Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

TANGA UWASA YATOA UFAFANUZI KUHUSU CHANGAMOTO YA MTANDAO WA MAJI TAKA

$
0
0
 Mafundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) wakiwa kazini kama wanaavyooekana
  Fundi kutoka Idara ya Ufundi Tanga Uwasa Kitengo cha  Maji Taka Sikujua Shabani  wa pili kutoka kulia akionyeshwa kitu na mafundi
 Eneo la barabara ya sita ambapo bomba limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji yamepita mengi na limeshindwa  kuhimili msukumo wa maji.
 Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA)  Mhandisi Rashidi Shaban akizungumza na waandishi wa habari leo


MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA)   wameeleza sababu za uwepo wa changamoto ya mtandao wa majitaka inatokana na  uchakavu wa  mabomba kuwa yamelazwa siku nyingi  na mengi yakiwa ya zege na udongo. 

Changamoto imesababisha uzibaji na utirishaji wa majitaka katika  baadhi ya maeneo ya makazi hivyo kusababisha malalamiko kwa wateja.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo  Mhandisi Rashidi Shabani alisema Tanga Uwasa imejipanga kutatua changamoto  hiyo kwa kufanya ukarabati kwa awamu katika maeneo korofi ili kuondoa kero hiyo.

Changamoto ya mfumo wa majitaka imeonekana katika eneo la barabara ya sita na ishirini ambapo ilisababishwa na kubanjika kwa bomba hilo kutokana na  msukumo mkubwa wa maji hivyo kupelekea mafuriko ya majitaka kwa maeneo  mengine. kuna bomba limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji mengi  kupita na limeshindwa kuhimili msukumo wa maji hayo.

Alisema kwamba tatizo hilo limekutokana na umri wa mabomba hayo yaliyopo  ardhini mengi yamekuwa mabovu na hayawezi kuhimili maji mengi  kunakosababiswa na watu kuongezeka maji yanayopita kwen ye mtandao huo  yamekuwa mengi kulinganisha na uwezo wa kuhimili mabomba hayo kutokana umri  yaliyokwa nayo

Mhandisi Shabani alisema kwenye eneo la barabara ya sita kuna bomba  limeharibika lenyewe kutokana na udhaifu maji yamepita mengi na limeshindwa  kuhimili msukumo wa maji.

“Hivyo sisi kama Tanga UWASA tumejipanga kufanya ukarabati tayari kijiko  kipo eneo la tukio kimeshaanza uchimbaji huku akiwaomba wananchi  wawavumilie ndani ya siku mbili kwenye eneo la barabara kwa sababu ya  kufanyia huo ukarabati”Alisema

Alisema kwamba wanaamini ndani ya siku mbili zijazo takuwa wamemaliza kazi
kubwa eneo hilo

“Lakini pia tutatumia ndani ya siku saba a au nane kukamilisha huduma hii hivyo wananchi wanaotumia barabara hii wapite pembeni kwa sababu hiyo ni  hatari kwa afya zao kutokana na maji taka”Alisema

Naye kwa upande wake fundi kutoka Idara ya Ufundi Tanga UWASA kitengo cha  Maji Taka Sikujua Shabani alisema tatizo lilpotokea mara moja wameanza kazi  kwani maji taka yanapomwagika ni athari kwa wananchi.

Hata hivyo alisema kwamba wameendalea kuwaelimisha wananchi kuwa wavumilivu  kwani wao hivi sasa wanalishughulikia tatizo hilo ili hali yake iweze  kurudi kawaida.

mwisho

ZURA YAWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA GESI YA KUPIKIA (LPG) NI SALAMA KWA MATUMIZI

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Hassan Juma Amour akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu matumizi sahihi na salama ya Gesi ya kupikia huko Ofisi kwake Maisara Zanzibar. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mafunzo kuhusu matumizi sahihi na salama ya Gesi ya kupikia huko Ofisi za ZURA) Maisara Zanzibar.
Picha na Kijakazi Abdalla -Maelezo Zanzibar.


Na Kijakazi Abdalla,Maelezo 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imewahakikishia wananchi kuwa gesi ya kupikia (LPG) ni nishati ambayo inazingatia misingi ya usalama ya kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea wakati wa matumizi.

Akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Maisara Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar Hassan Juma Amour kuhusu matumizi sahihi na salama ya gesi ya kupikia amesema kuwa gesi ya kupikia (LGP) ni nishati rafiki wa mazingira.

Alisema kuwa gesi ya kupikia inapatikana baada ya kusafisha mafuta ghafi hivyo haina madhara kwani sasa watu wengi hupelekea kutumia nishati hiyo na kondokana na matumizi ya kuni ambayo yamekuwa yakiathiri mazingira.

Aidha alisema kuwa gesi husafirishwa na kuhifadhiwa kwenye mitungi kwa sababu ni rahisi kubadilishwa kwa hali ya kumiminika na kuzingatiwa viwango vinavyostahiki.

Hata hivyo Afisa Hassan alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora za gesi ya kupikia imewahakikishia kuwa inafanya ukaguzi kila maduka ambayo yanauza bidhaa hiyo kwa kuhakikisha wanakuwa na mizani iliyohakikiwa na Idara ya Mizani na vipimo Zanzibar.

Pia alisema inahakikisha kuwa mfanyabiashara huyo anakuwa na ujuzi wa kutumia bidhaa hiyo ili kuhakikisha pale linapotokea hitilafu anaweza kukabiliana nazo.Vilevile alisema aliwataka wasambazaji wa gesi ambao wanatumia usafiri kuhakikisha bidhaa hiyo inasafirishwa wima kwani ni hatari kusafirisha mitungi ya gesi ikiwa imelazwa.

“Tusizingatie faida tu tuzingatie usalama wetu kwani bidhaa hiyo ikisafirishwa ikiwa imelala huwa inajigonga gonga na kusababisha gesi kuvuja na kuleta madhara”alisema Hassan.Aidha alisema kuwa mitungi ya gesi inatakiwa kuteremshwa taratibu kutoka kwenye gari na watumiaji amewataka watumie katika sehemu zenye kutoa hewa na muangaza zaidi ili kuepusha madhara.

Ni Muhimu kwa lugha kuwa na kanuni Zake -Dkt. Mwakyembe

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akionyesha kitabu cha Kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza jambo mara baada ya kuzindua kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa bao Bwana Twaha Mohamed (kushoto) katika hafla ya uzinduzi wa kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajasiliamali wa kazi za sanaa za ufundi alipotembelea banda hilo leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange (kulia) alipotembelea banda la uchapishaji wa vitabu la Mkuki (Mkuki Publishers) leo Jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua kanuni za Baraza hilo leo Jijini Arusha.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)

……………………

Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ni muhimu kwa lugha ya Kiswahili kuwa na kanuni ambazo zitasaidia katika kufanikisha mawasiliano kwa jamii ili kuleta maendeleo chanya.

Hayo aliyasema leo Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) lengo ikiwa ni kuwazesha kusimamia matumizi ya lugha.

“Ni muhimu kwa kila lugha kuwa na kanuni na sifa kubwa ya lugha ya Kiswahili ni unyumbulifu, hivyo ninaamini kupitia kanuni hizi tutakuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya lugha hii” Dkt. Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lazima kanuni hizo ziwe nyumbulifu na rafiki ili kuweza kuzifanyia marekebisho endapo kutakuwa na mapungufu yoyote wakati wa utekelezaji wake.

Pia aliwapongeza wataalamu wote kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali walioweza kufanikisha upatikanaji wa kanuni hizo na kuwataka kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kukuza, na kuendeleza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange alilezea kuwa kuzinduliwa kwa kanuni hizo ni mojawapo ya mafanikio makubwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Leo tunaweka historia nzuri katika nchi yetu kwa hatua hii muhimu ya kufanikisha uzinduzi wa kanuni za lugha ya Kiswahili ambazo pia zinatupa fursa ya kuwa na marekebisho kwa kadri zitakavyokuwa zinatekelezwa” Dkt. Sewange.



Historia inaeleza kuwa Baraza la Kiswahili la Taifa liliundwa na sheria ya bunge Na. 27 ya mwaka 1967 kwa shabaha ya kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili nchini na baadaye kufanyiwa marekebisho mwaka 1983 kwa sheria ya Bunge Na. 7 ikiwa imepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili nje ya nchi na baadaye sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho ya mwisho mwaka 2016.

IGP SIRRO APOKEA UWANJA WA MAFUNZO YA ASKARI SHULE YA POLISI MOSHI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro akisalimiana na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili katika Shule ya Polisi Moshi katika hafla ya kupokea Uwanja wa Mafunzo ya Askari uliojengwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akipokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro baada ya kuwasili katika Shule ya Polisi Moshi alipoudhulia hafla ya kupokea Uwanja wa Mafunzo ya Askari uliojengwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye ni mgeni rasmi akiwasili katika ufunfuzi wa Uwanja wa Mafunzo ya Askari katika Shule ya Polisi Moshi na kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro alie mkoni wa kushoto wa mgeni rasim (Picha na Jeshi la Polisi).

MWAKYEMBE ALITAKA BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA NA ZANZIBAR KUKAA PAMOJA KUONDOA TOFAUTI YAO YA LUGHA

$
0
0
Na Jusline Marco-Arusha

Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amelitaka baraza la kiswahili Tanzania na baraza la kswahili Zanzibar kukaa pamoja na kuondoa tofauti ya lugha ya kiswahili iliyopo katika pande zote mbili na kuifanya kuwa na maana moja.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo wakati akifungua Tamasha la Kimataifa la Kiswahili na Utamaduni katika chuo cha MS-TCDC Usa river Wilayani Arumeru Mkoani Arusha nwakutanisha wataalamu na wadau wa lugha ya kiswahili kutoja Zanzibar na Tanzania bara.

Aidha Waziri Mwakyembe amesema lugha ya kiswahili inaweza kutumika katika sekta zote na kuondoa zana potofu iliyopo kwa sasa ya kugeuza lugha hiyo kama sehemu ya masomo kwa wanafunzi na kuipa nafasi kubwa lugha ya kingereza hivyo ni vyema wanafunzi wakafundishwa lugha zote kwani wakizifahamu lugha zote mbili kwa Kiingereza na kiswahili wanaweza kufaulu vizuri katika masomo yao.

Naye katibu mtendaji baraza la kiswahili Zanzibar Mwanahija Juma amesema tofauti ya misamiati katika pande zote mbili zipo kutokana na usanifishaji wa baadhi ya maneno kuwa ya kiutamaduni.

Kwa upande wake Afisa utamaduni wa halmashauri ya Meru Senyaeli Pallangyo amesema kuwa jamii yoyote isiyokuwa na lugha yao utamaduni haupo hivyo lugha ya kiswahili inatumika kama kielelezo cha utaifa kwa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kati kwani ndiyo lugha inayowaonganisha watanzania ili kuondoa ukabila kwasababu karibu asilimia 90 ya watanzania huzungumza kiswahili.

Hata hivyo Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza Nchini Tanzania tangu kusitishwa mnamo mwaka 2007 na linatarajiwa kuhitimishwa kesho huku kauli mbiu ikiwa ni Tukienzi Kiswahili na Utamaduni kama nyenzo muhimu za maendeleo.
 Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na mwalimu wa lugha ya kiswahili katika chuo cha MS-TCDC Joachim Aloyce Kisanji katika Maadhimisho ya Tamasha la  Kimataifa la Kiswahili na Utamaduni lililifanyika Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akitoa nasaha zake mbele ya wataalamu na wadau wa lugha ya kiswahili waliohudhuria katika Tamasha hilo
Baadhi ya wadau wa lugha ya kiswahili wakiguatilia ujumbe unaotolewa na waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Harrison Mwakyembe

VIONGOZI ARUSHA WATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KIKAMILIFU

$
0
0

Na Jusline Marco-Arusha

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ameiagiza sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya kusimamia zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kikamilifu pamoja na kutoa ushirikiano kwa wasimamiza wa uchaguzi wa serikali za mitaa. 

Akizungumza katika zoezi la uapishwaji wa wazimamizi wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu pia ameagiza migogoro iliyopo baina ya wananchi na viongozi itatuliwe na amani idumishwe katika jamii ili kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanyika na kumalizika vyema.

Aidha pamoja na zoezi la uapishwaji kwa watumishi hao bado walikabidhiwa na changamoto ya vifaa vya uchaguzi ambavyo ni Tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, Muongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ramani ya mipaka.

Watumishi ambao wameapishwa chini ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha Mhe. Pendo Mushi ili kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Arusha ni pamoja na Msena Nyamwiling'i Bina Mkuu wa idara ya utumishi na utawala halmashauri ya Jiji la Arusha, Hussein Ramadhan Mgewa Mkuu wa idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Arusha, Pius John Haule Mkuu wa kitengo cha uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Aidha watumishi wengine ni Natang’aduaki Zakayo Mollel Mkuu wa idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Longido, Jonathan Peter Kima Mkuu wa kitengo cha sheria halmashauri ya wilaya ya Meru, Theresia Evarist Kyara, mkuu wa idara ya mipango, takwimu na ufuatiliaji halmashauri ya wilaya ya Monduli na Emmanuel Joseph Mhando Mkuu wa idara ya utawala na utumishi halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.

Sambamba na zoezi la kuapishwa, watumishi hao walikabidhiwa vifaa vya uchaguzi ambavyo ni Tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, Muongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ramani ya mipaka.
Mkuu wa idara ya Utumishi na  Halmashauri ya Jiji la Arusha,Msena Nyamwiling’i Bina, akiapishwa

DAR ES SALAAM YATOA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kitengo cha Afya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, kimeendesha zoezi la utayari kukabiliana na magonjwa mlipuko hususan Ebola ambayo imeendelea kushambulia nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

Zoezi hilo la utayari linafanyika kutokana na Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Kitovu cha Biashara kwa Taifa kwa Wageni wengi kufika kwa ajili ya Biashara hizo. Mikoa Tisa nchini iliyo jirani na nchi hatarishi, imetajwa kuwa kunyemelewa na ugonjwa huo.

Akizungumza na Michuzi TV, Michuzi Blog wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika Hospitali za Amana na Temeke, Mtaalamu wa Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Dkt. Elibariki Mwakapeje amesema zoezi hilo limefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam kutokana na tishio nchi za jirani.

Dkt. Mwakapeje amewapongeza Dar es Salaam kujiandaa vizuri katika zoezi hilo kwa kuandaa mazingira yakukabiliana na ugongwa huo katika maeneo ya vituo vya afya, ametoa wito kwa mikoa mingine nchini kufanya zoezi hilo ili kupima utayari wao katika kupambana na ugonjwa wa Ebola na magonjwa mlipuko.

Mratibu wa Huduma za Dharura na Maafa, Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava amesema Mkoa wa Dar umetoa mafunzo mbalimbali kwa wiki nzima kwa Watumishi wa Afya katika Halmashauri Tano ili wapate uelewa kuhusu ugonjwa huo, amesema elimu inaendelea kutolewa namna yakumfahamu mgonjwa na kuzuia ugonjwa wa Ebola.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Yunus Ngungile amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa huo, amesema Serikali inaimarisha mifumo ya ufuatiliaji ili kujikinga kwa wakati dhidi ya Ugonjwa huo, amesema mapungufu yaliyoonekana katika zoezi hilo yatafanyiwa kazi kuyaboresha na kuimarisha kwa kutoa huduma bora kwa Wagonjwa waliokumbwa na gonjwa hilo Ebola.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Amana, Dkt. Amani Malima amesema wamewapa mafunzo Watumishi wao na Watu wote wamepewa tahadhari ya ugonjwa huo, amesema vifaa kwa ajili ya kujinga vimeandaliwa, pia kutenga maeneo maalum endapo kuna viashiria vya ugonjwa huo, amethibitisha Hospitali ya Amana hakuna Mgonjwa yeyote aliyegundulika kuwa na Ebola.


DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA:

Homa kali ya ghafla, Joto la mwili kupanda, Kutapika, Kutokwa na Damu sehemu zote za mwili, Kuharisha, Historia ya kufanya kazi au kutoka maeneo yaliyokumbwa na tatizo hilo. 
 Wauguzi wa Hospitali ya Temeke wakiendelea na zoezi la utayari kwa Mogonjwa wa Ebola alipofikishwa kituoni hapo kwa matibabu.
 Mmoja wa Wauguzi katika Hospitali ya Amana akimsikiliza Mgonjwa wa Ebola aliyeletwa Kituoni hapo wakati wa  zoezi la utayari kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola.
 Mgonjwa aliyekumbwa na Ebola akishushwa katika Gari maalum la kubebea Wagonjwa (Ambulance).
 Maandalizi yakiwa tayari kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola 
Mratibu wa Huduma za Dharura na Maafa, Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava akizungumzia tahadhari inayotakiwa kuchuliwa dhidi ya Ugonjwa wa Ebola. 
 Mtaalamu wa Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Dkt. Elibariki Mwakapeje akizungumza na Michuzi TV wakati wa zoezi la utayari kupambana na magonjwa mlipuko yakiwemo Ebola.

KITUO CHA AFYA MURIET CHAKABILIWA NA TATIZO LA UHABA WA WAFANYAKAZI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi  Tv,Arusha

Uhaba wa wafanyakazi katika katika kituo Cha afya Cha muriet kilichopo jijini Arusha Bado ni changamoto  kubwa inayoikabili kituo hicho .

Akizungumzia swala hilo mganga mkuu  wa jiji la Arusha Dr Simon Chacha wakati akisoma historia ya kituo hicho mbele ya  katibu mkuu wa ofisi ya Rais (TAMISEMI)mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema kuwa kituo hicho Bado Kina  changamoto ya wafanyakazi  .

Alisema kuwa kituo hicho kina jumla ya wafanyakazi 25 na kuna  uhitaji waambao ni wachache sana na hawatoshi kwani walitakiwa watumishi  52   katika kila  kituo Cha afya .

Chacha ameendelea kusema kuwa katika kituo hicho Bado pia wanauhitaji wa vifaa  vya matibabu ikiwa  baadhi ya vifaa wamevipata kwa kupitia  mfuko wa ndani ya jiji katika mapato pia kwa kuwezeshwa na wawekezaji ikiwa mkuu wa mkoa na wengine.

Alisema kuwa ujenzi wa Kituo hicho kimegarimu kiasi cha shilingi  billion 1 na elfu 59  ambapo halmashauri ilichangia milion 359  na serikali  kuchangia milion 700 ,  huku akibainisha kuwa kituo hicho  kinahudumia mitaa 13  ambayo ina  wakazi wasiopungua  elfu  50  

Aidha alitaja majengo yaliokamilika had I sasa ni pamoja na jengo  ya exray, OPD, maabara, jengo la mama na mtoto  ,upasuaji pamoja na jengo la kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake   katibu mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI mhandisi  Joseph Nyamuhanga alifurahishwa na Kazi iliofanywa alishukuru  halmashauri kwa kununua vifaa vya utendaji kazi katika kituo hicho pia alisema kuwa wao kama serikali watahakikisha wanapata vifaa  pamoja na kuleta watumishi ili waweze kufikia idadi inayotakiwa ili waweze kutoa matibabu mazuri kwa wananchi .

"Tatizo Hilo la uhaba wa wafanyakazi kazi Bado lipo kwenye  vituo afya ,zahanati na hospital   sisi kama serikali tutajitahidi kukamilisha idadi ya watumishi hao inaongezeka napenda kumaliza kwa kuwashukuru wafanyakazi wa kituo hichi   kwa kuendelea kufanya kazi kwa umahiri na kuhakikisha wagonjwa wanavutiwa na huduma yenu " alisema Nyamuhanga

Akizungumza meya wa jiji  kalist Lazaro amesema kuwa anamshukuru Sana katibu mkuu kwa kutembelea kituo hicho ba kuendelea kusema  halimashauri yao itakapokuwa na uwezo hawatasubiri kufanya maendeleo  ili kuwasaidia wananchi wake.

"Tunahitaji kufanya maendeleo Kama halmashauri ili kuipunguzia serikali mzigo napenda kusema Mimi na  mkurugenzi wa jiji tunaendelea kushughulikia miradi ili kuinua maendeleo katika mkoa wetu " Lazaro.
 Picha ikionesha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI mhandisi  Joseph Nyamuhanga akizungumza na Wanahabari wakati wa ziara

Watoto 60 wa Makonda waendelea kuimarika kiafya

$
0
0

 Kati ya watoto 60 wanaosumbuliwa na tatizo la moyo aliojitolea RC Makonda kuwagharamia matibabu yao,Wazaizi wao wamefurahishwa na maendeleo yao, kiasi cha kutoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar,Mh Paul Makonda,kufuatia afya zao kuendelea kuimarika siku hadi siku.

RC Wangabo Ataka Shida ya Maji Namanyere Ifanyiwe kazi Kabla ya 2020

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa maelekezo.

………………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Mamlaka ya Maji Safi Sumbawanga (SUWASA) kukaa na Wizara ya Maji kuona namna ya kuweza kumaliza shida ya maji katika mji mdogo wa Namanyere, Wilayani Nkasi ili wananchi waweze kuepukana na shida hiyo ya muda mrefu na hatimae kuwa na Imani na serikali juu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.

Amesema kuwa awali wananchi waliaminishwa kuwa baada ya upanuzi wa bwawa la mfili shida ya maji ingekuwa imekwisha, lakini matokeo yake baada ya upanuzi huo bado shida ya maji imeendelea kuwepo ambapo sasa kuna mradi wa ujenzi wa matenki mapya ambayo hayatakidhi mahitaji ya maji katika mji huo unaokuwa kwa kasi na hivyo kuwataka kujipanga kumaliza tatizo hilo.

“Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inasema huku kwenye miji mikuu ya wilaya inatakiwa kupata maji kwa asilimia 85, ninyi mtatoa asilimia 46, sasa SUWASA mkae na Wataalamu wa Wizara husika ya Maji muandae utaratibu ukae tayari tayari juu ya namna gani ya kuweza kukimbiza huu mradi, watu wamechoshwa na subiri subiri hata waswahili wanasema ngoja ngoja yaumiza matumbo,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo alipotembelea mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi unaoendelea kujengwa katika mji mdogo wa Namanyere ili kujionea maendeleo ya mradi huo pamoja na kujua changamoto zinazoukabili na hatimae kuona namna ya kuupatia ufumbuzi huku akiwa ameambata na kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa pamoja na wataalamu wengine kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo meneja wa SUWASA Mhandisi Gibon Nzowa alisema kuwa shida inayosababisha mradi huo kutofikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji katika mji huo ni kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wa kuyasambaza maji hayo kwa kilomita 15 lakini maji yalipo katika chanzo yanatosheleza kwa asilimia 85 endapo tatizo la mtandao litatuliwa na kisha kueleza shughuli za mradi huo.

“Kazi zinazotekelezwa ni ununuzi na ufungaji wa pampu mbili za kusukumia maji, ulazaji wa bomba kuu kutoka bwawa la mfili hadi kwenye tenki takriban kilomita 3.7, pia ujenzi wa tenki la lita 500,000 ambalo limeinuliwa kwa mita 12 ili kuwezesha maeneo mengi ya Namanyere kupata maji, ulazaji wa mtandao wa usambazaji maji kwa kilomita 6.5, vile vile katika mradi huu kutakuwa na dira za maji za kuunganishia wateja,” Alimalizia

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda wakati akielezea hatua walizochukua kupambana kumaliza tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika mji wa Namanyere alisema kuwa kama wilaya walikaa na kuandika andiko na kuhitaji Shilingi Bilioni 2.5 na kuliwasilisha wizarani ambapo fedha hiyo ilipunguzwa hadi kufikia shilingi Bilioni 1.5 hali iliyopunguza asilimia ya upatikanaji wa maji katika mji huo.

“Tulitafuta wataalamu wakaandika huu mradi, wakaleta kwangu tukapitia tukaona ni mradi wa Shilingi bilioni 2.5 ambayo hiyo ingetuwezesha kusambaza maji maeneo yote yenye upungufu wa maji katika mji wetu, kwahiyo Waziri alipokuja tulimkabidhi akasema tuwape SUWASA nao baada ya kuipiti walipeleka wizarani ambapo wakapunguza kiwango cha fedha, huu mradi ulikuwa ni wa Bilioni 1.8 lakini Mheshimiwa waziri akasema ipungue hadi kufikia shilingi bilioni 1.5 lakini kama ingekuwa ule mradi wetu wa Shilingi bilioni 2.5 tungekuwa na mtandao wa kilomita 15 kuliko huu wa sasa wa kilomita 6,” alisema.

Mradi huo wa uboreshaji wa huduma ya maji safi katika mji wa Namanyere unatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwaka 2020 na kugharimu shilingi Bilioni 1.58 fedha zinazotolewa na serikali huku ukitarajiwa kuhifadhi maji kutoka lita 350,000 hadi lita 850,000 na kufikia asilimia 46 ya uaptikanaji wa maji katika mji huo.

RAIS MAGUFULI KUFUNGUA MKUTANO WA 21WA WAKUU WA POLISI KUTOKA NCHI ZA MASHARIKI MWA AFRIKA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Michuzi Tv,Arusha

Mkutano wa 21 Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika unatarajia kuanza Septemba 15 mwaka huu Jijini Arusha na utajumuisha wakuu wa polisi kutoka nchi 14.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana Jijini Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi (SACP)David Misime alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika ambapo Rais John Magufuli atafungua mkutano huo Septemba 19 mwaka huu .

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo kutatanguliwa na vikao mbalimbali vya wakuu wa vitengo vya Interpol na Septemba 16/17 kutakuwa na mkutano wa wakurugenzi wa upelelezi (DCI)kutoka nchi 14, pia kutakuwa na kikao cha kamati ndogo cha wataalam wa mafunzo , wataalamu wa sheria na kikao chakujadili unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha Kuzuia na Kupambana na ugaidi

Alisema kauli mbiu  itakuwa ni 'kuimarisha ushirikiano na ubunifu katika kupambana na uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo makosa ya kimtandao,ugaidi'.

Alisema maandalizi ya mkutano huo yapo vizuri chini ya msimamizi wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na jana wamekaa na wataalamu wa Interpol kutoka Kenya ambao wamefanya kikao

Pia watawapeleka wageni wa mkutano huo chuo cha Polisi Moshi kwa ajili ya kuona madarasa mapya na majengo ya hosteli lengo ni kuongeza wanafunzi wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali

Pia watawapeleka Gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kujionea utengenezaji wa viatu vinavyotumiwa na majeshi mbalimbali huku wengine wakuu wa Majeshi ya Polisi wakienda kutembelewa Hifadhi ya Ngorongoro kujionea Utalii uliopo Nchini

Alisema Septemba 20 kutakuwa na kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi hizo na alitoa rai kwa watanzania kuimarisha amani na utulivu 

Mada zitakazojadiliwa ni kuongeza ushirikiano kwa uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo mikakati ya kutoa mafunzo kwa askari wao kwani hivi sasa Sayansi na teknolojia imekuwa pamoja na kuangalia maazimio waliyoyatekeleza katika kikao kilichofanyika mwaka jana nchini Sudani huku Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Sirro akikabidhiwa rasmi uenuenyekiti mkutanor huo

Wajumbe Baraza la Wawakilishi watembelea eneo la kujenga Ofisi za SMZ Dodoma

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa
Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hiyo Mhe. Ali Selemani Ali
akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na viongozi mbalimbali
walipofika katika eneo walilokabidhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano.
Wajumbe wakiangalia ramani ya eneo hilo walilokabidhiwa kutoka kwa mtaalamuwa ardhi.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali yaJamhuri ya Muungano.
Muonekano wa sehemu ya eneo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
watakakalijenga Ofisi zake walilokabidhiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Jijini Dodoma.

**************************

Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wametembelea kiwanja kwa ajili ya kujengwaOfisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika eneo la Mahoma MakuluJijini Dodoma.

Ziara hiyo pia ilihusisha wataalamu kutoka Serikali hiyo na viongozi mbalimbaliakiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Mihayo JumaNhunga ambaye aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwakabidhi pa kiwanja hicho.

Mhe. Nhunga alisema kuwa SMZ inafarijika kupata kiwanja hicho ambacho kinaukubwa wa hekta 30 na kuwa itaanza haraka ujenzi wa izo uhusiano wa pandembili za Muungano utaendelea kuimarika.

Serikali hizi mbili zina uhusiano na ushirikiano mzuri na tunaona namna Serikaliya Jamhuri ya Muungano ilivyojitoa na kutupatia kiwanja hiki na tunaona thamaniya Dodoma sasa tofauti na zamani hivyo tunaanza haraka ujenzi wa ofisi zetu tuhamie hapa, alisema.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ali Selemani Ali wanashukuru kwa kupata ardhi hiyo na kuwa ina thamani kubwa kwa Serikali yaZanzibar hivyo undugu baina ya pande hizo mbili utaendelea kuimarika.

Mhe. Ali aliahidi kuwa kama Kamati wataishauri SMZ kuanzisha ujenzi wa Ofisi za serikali hiyo kwa kasi ili waweze kuhamia na kuanza shughuli zake katika Jijila Dodoma.Akitoa shukrani zake kwa ujumbe huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu waRais Balozi Joseph Sokoine aliyeambatana na wakurugenzi wa Idara yaMuungano aliwakarisha kuanza ujenzi na kuhamia.

Balozi Sokoine alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kutaimarisha Muungano na undugu baina ya wananchi wapande hizo mbili.

“Tunafarijika sana tunapoona mnafika hapa kwenye kiwanja chenu mara kwamara na kuona namna mtakavyoanza ujenzi na kukamilika kwa Ofisi hizi kutaletaushirikiano mzuri baina yetu sote”. Alisema.

MKUU WA MKOA KIGOMA AWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KUTOJINUFAISHA

$
0
0
Na Editha Karlo wa michuzi Tv,Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya ushirika kutoingia katika uongozi huo kwa lengo la kujinufaisha kwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu haraka.

Maganga ameyasema hayo Mkoani hapo, wakati akikabidhi kadi za Mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwa wanachama wa vyama vya ushirika kwenye mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.

Alisema kuwa kuchezea vyama vya ushiriika kwa Tanzania ya sasa ni kama kuchezea umeme kwa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa papo hapo.

“Kuna watu wakiona wamechaguliwa kwenye uongozi wa vyama vya ushirika wanaona kama wamepata ulaji, kumbukeni vyama hivi vilianzishwa na Baba wa Taifa letu marehemu Julius Nyerere sasa Tanzania imeamua kuvifufua, kuvichezea ni kama kuchezea umeme” Alisema Maganga.

Awali akibidhi vitambulisho kwa viongozi wa vyama vya ushirika kwa niaba ya wanachama wao alisema, enzi za nyuma matibabu yalitolewa bure lakini kwa sasa matibabu yanalipiwa hivyo kuwa na kadi ya Bima ya afya unakuwa na uhakika wa matibabu hata kama hauna pesa mfukoni taslimu pale unapougua.

"Kwakweli nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwaajili ya kupata matibabu,ugonjwa unapokuja hauna taarifa unaweza kuugua huna pesa mfukoni lakini kama una kadi ya bima ya afya utakuwa na uhakika wa matibabu na dawa"alisema Maganga

Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Kigoma Benard Katerangabo alisema NHIF imelenga kutoa huduma kwa watanzania wa kawaida ambapo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa Kasimu mwaka jana alizindua utaratibu wa wakulima wanaolima mazao ya kimkakati kama korosho,tumbaku,kahawa na mengine ambao wapo kwenye vyama vya ushirika kujiunga na mfuko wa bima ya afya kupitia ushirika afya.

Alisema wameanza na kundi la vyama vya ushirika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanajihusisha na kilimo cha mazao ya kimkakati nchini wanafikiwa na huduma za mfuko.

Katerangabo alisema kuwa wanachama wa vyama vya ushirika watakapo jiunga na huduma za mfuko na wategemezi wao ambao ni waume, wake, watoto, wazazi pamoja na wakwe nao pia watanufaika na huduma.

Alisema kundi la wakulima ni kubwa ukiangalia Mikoa yote ya Tanzania inayolima mazao kwa kupitia utaratibu waushirika hivyo watanzania walio wengi watafikiwa na huduma za mfuko.

Akizungumzia suala la malalamiko ambayo yamekua yakijitokeza kwa wanachama wa mfuko huo kuhusu kusumbuliwa wakati wa kupatiwa matibabu alisema, mfuko huo umeweka waratibu kila Wilaya kuwa na mratibu ili kuratibu changamoto zinazojitokeza kwa wanachama wao na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Alisema wakulima wa zao la tumbaku kwa Mkoa wa Kigoma wameonyesha muitikio mzuri wa kujiunga na mfuko mpaka sasa jumla ya wanachama 600 wamejiunga na mfuko huo huku wanachama 480 wakikabidhiwa kadi zao anaamini baada ya hapo idadi ya wakulima kujiunga ushirika afya itaongezeka.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi vitambulisho vya bima afya vya ushirika afya mmoja wa viongozi wa wanachama wa ushirika katika mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi vitambulisho vya bima afya vya ushirika afya mmoja wa viongozi wa wanachama wa ushirika katika mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika.
 Wajumbe wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Wajumbe wa mkutano mkuu wa vyama vya ushirika waliohudhuria mkutano mkuu wa jukwaa la maendeleo ya ushirika kwenye ukumbi wa NSSF Kigoma mjini.

MSANII MTANZANIA AISHIYE UINGEREZA SAIDI TUMBA AJIELEZEA YEYE, MUZIKI, SANAA NA UTAMADUNI WA TANZANIA

Dk Mpango awataka viongozi wa Saccos nchini kuwa waadilifu

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleka,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanachama mara baada ya kuzindua hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.



Charles James, Michuzi TV

BENKI Kuu ya Tanzania imetakiwa kufanya utafiti wa Taasisi zote ndogo za kifedha nchini ili kuona kama kweli riba wanazoweka kwenye mikopo zina faida za msingi au zinawaumiza wanachama.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati wa uzinduzi wa ugawaji hati za viwanja vya wanachama wa Taasisi Ndogo ya Fedha ya Hazina Saccos.

Taasisi hiyo inaundwa na wanachama kutoka wizara ya fedha pamoja na watumishi wengine kutoka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na Taasisi zingine za Umma." Niitake Benki Kuu kufanya utafiti huo ili kubaini endapo hizo riba zilizopo kwenye mikopo ambayo wanachama wa Saccos wanapata ni rafiki au zinawaumiza.

" Nafahamu changamoto kubwa kwenye taasisi nyingi ndogo za fedha (Saccos) ni ubadhirifu niwatake viongozi wote wa Hazina na Saccos zote nchini kuwa waadilifu na kulinda maslahi ya wanachama wao," Amesema Dk Mpango.

Waziri Mpango amewataka wanachama watakaopata mikopo ya viwanda hivyo kuhakikisha wanaendeleza viwanja hivyo kwa kujenga nyumba za makazi, za kupangisha na hata majengo ya ofisi.

Ameipongeza Saccos hiyo kwa namna walivyoamua kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kufanya uendelezaji wa Jiji la Dodoma ambalo Rais alilirasimisha kuwa Makao Makuu ya Nchi, Serikali na Chama na kuwaahidi kuwa Balozi wao katika kuitangasa Saccos hiyo.

" Nafurahi kuona hamjagawa viwanja tu mmenda mbali zaidi kwa kugawa hati kwa wanachama. Niwakumbushe Dodoma kuna fursa kubwa kila mmoja wenu azitumie kwa faida yake na Taifa kwa ujumla," Amesema Waziri Mpango.

Nae Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Aliko Mwaitegete amemshukuru Waziri Mpango kwa kukubali kuwa Balozi wao huku akimuahidi kuhakikisha wanakua Taasisi imara yenye kujali maslahi ya wanachama wake ambao wengi ni wa kada za chini.

Amesema wanahudumia watumishi zaidi ya 5000 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Taasisi zingine za Umma." Kazi yetu ni kukusanya michango ya wanachama wetu na kuwagawia mikopo ya bei nafuu. Tayari tumeshapata viwanja 450 ambavyo tutavigawa kwa wanachama wetu muda siyo mrefu, " Amesema Mwaitegete.

Aidha amemshukuru mlezi wa Saccos hiyo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dotto James kwa namna ambavyo amekua akijitoa kuwasimamia katika mambo mbalimbali ikiwemo ushauri wa namna gani wa kujiendesha kisasa lakini pia kwa kuwapa ofisi kwenye majengo ya Wizara ya Fedha.

UZINDUZI WA MAFUNZO YA STADI ZA KAZI KWA VIJANA NA MAADHIMISHO YA MIAKA MIA YA ILO

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vipuri vilivyo chongwa na wanafunzi wa Chuo cha Don Bosco Dodoma, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia dawati lililotengenezwa katika Chuo cha Don Bosco Dodoma, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mfano wa nyumba uliyojengwa na matofali ya kisasa ya kupachika , kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia ramani za nyumba zinazojengwa na matofali ya kisasa ya kupachika , kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019.
Makamu Mkuu wa Shirika la Don Bosco Kanda ya Afrika, Augustine Sellam akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu Mkuu wa Shirika la Don Bosco Kanda ya Afrika, Augustine Sellam akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 wa ILO, uliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akiwasili katika viwanja vya Don Bosco, kwenye uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana na uwekaji wa kumbukumbu ya miaka 100 ya ILO, jijini Dodoma, Septemba 14.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VIJANA ZAIDI YA 46,000 KUNUFAIKA NA MAFUNZO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zaidi ya vijana 46,000 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya stadi za kazi kwa njia ya uanagenzi kupitia taasisi ya Don Bosco Net Tanzaniakatika mwaka huu wa fedha.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 14, 2019) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo na maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kazi Duniani (ILO), katika viwanja vya Donbosco jijini Dodoma.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imeandaa Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini ambayo imelenga kutoa mafunzo ya stadi mbalimbali za kazi kwa vijana wa ngazi mbalimbali za elimu kuanzia wahitimu wa darasa la saba hadi vyuo vikuu.” 

Waziri Mkuu amesema miongoni mwa mafunzo yanayotolewa chini ya programu hiyo ni ya uanagenzi (apprenticeship) ambayo yalianza 2017 na 2018 walihitimu vijana 32,786.

Waziri Mkuu amesema katika awamu ya pili ya mafunzo hayo yaliyozinduliwa leo ambayo yanahusisha jumla ya vijana 5,875kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya ILO. 

Amesema licha ya mafanikio yaliyoonekana katika sekta ya Kazi na Ajira kwa kipindi cha miaka 100 iliyopita, suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni miongoni mwa changamoto inayoikabili dunia, hivyo linahitaji kuwekewa mikakati endelevu kwa miaka 100 ijayo. 

Waziri Mkuu amesema miongoni mwa sababu zinazotajwa kuchangia ukosefu wa ajira kwa vijana ni vijana kutokuwa na ujuzi sahihi wa kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika sekta mbalimbali za kiuchumi. 

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema hadi kufikia Juni 2019 jumla ya vijana 36,726 wamefaidika na programu ya kukuza ujuzi inayogharamiwa na Serikali wa asilimia 100.

Amesema kati yao vijana 6,455 walinufaika na mafunzo ya uanagenzi katika fani mbalimbali zikiwemo za ushonaji na nguo, useremara, uashi, terazo, uchongaji wa vipuri, ufundi magari, umeme na utengenezaji wa viatu vya ngozi.

Waziri huyo amesema mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo yametolewa kwa vijana 10,443 katika fani za uashi, useremara, ufundi wa magari, upishi na huduma za hoteli.

Pia, Waziri Jenista amesema kwa upande wa mafunzo ya kilimo cha kisasa jumla ya vijana 18,800 walinufaika na mafunzo hayo huku vijana wengine 1,028 walipatiwa mafunzo ya vitendo pahala pa kazi.

Naye, Mratibu wa Miradi wa Taasisi ya Donbosco Tanzania, Rosemary Terry Njoki amesema programu ya kukuza ujuzi imezingatia kuwawezesha vijana wa miaka kati 17 hadi 35 kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.



Amesema mafunzo hayo yataliwezesha Taifa kufikia lengo lake ya kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa yatakuwa yameongeza wafanyakazi wenye ujuzi ambao wanahitajika kwa wingi.

Awali, Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Wellington Chibebe amesema shirika hilo limedhamiria kupigania haki ya kijamii pamoja na haki za binadamu na kazi zinazotambulika kimataifa.

Amesema tangu mwaka 1919, ILO ni shirika pekee la Umoja wa Mataifa lenye mfumo wa utatu unaowaleta pamoja wafanyakazi, waajiri na Serikali katika nchi 187 wanachama wa shirika hilo katika kuweka viwango vya masuala ya kazi, kukuza sera na kupanga programu za zinazochagiza kazi zenye staha kwa watu wa jinsia zote.

“Maadhimisho ya karne moja ya ILO ni fursa nzuri ya kujitathimini wapi lilipotoka, kusheherekea historia na mafanikio yake na pia kutafakari siku zijazo. Pia ni jukwaa la kipekee la kuihakikishia dunia umuhimu wa jukumu na mamlaka yake ya kutetea haki ya kijamii na ajenda ya kazi zenye staha”

Baada ya uzinduzi huo, Waziri Mkuu alishiriki shughuli ya kupanda jumla ya miti 200 katika Mji wa Serikali, Mtumba kuashiria miaka 100 ya ILO iliyopita na miaka 100 ijayo. 

WAZIRI UMMY: HAKUNA MGONJWA ALIYETHIBITISHWA KUWA NA EBOLA NCHINI

$
0
0
Na Eric Msuya – MAELEZO 
Siku chache baada ya kutokea kwa Uvumi wa kuwepo kwa Ugonjwa wa Ebola Nchini, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Waziri wake Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wananchi wa Tanzania kutokuwa na hofu ya Ugonjwa huo kwani hakuna dalili wala Mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mhe. Ummy Mwalimu amewahakikishia Wananchi, kuwa tangu kuripotiwa kwa Ugonjwa huo wa Ebola Nchi jirani, Serikali ya Tanzania imeweka mikakati mbalimbali ya kulinda Afya za Watanzania. 

“Tumeimarisha utaratibu na ufuatiliaji wa Ugonjwa huu wa Ebola kupitia wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na kuimarisha Uchunguzi wa Wageni wanaoingia Nchini kupitia mipaka yetu ya Tanzania” Alisema Mhe. Ummy Mwalimu 

Sambamba na hilo Serikali kupitia Wizara ya Afya imenunua Vipima Joto vya Mkono na Mavazi kinga (PPE) seti 2,670 na kusambaza katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Rukwa na Katavi kutokana na kuwepo kwa hatari ya kukumbwa na Ugonjwa huo. 

Wizara ya Afya inaendelea kuandaa mpango mkakati wa kutengeneza Kitini na kutoa Elimu na Mafunzo ya kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kupitia Waganga Wakuu wa Mikoa yote nchini pamoja na Watumishi 724 wa sekta ya Afya na Ngazi ya Jamii. 

“Tumeanda Kitini chenye maelezo muhimu ya jinsi ya kukabiliana na Ugonjwa huu wa Ebola ikiwa sambamba na kutoa Elimu kupitia Vyombo vya Habari kwenye vitu mbalimbali kama vile Makala fupi zinazotolewa na Waandishi wa Habari kwa kuandaliwa na Wizara ya Afya” Alisema Ummy Mwalimu 

Aliongeza kuwa Wizara imetoa Mafunzo juu ya kujikinga na Ugonjwa wa Ebola kwa Watumishi wa Afya zaidi ya 460 na Ngazi ya Jamii zaidi ya 264, wakiwemo Viongozi wa Dini, Wanahabari, Vijana wa Bodaboda pamoja na Watendaji wa Vijiji walio katika Mikoa iliyo hatarini. 

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga uwezo na kununua Vifaa Tiba katika Maabara Kuu ya Taifa Jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya pamoja na Kituo cha Utafiti wa Magonjwa wa Tiba (KCRI) kilichopo katika Hospitali ya KCMC Mjini Moshi. 

Waziri Ummy amewataka Wananchi kutopuuzia Dalili zozote zitakazo tokea kwenye Miili yao kwa kufika katika kituo cha Afya sababu Ugonjwa wa Ebola hauna tofauti na Dalili za Homa na Maralia 

“Dalili kuu za ugonjwa wa Ebola ni Homa kali, kuumwa na kichwa, kutapika na kuharisha, viungo vya mwili kuuma, kutokwa na Vipele Mwilini na Damu katika Matundu ya Mwili” Alisema Ummy Mwalimu. 

Wizara ya Afya imewataka Wanachi katika Mikoa yote Tanzania kujikinga na kudhibiti Ugonjwa huu usiingie Nchini kwa kuepuka kugusa Damu, Mkojo, Jasho, Kinyesi, kunawa Mikono kupitia maji ya nayotiririka na kuepeuka Majimaji yanayotoka mwilini mwa mgonjwa mwenye Dalili za Ebola. 

“Lakini pia tuna namba za simu Bure ambazo tumekuwa tukizisambaza kwa Wananchi ambazo ni 0800110124 au 0800110125 hivyo wananchi watoa taarifa endapo akiziona dalili za ugonjwa wa Ebola” Alisema Ummy Mwalimu 

Aidha, Waziri Ummy amewataka Wananchi wasidanganyike na kuepuka kusikiliza Habari za Uvumi wa Ugonjwa huo kutoka kwa Watu Mbalimbali wenyenia Ovu kwa Watanzania hivyo chombo pekee chenye kuweza kutoa taarifa za Magonjwa ya milipuko ni Wizara ya Afya. 

“Kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya Mwaka 2009, dhamana ya kutoa Taarifa za Magonjwa ya milipuko ukiwemo huu wa Ebola ni Wizara yenye dhamana na Masuala ya Afya, hivyo kwa sasa hakuna Ugonjwa wa Ebola Nchini.” Alisisitiza Ummy Mwalimu

Pichani kushoto ni Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar

RAIS WA ZANZIBAR.DK. SHEIN AHUTUBIA HAFLA YA KUSHEREHEKEA MAFANIKIO YA SUZA TOKA KUAZISHWA KWAKE

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Cheti cha Utambuzi na Uthibati, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma kushoto kwa Rais, anayefuata ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa Mhe.Said Bakari Jecha na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kulia kwa Rais Makamu Mkuu wa SUZA Dk. Zakia Mohammed Abubakar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Skuli na Taasisi Mpya za SUZA, wakati wa hafla ya sherehe za Mafanikio ya SUZA toka kuazishwa kwake Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu SUZA. Wilaya yac Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Profesa Saleh Idrisa Muhammed, aliyekuwa Makamu Mkuu wa SUZA wa kwanza, kilipoazishwa kwake Zanzibar, wakati wa hafla ya kusherehekea Mafanikio ya SUZA toka kuazishwa kwake Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, SUZA Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Mhe. Haroun Ali Suleiman , aliyekuwa Waziri wa Kwanza wa Elimu wakati kikiazishwa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, (SUZA) (Picha na Ikulu

SEKTA YA UVUVI YAJA NA MIKAKATI YA KUONGEZAUZALISHAJI WA SAMAKI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao kazi cha wahariri , waandishi habari na watendaji wa Wizara katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Viumbe Hai wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt.Nazael Madalla akitoa maelezo hali ya sekta ya uvuvi nchini na hatua za serikali kuendeleza sekta hiyo.
Mkuruenzi wa Idara ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Magese Bulayi akitoa maada wakati wa kikao kazi cha wahariri , waandishi habari na watendaji wa Wizara katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waamdishi wa habari na wahariri katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah akiwa picha ya pamoja na watendaji, wahariri waandishi mara baada ya kuhitimisha kikao kazi.



Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema kuwa idadi ya samaki waliopo nchini haitoshelezi kulingana na idadi ya Watanzania ambayo inazidi kuongezeka kila na kushindwa kila mtu kula wastani wa kilogram 14 kwa mwaka .

Kwa mujibu wa Wizara hiyo kiasi cha samaki kinachozalishwa kwa mwaka ni tani 350,000 hadi 400,000 huku mahitaji ni tani 700,000 hali hiyo imesababisha kushuka kwa kiasi cha samaki kiliwacho kwa kila mtu kwa mwaka, kutoka kilo 14 mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi kilo Nane (8) kwa mwaka 2019.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah wakati akifungua kikao kazi cha Wataalamu wa Sekta ya Uvuvi na wahariri wa Vyombo vya habari nchini ikiwa ni kutoa mwelekeo wa sekta ya uvuvi nchini.

Dk. Tamatamah amesema kiasi cha samaki wavuliwao kuanzia miaka ya 90 hadi sasa, kimebakia kuwa ni kati ya tani 350,000 na 400,000 kwa mwaka huku idadi ya watu ikiongezeka kutoka takribani watu milioni 25 hadi kufikia milioni 55.

“Hali hii inatishia ustawi wa taifa kwa vile samaki huchangia asilimia 30 ya protini itokanayo na wanyama na asilimia 1.7 ya pato la Taifa. Vilevile inachangia katika ajira na kipato ambapo zaidi ya watu milioni 4 wameajiriwa au kujiajiri katika shughuli zinazotegemea uwepo wa samaki,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa taarifa za utafiti zilizofanyika katika vipindi tofauti, kiasi cha samaki kilichopo katika maji yetu ni tani 2,803,000 ambapo mchanganuo wa kiasi unajumuisha tani 2,210,000 katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika Tani 295,000 na Ziwa Nyasa tani 168,000.

Alisema maji madogo (maziwa madogo na ya kati, mito na mabwawa) tani 30,000 na Maji ya Kitaifa ya Bahari ya Hindi tani 100,000.

Pia alisema katika mwaka 2018/19 kulikuwa na jumla ya wavuvi 202,053 nchini walioshiriki moja kwa moja kwenye shughuli za uvuvi kwa kutumia vyombo vya uvuvi 58,930.

“Nguvu hii ya uvuvi iliwezesha kuvunwa kwa tani 448,468 zenye thamani ya Sh. Trilioni 2.11 sawa na ongezeko la asilimia 15.72 ya samaki (tani 387,543) zilivunwa mwaka 2017/18. Ongezeko hili limetokana na juhudi za Wizara katika kudhibiti uvuvi haramu nchini,” alisema.

Vilevile, alisema katika mwaka 2018/19 jumla ya tani 51,718.83 za mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 81,373 wenye thamani ya Sh.Bilioni 691.88 waliuzwa nje ya Nchi.

Aidha alisema katika kukabiliana na upungufu huo, serikali iliamua kuhamasisha uwekezaji katika tasnia ya ukuzaji viumbe maji, pamoja na kuanzisha idara ya ukuzaji viumbe maji kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza tasnia ili kuongeza uzalishaji wa samaki na viumbe maji wengine.

Pia Wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo(FETA) kwa kushirikiana na NORGES VEL (Asasi isiyo ya kiserikali ya nchini Norway) na chama cha Wakuzaji Viumbe Maji Nchini(AAT) ilipata ufadhili wa Sh. Bilioni 4.6 kutoka Shirika la Misaada la nchini Norway(NORAD) kutekeleza mradi wa uzalishaji wa samaki aina ya Sato na kufundisha Stadi za Ufugaji na Biashara.

Aliongeza kuwa, Wizara inaendelea na juhudi za kufufua lililokuwa Shirika la Uvuvi Tanzania(TAFICO) ili kuimarisha uwekezaji katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari, na Bahari Kuu ambapo Menejimenti ya kusimamia ufufuaji wa TAFICO ilizinduliwa Julai, 2018.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images