamali kutoka nchi sita za Jumuiya ya Afrika mashariki zikiwemo Kenya , Uganda , Burundi, Rwanda na Tanzania kwa kuonyesha tamaduni za nchi zao.

Tamasho hilo limeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya habari Utamaduni Sanaa na michezo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali  wa tasnia ya sanaa ili kuweza kufanikisha hilo.

Kwenye maadhimisho hayo wasanii wetu nchini wakiongozwa na Peter Msechu wameandaa wimbo maalumu utakaobaba ujumbe wa utamaduni wetu kwa ajili ya kulipamba tamasha hilo.

Dkt. Mwakyembe amesema tamasha hilo la kimataifa litawashirikisha wachonga vinyago, wabunifu wa mavazi,wasuka mikeka, watengenezaji wa nywele, wanamuziki wa dansi , watunga riwaya na michezo ya kuigiza.
Tamasha hilo litazinduliwa na Septemba 22 na Mmoja wa kiongozi wa juu.

Wateja kujishindia zawadi za pesa taslimu hadi Sh mil. 7 na safari za kwenda kushuhudia onesho Kenya.

0
0


Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)katika uzinduzi wa promosheni ya EAGT Trivia ambayo ni sehermu ya matumizi ya Kidigitali ya Tigo katika mkakati wake katika uzoefu kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa wateja wa Tigo.Kulia kwake ni Mratibu wa mradi wa EAGT Redemptus Caesar, Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam.
Mratibu wa mradi wa EAGT Redemptus Caesar, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa promosheni ya EAGT Trivia ambayo ni sehermu ya matumizi ya Kidigitali ya Tigo katika mkakati wake katika uzoefu kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa wateja wa Tigo.Kushoto kwake ni Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi ,Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam.



 Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imetangaza rasmi kuingia ushirikiano na kampuni maarufu ya kusaka vipaji 'Got Talent' na Clouds Media International. Maonyesho hayo kwa jina Kampuni maarufu kama ‘East African Got talent’ imedhamiria kukuza vipaji Afrika Masharika kwa upande wa kucheza na kuimba.

Ushirikiano huu unakwenda sambamba na uzinduzi wa promosheni ya EAGT Trivia ambayo ni sehermu ya matumizi ya Kidigitali ya Tigo katika mkakati wake katika uzoefu kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa wateja wa Tigo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi, alisema, mkakati huo wa Tigo umekuja kwa wakati muafaka ambapo tayari wamekwishapata kasi, na kuwa kazi iliyopo ni kuhakikisha wanafika ukanda mzima

“Kama kampuni ya mapinduzi ya kidigitali, kila mara tunaagalia majukwaa na mianya ambapo tunaweza kuunganisha wateja wetu pamoja. promosheni ya EAGT Trivia itatoa fursa sawa kwa wateja wetu kusimama pamoja kujishindia zawadfi za pesa taslimu na kwwenda kushuhudia onesha la moja kwa moja nchini Kenya,"

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa EAGT Redemptus Caesar, Redemptus Caesar, alisema “Tuna furaha kuugana pamoja na Tigo mojawapo ya kampuni kubwa zinazoongoza kwa mawasiliano nchini Tanzania- Tunatarajia kuweka msingi thabiti kwa vijana wa Tanzania kuonesha vipaji vyao duniani,"

Hata hivyo Ngowi alifafanua kuwa wateja wa Tigo watakiwa kuchamgamkia fursa hiyo, huko akisisitiza kila mteja kujitokeza kushiriki.

“Kupitia promosheni hii ya EAGT Trivia, wateja wa Tigo watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi za pesa taslimu hadi kufikia sh. mil. 7. Mbali na hiyo, wateja arobaini (40) watajishindia safari kwenda Kenya kutizama onesho.

Wateja wa Tigo wanaweza kujiunga na Trivia kwa kutuma neno 'TALENT'’kwenda 5572’ au kutembelea http://tigoquizkitaa.co.tz. Baada ya kujiunga mteja atakuwa akijibu maswali yanayohusiana na EAGT, ili kujishindia zawadi mbalimbali za shindano hilo.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kutizama onesho hilo kupitia intaneti ya Tigo 4G+ kupitia kifurushi cha YouTube chenye thamani ya Sh 1000 kwa GB1 kupitia menu yetu rahisi *147* 00#

Waziri Ummy Ahitimisha kambi Maalum ya Matibabu ya Moyo kwa Watoto ya Sharjah Charity Group kwa kuipongeza menejmenti ya JKCI kwa Huduma Bora za Matibabu ya Moyo

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi (kulia) pamoja na Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi wakimpatia zawadi mtoto mwenye magonjwa ya moyo anayepata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Shirika la Sharjah Charity Group kuwapongeza kwa jitihada wanazozifanya kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi kuthamini mchango unaotolewa na shirika hilo kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyotolewa na taasisi ya Islamic Foundation Tanzania kumpongeza kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha huduma za matibabu ya moyo katika taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na kiongozi wa madaktari wa shirika la Sharjah Charity Group kutoka nchi za Falme za Kiarabu Ahmed Mohammed Alkamali alipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari hao kwa kushirikiana na madaktari wa JKCI leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Kutoka kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakimsikiliza Daktari kutoka Shirika la Sharjah Charity Group wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali na watoto wenye magonjwa ya moyo wanaopata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa waziri ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi

Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

Airtel kutoa Tzs 2.5 bilioni kama faida kwa wateja wa Airtel Money

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za kidigitali ,imetangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT)

Faida itokanayo na Airtel Money ni fedha ambayo Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kiwango hicho cha faida kwa kila salio la mteja kinatolewa pia kulingana na jinsi mteja anavyotumia huduma ya Airtel Money, mteja atatumiwa faida yake kwenye akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kuamua kuzitoa,kutuma au kuzitumia kwa matumizi yoyote ikiwemo kulipia bili mbalimbali kama vile za DAWASCO, LUKU, MALIPO YA SERIKALI na mengine mengi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kugawa faida hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda alisema “faida itokanayo na matumizi ya Airtel Money itagawiwa kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wote nchini ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi kumi na mbili iliyopita kati ya September 2018 hadi March 2019.

“Airtel inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali zanazochochea kusambaa na upatikanaji wa huduma za kifedha hapa nchini kwa kutoa faida kila robo ya mwaka, faida hii itawawezesha wateja kupata jumla ya Tzs2.5bn zitakazokwenda kwa wateja na mawakala waliotumia huduma kwa kipindi hicho. Tunayo furaha kuona ukuaji mzuri kwenye huduma ya Airtel Money kwani mpaka sasa huduma zetu zimekuwa zikikuwa mfululizo kwa ukuaji wa tarakimu mbili, alisema Nchunda.

Nchunda aliongeza kuwa hii ni mara ya nane Airtel inatoa faida kwa wateja wake wote wa Airtel Money tangu mwaka 2015. Mpaka sasa jumla ya kiasi cha Tsh19 bilioni kimeweza kutolewa kama faida kwa wateja na mawakala wote nchini.

“Kuanzia leo wateja wote wa Airtel Money wataweza kutumia fedha zao za faida kwa kununua LUKU, kununua muda wa maongezi au bando au kwa matumizi yeyote yale”. Alisema Nchunda

Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta karibu huduma za Airtel Money ili kufikia maelfu ya Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki na hasa kwa maeneo ya vijijini. Kwa kufanikisha hilo, hivi karibuni Airtel ilizindua kampeni ya Tuko Nawe Kila Kona kwa lengo la kuimarisha huduma ya maduka ya Airtel Money Branches ambayo ni moja kati ya mikakati muhimu ya kusambaza huduma ya Airtel Money hapa nchini. Vilevile Airtel imezindua bando za Dabo Data Smatika kupitia Airtel Money kwa lengo la kuongeza huduma kwenye huduma zinazotolewa na Airtel Money branches zaidi ya 1000 nchini 

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa “Lengo letu ni kuendelea kuwafikia wateja wetu ambao ni muhimu sana kwenye biashara yetu. Tunaendelea na uzinduzi wa maduka ya Airtel Money Branches ili kuhakikisha kuwa na huduma za kifedha za Airtel Money zinaendea kupanuka na kuwafikia wateja wengi kuliko huduma yoyote ya kifedha nchini . Wateja wetu tunawahakikishia huduma ya papo kwa hapo za kutoa pesa ni BURE.

Airtel bado itaendelea kuhakikisha ya kwamba inapanua wigo wa mawakala kwa ajili ya kufikisha huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa Watanzania wote mjini na vijinini.

Mmbando alimalizia kwa kusema kuwa “Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa huduma ya Airtel Money pia tumejiunga na huduma zingine zenye tija kwa watumiaji kama vile e-government ambapo wateja wanaweza kufanya malipo ya huduma mbali mbali kama vile malipo ya tozo za ardhi, kodi za serikali, kwa wakati mmoja. Pia huduma ya Airtel Money imeunganisha zaidi ya benki 40 ili kuwawezesha wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu za mkononi kwenda benki na vile vile kutoa benki kuweka kwenye akaunti za simu za mkononi wakati wowote” .
Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Airtel Tanzania ikitangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT). Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Airtel Tanzania ikitangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT). Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isaack Nchunda.

WAFANYABIASHARA WA MJI WA IRINGA WAPEWA MAFUNZO NA BRELA YA KUPATA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO

0
0



WAFANYABIASHARA wa mji wa Mafinga Mkoani Iringa wamesema kuwa mfumo wa kusajili na kujipatia leseni kwa njia ya Mtandao inayotolewa na wakala wa usajili wa biashara na leseni(Brela).

Afisa Biashara Mwandamizi kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda,Boniface Mrema akizungumza mara aada ya kutoa mafunzo wezeshi kwa wafanyabiashara wa Mafinga Iringa. Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) yatawasaidia wafanyabiashara wa mji waMafinga kwaajili ya kujaza na kupata Leseni za biashara zao kwa njia ya mandao hapo hapo walipo kwa kutumia Kompyuta, Simu na kifaa chochote kinachoweza kuunganishwa na intaneti.
Mafunzo ya kiendelea kati wafanyabiashara wa mji wa Mafinga na maafisa Brela.
Mfanyabiashara kutoka mji wa Mafinga akizungumza jinsi alivyonufaishwa na mfumo wa kujipati leseni za Biashara kwa njia ya Matndao inayotolewa na wakala wa kusajili biashara na Leseni.
Afisa Leseni Mwandamizi -Brela, Abas Cothema.

KIKAO CHA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM TAIFA YAKUTANA LEO MJINI DODOMA

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Comred kheri Denice James leo ameongoza Kikao Cha Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa Katika Ukumbi wa Sekretarieti Jijini Dodoma. 
 Wajumbe wa kikao wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Comred kheri Denice James, Kikao hicho cha  Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa Katika Ukumbi wa Sekretarieti  kimefanyaika leo Jijini Dodoma. 


WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI MOROGORO

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa anatoka kwenye jengo la kituo cha afya Mkuyuni, baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho, katika Wilaya ya Morogoro, Septemba 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Mkuyuni, wilayani Morogoro, Septemba 18.2019.
Wananchi wa Mkuyuni, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wilayani Morogoro, Septemba 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Injinia, Godfrey Mlowe (kulia), baada ya kukagua jengo la kituo cha afya Mkuyuni, kilichopo katika Wilaya ya Morogoro, Septemba 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa kumi na tano, Hussein Ally Machaga (kulia), nje ya jengo la kituo cha afya Mkuyuni, katika Wilaya ya Morogoro, Septemba 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa kituo hicho, katika Wilaya ya Morogoro, Septemba 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

…………………..


*Amwagiza Mkuu wa Mkoa aungalie vizuri mkoa wake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuyuni.

Amemsimamisha kazi Mhandisi huyo leo (Jumatano, Septemba 18, 2019) baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Amesema hajaridhishwa na aina ya milango iliyotumika.

“Milango yote katika jengo hili ing’olewe leo leo, huwezi kuweka milango ya hovyo namna hii yaani mtu wa nje anamuona aliyeko ndani, nimesitisha kuendelea kukagua jengo. Yeye na usomi wake ameridhishwa na milango ya hovyo kama hii.”

Waziri Mkuu amesema aina ya milango iliyowekwa katika kituo hicho cha afya haiwezi kutumika hata kwenye nyumba ya mtu binafsi, lakini kutokana na uangalizi mbovu kutoka kwa watendaji walikubali kuweka milango hiyo mibovu.

Amesema Serikali imeamua kujenga vituo vya afya vitano kwenye wilaya hiyo ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hivyo amewataka watendaji wasimamie ipasavyo miradi hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao waendelee kuwa na imani na Serikali yao. 

Baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya, ambako nako ameagiza kuong’olewa kwa mbao zote zilizotumika kwa ajili ya kupaulia jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo kwa kuwa hazina viwango. “Fundi usiendelee na kazi hii ya upauaji kwa sababu mbao unazotumia hazikidhi viwango.”

Kwa upande wake, fundi anayejenga jengo hilo la mama na mtoto, Johnson Ishengoma amesema changamoto kubwa anayoipata katika ujenzi huo ni ucheleweshwaji wa vifaa pamoja na kulazimishwa kutumia vifaa vilivyo chini ya kiwango.

Fundi huyo ametolea mfano suala la mbao za kupaulia kuwa aliomba mbao za urefu wa futi 20 lakini aliletewa mbao zenye urefu wa futi 12 na kulazimishwa azitumie hivyo hivyo. “Mhandisi wa wilaya Brown Undule na mtu wa manunuzi Grace ndio wanaoniletea vifaa hivi. Baadhi ya vifaa huwa navikataa kutokana na kutokuwa na ubora.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe kuuangalia vizuri mkoa wake na kuhakikisha anauchunga vizuri kwa sababu umekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha za umma. 

“Wakati nikiendelea na ziara mkoani hapa, nimepata taarifa kwamba zaidi ya sh.milioni tisa zimetumika kwa ajili ya kilipana posho katika Halmashauri ya mji Ifakara . Posho hizo ni kwa ajili ya ziara ya Waziri Mkuu na imetoka kwa mtendaji wa kata ya Viwanja 60, hili jambo halikubaliki. Nakukabidhi risiti zote na uwachukulie hatua wote waliohusika. Mkoa wa Morogoro ni shida”

Wakingumzia kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano na ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, wakazi wa Tarafa ya Mkuyuni wameipongeza Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma.

Mmoja wa wananchi hao, Uwesu Mwichumu (71) mkazi wa kijiji cha Kibungo ameipongeza Serikali kwa usimamizi wa miradi na hatua inazochukua kwa baadhi ya watendaji wanaojihusisha na wizi wa fedha za umma.

Amesema Serikali inajitahidi kuwaletea miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao tatizo lililopo ni kwa watendaji wa chini. “Watendaji wengi huku chini wanashindwa kutekeleza majuku yao ipasavyo, wanashirikiana na wazabuni kuiibia Serikali.”

Mkazi mwingine wa Tarafa hiyo, Hanifa Shaban amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati. Amesema awali walikuwa wanakwenda zahanati na kuandikiwa vyeti bila ya kupewa dawa , hivyo walilazimika kwenda kununua kwenye maduka ya dawa jambo ambalo kwa sasa halipo.

Vihenge vya NFRA vyavutia uwekezaji eneo maalum la viwanda Sumbawanga

0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo baada ya kukagua mtambo wa kuponda kokoto zitakazotumika kwenye ujenzi wa vihenge katika eneo la maalum la viwanda la Kanondo.

**********************************

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesifu ujenzi wa vihenge vya kuhifadhia chakula unaoendelea kujengwa katika eneo maalum lililotengwa na Manispaa ya Sumbawanga kwaajili ya uwekezaji wa viwanda pamoja na maghala lililopo Kanondo katika Kata ya Ntendo na hivyo kuwataka wamiliki wengine walionunua viwanja katika eneo hilo kuhakikisha wanawekeza ili kuongeza ajira.

Amesema kuwa ujenzi huo wa vihenge ni mkubwa na unagemewa kutoa ajira mbalimbali na hivyo kuwataka wananchi wa mji wa sumbawanga na maeneo mengi ya Mkoa kutoa kuchangamkia fursa ya ajira katika ujenzi utakaogharimu karibu shilingi bilioni 15 na hivyo kuwataka Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Sumbawanga kuhakikisha wanasimamia vizuri kwa msaada na ushauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania wakihakikisha mkandarasi hafanyi makosa.

“Tulichelewa kuanza huu ujenzi lakini tulitaka huu ujenzi wa vihenge uje katika eneo hili la viwanda la Kanondo, Hii kazi naona mmeanza vizuri pamoja na kuchelewa tangu mwezi wa saba, tunategemea mwezi wa saba mwakani hivi vihenge sita viwe vimekamilika pamoja na ghala lake moja na uwezo wa vihenge pamoja na ghala ni kuhifadhi tani 26,000 na vikikamilika NFRA watakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,500 hii ni mara mbili ya uwezo tulionao sasa hivi, hivyo tunawahamasisha wakulima walime mahindi kwa wingi, uhakika wa soko upo,” Alisisitiza.

Wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo Meneja wa NFRA kanda ya Sumbwanga Abdillah Nyangasa alisema kuwa NFRA wana maghala katika maeneo matatu ndani ya mkoa wa Rukwa moja likiwa Halmasharu ya Wilaya ya Sumbawanga katika mji mdogo wa Laela na mawili yakiwa katika Manispaa ya Sumbawanga katika eneo la Mazwi pamoja na eneo la Kanondo.

“Kwa upande wa Mazwi tuna maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 18,500 ambapo hali yake mengi ni machakavu yanahitaji ukarabati pia mazwi hapo hapo tuna ghala la tani 4000 ambalo nalo ni chakavu na lilitakiwa kufanyiwa ukarabati kama mradi huu ungefanyika pale lakini hapo mazwi kuna maghala mawili ya tani 3000 na kufanya tani 6000 ambayo hayo hayahitaji ukarabati na ndipotulimohifadhia mahindi, lakini kuna ghala la Laela ambalo lina uwezo wa kuhafadhi tani 5000 hili linahitaji ukarabati kidogo kwa ndani, lakini pia kuna mradi huu mpya wa kanondo,” Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisema kuwa Eneo hilo la Viwanda na maghala lina viwanja 103 na viwanja 43 tayari vimeshauzwa na kuongeza kuwa ujio wa ujenzi wa vihenge hivyo utasaidia kuongeza thamani ya eneo hilo kwasababu ilikuwa inaonekana miundombinu bado haijafika lakini kutokana na ujenzi wa vihenge hivyo halmashauri imefanikisha kufikisha umeme na maji katika eneo hilo na kuongeza kuwa Manispaa inamradi mkubwa wa maji unaotarajiwa kusambaza maji katika eneo hilo.

“Tunawaomba wananchi wa Sumbawanga na wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza kwani sasa eneo letu lipo hai na limeanza kufanyiwa kazi, waje wawekeze viwanda mbalimbali, hata wafanyabiashara wetu wa pale mjini lakini mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa kuongeza tunategemea nasi Manispaa kuchukua viwanja viwili ambapo tutajenga sehemu kwaajili ya wafanyabiashara wadogowadogo walipo pale mjini waweze kuhamia hapa,” Alimalizia.

Ujenzi huo wa vihenge vipya vya kisasa unaojengwa na mkandarasi Elerai Construction Company Limited kwa ufadhili wa Serikali ya Poland wenye thamani ya Shilingi bilioni 13.6 unatarajiwa kumalizika mwezi July, 2020 na kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani 33,500 za sasa hadi kufikia tani 59,500 na hivyo kuongeza ununuzi wa zao la mahindi wa NFRA kutoka kwa wakulima.

MKUTANO WA KAMPENI YA CHANJO KWA WATOTO WAFANYIKA ZANZIBAR

0
0
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja.


Mkufunzi Ofisa Mpango wa Chanjo Fat-hia Said Bedui akiwasilisha mada ya Elimu ya Chanjo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja
*********************************

Na Rahma Khamis Maelezo 19/9/2019

Jamii imetakiwa kuwa tayari kuwapeleka watoto kupatiwa Chanjo ya kitaifa dhidi ya maradhi ya Surua Rubella na Polio ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na maradhi hayo. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fadhil Mohammed Abdalla wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Wizara ya Afya .

Amesema kuwa endapo jamii itajitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo hiyo itawakinga na madhara mbalimbali ikiwemo kupoteza baadhi ya viungo na kupelekea ulemavu .

Aidha amefahamisha kuwa kampeni ya chanjo hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini A’ na zoezi hilo litaendelea kwa siku tano hadi tarehe 30 ambapo itawalenga zaidi watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano ambao ndio waathirika zaidi wa maradhi hayo.

Nae Mkufunzi wa Kampeni ya Chanjo ya maradhi ya Surua Rubella na Polio Fathiya Saidi Bedui amesema lengo la kampeni hiyo ni kuzuwia na kupambana na maradhi yanayozuwilika kwa chanjo .

Amesema maradhi ya Surua na Rubella chanjo yake kuanzia miezi 9 hadi miaka mitano ambapo Polio kuanzia miezi 18 hadi 48 hivyo jamii iwapeleke watoto wao katika chanjo hiyo ingawa wameshawahi kupatiwa chanjo hiyo ili kupata chanjo zaidi.

Akifafanua dalili za maradhi ya Surua na Rubella Mkufunzi Fathiya amesema kuwa mtoto kuwa na homa kali kuchuruzika mafua macho kuwa mekundu na kumwaga machozi hivyo akina mama wanapoona hali hiyo wafike katika Vituo vya Afya kwa uchunguzi zaidi.

Wakijibu maswali Mratibu wa Chanjo za mama na mtoto Yussuf Haji Makame na Afisa Mipango wa Chajo Zanzibar Abdulhamid Amour Saleh wamesema iwapo

itatokea kupooza kiungo kwa ghafla cha mtoto kufikisha Hospitali kwa haraka ili kujulikana tatizo.

Wamesema kuwa ugonjwa wa Surua na Rubella hauna chanjo maalum hukingwa na chanjo ya Surua na Rubella hivyo ikitokea mtoto kupata maradhi hayo anatakiwa kupewa chakula na maji ya kutosha .

Wakizungumzia suala la vifaa vya chanjo hiyo wamesema kuwa tayari vimeshakamilika na kusambazwa sehemu husika hivyo wanajamii waachane na dhana potofu na kuwapeleka watoto wao katika chanjo hiyo.

Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella na Polio itashirikisha Hospitali zote za SerIkali na binafsi na sehemu maalum ambazo zimeteuliwa kwa shughuli hiyo.

Waziri Kabudi amuaga balozi wa Rwanda aliyemaliza muda wake

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kinyago cha umoja Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

……………………………………………………………………..

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemuaga Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura, ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi.

Akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Dar es Salaam Prof. Kabudi alimshukuru Balozi Kayihura kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha uwakilishi.

Aidha, Mhe. Waziri alielezea kwamba yapo maeneo ambayo nchi hizi mbili zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu na maeneo mengine Tanzania itaendelea kubadilishana uzoefu na Rwanda ikiwemo huduma za kusambaza madawa maeneo ya vijijini na TEHAMA.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kayihura aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Mhe. Balozi alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na alipongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo. Aliongeza kwamba hatua hizo zimefanikisha idadi ya wafanyabiashara wa Rwanda kutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizogo yao kuongezeka hadi kufika asilimia 98.

VETA kushirikiana na Ujerumani kuwezesha wahitimu kupata ajira

0
0
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia makubaliano na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) kuboresha hali ya upatikanaji wa ajira kwa wahitimu wa Ufundi stadi kupitia mradi  uliopewa jina la Ajira kwa Maendeleo.
Mradi huo unalenga katika kutambua mahitaji ya ujuzi katika viwanda na makampuni mbalimbali yanayowekeza kwenye mikoa ya kusini na kuingiza ujuzi huo katika mafunzo ili hatimaye kutoa wahitimu watakaoajirika kwa urahisi.
Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo Dar es Salaam jana Septemba 17, 2019 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kupitia Chuo cha VETA Lindi ambapo GIZ imeajiri mtaalamu ambaye atatumika kutoa ushauri kwa uongozi wa chuo, walimu na wanafunzi juu ya namna ya kuwezesha wahitimu wa chuo hicho kujipatia ajira mara wanapohitimu.
Alisema ushirikiano huo utaboresha mahusiano kati ya chuo cha VETA Lindi na waajiri ambapo wanafunzi wataweza kupatiwa nafasi za mafunzo kwa vitendo na kufundishwa juu ya mbinu mbalimbali za kuajirika na kujiajiri na hata kuunganishwa na nafasi za kazi katika makampuni mbalimbali.

Naye Msimamizi wa Masuala ya Ufundi Stadi wa GIZ Iris Rotzoll alisema kuwa GIZ imeamua kushirikiana na VETA ili kuwezesha vijana wanaohitimu katika chuo cha VETA Lindi kutumia vizuri fursa za ajira zinazopatikana kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanyika katika mikoa ya kusini mwa Tanzania hususani makampuni ya uzalishaji, uchakataji na usafirishaji wa gesi.




Alisema ushirikiano huo umekuja kutokana na mafanikio yaliyojitokeza chini ya Mradi wa Kuongeza sifa za Kuajiriwa kupitia mafunzo ya Ufundi ujulikanao kama EEVT uliokuwa ukitekelezwa na VETA, VSO Tanzania na Makampuni ya gesi chini ya mwavuli wa LNG kuanzia mwaka 2012 hadi 2018 ambapo jumla ya vijana 1,027 waliwezeshwa kuboresha ujuzi wao kwa viwango vya kimataifa huku wengi wao wakipata ajira kwenye miradi ya Kimataifa inayotekelezwa hapa nchini.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Lindi Mhandisi Cleophas Sikada alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia pia kuboresha utoaji ushauri wa kitaaluma kwa wanafunzi na kuboresha kanzi data ya wahitimu wa ufundi stadi pamoja na waajiri.

Alisema chuo cha VETA Lindi kitashirikiana kwa karibu na mtaalamu huyo ili kuhakikisha kuwa mradi huo unanufaisha walimu, wanafunzi na wahitimu wa chuo hicho.
C:\Users\dtesha\Desktop\ZA KUTUMIA\DSC_0023.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu(wa pili kulia) akipeana mkono na Msimamizi wa Masuala ya Ufundi Stadi wa GIZ Iris Rotzoll(wa pili kushoto) wakati wa kutiliana saini makubaliano ya kuwezesha wahitimu wa VETA kupata ajira. Kulia ni Mwanasheria wa VETA Mathias Kulwa na kushoto ni Afisa wa GIZ Awadh Milasi.

WANAOHARIBU VYANZO VYA MAJI WACHUKULIWE HATUA-SIMBACHAWENE

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibakwe
alipofanya ziara ya kikazi wilayani Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
George Simbachawene akifurahia wimbo wa kwaya iliyoandaliwa ktumbuizamkutano wa hadhara aliyofanya akiwa ziarani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
George Simbachawene akihutubia wananchi jimboni Kibwakwe wilayani
Mpwapwa.
Wananchi wakimkabidhi zawadi ya mbuzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene mara baada yakufanya mkutano wa hadhara jimboni Kibakwe wilayani Mpwapwa.


*******************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
George Simbachawene ameagiza wanaoharibu vyanzo vya maji katika maeneoyenye miinuko waondolewe mara moja na kuchukuliwa hatua kali za sheria.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa
Vijiji vya Chogola na Makosea wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Mpwapwakatika Jimbo la Kibakwe ambapo alikemea tabia ya baadhi ya watu kukata mitikwenye maeneo yenye miinuko hali inayosababisha uharibu wa vyanzo vya maji.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo aliagiza watendaji wa kata navijiji kuweka alama za mipaka kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji yenye umbaliwa urefu wa mita 500 kila upande ili kuhakikisha wananchi hawavivamii.

"Tunapokata miti ya asili tunafanya maisha yetu kuwa magumu na vyanzo vya maji vinategemea uhifadhi wa misitu ya asili, inashangaza watu wanafyeka miti hadi kwenye milima kitakachotokea mvua ikinyesha kwa kasi ule udondounaporomoka na kusababisha mmomonyoko wa udongo mtakuta kijiji chotekinasombwa," alitahadharisha.

Pamoja na hayo Simbachawene alibainisha kuwa changamoto ya mabadiliko yatabianchi imesababisha mabadiliko ya misimu na hivyo kuleta athari kwa
wanadamu kushindwa kuendesha shughuli za kilimo.

Aliongeza kuwa hali hii imechangia kubadilisha misimu na ndio maana wananchiwanalalamuka kukosa mvua za kutosha kuweza kufanya shughuli za kilimo.Akiendelea kutoa elimu kwa wananchi Waziri Simbachawene alisema kitendocha kukata miti kinaharibu ikolojia ya wanyama na mimea hali inayosababishakukosekana kwa mvua na hivyo mabadiliko ya tabianchi.

“Tarehe 23 ya mwezi huu (Septemba), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa
marais wote kujadili namna nchi hizi zimezalisha hewa ya ukaa ambayo tunaitakaboni kutokana na shughuli zetu wenyewe.“Hewa ya ukaa imeongezeka na kutengeneza joto gesi ambalo linatoboa anga la
dunia ambayo ni (ozoni layer) hali husababisha misimu kubadilika na hivyo ndomaana tunakabiliwa na changamoto ya mabadliko ya tabia nchi”. Alisema waziri huyo.

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA

0
0
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Fadhili Mbaga (aliyevaa shati la bluu) akitoa elimu kwa umma kuhusu namna ya uendeshaji wa mashauri kwa baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo leo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kimahakama.
Bi. Elizabeth Sendeu Huber (aliyesimmama nyuma) akiuliza kuhusu suala la uhairishwaji wa kesi na kupendekeza utoaji taarifa mapema juu ya suala hilo, wakati wa utoaji elimu kwa umma, uliofanyika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo. 
Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mganga Magesa, (aliyevaa suti) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa nakala ya hukumu wakati wa utoaji elimu kwa umma mahakamani hapo leo.
Bw. Yusuph Amiri akiuliza jambo wakati wa utoaji elimu kwa umma ukiendelea mahakamani hapo.(Picha na Aziza Muhali-SJMC)

BALOZI WA FALME ZA KIARABU AMUUNGA MKONO RC MAKONDA KAMPENI YA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA KUMPATIA MADAKTARI BINGWA WA MOYO.

0
0
Kampeni ya Matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 10 kila mwezi kwa muda wa miezi Sita kutoka familia duni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda imeendelea kuwa na mafanikio makubwa ambapo Balozi wa Jumuiya ya Falme za Kiarabu UAE Bw.Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amemuunga mkono kwa kuleta madaktari bingwa wa kufanya upasuaji kwa watoto hao.

RC Makonda amesema Balozi huyo ameamua kujitolea Madaktari hao baada ya kuona kipande cha Video kikimuonyesha RC Makonda akiwa yupo kwenye wodi ya watoto wenye matatizo ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya jambo lililomgusa balozi na kuamua kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo.


Aidha RC Makonda amesema kuwa hadi sasa jumla ya watoto 30 kati ya 60 wamefanyiwa upasuaji kwa kipindi cha miezi mitatu huku akitoa wito kwa wananchi na wadau kugusa maisha ya wenye uhitaji kwa kuwafika taasisi ya moyo Jakaya Kikwete na Kujitolea kugharamia upasuaji kwa watoto kwahuwa hadi sasa kuna zaidi ya watoto 500 wenye tatizo la moyo lakini wazazi hawana uwezo wa kumudu ghrama za matibabu.


MAHAKAMA KISUTU YAMHUKUMU MWANASIASA MIAKA 99 JELA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA MAKOSA 17

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,

MWANASIASA Salma Mntambo, amehukumiwa kifungo cha miaka 99 jela  baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka  17 yaliyokuwa yakimkabili yakiwemo ya kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 18,mwak 2019 na  Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mhina amesema, Mahakama kupitia mashahidi watano waliolioletwa na upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo.

 "Nimepitia sababu za upande wa mashtaka na utetezi katika kesi hii na ninamuhukumu mshtakiwa kuwa, katika makosa matatu ya kutoa nyaraka za uongo atatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kila kosa na pia katika makosa 14 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka sita jela kwa kila kosa,"amesema hakimu Mhina.

Hata hivyo Hakimu Mhina amesema adhabu hizo zitaenda pamoja hivyo mshtakiwa  atakaa gerezani kwa miaka sita tu. Pia Mahakama imesema kuhusu suala la fidia atatafakari na kufanya utafiti ili aje kutoa oda ambayo ni sahihi hivyo Oktoba 2, mwaka huu atatoa oda hiyo ya fidia


Katika kesi hiyo, mshtakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na mashtaka 24 hata hivyo ametiwa hatiani katika mashtaka 17 yakiwamo ya kutakatisha fedha jumla ya Sh. 1.027,000,000 kutoka kwa Ridhuan Mringo huku akijua fedha hizo zimetokana na zao la makosa tangulizi ya kugushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za uongo. 

Katika kosa la kugushi,  mshtakiwa Mntambo anadaiwa kati ya June mosi 2003 na Oktoba 31, mwaka 2011 maeneo yasiyojulikana Wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu aligushi risiti yenye namba 001226 ya tarehe 10/06/2003 ili kuonesha kwamba Ridhuan Mringo alinunua nyumba ya Shirika la Nyumba iliyopo Plot namba 710 mtaa wa Mfaume Upanga kwa Sh. Millioni 70 wakati akijua ni uongo. 

ZIARA YA WAZIRI MKUU NGERENGERE MKOANI MOROGORO

0
0
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akikagua darasa, kwenye shule ya sekondari ya Ngerengere, Septemba 18.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ngerengere Petro Tumai, wakati akikagua darasa, kwenye shule hiyo, Septemba 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

ENSULO, PROMISE NI ZAIDI YA MAPINDUZI BONGOMOVIE

0
0
Na Khadija seif, Michuzi TV

WAHITIMU wa mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya Kampuni ya Multichoice talent factory wajipanga kuleta mapinduzi kwenye soko la filamu duniani.

Akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kutambulisha rasmi filamu mbili zilizotengenezwa na wahitimu hao Wilson Nkya amesema wanapongeza uongozi wa Multichoice kwa kuendelea kukuza vipaji vya vijana wenye ndoto za kufanya vitu vikubwa katika sekta ya filamu.

"Mafunzo tuliyotapata yameweza kutupa akili na maarifa jinsi gani tunateweza kutengeneza filamu bora zenye kujenga jamii na kutumia vitu asilia vya kutambulisha utamaduni Kama vile maporomoko ya maji,ngoma za asili na vitu vyenye upekee ,"

Aidha ameeleza pia kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kuandaa filamu mbili Ensulo pamoja na promise ambazo zitarusha hivi karibuni kupitia King'amuzi cha dstv kupitia Maisha magic bongo.

Na pia miongoni mwa wahitimu hao Janet Moshi amesema pamoja na kupatiwa na mafunzo hayo bado wanania ya dhati kubadilisha soko la filamu kuanzia utengenezwaji wa miswada (Script) ,kuongoza filamu pamoja kutengeneza picha jongefu.

" Wasanii na waongozaji (directors) wanatakiwa kujifunza kutengeneza filamu kwa kutumia bajeti ndogo pamoja na kutumia vitu ambavyo vinaweza kueleweka kwa urahisi kwa watazamaji,"

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images