Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB YADHAMINI MAONYESHO YA VIWANDA MKOA WA PWANI 2019

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo akizungumza wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) kuzungumzia udhamini wa Benki hiyo kwenye Maonyesho ya Wiki ya Viwanda mkoa wa Pwani 2019 yatakayofanyika kati ya Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2019, Kibaha Mkoani Pwani. Benki ya CRDB imedhamini maonyesho hayo kwa kutoa kiasi cha Milioni 60.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo (kulia) wakati wa kuzungumzia udhamini wa Benki hiyo kwenye Maonyesho ya Wiki ya Viwanda mkoa wa Pwani 2019 yatakayofanyika kati ya Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2019, Kibaha Mkoani Pwani. Benki ya CRDB imedhamini maonyesho hayo kwa kutoa kiasi cha Milioni 60. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mmbando (aliyesimama) akizungumza jambo wakati akitoa utambulisho kwa ugeni aliofatana nao.


HOSPITALI YA BUGANDO YAFUFUA VIWANDA VYA OKSIJENI NA MAJI TIBA

$
0
0
Na.Catherine Sungura-Mwanza

Katika kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda,hospitali ya rufaa ya kanda Bugando (BMC) imefanikiwa kufufua viwanda viwili kwa ajili ya mahitaji ya hospitali za kanda ya ziwa

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Prof. Abel Makubi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando(BMC) mwishoni mwa wiki jijini hapa.

Prof. Makubi alisema kuwa katika kutimiza hayo wamefanikiwa kufufua viwanda ambavyo vilikua vinaelekea kufa.

Alitaja viwanda hivyo ni pamoja na kiwanda cha kuzalisha oksijeni na kingine ni cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko.

"Mahitaji ya oksijeni kwa  hospitali yetu ni mitungi 4000 ila hivi sasa tunazalisha zaidi ya mitungi 2000 na lengo letu ni kuzalisha mitungi 5100.

Aidha, Prof. Makubi alisema kuwa wamepanga kuzalisha mitungi mingi zaidi ili kuweza kuhudumia  hospitali nyingine za kanda ya ziwa kwa bei nafuu na ya nusu bei.

Kwa upande wa kiwanda cha kuzalisha maji tiba ya wagonjwa mkurugenzi huyo alisema "tumefanikiwa kuzalisha maji tiba ya wagonjwa katika chupa mchanganyiko na za kutosha kwa wastani tunazalisha chupa 6000 kwa mwezi na hivyo kuokoa pesa ambazo zingetumika kununua nje".

Hata hivyo Prof. Makubi alisema wanahitaji kiasi cha shilingi bilioni tano ili waweze kuzalisha maji tiba hayo ya kutosheleza kanda yote ya ziwa  na hivyo kusaidia hospitali zingine kutonunua maji ya wagonjwa kutoka nchi za jirani.

Naye Mkuu wa kitengo cha kuzalisha maji tiba Mfamasia Fransisco Chibunda alisema  kwa sasa upatikanaji wa dawa hospitalini hapo ni asilimia 96 ukilinganisha na asilimia 60 ya nyuma.

"Katika kiwanda cha maji tiba tunazalisha aina 17 za dawa,kati ya hizo aina tisa hazipatikani kabisa kwenye soko letu".Alisema Chibunda

Chibunda alisema katika kuwahudumia wagonjwa kwa wakati wamepanua  vituo nane vya kutolea dawa kutoka vituo vinne na kituo kimoja kinahudumia kwa masaa 24.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inayo wafamasia wabobezi katika kuzalisha madawa ya aina mbalimbali.
 Mfamasia Fransisco Chibunda akiweka majitiba kwenye chupa maalum tayari kwa matumizi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando Prof. Abel Makubi akifafanua jambo kwa Maofisa Habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake (hawapo pichani) walipotembelea Hospitali hiyo.
 Majitiba ambayo tayari yameshatengenezwa katika Kitengo cha Kuzalisha Majitiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando tayari kwa matumizi.
 Mitambo ya Oksejeni ambayo mgonjwa anapata moja kwa moja ambayo imeunganishwa wodini 
Kazi ya kujenga  sehemu ambayo itasimikwa mtambo mkubwa wa Oksejini 'oxygen' inaendelea kwenye hospitali ya rufaa ya kanda Bugando

BILION 30 ZATOLEWA KILA MWAKA KWA AJILI YA HUDUMA ZA CHANJO

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo ya gari kwa Mganga Mkuu wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile Katika shughuli ya ugawaji wa magari kwa Halmashauri 61 nchini, shughuli imefanyika katika ofisi za mpango wa chanjo taifa Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya magari ya yatayosaidia shughuli za chanjo yaliyoyolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa halmashauri 61 nchini, shughuli imefanyika katika ofisi za mpango wa chanjo wa taifa Jijini Dar es Salaam .
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasha gari ishara ya uzinduzi wa magari hayo yaliyotolewa na Serikali kwa Halmashauri 61 ili kurahisisha shugchanjo nchini.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati  wa mkutano na Waandishi wa habari wakati wa kukabidhi  magari ya  chanjo kwa Halmashauri 61 ili kurahisisha shugchanjo nchini.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya waliojitokeza katika shughuli ya ugawaji wa magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 nchini uliofanywa leo na Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua moja kati ya majokofu ya kuhifadhia chanjo, ameambatana na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt Leonard Subi (wakatikati) na Meneja wa mpango wa taifa wa Chanjo Dafrosa Lyimo (wakwanza kushoto) wakati wa kukabidhi magari ya chanjo kwa Halmashauri 61 nchini.


Na WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto yatoa kiasi cha shilingi Bilion 30 kila mwaka kwaajili ya huduma za Chanjo ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa mbali mbali.

Hayo yamesemwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati akikabidhi magari 71 ya chanjo kwaajili ya Halmashauri 61, na magari 10 kwaajili ya Mpango wa chanjo nchini ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma za chanjo kwa Wananchi.

Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali imetoa magari hayo ili kurahisisha shughuli za chanjo katika maeneo mbali mbali hivyo, ameagiza magari hayo yakafanye kazi kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa.
Waziri Ummy aliendelea kusema, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa Halmashauri zote zilizobaki zinapata magari ya chanjo ili kurahisisha utendaji kazi katika maeneo yote nchini. 

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali imetoa na kusambaza majokofu zaidi ya 1300 yanayotumia umeme wa sola katika Halmashauri zote nchini, jambo lililosaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa majokofu hayo. 

“Nafurahi kwamba tumeweza kugawa majokofu Zaidi ya 1300 yanayotumia umeme wa sola, lakini uzuri wa majokofu hayo ambayo tumeyasambaza mwaka huu, yanatumia umeme wa sola, hivyo kupunguza gharama za uendeshaji majokofu ambayo kwa mwezi yaligharimu kiasi cha shilingi Elfu 50 kwaajili ya mtungi wa gesi” Alisema Waziri Ummy. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha wanawapeleka Watoto katika vituo vya kutolea huduma za Afya kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya  magonjwa ya surau na lubena. 

 “Tumeona mafanikio mazuri katika kuwekeza kwenye chanjo, ikiwemo kupunguza vifo vya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kwa mfano mwaka 2005 tulikuwa na vifo 112 katika kila vizazi hai 1000, laini sasahivi takwimu rasmi zinaonesha vifo 67” Alisema Waziri Ummy

Hata hivyo, Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchini kuhakikisha wanawafikia Watoto wote nchini walio na umri wa chini ya miaka mitano, kuwapa huduma za chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa.

“Katika kila Watoto 100 ambao wanatakiwa kufikiwa kupatiwa chanjo, tumewafikia Watoto 98, kimataifa ni Zambia na Rwanda ndio waliotuzidi, lakini lengo letu ni kuwafikia hata hao Watoto wawili waliobaki” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy Amesisitiza Serikali itaendelea kuwekeza katika masuala ya chanjo kwani zipo shahidi ya kisayansi ambazo zinaeleza kwa kuwekeza kila dola moja huokoa kiasi cha dola 16.

“Kila mwaka serikali inatupa angalau sh. bilioni 30 kwa kuwekeza katika chanjo tumeweza kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 112 katika kila vizazi hai 1000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1000 hivi sasa,” amesema.

Amesema Tanzania kupitia jitihada ilizofanya sasa hivi katika kila watoto 100 ambao wanatakiwa kupatiwa chanjo, watoto 98 wanafikiwa.

“Ni watoto wawili ambao tunawakosa Barani Afrika, Tanzania ni nchi ya tatu, tumezidiwa na Rwanda ambayo imewafikia zaidi ya asilimia 99 na Zambia tupo nao sawa kwa asilimia 98,” amesema.

Ameongeza “Lengo letu japo tupo namba tatu kwanini tunawakosa hawa wawili katika 100 ambao wanatakiwa kupata huduma za chanjo.

Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dk. Dafrosa Liymo amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha chanjo zipo na zinapatikana kwa wakati.

“Hadi sasa hatuna upungufu wa chanjo, hatua hii (kukabidhi magari) ni muhimu sana, katika utunzaji wa chanjo tunahakikisha kuna utunzaji kuanzia ngazi ya Taifa na tunahakikisha zinasafirishwa katika mnyororo baridi na zinatunzwa vizuri,” alisema.

Timu ya Vijana wa Taifa kushiriki mashindano ya Kuogelea nchini Tunisia

$
0
0
Timu ya Taifa ya vijana ya kuogelea imeondoka nchini kwenda Tunisia kushiriki katika mashindano ya Afrika ya kuogelea.

Timu hiyo inajumuisha jumla ya waogeleaji wanne ambao ni Yuki Omori anayetokea klabu ya Mis Piranhas ya mkoa wa Morogoro, Khaleed Ladha (Mwanza), Aaron Akwenda (Bluefins) na Mohameduwais Abdullatif wa klabu ya Taliss-IST.

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal alisema kuwa waogeleaji wapo tayari kuiwakilisha nchi

Katika mashindano hayo ambayo yatajumuisha waogeleaji zaidi ya 1000 kutoka bara la Afrika.

Alisema kuwa waogeleaji hao wamechaguliwa baada ya kufikia vigezo vya mashindano.

Hilal alisema kuwa timu hiyo itakuwa chini ya mkuu wa msafara, Amina Mfaume ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TSA na kocha mkuu Samwel Mtupo kutoka klabu ya Mwanza.

“Tunatarajia kupata matokeo mazuri katika mashindano hayo pamoja na ugumu wake. Watanzania zaidi ya milioni 50 wanatarajia kuona mnarejea kishujaa,” alisema Hilal.

Kocha wa timu hiyo, Mtupo alisema kuwa wanajua ushindani katika mashindano hayo na kufanya maandalizi kwa lengo la kufanya vyema.

“Tumejiandaa kwa ajili ya kushindana na tunaamini tutafanya vyema. Naamini waogeleaji waliochaguliwa ambao wana ubora wa hali ya juu, tutajitahidi kuiwakilisha nchi vizuri,” alisema Mtupo.

Nahodha wa timu hiyo, Mohameduwais Abdullatif alisema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya kushinda na siyo vinginevyo.

“Tumefanya maandalizi kwa muda mrefu kwa lengo la kuleta matokeo ambayo Watanzania watayafuraia, ” alisema Abdulatif.
 Makamu Mwenyekiti wa chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal (kushoto) akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya vijana Mohameduwais Abdullatif.
Waogeleaji wa timu ya Taifa ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, viongozi wa chama cha kuogelea na wadau mara baada ya kukabidhiwa bendera.


NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WASANII, WATU MAARUFU KUTANGAZA UTALII WETU

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amewataka wasanii na watu maarufu nchini Tanzania kutumia akaunti za mitandao yao ya kijamii kuutangaza utalii wetu.

Pia amewahakikishia kuwa Wizara hiyo ipo tayari kushirikiana nao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kupata kibali pindi wanapohitaji kurekodi kazi zao za sanaa au kwenda kutembelea hifadhi za mbuga za wanyama na utalii.

Kanyasu amesema kuna kila sababu ya kundi hilo kutumika kutangaza utalii wa Tanzania na kuongeza amekutana na wasanii na watu maarufu ili wajadili kwa pamoja nini kifanyike kuendelea kuvitangaza utangaza vivutio vya utalii hasa kupitia kundi la wasanii na watu maarufu.

"Naamini kila msanii au mtu maarufu akitumia vema akaunti yake ya mtandao wa kijamii kutangaza utalii wetu na vivutio vilivyopo tutalifikia kundi kubwa sana.Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kushirikiana nanyi katika hili kwa wale ambao watajitolea kuwa mabalozi wa utalii,"amesema Kanyasu.

Akifafanua zaidi kuhusu mikakati ya Wizara kuutangaza utalii wa Tanzania, Kanyasu amesisitiza umuhimu wa wadau wa sekta ya utalii zikiwemo hifadhi za taifa kushirikiana na wasanii na watu maarufu ili kuongeza idadi ya watalii kuja nchini kwetu.

Ametumia nafasi hiyo kuwashauri wasanii kutumia fursa hiyo kuzitangaza kazi zao za sanaa na wakati huo huo kuutangaza utalii.

“Katika nchi yetu kuna vivutio vingi na vizuri ambavyo wasanii wetu wanakila sababu ya kuvitumia katika kazi zao. Kuna wasani wa hapa hapa kwetu hawapendi kuvitangaza vivutio vyetu, wapo tayari kutangaza vivutio vya nchi nyingine.Hivyo tumewaita ili tujadiliane kwa pamoja,"amesema Kanyasu.

Amesisitiza umuhimu wa watu maarufu na wasanii kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za taifa, na wakiwa huko matukio ambayo wanayafanya wawe wanaweka picha za matukio yao katika akaunti zao za mitandao ya kijamii ili wengine waone.

“Ikitokea msanii au mtu maarufu ukienda mbuga ya wanyama ukipiga picha na kutweet ukaeleza ulipo, watu wengine watatamani kufika hapo,"amesema.

Ameongeza Wizara hiyo inaweza isiwe na fedha kwa ajili ya kuwapa wasanii na watu maarufu lakini uwezo wa kutoa kibali na kulipia usiku mmoja lakini kwa maana anayekwenda atangaze utalii wetu, wako tayari.

“Uzalendo ni pamoja na kuwa tayari kufanya chochote kwa ajili ya nchi yako na mimi niko tayari kumsaidia msanii yeyote anayetaka kwenda kufanya kazi huko aje nitamuunganisha muhimu ni kufuata taratibu,”amesema Kanyasu.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akizungunza na wasanii na watu maarufu nchini jijini Dar es Salaam kuhusu namna Bora ya kufanikisha kampeni ya kutangaza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi nchi .
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akisalimiana na moja ya wadau wa Utalii nchini wakati wa kikao kati kati yake na wasanii na watu maarufu kilichokuwa na lengo la kujadili kampeni ya kutangaza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia kundi hilo
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo(kulia) akizungunza jambo wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu na wasanii pamoja na watu maarufu.Kushoto ni Muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi
 Ofisa Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Mariam Kobero akizungumza kuhusu Wakala huo unavyotunza misitu na kuhifadhi Misitu wakati wa kikao hicho
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu(katikati aliyeva shanti nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii na watu maarufu baada kumalizika kikao hicho

RAIS DKT.SHEIN AWAPONGEZA WANAFUNZI WALIOFAULU MITIHANI YA TAIFA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akimzawadia Mwanafunzi Nasma Talib Saleh wa Skuli ya Sekondari ya SOS katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pambe Juma.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akimzawadia Mwanafunzi Wahda Mbarak Uzia wa Skuli ya Sekondari ya Fedha katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pambe Juma.

 Wanafunzi wakichukua chakula katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja na chakula cha mchana katika hafla iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akiwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaalika chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu.] 09/09/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akimzawadia Mwanafunzi Ahmad Khamis Kassim wa Skuli ya Sekondari ya Limumba katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pambe Juma.

 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja na kuwaandalia chakula cha mchana, hafla iliyotayarishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
 Mwaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja na kuwaandalia chakula cha mchana, hafla iliyotayarishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne na Sita pamoja kuwaandalia chakula cha mchana katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

PSPTB YATOA ONYO KWA WACHELEWESHAJI WA MIRADI

$
0
0
Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini PSPTB wamewataka wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini kusimamia na kutoa ushauri wa manunuzi ili kutopoteza fedha za walipa kodi pamoja na serikali hasa katika miradi ya kimkakati maana hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa usajili.

Akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema ya wataalam hao wameonekana kusababisha ucheleweshaji mkubwa wa miradi na upotevu wa fedha kwa kutotoa ushauri na kusimamia vizuri utekelezwaji wa miradi hiyo.

Amesema kuwa lazima wataalamu hao wanaosimamia masuala ya ununuzi na ugavi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia kanuni pamoja na kutoa maoni pindi wanaposhauri michakato ya ununuzi na pindi maoni yao yanapopingwa watoe taarifa ili kuokoa miradi ambayo serikali imeelekeza kwa wananchi.

Vilevile amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na sio kusubiri malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya serikali ambayo imetekeleza kila kitu ila watendaji ndio wanaokwamisha mlolongo mzima wa utekelezaji.

Mbanyi amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli inafanya kazi kwa vitendo zaidi hivyo watendaji lazima waendane na kasi hiyo ili kujenga Tanzania ya viwanda na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.
 Mwezeshaji Aziz M. Kilonge akitoa mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi waliofika kwenye mazunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB) yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya Siku tano yaliyoandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB).

JAJI MSTAAFU THOMAS MIHAYO AWABANA WASANII, SHETTA ASHINDWA KUVUMILIA

$
0
0
Na said Mwishehe,Michuzi TV

MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Jaji mstaafu Thomas Mihayo amewabana wasanii na watu maarufu ambao wenyewe hawako tayari kuutangaza vivutio vya utalii hadi wapewe fedha au posho na Serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, wasanii, watu marufu na wadau wa sekta ya utalii nchini Jaji Mihayo amesema kuna wasanii bila kulipwa fedha hawataki kutangaza utalii.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuangalia namna ya kufanikisha kampeni ya kuutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia kundi hilo la wasanii na watu maarufu.

Amesema mbele ya wasanii hao kuwa anakerwa sana na watu ambao wanaoomba kuwezeshwa kwenda kwenye vivutio vya utalii."Hivi ukifanya tamasha ukaweka kiingilio cha Sh.5000 hupati fedha za kwenda huko? 

"Hili ni suala la uzalendo lakini nashindwa kuelewa kwanini hamjiamini kuwa mnaweza kufanya kitu kikubwa kupitia majina yenu".

Amesema haoni sababu ya msanii kupewa fedha ndipo ashiriki kufanya jambo la uzalendo kwa nchi yake na kuongeza wasanii wanao uwezo mkubwa wa kutumia sanaa yao kupata fedha ikiwemo fedha ya kumuwezesha kwenda katika vivutio vya utalii kufanya kazi zake au kupumzika.

“Watanzania wenyewe tuwe na hamu ya kuifahamu nchi yetu na kuwa mabalozi wa kuwaambia watu wengine kuhusu vitu vizuri vinavyopatikana hapa,”amesema Jaji Mihayo.Kwa upande wake Msanii wa Bongo Fleva Nurdin Bilal a.k.a Shetta ametumia nafasi hiyo kueleza mazingira magumu yaliyopo nchini pindi msanii anapohitaji kuredi kazi yake katika hifadhi za taifa na maeneo ya utalii.

Amesema kuwa ndio maana wengi wanakwenda kuredi nje ya nchi ambako kuna mazingira mazuri na mpangilio ambao unaeleweka wa msanii kufanya kazi."Kuna nyimbo ambayo nilienda kurekodi Dubai siku za karibuni.Nilieleza yale ambayo nahitaji yawepo katika nyimbo nikaambiwa gharama yake ni dola 200, hivyo nikalipa na kazi ikaenda haraka tu maana hakuna kucheleweshana kwa kuwa kila kitu kinaeleweka.

"Huku kwetu mazingira bado hajakaa vizuri, hivyo ni vema Wizara ikaweka utaratibu ili msanii anapohitaji kufanya kazi yake iwe rahisi,"amesema Shetta.Awali akizungumza kwa niaba ya wasanii, Msanii Mwijaku ametoa rai kwa wasanii wenzake kujitolea kuwa mabalozi wa kutangaza kazi zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo bila kutegemea kulipwa.

Wakati Msanii mkongwe katika muziki wa kizazi kipya nchini Seleman Msindi a.k.a Afande Sele amezungumzia umuhimu wa wasanii kuimba nyimbo ambazo zitahamasisha utunzaji mazingira na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda a.k.a Fid Q akisalimiana na Peter Msechu baada ya kukutana katika kikao kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu kujadili kampeni ya kutangaza Utalii ndani na nje ya nchi kupitia wasanii na watu maarufu
Ofisa Masoko kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Mariam Kobero akifuatilia majadiliano kati ya wasanii ,watu maarufu na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo(wa pili kulia waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu pamoja na wasanii

KADA CCM AVAMIWA DAR, AKATWAKATWA MAPANGA KICHWANI, ATUPWA BARABARANI

$
0
0
*Ni yule aliyegombea ubunge jimbo la Vunja..
*Akutwa roud about ya Kawe akiwa hajitambui


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia amewahi kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Inocent Shirima amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga kichwani akiwa karibu na nyumbani kwake eneo la Goga Kinzugi jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa Shirima anaendelea kupata matibabu katika moja ya Hospitali iliyopo jijini Dar es Salaam ili kuokoa maisha yake kutokana na hal yake kutokuwa nzuri kiafya.

Akizungumza na Michuzi Blogu leo Septemba 9,2019 kwa njia ya simu Shirima ameelezea hatua kwa hatua tukio la kuvamiwa kwake a kisha kujeruhiwa kwa kukatawa mapanga kichwani ambapo amesema tukio hilo lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita saa tano usiku.

Amesema kuwa akiwa anarejea nyumbani , umbali wa mita 300 kutoka katika nyumba yake kulikuwa na watu wenye bodaboda na mmoja alikuwa amesimama barabarani kama vile anatengeneza bodaboda na alipofika eneo hilo alisimamishwa kama anaombwa msaada.

"Kwa ilikuwa ni maeneo ya karibu na nyumbani sikuwa na wasiwasi, hivyo nikasimamisha gari yangu , baada ya kufungua kioo cha gari nikashtukia nimepigwa na kitambaa usoni.Hiyo ilitokea hata kabla ya kuuliza kuna kitu gani.

"Baada ya hapo inaonekana walichukua gari na kuanza kuzunguka na mimi hadi saa saba usiku.Walinipiga kwa mapanga na nadhani waliamini wameshaniua, hivyo wakaenda kunitelekeza katika eneo la round about ya barabara ya Kawe.Lengo lao ilikuwa ni kuniweka hapo ili nigogwe na gari itakayopita,"amesema Shirima.

Ameongeza kuwa wakati wanafanya hayo yote hakuwa anajitambua kwani alishapoteza fahamu na ndio maana waliokuwa wanafanya unyama huo waliamini ameshakufa."Wamenikata mapanga, wakaniburuza kwenye lami na kisha kunitelekeza nije nigongwe na gari."

Amefafanua kuwa baada ya kumjeruhi na kumuacha eneo hilo, watu hao wamechukua fedha zake Sh.milioni 11 ambazo alichelewa kuzipeleka katika duka la saruji kwani anajihusisha na biashara ya kuuza tofali.Pia wamechukua flashi mbili,simu ya mkononi la laptop.

Hata hivyo amesema kuwa baada ya kutupwa eneo hilo, kuna vijana wengine wa bodaboda wa maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumuona akiwa hapo walisimamisha bodaboda zao kwa ajili ya kumpa msaada na hata wao walikuwa wanajua ameshakufa.

"Walidhani ni maiti na baada ya kuniona napumua ndipo waliponchukua na kunipeleka Hospitali ya Kairuki ambapo pale nilifanyiwa opereshani kwa saaa nane,"amesema Shirima.

Alipoulizwa kwa sasa hali yake ikoje ?Amejibu hali yake bado mbaya na kuna eneo ambalo amehifadhiwa akiendelea kupata matibabu.Hata hivyo amesema kwa kuwa yeye ni mwanasiasa kuna maswali mengi anajiuliza katika tukio hilo.

"Kama ni majambazi walishanidhibiti na nikawa sijitambui kwanini watake kuniua kwa kunikata mapanga kichwani?Ndani ya gari kulikuwa na vitu muhimu zaidi wameacha, kulikuwa na nyaraka muhimu hawakuchukua, kwanini? Hili tukio linaleta wakati mgumu kwangu na familia yangu ambayo kwa sasa haina amani kabisa,"amesema Shirima.

Amesema kama lengo lao ni kumuua maana yake wataendelea kumtafuta tena kwani walichotarajia sicho ambacho kimetokea."Waliamini wameniua , lakini niko hai unadhani nini ambacho kitaendelea?"

Alipoulizwa kama tayari Polisi wanafahamu tukio hilo, Shirima amejibu Polisi wanazo taarifa na amesikia wanaendelea na uchunguzi lakini yeye kama yeye bado hajahojiwa na polisi kuhusu tukio hilo ikiwa pamona na kuchukua maelezo yake.

Alipoulizwa anahisi nini kutokana na tukio hilo, amejibu hana jibu la moja kwa moja lakini kwa kuwa yeye ni mwanasiasa huenda ndani yake imeingia siasa 

"Tukio hili lina mambo mengi, katika uchaguzi uliopita niligombea ubunge na kushika nafasi ya pili.Nakumbuka wakati wa uchaguzi kule nyumbani Moshi watu walivamia nyumba yangu, walimkuta baba yangu mdogo ambaye walimuua kwa kumchinja,"amesema Shirima.

Amesema anakumbuka siku hiyo alipanga kusafiri lakini alibadili safari , hivyo waliovamia nyumba yake waliamini yupo lakini baada ya kufika wakamkuta baba yake mdogo na ndipo walipoamua kumuua.

"Mawazo yangu nahisi hili tukio lina siasa na sasa tunakwenda kwenye uchaguzi sijui nini kitatokea tena.Siamini katika ujambazi maana kama ni majambazi walishanidhibiti iweje wanipige mapanga,"amesisitiza Shirima.

UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BIL. 32.7 KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 13, sawa na sh. bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama Tumaini la Mama.

Hafla ya utiaji saini mkataba wa msaada huo imefanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James kwa niaba ya Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov.

Msaada huo ni kwa ajili ya kutekeleza awamu ya tatu ya mradi huo unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo umelenga kuwapatia huduma akima mama na watoto wanaotoka katika kaya masikini

Alisema kupitia mradi huo pia vifaa tiba vinavyohusiana na afya ya uzazi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 900 katika vituo vya Afya vilivyoko katika mikoa iliyochaguliwa kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya vimetolewa.

Mradi huu ulianza mwaka 2012 ambapo Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) ilitoa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 25.5 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 2 Desemba 2009. 

“Awamu ya pili ya mradi ilianza mwaka 2016 ambapo Ujerumani ilitoa msaada wa Euro milioni 20 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 48.2 kupitia mkataba uliosainiwa tarehe 15 Machi 2015. Siku ya leo Serikali yenu imeahidi kupitia mkataba huu, kutoa msaada mwingine wa Euro milioni 13 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.4 kutekeleza awamu ya tatu ya mradi, tunaishukuru sana,” alisema Bw. James. 

James alisema mradi huo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba unaongeza nguvu katika juhudi za Serikali za kupunguza vifo vya mama na mtoto lakini pia kuongeza tabia ya kutumia bima ya afya kwa watanzania na hii inaenda sambamba na awamu ya Pili ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na awamu ya Tatu ya MKUZA. 

“Kwa mfano, katika awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Serikali imelenga kwamba, hadi mwaka 2020: Vifo vitokanavyo na uzazi vipungue kutoka 454 mwaka 2015 hadi 250 katika kila vizazi hai 100,000; muda wa kuishi uongezeke hadi miaka 66 kutoka miaka 56; na maambukizi ya VVU na UKIMWI yapungue kutoka asilimia 9 hadi 3,” alisema .

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani Dkt. Annika Calov alisema nchi yake inajivunia uhusiano mzuri na Tanzania na kwamba mradi huo wa Tumaini la Mama umelenga kuboresha afya akina mama wanaotoka katika familia maskini.

“Lengo kubwa ni kuboresha afya za mama na mtoto na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kwa kuanzia mradi huu umekijita katika mikoa mitano ya Mbeya, Songwe, Tanga, Lindi na Mtwara,” alisema Calov.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga alisema tangu mwaka 2012 mradi ulipoanza, jumla ya akinamama 1,157,191 wamenufaika na bima ya afya kupitia NHIF na kaya maskini 627,000 zimenufaika na huduma za CHF kwa kulipiwa ada za kujiunga. 

“Akina mama na watoto wao wanapatiwa huduma kwa njia ya bima ya afya kupitia vituo vya afya 1097 vilivyoko katika mikoa hiyo iliyolengwa pamoja na mfuko kutoa vifaa tiba kwenye vituo,” alisema Konga. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) hapa nchini Dkt. Anna Calov (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga wakionesha Mikataba ya msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akitia saini Mkataba wa msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. Kushoto ni Mkurugenzi wa KFW nchini, Dkt. Anna Calov na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akitia saini Mkataba wa msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) wa Euro milioni 13, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama “Tumaini la Mama. Kushoto ni Mkurugenzi wa KFW nchini, Dkt. Anna Calov na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) Bw. Bernard Konga. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango) 

WAFANYABIASHARA 10 WA NADINI WAFIKISHWA KORTINI,WASOMEWA MASHITAKA YA UHUJUMU UCHUMI,UTORASHAJI MADINI

$
0
0
Wafanyabiashara 10 wa madini wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya ambako watano kati yao wamesomewa mashtaka tofauti ya uhujumu uchumi ikiwemo utoroshaji wa madini .

Katika kesi ya kwanza ambayo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Andrew Scoout inawahusu watumiwa watatu ambao ni Mike Konga, Sauli Solomon na Emmanuel Kessy ambao wamesomewa mashtaka matatu.

Akiwasomea mastaka yao Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe amesema shitaka la kwanza ambalo linawahusu watuhumiwa wote watatu ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alisema kuwa kati ya Juni Mosi na ‪Juni 30‬, mwaka huu watuhumiwa hao walijipatia fedha za Zambia kiasi cha Kwacha 290,000 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa raia mmoja wa Zambia kwa kumuuzia dhahabu.

Wakili na Namkambe alisema kosa la pili la watuhumiowa hao ni utakatishaji wa fedha kiasi cha kwacha 290,000 ambazo walizipata kwa udanganyifu kutoka kwa raia wa Zambia.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakam hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na Wakili Namkambe akadai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Andrew Scoult akaailisha kesi hiyo hadi ‪September 23‬ itakapotajwa tena mahakamini hapo.

Katika kesi ya pili, watuhumiwa wawilI, Mike Konga na Sauli Solomoni wamesomewa mastaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha mbele ya Hakimu Denis Luwongo.

Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe ameiambia Mahakama kuwa watuhumiwa kwa pamija kati ya Juni Mosi na ‪Juni 30‬ mwaka huu walijipatia fedha kiasi cha dola za Marekani 115,000 kwa njia ya udanganyifu baada ya kumuuzia Henry Clever, raia wa Ujelumani amdini aina ya dhahabu kilo moja.

Wakili Namkambe alisema kosa la pili la watuhumiwa hao ni kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 115,000 ambazo walizipata kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa raia wa Ujerumani aitwaye Henry Clever.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa vile Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakalika na akawasilisha maombi ya kutaka baada ya kuahilishwa kwa kesi hiyo, Mtuhumiwa wa Pili, Sauli Solomon achukuliwe na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi.

Maombi hayo yalisababisha mvutano na wakili wa utetezi Baraka ambaye alisema kuwa mteja wake alikamatwa tangu Septemba Mosi mwaka huu na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa mahojiano na muda wote huo alikuwa mikononi mwa Polisi, hivyo ni vema apelekwe gerezani na kama watamuhitaji kwa upelelezi wamfu

Hata hivyo Wakili wa Serikali, Namkambe alisema kuwa ombi lake ni sahihi kwa vile hata kama ni kumfuata huko ni lazima Mahakama itoe idhini hivyo ni busara aruhusiwe kwenda Polisi ili kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo kuepuka malalamiko yanayoweza kujitokeza baadaye kuhusu upelelezi kuchelewa kukamilika.

Hakimu Denis Luwongo akatoa uamuzi wa kuruhusu mshtakiwa kuchukuliwa na Polisi kwa ajili ya upelelezi na kuahilisha kesi hiyo hadi ‪September 23‬, mwaka huu.






MBUNGE MGIMWA KUTATUA KERO YA MAJI KIJIJI CHA IHANZUTWA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa sambamba na diwani wa kata ya Sadan wakati akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ihanzutwa kwenye ziara ya kawaida jimboni 
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Sadan wakifurahia ujenzi wa ubora uliojengwa katika darasa la shule ya msingi Ihanzutwa kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Hili ni moja kati ya madarasa yaliyojengwa kwenye ubora wa hali ya juu kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo na watoto wa kijiji cha Ihanzutwa mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wa Ihanzutwa wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ihanzutwa na kukosekana kwa maji safi na salama katika kijiji hicho hivyo wamemuomba mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini kusaidia kutatua kero hizo.

Wakizungumzana kwenye mkutano wa hadhara,wananchi hao wamesema kuwa wanashukuru kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini bado wanakabiliwa na ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasani katika shule hiyo.

“Sambamba nashukrani za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi za walimu na ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa kwa fedha za serikali lakini bado tunaomba kusaidiwa ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani” walisema wananchi 

Aidha wananchi wa kijiji cha Ihanzutwa walisemakuwa wanakabiriwana uhaba wa maji kwa miaka mingi hali inayosababisha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji hivyo walimuomba mbunge wa jimbo hilo kuwatafutia njia ya kutatua tatizo hilo

Akijibu maswali ya wananchi mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amesema kuwa ameipokea changamoto hizo na atazifanyia kazi kwa kushirikianana wadaumbalimbali.

“Leo nikitoka hapa nitaendeleza mazungumzo na TANAPA ili waendelee kutusaidia kama ambavyo wametusaidia katika ujenzi wa madarasa na madarasa yaliyojengwa katika kijiji hiki huwezi kuyapata kijiji chochote kile kwa kuwa wanaubora wa aina yake” alisema Mgimwa 

Aidha Mgimwa amesema kuwa amewapata wadau ambao watasaidia kutatua kero ya maji kwakuchimba kisima kimoja katika kijiji hiki cha Ihanzutwa.“Tunamarafiki zetu wa Water For Africa ambao wametuahidi kutuchimbia kisima kimoja kirefu kwa lengo la kutatua changamoto hii ya maji katika kajiji hiki” alisema Mgimwa

PSS FORUM YAWEKA MIKAKATI YA ULINZI KWA WATOTO AFRIKA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REPPSI Lynette Mudekunye na Mwenyekiti wa Bodi ya REPPSI Tanzania wakiwa kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia.
Mkurugenzi Mkazi wa REPPSI Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia
wadau na viongozi wakiwa kwenye kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia



Tumaini Godwin, Namibia


Nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zinaweza kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia.

Profesa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Hosea Rwegoshola amesema hayo wakati akiwasilisha utafiti wake kuhusu kuimarisha malezi mbadala ya watoto, katika mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto (PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.

Profesa Rwegoshola amesema kupitia utafiti alioufanyia katika kata ya Chanika jijini Dar es Salaam, watoto wanaweza kuwa salama ikiwa ulinzi wao utaanza kuimarishwa kuanzia ngazi ya familia.

"Kwa hiyo matokeo ya utafiti wangu ni kwamba familia mbadala zinaweza kusaidia malezi ya watoto, na hizi zikiimarishwa tatizo la watoto mitaani linaweza kupungua, ukatili majumbani utakoma," amesema.

Ametaja familia mbadala kuwa ni pamoja na ndugu wa ukoo kulea watoto, walezi wakujitolewa na wale wanaorithi watoto kisheria.Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF)nchini Namibia Rachel Odede amesema mazingira bora ya mtoto kukua ni kwenye familia.

"Mamilioni ya watoto wameachwa nyuma kwenye malezi na takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watano analelewa bila familia, mtoto anatakuwa kukua kwa furaha," amesema Odede.

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) Tanzania Edwick Mapalala amesema ulinzi wa mtoto unapaswa kuanzia ngazi ya familia.

HALMASHAURI ZIHAKIKISHE MAGARI HAYA YANATUMIKA KWA SHUGHULI ILIYOKUSUDIWA-WAZIRI WA AFYA

WAHITIMU SHAHADA ST. JOSEPH, TANZANIA WASAFIRISHWA ITALIA KWA MASOMO YA URUSHAJI SATELLITE YA KWANZA NCHINI

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Wahitimu wawili wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania (Bachelor in Electronics and Communications Engeneering) wamesafiri kuelekea nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kuendelea na masomo yao ya Shahada ya Uzamili.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3), Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Innocent Ngalinda amesema Wanafunzi hao wanaenda Italia kujifunza namna yakurusha Satellite wakati Tanzania ikijiandaa kufanya hivyo, amesema hivi karibuni Wanafunzi wengine Kumi wataelekea India kujifunza masuala hayo.

Prof. Ngalinda amesema Wahitimu wengine wataenda nchini India kujifunza masomo hayo yaurushaji wa Satellite angani, kutokana na India kuongoza katika kurusha Satellite nyingi duniani.

Pia amesema Wahitimu hao wanaenda masomoni Italia ikiwa ni mpango wa ushirikiano wao na Vyuo vya nje ya nchi katika kuwapeleka Wanafunzi kusoma masuala mbalimbali bila gharama yoyote kuhakikisha Tanzania inafika katika Uchumi wa Viwanda kwa vitendo.

Prof. Ngalinda amewataka Wanafunzi wengine chuoni hapo kusoma kwa bidi ili kufika malengo yao kwa wakati sahihi kama walivyofanya wenzao wanaoelekea Italia na India.

Kwa upande wa Penina Mbwilo ambaye ni mmoja wa Wahitimu wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania amesema ilikuwa ndoto kwake kumaliza masomo ya Shahada nakuendelea na masomo ya juu zaidi.

Penina amewaasa Wanafunzi wenzake kusoma kwa bidii sambamba nakufaulu vizuri darasani ili kufikia malengo yao kama yeye alivyofikia, amesema pia ili kufika malengo hayo Mwanafunzi anapaswa kujiongeza katika masomo yake, nidhamu na utii.Amesema malengo yake kupata ujuzi zaidi na kuwasaidia wengine katika ujuzi huo kwa kuwafundisha ili na wao kupata nafasi kama aliyopata yeye.

Naye Frank Charles aliyehitimu Shadaha hiyo ameshukuru kupata nafasi hiyo kuelekea kusoma nje ya nchi sambamba na kuongeza ujuzi katika msomo hayo ambayo yatasaidia Taifa, pia amesema anaenda kujifunza kwa Mataifa mengine masuala ya mawasiliano namna ambavyo mataifa hayo yameendelea katika Sekta hiyo.

Wahitimu hao wanaelekea nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kutokana na kusoma, ufaulu mzuri katika masomo yao hivyo kuchaguliwa kuwakilisha wengine nchini humo. Wahitimu wengine wanaelekea nchini India kwa masomo hayo na kurusha Satellite ya kwanza nchini Tanzania.
Penina Mbwilo ambaye ni mmoja wa Wahitimu wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya safari yao
Frank Charles aliyehitimu Shadaha hiyo akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya safari yao ya nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kwa ajili ya masomo.
Wahitimu wawili wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania (Bachelor in Electronics and Communications Engeneering) wakiwa katika picha ya pamoja na Ndugu, Jamaa na marafiki kabla ya safari.

WAFANYABIASHARA KUJIPATIA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0


Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WAFANYABIASHARA wengi zaidi kujipatia Leseni za biashara zao kwa njia ya mtandao Oktoba mwanzoni wakiwa huko waliko, huku wakitumia kompyuta na simu zao.

Akizungumza na waandishi wa haari Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andrew Mkapa wilayani Chalinze leo amesema kuwa mafunzo yanayotolewa leo ni kuwajengea uwezo wa watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili kuweza kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao ili kuwasaidia wafanyaiashara kujipatia Leseni hizo kiusahisi.

"Mafunzo haya yanawajengea uwezo wezeshi watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu uanze kutumika kwa majaribio mfumo katika kutoa leseni za biashara kwa njia ya mtandao kwa wafanyabiashara wote nchini".

Amesema kuwa serikali imetoa uamuzi wa kutoa leseni kwa njia ya mtandao kupitia kifungu cha sheria ya biashara namba 25 ya mwaka 1972 zianze kutolewa kwa njia ya mtandao ikiwa Halmashauri sita zimeteuliwa kwaajili ya kutoa mafunzo ya utoaji leseni ya kibiashara kwa njia ya mtandao.

Mfunzo hayo ya utoaji Leseni kwa njia ya mtandao yanatolewa kwenye halmashauri sita nchini ambazo ni Ilala, Chalinze, Mfinga, Mwanza, Bukoba na Karagwe.

Amesema utoaji wa Leseni kwa njia ya mtandao utasaidia kwa urahisi serikali kukusanya mapato, Kupunguza gharama kwa halmashauri zote nchini na kupunguza ghara za kupata Leseni za kibiashara kwa wafanyabiashara.

Licha ya kutoa mafunzo kwa watendaji wa halmashauri zilizoteuliwa hapa nchini changamoto ni uelewa wa wafanyabiashara kwenye mambo ya mtandao.


Ufunguzi wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao utakapozinduliwa hapo mwanzoni mwa Oktoba leseni zitapatikana kupitia websiti ya www.business.go.tz
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andrew Mkapa akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chalinze leo wakati wa utoaji mafunzo ya kuwajengea uwezo wa watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili kuweza kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao.
Aliye simama ni Afisa Tehama kutoka Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Samwel Maregeri akitoa mafunzo wa watendaji wa halmshauri ya manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za kibiashara kwa njia ya mtandao. 
Afisa Biashara wilaya ya Chalinze, Zamzam Meja akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipewa mafunzo ya mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa Utoaji wa Leseni za kimbiashara kwa njia ya mtandao utasaidia sana katika kutunza muda pamoja na wafanyabiashara hawatapoteza fedha kwaajili ya kufata huduma za utoaji leseni zinapopatikana.
 Afisa Biashara halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Samson Moris akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Chalize leo wakati wakipewa mafunzo ya utoaji leseni mpya za kibiashara kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa wataweza kuwahudumia watu wengi zaidi hukohuko waliko na wataweza kupata leseni kwaajili ya kuzitumia katika kufanya biashara zao.
Afisa Tehama wilaya ya Chalinze, Sabuni Joseph akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chalinze leo wakati wakipewa mafunzo ya utoaji Leseni Mpy za kibiashara kwa njia ya Mtandao. amesema kuwa amesema kuwa mafunzo hayo ya kutoa Leseni kwa njia ya mtandao yamekuja muda muafaka kwa wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipata adha ya kutembea umbali mrefu wakifuata huduma ya kupata Leseni sasa mfumo mpya utawarahisishia kupata Leseni wakiwa hukohuko waliko.
 Watendaji na maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze wakipatiwa mafunzo ya utoaji wa Leseni Mpya za Biashara.

Kulia aliyesimama Afisa Tehama kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Samwel Maregeri akitoa mafunzo wa watendaji wa halmshauri ya manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za kibiashara kwa njia ya mtandao.

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUTOKEA KWA TETEMEKO LA ARDHI KATIKA MKOA KATAVI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MADINI

TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA (GST)

Mnamo tarehe 9/09/2019 majira ya saa 9:38 usiku kumetokea tetemeko la ardhi katika kijiji cha Sibwesa Kata ya Sibwesa karibu na ziwa Tanganyika katika mkoa wa Katavi Wilayani Mpanda DC (Wilaya ya Tanganyika). Taarifa zilizokusanywa na kuchakatwa kutoka kwenye kituo cha kuratibu matetemeko ya ardhi kilichopo Dodoma katika ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), zinaonesha kuwa tetemeko hilo lina ukubwa wa 5.5 katika kipimo cha Ritcher. Kitovu cha tetemeko hilo  kipo umbali wa kilometa 35.5 Kusini– Magharibi ya mji wa Mpanda kwenye latitude 6.47°S na longitude 30.77°E.  Eneo hili lipo katika ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki, mkondo wa Magharibi ambao ni njia kubwa ya matetemeko ya ardhi. 
Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mashuhuda mbalimbali, tetemeko hili limesikika katika maeneo ya miji ya Mpanda, Mpanda DC na Sumbawanga, 
Ukubwa wa tetemeko hili la ardhi kitaalamu ni tetemeko linaloweza kuwafanya watu waliolisikia kukimbia kwa hofu toka nje ya majengo, kusababisha uharibifu wa majengo kutegemeana na ubora wa majengo hayo. 
Hadi sasa, GST imepokea taarifa ya baadhi ya nyumba kuwa na nyufa katika Kata ya Sibwesa na nyumba mmoja katika Kata ya Mishamo kijiji cha Isenga  imebomoka na kujeruhi mtoto. 
GST inaendelea kuwatahadharisha wananchi juu ya kuzingatia ujenzi wa nyumba imara zinazoweza kukabiliana na athari za matetemeko ya ardhi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. Pia wananchi wanaombwa kuacha kutaharuki wakati wa tetemeko kwa kukimbia kwani inaweza kusababisha madhara mengine ya kuumizana na kupata mshtuko.

Imetolewa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania
9/09/2019

KIWANDA CHA TANICA CHAZIDI KUPAA ZAIDI

$
0
0
 Meneja Mkuu wa kiwanda cha TANICA, Linus Leopord  kilichoko mkoani Kagera
Kiwanda cha kahawa TANICA kilichoko mkoani Kagera

Na  Eben-Ezery   Mende
KIWANDA cha Tanganyika Instant Cofee Co. Ltd (TANICA) kilichohujumiwa na kusababisha kubadilishwa uongozi wa kiwanda hicho sasa kiko kwenye hatua za mafanikio kwa asilia 89.

Akizungumza na   Michuzi Blog,  Meneja Mkuu wa TANICA, Linus Leopord amesema waliokihujumu kiwanda hicho na kusababisha kufukuzwa kazi wanatapatapa kukichafua kiwanda hicho lakini hawawezi kwani mafanikio ya uzazishaji yanapanda kila siku.

Leopord amesema kiwanda hicho kilichoko mkoani, Kagera kinachozalisha kahawa ya unga (instant coffee) na kahawa ya kukaanga (roasted coffee) tangu mwaka 2012 hadi 2017 kilikuwa kikiendeshwa kwa kutengeneza hasara ya wastani wa sh. milioni 576 kwa mwaka.

Aidha amebaibisha kuwa baada ya kufanyika uchunguzi na viongozi waliohusika kusababisha hasara hiyo kufukuzwa kazi kumekuwepo vurugu na hujuma mbalimbali za kutaka kiwanda hicho kiporomoke lakini jitihada hizo zimegonga mwamba.

Amesema kiwanda hicho kwa msimu wa 2018/2019 kimepata mapato ya sh. bilioni 7.6 ambayo ni asilimia 85 ya bajeti ya kampuni hiyo kwa mwaka.

Kwa mujibubwa, Leopord TANICA inampango wa kutoa gawio kwa faida iliyopatikana ambayo ni sh. milioni 330 ikilinganishwa na faida iliyopatikana mara ya mwisho mwaka 2012 ya sh. milioni 10.

Amesema menejimenti ya awali iliyokuwa inakihujumu kiwanda hicho ilisababisha hasara ya deni la sh bilioni 3 ambapo hadi sasa TANICA imeshalipunguza deni hilo na kubaki sh bilioni 1.4.

Hata hivyo, Leopord amesema viongozi waliofukuzwa kazi kutokana na hujuma hizo wamekuwa wakisababisha atumie muda mwingi kujibu malalamiko yao ikiwemo mashauri mahakamani badala ya kuutumia muda huo kuendeleza mipango ya maendeleo ya kiwanda.

Alisema TANICA inampango wa kuongeza kipato chake kutoka sh bilioni 3-5 cha awali na kufikia sh bilioni 13 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

TANICA ni kampuni binafsi iliyosajiliwa chini ya sheria ya kampuni mwaka 1963 na kuanza uzalishaji rasmi mwaka 1967 baada ya kuzinduliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Soko kuu la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha TANICA liko, Uganda, Dubai, China na Uholanzi.

Wamiliki wa kiwanda hicho ni Serikali/hazina, vyama vya ushirika ikiwemo Kagera cooperative union, (KCU) Karagwe District Cooperative union (KDCU) na Shirikisho la vyama vya Ushirika (TFC).

MCHUNGAJI NA WAKE ZAKE WAWILI WAHUKUMIWA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33), akiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kabla ya kusomewa humumy ya kwenda jela mwaka mmoja ama kulimba faini ya shilingi milioni moja.
Wake wa mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
MCHUNGAJI  wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33), wake zake wawili na mdogo wake, wamehukumiwa kulipa faini ya ya jumla ya Sh. Milioni tano ama kwenda jela miaka miwili baada ya kukiri kosa la kuingia nchini na kufanya kazi ya kichungaji bila ya kuwa na kubali cha makazi. 

Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 10, 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando baada ya washtakiwa wenyewe kukiri makosa na kuongeza kuwa baada ya washtakiwa hao kulipa faini au kutumikia kifungo hicho watuhumiwa hao ambao ni raia wa Kongo wanatatakiwa kurudishwa nchini kwao.

Akifafanua adhabu hiyo, Hakimu Mmbando amesema, katika shtaka la  kwanza washtakiwa wote kwa pamoja wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja na katika shtaka la pili linalomuhusu mchungaji peke yake amehukumiwa kulipa faini ya  Sh. milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja.

Kwa maana hiyo,  mchungaji  peke yake anahukumiwa kulipa faini ya Sh, milioni mbili ama kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.
Washtakiwa wengine ni wake wa Mchungaji ni Esther Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) na Mshtakiwa mwingine mdogo wa Mchungaji, Samuel Samy (22).

Mapema, wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji Godfrey Ngwijo  akisaidiana na Sitta Shija, waliwakumbushia washtakiwa mashtaka yao na walidai kwamba, Septemba 2 mwaka huu eneo la Salasala Kilimahewa, Dar es Salaam, mchungaji huyo na wenzake walibainika kuingia nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa mchungaji huyo pekee alibainika  kujihusisha na kazi za kanisa akiwa hana kibali cha makazi.

 Hata hivyo, kabla ya kusomewa adhabu yao washtakiwa wote waliomba mahakama iwasamehe, isiwape adhabu kali, Mchungaji amesema kazi alivyokuwa akiifanya ya kuhudumia jamii si biashara pia kusimamia sheria.

UNESCO na Ireland kushirikiana na Serikali kufanikisha Africa Code Week Tanzania

$
0
0
SERIKALI ya Tanzania imeishukuru UNESCO na serikali ya Ireland kwa kufadhili programu ya kuwaendeleza vijana wa kitanzania kidigitali.
Programu hiyo, Africa Code week In Tanzania, imelenga kuwezesha vijana sio tu kujua dunia ya digitali lakini pia kuwa na uwezo wa kubuni na kutengeneza programu mbalimbali zinazogusa teknolojia ya digiti.

Akizungumza wakazi wa uzinduzi wa programu hiyo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha alisema msaada huo wa serikali ya Ireland  ni muhimu kuwawezesha vijana wa Tanzania kupata mafunzo ya tehama ili kusaidia katika mipango ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Naibu Waziri Ole Nasha  alisema pamoja na kushukuru Ireland kwa kukubali kudhamini programu hiyo aliwasifu COSTECH na programu yake ya atamizi ambayo inachochea fikira za vijana katika matumizi na maendelelo ya teknolojia hasa upande wa digiti.
Alisema kitendo cha Ireland kusaidia programu hiyo inaamananisha kwamba inasaidia taifa la Tanzania kujenga uwezo wa matumizi ya teknolojia katika dunia ya viwanda na kuwawezesha vijana kutengeneza uwezo wa kujiajiri.

Awali katika uzinduzi huo Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock alisema nchi yake imeamua kutoa msaada huo kutokana na kuelewa umuhimu wa kuendeleza vijana ambao ndio wajenzi wa uchumi wa taifa hili kwa miaka mingi ijayo.
Alisema wanaamini kwa kuwa na vijana wengi wenye uwezo wa teknolojia watakuwa wamesaidia kuleta mapinduzi makubwa ya viwanda na pia kutengeneza idadi kubwa ya vijana wenye uwezo mkubwa wa kufanya shughuli zao kisayansi hasa kwenye upande wa uzalishaji.

Alisema kwa miaka ijayo, dunia itategemea zaidi teknolojia ya dijiti kufanya utatuzi mbalimbali wa masuala muhimu yanayohusu uchumi na jamii hivyo vijana zaidi ya milioni 15, wanaotarajiwa kuwapo nchini ifikapo mwaka 2030 watakuwa  ni nguvu kubwa kwa nchi ya Tanzania kama watakuwa wanakwenda sambamba na teknolojia ya digiti.

Alisema kwa kuielewa tehama vijana wengi watakuwa wametanzuka na changamoto ya ajira kwani watakuwa wabunifu na wenye uhakika wa kile wanachokitaka katika maisha ya kisasa.
Alisema ni matumaini yake kwamba vijana watatumia programu hiyo vyema kuhakikisha kwamba wanatoka kiushindani.

Awali ilielezwa kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2016 kwa mwezi mmoja ujao utafunza walimu 500 ambao watatumika kusambaza maarifa ya code katika mashule mbalimbali, elimu ambayo itatumika kutatua matatizo ya msingi ya jamii.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa SAP Ireland, Bw. Liam Ryan amesema kwamba tangu mwaka 2016 ilipoanzishwa Africa Code Week zaidi ya watu 50,000 wamefundishwa na  zaidi ya watu milioni 1 wameanza kuifuatilia katika utekelezaji wake.

Alisema wamefurahishwa na mwitikio wa serikali ya Tanzania na anaamini kwamba kwa kuwezesha mafunzo hayo, tehama itafunguliwa kwa mapana yake.
Hata hivyo alisema kwamba wakati umefika wa kuingiza code katika mitaala ili itumike kunoa bongo za vijana ambao ndio dira ya miaka ijayo.

Wakati huo huo Mwalimu Miraji Kunoana kutoka shule ya sekondari ya Twiga alisema ni vyema serikali ikafikiria kuingiza masomo hayo katika mtaala kwa kuwa yatachangamsha akili ya vijana na kunoa bongo zao katika dunia ya digitali.

Alisema mafunzo ambao wameyapata yanawawezesha kufikiria nje ya boksi na kutengeneza chochote wanachotaka katika ubunifu wa teknolojia ikiwamo uumbaji wa vikaragosi na vitu vya kufundishia.

Mwanafunzi aliyefaidika na awamu ya kwanza ya mafunzo hayo Juliet Sewava  kutoka Shule ya sekondari ya Tambaza, alishukuru kwa  wafadhili wa mradi huo kwani wameweza kutengeneza uwezo wa kiteknolojia na ubunifu.

Anasema wanaweza kwa sasa kutengeneza michezo mbalimbali ikiwemo ya vikaragosi kwa kutumia Code.
Wakati huo huo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege alisema kwamba mradi huo umelenga kuwezesha vijana kuwa jukwaa la mabadiliko katika matumizi ya tehama kwa manufaa yao na jamii.

Alisema UNESCO YouthMobile imeungana na SAP na wafadhili wengine kuendesha kwa mwaka wa tano  Africa Code Week (ACW) kuhakikisha kwamba wanasambaza elimu ya code ili kuwawezesha kukuza zaidi ushiriki wao katika dunia ya teknolojia.

Alisema kuanzia mwaka 2015, zaidi ya watoto milioni 4.1  wameshiriki katika makongamano hayo na kwamba mwaka huu tukio kama la  Dar es Salaam katika bara la Afrika wanatarajia kufikia vijana milioni 1.5.

Huku asilimia 43 ya wakazi wake wakiwa na uwezo wa intaneti ukuaji wa teknolojia utabadili maisha ya wananchi wengi katika bara la Afrika na kutengeneza nafasi ya ajira.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa SAP Ireland, Bw. Liam Ryan (aliyeipa kamera mgongo) akiwa na Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock (kulia kwa Ryan) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya  Africa Code week Tanzania iliyofanyika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAP Ireland, Bw. Liam Ryan, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha, Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock, Mkurugenzi wa CSR EMEA na Africa Code Week Global Lead wa SAP Ireland, Bi. Claire Gillissen-Duval pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege wakiwa meza kuu wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock akitoa salamu za serikali ya Ireland wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege akitoa salamu za UNESCO YouthMobile wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa SAP Ireland, Bw. Liam Ryan akizungumzia wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi), Mramba Makange akitoa salamu za DTBi wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu akizungumza wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege (kulia) na Mkurugenzi wa CSR EMEA na Africa Code Week Global Lead wa SAP Ireland, Bi. Claire Gillissen-Duval (katikati) wakifurahia jambo wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock.
 Mwalimu Miraji Kunoana kutoka shule ya sekondari ya Twiga akitoa ushuhuda wa Programu ya Africa Code Week ilivyokuwa msaada kwa wanafunzi wa shule yake wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa CSR EMEA na Africa Code Week Global Lead wa SAP Ireland, Bi. Claire Gillissen-Duval.
 Mwanafunzi aliyefaidika na awamu ya kwanza ya mafunzo ya CODE, Juliet Sewava  kutoka Shule ya sekondari ya Tambaza akitoa shukrani kwa wafadhali na ujumbe kwa serikali kupitia Wizara ya elimu wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliohudhuria hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walionufaika mafunzo ya Coding kupitia Programu ya Africa Code Week wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu hiyo ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha na meza kuu katika picha ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu hiyo ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha na meza kuu katika picha ya pamoja na kamati ya uratibu wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu hiyo ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege (katikati) katika picha ya pamoja na Mwasisi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu hiyo ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa SAP Ireland, Bw. Liam Ryan akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Mh.William Ole Nasha (wa pili kushoto) wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha Kushoto ni Mkurugenzi wa CSR EMEA na Africa Code Week Global Lead wa SAP Ireland, Bi. Claire Gillissen-Duval, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu (katikati), Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock (wa pili kulia).
Balozi wa Ireland nchini, Mh. Paul Sherlock (kulia)akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa CSR EMEA na Africa Code Week Global Lead wa SAP Ireland, Bi. Claire Gillissen-Duval (katikati) wakati wa hafla mchapalo ya uzinduzi wa Programu ya Africa Code week Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images