Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA KILIMO WA TANZANIA MHE JAPHET HASUNGA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA KILIMO NA MAENDELEO VIJIJINI WA ISRAEL MHE URI YEHUDA ARIEL HACOHEN

$
0
0
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen, mkutano huo umefanyika Mjini Bet Dagan 50250 nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Bet Dagan-Israel


Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 5 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli moja kuwa serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.


Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima, Mhe Hasunga ametoa shukrani kwa Serikali ya Israeli kuipatia Tanzania nafasi 100 za kujifunza kuhusu sekta ya kilimo kwa vijana kupitia programu inayosimamiwa na Agrostudies.


Waziri Hasunga ameeleza katika mkutano huo dhamira ya Serikali ya Tanzania inayoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ya kuwasaidia vijana waliorudi nyumbani baada ya mafunzo hayo kwa kuanza kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo ardhi ambayo ipo eneo litakalowawezesha kujiendeleza.


Vilevile ameeleza kuwa katika wizara ya kilimo hakukuwa na kitengo cha masoko hivyo ili kuwaunganisha vijana hao na masoko ya biashara watakazozalisha serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo maalumu cha kushughulikia masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima.


Waziri Hasunga pia amezungumzia kuhusu maeneo yanayoweza kuwavutia wawekezaji kutoka Israeli ili kuwekeza nchini Tanzania kwa kutoa takwimu za ukubwa wa ardhi yenye rutuba, uwepo wa maji na hali ya hewa inayoruhusu ukuaji wa aina nyingi ya mazao.


Serikali ya Israeli ipo tayari kusaini hati ya makubaliano ya kilimo (Memorandum Of Undarstanding-MOU) ya kilimo pale itapowasilishwa na Serikali ya Tanzania, hii imekuja baada ya Mheshimiwa Waziri Hasunga kuona umuhimu wa kuingia makubaliano ili iwe rahisi wawekezaji kutoka Israel kuzuru Tanzania kuwekeza pamoja na kupata mikopo kutoka katika Serikali yao.


Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Israeli Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa nchi hiyo Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen imehaidi pindi Serikali ya Tanzania itakapowasilisha mahitaji hasa kwenye mazao ambayo muhimu ya kuanza nayo kwa ajili ya soko la Israel itakuwa tayari kushirikiana kwa kutoa ujuzi pamoja na uwezeshaji wa wataalamu.


Hata hivyo itakapotokea mwekezaji wa Israeli ataposhirikiana na kampuni ya Tanzania, Serikali inawajibu kuingilia kati kusaidia maeneo ya uwezeshaji na rasilimali watu.

RC MTAKA APEWA TUZO YA KIONGOZI BORA ALIYELETA MAPINDUZI KATIKA ELIMU

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akionesha tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.






Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi hiyo kwake ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
******************

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa Mkoa wa Simiu, Mhe. Anthony Mtaka amepewa tuzo ya elimu ya Tanzania Elimu Awards na Taasisi ya Elimu Solutions, ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed, Mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu(daraja sifuri) katika mtihani wa Mock kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Swed amesema Taasisi hiyo imefuatilia na kuona juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika mapinduzi ya elimu ikiwemo ubunifu wa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo zimeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ufaulu wa mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutoka mwaka 2016 hadi mwaka 2018.

“Anayoyafanya Mhe. Mtaka hayaishii Simiyu peke yake Tanzania inayaona, tulifuatilia habari za kambi za kitaaluma na tukaangalia nafasi ya mkoa katika matokeo na namna mlivyofanya vizuri, mmeweka alama kwenye Taifa na tunatamani Mhe. Mtaka aziendeleze juhudi hizi zaidi ili mtoke kwenye kumi bora mwende tatu bora na mwakani tupate mwanafunzi bora kutoka Simiyu atakayepata tuzo hii” alisema Neithan Swed.

Katika hatua nyingine Swed amesema Taasisi ya Elimu Solutions itatoa ufadhili kwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2019 atakayefanya vizuri katika mtihani wa Taifa na kumpeleka nchini China kuendelea na masomo.

Akipokea tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi ya Elimu Solutions kwa kutambua juhudi zinazofanywa na mkoa wa Simiyu na kutoa tuzo huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaithamini sana tuzo hiyo.

Aidha, Mtaka ameipongeza Taasisi ya Elimu Solutions namna wanavyohamasisha maendeleo ya Elimu ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenda kusoma nje ya nchi.

Tuzo za Elimu Tanzania Elimu Awards zimetolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa wadau mbalimbali wa elimu waliochangia na kusaidia kuleta mabadiliko kwa ubunifu na juhudi zao binafsi, taasisi zinazoihudumia sekta ya elimu; pia hutolewa kwa viongozi, walimu, wanafunzi waliofanya vizuri kwenye elimu

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango kazi wa Ofisi hiyo kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akisoma ripoto ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019. uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, kushoto Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mihayo Juma Nhnga na kulia Kaimu Katibu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Maulid.(Picha na Ikulu).
BAADHI ya Watendaji wa Idara za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wakati wa kusoma kwa ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Ofisi yao, kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, ulifanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Piliu wa Rais wa Zanzibar Ndg Shaban Seif Mohammed, akisoma Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yao,kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, kulia Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)

Rais Dkt. Magufuli afanya mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wakeRais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveniwakiangalia mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara waTanzania na Uganda kabla ya kuzungumza na wafanyabiashara
wa Mataifa hayo katika Ukumbi wa Julius Nyerere Convention
Centre jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha yapamoja na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni kabla ya kuelekea katika mkutano wa
Wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania uliofanyika katika
ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katikamazungumzo na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wakeRais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveniwakiangalia mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara wa
Tanzania na Uganda kabla ya kuzungumza na wafanyabiasharawa Mataifa hayo katika Ukumbi wa Julius Nyerere ConventionCentre jijini Dar es Salaam.
Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri KagutaMuseveni akizungumza na wadau mbalimbali wa biasharakutoka Uganda na Tanzania katika mkutano wao wamajadiliano uliofanyika katika Ukumbi wa Julius NyerereConvention Centre jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza nawadau mbalimbali wa biashara kutoka Uganda na Tanzaniakatika mkutano wao wa majadiliano uliofanyika katika Ukumbi
wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli atangaza siku 3 za maombolezo ya Kitaifa na bendera kupepea nusu mlingoti

Rais Magufuli na Rais Museveni wafungua jengo la Taasisi ya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufulivakipeana mikono na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kufungua rasmi jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisaidiwa na viongozi  wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi  rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakitembezwea na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere ndani ya jengo walilolifungua kwa pamoja  jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage nyerere wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akimwonesha  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baadhi ya picha na maelezo ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa walipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini kwa
ajili ya Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maeleo  kutoka kwa  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Bw.Abdulmajid Nsekela walipotembelea vibanda vya maonesho  wakati wa Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda vkatika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019 .PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akiomba wahudhuriaji kusimama kwa dakika tatu za heshima ya kumkumbukaaliyekuwa Rais wa Zimbabwe Marehemu Robert Mugabe aliyefariki jana huko Singapore akiwa katika matibabu. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanzakuhutubia Kongamano la Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda lililohudhuriwa pia na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Ijumaa Septemba 6, 2019

UONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI DAWASA WATEMBELEA MIRADI YA KIJAMII NA MAJITAKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Neli Msuya akizungumza na uongozi wa wafanyakazi wa DAWASA FIBUCA na TUICO kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya majisafi na majitaka. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii wa Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya akielezea mradi wa kuchakata majitaka wa Toangoma baada ya kutembelewa na Uongozi wa vyama vya wafanyakazi wa DAWASA vya FIBUCA na TUICO wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya akielezea mradi wa majitaka Vingunguti uliowezesha kujenga vyoo 117 kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na mabwawa ya kuchakata majitaka na kupunguza magonjwa ya mlipuko.


 Uongozi wa Vyama vya wafanyakazi wa mamlaka ya Majisafi an Majitaka Dar es Salaam wa FIBUCA na TUICO wakitembelea miradi mbalimbali ya maji safi na majitaka.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Uongozi wa Vyama vya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) FIBUCA na TUICO wametembelea miradi mbalimbali  ya Mamlaka hiyo inayopatikana ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na kufurahishwa na hatua zinazofanywa na Menejimenti inayoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Ziara hiyo imehusisha miradi ya maji ya jamii na miradi ya kuchakata maji taka ya Vingunguti na Toangoma.

Akizungumza baada ya kutembelea miradi hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi FIBUCA Eli Achahofu amesema kuwa wamefurahi sana kutembela miradi ya Dawasa ambapo itakapokuja kukamilika itamtua mama ndoo kichwani.

Amesema,” miradi yote ni mizuri hususani huu wa Vijibweni ambao utakapokuja kukamilika kero ya maji kwa wakazi wa Kigamboni itakuwa historia,”

Achahofu ameeleza kuwa, wamepata elimu kubwa sana katika ziara hiyo, na Mamlaka imepiga hatua kubwa sana katika mradi wa kuchakata maji taka na hilo limesaidia hata kupunguza magonjwa ya mlipuko ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

“Kuna vyoo 117 vimejengwa na Dawasa kwa wananchi wanaoishi Vingunguti karibu na mabwawa ya kumwaga majitaka, walielimishwa wakaelewa na kwa sasa wanaishi vizuri, vyoo vyao ni vizuri na hilo limepunguza hata magonjwa ya mlipuko ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam,”

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema miradi ya jamii yote iliyokuwa chini ya Halmashauri pamoja Jumuiya za watumiaji maji kuanzia sasa zitakuwa chini ya Mamlaka hiyo ikiwano na visima vya watu binafsi.

Amesema, hatua hiyo itasaidia kufikisha maji kwa wananchi waliopo nje ya mtandao wa Dawasa ambapo visima hivyo vimekuwa na msaada mkubwa sana ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Miradi ya watumiaji maji na ile halmashauri imekuja chini yetu Dawasa, kuanzia sasa tutaiendesha na kuboresha huduma na zaidi vipo visima vya watu binafsi ambavyo na vimesaidia wananchi kwa kipindi kirefu kupata huduma ya maji,”amesema Msuya.

“Mradi wa majitaka ambapo upo Vingunguti ambapo ni mradi mkubwa wa kuwajengea vyoo wananchi wapo waliokubali na wengine walikataa lakini mfumo uliopo ni kuwa vyoo hivyo mtu anapokitumia maji hayakai pale bali yanaenda moja kwa moja mpaka kwenye mabwawa yetu ya majitaka na hilo limesaidia sana kuondokana na magonjwa ya mlipuko,”amesema

Naye Mkazi wa Vingunguti Nuru Selemani ameishukuru Dawasa kwa kuweza kuwajengea vyoo vizuri na hatua hiyo imeweza kupunguza magonjwa ya mlipuko na pia vinadumu kwa muda mrefu.

Ameeleza kuwa kabla ya kujengewa vyoo hivyo , walikua wanatiririsha majitaka wakati wa mvua tena kwa kujificha nyakati za usiku ila mpango ulioletwa na Dawasa wa kuwajengea vyoo umesaidia sana na hata sasa watoto wao hawaumwi mara kwa mara.

Nuru amewashauri wananchi wengine wa maeneo hayo ambao hawajajengewa vyoo waweze kukubali ili waondokane na adha ya majitaka.

Uongozi huo wa Wafanyakazi uliweza kutembelea miradi ya jamii ya watumia maji Domu, Mradi wa watumia maji Moringe na Mradi wa Vijibweni  na kwa upande wa majitaka walitembelea mabwawa ya Vingunguti na Mradi wa kuchakata majitaka Toangoma.

BUGANDO YAOKOA BILIONI 2 KWA MATIBABU YA SARATANI

$
0
0
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni mbili kwa wananchi wa kanda ya ziwa kusafiri kwenda jijini Dar es Salaam kupata matibabu ya saratani kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akiongea na Maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake waliokuwepo jijini Mwanza kwa ajili ya kujionea mafanikio ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Prof. Makubi alisema kuwa kuanza kwa tiba ya saratani katika Hospitali ya Kanda Bugando imesaidia kuokoa kiwango cha fedha hizo kutoka kwa wananchi wa kanda ya ziwa ambapo awali iliwalazimu kusafiri hadi Jijini Dar es Salaam kupata huduma hizo kwenye Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

“Tunaishukuru Wizara ya Afya ambayo ilitupatia kiasi cha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kujenga jengo la saratani. Kama hospitali tumeweza kununua mashine nne za mionzi na dawa kwa kushirikiana na wafadhili wengine".

Aidha, alisema, hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa hawapelekwi wanapata huduma hapa hivyo kuwaondolea adha ya kusafiri na kupata huduma mbali wananchi wa kanda ya ziwa ambapo awali zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa wa saratani wa Ocean Road walikuwa wakitoka kanda hiyo.

Naye Mtaalam wa Tiba Mionzi wa Idara ya Saratani wa BMC, Alex Mpugi alisema kabla ya mashine hizo walikua wakitoa huduma za saratani kwa kutumia kemikali.

"Naomba nitoe wito kwa wananchi hususan wanawake kujitokeza kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti kila siku ya Jumanne na Alhamis".Alisisitiza Mpungi.

Kwa upande wa Upasuaji Mkurugenzi wa Upasuaji Dkt.Fabian Massaga alisema kuwa,Hospitali imefanikiwa kufanya ukarabati na upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka vyumba sita hadi kumi na tatu ambapo vyumba viwili hutumika kwa upasuaji wa dharura na kimoja kwa ajili ya upasuaji kwa akina mama wajawazito.

Aliongeza kuwa kwa upande wa upasuaji wameweza kuongeza idadi ya wagonjwa kutoka ishirini na tano hadi hamsini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wengi waliokuwa wanasubiri upasuaji kwa miezi mitatu lakini hivi sasa wanafanyiwa upasuaji ndani ya wiki moja.

Hata hivyo Dkt. Massaga alisema upanuzi huo umeendana na ununuzi wa vifaa vipya na vya kisasa ikiwemo vitanda vya kufanyia upasuaji, taa maalumu za vyumba vya upasuaji na mashine za kisasa kabisa za kutolea dawa ya usingizi. Vifaa hivi vimeagizwa moja kwa moja viwandani kwa takribani Shilingi bilioni 1.4 badala ya Shilingi bilioni 3 kama wangenunua kwa wauzaji hapa nchini.
 Mtaalam wa mionzi Alex Mpugi akitoa maelezo jinsi mashine ya mionzi inavyofanya kazi
 Mashine ya kisasa ya kutambua(kupanga) sehemu inayotakiwa kupatiwa mionzi iliyoko kwenye hospitali  ya kanda ya rufaa Bugando
 Mfizikia Tiba wa Idara ya Saratani katika hospitali ya Bugando Prof. Pradumna Chaurassia  akiwaelekeza maofisa habari jinsi wanavyozuia eneo jingine ambalo halijaathirika na saratani isipate mionzi pia saratani isienee mahali pengine
 Mfizikia Tiba wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Bugando Prof. Pradumna Chaurassia  akiwaelekeza maofisa habari jinsi wanavyozuia eneo jingine ambalo halijaathirika na saratani isipate mioni piasaratani isienee mahali pengine
 Mkurugenzi wa upasuaji wa BMC Dkt. Fabiani Massaga akifafanua jambo wakati  maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake walivyotembelea idara hiyo ambapo hivi sasa wamepunguza idadi ya wagonjwa kusubiri upasuaji kutoka miezi mitatu hadi ndani ya wiki moja
 Picha ya pamoja ya maofisa habari kutoka wizara ya afya na taasisi zake mara baada ya kutembelea idara ya upasuaji na kujionea maboresho makubwa ikiwemo upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka sita hadi kumi na tatu pamoja na vifaa na vifaa tiba vya kisasa.


INTRODUCING : Innoss'B Ft Diamond Platnumz - Yope Remix (Official Music Video)

WATUMISHI WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA WATAKIWA KUTAMBUA,KUKUBALI MFUMO WA UTENDAJI WA JESHI USU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Morogoro

WATUMISHI wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wametakiwa kutambua na kukubali mfumo wa utendaji wa Jeshi Usu ili kukabiliana na changamoto za uhifadhi nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy alipokuwa akifunga kikao cha pili cha bodi hiyo kilichofanyika mkoani hapa.

Amesema mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda katika mfumo wa Jeshi Usu yanalenga kuleta suluhisho la kudumu katika kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali misitu na nyuki nchini.

Mkeremy amesema kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji na hata matokeo katika mfumo wa kiraia na ule wa Jeshi Usu, na kwa hali ilivyo sasa mfumo wa Jeshi uso ndio mfumo pekee utakakwenda kunusuru misitu nchini.

“Niwapongeze TFS kwa kazi kubwa mnayoifanya licha ya changamoto nyingi mnazokabiliana nazo kiutendaji, changamoto hizi sasa zinakwenda kuisha, kinachotakiwa ni nyinyi watendaji sasa kutambua na kukubali mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia na kwenda kwenye mfumo wa Jeshi Usu,

“kwa bahati nzuri mimi nimefanya kazi katika mifumo yote miwili nachoweza kuwaeleza ni kwamba mnaweza msione matokeo sasa lakini with time mtaona, duniani kote majeshi ya uhifadhi yanaheshimika, hakutakuwa na mwenye uthubutu wakuingia kwenye hifadhi za misitu, kila mtu anajua nini maana ya jeshi,” amesema Brigedia Jenerali Mkeremy.

Kwa Brigedia Jenerali Mkeremy ni kikao chake cha kwanza kwa mwaka 2019/2020 na cha pili tangu Bodi izunduliwe mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kamishna Mhifadhi Misitu nchini, Professa Dos santos Silayo amesema zaidi ya watumishi 500 wamekwishapata mafunzo ya Jeshi Usu katika chuo cha Kijeshi Mlele na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Pansiansi na bado zoezi linaendelea.

Amesema tangu zoezi hilo la mabadiliko hayo ya mfumo wa utendaji lianze, baadhi ya maeneo yaliokuwa yana uharibifu mkubwa wa misitu yameanza kuwa salama kutokana na watendaji wake kufanya kazi kwa kuzingatia muda na taratibu.

Wajumbe wa Bodi walipata fursa ya kupanda miti katika maeneo ya Kituo cha Mbegu za Miti mkoani Morogoro kama sehemu ya kuhimiza uhifadhi kwa kupanda miti.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy  akipanda mti huku akishuhudiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi na menejimenti ya TFS
 Kamishina Mhifadhi Misitu Profesa Dos Santos Silayo akipanda mti
 Mmoja ya wajumbe wa bodi ya ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania akipanda mti
Wajumbe wa bodi wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya TFS mara baada ya kumaliza kikao cha pili cha podi hiyo tangu kuzinduliwa katika ukumbi wa Kituo cha Mbegu za Misitu Morogoro jana.

TCRA yawafikia wanasongwe Uhamasishaji usajili wa laini za simu kwa alama za vidole

$
0
0
Afisa TCRA akiwahudumia Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika Viwanja vya Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Mkuu wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akizungumza na Wananchi Viwanja vya Soko Mlowo mkoani Songwe wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama pamoja na Huduma zingine kwa kushirikiana na wadau.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma Thomas William akizungumza na Wananchi wa Songwe taratibu za upatikanaji wa vitambulisho vya taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA iliyofanyika katika Viwanja vya Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Sehemu ya matumizi ya Huduma mbalimbali ya Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Sehemu ya matumizi ya Huduma mbalimbali ya Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.

RAIS DKT SHEIN AHUTUBIA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar. [Picha na Ikulu] 07/09/2019.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC wakiwa katika ufunguzi mkutano huo uliofunguliwa leo na RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi Idrisa Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC wakiwa katika ukumbi Idrisa Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa mkuitano huo uliofanywa leo na RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi Idris Abdul Wakili, Vuga Mjini Zanzibar,(wa tatu kulia) Rais wa UTPC Deogratias Nsokolo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo katika ukumbi wa Idris AbdulWakil,Vuga Mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa UTPC Deogratias Nsokolo alipowasili katika viwanja vya ukumbi Idris Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC uliofanyika leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Anders Sjøberg alipowasili katika viwanja vya ukumbi Idris Abdul Wakili Vuga Mjini Zanzibar leo katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania-UTPC

HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA YAJIPANGA KUDHIBITI MIANYA YA WAKWEPA USHURU

$
0
0


MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

BAADHI ya madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Pwani wameielekeza halmashauri hiyo kuangalia namna ya kuongeza mashine( posi )na mageti kwenye maeneo ambayo yanaonekana ni njia za panya zinazotumika kukwepa ushuru.

Hatua hiyo wameieleza ,inalenga kuinua mapato ya ndani ,kudhibiti utoroshaji na kudhibiti mianya ya wizi.

Wakizungumzia kwa nyakati tofauti, wakati wa baraza la madiwani, diwani wa kata ya Dutumi Mkali Kanusu na diwani wa Kilangalanga Mwajuma Denge walisema, yapo maeneo ambayo makusanyo yanashuka kutokana na kukosa posi na mengine watu kukwepa kulipa ushuru.

Denge alisema, kumekuwa na wimbi kubwa la kutorosha mkaa pasipo kulipia ushuru eneo la Ruvu Madimla kutokana na kutokuwepo geti.Aliomba kwa mkurugenzi, kuweka geti pamoja na Mzenga Njiapanda ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Nae Kanusu alifafanua, suala la mapato ni la wote ambapo inastahili kusimamia wakusanyaji wa ushuru kwenye vizuizi na kuangalia namna ya kuongeza nguvu pasipo kuwepo mageti.

"Pia watendaji wa kata watoe taarifa ya makusanyo kwa madiwani,kutuambia kilichopatikana na changamoto zinazokwamisha kuongeza makusanyo,tubadilishe utaratibu wa kufanya tathmini wenyewe kuanzia kata,hii itatusaidia"alielezea Kanusu.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Butamo Ndalahwa alieleza, wanakusudia kuinua mapato katika vyanzo vya mapato ya ndani kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza na kusimamia kikamilifu vizuia vyote .Alielezea kuwa mbali ya hilo ,wameanza kudhibiti baadhi ya mageti ikiwemo geti la Madege kutoka makusanyo 0 hadi sasa wanakusanya milioni mbili kwa wiki.

"Kamati ya fedha tunatenga muda na kutembelea miradi mbalimbali na mageti hayo ambapo maeneo yasiyoridhisha wameongeza usimamizi na kuongeza mageti katika sehemu zinazotumiwa kukwepa kodi"alieleza 
Alibainisha ,ili kuongeza msukumo wanatarajia kuanza kushindanisha kata kwa kata na kutoa zawadi kwa kata itakayoongoza kwa makusanyo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mansoor Kisebengo alisema makisio ya makusanyo ya ndani yalikuwa bilioni 2.164.210, hali halisi ya makusanyo hadi sasa ni bilioni 1.370.278 sawa na asilimia 63.

Kisebengo aliainisha,wamepokea asilimia 80 ya mapato kutoka serikali kuu,hivyo aliiasa halmashauri na madiwani kujipanga kupitia mapato ya ndani ili kusonga mbele na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kibaha


WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MUHIMBILI KUNUFAIKA NA MAKTABA ILIYOTOLEWA NA WANAFUNZI WA 1988

$
0
0
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Muhimbili na shule ya msingi Umoja wa Mataifa kufaidika na Maktaba iliyokarabatiwa na kununuliwa vitabu na wanafunzi waliosoma shule ya Msingi Muhimbili kipindi cha nyuma cha mwaka 1988 ambao amejitolea katika kuboresha elimu katika shule hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi maktaba katika shule ya msingi Muhimbili, Mwenyekiti wa wanafunzi waliosoma katika shule ya msingi Muhimili mwaka 1988, Usia Nkoma amesema kuwa wanafunzi wanaosoma shule ya Muhimbili watumie vizuri Maktaba hiyo kwaajili ya kijiongezea uelewa.

"Maktaba hii itumike na wanafunzi pamoja na waalimu ili kujiongezea uwanda mpana wa kuelewa masomo mnayofundishwa hapa shuleni kwa kuwa mwalimu darasani anakufundisha kwa asilimia 25 na asilimia 75 wanafunzi ndio unatakiwa uelewe ili kukamilisha masomo mliyofundishwa na kutimiza asilimia 100".

Usia Amesema kuwa Maktaba hiyo iwe kielelezo kwa wanafunzi wengine ambao wataguswa kwaajili ya kuendeleza kuihudumia shule ya Msingi Muhimbili na wao wawe kama walenzi wa shule hiyo kwani wao ndio imewale na mpaka sasa wao bado ni wanafunzi wa shule hiyo.

Nae Mkuu wa shule ya Msingi Mhimbili pamoja na Mkuu wa shule ya Msingi Umoja wa Mataifa wamewashukuru wanafunzi wa shule hiyo wa mwaka 1988 kwa kuona umuhimu waikarabati pamoja na karabati Maktaba katika shule hiyo.

Amesema kuwa wazo la kuikarabati shule ya Msingi Muhimbili lilikuja mara baada ya wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule hiyo mwaka 1988 kuunda kikundi cha pamoja ili kuendeleza taaluma pamoja na shule hiyo.
 Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akizungumza na walimu wastaafu, walimu wa sasa na wanafunzi wa shule hiyo wa sasa na wa waliomaliza mwaka 1988 wakati wa kukabidhi Maktaba iliyotolewa na wanafunzi wa Mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili.
 Mwenyekiti wa Wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili, Usia Nkoma akizungumza na wanafunzi wa sasa na wa mwaka 1988 pamoja na walimu wastaafu na wasasa wa shule hiyo wakati wa kukabidhi Maktaba katika shule hiyo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mtaifa, Woindumi Siyao akiwashukuru wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili wa mwaka 1988 katika shule hiyo kwa kuikumbuka na kujitolea kuikarabati na kuifanya iwe na Maktaba.
 Kiongozi wa Dini ambaye pia ni mwanafunzi aliyesoma shule ya Msingi Muhimbili akiomba ili shughuli ya kukabidhi Maktaba katika shule hiyo iende vizuri.
 Baadhi ya walimu wa sasa wa shule ya msingi Muhimbili.

 Baadhi ya walimu wa Staafu wa shule ya Msinmgi Muhimbili wakiwa moja ya wageni walioalikwa na wanafunzi waliosoma katika shule ya Msingi Muhimbili mwak 1988 jijini Dar es Salaam.


 Katibu na Muweka hazina wa wanafunzi waliomaliza shule ya Msingi mwaka 1988.


 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muhimbili na wahitimu watarajiwa katika shule hiyo.
 Meza Kuu katika kukabidhi ukarabati wa Maktaba katika shule ya Msingi Muhimbili leo jijni Dar es Salaam.


 Badhi ya walimu wastaafu waliokuwa wakifundisha shule ya Msingi Muhimbili wakizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo leo wakati wa kukabidhi Maktaba iliyotolewa na wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo.



 Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akikata utepe kuzindua Maktaba iliyotolewa na wanafunz waliomaliza mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbiliwakishirikiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mtaifa, Woindumi Siyao, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili, Usia Nkoma na Mkuu wa shule ya Msingi Muhimbili, Jovita Mushi.


 Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akifungua kitabu cha Satadi za kazi mbele ya  walimu wastaafu, walimu wa sasa na wanafunzi wa shule hiyo wa sasa na wa waliomaliza mwaka 1988 wakati wa kukabidhi Maktaba hiyo kwa Mkuu wa shule ya Msingi Muhimbili na Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyotolewa na wanafunzi wa Mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili.



Maktaba katika shule ya Msingi Muhimbili iliyotolewa na akukarabatiwa na wanafunzi wa shule hiyo wa mwaka 1988.

KUMBUKUMBU YA KIFO

$
0
0
It has been 26 years since you recieved the call from the Lord. It seems like yesterday to All family members as we remember your wisdom, care and leadership.We miss you everyday and your sons, daughters, kids and great grand kids will always appreciate your legacy. May the almighty Lord Allah rest your soul in eternal Peace, till we meet again. Amen.

HOMERA MARATHON YAVUKA LENGO LA HARAMBEE YA KUCHANGIA HOSPITALI, YAFIKISHA MILIONI 242,064,570 KUVUKA LENGO LILILOHITAJIKA LA MILIONI 194.

$
0
0
Na Ripota Wetu-Mkoa wa Katavi.

Kufuatia harambee iliyoandaliwa kuanzi tarehe 26/8/2019 hadi kilele chake tarehe 6/9/2019 katika chakula cha hisani kuchangia ukarabati wa Hospitali teule ya rufaa ya Katavi.

Tarehe 6/9/2019 Homera Marathon imehitimishwa kwa kupatikana jumla ya Tsh. Milioni Miambili, Arobaini na Mbili na Sitini na Nne Elfu,Miatano na Sabini (Tsh 242,064,570) na kuvuka lengo lililohitajika la million 194).

Akitangaza kiasi hicho katika ukumbi wa Police Club wakati wa chakula cha hisani Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera amesema hiyo ni jumla kuu ambapo kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi.

RC Homera amesema, kiasi hicho kimevuka malengo ambapo amesema ili ukarabati ukamilike ilikuwa inahitajika Tsh. Milioni Mia Moja,Tisini na Nne Elfu (Milion194) na amewaomba walioahidi wakamilishe ahadi zao ndani ya Wiki moja ili ukarabati uanze haraka iwezekanavyo.

Aidha, amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Katavi, wafanyabiashara, Wabunge na viongozi wote kwa ujumla lakini pia amewashukuru na Wafanyabiashara wa katavi na nje ya katavi, Watumishi wa umma na Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, Bank za NMB,TPB, CRDB, NBC, Waandishi wa Habari, na pia amevishukuru Vyombo vya habari yakuitangaza Homera Marathon na dhamira ya Mkoa huo kufikia kilele chake tarehe 6/9/2019.

Ikumbukwe pia kabla ya chakula cha hisani, Asubuhi kulikuwa na mbio za KM 1,3,5,10 na KM 20 ambapo washindi watatu wa KM 5 wa kwanza alipewa Tsh 50,000/= mshindi wa Pili Tsh 30,000/= na watatu Tsh 20,000/= sanjari na kutunukiwa vyeti na medani. 

Waliokimbia KM 10 mshindi wa Kwanza Tsh 70,000/=, Mshindi wa Pili Tsh 50,000/= na mshindi wa Tatu Tsh 20,000/=.

Waliokimbia KM 20 mshindi wa kwanza na wa pili walifanafana ambao kila mmoja amepewa Tsh 100,000/=, Mshindi wa Pili Tsh 70,000/= na mshindi wa Tatu Tsh 50,000/= zawadi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa.

Mwisho Burudani ziliendelea kutoka kwa waimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Christopher Mwahangila, Sifael Mwabuke, Ambwene Mwasongwe pamoja na Zabron Singers kutoka Shinyanga.


NGUZA VIKING AFUNGA NDOA LEO JIJINI DAR NA KATIBU TAWALA WILAYA YA MUHEZA

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe nchini almaarufu kwa jina la Nguza Viking aka Babu Seya  amefunga ndoa takatifu leo jijini Dar na Katibu Tawala Wilaya ya Muheza (DAS), Bi Esterine Haule. Tunawatakia kila lakheri, afya njema na maisha marefu zaidi na Mungu akayabariki maisha yao mapya ya Ndoa. #harusi #ndoa #furahayapamoja
 Mwanamuziki Mkongwe nchini almaarufu kwa jina la Nguza Viking aka Babu Seya  akiwasili kanisani kufunga ndoa takatifu leo jijini Dar na Katibu Tawala Wilaya ya Muheza (DAS), Bi Esterine Haule. Tunawatakia kila lakheri, afya njema na maisha marefu zaidi na Mungu akayabariki maisha yao mapya ya Ndoa. 
 Bi Harusi, Katibu Tawala Wilaya ya Muheza (DAS), Bi Esterine Haule akiwa katika furaha

KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UGANDA LAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akifunga kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha zote  na Matokeo Chanya+
Wafanyabiashara wa Tanzani na Uganda wakifuatilia.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Edwin Rutageruka akielezea mambo machache wakati wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) wakifuatilia kwa makini. 

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro  (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye akihutubia wakati wa ufungaji wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.  
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMSINDIKIZA RAIS MUSEVEN

$
0
0
Rais wa Yoweri Museven wa Uganda akiagana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Sept 07,2019 baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi ya siku Tatu hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Sept 07,2019 baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi ya siku Tatu hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsindikiza Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Sept 07,2019 baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi ya siku Tatu hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Yoweri Museven wa Uganda wakiwapungia mikono Wananchi mbalimbali waliofika kwa ajili ya kumuaga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Sept 07,2019 baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi ya siku Tatu hapa Nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Yoweri Museven wa Uganda wakiwapungia mikono Wananchi mbalimbali waliofika kwa ajili ya kumuaga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam leo Sept 07,2019 baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi ya siku Tatu hapa Nchini.


NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WASOMI WAZIHUDUMIE JAMII ZAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.
Baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka katika familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond wakiwa wamesimama wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa anawasili ukumbini katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe.Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu mara baada ya kukabidhiwa cheti chake.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wakati wa hafla ya kuwapongeza Wahitimu wa Vyuo vikuu waliosomeshwa na Africa Foundation.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe.Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu, Mbarouk Salum aliyetunukiwa zawadi ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano za kitanzania kutokea Zanzibar kufuatia kuitumia vizuri elimu yake katika kujitolea mchango wake mkubwa kwa jamiii alikotoka. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe. Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu, Kalmat Tamal aliyetunukiwa zawadi ya hundi yenye thamani ya laki tano kufuatia kuitumia vizuri elimu yake katika kujitolea mchango wake mkubwa kwa jamiii alikotoka. 
.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe.Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu, Leyla Hassan mara baada ya kukabidhiwa cheti chake cha pongezi kwa kumaliza masomo yake ya Chuo Kikuu.

( PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)



……………………..

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka wahitimu waliomaliza Vyuo vikuu waliosomeshwa kupitia mradi wa kuzisaidia familia duni katika vijiji vinavyopakana na maeneo ya Hifadhi wakumbuke kurudi katika vijiji vyao ili wakawahudumie wananchi wa maeneo hayo.

Pia, Amewataka wahitimu hao wakawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa jamii zao juu ya umuhimu wa kulinda Hifadhi kwa vile wao miongoni mwa wanufaika wa shughuli za Uhifadhi nchini.



Akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wahitimu 50 katika ngazi ya Astashahada na Shadada katika kozi tofauti iliyofanyika Jana usiku mkoani Arusha, Mhe.Kanyasu ameitaja Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation kupitia kuwa ni moja ya wadau muhimu wa Uhifadhi ambao ni mfano wa kuigwa katika kuzisaidia familia masikini.

Africa Foundationi ni Asasi inayotekeleza mradi wake kwa kusaidia kulipa ada kwa wanafunzi kutoka familia duni zinazoishi karibu na Hifadhi kujiunga na vyuo vikuu nchini kama inavyofanya Bodi ya Mikopo ya Vyuo Vikuu ( HESLB).

Asasi hiyo inayoendesha baadhi ya Hoteli za kitalii ndani ya Hifadhi za Taifa nchini na imekuwa ikisaidia familia duni kwa kuwalipia ada wanafunzi hao ikiwa kurudisha kwa jamii kile walichopata kupitia Hoteli hizo.


Mkopo huo ni tofauti na ule wa HESLB ambapo mara baada ya kusomeshwa na Africa Foundation wanafunzi hao hulipa mkopo huo kwa kuihudumia jamii alikotoka kulingana na kozi aliyoisomea badala ya kurudisha pesa.

Naye, Waziri wa Habari, Utalii na Mambokale, Mhe.Mahamoud amewataka wahitimu hao wakaitumie elimu hiyo kwa kuwasaidia vijana wengine waweze kutambua thamani ya elimu katika maisha yao

” Nendeni huko mkaibadilishe jamii yenu ianze kutambua umuhimu wa kutunza maliasili tulizonazo, alisisitiza Mhe, Waziri Kombo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa mkoa Arusha, Jerry Muro amewataka wanafunzi hao wakaitumie vizuri elimu yao kwa kuanza kuzibadili kifikra familia zao pamoja na jamii kuhusu umuhimu wa kutunza Hifadhi na kuachana na vitendo vya ujangili ili watalii waendelee kuja nchini

” Elimu yenu ikawe silaha kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya ujangili” alisisitiza Mhe.Muro.

Naye Mkurugenzi wa Africa Foundation kwa nchi za Africa Mashariki, Dkt. Mkomeni Mgonho amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuzifanya familia hizo kuthamini na kuona thamani ya shughuli za Uhifadhi.

Aidha, Amesema kuwa pia ni mchango wao wanaourudisha katika jamii kwa kile wanachopata kupitia Hoteli za kitalii.

Mbarouk Salum ambaye ni mhitimu wa fani ya Udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Muhimbili amesema kitendo cha Asasi hiyo kuwasaidia kwa kuwalipia ada ni moja ya alama kubwa za matumaini kwa familia hizo ambapo zitaweza kubadili maisha kwa kuandaa kizazi bora kitakachopenda na kuthamini shughuli za Uhifadhi.

Africa Foundation imesaidia kuwalipia ada wanafunzi 45 wa Kitanzania pamoja wanafunzi wa 5 wa kutoka nchini Kenya wote wakiwa wanaishi kwenye vijiji vinavyopakana na Hifadhi.
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images