Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

Wanawake watakiwa kucheza Upatu kulipa Bima ya Afya

0
0
Mbunge Zaynabu Matitu Vullu akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Dimani Wilaya ya Kibiti
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani,Mh Zaynabu Matitu Vullu akikagua majengo ya Zahanati ya Dimani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi (UWT), Zaynabu Matitu Vullu akiwaeleza Wanawake wa wilaya ya Kibiti juu ya Umuhimu wa Bima ya Afya.




Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi (UWT) ,Zaynabu Matitu Vullu amewaomba Wanawake wa wilaya ya Kibiti kucheza Upatu wa kununulia bima za Afya na sio vyombo.

Mh Zaynabu amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanawake wa wilaya hiyo kwenye ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM Kibiti.

“Mimi nawaomba Wanawake wenzangu tuache kutunza vyombo badala yake tutunzane kadi za CHF Iliyoboreshwa ili tuweze zitusaidie kupunguza gharama za matibabu pindi tunapougua au kuuguliwa ndani ya familia” amesema Mh Zaynabu.

Amewaeleza kuwa Kama Kila mmoja atauza kuku wawili nakujipatia bima kwa gharama ya Shilingi 30,000 ambayo itaweza kutibia watu sita ndani ya familia moja ambao Ni Baba,Mama na wategemezi wanne.

Amesema matumizi ya Bima yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini usiokuwa wa lazima kwa kuokoa gharama za matibabu .
Aidha ametaja kuwa matumizi ya Bima yanapunguza presha pindi Mama anapokuwa mjamzito pindi unapofija wakati wa kujifungua kwa kusaidia kupata huduma kwa uhakika.

Pia aliwaomba wamama hao kufikisha ujumbe huo kwa kinababa na waume zao kwani swala la Afya ya familia ni jukumu la kila mmoja wetu.

Mazingira ya Uwekezaji Sasa ni Mvuto kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje – Bashungwa

0
0

Abraham Nyantori ,MAELEZO 

Wizara ya Viwanda na Biashara katika siku yake ya pili ya Kongamano la fursa za biashara baina ya Tanzania na Uganda imerudia kuwahakikishia wafanyabiashara wake kuwa Wizara yake itawahudumia kwa karibu kwa kila hatua ili kufanikisha lengo la kufanya biashara baina ya nchi hizi mbili. 

Akifunga Kongamano hilo leo, baada ya mjadala mrefu uliojumuisha wawekezaji, wafanyabiashara wa bidhaa, wasafirishaji na wajasiriamali katika Kituo cha Mikutano cha Julias Nyerere, Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, ametumia muda huo kusisitiza wafanyabiashra kutumia fursa ya maboresho ya sheria na mazingira ya biashara kuwekeza, ndani na wawekezaji wa nje. 

Waziri amewaeleza Waganda fursa zilizopo katika sekta za kilimo, madini, mali ghafi za mazao mbalimbali na bidhaa kwa walaji, na akawaeleza mazingira ya uwekezaji yamefanyiwa tafiti mbalimbali na serikali baada ya maboresho, mabadiliko yametengenezewa nyaraka (blue print). 

Waziri amekiri kuwa majukwaa mbalimbali yamekuwa yakifanyika lakini shughuli zote zinaishia kubaki katika makabati pasipo utekelezaji, “sasa tunatakiwa kuongea kidogo na kufanya vitendo zaidi” amesisistiza waziri hasa kwa wafanya maamuzi, “kwa haya maamuzi tuliofikia nitatoka ofisini na kufuatilia kila moja kuona utekelezaji wake” ametahadharisha Waziri Bashungwa. 

Katika Kongamano la leo, baada ya wachokozaji wa maada kadhaa katika sekta ya usafirishaji na wa vipimo kumaliza, washiriki wa Kongamano wamejikita katika eneo hilo muhimu huku wakieleza changamoto zinazokabili sekta za usafirishaji, pia, michakato ya usajili, ukakasi wa “njoo kesho” na kuwa baadhi ya wafanyamaamuzi huchukua muda mrefu kutekeleza ama kutoa vibali. 

Watendaji wa juu wa serikali za Uganda na Tanzania, wakiongozwa na Waziri wa Viwanda, ambaye mwenzake wa Uganda alikuwa na jukumu lingine hapa jijini walionesha umakini wa kuchukua mawazo na maswali ya washiriki wa Kongamano, na baadhi yao walipata nafasi ya kujibu maswali. 

Baadhi ya wafanyabiashara wasafirishaji walitaka kujua gharama za usafirishaji wa mzigo kutoka Mwanza/Uganda hadi Dar es Salaam, huku wakilinganisha na gharama za usafirishaji wa mzigo kama huo kutoka bandari ya Mombasa, Kenya; hata hivyo watendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) walisema bei zake zimeshushwa na mazingira yameboreshwa. 

Akichangia maada, Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro, amekumbusha historia ya undugu wa nchi hizi mbili, na kuwa Uganda haijawahi kupigana na Tanzania, akasema, “Vita ya Kagera 1977 ilikuwa ni mjumuisho wa Waganda na Watanzania kuondoa utawala wa kidikteta wa nduli Idd Amini, nchini Uganda. 

Waziri akakumbusha kuwa huduma ya TRC toka Dar es Salaam hadi Uganda huchukua siku tatu tu baada ya kuondolewa baadhi ya vikwazo, na reli ya kisasa ya mwendo kasi ikamilikapo safari hiyo itakuwa ya siku moja, pia akahimiza Waganda na Watanzania kuunganisha nguvu zao na kuliingia soko la Sudan. 

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri huyo akaeleza masikitiko yake ya nchi za kiafrika kuendelea kutumia lugha za kikoloni kama lugha rasmi za vikao vya kimataifa, akasema. “lugha pekee isiyo ya kabila fulani na isiyo lugha ya kikoloni ni Kiswahili, … tubadilike, tuwe na lugha ya kutuunganisha, nayo ni Kiswahili.” 

Akasema, “Natetea kiswahili kwa sababu sio lugha ya kabila lolote, ni lugha ya pili baada ya kiarabu katika bara la Afrika…. Ni lugha ya kumi katika mlolongo wa lugha za kimataifa, hii ni silaha kubwa kwetu, tusiendelee kutukuza tamaduni za wenzetu kwa kudharau zetu.”
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.

Minziro aitabiria kupanda Ligi Kuu Dodoma FC

0
0

Charles James, Michuzi TV

TIMU za Soka za Dodoma Jiji FC na Singida United zimetoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma.

Dodoma FC inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza ndio waliokua wenyeji wa mchezo huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiweka fiti na msimu mpya wa daraja la kwanza utakaoanza kutimua vumbi Septemba 14 ya mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Mbwana Makata amesema mchezo wa leo ni muendelezo wa michezo ya kirafiki ambayo wamekua wakiicheza kwa ajili ya kujiimarisha kabla Ligi hiyo haijaanza.

Amesema kitendo cha Timu yake kucheza michezo minne ya kirafiki na Timu za Ligi Kuu kimewapa mwanga wa wapi ambao wanapaswa kurekebisha kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

" Ni kweli suala la ufungaji limekua changamoto kwenye michezo yetu ya kirafiki lakini mabadiliko yamekuepo kuanzia mchezo wa kwanza dhidi ya Mbeya City hadi huu wa Singida.

" Tunaamini tumeimarika na tutafanyia kazi mapungufu machache kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Ombi letu kwa wanadodoma ni wao kuendelea kutuunga mkono na sisi tunawaahidi hatutowaangusha," amesema Makata.

Nae Kocha wa Singida United, Fred Minziro amekipongeza kikosi cha Dodoma FC kwa kiwango walichoonesha na kusema kama kocha Makata atafanyia mapungufu machache yaliyoonekana basi watakua na Timu bora itakayoweza kuhimili mikikimikiki.

" Tunashukuru Mungu mchezo wetu na Dodoma FC umemalizika salama. Timu Zote mbili zimekua na changamoto za ufungaji lakini naamini tutafanyia kazi kabla ya mchezo wetu wa pili dhidi ya Namungo utakaochezwa Septemba 14.

" Kwa upande wa Dodoma FC Niwapongeze wana kikosi chenye wachezaji wazuri na wazoefu. Pia wana kocha makini na mwenye kujua Ligi Daraja la kwanza. Wakifanyia kazi mapungufu kwenye eneo la ushambuliaji nawaona kabisa wakipanda Ligi kuu," amesema Minziro.
Kikosi cha Dodoma Jiji FC kinachojiandaa na Ligi Daraja la kwanza itakayoanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu

Wakala wa Tigo Pesa Tanzania wazidi kupata mafanikio

0
0


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Said Khatibu kutoka Zanzibar. Promosheni hii ilifanyika mwezi wa nne, mwaka huu.

Bwana Said Issa Khatib,alianza safari yake ya kuelekea kwenye mafanikio kwa kutumia kadi ya simu ya kuazima kutoka kwa jirani yake mwaka 2014, kwa sasa ni moja kati ya mawakala wakubwa zaidi wa Tigo Pesa, mjini Zanzibar. Biashara imekua kutoka ilivyokuwa mwanzoni na kufikia kufanikiwa kukuza biashara yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia kuwa biashara ya mamilioni, jambo ambalo liliwezeshwa na idadi ya wateja inayoongezeka kila siku ya wateja wa Tigo Pesa.

Bwana Khatib ambaye pia ni mshindi wa tuzo nyingi za Tigo Pesa zenye jumla ya milioni 15/- katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, alisema kwamba alianza biashara yake kwa kutumia line ya simu aliyoazima kutoka kwa jirani yake. Kama ilivyo kwa maelfu ya mawakala wengine waliosambaa nchi nzima, Khatib aliona fursa kubwa katika biashara ya kampuni ya simu ya Tigo ya kuhamisha pesa baada ya kujipatia line yake mwenyewe ya Till ya Tigo Pesa miaka mitano iliyopita.

"Nilitumia line ya jirani yangu kwa muda wakati huo nikiwa natunza pesa kwa ajili ya kuweza kupata line yangu mwenyewe. Nilikuwa nampa jirani yangu asilimia 70 ya mapato ya siku wakati mimi nakibakiwa na asilimia 30", bwana Khatib ambaye ni baba wa watoto watatu alisema wakati akibainisha kwamba mpango wake ulikuwa ni kuwa super dealer wa kampuni ya Tigo mjini Zanzibar, kampuni ya huduma za simu za mkononi inayokua kwa kasi zaidi.

MASHINDANO YA 'NMB CDF TROPHY' 2019 YAANZA LUGALO DAR

0
0


Mkuu wa Majeshi, Mstaafu Jenerali George Waitara akishiriki Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo. 

Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuanza rasmi kwa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi yanayofanyika kwa siku mbili viwanja vya mchezo huo Lugalo jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY". 
Baadhi ya wachezaji wa Golf wakipokea sehemu ya vifaa vya kucheza mchezo huo toka kwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, Benki ya NMB kabla ya kuanza kucheza. Benki ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY". 
Kushoto ni baadhi ya wachezaji wa Golf wakipokea sehemu ya vifaa vya kucheza mchezo huo toka kwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, Benki ya NMB kabla ya kuanza kucheza.

Mchezaji wa Golf, Tumwesige Mujwauzi toka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Club ya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam. 

Nahodha wa Timu ya NMB inayoshiriki Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini yaani "NMB CDF TROPHY" akizungumza na wanahabari kuelezea walivyojiandaa kushiriki mchezo huo.
Baadhi ya wachezaji wa Golf katika Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club wakiendelea na mchezo.
Baadhi ya wachezaji wa Golf katika Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club wakiendelea na mchezo.
Mchezaji wa Golf kutoka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club.
Mchezaji wa Golf kutoka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" linalofanyika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club.
Uzinduzi Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini "NMB CDF TROPHY" katika viwanja vya Golf Lugalo.

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAENDELEA KUWA KINARA UTOAJI WA MIKOPO ASILIMIA 10 -RC SHIGELLA

0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akiwasha pikipiki wakati kabla ya kuwakabidhi kundi cha vijana wa bodaboda cha Tanga One Youth.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa halfa hiyo
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akiwa na Mstahili Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakiteta jambo wakati wa ziara hiyo
RTO wa Mkoa wa Tanga Solomon Mwangamilo kushoto akiwa na na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Leons Rwegasira wakijitambulisha kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Vijana wa kikundi cha Tanga One Youth wakiwa kwenye pikipiki zao wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella baada ta kukabidhiwa
Sehemu ya wananchi wakimsikili za Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella



MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amesema kwamba Halmashauri ya Jiji la Tanga imeendelea kuwa kinara katika utaoji wa mikopo asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu.

RC Shigella aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea wilaya ya Tanga iliyokwenda sambamba na kukabidhi mikopo ya pikipiki 70 kwa kikundi cha vijana cha Tanga One Youth.

Huku akieleza pia na vyarahani vya kutosha ya zaidi ya milioni 100 wamekopeshwa kila kata na watu wenye ulemavu nao pia wamenufaika navyo .

Alisema mikopo hiyo imekuwa chachu kubwa kwa makundi hayo na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wao na jamii zinazowazunguka ikiwemo kujikwamua kimaendeleo.

“Kwa kweli ninayofurahi kuona Tanga Jiji mmeendelea kuwa kinara kwenye utoaji mikopo asilimia 10 kwa mkoa huu wa Tanga lakini niwaambie watu walionufaika nayo kuitumia vizuri mikopo hiyo iweze kurejeshwa halmashauri na watu wengine waweze kukopa kwani haina riba “Alisema

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka vijana watumie vizuri pikipiki hizo ikiwemo kuendesha kwa umakini huku akisema amefariji kuona RTO yupo eneo hilo huku akieleza kwamba hatarajii kusikia watu wanaondoa exosi na kuweka mfumo mwengine ambao unapiga kelele.

Awali akitoa taarifa ya mradi wa bodaboda kwenye kikundi cha vijana cha Tanga One Youth Afisa Maendeleo Jamii wea Jiji nla Tanga Dorah Ntumbo alisema kwamba halmashauri hiyo inatekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa vuikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Alisema kwamba kwa mwaka 2018/2019 Halmashuri hiyo ilitenga jumla ya sh.milioni 800.449,700 kwa ajili ya makundi hayo ambapo vijana walitengewa jumla y ash.335,094,000 na hadi kufikia June 29 jumla ya Tsh milioni 353,000,000 zimekwisha kutolewa kwa ujumla wa vikundi 20 vya vijana.

KUUNDWA KWA JUKWAA LA WADAU SEKTA YA SHERIA KUTALETA MAENDELEO KATIKA TAIFA-KATIBU MKUU.

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg George J. Kazi akitowa maelezo kuh kuanzishwa kwa Jukwaa la Sheria Zanzibar 
Muwezeshaji kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar Ndg Mohammed Khamis akitoa mada kuhusu taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika sekta ya sheria Zanzibar 

Na Raya Hamad - WKS 

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg George Joseph Kazi amesema kuundwa kwa jukwaa la wadau wa sekta ya sheria kutasaidia kuwaunganisha wadau wa sekta hio na kuleta maendeleo endelevu katika kada hio muhimu kwa maslahi yaTaifa 

Ameyasema hayo kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi na watendaji kutoka sekta ya sheria uliojadili taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika washeria Zanzibar 

George Kazi amewataka wajumbe hao kutoa michango na mawazo yao na kufanya upembuzi ili kuona mahitaji muhimu yatakayosaidia kufahamu sekta ya sheria, kwa kutambuwa kuwa sekta ya sheria ndio kiini katika masuala yote ya maendeleo ya nchi . 

Mbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu , Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Tume ya kurekebisha Sheria na Mahakama lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la wanasheria hata hivyo kinachokosekana ni kutokuwa na jukwaa la pamoja linalowaunganisha wanasheria hao 

Jukwaa ambalo litasimamia na kuangalia maendeleo ya sekta ya sheria hali ilivyo na jinsi gani itakuwa na uratibu ambao utasaidia kujuwa mambo mengi ya kuangalia wapi tulipotoka ,tulipo na tunakoelekea, matatizo gani yanayoikumba sekta sheria iwe ya Jinai na Madai kwa ajili ya maendeleo chanya ya sekta ya hio 

Katibu George amesema sekta ya sheria inaendelea kukuwa kwa kasi hivyo wizara imeona ipo haja ya kuwa na chombo ambacho kitasaidia kuzidisha kasi ya uwajibikaji ili kila mmoja atimize wajibu wake “muhimu kujielewa kama wanasheria kufahamu jukumu walilonalo na kazi wanazozifanya ikiwemo kufanya tathmini ya kile wanachokifanya badala ya kufanya kazi kwa mazoea, hii itasaidia kuleta chachu katika sekta ya sheria kujenga utamaduni wa kujisomea na kufahamu mambo mapya yanayotokea hivyo jukwaa hili litatusaidia tuweze kujitambua”alisema George 

Ameendelea kusema kuwa kupitia Jukwaa upo uwezekano wa kufanya utafiti na kufahamu kiwango cha ongezeko la wanasheria, kuwafahamu mawakili na mahakimu na kuona sekta ya sheria imekuwa kwa kiwango gani na je ni kweli wamebobea kuwa wataalamu wanaofikia kiwango na vigezo vinavyohitajika katika kada ya sheria 

Kuwepo kwa Jukwaa moja litawezesha pia kutoa mapendekezo na kuwasilisha taarifa zao ambazo zitapelekea Wizara kuweza kuzifanyia kazi kwa pamoja . 

Nao wawasilishaji kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ndg Mohammed Khamis na ndugu Mussa Kombo wamesema lengo la kuwa na chombo hiki nikusaidiana mawazo na ushauri ilikuona uwajibikaji unaimarika na sio kuingilia majukumu yaVyombo vya kisheria pia kuondosha migongano ya kisheria baina ya taasisi na kutekelezwa kwa vitendo mawazo na ushauri utakaotolewa . 

Nae Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar ndugu Ibrahim Mzee Ibrahim ameanisha mambo manne ambayo yakitekelezwa ipasavyo yatakuwa nichachu yamaendeleo ikiwemo vyombo vya mashtaka kufahamu majukumu yao yakiutendaji, pia kufuatwa kwa Maadili na taratibu zake, usimamizi pamoja na suala la uwajibikaji na ushirikiano baina ya vyombo vya Sheria vilivyopo nchini. 

Aidha amesema kinachounganisha taasisi hizi zote za sheria ni muongozo wa taasisi na kila chombo kinamamlaka yake na imewekewa sheria hivyo kuwepo kwa jukwaa hili kutasaidia kuondosha baadhi misuguano na kuwa na sauti ya pamoja katika utekelezaji wa masuala ya utowaji haki na sheria na mwisho wa yote ni taasisi yenyewe iliyopewa mamlaka kuona vipi inabadilika kwa kufuata taratibu 

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi Daima Mohamed Mkalimoto amewataka wawasilishaji ya mada kuyapitia majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na bajeti ya Wizara ili kujenga hoja kwa msingi imara itayosaidia kuundwa kwa kwa jukwaa la pamoja . 

Bi Daima ametoa mapendekezo kwa kuona tunaanajifunza pia mazuri yanayotekelezeka kutoka kwa wengine na kusema kuwa uhai wa sekta ya sheria utaonekana kwa kuangalia zaidi na kuona umuhimu wa kuweka jukumu la kulinda rasilimali za nchi kuangalia mikataba kiundani kutoa mapendekezo pia kuweka uwiyano katika jamii hata katika ngazi za Mikoa na Wilaya ili na wao waweze kuangalia masuala ya kisheria katika maeneo yao 

Kamishna wa Kazi Bi Fatma Iddi Ali amesema kuundwa kwa Jukwaa la pamoja kwa sekta ya sheria hakutakuwa na muingiliano bali ni kuondoa ukakasi lakini utazingatia umuhimu wa taasisi zinazoguswa kwani kila taasisi inayosimamia sheria ina taratibu zake namiongozo yake ya kiutendaji 

Aidha amesisitiza juu ya namna yakumuandaa na kumuuangalia mwanasheria na kazi anazozifanya ili aweze kuwa na maadili mazuri anakoelekea kwa vile mwanasheria ndie anaetegemewa kuwa Jaji, Mrajisi wa mahakama , Hakimu, Wakili ama kwa namna yeyote kuwa msimamizi katika masuala ya sheria na utowaji wa haki 

Bi Hamisa Mmanga Makame Mkurugenzi mipango uendeshaji na rasilimaliwatu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ameipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kutokana na jitihada zilizopo ukilinganisha na miaka yanyuma hivi sasa kila siku kunapiga hatua na maendeleo yanaonekana kupitia sekta ya sheria 

Wakili wa Mahakama kuu Zanzibar Bw Zaharani Mohamed Yussuf ametoa msisitizo kushirikishwa kikamilifu kwa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ambao nao wanasimamia utatuzi wa migogoro, mali hivyo kuwepo kwachombo hiki kutarahisisha utowaji wa haki kwaupande wao na kwa wanajamii . 

Mkutano huo uliowakutanisha viongozi na watendaji kutoka sekta ya sheria uliojadili taarifa ya utafiti juu ya uwezekano wa kuanzisha jukwaa la pamoja kwa wahusika wa sekta ya sheria Zanzibar umeandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la Mendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP umefanyika kwenye ukumbi wa mkutano uliopo Zanzibar Beach Resort Mazizini. 

RAIS WA UGANDA ALIVYOHITMISHA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI

0
0
Mhe. Makamu wa Rais akiagana na Mhe. Rais Museveni huku Mama Janeth Museveni akishuhudia

Mhe. Makamu wa Rais akiagana na Mama Janeth Museveni 
Mhe. Rais Museveni akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi 
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 5 hadi 7 Septemba 2019. Wakati wa ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais Museveni kwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli walifungua Kongamano la Kwanza la Biashara kati ya Tanzania tarehe 6 Septemba 2019. 
Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais wakiendelea na mazungumzo yao huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia. 
Waziri wa Elimu wa Uganda ambaye pia ni Mke wa Rais Museveni, Mhe. Janeth Museveni (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Joyce Ndalichako wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais 
Mhe. Rais Museveni akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima 
Mhe. Rais Museveni akifurahia burudani ya kikundi cha ngoma kilichkuwepo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuaga Rais huyo 
Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais wakiangalia moja ya kikundi cha ngoma wakati wa kumuaga Mhe. Rais Museveni
Mhe. Makamu wa Rais akiwaongoza viongozi wengine kupunga mkono wakati ndege iliyombeba Rais wa Uganda, Mhe. Museveni ikiondoka nchini kurejea Uganda 
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin akimsikiliza Balozi wa Uganda nchini, Mhe. Richard Kabonero mara baada ya kukamilisha hafla ya kumuaga Mhe. Rais Museveni kukamilika 
Wadau mbalimbali waliojitokeza kumuaga Rais wa Uganda Mhe. Museveni. 
Wadau wengine 
Wadau kutoka Jeshini nao walikuwepo uwanjani hapo 
Wadau kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Sekta zingine wakifurahia kukamilisha kazi salama 

YOUSSOU N’DOUR ALIUTAKA URAIS SENEGAL

0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.


Youssou N'dour alithubu kuwa na ujasiri wa kugombea kiti cha urais nchini mwake Senegal.

Ni mwanamuziki anayependwa nchini mwako, alikuwa akiitikia wito wa wananchi waliomtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais Abdoulaye Wade, aliyekuwa amepania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Katika hotuba iliyorushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki alitamka kwamba kama angelichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, angelipunguza matumizi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote.

N’Dour licha ya kuwa ni mwanamuziki, pia ni mfanyabiashara anayemiliki miradi mikubwa yenye mafanikio makubwa nchini humo.

Youssou ana historia ndefu katika talanta za uimbaji, uandishi wa nyimbo, na utunzi, mchanganyiko wa tamaduni pia ni mwigizaji.

Licha ya shughuli za muziki na harakati za kisiasa, amekuwa akijihusisha na masuala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia yeye ni balozi wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu masuala ya watoto (UNICEF).

Youssou N'Dour alikiri kuwa yeye sio msomi lakini alielezea wadhifa wa urais kuwa ni kazi na sio taaluma.

Kabla ya hapo N'Dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu, Youssou alimgeuka na kuwa mpinzani wake mkuu.

Alikuwa akisema kwamba Wade anatakiwa kutogombea mhula mwingine wa tatu kwa sababu anavunja Katiba.

Kabla ya upigaji kura ilibainika kuwa isingelikuwa kazi rahisi kwa Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.

Mwaka 2004, Rolling Stone alimuelezea kuwa, huko nchini Senegal na sehemu kubwa ya Afrika, "ndiye mwimbaji maarufu kati ya walio hai."

N’dour amesaidia sana kuutangaza na kuuendeleza mtindo wa muziki maarufu nchini Senegal, unaojulikana kwa lugha ya Serer kama Mbalax. Huo ni aina ya muziki ambao huelezea mbinu na mitindo yake mingi kutoka mapokeo ya kihafidhina ya muziki wa Serer wa ‘Njuup’.

Aidha amesaidia sana kuleta mafanikio makubwa na tuzo kwa filamu ya “Return to Goree” aliyoshiriki kuiongoza kwa kushirikiana na Pierre-Yves Borgeaud, na “I Bring What I Love” ilivyoongozwa na Elizabeth Chai Vasarhelyi, zilizotolewa na kuoneshwa katika majumba ya sinema duniani kote.

Msomaji wa makala hii yawezekana ukawa unataka kufahamu wasifu wa Youssou N'Dour.Wasifu wa Youssou N'Dour unaonesha kuwa alizaliwa Oktoba 1, 1959 mjini Dakar nchini Senegal, baba ambaye ni wa kabila la Serer.

Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 12, kwa miaka michache alikuwa akiimba mara kwa mara katika bendi ya Star, ambayo ilikuwa maarufu zaidi mjini Dakar, mnamo miaka ya 1970.Aidha aliwahi kupiga muziki katika bendi ya Orchestra Baobab nyakati hizo.

Ingawa Youssou N'Dour ana uhusiano wa tamaduni za Griot kwa upande wa mama yake, yeye hakulelewa katika utamaduni huo, ila alijifunza kutoka kwa ndugu zake.

Wazazi wake walimtia moyo wa kutazama mambo kwa njia za kisasa zaidi, wakiacha kuzizoea tamaduni zote mbili. Matokeo yake alijichukulia mwenyewe kama mtu wa kisasa katika jamii ya Griot.

Mwaka 1979, Yousou alianzisha kundi lake mwenyewe la Etoile de Dakar. Kazi yake ya mwanzo akiwa na kundi hilo ilikuwa katika mtindo wa kawaida wa Kilatini uliokuwa maarufu kote Afrika wakati huo.

Mnamo miaka ya 1980 alianzisha sauti ya kipekee wakati alipoanzisha kundi lake jingine la Super Etoile de Dakar akishirikiana na Jimi Mbaye, kwenye gitaa.Wapigaji wengine walikuwa akina Habib Faye aliyekuwa akipiga gitaa zito la besi, Tama alikuwa akizidunda ngoma na mchezaji Assane Thiam.

Yosou N’Dour ana mvuto wa upigaji ambapo muziki wake hauegemei upande wowote.Hupiga mitindo mingi kuanzia Samba ya Cuba hadi Hip hop, Jazz na Soul, zilizompatia mamilioni ya mashabiki Kimataifa.

Katika nchi za Magharibi, Youssou ameshirikiana na wanamuziki wengine akina Peter Gabriel, Red Axelle, Sting, Alan Stivell, Bran Van 3000, Neneh Cherry, Wyclef Jean, Paul Simon, Bruce Springsteen, Tracy Chapman, Branford Marsalis, Ryuichi Sakamoto, Dido na wengineo.

Nchini Senegal, Youssou ni nyota mwenye nguvu ya utamaduni anayeshiriki kikamilifu katika masuala mengi ya kijamii.Amejaaliwa kuwa na vipaji mbalimbali vya ajabu, mtunzi wa nyimbo, kiongozi wa bendi, na mtayarishaji na mwenye uwezo mkubwa katika muziki.

Gazeti la New York Times liliielezea sauti yake kama "Sauti nyembamba yenye kukamata, silaha nyumbufu iliyotumika kwenye mapambano na yenye mamlaka ya kinabii". Youssou N'Dour ameuteka wigo wa muziki wote wa Senegal katika kazi yake.

Mwezi Julai 1993, mchezo wa kuigiza wa Kiafrika uliotungwa na Youssou N'Dour ulioneshwa katika tamasha jijini Paris nchini Ufaransa. Aliandika na kutumbuiza wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 1998, akiwa na Axelle Red ‘La Cour des Grands’.

Youssou N'Dour aliteuliwa kuwa Balozi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) tarehe 16 Oktoba 2000.Rasilimali kubwa ya Youssou N'Dour ni kwamba ana ufahamu mkubwa sana katika utamaduni wake.

Hata kama aliamua kutafiti mahali pengine, mizizi yake ni imara. Baadhi wamekwenda mbali wakimuelezea kama Msanii wa Afrika wa Karne (jarida la Folk Roots).Ameshafanya ziara za kimataifa kwa miaka thelathini. Alishinda tuzo yake ya kwanza ya American Grammy Award (best contemporary world music album) kwa CD yake ya Egypt mwaka 2005.

Mwaka 1991 alifungua studio yake ya kurekodia, ya Xippi, na alitengeneza lebo yake mwenyewe ya Jololi mwaka 1995.N’Dour pia ni mmiliki wa L'Observateur, moja ya magazeti makubwa nchini Senegal, na kituo cha redio RFM (Radio Future Medias).

Youssou N'Doura amekuwa akijihusisha na masuala kadhaa ya kijamii na kisiasa. Mwaka 1985, aliandaa tamasha kwa ajili ya kutolewa kwa Nelson Mandela.Alishirikiswa kuimba katika matamasha ya Haki za Binadamu yalilojulikana kama ‘Amnesty International Human Rights Now’ mwaka 1988 duniani kote.

Ziara iliyomshirikisha Lou Reed kuchangia toleo la wimbo wa Peter Gabriel uliotolewa na Richard James Burgess na kushirikishwa kwenye albamu ya Amnesty International.Yousou amewahi kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa na UNICEF na alianzisha mradi wa Joko kwa kufungua migahawa ya Intaneti katika Afrika na kuunganisha jamii ya Senegal duniani kote.

Amewahi kutumbuiza katika matamasha maarufu ya Live manane likiwemo la Live 8, London, t Live 8, Paris na katika tamasha la Live 8, Mradi wa Edeni katika Cornwall tarehe 2 Julai 2005, akiwa na Dido.

Mwaka 2006, Youssou N'Dour alicheza katika filamu ya kustaajabisha ya Wafrika-Waingereza (African-British abolitionist Olaudah Equiano), iliyoelezea juhudi za William Wilberforce kumaliza utumwa katika Dola ya Uingereza.

Alishiriki katika "Jealous Guy" akiwa na John Lennon kaitka CD ya 2007, Karma Instant , kampeni ya Amnesty International Kuiokoa Darfur pia alishiriki katika kampeni ya pamoja ya Hispania na Senegal dhidi ya wahamiaji haramu.
Aidha Youssou N'Dour alishiriki katika Soko la Hisa la mradi wa Visions mwaka 2007. Tangu mwaka 2007 amekuwa mwanachama wa baraza la World Future Council.Mwaka 2008, Youssou N'Dour alitoa kama zawadi moja ya nyimbo zake za bebe, kwa mwimbaji wa Kifaransa, Cynthia Brown.

Mwaka 2009, aliachia wimbo wake "Wake Up (It's Africa Calling)" chini ya leseni ya Creative Commons ili kusaidia afya kimataifa katika kampeni ya IntraHealth Open ili kuleta chanzo cha maombi ya wazi ya afya kwa Afrika.

Wimbo uliorudiwa ukichanganya wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nas, Peter Buck wa R.E.M., na Duncan Sheik kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kampeni.

Mwaka 2011, N'Dour ilitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima katika Muziki kutoka Chuo Kikuu cha Yale.

ROSE MHANDO ‘ALIPUGWA’ KWA KUBADILI DINI.

0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.

“Mchumia Juani hulia kivulini” msemo huu unajionesha wazi kwa mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Mhando, alifukuzwa nyumbani na familia yake, hivi sasa yupo vizuri kimaisha.

Aliwahi kutamka kuwa maisha yake yalianzia katika hali duni sana, alikuwa akiombaomba baada ya kufukuzwa katika familia yake huko Dumila mkoani Morogoro kwa kosa la kubadili dini.

Rose Mhando kabla hajawa mkristo alikuwa Muislam, aliyesoma vyema Koraan.

“Nilikuwa mwimbaji mzuri sana wa Kaswida, nikihudhuria kila siku Madrasa nikiwa Dumila. Baadaye maisha yangu yalikuwa magumu sana, chanzo cha hayo yote ilikuwa ni ugonjwa uliosababisha afya yangu kudhoofu. Nilipimwa kila ugonjwa sikukutwa na tatizo. Ndipo siku nilipoamua kwenda kwenye maombi” alieleza Rose Muhando.

Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9.

Rose alisumbuka na maradhi hayo kwa kipindi cha mitatu, baada ya maombi hayo alipopona aliamua kubadili dini yake na kuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 12.

“Nilipobadili dini, wazazi wangu walichukizwa na uamuzi wangu, waliona ni busara kunifukuza nyumbani, kumbe walizidi kunihatarishia maisha yangu. Niliendelea kutangatanga na baadaye nilipata waume, ambao walinizalisha watoto watatu” anasimulia Rose.


Wasifu wa Rose Mhando unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1976, katika kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.Alianza muziki wa injili katika kwaya iliyoko Dodoma, akawa mwalimu wa Kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika Kanisa la Kianglikana la Chimuli.

Rose hutunga na kuimba nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili, ambaye weledi wake, Januari 31, 2005, alizawadiwa tuzo ya Mtunzi mzuri wa nyimbo, Mwimbaji Bora na Albamu Bora ya mwaka.

Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004.
Rose Desemba 2005, alihudhuria katika Tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane, jijini Dar es Salaam.

Aidha Februari 2011, alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal with sony Music.Hafla ya kusaini mkataba huo, ilitangazwa katika mkutano wa Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki.

Baadhi ya albam za Rose Muhando ni, ‘Mteule uwe macho’ ya mwaka 2004, ‘Kitimutimu’ ya mwaka 2005, ‘Jipange sawasawa’ ya mwaka 2008, ‘Utamu wa Yesu’ ya 2012 na ‘Kamata pindo la Yesu’ ya mwaka 2015.
Tuzo alizopata 2005 Tanzania Music Awards, Best Female Vocalist & Best Religious Song ya ‘Mteule uwe macho’ya mwaka 2009, The Best Tanzanian Gospel Singer Awards, Rose Mhando The Best Singer in Tanzania, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) lilimtunuku zawadi ya shilini 200, 000 kwa wimbo wa ‘Nibebe’ na mwaka 2008 alipata tuza ya Kenya groove kama msanii bora wa nyimbo za injili Afrika.

Baadaye nguli huyo alitangaza kurudi tena katika dini yake ya Kiislamu, akidai kugundua kuwa ule upendo aliwahi kuambiwa upo katika Ukristo hauoni zaidi ya majonzi na maumivu kila siku.

Habari za Rose Muhando zilisambaa sana kutokana kuwa mwanadada huyo kwa sasa aliyekuwa akinekana kama amechanganyikiwa, amefirisika na hata watoto wake hawana tena mahali pa kuishi. 

Ikumbukwe kwamba Rose alikuwa moja ya wasanii wakubwa sana wa injili huku akisifiwa kila kona ya humu nchini na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kazi zake ambazo zikipendwa na kila mtu bila kujali umri wala dini.

Maisha uliyoishi zamani hayawezi kukukwamisha kufikia malengo uliyojiwekea.

Leo hii hakuna mtu ambaye alifikiri Rose Muhando angeweza kuwa mwanamuziki mkubwa wa nyimbo za Injili anayelipwa fedha nyingi kutokana na muziki wake, hasa kwa wale waliomjua tangu utoto wake.

Msanii huyo alisaini mkataba mnono wa miaka mitano na Kampuni ya Sony Music Africa ya Afrika Kusini, alioanza kuutumikia mwaka huu 2014.

Rose Mhando aliendelea kusimulia machungu aliyokuatana nayo wakati akiwa na mtoto wake mchanga akisema:

“Nikiwa na mtoto wa miezi sita niliwahi kufukuzwa na mchungaji mmoja jijini Arusha kwa kuwa tu nilikwenda kumwomba msaada wa fedha kidogo za kurekodi studio. Kitu hicho kiliniuma sana na sitakisahau katika maisha yangu. Kila nikikaa hukumbuka na kuumia sana.”

Alisema kwamba alifika Arusha kwa ajili ya kurekodi wimbo wake wa kwanza, ambapo kutokana na kutokuwa na fedha, aliona ni busara kumuomba msaada mchungaji huyo, lakini ilishindikana.

“Alinifukuza nikiwa na mtoto mchanga aliyekuwa na mgonjwa wa pumu, niliumia sana na hapo ndipo nilipomwambia Mungu nikasema yeye anajua ameniandalia nini kwenye maisha yangu,” anaeleza Rose.

Alisimulia kuwa alianza safari ya kurejea nyumbani, lakini kwa bahati nzuri njiani alikutana na watu wenye asili ya Somalia, akajitambulisha kwao kuwa aliwahi kuwa muumini wa dini ya Kiislamu, nao walimsaidia na kumsafirisha hadi mkoani Morogoro.

Baada ya kufika Morogoro aliendelea na maisha na baadaye alirudi Dodoma ambako alijiunga na kwaya moja mjini humo, wakati huo alikuwa tayari ana watoto watatu, akiwa pia ameshaokoka.

“Nilianza muziki katika kwaya iliyopo Dodoma, baadaye nikawa mwalimu wa kwaya hiyo ya Dodoma St. Mary’s katika Kanisa la Kianglikana la Chimuli. Niliendelea hivyo mpaka nilipoamua kuanza kutunga nyimbo zangu mwenyewe kwa msaada wa mfuko wa kwaya yetu,” anabainisha na kuongeza:

“Januari mwaka 2005, ndipo nilipoanza kuona uwepo wa Mungu, nilipokea tuzo mbalimbali ikiwamo ya Mtunzi Bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na Albamu Bora ya Mwaka, zilizotolewa na Tanzania Gospel Music Awards 2004.”

Rose Mhando alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka. Pia Rose aliwaponda baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati ninaokoka niliambiwa maneno ya faraja sana kwamba nitakutana na upendo, badala yake nimekuwa nikikutana na matusi kila siku. Mfano mtu anakualika sehemu unashindwa kufika na unatoa taarifa, kesho yake unasikia kuwa anatangaza umemtapeli! Wanashindwa kujua na kukumbuka hata jema moja kutoka kwangu! Nafikiria kurudi kwenye dini yangu ninaamini nitapata faraja” alitamka Rose Mhando kwa uchungu.

Nyota huyo wa nyimbo za injili aliendelea kusimulia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo amewahi kutekwa mwanaume mmoja akiwa na bastola, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kufanya naye mapenzi, lakini ‘alidunda’.

"Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye, huyu Bwana ana jina kubwa sana Dodoma.

Alinichukuwa kwenye gari lake kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana tangu awali alikuwa ananisaidia katika kazi zangu.

"Nilishangaa kumuona anaelekeza gari nje ya mji, nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajuwa. Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, nikaamini kuwa walikuwa wasaidizi wake” alisimulia Rose.

Kumbe ulikuwa mpango kabambe, wale watu wakamuweka chini ya ulinzi, wakamfunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola usoni.

Rose huku aliendelea kudai kuwa, mpaka hapo hakuwa amejuwa kisa cha kuwekwa chini ya ulinzi, akaambiwa kuwa, anatakiwa kuwa chini ya himaya ya kimapenzi na mwanaume huyo aliyekuja naye, la sivyo siku zake zilikuwa zinahesabika.

“Niliona ni jambo la ajabu, kwani mwanaume kumtaka mwanamke ni mpaka silaha na kutishia kuua?" alihoji nyota huyo mkubwa wa nyimbo za ijili.

Ili kuyanusuru maisha yake, akatumia mbinu ya kuwa mpole kwa pale akakubali kuwa tayari kuwa mpenzi wake, lakini nikamwambia warudi mjini wakae waongee kwa kirefu. Kwa bahati njema bwana huyo akakubali.

“Tulifika mjini nikiwa najisikia kuumwa sana maana wale wasaizidi wake walikuwa wakinisulubu kwa kunipiga, pia ile kamba niliyofungwa ilichangia kunipa maumivu makali" alilalama Rose.

Mhando alisema walipofika mjini walipanga kukutana ili wayaongee, lakini yeye akakacha kutokea kwenye kikao hicho, badala yake akaenda polisi (hakutaja kituo) ambako alifungua jalada la uchunguzi.

“Nimekuwa nikisita kumwanika kwa jina huyo mwanaume huyo ambaye ni adui yangu mkubwa. Naishi kwa tahadhari kubwa sana, naamini siku nikimtaja ataniua”

"Mbaya zaidi najua mambo yake mengi, mabaya kwa mazuri lakini mabaya ni mengi sana kwani hata wakati ananisaidia kuhusu kazi zangu, alinitenda maovu mengi, nimemwachia Mungu" alisema Rose Mhando.

Akieleza sababu ya kuyaeleza haya katika kipindi hicho, Rose alisema:

"Nimeamua kusema ili moyo wangu uwe mweupe, nimekuwa nikiwaza siku hadi siku kuhusu lile tukio, ni kumbukumbu mbaya sana kwangu, lakini kwa kukiri kwangu huku sasa nitakuwa na amani."
Amani”

Alisema alifungua jarada Polisi, walisema watafanya uchunguzi wa kina lakini hakuwahi kuambiwa walifikia wapi!Rose, alisema kuwa jamaa huyo alishawahi kuanza kuonesha dalili za kunitaka kimapenzi, lakini yeye alimuonesha kuwa hataki, akisisitiza kuwa yeye anataka kazi kwake na si mapenzi.

Rose Mhando hivi sasa anatamba na wimbo ‘Wololo’ alioutoa chini ya kampuni ya Sony Music Africa.


Makala hii inatoa Kongole kwa ujasiri mkubwa kukabiliana na maovu ambayo ungelitendewa.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.

Mwandaaji anapatikana kwa namba: 0713331200, 0736331200, 0767331200 na 0784331200.

DC MTATIRO ATATUA MGOGORO WA POLISI NA BODABODA.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma Ndg. Julius Mtatiro, ametatua mgogoro wa muda mrefu kati ya jeshi la polisi na bodaboda wa wilaya yake.

Mgogoro huo uliibuka juzi Ijumaa na kupelekea polisi wakabiliane na vijana wa bodabida na kuwapiga mabomu ya machozi na kuwakamata.

Ndg. Mtatiro aliahirisha ziara ya kikazi wilayani Songea na kurejea Tunduru moja kwa moja, akaitisha kikao cha dharura katika kituo cha polisi na viongozi wa bodaboda na kuamuru bodaboda zote zilizoshikiliwa na vijana wote walioshikiliwa, waachiwe mara moja, jambo ambalo lilitekeleza na Kamanda wa Polisi wa Wilaya siku hiyo hiyo ya Ijumaa.

Jana Jumamosi Ndg. Mtatiro aliitisha kikao kikubwa zaidi kikiwahusisha bodaboda wote wa Tunduru ili kusikiliza na kutatua kero zao. Katika majumuisho kikao hicho kilikubaliana polisi waache kuwapiga vijana wa bodaboda katika oparesheni za kipolisi, DC Mtatiro amepiga marufuku tabia ya polisi kukimbizana na bodaboda wachache watovu wa nidhamu na badala yake amewataka polisi wachukue namba za pikipiki husika na kisha kumuita mmiliki na dereva na kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu kufukuzana kumekuwa kukileta ajali mbaya.

DC Mtatiro amewaonya vijana wa bodaboda na kuwataka wafuate sheria, wakisimamishwa na polisi wasimame na kutoa ushirikiano na amewataka polisi wasitumie nguvu bila sababu, akiwapa mfano wa tukio la Ijumaa la Mabomu na kulielezea kama halikuwa na uzito wa kupiga mabomu na kuwaumiza vijana.

DC Mtatiro ameaakumbusha polisi kuwa, Dkt. Magufuli, Rais wa Tanzania hataki kuona vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, wananyanyaswa na kupigwa maana ni vijana hao ndiyo watakaoipigia kura CCM na kuirejesha madarakani na kwamba kuwanyanyasa kunaenda kinyume na malengo ya CCM ya kuwalinda vijana.

Katika mkutano huo, DC Mtatiro alifanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Kangi Lugola (MB) kumuomba ufafanuzi juu ya maelekezo yake ya makosa ambayo polisi hawapaswi kuyatumia kuwakamata madereva wa bodaboda na bodaboda zao.

Mhe. Waziri Kangi Lugola alifafanua kuwa yeye hajasema bodaboda wasio na helmet, waliobebana "mishikaki" na wanaotenda makosa mengine wasiadhibiwe na kwamba alichosema ni kutaka polisi wawatoze faini (ya kulipa ndani ya siku 7) au kuwaonya bodaboda wote wanaokutwa na makosa ya helmet, kukosa leseni au mishikaki na kuwa polisi wasiwakamate madereva hao, abiria wao au bodaboda zao ikiwa wamewakuta na makosa hayo.

Katika simu hiyo ambayo ilikuwa inasikilizwa na wananchi wote kupitia vipaza sauti, Waziri Kangi aliwataka wananchi wa Tunduru kumtumia sana Mtatiro kutatua kero zao na kujiletea maendeleo haraka kwa sababu ya misimamo ya DC Mtatiro, weledi wake, uthubutu na kiu yake ya kuwasaidia wanyonge.

DC Mtatiro ameagiza sheria za barabarani zifuatwe lakini vijana wa Tunduru wasinyanyaswe na kuumizwa kwa sababu yoyote ile, jambo ambalo limekubaliwa na pande zote - polisi na madereva bodaboda.

Kikao cha DC Tunduru, Polisi na madereva wa bodaboda kimemalizika kwa amani sana na pande zote zikashikana mikono na kufurahi pamoja huku vijana wa Tunduru wakimpongeza sana DC wake.

Source; Mkutano wa DC Mtatiro, Bodaboda na Polisi.
07 Septemba 2019.

KUMBUKIZI YA MPIGA DRUM BORA NCHINI MAREHEMU ABUU SEMHANDO BABA DIANA"

0
0
Abuu Semhando (ua jekundu mfukoni kati) akiwa Orchestra Vijana jazz Wana-Pambamoto wakiwa .Morogoro siku Mandela alipotembelea baada ya kufunguliwa. Waliokaa mbele kushoto Mpenzi, Baker Semhando (Bassist), Juma Choka (Drummer) sasa yuko Sikinde, Waliosimama toka kushoto, John Kitime(guitaa na kuimba),sasa yuko Kilimanjaro Band-Wananjenje, Dereva wa msafala,Marehemu Aggrey Ndumbalo (Rhythm gitaa, Mhasibu), Abuu Semhando (Drummer) s Twanga Pepeta, Maerehemu Freddy Benjamin (Muimbaji), Said Mnyupe (Trumpetist) sasa yuko msondo, Saidi Ndula (Saxophone, Rashid Pembe (saxophone), Hassan Shaw (keyboards).....Pambamoto awamu ya pili

Na Moshy Kiyungi, Tabora.
Septemba, 2019.

Mungu aliumba kusahau, lakini historia haiwezi kuashaulika katu. Inakaribia miaka 9, tangu maisha ya mwanamuziki Abuu Ally Semhando yalipokatizwa hata kabla ya kutimiza ndoto alizokuwa amejiwekea.

Ajali ya pikipiki aliyokuwa akiiendesha mwenyewe, aliyopata nayo ajali akitokea kazini, iliyopelekea kifo chake Desemba 18, 2010, jijini Dar es Salaam akiwa ametimiza umri wa miaka 57.
Semhando wakati wa uhai wake alichangia mafanikio ya Kampuni ya African Star Entertainment Tanzania (ASET), kwa asilimia kubwa kutokana na kujitoa kwa kila hali.
Alidumu kwa kipindi kirefu katika bendi hiyo toka alipojiunga mwaka 1998, akitokea katika bendi ya Diamond Sound ‘Wana Kibinda Nkoi’.

Kifo chake kiliwatia simanzi watu wengi hususan mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya ASET Asha Baraka, aliyemuelezea Abuu kuwa aliitumikia Twanga kwa mapenzi makubwa kama mali yake binafsi.
Asha alitamka kuwa Semhando alikuwa ni chachu ya mafanikio ya albamu zote 10, ambazo wamezitoa kutokana na kushiriki katika kuandaa muziki na kusimamia nidhamu ya wanamuziki wa bendi hiyo.
Kifo cha Abuu Semhando katika familiya yake, kiliigusa kwa kiasi kikubwa hususan binti yake Sharifa, ambaye siku ambayo alikuwa anatakiwa kufungishwa ndoa, ndiyo siku baba yake mauti yalipomfika, sherehe hizo zikageuka msiba mkubwa.
Wasifu wa nguli huyo unaeleza kuwa jina lake kamili lilikuwa akiitwa Abuu Ally Semhando maarufu ‘Lokassa’ au ‘Baba Diana’
Alikuwa mcharazaji mahiri wa drums wakati huo huo alikuwa ndiye meneja wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Abuu Ally Semhando ‘Lokassa’ alizaliwa mwaka 1953 Kijiji cha Kibanda Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Alianza shughuli za muziki mwanzoni mwa miaka 1970, akiwa katika bendi ya Tanga International iliyokuwa ikitoa burudani mjini humo wakati huo.
Baadaye alikwenda kuwa mmoja kati ya waasisi wa bendi za Tanza Muzika na Orchestra Tomatoma kabla ya kutua Safari Sound Orchestra (OSS).
Abuu Semhando na Hamza Kalala ni miongoni mwa wanamuziki waanzilishi wa bendi ya Super Matimila, ni hao waliowakaribisha marehemu Mose Sengo Fan Fan na Dk. Remmy Ongala katika bendi hiyo.
Katika pilika za kutafuta maisha, Semhando alikwenda kujiunga na bendi ya Vijana Jazz ‘Pamba Moto’, ambako huko alionekana kuwa anao uwezo mkubwa wa kuongoza, akakabidhiwa nafasi ya kuwa Katibu wa bendi.
Semhando alishiriki kupiga drums kwa kiwango kikubwa katika nyimbo nyingi ambazo ziliiletea mafaniko bendi hiyo ya Vijana Jazz.
Aliyekuwa mtunzi na mwimbaji maarufu toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Selemani Kasalo Kyanga, alimpachika jina bandia la ‘Lokassa’, wakiwa katika bendi ya Tancut Alimasi iliyokuwa na makazi yake mjini Iringa.
Licha ya kuwa mpiga drums, Sembando alikuwa ni mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa cha uongozi wa bendi.  
Alishiriki katika kuandaa muziki kila bendi aliyopitia alihakikisha inapata mafanikio makubwa. Jambo hilo lilimjengea umaarufu maradufu.
Historia inaonesha kuwa kila bendi alizowahi kupitia akiwa kiongozi baada ya kuondoka, ziliyumba na zingine kutokomea kabisa katika medani ya muziki wa dansi.
Lakini si Super Matimila pekee yake hata alipokuwa na Vijana Jazz ‘Saga rhumba’ ambako alikuwa Katibu chini ya uongozi wa Hemed Maneti, alikuwa mmoja wanamuziki walioshiriki katika kuiletea mafanikio kwa miaka yote hiyo kabla ya kujiondoa.
Yaelezwa kuwa Abuu pia akiwa na bendi ya Vijana aliasisi ‘Vijana Day’ iliyokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa Vijana Hostel, Kindondoni jijini Dar es Salaam.
Alishiriki kwa kiwango kikubwa kutengeneza mashairi ya nyimbo nyingi akiwa na waimbaji akina Hemed Maneti, Saidi Hamis ‘Misukosuko’, Fred Benjamin, Cosmas Chidumule na Kida Waziri.
Aidha Semhando alishirikiana vyema na wapiga ala wenzake wakati huo wakiwamo Kulwa wa Milonge, Hamza Kalala, Hassan Dalali, Agrey Ndumbalo, Rashid Pembe, Hassan Shaw na Disfa Semhando (mdogo wake), aliyekuwa akiliungurumisha gitaa la besi.
Aidha alikuwepo mpiga gita la solo Shabani Yohana “Wanted” na wengine wengi.
Akiwa na safu hiyo ambao ni baadhi tu ya kundi alilokuwa nalo, walishiriki kutengeneza nyimbo kali kama ‘Bujumbura’, ‘Mary Maria’, ‘Tambiko la Pambamoto’, ‘Mundinde’, ‘Ali Hassan Mwinyi apewe Kura za Ndiyo’, ‘Wifi Zangu Wananinyanyasa’, Stella, ‘Penzi haligawanyiki’ na nyingine nyingi nzuri kupindukia.
Nyimbo hizo zilitikisa medani ya muziki chini ya uongozi shupavu wa viongozi wake akina Hemed Maneti aliyekuwa kiongozi, Hamza Kalala alikuwa ni kiongozi msaidizi na Abuu Semhando mwenyewe  aliyekuwa Katibu.
Katika kudhihirikisha uwezo aliokuwa nao alipojing’atua katika bendi hiyo, ndipo jinamizi na anguko la bendi ya Vijana Jazz lilipoanza kuinyemelea.
Baadhi ya wanamuziki aliofanya nao kazi walimzungumzia marehemu Semhando akiwemo  John Kitime ambaye alisema kuwa ataendelea kumkumbuka Abuu Semhando kwa ucheshi wake.
Kitime aliwahi kutamka kuwa yeye alimpokea na kumtafutia malazi jijini mwaka 1989, wakati anajiunga na Vijana Jazz akitokea Tuncut Almasi ya Iringa.
Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando, Kasaloo Kyanga, Fan Fan
Kwa upande wake mkung’utaji wa gitaa la solo Aldof Mbinga, hakusita kutamka kuwa tasnia ya muziki wa dansi imepoteza Jemedari ambaye alikuwa hayumbi katika misimamo yake jambo ambalo lilileta mafanikio kwa wanamuziki na bendi Vijana Jazz kwa ujumla.
Mbinga alifanya kazi na Semhando kwa kutengeneza albamu ya kwanza ya Twanga Pepeta ya ‘Kisa Mpemba’ na ‘Jirani’.
Wengine waliomzungumzia marehemu Semhanso ni pamoja na Waziri Ally ambaye ni mwanamuziki na kiongozi wa bendi The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’, alimtaja Semhando kama nguzo iliyokatika ghafla wakati watu wakiihitaji huduma licha ya ukongwe wake katika muziki.
Ushuhuda mwingine ulitolewa Isihaka Kibene, ambaye alisema, Twanga Pepeta imepoteza mpiganaji na mtawala mahiri kutokana na kuwa kiungo katika kufanya majukumu ya kila siku ya bendi.
 “Huyu jamaa alikuwa rafiki yangu sana ambaye niliwahi kufanya naye kazi kiwanda cha Uchapaji cha Printpak miaka ya 1970, na hata alipoanza shughuli za muziki tuliendelea kuwa marafiki..." alisema Kibene.
Abuu Ally Semhando aliacha mjane na watoto 10, alizikwa kijijini Kibanda Wilaya ya Muheza moani Tanga alikozaliwa.
Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0784331200, 0736331200, 0713331200 na 0767331200

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KAMATI YA SIASA MKOA WA KUSINI UNGUJA, AZUNGUMZA NA WAZIRI HAMAD RASHID MJINI ZANZIBAR

0
0
 Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ndg. Ramadham Abdala Ali wakati alipowasili katika Ofisi za Mkoa huo leo Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa kamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Unguja wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwasalimia viongozi hao katika Ofisi za Mkoa huo leo Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa kamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Unguja wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwasalimia viongozi hao katika Ofisi za Mkoa huo leo Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi wa kamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Unguja walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ndg. Ramadham Abdala Ali (wa tatu kushoto waliokaa ) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi za Mkoa huo Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ndg. Ramadhan Abdala Ali baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi za Mkoa huo Mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ndg. Hassan Khatibu Hassani
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizunguma na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed walipokutana leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Mjini Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu na Amali, Mhe. Simai Mohamed Said walipokutana leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Mjini Zanzibar. Katikati ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed walipokutana leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani, Unguja. PICHA NA OFISI ZA BUNGE

MKUU WA WILAYA UBUNGO AUPONGEZA UONGOZI WA DAWASA KWA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri.

Hayo aliyasema wakati wa kikao kazi mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo .

Akizungumzia utoaji wa huduma ya maji, Amesema kwa upande wa Wilaya ya Ubungo malalamiko ya maji yamepungua kwa asilimia kubwa tofauti na hapo awali.

“Napongeza uongozi wa DAWASA Ubungo kwa kuweza kusimamia mchakato mzima wa kutoa huduma ya maji hata wakati naenda kuzindua baadhi ya miradi ya maji kwenye Wilaya hii wananchi walikua na shamra shamra kubwa baada ya kukaa muda mrefu bila maji”

Amesema Makori , “katika Wilaya iliyokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ni hii ya Ubungo na kipindi nateuliwa kuja kuwa Mkuu wa Wilaya nilikuwa napokea malalamiko ya maji kila siku, ila kwa sasa idara ambayo inafanya kazi vizuri ni hii ya DAWASA nawapongeza sana,”


Naye Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ubungo, Pascal Fumbuka amesema eneo la huduma linalohudumiwa na Dawasa Ubungo linapokea Maji kutoka mtambo wetu wa Ruvu juu kilasiku lina sifa ya milima na mabonde kijiografia na kupelekea kuwa na mgawanyo wa huduma kulingana na maeneo kwenye kata 10 za Wilaya hiyo.

Amesema,  Dawasa Mkoa kazi wa Ubungo wamedhamiria katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma unafikia asilimia 95 ifikapo 2020, Pia Kuhakikisha Upatikanaji wa huduma ya Maji ni wa uhakika kwa kupunguza migao mikali na kuongeza usukumaji maji milimani.

Aidha, Fumbuka ameeleza mpango mkakati ni Kuhakikisha kuongeza kaya zinazopata maji kutoka 74,837 hadi kufikia 121,187(Sawa na asilimia 100% ya usambazaji wa huduma) pamoja na Kuhamasisha Wananchi kuendelea kupata huduma ya maji kwa njia ya mkopo

Fumbuka ameeleza zaidi, Dawasa wameweka malengo ya Kuhakikisha wanapunguza malalamiko ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutoka malalamiko 972 (2018/19) hadi malalamiko 0 (sifuri) kwa mwaka huu wa fedha 2019/20 na Kwa kushirikiana na jamii kuhakikisha kiwango cha maji yanayopotea kinapungua kutoka asilimia 25 (2018/19) hadi asilimia 10( 2019/2020) na baadae.

Mkuu wa Wilaya alitoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri na kuwataka waendelee kuwahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ubungo, Pascal Fumbuka akielezea mpango mkakati wa Mkoa wa Kihuduma Ubungo wa kuhakikisha wanaongeza  kaya zinazopata maji kutoka 74,837 hadi kufikia 121,187(Sawa na asilimia 100% ya usambazaji wa huduma) pamoja na Kuhamasisha Wananchi kuendelea kupata huduma ya maji kwa njia ya mkopo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akiupongeza  uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazis nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo .
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akitoa zawadi ya vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri katika utoaji huduma kutoka vitengo tofauti wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori  akitoa zawadi ya vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri katika utoaji huduma kutoka vitengo tofauti wakati wa kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.  
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia kikao kazi cha mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo.





KAILIMA ARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA IDARA YA UHAMIAJI DODOMA

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakimsikiliza Mhandisi Issa Mohamed Issa wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019.

Na Mwandishi Wetu-MOHA, Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 8 la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, linalojengwa Mjini Dodoma.

Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 30 na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2020 ila unaweza kumalizika kabla ya muda huo kama hakutatokea changamoto yoyote. Kailima aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Jengo hilo linajengwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT). Alisema ziara hiyo imelenga kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli juu ya kuhamia Dodoma.

Alifafanua kuwa, SUMA JKT ina Wakandarasi wazuri wenye uzoefu mkubwa kwenye ujenzi wa majengo mbalimbali. “SUMA JKT unapowapa mradi, ujenzi wake huwa unakamilika kwa wakati ndio maana hupewa kazi nyingi za ujenzi wa majengo ya Serikali,” alisema.

Kailima alisema hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye hatua ya awali (chini), lengo la Serikali ni kuifanya Idara ya Uhamiaji iondokane na uhaba wa majengo kwenye mikoa mbalimbali.

“Hivi sasa tunaendelea na ukarabati kwenye majengo ya Uhamiaji Mtwara, Lindi, ukarabati mwingine utafanyika Manyara,” alisisitiza Kailima.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (aliyekaa) akisisitiza jambo wakati akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji, Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019 kutoka kwa Mhandisi Issa Mohamed Issa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (watatu kushoto) na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Mhandisi Issa Mohamed Issa alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akisisitiza jambo wakati akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Ma;pinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania.Profesa Lucas Domingo Hemandez Polledo,alipofika Ikulu Zanzibar na Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje Nchini Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzelez,akiwa (katikati) hafla hiyo imefanyika leo,8,Septemba 2019 Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba.Mhe. Marcelino Medina Gonzalez,alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 8,Septemba 2019.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika mazungumzo na mgeni wake, Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Marcelino Medina Gonzalez, kushoto Balozi Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa.Lucas Damingo Hemandez Polledo,hafla hiyo imefanyika leo 8, Septemba 2019, Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzalez, wakitoka katika ukumbi wa Ikulu baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo, 8,Septemba 2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Naibu Waziri wa Kwanza waWizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzalez, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo, 8,Septemba 2019.(Picha na Ikulu, Zanzibar)

WATALII WAMIMINIKA KATA YA MAGATA MKOANI KAGERA,WASIFU UKARIMU WA WATANZANIA

0
0
IDADI kubwa ya watalii kutoka nchini Dernmark wamekuja wamefunga safari kwenda katika Kata ya Kata ya Magata mkoani Kagera kwa ajili ya kuona vivutio vya utaliii vilivyopo kwenye Kata hiyo.

Inaelezwa kuongezeka kwa idadi ya watalii kwenye Kata hiyo kutokana na mazingira mzuri ya uwepo wa huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kuwa na maeneo mengi ya Utalii.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Bukoba Tours William Rutta amesema kuwa katika hiyo kuna vitu vingi ambavyo vinapendwa na watalii na kuongeza wakazi wa eneo hilo ni wakarimu na wakulima wazuri wa Vanilla.

"Pamoja na kutembelea maeneo ya Utalii,watalii wengi wamefurahi uwepo wa huduma za kijamii,"amesema na kuongeza kuwa hifadhi ya mpya ya Burigi iliyopo Chato nayo itakuwa chachu ya kuongeza watalii katika Kata hiyo na Mkoa wa Kagera.

Rutta ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ishozi iliyopo mkoani Kagera amesisitiza watalii wake watakuwa wakiweka kambi kata ya Magata wanapokuwa wanaendaa Hifadhi mpya ya Burigi Chato na Rubondo.

Pia ametoa shukrani kwa mwenyeji wake ambaye ni Katibu Mwenezi ww CCM Kata ya Magata Mansoor Amr kwani amekuwa akishiriki hatua kwa hatua kuhakikisha watalii wanapokelewa vizuri.

Kuhusu watalii hao amesema wametoka nchini Dernmak na kuongeza wamefurahishwa na ukarimu wa Watanzania huku wakieleza namna ambavyo wanaguswa na Rais John Magufuli kwa jinsi anavyowatumikia wananchi pamoja na kutangaza vema Tanzania.


RC MAKONDA ATOA KIBALI KWA WATUMISHI WA MUNGU KUTANGAZA INJILI SEHEMU ZA CLUB NA DISKO.

0
0
Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 08 ametoa kibali kwa Watumishi wa Mungu wa Dini zote kuhubiri na kutangaza neno la Mungu kwenye Sehemu za Club, Disko na Kumbi za Starehe ili neno la Mungu lizidi kuenea na kuwafikia watu wote jambo litakalosaidia kujenga jamii inayomjua Mungu.

RC Makonda amesema Mtumishi wa Mungu atakapohitaji kuhubiri mziki utazimwa kwa muda wa Nusu saa na baada ya hapo watu wataendelea na starehe zao wakiwa tayari wamepokea Neno la Mungu na kuahidi kuwa Mmiliki wa Club atakaemkatalia Mtumishi Kuhubiri RC Makonda atamwombea Mtumishi huyo na ikibidi atamsindikiza.

Hatua hiyo ya RC Makonda imekuja baada ya kubaini uwepo wa Idadi kubwa ya watu kwenye sehemu za starehe na pindi watu hao wakienda Makanisani na Misikitini wanaishia kusinzia na wengine wanakuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kulisikiliza kwa ufasaha neno la Mungu.

Hayo yote yamejiri leo wakati alipokuwa akizungumza na Maelfu ya Waumini wa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa.


BUGANDO KUANZISHA TAASISI YA MOYO

0
0
Famasi ya dawa iliyoko kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya bugando iliyoko

Jengo la huduma za dharura na ajali ambalo linatoa huduma zote zikiwemo za upasuaji

******************

Na.Catherine Sungura-Mwanza

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando(BMC) ipo mbioni kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kuhudumia wananchi wa kanda ya ziwa.

Akiongea kwenye mkutano wa maofisa habari wa wizara na taasisi wake pamoja na waandishi wa habari jijini hapa mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi alisema kuwa wapo mbioni kuanzisha taasisi hiyo itakayokuwa na majengo mawili yenye ghorofa kumi na kumi na tano.

Prof. Makubi alisema kuwa hadi kukamilika kwa majengo hayo wanatarajia kutumia shilingi bilioni 59 .

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kutoa huduma zote za kibingwa na bobezi hapa nchini,hii itapunguzia mzigo serikali na wizara kupeleka wagonjwa nje ya nchi vilevile wananchi wa kanda hii kunufaika na huduma za moyo huku huku”.

Kwa upande wa watumishi Prof. Makubi alisema wameweza kuongeza wataalam wa fani mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwepo wauguzi,madaktari,madaktari bingwa na bobezi na hivyo kufanya kazi ya utoaji huduma katika idara zote bila kuteleleka.

Hata hivyo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kusomesha madaktari bingwa na bobezi kutoka hospitali hiyo na hivyo kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za kibingwa ikiwemo matatizo ya tumbo,mifupa,koo,pua na ndomo,macho,mfumo wa mkojo,meno,ubongo na mishipa ya fahamu pamoja na matatizo ya akina mama.

“Huduma za upasuaji kiujumla zimeboreka sana katika awamu hii kwa upande wa upasuaji mkubwa wa kawaida pia,upasuaji maalumu wa midomo sungura,kichwa maji na mgongo wazi pamoja na upasuaji wa fistula”.Aliongeza Prof. Makubi

Aidha,aliishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa MOI kwa,mashirikiano ya karibu katika kutoa huduma za kibingwa,za upasuaji katika mikoa mbalimbali ya kanda ya ziwa

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA.

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania.Profesa Lucas Domingo Hemandez Polledo,alipofika Ikulu Zanzibar na Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje Nchini Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzelez,akiwa (katikati) hafla hiyo imefanyika leo,8,Septemba 2019 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzalez, wakitoka katika ukumbi wa Ikulu baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo, 8,Septemba 2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Naibu Waziri wa Kwanza waWizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba. Mhe. Marcelino Medina Gonzalez, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo, 8,Septemba 2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Cuba.Mhe. Marcelino Medina Gonzalez,alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 8,Septemba 2019.(Picha na Ikulu)
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images