Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TANESCO, REA KUWAUNGANISHIA UMEME KWA ELFU 27 NYANKUMBU

$
0
0
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia), akimkabidhi kifaa cha Umeme Tayari (UMETA), mmoja wa wanakijiji wa Kabeho wilayani Chato, wakati wa hafla ya uwashaji rasmi umeme katika kijiji hicho, Septemba 16, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Shule ya Msingi ya Kabeho, iliyopo wilayani Chato, Septemba 16, 2019.
Na Veronica Simba - Geita
SERIKALI imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuwaunganishia umeme wananchi wa vijiji vyote 11 vya Kata ya Nyankumbu iliyopo Geita mjini, kwa gharama ya shilingi 27,000 tu kuanzia sasa.

Agizo hilo lilitolewa jana, Septemba 16 mwaka huu na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu, akiwa katika ziara ya kazi.

Waziri alisema, awali, Kata hiyo haikuwa katika mpango wa umeme vijijini, ambao wanufaika wake ndiyo huunganishiwa umeme kwa gharama hiyo lakini baada ya serikali kujiridhisha kuwa eneo hilo halina tofauti na maeneo mengi ya vijijini, imeamua nao wapatiwe huduma hiyo kwa gharama inayotozwa vijijini.

Aidha, Waziri aliwaagiza viongozi wa taasisi husika kwa kushirikiana na mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme vijijini, awamu ya tatu, wilayani humo, kuweka magenge 10 katika Kata hiyo na waanze kuunganishia wananchi umeme mara moja.

Hata hivyo, Waziri Kalemani alibainisha kuwa, watakaounganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 katika eneo hilo, ni wale tu wateja wapya na kwamba wale ambao walikwishaunganishiwa awali kwa gharama tofauti, hawatahusika na hawatarejeshewa fedha.

Katika hatua nyingine, Waziri aliendelea kusisitiza agizo lililotolewa na serikali kuwa wananchi vijijini hawapaswi kulipia nguzo wala kifaa kingine chochote isipokuwa gharama za kutandaza mfumo wa nyaya kwenye majengo yao (wiring), ambazo ni makubaliano yao binafsi na wakandarasi watakaowafanyia kazi hiyo.

Alitoa onyo kali kwa yeyote atakayebainika kumwambia mwananchi kulipia nguzo au kumtoza gharama nyingine yoyote zaidi ya shilingi 27,000 tu ambayo ndiyo bei halali iliyotangazwa na serikali kwa ajili ya kuunganishia umeme wananchi wa vijijini.

Katika ziara hiyo, Waziri pia alitembelea kijiji cha Kabeho kilichopo wilayani Chato mkoani humo, ambapo aliwasha rasmi umeme katika Shule ya Msingi ya kijiji hicho.

Aliwataka wanafunzi kuutumia umeme huo kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.

MTOTO WA NAIBU WAZIRI WA ARDHI DAVID NA SANDRA WALIVYOMEREMETA

$
0
0

David Mabula na mke wake Sandra Ndiwu wakiwasili katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe ya kupongezwa baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Kirumba Mwanza mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifurahia jambo na Sandra Ndiwu (Mke wa mtoto wake) wakati wa hafla ya kusheherekea kufunga ndoa takatifu kwa mtoto wake David iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akiwa na mtoto wake David Mabula (wa tatu kushoto) na mkewe Sandra Ndiwu wakisikiliza maelekezo kwa makini wakati wa hafla ya kuwapongeza kufunga ndoa. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta akimvisha Khanga Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt. Mabula aliyefunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akisalimiana na Masajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Stela Tullo wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Tutubi Mangazeni.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (Kushoto) akiongoza watumishi wa Wizara yake kwenda kutoa zawadi wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara yake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
David Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kufunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni watoto wa mhe Dkt Angeline Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora Magreth Sitta akizungumza kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Bendi ya Twanga Pepeta ikitumbuiza wakati wa hafla ya kumpongeza Mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki.
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

BENKI YA CRDB KUWANEEMESHA WAJASIRIAMALI WAMACHINGA WILAYA YA KIGAMBONI, VITAMBULISHO VYA MAGUFULI KUTUMIKA KAMA DHAMANA KUPATA MIKOPO

$
0
0
Benki ya CRDB na Manispaa ya Wilaya ya Kigamboni leo zimeingia mkataba wa makubaliano wa mikopo ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wamachinga na katika wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema Benki ya CRDB ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji mikopo hiyo ijulikanayo kama ‘Machinga Loans’.

“Mikopo hii imegawanyika katika sehemu mbili, kwanza tutakuwa na mikopo kwa mjasiriamali mmachinga mmoja mmoja, lakini pia tutakuwa na mikopo kwa wajasiriamli hawa waliopo kwenye vikundi,” alisema Nsekela.

Nsekela alisema uanzishwaji wa mikopo hiyo unatokana na juhudi za Serikali katika kuwarasimisha wajasiriamali wamachinga zilizofanyawa na Rais wa awamu ya tano Dokta John Magufuli mwishoni mwaka jana 2018 ambapo vitambulisho 1,850,000 vimetolewa.

“Vitambulisho vya wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga vilivyotolewa na Mheshimiwa Raisi Magufuli, vimesaidia kuwarasimisha na hivyo kusaidia sana zoezi la utambuzi, hili ni jambo la muhimu sana ili kuwafanya wawe wanakopeshaka. Kipekee kabisa nimshukuru Mheshimiwa Raisi Magufuli na Serikali nzima ya awamu ya tano kwa kuendelee kutengeneza mazingira rafiki ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo kiuchumi.

Nikupongeze pia Mheshimiwia Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kwa mikakati mizuri mnayoifanya ya uwezeshaji wajasiriamali katika Wilaya hii. Tukiwa Benki ya kizalendo tumevutiwa sana juhudi zenu na ndio maana tumeanza na mpango huu wa uwezeshaji wajasiriamali katika wilaya hii,” alisema Nsekela. Akiongelea namna ya utoaji mikopo hiyo, Nsekela alisema Benki ya CRDB inatumia mfumo wa kidijitali, kupitia huduma yake ya SIMAccount, ambapo mteja atawasilisha maombi ya mkoo kupitia simu yake ya mkononi na kupata mkopo wake ndani ya saa 24.

“Tumefanya hivi ili kuwaondolea wateja mlolongo mrefu wa kupata mkopo, hasa ukizingatia muda mwingi wanautumia katika sehemu zao za biashara,” aliongeza Nsekela.

Nsekela alisema katika utekelezaji wa mpango huo wa uwezeshaji ambao pi utahusisha elimu juu ya masuala ya fedha, uwekezaji, Bima na mikopo, Benki ya CRDB imeanza kwa kuwaunganisha wajasiriamali wamamchinga na huduma ya SimAccount ambapo mpaka sasa wajasiriamali 3,000 katika wilaya ya Kigamboni pekee wameshaunganishwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kuitikia wito uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa kuwawezesha wajasirimali wadogo maarafu kama wamachinga.

“Hii ni fursa ya kipekee sana si tu katika wilaya yetu ya Kigamboni bali kwa Taifa letu kwa ujumla, ni imani yangu wajasiriamali wengi watakwenda kunufaika na mikopo hii pale itakapo sambaa katika wilaya zote nchi nzima,” aliongezea Sara Msafiri.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni alitumia fursa hiyo pia kuwasihi wajasiriamali wamachinga wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kujiunga na SimAccount ya Benki ya CRDB ili waweze kunufaika na mikopo hiyo pale itakapoanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akibadilishana mikataba ya makubaliano wa mikopo ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wamachinga na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Ng'ilabuzu Ludigija, huku ikishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sarah Msafiri (katikati) katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es salaam Septemba 17, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Ng'ilabuzu Ludigija wakisaini mkataba wa makubaliano wa mikopo ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wamachinga wa Kigamboni, huku ikishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sarah Msafiri (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa na kulia ni Mwanasheria wa Manispaa ya Kigamboni, Charles Lawisso.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini baina ya Manispaa ya Kiganmboni na Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es salaam Septemba 17, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini baina ya Benki yake na Manispaa ya Kiganmboni, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es salaam Septemba 17, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri na kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Ng'ilabuzu Ludigija.





Mkemia Mkuu wa Serikali:Uchunguzi wa vinasaba matokeo kupatikana ndani ya Siku 21

$
0
0
 Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKEMIA Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika maabara ya mamlaka hiyo hufanyika ndani ya siku 21 pekee na sio zaidi ya hapo huku gharama ya uchunguzi huo wa vinasaba ikiwa ni shilingi laki moja kwa kila sampuli.

Akizungumza leo wakati akifunga mafunzo  maalumu ya siku mbili kwa waandishi wa habari jijini Dar esSalaam yaliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya majukumu ya mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali (GCLA)

"Ni siku 21 pekee ndizo zinazotumika kuchunguza vinasaba mbalimbali na sio zaidi ya hapo labda itokee janga la dharura kama lile la moto Morogoro  ambalo ilitulazimu kutumia siku kumi usiku na mchana kwa kufuata hatua zote ili kupata vinasaba na kuweza kuwapumzisha wapendwa wetu." Ameeleza  Dkt. Mafumiko.

Aidha Dkt.Mafumiko amesema kuwa mamlaka hiyo ina dawati la malalamiko ambalo lipo wazi wakati wote kuwahudumia wananchi na amesisitiza kuwa huduma zote za kiuchunguzi wa kimaabara kutoka katika mamlaka hiyo zinatoka kwa vibali maalumu kwa kuzingatia sheria na kanuni.

Mkurugenzi wa idara ya sayansi, jinai na vinasaba (DNA), Khadija Mwema amesema kuwa uchunguzi huo hufanywa na makundi mbalimbali kwa kuwahusisha madaktari wenye sifa na waliosajiliwa na kutambulika na Serikali, wakemia wenye sifa na askari wa jeshi la polisi kuanzia ngazi ya Inspekta na hufanywa kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu.

Mwema ameeleza kuwa majukumu ya mamlaka hiyo  yamegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni uchunguzi wa kimaabara wa sampuli na vielelezo mbalimbali, utekelezaji wa sheria tatu ambazo mamlaka hiyo inazisimamia pamoja  na kutoa ushahidi wa kitalaamu kwenye masuala yanayohusu uchunguzi wa kimaabara katika  mahakama mbalimbali nchini.

Mamlaka hiyo ambayo ni maabara ya rufaa ilyoanza mwaka 1895 na kuwekeza zaidi katika mitambo, wataalamu na kuimarisha maabara katika kanda zote sita imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia afya, haki, amani na utulivu kote nchini.

Mwandishi mwandamizi kutoka Michuzi Blog, Chalila Kibuda  kwa niaba ya waandishi ameiomba mamlaka hiyo kuendelea kutoa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo zaidi wa kuandika kwa mapana na kwa weledi kuhusiana na mamlaka hiyo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Mamlaka hiyo imekutana na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali zaidi ya 100 ambao wamepata nafasi ya kufahamu kwa kina zaidi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo.


 Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Bidhaa wa Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Sabanito Mtega akitoa mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya mamlaka hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkrugenzi wa Idara SayansiJinai na Vinasaba wa Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Khadija Mwema akitoa jinsi ya taratibu za kuomba uchunguzi katika maabara ya Mamlaka ya Maaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika  mafunzo ya waandishi wa habari  mamlaka hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugunzi wa Idara ya Usimamizi  wa Kemikali wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo akitoa maalezo kwa waandishi wa habari namna wanavyosimamia kemikali na sheria zinazotumikuingiza nchini kukiwepo na mikataba mbalimbali ya Kemikali katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Sehemu  ya waandishi wa katika mafunzo ya maamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari wakati akifunga mafunzo ya waandishi habari yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Michuzi Media Group (MMG) Chalila Kibuda akitoa neno shukrani kwa niaba ya waandishi walioshiriki mafunzo ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja waandishi katika mafunzo ya waandishi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Makamu wa Rais yakutanisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (katikati) akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT). Kikao hicho kimejadili uratibu wa masuala ya Muungano ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila Wizara na  kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la Bima ya Afya Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano, Sifuni Msangi na Lupi Mwaikambo Mkurugeni Msaidizi Idara ya Muungano. 
 Mariam Silim Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ezekiel Chundu Mchumi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) wakifuatilia maelezo ya Naibu Katibu Mkuu (hayupo pichani) katika Kikao cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Tanzania Bara. Kikao hicho kimefanyika hii leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika hii leo Jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU AAGIZA GARI LA WAGONJWA LIPELEKWE IFAKARA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupeleka gari la kubebea wangonjwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni kilichopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara ili kuwapunguzia wananchi gharama ya kukodi gari kwa sh. 800,000 pale wagonjwa wao wanapopata rufaa.

Wananchi wa Mji wa Ifakara wameiomba  Serikali iwasaidie kuwapatia gari la wagonjwa kwani kitua chao hakina gari na wagonjwa wao wanapopata rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro wanalazimika kukodi gari kutoka hospitali ya Mtakatifu Francis kwa gharama ya sh. 800,000 ambazo baadhi yao wanashindwa kuzimudi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa Mji wa Ifakara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kituo cha mabasi cha mji huo. Amesema iwapo fedha za makusanyo ya mapato ya ndani  katika halmashauri husika zingekuwa zinatumika vizuri kusingekuwa na changamoto  kama hizo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani na Serikali yao. “Nitampigia simu Waziri Ummy (Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) katika mgao ujao alete gari la wagonjwa hapa.”

Pia, Waziri Mkuu ameielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ihakikishe katika mgawo wa ujenzi wa hospitali za wilaya, Halmashauri ya Mji wa Ifakara ipewe kipaumbele kwa sababu eneo hilo ni kubwa na lina watu wengi lakini hakuna hospitali ya wilaya hivyo kusababisha msongamano mkubwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni.

“Nimetembelea mwenyewe kituo cha Afya cha Kibaoni na nimeshuhudia msongamano wa wagonjwa, mgao wa pili wa ujenzi wa hospitali za wilaya Mji wa Ifakara lazima upewe kipaumbele. Suala la huduma za afya ni suala nyeti, hivyo ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.”

Awali, Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Dkt. Happyness Ndosi alisema kituo cha Afya cha Kibaoni kinapokea na kuwahudumia wagonjwa wa  nje 225 hadi 250 kwa siku na wagonjwa wanaolazwa ni kati ya 50 hadi 80 kwa siku. Wakinamama wanaojifungulia kituoni hapo ni 400 kwa mwezi.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazikabili kituo hicho amesema kina upungufu wa watumishi 92, kwani kina jumla ya watumishi 83 huku mahitaji yakiwa ni watumishi 175,  ukosefu wa gari la wagonjwa na pia hakina gari lolote la kutolea huduma zikiwemo za chanjo, na usambazaji, uchakavu kwa baadhi ya majengo kama la wagonjwa wa n je.

Pia, kituo kinakabiliwa na ukosefu wa jengo la kutunzia watoto njiti, watoto wachanga na wale wanaohitaji uangalizi maalumu baada ya kuzaliwa (neonatal unit), ufinyu wa chumba cha kujifungulia pamoja na ukosefu wa mashine ya kutolea dawa za usingizi (anesthesia machine).

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali haitokuwa na msamaha  na watendaji wa halmashauri watakaobainika kutafuna fedha za makusanyo ya mapato ya ndani pamoja na fedha zinazotolewa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao.

“Fedha za mapato ya ndani hazitumiki vizuri watu wanadukua mifumo, wanapaswa watambue kwamba Serikali ipo makini wakati wote. Watumishi wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vya ubadhilifu hatua kali za kinidhami zitachukuliwa dhidi yao. Watumishi wa umma mnatakiwa kutekeleza majukumu yenu kwa weledi.”

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa kujiepusha na  migogoro kwa kuwa ni kunyume na taratibu za kiutumishi. “Haiwezekani viongozi wakagombania zabuni zitokanazo na fedha za kodi za wananchi, kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Serikali itasimamia zabuni zote.”
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019.

Hospitali, Vituo vya Afya na maduka ya madawa kupata mkopo wa hadi Bil 5/-

$
0
0
Hospitali binafsi, zahanati, vituo vya afya, wasambazaji huduma za matibabu kupata mikopo yenye bei nafuu.

Inatarajiwa kuboresha utoaji huduma za afya nchini

BENKI ya NMB imezindua huduma mpya kwa lengo la kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati iliopewa jina la 'NMB Afya loan'

Huduma hii mpya ni matokeo ya ushirikiano kati ya Benki ya NMB na shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF) ambapo NMB itatoa mikopo kuanzia Sh Milioni 2 hadi Bil 5 wakati MCF inatoa dhamana ya asilimia 50 katika mikopo yote.

Wafaidika wa Mkopo wa Afya ni hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati, maduka ya dawa na wasambazaji dawa ili kuwezesha, kuiinua na kuboresha biashara za huduma za afya nchini.

Aidha, Benki ya NMB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kuingia katika ushirikiano kama huo na MCF nia ikiwa kujenga uwezo Sekta ya Afya.

Kwa pamoja NMB na MCF watashirikiana kutekeleza ufadhili wa huduma ya afya, kupanua na kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.

Huduma hii itawawezesha watoa huduma ya afya kupata fedha pamoja na kupata utaalum wa kiufundi, ambao utasaidia kutambua wauzauji na vifaa vya matibabu bora pamoja na upatikanaji wa vifaa vya tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mkuu wateja binafsi, biashara ndogo na za kati Filbert Mponzi alisema, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.

"Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Benki ya NMB leo. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza. Tunaimani huduma hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji mkubwa wa utoaji huduma za afya za bei nafuu, "alisema Mponzi.

Itakumbukwa, Benki ya NMB imepigiwa kura kuwa benki nzuri zaidi nchini kwa miaka saba mfululizo na tuzo za kifahari za kimataifa za Euromoney; vilevile ndio benki inayoongoza katika kufadhili biashara ndogo na za kati kwa sekta mbalimbali.

Mkurugenzi wa MCF Tanzania, Dk. Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha watanzania wengi wapata huduma nafuu za afya na tiba.

"Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi za Kiafrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya.Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa, na tunafurahi kushirikiana na benki bora nchini Tanzania kufanikisha upatikanaji wa mitaji ya biashara nchini,” alisema Dk. Heri Marwa.




Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akimpongeza Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati baada ya kuzindua huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heamed Bunju jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wakubwa na wakati wa benki hiyo, Donatus Richard, Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri Marwa na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Edwina Lupembe




Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heamed Bunju jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizugumza wakati uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam

Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati akizugumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri Marwa akizugumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo


Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano asajili laini

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akijisali laini yake kwa mtandao wa simu ya mkononi kwa njia ya alama za vidole katika banda la Airtel  alipotembelea banda la kampuni hiyo jana wakati wa mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuia za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaohusu  Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya  Hewa unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

UBAGUZI NA KUNYANYAPALIWA BADO NI CHANGAMOTO KWA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI

$
0
0
   Na Khadija seif, Michuzi tv
TUME ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) imesema haitosita kushirikiana na makampuni mengi nchini kutoa elimu ya virusi vya ukimwi (VVU)katika shughuli zote za kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi idara ya habari na Mawasiliano Jumanne Issango wakati wakupokea hundi ya milioni 2 kutoka kwa makamo wa rais wa Kampuni ya startimes Bi.zuhura  amesema tume inajisikia faraja na fahari kuona makampuni mengi yanaunga mkono juhudi mbalimbali za kudhibiti maambukizi ya ukimwi.

"Majukumu ya tume ni kutengeneza sera na Mikakati ya kudhibiti ukimwi,kufuatilia na kutathimini ugonjwa huo,kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa afua za ukimwi pamoja na kusaidia juhudi za kutafuta tiba,"

Hata hivyo Issango amefafanua kuwa utafiti wa viashiria vya virusi vya ukimwi (VVU) wa mwaka 2016 hadi 2017 umebainisha kuwa maambukizi mapya ni makubwa kwa kundi la vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24.

"Tafiti hiyo inaonyesha kuwa wastani wa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) kila mwaka ni 72,000,"

Na pia amesema bado  tume hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo sekta ya elimu ya elimu pamoja na afya wameelekeza nguvu zaidi katika kundi la vijana kwa kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa walio mashuleni,vyuoni na hata walio nje ya mfumo wa elimu.

Vilevile amebainisha changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na unyanyapaajwi na ubaguzi kwa watu wanaoishi virusi vya ukimwi (VVU) pamoja  na jitihada za Serikali za kuhakikisha maambukizi yanapungua ifikapo mwaka 2020.

"Pamoja na changamoto ya unyanyapaajwi pia ipo changamoto nyingine ambayo ni upungufu wa rasilimali fedha pamoja na utegemezi mkubwa wa wahisani ,kwani asilimia 93 ya fedha za utekelezaji wa afua za ukimwi unategemea wafadhili wa nje ya nchi "

Pia ameipongeza serikali kwa kuanzisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti ukimwi (ATF) kwa lengo la kukusanya rasilimali fedha za ndani kwa ajili ya kuimarisha mwitikio wa udhibiti wa ukimwi nchini.
Mkurugenzi idara ya habari na Mawasiliano Jumanne Issango akipokea hundi ya milioni 2 kutoka kwa Makamo wa rais wa Kampuni ya startimes katika kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi(VVU) nchini.

Biteko-Sijaridhika ushirikishwaji Wananchi Migodini

$
0
0
 Sehemu ya Washiriki wa mkutano baina ya wafanya biashara, watoa huduma na Uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita (GGM) mjini Geita.
 Waziri wa Madini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara, watoa huduma na uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita (GGM) mjini Geita.
Waziri wa Madini akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mha. Robert Gabriel baada ya kufungua mkutano wa wafanya biashara, watoa huduma na uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita (GGM) mjini Geita.


Na Issa Mtuwa - Geita
PAMOJA na kuupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) katika masuala ya ulipaji kodi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii (CSR) na kuwa mgodi namba moja nchini kwa utekelezaji wa Sheria za Madini, bado serikali hairidhishwi na namna mgodi huo na mingine inavyowashirikisha wananchi moja kwa moja.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 16 na Waziri wa Madini Doto Biteko mjini Geita kwenye mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali mkoani Geita , wananchi na uongozi wa GGM. Mkutano huo uliokuwa na lengo la kufahamishana fursa za kibiashara na utoaji huduma zilizopo kwenye mgodi wa GGM.

“Naomba niwe mkweli, mgodi wa GGM ni wakwanza hapa nchini katika ulipaji wa kodi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii (CSR) lakini sijaridhishwa na namna ambavyo mgodi unavyo washirikisha wananchi moja kwa moja ili waone umaana wa uwepo wa raslimali hii katika mazingira yao,” alisema Biteko.

Aliongeza kuwa, ni wajibu wa GGM kuwaeleza wananchi fursa zilizopo na namna mgodi unavyowashirikisha ili madini yanapokwisha wananchi wabaki na kumbukumbu ya uwepo wa dhahabu hapa mkoani humo. 

Pia, Waziri Biteko alitaka baada ya mkutano huo kuwe na maazimio yatakayo ratibiwa na kusimamiwa na Mkuu wa Mkoa huku akisisitiza maazimio hayo kueleza namna mgodi huo unavyokwenda mkieleza namna mnavyokwenda kuwahusisha wananchi.

Kwa upande mwingine, Waziri Biteko amekemea vikali vitendo vya udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wanaopewa fursa ya kufanya biashara na migodi na kueleza kwamba, amekuwa akipokea malalmiko ya udanganyifu na wizi kwenye migodi unaofanywa na baadhi ya wasio wema na amewataka kubadilika na kutenda haki ili kuongeza imani ya kuendelea kuwatumia watoa huduma wa ndani.

Waziri Biteko alisema kuanzia sasa Kamishna Msaidizi anaye shugulikia masuala ya Ushiriki wa Nchi na Wananchi katika Sekta ya Madini (Local Content) kutoka ofisi ya Kamishna wa Madini atakuwa anapita kukagua namna utekelezaji wa masuala ya Local content yanavyo tekelezwa na hii sio kwa mgodi wa GGM peke yake bali kwa migodi yote hapa nchini.

Pamoja na kuelezwa kuwa mpaka sasa mgodi wa GGM una asilimia 97 ya wafanyakazi ni wazawa, bado haitakuwa na maana kama maamuzi ya mambo mbalimbali yatakuwa yanasubiri asilimia 3 ya wafanyakazi wanaotoka nje. 

Halikadhalika, Waziri Biteko aliwakumbusha watendaji wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake zote kuhusu agizo alilolitoa akiwa ziarani Mkoani Lindi wiki mbili zilizopita kuendelea kufuatilia yanayojiri kwenye ziara zake hususani viongozi kwani patafika mahali wananchi na wadau watatakiwa kupatiwa majibu ya papohapo ili kuondokana na kero bila kusubiri muda mrefu. Hivyo, alimtaka kila mtendaji kuwa tayari kupokea simu pindi atakapo muhitaji na kutolea majibu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema bado kwenye mgodi wa GGM kuna “figisu figisu” katika kuwapatia ajira wana Geita kwa visingizo mbalimbali na hususan ujuzi wa lugha ya Kiingereza na kuwataka kubadilika katika hilo.

“Kuna figisu figisu ya utoaji wa ajira pale mgodini, moja ya sababu mnasema lugha, hicho Kiingereza sio ndio kinachofanya kazi, hiyo lugha sioni ulazima wake na sio wakati wote watakuwa wanaongea muda mwingi ni wakufanya kazi wakiwa wenyewe hata kisukuma watakuwa wanaimizana kufanya kazi,” alisema Mhandisi Gabrile. 

Naye. Meneja Mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson alisema kama mgodi wamedhamiria kuifanya jamii ya Geita kuwa sehemu ya mgodi na ndiyo sababu tayari wamewisha sainishana mikataba mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Na kuongeza, ni dhamira yao kuiona Geita yenye dhahabu inakuwa na nuru ya dhahabu na wako tayari kushirikiana na jamii na serikali, kutii mamlaka za serikali na kufuata marekebisho yote yaliyofanywa kwenye sheria ya madini na ndio maana wameamua kukutana na wadau ili wajadili masuala yote.

Aidha, Uongozi wa GGM umemshukuru Waziri Biteko na wafanyakazi wote wa wizara kwa ushirikiano wanao upata mara kwa mara kwani wanaifanya kazi yao kuwa rahisi, mara zote wamekuwa wakijadiliana na kukubaliana katika masuala mbalimbali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglo Gold Ashanti Bara la Afrika, Sicelo Ntuli alisema mgodi GGM mwaka 2018 ulitenga bilioni 9.2 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Geita peke yake na wanatarajia kuanza kutekeleza miradi hiyo mwaka wa fedha wa 2019/20.

TUTACHUKUA HATUA DHIDI YA WALA RUSHWA KATIKA WIZARA YA KILIMO – MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akizungumza wakati wa kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi za wizara ya Kilimo wakifatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi kilichoitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhabdisi Mathew Mtigumwe akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo kwa ajili ya kufungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
SERIKALI imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wanaobainika endelea kubainika wakijihusisha na vitendio ovu vya rushwa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 17 Septemba 2019 wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea.

Alisema kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua kukabiliana na wala rushwa hivyo yeyote anayebainika hakutakuwa na huruma badala yake atapelekwa mahakamani.

“Wenyeviti na Wakurugenzi msipoisaidia serikali kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaotoa au kupokea rushwa maana yake na ninyi ni sehemu yaw ala rushwa na kama sio sehemu lazima tuchukue hatua” 

“Nimeyasema haya hadharani sina lengo la kumtishia mtu yeyote katika hili badala yake nimelisema ili hatua zichukuliwe” Alisisitiza Mhe Hasunga

Ni lazima kukumbuka kuwa wajibu mkubwa wa watumishi ni kuhakikisha kuwa dira inafikiwa kwa mujibu wa mkakati uliowekwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo itapimwa katika ammbo makubwa matano, ambayo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na tija katika kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Jambo la pili ni kwa namna gani wizara imewezesha upatikanaji wa fedha za kigeni jambo huku jambo la tatu ikiwa ni kupimwa kuwa kilimo kinakuwa kwa asilimia ngapi na kinachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa.

Jambo la nne alilolitaja Mhe Hasunga ni kuhusu upatikanaji wa malighafi sahihi kwa ajili ya viwanda nchini, huku jambo la tano ikiwa ni kipimo cha idadi ya ajira zitakazokuwa zinapatikana kwenye sekta ya kilimo, huku jambo la sita ikiwa ni namna ushirika utakavyokuwa umeimarika pamoja na usimamizi madhubuti wa ardhi kwa ajili ya kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji.

Mhe Hasunga alisema kuwa endapo maeneo hayo matano yatafanyiwa kazi ipasavyo ni wazi kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kabisa kukibadilisha kilimo kuwa cha kibiashara na sio cha kujikimu.

Alisema kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini itaimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za Serikali za kurasimisha mifumo ya masoko ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu; kwa kuwaunganisha Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.

Amesema kuwa mbali na soko la bidhaa pia kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kielektoniki wa usajili wa wakulima na mfumo wa kielekroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System – ATMIS) utaimarisha makusanyo ya maduhuli na tozo kwa kuhakikisha huduma zote za utoaji vibali, leseni na vyeti unafanyika kielektroniki na pia kudhibiti udanganyifu katika hati na nyaraka za huduma hizo.

TANESCO WAJIPANGA KUMALIZA KABISA TATIZO LA UKATIKAJI UMEME

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi TV,Arusha

Shirika la umeme Tanzania limesema kuwa limejipanga kuhakikisha adi ifikapo mwaka 2025 tatizo la ukatikaji wa umeme mara kwa mara litakuwa limeisha kabisa na wananchi wao watakuwa wamesahau kabisa shida hiyo.

Hayo yamebainishwa na kaimu Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika la umeme (Tanesco )Muhandisi Raimondi seya wakati akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kufunga semina ya kuwajengea uwezo waandisi wa matengenezo,mameneja wa shirika hilo wa mikoa na kanda iliokuwa ikifanyika leo katika ukumbi wa Corridor uliopo ndani ya jiji la Arusha ambapo alisema kuwa nakulikuwa tatizo la kukatika umeme mara kwa mara lakini sasa hivi limepungua kwani wameboresha zaidi katika sehemu mbalimbali na umeme haukatiki tena mara kwa mara.

Alisema kuwa shirika hilo wanataka waendelee kuboresha zaidi kwa viwango vyakimataifa vya umeme ambapo umeme unatakiwa kutokatika kabisa na kama utakatika ukatike mara nne kwa mwaka na mkakati wa kutekeleza hayo umeanza leo katika kikao hicho ambacho wanaamini ni sehemu ya muarubaini wa tatizo hilo ,maana waandisi hawa wametengeneza matatizo na sababu ambazo zinasababisha umeme huu kukatika na wanaanza kuyafanyia kazi.

‘’dhana kamili ya semina hii ni kuhakikisha waandisi hawa wanaa na kuhakikisha moja ya kazi ambayo waandisi hawa watafanya ni kuhakikisha kwamba umeme haukatiki umeme kabisa kwa sababu umeme unavyokatika hata kwa dakika moja ni hasara kubwa sana kwani kwanza kabisa umeme unavyokatika unailetea serikali hasara kwani inakosa pesa,kwa upande wa viwanda vyetu navyo vinapata hasara kwa mfano kiwanda cha kutengeneza plastiki umeme ukikatika gafla kama wanaendelea kuzaliha wanakuwa wameharibu matirio yale waliokuwa wanatengenezea kwa hiyo hii itachangia kufukuza wawekezaji wa viwanda hivyo ndio maana tumekaa tukaaamua kujadli na kuwapa mafunzo ya wiki mbili na tumetoka na makubaliano yakuhakukisha umeme haukatiki ovyo”alisema Seya

Alisema kuwa wanataka kuhakikisha kili mwananchi anapokea na kunufaika na umeme wa uhakika lakini pia katika sera yetu ya Tanzania ya viwanda haiwezi kufanyakazi vizuri kama umeme utakuwa sio wa uhakika ,na pia kama umeme hautakatika mara kwa mara pia tutawavutia wenye viwanda kuja kuwekeza hapa nchini kwetu na wakija kuwekeza serikali yetu itaongeza mapato , na pia ajira zitaungezeka kwa wananchi wetu.

Kwa upande wa muhandisi Mahende Mgaya meneja mwandamizi wa usambazaji wa shirika la umeme Tanzani alisema kuwa alisema wamechukua kumbukumbu za chanzo cha kukatika umeme za kuanzia mwaka 2015 iliopita wakazi chakata na kujua tatizo ninini na baada ya hapo wakatengeneza mkakati ambao wameugawa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza wataangalia tatizo,watalifanyia tatizo na mwisho wataakikisha tatizo limeisha kabisa.

‘lengo letu ninini kwanza tunaanza na kwendana na sera Tanzania na ili tuweze kufikia uchumi wa kati nilazima kwanza tuhakikishe tuna Umeme wa uhakika wakutosha na usio katika katika Mara Kwa Mara tukishakuwa nao tutaweza kupata au kuwavutia wawekezaji wengi kuja kujenga viwanda hapanchini kwetu"alisema Mgaya 

alisema kuwa kama wazungu wameweza kumaliza tatizo la kukatika umeme katika nchi zao na kwa afrika alisema pia nchi ya Misri imeweza kumaliza tatizo hilo wanaamini na nchi yetu ya Tanzania wakisimama imara wanaweza kabisa tatizo hilo ,

alisema kuwa kitu kinachosababisha matatizo ya kukatika umeme kwanza ni miti kuwa karibu na miundo mbinu ya umeme kwa iyo watasafisha njia zote za umeme ,pia watabadilisha nguzo zote ambazo zimeoza na kuweka mpya na kubadilisha viungio au vifaa vyovyote vyakuunganisha umeme ambavyo vimechoka na wanaamini kwa kufanya hivyo tatizo hili la kukatika umeme mara kwa mara litakuwa limeisha kabisa. 
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme (Tanesco ) Muhandisi Raimondi seya akimpatia cheti cha kushiriki semina mmoja wa wafanyakazi wa Tanesco anaetokea mkoani mwanza





Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la upande wa utetezi la kuahirisha ya viongozi wa Chadema

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la upande wa utetezi la kuahirisha  kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na wenzake kwa siku 20.

Pia imesema katika kesi hiyo kumekuwa na migogoro kuanzia kusikilizwa hadi wakati wa kuahirisha.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema kuwa kesi hiyo haiwezi kuendelea kwa siku tatu zilizopangwa kuanzia jana, leo na kesho (Septemba 19,mwaka huu)  kutokana na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi  kwamba mawakili wapo Mahakama Kuu na washitakiwa wawili wamefiwa.

Hakimu Simba amesema anaamini hati za wito zilizotolewa mahakamani hapo ni sahihi na kwa maelezo ya mshitakiwa Peter Msigwa amefiwa na bibi yake mkoani Iringa na John Heche amefiwa na mtoto wa kaka yake Musoma.

Amesema, analazimika kuahirisha kesi hii lakini kwa sababu zilizotolew na upande wa utetezi lakini haridhishwi kuahirisha kesi hiyo kwa siku 20 kwa sababu wakili hajapeleka udhibitisho kwamba mawakili watakuwa busy mpaka Oktoba 7 na 10, mwaka huu kama walivyoomba tuahirishe lakini pia katika kesi hiyo kuna jopo la mawakili wengi.

"Kesi hii imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara na kusababisha mahakama kulalamikiwa kwa kuchelewesha kesi hivyo, ni lazima wahakikishe wanamaliza kesi kwa wakati", amesema Hakimu Simba.

Aidha ameongeza kuwa, migogoro inayotokea imesababisha kesi hiyo ichelewe mpaka sasa pamoja na kwamba ilianza kusikilizwa kwa hakimu mwengine

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa utetezi kuanzia Septemba 24 hadi 27 na Oktoba Mosi na 10 mwaka huu.

Mapema, wakili wa utetezi, Gaston Garubindi alidai mawakili wa utetezi wanaosikiliza kesi hiyo, Peter Kibatala anakesi zingine ahakama Kuu mbele ya Msajili Tiganga na Profesa Abdallah Safari yupo Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga mbele ya Jaji Cyprian Mkeha na Hekima Mwasipu yupo Mahakama Kuu Tanga.

Pia amedai Msigwa na Heche wamefiwa na ndugu zao na wameomba kuondoka mchana wa leo (jana) hivyo, kesi hiyo haiwezi kuendelea na kuomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Oktoba 7 au 10, mwaka huu.

Hata hivyo,  Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai washitakiwa hao wanawakilishwa na mawakili wengi ambao mahakama haijaelezwa wako wapi  endapo mahakama itapendekeza kuahirisha kesi hiyo, lipangwe kwa haraka kwa sababu muda walioomba upande wa utetezi ni mrefu.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

WATU SITA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

WATU sita wakazi wa Jijini  Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kukutwa na meno 413 ya tembo na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni nne.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amewataja wawhitakiwa haoni kuwa ni, Hassan Likwena maarufu Nyoni (39)  na ndugu yake, Bushiri Likwena, Oliver Mchuwa (35), Salama Mshamu (21), Hidary Sharifu maarufu White (44) na Joyce Thomas (33).

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa kati ya Januari Mosi, 2017 na Septemba 3, 2019 katika maeneo  tofauti ya Mtwara, Pwani na Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walishiriki genge la uhalifu.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kupokea vipande 413 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 1,755,000 pamoja na vipande vya meno ya kiboko mawili yenye thamani ya USD 1,500 vyote vikiwa na thamani ya Sh 4,043,463,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Imeendelea kudaiwa kuwa, Septemba 3, mwaka huu maeneo ya Saku Chamazi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao walikutwa na vipande hivyo vya meno ya tembo bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Katika shtaka la tatu, Wakili wa Serikali, Salum Msemo alidai tarehe na maeneo hayo, washitakiwa walikutwa na vipande viwili vya meno ya kiboko yenye thamani ya USD 1,500 sawa na Sh 3,453,000.

Pia imedaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2017 na Septemba 3, mwaka huu washitakiwa walikutwa na vipande 413 vya meno ya tembo na vipande viwili vya meno ya kiboko vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni nne wakati wakijua kwamba kitendo hicho ni kiashiria cha kosa la uwindaji haramu.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchimu hadi Mahakama Kuu au pale watakapopatiwa kibali kutoka kwa DPP. Kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelzi katika shauri hilo bado haujakamilika na waliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. kesi hiyo imeahirishwa hadi hadi Oktoba Mosi mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

UJUMBE WA WAZIRI ANAESHUHULIKIA MASHIRIKA YANAYOMILIKIWA NA SERIKALI YA INDONESIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (wa pili kulia)  leo  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (wa pili kulia)  leo  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (wa pili kulia)  leo  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitambulishwa kwa baadhi ya Viongozi mbali mbali katika ujumbe wa Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno (katikati) ujumbe huo ulipofika  Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika mazungumzo baina ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wa Waziri anayeshuhulikia Mashirika yanayomilikiwa na Serikali ya Indonesia Bibi.Rini M.Soemarno walipokutana  leo  Ikulu Mjini Zanzibar.
[Picha na Ikulu.] 17 Sept 2019. 

SHIRIKISHO LA FILAMU YAANZA MCHAKATO WA KUSAMBAZA RASIMU YA KATIBA YA FILAMU

$
0
0
Rais wa shirikisho la filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifamba akitolea ufafanuzi jinsi rasimu itavyowafikia wadau na watu wote nchini ili kutoa maoni yao na kupatikana kwa katiba itakayowaongoza wasanii kisheria.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Kiagho Kikonzo akizungumza na waandishi wahabari kwenye Mkutano huo uliofanyika ofisi za bodi ya filamu jijini Dar es salaam.

Na Khadija seif, Michuzi TV
BODI ya filamu nchini kwa kushirikiana na shirikisho la filamu nchini (TAFF) watambulisha rasmi mchakato wa kusambaza rasimu ya katiba ya filamu kwa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu.

Akizungumza na waandishi wahabari Kaimu Katibu wa bodi ya filamu Kiago Kilonzo amesema rasimu hiyo ikikamilika itaweza kufanya ya utetezi wa tasnia ya filamu pamoja na wasanii wenyewe.

Bodi inaunga mkono shirikisho la filamu kwa kuanza mchakato huo wakusambaza rasimu ili kufanikisha kupatikana kwa katiba itakayowaongoza wasanii kisheria kwenye kazi za kisanaa.

"Tutaendelea kuunga Mkono juhudi zinazoendelea na shirikisho Hilo kuanzia kusambaza katika kila kona ili kupata usawa wa maoni kutokana na zoezi hilo kufanyika kwa uwazi bila upendeleo,"

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba ameeleza kuwa baraza la sanaa (BASATA) pamoja na bodi ya filamu ndio mihimili mikuu kiutendaji wa kazi za Sanaa.

Aidha Mwakifamba amefafanua zaidi kuwa shirikisho hilo linajivunia kuipigania sera ya filamu tangu 2014 na Serikali imeshatoa ahadi ya kabla kuisha kwa mwaka huu itafanikisha kupatikana kwa katiba .

"Tumeazimia kuwa zoezi hili la ukusanyaji maoni litakua na takribani muda wa mwezi mmoja ikiambatana kusambazwa kwa njia mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii Facebook,magazeti pamoja blogs ,"

Pia Mwakifamba ametoa wito kwa wadau wote wenye nia njema kutoa mawazo yao ili kuujenga umoja huu wenyewe Tasnia ya filamu nchini ili kuijenga tasnia yenye mchango wa kiuchumi kwenda katika uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

DAWASA YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MTAA WA KILUNGULE KATA YA BUNJU

$
0
0
UHUJUMU wa Miundo mbinu unasababisha upotevu wa pesa na kusababisha maeneo mengine isiyokuwa na mtandao wa maji kukosa huduma kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa waaminifu.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendesha ukaguzi wa miundo mbinu katika Mikoa ya  kihuduma Dawasa wakianzia Kawe katika Mtaa wa Kilungule Bunju na kukuta wananchi wakihujumu miundo mbinu ya maji.

Hayo yamesemwa na Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo baada ya kutembelea Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe na kukuta wananchi wakijiunganishia maji kwa wizi.
Amesema, wananchi wamekuwa wanakosesha Mamlaka mapato na kusababisha miundo mbinu mingine kushindwa kujengwa, kusogeza maji kwa wananchi pamoja na kuboresha miundo mbinu mingine.

Zawayo ameeleza kuwa, katika eneo waliloanza kutembelea wamekuta wananchi wamejiunganishia maji kukiwa na mita mbili,  ambapo inayosoma ni moja na nyingine ikiwa haisomi huku wakijaza mabwawa ya maji na kupelekea maji kupotea na kulipa hasara Mamlaka.

“huu ukaguzi ni ili tuweze kuwabaini wale wote wanaohujumu miundo mbinu ya maji ambapo wanasababisha Mamlaka kushindwa kuendeleza miradi mingine, tumekuta wananchi hapa wanatumia maji yanayolipiwa ni kidogo tofauti na yale yasiyolipiwa ambapo wamekuwa wanamwagilia mboha mboga,” amesema Kulumbe

Aidha, amewaomba wananchi kuacha kuhujumu Mamlaka zaidi maji yote wanayotumia yapite kwenye mita zinazotambulika ili Mamlaka isipate  hasara na zaidi wale wote watakaokamatwa kwa makosa ya kujiunganishia maji kiholela watachukuliwa hatua za kisheria na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.

Kwa upande wa  Mtendaji wa Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju, Abdalla Mbupu amesema wananchi waache kutumia maji bila kufuata utaratibu na kusababisha serikali kukosa mapato ili DAWASA waweze kuendelea na uwekezaji wa miundo mbinu ya maji.

“Jambo wanalolifanya DAWASA ni zuri sana, na kinachoonekana ni tatizo na kumekuwa na upotevu wa pesa na wito kwa wananchi ni kuacha hizo tabia wafuate utaratibu na kuacha kutumia maji bila kulipia ikiwemo kumwagilizia maji mbogamboga,”

Mbupu amewasishi wananchi kuacha mara moja kuihujumu na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali ya mtaa au ofisi za DAWASA pindi wanapoona mmoja anatenda kosa la kujiunganishia maji.

Zoezi hilo litakuwa endelevu katika Mikoa 10 ya kihuduma DAWASA ambapo wataendelea na ukaguzi wa maeneo mbalimbali ili kubaini wale wote waliojiunganisia maji kiholela na kusababisha mamlaka hiyo kupata hasara.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo  akionesha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo pamoja na waandishi wa bomba hilo lililounganishwa kinyemela linapoelekea mara baada ya kugundua na kukatwa kwa Bomba la DAWASA.
 Muonekano wa Bomba la DAWASA likiwa limekatwa baada ya kugundulika kwa wizi wa maji ya kujiunganishia kiholela wakati wa Maafisa wa Mamlaka hiyo kufanya ukaguzi wa Miundombinu katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam DAWASA Martin Kulembe(kulia) akionesha Mafundi wa Mamlaka hiyo na waandishi wa habari  moja ya mota iliyokuwa inatumika kuvuta maji ya wizi kutoka kwenye bomba la  DAWASA eneo la  Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo
 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) akiangalia Bomba pamoja na Maji kama ni ya Mamlaka hiyo mara baada ya kukuta kisima hicho wakati wa kufanya ukaguzi wa Miundombinu ya Mamlaka hiyo eneo la Mtaa wa Kilungule Kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo  akionesha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo pamoja na waandishi(hawapo pichani) moja ya tenki la Maji lililokuwa linatumika kutunzia maji ya Wizi kwa ajili ya umwagiliaji wa Mbogamboga katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Mabwawa yaliyokuwa yanatumika kutunzia maji yaliyokuwa yanaibiwa kutoka kwenye bomba la maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
 Bomba la maji lililounganishwa kinyemela  kutoka kwenye bomba la maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) likitoa maji kwenye moja ya Shamba la mbogamboga.

 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakikata maji kwa mmoja wa wezi wa maji mara baada ya kukuta maungio yasiyoeleweka karibu na Mita ya maji ya Mamlaka hiyo leo katika eneo la Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Mashamba yaliyokuwa yaliyaliyokuwa yanamwagiliwa na Maji ya wizi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya ukaguzi wa miundo mbinu ya Mamlaka hiyo katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju jijini Dar es Salaam.
Mtendaji wa Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju, Abdalla Mbupu akizungumza na wandishi wa habari kwa kuwasisitiza wananchi kuacha mara moja kuihujumu na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali ya mtaa au ofisi za DAWASA pindi wanapoona mmoja anatenda kosa la kujiunganishia maji.

SERIKALI YAJA NA MCHAKATO MADHUBUTI WA UPIMAJI VIRUSI VYA UKIMWI BINAFSI

$
0
0
Na Jusline Marci-Arusha.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile amesema serikali ipo katika mchakato wa kuleta mpango madhubuti wa upimaji virusi vya UKIMWI binafsi.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha tathimini juu ya namna ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI Tanzania kilichoandaliwa na Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Jijini Arusha.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa mfumo wa upimaji binafsi unalenga kuwafikia zaidi makundi ambayo yapo kwenye mazingira hatarishi hasa ya vijana wakike na pia kutoa wigo mpana kwa wanaume na kuwapima kwani bado idadi yao ni ndogo ukilinganisha na wanawake.

Aidha amesema serikali katika kuhakikisha inatokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2016 imeweka mkakati uitwao 90, 90,90 yani (asilimia 90 ya watu wanatakiwa wawe wanajitambua hali zao,asilimia 90 waanze kutumia dawa na asilimia 90 kuhakikisha wamefubaza VVU).

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha mkakati huu umeweza kufanya vizuri sana kwa asilimia 90 ya kwanza kufanikiwa kwa asilimia 76,asilimia 90 ya pili kufanikiwa kwa asilimia 98 na asilimia 90 ya tatu imefanikiwa kwa asilimia 80.

Pamoja na hayo amesema serikali itaendelea kuboresha baadhi ya huduma kama vile; kuongeza muda wa uchukuaji dawa za kupungaza makali ya UKIMWI kutoka miezi 3 hadi 6 pamoja na kutoka mafunzo kwa baadhi ya wataalamu wa afya ili kuongeza wigo wa utoaji huduma.

Sambamba na hilo katika kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa na serikali ifikapo 2030 na ugonjwa huo umetokomezwa kabisa na serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi zote za serikali na binafsi zilizojikita katika kutokomeza ugonjwa huo.

Nae makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma ya maendeleo ya jamii Mhe. Juma Nkamia ambapo amezishauri taasisi zote zinazoshughulika na tafiti za mapambano dhidi ya UKIMWI na kuhakikisha zinatumia lugha ya Kiswahili kama lugha kuu ya mawasiliano ili jumbe ziweze kuwafikia walengwa kwa urahisi zaidi na kueleweka.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya bianadamu Profesa Yunus Mgaya, amesema lengo la tafiti mbalimbali zinazofanywa na NIMR ni kuhakikisha zinasaidia malengo mbalimbali ya wizara ya afya na kurekebisha sera kwa manufaa ya nchi kwa ujumla.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Jijini Arusha waliohudhuria mkutano huo

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YAKE,AWALIPIA ADA YA KIDATO CHA TANO NA SITA WANAFUNZI WA KIKE 100

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 17 ametimiza ahadi ya ufadhili wa Masomo kuanzia Kidato cha Tano hadi Sita kwa Watoto wa kike 100 kutoka familia duni waliofaulu masomo ya Sayansi lakini wakashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa Ada ambapo katika ufadhili huo amewalipia Ada na Vifaa ya shule ikiwemo Sare,mabegi, vitabu, madaftari na Nauli.

RC Makonda amesema lengo la ufadhili huo ni kumkomboa mtoto wa Kike kutoka familia duni aweze kupata elimu bora itakayosaidia kubadili maisha ya Familia na mwisho wa siku kuwa na Taifa lenye Wanawake Wanasayansi na Wagunduzi.

Aidha RC Makonda amesema ufadhili huo unaenda sambamba pia na kumuunga Mkono Rais Dkt.John Magufuli alieamua kumkomboa mtoto wa mnyonge kwa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi kidato cha nne na yeye ameamua kupokea kijiti kwa kuwasomesha kidato cha tano na Sita ili wakifika vyuo vikuu wanufaike na Mkopo.

Hata hivyo RC Makonda amesema zoezi hilo litakuwa endelevu kila mwaka ambapo amewahimiza wanafunzi waliobahatika kupata fursa hiyo waitumie vizuri huku akimshukuru Balozi kwa Kumuunga mkono katika kampeni hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amesema ufadhili huo ni Mwendelezo wa Kuunga Mkono juhudi za RC Makonda kwenye kila jambo kwakuwa amekuwa mtu wa kupigania maslahi ya Wananchi anaowaongoza.

MSAMA PROMOSHENI YASITISHA KUFANYA MATAMASHA YAKE KWA MUDA JIJINI DAR,AITUPIA LAWAMA WIZARA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni,Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kusikitiswa kwake na suala zima la kutopewa nafasi kuutumia uwanja wa Taifa kwa ajili ya Tamasha la Pasaka. 
Waandishi wa habari wakimsikiliza Bw Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni wakati akizungumza nao leo ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam.

......................................................

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni ya jijini Dar es salaam inayoandaa matamasha ya muziki wa injili Tamasha la Pasaka na Tamasha la Krismass Bw. Alex Msama amesema anasitisha kwa muda uandaaji wa matamasha hayo katika jiji la Dar es salaam.

Msama amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kunyimwa kibali cha kuutumia uwanja wa Taifa unaomilikiwa na Serikali kwa muda wa miaka mitatu sasa.

"Tangu mwaka 2017-2019  nimekuwa nikiandika barua kwenda wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutmia uwanja huo bila mafanikio,na barua zote ambazo tumekuwa tukiwaandikia hazikuwahi kujibiwa mpaka sasa",alisema Msama

Amesema kuwa Tamasha la Pasaka linachukua zaidi wa watazamaji 45,000 watu ambao ni wengi sana, hivyo maeneo mengine hayawezi kutosheleza zaidi ya uwanja wa Taifa au uwanja wa Uhuru.

Akifafanua kwa ufupi kwa njia simu  Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Wizara hiyo ni pana na ina mambo mengi, Hivyo yeye hana taarifa zozote kuhusiana changamoto hiyo.

Mwakyembe amesema muhusika anaepokea barua zote za Wizara ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo hivyo akawataka Wanahabari kuwasiliana na Katibu Mkuu kupata ufafanuzi zaidi wa jambo hilo.

Michuzi Blog ilipomtafuta Katibu Mkuu kwa njia ya simu yake ya Kiganjani,haikupatikana.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images