Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

JKCI kufanya upanuzi wa katika eneo la Mloganzila

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akizungumza na wajumbe kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wawakilishi kutoka China  Academy of Building Research waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa upanuzi wa JKCI wa awamu ya pili katika eneo la Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo ni miongoni mwa matunda ya ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyoifanya China mwaka 2018.
 Baadhi ya wajumbe kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wawakilishi kutoka China Academy of Building Research wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori (hayupo pichani) wakati wa kikao kifupi kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa upanuzi wa JKCI wa awamu ya pili katika eneo la Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wawakilishi kutoka China Academy of Building Research wakiangalia ramani ya eneo la Mloganzila wakati wa kikao kifupi kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa upanuzi wa JKCI wa awamu ya pili katika eneo la Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wawakilishi kutoka China  Academy of Building Research waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa upanuzi wa JKCI wa awamu ya pili katika eneo la Mloganzila leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo ni miongoni mwa matunda ya ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyoifanya China mwaka 2018
Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

TASAF Zanzibar kuzigusa shehia zote 388 katika mpango wa kuhudumia Kaya Maskini kwa mwaka 2019/2020

$
0
0
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini Tanzania (TASAF) upande wa Zanzibar unatarajia kuzigusa Shehia zote 388 katika muelekeo wake wa utekelezaji wa Mpango wa kuhudumia Kaya Maskini kwa Mwaka 2019/2020 Tasaf Awamu ya Nne.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) Kisiwa cha Unguja kwa niaba ya Kamati Mbili za Visiwa vyote vya Zanzibar Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema hayo wakati akizungumza na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 yanayounda Taifa la Nigeria waliowasili Nchini Tanzania kwa Ziara maalum.

Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi aliwaeleza Waratibu hao waliofika Zanzibar kujifunza Mpango Maalum wa kuhudumia Kaya Maskini kwamba Shehia zinazohudumiwa kwa sasa zimeshafikia 233 kati ya 388.

Alisema katika muelekeo huo hakutakuwa na Shehia hata Moja isiyoguswa katika masuala ya Kaya Maskini kazi itakayokwenda sambamba na mapitio ya Shehia ambazo kwa sasa zinaendelea kuhudumiwa kutokana na kuwa na sifa za kuingia katika Kaya Maskini lakini zilishindakana kutokana na ufinyu wa Bajeti katika Awamu iliyopita.

Mheshimiwa Ayoub alitanabahisha kwamba Mapitio hayo yatachambua katika kuzifanyia tathmini Shehia ambayo zilikuwa na Kaya Maskini lakini kwa sasa tayari zimeshakuwa Kiuchumi na kukosa sifa ya kuwa Kaya Maskini.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) Kisiwa cha Unguja aliwafahamisha Waratibu Wakuu hao wa Majimbo 36 ya Nigeria kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uimarishaji wa Ustawi wa Jamii kupitia Mfuko wa Tasaf.

Alisema uundwaji wa Vikundi vya Kijamii katika Shehia mbali mbali za Visiwa vya Unguja na Pemba umesaidia kuibua Miradi tofauti iliyowezesha Wananchi Kiuchumi na hatimae kupiga hatua kubwa ya mapambano dhidi ya kuondokana na ukali wa Maisha.

Hata hivyo Mh. Ayoub alisema Sekta ya Kilimo imeleta faida kubwa ndani ya Mfuko wa Tasaf ingawa bado zipo baadhi ya changamoto zinazowakazwa Wananchi katika maeneo yao hasa kwenye Sekta ya Afya na Elimu ambazo ndio kichocheo cha kuimarika kwa Ustawi na Maisha ya Jamii kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} Unguja ameipongeza Timu ya Waratibu hao Wakuu wa Majimo 36 ya Nigeria kwa uamuzi wao wa kufika Zanzibar kujifunza muenendo mzima wa harakati ya maendeleo yanayotokana na Mfuko wa Tasaf.

Akitoa Shukrani zake Kiongozi wa Timu hiyo ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 yanayounda Taifa la Nigeria Naibu Mkurugenzi wa Taasisi inayosimamia masuala ya Ustawi wa Jamii Bwana Ortutu alisema ziara yao Nchini Tanzania imekuja kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mpango wa kuhudumia Kaya Maskini.

Bw. Ortutu alisema Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache Duniani zilizofanya vizuri na kuchukuwa anafasi ya juu katika kuendeleza Mpango huo, huku Visiwa vya Zanzibar vikifanya vizuri zaidi ikilinganishwa na upande wa Tanzania Bara.

Alisema ujio wao wa kuja kujifunza Nchini Tanzania utawapa nafasi ya kuibua njia zitakazowasaidia kupata mbinu za muelekeo wa kupambana na changamoto zinazowakabili katika kutoa huduma kutokana na idadi kubwa ya Wakaazi wake zaidi ya Milioni 200 wanaoishi ndani ya Majimbo 36 ya Nchi hiyo iliyo Magharibi ya Bara la Afrika.

Mapema akitoa Taarifa Mwakilishi wa Mfuko wa Tasaf wa Kanda Bibi Saida Saleh Adam alisema zaidi ya Shilingi Bilioni 27 zimeshatolewa katika Mpango Maalum wa kuhudumia Kaya Maskini Unguja na Pemba.

Bibi Saida alisema fedha hizo zililengwa katika uimarishaji wa huduma za Afya na na Sekta ya Elimu katika kuwapatia mahitaji ya Vifaa Wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu ndani ya mpango wa stawisha Maisha Vijiji 20.

Ujumbe huo wa Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria walipata fursa ya kukagua Kituo cha Afya Kiyanga kilichojengwa kupitia mradi wa Kijamii ndani ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tasaf pamoja na kuona maeneo ya uzalishaji wa mazao ya viungo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} Kisiwa cha Unguja kwa niaba ya Kamati Mbili za Visiwa vyote vya Zanzibar Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza Kulia akizungumza na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 yanayounda Taifa la Nigeria waliowasili Nchini Tanzania kwa Ziara maalum. Kushoto kwa Mh. Ayoub Mohamed ni Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za SMT na SMZ anayesimamia Mfuko wa Tasaf upande wa Zanzibar Nd. Khalid Bakar Amran.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waratibu hao.
 Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Nigeria na Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) wakijadiliana mambo mbali mbali yanayohusu mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maendeleo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania(TASAF).
Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Nigeria waliowasili Nchini kwa ziara Maalum. Picha na – OMPR – ZNZ.

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA MISS TANZANIA 2019 NA UJUMBE WAKE MJINI DODOMA LEO, AMTAKA ATANGAZE UTALII

$
0
0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemtaka Miss Tanzania 2019, Sylivia Bebwa (19) ahakikishe anakuwa balozi mzuri wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali na aishi kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.

“Miss Tanzania lazima awe mbunifu na uelewa mpana katika masuala mbalimbali zikiwemo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wananchi kama kuhamasisha elimu hususan kwa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Septemba 11, 2019) wakati alipokutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Miss Tanzania na mshindi wa pili na watatu wa shindano hilo, ofini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Amesema Miss Tanzania anatakiwa kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, shughuli zinazofanywa na Serikali katika kukuza uchumi pamoja na kuhamasisha wananchi washiriki katika kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Miss Tanzania pamoja na washiriki wengine wa mashindano hayo wanatakiwa waishi kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania ikiwemo kuwa na nidhamu katika jamii ili waweze kuwashawishi wengine kushiriki.

Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Mwakyembe kwa namna anavyoratibu shughuli mbalimbali katika wizara hiyo. “Hata katika sekta ya michezo viwango vimeanza kuonekana.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inaunga mkono masuala ya michezo na inapenda kuona viwango vinapanda, hatua ambayo itawawezesha wahusika kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.

Kwa upande wake, Waziri Dkt. Mwakyembe amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kuonana na ujumbe huo hususani Miss Tanzania ambaye anajiandaa kwenda kushiriki katika mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika London, Uingereza Desemba 14 mwaka huu.

Waziri huyo amesema miaka ya nyuma Serikali haikuridhishwa na namna mashindano hayo yalivyokuwa yakiendeshwa lakini kwa sasa hali ni tofauti na yamekuwa na viwango vya kimataifa. Mashindano hayo kwa sasa yanasimamiwa na aliyekuwa Miss Tanzania 2008, Basilla Mwanukuzi kupitia kampuni ya The Look.

Naye,Mwandaaji wa Mashindano hayo, Basilla Mwanukuzi ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwao na pia ameiomba izidi kuwaunga mkono kwa kuwa watatumia mashindano hayo katika kulitangaza Taifa.

Awali, Miss Tanzania 2019, Sylivia ameishukuru Serikali kwa fursa aliyopewa ya kukutana na Waziri Mkuu na alisema kuwa atajitahidi katika kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss World na kwamba anakwenda kutumia lugha ya kiswahili.

“Nimefurahi kwa heshima hii niliyopewa na Serikali ya kukutana na Mheshimiwa Waziri Mkuu, naahidi kwamba niyatekeleza maagizo yote aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuishi kwa kuzingatia maadili ili wazazi wengine waweze kuwaruhusu watoto wao washiriki katika mashindano haya kwani urembo ni heshima.”
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, Septemba 11.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Miss Tanzania 2019, Sylivia Sebastian, nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma, Septemba 11.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Miss Tanzania 2019, Sylivia Sebastian, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, Septemba 11.2019, kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa The Look Company Ltd, Basilla Mwanukuzi, ambaye ndiye muandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2019, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, Septemba 11.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na waandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2019 ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, Septemba 11.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Standard Chartered bank yazindua programu ya 'future Makers' kusaidia vijana wa kizazi kijacho kupata elimu ya kifedha

$
0
0


Mkurugenzi wa fedha wa benki ya Standard Chartered duniani Bw, Andy Halford akizungumza jambo kwenye mkutano wa mafunzo ya elimu ya uchumi. kushoto ni bw. Bernard Dadi Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya taifa wa benki kuu ya Tanzania (BoT) na kulia ni Bi. Irene Madeje Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust.

Wakifuatilia kwa ukaribu mafunzo yanayofanyika kutoka kushoto ni Rayson Foya Mkuu wa kitengo cha fedha wa Standard Chartered bank tanzania, Kariuki Ngari Mkurugenzi mtendaji wa benki Standard Chartered Afrika Mashariki, Sanjay Rughani Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Bernard Dadi Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya taifa wa benki kuu ya Tanzania (BoT), Mkurugenzi wa fedha wa benki Standard Chartered duniani Bw, Andy Halford na bi. Irene Madeje Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust. 


Sarah Zacharia (19yrs) akizungumza jinsi alivyonufaika na mradi wa Goal initiativa ulioanzishwa na benki ya Standard Chartered kwa ajili ya kuwasaidia wasichana/mabinti. Sarah yupo katika klabu ya Ali Mbowa iliyopo Temeke akijifunza kutengeneza mazulia kwa kutumia uzi na kwa sasa anafanya biashara hiyo inayomsaidia kupata kipato.

Vijana na wanafunzi kutoka vyuo, shule na taasisi mbalimbali wakifuatilia mafunzo kuhusu elimu ya uchumi yanatolewa na watu na wadau mbalimbali kutoka benki ya Standard Chartered. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius nyerere jijini Dar es salaam.

  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,Sanjay Rughani, akizungumza na vijana pamoja na watu mbalimbali waliofika katika mkutano/ mafunzo kuhusu elimu ya uchumi (financial education) uliofanyika katika ukumbi wa julius nyerere Dar es salaam.

Mkutano ukiendelea.

Wakizindua rasmi program ya " Future Makers" ambayo inalenga kusaidia vijana na kizazi kijacho kuweza kupata elimu ya kifedha, kutoka kushoto Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Standard Chartered Tanzania Sanjay Rughani, Mkurugenzi wa mifumo wa malipo ya Taifa wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Bernard Dadi, Mkurugenzi wa fedha wa Standard Chartered bank duniani Mr. Andy Halford, Mkurugenzi mtendaji wa Standard Chartered Afrika mashariki Mr. Kariuki Ngari, Mkurugenzi wa shughuli mbalimbali katika sekta ya kifedha ya Deepening Trust Irene Madeje na kulia ni Rayson Foya ambaye ni Mkuu wa kitengo cha fedha wa benki Standard Chartered Tanzania

 
Standard Chartered Bank today launched its new community investment approach called Futuremakers by Standard Chartered. The initiative focuses on helping the next generation learn, earn and grow. The launch of Futuremakers by Standard Chartered was with a focus on Financial Education.

The launch of Futuremakers by Standard Chartered is a result of the Bank’s development of its community strategy to be more responsive to the changing social and economic needs across its markets around social and economic inequality and the limited opportunities for young people.

For the past 17 years in Tanzania, the Bank has been investing on areas of Youth, Health and Education. The Bank has been championing tackling avoidable blindness and visual impairment – through its programme, Seeing is Believing. Last year, the Bank achieved its global target of raising USD 100 Million towards Seeing is Believing, two years ahead of target.

“Seeing is Believing has reached more than 176 million people through 193 projects across 37 countries. The initiative has changed the lives of millions of individuals and families, making it easier for many to return to education and work. As a result, this has boosted local economies and strengthened communities” said, Mr. Andy Halford, the Bank’s Group Chief Executive Officer.

Mr. Andy said that, “according to the International Labour Organization, globally, more than 200 million young people are either unemployed, or they have jobs, but continue to live in poverty due to low income. At Standard Chartered Bank we believe everyone should have access to opportunities to realize his or her full potential and believe that we can make a difference in promoting greater economic inclusion in our markets”.

Speaking at the launch event, the Bank’s newly appointed East Africa CEO, Kariuki Ngari. said, that, “the launched Financial Education program plays a big role in enabling us achieve the goal of promoting equality and enabling youths achieve their full potential. In this regard, the Futuremakers builds on the success of our existing community programmes. We will, therefore, continue to incorporate financial education into all programmes. We will also expand GOAL, our existing girls’ education programme, and we will develop new global community programmes in employability and entrepreneurship.”

The Chief Executive Officer, Sanjay Rughani said that, “we want to use the unique skills of the Bank, and of our employees, to share skills and build the capacity of young people to access jobs and economic opportunities that will help close the inequality gap.”

The launch event was also attended by Irene Madeje, Director of Operations from the Financial Sector Deepening Trust (FSDT). Irene elaborated on the role of FSDT in supporting underserved individuals, households and enterprises, by offering them capacities and opportunities to improve their lives.

The event was officiated by the Director of the National Payment System from the Bank of Tanzania, Mr. Bernard Dadi who commended Standard Chartered Bank for developing and launching the Financial Education program as it will help close the inequality gap in our communities.

The launch of Futuremakers by Standard Chartered Bank fully aligns with the Bank’s purpose to drive commerce and prosperity through its unique diversity and reinforces its promise to be Here for Good. 

Asasi za Kiraia waaswa kufanya kazi kwa uwazi na Uzalendo nchini

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kuwa na Uzalendo,uwazi pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali kwani kufanya hivyo watasaidia kuleta mchango wa kuinua maendeleo na kukuza uchumi hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kuratibu na sekta na Asasi kutoka TAMISEM Dkt.Andrew Komba I Wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma.

Amesema kuwa asasi za kiraia hapa nchini zinatoa mchango mkubwa kwa serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuwafikia na kutoa huduma kwa wananchi jambo linalosaidia wananchi kupata maendeleo wao binafsi na taifa kiujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Asasi za kiraia Francis kiwanga  ameeleza ushirikiano kati ya asasi za kiraia,Serikali pamoja na wadau wengine wa kimaendeleo ni muhimu kwani ni moja ya njia ambayo itazisaidia asasi hizo kukua zaidia maendeleo wa binafsi pamoja na serikali kiujumla hivyo wataendelea kushirikiana na serikali katika kila sekta ili kuzitatua kero na matatizo mbalimbali ya wananchi.

Aidha ameongeza kuwa wiki ya asasi za kiraia itaanza rasmi Novemba 4 mpaka 8 mwaka huu jijini Dodoma na kauli mbiu ya wiki hiyo ni  kwa maendeleo ushirikiano ni nguzo muhimu ya maendeleo kwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Dkt. Andrew Komba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sherika la Foundation (FCS) Francis Kiwanga akizungumza kuhusiana na wiki ya Asasi Kiraia walivyipanga katika wiki itakapoanza Mjini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanganyika Law Sociaty (TLS) Kaleb Gamanya akitoa maelezo walijipanga katika utoaji wa elimu katika eneo la sheria katika wiki ya Asasi za Kiraia itakayofanyika Mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Asasi za Kiraia.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Andrew Komba akikata utembe kuashiria kufuanga wiki ya Asasi za Kiraia katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na viongozi wa Asasi za Kiraia

KESI YA UCHOCHEZI INAYOMKABILI MBOWE,WENZAKE YAFIKA PATAMU,SHAHIDI WA NANE ATOA USHAHIDI WAKE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

SHAHIDI wa nane katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Bernad Nyambali, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa maandamano ya wafuasi wa Chadema yalitokana na hotuba zilizotolewa wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu  Dk.Zainabu Mango mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, shahidi huyo amedai kauli zilizotolewa na viongozi hao zilihamasisha watu waandamane kutoka eneo la mkutano wa kampeni  kwenda Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Nyambali amedai maneno yaliyokuwa yakitamkwa yalichochea chuki kati ya wananchi dhidi ya serikali na vyombo vya dola hivyo, wafuasi wao walipata hisia hasi na kusababisha kuandamana.

Shahidi  Nyambali ambae wakati wa tukio alikuwa msaidizi wa mkuu wa upelelezi mkoa wa Kinondoni amedai, maandamano hayo pia yalisababisha athari mbali mbali ikiwemo kusababisha kifo cha  binti Akwilina Akwilini ambae matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa alifariki kutokana na jeraha la risasi ambayo alipigiwa akiwa eneo la Mkwajuni ambayo ndio ilikuwa center ya maandamano.

 Ameendelea kudai kuwa baadhi ya watu waliumia kwa kurushiwa na kupigwa mawe ambapo kati ya hao  maaskari wawili waliumia baada ya kupigwa mawe na waandamanaji  ambao ni CP Fikiri wa kituo cha polisi Osterbay na Koplo Hakimu.

Akijibu swali la Dr Mango  namna alivyohusika na upelelezi juu ya kifo cha Akwilina, shahidi a amedai kuwa, hakuhusika katika upelelezi wa tukio la kifo cha Akwiline Akwilina,  upelelezi wa tukio hilo ulifanywa na timu nyingine ya upelelezi.

Akielezea tukio hilo, shahidi Nyambali amedai February 16,mwaka 2018 akiwa katika shughuli zake za za kiupelelezi eneo la Kinondoni Hananasifu, alisikia kelele za kuashiria vurugu kutokea upande wa Barabara ya Kawawa lakini wakati akitafakari alipigiwa simu na Mkuu wa Upelekezi wa Mkoa wa Kinondoni, SSP Mungu Maluku na kumuagiza aelekee Barabara ya Kawawa kwa kuwa kulikuwa na watu wanaandamana.

Amedai, alipofika eneo la tukio alikuta kuna kundi kubwa la watu wanaokadiriwa kuwa 350 hadi 500 waliokuwa wakiandamana kuelekea eneo la Mkwajuni huku wakionekana wanajazba  na wakibishana na Polisi ambao  walikuwa wakiwataka kutawanyika.

Amedai watu hao walikuwa wanajibu kuwa hawaondoki wawaue huku miongoni mwao walikuwa wamebeba mawe, fimbo na kutanda barabara nzima huku wakiimba nyimbo za kuhamasishana.

Amesema, alienda moja kwa moja hadi kituo cha daladala cha mwendo kasi na kukuta viongozi kadhaa wa jeshi la polisi wakiongozwa na ASSP Gerlad Ngichi  ambapo walikuwa wakiwataka  waandamanaji kutawanyika na muda ule walikuwa wamefikia hatua ya kufyatua mabomu.

"Niliweza kuwatambua baadhi ya watu niliokuwa nawajua ambao walikuwa mbele kabisa kama vile, Freeman Mbowe, John Mnyika, Vincent Mashinji na Halima Mdee".

Shahidi Gerlad amedai baada ya waandamanaji kutawanywa barabara ilikuwa imetapakaa mawe, fimbo, chupa za maji huku meza ambazo zilikuwa zikitumiwa na wafanyabiashara pembeni ya barbara zilibinuliwa kutokana na vurugu zilizotokea na maduka yalifungwa.

"Baada ya maandamano yale kutawanywa na hali kuwa shwali nilianza upelelezi wangu wa kuweza kubaini watu (RAIA) ambao wanaweza kufaa kuwa mashahidi katika kesi ya maandamano  ambao waliweza kuona namna maandamano hayo yalivyokuwa yakifanyika.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk.Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

KUNA SOMO KUBWA TUNAJIFUNZA KWA RAIS DKT. MAGUFULI... KAMA UNABISHA KAJINYONGE TU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MTANZANIA mwenzangu kabla ya kuendelea na hiki ambacho nataka kukieleza kwa siku ya leo , naomba nitumie nafasi hii kukusalimia.Asalaam Eleikum, Bwana Yesu Asifiwe, Bwana awe nawe, Mambo vipi baharia wangu , natumai unaendelea vema ndugu mtanzania.

Nimetoa salamu zote hizo kwa kuamini kila mmoja atajibu anayooona inamfaa, hata hivyo kwa ujumla pamoja na salamu zote ambazo nimezitoa maana yake ibaki moja tu nayo ni kutoa salamu kwako.Natumai umeitikia na baada ya hapo niendelee na maelezo yangu.

Sina uhakika kama ambacho nitaekeleza kitaeleweka kwa msomaji , hata hivyo naomba Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo unijaalie busara na hekika ili ujumbe wangu ueleweke.Eee Mwenyezi Mungu naomba unipe ujasiri wa kuandika maelezo ambayo hayatakuwa magumu kueleweka. Mungu wa Said Mwishehe umekuwa ukinikubalia kwa kila niombalo kwako.Natumai na hili ambalo nimeomba nalo umenikubalia.

Iko hivi; kuna mambo mengi ya kujifunza katika maisha.Yapo ya kujifunza darasani, yapo ya kujifunza kupitia vitabu vilivyoandikwa na wasomi wa kada tofauti, kuna kujifunza kupitia jamii inayokuzunguka.Pia kuna kujifunza kupitia kwa wengine wenye uelewa katika jambo fulani na kuna kujifunza kupitia viongozi wanaokuongoza.Ndio !Na kama kuna aina nyingine ya kujifuza baki nayo.Ila yote iwe kujifunza tu.

Hadi hapo naamini tunakwenda sawa.Sina shaka nawe hata kidogo kuwa kuanzia hapo juu hadi hapa ulipofika umenielewa .Tuendelee na majadiliano.Kwanza meza mate na kisha tuendelee. Jamani binafsi naomba nikiri kuwa kupitia kwa Rais Dk.John Magufuli kuna mengi najifnza kutoka kwake. Ndio! Unashangaa nini?Najifuza mengi tu na kama hutaki basi jinyonge ingawa usipokufa kesi itabaki kuwa ya kwako ya kutaka kujia.Mimi simo kwenye hilo.

Kuna mambo ya kukaa nayo kimya lakini kwenye hili la kujifunza kutoka kwa Rais wangu mpendwa Dk.Magufuli ni muhimu nikaweka wazi yapo mengi najifunza na nitaendelea kujifunza siku hadi siku.Najifunza namna ambavyo anavyowaongoza Watanzania zaidi ya milioni 55 kwa weledi mkubwa.Najifunza alivyomnyenyekevu kwa anaowangoza .Najifunza namna ambavyo Rais anavyosimamia suala la kuhamasisha uzalendo miogoni mwa Watanzania.

Kwa Rais Magufuli najifunza namna ambavyo Watanzania tunakiwa kusimama imara kutetea raslimali za nchi yetu.Najifunza namna ambavyo Rais Magufuli pamoja na madaraka makubwa aliyonayo bado ameendelea kuwa mnyenyekevu kwa wananchi wake.

Hakika kuna mengi najifunza kutoka kwa Rais.Naamini wengi tunajifunza kutoka kwake.Ukweli ndio huo, sote tunajifunza .Kama unabisha nyoosha mkono juu kisha fanya kama unajikuna nikuone.Huna ujanja wa kunyoosha kidelo juu maana ukweli sote tunaendelea kujifunza.

Pamoja na kujifunza katika maeneo ambayo nimeyataja hapo juu, nirudie tena Rais Magufuli ametoa somo kubwa kwa Watanzania. Somo lenyewe ni hili la kusamehe kwani amethibitisha kuwa yeye ni mwenye kusamehe kwa vitendo kwa wale walimkosea.

Jamani hapa naomba tuelewane kidogo , tukubali kuna watu wengi wametofautiana kwa namna moja au nyingine huko mtaani lakini hawataki kusameehana.Wanaona kusamehe sio sehemu ya maisha yao.Wamebaki wanakunjiana ndita hadi uso unaota makunyanzi a.k.a mikunjo. Kila mmoja anabaki na kinyongo dhidi ya aliyemkosea.Haya mambo ya kutosameehana yapo kwenye ngazi ya mtu mmoja mmoja na hata kwenye familia.Unabisha?Acha ubishi kama sio wewe hutaki kusamehe basi kua ndugu yako hataki kutoa msamaha kwa aliyemkosea.Wenyewe wanasema akimwaga mboga, wewe unamwaga ugali.

Hakika Rais Magufuli ametoa somo la kujifunza , nalo ni kusamehe.Kwani uongo? Juzi tu hapa Rais ametangaza kuwasamehe wabunge Januari Makamba wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga na William Ngeleja wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza. Wawili hao walimkosea Rais Magufuli kwa kumsema vibaya kupitia simu zao za mkononi.Kama unavyojua mambo ya kukua kwa tekolojia ya habari na mawasiliano.Sauti za wawili hao zikadakwa na kusambazwa mtandaoni.

Ukweli walichafua hali ya hewa lakini tunaambiwa kila siku kuwa hakuna binadamu aliyekamilika bali mkamilifu ni Mwenyezi Mungu peke yake.Kwa kuwa Januari Makamba na Ngeleja waliona makosa yako, wakaamua kuomba msamaha kwa Rais.

Hivyo wakati Rais Magufuli anazungumza kwenye mkutano wa wakandarasi na wahandisi uliofanyika siku za karibuni jijini Dar es Salaam alitangaza kuwasemehe wabunge hao.Rais alisema amejiridhisha kwa asilimia 100 sauti hizo zilikuwa za kwako.

Akawaza namna ambavyo adhabu itakuwa kali wakipelekwa Kamati Kuu ya CCM.Akaamua kuwasamehe.Tena akaeleza kusamehe kunauma lakini ni vema akatoa msamaha kwa wabunge hao kwani wamekiri na kuomba msamaha. Hongera Rais wangu kwa kutoa msamaha na umma wa Watanzania ukasikia.

Ni nadara sana kuona kiongozi mwenye nafasi ya aina yako akakubali kusamehe kwa waliomkosea.Kuna mifano mingi ya watu wambao wamekosea huko nyuma na hawakuwahi kusamehewa.Kwa leo si wakati wake.Nambuka Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi alisema kila kitabu na zama zake.Kwa kweli zama hizi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.Magufuli kuna mengi tunajifunza.Ametufundisha umuhimu wa kusamehe aliyekukosea.

Hakuishia hapo kwa Januari Makamba na Ngeleja peke yake, bali ni jana tu ya Septemba 10 , Rais Magufli ametoa msamaha kwa mbunge wa Mtama Nape Nnauye.Nape naye anahusishwa na kumsema vibaya Rais Magufuli baada ya sauti yake kusikika akizungumza kwenye simu.

Nape katika sauti yake ambayo nayo ilisambaaa katika mitandao ya kijamii alisikika akitoa maneno yasiyofaa dhidi ya Rais wetu mpendwa. Hata hivyo Rais Magufuli hakuzungumza lolote baada ya Nape sauti yake kusikika kwenye mitandao.

Rais aliamua kukaa kimya na hapa kuna kitu cha kujifunza.Nacho ni kuwa kimya jambo linapotokea kwani hakuna sababu ya kuhangaika kulijibu.Ametumia hekina na busara kubwa kama kiongozi wa nchi yetu, Tunafahamu Rais alikaa kimya kwa kipindi chote na jana alipoamua kulizungumzia suala la Nape na sauti yake alisikika akisema amemsamehe kwani mbunge huyo bado ni kijana.

Hakusita kueleza hatua mbalimbali ambazo Nape alipita kabla ya kufika kwake.Nape amehangaika sana kutafuta nafasi ya kumuona Rais.Alilazimika kwenda kuomba msaada wa mzee Philip Mangulla, mzee Apson na Mama Maria Nyerere. Kote huko alikwenda ili wamsaidie kupata nafasi ya kumuona Rais.

Pamoja na mambo mengine Rais hakusita kueleza kuwa alivyokuwa anatumiwa meseji za kuombwa msamaha na Nape.Tena meseji nyingine zilikuwa zinatumwa saa nane usiku.Na Rais amekiri kwa namna ambavyo alikuwa anasoma meseji za Nape za kuomba msamaha amejiridhisha kuwa ni kweli anajutia kosa alilofanya na sasa amemsamehe kutoka kwenye moyo wake.

Akatumia nafasi hiyo kumtaka aende akafanye kazi za kuwatumia wananchi wa jimbo lake , familia yake na watanzania.Hongera Rais somo ambalo nalipata si kumsamehe Nape, Januari Makamba au Ngeleja bali najifunza hata ukiwa kwenye nafasi bado unapaswa kusamehe tena ikiwezekana samehe saba mara sabini. Mwito wangu kwa Watanzania tujifunze kusamehe kama ambavyo Rais wetu anavyosamehe. Si dhambi kujifunza jambo jema na Rais wetu ameonesha njia.

Pia ushauri wangu , linapotokea jambo hakuna sababu ya kukimbilia kulizungumza maana unaweza kuzungumza ukapatia na unaweza kulizungumza ukakosea.Tuwe makini.Nakumbuka kwenye hili sakata la sauti za kumsema vibaya Rais kuna wana CCM na viongozi mbalimbali walianza kutoa matamko.Wakati wao wanatoa matamko Rais amebaki kimya tu, anatafakari kimya kimya kama hajui kinachoendelea.

Kuongeza kwa matamko kulisababisha Katibu Mkuu wa CCM DkBashiru Ally kutoa tamko la kuonya yoyote atakeyezungumzia suala hilo na kutoa tamko atachukuliwa hatua.Kweli kukawa kimya na ukimya huo leo umekuja na jibu ambalo nalo ni msamaha kati ya waliokosa na aliyekosewa.

Inatosha kwa leo , nikutakie kazi njema na tuendelee kuijenga Tanzania yetu ambayo haipatikani mahali kokote duniani zaidi ya Tanzania.Naipenda nchi yangu, naipenda Serikali ya Awamu ya tano na kubwa zaidi nampenda Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajili ya Watanzania wote.

Simu 0713833822

MKURUGENZI MTENDAJI KATIKA HALMASHAURI YA ARUSHA ATOA RAI KWA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA BIDII KUFIKIA MALENGO WALIYOJIWEKEA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano kama timu, bila kujali nafasi walizonazo, ili kufikia malengo ya yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo.

Ametoa rai hiyo alipokutana na watumishi wa sekta zote za halmshauri hiyo, katika kikao kazi cha kawaida, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, mwanzoni mwa wiki hii.

Mkurugenzi Dk. Mahera amefafanua kuwa lengo la kikao hicho ni kukumbushana wajibu na majumumu ya kila mtumishi, kwa kujengeana uelewa wa pamoja kwa watumishi wote katika uwajibikaji wenye tija ya kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi wa halmashauri hiyo pamoja na kujadili changamoto zinazokwamisha utendaji kazi.

Pia amewakumbusha watumishi hao, kutambua kuwa utumishi wa umma ni dhamana waliyopewa na Serikali, na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na za utumishi wa umma pamoja na miongozo ya serikali, kwa kutumia taaluma zao katika kutekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia haki na usawa.

"Serikali imewaamini na kuwapa dhamana ya kuwatumikia wananchi, tumieni taaluma zenu kutekeleza majukumu yenu, tushirikiane kama timu ili kuijenga Arusha DC na Serikali yetu kwa ujumla" amesema Dk. Mahera.

Sambamba na hayo Dk. Mahera amewaagiza Maafisa watendaji wa kata, kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha wananchi, wanatozwa tozo stahiki za taka na kupewa risiti za fedha zilizolipiwa, sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria, wananchi ambao wanakaidi na kunyanyasa wengine.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Utumishi katika halmashauri hiyo ya Arusha Hamis Mpume, amewaahidi watumishi hao kuendelea kusimamia haki zao, wajibu na usawa, na kuwakumbusha watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni apamoja na kutekeleza wajibu wao na kuahidi kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume.

“Nina imani kila mtumishi anafahamu vizuri majukumu yake, niwatake kila mmoja wenu kuyatekeleza kazi zenu kwa ufanisi, naahidi kutenda haki kwa kila mtumishi, sitamuonea mtu lakini sitasita kumchukulia hatua stahiki mtumishi asiotekeleza majukumu yake" amesema Mpume

Wakati huo huo Ofisa Mtendaji kata ya Mateves, Muyai Kivuyo,licha ya kumshukuru Mkurugenzi huyo, kwa kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili, wamemuomba mkurugenzi huyo kuwapa taarifa za shughuli za miradi ambozo huendelea katima kata zao ili wafahamu na kushiriki katika kufuatilia miradi hiyo.

Kikao kazi hicho kimewakutanisha, watumishi wa ngazi za kata, ikiwemo maafisa watendaji kata, moafisa ugani na mifugo, maofisa maendeleo ya jamii, maofisa afya, maofisa elimu kata, pamoja na wakuu wa idara na vitengo.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera  akiongea na watumishi Wa halmashauri yake.

WANASHERIA WAKUU WA SERIKALI BARA NA VISIWANI KUANZISHA UTARATIBU RASMI WA MASHIRIKIANO

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akizungumza na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar Bw. Mzee Alli Haji ambaye aliongoza ujumbe wa watu sita katika ziara yao ya kuitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( Bara) kwa madhumini ya kubadilishana mawazo na uzoefu na kuangalia maeneo ya kushirikiana hususani kwa yale yenye sura ya Muungano ikiwamo Mikataba ya Kikanda na Kimataifa.
Ujumbe Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar ukiwa katika mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi ambaye katika mazungumzo hayo alieleza kwamba Ofisi hizo mbili zinakusudia kuanzisha utaratibu au mfumo rasmi wa mashirikiano na uhusiano baina ya Taasisi hizo.

Na Mwandishi Maalum, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG) Profesa Adelardus Kilangi amesema, Baada ya majadiliano na mashauriano ya kina na Mwenzake, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Said wanakusudia kuanzisha utaratibu rasmi utakaoratibu mashirikiano na mahusiano baina ya Ofisi hizo mbili.

Ameyasema hayo siku ya Jumatano jijini Dodoma, wakati alipokutana na kuwa na mazungumzo na Ujumbe wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali wa Zanzibar ulioongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mzee Alli Haji.

AG kilangi ameuambia ujumbe huo kwamba, ingawa Ofisi hizo hivi sasa zinashirikiana katika masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa kwa pande zote mbili za Muungano, ushirikiano huo haujawekewa utaratibu unaoeleweka

"Tumeliona hili mimi na mwenzangu na kwa kweli tunashirikiana vizuri sana lakini katika namna ambayo ni ad hoc, sasa tumekubaliana na kudhamiria kuwa na utaratibu rasmi utakaosaidia na kurahisisha mashirikiano haya ili kwayo tuweze kuzishauri vema serikali zetu na hatimaye ziwatumike vizuri na kwa tija wananchi wake"

Akaongeza kuwa kwa Watumishi wa Ofisi hizo mbili, kutembeleana, kubadilishana mawazo, uzoefu na kupeana ushauri kunaimiarisha na kuboresha utekelezaji wa majukumu.

Kauli ya AG Kilangi inatoka na hoja iliyotolewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar kwamba, moja ya madhumuni ya ziara yao iliyowafikisha Ofisini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( Bara) ni kujadiliana namna ya kukuza, kuendeleza na kudumisha uhusiano na mashirikiano baina ya Ofisi hizo.

Profesa Kilangi akatoa mfano kwa kusema kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limejiwekea utaratibu au mfumo wa kuwa na mashauriano na Serikali ya Zanzibar pale linapotaka kutunga sheria ambayo inagusa pande zote mbili za Muungano

Naibu Mwanasheria huyo aliongeza kuwa Ofisi zote mbili zinajenga nyumba moja kwa hiyo suala la uhusiano na masharikiano haliepukiki.

Akasisitiza kwamba, endapo Ofisi hizo zitashirikiana kwa karibu, hata zile hoja zinazojitokeza kama kero za Muungano zitaweza kushughulikiwa vizuri zaidi ikiwa Wanasheria Wakuu hao wa Serikali watakuwa na utaratibu rasmi wa kukutana na kujadiliana.

Pamoja na kusudio la kuweka rasmi utaratibu wa kushirikiana, Ofisi za Wanasheria Wakuu wa Serikali Bara na Zanzibar pia zimekubaliana kuangalia namna ya zitakavyobadilishana uzoefu katika maeneo ya uandishi wa Sheria,maandalizi na uhakiki wa mikataba hususani ile ya Kikanda na Kimataifa na ambayo utekelezaji wake utahusu pande zote mbili za Muungano.

Taasisi hizo pia zimekubalianakuangalia pia namna zitakavyoshirikiana katika kuwajengea uwezo na maarifa Mawakili wa Serikali na watumishi wengine kwa kushirikiana katika nafasi za mafunzo ya ndani na nje ya nje.

Kuhusu eneo hilo la mafunzo na kuwajengea uwezo watumishi wa Taasisi hizo, Profesa Kilangi amesema Zanzibar inaouzeofu mkubwa katika baadhi ya maeneo ambayo pia yanahistoria ndefu.

Aidha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Mzee Alli Haji pia alishauri kwamba, Taasisi hizo mbili pia zinaweza kushirikiana kwa kubadilishana mawazo na uzoefu katika kesi ambazo zina sura ya Muungano. Hoja ambayo imeungwa Mkono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.

Wizara ya Afya yaingia makubaliano na Shirika la GIZ kuboresha sekta hiyo nchini

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeingia makubaliano na Shirika la GIZ kutoka nchini Ujerumani yenye lengo la kuboresha sekta ya Afya nchini.

Makubaliano hayo yamekwenda sambamba na kutiliana saini kwa mkataba wa kufanya kazi pamoja kwa miaka mitatu utakaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 26.

Akizungumza baada ya kutiliana saini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula amelishukuru Shirika la GIZ kwa namna ambavyo limekua likijitoa katika kusaidia ukuaji wa sekta hiyo muhimu.

" Kwa kweli niwashukuru sana wenzetu wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani kwa namna ambavyo wamekua bega kwa bega na sisi, zaidi niwapongeze na kuwashukuru ndugu zetu wa GIZ hawa wamekua wadau wakubwa wa Afya nchini.

" Tunawaahidi kuwapa ushirikiano na kusimamia kwa ukamilifu yale yote tuliyokubaliana kuyatekeleza, lengo letu sote ni kuona sekta hii ya afya inakua na inawanufaisha Watanzania ambao ndio haswa walioipa dhamana Serikali ya awamu ya tano kuwatumikia," Amesema Dk Chaula.

Aidha amelipongeza Shirika hilo kwa kukubali kuwapatia fedha hizo kwa wakati mmoja ili iwe rahisi kuweza kutekeleza maazimio yote kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.

" Ndugu zangu kazi ya Serikali ni kuwaletea wananchi wake Maendeleo na Rais wetu Dk John Magufuli ni mtu wa vitendo haswa, amedhamiria kuifanya Nchi yetu kuwa imara katika kila nyanja na afya ikiwemo, haya yote tunayoyafanya leo ni matokeo ya juhudi kubwa ambazo yeye kama Kiongozi wetu wa Nchi amekua nazo," Amesema Dk Chaula.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Shirika la GIZ, Dk Mike Falken amesema makubaliano waliyoyafikia na Wizara ya Afya ni matokeo ya utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania katika kuwatumikia wananchi wake.

Amesema mkataba huo umejikita katika afya ya msingi hasa katika zahanati na vituo vya afya na utalenga maeneo matano ambayo ni Uboreshaji wa Taarifa, Mama na Mtoto, Bima, Uzazi wa Mpango na Utawala Bora.

" Sisi tunawaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati yetu, sisi tunaridhishwa na kasi ya Rais Magufuli katika kuwatumikia Watanzania na ni wazi tunamuunga mkono kwa vitendo," amesema Dk Falken.

Awali Shirika hilo lilikabidhi kwa Serikali kupitia Wizara ya Maji mradi wa Maji katika eneo la Ng'ong'onha jijini Dodoma ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 331 na utahudumia wananchi takribani 12000.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula (kushoto) akitiliana saini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la GIZ, Dk Mike Falken katika hafla ya makubaliano ya Uboreshaji afya nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula akizungumza na viongozi wa Wizara yake pamoja na viongozi kutoka Shirika la GIZ LA Nchini Ujerumani katika hafla ya kutiliana saini makubaliano ya Uboreshaji sekta ya afya.

NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS ATOA AGIZO KWA MAAFISA MADINI KOTE NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na watumishi wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakati wa ziara yake.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Marryprisca Mahundi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akilakiwa mara alipowasili wilaya ya Chunya mkoani Mbeya leo wakati wa ziara yake

NAIBU Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameagiza maafisa Madini nchini (RMO) kuhakikisha mialo yote inayoosha udongo wa dhahabu inasajiliwa na kutambulika ikiwemo kusimamiwa.

Ameyasema hayo jana wakati akiwa kwenye ziara yake wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ambapo alisema pia suala la uchomaji wa dhahabu usifanyike kiholela ichomwe sehemu moja japo kuna changamoto maeneo mengine inakuwa vigumu.

Amesema maafisa hao wanapaswa kuweka maeneo yanayofahamika ya kufanya uchenjua lakini wakati wa kuchoma waende sehemu moja huku akieleza kwamba wanafanya hivyo kwa sababu dhahabu ya mecury bado inapotea .

“Mnafanya vizuri sana lakini kuna baadhi yetu bado wapo miaka ya nyuma wanafikiria kutorosha dhahabu…mnafahamu uchenjuaji wa dhahabu asilimia 30 ya dhahabu inapatikana inayobaki inakwenda kuchenjuliwa kwenye Vatirichingi”Alisema

“Lakini niwaambia kwamba bado sijaridhishwa na dhahabu inayoonekana kwenye mecury kutokana na kwamba bado inapitishwa njia za panya wataalamu wetu wanaona kilo 20 tu kwa mwezi lakini sasa hivi tunaona kilo 120 “Alisema

Naibu Waziri huyo amesema kwamba hivi sasa wameanza operesheni maalumu kanda ya ziwa na maeneo mengine kudhibiti dhahabu ya mercury iende kwenye soko.

“Nikasema ujumbe wana chunya wangu nikuwaeleza mabroka na madila hakikishani mnanunua dhahabu na iwekeni kwenye soko kuna watu maeneo mengine unakuta dhahabu bei ya gramu ni sh.elf 96000 ukileta kwenye soko utakatwa asilimia 7 hivyo unaona fedha zitapungua atapotokea mnanuzi mwengine pembeni anakuambia atakupa elfu 95 usipeleka kwenye soko wewe unakubaliana naye unamuuzia “amesema

Hata hivyo am,ameeleza kwamba lazima wachimbaji watambue kwamba hiyo dhahabu wanayochimba ni mali ya serikali na wamepewa leseni ya uchimbaji kwa niaba ya serikali hivyo wakisha chimba kwa gharama zako zirudishe lipa mrabaha wa serikali baki na faida yako upeleke nyumbani ukikwenpa kodi unakuwa adui namba moja kwa sababu unainyima serikali mapato ambayo yangeweza kuwaaid kusukuma gurudumu la maendeleo.

Wahitimu wa Akademi ya MultiChoice watinga Bungeni

$
0
0
Mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto) akiwatambulisha wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada ya wahitimu hao kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika kupitia program yake ya MultiChoice Talent Factory. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya.

Wanafunzi wanne waliohitimu hivi karibuni mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya MultiChoice Talent Factory wamehudhuria kikao cha bunge la Tanzania kama wageni maalum wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Katika ziara hiyo pia wanafunzi hao walikutana na wadau mbalimbali akiwemo naibu spika Dr. Tulia Akson waziri Dr. Harrison Mwakyembe, naibu waziri Juliana Shonza, naibu waziri Anthony Mavunde na katibu mkuu wa wizara Suzan Mlawi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wahitimu hao katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, viongozi hao waliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo maalum waliyoyapata katika kuleta mapinduzi ya tasnia ya filamu hapa Tanzania. 

Kwa pamoja wamekiri kuwa tasnia ya filamu ni moja ya tasnia zinazokuwa kwa haraka hapa nchini hivyo ni muhimu wanatasnia wawe na mafunzo ya kutosha na yanayoendana na wakati ili iweze kupambana na nchi nyingine katika soko la filamu ulimwenguni huku tukihakikisha kuwa kazi zetu zinaakisi mila, desturi, utamaduni na uzalendo wetu.

Akizungumza na wanafunzi hao baada ya kumtembelea ofisini kwake, Katibu Mkuu Suzan Mlawi amesisitiza ahadi ya serikali kushirikiana na wadau wa tasnia mbalimbali ili kuharakisha ukuaji wa tasnia hizo. Amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau ni muhimu na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kuwa sera na kanuni zinaboreshwa ili kuakisi hali halisi ya ukuaji wa tasnia ya filamu.

Wanafunzi hao wanne – Wilson Nkya, Jane Moshi, Jamal Mohamed na Sarah Kimario wamehitimu mafunzo maalum ya mwaka mmoja yanayofadhiliwa na MultiChoice ambapo vijana 60 kutoka kote barani Afrika huchaguliwa kwa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali. Programu hiyo ina vituo vitatu vya mafunzo ambapo kwa upande wa kusini mwa Afrika kipo Lusaka Zambia, kwa Afrika Mashariki na kati kipo Nairobi Kenya na kwa Afrika Magharibi Lagos Nigeria.

Awamu ya pili ya program hii itaanza mwezi Octoba 2019 ambapo wanafunzi wengine 60 watapata mafunzo hayo. Tanzania kwa mara nyingine tena itapeleka wanafunzi wanne.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana.
Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane Moshi, Sarah Kimario na Jamal Mohamed.
Naibu Spika Dr. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kushoto ni Jane Moshi, Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya.

WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI (SME) WAENDELEA KUNUFAIKA NA BENKI YA KCB

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB Christina Manyenye, (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB, Masika Mukule akijibu swali kutoka kwa mmoja ya wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.
 Mkuu wa Kitengo Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME) wa Benki ya KCB, Abdul Juma (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Benki ya KCB Tanzania imeendelea kusimama na wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuandaa kongamano la pili la KCB Biashara Club na kuwaoeta pamoja wafanyabiashara zaidi ya 300.

Programu KCB Biashara Club ilibuniwa na benki hiyo kwa dhumuni la kutoa fursa mbali mbali kwa wafanyabiashara zikiwemo mafunzo ya uendeshaji biashara, kuwapa wafanyabiashara jukwaa la kushirikiana pamoja na kuwakuzia mtandano wa masoko ndani na nje ya Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Akizungumzia kongamano hilo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye amesema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Injinia Jane Kadoda kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye aligusia athari za biashara kwa mazingira pamoja umuhimu wa kutii sheria za kulinda mazingira zilizowekwa na serikali ya Tanzania

Amesema, Mwezi Machi Mwaka 2019, Benki ya KCB iliendesha kongamano kama hili jijini Arusha hususan kwa wafanyabiashara walio katika sekta ya utalii.

Akiongea wakati wa kufungua semina hiyo, Kwa upande wake mdau kutoka European Investment Bank (EIB), Fasili Boniface ameongelea umuhiumu wa kuweka kumbukumbuku za kifedha na jinsi ya kuainisha matumizi ya binafsi na ya kibiashara.

Naye Saada Sipemba ambaye ni mtaalamu wa safari za kibiashara kutoka Sadio Travel and Tourism ameongelea fursa za kibiashara zinazopatikana nchini China na juhudi za benki hiyo kuhakikisha inawatengenezea wateja wake mianya ya kuchukua fursa hizo kwa urahisi.

KCB kupitia Biashara Club imekuwa ikiandalia wadau wake safari za kibiashara kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini kwa gharama nafuu kwa dhumuni la kuwafungulia masoko mapya na bidhaa nafuu za kuleta kwenye soko la Tanzania.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa kupitia semina na safari mbalimbali zinazoandaliwa na KCB Biashara Club, wanachama pia wanafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao unaopelekea kuongeza ujuzi na kupanua wigo wa biashara.

KCB inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wa kati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AZINDUA AWAMU YA PILI YA MRADI MZUMBE

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapoa kihutubia wakati wa uzinduzi wa Awamu ya pili ya Mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe. 
Balozi wa Ubelgiji Nchini Tanzania Mhe, Balozi. Peter Van Acker akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe. 
 Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kuzindua rasmi awamu ya pili ya mradi.ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo (katikati Kushoto mwenye suti nyeusi), Mhe, Balozi. Peter Van Acker katikati kulia mwenye tai nyeusi), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ugent na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe (wenye sare ya batiki kulia na kushoto)na waratibu wa mradi kwa Tanzania na Ubelgiji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo (kulia) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Mohammed Utali wakiwasili Chuo Kikuu Mzumbe kwenye sherehe za uzinduzi awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4. 
 Baadhi ya washikiri wa sherehe za Uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe.
Mratibu wa Mradi wa Vlirous wa nchini Ubelgiji Pro Koen, akielezea malengo ya mradi na mipango ya utekelezaji kwa awamu ya pili, wakati wa uzinduzi Chuo Kikuu Mzumbe. 

KATIBU Mkuu Wizaraya Elimu, Sayansina Teknolojia Dr. Leonard Akwilapo leo amezindua awamu ya pili ya mradi “VLIROUS P4”unaofadhiliwanaSerikaliyaUbelgijikupitia Chuo KikuuUgent. 

Kuzinduliwakwaawamuya pili ya mradi huo kumetoka na na mafanikio makubwa ya awamuya kwanza ya mradi ambapo jumla ya miradi minne imetekelezwa ikiwemo ufadhili ya masomo kwa wanafunzi wa ngazi ya shahada ya Uzamili, Shahada yaUzamivu, Tafiti mbalimbali na huduma kwajamii. 

Akizundua mradi huo Katibu Mkuu Akwilapo amepongezana kushukuru Serikali ya Ubelgiji kwa ufadhili wa miradi mbalimbali sekta ya Elimu, na kuahidi Wizara yake kuendelea kuisimamia ili kuwa na matokeo ya nayotarajiwa katika ustawi wa Chuo na Maendeleo ya jamii kwa jumla. 

Amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kutekeleza malengo ya Mpango Mkakati wake wa miaka mitano kwa vitendo kwa kuimarisha na kuinua viwango vyatafiti, na kutumia vizuri fursa zilizopo kuimarisha ubora na kiwango cha elimu kina chotolewa chuoni hapo. 

Naye balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Balozi Peter Van Acker amesema matarajio yake ni kuona namna Vyuo Vikuu vinavyoweza kuhusianishwa moja kwa moja na  maendeleo ya jamii kupitia miradi ya maendeleo kama huu wa Vlirous, na kuahidi Serikali ya Nchi yake kuendelea kufadhili miradi mingi zaidi ya Elimu nchini Tanzania. 

Akitoa salamu za Chuo Kikuu Mzumbe, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano kusiluka amesema mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa husani katika kuonyesha kiuhalisia mchango wa Vyuo Vikuu katika maendeleo ya jamii, na kuunga mkono jitihada za Serikali kufikia uchumi wa viwanda. 

Awamu ya kwanza ya mradi imeleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya Teknolojia ndani ya Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na kubuni mifumi ya Tehama katika kutatua changamoto ya Afya, Ujenzi wa kituo cha kuchakata malighafi ya asali Turiani, kutoa mafunzo ya mbinu za ujasiriamali kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero, mafunzo kwa walimu wa Sekondari kuhusu mbinu bora za ufundishaji n.k 

Uzinduzi huo umekwenda sambamba na uwasilishaji wa mafanikio na changamoto za kila mradi pamoja na kuonyesha washiriki matokeo ya tafiti zilizofanyika. 

Mbali na kuzindua awamu ya pili ya mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa eneo la Maekani unaofadhiliwa na Serikali. 

KABENDERA AIELEZA MAHAKAMA MATIBABU ALIYOPEWA SEGEREA HAYAJATOSHELEZA

$
0
0
Na Karama Kenyunjo, Michuzi Tv.

MWANDISHI wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera anayekabiliwa na mashitaka ya utakatishaji fedha, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, matibabu aliyopatiwa na madaktari wa Gereza la Segerea  ya kumpima damu na kumchoma sindano tatu kutokana na kushindwa kupumua na mguu mmoja kukosa nguvu bado hayajatosheleza.

Amedai kuwa,  anapata maumivu makali katika mguu wa kulia na mfupa wa paja  na kumfanya ashindwe kutembea na kusababisha kuburuza mguu lakini bado hajapata huduma nyingine.

Mshtakiwa Kabendera amedai hayo leo Septemba 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile  baada ya kutakiwa kueleza kama madaktari wamempatia tiba yoyote.

Amedai madaktari wa gerezani hawana vifaa vya kuwasaidia kugundua tatizo linalomkabili, hivyo wamemshauri kufanya mazoezi lakini amedai mguu wake wa kulia na mfupa wa paja wa mguu huo una maumivu makali 

"Nimefanya jitihada za kuzungumza na madaktari na niliomba dawa za kutuliza maumivu kwa sababu sipati usingizi lakini Madaktari wameahidi kuendelea kuniangalia, na akaongeza kudai kuwa, alionana na daktari Alhamis iliyopita na jana  lakini hakumfanyia vipimo kwa sababu walikuwa na wageni, hivyo aliahidi kuonana naye leo.

"Nipo Segerea na kuna utaratibu wa madaktari kufanya matibabu kwa wagonjwa kila siku," alidai.

 Kabendera ameeleza hayo kufuatia Wakili wake, Jebra Kambole kudai kuwa hali ya mshitakiwa huyo inazidi kutetereka kwa sababu anashindwa kutembea vizuri na kushindwa kupumua.

Kambole amedai mteja wake hajafanyiwa matibabu vizuri kujua tatizo linalomsumbua na kuomba mahakama ielekeze magereza wampeleke hospitali yoyote ya Serikali ikiwamo Muhimbili ili wapate ripoti ya ugonjwa unaomsumbua.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Wankyo Simon amedai amewasiliana na Mkuu wa Gereza na amemueleza kuwa Kabendera anapatiwa matibabu na madaktari wamekuwa wakimuangalia mara kwa mara.

Amedai magereza wana utaratibu  wao endapo wataona ugonjwa unaomsumbua unahitaji rufaa, watampeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18, mwaka huu na kumuelekeza Kabendera kuonana na daktari na kesi itakapotajwa ataieleza mahakama kama amepata matibabu au la ili mahakama itoe maelekezo.

Kabendera alifikishwa  Mahakamani kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu, ambayo ni kuongoza genge la Uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh. 173.2Milioni.

Anadaiwa katika siku tofauti tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es, Salaam, mshtakiwa Kabendera alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa  bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya sh. 173, 247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Inadaiwa  kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha sh. Milioni 173.2 wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa Kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

Multichoice Talent Facotry Academy wapongezwa kwa kuiwakilisha vyema Nchi.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawiakiwa katika picha ya pamoja na Vijana waliorejea kutoka nchini Kenyawalikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama“Multichioce Talent Factory Academy” baada ya kupokea taarifa ya mafunzowaliyopata walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.
Meneja Biashara kutoka Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson Mshana (kulia)
akitoa maelezo mafupi kuhusu “Multichioce Talent Factory Academy” iliyodhaminivijana wanne katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni hiyo Nchini Kenya walipofika ofisi ya Katibu MkuuWizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi (kulia) kuelezeanamna walivyonufaika na mafunzo hayo.
Jamal Mohamed Kishuli ambaye ni miongoni mwa Vijana wanne
waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamukwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawatilijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakatiwalipomtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo BibiSusan Mlawi ofisini kwake Jijini Dodoma.
Bw.Wilson Nkya miongoni mwa Vijana wanne waliorejea kutoka nchini Kenyawalikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmojayaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama“Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati walipomtembeleaKatibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi(hayupo katika picha) ofisini kwake Jijini Dodoma.
******************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawiamewapongeza vijana wanne waliofanya vizuri katika mafunzo ya uaandaaji waFilamu yalioandaliwa na Kampuni ya Multichoice yaliyofanyika nchini Kenyaambapo amewataka kutumia taaluma waliyopata kutengeneza filamu bora zenyemaudhui ya kuitangaza nchi yetu na kuleta ushindani katika soko.

Katibu Mkuu Bibi. Susan ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dodoma baada yakutembelewa na vijana hao ambao amewataka kufika katika Bodi ya FilamuTanzania kuwasilisha uelewa waliopata na kushauri namna ambavyo Bodi hiyoinaweza kuwatumia katika tasnia hiyo.

“Nawapongeza sana kwa kufanya vizuri katika mafunzo mliopewa,naamini
mtayatumia vizuri katika kukuza vipaji vyenu na kusaidia mawazo kwa wengineambao hawajapata nafasi hii,Lakini pia mtatumia ujuzi na taaluma mliyopatakatika kuleta mapinduzi ya utengenezaji wa filamu hapa nchini”alisema Bibi Susan.

Naye Meneja wa masuala ya Biashara wa Kampuni ya Multichoice Bw.JonsonMshana amesema kuwa Kampuni hiyo imeanzisha dawati la kusaka vipaji vyauandaaji wa kazi za filamu (Multichoice talent Factory Academy) kwa Bara laAfrika ili vijana wenye uwezo na vipaji kupata fursa ya kuongezewa maarifapamoja na kutafuta ajira kwa njia rahisi.

Bw.Jonson ameongeza kuwa Kampuni hiyo kila mwaka inatafuta vijana wanneambao wanapatikana kwa kuomba nafasi hiyo na hatimaye kufanyiwa usaili nakujiunga na wenzao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya,Ethiopia,Uganda na Nigeria.

Naye Kijana Jamal Mohamed Kishuli ambaye amejifunza “Art Designer” amesemakuwa vijana wanapaswa kujiamini katika kila wanachokifanya na kutokata tamaalakini pia zinapotokea fursa za kuonyesha uwezo wao basi wasisite kujitokeza ilikupata nafasi ya kujitangaza kupitia vipaji walivyonayo.

Vijana hao walikua katika mafunzo ya Uandishi wa Mswada (Script Writer),
Uandaaji (producer) Uongozaji (Directing) na Art Desgner ambayo wamejifunzakwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu cha Kenyata nchini Kenya.

MATUKIO YA SPIKA JOB NDUGAI YALIYOJIRI LEO KATIKA OFISI ZA BUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akisisitiza jambo wakati akikagua ujenzi wa nyumba ya katibu wa Bunge uzunguni Jijini Dodoma. Wageni wengine ni Wajumbe wa Tume ya utumishi ya Ofisi ya Bunge
 Mkurugenzi  wa Taarifa Rasmi za Bunge, Hanifa Massinga akizungumza jambo mbele ya Wajumbe wa Tume ya utumishi wa Ofisi ya Bunge wakati walipotembelea kwa ajili ya ukaguzi wa mashine mpya zilizoletwa katika Ofisi hiyo leo Septemba 12, 2019 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akizungumza jambo mbele ya Wajumbe wa Tume ya utumishi wa Ofisi ya Bunge wakati.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akisisitiza jambo wakati akikagua ujenzi wa nyumba ya katibu wa Bunge uzunguni Jijini Dodoma. Wageni wengine ni Wajumbe wa Tume ya utumishi ya Ofisi ya Bunge.
Spika wa Bunge,  Job Ndugai (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na Washindi wa Shindano la Miss Tanzania 2019, na Waandaaji wa Mashindano hayo walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BREAKING NYUZZZZZ.....: VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHADEMA WANAOKABILIWA NA KESI YA UCHOCHEZI, WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

$
0
0
VIONGOZI tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi  wamekutwa na kesi ya kujibu na wataanza kujitetea wiki ijayo kwa siku tatu mfululizo. Septemba 17,18,19 mwaka 2019

Hatua hiyo imefikwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuita mashahidi nane

 Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

habari kamili itafuata hivi punde.

DKT. NDUGULILE AWAAGIZA KUFUATILIA MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa hoteli ya Veta jijini Dodoma.

Na. Catherine Sungura –Dodoma
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee wa Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Msajili wa  Baraza la Madaktari la Tanganyika kushirikiana na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania kufuatilia mtoto aliyekatwa mkono baada ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala.

Dkt. Ndugulile ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi ya nane ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa Veta jijini hapa.

“Nilitegemea baraza la madaktari muwe mmeanza uchunguzi, kwahiyo nakupa maagizo kesi hiyo muanze kufuatilia na kama itathibitika ni uzembe waliohusika wachukuliwe hatua, ndani ya wiki mbili mtuletee majibu ili mimi na Mhe. Waziri tujue tunachukua hatua gani.

Dkt. Ndugulile amesema kwenye mabaraza bado kuna changamoto ya baadhi ya mashauri kuchukuliwa hatua hivyo kama mabaraza ya kitaakluma ni vyema kuangalia ufanisi wa majukumu yao na kuchukulia hatua pale taaluma inapokosewa na waliokosea wachukuliwe hatua. 

Dkt. Ndugulile ameitaka bodi hiyo kusimamia usajili wa maabara zote nchini kwani hivi sasa imetokea uanzishwaji wa maabara kiholela zinazotoa huduma kwa wananchi bila ya kusajiliwa hivyo kufanya ukaguzi ili kubaini maabara hizo na kuzichukulia hatua.

“Naomba sheria ifuate mkondo wake ili kubaini wale wote walioanzisha huduma za maabara bila kufuata sheria na taratibu za usajili, tushirikiane kuhakikisha kuwa hakuna taasisi au mtu atakayefungua au kutoa huduma za maabara bila kusajiliwa”. Amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema baraza hilo ni chombo muhimu na ndio moyo wa sekta ya afya kwani maabara inatoa muelekeo wa mgonjwa kwa kuthibitisha tatizo, hivyo inahitajika maboresho katika utoaji huduma za maabara. 

“Sasa hivi huduma hizi zimekua ni biashara kwani asiliamia 70 ya homa wala sio Malaria ni virusi watu wanakunywa dawa sana pasipo kuzingatia misingi kwani maabara hizi zinatumika kama sehemu ya matibabu na hata upasuaji, mtu anaenda maabara anakaa dakika kumi na tano anaambiwa ana UTI wakati mwingine anaambiwa ana malaria plasi plasi hii maana yake ni nini hili linahitaji ufuatiliaji”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Hata hivyo aliitaka bodi hiyo mpya  kusimamia ubora wa huduma za maabara  ili kuinufaisha jamii na kuhakikisha huduma za afya katika jamii zinaboreshwa kukidhi viwango vitavyotarajiwa na hivyo kuboresha afya na maisha ya watanzania.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la maabara binafsi Prof. Said Abood  aliahidi kutekeleza maagizo yote waliyopewa na Naibu waziri ikiwemo ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini maabara bubu na  ambazo hazijasajiliwa pamoja na kuhakikisha maabara zinatoa huduma zinazostahili ili kuweza kumsaidia daktari kumpatia mwananchi huduma stahili.
-Mwisho-

PCHA 1: Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokua akiongea wakati wa uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa hoteli ya Veta jijini Dodoma

TRC NA DIT ZATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA KUKUZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA HUDUMA ZA USAFIRI WA RELI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kutiliana saini ushirikiano wa mafunzo, utafiti na kuendeleza matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa mafunzo, utafiti na kuendeleza matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa mafunzo, utafiti na kuendeleza matumizi ya teknolojia, Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Prof. Preksedis Ndomba (kushoto) wakibadilishana Makabrasha ya Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kutiliana saini katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Makao makuu TRC Dar es Salaam Septemba 11, 2019.
…………………

Shirika la Reli Tanzania – TRC limetiliana saini mkataba na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam – DIT kwa lengo la kushirikiana katika kutoa mafunzo, kufanya utafiti, na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika huduma za usafiri wa reli, makubaliano yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makao Makuu TRC jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2019.

Makubaliano hayo yametiliwa saini kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Ndomba pamoja na wanasheria kutoka pande zote mbili ambapo hafla hiyo fupi imehudhuriwa na Wakuu wa Idara mbalimbali kutoka TRC, wawakilishi kutoka DIT na waandishi wa habari.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ameeleza dhumuni la makubaliano hayo ni kuwa ni kutokana na mabadiliko yanayotarajiwaa kutokea katika Shirika hususani katika huduma, amesema kuwa matumizi ya teknolojia ni muhimu kwa kuwa tayari Shirika linasimamia miradi mikubwa ukiwemo wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR, Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP na ukarabati wa Mabehewa hivyo kuwa na wataalamu wa kutosha watakaoleta chachu katika matumizi ya teknolojia ni muhimu.
“TRC tuko kwenye mageuzi na mageuzi yanakuja na teknolojia na vitu vipya, tunajenga reli ya kisasa – SGR kwahiyo tunahitaji kujua mifumo ya uendeshaji jinsi ilivyo kwahiyo sisi tumelikaribisha hili,” alisema Kadogosa

Naye Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam amesema kuwa hatua hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alizitaka taasisi, Mashirika na serikali kufanya mageuzi ya teknolojia hivyo Taasisi hiyo ikaamua kuzishirikisha taasisi, serikali na makampuni katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi wake, pia amesema kuwa TRC ni taasisi ya kimkatati kwa ajili ya kujifunza
“tunaiona TRC kwa ukubwa wake, umaarufu wake na historia yake ni darasa moja kubwa sana si kwa wanafunzi tu hata kwa wafanyakazi, TRC ni taasisi ya kimkakati ambavyo tunaweza kujifunza” alisema Prof. Ndomba

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images