Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 310 | 311 | (Page 312) | 313 | 314 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Habari Kaka Michuzi, 
  Swali langu ni fupi tu, Hivi unapotuma kajimzigo chako kutoka ulaya kisichokuwa na thamani yoyote Main destination ni Zanzibar lakini unaambiwa uende ukagomboe mwenyewe JNU Airport ni maana yake nini?

  Mara ya tatu natuma kwa njia ya UPS courier mzigo unafikia Dar es Salaam agent wa UPS anakwambia ukitaka mzigo ukomboe mwenyewe safiri uje Dar es Salaam ulipe Document hand-over fees Tsh.55,000/ uende mwenyewe Airport au 

  Lipa Tsh.90,000/- ya agent wa UPS na hatujui Malipo ya TRA na vile vile hatujui muda gani inaweza kuchukua mwezi au miwili 

  Mzigo wangu tokea tarehe 12 December umewasili Dar es Salaam hadi hii leo haujapatiwa ufumbuzi na kumbuka hii ni DOOR TO DOOR service SIO DOOR TO AIRPOT 
  Ndani ya mzigo kuna 

  Audio Mixer ambayo haina thamani yoyote clearance ya kazini tu nimeona niitume Tennis table bat 1 na mipira ya mazoezi (£10.00 nimenunua ebay)  

  jumla mzigo hata thamani ya £100 haufiki lakini imeshakuwa big deal 
  sasa je kama huu mzigo unaenda ZANZIBAR kwani ni usifanyiwe Clearance ZNZ wakati pia ipo TRA kule? hadi mtu aende Dar es Salaam hivi hii ni haki?

  Na hizi fee za hawa UPS hii ni haki mbona unapo book mzigo huambiwi kama utahitaji kulipa fee ya agent au ya kupewa document?

  Wenye data naomba ufafanuzi au opinion zaidi nimeshalalamika UPS UK na wao wanasema wanasubiri info kutoka TZ kila nikiwapigia hapa Ila hadi hii leo ni 12 days sasa hakuna info yoyote....

  Thanks na nawatakia sikukuu njema

  0 0

  Ndugu Joseph Rugumnyamheto wa Mbezi Beach Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha mke wake mpendwa ALICE KIDERE RUNGUMYAMHETO kilichotokea Tarehe Jana 25.12.2013. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam.
  Tutaendelea kutoa updates za msiba huu mara kwa mara.

  0 0

  Mtalii  akimsaidia kijana huyu wa shule ya vidudu kufunga nyuzi za viatu katika eneo la Mji Mkongwe  Picha na Sabry Juma


  0 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Rasimu ya Mahakama ya Kadhi imekamilika na inatazamiwa kuwasilishwa katika ngazi za makatibu wakuu kabla ya kufikishwa  kwenye Baraza la Mapinduzi.


  Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakary, amesema kuwa Rasimu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na makundi ya watu wakiwamo wanaharakati baada ya kupata baraka za Baraza la Mapinduzi itawasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi mwakani.

  Alisema Rasimu hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuboresha mfumo wa kuendesha Mahakama za Kadhi ili uwe na ufanisi na
  kutatua migogoro ikiwamo ya ndoa kwa Waislamu.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mdungi Ussi, amesema  Rasimu hiyo ina lengo la kuimarisha na kuweka mfumo mzuri wa kuendesha mahakama za kadhi nchini.

  Alisema kwa muda mrefu yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu muundo wa Mahakama ya Kadhi na utaratibu wa kuendesha kesi na kutoa uamuzi: "Rasimu ya Mahakama ya Kadhi kwa kiasi kikubwa itaondoa malalamiko yaliyokuwapo awali ikiwamo wanaume kutelekeza wake na matunzo ya watoto," alisema.

  Miongoni mwa mambo ambayo yalijadiliwa kwa kina likiwamo suala la wanawake kupata mgawo wa mali  wanapoachwa na waume zao na suala la matunzo ya watoto, ambapo kwa kawaida mwanamke anapopewa talaka huachiwa malezi ya watoto.
  Kwa mujibu wa utafiti lipo wimbi kubwa la talaka na tatizo la wanawake kutelekezwa na waume zao  na watoto.

  Katika mkoa wa Kaskazini Unguja mwaka 2012/13 talaka 53 zilitolewa huku wanawake wakitelekezwa na waume zao na watoto kwa mujibu wa karani ya Mahakama ya Kadhi Mkokotoni, Asma Francis.

  Aidha, kesi 10 za wanawake kutelekezwa na kudai matunzo ya watoto zilifikishwa katika Mahakama ya Kadhi ili kupata ufumbuzi huku wanaume wawili wakikubali kutoa fedha za matunzo ya watoto.


  0 0

   Umati wa watu kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar,wakiwa wamefurika kwa wingi katika eneo la ufukwe wa Coco Beach kwa ajili ya kupunga upepo na kuendelea kuisherehekea sikukuu ya Krismas.Coco Beach ndio eneo pekee linaloweza kuwakutanisha watu mbali mbali hasa wale wa hali ya kawaida kama kina sie na kutufanya tuzisherehekee sikukuu mbali mbali kwa furaha zote.
   Kijani kikiwa kimetawala kwenye Ufukwe wa Coco.
  Hivi ndio mambo yalivyokuwa katika Ufukwe wa Coco leo. 
   Hii ndio raha ya Beach,hata kama hujui kuogelea kama mie basi utachezea maji namna hii. 


  0 0


  0 0
 • 12/26/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Mzee mzima George Benson aliturusha na 'Give Me The Night'

  0 0

  DSC_1678
  Chief Judge wa Shindano la vipaji vya watoto na vijana wadogo la “MO Kids Got Talent”, Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki walioingia semi finals za shindano hilo linalofanyika kwenye hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza kuu.
  DSC_1706
  Pichani juu na chini ni baadhi ya kati ya watoto 15 wakionyesha vipaji vyao kwenye semi finals za shindano la kusaka vipaji kwa watoto na vijana la "MO Kids Got Talent" lililoandaliwa na Kampuni ya Frost Africa na kudhaminiwa na kampuni ya MeTL Group, ambapo leo jioni kutafanyika fainali za mashindano hayo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar na mshindi kujinyakulia fedha taslim shilingi Milioni 5 za Kitanzania.
  DSC_1745DSC_1789
  Sehemu ya watoto wakisubiria kuingia kwenye chumba maalum kuonyesha vipaji vyao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Mkurugenzi wa Doricas Aide International - Tawi la Tanzania, Bi. Stella Sozigwa(kushoto) akikabidhi Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa Waliopo Magerezani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kupokea Misaada ya Kibinadamu kwa Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New Life In Christ" leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga - Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
  Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wa Gereza Kuu Karanga - Moshi wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati wa Makabidhiano ya Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya "New life In Christ".
  Aina mbalimbali ya Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo Magerezani na Asasi ya "New Life In Christ". Hafla ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya "New Life In Christ" mara baada ya kupokea Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani (wa tatu kulia) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas Aide International - Tawi la Tanzania, Bi. Stella Sozigwa(wa tatu kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Hamis Nkubasi na wa kwanza kulia ni Mratibu wa Huduma za Magereza toka Asasi ya "New Life In Christ", Bw. Charles Shang'aa.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0
 • 12/27/13--01:23: APPRECIATION

 • The family of The Late Mr. D.S Mashiku would like to take this opportunity to express our deepest and heartfelt gratitude for the love, care and support you have provided throughout the difficult and emotional events of the funeral and burial of our beloved dad.

  Special thanks goes to Mosinyorre Deogratius Mbiku, Fr.Cosmas Mogella, St Don Bosco & Augustino Choir, Jumuiya ya Mt.Augustino na Monica for their spiritual support and service during his sickness and at the burial service of our beloved baba.

  We would like to direct our sincere appreciation to all of you for the pronounced involvement, our special thanks goes out to all friends and neighbours, the entire management and staff of NMB, TIB, VODACOM, UTT, PPF and Aga Khan Hospital for their tireless efforts to save his life, evidently everyone touched our hearts in a very profound way.

  As it is not possible to mention everyone, the entire family would like to take this very moment and extend our heartfelt appreciation to each one of you for the support and the great love that was expressed throughout the trying times.

  Dec 30th 2013 marks the 40th day of his passing. Please join us during the night of prayers on Dec 31st into the New Year Jan 1st 2014 followed by an appreciation holly mass service and lunch from 1300hrs onwards. Please join us celebrating his beautiful life at his residence in Mapinga on both days.

  May baba, babu, uncle soul Rest in Peace. Amen.

  0 0


  0 0

   Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo (kushoto), akisoma nakala ya kwanza ya gazeti la Mtanzania baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa miezi mitatu na Serikali. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda.
  Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda (kushoto) na  Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo wakisoma nakala ya kwanza ya gazeti la Mtanzania baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa na Serikali. 
   Askari wa Usalama Barabarani akisoma nakala ya gazeti la Mtanzania.
   Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absalom Kibanda (kulia) akigawa nakala ya gazeti la Mtanzania kwa wasomaji wake.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Nathan Mpangala

  Help for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.

  Akizungumzia ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa, alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.

  Majina, kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni;  Joseph Mboya, Saidi Makope,  Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro), Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba (udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam) na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).

  HUC ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii. Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
  Baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa kozi mbalimbali za ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakisubiri taratibu za ujazaji fomu za kujiunga katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA) jijini Dar es salaam, hivi karibuni.
  Ujazaji fomu za kujiunga na masomo ya ufundi VETA ukiendelea. Vijana hawa ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
  Baadhi ya vijana walipata ufadhili wa masomo ya ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakijaza fomu za kozi mbalimbali walizoomba VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Monica Mhelela, Joseph Mboya na Hassan Bakari.
  Jamila Mwenda na Joseph Mboya wa Dar es Salaam, wakionesha nyuso za furaha baada ya ndoto zao za kusomea usekretari kwa Jamila na ufundi magari kwa Joseph kutimia. Jamila na Joseph ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC)

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la TMK Wanaume "Chege "akionyesha umahiri wake wa kutawala jukwaa wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei kwaajili ya wateja wao wakati huu wa sikukuu ya Krismasi.
  Msanii wa kundi la Tiptop Connection Madee akiwaburudisha mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach, wakati wa kusherehekea sikukuu ya krismasi na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei ,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa kampuni hizo.
  Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawaisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti kwaajili ya wateja wao wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0
 • 12/27/13--04:06: Article 8


 • 0 0

  Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

  Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

  Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.

  Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, anuani za posta, tovuti (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).

  Imetolewa na:
  Assaa Rashid,
  Katibu,
  Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
  Dar es Salaam
  Disemba 27, 2013.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  KAMPUNI ya Megatrade Investiment Ltd ya jijini Arusha imekabidhi zawadi katika kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha Kili Center kwa ajili ya msimu wa siku kuu za mwisho wa mwaka.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi zwadi hizo meneja mauzo na masoko wa Megatrade Goodluck Kway alisema msaada huo ni sehemu ya faida iliyopatikana kutokana na utumiaji wa kinywaji cha K-Vant Gin hivyo kampuni ikaonelea ni vyema ikarejesha kwa jamii hususani watoto waishio katika mazingira magumu.

  Alisema Mega trade investment ltd imetoa zawadi ya kilogram 50 za mchele, kilogram 100 za Unga wa Sembe,kilogramu 50 za unga wa ngano.kilogramu 75 sukari na kwa ajili ya kupikia lita 50.

  Vitu vingine ni Katoni mbili za sabuni za kufulia,Dawa za meno,Mafuta ya kupaka mwilini,Vinywaji vya aina tofauti sanjari na madaftari kwa ajili ya maandalizi ya mwaka mwingine wa masomo utakao anza January mwakani .

  “Megatrade tunatambua kuwa watoto yatima pia wanayo haki ya kusherehekea siku kuu za Krismas na mwaka mpya kama walivyo watoto wenzao na ndio sababu tumekuwa na utaratibu wa kuwapatia msaada kila mara pindi tunapo pata nafasi”alisema Kway.

  Aliziomba taasisi nyingine na makampuni mbalimbali kujitokeza kulisaidia kundi hilo ambalo hivi sasa linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa vifaa vya shule hususani kwa watoto wanao bahatika kuendelea na masomo.

  Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake Neema Omary aliishukuru kampuni ya Megatrade kwa kuwakumbuka kwa msaada huo huku wakiendelea kutoa wito kwa watu binafsi na makampuni mengine kujitokeza kutoa msaada ambao utawasaidia katika shughuli zao mablimbali za kimaendeleo.
  Meneja mauzo wa kampuni ya Megatrade ya jijini Arusha Goodluck Kway (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio kwenye mazingira magumu wa kituo cha Kili center cha mjini Moshi kabla ya kukabidhi zawadi kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka.

  0 0


  0 0

  Mwili unatarajiwa kuwasili nchini kutokea India jumapili mchana tarehe 29 Desemba 2013 na Qatar Airways.

  Jumatatu tarehe 30 Desemba 2013 saa 3 asubuhi kutakuwa na Ibada Maalum na ratiba ya kutoa heshima za mwisho katika Kanisa la Anglican la Mtakatifu Albano jijini Dar es Salaam.

  Jumanne tarehe 31 Desemba 2013 Mwili wa Marehemu utasafirishwa kuelekea Ngara kwa ajili ya mazishi.

older | 1 | .... | 310 | 311 | (Page 312) | 313 | 314 | .... | 3272 | newer