Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Kaseja kulamba Milioni Kumi za Makonda

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), Paul Makonda  ameahidi kutoa Shilingi Milioni Kumi kwa Golikipa wa timu hiyo Juma Kaseja baada ya kufurahishwa na kiwango alichokionesha kwenye mchezo kati ya Stars na timu ya Taifa ya Burundi.

Kaseja ameingoza Stars  kupata ushindi wa penati 3-0 dhidi ya Burundi huku akifuta penati moja na kuiwezesha timu hiyo  kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.

Katika dakika 90 za mchezo huo wa marudiano uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1.

Goli la Tanzania lilifungwa na mchezaji wa Kimataifa ambaye ni  Nahodha wa Stars, - Mbwana Samatta katika dakika ya 29,  huku lile la  Burundi likifungwa katika dakika ya 45 ya mchezo huo na Abdul Fieston.

Baada ya kukamilika kwa dakika 90, zikaongezwa nyingine 30, lakini hata hivyo  zilipomalizika dakika 120 magoli yalikua 1-1 na ndipo ikafuata mikwaju ya penati.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Bujumbura nchini Burundi, timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli 1-1.

Bashe, Ndugai walivalia njuga Korosho, waapa kulikuza zao hilo kuwa la kibiashara

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuanzisha kituo maalumu cha kukuza kilimo cha korosho ikiwa ni baada ya kuzindua mkakati mahususi wa kulifanya zao hilo kuwa la kimkakati.

Mhe Bashe ameyasema hayo wakati alipohudhuria Baraza la Biashara na Wadau wa Kilimo katika kuhamasisha kilimo cha korosho na mtama Wilaya ya Kongwa.

Katika mkutano huo Mhe Naibu Waziri alimtaka Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho hadi kufikia Oktoba 15 awe amehamisha kituo cha pembejeo za korosho kilichopo Wilaya ya Mpwapwa kinahamia Wilaya ya Kongwa na haswa eneo la Kibaigwa kwa sababu ndipo mahitaji ya zao hilo yapo kwa asilimia kubwa.

Mhe Bashe alimuahidi Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Job Ndugai kuhakikisha analisimamia zoezi hilo na kwamba yeye mwenyewe atafika wilayani hapo Oktoba 15 kushuhudia kituo hiko kikianzishwa.

" Naiagiza Halmashauri kupitia Mkurugenzi kuanzisha vituo vidogo vijijini ambavyo vitakua na kazi ya kuzalisha mbegu za korosho ili kuwarahisishia wakulima badala ya kufuata mbegu hapa Kibaigwa wawe wanazipata ndani kwenye maeneo yao.

" Ndugu zangu wakulima, mimi niwahakikishie sisi kama Wizara tumejipanga haswa. Suala la upatikanaji wa mbegu, madawa na elimu ya zao hili tunaitoa kwa kasi na kwa namna ambayo kila Mwananchi atanufaika. Tumuunge mkono Rais wetu kwa kulipigania zao hili la Korosho," amesema Naibu Waziri Bashe.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Mh Job Ndugai amewataka viongozi wa Dini, Chama na Serikali kulivalia njuga zao la kilimo kwani kupitia utafiti uliofanyika unaonesha Wilaya ya Kongwa ina Ardhi nzuri ya kufanya kilimo hicho ambacho yeye anaamini ndio Dhahabu ya Kongwa.

Amesema kama viongozi wana wajibu mkubwa wa kuwa mfano kwa wananchi katika kulipambania zao hilo kwa kupanda mikorosho ambapo amewaonya pia viongozi ambao wana mpango wa kugombea mwakani kuwa watapitishwa na chama kwa kuangalia ushiriki wao katika kulikuza zao hilo.

" Mimi ni mjumbe wa kamati kuu, mwakani kama haujalima korosho basi ujue jina lako tutalikata. Sisi kama viongozi tuna jukumu zito la kukuza zao hili la korosho na kulifanya kuwa zao la Biashara.

" Simaanishi tuache kufanya kilimo kingine lakini ndugu zangu nawaambia kwa Dunia ya sasa biashara ya kilimo hivi sasa ipo kwenye mazao ya miti. Ndio maana unaona maeneo yenye maparachichi, mapapai, kahawa wanafanikiwa zaidi. Tuamke sasa na kuikijanisha Kongwa yetu kwa kupanda Mikorosho," amesema Mhe Ndugai.
 Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai akizungumza kwenye Baraza la Biashara na Wadau wa Kilimo cha Korosho na Mtama ambapo amewataka viongozi wa Kisiasa, Kidini na Serikali kushirikiana kukuza zao hilo
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akizungumza wakati wa Baraza la Biashara na wadau wa kilimo cha korosho na mtama wilayani Kongwa.
 Wananchi, wakulima na watumishi wa Serikali waliojitokeza kwenye mkutano huo was Baraza la Biashara la Wilaya ya Kongwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akizungumza katika mkutano maalumu wa Baraza la Biashara la Wilaya hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akihutubia wananchi, wakulima na watumishi waliojitokeza kwenye mkutano maalumu wa Baraza la Biashara la Wilaya hiyo.

DC Ndejembi afunguka walivyodhamiria kuifanya Korosho kuwa zao la kibiashara

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi amesema mkakati wao kama Wilaya ni kuhakikisha wanahama kutoka kufanya kilimo kwa ajili ya chakula na kuwa biashara lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa Nchi yenye uchumi wa kati.

Hayo ameyasema katika mkutano maalumu wa Baraza la Biashara na wadau wa kilimo cha Korosho na Mtama wilayani Kongwa ambapo kwa pamoja ndani ya wilaya hiyo walikubaliana kuifanya Korosho kuwa zao la kimkakati.

Amesema kutokana na utafiti uliofanyika unaonesha kilimo cha korosho ndani ya Mkoa wa Dodoma kinawezekana na wao kama Wilaya wamechagua kuwa viongozi na vinara wa kilimo hicho ndani ya mkoa huo na hivyo wameamua kupanda michez Milioni mbili na laki mbili ndani ya Wilaya nzima.

" Ndugu zangu hii heshima ambayo Rais Magufuli ametupa ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ni kubwa sana, lazima tuwe wabunifu kama Wilaya ili kuweza kwenda na spidi ya Mhe Rais wetu. Hivyo hizo miche Milioni mbili za korosho tutakazopanda maana yake kila kaya italima walau ekari moja yenye miche 30 ya korosho, lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha tunakuza zao hili na kuwa zao la kibiashara lenye tija kwa wana Kongwa na Taifa kwa ujumla, " amesema Mhe Ndejembi.

Amesema mkakati huo ni muendelezo waliouanzisha miaka miwili iliyopita walipozindua kampeni ya Ondoa Njaa Kongwa (ONJAKO) na sasa wameamua iende sambamba na kampeni hii yenye kuhakikisha Kongwa inakua ya kijani na kijani yenyewe ikitokana na kilimo cha korosho.

" Tuna kaya 74,000 kila kaya moja ikilima ekari moja tunaamini kwamba tutasogea na tutakua tunatengeneza kama mzunguko wa Sh Bilioni 6 ndani ya Wilaya yetu na hiko kiwango ni cha wananchi hapo bado wakulima wakubwa watalima zaidi ya kiwango hicho na sisi kama Halmashauri tutaanzisha ekari 1000 ili kukuza zao hili," amesema DC Ndejembi.

Amesema mkakati wa kilimo cha korosho katika Wilaya ya Kongwa ni uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambao ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/20. MKUKUTA na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ili kufikia uchumi wa kati.

Waziri Jafo aipongeza Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo, awataka kujiandaa na Muungano

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ameutaka uongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Wizara hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi mapungufu yaliyopo kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya Muungano.

Waziri Jafo amesema ni vema mapungufu yakafanyiwa kazi mapema ili wanapokwenda kwenye mashindano hayo mwezi Novemba mwaka huu wawe na timu bora itakayoweza kutwaa vikombe na zawadi mbalimbali.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu hiyo ambayo imekua ya nne katika mashindano yaliyomalizika Jumapili jijini Dodoma.

" Kama Waziri niwapongeze sana, mmefanya kazi kubwa na wote tumeiona. Nafasi ya nne siyo haba maana sasa tumepata nafasi ya kushiriki mashindano ya Muungano, hayo sasa naamini tunaenda kushinda vikombe na kuweka heshima.

" Lakini kama Timu tunapaswa tuanze maandalizi mapema, Novemba siyo mbali tusije tukachelewa tuangalie mapungufu yaliyoonekana kwenye mashindano haya ya Dodoma tuyafanyie kazi tuende Zanzibar tukiwa kamili.

" Najua mnaweza kuona haja ya kuongeza nguvu kwa kufanya usajili, niwasihi msisite kufanya hivyo, maana malengo yetu ni kwenda kufanya vizuri na kuwaonesha kuwa TAMISEMI na sisi tupo vizuri, " amesema Mhe Jafo.

Waziri Jafo pia ameagiza kupatiwa kiasi cha Sh Laki Tano hadi Milioni Moja kwa kila mchezaji lengo likiwa kuongeza motisha na hamasa kwa namna walivyopambana kwenye mashindano yaliyoisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja  ofisi kwake jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh Selemani Jafo akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu ya Netiboli ya Wizara hiyo ofisini kwake jijini Dodoma

WAZIRI KALEMANI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI MRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE

$
0
0

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akitoa tathmini yake mbele ya sehemu ya kuingilia kwenye handaki la kuchepusha maji (diversion channel) la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji Mkoani Pwani leo Jumapili Septemba 8, 2019 wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme wa Megawati 2115.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KASI ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye mifereji mikubwa ya kuchepusha maji) (diversion tunnel), pamoja na miundombinu wezeshi ikiwa imekamilika.

Sambamba na kupigwa kwa hatua hizo muhimu katika utekelezaji wa mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Julai 26, 2019 na ambao utazalisha Megawati 2115, pia amepongeza usimamizi na utawala katika mradi huo.

“Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.

Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.

Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji ardhini (diversion tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na ikamilike. ADIT hiyo yenye urefu wa wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.

Mheshimiwa Dkt. Kalemani pia alisisitiza kuwa ni matumaini ya serikali kwamba wakandarasi watamaliza kazi ya ujenzi ndani ya muda na kwamba hakuna muda utakaoongezwa.
 
“Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu pia watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri ili na mimi niukabidhi kwa Watanzania.” Alisisitiza na kuongeza…asitokee mtu atakaejaribu kuuchelewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo muhimu kwa taifa letu.” Alionya.
Alisema mradi huo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni muhimu, bwawa hilo ni kubwa sana aliwataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye mto Rufiji ili kuwepo uhakika wa upatikanaji wa maji ya kutosha ni bwawa hili litahitaji maji kwenye ujazo wa mita za ujazo bilioni 33.2 hivyo maji ya kutosha yatahitajika.

"Bwawa hili ni kubwa kati ya mabwawa 70 duniani bwawa la JNHPP ni bwawa mojawapo, kati ya mabwawa manne makubwa Afrika bwawa hili ni mojawapo na ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki kwa hivyo Watanzania wanayo kila sababu ya kujivunia na ni wajibu wetu kuyinza na kuhifadhi vyanzo vuya maji." Alisisitiza.

Alisema manufaa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa, kusambaza umeme vijijini na kwenye viwanda, pia utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira.

Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa tangu uzinduliwe na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.


Daraja namba mbili la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika leo Jumapili Septemba 8, 2019.

Kijiko kikitoka kwenye handaki la kuchepusha maji leo Septemba 8, 2019.

Waziri Dkt. Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali kwenye eneo la mradi.

Msafara wa magari ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ukipita kwenye daraja namba mbili linalokatisha mto Rufiji leo Septemba 8, 2019.

Ujenzi wa nguzo za daraja namba moja litakalounganisha pande mbili za mto Rufiji ukiwa unaendelea. Daraja hilo litasaidia kuvusha vifaa vya ujenzi (mashine) kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili ili kusaidiana na daraja namba mbili ambalo tayari linafanya kazi.
Waziri Mhe. Dkt. Kalemani (katikati) akipatiwa maelezo na Mratibu wa mradi huo Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara
Eneo la kuingilia ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Dkt. Kalemani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephene Kebwe na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Rufiji (OCD) Lepold Fungu, akipatiwa maelezo na Mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.




Mhe. Dkt. Kalemani akimsikilzia Meneja Mradi kutoka kampuni ya Arab Contractor ya Misri, Mhandisi Mohammad Samaha.(kushoto).
Daraja namba mbili likiwa limekamilika na kufanya kazi
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (JNHPP), ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Steven Manda, mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019.

EfG YATOA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA WANAWAKE MASOKONI KUHUSU SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita,akichangia mada katika semina iliyohusu Sheria ya huduma ndogo za fedha iliyotolewa kwa wanawake wafanyabiashara masokoni jijini Dar es Salaam juzi.
Mwezeshaji a Semina hiyo, Emmanuel Joseph akitoa mada.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wafanyabiashara katika Soko la Mchikichini, Adela Swai, akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wafanyabiashara katika Soko la Ilala, Consolatha Cleophas akichangia jambo kwenye semina hiyo. 
Ofisa Miradi wa EfG,Susan Sitta akizungumza.
Majadiliano ya vikundi yakifanyika.
Majadiliano ya vikundi yakifanyika.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA lisilokuwa la kiselikari la Equality for Growth (EfG) linalopinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wanawake masokoni, limeendesha semina kwa wanawake hao ya kuwapa uelewa wa sheria ya huduma ndogo ya fedha, 2019.

Akizungumza na vikundi vya wafanyabiashara wanawake kutoka masoko 16 ya jijini Dar es Salaam juzi, Mwezeshaji wa semina hiyo, Emmanuel Joseph alisema mtu yeyote au kikundi kinaweza kusajiliwa kwa kufuata taratibu zilizoainishwa katika sheria ya huduma za fedha za mwaka 2018.

“Kikundi cha kijamii kinachotarajia kutoa huduma ndogo za fedha kitatakiwa kufanya maombi ya usajili katika ngazi ya serikali za mitaa kwa kujaza fomu maalumu,” alisema Joseph.

Alisema maana ya huduma ndogo za fedha ni huduma zinazotolewa na mtu au taasisi za fedha ikiwemo kutoa na kuzipokea kwa njia mbalimbali kama vile mikopo na kuzihifadhi.

Joseph alizitaja huduma zinazoruhusiwa kutolewa na kikundi cha huduma ndogo za fedha kuwa ni kutoa hisa za uanachama, kuhamasisha akiba kutoka kwa wanachama wake,kutoa mikopo, kuhamasisha hisa za wanachama na kununua hisa katika masoko salama.

Alitaja adhabu zinazoweza kuchukuliwa kwa atakayekwenda kinyume cha matakwa ya sheria na kukutwa na hatia kuwa atalipa faini isiyo chini ya sh. milioni tano na isiyozidi milioni ishirini au kifungo kisicho chini ya miezi mitatu au kisichozidi miaka mitano au vyote.

Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita alisema wameupokea mswada huo ndiyo maana wameamua kutoa semima ya uelewa kwa vikundi hivyo vya wafanyabiashara wanawake sokoni.

Magigita alisema wanawake wanaofanya biashara sokoni wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa lakini viongozi wa serikali wamekuwa hawawaungi mkono.

“Tunawaomba viongozi wa serikali kuanzia maafisa watendani, madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na wale wa ngazi ya juu wawatembelee wanawake wanaofanya biashara sokoni kujua changamoto zinazowakabili kwa sababu wanamchango mkubwa katika taifa letu,” alisema.

Alisema tangu shirika hilo lilipoanzisha vikundi na kuwapa elimu ya uelewa wa haki zao na kupinga vitendo vya kikatili na unyanyasaji dhidi ya akina mama sokoni, kiongozi pekee wa ngazi ya juu aliyewahi kutembelea Soko la Buguruni ni alikuwa Makamu wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Gharibu Billal.

Mwenyekiti wa Kikundi cha akina mama wanaofanyabiashara katika Soko la Kisutu, Shamsia Ulimwengu aliipongeza EfG kwa kuwapa uelewa wa kuzitambua haki zao tofauti na zamani walipokuwa wakikumbana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kukosa msaada.

Vikundi vilivyohudhuria semina hiyo ni kutoka masoko ya Mbagala, Gongo la Mboto, Kinyerezi, Ilala, Mchikichini, Buguruni, Feri,Kisutu, Kigogo Fresh, Kigogo Sambusa, Kiwalani, Gezaulole, Mombasa,Temeke Stereo, Kampochea na Tabata Muslim.

Hivi karibuni serikali ilitoa mswada kuhusiana na usajili wa vikundi kulingana na Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha za Mwaka 2019 ambapo wahusika wanaujadili ili kupata maoni kabla ya kutoka kanuni.

TUME YA MADINI ANDAENI UTARATIBU BIASHARA YA MADINI IFANYIKE KIKANDA - BITEKO

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo wakati akifungua mkutano wa Wafanyabiashara wa Madini uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia semina iliyotolewa na Wizara kuhusu Serikali kuamua Chuo Cha Madini Dodoma kilelewe na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Sehemu ya Wafanyabiashara wa Madini wakifuatilia mkutano baina yao, Wizara ya Madini na Taasisi zake.
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na baadhi ya Wafanyabiashara wa Madini,. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula.

Asteria Muhozya na Tito Mselem, Dodoma

Waziri wa Madini Doto Biteko ameiagiza Tume ya Madini kuandaa haraka utaratibu utakaowawezesha Wafanyabiashara wa Madini nchini kufanya shughuli zao katika ngazi ya Kanda tofauti na ilivyo sasa ambapo taratibu zinawataka kufanya shughuli hizo katika Mikoa zilipotolewa leseni zao. Aliyasema hayo Septemba 7, 2019 wakati wa mkutano wa wafanyabiashara hao na wizara uliofanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi na Wataalam wa wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Aidha, Waziri Biteko alieleza kuwa, endapo wadau hao watafanya shughuli zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa, serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kutanua wigo kuwawezesha kufanya biashara ya madini katika maeneo mengi zaidi.

Waziri Biteko alisisitiza kuhusu ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya kutaka rasilimali madini kulinufaisha taifa na watanzania na kueleza kuwa, ndoto hiyo ndiyo iliyopelekea kufanyika kwa mageuzi mkubwa katika Sekta ya Madini.

Alikiri kuwa, kabla ya mabadiliko hakukuwa na mfumo rasmi uliowaonesha wachimbaji kujua sehemu sahihi ya kuuzia madini yao vivyo hivyo kwa wanunuzi wa madini suala ambalo lilipelekea kuwepo vitendo vya utoroshaji madini jambo ambalo lilionekana ni la kawaida. Waziri Biteko aliwataka wafanyabishara hao kuyatumia masoko yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa, serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji madini na kueleza kuwa, waliobainika kufanya vitendo hivyo wataanza kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na hivyo kuwataka kuwa chanzo cha mabadiliko ili kuzuia vitendo vya utoroshaji madini.

‘’ Tumekutana mpaka na wakemia wanaotengeneza madini feki. Kuna wengine wataanza kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunataka chumba cha madini kiwe na hewa ya kutosha,’’ alisisitiza Biteko. Akijibu hoja zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabishara wa Madini ya Vito (TAMIDA) Sam Mollel, kuhusu changamoto ya ucheleweshaji wa vibali vya kusafirisha madini nje ya nchi, Waziri Biteko aliwataka kuwa na subira wakati serikali ikishughulikia suala hilo.

Aidha, akijibu changamoto ya Masonara kusimamiwa na wizara nyingine, Waziri Biteko aliwataka wafayabiashara hao kuwasilisha maoni kuhusu suala hilo kama ilivyofanyika katika kuandaa Kanuni za Masoko na kuongeza kwamba, ‘’ Tunataka kuwa wizara ambayo inatatua matatizo’’. Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisisitiza kuhusu suala la kulipa kodi kama inavyowapasa na kuwataka kuyafahamu mabadiliko yaliyofanywa katika sekta na kuwa sehemu ya mabadiliko hayo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula, aliipongeza wizara kwa kazi ya kuwalea wadau wa madini na kueleza kwamba, miaka ya nyuma mambo kwenye sekta hayakuwa yakienda vizuri. Aidha, aliwapongeza wafanyabiashara wa madini na kueleza kuwa, hivi sasa wameanza kubadilika huku tabia ya kufanya biashara ya madini kiholela ikianza kutoweka.

‘’ Sisi Kamati tunapoona mambo yanakwenda vizuri mnaturahisishia kazi yetu’’, alisisitiza Mwenyekiti wa Kamati. Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni jitihada za wizara za kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini ikiwemo kusikiliza na kutatua changamoto kwenye sekta ili kuwezesha biashara ya madini kufanyika katika mazingira mazuri yanayoleta tija kwa pande zote.

Aidha, sambamba na mkutano huo, imefanyika Semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kubwa ikiwa ni serikali kueleza nia yake ya kukifanya Chuo Cha Madini Dodoma kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Akifunga semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Dustan Kitandula alitaka mchakato wa wa kukilea Chuo hicho kutochukua muda mrefu na alikitaka kijisimamie chenyewe ndani ya muda mfupi baada ya kulelewa na kutoa elimu bora.

Pia, alitaka kozi ya Mafundi Mchundo kuwekewa msingi mzuri. Pamoja na hayo, Mwenyekiti wa Kamati aliitaka wizara kukiongezea nguvu Kituo Cha Jimolojia Tanzania (TGC) ikiwemo bajeti ya kutosha kukiwezesha kuboresha miundombinu yake.

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAOMBI YA LISSU UBUNGE JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kusema kuwa ili kutekelezeka kwa maombi hayo ni lazima kuwepo na uvunjwaji wa katiba

Jaji Sirilius Matupa amesema mleta maombi (Lissu) katika maombi yake ana hoja katika  lakini alipaswa kupinga uchaguzi na sio kuapishwa kwa Mbunge wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu kwani kuapishwa ni haki yake.

Amesema haiwezekani Jimbo moja likawa na Wabunge wawili  na kwamba ili haki itendeke lazima katiba ivunjwe jambo ambalo haliwezekani.

MTANDAO WA YOUTUBE WAFUTA MAONI MILIONI MIA TANO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MTANDAO wa Youtube umeendelea na jitihada zake na kulingana na matamshi yenye chuki ambapo mapema katika awamu ya pili ya utakatishaji wa maudhui, mtandao huo umeondoa maoni milioni 500 ikiwa ni kutekeleza sheria hasa katika kupambana na matamshi ya chuki katika mtandao.

Kupitia blog ya mtandao huo imeelezwa kuwa maoni yenye chuki yameongezeka mara mbili ya maoni yaliyoondolewa awamu ya kwanza, pia picha mjongeo (video) laki moja zenye matamshi yenye chuki zimefutwa huku chaneli elfu kumi na saba zikibainika kuvunja sheria kwa kuweka matamshi yenye chuki katika chaneli zao.

Mkurugenzi wa mtandao huo Susan Wojcicki  ameeleza kuwa uwazi wa kutoa maoni katika mtandao wa Youtube utaendelea ila wataendelea kupiga vita maudhui yanayovunja sheria.

Kutokana na kuendelea kuchapishwa kwa maandiko na picha zenye chuki katika mtandao wa Youtube mwezi Juni mwaka huu walizifungia video ambazo zilikiuka sheria na kuwa na maudhui yenye chuki, udini, ubaguzi wa kijinsia na ukabila.

MASHINDANO YA MCHEZO WA GOFU 'NMB CDF TROPHY 2019' YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR,

$
0
0



Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (wa tatu kushoto) akimkabidhi kikombe na zawadi ya Mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019', Bw. A. Mcharo (kulia). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (wa tatu kushoto) akimkabidhi kikombe na zawadi ya Mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019', Bw. A. Mcharo (kulia). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(JWTZ), Mohamed Yacoub akifunga rasmi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo akimshukuru, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla hiyo. Benki ya NMB ni mdhamini mkuu wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NMB katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' akizungumza katika hafla hiyo.



Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi akimkabidhi mmoja wa washindi (kushoto) katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.
Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi akimkabidhi mmoja wa washindi (kushoto) katika hafla ya ufungaji Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019'.



MNADHIMU Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mohamed Yacoub amefunga rasmi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi 'NMB CDF trophy 2019' kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, huku Benki ya NMB ikiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo.

Akizungumza jana katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam, Mnadhimu Mkuu JWTZ, Luteni Jenerali Yacoub ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo, hivyo jeshi litaendelea kushirikiana na benki hiyo.

Aliwataka majenerali wa jeshi na wananchi wengine kuupenda na kuucheza mchezo wa golf na kuachana na mawazo ya baadhi ya watu wanaoamini kwamba mchezo huo ni wa matajiri pekee.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi alisema NMB ni wadau wakubwa wa Jeshi la Wananchi hivyo, itaendelea kusaidia mchezo wa golf hasa mashindano ya Club ya Mchezo wa Golf Lugalo ya jijini Dar es Salaam.

Alisema katika udhamini wa mwaka huu Benki ya NMB imetoa udhamini wa pesa ya kununua vifaa mbalimbali pamoja na zawadi za washindi kunogesha mashindano hayo na itaendelea kufanya hivyo.

Aidha aliongeza kuwa, NMB ni wadau wa Serikali na wabia pia kibiashara na Serikali hivyo inaamini inastahili kulihudumia Jeshi. "Mtandao tulionao ni mkubwa zaidi nchini nzima, tuna matawi zaidi 220, mashine za ATM zaidi ya 800 ambazo zingine zipo karibu na kambi za Jeshi la Wananchi na sasa tunaendelea kutanuka kupitia mtandao wa mawakala ambapo tuna zaidi ya mawakala 7000 maeneo mbalimbali ya nchini." Alisema Bw. Mponzi.

Katika mashindano ya 'NMB CDF trophy 2019' mwaka huu yalioshirikisha makundi mbalimbali ya wachezaji nchini wakiwemo wa kulipwa takribani washindi 22 wamejinyakulia vikombe na zawadi anuai kulingana na nafasi walizoshinda.

LUKUVI AZINDUA ULIPAJI KODI YA ARDHI KWA AIRTEL MONEY

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amezindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi kupitia Airtel Money.

Uzinduzi wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya Airtel Money unarahisisha huduma hiyo ambapo wamiliki wa ardhi wataweza kufanya malipo kupitia mtandao huo wa simu bila kwenda ofisi za Ardhi.

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 9 Septemba 2019 wakati wa kuzindua huduma hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema ubunifu wa serikali kufanya malipo ya Ankara za serikali kwa kutumia mfumo wa GePG umerahisisha malipo ya tozo mbalimbali za serikali ikiwemo kodi ya pango la ardhi.

Alisema mfumo huo wa malipo ya serikali umekuja na faida nyingi kama vile kuweka kumbukumbu vizuri, kulipa kwa muda, kupunguza upotevu wa mapato ya serikali, kuondoa mianya ya rushwa pamoja na kuongeza mapato ya serikali.

‘’Tunayo furaha kubwa kwa mara nyingine kutangaza kuwa kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel imerahisisha malipo ya kodi ya pango la ardhi kupitia Airtel Money. Hii ni huduma rahisi na itapunguza kero nyingi wakati wa kufanya malipo’’ alisema Lukuvi.

Aliitaka kampuni ya simu ya Airel kusaidia kuhimiza wananchi wanaotumia mtandao wa simu wa kampuni hiyo kulipia tozo mbalimbali za serikali ikiwemo kodi ya pango la ardhi kwa airtel money kwa kuwa inarahisisha kufanya malipo mahali popote.

Waziri Lukuvi amesema lengo la wizara yake kwa sasa ni kutaka kutumia makampuni ya simu kuwakumbusha wananchi kulipia kodi ya pango la ardhi kupitia jumbe za simu badala ya utaratibu uliopo sasa wa kwa kuwafuata wadaiwa.

‘’Sasa ofisi za ardhi za kulipia kodi ya pango la ardhi ziko viganjani mwenu mnaweza kulipia bila kwenda katika ofisi za ardhi’’alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema, kuunga mkono juhudi za serikali ni moja ya ajenda kubwa ya kampuni ya Airtel na kubainisha kuwa kampuni hiyo inaelewa umuhimu wa kukusanya kodi na kulipa malipo ya serikali kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo.

Kwa mujibu wa Singano, Airtel itaendelea kushirikiana na taasisi pamoja na mashirika mengine ya serikali kwa ajili ya kutimiza azma ya Serikali katika kukusanya mapato na kutoa wito kwa watanzania kuendelea kutumia huduma za kielektroniki kwa kuwa zina ubunifu mkubwa na kusisitiza kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na watanzania kwa asilimi 49 na matumizi ya mtandao  huo ni kutumia kilicho cha watanzania.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipeana mkono na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano wakati wa kuzindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kupitia Airtel Money katika ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kupitia Airtel Money katika ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja Airtel mkoa wa Dodoma Delphina Msangi.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kupitia Airtel Money katika ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni Meneja Huduma kwa Wateja Airtel Dodoma Delphina Msangi  (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

TUNAHITAJI WAWEKEZAJI KWENYE KILIMO CHA MIWA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez ambapo amewakaribisha Wacuba waje wawekeze kwenye sekta ya kilimo, hususan cha miwa.

Amekutana na kiongozi huyo leo (Jumatatu, Septemba 9, 2019) ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma. Waziri Mkuu ameishukuruSerikali ya Cuba kwa ushirikiano mzuri inaoutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kuboresha maendeleo ya jamii.

“Tanzania na Cuba zina uhusiano wa kihistoria. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, yaliyokuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere na Rais wa zamani wa Cuba, hayati Fidel Castro.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Cuba imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa sukari, hivyo amewakaribisha Wacuba waje nchini washirikiane na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kuboresha kilimo cha miwa na kuanzisha viwanda vya sukari.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati yake na Serikali ya Cuba kwa kuwa nchi hiyo ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania katika masuala ya kisiasa, kijamii, kiafya na kiuchumi.

”Mfano katika sekta ya afya, madaktari wengi kutoka Cuba wamekuwa wakija Tanzania kutibu wagonja waliokuwa na maradhi makubwa na pia Serikali ya Cuba imekuwa ikitoa fursa kwa Watanzania kwenda kusomea fani ya udaktari.”

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha Wacuba waje wawekeze katika sekta ya utalii hususani wa fukwe kwa sababu Tanzania ina fukwe nzuri. Amesema mji mmoja wa Varadero wa nchini Cuba unaingiza watalii zaidi ya milioni moja kwa mwaka na unategemea kivutio kikubwa kimoja tu cha fukwe ambayo ina urefu wa kilomita 22.

Akizungumzia kuhusu ofisi ya ubalozi wa Tanzania zilizofunguliwa nchini Cuba, Waziri Mkuu amesema zimesaidia kurahisisha mawasiliano kwa sababu awali kulikuwa na balozi mmoja tu ambaye alikuwa akiwakilisha nchi ya Cuba nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez alisema Serikali ya Cuba itahakikisha uhusiano wake na Serikali ya Tanzania unakuwa endelevu. Pia alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi.

Kadhalika kiongozi huyo amesema Serikali ya Cuba imefurahisha na kitendo cha Serikali ya Tanzania kufungua ofisi ya ubalozi nchini Cuba kwa sababu imezidi kuimarisha mahusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili. Kiongozi huyo pia amefanya ziara Zanzibar kabla ya kuja Dodoma. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na ujumbe kutoka nchini Cuba, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez, kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9.2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi zawadi ya kinyago, Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez, kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya kitabu cha Rais wa kwanza wa Cuba, Fidel Castro, kutoka kwa Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez, kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Marcelino Medina Gonzalez, kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 9, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YAKE KWA GOLIKIPA JUMA KASEJA,AMKABIDHI KITITA CHA SHILINGI MILIONI 10

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 09 amemkabidhi Mlinda Mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja kitita cha Shilingi Milioni 10 taslimu ikiwa ni sehemu ya Motisha na zawadi ya Kazi nzuri aliyoifanya jana wakati wa Mchezo baina ya Tanzania na Burundi.

RC Makonda amemkabidhi Kaseja fedha hizo mbele ya Kocha wa Taifa Stars, Katibu Mkuu TFF na baadhi ya wachezaji waliomsindikiza ambapo amekipongeza kikosi kizima cha Timu ya Taifa Stars kwa Kututoa kimasomaso kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022.

Kwa upande wake Mlinda mlango wa Timu ya Taifa Juma Kaseja amemshukuru RC Makonda kwa kutimiza ahadi aliyoitoa ndani ya Masaa machache ambapo ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kitamsaidia katika mambo mbalimbali ya kusongesha gurudumu la Maisha.

Itakumbukwa Jana Tanzania iliibuka na ushindi wa Penati 3 - 0 dhidi ya Timu ya Burundi ambapo Mlinda mlango Juma Kaseja alifanikiwa kupangua mkwaju wa Penati.

BUNGE LA WANAFUNZI LAIBUA CHANGAMOTO KUHUSU BAJETI KUU YA SERIKALI

$
0
0
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ntinko, Editha Mtinda akichangia hoja katika Bunge la Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini lililofanyika mjini Singida juzi.
Majadiliano yakiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida

BUNGE la Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wila ya Singida Vijijini limeibua changamoto zinazotakiwa kufikiwa na Serikali kupitia bajeti yake ya kila mwaka.

Changamoto hizo zilibainishwa mwishoni mwa wiki wakati wa majadiliano ndani ya bunge hilo liliketi kwa siku tatu mjini Singida ambalo liliandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Mtinko Education Development Organization (MEDO) kwa ufadhili wa Shirika la Norad kupitia ActionAid.

Akichangia hoja katika Bunge hilo lililowakilishwa na wanafunzi 40 kutoka katika halmashauri hiyo Editha Mtinda ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ntinko alisema katika maeneo ya vijiji yenye watu wengi miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikisuasua kutokana na bajeti inayotengwa kuwa ndogo na kutofika kwa kiasi kinachotakiwa.

"Bajeti inapotengwa kwenda katika maeneo hayo haifiki kama inavyotakiwa hivyo kusababisha miradi mingi ya maendeleo kama ujenzi wa shule, zahanati na miradi mingine kushindwa kukamilika" alisema Mtinda.

Mratibu wa Miradi wa Shirika hilo Iddy Mruma alisema walianzisha bunge hilo la wanafunzi ili waweze kuibua changamoto zilizopo katika maeneo wanayoishi na kuzionesha kwa serikali ili zifanyiwe kazi.

Alisema shirika hilo limekuwa likihimiza jamii kujenga tabia ya kulipa kodi itakayosaidia kuongeza ukubwa wa bajeti ya serikali pamoja na kuanzishwa kwa miradi inayopaswa kuhojiwa na kusimamiwa na jamii.

"Jamii inapaswa kuwa na uwezo wa kuhoji miradi yote inayofanywa na serikali katika maeneo yao pamoja na kuisimamia" alisema Mruma.

Alisema bajeti inapotengwa inatakiwa kutoa kipaumbele kwa makundi kama ya wanawake na walemavu kutokana na makundi hayo kusahaulika mara kwa mara.

NAIBU KATIBU MKUU WAZAZI ATOA SOMO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Kija Magoma amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilipoteza baadhi ya vijiji, vitongoji,mitaa, kata na majimbo kwa fitna na uzembe wa wanachama wake na kuwataka wasirudie makosa kwenye chaguzi zijazo.

Pia kimeonya wana CCM wanaojipitisha kwenye majimbo na kata wakifanya kampeni za siri na kuanza kuchafuana na kuagiza majina yao yaorodheshwe ili washughulikie kwa sababu wanakichafua Chama.

Magoma alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, kwenye kongamano la elimu, maadili,afya,mazingira, siasa na uchumi lililoandaliwa na Wazazi Wilaya ya Nyamagana, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Alisema mwaka 2014 na 2015 CCM ilishindwa kwenye baadhi ya maeneo kwa sababu ya fitna, majungu, kusemana vibaya (kuchafuana) na uzembe wa wanachama wake pindi uchaguzi unapokaribia, hivyo uchaguzi wa mwaka huu wasirudie makosa hayo.

“Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ni wa kuonyesha dira ya 2020.Chama kwanza, mtu baadaye na tuache majungu, fitna,kuchafuana na kutukanana, ikitokea hivyo hao tunaowachafua tukawapitisha itakuwa fimbo ya kutuadhibu itakayotumiwa na wapinzani,”alisema Magoma.

Alisema wapo wana CCM kote nchini wanajipitisha kabla ya wakati wakifanya kampeni za siri ili wapitishwe kugombea uongozi na kuonya muda huo haujafika na wanaofanya hivyo wasidhani wako salama,wataanza kuchukuliwa hatua wilayani kwa sababu wanaichafua CCM.

“Angalizo, serikali ya Rais John Magufuli si ya mchezo, wanaofanya kampeni za ubunge na udiwani kabla ya wakati wanafahamika na taarifa zao zipo mezani,na safari hii hakuna ujinga wa CCM kushindwa.Hapa Nyamagana kuna watu wanamvuruga mbunge ili kumuondoa, muda bado haujaisha.Wabunge na madiwani waheshimiwe ,waachwe wafanye kazi,”alisistiza Magoma.

Akizungumzia utaekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi alisema imetekelezwa ndani ya miaka mitatu na nusu ya uongozi wa Rais Magufuli kutokana na ualidifu na uzalendo wake wa kuhakikisha nchi inapata maendeleo ya kweli aliyoahidi wakati wa kampeni.

Alisema Rais Dk. Magufuli kwa aliyoyafanya ni dhahiri ameshaifanyia CCM kampeni kwa asilimia 80 hata kabla ya uchaguzi, hivyo ni jukumu la wana CCM kutafuta takwimu na kuwaeleza wananchi yaliyofanyika kwa sababu hakuna mwingine wa kuyasema lakini wakikaa kimya ni kutomtendea haki.

“JPM anastahili pongezi kwa namna alivyotekeleza ilani ya CCM katika muda mchache,amejenga miundombinu ya barabara km 12,885, fly over na Ubongo Interchange kwa bilioni 247,litajengwa daraja la Kigongo-Busisi (Milioni 700),amenunua ndege sita tayari,amelipa madeni ya watumishi sh. bilioni 595.2,”alisema Magoma.

Aliongeza kuwa amefanikiwa kujenga vituo vya afya 118, zahanati 522, hospitali 67 za wilaya ambapo 34 zimekamilika,ujenzi wa majengo ya ukaguzi wa elimu kote nchini kwa bilioni 15.2, umeme umeunganishwa kwenye vijiji 7,100, ujenzi wa mradi wa umeme Stiglers kwa Trilioni 6.5, Reli ya kisasa (SGR) kwa Trilioni 7 kwa fedha za ndani.

“Anataka Tanzania iwe nchi ya mfano ambapo bajeti ya mwaka huu ni Trilioni 33.11 kati ya hizo trilioni 12.15 za maendeleo, mikopo trilioni 2.52, bajeti ya dawa sh. milioni 415 (2019/2020) na elimu bilioni 450,”alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wazazi na kuhoji ,tulichelewa wapi kumpata Rais wa aina hii mwenye maono makubwa na nchi, uchumi unapanda.sssss

SERIKALI KUFUATILIA TOFAUTI YA MALIPO YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA MUTEX

$
0
0
Na Peter Haule na Farida 
Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina inaendelea na taratibu za kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo cha Musoma (Musoma Textile Mills Limited Mutex) kwa mwaka wa fedha 2019/20, baada ya uhakiki kukamilika mwezi Juni, 2019.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Joyce Sokombi, aliyetaka kujua utofauti wa malipo kwa waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Mutex baada ya kufungwa mwaka 1984.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali inafuatilia kwa karibu malalamiko yote yanayohusu tofauti ya kiwango cha malipo yaliyofanyika hivi karibuni ikilinganishwa na kiwango kilichoidhinishwa kwenye kikao cha pamoja kati ya Mfilisi wa Kiwanda hicho, wadau na Serikali ili kuona kama yana ukweli wowote.

“Baada ya Serikali kupokea maombi ya malipo kutoka kwa wafanyakazi hao mwaka 2018, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilifanya uhakiki wa wafanyakazi hao ili kujiridhisha na hatimaye kufanya malipo”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa awali jumla ya wafanyakazi 219 walijitokeza na wasimamizi wa mirathi 14 na hivyo  kulipwa jumla ya Sh. milioni 44.5, pia Ofisi ya Msajili wa Hazina ilifanya tena zoezi la uhakiki mwezi Juni, 2019 kwa wafanyakazi ambao hawakujitokeza katika uhakiki wa awali  ambapo jumla ya wafanyakazi 115 walijitokeza pamoja na wasimamizi wa mirathi 22 ambao kwa ujumla wanastahili kulipwa takribani Sh. milioni 20.7.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali ilisimamisha uzalishaji katika kiwanda cha Nguo Mutex mwaka 1994 baada ya kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mtaji na ongezeko kubwa la madeni kutoka iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)

Aliongeza kuwa Kiwanda cha Mutex kilifilisiwa na hatimaye kuuzwa mwezi Machi, 1998 kwa Kampuni ya LALAGO Cotton Ginnery and Oil Mills, kisha Wadai, Serikali na Mfilisi waliridhia mapendekezo ya kulipa kiasi cha Sh. milioni 161.3 kwa wafanyakazi 935 waliokuwepo kiwandani baada ya kikao kilichofanyika Septemba 23, 2005.

Alisema kuwa baada ya zoezi la ufilisi kukamilika, wafanyakazi 512 pekee ndio waliojitokeza kuchukua mafao yao na wafanyakazi 423 waligoma kupokea mafao yao kwa madai kwamba nauli ya familia na gharama za kusafirisha mizigo ni ndogo.

Wafanyakazi hao 423 walifungua kesi katika Mahakama ya Kazi ya Tanzania na baadae Mahakama hiyo ilitoa tuzo Juni 10, 2008 ambapo ilitupilia mbali shauri hilo na kuamuliwa wadai waende kwa mufilisi kuchukua stahili zao.

Aidha wadai hao walifungua shauri  jingine la maombi ya marejeo ambapo  Februari, 2010 Mahakama hiyo  iliamua tena wadai waliogoma kuchukua mafao yao waende kwa Mufilisi kama ilivyoridhiwa katika kikao cha wadau.


1.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

MWAKYEMBE ANOGESHA MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE ZA BETHEL MISSION UBUNGO NA MSAKUZI,AAHIDI WIZARA YAKE KUIPIGA JEKI YA SH. MILIONI 5 UJENZI BWALO LA WANAFUNZI

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Abdulkadri Shayo, wakati wa Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, leo, Septemba 8, 2019. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote Jumatano ijayo. Wapili kulia ni Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Wapili kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe (kushoto) baada ya kumpokea ofisini kwake, Waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Justine Sangu. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana. akimpa kitabu cha wageni Waziri Dk. Harison Mwakyembe kwa ajili ya kusaini baada ya kuwasili. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kabla ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana . Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizungumza baada ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana . Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akitazama eneo ambalo ujenzi wa Bwalo hilo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School unafanyika, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana "Hawa ndiyo wahitimu wenyewe?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiuliza alipowaona wanafunzi wa darasa la saba alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana "Watoto hamjambo?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiwasalimia wanafunzi hao Wanafunzi wa darasa la saba na chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Wanafunzi wa darasa la saba na Chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Waziri Dk. Mwakyembe akifuatana na Ndugu Mshana wakati akiwasili eneo la shughuli ya mahafali hayo. Kulia ni Ndugu Sangu. Wazazi na wageni waalikwa wakishangilia wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali. Wazazi na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali. Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakiingia ukumbini tayari kwa shughuli za mahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana. Waziri Dk. Mwakyembe akiwa amesimama pamoja na meza kuu kuwalaki ukumbini wanafunzi hao.
Waziri Dk. Mwakyembe akishiriki kuimba wimbo wa Taifa mwanzoni wa shughuli za mahafali hayo. Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akimsikiliza kwa makini Waziri Dk. Mwakyembe wakati akielezwa jambo wakati wa mahafali hayo. Baadhi ya Wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akizungumza Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Wawakilishi wa wanafunzi wa darasa la saba wakisoma risala wakati wa mahafali hayo. Wanafunzi hao wakimkabidhi risala yao waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuisoma. Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Waziri Dk. Mwakyembe na viongozi wa meza kuu wakishangilia bada ya kuvutiwa na namna wahitimu wa tarajiwa wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, walivyokuwa wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Meneja wa Bethel Mission School akitoa hotuba wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Waziri Dk. Mwakyembe na kulia ni Mtunza hazina wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Kanda ya Afrika Mchungaji Perminar Shirima. Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue akimkaribisha Dk. Mwakyembe kuzungumza. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Mwakyembe akihyutubia kwenye mahafali hayo. Dk. Mwakyembe alionyesha kuvutiwa na wanafunzi wa darasa la saba kwa namna walivyoonyesha vipaji na weledi mkubwa katika kuzungumza kiingereza. Aliipongeza shule hiyo kwa kazi nzuri ya kueleimisha watoto huku ikijikita pia katika kuwalea vizuri kimaadili. Kutokana na kukunwa na shule hiyo aliahidi Wizara yake kutoa sh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Bwalo la wanafunzi kwenye shule ya Bethel Mission Ubungo. Waziri Dk. Mwakyembge akishauriana jambo na Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue

KUKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU⇓














Waziri Dk. Mwakyembe akionyesha zawaidi baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayo Waziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya shati baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayo Waziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya kitabu cha tiba kutoka kwa Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue Waziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Chekechea wa Bethel Mission School Ubungo wakati wa mahafali hayo Waziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu watarajiwa wa Darasa la saba wa Bethel Mission School Ubungo na Mbezi Msakuzi, wakati wa mahafali hayo Waziri Dk. Mwakenye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bethel Mission School na baadhi ya wageni waalikwa mwishoni wa shughuli za mahafali hayo.

INTRODUCING D MOE FT BRIGHT - TWENDE (Official Video)

RC Makonda atoa neno kwa Taifa Stars,atimiza ahadi yake kwa Juma Kaseja

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images